You are on page 1of 75

MT.

KENYA UNIVERSITY

BLA 2113: INTEGRATED KISWAHILI 11 (FONETIKI NA FONOLOGIA)

NA

MURITHI JOSEPH JESSEE

1
YALIYOMO
SOMO LA KWANZA ....................................................................................................................................... 3

DHANA YA LUGHA,FONETIKI NA FONOLOJIA ............................................................................................... 3

SOMO LA PILI .............................................................................................................................................. 12

SAUTI ZA LUGHA ......................................................................................................................................... 12

SOMO LA TATU ........................................................................................................................................... 23

SIFA ZA SAUTI .............................................................................................................................................. 23

SOMO LA NNE ............................................................................................................................................. 33

SILABI .......................................................................................................................................................... 33

SOMO LA TANO........................................................................................................................................... 47

ARUDHI YA SAUTI ........................................................................................................................................ 47

SOMO LA SITA ............................................................................................................................................. 62

MAGEUKO YA SAUTI ................................................................................................................................... 62

2
SOMO LA KWANZA

DHANA YA LUGHA,FONETIKI NA FONOLOJIA


Utangulizi

Katika somo hili tutaangazia dhana hizi tatu:lugha,fonetiki na fonolojia kwani ndio misingi ya

kozi hii ya fonetiki na fonolojia.

 Shabaha

Kufikia mwisho wa somo,uweze:

1.Kufafanua maana ya dhana:

 lugha

 fonetiki

 fonolojia

2.Kubaini ulinganifu wa fonetiki na fonolojia

Lugha

Kamusi ya Kiswahili Sanifu (2004) inaeleza lugha kama; ni mpangilio wa sauti na maneno

unaoleta maana na hutumiwa na watu wa taifa au kabila fulani kwa ajili ya kuwasiliano; maneno

na matumizi yake. Pia inasema ni mtindo anaotumia mtu kujieleza.

3
Baye Good, mhariri wa Dictionary of Education, (1973) anaeleza lugha kama ni kiashiria cha

kuwasiliana mawazo na hisia kutika kwa mwanadamu mmoja kwenda kwa pande mbili, lugha

yaweza kuwa ya kuzungumzwa (mdomo) ama la, ya kinaandishi.

Kulingana na Mgullu, (1999), lugha ni chombo cha fikra.

Trudgil (1974) anayeonyesha kuwa lugha ni mfumo wa sauti nasibu zinazotumiwa kwa

mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani yenye utamaduni wake.

Sapir (1921) anasema kuwa lugha ni mfumo ambao mwanadamu hujifunza ili kutumia

kuwasilishia mawazo, maana na mahitaji. Mfano huu hutumia ishara ambazo hutolewa kwa

hiari. Kutokana na maelezo ya kamusi na watu tuliowataja, lugha inaweza kufasiriwa kama

ifuatavyo:

(a) Lugha ni njia ya mawasiliano

(b) Lugha ni ya kusema

(c) Lugha ni kama Kiswahili, kibukusu, kikamba n.k

(d) Lugha ni chombo cha fikra

(e) Lugha ni mfumo (wa jamii)

(f) Ni sauti nasibu zinazotumiwa na binadamu

(g) Lugha ni ya binadamu pekee. n.k

Lugha ni mfumo wa sauti zenye kubeba maana na ambazo zimekubaliwa na jamii ya watu Fulani

zitumike katika mawasiliano.

4
Lugha pia huweza kuelezwa kama mfumo wa ishara nasibu amabayo hutumika katika

mawasiliano na binadamu.ni mfumo kwa kuwa vipengele vyake vinajitokeza kwa mpangilio

maalum amabao hutegemeana na kukamilishana.unasibu hujitokeza kwa kuwa hakuna uhusiano

wa moja kwa moja kati ya kielekezi na kielekezwa .

Lugha huhusishwa na binadamu,hii ina maana kuwa ,ingawa wanyama wana uwezo wa

kuwasiliana,wao hawana lugha,hata hivyo mawasiliano huenda yakawepo bila lugha.kuna sifa

bainifu zinazoonyesha kuwa lugha ni chombo cha binadamu.

Sauti zitokazo kinywani mwa binadamu ndizo zinazohusishwa na lugha.sauti hizi huwa na

utaratibu au mfumo Fulani.utaratibu huu umepewa kibali na jamii inayotumia lugha.utoaji tu wa

sauti hautoshi kuleta mawasiliano,sauti hizi huhitaji kuwekwa kwenye muundo maalumu ili

kuleta maana inayotakikana.muundo huu huitwa mpangilio wa sauti.

Sauti k.v /a/,/b/,/e/hazina maana ikiwa hazikuunganishwa lakini /b/ na /a/ zikiunganishwa huleta

silabi ba.silabi ba ikiunganishwa na silabi ingine ba huleta neno baba lenye maana ya mzazi

katika lugha ya Kiswahili.

Mawasiliano hayajitokezi kwa kutumia neno moja tu,yahitaji maneno mengine ambayo

hupangwa katika utaratibu wa kiwango cha juu unaoitwa sentensi

Tukirejelea fonetiki na fonolojia tunabaini kuwa lugha inahusiana kwa kiwango kikubwa na sauti

zinazotamkwa.

5
Fonetiki

Kulingana na Ladefoged(1982) na CatfordNi tawi la isimu ambalo huchunguza sauti za

binadamu.Hujihusisha na ala(njia) za kutamkia sauti,namna ya kutamka kuelewa kwa sauti

ilivyotamkwa na jinsi sauti inavyopokelewa na mskilizaji kutoka kwa msemaji.

Fonetiki huwa imegawika katika viwango vitatu:

 Foenetiki matamshi

 Foenetiki akustiki

 Fonetiki sikizi

1.Fonetiki matamshi

Ni kiwango cha fonetiki ambacho hujishughulisha na na ala(njia) za kutamkia sauti,hueleza

utaratibu wa uundaji na utoaji wa sauti za lugha kupitia ala mbalimbali.

Ala (njia) hufahamika kama vitamshi.Kuna aina nne kuu ya vitamshi:

 Ulimi

 Midomo

 Meno

 Paa la kinywa

Ulimi

Huwa na sehemu nne kuu bainifu zaidi:sehemu ya mbele hufahamika pia kama ncha ya

ulimi,sehemu mbili za ndani(bapa la mbele na bapa la nyuma) na sehemu ya nyuma(shina la

ulimi).

6
Midomo

Midomo miwili huweza kutumika konsonati za Kiswahili,ilhali unapotamka vokali umbo la

mdomo hubadilika ili kuzitamka kwa mfano mdomo huweza kuviringwa kutamka sauti [o] na

[u] ilhali mdomo hutandazwa kutamka sauti [a],[e] na [i]

Meno

Meno huweza kutumika kutamkia sauti za Kiswahili.Meno haya huweza kushirikiana na ala

zingine ili kutamka sauti hizi kwa mfano meno ya juu hushirikiana na mdomo wa chini kutamka

sauti [f] na [v]

Meno ya pande mbili hushirikiana na ncha ya ulimi ili kutamka sauti [d] na [nd]

Paa la kinywa

Paa la kinywa huweza kugawikia mara tatu:

1.Sehemu ya mbele

Huweza kufahamika kama masine.Huweza kushirikiana na sehemu ya mbele ya ulimi(bapa la

mbele) kutamka sauti [t],[d],[s] na [z]

2.Sehemu ya katikati

Hujulikana kama burutio.Huweza kuishirikiana na sehemu ya nyuma ya ulimi(bapa la nyuma)

kutamka sauti [c] na [s]

3.Sehemu ya nyuma

7
Sehemu hii hujulikana kama kaakaa,sehemu hii huwa laini.huweza kugusana au kukaribiana na

shina la ulimi wakati wa kutamka sauti [k] na [g]

Zoezi

Tamka sauti [s] na [g]..baini ulipozitamkia

2.Fonetiki Akustiki

Fonetiki akustiki hujihusisha na namna ya kutamka na kuelewa kwa sauti ilivyotamkwa.kwa

mfano vokali [a] hutamkwa midomo ikiwa imetandazwa ilhali vokali [o] hutamkwa midomo

ikiwa imeviringwa.

3.Fonetiki Skiizi

Kiwango hiki cha fonetiki hujishughulisha na jinsi sauti inavyopokelewa na mskilizaji kutoka

kwa msemaji.kwa mfano ikiwa msemaji ametamka sauti[f] mskilizaji anaeza akaipokea kama

sauti [f] au [v] kulingana na mskilizaji.

Fonolojia

Kulingana na Taz.Fromkin,Rodman(1996) anafafanua fonolojia kama taaluma inayohusu

uamilifu wa sauti za lugha,husisitiza zaidi uyakinifu unaodhihirika.

8
Fonolojia huwa ina viwango vitatu:

 Fonolojia nadharia

 Fonolojia zalishi

 Fonolojia tendaji

Fonolojia nadharia

Fonolojia nadharia husimamia maelezo yanayojaribu kusimamia maelezo husika.hujaribu

kueleza umilisi mahususi wa fonolojia tendaji.

Fonolojia zalishi

Fonolojia zalishi huzingatia lugha kama mfumo wa sheria unaowakilisha ujuzi wa mtu

binafsi.kupitia fonolojia zalishi mtu huweza kuzalisha sauti za lugha kwa kuzingatia mfumo wa

sheria.

Fonolojia tendaji

Fonolojia tendaji ni ulimisi wa mfumo bayana wa sauti ambao humwezesha msemaji kueleweka

na kuelewa wasemaji wengine wa lugha yake.

Muhtasari

Katika somo hili tumweza kubaini maana ya lugha,fonetiki tukabaini imegawaika katika

viwango vitatu,fonetiki matamshi,fonetiki akustiki na fonetiki skiizi.Tukabaini dhana ya

fonolojia ambayo tumeona ina viwango vitatu pia ,fonolojia nadharia,fonolojia zalishi na

fonolojia tendaji.

9
Zoezi

1.Taja uhusiano uliomo kati ya fonetiki na fonolojia

2.Fafanua dhana hizi:

 Lugha

 Fonetiki

 Fonolojia

10
Marejeleo

Abercrombie,O.(1967).Elements of Phonetics.Edinburgh:Edinburgh Univeristy Press.

Catford.J.C.(1988).A Practical Introduction to Phonetics.Oxford:Claredon Press.

Fromkin,V&Rodman,R.(1996).An Introduction to Language:4th ed.Newyork:CBS.

Lyons,J.(1981).Language and Linguistic.Cambridge:Cambridge University Press.

11
SOMO LA PILI

SAUTI ZA LUGHA
Utangulizi

Sauti ni dhati ya chochote kinachoweza kusikika kutokana na mgongano au msuguano wa vitu

kama vile mlio na usemi kulingana na kamusi ya Kiswahili(1981).katika somo hili tutaangazia

dhana ya sauti,maumbo ya sauti na dhana zinazohusika katika sauti:foni,fonimu na alofoni.

 Shabaha

Kufikia mwisho wa somo,uweze:

 Kufasili dhana ya sauti.

 Kutofautisha foni,fonimu na alofoni.

 Kubainisha maumbo ya sauti.

 Kutambua na kuwakilisha sauti kifonetiki.

1.Foni

Foni ni sauti ya lugha,sauti za lugha huweza kubainishwa kwa vikundi viwili vikuu:

 Vokali

 konsonati

12
2.Sauti

Sauti huunda maneno ambayo hutumika na watu katika mawasiliano.kulinagana na

Hyman(1975) na Lass(1984)wanasema kuwa sauti huweza kujirudia katika maneno husika na

kauli ndefu ndefu.

kwa mfano neno #baba# limeundwa na sauti [b] na sauti [a] ambazo zimejirudia.

Kila lugha huwa na sauti zake .Kiswahili kina sauti zake zenye kugawika katika makundi mawili

makuu kutegemea jinsi zinavyotamkwa,Makundi yenyewe ni vokali na konsonanti.

Maana ingine ya sauti ni kuwa ni kipashio kidogo zaidi cha mfumo wa sauti ambacho hubainika

kimatamshi.

Sauti ya lugha inawakilishwa kwa mabano mraba [ ].

Ebu sasa tutazama sauti kuu amabazo ni vokali na konsonati.Konsonanti ni sauti amabazo

hutamkwa kwa uzuilifu Fulani wa mkondo hewa kinywani au kooni.

Jedwali hili linaonyesha konsonanti za Kiswahili pamoja na zingine chache kutoka lugha

zingine,ambazo hupatikana kwa wingi

A)KONSONANTI(K)

FONI TAHAJIA NENO MAANA LUGHA

B B baraka kiswahili

P P penzi kiswahili

Mp Mp mpembe Mahindi kimeru

Mb Mb mbuzi kiswahili

13
ɸ B bata Thamani kikuyu

ß B vandu Watu kiluya

F F figo kiswahili

V V vazi kiswahili

Ɵ Th thama kiswahili

Ð Dh dhana Kiswahili

M M maji kiswahili

T T tendo kiswahili

D D dawa kiswahili

Nd Nd ndovu kiswahili

Nð Nth nthe Nchi kikamba

Nz Nz nzaũ Dama Kikamba

N N neno kiswahili

S S sifa kiswahili

Z Z zana Kiswahili

Ts Ts tsia Nenda kiluya

Dz Dz dzia Nenda kiluya

L L leso kiswahili

R R radhi Kiswahili

Š Sh shule kiswahili

Ž S measure Pimo kiingereza

Č Ch chama kiswahili

J J jina kiswahili

14
ɲ Ny nyani kiswahili

ɲǰ Nj njama kiswahili

J Y yungi kiswahili

K K kambi kiswahili

X Kh kheri Kiswahili

ŋɡ Ng ngoma Kiswahili

ŋk Nk nkoro kikisii

ɡ G gereza kiswahili

Ŋ ng’ ng’ombe kiswahili

H H hali kiswahili

Y gh(g) ghala Kiswahili

b)Vokali

Vokali ni sauti inayotamkwa kwa mkondohewa pana,na kwa hivyo,mkondohewa huwa huru

zaidi kuliko konsonanti.

Mfano wa vokali za kimsingi ni kama zifuatazo.

FONI TAHAJIA NENO MAANA LUGHA

I imba Kiswahili

I I image Taswira kiingereza

E E miti Miti Kikuyu

Ɛ E embe Kiswahili

15
Æ A animal Mnyama kiingereza

A A ada Kiswahili

ɑ ar(al) arm Mkono kiingereza

ɒ O pot Nyungu Kiingereza

Ɔ O ono Kiswahili

O O mundu Mtu Kikuyu

ʋ u(oo) pull Vuta kiingereza

U u(oo) uso kiswahili

ɜ ear(er)(ur)(ir) early Mapema kiingereza

ʎ u(o) up Juu kiingereza

Ikumbukwe !!!

Utambuzi wa sauti huzingatia matamshi badala ya maandishi.

Zoezi

Amdika maneno haya kwa kuzingatia abdaji za

kifonetiki:

 Mchochezi

16
 Dhahabu

 Juu

 Tamthil

3.Fonimu

Fonimu ni kipashio kidogo zaidi cha mfumo wa sauti ambacho hutumika kubainisha maana za

maneno mawili ya lugha moja.

Fonimu huwakilishwa kwa kutumia micharazo,yaani //.

Kwa mfano neno #Vua# Tukibadili sauti [v] kwa sauti [f] tutapata neno #fua# ambalo maanake

ni tofauti kabisa na vua. Kwa hivyo ni bayana kusema kuwa sauti [v] na [f] ni fonimu za lugha

ya Kiswahili.

Mfano katika vokali

Neno #Oa# tukibadili sauti [o] kwa sauti [u] tutapata neno #Ua# ambalo ni tofauti kimaana na

neno oa.hivyo sauti [o] na sauti [u] ni fonimu za lugha ya Kiswahili kwani ni vipashio vidogo

vinavyotumika kubainisha maana.

Msingi wa fonimu ni foni yaani sauti za lugha hutambuliwa kuwa foni kwanza,kisha fonimu

ambao husisitiza uamilifu wa sauti.

17
Fonimu huweza kutambuliwa kwa kuangalia ulinganifu wa matamshi ndiposa uweze kubaini

jinsi sauti zinatumika kutofautisha maana.kuna njia tatu kuu za kutambua fonimu:

1.Ukuruba Wa Muundo Wa Sauti

Hapa unastahili kurejelea ulinganifu wa sifa kuu za konsonanti na vokali(foneta) linganuzi.kwa

mfano vokali [a] ina sifa tofauti na vokali [o] kwa kuwa vokali [a] inapotamkwa sifa kuu ni

kuwa midomo hutandazwa ilhali unapotamka vokali [o] midomo huwa imeviringwa.

2.Ufinyu Wa Mazingira Ya Kifonetiki

Mbinu hii ya kutambua fonimu husisitiza matumizi ya sauti moja pekee pahala sawa,inasisitiza

kuwa fonimu itokee mwanzoni,kati au mwisho lakini isiwe pahala pawili.

3.Ubainifu Wa Maana

Mbinu hii husisitiza tofauti za maana za maneno linganuzi.Kunaweza kutokea tabadili ya sauti

na kwa hivyo tofauti za matamshi,bila kuleta ubainfu wa maana.aina hii ya tabadili ikitokea basi

foni husika huwa hazitambuliki kuwa fonimu tofauti bali huwa ni alofoni za fonimu moja.

Zoezi

Tumia fonimu mwafaka kuunda maneno

mengine,kutokana na haya:

a)Imba

b)Pika

c)Ota

18
4.Alofoni

Huwa ni sura tofauti za fonimu moja,kwa kifupi ni foni tofauti ambazo hurejelea fonimu moja.

Kwa mfano maneno

#heri#

#habari#

Huweza kutumika na wengine kama

#kheri#

#khabari#

Katika mifano hii yetu wengi hutumia sauti [h] badala ya [x]-kh. Kwa hivyo sauti [h] na sauti [x]

ni alofoni za fonimu /h/.

Zoezi

 Tambua maneno mengine yenye

kudhihirisha kuwepo kwa alofoni

kisha ubainishe alofoni zake.

19
Maumbo Ya Sauti

Umbo la sauti hurejelea vipengele vya muundo wake.Umbo hili hudhihirishwa na idadi na hali

ya herufi zinazojumuika kwa wakilisho la sauti bayana.

Kutumia kigezo hiki tunapata maumbo matatu ya sauti:

 Sauti sahili

 Sauti wakaa

 Sauti changamano

1.Sauti sahili

Huundwa kwa kipengele kimoja na kuwakilishwa kwa herufi moja.sauti sahili hurejelea foneta

ya konsonanti au vokali moja kwa moja,kwa mfano neno #kisu#

#kisu# tukibaini herufi zake ni konsonati na vokali moja moja:

a)K K V V

K S I U

2.Sauti Wakaa

Aina hii ya sauti hujumuisha sauti mbili zenye muundo sawa.Ishara ya nukta mbili,[:] hutumika

kuashiria sauti wakaa

Kwa mfano neno #juu#tukibainisha kimchoro itakuwa:

20
K VV

P a:

A: inashiria kuwa ni [a] mbili

3.Sauti changamano

Aina hii huwa ni mseto wa sauti sahili mbili au zaidi zenye muundo tofauti.Mseto huu unaweza

kuwa wa kiasilia au wa kimelea cha mageuko Fulani ya sauti.

Mfano wa sauti changamano za asilia ni [mb] na [nd] sauti hizi hutumika katika

maneno:#mbwa# na #ndizi#

Mfano wa sauti vimelea ni [mw],[pw],[ngwa][ai] na kadhalika.Sauti hizi vimelea huweza

kutumika kuunda maneno kama #pwani#,#mwizi#.#aina# na kadhalika.

Sauti changamano huweza kuchorwa hivi:

Mfano neno pwani

K K V V

PW N a i

Muhtasari

21
Katika somo hili tumweza kubaini dhana ya sauti,foni,fonimu na alofoni.tumeona kuwa msingi

wa fonimu ni foni.na baadaye tukaangazia maumbo ya sauti,sauti inaweza kuwa ya umbo

sahili,wakaa au changamano.

Zoezi

1.Fafanua dhana hizi:

 Fonimu

 Foni

 Alofoni

2.Tathmini mbinu moja ya utambuzi wa fonimu kwa kuambatisha mifano mwafaka.

3.Tathmini maumbo ya sauti kwa kutumia mifano mwafaka

Marejeleo

Clark,J. & Yallop,C/(1990).An Introduction to Phonetics and Phonolgy.Oxford:Blackwell.

Lass,R.(1984).Phonolgy:Introduction to Basic Concepts.Cambridge:Cambridge University

Press.

Polome,E.(1967).A Handbook of Swahili Language.London:Institute of African Studies.

22
SOMO LA TATU

SIFA ZA SAUTI
UTANGULIZI

Katika somo la pili tuliweza kubaini kuwa kuna aina mbili kuu za lugha ya Kiswahili:konsonanti

na vokali.katika somo hili tutaangazia sifa za kila mojawapo ya sauti hizi kuu mbili.

 Shabaha

Kufikia mwisho wa somo,uweze:

 Kueleza sifa za konsonati

 Kueleza sifa za vokali

 Kubainisha umuhimu wa sifa za sauti

Sifa ni sura yoyote ya kimatamshi ambayo hutumika kubainisha sauti moja au aina ya sauti.

Sifa Za Konsonanti

Konsonati ni sauti ambazo hutamkwa kwa ukuruba ambao husababisha uzuilifu Fulani wa

mkondohewa pahali na jinsi ya kuvitamka.kutokana na maelezo haya tunapata sifa mbili kuu za

konsonanti:

 Jinsi ya kutamka

 Pahali pa kutamkia

23
1.Jinsi Ya Kutamka

Tukizingatia ya jinsi ya kutamka,tunabaini kuwa vitamshi hukaribiana na kutengana viwango na

hali mbalimbali,hali hii husika husababisha athari ya mpito wa hewa.Kipengee hiki huoreshesha

konsonanti kuwa za aina saba kama ifuatavyo:

A)Vipasuo

Hizi zinapotamkwa hewa itokayo mapafuni husukumwa kwa nguvu na kuzuiwa kinywani kisha

huachiliwa kwa ghafla na kutoa mlio unaofanana na baruti inapolipuka.nazo katikia Kiswahili ni

[p],[b],[t],[d],[k] na[g]

B)Kizuio-Kwamiza

Hizi zinapotamkwa hewa toka mapafuni husukumwa nje kwa nguvu kisha huzuiwa kinywani.

Nafasi ndogo huachwa baina ya ala za kutamkia,hewa hii hupita kwa kukwaruza na kusababisha

sauti hii,k.m ni [č],[ǰ],[dz] na [ts]

Zoezi

Tamka sauti /ch/

Unagundua nini?

C)Vikwamizi/Vikwamizo/Vikwaruzo

Hizi zinapotakwa hewa toka mapafuni hupitishwa taratibu na polepole ,ala za kutamkia nazo

hukaribiana sana.hewa hii inapopita hukwamiza na kutoa mlio kama mkwaruzo.

24
Sauti hizi katika Kiswahili ni [s],[t],[Š],[gh],[h],[ž],[z][x],[y],[f] na [v]

D)Kitambaza

Hizi zinapotamkwa hewa huachiliwa kwa namna ya kutambaa kinywani kisha huzuiwa na

kuruhusiwa ipite taratibu pembeni mwa ufizi na ncha ya ulimi.kitambaza katika lugha ya

Kiswahili ni [l]

E)Kimadende

Kimadende kinapotamkwa ncha ya ulimi hugusishwa ufizi,hewa husukumwa kwa nguvu na

kusababisha ncha ya ulimi kupigapiga kwenye ufizi kwa harakaharaka

Mfano wa sauti hii ni [r]

F)Ving’ong’o

Hivi vinapotamkwa hewa kutoka mapafuni huzuiwa kuingia kinywani,badala yake huingia

puani.kwa sababu ya msukumo wa hewa hii,mlio huskikia kama wa kunongona.sauti hizi ni

[m],[n],[Ŋ] na [ɲ]

G)Viyeyusho

Hivi hutamkwa kwa kusukuma hewa kwa nguvu hadi kwenye kinywa,huzuiliwa

mdomoni.Midomo nayo hufanya umbo la mviringo kisha ulimi hupindwa na kugusa ala

husika.sauti hizi ni [w] na [j].

25
2.Pahala Pa Kutamkia

Tukirejelea sifa ya pahala pa kutamkia pa konsonanti tunapata konsonanti za aina sita,kama

ifuatavyo:

A)Vimeno

Konsananti zinazotamkiwa menoni ni kama [f],[v] ambazo meno ya juu hushirikiana na mdomo

wa chini kuzitamka na[Ɵ],[ð] meno ya pande zote mbili hushirikiana na ncha ya ulimi

kuzitamka.

B)Vimidomo

Midomo miwili huweza kutumika kutamka konsonanti za aina hii.konsonanti hizi ni kama

[p].[b],[mp],[m],[O] na [3]

C)Viburutio

Konsanati hizi hutamkiwa katika burutio,burutio ni sehemu ya katikati ya juu zaidi la paa la

kinywa ambayo hushirikiana na bapa la nyuma la ulimi kutamka konsonati kama

[č].[Š],[ž],[ǰ],[ɲǰ],[ɲ] na [j]

D)Vimasine

Vimasine hutamkwa katika masine,Masine ni sehemu ya mbele ya paa la kinywa ambayo pia ipo

nyuma ya ufizi wa juu,kutamka konsonanti za aina hii masine hushirikiana na bapa la mbele la

ulimi.

Aina hii ya konsonanti ni kama:[t],[d],[nt],[nd],[n],[s],[z],[l],[r],[ts],[dz],[ns],[nz],[nts] na[ndz].

26
E)Viglota

Glota ni mwanya unaopenye katikati mwa kongomeo na kooni ambayo pia huzingirwa na nyuzi

mbili za sauti.mfano wa viglota ni [h]

F) Vikaakaa

Konsonanti zinazofahamika kama vikaakaa hutamkwa katika kaakaa.kaakaa ni sehemu ya

nyuma kabisa ya paa la kinywa ambayo pia huhisika kuwa laini.

Katika kutamka vikaakaa,kaakaa huweza kugusana au kukaribiana na shina la ulimi.

Mfano wa konsonanti hizi ni:[k],[g],[ŋg],[ŋk],[ŋ],[x],[y] na [w]

Sifa hizi mbili za kuanisha konsonanti zinaweza kuonyesha kwa kupitia jedwali lifutalo.

Jinsi ya Pahala pa kutamkia

kutamka midomoni menoni Masineni burutio kaakaa Glota

Vipasuo Pb t d k g

Vizuiwa ts dz č ǰ

Vikwaruzo Øß f vøð s z Šž x y H

Kitambaza mp mb mf mv nƟ nt nd ns ɲč ɲǰ ŋg ŋk

nð nz

Nazali m n ɲ Ŋ

Vilainisho rl

Viyeyusho w j W

27
Konsonanti za Kiswahili zinaweza kuaainishwa pia kwa sifa ya ughuno.Mghuno ni mrindimo

unaoletwa na mtetemo kasi wa nyuzi za sauti,hali hii huweza kubainsha konsonanti kwa

makundi mawili:

 Konsonanti ghuna [+GH]

 Konsonanti si ghuna [-GH]

Jedwali lifuatalo linadhihirisha haya:

Hali ya

ukwamizo Vikwamizo msingi Nazalishi awali

Jinsi ya kutamka -ghuna +ghuna -ghuna +ghuna

Vipasuo P b mp mb

t d nt nd

k g ŋk ŋg

Vizuiwa ts dz nts ndz

č ǰ ɲč ɲǰ

Vikwaruzo f ß mf mß

Ɵ v nƟ mv

s ð ns nð

Š z ɲŠ ndz

x ž ŋx ɲž

ɸ y mɸ ŋy

28
Sifa Za Vokali

Matamshi ya vokali huwa hayana uzuilifu wa hewa kama ule wa konsonanti ,hivi ni kusema

kuwa kutamka vokali ni rahisi kuliko konsonanti.

Vokali za Kiswahili huweza kuanishwa kupitia sifa tatu,ambazo ni:

 Umbo la midomo

 Ulalo wa ulimi

 Uinuko wa ulimi

A)Umbo La Midomo

Sifa hii hurejelea jinsi mdomo huwa wakati wa kutamka vokali hizi,midomo aidha huviringwa

au kutandazwa.

Kupitia sifa hii tunapata vokali viringe na vokali tandaze.

1.Vokali viringe

Hizi hutamkwa midomo ikiwa imeviringwa,mfano wa vokali hizi ni:[o] na [u]

2.Vokali tandaze

Hizi huweza kutamkwa midomo ikiwa imetandazwa,mfano wa vokali hizi ni:[a],[e] na [i]

B)Ulalo Wa Ulimi

Vokali za Kiswahili zinapotamkwa ulimi huweza kulala aidha ukielekea bapa la ulimi,nyuma

kulekea shina la ulimi au ndani katikati mwa mwili wa ulimi hivyo basi tukirejelea haya tunapata

vokali za lugha ya Kiswahili za aina tatu ambazo ni:

29
Vokali za mbele:[i] na [e]

Vokali za ndani:[a]

Vokali za nyuma:[u] na [o]

C)Uiniko Wa Ulimi

Wakati wa kutamka ulimi huweza kushuka au kuinuka viwango mbalimbali kutegemea na sauti

inayotamkwa,kwa kurejelea vokali ulimi huweza kuinuka juu,chini au kuwa kati.kutokana na

hali hii tunapata kuanisha vokali za Kiswahili kwa makundi matatu:

Vokali za juu:[i]na[u]

Vokali za chini:[a]

Vokali za kati:[e] na [o]

Sifa hizi mbili kuu za vokali[uiniko na ulalo wa ulimi) zinadhirishwa katika jedwali lifuatalo.

Uiniko wa ulimi Ulalo wa ulimi

Mbele Ndani Nyuma

Juu I u

Kati ɜ o

e ɔ

Chini ɒ

æ a ɑ

30
Zoezi

Sifa gani hubainisha jozi zifuatazo za sauti:

[m]

[b]

[o]

[e

Muhtasari

Katika somo hili tumeweza kufafanua sifa za sauti za Kiswahili(vokali na konsonati)katika soma

linalofuata tutaangazia ruwaza za sauti.

31
Marejeleo

Clark,J. & Yallop,C/(1990).An Introduction to Phonetics and Phonolgy.Oxford:Blackwell.

Hyman,L.M(1975).Phonolgy:Theory &Anaysis.Newyork:HRW

Schane,S.(1973).Generative Phonology.Englewood Cliffs,N.J:Prentice Hall,Inc

Sloat,C(1978).Introduction to Phonolgy.Englewood Cliffs,N.J:Prentice Hall,Inc

32
SOMO LA NNE

SILABI
Utangulizi

Katika somo hili tutaangazia silabi inavyodhihirisha ruwaza za sauti za lugha.kufanya haya

tutabaini maana ya dhana silabi,tubaini maumbo ya silabi na muundo wake na baadaye

tutofautishe aina za silabi.

 Shabaha

Kufikia mwisho wa somo,uweze:

 Kufafanua maana ya silabi

 Kutathmini maumbo ya silabi

 Kufafanua aina za silabi

 Kuwakilisha muundo wa silabi

Dhana Ya Silabi

Silabi huwa ni tamko katika mfumo wa sauti ambalo huwa ni irabu au konsonati na irabu.

Silabi ni kiungo cha neno ambacho kwa kawaida hujumuisha vokali moja au badili la

vokali.maneno yote ya lugha moja inafaa iweze kijigawa silabi zenye ruwaza dhahiri

Silabi za neno au kauli moja hutenganishwa kwa ishara ya ($)

Kwa mfano neno #baba# limeundwakwa silabi mbili ambazo ni SbaS na SbaS

33
Mwambatanisho wa sauti ndiyo hali ya kawaida ya kipashio cha silabi,ijapokuwa pia sauti moja

pekee huweza kuunda silabi. Kwa mfano katika neno #mti# sauti ya kwanza imeundwa kwa

silabi moja- SmS

ZOEZI

Bainisha maneno haya yamaundwa kwa silabi

ngapi.

 Ndege

 Mtu

 Kazi

Maumbo Ya Silabi

Umbo la silabi hurejelea idadi ya vokali na konsonanti zilizotumika kuunda silabi hio.Maumbo

ya silabi za Kiswahili huwa ya aina tofauti kulingana na idadi ya foneti na aina ya mpangilio wa

foneti hizi.

Maumbo yenyewe yanadhrishwa katika makundi manne yafuatavyo:

1.Umbo la KV

2.Umbo la V au N

3.Umbo la KK

34
4.Umbo la KVK

1.Umbo la KV

Umbo hili ndilo umbo bia la silabi,hurejelea konsonanti mwanzo kisha vokali,kwa mfano hili

linadhirika katika maneno:

#pa# SpaS:KV

#juu# Sju:S:KV

2.Umbo la V au N

Umbo hili hurejelea silabi za Kiswahili ambazo huwa na sauti moja aidha vokali au nazali.sauti

ikirejelea vokali moja ,vokali hii huwa mwanzoni mwa neno

kwa mfano katika neno #uzi#-neno hili limundwa kwa silabi mbili ambazo ni SuS na SziS

Nazali inapotumika mwanzoni mwa neno huchukuliwa kama silabi moja,kwa mfano katika

maneno:

#mti#----------

#nzi#.............

35
Zoezi

Fikiria maneno mengine yenye umbo hili la

silabi.

3.Umbo la KK

Silabi zenye umbo hili la KK huwa na silabi mbili zenye umbo la konsonanti,konsonanti ya pili

ya umbo hili huwa ni nazali au kilainisho.Umbo la aina hili linadhihirika vyema katika lugha ya

kiingereza.

Kwa mfano katika maneno:

#table#

4.Umbo la KVK

Umbo hili hudhirisha kuwepo kwa silabi iloundwa na silabi konsonanti,vokali kisha konsonanti

mtawaliwa.Katika lugha ya kineloti umbo hili hudhirika vyema,katika lugha ya Kiswahili

huweza kutokea wakati neno limekopwa bila kutoholewa vyema.

kwa mfano katika neno #333333333333333

Muundo Wa Silabi

Kulingana na kamusi ya Kiswahili sanifu (1981)Muundo ni umbo la kitu kutokana na jinsi

kilivyounda.Silabi za Kiswahili huwa za miundo mitatu:

36
 Kilele

 Fungio

 Tangulio

1.Kilele(LE)

Katika lugha ya kiswahili kilele huwa ni kiungo ambacho kwa kawaida huwa sauti ya

vokali.Ingawa katika lugha zingine hutumia nazali au kilainisho

Kanuni ya muundo wa kilele huwa ni :

LE V(N)(L)

Ambamo N=n(m)

L=l

2.Fungio(FU)

Fungio ni kiungo cha silabi ambacho hufuata kilele.huweza kuundwa kwa konsonanti moja au

zaidi.

Kanuni ya muundo wa fungio ni:

FU K (O)

3.Tangulio(TA)

Tangulio ni sehemu inayounga sauti zote ambazo huja awali ya kilele(yaani kabla ya

vokali).Tangulio huundwa kwa konsonanti mbili au zaidi.

Kwa mfano silabi #ni# ina tangulio moja tu ambayo ni /n/

37
Viungo hivi viatatu vya muundo wa silabi huweza kujiunga na kudhirisha vipengele viwili

ambavyo ni :Tangulio na kina(KI)

Kina hujumuisha kilele na fungio,lakini iwapo silabi haina fungio basi kilele pekee huwa kama

kina.

Kanuni ya kina ni:

KI LE -FU (LE)

Mahusiano haya ya silabi yanadhirishwa vyema kwa kutumia mchoro wa matawi kama

ifuatavyo:

SI KVK:$nam$ ya neno#nam#

SI

TA KI

LE FU

K V K

N a m

38
(4:12) SI V: $a$ ya #a $ da#

(4:13) SI VK: $ tya neon #ot#

(4:14) SI KN: $ ņŝ $ ya #fa$ shion#

39
(4:15) SI N: $m$ ya #m $ tu#

(4:16) SI KL: $bl$ ya #ta $ ble#

40
Sifa Za Silabi

Katika kutathmini sifa za silabi,mtu hurejelea muundo wa kina,awali tulisema kuwa kina ni

muungano wa kilele na fungio au kilele pekee.

Kuna aina nne kuu za silabi:

 Silabi wazi

 Silabi funge

 Silabi nyepesi

 Silabi nzito

1.Silabi wazi

Silabi wazi huwa hazina fungio hivyo basi huweza kuishia kileleni.Huweza kukomea kwenye

vokali au konsonanti silabu.

Mfano $ ndoa$ ,na $pa:$

41
(4:17)

(a)

2.Silabi Funge

Aina hii ya silabi huishia kwa sauti ya konsonanti.konsonanti hi indo hutumika kufungia silabi.

Mfano wa silabi funge:$iŋk$ na $ča:t$ (wino-ink) na (jedwali-chair)

4:18

42
3.Silabi Nyepesi

Silabi nyepesi huundwa kwa kina cha vokali sahili,vokali changamano,mseto wa konsonanti

sahili na vokali fupi au badili la vokali.

Silabi inaweza kuwa nyepesi wazi au nyepesi funge.mfano wa nyepesi wazi ni kama $ni$ na

$rai$,silabi nyepesi funge ni kama $pen$ na $line$

4:19

4:20

43
4.Silabi Nzito

Aina hii ya silabi huundwa kwa kina cha vokali wakaa,mseto wa vokali wakaa na konsonanti

moja au mseto wa vokali fupi na konsonanti mbili au zaidi,yaweza kuwa silabi nzito wazi kwa

mfano $ta:$ na $ndo:$ au silabi nzito funge kama $ri:d$ na $desk$

Muhtasari

44
Katika somo hili tumweza kufasili maana ya silabi,maumbo ya silabi na sifa za silabi na

mwishowe tukaangazia sifa za silabi ambazo tumedhihirisha sifa nne kuu,wazi,funge,nyepesi na

nzito. Katika somo linalofuata tutaangazia arudhi za sauti(ruwaza za sauti.)

Zoezi

1.Fafanua dhana ya silabi

2.Orodhesha maumbo ya silabi kama yalivyobainika kwa kuambatanisha na mifano mwafaka.

3.Silabisha maneno haya:

 Ofisi

 Dawati

 Akustikia

4.Huku ukiambatisha mifano mwafaka bainisha aina tano za silabi ya kiswahili

Marejeleo

Hyman,L.M(1975).Phonolgy:Theory &Anaysis.Newyork:HRW

Lass,R.(1984).Phonolgy:Introduction to Basic Concepts.Cambridge:Cambridge University

Press.

Mbugua,A.N.(1990).A Phonology Reality of The Syllable.M.A.Thesis:K.U

45
46
SOMO LA TANO

ARUDHI YA SAUTI
Utangulizi

Katika somo lililotangulia tuliweza kuangazia ruwaza na mahusiano ya sauti,katika somo hili

tutaangazia arudhi ya sauti inavyojitokeza katika vipashio vilivyozidi foni.

 Shabaha

Kufikia mwisho wa somo hili,uweze:

 Kutathmini mitazamo ya arudhi

 Kudhihirisha uamilifu wa sifa arudhi

 Kuonyesha mahusiano ya maumbo ya arudhi

Maana ya arudhi sauti

Arudhi sauti husimamia muundo,maumbo na mahusiano mwafaka wa vipashio vya sauti

vilivyozidi foni,haya huangaliwa kupitia arudhi maumbo na arudhi sifa.

Arudhi maumbo

Huhusisha vipashio vikubwa kuliko foni,vipashio hivi ni vitatu:silabi,neno na kirai.

Arudhi maumbo huzingatia jinsi vipashio hivi hujengwa.kwa mfano husisitiza kuwa silabi ni

kiungo cha neno na pia kiungo cha kirai tonishi.

47
Nayo neno licha ya kuwa kiungo chake ni silabi,inafasiriwa kuwa kipashio kinachojisimamia

katika sentensi,kwa mfano

Sentensi :Baba anapika chakula.-sentensi hii yetu imeundwa kwa maneno matatu:#baba#

#anapika# #chakula#.ambayo yanajisimamia na yanaowakilisha maana Fulani ya kileksia.

Maneno katika sentensi huwa yameundwa kwa silabi tofauti kwa mfano mengine yameundwa

kwa silabi moja,mbili,tatu au nne.

Umbo la neno hurejelea idadi ya silabi wala sio foni manake silabi kamili ni rahisi kutamka na

kubainisha kuliko kubainisha foni.

Mfano maneno yetu:

a)#juu# $ju:$

b)#sema# $S)ma$

c)#usomaji# $u$ so $ ma$ ji

Maumbo haya ya maneno huwakilishwa kwa michoro matawi.michoro hii inaonyesha moja kwa

moja uhusiano wa umbo la neno(NE) na idadi ya silabi(SI)

A) NE

(NE)--------Ni neno

SI (SI)……..Ni silabi

48
Ju:

B) NE

SI SI Neno soma limuundwa kwa silabi mbili kama inavyodhohorika.

So ma

C) NE

SI SI SI SI

U so ma ji

Kirai tonishi

49
Ni mfululizo wa usemi wenye mawimbi bayana ya sauti.Mawimbi haya ya sauti hujengwa

kupitia kwa kidatu cha sauti.kidatu cha sauti ni kule kupaa kwa silabi moja ikilinganishwa na

nyingine ambata.

Mfano kauli “kingereza ni lugha ya silabi ngumu”,Kauli hii ina virai viwili ambavyo ni:

a)kingereza ni lugha

b)ya silabi ngumu

kirai cha kwanza(kingereza ni lugha) kina silabi saba ilhali kirai cha pili(ya silabi ngumu)ina

silabi sita.

[ki $ nge $ re $za $ ni$ lu $ gha ] [ya$ si $ la $ bi $ngu $mu]

Ni wazi kuwa umbo la kirai linabainika kupitia idadi ya silabi.Mahusiano kati ya

silabi(SI),kirai(KI)) na kauli(KA)kamilifu yaweza kuwakilishwa kimchoro ifuatavyo:

KA

KI KI

50
SI SI SI SI SI SI SI SI SI SI SI SI SI

Ki nge re za ni lu gha ya si la bi ngu mu

Kwa jumla siabi ni msingi wa arudhi maumbo na pia arudhi sifa.

Arudhi sifa

Arudhi sifa ni sura ambazo hutumika kutofautisha maumbo linganifu kimuundo au

kiwamilifu.Sifa arudhi kimatumizi hurejelea umbo la silabi.

Arudhi sifa huwa na sifa za kimsingi tatu:

 Wakaa wa sauti

 Kidatu cha sauti

 Shadda ya sauti

1.Wakaa wa sauti

Wakaa husimamia wingi wa muda wa matamshi ya silabi moja ulio tofauti na umbo lingine

linganifu kimuundo.

Wakaa wa sauti huonyeshwa kwa kutumia nukta mbili[:] kwa mfano neno

Juu -----ju: nukta mbili mwisho wa silabi u inashiria kuwa ni wakaa.

Kuna aina mbili kuu za wakaa

51
 Wakaa fonetiki

 Wakaa leksia

Wakaa fonetiki

Wakaa fonetiki ni kikwazo cha matamshi sahihi.

Mfano

#kondoo# ko$ ndo:

#paa# pa:

Wakaa leksia

Wakaa leksia hubainisha maana za kimsingi.

Kwa mfano katika maneno

a)#mchuzi# na #mchuuzi#

b)#bidi# na #bidii#

maana ya maneno haya huwakilisha dhana tofauti kileksia,tukizibaini zitakuwa:

#mchuzi# [mcuzi]

#mchuuzi# [mcu:zi]

#bidi# [bidi}

#bidii# [bidi:]

52
Wakaa huzingatia hoja kwa muda wa kutamka sauti moja,muda mfupi unaotumika huitwa mora.

Mora moja huweza kukadria muda wa kutamka vokali sahihi kama vile [a],[e] nakadhalika au

mseto wa konsonanti na vokali kama vile [ba] na [ma]

2.Kidatu Cha Sauti

Kidatu ni hali ya kupaa kwa silabi moja ikilinganishwa na nyingine ambata.au yaweza

kufasiriwa kuwa ni ile hali ya kupanda au kushuka kwa sauti wakati wa matamshi.

Kwa mfano unapotamka neno #mwashi#

Neno hili#mwashi# limeundwa kwa silabi mbili-----mwa$ shi

Katika kutamka silabi -mwa sauti huwa inapanda ilhali ukitamka silabi -shi sauti huwa inashuka

Kushuka au kupanda huku kwa sauti hutegemea mtetemo wa nyuzi za sauti ndani ya glota.

Mtetemo huu huweza kuzua vidatuu vya aina tatu:

 Kidatu cha juu(JU)

 Kidatu cha kati(KA)

 Kidatu chachini(CH)

Zoezi

Tamka maneno haya:

 ukucha

 lala

53
 mwaki

Bainisha kidatu cha kila silabi,kutegemea ulivyotamka

Matumizi ya kidatu huwa imegawika katika daraja mbili:

 Toni

 Tonisho

Toni

Toni ni daraja ya kidatu ambayo huhusika na maneno,toni hii yaweza kuwa toni fonetiki au toni

ya kileksia.

Toni fonetiki huzingatia matamshi sahihi,ambayo yaweza kuwa toni sahili au toni mseto.Toni

sahili huenda sawa na idadi ya silabi katika neno,hii ni kusema kuwa idadi ya toni na ile ya silabi

katika neno huwa sawa.

kwa mfano katika neno #baba# idadi ya silabi ni mbili sawia na idadi ya toni ambazo ni mbili.

Silabi: ba $ ba

Toni: KA KA

Neno letu #baba# limeundwa na silabi mbili,limeundwa na toni mbili ambazo ni za kidatu cha

kati(KA)

54
ZOEZI

Bainisha maneno matano,kisha

ubainishe idadi ya silabi na idadi ya

toni katika maneno hayo.

Toni mseto hujumuisha ufululizo wa upinde wa viwango viwili au zaidi vya kidatu katika silabi

moja.upinde wa toni hudhihirika katika maneno ya silabi moja.

Tonimu

Ni ruwaza za toni bainifu,lugha moja huenda ikawa na tonimu zaidi ya mbili au nne.Tonimu ndo

hutumika kubainisha toni leksia.

Mfano umbo la Kiswahili #paka#

Neno tonimu maana

Paka CHJU mnayama

Paka KAKA kitenzi

Umbo la kikuyu #iria#

Neno tonimu maana

Iria CHJU maziwa

55
Iria JUCH ziwa

Iria JUJU zile

Iria CHCH zile

Lugha nyingi hutumia kidatu cha juu na chini,ni baadhi ya lugha tu hutumia vidatu vyote vitatu.

Tonisho

Jina lingine la tonisho ni kiimbo,huweza kutumiwa kusimamia ruwaza ya kidatu cha daraja ya

kirai.

Watu wanapozungumza ,matamshi yao hutegemea hali zao au maumbile yao na yale

wanayozungumzia.k.m mtu akizungumza akiwa na furaha ,matamshi yake yatukwa tofauti na

wakati akiwa na huzuni,vivyo hivyo iwapo anatoa maelezo ,matamshi yake yatakuwa tofautu na

anapouliza swali k.m

a)Amefika?

B)Amefika.

c)Amefika!

Katika mfano huu wetu tukianiisha kutumia aina ya kidatu tutapata:

Kauli tonisho maana

Amefika KA JU KA CH arifa ya kawaida

56
Amefika? KA CH KA JU swali la kawaida

Amefika! CH CH JU JU mshangao

3.Shadda Ya Sauti

Shadda ni mkazo mzito wa silabi moja ikilinganishwa na nyingine yenye umbo sawa .Hii ni sifa

inayoshughulikia namna watu huongeza nguvu katika baadhi ya sauti za maneno na ukali ilhali

nyingine ambazo hazikutiliwa huwa hafifu.

Baadhi ya maneno hubadilisha maana kutegemea sehemu ya sauti inayotiliwa mkazo kwa mfano

neno barabara likitamkwa kwa kutilia mkazo(bar-r-abara) yaani sawasawa lina maana tofauti na

unapotamka barabara(bila mkazo mahali popote)-yaani njia.

Kiwango cha uzito wa shadda hutegemea wingi wa nguvu za hewa inavyosukumwa kutoka

mapafuni hadi kooni.

Lugha nyingi hugawa shadda katika viwango viwili:

 Shadda neno

 Shadda silabi

Mfano katika neno #barabara# hamna mkazo ambao hutuliwa katika kutamka hivyo maana kuwa

ni njia

#bar-a-bar-a# katika mfano huu mkazo umetiliwa katika silabi hivyo basi maana kubadilika na

kuashiria (sawa)

57
Baadhi ya lugha hudhirisha daraja zingine mbili za shadda:

 Shadda nzito

 Shadda hafifu

Shadda nzito huwakilishwa kwa ritifaa ya juu(‘) mfano neno ng’ombe shadda nzito ni ng’

Shadda hafifu huwakilishwa kwa ritifaa ya chini(,).

Njia mwafaka inayotumika kuashiria shadda ni uwakilishi kigridi unaotumia alama ya

makasi(x),inayowekwa juu ya kilele cha kila silabi.

Viwango vingine vya shadda huonyeshwa kwa kuongeza alama(x) juu ya ile ya silabi.

Kwa mfano “kingereza ni lugha ya silabi ngumu”

Shadda nzito x x x

Shadda silabi x x x x x x x x x x x x x

Kauli :ki nge re za ni lu gha ya si la bi ngu mu

Ikumbukwe kuwa.

Shadda nzito huashiriwa kwa ritifaa ya juu ilhali

shadda hafifu huashiriwa kwa ritifaa ya chini

Uamilifu wa shadda unategemea aina za shadda neno(shadda nzito)ambazo hutumika katika

lugha kwa ujumla.

Aina ingine ya kubainisha shadda ni:

58
 Shadda tuli

 Shadda huru

Shadda tuli hubaki au kutua kwa silabi bayana licha ya urefu wa umbo la neno.huweza kuelezwa

kwa kifupi kwa kutumia sheria ya kijumla inayosema shadaa(SHA) huwekewa silabi(SI) ya pili

kutoka mwisho wa neno.

SI [+SHA] /-SI#

Shadda tuli hujulikana kama shadda fonetiki kwani hutawaliwa na kanuni za matamshi pekee.

Shadda huru huwekewa silabi tofauti za maneno,kutegemea vikwazo vya kisarufi.s

Kwa mfano maneno ya kiingereza #ma’chine# na #mashine#

Shadda nzito:x

Shadda silabi:xx

Umbo –neno:ma Ši:n

Shadda huru huweza kutumika kileksia ambapo ruwaza za shadda hubainisha maana za

kimsingi.mfano

Maneno #invalid# na #content# ya kingereza.

Shadda nzito:x x x x

Shadda silabi:xxx xxx xx xx

59
Umbo-neno:in valid in vaelid kon tent kan tent

Maana : mgonjwa haramu yaliyomo kuridhika

Ni bayana kuwa ruwaza ya shadda huleta tofauti za kimofolojia pia kwa mfano katika neno la

kingereza.#research# laweza kurejela kutafiti-kitenzi au utafiti-nomino.

Shadda nzito:x x

Shadda silabi:xx xx

Umbo-neno:ri S3:c re s3:c

Aina-neno: tenzi nomino

Muhtasari

Katika somo hili tumeweza kuangazia maana ya arudhi ya sauti,mitazamo yake,sifa za arudhi za

wakaa,kidatu na shadda.katika somo letu la mwisho linalofuatia tutaangazia mageuko ya sauti.

Zoezi

1.Fafanua maana ya arudhi sauti.

2.Bainisha dhana zifuatazo kwa kutoa mifano mwafaka

 Wakaa wa sauti

 Kidatu cha sauti

 Shadda ya sauti.

60
Marejeleo

Clark,J. & Yallop,C/(1990).An Introduction to Phonetics and Phonolgy.Oxford:Blackwell.

Hyman,L.M(1975).Phonolgy:Theory &Anaysis.Newyork:HRW

Schane,S.(1973).Generative Phonology.Englewood Cliffs,N.J:Prentice Hall,Inc

Sloat,C(1978).Introduction to Phonolgy.Englewood Cliffs,N.J:Prentice Hall,Inc

61
SOMO LA SITA

MAGEUKO YA SAUTI
Utangulizi

Katika masomo yote yalotangulia tuliangazia sauti za lugha,sifa za sauti hizi za lugha,ruwaza ya

sauti na arudhi ya sauti,katika somo hili tutangazia mageuko ya sauti kwani sauti huenda

ikageuka kulingana na vigezo kadha kama tutakavyoangazi

 Shabaha

Kufikia mwisho wa somo,uweze:

 Kufafanua maana ya mageuko ya sauti

 Kutathmini aina tano ya mageuko ya sauti

 Kuonyesha mageuko haya kwa kutumia michoro

 Kufafanua umuhimu wa mageuko ya sauti

Maana Ya Mageuko Ya Sauti

Mageuko ya sauti ni ubadiliko wa muundo wa sauti katika neno moja likilinganishwa na hali

katika umbo asilia au matumizi ya kimsingi zaidi

Kwa mfano neno#afya# huweza kutamkwa na wengine kama #afia#

Katika mfano huu wetu y imegeuka na kuwa i

Y i

62
Kuna mageuko ya kihistoria na mageuko ya muda wa usemi

Mageuko haya ya sauti huweza kusababishwa na mambo kama:

 Aina ya sauti kwa aina nyingine

 Athari ya sauti moja kwa nyingine

 Vikwazo vya ruwaza ya sauti moja katika maumbo ya silabi na hata maneno

Mageuko ya sauti hutegemea kanuni Fulani za matumizi ya lugha husika kwa ujumla.kanuni hizi

hushirikiana na ishara maalumu ambazo huweza kubainisha mageuko haya pamoja na mazingira

ya mageuko haya.

Kwa mfano vokali[u] ambayo inapatikana katika sehemu ya juu nyuma huweza kuyeyuka na

kuwa [w]

Kwa mfano neno#mwaka#

Vokali [u] huweza kugeuka na kuwa Konsonanti[w] katika mazingira ya [a]

U w / -a

Ugeuko wa aina huu hutokea wakati tunapofululiza matamshi.

Mageuko ya sauti huweza kuwekwa katika viwango/vikundi vitano vikuu:

 Muungano wa sauti

 Udodonsho wa sauti

 Uchopeko wa sauti

 Usigano wa sauti

 Usimilisho wa sauti

63
1.Muungano wa sauti

Ni aina ya mageuko ya sauti ambayo huwa ni mseto wa sauti mbili ambazo huungana kuunda

sauti moja tofauti.

Sauti hii mpya iloundwa hushirikisha sifa toka kila moja ya sauti asilia.

Kwa mfano vokali ya chini[a] huungana na ya juu mbele[i] kuunda vokali ya kati mbele[e]

a+i e

mifano ya maneno

/wa+izi [wezi]

/wa+ingi [wengi]

/ma+iko [meko]

Muungano wa vokali hizi mbili ni mseto wa sifa.sifa za chini(CH) na juu(JU) kabisa au juu-

kati,hufumana ili kuunda vokali ya kati(KA)

64
ZOEZI

Tathmini vokali zingine za lugha ya

Kiswahili ambazo huungana ili kuunda

sauti moja.

2.Udondosho Wa Sauti

Hii ni aina ya mageuko ya sauti ambapo sauti au silabi hutoweka katika muundo Fulani wa

kipashio cha lugha kulingana na umbo zaidi asilia.

Utowekaji huu hutokea wakati wa matamshi.

kwa mfano

a) Vokali [a] inapotumika katika tamati ya neno tangulizi na pia awali ya neno ambata,husikika

kutoweka wakati wa usemi

/wataka#aje/ [watakaje]

/dada#amefika/ [dadamefika]

ZOEZI

Tathmini maneno mengine yenye

kudhihirisha kielezo hiki cha

udondosho.

65
B)Udondosho wa silabi

Udodonsho wa silabi huweza kudhirika katika lugha ya Kiswahili ambapo baadhi ya kauli

huweza kudodonsha silabi ya kwanza katika neno la pili.

Kwa mfano:

/Mbwa#wangu/ mbwangu

/Kaka#yangu/ kakangu

/Shangazi#yao/ shangazio

ZOEZI

Tathmini maneno mengine yenye

kudhihirisha kielezo hiki cha udondosho

C)Udondosho wa vimilikishi

Udodonsho wa vimilikishi huweza kutokea katika lugha ya Kiswahili ambapo vokali ya

kiambishi hudondoshwa kama ifuatavyo:

/ja+aŋgu/ [jangu]

/li+akƐ/ [lakƐ]

/ja+Ɛtu/ [jƐtu]

/pa+akƐ/ [pakƐ]

66
Kuna baadhi ya mgeuko unaohusu utohozi wa mikopo,kwa mfano lugha ya kidholuo inapokopa

maneno kutoka kwa lugha ya Kiswahili na kuyatohoa,vokali tamati ya neno hudondoshwa.kwa

mfano

Kiswahili kidholuo

Kitabu kita:b

Kalamu kala:m

3)Uchopeko Wa Sauti

Uchopeko wa sauti hurejelea hali ya kuingiza sauti katika umbo asilia au kauli ya kimsingi zaidi.

Kwa mfano badala ya kutamka neno #fua# utapata msemaji ameongeza silabi $w$ na hivyo

kuishia kulitamka [fuwa].Huu ndio unaitwa uchopeko wa sauti.

Mifano zaidi

[kua] [kuwa]

[arusi] [harusi]

[lia] [liya]

Uchopeko huweza kutokea katika uambishi wa nomino na vitenzi ambazo huchopeka sauti

katika aina tatu za mazingira ya neno:awali.ndani na tamati.

Kwa mfano tukirejelea lugha ya Kiswahili,Kiswahili sanifu huchopeka vokali ya juu[i] ndani ya

neno la umoja ili kuunda umbo la wingi.

67
Mfano

Mtaro mitaro

Mti miti

Mstari mistari

Mageuko haya hubainisha majina ya ngeli za {M}-{MI}kama ilivyodhihirika katika mifano

yetu.

Utohozi wa mikopo unaweza kuchopeka silabi kamili kwa mfano lahaja ya kimaasai,huchopeka

silabi kamili yenye kurejelea umbo la $VK$

Mfano:

Kiswahili kimaasai

Birika Ɛmbirika

Kikombe Ɛŋkikombe

Utohozi wa mikopo ya Kiswahili kutoka kingereza huchopeka vokali ndani ya tamati ya neno

kama ifutavyo:

Kingereza kiswahili

Card kadi

Hospital hospitali

Office ofisi

68
Kila mazingira ya uchopeko inahusu sauti ya konsonanti.

Ǿ V / K-

4.Usigano wa sauti

Haya ni mageuko yanayozidi kutofautisha muundo wa sauti mbili.Usigano huu hudhihirika

kupitia uyeyusho wa vokali katika baadhi ya lugha.

Mfano vokali za juu katika lugha ya kiswahili [i],[e],[u] na [o] huweza kuyeyuka na kuwa [j] au

[w]ikitangulia vokali ya chini au ya kati.

Mfano #mwaka#,#mwili# na #afya#

A) u+v-------------w:

/mu+aka/ [mwaka]

/mu+ili/ [mwili]

b) i+v----------------j:

/afi+a/ [afyia]

/Vi+ama/ [vyama]

Uyeyusho huu wa vokali hutokea sawia na umilisho wa kiyeyusho kwa konsonanti ambata na

matokeo yake huwa ni konsonanti changamano.

69
Usigano mwingi hudhihirika vyema katika lugha ya kikuyu. Kwa mfano katika mazingira ya

vikwamizo sighuna[-GH] vya ulimi na paa la kinywa,kiambishi {ko} hugeuka na kuwa [yo],

Mageuko haya huhusu vikwamizo vine:[ø],[t],[Š] na[k]:

a)ko yo/Ǿ:

ko+Ɵama yoƟama ‘kuhama’

ko+Ɵŋga yoƟŋiga ‘kuziba’

b)ko yo/-t:

ko+tara yotara ‘kuhesabu’

ko+tinda yotinda ‘kukawai

c)ko yo/-Š:

ko+Šaria yoŠaria ‘kutafuta’

ko+Šinda yoŠinda ‘kushinda’

d)ko yo/-k:

ko+kima yokima ‘kuponda’

ko+kama yokama ‘kukama’

5.Usilimisho Wa Sauti

70
Aina hii ya mgeuko hueleza athari za sauti moja kwa nyingine zinazoleta ukuruba zaidi wa

kimuundo,Hii ni kusema kuwa sauti husilimisha mojawapo ya mambo mawili:

 Pahala pa kutamka

 Jinsi ya kutamka

Usilimisho huweza kubainika kwa kutegemea mazingira ya sauti inayosilimishwa,usilimisho

huweza kuwa wa aina mbili:

 Usilimisho tangulizi

 Usilimisho fuatilizi

Usilimisho Tangulizi

Usimilisho tangulizi wa pahala pa kutamkia hutokea kwa wingi pale ambapo sauti ya nazali

inaambata kikwamizo hivyo sauti ya nazali husilimishwa na kufanywa kuchukua umbo la nazali

ya pahala pa kutamkia.

Kanuni ni: N N / -K

[+PA] [+PA]

Vikwamizo vya Kiswahili [b],[d],[g] na [j] huaminika kuwa msingi wa nazalishi awali

linganifu:[mb],[nd],[ŋg] na[nj].

71
Mofimu {n}huweza kuchukua umbo la nazali ya pahali pa kutamkia kikwamizo kinachotumika

mwanzoni mwa shina.

Mfano

/N+buzi/ [mbuzi]

/N+dovu/ [ndovu]

/N+gazi/ [ngazi

Katika lugha ya kingereza usilimisho unadhihirika katika ukanusho,mojawapo wa vikanushi{il}

huweza kusilimisha maneno yanayoanza na sauti [l] na kuyafanya yawe katika hali ya

ukanusho,kwa mfano:

Literate illiterate(asiyesoma)

Legible illegible(isiyosomeka0

Legal illegal(haramu)

Iwapo sauti ya awali ya shina ni [r] basi usimilisho wa [l] hugeuka kuwa [r]

il ir /r:

il+relevant irrelevant

il+religious irreligious

il+regular irregular

72
Usimilisho tangulizi wa vokali hutokea katika lugha ya Kiswahili katika wingi wa vitenzi

vyake.kwa mfano katika umoja kitenzi huwa kinamalizia kwa vokali ya chini[a],lakini

inapokuwa katika hali ya wingi huweza kuchopeka mofimu{ni}ivo basi kufanya kiishio {a}

kuwa {Ɛ}

Mfano :

Umoja kitenzi wingi wa kitenzi

/Andika+ni/ [andikeni]

/pika+ni/ [pikeni]

/fua+ni/ [fueni]

/Soma+ni [someni]

Kutokana na mifano hii yetu ni bayana kuwa vokali ya juu[i] inasilimisha ile ya chini[a] na

kuigeuza kuwa vokali[Ɛ] ambayo ni ya kati.Hii ni kudhihirisha kuwa vokali ya chini hugeuzwa

kuwa ya kati katika mazingira ya vokali ya juu.

V V/ -V

[CH] [KA] [JU]

Muhtasari

73
Katika somo hili tumweza kubaini mgeuko wa sauti na tukaweza kubaini aina tano ya

mageuko,muungano,usilimisho,udondosho,usigano na uchopeko wa sauti.Kila aina mgeuko

umefafanulia wazi.

Zoezi

1.Eleza mifanyiko hii ya kifonolojia na utolee mifano mwafaka:

 Muungano wa sauti

 Kudondoshwa kwa sauti

 Uchopeko wa sauti

 Usigano wa sauti

 Usilimisho wa sauti

2.Mageuko ya sauti inabainika katika viwango vitatu,tathmini viwango hivi.

74
Marejeleo

Hock,H.H(1986).Principles in Historical Linguistic.Berlin:Mouton de Gruyter.

Kenstowics,M. & Kisseberth C.(1977).Topics in Phonological Theory.Newyork:AP

Mwihaki,A.(1998).Loanword Nativization:A Phonological Adaption of Gikuyu

Loanwords.Ph.D.Thesis:Kenyatta University.

Schanes,S.(1973).Generative Phonology.Englewood Cliffs,N.J:Prentice Hall,Inc.

Sloat,C.(1978).Introduction to Phonology.Englewood Cliffs,N.J:Prentice Hall,Inc.

75

You might also like