You are on page 1of 85

B A K I SWAH I LI

OSW 1 3 1

1 : U t a ngulizi w a Lugha na I sim u

Malengo ya Jumla ya Somo

Madhumuni ya jumla ya somo hili ni kumwelewesha mwanafunzi anayetaka


kujifunza masomo ya isimu/Lughawia aweze kuielewa vizuri dhanna ya lugha na
isimu kwa ujumla. Maarifa ya somo hili ni msingi mkubwa kwa masomo mengine
ya isimu katika ngazi hii ya shahada ya mwanzo na ngazi nyengine zilizo juu
yake. Kwa kujifunza na kuhitimu kozi ya Utangulizi wa Lugha na isimu
mwanafunzi atakuwa tayari amepata maarifa ya awali yanayohusu kozi kadhaa
wa kadha za Kiswahili zilizo chini ya Tawi la Isimu. Kozi hii inaonekana kuwa
ndio chanzo na kitangulizi cha kozi za OSW 122- Historia ya Kiswahili na
Lahaja zake, OSW 221- Sarufi ya Kiswahili na Sintaksia, OSW 222-Fonetiki
na fonolojia, OSW 223- Mofolojia, OSW 321-Isimu jamii, OSW 322-Kunga za
Tafsiri na Semantikia na hata Elimu mtindo na Leksikografia ya Kiswahili.

MUHADHARA WA KWANZA
DHANNA YA ISIMU NA LUGHA
MALENGO YA MUHADHARA
Unatarajiwa mwishoni mwa muhadhara huu :-
(i) Uweze kufasili dhanna ya Lugha
(ii) Uweze kubaini tabia na sifa za Lugha za asili za mwanaadamu
iii) Uweze kuzibainisha waziwazi dhima za lugha.
iv) Uweze kubainisha umuhimu na kazi za Lugha.
v) Ubainishe waziwazi maana ya ujuzi wa lugha.
vi) Ufasili dhanna ya isimu na kuainisha matawi ya isimu.
1.0 Dhanna ya Isimu na Lugha

1.1 Maana ya Lugha


 Lugha ni mfumo wa sauti nasibu zinazotumiwa na watu wa jamii wenye
utamaduni unaofanana ili kuwasiliana.
 Lugha ni mfumo wa sauti nasibu zenye kubeba maana na zilizokubaliwa na
jamii ya watu ziendelee katika kuwasiliana.

1.2 Sifa za Lugha


 Lugha ni lazima umuhusu Mwanadamu
Kimsingi hakuna kiumbe kisichokuwa mwanaadamu (mtu) kinachoweza
kuzungumza Lugha. Lugha ni chombo maalumu wanachokitumia binaadamu kwa
lengo la mawasiliano.
 Sauti:
Lugha huambatana na sauti za binaadamu kutoka kinywani mwake. Binaadamu
lazima atamke jambo kwa kutoa sauti, zinazotamkwa kwa utaratibu maalumu
kutoka kwenye maalumu yaliyo ndani ya mwili wa mwanaadamu, ambayo
kiisimu huitwa ala za sauti.
 Lugha huzingatia utaratibu maalum;
Sauti za lugha yoyote huwa zimepangwa kwa kufuata utaratibu fulani unaokubaliwa
na jamii ya watu wanaotumia lugha inayohusika. Kwa maneno mengine, si kila sauti
itokayo kinywani mwa mwanaadamu kuwa ni lugha. Sauti za vilio vya watoto, hoi
hoi na vigeregere vya waliofurahi, vikohozi vya wagonjwa wa pumu na vifua,
vicheko, sauti za kupenga kamasi, pinja na kelele nyenginezo haziwezi kuitwa lugha.
Utaratibu huo maalumu unaofuatwa na lugha za wanaadamu huitwa sarufi.
 Lugha hufuata misingi ya fonimu
Wanaisimu wanakubaliana kwa ujumla kwamba fonimu ni sauti yenye uwezo wa
kuleta tofauti katika maana ikipachikwa katika neno la lugha husika. Dhana ya
fonimu inatarajiwa kuzungumziwa kwa kirefu sana katika muhadhara wa sabaa. Kwa
mfano baadhi ya fonimu za Kiswahili ni .
/a/, /e/, /i/, /o/, /u/, kama zinavyoweza kubadilisha maana katika maneno
yafuatayo:-
/tata/~ /teta/~/tita/~/tota/~ /tuta/.
/p/, /b/, /t/, /d/, /c/, /k/, /g/, /s/, /z/. kama zinavyoweza kubadilisha maana
katika maneno yafuatayo:-
pawa~ bawa~ tawa~ dawa~ chawa~ jawa~ kawa~ sawa~ zawa, n.k
 Lugha hufuata mpangilio wa vipashio unaoleta maana
Muundo wa Lugha huwa unafuata mpangilio wa vipashio vyake maalumu na
lazima vipashio hivyo vifahamike. Mpangilio wa vipashio huo huanza na
fonimu, neno ambalo huundwa kwa mkusanyiko wa silabi au muunganiko wa
mofimu mbalimbali, kirai, kishazi na sentensi.
 Lugha inajizalisha
Vipashio vinavyoiunda lugha husika huwa na sifa ya kuweza kunyumbulishwa ili
kupata maneno mapya. Kwa mfano vitenzi hunyambulishwa kwa kuongezwa
viambishi nz kwa hivyo, lugha hujiongezea maneno mapya. Kwa mfano tuangalie
mifano ifuatayo.

i) chez-a-------ku-chez-a-------ku-m-chez-a-------tu-li-m-chez-a.
ii) chez-e-a-------chez-ek-a----------chez-e-an-a-------chez-esh-a-------chez-w-a
iii) chez-esh-a- chez-esh-an-a- chez-esh-e-an-a
 Lugha husharabu
Lugha husharabu kwa maana ya kwamba huchukuwa maneno kutoka lugha
nyengine ili kujiongezea msamiati wake.Tabia hii inazisaidia sana Lugha
zinazokua.

1.3 Tabia za Lugha


 Lugha ina tabia ya kukua
Lugha hukua kadiri inavyoendelea kutumiwa na jamii. Kukua kwa Lugha
kuna vigezo kadhaa vinavyozingatiwa. Miongoni mwa vigezo hivyo ni
kubadilika na kuongezeka kwa msamiati wa Lugha hiyo. Maneno ya zamani
yanabadilika na maneno mapya yanaingia katika Lugha mbalimbali. Hii ni
kutokana na mahitaji ya umma au jamii katika harakati mbali mbali
yanayotokana na maendeleo ya ulimwengu kwenye njanja tofauti tofauti
zikewemo za kiuchumi, kisiasa, kisayansi na kiteknolojia.Tukichukua mfano
wa Lugha ya Kiswahili, tunagundua maneno mengi ambayo yameingia
kwenye Lugha hii kwa sababu kadhaa. Baadhi ya maneno ambayo sasa hivi
yanatumika katika Kiswahili ambayo miaka kama kumi nyuma hayakuwemo
katika Lugha ya Kiswahili ni pamoja na kasheshe, dingi, miundombinu,
mikakati,mdau, ngangari na mengi mengineyo. Kuongezeka kwa watumiaji
pia ni kigezo chengine kinachoashiria kukua kwa Lugha ambacho kinaenda
sambamba na kigezo cha kutanuka na kuongezeka maeneo ambapo lugha hiyo
inatumiwa.
 Lugha ina tabia ya kuathiri na kukubali kuathiriwa.

Lugha inaweza kuathiri na kuathiriwa na Lugha nyengine .Mfano lugha ya


Kiswahili imeathiriwa sana na Lugha za Kiarabu, Kiingereza na hata Lugha za
Kibantu. Yawezekana pia kwa kiasi fulani ikawa Kiswahili kimeziathiri
Lugha hizo. Mfano wa maneno yenye asili ya Kiarabu ambayo yameingia
katika Lugha ya Kiswahili ni kalamu, kitabu, daftari, adhadu, thawabu,
dhambi, dhahabu, sababu,aibu, laana, zina, dhima, wajibu, mahaba,sakafu,
karibu, tafadhali,nafsi, roho, safari, salamu, amali, tabia, sifa, n.k. Mfano wa
maneno yenye asili ya Kiingereza yaliyoingia katika Kiswahili ni buku, peni,
begi, kabati, rula, buti,bia,springi, stoo, skrubu ,n.k .Mfano wa maneno yenye
asili ya Lugha za Kibantu ni pamoja na ikulu kutoka lugha za Kigogo,
Kisukuma na Kinnyamwezi, bunge kutoka katika lugha za Kigogo, Kisambaa,
Kiha na Kiganda, ugiligili kutoka katika lugha ya Kinyakyusa, ngowela
kutoka katika lugha ya Kikaguru, Kitivo kutoka katika lugha Kipare na
Kisambaa, kivunge kutoka katika lugha ya Kipare, unga kutoka katika lugha
ya kizigua na misamiati mingi mingineyo kutoka lugha tofauti tofauti za
kibantu.
 Ubora wa lugha
Lugha zote ni bora. Hakuna lugha iliyo bora zaidi kuliko lugha nyengine. Ubora
wa lugha upo kwa wale wanaoitumia.
 Kujitosheleza
Kila lugha inajitosheleza kulingana na mahitaji ya jamii ambayo inatumia
lugha yenyewe katika kipindi husika cha maisha yake

1.4 Dhima za Lugha


 Ujumi: ujumi ni hali ya kutumia maneno ya lugha fulani kwa ufundi na ustadi
wa hali ya juu kwa lengo la kuburudisha na kuwavutia watu wengine. Baadhi
ya watu hutumia lugha kwa dhima hiyo, ili maksudi wasomaji au wasikilizaji
wao wavutike na kuburudishwa na Lugha hiyo. Maeneo yatumikamo lugha
yenye ujumi wa kiwango cha juu ni kwenye matangazo na kwenye fani ya
utunzi wa mashairi.
 Utambuzi: Ni hali ya kufikiria kwa makini, kukokotoa na kutoa majibu ya
maswali tofauti ndani ya ubongo. Chombo kikuu kitumikacho kutoa majibu
hayo ni lugha. Kutokana na muktadha huo tunaweza kusema kwamba lugha
hutumika kama chombo cha utambuzi.
 Hisia: ni fikra za ndani alizokuwa nazo kiumbe mwanaadamu. Tunapotaka
kuonyesha hisia zetu na vilevile kuwavuta wengine kwa maneno mazito
yanayoweza kumtoa msikilizaji machozi ya huzuni au ya furaha tunachagua
maneno makali yenye hisia.
 Kujielezea: Hali ya mtu kudhihirisha mambo mbalimbali aliyokuwa nayo
ndani ya moyo wake. Kwa mfano mtu anaposema nina furaha sana. Hapa mtu
anatowa msisitizo wa kuonyesha kiwango cha furaha alichonacho, hili
linafanyika kwa kutumia lugha. kwa ufupi tunachoweza kusema hapa ni
kwamba lugha hutumika kwa ajili ya kujielezea.
 Kuamuru: Ni kutoa maelekezo kwa njia ya kuamrisha. Kwa mfano jaji
anamuhukumu mshitakiwa kwa kumuamuru ‘Ninakufunga miaka mitatu
jela’. Hapa lugha inatenda kazi ya kuamuru.
 Kushirikiana: ni hali ya kutenda kitu kwa pamoja au hali ya kuwa na ubiya
kwenye jambo. Lugha huwezesha watu kujenga mahusiano ya siri baina ya
watu wawili au zaidi na kuweza kujitengenezea njia zao za kuwasiliana pasina
wengine kuelewa.
 Kuonesha: kumuelekeza mtu kitu kwa njia ya kuashiria. Unapotaka
kuonesha jambo ni lazima utumiye lugha kwa nija moja au nyengine.

1.5 Matumizi na umuhimu wa Lugha


 Kuwasiliana:- Lugha hutumika kupashana habari
 Kuunganisha- Lugha hupatanisha na kuleta uelewano miongoni mwa wana
jamii. pia lugha huweza kutofautisha jamii moja na nyengine.
 Kujenga jamii- lugha huleta/huhimiza shughuli za maendeleo ya jamii, huleta
amani na mshikamano katika jamii.
 Kufundishia- Lugha hutumika katika kufundishia elimu.
 Kutambulisha- Lugha hutumika kutambulisha jamii ya watu Fulani.
 Kuhifadhi- Lugha ndicho chombo cha kuhifadhi na kueneza utamadun.

1.6 Ujuzi wa lugha: umilisi na utendaji.


Je, tunamaanisha nini tunaposema fulani anajua Lughafulani?
Jibu ni kwamba, tunakusudia kusema kwamba mtu huyu
 ana ujuzi wa aina na mpangilio wa sauti za lugha hiyo
 ana ujuzi wa maana ya maneno na sentensi za lugha hiyo
 ana ujuzi wa sentensi na zisosentensi katika lugha hiyo.
Ujuzi wa mambo hayo unajulikana kama umilisi wa kisarufi ambao unatofautishwa na
hali halisi ya matumizi ya lugha hiyo tuiitayo utendaji wa kisarufi. Ikumbukwe kwamba
ujuzi huu hunaswa katika mpango uliokwisha kutayarishwa katika ubongo wetu kuanzia
utoto wetu pale tunapoanza kujifunza lugha kutoka kwa mama zetu. Hakuna darasa la
wazazi linalotufunza aina za sauti, maana ya sauti hizo na hata namna ya kuzitumia sauti
hizo katika muktadha husika. Haya huzuka pengine bila sisi wenyewe kujua tumejifunza
lini swali hili la ujuzi wa lugha katika ubongo katika akili yetu, hushughulikiwa na tawi
maalumu la isimu liitwalo isimu- neva ambalo katika kiwango chetu hiki
halitoshughulikiwa.

1.7 Lugha asilia na lugha unde.


Lugha asilia ni lugha inayotokana na jamii mahsusi ambamo imeibuka na
kufungamana kiutendaji na katika utamaduni na maendeleo ya jamii husika. Kwa
mfano Kiingereza, Kiswahili, Kichina n.k. Hizi ni lugha asilia zilizoibukia katika jamii
hizo.

Lugha unde ni lugha ya kubuni isiyotokana na jamii yoyote, ni lugha iliyobuniwa na


watu wachache na kuundwa kufuatana na misingi ya lugha asilia na kisha kuenezwa
ili itumike kwa mawasiliano baina ya jamii au mataifa tofauti. Kwa mfano:
Kiesperanto, Kivolapuk n.k. ni lugha unde ambazo hazitokani na jamii yoyote
mahsusi.

1.8 Maana ya Isimu


Isimu ni uchunguzi wa lugha kisayansi. Ipo taaluma kama falsafa ambayo nayo
inaweza kujishughulisha na uchunguzi wa maswala ya lugha lakini si kwa
kutumia vigezo vya kisayansi. Wanaisimu hukhakikisha kwamba wakati wa
kutafiti na hatimaye kuwasilisha matokeo ya utafiti wao wanatumia vigezo vya
kisayansi hatua kwa hatua. Kwanza huchunguza na kukusanya data. Halafu
wanafanya malinganisho kabla ya kuunda nadharia na kuzipima nadharia na
kuzipima matukio yake. Baadae hujiundia nadharia na kutoa kanuni ambazo
zinapimika.

1.9 Uainishaji wa makundi ya Isimu


1.9.1 Isimu fafanuzi: ni taaluma ya utambuzi wa vipengele vya lugha au namna gani
lugha imepangika. Kozi hii itajishughulisha na kujadili baadhi ya matawi ya Isimu
fafanuzi pekee. Ndani ya taaluma hiyo kuna vitawi vidogo vidogo ambavyo baadhi yake
vitashughulikiwa katika kozi hii nzima.

Tunaorodhesha baadhi ya vitawi hivyo na kuvifasili na kuonesha tofauti zake.


Fonetiki Ni tawi la isimu linaloshughulikia sauti za vitamkwa ikiwa ni pamoja na
kuchunguza ala za matamshi, namna ya kutamka, uelewa wa sauti, aina
za vitamkwa, kusafiri kwa sauti na jinsi zinavyofasiliwa katika ubongo.
fonolojia Ni tawi la isimu linaloshughulikia Uchambuzi wa mfumo wa sauti
zinazotumiwa katika lugha Fulani.
Mofolojia Ni tawi la isimu linaloshughulikia uchunguzi wa maneno na aina za
maneno.
Sintaksia Ni tawi linaloshughulikia uchanganuzi uchanganuzi wa mpangilio na
uhusiano wa vipashio katika sentensi.
Isimu historia Tawi la isimu linalofuatilia mabadiliko katika Lugha kama vile
mabadiliko ya sauti , leksika, maumbo ya maneno na hata mabadiliko ya
maana.
Isimu jamii Tawi linaloshughulikia uhusiano uliopo baina ya Lugha na jamii.
Isimu Amali Tawi linaloshughulikia uchanganuzi wa Lugha kwa kutegemea maoni ya
mtumiaji, hasa uchaguzi wa miundo ya maneno anaoufanya, vikwazo
vya kijamii anavyokabiliana navyokatika kutumia lugha na athari za
kijamii katika katika matumizi ya lugha yake.
Isimu Neva
Isimu Nafsi Tawi la isimu linalochunguza jinsi mtu anavyojifunza lugha kwa kutumia
misingi ya kisaikolojia.
Isimu Tawi linaloshughulikia mahusiano baina ya lugha na utamaduni.
Anthoroplojia
Isimu Tawi la isimu linaloshughulikia uchanganuzi wa vipengele vya kiisimu
kokotozi kwa kutumia mbinu za ukokotozi.
Chanzo Kipacha Ahmed (2007).
1.9.2 Isimu matumizi: inajishughulisha na kutumia nadharia, mbinu na maarifa ya
kiisimu katika kuelezea matumizi ya lugha, kwa mfano katika kufundisha lugha,
kutunga kamusi, kuunda sera za lugha, leksikografia, tafsiri, lugha za matangazo,
mahakama n.k

MAREJELEO.
Besha, R (1994), Utangulizi wa Lugha na Isimu . Dar es Salaam University Press.
Habwe, J. and Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi, Phonix
Publishers
Kipacha, Ahmed (2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Open University of Tanzania, Dar
es Salaam
Massamba, D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004) fonolojia ya Kiswahili Sanifu (Fokisa)
Sekondari na vyuo. TUKI.
Masebo, J.A na Nyangwine, N,(2009) Nadharia ya Lugha KISWAHILI 1 Nyamburi
Nyangwine Publishers, Dar-Es Salaam, Tanzania.

MUHADHARA WA PILI
UHUSIANO WA LUGHA NA JAMII PAMOJA NA TAMADUNI
ZA JAMII

MALENGO YA MUHADHARA

 Uweze kueleza uhusiano uliopo baina ya Lugha na jamii


Baada ya kumalizika muhadhara huu, mwanafunzi unatakiwa:-

 Uweze kueleza uhusiano uliopo baina ya Lugha na utamaduni

2.0 UHUSIANO WA LUGHA NA JAMII PAMOJA NA TAMADUNI


ZA JAMII.

2.1 Lugha na jamii


2.1.1 Maana ya lugha: Lugha ni sauti za nasibu zinazotumiwa na
watu katika kuwasiliana miongoni mwao.
2.1.2 Maana ya jamii: Jamimi ni kundi la watu wanaoishi
pamoja na wenye kuhusiana kijamii, kikazi au kiuchumi na
yenye kutumia lugha moja kwa ajili ya mawsiliano yao.

2.1.3 Mahusiano ya lugha na jamii:
Lugha imefungamana na jamii kiasi kwamba haiwezi


kutenganishwa na jamii ya maisha ya mwanaadamu.
Lugha ni sehemu ya jamii, kwani jamii haiwezi kutumia na


kasha kuiwacha na kuchukuwa nyengine.
Lugha ni kielelezo cha mahusiano ya jamii yaani hueleza jinsi
jamii inavyohusiana na mazingira yao halisi na namna


wanajamii wanavyohusiana wenyewe kwa wenyewe.
Lugha hubadilika kulingana na mabadiliko ya kijamii.
2.1.4 Kutokuwepo uhusiano wa moja kwa moja wa
lugha na jamii.
Mbali na uhusiano uliuopo baina ya jamii na lugha, hakuna
uhusiano


wa moja kwa moja baina ya lugha na jamii kwa sababu
Lugha sio lazima iwe ya watu wa jamii ile ile. Mathalani Kiswahili


sio lugha ya lugha ya waswahili peke yao.
Watu wanao ishi katika nchi sio lazima wawe wa asili ya nchi
hiyo, kwa hivyo jina la jamii hailwezi kuwiana na lugha


wanayoongea.
Lugha moja huwa na vilugha kadhaa ndani mwake, mfano lugha
kiingereza ina viingereza kadhaa ndani yake, yaani lahaja nyingi


mno.
Kuna jamii yenye jina tofauti na lugha wanayozungumza,
mathalani wamarekani, hawazungumzi kimarekani bali kiingereza.


2.2 Lugha na utamaduni- Nadharia ya sapir –Whorf.
Lugha hutawala namna ya wazungumzaji wake waionavyo

 Ukichunguza baadhi ya misamiati ya wana lugha fulani


dunia.

utakuta kuwa yapo maneno pekee yanayowakilisha yale


wayaonayo mbele ya macho yao au mazingira yao tu na
kutokuwepo kwa neno kuna maanisha kwamba jambo hilo
halipo ‘machoni’ pao. Sawa na kusema kuwa ‘lisilokuwepo

 Lugha ya mtu hutawala mawazo yake.


machoni na moyoni halipo’.

 Dhana tulizonazo huunda kile tukionacho, kutuzunguuka na

 Mfumo wa dhana ndiyo muhimili wa jinsi tuionavyo dunia


kinachotuhusu.

yetu ya kila siku.


Nida ( 1986) anasema kuwa, lugha ni kielelezo cha utamaduni wa
wazungumzaji wake na sio muhimili wa uoni wao. Lugha hufuata
jamii na wala si kuoingoza jamii hiyo.

Marejeleo:
Habwe, J. and Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi, Phonix
Publishers.
Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam.

Massamba, D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004) Isimu jamii. Sekondari na vyuo. TUKI.

MUHADHARA WA TATU

VIJILUGHA MBALIMBALI KATIKA LUGHA MOJA PAMOJA NA


UMAHIRI KATKA LUGHA.
MALENGO YA MUHADHARA

 Kufasili dhanna za vitarafa, vibinafsi, lahaja, rejista na lugha rasmi


Baada ya kumalizika Muhadhara huu mwanafunzi unatakiwa uweze:

 Kueleza maana ya umahiri katika Lugha.


 Uweze kubainisha mambo yanayowezesha mtu kuwa mmahiri wa Lugha
 Uweze kubainisha mambo yanayopoteza umahiri
 Uweze kuainisha vigezo mbalimbali vinavyotumika kupima umahiri wa lugha.

3.0 VIJILUGHA MBALIMBALI KATIKA LUGHA MOJA PAMOJA


NA UMAHIRI KATKA LUGHA.

3.1 Vitarafa: ni vilugha ambacho huzungumzwa na wat u wa eneo dogo


kat ika eneo kubwa la wat u wanaozungumza lugha moj a.

3.2 Vibinafsi: ni kilugha cha mt u binaf si ambacho humbainisha yeye kwa


namna anavyot amka au kuendeleza maneno.

3.3 Lahaja: Lugha moja wapo kati ya lugha ambazo kimsingi huhesabiwa kuwa
lugha moja ispokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani fulani, kama
vile lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au muundo kutokana na eneo
lugha hiyo linakozungumzwa.

3.4 Rejista: Rej ist a ni mt indo wa lugha inayot umika mahali penye
shughuli f ulani au inayot umiwa na kundi maalum la kij amii ambayo ni
t of aut i na l ugha ya kawaida.
3.5 Kitabaka: Hiki ni kilugha cha wazungumzaj i wa lugha ambao ni wa
t abaka f ulani kat ika j amii ambao huj ibagua kulingana na naf asi yao
kiuchumi, kisiasa au kielimu, n. k

3.5 Lugha rasmi: Lugha iliyochaguliwa katika jamii kwa matumizi ya shughuli
za kijamii za kila siku.

3.6 Misimu: Misimu ni maneno yasiyosanifu yazushwayo na kikundi cha watu


wachache wenye utamaduni mmoja ili kueleza mahusiano yao kama kikundi au
kuhusu jamii kubwa ambamo vikundi hivyo vinaishi katika kipindi fulani cha wakati;
na hatimaye maneno hayo hupotea na yanayodumu husanifiwa na kuwa msamiati
rasmi wa lugha inayohusika.

3.7 Umahiri katika Lugha:


3.7.1 Mambo yanayomwezesha mtu kuwa mahiri wa lugha.


Kusomea lugha hiyo kwa kiwango cha juu


Kutumia lugha hiyo kwa matumizi ya kila siku.


Kuepuka athari za lugha nyengine katika lugha hiyo.
Kuwakosoa na kuwasahihisha waharibifu wa lugha.

3.7.2 Athari za umahiri:-

 Matamshi
Umahiri wa lugha wa mzungumzaji huathirika kwenye vipengele:-

 Msamiati
 Sarufi
 Maana


3.7.3 Mambo yanayopoteza umahiri wa Lugha


Kutotumia lugha hiyo kwa matumizi ya kila siku.


Kutosomea lugha hiyo kwa kiwango cha juu


Hamahama ya watu


Mfumo wa elimu


Kutokuwa karibu na wajuzi wa lugha.
Kasumba


3.7.3 Vigezo vinavyotumika kupima umahiri wa Lugha
Kutambua ni sauti zipi zinazotumika kuunda maneno ya lugha yake na


mfuatano upi unakubalika na upi haukubaliki.
Kutambua mfuatano sahihi wa vipashio katika maneno au sentensi za


lugha yake.
Kutambua tungo ambazo zinavunja /hazivunji kanuni za sarufi ya


(upatanisho wa kisarufi).
Kutambua kwa urahisi sentensi ambazo ni tata na pia kutambua jinsi ya
kuondoa utata huo.
 Kutambua kwa urahifi kusudio la sentensi.

Marejeleo

Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam.

Massamba, D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004) Isimu jamii. Sekondari na vyuo. TUKI.


Masebo, J.A na Nyangwine, N,(2009) Nadharia ya Lugha KISWAHILI 1 Nyamburi
Nyangwine Publishers, Dar-Es Salaam, Tanzania.

MUHADHARA WA NNE
UCHAMBUZI WA DHANNA YA LAHAJA NA MISIMU

MALENGO YA MUHADHARA

 Maana ya lahaja
Mwishoni mwa muhadhara huu unatakiwa uelewe

 Aina za lahaja
 Maana ya vizinga sifa na atlasi lahaja.
 Dhanna ya misimu/simo/
 Chanzo cha misimu na sababu za kuzuka kwake.
 Njia zitumikazo kuundia misimu
 Sifa na aina mbalimbali za misimu
 Matumizi na matatizo ya misimu.

4.0 UCHAMBUZI WA DHANNA YA LAHAJA NA MISIMU


4.1 DHANNA YA LAHAJA
4.1.1 Maana ya Lahaja
4.1.1.1 M aana ya lahaja kw a mtazamo pungufu : Katika mtazamo huu
lahaja inafafanuliwa kuwa ni ki- lugha ambacho hakijaandikwa kisicho na maandishi,
na kwa ufupi huchukuliwa kuwa ni lugha pungufu. Huu ni mtazamo wa kimapokeo
wenye misingi ya Kigiriki ambao unadunisha lahaja na kuikweza lugha.
4.1.1.2 M aana ya lahaja kw a mtazamo w a kimaelew ano : M tazamo huu
unafasiri lahaja kuw a ni lugha yeyote ile iw e imeandikw a au haikuandikw a, unaifafanua lahaja
kama sehemu ya kundi- lahaja ambalo linatambulika kama lugha fulani.
4.1.2 Sababu za kuzuka kwa Lahaja
 Sababu za kijografia
 Sababu za kijamii
 Sababu za kiuchumi

4.1.3 Aina za lahaja

 Lahaja za kijografia
Wazungumzaji wawili wa lugha moja wanaweza kuwa na tofauti ndogo
ndogo za kimatamshi au msamiati baina yao kwa sababu wanatoka katika
maeneo yanayotenganishwa na milima, bahari au mito.

 Lahaja za kijamii
Wazungumzaji wawili wa lugha moja wanaweza kuwa na tofauti ndogo
ndogo za kimatamshi au msamiati baina yao kwa vile wanatoka katika
matabaka, rika, ujuvi, jinsia au itikadi tofauti.

4.1.4 Mgawanyiko wa lahaja za Kiswahili


 Lahaja za kaskazini
Kwa mujibu wa Nurse (1982) lahaja za kaskazini ni lahaja za kutoka
Somalia hadi kusini mwa Mombasa. Lahaja hizo ni Chimwiini, Kiamu,
Kipate, Kisiu, Kivumba, Kimvita na Chifundi.
 Lahaja za kusini
Lahaja za kusini ni zile zinazoanzia Vumba ya kusini hadi M sumbiji, nazo ni :
Kimtang’ata, Kimrima, Kipemba, Kihadimu (Kimakunduchi), kitumbatu, Kiunguja,
Kimafia (Kingome), Kimwani na Kiekoti.

4.1.5 Maana ya Vizinga sifa: hii ni mistari inayochorwa kuonesha


tofauti za matamshi baina ya lahaja moja na nyengine
4.1.5.1 Aina ya vizinga sifa: Zipo aina nne za vizinga sifa:

 vizinga sifa vya msamiati, mfano nyanya Tanzania bara, huitwa tungule

kule Tanzania visiwani.

 Vizinga sifa mofu, mfano nitakuja kama itamkwavyo kwenye Kiswhili

sanifu, hutamkwa kama takuja kama litamkavyo Pemba au sakuja kama

litamkwavyo hukom utumbatuni.


 Vizingasifa sauti: njia katika Kiswahili sanifu, hutamkwa ndia katika

Kimvita

 Vizinga sifa vya maana, mf. Mfereji- bomba.

4.1.5.2 Uwelewano katika lahaja:

Uelewano ni hali ya vikundi lugha tofauti vilivyotengana kimasafa

hufahamiana baina yao. Mfano, Kwa mfano wapemba hufahamiana na

watumbatu hata kama ni watu wa makundi Lugha tofauti.

4.1.5.3 Atlasi Lahaja : At lasi lahaja ni uw ekaji w a vielelezo vinavyoonyesha


mat amshi mbalimbsali , vipengele mbalimbali vya kisarufi na msamiat i w a lugha
fulani. Kw a maneno mengine, at lasi lahaja ni mkusanyiko w a ramani na vielelezo
vinavyoonyesha maneno ya lugha( au lahaja) mbalimbali kat ika nchi au eneo lahaja
jiografia.

4.1.6 Vigezo vya kiisimu vinavyotofautisha lahaja.


 Kigezo cha kifonolojia
 Kigezo cha kimofolojia
 Kigezo cha kisemantiki/maana
 Kigezo cha kisintaksia
4.1.7 Dhima za lahaja
 Kusanifisha lugha
 Kukuza lugha
 Kupamba lugha
 Kuongeza msamiati katika lugha rasmi.
 Kurahisisha maw asiliano.

4.2 .0 Dhanna ya misimu


4.2.1 Maana ya misimu:
Misimu ni maneno yasiyosanifu yazushwayo na kikundi cha watu wachache wenye
utamaduni mmoja ili kueleza mahusiano yao kama kikundi au kuhusu jamii kubwa
ambamo vikundi hivyo vinaishi katika kipindi fulani cha wakati; na hatimaye maneno
hayo hupotea na yanayodumu husanifiwa na kuwa msamiati rasmi wa lugha
inayohusika.

4.2.2 Chanzo cha misimu:


 Misimu huzuka kutoka na na mabadiliko ya kihistoria yanayokumba jamii katika


nyakati mbalimbali.
Misimu mingine huzuka kutokana na hali ya utani miongonim mwa watu


mbalimbali.
Mara nyingi misimu ya aina hii hubeba kebehi, dhihaka, kejeli, mabezo, dharau au
kusifu kusiko kwa kawaida.


4.2.3 Sababu za kuzuka kwa misimu:


Kutaka mazungumzo yawe siri.

 Kufanya mambo mazito nay a maana kuwa mepesi nay a kawaida.


Kudhania matumizi ya misimu ndio ujuzi wa lugha.


4.2.4 Njia zitumikazo kuundia misimu:


Njia ya kufupisha maneno


Njia ya kutohoa kutoka lugha za kigeni.


Njia ya kutumia sitiari


Njia ya kutumia tanakali
Njia ya kubadili maana ya msingi

4.2. 5 sifa za misimu:


Misimu huzuka na kutoweka.
Misimu ni lugha isiyo rasmi.
Misimu ni lugha ya mafumbo.
Misimu ina chuku nyingi.
Misimu ina maana nyingi.
Misimu hupendwa sana na wengi.
Misimu ina mvuto na kwa sababu hii hupendwa na watu wengi.
Misimu huhifadhi historia ya ya jamii.

4.2. 6 Aina mbalimbali za misimu


4.2.6.1 Kwa kutumia kigezo cha mada.
Misimu inayohusiana na pesa
Misimu inayohusiana na majina ya vyakula.
Misimu ya ulevini
Misimu ya nguo
Misimu yanayohusiana na usafiri
Misimu inayohusiana na wana wake

4.2.6.2 Kwa kutumia kigezo cha kufuatana na makundi ya watu


wanaozitumia.
Misimu ya wanafunzi
Misimu ya wafanya biashara
Misimu ya majangili
Misimu ya majambazi
Misimu ya wana michezo
Misimu ya walanguzi n.k

4.2.6.3 Kwa kutumia kigezo cha jumla/kawaida


i) Misimu yenye maneno ya kawaida lakini usemi wake unajitokeza yanapotumika
katika mazingira maalum.
ii) Misimu ya maneno ya kujitokeza tu.
a) Misimu ya pekee
b) Misimu ya kitarafa
c) Misimu zagao


4.2. 7 Matumizi ya misimu


Kukuza Lugha


kupamba lugha


Kufanya mawasiliano yawe mafupi na yanayoeleweka kwa haraka


Kuficha lugha ya matusi


Kuwaunganisha watu wa makundi (matabaka) mbalimbali


Kuhifadhi historia ya jamii.


Kuibua hisia mbalimbali za wazungumzaji


Kufurahisha na kuchekesha


Kukosoa na kuiasa jamii


Misimu huleta msamiati wenye matusi
Misimu hupunguza hadhira


4.2. 8 Matatizo ya misimu


Misimu huharibu lugha kwa sababu siyo lugha sanifu


Misimu baadhi ya wakati huleta msamiati weye matusi
Misimu ni lugha ya mafumbo na hufahamika na kikundi kidogo kinachotumia


misimu hiyo.


Misimu imetiwa chumvi nyingi kwa hivyo haiaminiki katika jamii


Misimu huzuka na kutoweka
Misimu ina maana nyingi

MAREJEO YA LAZIMA

 Massamba, D.P.B (2002) Historia ya Kiswahili 50BK hadi 1500 BK JKF.


Nairobi
 Maganga.C (1997) Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Dar
es Salaam.
 Kipacha Ahmad (2003) Lahaja za Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania,
Dar es Salaam.
 TUKI(2010) Lugha ya Kiswahili 1: Makala za Semina ya Kimataifa ya
Waandishi wa Kiswahili. TUKI. Dar es Salaam

MAREJEO YA ZIADA

 Massamba, D.P.B (1995) ‘Lahaja na Mitindo katika Kiswahili Sanifu’ katika


Kiango, J. (mh),Dhima ya Kamusi katika Kusanifisha Lugha. uk. 1 – 17.
 Mbaabu, I. (2007) Historia ya Usanifishaji wa Kiswahili. TUKI. Dar es Salaam
 TUKI (1983) Lugha ya Kiswahili: Makala za Semina ya Kimataifa ya
Waandishi wa Kiswahili. TUKI. Dar es Salaam
 Chiraghdin & Mnyampala (1977) Historia ya Kiswahili. OUP
 Bosha, I (1993) The Influence of Arabic Language in Kiswahili with
Trilingual Dictionary (Swahili – Arabic – English). Dar es Salaam University
Press
 Kihore, Y.M. (1983) “Nafasi ya Kiswahili Barani Africa” in Masoko, D.L.W. and
Mdee, J.S. (ed) Mulika Vol 15. TUKI, Dar es Salaam pp 32 – 39
 Kihore, Y.M. (1984) “Kiswahili katika Hati za Kiarabu” in Masoko, D.L.W. and
Mdee, J.S. (ed) Mulika Vol 16. TUKI, Dar es Salaam pp 34 – 45
 Msanjila, Y.P. (1997) “Towards the Policy on the Use of Kiswahili in Africa” in
Massamba, D.P.B. and Mulokozi, M.M. (ed) in Kiswahili Vol. 60. TUKI, Dar es
Salaam. Pp 61 – 67
 Msanjila, Y.P. (2002) “Dhima ya Lugha ya Kiswahili Katika Karne ya Ishirini na
Moja” in Kiswahili Vol. 65. TUKI, Dar es Salaam
 Ryanga, S. (2002) “The African Union in the Wake of Globalization: The
Forgotten Language Dimension” in Kiswahili Vol. 65. TUKI, Dar es Salaam
 Mkude, D. J. (1983) Mtawanyiko wa lahaja za Kiswahili, Makala za Semina ya
Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili 1. TUKI
 Steere, E. (1930) A handbook of the Swahili Language. East African Language
Committee
 Stigand, C.H. (1915) Dialects in Swahili. Cambridge University Press
 Whiteley, W.H. (1956) Kimtang’ata (Studies in Swahili Dialects – 1) East
African Swahili Committee.

MUHADHARA WA TANO
5.0 UCHAMBUZI WA DHANNA YA REJISTA
MALENGO YA MUHADHARA
Mwishoni mwa muhadhara huu unatakiwa:-
 Uweze kueleza maana ya rejista
 Uweze kubainisha aina mbalimbali za rejista
 Uuweze kufafanuwa umuhimu wa rejista
 Uweze kuainisha sababu mbalimbali zinazosababisha kuzuka kwa rejista.

5.1 Maana ya rejista


Rej ist a ni mt indo wa lugha inayot umika mahali penye shughuli f ulani au
inayot umiwa na kundi maalum la kij amii ambayo ni t of aut i na lugha ya
kawaida.

5.2 Aina ya rejista


 Rej ista za mitaani:-

Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa magengeni ambayo hueleweka


na wazungumzaj i wenyewe. Ni lugha ambayo huchipuka kut okana na
kikundi cha wat u ambacho ni kidogo. Lugha hii hudumu kwa muda mf upi
t u, halaf u huf if ia. Wakat i mwingine hukubaliwa na j amii na kuweza
kuingizwa kat ika msamiat i wa l ugha hiyo.

 Mazungumzo ya kwenye shughuli maalum(Rej ista za mahali):


Mazungumzo ya kwenye shughuli maalum hayaf anywi kiholela, bal i
yanaf uat a t arat ibu na kanuni maalum zinazoj it okeza kat ika mazingira ya
sehemu hiyo. Kut okana na kut umiwa kwake kwa muda mref u kwenye
mazingira ya aina hiyo hiyo.

 Rej esta zinazohusu watu:


Ni yale mawasiliano yasiyo rasmi ni yale maongezi ya kawaida ya kila
siku yanayoenda baina ya wat u .

 Lugha ya Kitarafa:
Hiki ni Kiswahili cha t araf a f ulani, ambacho pindi kikisemwa kat ika t araf a
nyengine huwa ni vigumu kwa wat u wa sehemu hiyo kuf ahamu kisemwacho.

 Kiswahili Rasmi/ Sanifu :


Haya ni masawazisho kut okana na vilugha mbalimbali vya Lugha ya
Kiswahili. Ni Kiswahili kikubaliwacho na wengi kat ika nchi na ndicho
kit umikacho kat ika shughuli rasmi za Taif a.

5. 3 Umuhimu wa Rej ista:


 Rej ista hutumika kama kitambulisho :-

Rej ist a hut of aut isha mt indo wa lugha miongoni mwa wazungumzaj i. Rej ist a
inawat ambulisha wazungumzaj i kuwa wao ni wahusika wa kundi f ulani.

 Rejista hupunguza ukali wa maneno.


Rejista inapotumiwa na kundi la watu, huficha jambo Fulani linalozungumziwa
lisieleweke kwa wengi. Hivyon hadhira inapuuzwa kwa sababu siyo watu wengi
wanaoelewa.
 Rej ista inatumika ili kurahisisha mawasiliano.

Rej ist a inat umika ili kurahisisha mawasiliano au kupunguza muda wa


kuwashughulikia wat u au wat ej a wengi.

 Rej ista hupamba lugha miongoni mwa wazungumzaj i.

Lugha ya rej est a, kut okana na mt indo wake mara nyingi huonekana kama
pambo la Lugha miongoni mwa wazungumzaj i wa kundi f ulani la j amii
inayot umia rej ist a hiyo.

 Rej ista huweza kuwa kiungo cha ukuzaj i wa Lugha. Kut okana na
mat umizi ya rej ist a mbalimbali, lugha inayohusika inaweza
kuchukuwa baadhi ya maneno ya rej est a na kuj iongezea msamiat i
wake.

Baadhi ya maneno yanayokuwa yakit umika kwenye rej ist a ya aina


f ulani yanaweza kuingia na kudumu kat ika lugha ya kawaida.

5.4 Sababu za kuzuka kwa rejista


 Ubinafsi
Ubinaf si ni t abia aliyonayo mt u, iwe ya muda au ya kudumu hasa inayohusu
namna ya uwasilishaj i wa mazungumzo yake.
 Maingiliano

Makundi ya wat u mbalimbali yanapochangamana husababisha mwingiliano


miongoni mwao.
 Kupita kwa wakati
Kila mahali kat ika j amii, huj it okeza mt indo kat ika kipindi maalum.
 Shughuli iliyopo

Hapa hut egemea ni mazingira gani ambapo shughuli hiyo inaf anyika.
 Tofauti za hadhi za wahusika (uhusiano wa wahusika):

Mf ano msomi/ wasiosoma, mwaj iri/ mwaj iriwa, t aj iri/ maskini.


 Matumizi ya uficho/ Tafsida
Hali hii pia husababisha kuzuka kwa rej ist a kwani husababisha mit indo
mbalimbali miongoni mwa wazungumzaj i.

MAREJELEO:
Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam.

Massamba, D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004) Isimu jamii. Sekondari na vyuo. TUKI.

Masebo, J.A na Nyangwine, N,(2009) Nadharia ya Lugha KISWAHILI 1 Nyamburi


Nyangwine Publishers, Dar-Es Salaam, Tanzania.

MUHADHARA WA SITA
DHANNA YA FONETIKI
MALENGO YA MADA
Mwishoni mwa muhadahara huu mwanafunzi anatakiwa aweze
 Kueleza maana ya fonetiki.
 Kubainisha matawi mbalimbali ya fonetiki
 Kufafanua dhana ya alasauti
 kufafanuwa dhanna ya nyuzi sauti
 Kueleza na kufafanua dhanna ya sifa bainifu
 Kubainisha Mitazamo tofauti juu ya dhanna ya fonimu

6.0 DHANNA YA FONETIKI


6.1 Maana ya fonetiki:
Ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa taratibu zote
zinazohusiana na utoaji utamkaji, usafirishaji, usikiaji na ufasili wa sauti za lugha za
binaadamu kwa jumla”.

6.2 Matawi ya fonetik:-


 fonetiki matamshi au fonetiki utamkaji:
Tawi hili hujishughulisha na uchunguzi wa sauti namna zinavyotamkwa na mahali
ambapo sauti hizo zinatamkiwa, yaani mahali pa matamshi.

 fonetiki mawimbi sauti au fonetiki akustika


Hili ni tawi la fonetiki ambalo hujishughulisha na jinsi mawimbi ya sauti ya Lugha
yanavyosafiri kutoka katika kinywa cha msemaji hadi katika sikio la msikilizaji.
 fonetiki masikizi au fonetiki sikivu:
Kimsingi tawi hili la fonetiki hujishughulisha na jinsi utambuzi wa sauti mbalimbali za
Lugha unavyofanywa, na uhusiano uliopo baina ya sikio, neva masikizi (yaani neva
zinazohusika na usikiaji wa sauti) na ubongo.
 fonetiki-tiba matamshi:
Tawi hili hujishughulisha na matatizo yanayo ambatana na usemaji au utamkaji wa sauti
na jinsi ya kuyatatua
 fonetiki kokotozi:
Hii ni taaluma ambayo inachambua mawimbi sauti na kuweza kutumia mchoro wa
spektogramu kuonyesha picha ya sauti katika vipengele vyake vya kasimawimbi.
 fonetiki ushawishi
Ni taaluma inayohusiana na kurikodi sauti kwa kutumia kinasa sauti na baadae
kuchambua kwa kusikiliza tu.
 fonetiki majaribio
Inahusika na uchukuwaji wa sauti iliyorikodiwa na kuingizwa katika kompyuta kwa ajili
ya kutafuta matokeo ya uchambuzi.

6.3 Ala sauti:


Sehemu mbalimbali za maungo ya mwanaadamu yatumikayo katika utoaji wa sauti za
Lugha huitwa.

6.3.1 Aina za Ala sauti


 Ala sauti tuli- Ala sauti tuli- ni sehemu au maungo mbalimbali ya
binaadamu ambayo hayawezi kujongea au kusogea wakati wa utamkaji wa
sauti za lugha, kama ufizi, kaakaa, nyuzi za sauti n.k
 Ala sauti sogezi- Ni zile sehemu au maungo mbalimbali ya binaadamu
ambayo yana uwezo wa kujongea au kusogeasogea wakati wa utamkaji wa
sauti za lugha, kama vile ulimi na midomo.

6.4 Nyuzi sauti


Nyuzi sauti ni nyama laini zilizoko katika koromeo ambazo zinauwazi
katikati unaoruhusu mkondo wa hewa kutoka nje na ndani ya kifua.
6.5 Vitamkwa na uainishaji wake
6.5.1 Maana ya vitamkwa
Vitamkwa ni sauti dhahiri inayosikika wakati wa utamkaji wa maneno,
na ambayo huweza kubainishwa kama kitu kimoja ambacho huweza
kuwakilishwa kimaandishi kwa kutumia alama zijulikanazo kama herufi
za alfabeti.
6.5.2 Aina za vitamkwa ni
 Konsonanti- Konsonanti ni aina ya sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondo
hewa kutoka mapafuni, ukipitia chemba ya kinywa na chemba ya pua kwenda nje
 Viyeyusho-“ viyeyusho ni aina ya vitamkwa ambavyo si konsonanti na wala si
irabu; yaani ni vitamkwa ambavyo huchukuliwa kuwa katikati kati ya irabu na
konsonanti.
 Irabu- Irabu ni aina ya vitamkwa ambavyo hutolewa pasina kuwepo kizuizi
chochote katika mkondo hewa utokao mapafuni ukipitia katika chemba ya kinywa
na chemba ya pua”.

6.6 Sifa bainifu za kifonetiki.


Hizi ni sifa za kifonetiki zinazoweza kuitafautisha sauti moja kutokana na
sauti nyengine kwa kutumia vigezo vya kifonetiki.
6.6.1 Vigezo vitumikavyo kubainisha konsonanti mbalimbali
 namna ya kutamka

 mahali pa kutamkia

 mkondo wa hewa

 hali ya glota

6. 6. 1. 1 Namna ya kutamka
Kwa kuzingat ia kigezo hiki konsonant i zimegawanyika kat ika makundi :
 Vipasuo: “Sauti za vipasuo hutamkwa wakati mkondo hewa unapofungiwa

kabisa katika sehemu yoyote ya bomba la sauti na kisha kuruhusiwa upite ghafla”.

 vikwamizi: Kwa jina jengine vipasuo huitwa vikwaruzo: “hizi ni sauti

ambazo hutamkwa wakati alasauti zinapokaribiana na kupunguza upenyo wa


bomba la sauti kiasi cha kufanya hewa ipite kwa shida na hivyo kusababisha

mkwaruzo.”

 vipasuo kwamizi: “hizi ni sauti ambazo hutolewa kwa kuchanganya mzuio wa

muda mfupi (kama katika kipasuo) na mzuio nusu unaosababisha ukwamizi. Hizi

ni konsonanti ambazo utamkaji wake unahusu mkondohewa kuzuiwa na

kuachiwa taratibu kwa kukwamizwakwamizwa.”

 Nazali:- Nazali ni konsonanti ambazo hutamkwa kwa kuruhusu mkondo hewa

kupitia puani

 Likwidi:- Hizi ni sauti ambazo hutamkwa wakati ala za sauti zinapokaribiana na

kutatiza hewa kwa namna maalum. Hutamkwa huku hewa ikiendelea kupita.”

Wanaisimu wamebainisha aina mbili za likwidi, ambazo ni vitambaza na

vimadende.Vitambaza hutamkwa wakati ncha ya ulimi ikiwa imekita katika ufizi

huku hewa ikiruhusiwa kupita kandokando mwa ulimi. Vimadende hutamkwa

wakati ncha ya ulimi ikigotagota kwenye ufizi huku hewa ikiendelea kupita.

6.6.1.2 Mahali pa kutamkia

Kwa kuzingat ia kigezo hiki konsonant i zimegawanyika kat ika makundi :

 Sifa ya kwanza ni midomo:

Mkondo hewa unapozuiwa kwa kubana mdomo wa chini na mdomo wa juu kisha
ikaachia au ikabanwa kwa kuviringwa huku ikiwa imeacha upenyu kidogo huwezesha
sauti kadhaa hutolewa.
 Sifa ya pili ni midomo-meno:
Sifa hii inahusu utamkaji wa sauti ambao kwao meno ya juu, ambayo ni alatuli,hugusana
na mdomo wa chini, ambao ni alasogezi, na wakati huohuo hewa inaruhusiwa kupita kwa
kukwamizwakwamizwa katikati ya meno.
 Sifa ya tatu ni ya meno:

Sauti hizi hutamkwa kwa ncha ya ulimi ikiwekwa katikati ya meno ya juu na ya chini.

 Sifa ya nne ni ya ufizi:

“Sauti hizi zinapotolewa, ncha ya ulimi hugusana na ufizi.

 Sifa ya tano ni ya kaakaa gumu:

Sifa hii unahusu utamkaji wa sauti ambapo ulimi hufanya kazi ya ala sogezi. Ulimi
hugusana na kaakaa gumu ambalo ndiyo alatuli.
 Sifa ya sita ni ya kaakaa laini

Sifa hii huhusu utamkaji wa sauti ambao huandamana na sehemu ya nyuma ya ulimi,
ambayo ni alasogezi, kugusa kaakaa laini, ambalo ni alatuli.

6.6.13 Mkondo wa hewa

“ Mkondo hewa kutoka mapafuni waweza kupititia katika chemba ya kinywani au ya

puani”. Kinachosababisha hali hii ni kilimi. Kilimi chaweza ama kuteremka chini

kuelekea shina la ulimi na kuruhusu hewa kupita puani au kuinuliwa juu kuelekea

upande wa juu wa ukuta wa koo na kuruhusu hewa kupita kinywani. Sauti inayotamkwa

huku mkondo wa hewa ukipita puani huitwa sauti ya nazali . Mfumo huu wa upokeaji wa

sauti wakati mkondo wa hewa unapita puani huitwa kuwa ni Ung’ong’o.

6.6.1.4 Hali ya glota au koromeo

Katika koromeo au glota kuna kitu kinaitwa nyuzi sauti. Nyuzi sauti ni nyama laini

zilizoko katika koromeo ambazo zinauwazi katikati unaoruhusu mkondo wa hewa kutoka
nje na ndani ya kifua. Nyuzi hizo huwa katika nafasi za aina mbili wakati hewa

inapopita. Kuna wakati nyuzi hizo zinakaribiana au kuwa pamoja na wakati mwengine

zinakuwa zimeachana. Hewa inapotoka ndani ya mapafu kuja nje kupitia kwenye pango

la kinywa au la pua nyuzi hizo zikiwa zimekaribiana au kuwa pamoja, nyuzi hizo

husukumwa na kutetemeka.Sauti zinazotolewa wakati huo huwa na mghuno na huitwa

sauti ghuna. Zikiwa nyuzi hizi zimeachana, hewa hupita kwa urahisi bila kuzuiliwa, na

hivyo hazikwami na kusababisha sauti zinazotolewa kutokuwa na mughuno.

6.6.1 Vigezo vitumikavyo kubainisha irabu mbalimbali


Irabu hupangwa kutokana na vigezo vitatu: Ulimi uko juu kiasi gani kinywani (ujuu), ni

sehemu gani ya ulimi inainuliwa au kushushwa (Umbele), na midomo iko wakati huo

katika hali ya (Uviringo).

 Ujuu

Wakati wa kutamka irabu juu , ulimi unakuwa umeinuliwa juu katika kinywa, ambapo

irabu chini hutolewa wakati ulimi umeteremshwa chini.

 Umbele

 uviringo

Wakati unainuliwa kinywani, unaweza kupelekwa mbele katika kinywa, na hivyo

kutolewa irabu mbele. Ikiwa ulimi utarudishwa nyuma , basi irabu zitolewazo zitakuwa
irabu nyuma. Irabu [a] kama ya Kiswahili hutolewa ambapo ulimi hauko mbele au

nyuma, bali uko katikati.

6. 7 Sifa za AKIKI/ Msingi wa AKIKI.

 Kuwekwa vigezo vya kuainisha vitamkwa ambavyo ni:-

-Jinsi (namna) vitamkwa vinavyotolewa [maner of articulation]

-Mahali vitamkwa vinapotolewa [place of articulation]

 Kutenganisha vitamkwa katika makundi ya Irabu na konsonanti ; kama ndio aina

kuu za vitamkwa kwa kutumia vigezo vya jinsi na mahali vinapotamkwa.

 Hudai kuwa kila herufi huwakilisha kipashio kidogo kabisa cha sauti chenye ubainifu,

yaani FONI.

 Foni huwakilisha jinsi sauti zinavyotamkwa na si jinsi zinvyoandikwa. Foni hizi

huorodheshwa katika jeduweli la alfabeti ya kifonetiki ya kimataifa (AKIKI) kwa

kuzingatia mahali zinapotamkiwa, na jinsi/namna zinavyotamkwa.

Marejeleo

Besha, R (1994), Utangulizi wa Lugha na Isimu . Dar es Salaam University Press.


Habwe, J. and Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi, Phonix
Publishers
Kipacha, Ahmed (2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Open, University of Tanzania,
Dar es Salaam
Massamba, D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004) fonolojia ya Kiswahili Sanifu (Fokisa)
Sekondari na vyuo. TUKI.
Massamba, D. 1990. Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha. TUKI.
Massamba, D. 2004. Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha. TUKI
Masebo, J.A na Nyangwine, N,(2009) Nadharia ya Lugha KISWAHILI 1 Nyamburi
Nyangwine Publishers, Dar-Es Salaam, Tanzania.

MUHADHARA WA SABAA
DHANNA YA FONOLOJIA
MALENGO YA MUHADHARA
Unatarajiwa mwishoni mwa muhadhara huu :-
 Uweze kufasili maana ya fonolojia
 Uweze kubainisha uhusiano na tofauti kati ya fonetiki na fonolojia
 Uweze kuzibainisha kipashio cha msingi cha kifonolojia.
 Kueleza jinsi fonimu mbalimbali za lugha zinavyoainishwa.

7.0 Dhanna ya fonolojia


7.1 Maana ya fonolojia
 Fononolojia ni tawi la isimu ambalo hujishughulisha na uchunguzi , uchambuzi na

uainishaji wa sauti pambanuzi ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya

sauti za lugha za binaadamu.

 Fonolojia hujishughulisha hasa na zile sauti ambazo hutumika katika kutofautisha

maana za maneno katika lugha mahsusi.

 Fonolojia hujihusisha na sheria au kanuni zinazoandamana na utowaji na utumiaji

wa sauti hizo pambanuzi.

7.2 Uhusiano na Tofauti kati ya fonetiki na fonolojia


Fonetiki na fonolojia zinalingana kwa kuwa, malighafi ya mwanafonolojia huwa ni
sauti za lugha ambazo huwa zimeelezwa na kuainishwa na mwanafonetiki. Katika
kutumikizwa sauti za Lugha huweza kubadili sifa zake bainifu kutokana na
kuathiriana kwa sauti jirani katika neno. Ingawa kuyachunguza haya ni kazi ya
mwanafonolojia , lakini sifa bainifu hizi zinazochunguzwa na mwanafonolojia huwa
tayari zimeshaelezwa na mwanafonetiki. Kwa jumla tanzu hizi mbili zinauhusiano wa
moja kwa moja kwa vile zote hushughulikia sauti za lugha, lakini katika viwango
tofauti. Zote ni taalimu za kiisimu.
 Fonetiki ni tawi la isimu linalojishughulisha na uchunguzi na uchambuzi wa

taratibu na mambo yote yanayohusu utoaji, usikiaji, usafirishaji, na ufasili wa

sauti za lugha ya mwanaadamu, wakati fonolojia ni tawi la isimu ambalo

hujishughulisha na uchunguzi , uchambuzi na uainishaji wa sauti pambanuzi

ambazo hutumika katika mifumo mbalimbali ya sauti za lugha za binaadamu.

 Kazi kubwa ya fonetiki na mwanafonetiki ni pamoja na kuchunguza jinsi sauti


za Lugha zinavyotamkwa, zinavyosafirishwa kati ya kinywa cha mnenaji na sikio
la msikilizaji na jinsi zinavyotafsiriwa katika ubongo wa msikilizaji ili kutowa
ujumbe wenye maana. Mwana fonetiki pia huchunguza muundo wa mawimbi ya
sauti na jinsi yanavyoathiri hewa kwa kuangalia hali ya hewa wakati wa kutoa
sauti. Katika harakati hizi mwanafonetiki hutoa sifa mbali mbali za sauti na
kuzitambulisha, wakati kazi kubwa ya fonolojia na mwanafonolojia ni
kujishughulisha hasa na zile sauti ambazo hutumika katika kutofautisha maana za
maneno katika lugha mahsusi. Fonolojia hujihusisha na sheria au kanuni
zinazoandamana na utowaji na utumiaji wa sauti hizo pambanuzi.
 Matawi ya fonetiki ni fonetiki matamshi au fonetiki utamkaji; Tawi hili

hujishughulisha na uchunguzi wa sauti namna zinavyotamkwa na mahali ambapo

sauti hizo zinatamkiwa, yaani mahali pa matamshi. Fonetiki mawimbi sauti au

fonetiki akustika; Hili ni tawi la fonetiki ambalo hujishughulisha na jinsi

mawimbi ya sauti ya Lugha yanavyosafiri kutoka katika kinywa cha msemaji hadi

katika sikio la msikilizaji. Fonetiki masikizi au fonetik sikivu; Kimsingi tawi


hili la fonetiki hujishughulisha na jinsi utambuzi wa sauti mbalimbali za Lugha

unavyofanywa, na uhusiano uliopo baina ya sikio, neva masikizi (yaani neva

zinazohusika na usikiaji wa sauti) na ubongo. Fonetiki-tiba matamshi;Tawi hili

hujishughulisha na matatizo yanayo ambatana na usemaji au utamkaji wa sauti na

jinsi ya kuyatatua. Fonetiki kokotozi; Hii ni taaluma ambayo inachambua

mawimbi sauti na kuweza kutumia mchoro wa spektogramu kuonyesha picha ya

sauti katika vipengele vyake vya kasimawimbi. Fonetiki ushawishi; Ni taaluma

inayohusiana na kurikodi sauti kwa kutumia kinasa sauti na baadae kuchambua

kwa kusikiliza tu. Fonetiki majaribio; Inahusika na uchukuwaji wa sauti

iliyorikodiwa na kuingizwa katika kompyuta kwa ajili ya kutafuta matokeo ya

uchambuzi. Fonolojia kwa upande wake haina matawi maalumu kakini

hujishughulisha na vipengele kadhaa vya kifonolojia kama matamshi, kiimbo,

mkazo, lafudhi, toni, mfuatano wa sauti katika kuunda silabi, mfuatano wa sauti

katika kuunda mofimu, mfuatano wa mofimu katika kuunda maneno na otografia.

 Kipashio cha msingi kinachotumika katika uchunguzi katika fonetiki ni foni,

ambacho kinafasliwa kuwa ni kiungo kidogo kabisa cha sauti kisichohusishwa na

lugha mahsusi, wakati kipashio cha msingi cha kifonolojia kinachotumika katika

uchunguzi ni fonimu, ambacho kinafasiliwa kuwa n ni kipashio kidogo kabisa cha

sauti katika lugha kinachobadili maana ya neno.

 Fonetiki ni sayansi huru, kwa sababu tawi hili hutoa nadharia za sayansi halisi

kama vile bailojia na nyenginezo na hufaidi matokeo ya kiutafiti ya taaluma hizi,

kwa mfano ili kuelewa jinsi ala za sauti zinavyofanya kazi, mwanafonetiki

atafaidika na maelezo ya kibayolojia huhusu jinsi mwili wa mwanaadamu


unavyofanya kazi. Fonolojia kwa upande wake ni taaluma ya kiisimu ambayo

huongozwa na misingi na taratibu za kinadharia za kiisimu. mwanafonetiki si

lazima awe mwana isimu.

 Mwanafonetiki si lazima awe mwana isimu, wakati ambapo mwanafonolojia ni

lazima awe mwana isimu.

 “Fonetiki ni taaluma ya jumla wakati fonolojia zipo nyingi jinsi lugha zilivyo.

Kwa mfano tunafonolojia ya Kiswahili, Kidholuo, Kihehe.

 Machine hutumika katika uchunguzi wa kifonetiki, wakati ambapo kanuni za

kifonolojia hutumika katika uchunguzi wa vipashio vya kifonolojia.

7.3 Kipashio cha msingi cha fonolojia (Fonimu)


7.3.1 Maana ya fonimu: Fonimu ni vitamkwa vinavyoweza kujenga manen
yenye maana tofauti au vinavyoweza kubadili maana za maneno.
7.3.2 Uainishaji wa fonimu: Fonimu za lugha huainishwa kwa kile
kiitwacho na wana isimu kuwa ni jozi mlingano finyu, ambao unafasiliwa
kuwa ni utaratibu kulinganisha maneno mawili yenye idadi sawa ya sauti
lakini yenye tofauti ya sauti moja kwa mtazamo wa neno moja katika jozi
inayohusika.

7.3.3 Mitazamo tofauti juu ya dhanna ya fonimu:


 Fonimu kama tukio la kisaikolojia
 Fonimu kama kipashio cha kifonetiki
 Fonimu kama dhana ya kidhahania yenye utenda kazi.

M AREJELEO

Anderson, S. (1985). Phonology in Twentienth Century. Chicago University of Chicago


Press.
Besha, R (1994), Utangulizi wa Lugha na Isimu . Dar es Salaam University Press.
Godsmith, J (Mh). (1996), The hand book of Phonological Theory . Oxford: BlackWell.
Gussman, (2002), Phonology: Analysis and Theory. Cambrege: Cambredge University
Press.
Jones, J. (1957). The History ana The Meaning of the term ‘Phoneme’; Suppliment to
Le Maitre Phonetique.
Katamba, F (1989). An Introduction to Phonology: London anad Newyork:Longman.
Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam.
Lyons, J. (1971). Introduction to Theoritical Linguistics, London:Cambredge
Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004).fonolojia ya Kiswahili Sanifu (Fokisa)
Sekondari na vyuo. TUKI.
Roca, I and W. Johnson (1999), A course I Phonology.Oxford: Blackwel
Trubetzkoy, N (1973) ‘ Phonemes and how to Determine Them’ katika Fudge E(Mh)
Phonology. Penguin Education, Uk 47-73

MUHADHARA WA NANE
FONOLOJIA ARUDHI
MALENGO YA MADA
Baada ya muhadhara huu, mwanafunzi unatakiwa:-
 Kuelezea maana ya fonolojia arudhi.
 Kueleza maana ya matamshi kifonetiki
 Kueleza maana ya lafudhi
 Kueleza maana shada/mkazo katika fonolojia.
 Kufafanua dhanna ya kidatu na kiimbo katika Lugha.
 Aweze kuainisha aina na miundo mbalimbali ya silabi za lugha ya Kiswahili.
8.0 FONOLOJIA ARUDHI
8.1 Fonolojia Arudhi
8.1.1 Maana ya fonolojia arudhi
8.1.1.1 Matamshi:
 Kifonolojia matamshi ni utaratibu maalum utumikao katika utoaji wa sauti za
maneno ya lugha ya binaadamu. Matamshi huhusu lugha za wanaadamu peke
yake.
 Utaratibu wa matamshi ya sauti za lugha huzingatia mambo mawili: Mahali pa
matamshi, yaani sehemu katika mkondo wa utamkaji wa sauti mbalimbali
ambapo sauti fulani hutamkwa. Jambo la pili ni jinsi ya matamshi yaani namna
ambavyo sauti fulani hutolewa.
8.1.1.2 Lafudhi
 Lafudhi ni matamshi ya msemaji wa lugha fulani ambayo yanatokana na athari za
kmazingira.
 Mazingira hayo yanaweza kuwa eneo atokalo mtu, mahali alikosomea, kiwango
chake cha elimu
8.1.1.3 Shada/mkazo

 Ni utaratibu wa utamkaji wa maneno ambapo silabi fulani hutamkwa kwa nguvu


nyingi zaidi kuliko ilivyo katika silabi nyingine za neno hilohilo.
 Mkazo unaweza kuchukuliwa kama kilele cha kupanda na kushuka kwa sauti
katika utamkaji wa neno.
 Silabi yenye mkazo inakuwa na msikiko mkubwa zaidi kuliko silabi nyingine za
neno hilohilo.
 Lugha nyingi hasa za kibantu hazitumii mkazo. Lugha nyingi hutumia toni .
Kiswahili sanifu hakitumii toni na zaidi hutumia mkazo.
8.1.1.4 Kidatu:
 kidatu kina maana ya kiwango cha sauti isikikayo, wakati wa utamkaji ama
kuwa juu, kuwa katikati au kuwa chini.:

8.1.1.5 Kiimbo
 Ni utaratibu maalum wa upandaji na ushukaji wa mawimbi ya sauti unaojitokeza
katika utamkaji wa lugha fulani.
 Katika utaratibu wa utamkaji dhanna ya Kiimbo huandamana pia na dhanna ya
kidatu ( yaani , kiwango cha juu, cha chini au cha kati cha sauti katika usemaj),
Kwa hivyo ni muhimu hapa kueleza tofauti zilizopo baina ya kiimbo na kidatu.
Wakati kiimbo kina maana ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti ya
lugha, kidatu kina maana ya kiwango cha sauti isikikayo, wakati wautamkaji ama
kuwa juu, kuwa katikati au kuwa chini.
8.1.1.5.1 Aina za viimbo

 Kiimbo cha maelezo: Kiimbo cha maelezo ni kile ambacho kwa kawaida
msemaji wa lugha akiwa kwenye kidatu chochote kile mawimbi sauti ya usemaji
wake yanakuwa takriban katika mstari ulionyooka.
 Kiimbo cha maulizo: Kiimbo cha kuuliza hujitokeza kwa kutumia viwango
tofauti vya kidatu kutegemeana na aina ya swali linaloulizwa .
 Kiimbo cha amri: kiimbo cha amri hakitofautiyani sana na kiimbo cha
maulizo.Uchunguzi wa kifonetiki, unaonyesha kuwa katika kutowa amri,
mzungumzaji hutumia kidatu cha juu zaidi kuliko ilivyo katika kiimbo cha
maelezo.
8.1.1.6 Otografia
 Kila lugha ina mfumo tofauti wa usemaji na hutumia mfumo tofauti wa sauti .
 Kila lugha inakuwa haina budi kubuni mfumo wake wa kuziwakilisha sauti zake
katika maandishi.
 Mfumo huo wa maandishi ndio ujulikanao kama othografia.
 Mfumo huu huwa unawasilisha herufi maalumu zinazobuniwa ili kuwakilisha
sauti za lugha inayohusika kimaandishi.
 Neno utografia lina asili ya kigiriki na maana yake ni utaratibu wa kutumia alama
au michoro ya maandishi kuwakilisha sauti zisikikazo katika lugha.
8.1.1.7 Silabi:
Silabi ni kipashio cha kifonolojia kinachohusu matamshi ambacho kwacho sauti za
Lugha hutamkwa mara moja kwa pamoja kama fungu moja la sauti.
Kuna aina mbili za silabi, yaani silabi funge na silabi huru.
Silabi huru ni zile ambazo huishia irabu na silabi funge ni zile zinazoishia na
kuonsonanti. Silabi za Kiswahili sanifu mara nyingi huangukia katika kundi la silabi
huru.
8.1.1.7.1 Miundo asilia ya silabi ya Kiswahili

 Miundo ya silabi ya irabu peke yake (I).


 Miundo ya silabi ya konsonanti na irabu (KI).
 Miundo ya silabi ya nazali pekee (N)
 Miundo ya silabi wa konsonanti, konsonanti na irabu (KKI)

8.1.1.7.2 Muundo wa silabi za Kiswahili sanifu za mkopo

 Muundo wa silabi wa Konsonanti, konsonanti na irabu


 Muundo wa silabi wa kosonanti, consonanti, konsonanti na Irabu (KKKI)

Besha, R. (1994), Utangulzi wa Lugha na Isimu Dar es Salaam University Press.


Massamba, D. (2004) Kamusi ya Isimu na falsafa ya Lugha, TUKI.
Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2001).Sarufi maumbo ya Kiswahili Sanifu
(Samikisa) Sekondari na vyuo. TUKI.Dobrovolsky. M.Katamba F na O’Grady. W
(Wah.) (1997). Contemporary Linguistics An Introduction.Longman London and New
York.
Anderson, S. (1985). Phonology in Twentienth Century. Chicago University of Chicago
Press.
Godsmith, J (Mh). (1996), The hand book of Phonological Theory . Oxford: BlackWell.
Gussman, (2002), Phonology: Analysis and Theory. Cambrege: Cambredge University
Press.
Katamba, F (1989). An Introduction to Phonology: London anad Newyork:Longman.
Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam.
Lyons, J. (1971). Introduction to Theoritical Linguistics, London:Cambredge
Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004).fonolojia ya Kiswahili Sanifu (Fokisa)
Sekondari na vyuo. TUKI.
Roca, I and W. Johnson (1999), A course I Phonology.Oxford: Blackwel
Trubetzkoy, N (1973) ‘ Phonemes and how to Determine Them’ katika Fudge E(Mh)
Phonology. Penguin Education, Uk 47-73

MUHADHARA WA TISA
DHANNA YA MOFOLOJIA KWA UJUMLA

MALENGO YA MADA

 uweze kueleza maana ya mofolojia


Baada ya muhadhara huu mwanafunzi utapaswa:

 uweze kueleza maana mofu, mofimu na alomofu.


 Uweze kubainisha aina mbalimbali za mofu.
 Uweze kubainisha aina mbalimbali za alomofu
 Uweze kubainisha njia mbalimbali za kuunda maneno.
9.0 Dhanna ya Mofolojia kwa ujumla
9.1 Maana ya mofolojia:
Mofolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na maneno jinsi
yanavyoundwa, vipashio vinavyounda maneno hayo na jinsi vipashio
hivyo vinavyoainishwa.
9.2 Mofo , Mofimu na Alomofu
9.2.1 Mofu:
ni kipashio kidogo kabisa ambacho kina uwezo wa kusitiri maana ya neno ambalo
kwalo limeundwa.
Mofu ni umbo linalowakilsha mofimu katika maandishi.
Mofu ni Kipashio cha kimaumbo kinachowakilisha mofimu.
“Mofu ni umbo lenye kubeba mofimu.”

9.1.1.1 Aina za mofu kwa kuzingatia kigezo cha maana .

Mofu huru

Mofu funge

Mofu tata

9.2.1.2 Aina za mofu kwa kuzingatia kigezo cha mofololojia au maumbo

ya mofu tunapata aina mbili za mofu:

Mofu changamani/changamani

Mofu kapa

9.2.1.3 Aina za mofu kwa ujumla

Mofu huru

Mofu funge

Mofu tata

Mofu changamani/changamani.

Mofu kapa
9.2.2 Mofimu: ni maana ambayo imestiriwa/imehifadhiwa /imefichwa

nadani ya umbo la mofu

9.2.3 Alomofu:
ni maumbo mbalimbali ambayo yanasitiri maana ya aina moja.
Maumbo tofauti yanayowakilisha mofimu ya aina moja ndiyo yanayoitwa alo-mofu.

 Alomofu zinazowakilisha mofimu ya nafsi

 Alomofu zinazowakilisha mofimu ya njeo ya wakati

 Alomofu zinazowakilisha mofimu ya kutendea

 Alomofu zinazowakilisha mofimu ya kutendeka

 Alomofu zinazowakilisha mofimu ya usababishi

9.3 Neno na leksinu


9.3.1 Neno: Ni silabi au mkusanyiko wa silabi zinazotamkwa au kuandikwa ambazo
huwa na maana (maana yaweza kuwa ni ya kileksika au kisarufi.)
9.3.2 leksinu: Ni kipashio kidogo cha msamiati ambacho kinaweza kusimama peke
yake kama kidahizo katika kamusi. Ni neno lenye maana ya kileksika
9.4 Mzizi na shina
9.4.1 Mzizi: ni sehemu ya neno ambayo haibadiliki wakati neno hilo
linaponyambuliwa katika hali tofauti.
9.4.2 Shina: ni sehemu ya neno ambayo huongezwa viambishi fuatishi (tamati) au ni
sehemu ya neno ambayo hubakia baada ya kuondolewa viambishi tangulizi
9.5 Mofimu na leksimu
9.5.1 Mofimu: ni maana ambayo imestiriwa/imehifadhiwa /imefichwa nadani ya

umbo la mofu

9.5.2 Leksimu: Ni kipashio kidogo cha msamiati ambacho kinaweza kusimama peke
yake kama kidahizo katika kamusi. Ni neno lenye maana ya kileksika

9.6 Njia za kuunda Maneno


-Uambishaji na Unyambuaji

-Uambatishaji
-Udurufishaji
-Akronimu
-Uhulutishaji
- Uundaji wa maneno mapya.

Lyons, J. 1970 (Mh.) New Horizons in Linguistics Mary land/Middlesex; Penguin

Books.

Mathews, P. II 1970. Recent Development in Morphology. Katika Lyons, J. Uk. 96-

114.

Schachter, P. 1985 “Parts of speech Systems”. Katika T- Shopen (mh), Language

Typology and Sytactic Description, Juzuu 1. Cambridge. University Press Uk, Uk-3-

61.

Stump, G. 1998. “Inflection”. Katika Spencer. A na Zwicky, A. The Handbook of

Morphology. Oxford: Black well Pubishers Ltd.

MUHADHARA WA KUMI
MALENGO YA MUHADHARA


Mwishoni mwa muhadhara huu wanafunzi unatakiwa:

 Uweze kueleza maana ya vivumishi na kuainisha aina mbalimbali za


Uweze kueleza maana ya nomino na kuainisha aina mbalimbali za nomino.


nvivumishi.


Uweze kueleza maana ya vitenzi na kuainisha aina mbalimbali za vitenzi.
Uweze kueleza maana ya viunganishi na kuainisha aina mbalimbali za


viunganishi.


Uweze kueleza maana ya viwakilishi na kuainisha aina mbalimbali za viwakilishi.


Uweze kueleza maana ya vihusishi na kuainisha aina mbalimbali za viunganishi.
Uweze kueleza maana ya viingizi na kuainisha aina mbalimbali za viingizi.
AINA ZA MANENO NA UAINISHAJI WAKE
10.0 AINA ZA MANENO NA UAINISHAJI WAKE
10.1 Nomino
10.1.1 Maana ya Nonimo :
10.1.2 Aina za nomino:
 Nomino za pekee: Nomino za pekee hutaja na kutambulisha nomino mahsusi
na za kipekee. Yaani kuwa kitu ni hicho na wala si chengine chochote. Hizi ni
nomino zinazohusisha majina kama vile ya watu, nchi, miji, mito, milima,
maziwa na bahari. Herufi za kwanza za nomono za pekee huwa kubwa hata kama
nomino hizi zinapatikana katikati ya sentensi.
 Nomino za kawaida: Hizi kwa jina jengine huitwa nomino za jumla. Nomino hizi
hazibainishi wazi wazi vitu ambavyo habari zake zinatolewa. Kwa mfano ikiwa ni
mtu, mahsusi hatambuliwi. Haituambii kama ni Kelvin, Tuafu ama Zawadi.Ikiwa
ni ziwa halitambuliwi kama ni Michigan , Victoria au Nyasa, yaani hutaja vitu
bila kutaja umahsusi wake kama ilivyo katika nomino za pekee. Hizi
zinapoandikwa si lazima zianze na kwa herufi kubwa ispokuwa zimetumiwa
mwanzoni mwa sentensi au zimetumika kama anuani ya kutajia kitu kama vile
Mkuu wa Sheria. Katika mfano huu ‘sheria’ kwa kawaida ni nomino ya kawaida,
lakini hapa inaanza kwa herufi kubwa kwani inataja anuwani ya kipekee.
 Nomino za mguso: Nomino za mguso hurejelea vitu vinavyoweza kuhusika na
mwanaadamu kupitia milango ya hisia kama macho, mapua, masikio vidole na
ulimi- yaani vitu vinavyoweza kushikika, kuonekana, kunusika na kuonjeka.
Nomino za jamii: Hizi ni nomino ambazo zinawakilisha vitu vingi katika jina moja,
yaani nimino zinazotaja umla ya vitu vingi.
Nomiono dhahania: Kundi hilo la nomino hutumia kigezo cha uwezekano wa
kuhesabika kuziainisha. Hapa tunatofautisha kati ya nomino zinazowakilisha vitu
vinavyohesabika kwa upande mmoja, na vile visivyohesabika kwa upande
mwengine. Nomino ya vitu vinavyohesabika vitanda, nyumba, vikombe vitabu na
kadahlika. Zile zisizohesabika hurejelea vitu ambavyo hutokea kwa wingi na
haviwezi kugawika, kwa mfano maji, mate, makamasi, maziwa, moshi, mafuta.
Aghlabu nomino hizo huwa sawa katika umoja na wingi.
Nomino za kitenzi jina: Hizi ni nomino zinazohusu vitenzi . Huundwa kwa
kuongezwa kiambishi {ku-} cha unominishaji kwenye mzizi wa kitenzi cha
kitendo halisi ili kukifanya kiwe nomino.
10.2 Vivumishi
10.1.1 Maana ya kivumishi:
10.1.2 Aina za vivumishi.
 Vivumishi vya sifa: hutoa sifa za nomino /kiwakilishi cha nomino. Sifa hizi
huweza kuwa nzuri , mbaya au yoyote ile.

 Vivumishi vya idadi: vinaweza kujitokeza katika aina tatu ndogondogo.


-Vivumishi vya aina hii hutoa taarifa kuhusu idadi ya nomino ambazo kiwango chake
kimetajwa.
- vivumishi vya idadi vinavyoweza kuvumisha nomino kwa kutaja idadi ya nomino
hizo kiujumla jumla bila kudhihirisha idadi halisi.
vivumishi vya idadi ambavyo huonyesha nafasi iliyochukuliwa na nomino fulani katika
orodha.
 Vivumishi vya kumiliki:-
Ni vivumishi vinavyoonesha kuwa kitu fulani kina milikiwa na mtu au kitu chengine.
 Vivumishi Vioneshi:-
vivumishi vya aina hii huonyesha mahali au upande kitu kilipo. Vivumishi vya aina hii
hujengwa na mzizi {h} kwa vitu vilivyopo karibu na mzizi {le} kwa vitu vilivyo mbali.
 Vivumishi vya kuuliza
Hivi ni vivumishi ambavyo hufafanua nomino kwa kuuliza habari zake. Hujibu swali
“gani?ipi? ngapi?”
Vivumishi vya pekee:
Vivumishi hivi huitwa vya pekee kwa sababu kila kimojawapo huwa na maana maalumu.
Pia kila kimojawapo huchukua upatanisho wake wa kisarufi kulingana na ngeli ya
nomino ambayo kinaivumisha. Mizizi vivumishi hivi ni ote, o-ote, -enye, -enyewe, -
ingine, -ingineo.
-ote
Huonyesha ujumla wa kitu au vitu
-o-ote
Kivumishi cha aina hii kina maana ya “kila”, “bila kubagua”
– enye
Kivumishi cha aina hii hutumika kuleta dhanna ya umilikishaji nomino Fulani.
- enyewe
Kivumishi cha aina hii hutumika kuisisitiza nomino fulani.
– ingine
Kivumishi cha aina hii huonyesha/huonesha ‘tofauti na’ au ‘zaidi ya’ kitu fulani
– ingineo
Kivumishi cha aina hii hutumika kuonesha/kuonyesha ziadi.

 Vivumishi vya A- unganifu


Vivumishi vya aina hii huundwa kwa mzizi wa kihusishi a- unganifu. Kihusishi hiki
huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho huvumisha nomino iliyotajwa
awali. Vivumishi vya aina hii hutumika kuleta dhanna zifuatazo:-

-Umilikaji
-Nafasi katika orodha
 Vivumishi vya jina kwa jina
Hizi ni nomino zinazotumika kama vivumishi ambazo hutumika kufafanua nomino .

10.3 Vielezi
10.3.1 Maana ya vielezi: Vielezi ni maneno yanayofafanua vitenzi, vivumishi au
vielezi vyengine. Huweza kuarifu kitendo kilichotendeka kilitendeka wapi , namna
gani na hata mara ngapi?
10.3.2 Aina za vielezi
 Vielezi vya namna au jinsi.
Vielezi vya namna hii huonyesha jinsi au namna kitendo kilivyotendeka. Vielezi vya
namna vipo vya aina kadhaa.
- Vielezi vya namna halisi.
Hivi ni vielezi vinavyotumia maneno ambayo kimsingi yana sura ya vielezi moja kwa
moja katika uainishaji wa aina za maneno.

-Vielezi vya namna mfanano


Hivi ni vielezi ambavyo hutumika kufananisha vitendo na vivumishi au nomino
mbalimbali. Hujengwa kwa kuongeza kiambishi (ki-) au kiambishi (vi-). Viambishi hivi
hujulikana kwa jina la viambishi vya mfanano.
Ulifanya viuzuri kumsaidia mwanangu.

-Vielezi vya namna vikariri


Hivi ni vielezi ambavyo hufafanua vitenzi kwa kurudiarudia neno moja mara mbili.

- Vielezi vya namna hali


Hivi ni vieelezi ambavyo hufafanua juu ya kitendo kilichotendeka kimetendeka katika
hali gani.
- Vielezi vya namna ala/kitumizi
Hivi ni vielezi vinavyotaja vitu ambavyo hutumika kutendea kitendo.

- Vielezi vya namna viigizi.


Hivi vinaelezea zaidi jinsi tendo lilivyofanyika kwa kuigiza au kufuatisha sauti
inayojitokeza wakati tendo linapofanyika au kutokea.

 Vielezi vya idadi


Vielezi vya namna hii huonyesha kuwa kitendo kilitendeka mara fulani au kwa kiasi
fulani.

 Vielezi vya mahali.


Vielezi vya namna hii huonyesha mahali ambapo kitendo kinatokea.Huweza kudokezwa
kwa viambishi au kwa maneno kamili.
 Vielezi vya wakati:
Vielezi vya namna hii huonyesha wakati wa kutendeka kwa kitendo.Huweza kutokea
kama maneno kamili au hodokezwa kwa kiambishi {po.}

10.4 Vitenzi
10.4.1 Maana ya vitenzi:

 Kitenzi ni neno linaloeleza jambo lililotendwa au lililotendeka.


 Kitenzi huarifu lililofanyika au lililofanywa na kiumbe hai chochote kinachoweza
kutenda jambo.
10.4.2 Muundo wa kitenzi cha Kiswahili
Kitenzi cha Kiswahili huundwa na mzizi pamoja na viambishi vyenye
uamilifu wa aina tofauti.

 Vitenzi halisi: Hivi ni vitendo ambavyo huonyesha kutendeka


10.4.3 Aina za vitenzi

kwa kitendo.Wakati mwingine vitenzi hivi huitwa vitenzi vya


kutenda.
-vitenzi elekezi: Hivi ni vitendo vya kutenda, ambavyo vinaweza
kuchukuwa kitendwa/kitendewa (Yambwa). Muundo wake unadokeza
kuw, kuna kitendwa au kitu kinachoelezewa tendo hilo.
-vitenzi visivyoelekezi: Hivi ni vitendo vya kutenda, ambavyo
havichukuwi kitendwa/kitendewa (Yambwa). Muundo wake
haudokezi uwezekano wa kuwepo kwa yambwa. Tendo halielekezwi

 Vitenzi vishirikishi
kwa yoyote.

10.4.4 Aina za vitenzi halisi


 Vitenzi vikuu: Vitenzi vikuu ni vile ambavyo hubeba ujumbe


muhimu wa kiarifu cha sentensi.
Vitenzi visaidizi: Hivi hutoa taarifa ya kusaidia vitenzi vikuu.
Hutoa taarifa kama vile uwezekano , wakati, hali n.k.Vitenzi
visaidizi daima hutumika na vitenzi vikuu, ndivyo vinavyobeba
viambishi vya wakati.
10.4.5 Vitenzi vishirikishi: Hivi ni Vitenzi vishirikishi ambavyo vilevile

 Vitenzi vishirikishi vipungufu: Hivi ni vitenzi vishirikishi


sielekezi. Vitenzi hivi hufanya kazi ya kuunga sehemu mbili za sentensi.

ambavyo havichukui viambishi vya nafsi, njeo ama hali.


Vitenzi vishirikishi vipungufu ni vya aina mbili, ambavyo ni
kitenzi kishirikishi “ni” cha uyakinishi na kitenzi shirikishi

 Vitenzi
“si” si cha ukanushi.
vishirikishi vikamilifu:Hivi huchukuwa
viambishi viwakilishi vya nafsi, njeo na hata hali.
10.4.5.1 Kazi za kitenzi kikuu:
-kueleza tendo linalofanywa na mtenda/mtendwa.
- kuonyesha wakati tendo linapotendeka
- kuonyesha hali ya tendo
- Kuonyesha nafsi
- kuonyesha kauli mbali mbali za tendo
-Kuonyesha urejeshi wa mtenda/mtendwa/ mtendewa/ kujitendea
10.4.5.2 Kazi za kitenzi kishirikishi
-kushirikisha vipashio vyengine katika sentensi
-Kuonyesha tabia fulani iliyopo au isiyokuwepo ya mtu Fulani au
kitu fullani.
-Kuonyesha cheo au kazi anayofanya mtu.
-kuonyesha sifa za mtu.
- kuonyesha umoja wa vitu au watu
-kuonyesha mahali
-kuonyesha msisitizo
-kuonyesha umilikishi wa kitu chochote.
10.4.5.3 Aina za wakati katika kitenzi.
-wakati uliopita
-wakati uliopo
-wakati ujao
10.4.5.4 Hali mbalimbali za kitenzi
-Hali ya masharti
-Hali ya kuendelea kwa tendo
-hali ya kutarajia, kuamuru na kuhimiza

10.5Viwakilishi
10.5.1 Maana za viwakilishi: Viwakilishi ni aina ya neno linaloweza
kutumika badala ya jina .
10.5.2 Aina za viwakilishi
Zifuatazo ni baadhi ya aina ya viwakilishi na mifano yake.
 Viwakilishi vioneshi au viwakilishi vya kuonesha
 Viwakilishi vya nafsi ambavyo vipo vya aina tatu; amba
-viwaakilishi nafsi huru
-viwakilishi –nafsi viambata
-viwakilishi –nafsi rejeshi

 Viwakilishi vya kuuliza/viwakilishi viulizi ambavyo huashiriwa na mofu /


kiambishi {-pi} ambavyo katika tungo hutanguliwa na kiambishi ngeli cha jina
husika.
 Wiwakilishi vya urejeshi ambavyo vinajengwa na shina amba pamoja na
vipande vidogo vidogo –ye-, -o-, -cho-, vyo, lo, po, mo, ko n.k ambavyo
vinachaguliwa kilingana na ngeli ya majina yanayorejeshwa navyo.
 Viwakilishi vya idadi: Viwakilishi hivi hutuarifu kuhusu idadi ya nomino hiyo
huweza kuwa kamili (halisi) au ya jumla.
 Viwakilishi vya pekee:- Hivi ni aina ya vivumishi vya pekee kuwakilisha
nomino. Hufuata sheria za upatanisho za nomino zinazowakilishwa.
 Viwakilishi vya A-unganifu:-
Viwakilishi hivi huundwa kwa kihisishi cha A-unganifu kusimamia nomino
iliyomilkiwa, inayochukuwa nafasi fulani katika orodha au nomino ya aina fulani.
kihisishi a-unganifu huandamana na nomino kuunda kirai husishi ambacho husimama
mahali pa nomino.
 Viwakilishi vya sifa
Haya ni maneno ya sifa ambayo huchukua nafasi ya nomino katika setensi.

10.6 Viunganishi
10.6.1 Maana ya viunganishi. Ni maneno, kikundi cha maneno au kiambishi
chenye kuunganisha maneno, kirai, kishazi au sentensi.Dhima ya kiunganishi ni kuunga
vipashio viwili au zaidi vyenye hadhi sawa kisarufi.

10.6.2 Aina za viunganishi:


 viunganishi huru: hivi ni viunganishi vinavyosimama pekee katika tungo,
katikati ya vipashio vinavyo ungwa.
-Viunganishi nyongeza/vya kuongeza
- Viunganishi vya sababu/visababishi
- Viunganishi vya uteuzi/chaguo
- Viunganishi linganishi/vya kinyume
- Viunganishi vya wakati
- Viunganishi vya masharti
- Viunganishi vihusishi
 Viunganishi tegemezi: ni viambishi ambavyo hutiwa katika kitenzi cha kishazi
tegemezi ili kukiunga na kitenzi kikuu cha kishazi huru ambavyo kwa pamoja
huunda sentensi changamano au shurtia.
10.7 Vihusishi:
Ni maneno ambayo huonyesha uhusiano uliopo baina ya neno moja na jengine.
Vihusishi aghlabu huonyesha uhusiano kati ya nomino au kirai nomino na maneno
mengine.
10.7.1 Mambo mbalimbali yanayoweza kuonyeshwa na vihusishi
- huonyesha uhusiano wa kiwakati
- huonyesha uhusiano wa mahali
- huonyesha uhusiano wa kulinganisha
- huonyesha uhusiano wa umilikaji
- huonyesha uhusiano wa sababu/kiini
10.7.2 Aina za vihusishi
-vihusishi vya wakati
-vihusishi vya mahali
- vihusishi vya ulinganishi/ vya kulinganisha
-vihusishi vya sababu/ kusudi/nia
-vihusishi vya ala (kifaa)-kwa
- vihusishi vimilikishi
-vihusishi vya namna/jinsi/hali
-vihusishi ‘na’ cha mtenda
10.7.3 Matumizi ya ziada ya kihusishi “kwa”
-kihusishi hiki huonyesha mahali au upande
-kihusishi hiki huonyesha sababu au kisababishi cha jambo
-kihusishi hiki huonyesha wakati
-kihusishi hiki huonyesha sehemu Fulani ya kitu kikubwa
-kihusishi hiki hutumika kuonyesha ‘nia ya pamoja na’
-Kihusishi hiki huonyesha jinsi kitendo kilivyotendeka
10.7.4 Viingizi: Ni maneno ambayo hutumiwa kuwakilisha hisia fulani.
10.7.5 Aina za viingizi: Viingizi vinaweza kugawanywa kwa kutumia vigezo vya
kisemantiki. Mkabala huuunatumika kuvigawa viingizi kulingana na maana
zinazowakilishwa na viingizi. Maana hizo ni hisia zinazobebwa na viingizi hivyo.
 Viingizi vinavyoonyesha mhemko au hisi kali
-viingizi vya furaha
-viingizi vya huzuni
-viingizi vya mshituko
-viingizi vya mshangao
 Viingizi vya maamrisho au msisitizo wa jambo au tukio.
 viingizi vya maadili
-viingizi vya mwiitiko
-viingizi vya ombi
-viingizi vya bezo
-viingizi vya kutakia heri
-viingizi vya kukiri afya/jambo
-viingizi vya kiapo
-viingizi vya salamu
Marejeleo:
Besha, R. (1994), Utangulzi wa Lugha na Isimu Dar es Salaam University Press.
Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam.
Massamba, D. (2004) Kamusi ya Isimu na falsafa ya Lugha, TUKI.
Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2001). Sarufi maumbo ya Kiswahili Sanifu
Masebo, J.A na Nyangwine, N,(2009) Nadharia ya Lugha KISWAHILI 1 Nyamburi
Nyangwine Publishers, Dar-Es Salaam, Tanzania.

MUHADHARA WA KUMI NA MOJA


UAMBISHAJI NA UNYAMBULIHAJI

MALENGO YA MUHADHARA

 Uweze kueleza maana ya Uambishaji


Mwishoni mwa muhadhara huu mwanafunzi unatakiwa:-

 Uweze kueleza maana ya viambishi


 Uweze kueleza aina mbalimbali za viambishi
 Uweze kubainisha dhima mbalimbali za viambishi
11.0 uaimbishaji na unyambulishaji.
11.1 Maana ya uambishaji: Uambishaji ni ule utaratibu wa kuongeza
viambishi katika mzizi wa neno, ili kulipa neno maana ya ziada.
11.I.1 Viambishi: Kiambishi ni sehemu (mofo) ambayo huambikwa kwenye
mzizi wa neno ili kulipa neno maana ya ziada.

 Kwa kuzingatia nafasi zikaamo vianmbishi katika neno


11.1 .1.1 Aina ya viambishi:

- viambishi awali
- viambishi kati
-viambishi tamati


11.1.1.1.1 Aina za viambishi kiuamilifu
Viambishi vya nafsi
Nafsi ya kiima:


Nafsi ya yambwa
Viambishi nyambulishi
-Vya vitenzi


-Vya nomino:
Viambishi vya njeo
-viyakinishi
- vikanushi



Viambishi Vya Hali
Viambishai vya upatanishi wa kisarufi.

11.1.1.1.2 Aina za uambishaji


 Unyambuaji au unyambulishi : Huu ni aina ya uambishaji


unaosababisha neno kubadilika kutoka katagoria moja hadi nyingine.
Mnyambuliko :Ni aina ya uambishaji ambao huhusisha kurefusha neno
na kuliweka katika hali tofauti za katagoria ilelie.

Besha, R. (1994), Utangulzi wa Lugha na Isimu Dar es Salaam University Press.


Massamba, D. (2004) Kamusi ya Isimu na falsafa ya Lugha, TUKI.
Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2001).Sarufi maumbo ya Kiswahili Sanifu

(Samikisa) Sekondari na vyuo. TUKI.

Dobrovolsky. M.Katamba F na O’Grady. W

Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam.

Lyons, J. (1971). Introduction to Theoritical Linguistics, London:Cambredge


Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004) fonolojia ya Kiswahili Sanifu (Fokisa)
Sekondari na vyuo. TUKI.

Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam.

Lyons, J. (1971). Introduction to Theoritical Linguistics, London:Cambredge

Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004) fonolojia ya Kiswahili Sanifu (Fokisa)


Sekondari na vyuo. TUKI.

Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004).Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu


Samakisa Sekondari na vyuo. TUKI.

MUHADHARA WA KUMI NA MBILI

TUNGO ZA KISWAHILI NA UCHAMBUZI WAKE

MALENGO YA MUHADHARA
Mwishoni mwa muhadhara huu mwanafunzi unatakiwa:
Uweze kueleza maana ya tungo
Uweze kubainisha aina mbali mbali za tungo
Uweze kueleza maana ya neno na uainishaji wake
Uweze kueleza maana ya kirai na uainishaji wake
Uweze kueleza maana ya kishazi na uainishaji wake
Uweze kueleza maana ya sentenzi na uainishaji wake

12.0 TUNGO ZA KISWAHILI NA UCHAMBUZI WAKE


12.1 Maana ya tungo: Ni kipashio cha kisarufi kilichoundwa kwa kuunganisha
pamoja vipashio vidogovidogo vilivyo chini yake.
12.2 Aina za tungo:
12.2.1 Tungo neno: Tungo neno na uainishaji wake imeelezwa kwa kina
katika sura ya 10.
12.2.2 Tungo Kirai: ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja au zaidi lakini
ambacho hakina muundo wa kiima kiarifu.
12.2.2.1 Sifa za Kirai
Hapa tunakusudia kuainisha sifa kumi za viai
 Kirai huwa ni kipashio cha kimuundo kisichokamilika ; yaani ni kipashio
kisichokuwa na muundo wa kiima – kiarifu kama zilivyo sentensi ambazo
zinahusisha mtendaji wa tendo na tendo linalotendwa.
 Kirai huainishwa kimuundo kulingana na neno kuu la kirai husika.
 Kirai ni tungo, yaani ni aina moja wapo ya tungo, aina nyengine za tungo ni neno,
kishazi na sentensi.
 Kirai hudokeza maana, lakini maana hiyo si kamili.
 Maneno katika kirai lazima yapangwe kimantiki kwa mpangilio unaokubalika
katika sarufi ya lugha husika.
 Japo virai huainishwa kimuundo, huweza kutumika kutekeleza majukumu
mbalimbali ya kisarufi.
 Kirai huweza kutokea upande wowote, wa kiima au kiarifu katika sentensi.
Kirai ni kikubwa ku

12.2.2.2 Aina za virai


Kama tulivyobainisha hapo juu aina ya virai hukitwa katika aina za maneno ambazo
ndizo chimbuko la mahusiano maalumu ndani ya vipashio hivyo.
 Kirai nomino (KN)
Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa kwenye nomino au mahusiano ya
nomino na neno au mafungu ya maneno.
 Kirai kitenzi (KT)
Kirai-kitenzi ni kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi au katika mahusiano ya
Kitenzi na neno au mafungu mengine ya maneno.Hii in maana kuwa neno kuu
katika aina hii ya virai huwa ni kitenzi.
 Kirai kivumishi (KV)
Kirai-kivumishi ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika kivumishi. Kwa
kawaida muundo huu huwa ni wa kivumishi na neno au fungu la maneno
linaloandamana nacho.
 Kirai Kielezi (KE)
Tofauti na aina nyengine ya virai miundo ya virai vielezi haielekei kukitwa kwenye
mahusiano ya lazima baina ya neno kuu (yaani kielezi ) na neno au fungu la maneno
linaloandamana nalo. Badala yake miuundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo
hufanya kazi pamoja katika Lugha kama misemo, neno au maneno yanayofuata neno
lililotangulia yakifafanua zaidi neno hilo.
 Virai viunganishi (KV)
Ni kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina ya kwa na katika,
au kwenye na fungu na fungu la maneno linaloandamana nacho. Kwa maneno mengine
kirai hicho ni kile ambacho neno kuu ni kiunganishi.

12.2.3 Tungo kishazi: Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho chaweza


kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa
na kitenzi kisichoweza kujitegemea wenyewe.


12.2.3.1 Sifa za kishazi:


Kishazi hupatikana katika/ ndani ya sentensi.
Lazima kishazi kiwe na kitenzi, sehemu yoyote ya sentensi isiyo na kitenzi,
haiwezi kuwa kishazi. Kishazi huru hutawaliwa na kishazi kikuu na kishazi


tegemezi hutawaliwa na kishazi tegemezi.
Baadhi ya vishazi huweza kujitegemea kama sentensi hata vikiondoshwa
katika muktadha wa sentensi kuu. Kishazi kinachoweza kujisimamia kama
sentensi huitwa kishazi huru kikiwa ndani ya sentensi kuu na huitwa “sentensi


sahili” kikiwa sentensi inayojitegemea.
Baadhi ya vishazi haviwezi kujitegemea kama sentensi ikiwa vitaondoshwa


katika muktadha wa sentensi kuu.


Vishazi vingi, hata vishazi huru huwa na kiima dhahiri.
Kishazi kwa kawaida, hasa kishazi huru huwa na kitenzi kimoja kikuu.
Kitenzi hicho huweza kuandamana na kitenzi kisaidizi. Pia, kitenzi katika


kishazi huweza kuwa kitenzi kishirikishi.


Kishazi hutekeleza majukumu mbalimbali ya kisarufi.
Tofauti ya kishazi na sentensi ni kwamba kishazi hupatikana ndani ya sentensi
lakini sentensi hujisimamia kimuundo na kimaana.Kishazi huwa na kiarifu
kimoja na kiima kimoja, Lakini sentensi huweza kuwa na kiima kimoja.


12.2.3.2 Aina za vishazi
Vishazi huru:Kishazi huru ni kishazi kinachotaewaliwa ka kitenzi
kikuu, ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe kamili usiohitaji maelezo
zaidi ya kukamilisha maana. Ni kishazi ambacho hata kikiondolewa
katika muktadha wa sentensi ambamo vimejikita huweza kujitegemea
kama sentensi.
 Vishazi tegemezi: Kishazi huru ni kishazi kinachotaewaliwa ka
kitenzi kisaidizi, ambacho muundo wake hukifanya kutegemea kitenzi
cha kishazi huru ili kuweza kutoa ujumbe uliokusudiwa. Kishazi
tegemezi peke yake hakitowi ujumbe unaojitosheleza.
12.2.3.3 Sifa za Kishazi tegemezi:
-Kishazi tegegemezi kutoa maana kamili kinapoandamana na kishazi
huru.
-Kishazi tegemezi kinaweza kufutwa katika sentensi bila kuharibu maana
ya sentensi
nzima.
-Kishazi tegemezi hutambulishwa na viambishi vya utegemezi
Vinavyoambatanishwa kwenye kitenzi.
-Kishazi tegemezi vile vile kinaweza kutambuliwa kwa kuwepo vishazi
kama vile
ingawa, kwamba, ili, kwa sababu, mzizi wa amba, mofu ya masharti n.k

 Vishazi tegemezi vivumishi


12.2.3.4 Aina ya vishazi tegemezi

-Vishazi tegemezi vinavyotokea pamoja na nomino inayovumishwa.

 Vishazi tegemezi vielezi


-Vishazi tegemezi visivyoambatana na nomino inayovumishwa

-vishazi tegemezi vya mahali


-vishazi tegemezi vya wakati
-vishazi tegemezi vya namna au jinsi
-vishazi tegemezi vya masharti
-vishazi tegemezi vya hali, hitilafu au kasoroiliyoko katika tendo.
-vishazi tegemezi vya sababu/chanzo

12.2.3.5 Dhima na hadhi ya vishazi


Kishazi chaweza kuwa huru kikajitegemea wenyewe kwa kuwa na maana kamili
inayojitosheleza. Lakini kuna vishazi ambavyo havijitoshelezi wenyewe, bali hutegemea
vishazi vingine.Kishazi huru kina hadhi ya sentensi (sahili). Kishazi tegemei hakina
hadhi hii, vishazi tegemezi ambavyo hutegemea vishazi vingine hushuka daraja
nakuchukuwa dhima ya kikundi. Baadhi ya vishazi tegemezi huchukuwa dhima (hufanya
kazi) ya kivumishi katika tungo ambayo kwa kawaida ni dhima ya kikundi au neno.
Vishazi hivi huvumisha nomino katika tungo hiyo.

12.2.4 Sentensi: sentensi nin kifungu cha maneno kuanzia neno moja na kuendelea
chenye kiima na kiarifu na inaleta maana kamili.
12.2.4.1 Sifa za sentensi
-Sentensi lazima iwe na mpangilio wa maneno ambao unakubalika na
wazungumzaji wa lugha husika.
- Sentensi lazima ikamilike kimaana, kimuundo na kisarufi.
- Sentensi huwa na muundo wa kiima na kiarifu /huwa nakirai
nomino na kirai kitenzi.
-Sentensi huweza kuwa na zaidi ya kiima kmoja na kiarifu zaidi ya kimoja.
-Sentensi inaweza kuundwa na kitenzi kikuu kimoja au zaidi.
-Sentensi inaweza kuundwa na kishazi huru kimoja au zaidi na kishazi
tegemezi kimoja au zaidi.
-Sentensi huonyesha halio mbalimbali, kama vile amri, ombi, mshangao,
swali n.k

 Kiima: Ni sehemu katika sentensi ambayo hujaza sehemu ya mtenda


12.2.4.3 Muundo wa sentensi kimapokeo/kikazi/kidhima

au mtendwa wa jambo linaloelezwa. Katika tungo kiima hutokea


kushoto mwa kitenzi.
Kiarifu: Ni sehemu katika sentensi inayojazwa na maneno yanayo
arifu tendo lilofanywa, linapofanywa au litakapofanywa. Kiarifu
ndiyo sehemu ndiyo sehemu muhimu zaidi katika sentensi ambayo
wakati mwengine huweza kusimama pekee, kwani wakati mwengine
huchukuwa viwakilishi vya kiima.
12.2.4.2 Vipashio vya kiima
- Nomino peke yake
- Nomino, kiunganishi na nomino
- Nomino na kivumishi
- Kivumishi na nomino
- Kiwakilishi peke yake
- Kiwakilishi na kivumishi
- Nomino na kishazi tegemezi vumishi
- Kitenzi jina
- Nomino na vivumishi zaidi ya kimoja
- Kitenzi jina na nomino
- Umbo kapa
12.2.4.3 Taarifa zitolewazo na kiarifu kuhusu kiima
-kiima ni nani
-kiima kina nini
-kiima hufanya nini
- kiima kinahisi nini
12.2.4.4 Sifa za kiarifu:
-Huwa na kitenzi nap engine na maneno mengine.
-Kiarifu kwa kawaida huja baada ya kiima
12.2.4.5 Vipashi vya kiarifu
- Kitenzi kikuu peke yake.
-Kitenzi kisaidizi au vitenzi visaidizi vilivyosambamba na kitenzi
kikuu.
-Kitenzi kishirikishi na kijalizo
-yambwa (shamirisho)
-kijazalio
-chagizo
12.2.4. 6 Sifa za chagizo
Chagizo kwa kawaida
-Chagizo kwa kawaida huwa ni kielezi au kirai husishi ambacho kinafanya kazi kama
kielezi.
-Kwa kawaida ni vipashio vya ziada. Si lazima viwepo katika sentensi ili ijisimamie.
-Huwa cha lazima akiwa kinafuata kitenzi kishiriki. Hali ikiwa hivyo, kinatika kama
kijalizo.
- Hutumika kufafanua kitenzi/kivumishi /kielezi.
- Hutumika kujaliza kiima/kama kijalizo.

12.2.5 Muanisho wa sentensi


Kuainisha sentensi kulingana na uamilifu wake kimawsiliano
-sentensi za taarifa
-sentensi ulizi
-sentensi agizi
-sentensi hisishi
-sentensi ya masharti
-sentensi za rai
-sentensi za kukanusha
-sentensi tatanishi
12.2.6 Aina za sentensi kimuundo
12.2.6.1 Sentensi sahili
Miundo ya sentensi sahili
-muundo wa kitenzi kikuu peke yake.
-muundo wa kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi
-muundo wa kirai-nomino nakira-tenzi
-muundo wa vira-vitenzi vilivyokitwa katika kitenzi ‘kuwa’
-miundo ambamo virai-nominona vimeandamana na vijalizo

12.2.7 Sifa za sentensi sahili


-Ina kiima ambacho kimetajwa wazi au kimeachwa kutajwa kwa
kuwa kinaeleweka.
- Ina kiarifu ambacho kimeundwa na kitenzi kikuu kimoja au
kitenzi kikuu na kitenzi kisaidizi au kitenzi kishirikishi na kijalizo
na chagizo.
- haifungamani na sentensi nyingine na hivi inajitosheleza
kimuundo na kimaana.
12.2.7.1 Sentensi changamano: Hii ni sentensi yenye kishazi huru
kimoja au zaidi na kishazi tegemezi kimoja au zaidi. Sifa moja kubwa
ya sentensi changamano ni kuwa na kishazi tegemezi ambacho
hutegemea kishazi kingine huru ndani ya sentensi hiyo. Msingi muhimu
wa uhusiano ndani ya sentensi hizo ni ule wa kishazi kimoja kutegemea
kingine.
Miundo ya sentensi changamano
-muundo yenye vishazi virejeshi.
-muundo yenye vishazi vielezi

12.2.8 Sentensi ambatano: Hii ni sentensi inayojengwa na sentensi mbili


au zaidi zilizounganishwa kwa kutumia viunganishi kama vile likini,
wala, au nakadhalika.

Miundo ya sentensi changamano


-miundo yenye sentensi sahili tu.
-miundo yenye sentensi sahili na changamano
-miundo yenye sentensi changamano tu
-miundo yenye vishazi visivyounganishwakwa viunganishi.

 Hatua za uchanganuzi wa sentensi


12.2.9 Uchanganuzi wa sentensi

-kutaja aina ya sentensi, yaani kama ni sahili, changamano au ambatano.


- Kutaja sehemu zake kuu, yaani kiima na kiarifu au kirai nomino na kirai kitenzi.
- Kutaja sehemu kuu za kiima na kiarifu au sehemu kuu za kirai nomino na kirai
kitenzi.

 Mikabala ya uchanganuzi
-Kutaja sehemu zote za maneno yaliyomo katika sentensi hiyo.

i) Mkabala wa kikazi/kimapokeo
-njia ya mishale/mistari
-njia matawi
-visanduku/jeduweli.
-njia ya maneno/maelezo
ii) Mkabala wa kimuundo/kimambo leo
-njia ya mishale/mistari
-njia matawi
-visanduku/jeduweli.
-njia ya maneno/maelezo

Besha, R. (1994), Utangulzi wa Lugha na Isimu Dar es Salaam University Press.


Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam
Massamba, D. (2004) Kamusi ya Isimu na falsafa ya Lugha, TUKI.
Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2001).Sarufi maumbo ya Kiswahili Sanifu

(Samikisa) Sekondari na vyuo. TUKI.

Masebo, J.A na Nyangwine, N,(2009) Nadharia ya Lugha KISWAHILI 1 Nyamburi


Nyangwine Publishers, Dar-Es Salaam, Tanzania.
MUHADHARA WA KUMI NA TATU
NGELI ZA NOMONO NA UAINISHAHI WAKE PAMOJA NA
DHANNA YA O-REJESHI.

MALENGO YA MUHADHARA
Mwishoni mwa muhadhara huu mwanafunzi unatakiwa:
Uweze kubainisha vigezo mbalimbali vinavyotumika kuainisha ngeli za nomino
Uweze kueleza maana ya O-rejeshi
Uweze kubainisha masharti ya upachikaki wa O-rejeshi

13.0 NGELI ZA NOMONO NA UAINISHAHI WAKE PAMOJA NA


DHANNA YA O-REJESHI

13.1 Mitazamo mbalimbali inayohusiana na uainishaji wa ngeli za


nomino
13.1.1 Kigezo cha kimofolojia/maumbo ya umoja na wingi:

1-mu- i) Majina ya viumbe vyenye uhai

2-wa- ispokuwa mimea


ii) Majina yanayotokana na vitenzi
vinavyotaja watu
3-m- i) Majina ya mimea

4-mi- ii) majina ya vitu yanayoanza na m-

5-ji- iii)Majina yanayoanza na ji- umoja

6-ma- na ma- uwingi.

iii) Majina ya mkopo yenye ma-


(wingi)
iv) Majina yenye kueleza dhanna
ya wingi japokuwa hayahesabiki

7-ki- i) –majina ya vitu yanayoanza na


ki- (umoja) na vi- (wingi).
8-vi- ii) Majina ya viumbe
yanayoambishwa na ch- umoja na
vy-uwingi
9-N- i) Majina ambayo huanza na N

10 inayofuatwa na konsonanti, ch-, d-,


g-, j-, z-, na y- katika umoja na
wingi.
ii)Majina yanayoanza na mb-, mv.
iii) Majina ya mkopo.
11- U- Majina yote yanayoanza na u umoja

12- N- na N-, mb (wingi)

13- U- Majina yote yanayoanza na u-

14- Ma- umoja na ma- wingi

15-Ku- Majina yanayotokana na vitenzi


yanayoanza na ku- (vitenzi-jina)

16-PA- Huonyesha mahali hasa

17- Mu- Huonyesha mahali pa ndani.

18-Ku- Huonyesha mahali pa mbali na


mahali pakubwa zaidi au hata
mahali popote.

13.1.1 Kigezo cha sintaksia /upatanisho wa kisarufi: Huu ni mtazamo wa


kisasa wa uainishaji wa ngeli ambao umeyagawa majina katika makundi kulingana na
upatanisho wa kisarufi kat ya jina na viambishi awali vilivyo katika vitenzi yaani
vipatanishi.
Ngeli ya A-WA
Ngeli ya LI-YA
Ngeli ya KI-VI
Ngeli ya U-I
Ngeli ya U-ZI
Ngeli ya U-YA
Ngeli ya KU-
Ngeli ya PA/MU/KU-


13.1.2 Faida ya kigezo cha kimofolojia:
Kigezo hiki kinasaidia kuonyesha: Kigezo kili kinasaidia kuonyesha uhusiano
kati ya lugha za kikoa kimoja; na ni moja wapo ya vithibitisho kuwa lugha ya


Kiswahili inaingia katika kundi la lugha zakibantu.
Asilimia kubwa ya nomino za Kiswahili zinaonyesha maumbo dhahiri ya
viambishi ngeli, na tuichukulia kuwa angalau (10) za kwanza zinajigawa katika
jozi za umoja na wingi,inawezekana kabisa kuzigawa nomino katika makundi


yake kwa kutumia kigezo hiki cha maumbo.
Husaidia kutambulisha ngeli na pia kuonyesha idadi (umoja na wingi) katika
nomino za Kiswahili.


i. 1.3 Matatizo ya kigezo cha kimofolojia
Kuna nomino ambazo zina kigezo maalum, lakini zinatawanyika katika


ngeli tofauti.
Baadhi ya nomino huwa na viambishi vya umoja na wingi ambavyo ni


tofauti na viambishi vinavyoitambulisha ngeli hiyo


Baadhi ya nomino hazina viambishi vyovyote.
Ngeli PA-MU- KU-zinatambulisha kwa kuzingatia kwa kuzingatia
upatanisho wa kisarufi kwa kuwa kuna nomino moja pekee inayopatikana


hapa ambayo ni “mahali” na haina viambishi.
Ufundishaji wa ngeli kwa kutumia umbo la nomino hauzingatii


upatanisho wa kisarufi.


Kuna viambishi ambavyo vinafanana.
Kutokidhi mahitaji ya sulubu ya sentensi.


13.1.4 Faida za Kigezo cha kisintaksia
Kigezo hiki kilionekana ni bora kwa sababu majina mengi yanayohusiana na


mengine, na kila jina lina kipatishi katika kitenzi.
Mwishoni mwa upatanishi wa kisarufi hautatanishi kwa vile kiambishi awali


katika kitenzi huwa bayana sana;
Majina yasiyo na viambishi mwanzoni, ngeli zake hujulikana kwa urahisi
zaidi kwa kutumia upatanishi wa kisarufi kuliko kwa viambishi vya mashina
ya majina.


13.1.5 Matatizi ya kigezo cha kisintaksia


Kuna vipatanishi vinavyofanana katika ngeli hizi.
Katika ngeli ya kwanza, kuna vipatanishi viwili vya umoja, YU/A-
lakini ukweli ni kwamba, matumizi ya kiambishi YU- ni ya kilahaja
zaidi Kuliko ya Kiswahili sanifu.


Huyaweka majina ya maumbo tofauti katika ngeli moja.
Yapo baadhi ya maneno ambayo yana utata katika upatanisho.


13.1.6 Matumizi ya ngeli
Hutumika kupanga majina ya lugha katika makundi yaliyoshikamana

 Hutumika kutambulisha maumbo ya umoja na wingi katika majna na


na kutofungamana kutokana na kigezo muhimu.

 Hutumika katika upatanishi wa kisarufi katika sentensi.


vivumishi.

 Hutumika katika kuonyesha uhusiano uliopo baina ya lugha za


Kiswahili na lugha zingine.
13.2 Dhanna ya O-rejeshi: Ni kiambishi kinachotumiwa kurejelea kwenye
nomono ambayo huwa imetajwa kabla ya kitenzi
chenyewe kutajwa. Viambishi hivyo ndivyo
vinavyosababisha utegemezi katika sentensi.
Dhimma ya muundo wa O-rejeshi
- Hutumika kama kirejeshi
- O-rejeshi hudokeza mahali
- O- rejeshi hudokeza wakat
- Hutumika kama kiunganishi
- Hudokeza namna.
Besha, R. (1994), Utangulzi wa Lugha na Isimu Dar es Salaam University Press.
Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam
Massamba, D. (2004) Kamusi ya Isimu na falsafa ya Lugha, TUKI.
Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2001).Sarufi miundo ya Kiswahili Sanifu
(Samikisa) Sekondari na vyuo. TUKI.
Masebo, J.A na Nyangwine, N,(2009) Nadharia ya Lugha KISWAHILI 1 Nyamburi
Nyangwine Publishers, Dar-Es Salaam, Tanzania.

MUHADHARA WA KUMI NA NNE


DHANNA YA MOFOFONOLOJIA:

MALENGO YA MUHADHARA:

 Uweze kueleza maana ya mofofonolojia


Baada ya kumalizika muhadhara huu mwanafunzi unatakiwa:

 Uweze kueleza na kutofautisha kati ya dhanna ya utawala wa kifonolojia na

 Uweze kueleza dhanna ya vighairi


utawala wa kimofofonolojia.

 Uewze kuzichambua na kuzifafanua kaununi mbalimbali za kimofofonolojia.


14.0 DHANNA YA MOFOFONOLOJIA:

14.1.1 Maana ya mofofonolojia

 Mofofonolojia ni muunganiko wa taaluma za aina mbili za kiisimu: taaluma ya

mofolojia (mofo) +taaluma ya fonolojia (fono) =Mofofonolojia.

 Tunaweza kusema kwamba Mofofonolojia ni taaluma inayojishughulisha na

uchanganuzi na uainishaji wa vipengele vya kifonolojia vinavyoathiri maumbo

ya mofimu katika mfuatano wake.

 Hii ni taaluma inayojishughulisha na uchanganuzi wa vipengele vya kifonolojia

ndani ya maumbo ya mifolojia.

14.1.2 Utawala wa kifonolojia: Ni mazingira ya kifonolojia yanayotawala


utokeaji au utofauti wa maumbo ya maneno. Yaani, kuwepo kwa umbo fulani
ni matokeo ya kuwepo au mfuatano wa fonimu fulani

14.1.3 Utawala wa Kimofofonolojia: Ni mazingira ya kifonolojia


yanayoshindwa kutawala utokeaji au utofauti wa maumbo ya maneno. Yaani,
kuwepo kwa umbo fulani hakutegemei kuwepo au mfuatano wa fonimu
fulani. Mara nyingi hujitokeza kama vighairi.

14.1.3 Vighairi: ni mifano ya maumbo au miundo inayopingana na kanuni ya


jumla ya utokeaji wa vipashio vya kimofolojia.

14. 2 Kanuni mbalimbali za mofofonolojia:


14.2.1 Kanuni ya udondoshaji.

Kanuni ya udondoshaji inasema kwamba, “irabu u inapokabiliana na


konsonanti halisi, katika mpaka wa mofimu, hudondoshwa, lakini
inapokabiliana na irabu inayofanana nayo hubakia kama ilivyo.
14.2.2 Kanuni ya uyeyushaji.

Kanuni ya viyeyusho inasema kwamba iwapo irabu inayokabiliana na ama u

au i inafanana kabisa na irabu hizo basi irabu u au i itabaki jinsi ilivyo; lakini
inapokuwa irabu inayokabiliana nazo haifanani nazo basi ama irabu hizo

hubakia kama zilivyo au huyeyuka ( yaani hupoteza nguvu zake za usilabi) na

kuwa kiyeyusho.

14.2.3 Kanuni ya muungano wa sauti.

ii) Kanuni ya muungano wa sauti inasema kwamba kuna uwezekano wa irabu ya mofimu

moja kukabiliana na irabu ya mofimu nyengine katika mipaka ya mofimu mbili kisha

irabu hizo mbili zikaungana na kuzaa irabu moja tu na aghlabu irabu inayozaliwa

hailingani na yoyote kati ya irabu hizo mbili.

14.2.4 Kanuni ya nazali kuathiri konsonanti

Kanuni ya nazali kuathiri konsonanti inasema kwamba kuna baadhi ya sauti


ambazo huathiriwa na nazali n inapokuwa sauti hizo zinaindamia. Hii ina maana
kwamba sauti hizo zikikabiliana moja kwa moja na nazali n huathiriwa nayo

14.2.5 Kanuni ya konsonanti kuathiri nazali

Kanuni ya konsonanti kuathiri nazali inadai kwamba katika maneno umbo na nazali

linategemea mahali ambapo konsonanti halisi, ambayo inakabiliana moja kwa moja na

nazali hiyo , hutamkiwa.

14.2.6 Usilimisho (Usimilisho)

 Ni kufanana kwa fonimu kwa kiasi au kabisakabisa kutokana na kuathiriana.

 Hali hii husababishwa na sauti jirani katika neno kuathiriana hivi kwamba fonimu

ama hupokeaau kupoteza sifa za kifonetiki kwa fonimu jirani.


 Kwa mfano kikitamkwa chenye sifa ya kikwamizi kinaweza kuathiriwa na

kufanywa kuwa kitamkwa chenye sifa ya kipasuo. Usilimisho huweza kuhusisha.

-Kuimarika na kodhoofika kwa fonimu

-Kuungana kwa sauti/fonimu

-Kuingizwa na kudondoshwa kwa fonimu.

-Kuimarika na kudhoofika kwa fonimu

 Mfano : sauti za vipasuo zinazotamkwa, wakati zimeshikana kabisa huhitaji

nguvu zaidi katika kuzitamka kuliko wakati wa utamkaji wa sauti za vikwamizi.

 Hapa vipasuo hudhoofishwa na kuwa vikwamizi.

 Kwa maneno mengine tunaweza kusema kwamba kudhoofika kwa sauti

kunaweza kutokea pale ambapo nguvu chache za msuli katika ala za sauti na

msukumo kidogo wa mkondo hewa hutumika katika alofoni kuliko kutamka

fonimu yake.

 Mengi ya mabadiliko ya aina hii huwa ni ya kimazingira.

 Kudhoofika kwa konsonanti za Kiswahili aghlabu huhusisha kubadilika kwa

konsonanti za mpasuo na kuwa za mkwaruzo.

 Hii inaweza kuwasilishwa kama ifuatavyo kwa kutumia sifa bainifu:-

[+mpasuo] [-mpasuo]-/vokali [i]. Tuangaliye mifano ifuatayo.

/p/ [f]- /i/ sheria hii inamaanisha kuwa

Kuungana kwa sauti

Sauti zinapoathiriana kiasi kwamba sauti moja hupoteza sifa bainifu zake zote kwa sauti

jirani, au pengine sauti zote mbili huungana na kuzua alofoni mypya ya fonimu

inayohusika.
Kwa mfano:[ pa+iηgin ] huwa [pἐηgin ] yaani

[a+i]-------->[ ἐ ]

Kuingizwa na kudondoshwa kwa fonimu

 Uingizaji hapa unarejelea uchopekaji wa sauti moja au zaidi katika neno.

 Kwa upande mwengine udondoshaji hurejelea utoaji wa sauti moja au zaidi katika

neno.

 Uingizaji na udondoshaji waweza kuwa wa kimaksudi au kutokea kibahati katika

historia ya fonolojia ya lugha.

 Hali huzi aghlabu hutokea ili kuleta muundo wa silabi wa neno unaokubalika

katika lugha husika, hasa kwa maneno yaliyokopwa.

 Kwa mfano, sauti ya likwidi /l/ imedondoshwa katika baadhi ya maneno ya

Kiswahili sanifu kihistoria. Kwa mfano neno ‘oa’ zamani lilitamkwa, ‘lola’. Kuna

aina tatu za udondoshaji . Odondoshaji sauti awali, udondoshaji sauti kati, na

udondoshaji sauti tamati.

14.2.7 Tangamano la irabu:


 Ni hali ya irabu kuathiriana. Irabu iliyoko katika mzizi wa kitenzi hasa kwenye
silabi moja kabla ya ile ya mwisho huathiri irabu ya mnyambuliko.Mfano: ikiwa
katika mzizi wa neno utakuwa na irabu a, i, au u basi irabu ya mnyambuliko
itakuwa i katika kauli zote za unyambulishi ; kauli ya kutendea, kutendeka,
kutendesha/ kusababisha.
 Ikiwa irabu ya mzizi iliyo kwenye silabi moja kabla ya ile ya mwisho ni e au o
basi irabu ya mnyambuliko itakuwa e katika kauli zote za unyambulishi; kauli ya
kutendea, kutendeka, kutendesha.
Marejeleo

Besha, R (1994), Utangulizi wa Lugha na Isimu . Dar es Salaam University Press.

Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam.

Lyons, J. (1971). Introduction to Theoritical Linguistics, London:Cambredge

Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004)fonolojia ya Kiswahili Sanifu (Fokisa)


Sekondari na vyuo. TUKI.

Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania, Dar-es-
Salaam.

Lyons, J. (1971). Introduction to Theoritical Linguistics, London:Cambredge

Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004) fonolojia ya Kiswahili Sanifu (Fokisa)


Sekondari na vyuo. TUKI.

Massamba D.Kihore, Y. na Msanjila Y. (2004).Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu


Samakisa Sekondari na vyuo. TUKI. .

MUHADHARA WA KUMI NA TANO


DHANNA YA SEMANTIKIA
MALENGO YA MUHADHARA
Mwishoni mwa muhadhara huu mwanafunzi unatakiwa :
 Uweze kueleza maana ya semantikia
 Uweze kufafanua maana ya maana katika Lugha.
 Uweze kubainisha aina za maana.
 Uweze kuainisha nadharia mbalimbali za maana

15.DHANNA YA SEMANTIKIA
15.1 Maana ya semantiki
 Semantiki ni stadi inayojishughulisha na maana katika muktadha wa lugha ya
mwanaadamu.
 Semantiki hutafiti maana za fonimu, mofimu, maneno na tungo.
 Maana hushughulikiwa katika viwango vyote vya lugha, kama vile sauti, maneno
na sentensi.

15.2 Maana ya maana


Hakuna jibu la mkato au jibu rahisi linaloelezea juu ya dhanna ya maana.Tuangaliye
maana mbalimbali za maana zilizopo hapo chini.
 Maana ni maelezo yanayotumiwa kukitambulisha au kukifafanua kitu

 Maana ni kusudio au dhamira ya mtu.

 Maana ni ishara au dalili ya jambo.

 Maana ni thamani, umuhimu au nafasi ya kitu au jambo fulani kwa mtu.

 Maana ni sababu.

15.3 Aina za maana

G.Leech (1974) amedhihirisha aina saba za maana kama ifuatavyo:-


Maana halisi. Hii ni ile maana ya msingi ya neno. Pia hujulikana kama maana
ya kikamusi au maana tambukizi;

Maana ya ziada/Maana ya kimatlaba/ashirifu( connotative meaning


Hii ni maana ya ziada ambayo neno hupata yaani maana ya kimatlaba. Maana hii
hutokana na maana ya msingi ya neno. Maana hii huhusishwa na kitajwa cha msingi.

Maana ya kimtindo/stylistic meaning. Hii ni maana ya kimuktadha; hii ni


maana inayotokana na matumizi ya Luhga kulingana na mazingira halisi ya
wakati wa mazungumzo.
Maana akisi/ Reflective meaning. Hii ni maana inayopewa kitu kwa kufananisha
na kitu kingine. Kwa mfano mtu anapommwita mpenzi wake mtoto au malaika
anamaanisha mzuri , asiye na makosa.
Maana dhamirifu (thematic meaning) Maana hii inapatikana kutokana na namna
mtumiaji wa Lugha anavyopanga maneno yake katika sentensi. Aghlabu, ile
taarifa ambayo muhusika anaiona kuwa ndiyo muhimu huiweka mwanzoni.)
Maana shawishi (affective meaning) Hii ni maana inayotokana na hisia na
mtazamo wa mzungumzaji au mwandishi juu ya kitu. Je, ana mtazamo hasi au
mtazamo chanya?
Maana endefu/Tangamano /collocative meaning. Kuna baadhi ya maneno
ambayo maana zake hupatikana kwa kuwa kwao pamoja na maneno maalum;
kinyume chake haiwezi kukubalika katika hali ya kawaida.
15.4 Nadharia tano za maana ni:-
 Nadharia za urejeleo za maana: Hii ni maana inayoelezea kitu halisi.
 Nadharia za kidhana za maana: Haya ni mawazo yanayohusishwa na
neno.
 Nadharia za kitabia za maana: maana hutolewa kutokana na tabia ya
kitu.
 Nadharia za masharti ya ukweli za maana:- maana ni ukweli.
 Nadharia za tendo -usemi za maana.

Marejeleo
Chiduo, E. 2002. “Synonymy: A defining method in the Standard Swahili
Dictionary: In Strengths and Weakness”, Kiswahili juzuu 65:43-58.
Kahig, K. 1995. Lugha katika vitabu vya watoto. Kioo cha Lugha (mfululizo mpya)
Juzuu 1:21-35.
Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania,
Dar-es- Salaam
Lakoff, G. 1987. Women, Fire and Dangerous Things, What categories Reveal
About the Mind. Chicago: University of Chicago Press.
Lyons. J. 1977. Semantics: Cambridge : Cambridge University press.
Mkude. D. 1995. Towards a Semantic Typology of the Swahili
Language . Institute for the Study of Languages and Cultures of Asia
and Africa (IL CAA)

MUHADHARA WA KUMI NA SITA


16.0 UHUSIANO WA KIMSAMIATI
16.1 Dhanna ya uhusiano wa kimsamiati:
Huu ni uhusiano wa maneno unaozungumzia maingiliyano yaliyopo baina ya
maneno.Uhusiano utakaoongelewa hapa ni wa sinonimia, antomia, homonimia, polizimia
na haiponimi
16.1 Sinonimia
16.1.1 Maana ya sinonimia: ni uhusiano wa kileksikia au kimsamiati
ambapo huwa kuna maumbo tofauti katika lugha ambayo maana zake ni sawa.
Maneno yanayotofautiana kimaumbo lakini yakafanana au kulingana kimaana huitwa
sinonimu.
16.1.2 Mambo yanayosababisha kuzuka kwa sinonimia:
 Ukopaji wa msamiati: Maneno yakiwa na asili tofauti huleta hali ya
usinonimia.

 Jinsia: Sinonimu nyengune hutokana na visawe vinavyorejelea wanawake na


wanaume. Kuna maneno yenye maana moja kimsingi lakini huwa na umbo
tofauti kutegemea jinsia.Kwa mfano hali ya kuwa na sura nzuri hurejelewa
kwa kisawe cha “urembo” kwa wanawake na “ujamali” au “umaridadi” kwa
wanaume.

 Dini: Dini tofauti huwa na maneno tofauti kuelezea dhana zinazolingana. Kwa
mfano dhana inayorejelea mahala pa kuabudia kwa waisilamu msikitini, kwa
wakiristo kanisani na sinagogi kwa mayahudi.
 Tofauti za kimaeneo: Wazungumzaji wa Lugha wanapogura au kuhama
Kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyengine, Lugha yao hubadilika
kimuundo na kimsamiati ili kukidhi mahitaji ya mazingira mapya.
 Tofauti za kilahaja: Dhana moja huweza kutajwa kwa maneno yenye
matamshi tofauti. Kwa mfano neno nchi katika Lahaja sanifu ya Kiswahili
huwa ni nti kimvita au chi Kitumbatu.
 Taaluma: Visawe vya Kitaaluma huitwa istilahi. Mfano wa sinonimu za aina
hii ni aya katika riwaya na ubeti katika ushairi vinavyorejelea kitengo katika
mfululizo wa maandishi.
 Wakati: Baadhi ya sinonimu za Lugha huzuka kutokana na mabadiliko ya
kihistoria.

16.2 Antonimia
16.2.1 Maana ya antonimia:
Antonimia ni uhusiano ambapo kuna maneno katika Lugha ambayo maana zake
ni vinyume”. Kinachokusudiwa kusemwa hapa ni kwamba maana za maneno
hayo huwa zinapingana. Maneno yenye maana zinazopingana huitwa antonimu.
16.2.2 Aina za antonimia:
Antonimia za kiukinzani: ambapo zipo tofauti kabisa kimaumbile au kimaana.

Antonimia za kipiimo: Kinachozingatiwa hapa ni tofauti ya wingi wa


kinachopimwa

Antonimia za uhusiano: Kinachozingatiwa hapa ni uhusiano uliopo baina ya


vinyume

16.3 Haiponimia
16.3.1 Maana ya hamonimia:

 Huu ni uhusiano wa kimsamiati unaohusu maneno tofauti yaliyosadifu

kuwa na maumbo sawa lakini yaliyotofautiana kimaana. Kufanana kwa

maumbo hayo ni kwa kusadifu tu.


 Maneno hayo huwa hayana usuli mmoja wala kihistoria.
 Maneno mawili au zaidi yanayofanana kwa maumbo na kutofautiana kwa
maana huitwa homonimu.
16 .3.2 Aina za homonimia:
 Homofoni: Ni kuwepo kwa maneno yenye matamshi sawa ,
lakini maana zinatofautiana kabisa.
 Homografia: Ni hali ya maneno mawili au zaidi kuwa na tahajia
sawa lakini maana zake tofauti.

16.4 Polizimia: polizimia ni hali ambapo maneno huwa na maana zaidi ya moja”.
Katika polizimia maneno huwa yana uhusiano wa kihistoria.Huu ni uhusiano unaohusu
umbo moja la neno lenye maana mbalimbali.

16.4 Haiponimia:
Huu ni uhusiano wa kimsamiati ambapo maana fulani ya neno ni sehemu ya
maana kubwa ya neno.
 Neno lenye maana kubwa huitwa maana jumuishi ili hali maneno yenye maana
ndogo huitwa haiponimu

Chiduo, E. 2002. “Synonymy: A defining method in the Standard Swahili


Dictionary: In Strengths and Weakness”, Kiswahili juzuu 65:43-58.
Kahig, K. 1995. Lugha katika vitabu vya watoto. Kioo cha Lugha (mfululizo mpya)
Juzuu 1:21-35.
Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania,
Dar-es- Salaam
Lakoff, G. 1987. Women, Fire and Dangerous Things, What categories Reveal
About the Mind. Chicago: University of Chicago Press.
Lyons. J. 1977. Semantics: Cambridge : Cambridge University press.
Mkude. D. 1995. Towards a Semantic Typology of the Swahili
Language . Institute for the Study of Languages and Cultures of Asia
and Africa (IL CAA)
Masebo, J.A na Nyangwine, N,(2009) Nadharia ya Lugha KISWAHILI 1
Nyamburi Nyangwine Publishers, Dar-Es Salaam, Tanzania.

MUHADHARA WA KUMI NA SABAA


UTATA KATIKA LUGHA NA DHIMA ZA KISEMANTIKIA
PAMOJA NA UPANA WA DHANNA.

MALENGO YA MUHADHARA

 Dhanna ya utata katika Lugha


Baada ya muhadhara huu unatakiwa uelewe:-

 Aina za utata katika Lugha


 Sababu za kuzuka kwa utata kwenye lugha
 Dhanna ya dhimma za kisemantikia
 Dhimma mbalimbali za kisemantikia

17.0 Utata Katika Lugha na Dhima za Kisemantikia pamoja na Upana


wa dhanna.

17.1 Dhanna Ya Utata Katika Lugha


17.1.1 Maana Ya Utata:
Ni hali ya kipashio cha kisarufi kama neno, kirai, kishazi na hata Sentensi kuwa na
maana zaidi ya moja.

 Utata wa kimuundo
17.1.2 Aina za Utata:

 Utata wa kimsamiati

17.1.3 Sababu za kuwepo utata katika Lugha


 Neno kuwa na maana zaidi ya moja, kama ilivyo neno endesha , mbuzi kaa,
bui bui na mengi mengineyo.
 Kutumia neno bila kuzingatia mazingira au muktadha unaohusika na
matumizi ya maneno hayo.
 Utumiaji wa maneno yenye maana ya picha au maana iliyofichikana yaani
viashiria husababisha utata.
 Kuwepo kwa mofimu ya kauli ya kutendea /li/, /le/, /i/, na /e/.
 Kuwepo kwa kiambishi nafsi kiambata ‘a’ na ‘wa
 Matumizi ya vimilikishi –ake na -ao
 Matumizi ya mzizi ‘ingine’

 Matumizi ya baadhi ya viunganishi.


 Matumizi ya baadhi ya vihusishi
 Makosa ya kisarufi na kimantiki
17.1.4 Dhanna ya dhima za Kisemantikia
 Maana ya dhima za Kisemantikia:
-Ni dhima inayosimamia kazi na majukumu ya nomino mbalimbali
zilizomo ndani ya sentensi.
-Kwa ufupi hizi ni dhima za kitajwa katika sentensi.
-Kinachoshughulikiwa hapa ni “nani amefanya nini kwa nani na kwa
njia gani na kwa kutumia kifaaa kipi” Kila nomino katika tungo
kishazi au sentesi kamili inadhima au jukumu maalumu.
17.1.5 Dhima za kisemantiki zijulikanazo ni:
 Mtenda :mtenda ni jukumu linalohusu nomino inayorejelea mtu au

kitu chenye uhai kinachosababisha kitendo fulani

kutendeka.Kitendo kinachotendeka kinaakisiwa na mtenda.

 Mtendwa: Ni jukumu la mtu, watu, au vitu vinavyopata athari.

Mara nyingi athari hizi huwa zinapatikana au kusababishwa na

mtenda.

 Kifaa :Hili ni jukumu linalohusu nomino inayorejelea kifaa cha

utendakazi. Kifaa hiki hutumiwa mara nyingi na mtenda.

 Mwathiriwa:- Mwathiriwa ni dhima/jukumu linalotekelezwa

wakati ambapo nomino inarejelea mtu au kitu kinachopata athari

fulani.Athari hizi mara nyingi huwa hazitokani na mtenda.


 Nguvu:- Jukumu la nguvu hutekelezwa na kIrejelewa au kitu

kisichoonekana kwa uwazi.Mara nyingi nguvu huwa ni vitu vya

kidhahania. la mtenda.

 Chanzo :- Jukumu la chanzo hutekelezwa na na nomino zinazorejelea

mahali, wakati au mwanzo wa kitu fulani .

 Lengo: Lengo tofauti na chanzo , ni mahali au wakati wa kuishia

kitendo fulani.

 Wakati: Jukumu hili hutekelezwa na nomino zinazorejelea wakati.

 Mahali: Jukumu la mahali ni lile linalotekelezwa na nomino

zinazorejelea mahali fulani. Nomino za mahali hurejelea mahali

maalum bila kuhusisha nomino ya chanzo au lengo

 Malighafi: Mali ghafi ni jukumu linaloakisiwa na nomino

inayorejelea vitu vinavyotumika katika utendaji wa kazi. Katika hali

hii vitu hivyo havitumiki kama vifaa, bali vinatumika kama mali ghafi

ya kazi.

 Matokeo: Haya ni matokeo ya kutumika mali ghafi. Katika sehemu ya

mali ghafi hapo juu udongo na kitambaa ni mali ghafi suti na vyungu

ni matokeo.Ifuatayo ni mifano mingine zaidi

17.1.6 Mfumo wa udhahania

17.1.6.1 Dhana ficho/Kengeushi: Dhana zilizo katika sentensi za

mazungumzo, zisizo wazi.

17.1.6.2 Umenyu ( Typicality): Hali ya kuwa mashuhuri zaidi kuliko vyengine

vyenye umashuhuri katika fani au kada fulani.


17.1.6.3 Upana wa dhanna: Ni hali ya kuiwasilisha dhanna moja kwa maneno

tofautitofauti kutokana na tofauti ndogondogo zinazojitokeza ndani

yake.

Marejeleo
Chiduo, E. 2002. “Synonymy: A defining method in the Standard Swahili
Dictionary: In Strengths and Weakness”, Kiswahili juzuu 65:43-58.
Kahig, K. 1995. Lugha katika vitabu vya watoto. Kioo cha Lugha (mfululizo mpya)
Juzuu 1:21-35.
Habwe, J. and Karanja, P (2004) Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi, Phonix
Publishers
Kipacha, A(2007) Utangulizi wa Lugha na Isimu Chuo Kikuu Huria Tanzania,
Dar-es- Salaam
Lakoff, G. 1987. Women, Fire and Dangerous Things, What categories Reveal
About the Mind. Chicago: University of Chicago Press.
Lyons. J. 1977. Semantics: Cambridge : Cambridge University press.
Mkude. D. 1995. Towards a Semantic Typology of the Swahili
Language . Institute for the Study of Languages and Cultures of Asia
and Africa (IL CAA)

18.0 MUHADHARA WA KUMI NA NANE


18.1 Isimu jamii:
18.1.2 Maana ya isimu jamii: Isimuj amii ni t aaluma inayochunguza
mat umizi ya lugha kat ika j amii.


18. 1.3 Malengo ya Isimu jamii:
Kuchunguza na kuf af anua t of aut i zilizo kat ika lugha na uhusiano ulio


kat ika lugha hizo, na t of aut i zilizo kat ika j amii.
Kuchunguza uhusiano uliopo kat i ya lugha na wazungumzaj i. Lugha


inamt ambulisha mzungumzaj i na kundi analoliwakilisha.
Kut af it i na kuf af anua naf asi ya lugha kat ika j amii ili kuf af ahamu idadi
ya lugha zilizopo kat ika j amii, kubaini uamilif u na uwezo wa kila


lugha.
Kut af it i na kuf af anua t of aut i zilizomo ndani ya lugha na namna
zinavyohusiana na t of aut i zilizomo ndani ya j amii.
18.4 Nafasi ya lugha katika jamii:

 miongoni mwa wanaj amii husika t u hivyo kuwa ni lugha ya kij amii.

 kat ika eneo f ulani la kij iograf ia k. v. mkoa na kuwa lahaj a ya lugha f ulani.

 kit aif a kama lugha inayowaunganisha wat u wa t aif a zima au lugha ya elimu

kwa viwango f ulani na kuwa ama lugha ya t aif a au l ugha rasmi n. k.

18.5 Uamilifu wa Lugha:

 kut olea elimu k. v. kuf undishia masomo shul eni

 kuendeshea shughuli za serikali, siasa, mahakama

 kuf anya mawasiliano ya kawaida miongoni mwa j amii husika ambayo ni

pamoj a na shughuli za kila siku za j amii k. v. mat ambiko, misiba, harusi,

ngoma na sharehe mbalimbali.

 kut umika kat ika mawasiliano mapana hususan kat i ya j amii zenye kuongea

lugha t of aut i hasa kat ika biashara.

 Dhima kuu ya lugha ni kuf anya mawasiliano kat i ya mt u na mt u


18.6 Dhima ya Lugha

 Lugha huwawezesha wat u wa j amii moj a au j amii t of aut i kuwasiliana na


kuwawezesha waelewane.

18.7 Binaadamu na Lugha

 Binadamu huwasiliana miongoni mwao kwa lugha it umiayo maneno

ambayo ni saut i zilizokubaliwa na kuwekwa pamoj a ili kulet a maana

mahsusi.
 Lugha it umiayo maneno ni saut i za nasibu zilizot euliwa na kukubaliwa

na binadamu ili wazit umie kuwasiliana. Lugha it umiayo maneno ni

mahsusi kwa binadamu pekee.

 Kat ika kuwasiliana kwa kut umia maneno, binadamu huweza kuunda

lugha za aina mbalimbali k. v. rej est a, lahaj a, simo, vit araf a n. k. na

kuzalisha maneno na t ungo zisizo na kikomo kwa lengo la kuf anikisha

mawasiliano.

 Binadamu hut umia pia ishara kuwasiliana miongoni mwao.

Lugha ya ishara ni lugha inayot umia viungo vya mwili k. v. mikono, vidole,

kope za macho, kichwa n. k. ambavyo huchezeshwa kwa namna f ulani na

kut oa uj umbe unaoeleweka kwawazungumzaj i na wasikilizaj i.

 Ishara hizi zimet euliwa kinasibu pia kwa maana kuwa hakukuwa na

ut arat ibu wa kuziunda na kuzipa maana, il a ziliibuliwa na wanaj amii,

zikazoeleka na kukubalika.

 Kwa kut umia viungo vya mwili binadamu huunda lugha ya ishara f ulani

zenye kuwasilisha uj umbe kwa msikilizaj i.

 Aidha binadamu hut umia saut i za mkururo k. v. kuguna, kuf yonza,

kukoroma, kucheka n. k. kueleza hisia zake ambazo ni uj umbe kwa

msikilizaj i ama kwa kudhamiria k. v. kuf yonza kama ishara ya dharau, au

kukoroma kukiashiria kulala pasi na mhusika kusema ‘ nimelala’ .

18. 8 Lugha na viumbe wasio wanaadamu:


 Wanyama hut umia ishara kuwasiliana. Mara nyingi wanyama hut oa milio

maalum kuwasilisha uj umbe kwa wenzao, kama vile mlio wa kuwaarif u

wenzao kuwa na hadhari kwani kuna adui au kiumbe asiye mwenzao

j irani nao.

 Wanyama wengine hut umia milio maalum kut af ut ana na wengine hut oa

mlio wa kuf urahia mlo uliopat ikana, kwa mf ano f isi, bila shaka ikiwa ni

kuwait a wengine waj e.

 Lugha ya ishara ndio nj ia ya mawasiliano pekee it umiwayo na wanyama.

Wanyama pia hut umia haruf u kuwasiliana.

18. 9 Nadharia ya chimbuko la Lugha:

18. 9. 1 Krioli na Pij ini

18. 9. 1 Maama ya krioli na pij ini:

 Lugha yenye mf umo uliorahisishwa sana ambao hut umiwa na


wazungumzaj i wenye lugha t of aut i kat ika mazingira maalum na kwamba


pij ini sio lugha mama kwa mzungumzaj i yoyot e.
Lugha mama inayot umiwa na wazungumzaj i wazawa ambao kihist oria
wamet okana na j amii lugha ya pij ini.

18.10 Launi za Lugha

18.10. 1 Lahaja jamii: Wazungumzaji wawili wa lugha moja wanaweza kuwa na


tofauti ndogo ndogo za kimatamshi au msamiati baina yao kwa vile wanatoka katika
matabaka, rika, ujuvi, jinsia au itikadi tofauti.

18.10.2 Lahaja Jiografia: Wazungumzaji wawili wa lugha moja wanaweza kuwa


na tofauti ndogo ndogo za kimatamshi au msamiati baina yao kwa sababu wanatoka
katika maeneo yanayotenganishwa na milima, bahari au mito.
18.10.3 Rejista: Rej ist a ni mt indo wa lugha inayot umika mahali penye
shughuli f ulani au inayot umiwa na kundi maalum la kij amii ambayo ni
t of aut i na l ugha ya kawaida.

18.10.4 Lugha sanifu: Lugha iliyochaguliwa katika jamii kwa matumizi ya


shughuli za kijamii za kila siku.


18.10. 4.1 Vigezo vitumikavyo kuteuwa lahaja rasmi:
Uteuzi: Kwa njia moja au nyengine lahaja rasmi imekuwa itakuwa imeteuliwa

 Uandishi: baadhi ya taasisi kama vile TUKI, wanakuwa wanatunga kamusi na


miongoni mwa lahaja.

 Dhima: Lugha rasmi haina budi itumike katika shughuli za serikali na elimu
vitabu vya sarufi ambavyo watu huvifuata.

 Ukubalifu: launi lazima ikubalike na mzungumzaji au jamii kwa ujumla.


ya juu.

Ikesha kubalika hubeba dhanna ya kuunganisha jamii na huwa ni ishara ya


uhuru wa jamii hiyo.

18.11 Mambo mengine yanayohusu jamii na Lugha


18.11.1 Nadharia ya Pijini na krioli

 Pijini ni lugha yenye mfumo uliorahisishwa sana ambao hutumiwa na


18.11.2 Maana ya pijini na krioli

wazungumzaji wenye lugha tofauti katika mazingira maalumu na kwamba pijini


sio lugha mama kwa mzungumzaji yoyote.
Krioli ni lugha mama inayotumiwa na wazungumzaji wazawa ambao kihistoria
wametokana na jamii lugha ya pijini.


18.11.3 Sifa za pijini na krioli


Kwa asili ni lugha chotara

 Hutumika zaidi katika mawasiliano yasiyo rasmi


Zina mfumo wa lugha sahili


18.11.4 Umuhimu wa kujifunza lugha za pijini na krioli


Sababu za kihistoria na kijamii


Chanzo muhimu cha Data za Isimujamii
Changamoto kwa watunga sera za lugha.

18.11.5 Usanifishaji wa lugha ya pijini na krioli.


18.11.6 Matatizo ya lugha za pijini na krioli
Lugha duni
 Wazungumzaji hawako tayari kusahihishwa.

18.12 ULUMBI

 Ulumbi ni hali ya matumizi ya Lugha mbili au zaidi katika miktadha maalum.

 Ni hali ya mzungumzaji binafsi kuwa na umilisi wa lugha mbili au zaidi ambazo

anaweza kuzitumia katika mazingira tofauti.

 Hali hii pia hujulikana kuwa ni uwililugha.

18.12.1 Aina za ulumbi

 Ulumbi Taifa: Unatokana na kugawa lugha mbalimbali katika majukukumu

tofauti tofauti kama vile; lugha ya kisheria, lugha ya shule, lugha ya ibada.

 Ulumbi taasisi: Hapo tunaona kuwa kunakuwa na lugha mbili au zaidi

zeny hadhi ya lugha rasmi. Kwa mfano ulkiangali hapa petu Tanzania

utakuta kuwa maofisi yetu yanatumia Lugha ya Kiingereza na Kiswahili

kama Lugha mbili rasmi

 Ulumbi binafsi: Hii ni hali ya mtu mmoja kutumia Lugha mbali mbali

katika mazingira tofauti.Mfano huu unaelezea hali ya Watanzania

waliowengi, hasa wasomi huwa wanajuwa kwanza Lugha za kikabila, pili

Kiswahili na tatu Lugha ya kigeni yaani Kiingerza au hata Kifaransa.Lugha

zote hizo anazitumia katika mazingira tofauti. Kazini anaweza kutumia

Kiingereza na Kiswahili. Mtu huyohuyo yawezekana akawa anatumia Lugha

yake ya asili kama vile Kisukuma na Kinyakyusa. Ulumbi Binafsi pia

unahusika na kipengele cha kubadilisha msimbo.Hii ni hali ya kubadilisha

Lugha zaidi ya moja katika mazungumzo kwa mzungumzaji


yuleyule.Kubadili msimbo ni mbinu ya mazungumzo inayovunja mipaka ya

mawasiliano ili kujenga njia bora ya mawasiliano.Moja ya sababu

zinazopelekea kuwa na msimbo ni hali ya mzungumzaji kuwa na umilisi

mdogo wa Lugha mojawapo hivyo huibia ile Lugha nyengine ili kukamilisha

mawasiliano.Pengine huweza kutokea kuwa na mapengo ya kiisimu ambayo

hayanabudi kuzibwa kwa kubadilisha msimbo.

Marejeleo:

Besha. R. M (1999) Nafasi ya Kiswahili katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia

katika Z.N. Tumbo -Masabo na E.K.F Chiduo (Wahariri). Kiswahili katika Elimu. Dar

es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.

Bright, W. (ed.)(1977). A Handbook of Sociolinguistics. Oxford: Blackwell Publishers.

MUHADHARA WA KUMI NA TISA


ISIMU- NAFSI: UCHAMBUZI WA MICHAKATO YA LUGHA
MALENGO YA MUHADHARA

 Kueleza maana ya isimu nafsi.


Baada ya muhadhara huu unatakiwa:-

 Kueleza mbinu za uchambuzi wa Lugha kiisimu nafsi.


 Aweze kubainisha Michakato mbali mbali ya lugha katika nyanja za fonetiki,
fonolojia, mofolojia na sintaksia.

19.0 ISIMU- NAFSI: UCHAMBUZI WA MICHAKATO YA


LUGHA.
19.0 Dhanna ya isimu nafsi


19.1.1 Maana ya isimu nafsi:


Taaluma inayoshughulikia uchambuzi wa michakato ya lugha.
Taaluma hii niachunguza ni kiasi gani maana ya maneno, sentensi na
mazungumzo yanavyokokotozwa katika ubongo.

19.1.2 Matawi ya isimu nafsi.
Elimu tambuzi (cognitivism)-Hii hujishughulisha na saikolojia ya


kujifunza lugha.
Isimu- nafsi matumizi (Applied Psycholinguistics)-Hujishughulisha na
maendeleo ya lugha hasa upande wa neva.


19.1 Kuteleza kwa ulimi –Uspuna
Dhanna ya uspuna: ni tendo la kuchanganya herufi za mwanzo za


maneno bila kukusudia.
Historia fupi ya uspuna: Dhanna ya uspuna imetokana na
mchungaji Willium A. Spunner wa New College, Oxford, kwa jinsi
alivyokuwa akitunga misemo au mashairi yenye kuchekesha kwa
maksudi ili kupotosha nmna ya usemaji.


19.2 Mpangilio wa maneno katika ubongo
Kila mtu ana hazina ya msamiati ambayo ndiyo msingi wa

 Tunaitumia misamiati hiyo kama tutumiavyo kamusi.


mawasiliano kwa kutumia lugha.

 Huwa tunanukuu hazina hiyo, tunapotaka kujua maana ya maneno


yanaandikwaje na jinsi yanavyotamkwa.

19.3 Michakato ya Lugha na isimu


19.3.1 Mchakato wa fonetiki na fonolojia:-
 Uchambuzi wa fonetiki na fonolojia unaonyesha muundo wa lugha
umejengwa katika ngazi mbalimbali za uwakilishi.
 Vipashio vinagawika kimahali na namna ya utamkaji.
 Vipashio vinagawika katika mfuatano wa silabi na alofoni.
 Je, ni kwakiasi gani mgawanyiko huu unachangia katika
kuchanganua lugha?

19.3.2 Mchakato wa kimofolojia


 Uchambuzi wa mofolojia hujishughulisha na muundo wa neno.
 Ni mfumo wa uchunguzi wa katagoria na kanuni za uundaji wa
maneno.
 Uchambuzi wa isimu –nafsi wa michakato ya kimofolojia
hujishughulisha na namna huo uundaji wa maneno unavyosaidia.

19.3.2 Mchakato wa kisintaksi.


 Tumeona kuwa katika nadharia ya uzalishaji sentensi ya Chomsky,
ili kufikia maumbo ya nje ya sentensi, kwanza huwepo kwa maumbo
ya ndani.
 Maumbo hayo ya ndani yanapitia mchakato wa uzalishaji hadi
kufikia hayo maumbo ya nje.
 Wana- isimu nafsi wamejaribu kuchunguza iwapo sentensi yenye
mfumo uzalishi mwingi huchukua mchakato mrefu zaidi kuliko
sentensi yenye mfumo uzalishi mchache.
Marejeleo
Gemsbacher, M. (1994). Handbook of psycholinguistics, New York: Acadamic Press.
Kess, J.(1992). Psycholinguistics. Pheldelphia: John Benjamins.
Libben, G. (1997). “Psycholinguistics”: The study of Language Processing” . katika O
Grady W. Dobrovolsky M. na Katamba F. (Wah) Contemporary Linguistics An
Introduction: Longman. UK 438-463
Neilson, J. (1936). Agnosia, Apraxia, Aphasia. New York: Holber.

MUHADHARA WA ISHIRINI.
ISIMU HISTORIA- UCHAMBUZI WA MABADILIOKO YA LUGHA
MALENGO YA MUHADHARA
Baada ya kumaliza muhadhara huu mwanafunzi unatakiwa:
 Chanzo cha mabadiliko ya lugha
 Utaje kanuni na nadharia za mabadiliko ya lugha
 Ueleze mabadiliko ya kategoria mbalimbali za kisimu

ISIMU HISTORIA- UCHAMBUZI WA MABADILIOKO YA LUGHA.


Chanzo cha mabadiliko ya lugha.
Kanuni na nadharia za mabadiliko ya lugha
Mabadiliko ya kileksia na kisemantiki
ukopaji
uundaji wa maneno mapya
mabadiliko kataika maana ya maneno
mabadilko ya kifonolojia
mabadiliko ya kimofoljia
-analojia na usawazisho
-usarufishaji
20.3.6 Mabadiliko ya kisintaksia
Marejeleo
Antchison, J. 1991. Language change; progress or decay? Toleo la pili.
Cambridge: Cambridge University Press.
Antilla, R. 1972, An Introduction to Historical ana comparative
linguistics;New York: The Macmillan Company.
Kipersky,P. 1970. “Historical linguistics”, katika J. Lyons (Mh.) New
horizons in Linguistics. Penguins Books. 302-315.
Antchison, J. 1991. Language change; progress or decay? Toleo la pili.
Cambridge: Cambridge University Press.
Li. C na S. Thompson. 1974. An explanation of Word order change
SOV—SOV, foundations of language 12: 201-14.
Macauley, R. 1994.The social Art : Language and its uses. New york:
Oxford University Press.
Bynon, T. 1977. Historicakl linguistic. Cambridge: Cambridge University
Press.
Hombert, J and L. Hyman. (Wah) 1999. Bantu Historical Linguistics:
Theoretical and Emprical perspectives. CSLI Publications.
Labov, W.1994. Principles of Linguistics Change:Volume1:Internal
Factors.Oxford: Black well Publishers.
Lehman, W. 1992. Historica linguistics, (Toleo la Tatu): London:
Routledge.

You might also like