You are on page 1of 7

Muundo

Bahari za Ushairi
Bahari za ushairi ni nyingi sana. Shairi huainishwa katika bahari fulani kulingana na mtindo
wake, umbo lake na matumizi ya lugha.

Baadhi ya bahari za ushairi kwa kuzingatia vipande

1. Utenzi – shairi ndefu lenye kipande kimoja katika kila mshororo.


2. Mathnawi – ni shairi la vipande viwili (ukwapi na utao) katika kila mshororo.

Ewe mtunga silabi, na sauti ya kinubi,


Majukumu hatubebi, maadamu hatushibi,
Mateso kwa ajinabi, kwa mabwana na mabibi
Ukija hayatukabi, karibia karibia

3. Ukawafi – ni shairi la vipande vitatu (ukwapi, utao na mwandamo) katika kila mshororo.

Nashindwa nikupe nini, nishukuru kwa malezi, mapenzi na riziki,


Ni pendo kiasi gani, lishindalo la mzazi, kweli mama hulipiki,
Ulinilinda tumboni, ukilemewa na kazi, ila moyo huvunjiki,
Kanilisha utotoni, mavazi pia malazi, ukitafuta kwa dhiki.

4. Bantudi – Shairi la vipande vinne (ukwapi, utao, mwandamo na ukingo) katika kila
mshororo.

Sisi walipa ushuru, wajenga taifa, tena kwa bidii, twahangaishwa,


Tumenyimwa uhuru, tuna mbaya sifa, hatujivunii, tunapopotoshwa,
Kila tunapopazuru, damu na maafa, hatutulii, hali ya kutishwa

B. Baadhi ya bahari za ushairi kwa kuzingatia vina

5. Ukaraguni – shairi ambalo vina vyake vya kati na vya mwisho hubadilika kutoka ubetio
mmoja hadi mwingine.

Vina Ubeti 1: —ni, —mi,


ubeti 2: —ta, —lo,
ubeti 3: —po, —wa,

6. Ukara – shairi ambalo vina vya kipande kimoja havibadiliki kutoka ubeti mmoja hadi
mwingine, lakini vina vya kipande kingine hubadilika. Kwa mfano, vina vya kati
vinafanana kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho lakini vina vya kipande cha mwisho
vinabadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.

vina Ubeti 1: —shi, —ma,


ubeti 2: —shi, —ko,
ubeti 3: —shi, —le,
ubeti 4: —shi, —pa

7. Mtiririko – shairi ambalo vina vyake vya mwisho na vya kati havibadiliki kutoka ubeti
wa kwanza hadi wa mwisho.

kwa mfano vina vikiwa ( —ni, —ka) kutoka ubeti wa kwanza hadi wa mwisho.

Baadhi ya bahari za ushairi kwa kuzingatia maneno

8. Mkufu/pindu – Shairi ambalo neno la mwisho au kifungu cha mwisho cha maneno
katika ubeti mmoja, hutangulia katika ubeti unaofuatia.

Hakika tumeteleza, na njia tumepoteza,


Nani wa kutuongoza, aliyepewa uweza,
Filimbi akipuliza, tusiyeweza kupuuza,
Bali twaisikiliza, bila ya kuzungumza,

Bila ya kuzungumza, wala mwendo kulegeza,


Tumwandame ja mwangaza, kututoa palipo giza,
Penye dhiki ya kuliza, bila sauti kupaza
Pengo hili kulijaza, ni nani anayeweza,

9. Kikwamba – Neno moja au kifungu cha maneno hurudiwarudiwa kutanguliza mishororo


au ubeti katika shairi.

Jiwe hili lala nini, ila moshi na majani,


Jiwe linalala lini, litokapo vileoni,
Jiwe hili halineni, lina macho halioni,
Jiwe na tulibebeni, tulitupe mitaroni

Baadhi ya bahari za ushairi kwa kuzingatia mizani

10. Kikai – Shairi lenye kipande kimoja kifupi (chenye mizani chache kuliko kingine) Mfano
(8,4)

Nani binadamu yule, adumuye,


Anayeishi milele, maishaye
Jenezani asilale, aluliye,
Kaburi liko mbele, sikimbiye.
11. Msuko – Shairi ambalo kibwagizo/mshororo wa mwisho ni mfupi kuliko mishororo
mingineyo. K.v (8,8) (8,8) (8,8) (8).

Hawajazawa warembo, usidhani umefika,


Ukisifiwa mapambo, jinsi ulivyoumbika,
Akipata jipya umbo, ‘tabaki kihangaika,
Usidhani umefika.

Bahari kutegemea ishororo

Tathmina/umoja

Ni shairi lenye mshororo mmoja kaka kila ube. Mashairi ya aina hii hayapakani kwa
wingi. Vielelezo vifuatavyo vinaashiria aina hii ya shairi.

Tathnia/uwili

Ni shairi lenye mishororo miwili katika kila ubeti. Mashairi haya ingawaje yapo, lakini pia kwa
uchache

Tathlitha/utatu/wimbo

Ni shairi lenye mishororo mitatu katika kila ubeti. Shairi la aina hii wakati mwingine pia huitwa
wimbo. tazama shairi lifuatalo;

1. Wakale metenda mengi, milele ya kukumbuka,


Walioanzisha misingi, ambayo yaaminika,
Waleo hutupingi, baadhi tungekenka.

2. Wakale metuongoza, njia zilizo nyooka,


Ukulima walianza, mvua zinapofika,
Waleo twajipoteza, kuiaga wasioigika.

Tarbia/unne

Ni shairi lenye mishororo minne katka kila ubeti. Mashairi mengi ambayo yametungwa huwa ni
ya aina hii. Mfano ni kama ufuatao;

Binadamu hatosheki, ni kiumbe chenye zani, kweli mja hapendeki,


Kwa kweli haaminiki, hila ameficha ndani, la wazi ni unafiki,
Ukweliwe haafiki, njama zake zi moyoni,usimwone ni rafiki,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake,ni hatari kama nyoka.

Wengine watakuua,wakiona una pesa,hata zikiwa kidogo,


Hizo kwao ni maua,hupupiwa zikatesa,wakizifuata nyago,
Hadi kwenye wako ua, pasipo hata kupesa, wala kukupa kisogo,
Mtu kuwa na tamaa, akitaka kiso chake, ni hatari kama nyoka.
Takhmisa/utano
Ni shairi lenye mishororo mitano katika kila ubeti. Rejelea mfano ufuatwao;
Kwenye shamba hilo kubwa asilani hakunyi mvuwa!
Ni kwa mitilizi ya jasho langu ndiyo hunweshezewa
Kwenye shamba hilo kubwa sasa imeshaiva kahawa
Na bunize ni matone ya damu yangu niliyotowa
Ndipo mte ukatipuza!

Tasdisa/usita
Ni shairi lenye mishororo sita katika kila ubeti. Tazama shairi linalofuata ambalo pia wakati
mwingine hujulikana kama tashlita.
Ewe hisia!
Umeniamshia ndoto niloisahau zamani
Umelimsha mwangu moyoni
nyimbo ya kale
na mdundo usomvutia
ila hayawani wa mwangu rohoni.

Tulia sasa tulia.


Hebu tulia ewe hisia ulo mtimani.
Nakataa katu kusisimkakwa sauti yako laini
Kwani njia zetu ni panda
Daima hazioani

Tasbia/usaba – ni shairi lenye mishororo saba katika kila ubeti.

Naudi/unane – ni shairi lenye mishororo minane katika kila ubeti

Telemania/utisa – ni shairi lenye mishororo tisa katika kila ubeti

Ukumi– ni shairi lenye mishororo kumi katika kila ubeti. Pia shairi hili huitwa ushuri.

Soneti- ni shairi lenye mishororo kumi na minne katika kila ubeti.

Bahari nyingine
Malumbano – Mashairi mawili ambapo mshairi mmoja hutunga shairi akijibu au kupinga utunzi
wa mshairi mwengine.

Ngonjera – Shairi lenye wahusika wawili wanaojibizana. K.m. Ubeti wa kwanza, mwalimu, na
wa pili, mwanafunzi.

Sakarani – Shairi lenye bahari zaidi ya moja.


Sabilia – Shairi lisilokuwa na kibwagizo. Kituo (mshororo wa mwisho) hubadilika kutoka ubeti
hadi ubeti.

Shairi huru – shairi lisilozingatia sheria za ushairi

Shairi guni – shairi lenye makosa ya arudhi za shairi

Masivina- Ni bahari la shairi lisilo na urari wa vina katika mishororo yake. Hii ina maana kuwa
vina vyake vyote aidha vya kati au vya nje vinatofautiana baina ya mishororo. Vielelezo
vifuatavyo vinaelezea mfano wa bahari hii ya shairi.

Matapeli
Salamu naanza mimi, niwajuvye walimwengu
Muyatege masikiyo, uneni pate lipuka
Pia mutiye manani, asilani musipuze
Kina matapeli ndugu, hutokea kama njozi.

Wanooitwa matapeli, hao watu walaghai


Wonapo pato unalo, kukupoka hutamani
Wataja kufanya zuzu, japo wewe mashuhuri
Kina matapeli ndugu, hutokea kama njozi.

Taabili
Ni shairi ambalo limetungwa kwa nia ya kumsifu mtu aliyeaga dunia.
Mandhuma
Ni bahari ya shairi ambalo upande mmoja (ukwapi) hueleza hoja au huuliza swali na kisha
upande wa pili (utao) hutoa jibu au suluhu ya swali hilo.
Kisarambe
Ni shairi ambalo haswa limejikita kwa maudhui ya kidini. Huweza kuitwa pia
kasida
Sabilia
Ni shairi ambalo halina kibwagizo bali huwa na mstari wa kituo/kiishio/kimalizio.
Togoo
Ni aina ya shairi ambalo limetungwa kwa kusudi la kusifia uzuri wa mahali, mtu au kitu fulani.
Kumbukizi
Ni aina ya shairi ambalo huwakumbusha watu kuhusu matukio mahsusi katika jamii. Matukio
haya yaweza kuwa ya kihistoria, kidini au hata kishujaa. Kwa mfano ujio wa Rais wa Marekani
nchini Kenya, ujio wa Papa Mtakatifu (2015) ni matukio ya kihistoria

DHINI /KIBALI/ UHURU/ LESENI YA KISHAIRI

Kazi za sanaa huhitaji ubunifu wa hali ya juu. Hali hii hupelekea wakati mwingine watunzi kuenda kinyume na
kaida za matumizi ya lugha kimaksudi. Jambo hili huibua dhana ya uhuru wa kishairi. Uhuru wa kishairi ni idhini
au ruhusa ya mwandishi kutunga shairi kwa namna fulani bila kuzingatia kanuni za kisarufi. Uhuru wa kishairi
huhusisha yafuatayo:
A.Inkisari

Huu hapa ni uhuru wa mshairi kufupisha au kupunguza idadi ya ya mizani ya maneno


katika utungo wake ili kuwe na ulinganisho au urari wa mizani.

Mfano; Nalisifu langu Bara, Bara hili la afrika,


             Nalandika langu Bara, BAra lilosetirika,
             Nalitaja langu Bara, Bara lilowajibika,
             Naliweka kileleni, Bara langu la Afrika.

.Nalandika-Ninaliandika
Nalisifu-Ninalisifu
Nalitaja-Ninalitaja
Naliweka-Ninaliweka
Lisosetirika-Lisilosetirika
Lilowajibika-Lililowajibika

B.Mazida

Huu ni uhuru wa mshairi wa kuzidisha idadi ya mizani ya maneno ili kuwe na usawa katika idadi
ya mizani.

Mfano; Leo naja wajuzeni, hatua zake tohara,


              Taka waelimisheni, mwisho isilete dhara,
              Tohara ni kitu gani, si jambo la msihara...

Wajuzeni-wajuza
Waelimisheni-waelimisha

C.Tabdila.
Huu ni uhuru unaomwezesha mtunzi wa shairi kibadili muundo wa neno ili kutosheleza utamu
au matakwa ya lugha alidhamiria yeye binafsi.

Mfano; Kwa muovu sheithwani, nazichapisha sheria,


              Kumtoa duniani, jenamu kumwachilia,
              Hata na iwe sindani, fulani tamchomea...

Sheithwani-shetani
Sindani-Sindano
Jenamu-Jehanamu.

D.Utohozi

Huu ni uhuru unaomwezesha mtunzi au mshairi kuiga au kukopa neno au maneno kutoka lugha
nyingine.

Mfano; Siasi nalumba mie, makuu ya duniani,


              Sijasema situmie, simu na televisheni,
              Bali nasema mjue, dhahiri mwandike chini...

Televisheni-Runinga

E.Kuboronga Sarufi

Huwa ni kubadili mpangilio wa neno katika shairi .

Mfano; Nieleze nami hebu, kwani kuninyamazia.


              Au kuna gani tabu, iliyokuzuwiiya.
              Nataka juwa sababu, inipunguze udhiya.
              Kimya kingi ni kibaya, usikawakane nacho.

Nieleze nami hebu-Hebu nieleze nami


Au kuna gani tabu-Au kuna tabu gani

F. Ritifaa

Hii ni mbinu ya kukatiza neno ili kusawazisha mizani. Ritifaa inapo tumika ni kumaanisha
kwamba kuna baadhi ya neno au maneno yaliyoochwa.

Mfano; N'tatumwa ya kutumwa, mradi ni rambirambi,


              N'tpunguza kusema, maneno tupu siambi...
Kikale
 – ni matumizi ya msamiati wa kale, kwa mfano, nyuni badala ya ndege, mgunda badala ya shamba  n.k 

Vilugha/vilahaja
 – ni matumizi ya msamiati wa lahaja za Kiswahili badala ya Kiswahili sanifu.

You might also like