You are on page 1of 2

CHUO KIKUU CHA KIMETHODIST, KENYA

MTIHANI WA MWISHO WA TREMESTA YA PILI 2021

KITIVO : ELIMU NA SAYANSI YA JAMII


IDARA : ELIMU
KODI : KISW 421
ANWANI : SINTAKSIA YA KISWAHILI
MUDA : SAA MBILI

MAAGIZO:
 Jibu Maswali Matatu
Swali la Kwanza
(a) Fafanua aina tano za vivumishi na uvitolee mifano katika muktadha na sentensi. [alama 7]
(b) Eleza mchango wa wanasarufi wowote watano wa kimapokeo huku ukieleza mchango
wao kwa sintaksia kama tuijuavyo leo. [alama 10]
(a) Pambanua dhana ya KN na KT kama inavyotumia katika sintaksia. Toa mifano miwili kwa
kila mojawapo. [alama 6]
(b) Chambua sentensi zifuatazo ukitumia matawi [alama ]
i. Alitutembelea juzi
ii. Askari aliyefutwa kazi amehamia kwao
iii. Jirani amehamia shamba lake na yeye alimsaidia sana

Swali la Pili
a) Fafanua aina za sentensi zifuatazo ukitoa mifano ya Kiswahili
i) Sentensi sahihi [alama 2]
ii) Sentensi ambatano [alama 3]
iii) Sentensi changamano [alama 3]

KISW 421/Page 1 of 2
b) Tofautisha aina tatu kuu za vitenzi kwa kuitungia sentensi mbili kila mojawapo. [alama
9]

Swali la Tano
(a) Jadili uhusiano uliopo kati ya sintaksia na mofolojia. [alama 8]
(b) Fafanua dhana ya kihusishi katika sentensi ya Kiswahili [alama 10]

Swali la Tatu
a) Ainisha nomino za Kiswahili na kisintaksia [alama 10]
Jadili kwa nini uanishaji wa maneno ya Kiswahili kisintksia ni mwafaka Zaidi kuliAinisha ngeli
za Kiswahili kisintaksia. Toa mifamo mahsusi. [alama 10]

KISW 421/Page 2 of 2

You might also like