You are on page 1of 38

UPIMAJI KATIKA ELIMU

Upimaji katika elimu ni kitu muhimu sana unapotaka kujua

maendeleo yaliopatikana wakati wa kujifunza au kufundisha.

Upimaji humuonyesha

anaejifunza ni mahali gani amefanikiwa na ni

mahali gani ana mapungufu.

Vilevile anaefundisha

anajua ni mahali gani amefanikiwa au niwapi

hajafanikiwa.
MAANA YA UPIMAJI KATIKA ELIMU

Katika elimu upimaji Upimaji katika elimu pia hujni tendo la

kutafuta ni kwa

kiasi gani mwanafunzi amepata maarifa au stadi

zilizofundishwa kufuatana na malengo ya

ufundishaji wa mada za somo yaliyopo kwenye

muhtasari.umuisha

mwenendo na tabia ya mwanafunzi na uwezzo

wake wa kufanya mambo mbalimbali.

UMUHIMU WA UPIMJI KATIKA ELIMU

Matokeo katika upimaji wa elimu hutumiwa na

watu mbalimbali kwa mfano

mwanafunzi,shule,wazazi,waajiri walimu na watafiti.

MWANAFUNZI

Matokeo ya upimaji wa mwanafunzi

Huwa ni kigezo cha chake cha kutambua ameelewa

kwa kiasi gani cha kitu au vitu/ mada

alizofundishwa.

Huumpa changamoto ya kujifunza. Endapo

amepata alama za juu hupenda kuziendelezana


kama amepata alama za chini,hufanya bidii ya

kujikwamua.

Huumfanya awe makini katika kujifuza maana

anajua fika kuwa atapimwa. Hii humfanya asiwe

mtoro au mzembe wakati wa masomo.

Steven Georges’ property.

MWALIMU

Matokeo ya upimaji wa mwanafunzi humuwezesha

mwalimu.

Kutambuwa kiwango cha uelewa wa wanafunzi

katika maada mbalimbali za somo.

Kutambua matatizo wanayopata wanafunzi wakati

wa kujifunza na kuyatafutia ufumbzi.

Kutambua wanafunzi wenye matatizo ya kuelewa

somo au sehemu ya somo ili aweze kuwapa

mafunzo ya ziada.

Kugundua malengo ya somo ambayo wanafunzi

hawakufanikiwa na kuchunguza sababu.

Kuangalia mapungufu na mafanikio ya mtaala na

kutoa taarifa kwa wahusika.

Kurekebisha mbinu za kujifunzia na kubuni/


kufaragua vifaa vipya ili malengo mengi zaidi

yafikiwe.

SHULE

Matokeo ya upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi

huiwezesha shule :-

Kujua ufanisi wake katika elimu kwa kulinganisha

na shule nyingine.

Kujua malengo ya mtaala yaliofikiwa.

Kupanga wanafunzi katika mikondo (si lazima

wenye uwezo mmoja wakawa pamoja)

Kumshauri mwanafunzi kuendelea na ngazi ya

masomo inayofuata au kurudia.

Kushauri viongozi wa elimu kuhusu mwanafunzi

anaeonekana kuwa na uwezo au kipaji maalumu ili

aweze kuendelezwa.

Kuwasiliana na mzazi kuhusu maendeleo ya

mwanafunzi kwa kutumia ripoti.


Kushauri wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi

kuhusu ubora au mapungufu ya mitaala ili hatua

zinazofuata zichukuliwe.

MZAZI

Matokeo ya upimaji wa maendeleo ya mwanafunzi

humwezesha mzazi

Kufahamu maendeleo ya mtoto wake

Kuchunguza chanzo cha matatizo kama yapo na

kushirikiana na shule kuyatafutia ufumbuzi

Kummotisha mtoto wake ili aongeze bidii.

MWAJIRI

Matokeo ya upimaji wa mwanafunzi humwezezha

mwajiri;
Kuchagua mfanyakazi kwa kuangalia uwezo wake

kitaaluma na mwenendo tangu akiwa shuleni.

Kumpangia mfanyakazi aina ya kazi inayoendana

na uwezo wake kitaaluma.

MADHUMUNI YA UPIMAJI KATIKA ELIMU

Tunaweza kuorodhesha madhumuni ya upimaji

katika elimu ambayo ni;

Kujua maendeleo ya mwanafunzi kitaaluma, kitabia,

na kistadi.

Kubaini matatizo ya mwanafunzi katika kujifunza.

Kuangalia kiwango cha kufanikawa cha malengo ya

kila mada.

Kuamsha ari ya mwanafunzi kujifunza zaidi

Kuboresha ufundishaji.
Kuandaa vigezo vya kutumia wakati wa kuchagua

wanafunzi kwa masomo ya juu au kozi mbalimbali.

NYANJA ZA UPIMAJI KATIKA ELIMU

Katika elimu vipengele ya kuzingatia katika upimaji

ni uwezo wa
kitaaluma, kufanya vitendo,na kumudu

matatizo au shinikizo mbalimbali katika maaisha.

Nyanja za upimaji ni maerneo ambayo ujuzi,

mwelekeo na matendo tarajiwa kwa mwanafunzi

kuwa nayo,kujenga au kupata baada ya mafunzo.

Nyanja za utambuzi hujumuisha

Nyanja za utambuzi

Nyanja za mwekekeo

Nyanja za vitendo

NYANJA ZA UTAMBUZI

Nyanja hiii inahusika na ujuzi /uzoefu ambao

mwanafunzi anatarajiwa kuwa nao baada ya

kujifunza na kupewa mtihani au majaribio. Nyanja

hii Benjamin Bloom (1956) ameigawa katikavifungu

(ngazi) sita vilivyopangwa kuanzia kifungu kilicho

rahisi hadi kilicho tata. Vifungu hivyo ni

Maarifa

Ufahamu

Matumizi

Uchambuzi

Uunganishaji/ uundaji
Tathimini

NGAZI YA MAARIFA

Maswali yanayoulizwa hupima uwezo wa

mwanafunzi kukumbuka maarifa, stadi za jumla

alilzojifunza.(Je, mwanafunzi anaweza kukumbuka

alichofundishwa?). Vitenzi vinavyotumika katika

maswali yanayopima ngazi hii ni kama , Taja,

andika, orodhesha, eleza.

Mfano wa maswali ni kama

Taja makundi mawili ya viumbe hai

Orodhesha mambo yanayoathiri kinga ya mwli

Nini maana ya mashine?

NGAZI YA UFAHAMU

Mwanafunzi anapimwa katika ngazi hii ni kutaka

kujua kama anaweza kuhusisha maarifa mapya na

marifa aliokuwa nayo.(Je,mwanafunzi anaweza

kukueleza nakutafsiri maana ya kitu

kilichofundishwa?) Vitenzi vinavyotumika katika

maswali yanayopima ngazi hii ni kama Toa,

fupisha, eleza.

Mfano wa maswali ni kama


Toa tofauti kati ya wanyama na mimea.

Eleza athari za UKIMWI katika jamii.

NGAZI YA MATUMIZI

Ngazi hii huhusisha maswali yanayomtaka

mwanafunzi kutumia habari anayoifahamu kupata

jibu. (Je, mwanafunzi anaweza kutumia maarifa na

stadi katika mazingira mapya kuhusu mambo

aliyofundishwa?) Vitenzi vinavyotumika katika

maswali yanayopima ngazi hii ni kama

Kokotoa mlinganyo ufuatao

2x+y= 1 na 2x-y=2

Elezea kwa ni meli inaelea juu ya maji.

NGAZI YA UCHAMBUZI

Ngazi hii mwanafunzi hutakiwa kufikiri kwa makini

na maswali yanayotungwa ni yanayomtakaka

mwanafunzi kuchambua maarifa na kubainisha

sehemu zake na kuonyesha uhusiano.(Je,

mwanafunzi anaweza kutambua na kuhusianisha

sehemu mbalimbali za kitu au taarifa?).

Mfano wa vitenzi vinavyotumika ni kama

kuhusianisha,changanua, gawanya,tenga.
Mfano wa maswali ni kama

Kwa nini karafuu haiwezi kustawi Lushoto?

Andika kwa kifupi kifungu cha habari kifuatacho.

Chora ramani ya Tanzania na uoneshe maziwa ma

mito.

NGAZI YA UUNDAJI

Katika ngazi hii mwanafunzi hupimwa uwezo wake

wa kuunganisha vitu mbalilmbali kuunda kitu

kizima.(Je mwanafunzi anaweza kutoa uamuzi au

kuanzisha mambo kutokana na taarifa

zilizochanganuliwa?) Vitenzi vinavyotumika ni

kama husianisha, jenga upya, pangilia, unda

fupisha. Mfano wa maswali ni kama

Hatua gani zichukuliwe ili kupunguza matatizo

kwenye utafiti?

Eleza namna utakavyoboresha mazingira

yaliyoharibika kwa ajili ya ukataji miti.

NGAZI YA TATHMINI

Katika ngazi hii mwanafunzi anatakiwa kutathmini

uzuri au ubaya wa matumizi ya kitu fulani na

kufanya maamuzi.(Je,mwanafunzi anaweza kuamua


kitu kina thamani gani au kinafaa au hakifai

kufuatana na kipimo sanifu kuchunguza sifa za kitu

hicho). Vitenzi vinavyotumika ni kama hakiki,

hitimisha, kubaliana, tetea, toa ufupisho, toa

makosa.

Mfano wa naswali ni kama

Elimu ni bora kuliko mali. Je, unakukbaliana na

usemi huu? Eleza jibu lako.

Fafanua kauli hii kwa kutumia hoja tano. Utafiti wa

matumizi ni bora zaidi kuliko utafiti wa msingi.

Steven Georges’ property

NYANJA YA MWELEKEO

Ni nyanja ya malezi ya hisia ambayo inahusika

katika kupima tabia ya mwelekeo na mwenendo wa

mwanafunzi. Lengo ni katika kujua; usafi,

ushirikiano, uvumilivu juhudi na kujadili mambo.

NGAZI ZA NYANJA YA MWELEKEO

Ngazi ya kuwa tayari kupokea mambo mbalimbaali

Ngazi ya kushiriki/ kuitikia

Ngazi ya kutathmini na kuhusianisha

Ngazi ya msimamo/ Ngazi ya kuoanisha maswala


mbalimbali

NGAZI YA KUWA TAYARI

Hii ni ngazi ya kwanza ambayo huonesha utayari

alionao mwanafunzi kujifunza.(Je, mwanafunzi

yuko tayari kupokea kichokoo,kwa mfano kukubali

kushauriwa?). Vitenzi vinavyotumika ni kama

chagua jibu sahihi, elekeza, fuata.

Mfano wa maswali ni kama

Utakapochelewa kipindi cha ualimu utafanya nini?

Uko tayari kusoma na mwanafunzi mlemavu

NGAZI YA KUITIKIA / KUSHIRIKI

Katika ngazi hii mwanafunzi yuko tayari kujifunza,

kuonyesha mwitikio alionao kama kwa kuwa

mchangamfu muda wote.(Je, mwanafunzi anaweza

kushiriki katika shughuri mbalimbali yaani

kuchangia mawazo na utendaji?) Vitenzi

vinavyotumika ni kama amkia, saidia tambulisha,

simulia, nyumbulisha . Mfano wa maswalli ni kama

Utamsaidiaje mtu alieumwa na nyoka?

Ngoma zinapochezwa usiku zinachochea

maambukizi ya UKIMWI. Jadili


NGAZI YA KUTHAMINISHA

Mwanafunzi hupimwa jinsi gani anavyojisamini

yeye mwenyewe, anavyothaminiwa na wenzake

walimu wake na jami ikwa jumla.(Je

mwanafunzianaweza kuthamini kitu wazo na watu

yaani kuwajibika?) Vitenzi vinavyotumika ni kama

fanya kazi, toa taarifa, shirikiana, pendekeza,

pambanua.

Mfano wa maswli ni kama.

Badili asilimia kuwa desimali

Oanisha maneno kwenye orodha A nay ale yalioko

kwenye orodha B.

KUOANISHA MASWALA MBALIMBALI

Mwalimu hupima uwezo wa mwanafunzi katika

kulinganisha na kutofautisha vitu mbalimbali.

(Je,mwanafunzi anaweza kuwa na msimamo wa

fikra?) Vitenzi vitumikavyo ni kama; Unda, zingatia,

husianisha tayarisha unganisha, linganisha.

Mfano wa maswali ni kama

Binadamu wote ni sawa thibitisha kauli hii.

KUWA NA MSIMAMO
Mwalimu kupima msimamo wa wanafunzi juu ya

maamuzi ya maswala mbalimbali

NYANJA YA STADI

Kipengele hiki hupimwa kwenye vitu vinavyohusu

utumiaji wa mikono,miguu, na sehemu nyingine za

mwli. Vitu muhimu vinavyoangaliwa ni kama

uwezo wa

Kutumia vifaa au zana

Kuchagua vifaa au zana muafaka

Kutunza au kurudisha vifaa/zana mahali pake

Kupata matokeo mazuri au zao bora

Nyanja ya stadi imegawanyika katika ngazi kuu tatu

ambazo ni

Kuchunguza

Kuiga

Kurekebisha

KUCHUNGUZA

Je, mwanafunzi anaweza kuangalia na kusikiliza

kwa makini kinachotendeka?

KUIGA

Je, mwanafunzi anaweza kkufuatisha maelekezo


kwa vitendo ili kujenga mazoezi ya utendaji?

KUREKEBISHA

Je mwanafunzi anaweza kutumia misingi ya

utendaji kubuni kitu kipyaau utendaji mpya?

Steven Georges’ property

ZANA ZA UPIMAJI KATIKA ELIMU

Zana kuu zinazotumika katika upimaji wa

maendeleo ya elimu ni pamoja na mazoezi,

mitihani, muongozo wa usaili,majaribio na jedwali

la kupima tabia na mwenendo wa wanafunzi.

MAZOEZI

Unapokuwa unafundisha kwa njia shirikishi ni

jambo la kawaida kuwauliza wanafunzi wako

maswali. Maswali haya huwa ni sehemu ya

mazoezi ya kujenga somo. Vilevile hukupa

mwanga ni mwanafunzi gani anafuatana na wewe

unavyofundisha. Si kila mwanafunzi atapata nafasi

ya kujibu maswali, njia hii haitoshi kupima

ufundishaji.Ili kufanya ikamilike inabidi utoe zoezi

kila amalizapo dhana,mada au sura.

MAJARIBIO
Majaribio ni mazoezi yanayotolewa na mwalimu

kwa mwanafunzi ili kumpima mafanikio yao katika

kujifunza. Majaribio hufanyika kuwapima wanafunzi

katika mada kuu au mada nyingi.Majaribio haya

hufanywa mara moja kwa kila majuma mawili,

mwezi au nusu mhula, Njia hii huweza kumpima

mwanafunzi anavyoendelea kupokea na kuhifadhi

taaluma.

MITIHANI

Mitihani hutolea kwa shule za msingi, sekondali,

vyuoni mwishoni mwa mhula. Matokeo ya mitihani

huonyesha mwanafunzi anavyoendelea katika

masomo yake mbalimbali iklinganishwa na

wenzake.

Mitihani mikuu inayofanyika ni pamoja na

Mtihani wa kualilza darasa la saba ambao

hutumika kuchagua wanafunzi kuingia sekondari

kikdato cha kwanza.

Mtihani wa kidato cha pili.

Mtihani wa kkumaliza kidato cha nne ambao

hutumika kuchagua wanafunzi watakaojiunga na


kidato cha tano na watakao fanya kozi mballimbali

za kitaaalam

Mtihani wa kidato cha sita ambao hutumika

kuchagua wanafunzi watakaoendelea na masomo

zaidi ya sekondari ikwapo vyuo kikuu.

JEDWALI LA TABIA NA MWENENDO

Ni jukkumu la mwalimu kumlea mwanafunzi awapo

shuleni. Hivyo inakubidi ujue tabia na mwenendo

wake kila mara. Ili kuweza kufanya hivyo inakubidi

kuwa na jedwali la kuchunguza mwenendo na

tabia wa wanafunzi.

Steven Georges’ property

JEDWALI LA KUPIMA TABIA NA MWENENDO WA

WANAFUNZI

GREDI

MAELEZO

Darasani

Huwahi kuingia darasani

Hufanya kikamilifu kazi anazopewa

Hushirikiana na wenzake katika masomo

Huondoka tu baada ya kumaliza kazi


Tabia nyingine.

Hutmiza majukumu anapopewa nafasi ya kuongoza

wenzake

Ana heshima kwa walimu, watu wengine na

wanafunzi wenzake

Anatunza usafi wa mwili wake na mavazi

Ni mwaminifu

Anafanya kazi kwa bidiii na stadi

Huonwa na wanafunzi wenzake kwa ushauri

Shughuri za ujenzi wa taifa

Hushiriki bila kinyongo katika kazi za ujenzi wa

taifa, shuleni na nje ya shule

Hushirikiana na wenzake katika kukamilisha kazi

iliyotolewa

Huwatia moyo wenzake katika kukamilisha kazi

iliyotolewa

Mambo mengineyo

Anashiriki kikamilifu katika kukamilisha kazi

aliyopewa

Anashiriki kikamilifu katika shughuri za utamaduni

Tumia A,B,C,D,E kupima mwanafunzi katika safu ya


gredi

Ufunguo; A= Vizuri sana, B=Vizuri, C= Wastani, D=

Dhaifu, E=Mbaya.

Wakati unapojaza jedwali unapaswa kuzingatia

mambo yafuatayo

Usiwe na jazba kutokana na tukio moja.Chunguza

kwa muda endapo tukio limekkuudhi

Mshirikishe mwalimu mwenzako endapo anamjua

zaidi mwanafunzi

Usitoe upendeleo

Steven Georges’Property

MWONGOZO WA USAILI

Upimaji kwa kusaili hufanyika ana kwa ana.

Unapopata mwanafunzi mgeni na unapenda kujua

uwezo wake au historia ya alikotoka unaweza

kumuita na kuongea nae. Ili uhakikishe mambo

yote unayoyataka kujua unayauliza ni vizuri

kuandaa mwongozo wa usaili.

Mwongozo wa usaili haya ni maswali

yalioorodheshwa kwa mpangilio maalum ili kuwa

na mtiririko mzuri wa mawazo. Usaili huu pia


huweza kutumika kuchunguza matatizo ya

mwanafunzi katika kujifunza.

Steven Georges property

UTUNZI WA MAJARIBIO NA MITIHANI

Misingi ya utunzi wa majaribio na mitihani

majaribio na mitihani yana umuhimu mkubwa sana

katika upimaji wa maendeleo ya wanafunzi.

Yanajumuisha vitu halisi vinavyotarajiwa na

mwalimu kutoka kwa wanafunzi baada ya

kujifunza/ ujifunzaji.

Dhumuni kubwa la majaribio na mitihani ni

1.Hutupatia taarifa kamili na halisi kuhusu

maendeleo ya mwanafunzi. Mwalimu anatakiwa

kutoa majaribio na mitihani kwa wanafunzi ili kujua

kile kinachotakiwa kupimwa kwa wakati ule.

Mwalimu anpoazimia kutunga jaribio/ mitihani

anatakiwa kufuata hatua zifuatazo.

Mwalimu anapaswa kufahamu vema mambo

anayotaka kuyapima. Kitendo hicho kitakufanya

ufanye uamuzi kuhusu maswali utakayo yatumia.

Maswali ya mitihani yagusie vipengele vingi vya


maudhui yaliofundishwa kwa kipindi hicho.

Mwalimu aamue ni aina gani ya maswali

atakayoyatumia. Kimsingi kuna aina kuu mbili za

maswali, maswali ya kujieleza ambayo yanadai

majibu yatolewe na mtahiniwa lakini kiwango cha

usahihi wa majibu hayo yanatolewa na mtahini.

Maswali haya yanataka mtahiniwa kujua kweli ya

mambo mbalimbali na kuonyesha mambo

yanayohusiana na yasio husiana. Utoaji wa majibu

katika maswali ni kwa kutumia insha au majibu

mafupi. Aina ya pili ya maswali ni maswali

yakinifu. Maswali haya yanamtaka mtahiniwa

kutambua jibu lililosahihi miongoni mwa majibu

yaliotolewa na mtahini. Katika maswali haya

mtahiniwa hana uhuru wa kuchagua majibu

mengine yalio tofauti na yale yaliotolewa.

JEDWALI LA KUTAHINI

Kabla mwalimu hajaanza kutunga maswali

anapaswa kutayarisha jedwali la kutahini. Jedwali

la kutahini ni utaratibu unaonyesha maada za

kupima na idadi ya maswali kwa kila maada.


Jedwali hili huonyesha malengo yanatarajiwa

kufikiwa pamoja na idadi ya maswali kwa kila

maada. Jedwali hupangwa kwa safu. Safu ya

kwanza upande wa kushoto huwekwa maudhui kwa

kuorodhesha maada zinazopimwa. Safu inayofuata

kulia huwekwa malengo ya kupimwa.

Watahini wengi hutumia mgawanyo wa bloom

(1956) kuainisha stadi hizo. Hata hivyo hufungwi

na utaratibu huu ikiwa somo lako haliwezi

kupimwa kikamilifu kwa mgawanyo huo.unaweza

kuweka utaritibu mwingine kama utaona unafaa

zaidi.

Idadi ya maswali huonyeshwa katika mkato wa

chumba cha maudhui kuelekea kulia na kile cha

safu ya stadi zinazopimwa.

Jumla ya maswali kwa kila maada huandikwa

upande wa kulia. Jummla ya maswali kwa kila

ngazi ya utambuzi huandikwa kwenye mstari wa

chini ya jedwali.

STADI ZA KUPIMWA

1
2

Jumla

Asilimia kwa kila

Maada za kupimwa

Maada za kupimwa

Jumlaya maswali

Asilimia kwa kila ngazi

UTAYARISHAJI WA JEDWALI LA KUTAHINI

Mambo ya kufanya wakati wakuandaa jedwali la

kutahini

1.Chukua muhtasari wa somo na maandalio ya

somo

2.Chunguza katika maandalio ya somo maada

ambazo zimekishwa fundishwa

3.Chagua mada ambazo unaona ni muhimu

zitungiwe jaribio/ mitihani kisha orodhesha mada

hizo.

4.Chunguza kwa makini katika muhtasari na

maandalio ya somo ya somo malengo mahsusi ya


mada zinazotungiwa maswali

orodhesha malengo hayo kisha amua

i/ aina ya maswali yatakayotumika katika upimaji

ii/ idadi ya maswali yote katika mtihani

iii/ muda wa kufanya jaribio hutegemea na wingi

wa mada na hali ya malengo yenyewe 5. chora

jedwali la kutahini

6.jaza jedwali la kutahini kwa kufuata hatua hizi

i/ orodhesha mada zote za kutungiwa maswali.

ii/ orodhesha malengo mahususi katika safu

inayofuata

iii/ Amua ngazi zipi za nyanja ipi za kupimwa

zipewe umuhimu wa kupewa maswali mengi na

zipi zipewe maswali machache.

UMUHIMU WA JEDWALI A KUTAHINI

I/ Linahakikisha kuwa maudhui yote yanayotakiwa

kutahiniwa yanatahiniwa.

Ii/ Linahakikisha kuwa kiwango cha kuelewa

maarifa , kumudu stadi za utendaji na kubadilika

kwa mwelekeo wa watahiniwa kinatahiniwa

iii/ Linahahakikisha uwiano wa idadi ya maswali


katika kila eneo na kila kipengele cha nyanja

kinapimwa .

Mfanowa jedwali la utahini kwa somo la maarifa ya

jamii darasa la tano katika nyanja ya mwelekeo

STADI ZA KUPIMWA

MADA Z KUPIMWA

MALENGO YA KUPIMWA

Kuwa tayari

kuitikia

Kutathmini

Kuwianisha maswala

Msimamo

Jumla

% kwa kila mada

Mahusiano ya jamii za Tanzania

15%

Mila na desturi

1
1

15%

Kufanya kazi

15%

Kusoma ramani

15%

Muundo wa serikali ya kijiji

15%

Ushiriki wa jamii
2

15%

Idadi ya maswali

20

15%

% kwa kila ngazi

25%

30%

10%

20%

15%

100%

100%

UCHAMBUZI WA TAFSIRI YA MATOKEO YA


MAJARIBIO NA MITIHANI

Baada ya mwalmu kusahihisha jaribio / mtihani na

kutoa alama hatua inayofuata ni uchambuzi wa

tafsiri ya jaribio/ mtihani.

Kuna mambo mawili makubwa yanayojumuishwa ;

i.Kufanya uchanganuzi na tafsiri ya takwimu ya

maksi (alama) inayokusudiwa kutathimini kiasi cha

mafanikio ya utendaji wa mtahiniwa.

ii.Kufanya uchanganuzi wa maswali ya jaribio ili

kuona iwapo jaribio lilitumika kupima ufanisi wa

utendaji wa watahiniwa katika nyanja mbalimbali za

kujifunza lilifaa kwa kiasi gani.

UCHAMBUZI WA MATOKEO YA MTIHANI NA TAFSIRI

Uchambuzi wa matokeo ni mchakato mzima wa

kurekodi kuzipanga alama kulingana na mahitaji ya

mtumiaji .

MADHUMUNI YA KUCHAMBUA

Kuelewa ujuzi uliotarajiwa kujengwa na mwanafunzi

kama ilivyokusudiwa.

Kupima mafanikio ya kazi ya mwalimu.

UMUHIMU WA KUCHAMBUA NA KUTAFSIRI DATA


Inamsaidia mwalimu kujitathimini mwenyewe katita

utendaji wa kazi

Inamsaidia mwalimu kufahamu viwango vya ujuzi

walionao wanafunzi

Inamsaidia kufanya maamuzi sahihi juu ya mbinu

na njia za kufundishia

Inamsaidia kupanga mikakati ya kuwasaidia

wanafunzi wenye matatizo ya kujifunza

Inasaidia wanafunzi kujitathimini wao wenyewe kwa

kufahamu maeneo wanayoyamudu na

wasiyoyamudu.

Inatoa nafasi kwa jamii kuelewa/kufahamu jinsi ya

kufanya marekebisho juu ya mitaala.

Istilahi zinazotumika katika kuchambua matokeo ya

mitihani ni ukokotoaji wa :Wastani, modi, mfiko

alama yakati (mediani ).

Wastani

Wastani ni kiwango cha kati cha hesabu.

Hupatikana kwa kujumlisha maksi zote halafu

kugawanya kwa idadi ya watahiniwa.

i.e
Wastani = Jumla ya alama

Idadi ya watahiniwa

Endapo alama zimetolewa kwa jedwali la marudio,

idadi ya watahiniwa ni

X=∑fx/∑f

Mfano 12,24, 36, 25.

Alama

Chale

Marudio

fx

67

67

66

66

64

1
64

61

61

55

11

110

45

45

35

35

27

27
25

25

Dosari za alama za wastani

Haituelezi ubora au ufanisi wa kujifunza na

maendeleo ya wanafunzi.

Manufaa ya alama ya wastani

Hutumika kutafuta ukatikati wa maendeleo ya

mwanafunzi.

Hutusaidia kutupa picha ya maendeleo ya

mwanafunzi ikiwa idadi ni kubwa.

MODI

Modi ni alama iliyojitokeza mara nyingi kupita

alama nyingine. Ni alama yenye marudio (f) mengi

zaidi.

Mfano 23,33,24,24,32,25,22,24,26 na 25.

modi yaweza kuwa ni namba moja au zaidi ya

moja endapo marudio yanalingana au hakukua na

alama zisizojirudia.

MFIKO
Mfiko ni tofauti iliyopo kati ya alama ya juu kabisa

na alama ya chini kabisa katika seti ya maksi za

watahiniwa. Mfano

tafuta mfiko kwa alama zifuatazo

73,35, 42, 85, 36 na 78

Mfiko = 85-35=50

Endapo mfiko (range) ni ndogo, tafsiri yake ni kuwa

watahiniwa walikuwa nauwezo uliokaribiana au

unaokaribia kulingana.

Endapo mfiko ni mkubwa hiyo inaonyesha kuwa

watahiniwa wana uwezo tofauti, yaani wapo wenye

uwezo wa juu zaidi na wapo wenye uwezo wa chini

zaidi.

UWEZO WA SWALI KUPAMBANUA

Katika upimaji, swali zuri ni lile ambalo wanafunzi

walio hodari wenye uelewa na ujuzi wa kiwango

cha juu zaidi kitaaluma watalifanya vizuri na wale

wenye kiwango cha chini zaidi kitaaluma wtalifanya

vibaya.

Hii ina maana kuwa swali zuri(pamoja na sifa au

vigezo vingine) ni lazima liwe na uwezo wa


kupambanua wanafunzi walio hodari na wasio

hodari.

Namna ya kukokotoa uwezo wa swali kupambanua

1. Panga wanafunzi kuanzia alama za juu hadi za

chini

2.Gawa watahiniwa katika makudi matatu. H: maksi

za juu (1⁄3N), kundi la kati (1⁄3N) na L. maksi za

chini (1⁄3N).

sampuli ya uchanganuzi ambayo hasa ndio

inayohusika na ukokotozi wa upambanuzi wenyewe

huitwa T, nayoundwa na kundi la Juu la H na lile la

chini L.

T= H+L

3.Kokotoa uwezo wa kupambanua (D) kwa kutumia

kanuni hii

D =RH-RL⁄½T

Wakati D= ni uwezo wa swali kupambanua

RH= ni idadi ya H waliopatwa swali.

RL= ni idadi ya L waliopatwa swali

T= ni idadi ya walioshirikishwa. Kundi shiriki

ambalo ni (1⁄3N) ya juu na (1⁄3N) wa chini


mfano wa ukokotozi.

Kwenye mtihani uliofanywa na wanfunzi 18,

wanafunzi 4 bora walipata swali la tano na

wanfunzi 2 duni walipata swali hilo.

Kutoka kwenye kanuni

D =RH-RL⁄½T

H= 1/3* 18= 6

L= 1/3* 18= 6

T= H+L=12

D= (4-2/½*12)= 2/6

D= 0.3

Kwa hiyo kiwango cha ugumu wa swali mla 5 D5=

0.3.

unapopata D= +1; hii ni namba ya juu kabisa.

Namba hii tafsiri yake ni kuwa wanafunzi wote

hodari wamelipata swali na wasio hodari

wamelikosa.

Ukipata D= 0 hii ina maana kuwa swali husika

halina uwezo wowote wa kupambanua.

Endpo D=-1 tafsiri yake ni kuwa wa wanafunzi

wengi wenye uwezo wa chini wamelipata swali hilo


ukilinganisha na wanafunzi wenye uwezo wa chini.

Swali au maswali kama hayo hayafai kwenye

mtihani.

Mwongozo wakutambua maswali ya mtihani yalio

bora

Kiwango cha D

Tafsiri yake

Uamuzi wa kuchukua

0.4 na zaidi

Swali linafaa

Libaki katika mtihani

0.2- 0.39

Haliridhishi

Lilekebishwe kisha lijaribiwe tena,

0.1- 0.19

Halilidhishi

Liondelewe katika mtihani

D=-(Hasi)

Halilidjishi

Liondelewe katika mtihani

You might also like