You are on page 1of 36

SINTAKSIA/sarufi miundo

UTANGULIZI
DHANA YA SINTAKSIA

 TUKI (1990): Tawi la isimu la sarufi linaloshughulikia


uchanganuzi wa mpangilio wa uhusiano wa vipashio katika
sentensi
 MASSAMBA (2009): taaluma ya isimu inayojishughulisha na
uchunguzi wa mahusiano yaliyopo kati ya maneno na
tungo.
 Vipashio muhimu katika sintaksia ni maneno, virai na
vishazi.
 Philipo na kuyenga (2017) Kigiriki Syntax-Syn-kuwa pamoja
na taxis-panga vitu kwa mpangilio maalumu.
KAZI YA SINTAKSIA

 Kutambua usahihi wa sentensi kimuundo. Mf.


 Kutambulisha uhusiano wa maneno ndani ya sentensi
mf
 Kumpa mtumiaji lugha uwezo wa kutunga sentensi
zenye urefu wowote na nyingi iwezekanavyo hata zile
ambazo hazijawahi kusikika na msemaji huyo.
 Kutambulisha maana katika sentensi na iwapo
mpangilio wa sentensi ni mzuri, lazima itakuwa na
maana.
Mawanda ya sintaksia

 Uainishaji wa maneno na viambajengo vingine vya


sentensi
 Uchambuzi wa mpangilio wa maneno katika
sentensi
 Uchunguzi wa uhusiano wa maneno na vipashio
vingine vya sentensi
 Uchambuzi wa miundo ya sentensi
 Uchambuzi wa nadharia na sharia zinazotawala
miundo ya sentensi
Msingi wa sintaksia

Sentensi huundwa na kishazi k1+


Kishazi huundwa na kirai k1+
Kirai huundwa kwa neno 1+
Neno huundwa na mofu 1+
VIGEZO VYA UAINISHAJI SENTENSI ZA
KISWAHILI
 Kigezo cha muundo
sentensi ya Kiswahili inaweza kuainishwa kunne: sentensi sahili,
ambatani, changamani na ambatani changamani

 Sentensi Sahili
 Sentensi sahili huundwa na kishazi huru kimoja ambacho
maana yake ni kamilifu. Mara nyingi sentensi sahili huwa na
muundo wa kiima au kikundi nomino na kiarifu au kikundi
kitenzi (Matinde, 2012). Kwa mfano:
 Mwalimu anafundisha.
 Salamba anaimba.
Uainishaji wa sentensi

 Sentensi ambatani
 Sentensi ambatani ni sentensi yenye vishazi viwili au zaidi
vilivyounganishwa kwa kutumia viunganishi, hususani na,
lakini, wala, au, tena, ila, ingawa na pia. Kila kishazi
katika sentensi ambatani huweza kujitegemea kama
sentensi, kwa mfano:

 Mwalimu anaimba na wanafunzi wanamsikiliza


Uainishaji wa sentensi

Sentensi changamani
 ni sentensi inayoundwa na kishazi kimoja huru ambacho
ndicho kikuu na kishazi tegemezi. Pia, sentensi hii inaweza
kuwa na vishazi viwili vitegemezi. Mifano ya sentensi
zifuatazo inadhihirisha sentensi changamani.
 Mwanafunzi aliyefika jana ameondoka.
 Mawingu yakitanda mvua hunyesha.
Uainishaji wa sentensi

 Sentensi ambatani changamani


 Sentensi ambatani changamani huundwa kwa vishazi viwili au zaidi. Kimsingi,
huundwa kwa sentensi changamani na kishazi huru. Sentensi changamani
huunganishwa na kishazi huru kwa kutumia viunganishi ambatani (Matei,
2008). Kwa mfano:
 Maasi yaliyotokea hapa iliwatisha wengi, ila hayakusababisha maafa.
 Magauni ambayo hufanyiwa ukarabati hudumu, lakini mengine hayadumu
kigezo cha kiuamilifu / kidhamira/ kimaana

 Kwa kuzingatia kigezo cha uamilifu, sentensi ya Kiswahili


huainishwa kwa kuzingatia kazi inayotekelezwa na
sentensi husika. Haitegemei mpangilio wa vipashio au
muundo.
 Sentensi arifu
 Sentensi arifu hutoa taarifa au ujumbe fulani na huishia
kwa kitone au nukta. Sentensi hizi pia hutoa kauli. Kwa
mfano:
 Badokufa anacheza ngoma.
 Nyati wanamshambulia simba.
Kigezo uamilifu

 Sentensi Swalifu
 Sentensi swalifu huuliza swali kuhusu jambo fulani
na huishia kwa alama ya kuuliza.
Kwa mfano:
 Wazee wamehitimisha kikao?
 Mkuu wa sheria amefika kortini?
uamilifu

 Sentensi amrishi
 Sentensi amrishi huwa na kazi ya kuamrisha. Kimsingi
humwagiza anayesikiliza kutenda jambo fulani,
ndiposa Matei (2008) anaziita sentensi agizi. Sentensi
hizi huishia kwa alama ya hisi au nukta. Mara nyingi
sentensi hizi huwa na sehemu ya kiarifu tu. Baadhi ya
mifano ya sentensi hizi ni:
 Zima runinga!
 Kuja hapa!
uamilifu

 Sentensi mshangao
 Kiuamilifu, sentensi mshangao hudhihirisha hisia
za mshangao kutoka kwa msemaji, kuhusu jambo
fulani. Aghalabu, huishia kwa alama ya hisi au
mshangao. Tazama mifano ifuatayo:
 Siamini wazee walitindi mpaka wakadondoka!
 Hata wewe unanichezea!
uamilifu

 Sentensi shurutia

 Sentensi shurutia ni za masharti na huundwa kwa vitenzi viwili.


Kitenzi cha kwanza hukamilishwa na kitenzi cha pili ili
kudhihirisha uhusiano wa masharti. Kimsingi huonyesha
kutegemeana kwa matukio, kutokuwa na uhakika na kuwezekana
kwa jambo fulani. Sentensi zifuatazo zinadhihirisha hali hii:
 Kama wakoloni Waingereza wangehimiza ufundishaji wa Kiswahili
mapema, kama Wajerumani, kingekuwa kimeimarika zaidi nchini
Kenya.
 Ukisoma kwa bidii utafaulu mitihani yote ya shahada ya uzamifu.
uamilifu

 Sentensi rai
 Sentensi rai huonyesha ombi la kufanyiwa jambo fulani.
Kwa mfano:
 Tafadhali, peleka mifugo malishoni.
 Samahani, singeweza kufika chuoni jana.
Sifa za sentensi za kiswahili

 Huzingatia upatanisho wa kisarufi


 Zinaweza
kuwa na miundo ya Virai–Vitenzi peke yake
(ANAIMBA< ANAENDA…)
 Sentensi zenye viambishi vinavyobadilisha hadhi ya
vipashio vya sentensi- Viambishi kama vile -po-, -ki-,
-nge-, -ngali- huzalisha vitenzi–vitegemezi ndani ya
sentensi. Vivyo hivyo, viambishi vingine kama -ye- ,
-cho- , -vyo-, -lo- huunda vishazi ambavyo hubebwa
na Virai–Nomino.
Muundo wa senteni

Kimsingi,
muundo wa sentensi una
sehemu mbili kuu:
kiima;
kiarifu
Kiima: dhana na miundo yake

 Ni kipashio amilifu katika sentensi kinachohusika na


utendaji/nomino inayosababisha utendaji wa tendo
 Nomino za kawaida na za pekee
 Viwakilishi
 Nomino kadhaa zilizounganishwa na kiunganishi
 Nomino na kishazi tegemezi
 Nomino na kivumishi
 Nomino zilizotokana na vitenzi
kiarifu

 Ni sehemu ya 2 katika mgawanyo wa sentensi-hueleza


alichofanya kiima/hueleza tendo
 Kiima huundwa kwa elementi mbalimbali:
 Kitenzi
 Shamirisho (Yambwa)
 Kielezi
 Kikumushi
 kijalizi
kitenzi

 Mtoto anacheza
 Baba anaimba
 Kakake anaroga
kielezi

Purity
yuko nyumbani
Jumba anakimbia sana
shamirisho

 Ni jina la mtu/kitu kinachotendewa tendo na huja baada ya kitenzi kikuu-


hukaliwa na mtendwa au mtendewa
 aina zake: shamirisho kipozi-hupokea tendo moja kwa moja-baba
anasoma kitabu
 Shamirisho ala/kifaa/kitumizi-chombo kitumikacho kutekeleza tendo –
walilima shamba kwa majembe; waliandika barua kwa kalamu
 Shamirisho kitondo-kitu/mtu anayefaidika na tendo la yambwa. Pia
huitwa yambiwa: mkalimani aliwatafsiria waumini kifungu cha mathayo
chagizo

 Hutoa maelezo ya jinsi na wapi tendo


lilifanyika
 Gury alimpiga mwanafunzi vibaya sana
 Watoto wote wamekusanyika ukumbini
kijalizi

 hutoa
Kipashio amilifu katika sentensi ambacho
maelezo ya kitenzi-hukamilisha kitenzi
 Maria ni mwanasheria; calisters anaenda Uganda

Kijalizi kinaweza kuwa nomino, kivumishi au


kielezi
Kikumushi-furushi/kumsha/toa taarifa

 Neno, kirai au kishazi kinachotoa maelezo ya ziada kuhusu


nomino, viwakilishi, vielezi, vitenzi, vivumishi na vihusishi
(Philipo na kuyenga, 2017)
 Si vivumishi asilia ila hufanya kazi kama vivumishi (khamisi
na kiango, 2002)
 Tofauti kati yake na vivumishi ni upana wa utendakazi.
 Aina za vikumushi-kikumushi nomino; kikumushi kionyeshi;
kikumushi kimilikishi; kikumushi kiulizi; kikumushi kirai;
kikumushi kishazi
kishazi

 Neno/mpangilio wa maneno wenye kirai kitenzi kimoja


ndani mwake. Chaweza kuwa kitenzi kukuu au kitenzi
kirejeshi (Philipo na kuyenga, 2017)
 Neno/fungu la maneno lenye kiima na kiarifu au kiarifu
pekee ambacho huwa ni sehemu ys sentensi kuu
 Kuna aina mbili: huru na tegemezi
Kishazi huru/kishazi kikuu

 Husimama pekee na kutoa maana kamili au kwa


mtazamo wa kisintaksia, ni kishazi chenye kitenzi
ambacho hakijashushwa hadhi, yaani uarifishwaji
wake ni mkamilifu
 Mfano:yule mhadhiri ni mwizi; gari lake
limepotea
Kishazi tegemezi

 Ni kishazi kilicho na kitenzi kilichoshushwa hadhi


na hivyo kusababisha uarifishaji usokamili.
 Ushushwaji hadhi huu hutokana na urejeshi au
viambishi masharti
 Mfano: akija nitamwambia;angejua yatampata
asingekuja leo; aingiapo darasani…; ameda
alipoteuliwa…;
AINA YA vishazi tegemezi

 Aina mbili: vishazi tegemezi vivumishi na vishazi tegemezi vielezi


 Vishazi tegemezi vivumishi-huandamana na jina linalovumishwa mf-mwanafunzi aliyefukuzwa,
mchungaji aliyekula kondoo; kitabu kilichoibwa au haviambatani na jina mf.waliofuzu wameondoka;
aliyekuja…;
 Vishazi tegemezi vielezi-
 Vya mahali-alikoenda hakujulikani; alimolala mnanuka
 Vya njeo-utakapomaliza masomo; walipotajirika walisahau walezi wao
 Vya jinsi-wanavyocheza handiboli;
 Vya masharti-viambishi ki, ngali, ngeli-ungerauka ungemkuta; ukifaulu kupata kazi usinisahau
 Vya ukinzani-japokuwa, ingawa,-ingawa walicheza vizuri, hawakufua dafu
 Vya sababu-alizawidiwa kwa sababu, utaadhibiwa kwa kosa…
Sifa za kishazi

 Vishazi hupatikana ndani mwa sentensi au nje ya sentensi


 Lazima viwe na kitenzi-kikuu au kilichoshushwa hadhi
 Baadhi ya vishazi huweza kujitegemea kama sentensi kuu-
kishazi huru
 Baadhi ya vishazi haviwezi kujitegemea kama sentensi
 Vishazi vingi huwa na kiima Dhahiri
 Vishazi hutekeleza majukumu mbalimbali ya
kisarufi/kisintaksia-laweza kuwa jukumu la kiima, yambwa nk.
 Vishazi vya kawaida, hasa vikuu, huwa na kitenzi kikuu kimoja.
kirai

Ni mpangilio wa maneno


ambao una neno kuu moja
Hauna muundo wa kiima
na kiarifu
Sifa za kirai

 Hufanya kazi kama neno moja/huwakilisha dhana


moja/hufanya kazi kama nomino
 Hudokeza maana ila si kamili-maembe mengi?
 Si kamili kimuundo-kiima na kiarifu
 Huainishwa kutegemea neno kuu
 Huundwa kwa maneno yanayoendana
 Lazima maneno yapangwe kimantiki…mpira anacheza…
anacheza mpira
Aina za virai
 KIRAI NOMINO- Neno kuu ni nomino-Mtoto yule…[kn]

 KIRAI KITENZI-Neno kuu ni Kitenzi-Anacheza [kt]

 KIRAI KIVUMISHI..Neno kuu ni kivumishi-Mzuri sana, [kv]

 KIRAI KIELEZI-Neno kuu ni kielezi-Mwerevu sana, sawasawa, [ke]

 KIRAI KIHUSISHI-neno kuu ni kihusishi-Mbele ya/nyuma ya [kh]

 KIRAI KIBAINISHI-engine, engi/ingi,ote/oote,hiki, kile, yule [kb]


KIRAI NOMINO:muundo

 Neno kuu ni nomino au kiwakilishi.


 Muundo wake:
 [N]-baba
 [N]+[n]+[n]+…baba, mama, shangazi na watoto
 [N]+[v1] au+[v+v…] baba mmoja; mabati yale manne makundu…
 N+S-mbuzi ambao chikamai alitoa kama mahari ya muhalia…
 N+kirai-kivumishi-wanafunzi wengine ambao hawajielewi huwa na
matatizo ya kusajili kozi mkondoni.
 Kitenzi-jina na kivumishi-kuondoka kwake…
 [w]Kiwakilishi pekee- sisi, wao, nyinyi..nk
Kirai kitenzi
 Neno kuu ni kitenzi
 [T]-tutapendana
 [T]+[N1]-wamebomoa nyumba
 [T]+[n+n]-amempa mtoto chakula; alimpiga mama kofi
 [T]+[T]-anapenda kusoma;ameamua kuoa
 [T]+[n]+[T]-oroni anafundisha lizzy kuomba
 [T]+[s]-amesema (kwamba) atarudi kesho; analalamika (kuwa) amelazimishwa kuenda shule
 [T]+[e]-moto umewaka sana; mwalimu ameenda shuleni
 Ruwaza za kitenzi “kuwa”-ni mzuri, alikuwa na pesa; yumo shuleni; itakuwa vizuri kumzuru; ni vyema
kumwona kwanza
 T+ VITENZI SAMBAMBA+ E-ALIZALIWA, AKAISHI, AKAFA ASUBUHI/MAPEMA
Virai Vivumishi

 Neno kuu ni V
 Aina zake:
 V+KN-anapenda mwenye kandarasi; mwenye mali; wenye watoto
 V+E-mrembo sana; mweusi ti; mkali ajabu;
 V+KT-mwema ameenda; chenyewe kimechafuka; changu hakipo; kibaya chajiuza
 V+Kirai Kiunganishi-Mpungufu wa akili; nzuri ya kupendeza; hodari wa mapenzi

You might also like