Professional Documents
Culture Documents
WAKUMBUKUMBU
NA
DAKTARI WA KISWAHILI
FAGIL
Kumbukumbu ni kuhifadhi kimaandishi ya mambo
yanayojadiliwa katika mkutano. Kumbukumbu hutumiwa
kama ithibati na ukumbusho wa yale yaliyozungumzwa katika
mkutano. Katika uandishi wa kumbukumbu, mwandishi
afuatie utaratibu maalum kwa kuzingatia sifa zifuatazo;
Andika mada au kichwa cha kumbukumbu; kichwa lazima
kionyeshe-jina rasmi la kikundi/shirika, mahali pa mkutano,
tarehe na saa za mkutano. Kwa mfano;
KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA SHIRIKA LA MSALABA MWEKUNDU ULIOFANYIKA
KATIKA UKUMBI WA SHULE YA KIJENSI MBARARA MNAMO IJUMAA TAREHE
08.09.20173SAA SITA ADHUHURI
WALIOHUDHURIA. CHEO
1. Bw. Mapese.mnene Mwenyekiti
2. Bi.Atim Kosoro Katibu mkuu
3. Bw. Lusidu Sango Mwanakamati
4. Bw. Oken James Mwanakamati
5. Bi.Juma Mpole Mwanakamati
6. Bi.Nazifa Lenana Mwanakamati
Waliokosa kuhudhuria kwa udhuru
1.Bw. Aijuka Samson
Mwanakamati
Waliokosa kuhudhuria bila ya udhuru
Bi. Polina Okoth
Mwanakamati
Ajenda
Dua la kwanza
Mawaidha ya mwenyekiti
Usajili wa wanafunzi
Ulipaji wa Karo
Mengineyo
Kumb:01/mk/01/2023; Dua la kwanza
Mkutano ulianza saa sita za mchana na maombi kutoka kwa mwanakamati ambaye
akamuomba mola kuwa kiongozi wayatakayo jadiliwa.
Kumb:02/mk/01/academia2017; Mawaidha ya mwenyekiti
Mwenyekiti alianza mkutano kwa kumshukuru Rabana ambaye aliwawezesha
kusikiliza.
Kumb:03/mk/01/2023;Usajili wa wanafunzi.
Wanakamati walikubaliana kwamba shule iwasajili wanafunzi wengine arobaini
wa
ziada (40) katika kidato cha tano ili kukidhi mahitaji.
Kamati iliamua kwamba viti zaidi vinunuliwe kutosheleza ongezeko hilo la
wanafunzi.
Kamati ilipendekeza wanafunizi wafike shuleni tarehe 07/07/2023.
Kumb:04/mk/01/academia2023;ulipajiwakaro
Wanakamati walikubaliana kwamba gharama ya chakula ipandishwe ili kukidhi
malalamiko ya wanafunzi kuhusu chakula kidogo kinachowapewa.
Waliamua kwamba kila mwanafunzi alipe karo kamili kabla ya kusajiriwa.
Kamati iliamua kwamba kila mwanafunzi alipe shilingi elfu mbili (2000/=)
za ukarabati na ununuzi wa vifaa vya ziada.