Professional Documents
Culture Documents
Majukumu ya kupanga
Moshe Nahir (1977) anapendekeza kwamba upangaji wa lugha una majukumu
matano bainifu.
(i) Uchujaji na utakaso wa lugha (Language purification). Kueleza matumizi
sahihi na kuhifadhi usafi wa lugha. (Korean language (1949) Maneno
mkopo ‘hanja’ Korea waliondoa maneno ya kijapani na kuyafanya
Kiswahili sanifu.)
(ii) Ufufuaji lugha, hasa lugha ya kale na kuweka katika hadhi yake ya
zamani. Uhaishaji wa lugha iliyokufa. (Hebrew language 1980-1914).
(iii) Ugeuzaji na urekebishaji lugha (Language reform) kuwezesha
matumizi ya lugha kupitia usahihishaji au urahisishaji wa msamiati na
tahajia yake.
(iv) Usanifishaji kuwa lugha (Standardisation). Kuhakikisha kuwa lugha
moja au lahaja moja katika eneo au taifa fulani inakubaliwa kama lugha
kuu.
(v) Uingizaji usasa au upya wa msamiati (Lexicomodernisation). Kujaza
pengo kati ya msamiati wa lugha na istilahi mpya zinazotokana na
teknolojia ya kisasa.
2
(a) Upangaji Lugha Kifahari (Prestige Planning). Upangaji lugha kifahari
hulenga katika kutoa mielekeo chanya ya kisaikolojia ambayo ni
muhimu ikiwa kutakuwepo na ufanisi wa muda mrefu katika upangaji
lugha; mfano mzuri ni fahari kuu ambayo Kiebrania kilikuwa nayo kama
lugha ya kidini ilisababisha kutokuwepo na haja ya kuwa na upangaji
kifahari. Upangaji kifahari huwa muhimu pale ambapo lugha ambayo
imeteuliwa ilikuwa ya hadhi ya chini (kama ilivyo katika diglosia). Ili
watu wakubali hadhi ya lugha hiyo iliyotwazwa, kuna haja ya kuboresha
na kuendeleza ufahari wa lugha hiyo. Hivyo basi, upangaji kifahari
aghalabu hutangulia upangaji kihadhi.
(b) Upangaji Lugha Kiurithi (Acquisition Planning). Hizi ni juhudi za
kusambaza ujifunzaji wa lugha. Hapa tunaona taasisi za kitamaduni
zinazosambaza na kuendeleza lugha mbalimbali. Kwa mfano, Britishi
Council, French Cultural Center, Japanese Cultural Center na
kadhalika. Taasisi hizi hutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa walimu
wanaofundisha lugha hizi.
(c) Upangaji Lugha Kihadhi (Status Planning). Upangaji huu hurejelea utoaji
wa dhima kwa lugha (kama vile kutumia lugha hiyo kufunzia shuleni au
kama lugha rasmi). Jambo hili huathiri dhima ya lugha katika jamii.
Kwa mfano, uamuzi wa kutumia Kiebrania kama lugha ya mafunzo
katika shule za Wayahudi kule Palestine. Kabla ya hapo, Kiebrania
hakikuwa kikitumiwa katika mawasiliano ya kila siku ila katika maombi
na maandishi ya kidini na kiusomi. Hadhi ya Kiswahili nchini Kenya
imeinuliwa kwa njia hiyo, matumizi ya Kiingereza nchini Rwanda,
Kiswahili nchini Tanzania na Uganda.
(d) Upangaji Lugha Kiukongoo (Corpus Planning). Kongoo ni kusanyiko la
data za semi zilizoandikwa au kunukuliwa ambazo hutumiwa kama
kianzio cha ufafanuzi wa kiisimu. Upangaji lugha kiukongoo unahusika
na muundo wa ndani wa lugha. Mambo yanayozingatiwa ni pamoja na
kuunda othografia kwa lugha ambazo bado hazijaandikwa, kuanzisha
3
mabadiliko katika tahajia, kubuni maneno mapya na kuchapisha vitabu
vya sarufi. Jambo la kimsingi katika aina hii ya upangaji lugha ni
usanifishaji wa lugha. Huu hueleweka kuwa ni uanzishaji na uendelezaji
wa kaida za kiisimu.
Majukumu ya Lugha katika Jamii
(i) Lugha rasmi hutumiwa katika miktadha ya kitaifa na inaunganisha
watu kisiasa na kitamaduni. Aghalabu hadhi hii huwa imetangazwa
kwenye katiba.
(ii) Mawasiliano mapana; matumizi ya lugha kama chombo cha
mawasiliano kinachovuka mipaka ya lugha mbalimbali katika nchi
moja. Hii ni kama lingua franka; kwa mfano Kiswahili nchini
Tanzania, Kihindi, Kiingereza n.k.
(iii) Mawasiliano ya kimataifa (Lugha ya Kimataifa); kwa mfano
Kiingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kiarabu, n.k.
(iv) Kuendeleza elimu; katika shule na taasisi za elimu.
(v) Dini
(vi) Vyombo vya habari
(vii) Kazini
(viii) Fasihi
Mchakato wa Upangaji Lugha
Haugen (1966, 1972, 1987) alisema kuwa mchakato wa upangaji lugha unazo
hatua nne ambazo zinaweza (ingawa si lazima) kufuatana;
1. Uteuzi (Selection)
2. Ukuzaji msimbo (Codification)
3. Utekelezaji (Implementation)
4. Upanuzi (Elaboration)
Uteuzi
Upangaji lugha huanza kukiwepo na uwezekano wa kuchagua moja kati ya
vibadala vingi vya kiisimu. Uteuzi huu utatokea baada ya watu kutambua
kwamba kuna shida fulani ya kiisimu. Basi lahaja au lugha moja kati ya zile
4
zinazotumika katika jamii husika huchaguliwa kuwa msingi wa usanifishaji.
Uteuzi ni ule uchaguzi wa lugha au lahaja ili ipewe dhima fulani katika jamii;
kwa mfano iwe rasmi, ya kufunzia, ya dini, n.k. Hii ina maana kwamba lugha
au lahaja ya fahari zaidi ndiyo inayochaguliwa. Uchaguzi unazingatia
umuhimu wa lahaja hiyo kijamii, kisiasa, kibiashara, kielimu, n.k.
Uteuzi huu unaweza kutanguliwa na mijadala mikali kati ya watu hadi pale
wanapokubaliana, au wanaweza kuamuliwa na viongozi K.mf uteuzi wa hijai
ya Kituruki kutoka kwa Kiarabu hadi Kiroma. Uteuzi huu hutekelezwa na jamii
kupitia kwa viongozi wao na wanaohusika katika uteuzi huu si taasisi za
serikali bali ni watu binafsi, vikundi kama makanisa, vyama vya kisiasa, mikoa
na nchi yote.
Ukuzaji Msimbo
Sehemu hii hutekelezwa na wanaisimu au wataalamu wa lugha. Lahaja
iliyoteuliwa huwekewa kanuni au utaratibu za matumizi. Huku ni kukuza
mfumo wa lugha hiyo k.v fonolojia (othografia na matamshi), sarufi, msamiati
na maana.
Ukuzaji msimbo ni uundaji wa kiwangogezi (norm or standard) cha kiisimu
kwa msimbo fulani wa kiisimu. Shughuli hii hufanywa kupitia kwa hatua
zifuatazo;
5
(a) Kukuza mfumo wa maandishi (graphisation)
(b) Usarufishaji (grammatication)
(c) Uleksikishaji (lexicalilsation)
Kukuza mfumo wa maandishi. Ikiwa lugha husika ilikkua ya mikazungumzo
tu, basi inatayarishiwa mfumo wa maandishi. Wakati mwingine
kinachofanyika ni kwamba wataalamu wanakopa mfumo wa kimaandishi wa
lugha nyingine. Wataalamu wanamua mfumo wa maandishi utakaoifaa lugha
hiyo. Ni ule wenye msingi wa sauti (vokali na konsonanti), silabi au maneno?
Kwa mfano lugha ya Kiswahili kwanza iliandikwa kwa herufi za Kiarabu kabla
ya kutumia zile za Kirumi.
Usarufishaji. Hii ni sehemu nyingine ya mchakato wa upangaji lugha. Inahusu
kuunda kanuni za kisarufi. Wanaamua maumbo na miundo ambayo itakuwa
sanifu. Hali hii hupunguza vibadala au tofauti katika matumizi ya kisarufi.
Vitabu vya sarufi hutayarishwa.
Uleksikishaji. Hurejelea uchaguzi na utayarishaji wa msamiati unaofaa.
Kimsingi, hatua hii inahusu kuamua maneno fulani yatumiwe katika mitindo
ipi. Mara nyingi, uleksikishaji hushughulikia uondoaji wa maneno yenye asili
ya kigeni kutoka kwa lugha. Kamuzi za lugha hiyo hutayarishwa kama
ilivyokuwa wakati Kihindi kiliposanifishwa kwa kutumia maneno ya mkopo
kutoka Kiajemi, Kiingereza, n.k.
Utekelezaji
Utekelezaji unahusisha shughuli za waandishi, taasisi, na serikali katika
kuitumia na kuisambaza lugha ambayo imeteuliwa na kukuziwa msimbo. Hili
linafanyika kwa kutoa au kuchapisha vitabu, majarida, magazeti, na makala
katika lugha hiyo iliyokuziwa msimbo. Wenye mamlaka huhakikisha kwamba
lugha hii inatumiwa pia kwenye vyombo vya habari kama redio, televisheni na
magazeti.
Huku wanaisimu wakihusika sana na sehemu ya ukuzaji msimbo, sehemu hii
ya utekelezaji hushughulikiwa na dola/taifa. Inabidi kuwepo na mbinu za
6
kibiashara za kusambaza lugha hii. Waaandishi wanachapisha vitabu kwa
lahaja hii sanifu wanatuzwa, wafanyakazi serikalini wanaoifahamu lahaja hii
sanifu wanapandishwa vyeo kazini, na lugha au lahaja hii inatangazwa sana.
Wakati mwingine kunawekwa sharia ambazo zinahimiza matumizi yake.
Upanuzi
Hii inarejelea ukuzaji wa istilahi na mitindo ili lugha iliyokuziwa msimbo
itemize mahitaji ya kisasa ya mawasiliano katika ulimwengu unaoendelea
kisayansi na kiteknolojia. Huku ni kuendelea tu na utekelezaji wa kiwangogezi
ili kutimiza dhima za lugha katika ulimwengu wa kisasa. Sehemu hii ya
upanuzi lugha ni hiyo ya kuunda na kusambaza istilahi mpya, na kuhakikisha
kuwa kuna mbinu mbalimbali za kuundia msamiati; hali hii inaweza
kukamilika kwa kukopa kutoka lugha zingine, kupanua maana ya istilahi, na
kubuni maneno mapya.
Upanuzi wa lugha huendelea kila wakati. Hii ni kwa sababu lugha inahitaji
kujengwa upya kila siku kwani kuna dhana na vyombo vipya vinavyojitokeza
7
kila siku. Kuna haja ya kuwa na taasisi za kushughulikia upanuzi wa
msamiati.
Lingua Franka
Lugha hii hutumiwa na watu walio na lugha tofauti kwa ajili ya mawasiliano.
Mfano mzuri ni Kiswahili ambayo ni lingua franka katika eneo la Afrika
Mashariki.
Sababu za kuzuka kwa Lingua Franka
Zipo sababu tofauti tofauti, ambapo kwa mujibu wa Iribemwangi (2011),
ametoa sababu zifuatazo:
Lingua Franka huibuka kwa sababu ya Hali ya kutaka ushirikiano.
Ushirikiano unaotafutwa kupitia Lingua Franka ni ule wa kisiasa, kibiashara,
kiutamaduni na kielimu. Mfano Tukirejelea Kiswahili, lugha hii imetumika
katika kujenga, kuendeleza na hata kudumisha uchumi, biashara na umoja
miongoni mwa watu wa Afrika Mashariki.
Aidha Lingua franka huzuka kutokanana kuleta umoja miongoni mwa
watumiaji wake. Hii humaanisha kuwa miongoni mwa watu walio na
utamaduni mbalimbali, lingua franka ndiyo inayotumika kuwaleta pamoja.
8
Vita, mfano kupitia vita lugha ya Kigiriki iliweza kuenezwa. Pia Kifaransa
kiliweza kuenea hasa enzi ya utawala wa Napoleon Bornaparte. Pia katika
lugha ya Kiyunani iliweza kuenea kupitia vita, ambapo tawala zilizoshindwa
zililazimika kutimia lugha ya mtawala wao mpya. Hivyo basi kupitia vita lingua
franka iliweza kuenea maeneo mbalimbali.
Biashara, kupitia njia hii lingua franka huwezwa kuenezwa . Mfano Lugha ya
Kiswahili na Kihausa zimeweza kuenea kutokana na dhima zao za Kibiashara.
Hivyo sio ajabu kupata watafiti kadhaa wakiziita Lingua franka kwa lugha za
biashara.
9
4. Hutumiwa na watu ambao lugha mame zao ni tofauti.
5. Ni lugha ya mawasiliano kati ya watu wenye lugha zaidi ya moja.
6. Yaweza kuwa lugha ya kwanza au ya pili ya mzungumzaji na kwa
wengine lugha ya kigeni.
Lugha ya Taifa
Pijini (Pidgin)
10
Hii ni lugha inayobuniwa na kutumiwa kwa mawasiliano baina ya watu ambao
lugha zao ni tofauti na hawana lugha moja wanayoielewa kwa pamoja.
Marejeo
11