You are on page 1of 13

Kiswahili Lugha Tamu Duniani.

Umilisi katika lugha ya


kiswahili,faida za umilisi,Dhana ya
utendaji, Mambo ya kuzingatia
katika utumizi wa lugha,umbo la
ndani na umbo la nje la sentensiDhana
ya sarufi zalishi,maana ya sarufi
April 19, 2017

Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu, sehemu ya kwanza ni


utangulizi ambao unahusisha fasili za sarufi na sarufi zalishi, sehemu ya
pili kiini cha swali na sehemu ya tatu ni hitimisho.
Dhana ya sarufi imefasiliwa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo:
Sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria na kanuni za
matumizi yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji wake
(Pei na Gaynor, 1969:88)
Sarufi ni taaluma ya lugha inayohusu uchunguzi na uchanganuzi wa
kanuni na vipengele mbalimbali vya lugha (Massamba na wenzake,
2004).
Sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria, kanuni na
matumizi yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji
wake(Kihore 2012).
Sarufi ni kanuni na sheria au taratibu za uchambuzi zinazotawala
lugha(Massamba na wenzake, 2001).
Sarufi ni utaratibu wa kanuni ambazo humwezesha mtumiaji wa lugha
kutunga tungo sahihi zinazoeleweka mara zinapotamkwa (Kapinga,
1983).
TUKI, (1999) Sarufi ni sayansi ya lugha.
TUKI, (1999) Sarufi ni sayansi ya lugha.

Kutokana na fasili za wataalam hapo juu sarufi ni taratibu na kanuni


zinazotumika katika kuunda lugha kwa kuzingatia ukubalifu wa
watumiaji wake huku ikizingatia viwango vyote vya uchambuzi yaani
kiwango cha maana,matamshi, miundo, na maumbo katika lugha husika.
Sarufi zalishi ilizuka kutokana na kasoro za sarufi mapokeo na sarufi
miundo katika uchanganuzi wa lugha. Mtazamo huu uliasisiwa na Noam
Chomsky katika kitabu chake cha syntactic structurecha mwaka (1957).
Mtazamo wa sarufi zalishiulijikita katika uundji wa nadharia ambayo
ingeeleza namna lugha hutumiwa na watumiaji wake hususani, jinsi
wanavyotumia kanuni chache katikalugha yao kuzalisha sentensi nyingi
na zisizo na kikomo. Kutokana na uwezo huu mzawa wa lugha huweza
kuunda tungo ambazo ni sahihi na ambazo si sahihi (Matinde,2012).

Chomsky, amewasilisha mtazamo wa Sintaksia unaotambuliwa kama


Sarufi zalishikatika kaziyake.Chomsky alikusudia kukuza fafanuzi
mwafaka za hali ya sintaksia ya lugha mbalimbali,yaani jinsi lugha
mahususi zinavyounganisha maneno kuunda sentensi.Vile vile kazi hiyo
ilidhamiria kukuza nadharia ya kijumla ya sintaksia inayobainisha ni
mambo yapi ya kijumla yanayopatikana katika lugha mbali mbali na
jinsi gani masualahayo yanavyotofautiana katika uwanja huu wa
sintaksia.
“In linguistics, generative grammar is a grammar (or set of rules) that
indicate the structure and interpretation of sentences which native
speakers of a languages accept as belonging to the language”
Sarufi zalishi ni sarufi mkusanyiko wa kanuni inayoonesha muundo na
tafsiri ya sentensi ambayo mzungumzaji wa lugha (mzawa) au mmilisi
wanavyo ipokea kama ilivyo.
Dhana za msingi za nadharia za sarufi zalishi;
Umilisi, ni ujuzi au uelewa wa kanuni zinazotawala lugha fulani ambazo
kila mzungumzaji wa lugha asilia huwa nao. Ujuzi huu huhodhiwa
ubongoni mwa mzawa wa lughana ndio humwezesha kutunga tungo
nyingi na zenye urefu wowote.
Ujuzi huu huhusu kanuni zinazotawala lugha hiyo husika. Ujuzi huu
humwezesha kutambua sentensi sahihi, zisizo sahihi na kupambanua
sentensi zenye utata. Pia humwezesha kupuuza makosa katika
mazungumzo kama vile kuteleza kwa ulimi, na kukatisha sentensi.
Chomsky anaeleza kuwa mtu anapojifunza lugha huanzia na umilisi na
anaendelea kudai kuwa kwa kiasi kikubwa umilisi wanaokuwa nao
wazawa wa lugha moja hufanana na hii ndiyo inayowafanya waelewane
katika mazungumzo yao kwamba mzungumzaji anasema kile
anachotaka kusema na msikilizaji anaelewa kile kilichosemwa na
msikilizaji.(Rubanza,2003).
Umilisi humwezesha mzawa wa lugha;
Ø kutambua sentensi sahihi na ambazo si sahihi mfano:
i) (Sahihi) Mwalimu anafundisha wanafunzi darasani.
(Si sahihi)Wanafunzi anafundisha mwalimu darasni.
ii) (Sahihi) Mtoto mdogo anaimba.
(si sahihi) Anaimba mdogo mtoto.

Ø Kutunga sentensi nyingi zenye urefu wowote :


i) Msichana mrembo mrefu mweusi alikamatwa bustanini
jana jioni, akiiba matunda ya mzee Juma na kupelekwa
kituo kidogo cha polisi kwa maelezo zaidi.
ii) Mtoto mdogo aliyeanguka jana jioni na kuvunjika mkono,
amepelekwa hospitalilakini bado hali yake ni mbaya hivyo
madaktari wameamua kumpeleka hosipitali ya mifupa kwa
uchunguzi zaidi ili kupata suluhisho la tatizo lake.
Ø kutambua sentensi zenye maana sawa.
Mfano;
i) Watoto wanakula chakula.
Chakula kinaliwa na watoto.
ii) Mama anapika chakula.
Chakula kinapikwa na mama.
Ø kutambua sentensi zenye utata, mfano;
i) Juma amenunua mbuzi.
Utata upo katika neno mbuzi lenye maana zaidi ya moja.
Mbuzi kama kifaa cha kukunia nazi
Mbuzi kama mnyama.
ii) Mama ana paa.
Utata upo katika neno paa lenye maana zaidi ya moja.
Paa kama kitendo cha kukwea juu ya, mfano mti, mlima,
angani.
Paa kama mnyama aishie polini.
Ø Kutambua muundo wa tungo katika lugha yake na vipashio vyake.
Mfano;
i) Mbunnge wetu amewasili jimboni.(Tungo sahili)
ii) Kitabu kilichopotea kimepatikana. (Tungo changamano).

Ø Kutambua aina mbalimbali za sentensi katika lugha yake


Mfano;
i) Mwalimu anafundisha Kiswahili. (Sentensi arifu).
ii) Shika chini. (Sentensi amrishi).
iii) Wanafunzi wangapi wamefika? (Sentensi ulizi).
iv) Mapunda, na wewe umefika! (Senteansi mshangao).
v) Lugano angalikuja mapema angalimkuta Amiri. (Sentensi
shurutia).

Ø Kutambua sentensi zenye maana na zile zisizo na maana.


Mfano;
i) Baba analima shamba.
ii) Shamba analima baba.
Hivyo ili kutambua sentensi zenye maana na zile zisizo na maana,
kulingana na muundo wa sentensi za kiswahili, muundo wa sentensi
zilizopo katika mfano wa pili si sahihi kwani zimekiuka sintaksia ya
lugha yaKiswahili.
Utendaji ni dhana mojawapo ya sarufi zalishi, hurejelea usemaji na
utumizi wa ujuzi wa mzawa wa lugha katika kutumia lugha yake ndani
ya muktadha wa lugha mahususi. Utumizi huu wa lugha huzingatia :-
· Muktadha:
Mifano,
- Kaniletee chaki ofisini (shuleni)
- Nani wa kuondoka? (stendi).
- Amependeza hajapendeza? Bibi kampata bwana na bwana kampata
bibi ( ukumbini).

· Uhusiano baina ya wahusika,


Mifano;
Mchungaji na waumini;
Mchungaji: Bwana Yesu asifiwe.
Waumini: ameeeen.
Mchungaji: leo bwana amenionesha
Waumini: ameeeeeni.

Mzazi na mtoto
Mzazi: Amina leo mmejifunza nini shuleni?
Mtoto: Tumejifuna kiswahili mama.
Mzazi: Vizuri mwanangu, sasa kabadilishe nguo chakula
kiko jikoni,
alafu uoshe vyombo.
Mtoto: Sawa mama.
Hakimu na mshtakiwa.
Hakimu: Mshtakiwa una lolote la kujitetea?
Mshtakiwa: Ndio mweshimiwa hakimu.
Hakimu: Jitetee.
Mstakiwa: Mheshimiwa naomba mahakama
inipunguzie adhabu kwa
sababu nikosa langu la kwanza pia nina familia
inayonitegemea.
Daktari na mgonjwa.
Daktari: Meza mbili kutwa mara tatu (2×3×7)
Mgonjwa: Sawa daktari.
Daktari: Hakikisha unakunywa maji ya kutosha.
Mgonjwa: Sawa daktari.
Hivyo basi katika utumizi wa lugha uhusiano baina ya wahusika
huwawezesha kuteua aina ya mazungumzo yanayostahili kulingana na
mazungumzo husika.
Mada ya mazungumzo
Mfano;
Mada ya kisiasa.
Kiongozi: “People’s”
Wananchi: “Power”
Kiongozi: Leo ni siku pekee ya kuzungumza na
wananchi, naomba
mniskilize kwa makini.
Mada ya afya.
Bwana afya: Ndugu zangu chimbeni mashimo ili tuondokane na
magonjwa ya
kuambukiza kama yanayojitokeza katika kijiji chajirani.
Wanakijiji: Sawa mkuu, tutatekeleza.
Dhumuni la mazungumzo.
Mfano;
Dhumuni la kuelimisha;
Mshauri nasaha: Kutokana na majibu ya vipimo vyako, inabidi ule
vizuri chakula bora
ikiwa ni pamoja na matunda,pia upate muda wa kupumzika.
Ukizingatiahaya utaishi kwamatumaini.
Mgonjwa: Sawa.
Dhumuni la kuonya.
Mazungumzo kati ya mzazi na mtoto:
Mzazi: Siku hizi umekua ukichelewa kurudi nyumbani,
kinachokuchelewesha
kinachokuchelewesha

nini?
Mtoto: Usafiri mama.
Mzazi: Usafiri gani huo mpaka saa nne za usiku? mbona Aisha
amewahi
kurudi?
Mtoto: (kimya).

Mtoto: (kimya).
Mzazi: Mwanangu dunia haiko hivyo unavyodhani, umebadilika
sana siku hizi. Ujana
una mambo mengi, ni vyema uutumie ujana wako vizuri,
kumbuka kuna
magonjwa hatari na yasiyotibika.
Dhumuni la kuburudisha:
Mfano;
Mshereheshaji na wageni waalikwa:
Mshereheshaji: Piga vigelegele kwa maharusi wetu jamani.
Wageni waalikwa: Kilililiiiiiiiiiiiii ………………..
Mshereheshaji: Mwenye wivuuuuu…………...
Wageni waalikwa: Ajinyongeeeee ……………….
· Jinsi.
Tofauti za kimaumbile baina ya ke na me hupelekea wazungumzaji
wazawa wa lugha kuteua aina fulani ya lugha ya mazungumzo kutokana
na jinsi zao.
Mfano;
Mazungumzo kati ya mwanamke na mwanamke:
Asha: Mambo shosti?
Getrude: Safi tu shoga angu.
Asha: Nakuona umepodoka si mchezo?
Getrude: Mambo ya mfikemo hayooo ………..
Mazungumzo kati ya mwanaume na mwanaume,
Juma: Nambie kamanda.

Hamisi: Poa jembe langu.


Juma: Ishu zinaendaje?
Hamisi: Burudani, kuchakarika tu.
Hata hivyo utendaji huweza kuathiriwa na kasoro za kimatamshi, hasira,
furaha, uchovu,ulevi na matatizo ya kumbukumbu.
Umbo la ndani.
Katika umbo hili hujitokeza katika sentensi kabla haijafanyiwa mchakato
wa kimofofonolojia. Umbo la ndani hubeba maana kamili ya tungo na
vipashio vya tungo hubainika bayana, kwani huwa havijafanyiwa
michakato yoyote.
Sentensi zifuatazo zina umbo la ndani:
Kitabu alikionipa.
Mjengi wa nyumba.
Mpiki wa chakula.
Baada ya sentensi hizi kuambikwa viambishi vipatanishi vya
kisarufi(baada ya mchakato wa kimofofonolojia) tunapata sentensi
ambazo zipo kweny umbo la nje.
Kitabu alichonipa.
Mjenzi wa nyumba.
Mpishi wa chakula.
Umbo la nje;
Umbo hili hutokea baada ya umbo la ndani kufanyiwa mageuzi au
mchakato wa kimofofonolojia muhimu hadi kufikia kiwango cha usemaji
sahihi na unaokubalika, kwa hivyo umbo la nje hudhihirika kimatamshi
na kiothografia. Umbo hili haliwezi kufanyiwa michakato zaidi.

Mifano,
Umbo la ndani Umbo la nje
Juma umwa maino. Juma anaumwa meno
Mama piki kiakula. Mama anapika
chakula
Kijana mwibi. Kijana mwizi.
Uchamko;
Uchamko ni utaratibu wa kutumia sheria fulani ambazo huweza
kutumika mara kwa mara katika kuunda sentensi ambazo zina urefu
usio na kikomo.Uchamko, hutokana na sentensi zaidi ya moja
kupachikwa katika Sentensi ile ya kwanza ili kuunda sentensi moja isiyo
na kikomo, uchamko hujitokeza katika aina kuu mbili, ambao ni
utegemezi na uambatanishaji.
Utegemezi;
Uteggemezi ni aina ya uchamko ambao hutokana na matumizi ya
maneno kama: kuwa, kwamba, kama, na ili. Pia hutokana na hali ya
kuwepo au kutokea kwa kipashio kimoja cha kiisimu ambacho
hutegemea uwepo wa kipashio kingine. Utegemezi huweza kutokana na;
Upachikaji kwa kutumia vijalizi na urejeshi ambao hutumiwa kuunda
sentensi changamano.
Mfano,
Mbuzi aliyechinjwa jana amepikwa leo.
S
KN KT

N βv T E

Mbuzi aliyechinjwa jana amepikwa leo.


Uambatanishaji;
Uchamko pia huweza kudhihiriishwa na uambatanishaji wa sentensi,
huu ni uchamko ambao hutokana na sentensi ambbatano.
Mfano,
S
KN1 KT1

N1 T1 S2
KN2 KT2

N2 T2 U S3

KN3
KT3

N3 T3

Mtoto anacheza baba analima na


dada anaimba.
Dhana ya mwisho ya sarufi zalishi ni uchamko, uchamko ni utaratibu
wa kutumia sheria fulani ambazo huweza kutumika mara kwa mara
katika kuunda sentensi ambazo zina urefu usio na kikomo. Uchamko
hutokana na sentensi zaidi ya moja kupachikwa katika Sentensi ile ya
kwanza ili kuunda sentensi moja isiyo na kikomo. Pia hutumia kanuni
chache kutunga sentensi nyingi zisizo na kikomo. Uchamko
umegawanyika katika sehemu mbili yaani utegemezi na uambatanishaji.

Utegemezi
Ni uchamko ambao hutokana na hali ya kuwepo au kutokuwepo
Ni uchamko ambao hutokana na hali ya kuwepo au kutokuwepo

kipashio kimoja cha kiisimu ambacho kinategemea uwepo wa kipashio


kingine. Utegemezi hutambulishwa na maneno kama vile; ili, kwamba,
kama na kuwa. (Matinde, 2012)
Mfano; Ambakisye alijua kuwa Ndope anafahamu kuwa shule itafunga
kesho.
Asha anajua kuwa mimi najua kuwa atafaulu mtihani.

Uambatanishaji.
Ni aina ya uchamko ambao hudhihirishwa na uambatishaji wa sentensi
sahili mbili au zaidi. Kwahiyo, huu ni uchamko ambao hutokana na
sentensi ambatano.
Mfano;
Shangazi anapika, mama anaandaa chakula na baba anakula.

S1

KN KT

N T S2

Shangazi anapika KN KT

N T N U
S3

mama anaandaa chakula


na KN KT

N
T
T

baba
anakula

Kama ilivyo kwa nadharia zingine, nadharia hii pia ina ubora na udhaifu
wake.
Ubora wa nadharia hii.
· Imeweza kuonesha umilisi alionao binadamu katika lugha yake, kuwa
anaweza kuzalisha tungo au sentensi mbalimbali kwa kutumia kanuni
chache zilizopo katika lugha yake.Umilisi huo humsaidia mtumiaji wa
lugha kuunda sentensi hizo hata kama hajui kusoma na kuandika.
· Pia nadharia hii inaonesha kuwa kila mzungumzaji wa lugha
huzifahamu vizuri kanuni chache zilizopo katika lugha yake na
kuzitumia kanuni hizi katika kuwasiliana na jamii inayomzunguka.
· Vilevile nadharia hii ya sarufi zalishi imeweza kuonesha kuwa
binadamu anao uwezo wa kufafanua kipi ni sahihi na kipi sio sahihi
katika uteuzi wa maneno wakati wa uzungumzaji.
· Nadharia hii inamchukulia binadamu kama kiumbe chenye uwezo
endelevu wa kuzalisha sentensi ambayo inaweza kueleweka kwa jamii
inayomzunguka.
· Pia nadharia inatuonesha kwamba upo uhusiano mkubwa kati ya akili,
kufikiri na lugha.Hususan katika dhana ya utendaji mtumiaji wa lugha
anatakiwa kutumia akili anapoteua lugha ya kutumia ili kuendana na
muktadha.
Udhaifu wa nadharia hii.
· Inafafanua namna au jinsi watu wanavyozungumza lugha na sio
kuwaeleza wazungumze vipi lugha hiyo itumike.
· Haitilii mkazo mabadiliko katika lugha hata kama yapo.
· Vipengele kama umbo la ndani na umbo la nje vinaweza kumchanganya
mtu anaejifunza lugha.
Hivyo ni kweli kwamba nadharia ya sarufi zalishi imeleta mapinduzi
makubwa katika taaluma ya sarufi miundo.
MAREJEO
Kapinga, (2012), Katika Dafina ya Lugha: Serengeti Education Publishers
(T) Ltd, Mwanza.
Kihore Y, M. Massamba, D.P. B na Msanjila, Y. P. (2012),Sarufi Maumbo ya
Kiswahili
Sanifu (SAMAKISA): TUKI, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Massamba, D. P. B, Kihore, Y, M na Hokororo, J. I,(2001), Sarufi Miundo ya
Kiswahili
Kiswahili Lugha
Sanifu(SAMIKISA): Tamu
TUKI: Duniani.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Massamba, D. P. B, na wenzake(2004),Kamsi ya Isimu Falsafa ya Lugha:


TUKI,

Dar es Salaam.
Matinde, L. (2012),Dafina ya Lugha: Serengeti Education Publishers (T)
Ltd, Mwanza.
Pei na Gaynor, (2012), Katika Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu
(SAMAKISA): TUKI,
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
TUKI, (1999), Kamsi Sanifu ya Isimu ya Lugha: Chuo Kikuu cha Dar er
Salaam.

Anonymous 12 October 2022 at 00:02

tofauti kati ya dhana za utedaji na umilisi ni zipi???

REPLY

Anonymous 9 December 2022 at 21:54


Anonymous 9 December 2022 at 21:54

Judikay nerfuler

REPLY

Anonymous 9 December 2022 at 21:55

Hongera
REPLY

Enter comment

Popular posts from this blog

notes za malenga wapya,uhakiki wa shairi la malenga wapya.


May 07, 2017

UHAKIKI WA MASHAIRI YA MALENGA WAPYA \MWANDISHI: TAASISI YA


KISWAHILI, ZANZIBAR WACHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS MWAKA:
2001 JINA LA KITABU Jina la kitabu linasadifu yaliyomo katika kitabu. Kwa upande …

READ MORE

maana ya sintaksia,uhusiano wa sintaksia na matawi mengine,malengo ya


sintaksia au isimu miundo, vipashio vya lugha ni vipi?,
April 20, 2017

TUKI (1990) wanaeleza na wanafasili dhana hii ya sintaksia au


isimu miundo kuwa ni tawi la sarufi linaloshughulikia uchanganuzi
wa mpangilio na uhusiano wa vipashio katika kila sentensi. …

READ MORE

Powered by Blogger
Theme images by Galeries

trix titus

You might also like