Professional Documents
Culture Documents
SHUGHULI
1. Katika makundi,
(a) Tajeni viongozi mbali mbali katika jamii yenu.
(b) Eleza majukumu ya voiongozi hawa.
Viongozi Wa Shule Viongozi Wa Kijiji/ Kata/ Mtaa Viongozi Wa Taifa
Mwalimu mkuu Mwenyekiti wa kijiji Rais
Naibu Mwalimu Mkuu Makamu wa mwenyekiti Makamu wa rais
Mwalimu wa zamu Katibu Spika wa bunge
Mkurugenzi wa masomo Diwani Jaji/ Hakimu mkuu
Mwalimu mshauri wa wanafunzi Mjumbe Waziri mkuu
Kiranja mkuu wa shule Meya Waziri
Kiranja wa darasa Katibu wa mji Mbunge
Mpishi mkuu Halmashauri ya kijiji Mkuu wa majeshi
Mhasibu wa shule Halmashauri ya mji Mkuu wa polisi
Mkutubi wa maktaba ya shule Mkuu wa askari wa majeshi
1
MAELEZO YA MAJUKUMU YA VIONGOZI:
SHUGHULI
1. Katika makundi,
(a) Tajeni majukumu matano ya Mwalimu Mkuu.
(b) Elezeni majukumu ya Spika wa bunge la taifa.
(c) Orodhosheni majina ya viongozi watano katika jamii na kueleza majukumu yao.
(d) Elezeni umuhimu wa viongozi katika jamii.
Majibu
1. Mwalimu Mkuu
(a) Kudumisha nidhamu shuleni. (to ensure that there is discipline in school)
(b) Kutunza mali ya shule. (to protect school properties)
(c) Kutunza pesa za shule na matumizi yake, (proper planning and allocation of school
resources)
(d) Kuandikisha wanafunzi shuleni. (admitting of new students at school)
(e) Kuratibu na kusimamia shughuli zote shuleni. (to supervise all school activities)
2. Majukumu ya Spika wa Bunge
(a) Mwenyekiti wa shughuli za bunge. (chairperson of parliament)
(b) Mratibu wa shughuli za bunge.
(c) Kuongoza vikao vya bunge.
(d) Kuongoza shughuli ya kutunga sharia.
(e) Kutangaza matokeo ya kura bungeni.
Umuhimu Wa Viongozi Katika Jamii
Kudumisha Amani.
Kupanga na kutekeleza miradi ya serikali.
Kutatua mizozo
Kuwajibika kwa mahitaji ya jamii.
Kudumisha utulivu na maendeleo.
Majukumu ya viongozi katika jamii:
SHUGHULI:
Katika makundi,
(a) Tajeni majukumu ya kiranja wa darasa.
Kudumisha usafi darasani.
Kudumisha nidhamu darasani.
Kutunza vifaa vya darasa.
Kukusanya vitabu vya wanafunzi na kupeleka kwa mwalimu ili visahihishwe.
Kufunga na kufungua darasa.
Kuwakilisha darasa katika shughuli zote za shule.
2
(b) Mwenyekiti wa Kijiji.
husimamia shughuli za uongozi kijijini.
Kudumisha usalama kijijini.
Kukata kesi za wanakijiji.
Kudumisha ushirikiano wa wanakijiji.
Kuendeleza sera za serikali.
KUPIGA KAMPENI ZA UCHAGUZI:
SHUGHULI:
Katika makundi
(a) Elezeni utaratibu wa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia.
(b) Jadili umuhimu wa kampeni za uchaguzi wa kidemokrasia.
(c) Manifesto ina umuhimu gani kwa mgombea uchaguzi na wanajamii kwa jumla?
(d) Jifikirie kwamba wewe ni mgombeaji wa nafasi fulani ya uongozi hapo shuleni. Fanya
kampeni mbele ya darasa kwa kujitambulisha na kuelezea manifesto yako. Tumia lugha ya
kushawishi.
Utaratibu wa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia:
Kuwa na kitambulisho kama mpigaji kura halali.
Kujisajilisha.
Jina kupatikana katika kitabu cha usajili.
Kupiga kura moja kwa yule umtakaye.
Kupiga kura yako kwa hiari bila kuamuliwa na mtu mwingine.
Baadhi ya sababu za kufanya kampeni za uchaguzi:
Kueleza manifesto.
Kujitambulisha kwa wapiga kura.
Kutoa ahadi za mambo ambayo watawafanyia wapiga kura.
Kuelimisha wapiga kura kuhusu utaratibu wa uchaguzi.
Kuwashawishi watu kuwapigia kura.
Kuwapa nafasi wapiga kura kuwauliza maswali.
Umuhimu wa manifesto:
Kuonyesha mambo ya kufanywa na mgombea uchaguzi.
Rekodi ya ahadi kati ya mgombea uchaguzi na wapiga kura.
Mwongozo wa utekelezaji/ utendaji kazi kwa viongozi.
Inaonesha uwajibikaji wa kiongozi.
3
SIFA ZA KIONGOZI BORA
SHUGHULI
Katika makundi,
(a) Tajeni sifa za uongozi bora katika jamii.
(b) Elezeni manufaa ya uongozi bora katiak jamii.
4
13 Amani Amani
14 Petrol Petrol
15 Huruma Huruma
16 Subira Subira
NB:
Kwa sababu nomino hizi hasihesabiki, mara nyingi tunatumia maneno; kidogonanyingi kuonyesha
kiasi.
NO UDOGO WINGI
1 Mvua kidogo Mvua nyingi
2 Chumvi kidogo Chumvi nyingi
3 Kahawa kidogo Kahawa nyingi
4 Saruji kidogo Saruji nyingi
5 Asali kidogo Asali nyingi
6 Chai kidogo Chai nyingi
7 Sukari kidogo Sukari nyingi
8 Siagi kidogo Siagi nyingi
9 Furaha kidogo Furaha nyingi
10 Theluji kidogo Theluji nyingi
SHUGHULI:
Tunga sentensi tano kutokana na jedwali hili.
Kukanusha sentensi katika wakati ujao:
KUKUBALI KUKANUSHA
Chumvi itatanunuliwa kesho Chumvi haitanunuliwa kesho
Sukari itawekwa katika maziwa Sukari haitawekwa katika maziwa.
Mvua itanyesha jioni Mvua haitanyesha jioni
Kahawa itawekwa kwenye chai Kahawa haitawekwa kwenye chai
Asali itauzwa jijini Kampala Asali haitauzwa jijini Kampala.
5
FASIHI SIMULIZI: VITENDAWILI
Katika makundi,
(a) Tajeni vitendawili vitano vinavyojulikana sana katika jamii yenu.
(b) Elezeni utaratibu wa kufuata wakati wa kutega na kutegua vitendawili.
Mkondo wa 1
Mtegaji : Kitendawili! Kitendawili!
Msikilizaji: Tega!
Mtegaji: Nyumba yangu haina mlango.
Msikilazaji: Ni jiwe.
Mtegaji: Hapana, umekosea.
Msikilizaji: Ni yai.
Mtegaji: Ndiyo, umepata.
Mkondo wa 2:
Mtegaji : Kitendawili! Kitendawili!
Msikilizaji: Tega!
Mtegaji: Yeye ni mdogo lakini ni mkali.
Msikilazaji: Ni jiwe.
Mtegaji: Hapana, umekosea.
Msikilizaji: Ni mtoto.
Mtegaji: Hapana, umeshindwa. Nipe mji/ nchi.
Msikilizaji: Nimekupa nchi ya Kongo.
Mtegaji: Mimi nitasafiri kwa ndege hadi Kongo. Nikifika huko nitazungumza lugha ya
Lingala, nicheze muziki wa kilingala, nichimbe madini kisha nirudi hapa kwa ndege pamoja na
jibu.
Jibu: Pilipili
6
Mifano:
1. Nyumba yangu haina mlango. (yai)
2. Yeye ni mdogo lakini ni mkali. (pilipili)
3. Kamba yangu ni ndefu lakini haiwezi kufunga kuni. (njia)
4. Kuku wangu anatagia miibani. (miwani)
5. Yeye anajenga lakini hana mikono. (ndege)
7
20. Nina watoto wengi lakini nikimpiga mmojawapo wote Sahani (plates)
hulia. ( I have many children but whenever I beat one all
cry)
21. Nilianika mchele juani lakini kulipopambazuka sikuuona. Nyota ( stars)
(I spread rice in the sun to dry but at dawn I never saw it)
22. Nina mgeni nyumbani anayemaliza mafuta. ( I have a Koroboi ( a lamp)
visitor at home who finishes paraffin)
23. Mama, twendeni haraka nyumbani, miguu yake mirefu. Mvua ( Rain)
( Mummy, lets hurry home, his legs are long)
24. Ubwabwa wa mtoto mtamu. (It’s very sweet for children) Usingizi (sleep)
25. Pana visu vingi mkono mmoja tu. (There are very many Ndizi ( a banana bunch)
knives in one hand)
26. Mzazi ana miguu bali mzaliwa hana. (The parent has legs Kuku na yai ( A hen and an
but the child doesn’t have.) egg )
27. Mtoto wangu analia mwituni. (My child is crying in the Shoka (an axe)
forest)
28. Nina watoto wangu wanne ambao wanafukuzana lakini Magurudumu ( tyres)
hawakamatani. (I have four children running after each
otherbut can’t get each other)
29. Nina saa yangu ambayo haijawahi kusimama. ( I have a Moyo ( The heart)
clock that has never stopped)
30. Haukamatiki wala haushikiki. ( It cannot be touched) Moshi ( smoke)
31. Maiti anasema bali waliomchukuwa wamenyamaza. (The Mafiga na chungu
corpse is talking while the people carrying it are silent) (Cooking stones and a pot)
32. Nina wasichana wangu watatu, mmoja akiondoka wengine Mafiga (cooking stones)
hawafanyi kazi. (I have three girls but when one is missing
others can’t work)
33. Nina watoto wanne, lakini akiondoka mmoja wengine Matendeguu (Bed stands)
waliobaki hawawezi kufanya kazi
(I have four children but when one is not there, three can’t
work.)
Faida za vitendawili:
Kukuza ustadi wa kusema/ kuongea.
Husaidia kufikiri.
Ni chemsha bongo.
Huimarisha utamaduni.
Kupitisha muda.
Kupata msamiati.
Kupata maarifa kuhusu mazingira na utamaduni.
SHUGHULI
8
Katika makundi,
(a) Umewahi kupiga kura au kuona watu katika jamii yako wakipiga kura? Eleza utaratibu wa
kupiga kura kwa kuzingatia yafuatayo.
I0Ulinzi (askari)
Vifaa vya kupigia kura. (sanduku, meza, daftari la majina, viti, karatasi, vitabu, kura
zenyewe, kalamu)
Wasimamizi wa kupiga kura.
Uga wa kupigia kura.
Ulingo wa kuzuia watu wasisongamane.
Ofisi/ nyumba karibu.
Mifuko
MADA YA PILI
AFYA NA USAFI
Afya ni hali ya mtu kuwa na uzima bila ugonjwa. Usafi ni hali ya kutokuwa na uchafu.
MSAMIATI WA USAFI
SHUGHULI:
Katika makundi,
(a) Tajeni vifaa mnavyotumia kudumisha usafi pale nyumbani.
(b) Eleza umuhimu wa kudumisha usafi wa kibinafsi, nyumbani na katika jamii.
KIFAA CHA USAFI MATUMIZI YAKE
Wembe Kukata kucha ndefu, kunyoa
Ufagio Kufagia vumbi na takataka
Kitambaa Kufuta kamasi
Dodoki Kuoga mwili
Sabuni Kuoga na kunawa
Kifyekeo Kufyeka nyasi
Pipa Kutia takataka
9
Pasi Kunyosha nguo
Kitana Kuchana nywele
Dawa ya meno Kusafisha meno
Dawa ya viatu Kusafisha viatu.
Karatasi laini Hutumiwa msaalani
Beseni Kunawa, kuoga, kusafisha vyombo
Kioo Kujitazama ili kusafisha uso na mwili
Kabati Kutia vyombo
Jokofu Kutunza vyakula na vinywaji
Kichanja cha vyombo Kuwekea vyombo ili vikauke
10
SHUGHULI
Katika makundi,
(a) Tungeni sentensi mkitumia wa usafi ufuatao.
(i) Oga
(ii) Sugua meno.
(iii) Nawa mikono
(iv) Piga nguo pasi.
(v) Fyeka
MSAMIATI WA AFYA
SHUGHULI:
Katika makundi,
(a) Tajeni msamiati wa afya ambao mnaujua.
(b) Tungeni sentensi kumi mkitumia msamiati wa afya.
(c) Elezeni vifaa vitano vya afya na matumizi yake.
(d) Elezeni vitu vitatu ambavyo vinaweza kudhuru afya yako.
11
(c) Vifaa na matumizi
Kifaa cha afya Matumizi yake
Kipimajoto Hupima joto la mwili
Machela Kubebea wagonjwa
Gari la wagonjwa Kubeba wagonjwa mahututi
Kiti cha magurudumu Kiti cha mgonjwa mahututi.
Sindano Kuingiza dawa mwilini
Hudubini Kuchunguza vidudu vidogo
Stethoskopu Kusikiliza mapafu na mapigo ya moyo
Glavu Kuvaa mikononi ili kujilinda dhidi ya uchafu
Bendeji Kufungia mahali palipoteguka au chubuka
Uyoka Kuonea sehemu za ndani za mwili
Plasta Kufungia kidonda
12
Kiroboto
Funza
Mnyoo
13
Fagia nyumba
Fungua madirisha
Kichocho Usitembee majini bila viatu
Chemsha maji ya kunywa
Minyoo tumboni Chemsha maji ya kunywa
Usile chakula baridi au kilichooza
Siku ya Jumamosi na Jumapili Amos na Hilda hushirikiana na wazazi wao kufagia nyumba,
kufyeka nyasi zilizo karibu na nyumba. Pia wao hufunika mashimo yaliyo karibu na nyumba yao
ili mbu wasije wakazaliana humo. Baada ya shughuli hizo wao huosha nguo zao, shuka za
0vitanda vyao na mikoba ya kubebea vitabu. Amos na Hilda huoga kila siku, hunawa mikono
kabla yao kabla kula chakula na baada ya kutoka msaalani. Wao pia hupiga pasi nguo zao za
nyumbani na sare ya shule.
14
Maswali:
(a) Hilda na Amos wanaitanaje?
(b) Hilda ana miaka mingapi?
(c) Amos anasoma kidato cha ngapi?
(d) Amos hufanya usafi gani anapoamka kila asubuhi?
(e) Hilda akiamka hufanya nini kabla kwenda shuleni?
(f) Wanafunzi hufanya usafi gani asubuhi kabla kuingia darasani?
(g) Baada ya masomo Amos na Hilda huwasaidia wazazi kufanya nini?
(h) Taja usafi ambao Hilda na Amos hufanya wikendi?
(i) Kwa nini Amos na Hilda hufanya usafi?
15
Siku ya wanawake (tarehe 8 Kuandhimisha siku ya wanawake duniani
machi kila mwaka)
Siku ya shahidi wa Uganda ( Kuadhimisha siku ya mashahidi waliokufa kwa imani yao
tarehe 3 juni kila mwaka) yamkidini nchini uganda
16
UMUHIMU WA SHEREHE MBALIMBALI KATIKA JAMII
Shughuli
1. Elezeni sherehe zinazoffanyika kila mwaka katika jamii yako
2. Elezeni sherehe za kisasa na kitamaduni katika jamii yako
3. Tajeni mambo yanayotendeka kwenye sherehe na umuhimu wake
Sherehe za kila mwaka
17
Sherehe ya mwaka mpya, noeli/krismasi
Pasaka
Idi fitri
Idi adhuha
Siku ya uhuru
Siku ya wanawakes
Siku ya mashujaai
Siku ya mashahii waUganda
Sherehe za kisasa
Siku ya kupata uhuru
Siku ya mashujaa
Sherehe za kiutamaduni
Unyago
Jando
Kupewa jina
Matanga
Mazishi
Ndoa
Mambo yanayotendeka kwenye sherehe ni kama vile
Kucheza dansi/ngoma
Kucheza michezo
Kula na kunywa
Kuimba
Magwaride
Mahitaji ya maarusi kwa sherehe ya ndoa
Mavazi rasmi ya maarusi na pete
Keki ya sherehe
Wacheza ngoma
18
Vipaza sauti
Mahema
Vyakula/mapochopocho/vinywaji
Meza na viti
Magari
Wapampe
Wahudumu na wafanyakazi
Maigizo ya sherehe ya ndoa
Bwana arusi
Bibi arusi
Wapambe yaani mpambe wa bwana arusi na mpambe wa bibi arusi
Wacheza ngoma
Wageni
Wazee
Mfawidhi
Maelezo kuhusu maigizo ya ndoa
1. Elezeni tofauti za kufanya maigizo ya sherehe ya ndoa kwa imani tofauti za
kidini na kitamaduni.
Muvulana kutokamata msichana kiuononi au mkononi
Mvulana au msichana kutovaa mavazi ya mwenziwe yasiyomstahili
Imani za kishirikina
Maigizo kuhitilafiana na imani na maadili ya kitamaduni
2. Tajeni hisia zinazojitokeza wakati wa kufanya maigizo ya sherehe ya ndoa
Furaha
Aibu kwa kuvaa mavazi yasiyo ya kawaida
Fahari kwa kuhisi mtu ni bwana au bibi arusi
3. Ni maandalizi yapi yanayohotajika kwa maigizo ya sherehe ya ndoa
Mavazi/maleba ya maarusi
Viti/meza
Mkate/keki ya sherehe
Wapampe
Vyakula na vinywaji
Mpiga picha
19
4. Tumieni simu ya mwalimu tarakilishi na projekta kutazama picha na video za
sherehe ya ndoa
Tazama video na picha
NDOA NA MASHARTI YAKE
Riadhaa ya mwanamume ni mwanamke
Kutangaza ndoa katika makanisa na misikiti kabla ya kufunga ndoa yenyewe
Kulipa mahari
Kuwepo kwa mashahidi wakati wa kufunga ndoa
Maarusi wasiwe na uhusiano wa kiukoo
Maarusi wawe waliojiheshimu na mwenye kijihifadhi
Ridhaa ya wazazi
Sherehe ya kufunga ndoa ya kidini, kiserikali au kiutamaduni
Kutofanya mapenzi na mtu mwingine asiye mume wala mke wako
MADHARA YA KUSHIRIKI MAPENZI KABLA YA NDOA
Kuambukizwa magonjwa ya zinaa kama vile kaswende, kisonono, vidonda katika sehemu za siri
Kupata ugonjwa hatari wa ukimwi
Kupata ugonjwa wa saratani ya maini
20