You are on page 1of 10

Hatua za kustawisha pendekezo la utafiti

na
shehe mutwiri
Chuo kikuu cha CHUKA
YOUTUBE: MUTWIRI FRED

0713311971
UTAFITI – Ni uchanganuzi wa data fulani kwa undani
na kwa kufuata utaratibu wa kisayansi ili kupata
uvumbuzi wa tatizo mahususi na kuongeza maarifa
SIFA ZA UTAFITI
USAHIHI
KUTOPENDELEA
KUTHIBITIKA
USTADI
MAARIFA MAPYA
UMUHIMU WA UTAFITI
MIRADI
SERA
VIONGOZI WA SERIKALI
WANABIASHARA
WANAFUNZI
WAHAKIKI
WANALUGHA
SEHEMU ZA PENDEKEZO LA UTAFITI
MADA YA UTAFITI
1.0 USULI WA MADA
1.2 SUALA LA UTAFITI
1.3 MADHUMUNI YA UTAFITI
1.4 MASWALI YA UTAFITI
1.5 UMUHIMU WA UTAFITI
1.6 UPEO WA UTAFITI
1.7 MAELEZO YA ISTILLAHI
2.0 MWAUO WA MAANDISHI
2.1 NADHARIA YA UTAFITI
3.0 MBINU ZA UTAFITI
3.1 ENEO LA UTAFITI
3.2 WALENGWA WA UTAFITI
3.3 SAMPULI YA UTAFITI
3.4 MAADILI YA UTAFITI
3.5 UKUSANYAJI WA DATA
3.6 UCHANGANUZI WA DATA
MADA YA UTAFITI
SIFA ZA MADA YA UTAFITI
Inapaswa kuwa ya kuvutia

Mada inayolingana na taaluma inayotafitiwa


Mada iliyo na marejeleo yanayofaa
Haipaswi kuwa pana sana au finyu sana
Lazima iwe na umuhimu fulani
Ilenge kutatua tatizo fulani
Kila mada lazima iwe na malengo mahususi
NAMNA YA KUPATA MADA
 Mazungumzo katika mihadhara na semina , usomi wa vitabu, mapendekezo katika
tasnifu, vyombo vya habari , kushiriki mijadala au suala linalomsumbua mtafiti
USULI WA UTAFITI
Usuli wa mada hutekeleza dhima ya utangulizi katika pendekezo. Hutumika kuthibitisha kuwa kweli
kuna tatizo ambalo linahitaji suluhu hivyo kuipa mada yako uhalalisho.
SUALA LA UTAFITI
Ni sehemu ambayo huonyesha tatizo linalotafitiwa. Sharti mtafiti aonyeshe mwanya uliopo katika
kazi tangulizi na jinsi mianya hiyo itakavyozibwa.
Umuhimu wa utafiti - Kila utafiti una mchango wake.
UPEO WA UTAFITI - Hii ni mipaka ya utafiti wako.
MAELEZO YA ISTILLAHI - Hizi ni istillahi zitakazotumika katika muktadha wa utafiti wako.
MWAUO WA MAANDISHI
Ni utaratibu wa kutambua yaliyo na umuhimu kuhusu mada ya utafiti. Huwasilishwa kwa kueleza
kazi hiyo inahusu nini, uhusiano uliopo baina ya kazi hiyo na yako, kufafanua jinsi kazi hiyo
itakuwa ya muhimu katika utafiti wako na tofauti iliyopo baina ya utafiti wako na kazi hiyo ya
awali.
NADHARIA YA UTAFITI
Nadharia ni maelezo ya kisayansi yanayotolewa kuhusu jambo
fulani ambalo halijathibitishwa kuwa la kweli.
Mtafiti anaweza kutumia nadharia moja au zaidi ya moja.
Mtafiti aonyeshe waasisi wa nadharia kwa kutaja majina yao na
mwaka.
 Vilevile aonyeshe mihimili au nguzo za nadharia hiyo na jinsi
itakavyomsaidia katika utafiti wake.
Iwapo nadharia ina mitazamo tofauti itaje huku ukionyesha jinsi
ilivyoanza na kuendelea kuboreshwa.
MBINU ZA UTAFITI
Hii ni sehemu inayoonyesha aina ya data atakayokusanya mtafiti na iwapo utafiti
wake ni wa nyanjani au maktabani.
UTAFITI HUCHUKUA MIKONDO MBALIMBALI

Utafiti wa kukadiria kiasi (quantitive research)


Utafiti wa upelelezi (exploratory research)
Utafiti wa fafanuzi (descriptive research)
Utafiti wa ukadiriaji ubora (qualitative research)
ENEO LA UTAFITI - Hili ni eneo la kijiografia na ni lazima litajwe kwa majina na
kueleza sababu ya kuteua sehemu hiyo.
WALENGWA WA UTAFITI – Huteuliwa kulingana na jinsia, umri, cheo katika jamii.
Uteuzi wao lazima utolewe sababu
UTEUZI WA SAMPULI - Huu ni uteuzi wa sehemu ya utafiti au watu kwa kuzingatia sababu
maalum.
VIFAA VYA UTAFITI – Katika sehemu hii mtafiti huonyesha vifaa atakavyotumia katika utafiti wake.
MAADILI YA UTAFITI – Maadili ni suala muhimu sana katika utafiti kwani utafiti unapaswa kuwa
wa uwazi na uadilifu
UKUSANYAJI WA DATA – Mtafiti aonyeshe namna ambavyo data itakusanywa maktabani na
nyanjani.
UCHANGANUZI WA DATA - Aonyeshe hatua ambazo atazingatia katika uchanganuzi wa data. Ili
zizalishe matokeo.
SEHEMU ZINGINE ZA PENDEKEZO
BAJETI YA UTAFITI – Hii huonyesha kiwango cha pesa atakazotumia mtafiti kugharamia utafiti
wake.
RATIBA YA UTAFITI – Huu ni mukhtasari wa yatakayofanyika wakati wa kuandika ripoti.
MAREJELEO - Kazi ambazo zimerejelewa katika pendekezo
KILA LA HERI UNAPOANDIKA
PENDEKEZO LAKO. MWENYEZI
MUNGU AKUNEHEMESHE KATIKA
SAFARI HII. HUHITAJI BIDII WALA
SI KULAZA DAMU. INSHALLAH.
SHEHE MUTWIRI
0713311971.

You might also like