You are on page 1of 62

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili

­­­______________________________________________________
_______

Kongamano la Jubilei ya Miaka 75 ya TUKI

Tarehe 4 – 7 Julai, 2005

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

John P. Mbonde
Utangulizi

Katika kuziainisha methali, watu hupenda kuziita kuwa hizi ni za


asili ya jamii fulani kama vile ya Kihispania na zile ni za Kiafrika
au hizi ni za Kimaasai na hizo ni za Kingoni n.k. Aina hii ya
methali, jamii huzidai kuwa ni za asili ya jamii yake (kabila
fulani), na hivyo, huzifanya kuwa ni mali yake kiutamaduni
kama zilivyo mila na desturi tofauti mbalimbali katika jamii hiyo
husika. Kumbe kati ya methali hizo zote, baadhi yake hutumika
mahali pote duniani. Aina hii ya methali zitumikazo mahali pengi
duniani, ingawa huundwa katika lugha tofauti mbalimbali na
wakati mwingine kwa mipangilio yake ya maneno hutofautiana,
lakini maana yake huwa ni ileile.

Ni kwa mantiki hiyo, nimeamua kuziita Methali za Kiutandawazi.


Nafahamu pia kwamba baadhi ya wanataaluma wangependa
kuziita ni
Methali za Kimataifa
. Jina lolote linaloweza kutumika kuainisha methali hizo, halina
utata wala mjadala kwa kuwa zinatumika miongoni mwa
mataifa mengi duniani kote. Kamwe methali hizo siyo mpya
wala za ajabu wala hazina hadhi ya milenia ya tatu kwa
maumbile, bali ni zilezile ambazo zimezoeleka katika matumizi
ya kila siku. Ila inawezekana kwamba zinaweza kuwa za asili
ya jamii fulani zilizoanza kuzitumia, au hupendelea kuzitumia
mara nyingi zaidi kuliko jamii nyingine kwa msukumo wa

2 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

mazingira. Kwa mfano, lugha ya Kispanishi ina utajiri mkubwa


sana wa methali kuliko lugha nyingi duniani. Hali kadhalika,
Kichina kimefaulu kuhifadhi methali zake kwa wingi tangu karne
na karne.

Madhumuni ya kuzikusanya na kuzihifadhi pamoja ni


kurahisisha upatikanaji wake. Fauko ya hayo, huu ni wakati
muafaka wa kuzijengea uhalali na hadhi yakinifu methali za
kiutandawazi ili kwenda sambamba na maendeleo endelevu ya
kisayansi na kiteknolojia. Ifahamike wazi kuwa bado suala hilo
linahitaji kufanyiwa tafiti za kina kirefu ili kuboresha dhana hiyo.

Mwenendo wa methali za kiutandawazi hautofautiani na ule wa


methali za kawaida. Ni dhahiri kuwa baadhi ya vigezo vya
kubainisha methali za kiutandawazi ni ile tabia ya taswira za
kimataifa zilizobebwa nazo. Baadhi ya methali huhusishwa na
vitu vya eneo dogo la nchi, lakini zile za kiutandawazi hazina
mipaka. Kwa mfano, Waarabu wa Pemba hujuana kwa
vilemba. Pemba ni kisiwa katika bahari ya
Hindi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilemba ni
vitambaa wafungazo vichwani. Tabia ya kufunga vilemba vya
aina hiyo, hujitokeza huko Pemba miongoni mwa Waarabu
katika mashamba ya karafuu. Ingawa maana ya ndani ya
methali hii yaweza kabisa kuwa ya kimataifa, yaani ya
kiutandawazi. Mathalani, wazungu watawapendelea wazungu
wenzao. Ufinyu wa methali za mahali ni sawa na jinsi aina

3 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

fulani za mila hutawala jamii ndogo ya mahali hapo tu. Kumbe


methali Wapiganapo tembo, nyasi
huumia (When elephants fight, the reeds get hurt),
hii ni methali ya kiutandawazi.

Kwa upande mwingine, baadhi ya methali huwa hazitumiki kila


siku, katika ufinyu au utandawazi wake, badala yake huwa
zimebaki katika vitabu tu. Ukweli ni kwamba hata baadhi ya
misamiati katika kamusi za aina zote za lugha, hubaki katika
vitabu kwani matumizi yake ni ya nadra mno kwa sababu au
bila sababu za kimsingi. Na kila zinapotumika husikika kuwa ni
ngeni katika masikio ya wasikilizaji wake. Hata nchini Tanzania
ambako ni chimbuko la historia ya Kiswahili, hususan Zanzibar,
kwa namna moja au nyingine, Waswahili hao, si hoja kama ni
wasomi au watu wa kawaida, wanaposikia mtu akitumia
msamiati au istilahi iwayo utawasikia wakishutumu, “Kiswahili
cha siku hizi ni kigumu, jamani! Afadhali ya Kiingereza.” Vivyo
hivyo, iwapo Mwiingereza msomi akitumia misamiati
isiyotumika katika maisha ya kila siku ya jamii ya Waingereza,
wanaposikia hayo hulaani na kusema, “Kiingereza cha wasomi
wa siku hizi ni kigumu (bombastic).

4 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Nini maana ya methali?

Methali ni lugha nyepesi ipenyayo moja kwa moja katika mioyo


ya wasikilizaji. Aidha, methali au misemo huondoa wingu au
ukungu katika mawasiliano ya kisayansi na ya teknolojia nzito
za kitaaluma. Pia, methali ni kielelezo cha utashi wa uhai wa
jamii husika, historia na falsafa ya utu wa binadamu, hekima na
busara. Mwanafasihi mashuhuri katika Afrika, Chinua Achebe,
katika kitabu chake Things Fall Apart (1959: 7) anaandika, “Met
hali ni mafuta ya mawese ambayo kwayo maneno huliwa.”
Kauli hii ikizingatiwa barabara huyafanya maandishi kukubalika
kuwa ni fasihi, maana matumizi ya methali na fani nyingine
hukoleza simulizi kama tui la nazi na viungo mbalimbali kama
vile vitunguu, nyanya, zinavyoifanya mboga iwe na riha na
ladha tamu zaidi. Methali ni njia ya mkato ya kuelimisha,
kuadilisha, kukosoa na kuelekeza jamii, husuan vijana katika
kuzingatia tunu za jadi kwa kina ndani ya mazingira ya asili ya
jamii.

5 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

“ Methali ni aina ya usemi nzito na ambao unakusudiwa


kusema jambo maalumu lakini ya fumbo. Usemi huu
mzito mara nyingi hukusudiwa kumuonya, kumuongoza,
na kumuadilisha mwanadamu. Kwa umbile la nje methali
huwa na muundo maalumu, muundo wenye baadhi
(pande) mbili. Upande mmoja wa methali huwa unaeleza
mazoea au tabia ya mtu au kitu juu ya utendaji wa jambo;
na upande wa pili unaeleza matokeo yatokanayo na
mazoea hayo au tabia hiyo ambayo imeelezwa katika
upande wa kwanza.” (S. Y. A. Ngole na Lucas N.
Honero, Fasihi- Simulizi Methali: Kitabu cha pili, (uk viii)
TUKI, DUP 1981
.

Lugha ya Kiswahili ni tajiri sana kwa semi zake. Licha ya


methali, kuna misemo, misimu, nahau. Tofauti na methali
misemo ni tungo zitumiazo picha, ishara na tamathali kueleza
kitu au wazo kwa kifupi, ili litolewe maadili au maonyo au sifa
fulani. Kumbe vitendawili ni semi fupifupi za fumbo zenye
kutumia picha, tamathali na ishara kueleza wazo lililofichika
ambalo ndilo jawabu la fumbo. Kwa mfano, Koti la mzee
halikosi chawa.

6 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Na kwa upande wa misimu ni semi ndogondogo za kuibuka na


kufifia au kufa kabisa ambazo huzushwa katika mazingira
fulani, hufa baada ya mazingira yale kutoweka. Kwa mfano, Kla
bu ya Simba ilishinda kwa kishindo cha tsunami.(This coinage
was heard by the author while travelling in Dar es Salaam
comuters known as “Daladala” hence I personally call such
sayings as “Daladala Philosophy” which associate with
contemporary events such as ‘tsunami’ impact in which Simba
soccer club beat their long time rival, the Younger soccer club
with such impact as that of tsunami).
Pia, matumizi ya
msimu, k.m.
Mambo! Poa!
Huu ni msimu uliochipua na kuchanua miaka hii ya karibuni,
ambao nao siku itafika utanyauka na kufa. Hata Rais wa
awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Benjamin William Mkapa ameondokea kuupenda
na kuutumia mara nyingi sana anaposalimiana na wananchi
kabla ya kuzungumza au kuwahutubia. Akisha sema, “Mambo!”
Hadhira humkubalia kwa mkupuo mmoja, “Poa!”

“Methali hutupa maarifa;

hutupa ukweli kwa kifupi;

7 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

hufanana katika lugha mbalimbali za nchi kadha za


ulimwenguni;

hutumika hasa na wazee kufundisha vijana na watoto,


hali ya maisha duniani.” Kutoka katika Utangulizi wa
kitabu 500 Haya Proverbs kilichotungwa na Nestor, H.
Byera, EALB (1978).

Aidha, kuna ufafanuzi wa aina mbalimbali kutoka kwa


wanataaluma wa nyakati mbalimbali kuhusu dhana “methali”.
Katika Kamusi ya Kiswahili Sanifu 1981: 165 “Methali ni kifungu
cha maneno yanayotumiwa pamoja kisanii kwa njia ya kufumba
au kupigia mfano na ambacho kinachukua maana ndefu na
pana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa; muhtasari wa
maneno ya kisanii wenye maana pana k.v.
Mcheza kwao hutunzwa.”
Kuna baadhi ya hadithi nyingi huanza na methali na kumalizia
kwa methali. Kwa mfano, katika kitabu kilichotungwa na
Kayombo, Innocent Kapilima,
Hadithi za Babu Zetu wa Tanganyika,
TMP (1959), ametumia mtindo huo wa kuanza na ‘methali’ na
kumalizia na methali katika kusimulia hadithi zake.

Zipo methali nyingi ni za Kiafrika pale zinapohusisha na ishara

8 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

au vitu vipatikanazo katika mazingira yao. K.m. “Jifya moja


haliinjiki chungu.”

1.

Nini Maana ya Utandawazi?

Dhana ya utandawazi ilizuka mwishoni mwa miaka ya 1980 na


kushamiri miaka ya 1990 na kuwa changamoto katika nyanja
mbalimbali. Utandawazi ni upanukaji kwa kina kirefu zaidi na
kusambaa kwa masafa marefu mahusiano miongoni mwa jamii
mbalimbali mintarafu uhalisia wa maisha, kuanzia yale ya
ustawi wa jamii hadi yale ya harakati za kujikimu, kiuchumi,
kiutamaduni, kiulinzi, kibiashara, kiuwekezaji, kimawasiliano,
kiteknolojia na kuufanya mchakato mzima kuipelekea dunia iwe
mithili ya kijiji kimoja kidogo. Mvuvumko huo wa kiutandawazi
kiuchumi na kiutamaduni umeipa Marerkani nafasi ya kasi
kubwa ya katika kuhodhi na kudhibiti mageuzi hayo.

9 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

“ Kwa ufafanuzi wa jumla, dhana utandawazi inamaanisha


kuifanya dunia nzima ionekane

kama kijiji kimoja kwa kupanuka kwake kimawasiliano,


kijamii na kiuchumi katika uhalisia

wa mambo ulivyo katika nyanja mbalimbali kama vile


uchumi, utamaduni, biashara,

uwekezaji, kiteknolojia hata kiroho. Kutokana na welewa


huu inadaiwa kwamba uchumi wa

dunia umo katika mchakato wa kuoanishwa kwa kuvunja


mipaka na nguvu za kiuendeshaji

kuwa kitu kimoja.” S.M.Rugumamu, Globalization


Demystified, DUP
(2005).

10 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Waandishi wengine, kama vile C.K. Omari, Prof. E. Kezilahabi


na W.D. Kamera wanasisitiza katika vitabu vyao Misemo na
MethaliToka Tanzania (Kitabu cha I&II):

“ Misemo na Methali zimejaa wingi wa hekima na


mafundisho yanayoweza kutumika katika

kufafanua utamaduni wa jamii, muundo na mfumo wake,


siasa yake, uchumi na mazingira

yake.”

1.

Mantiki ya Methali za Kiutandawazi

11 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Nimeorodhesha baadhi tu ya methali zenye hadhi ya


utandawazi na kuelezea kwa kifupi kwa lugha ya Kiswahili na
Kiingereza, ingawa ingependeza sana kama tafsiri yake
ingeweza kuwa katika lugha ya Kifaransa, Kijerumani, Kichina
na katika lugha zingine za kimataifa. Ukweli huu wa methali za
kiutandawazi unaenda sambamba kama alivyoandika Hellen
Byera Nestor katika utangulizi: “…methali hufanana katika
lugha mbalimbali za nchi kadha za ulimwenguni.”
Hapa mwandishi huyo kwa kutumia dhana ‘hufanana’ kimsingi
alimaanishwa kuwa baadhi ya methali hutumika mahali pengi
duniani ingawa ni kwa lugha tofauti lakini maana iliyobebwa
katika maudhui yake ni ileile.

Zimepangwa kwa kuzingatia alfabeti ya Kiswahili. Methali za


kiutandawazi ni changamoto kwa upande wa maendeleo ya
mawasiliano ya kiuhusiano miongoni mwa mataifa. Ikumbukwe
kwamba madai kwamba methali za kiutandawazi asili yake ni
Ulaya au Marekani kama inavyodaiwa katika masuala mengine
mengi ya kiutamaduni na kihistoria. Utajiri uliomo katika methali
za kiutandawazi kamwe usimithilishwe na utajiri au maendeleo
mengine ya kisayansi na kiteknolojia kutoka katika nchi tajiri
duniani na kwenda nchi maskini duniani!

Ni matumaini yangu kwamba mkusanyiko huu wa methali za


kiutandawazi utatoa changamoto kwa wanataaluma kujenga
wigo mpana na kukita katika kina kirefu cha uchambuzi na

12 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

upembuzi yakinifu.

4.0 Changamoto

Watu binafsi, serikali na taasisi mbalimbali zinaendelea kupania


katika kukikuza Kiswahili. Kutokana na hali halisi ya baadhi ya
methali kuweza kupotea miongoni mwa jamii mbalimbali za
Kiafrika, mpango maalumu umeanzishwa ili kuweza kuziandika
na kuzitolea maelezo methali za makabila mbalimbali ya Afrika
kwa kuandika vitabu kadha wa kadha. Mradi huo ambao kila
mwezi hutoa methali moja kutoka nchi moja ya Kiafrika,
unaweza kuwanufaisha wengi kwa kutumia mtandao kama
ulivyo katika tovuti ifuatayo: African Proverbs, Sayings and
Stories Website : www.afriprov.org .

Hali kadhalika, kuna vitabu vingi vya methali vilivyoandikwa na


watunzi mbalimbali duniani. Katika mradi nilioutaja hapo juu,
jitihada zimefanywa na kila mwandishi katika kukumekusanya

13 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

methali zisizopungua mia moja za jamii yake kwa shabaha ya


kuzihifadhi ili zisije zikapotea. Mradi wa methali adimu za
Kiafrika ulioanza mwaka 1999 ilimradi kusalimisha methali na
misemo ambayo iko hatarini kupotea, hadi 2004 ulikuwa
umefaulu kuzikusanya na kurudufu vijitabu kumi na tatu. Kuna
tegemeo kubwa kupata ongezeko kubwa kabla ya mwisho wa
mwaka huu 2005.

5.0 Hitimisho

Tunaposherehekea Jubilei ya Miaka Sabini na Tano (75) ya


mchakato wa kukistawisha Kiswahili (The Inter-Territorial
Language [Swahili] Committee
iliyoundwa 1930
hadi Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI), iliyopandishwa
hadhi mwaka 1964), bado safari ni ndefu. Juhudi mbalimbali
zilifanywa na serikali hata ikaunda Baraza la Kiswahili la Taifa
(BAKITA) 1967; Idara ya Kiswahili-Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam 1970; Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni,
Zanzibar 1979. Na wakereketwa waasisi walianzisha Chama
cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA) tangu

14 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

miaka mingi kabla ya kupata Uhuru mwaka wa Tanganyika.


Kiswahili hutumika katika nchi nyingi duniani; hufundishwa
katika taasisi na vyuo vikuu kadha wa kadha duniani; hutumika
katika vituo vya redio na televisheni nyingi duniani; aidha, ni
moja ya lugha rasmi za Umoja wa Afrika (AU).

Zifuatazo ni baadhi tu ya methali za kiutandawazi:

METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Ada ya mja hunena muungwana ni kitendo

15 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Kutokana na tabia ya kibinadamu, mtu hutambulika kwa


uungwana wake kwa vitendo vyake wala siyo kwa mavazi,
maumbile au maneno ayasemayo.

Public opinion maintains, a gentleman is judged by his actions.


(Manners make man; or Handsome is as handsome does).

1.

Akili ni nywele kila mtu ana zake

Akili za watu ni za aina nyingi na ni tofauti kama vile nywele za


kila binadamu ni tofauti. Brains are like hair, every humankind
has her/his own kind.

16 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Baada ya dhiki faraja

Baada ya shida huja raha.

After hardship comes relief. (Every cloud has a silver lining;


After storm comes a calm).

1.

Bandubandu huisha (humaliza) gogo

Hata gogo liwe kubwa namna gain, unapolichanachana mwisho

17 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

gogo hilo humalizika.

Chip! Chip! Finishes the log. (Little strikes fell great oak.
Constant dripping wears away a stone).

1.

Chanda chema hufikwa (huvishwa) pete

Jambo jema husifiwa na hushangiliwa ili liweze kufana zaidi. Ni


wana kama kidole kizuri kinapovalishwa pete ili kizidi
kupendeza.

A handsome finger gets a ring put round it.

18 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Chema chajiuza kibaya chajitembeza

Kitu kizuri huonekana bila ya kunadiwa, lakini kibaya hupigiwa


debe ili kukitangaza.

A good thing sells itself, a bad thing advertises itself for sale.
(Good wine needs no bush).

1.

Dalili ya mvua ni mawingu

19 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Ishara ya kuwa mvua itanyesha hivi punde ni mawingu meusi


makubwa. Na yasipokuwepo mawingu haiwezi kunyesha. Hali
kadhalika, katika juhudi zako waweza kujua mapema kama
utafanikiwa.

Clouds are the sign of rain. (Morning shows the day as the
childhood shows the man. Cunning events cast their shadows
before. No smoke without fire).

1.

Damu ni nzito kuliko maji

Watu wa ukoo mmoja husaidiana sana katika matatizo yao


kuliko marafiki au jamaa wa mbali.

Blood is thicker than water.

20 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Elimu haina mwisho

Elimu ni za aina nyingi. Kila siku maarifa ya aina mpya


yanagunduliwa na kuzuka, hivyo haiwezekani kuielewa elimu
yote duniani.

Education has no limits. (One has to continue to learn all his/her


life time).

1.

Elimu ni bahari

Elimu ni pana hivi sawa na upeo wa bahari ambayo huelezwa


na kusambazwa miongoni mwa binadamu.

21 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Education is like an ocean which spread all over the horizons of


people’s life.

1.

Fadhili za punda ni mashuzi

Shukrani za mtu mjinga ni kumtukana yule aliyemtendea


mema.

The gratitude of a donkey is a breaking of wind.

22 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Fimbo ya mbali haiuwi nyoka

Fimbo iliyo karibu nawe ndiyo ikufaayo wakati inapotokea


shida. Methali hii inalenga kuwatanabaisha watu kuwa
binadamu anapopata shida ni watu walio karibu naye ndio
watakaomsaidia.

A stick in the hand is the one that kills a snake.

1.

Ganda la muwa la jana, chungu kaona kivuno

23 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Ganda la jana la muwa huwa limekauka, lakini chungu


anapolipata huona ni mavuno maridhawa. Maana asiyezoea
kuwa nacho, akipatapo hata kama ni kitu duni au hafifu namna
gani na kidogo, hushangilia. Mathalani, kukengeuka kwa
maadili kwa vijana barani Afrika na kuzamia tamaduni za kigeni.

The skin of yesterday’s sugar-cane is a whole harvest of an ant.

1.

Gonga gogo usikie mlio wake

Ukitaka kujua mlio wa gogo, lipige na usikilize. Hili lina maana


kuwa yakupasa kulichunguza jambo kwanza kabla ya
kulihukumu (kulikabili).

24 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Knock a log in order to hear the sound it makes.

1.

Haba na haba hujaza kibaba

Ukiweka akiba kidogo ya kitu kila mara, mwishoni utakuwa na


akiba kubwa. Mwanzo wa makubwa ni madogo.

Little by little fills up the measure. (Little drops of water, little


grains of sand, make a mighty ocean and a pleasant land).

25 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Harakaharaka haina baraka

Jambo lifanywalo harakaharaka, haliwezi kufana. Mambo


lazima yaende kwa kuzingatia mchakato wenye mpango na
taratibu madhubuti.

Hurry, hurry, has no blessing. (More haste, less speed).

1.

Iliyopita si ndwele, ganga ijayo

26 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Mambo yaliyopita, yasishughulikiwe sana, bali tujizatiti


kuyakabili na kuyadhibiti yale yajayo.

That which has passed is not a diease, cure what is coming.

1.

Iwapo nia, njia hupatikana

Mtu anapofanya dhamira ya dhati ya kutaka kulitekeleza jambo,


hawezi kukosa njia ya utekelezaji.

Where there’s a will, there’s a way.

27 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza

Chochote usichokifahamu vizuri huwezi kukieleza kwa ufasaha.

A matter of which you are ignorant is like a dark night.

1.

Jogoo la shamba haliwiki mjini

Jogoo lililozoea kuishi shamba, likihamishiwa mjini hushindwa


kuwika kwa sababu ya mabadiliko ya mazingira yake. Maana,

28 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

ye yote aliye ugenini yampasa kufanya mambo kwa tahadhari ili


kulingana na mazingira ya hapo.

The country cock does not crow in the town.

1.

Kata pua uunge wajihi

Mtu akikata pua yake kwa ajili ya kujirembesha anakuwa


anaiharibu sura yake zaidi.

Cut off your nose to mend your face. (Keep up appearances


even at the price of losing your property. Cut off your nose to
spite your face).

29 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Kidole kimoja hakivunji chawa

Mtu mmoja peke yake hawezi kutenda mengi. Umoja ni nguvu


na utengano ni udhaifu.

One finger cannot kill a louse.

1.

Kuishi kwingi kuona mengi

Kuishi katika dunia kwa muda mrefu humpa mtu nafasi ya

30 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

kujifunza mengi. Tuwaheshimu wazee kwa vile wanaweza


kutushirikisha katika mang’amuzi mengi yenye hekima na
busara.

To live long is to see much.

1.

La kuvunda halina ubani

Harufu mbaya ya kitu kilichooza haiwezi kufichika au kuzuiwa


kwa kufukizia ubani. Hali kadhalika, jambo lililoharibika
halifichiki.

There is no incense for something rotting (it is impossible to


conceal its evil odour).

31 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Lililoandikwa ndilo liwalo

Lile aliloliweka Mungu litendeke, halishindwi kutendeka kama


alivyolipanga. Hii ina maana kuwa Mwenyezi Mungu ni muweza
wa yote, hivyo alipendalo hutokea vivyo hivyo. Hakuna
awezaye kushindana na matakwa (mapenzi) ya Muumba.

That which is written (by God) is what is (i.e. must surely come
to pass).

1.

Maji yaliyomwagika hayazoleki

32 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Maji yakisha mwagika haiwezekani kuyazoa au kuyakusanya


tena. Yaani, jambo likiharibika huwa limeharibika, hata kama
likitengenezwa kamwe halitaweza kuwa kama lilivyokuwa hapo
awali.

If water is spilt, it cannot be gathered up.

1.

Milima haikutani, lakini binadamu hukutana

Milima haina uwezo wa kukutana, lakini binadamu wakiwa hai


huweza kukutana hata baada ya kuwa mbalimbali kwa muda
mrefu. Hii ni methali inayotumika katika kutiana moyo wakati
wanapoagana kwamba wakijaliwa watakutana. Pia hutumika
katika kuwaonya watu kuacha tabia ya kuwatendea vibaya
wengine kwani huenda wao pia wakatendewa hivyo siku za
usoni.

33 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Mountains do not meet, but people meet each other.

1.

Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo

Malezi umpatiayo mtoto huwa ni msingi wa mustakabali wake.


Maisha ya mtu yanategemea sana msingi wa malezi
aliyoyapata tangu angali mchanga. Ni vigumu kwa mtu kuacha
tabia aliyoizoea katika makuzi yake.

As you bring up the child, so he/she will be.

34 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Njia mbili zilimshinda fisi

Kutokana na tamaa yake kubwa, fisi alijaribu njia mbili ya


kushoto na kulia, lakini alishindwa. Mwangata mbili, moja
humpokonya.

Two ways failed the hyena.

1.

Nyumba usiyolala ndani yake hujui ila zake

35 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Mtu hufahamu tu mambo ya nyumba ambamo amelala. Ni


jambo la kijinga kwa mtu kujifanya kuwa anaelewa mambo
ambayo kwa yamkini hayaelewi.

You cannot know the defects of a house you have not slept in.
It is the wearer who knows where the shoe pinches.

1.

Ombaomba huleta unyonge

Tabia ya kuombaomba vitu humfanya mwombaji kuwa


mnyonge au duni. Mlegevu, mzembe, goigoi na mvivu
kuwategemea watu wengine, maana hana bidii ya kujitafutia
riziki yake kwa kufanya kazi mwenyewe. Mtegemea cha ndugu,
hufa maskini.

36 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Begging makes somebody become inferior.

1.

Ondoa dari uezeke paa

Acha kujenga dari mpaka umalize kuezeka. Mtu anatakiwa


kwanza kufanya jambo lililo muhimu kwanza kabla ya mengine
yasiyo muhimu.

Remove the ceiling in order to thatch the roof.

37 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Panapofuka moshi pana moto

Moshi ni ishara ionyeshayo uwepo wa moto. Watu


wanaogombana mara kwa mara si ajabu kuwa siku moja
wataingia vitani na kusababisha maafa.

Where there is smoke there is fire.

1.

Paka akiondoka, panya hutawala

38 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Paka na panya ni maadui wakubwa. Paka hutishia sana uhai


wa panya kwa kuwakamata na kuwala nyama. Kwa jinsi hiyo,
paka anapoondoka, panya hupata nafasi ya kufanya vitu vyao
bila ya kuwa na hofu yoyote. Ndivyo ilivyo kwa wafanyakazi,
endapo mkubwa wao akiondoka, walio chini hujiona kuwa huru
na hufanya mambo wapendavyo.

When the cat goes away, mice do reign. When the cat’s away,
the mice do play.

1.

Penye watu wengi hapaharibiki neno

Mahali ambapo kuna watu wengi hapaharibiki neno. Walipo


watu wengi hubadilishana mang’amuzi na hivyo fikira na nguvu
zao hukusanywa pamoja ili kulitengeneza jambo. Penye wengi
pana Mungu ambaye ni muweza wa yote.

39 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Where there is a gathering of people nothing goes bad. Where


there are many people, there God is (Vox populi vox Dei).

1.

Radhi ni bora kuliko mali

Kupata radhi ya wazazi ni bora kuliko kupata mali. Baraka ya


wazazi haiwezi kupatikana hivihivi tu, lakini mtu anaweza
kutafuta mali wakati na mahali popote. Kwa hiyo, yatupasa
kuwatii wazazi (wakubwa) wetu ili watubariki ndipo hata
tutafutapo mali au riziki huwa tumekwisha pata baraka ya
mafanikio maishani kutoka kwa wazazi.

Blessings are better than wealth.

40 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Rahisi haihalisi

Kitu au bidhaa ipatikanayo kwa bei poa ni kitu hafifu hivyo huwa
si kizuri na hakifai. Cheap things are not worthy spending
money on them.

1.

Sikio halilali njaa

Hapana siku ipitayo bila ya sikio kusikia maneno fulanifulani


yawe mabaya au mazuri. Hivyo sikio halilali bila ya kusikia
neno.

41 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

An ear does not go to sleep hungry (there’s always plenty of


gossip).

1.

Sumu ya neno ni neno

Moto huzimwa kwa maji na pia neno humalizwa na neno.


Likizuka neno au jambo linalowafanya watu kulisema sana au
uvumi fulani, ule uvumi huendelea hadi pale uvumi mwingine
tofauti utakapotokea. Basi, hapo watu husahau ule uvumi wa
kwanza wakaushika ule uvumi mpya.

The poison for a word is a word. Tit for tat.

42 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Tamaa mbele, mauti nyuma

Mtu mwenye tamaa nyingi mwishowe hupatwa na misiba


mibaya. Anayetanguliza tamaa na ubinafsi mbele ajue hana
mwisho mzuri.

Desire first, death afterwards (i.e. No one ever thinks of the


possibility of death when concentrating on achieving a particular
end). Man proposes, God disposes.

1.

Taratibu ndio mwendo

43 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Mwendo wa polepole ndio ufaao. Yaani, jambo lolote lile halina


budi kufanywa kwa kuzingatia kanuni.

Slowly is indeed the way to walk. He that goes slowly goes


surely. Hasten slowly. Slow but sure.

1.

Uchungu wa mwana, aujua mzazi

Mzazi ndiye anayepata uchungu mwingi zaidi ya watu wote


anapomzaa mtoto wake. Yaani mwenye kuthamini kitu
chochote kile ni yule mwenye kitu hicho. Kwani ni yeye ndiye
aliyetaabika katika kukitafuta na kukipata.

The labour of childbirth is known to the mother.

44 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Ukiona vinaelea, vimeundwa

Ukiviona vyombo vya kusafiria vinaelea juu ya maji, ujue


kwamba ni matokeo ya juhudi na maarifa ya watu
waliovitengeneza. Kizuri chochote ukionacho, ufahamu
kimepatikana kwa bidii na jasho na siyo kwa miujiza.

If you see vessels afloat, remember that they have had to be


built.

1.

Usipoziba ufa, utajenga ukuta

45 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Usipoukarabati ufa kwenye ukuta mapema, ukuta utabomoka


na hivyo utalazimika kuujenga ukuta tena. Usipolirekebisha
kosa dogo tangu mwanzo, utapata hasara kubwa hatimaye.

If you do not fill up a crack, you will have to build a wall. A stitch
in time saves nine.

1.

Vita havina macho

Wakati wa vita mtu ye yote yule anaweza kuumizwa, kuuawa


au kupata madhara ya aina yoyote ile. Ni vema kujiepusha na
vita.

War has no eyes (i.e. it kills indiscriminately).

46 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

1.

Vita vya panzi furaha ya kunguru

Panzi wanapopigana na kuuana kwa wingi ni furaha ya kunguru


kwani hupata chakula chao kwa urahisi. Hali kadhalika, maafa
ya wanyonge huweza kuwa furaha ya wakubwa.

A fight between grasshoppers is a joy to crows.

1.

Wapiganapo tembo, nyasi huumia

47 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Ndovu wawili wakipigana, husababisha nyasi


kukanyagwakanyagwa na kuharibika. Yaani viongozi wawili
wanapopigana wanaoumia ni wafuasi au watu walio chini ya
himaya zao. Wakati mataifa makuu mawili (k.m.Warusi na
Marekani wakati wa vita baridi) yanapopigana, mataifa madogo
ndiyo yanayoumia.

Where elephants fight, the reeds get hurt.

1.

Ya kale hayapo

Yale yaliyotokea zamani yamekwisha na yanapaswa


kusahauliwa. Hapana haja ya mtu kuwa na kifundo cha moyo
kwa ubaya aliofanyiwa hapo zamani.

48 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

The ancient (things) are no longer with us. Let bygones be


bygones.

1.

Yote yang’aayo si dhahabu

Si kila kionekanavyo kinameremeta ni dhahabu. Kwani viko


vingi ving’aavyo, lakini ambavyo si dhahabu na ni vya thamani
ndogo mno kuliko dhahabu. Usikipende kitu kwa uzuri wake wa
nje, bali ukichunguze sana ili ujue ubora wake. Uzuri wa
mkakasi ndani kipande cha mti.

All that glitters, do not think it is gold.

1.

Ziba mwanya, asipite panya

49 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Ukisha kugundua mwanya wa panya, fanya hima ili uuzibe ili


panya wasifanye mazoea ya kuutumia mwanya huo. Mathalani,
serikali ikisha gundua mwanya wa bidhaa za magendo haina
budi kuharakisha kuuziba mwanya ili kuondokana na ugumu wa
kulikabili tatizo hilo baada ya kuzoeleka na walanguzi seuze na
wafanyabiashara ya magendo.

Seal the small path so that the rats should not create the habit
of using it.

1.

Zimwi likujualo halikuli likakwisha

Shetani akujuaye hakuli akakumaliza. Watu wa jamii au ukoo


moja hawadhuriani kabisa. Endapo wakifanya hivyo, basi
huhesabika kuwa ni wachawi.

50 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

A devil that knows you will not devour you completely.

Vitabu vya Rejea

1.

Ahmed Ndalu & Kitula G. King’ei, Kamusi ya


Methali za Kiswahili,
EAEP (1989).

51 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

2.

Charlotte and Wolf Leslau, African Proverbs,


The Peter Pauper Press, NY (1962).

3.

Farsi, S.S., Swahili Sayings, EALB

4.

Healey, Joseph G., Towards an African


Narrative Theology, Pauline
s Publications Africa (1996);
Once Upon a Time in Africa: Stories of Wisdom
and Joy,
Orbis Books (2004);
African Stories for Preachers and Teachers,
Paulines Publications Africa
(2005);
Kueneza Injili kwa Methali,
Benedictine Pulications Peramiho (1984).

52 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

5.

Johnson, Frederick, Swahili-English Dictionary


& English-Swahili Dictionary,
OUP
(1939).

6.

Kalugila, Omushumba Leonidas, Emigani na


Ebikoikyo,
North Western Publishers, Bukoba (1992).

7.

Kamati ya Utafiti wa Utamaduni Bujora,


Kugundua Mbegu za Injili,
Benedictine Peramiho Publications (1993).

8.

53 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Madam, Swahili-English Dictionary, (1894).

9.

Mayoka, J.M., Nahau za Kiswahili, Mathews


Bookstore & Stationers, Dar es Salaam,
Tanzania.

10.

Mbonde, J. P., Wisdom from Ngoni Proverbs,


privately duplicated (2004).

11.

Muwanga, Aminieli Stephano, Methali kwa


Picha,
Utamaduni Publishers (1984).

54 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

12.

Ngole S.Y.A. & Honero Lucas N. (Wahariri),


Fasihi Simulizi Methali (kitabu cha Pili
(TUKI) DUP (1981).

13.

Nestor, Hellen Byera, 500 Haya Proverbs,


East Africa Literature Bureau (1978).

14.

Omari,C.K., Kezilahabi, E., and Kamera,W.


D., Misemo na Methali Toka Tanzania
Kitabu cha 1 (Toleo Jipya 2000) & Kitabu
cha 2
(Toleo Jipya 2004) Mathews Bookstore &
Stationers, Dar es Salaam, Tanzania.

55 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

15.

Rugumamu, Severine M., Globalization


Demystified: Africa’s Possible Development
Futures, DUP
(2005).

16.

Scandinavian Institute of African Studies: S


wahili Proverbs from East Africa,
Uppsala (1977).

17.

TUKI: Kamusi ya Kiswahili Sanifu, OUP


(1981).

18.

56 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

TUKI: Kiswahili cha Utandawazi, DUP

19.

TUKI: Kamusi ya Kiswahili Sanifu (toleo la


pili), OUP (2004).

20.

Wamitila, K.W., Kamusi ya Methali,


Longhorn Publishers, (2001).

21.

Wanjohi, Gerald Joseph, Under One Roof-


The Gikuyu Proverbs; & The Wisdom and
Philosophy of African Proverbs: The Gikuyu
World-View,
Paulines Publications Africa (1997)

57 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Note: This paper was originally delivered during


the 75th anniversary of TUKI or the Institute of
Kiswahili Research (1930-2005) at the
University of Dar as Salaam, Tanzania (4 th

-7
th

July, 2005). The author decided to select only


51 proverbs that are commonly used around
the globe. Hence, he calls them "global
proverbs." Actually, globalisation as a process
commenced many centuries ago. Think of the
early travellers such as Christopher Columbus,
Vasco da Gamma, missionaries, slavery and
slave trade, the First and Second World Wars
and other periods and other events. One
evidence is Negro-Americanism with its
complexity of cultures. But globalisation takes a
new face in the development of economy and
culture particularly science and technology in
communication. The third millennium appears
to have overshadowed the entire meaning of
globalisation
. The

58 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

contextulisation
of each global proverb varies according to its
environment and culture. But those of African
origin have their flavor or touch notched in each
one of them:

e.g. Proverbs are the daughters of


experience (Sierra Leone); A proverb is the
horse of

conversation: when the conversation lags, a


proverb will revive it (Yoruba); A wise man

59 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

who knows proverbs reconciles difficulties


(Yoruba).

Indeed, these few selected global proverbs in


this paper are intended to represent all those
that which are universally or popularly used
and/or recognised. Most of these global
proverbs have diversified origins: some of them
originated from Africa, and some from Europe
and many others from Asia.

60 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

J. P. Mbonde

Retired civil servant (teacher/headmaster);


a graduate from Sydney University,
Australia and the De Montfort University,
UK; Freelance journalist; author of several
books; Analyst of both oral and written
African Literature; Educational
Consultant; a regular book reviewer; has
traveled all over the globe on academics
and study tours.

P.O. Box 3479, Dar es Salaam, Tanzania,


East Africa.

Email: jopahanya@yahoo.com

61 / 62
METHALI ZA KIUTANDAWAZI

Revised 23 August, 2005

62 / 62

You might also like