You are on page 1of 7

Dhana ya lahaja

Dhana ya lahaja ni changamani, hutokana na jinsi mtu aliyefasili dhana hiyo


anatumia kigezo kipi. Mfano, kuna kigezo cha isimujamii, hiki ni kigezo cha
kuwashirikisha wanajamii au wazungumzaji wa lahaja hiyo na ukapata
msimamo wao kuhusu lahaja hiyo. Pia kuna kigezo cha kiisimu; hiki kigezo
cha kutofautisha lugha na lahaja nyingine kwa kutumia vigezo vya msamiati
wa msingi, fonolojia, pamoja na mofolojia.

Lahaja pia inaweza kufasiliwa kwa kuzingatia utengano wa kijiografia au


kijamii. Hii ana maana kwamba unaweza kusikia kuwa lahaja fulani
inazungumzwa mahala fulani au huzungumzwa na kundi la watu fulani.
Mfano, lahaja ya kitumbatu huzungumzwa sehemu za kisiwa cha Tumbatu
vivyo hivyo lahaja ya kipemba huzungumzwa na watu wa Pemba.

Hebu tuangalie uchangamani wa dhana ya lahaja kwa kuangalia


fasili zifuatazo:
Msanjila (2009:124) anasema lahaja ni lugha mojawapo kati ya lugha
ambazo kimsingi kuhesabiwa kuwa lugha moja isipokuwa zinatofautiana
katika baadhi ya vipengele fulani fulani kama vile lafudhi, fonolojia, msamiati
usiokuwa wa msingi au muundo kutokana na eneo lugha hiyo
inazungumzwa.

Massamba (2002) anasema kuwa lahaja ni lugha mbalimbali za pwani


zilizokuwa na uhusianao wa karibu sana. Lugha hizo ni kama vile ci-mbalazi,
ki-amu, ki-mvita, ki-jomvu, ki-mtang’ata, ki-makunduchi, ki-tumbatu, ki-
mgao na ki-unguja. Wakati wengine wanaziita lahaja mfano, Polome (1967),
Bryan (1959) pamoja na Temu (1980).

Kwa mujibu wa Wikipedia, Kamusi elezo huru lahaja ni vilugha vidogo


vidogo vya lugha moja ambavyo hubainika kijamii au kijiografia.

Mwingisi – Chuo Kikuu cha Nairobi


Ukizitazama fasili hizi kwa makini utagundu kuwa kila mtu ana mtazano
wake kuhusu lahaja, wengine wanasema ni vilugha, ni lugha inayojitegemea,
wengine wanasema ni tofauti ndogondogo hasa za kimatamshi katika lugha
moja. Lakini pia wengine wanaona lahaja ni tofauti za lugha kwa kigezo cha
kijiografia na wengine wanaona ni tofauti za kijamii na kijiografia. Kwa hiyo
mitazamo hii ndio hulete utata na uchangamani katika kufasili dhana ya
lahaja.

Kimsingi fasili iliyotolewa na Msanjila (keshatajwa) inaweza kutusaidia kujua


dhana ya lahaja kwani fasili hii ni ya kiutendaji.Kwa hiyo lahaja ni lugha
mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi kuhesabiwa kuwa lugha moja
isipokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani fulani kama vile
lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au muundo kutokana na
eneo lugha hiyo inamozungumzwa.

Mjadala kuhusu idadi ya lahaja za kiswahili na namna lahaja hizi


vilivyoinukia:
Mjadala hu ulianza siku nyingi kidogo na hadi sasa hivi hakuna utafiti wa hivi
karibuni unaoweza kutusaidia kuthibitisha idadi kamili za lahaji za Kiswahili.
Hebu tuangalie wataalam jinsi wanavyojadili idadi ya lahaja za Kiswahili.

Chiraghdin na Mnyampala (1977) wametaja idadi ya lahaja ishirini, lahaja


hizo ni kama vile; Kiunguja, Kimrima, Kimgao, Kimvita, Kihadimu, Kipemba,
Kirumba, Kiamu, Kipate, Kisiu, Kitikuu, Kingazija, Kingozi, Kitumbatu,
Kimtang’ata, Chichifundi, Chibalanzi, Kingwana, Kinyare, na Kijomvu.

Nurse na Spear (1985) wametaja idadi ya lahaja kumi na sita (16), na


wamezigawa katika makundi mawili ambayo ni kundi la kaskazini na kundi la

Mwingisi – Chuo Kikuu cha Nairobi


kusini. Mfano kundi la kaskazini lina lahaja saba (7) wakati kundi la kusini
lina lahaja tisa (9). Baadhi ya lahaja hizo ni;- Kipate, Chimiini, Kibajuni,
Kisiu, Kijomvu, Chifunzi, Kipate, Kiunguja, Kimtang’ata, Kimakunduchi na
kuendelea.
Utata kuhusu idadi za lahaja za kiswahili unatokana na sababu zifuatazo;

Kigezo kilichotumika katika kufanya utafiti wa lahaja za kiswahili. Unaweza


kufanya utafiti wa lahaja za kiswahili kwa kutumia kigezo cha kijiografia,
kijamii, pamoja na kiisimu. Vigezo hivyo vyote vinaweza kukupatia idadi
tofauti za lahaja mfano, Massamba katika utafiti wake kwa kutumia kigezo
cha kiisimu (1977) alifanya utafiti katika jamii za chi-ruri, chi-jita, na ki-
kwaya akathibitisha kuwa hizi ni lahaja za lugha moja na si tofauti, pia kwa
kutumia kigezo cha utengano wa kijiografia na kijamii mfano katika lugha ya
Kiswahili kwa kiasi kikubwa uanishaji umefanywa kwa utengano wa
kijiografia kama vile, kipate kinazungumzwa sehemu za Pate na lahaja ya
kipemba huzungumzwa Pemba. Hivyo kutokana na sababu kama hizi
husababisha watafiti wengi kutofautiana katika kupata idadi kamili za lahaja.

Kutokana na kukurubiana na kusigana kwa namna fulani kwa lahaja za


Kiswahili, kukurubiana huko kwa lugha na mipaka ndiko kunakofanya
wazungumzaji wake wajihisi wanazungumza lugha moja. Pia kusigana kwake
kwa lahaja hizi husababisha hawa watu wajihisi wanazungumza lugha
tofauti. Mfano, lakabu ya lugha ya Kiswahili tunaweza kuifananisha na lugha
ya kichaga. Wachaga na lugha zao zote kuhesabiwa kuwa kichaga lakini
lugha hizo pia zinatofautiana mfano, ki-machone, kinatofautiana na ki-
rombo, ki-marangu, ki-kibosho na kusababisha wasemaji wa lugha hii ya
kichagga kushindwa kuelewana kabisa ( Massamba 2002: 258) na hata
Wazaramo,Wakwele,Waruguru hujihisi wanazungumza lugha zenye nasaba
moja.

Mwingisi – Chuo Kikuu cha Nairobi


Kutokana na kutofautiana kwa majina ya lahaja kuna baadhi ya majina ya
lahaja moja hutajwa tofautitofauti na wataalamu mbalimbali, mfano
Chiraghdin na Mnyampala (1977) wanataja jina la lahaja ya kihadimu wakati
Temu (1980), anasema lahaja ya kihadimu aliita kimakunduchi. Vivyo hivyo
Nurse na Spear (1985) wanasema lahaja hiyo ni Kimakunduchi. Hivyo
inaleta utata katika kujua kwamba hii ni lahaja moja au ni lahaja mbili
tofauti. Pia Bryan (1959) anaitaja lahaja ya Kimbalazi na Polome (1967)
ameiita kibrava, Whiteley (1969) ameiita Chimiini, Chiraghin na Mnyampala
wanaiita Chibalazi.
Pia kutokana na maendeleo ya Kiswahili sanifu, mfano mpaka sasa
kunabaadhi ya lahaja zimebakia kimaandishi lakini kiuhalisia hazipo na
hazitumiki katika lugha ya Kiswahili, mfano, lahaja ya Kimgao iliyokuwa
inapatikana sehemu za Kilwa imo kwenye maandishi ya wataalamu kama
vile Chiraghdin na Mnyampala (1977), Nurse na Spear (1985), Temu (1980).
Lakini watumiaji wake hivi sasa wanatumia Kiswahili sanifu, kwa hiyo inaleta
utata katika kupata idadi kamili ya lahaja za Kiswahili.
Pia kuna baadhi ya lahaja zipo na zinatumika lakini baadhi ya wanazuoni
hawajaziweka katika maandishi. Mfano, kiunguja kinachopatikana Unguja
kipo lakini cha kushangaza baadhi ya wanazuoni kama vile Whiteley (1969),
Temu (1980) pamoja na Nurse na Spear (1985) hawajaziweka katika
maandishi.
Kwa ujumla hakuna idadi kamili ya lahaja. Unaweza kupata idadi ya lahaja
kwa kuzingatia mtaalamu na kigezo alichotumia, suala la muda, na mahali
unapoenda kufanyia utafiti wa hizo lahaja.

Kuinukia kwa lahaja

Mwingisi – Chuo Kikuu cha Nairobi


Kuna wataalam mbali mbali wanaeleza namna ambavyo lahaja mbalimbali
za lugha ya Kiswahili zilivyoinukia. Wataalamu hawa wamegawanywa katika
makundi mawili:

Kundi la kwanza; hili ni lile kundi la wanaoamini kuwa lahaja za lugha ya


Kiswahili kwa ujumla zilianza sehemu fulani maalum.

Kundi la pili; Wanaoamini kuwa lahaja zilianzia sehemu mbalimbali kwa


wakati mmoja japo kwa kiwango tofauti.

Wafuasi wanaoamini kuwa lahaja kwa ujumla zilianza sehemu fulani


maalumu au sehemu moja wanajikita katika hoja ya msingi kuwa lugha
huanzia sehemu moja maalum na kusambaa sehemu nyingine na hii
hutokana na kadri matumizi yanavyoongezeka na idadi ya watu
inavyoongezeka ndivyo watu hawa hutawanyika kwenda sehemu
tofautitofauti na kusababisha kutokea kwa lahaja tofautitofauti za kiswahili.

Kwa mujibu wa Nurse na Spear (1985) lugha huanzia mahali fulani pamoja
katika kipindi fulani kadri wasemaji wanavyoongezeka na lugha huanza
kubadilika na kuwa ya ana kwa ana. Hivyo kutokana na sababu ya
kutawanyika kunapelekea kutokea kwa lahaja tofautitofauti. Mfano; hawa
wanazuoni wanadai kuwa lahaja za kiswahili zilianzia kaskazini mwa
Mombasa katika eneo la Lamu na kuendelea sehemu nyingine ya pwani ya
Afrika Mashariki na hii ni kutokana na kwamba utafiti wa akiolojia unaonesha
kuwa mbantu wa kwanza kabisa aliishi katika mji wa Lamu. Udhaifu wa
mtazamo huu ni kwamba kama watu hao wametokea katika jamii moja
yenye lugha moja, hivyo ni vipi wanaweza kutambulishwa kutumia lahaja
zao yaani lahaja za kaskazini na lahaja za kusini.

Mwingisi – Chuo Kikuu cha Nairobi


Pia suala la muingiliano wa lugha kutokana na mabadiliko na maendeleo
katika jamii halina nafasi katika maendeleo ya lugha. Kutokana na udhaifu
huu kukapelea kutokea kwa kundi jingine.
Kundi la wale wanaoamini kuwa lahaja zilianzia sehemu mbalimbali kwa
wakati mmoja ila kwa kiwango tofauti. Ugunduzi wa kiakiolojia wa hivi
karibuni unaonesha maeneo mengine kama vile Unguja, Pemba na Kilwa.
Mfano, Mji wa Kilwa kuwa maarufu kuliko mji wa Lamu. Ugunduzi huu
unaonesha kuwa mbantu wa mwanzo aliishi Kilwa na sio Lamu kama
inavyoelezwa na Nurse na Spear (1985). Kwa hiyo maelezo hayo
yanatuonesha kuwa mji wa Kilwa ulikuwa maarufu zaidi kuliko Lamu.

Ni kutokana na ukinzani wa mji wa Kilwa na Lamu kiumaarufu ndipo


wataalum wengine wakasema kuwa lahaja za Kiswahili ziliinukia sehemu
mbalimbali kwa kipindi kimoja japo kwa kiwango tofauti.

Grenville (1959) katika makala yake ya “Medieval Evidence for Swahili”


anasema wazo la kuinukia mapema kwa Kiswahili katika Kilwa na
hakubaliani na fikra za kuwa lugha ilianzia Lamu kwani hata kumbukumbu
za kihistoria kipindi cha kati zinadai kuwa mji wa Kilwa ulikua maarufu kuliko
Lamu, hii ni kutokana na shughuli za kiuchumi zilizokuwa zinaendelea.

Pia Massamba (2007) anasema, hizi zinazoitwa lahaja za Kiswahili za sasa


ziliinukia sawia sawia katika maeneo mbalimbali na kwa sababu ya
kuingiliana kibiashara, kiuchumi na kijamii na huu ndio ukawa ndiyo mwanzo
ya lahaja ya Kiswahili sanifu. Kwa mtazamo wake, Massamba anadai kuwa,
lahaja za Kiswahili tunazozifahamu hivi sasa kama vile; kimakunduchi,
kipate, kiamu, kimvita pamoja na kiunguja hapo zamani ziliitwa lugha
zinazojitegemea. Lugha hizi ziliathiriana kutokana na ukaribu wake na zaidi

Mwingisi – Chuo Kikuu cha Nairobi


kwa sababu zilitokana na mame bantu moja. Hivyo ukizichunguza kwa
umakini utagundua kuwa zilizokaribu zinafanana sana kuliko zilizo mbali. Pia
lugha zilizo malikuu moja hufanana lakini lugha zilizokaribu hufanana zaidi.

Mwingisi – Chuo Kikuu cha Nairobi

You might also like