You are on page 1of 30

MASWALI WALIYOULIZA VIJANA KUHUSU

Kitabu hiki kimetolewa katika mfululizo wa vitabu vidogo tisa vikiwa


na vichwa vya habari vifuatavyo:

NA MAJIBU YAKE
1. Kuingia Utu Uzima
Kitabu cha 6
2. Uhusiano kati ya Msichana na Mvulana
3. Uhusiano wa Kimwili
4. Mimba
5. Usalama katika Mapenzi
6. UKIMWI na Kizazi Kipya
7. Dawa za Kulevya
RAFIKI
8. Pombe na Sigara MWENYE ATAENDELEA
9. Haki za Uzazi UKIMWI KUWA RAFIKI
YANGU

ISBN 978 - 9987 - 449 - 60 - 6

Tanzanian German
Mkuki na Nyota Publishers Programme to Support
S. L. P. 4246 Health (TGPSH)
Kitabu hiki kimetayarishwa kwa kushirikisha
Dar es Salaam S. L. P. 65350
vijana wa Tanzania na TGPSH-GTZ
www.mkukinanyota.com Dar es Salaam
www.tgpsh.or.tz
Shukrani
Kimechapishwa na:
Tunapenda kuwashukuru vijana wote waliohusika katika kuandaa vijitabu hivi kwa
Mkuki na Nyota Publishers Ltd mchango mkubwa walioutoa. Hawa ni vijana balehe kutoka shule za msingi mbalimbali
S. L. P. 4246 za mikoa ya Lindi, Tanga na Dar es Salaam waliochangia kwa kuibua maswali ya awali,
Dar es Salaam waelimishaji rika wa vikundi kutoka Student Partnership Worlwide (SPW) na wa
UMATI ambao walipitia na kuchambua maswali ya awali pamoja na wanachuo wa Chuo
Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam kwa mchango wao wakati wa kufanya marekebisho ya
Pepe: contact@mkukinanyota.com pili ya hivi vitabu.
Tovuti: www.mkukinanyota.com
Vilele tunatoa shukrani nyingi kwa watu wote kutoka katika makundi yote ya jamii
ndani na nje ya Tanzania amabo walisoma vijitabu hivi, na wakatupa mrejesho, kutupa
moyo na kuuliza maswali ambayo yameongeza ubora wa nakala hii.
Kwa hisani ya Serikali ya Ujerumani
Shukrani ziwaendee walimu wote wakuu wa shule za msingi ambazo zilihusika kwa
msaada wao, na kwa Bwana Walter Mbunda na marehemu Elisha Kapinga (UMATI) na
pia kwa Bwana Yassin Ally wa SPW kwa uwezeshaji.

Tunapenda pia kuwashukuru Dkt. Elizabeth Mapella (MoHSW-RCHS), Bi Rehema


Mwateba na Bi Akwillina Mlay kwa ushauri wao wa kitaalamu katika masuala ya afya
ya uzazi kwa vijana. Dkt. Clemens Roll na Dkt. Suzanne Mouton (CCBRT) kwa ushauri
wa uganga. Shukrani kwa Bi Magret Kilembe na Bwana Simon Kilembe kwa kutafsiri,
Bwana Benedict Raymond na Bi Dorothea Coppard (wataalamu wa Elimu – Mradi wa
© Tanzanian German Programme to PASHA) na Cordula Schuemer (Mshauri wa Afya ya Uzazi-gtz) kwa ushauri wao mzuri
Support Health (TGPSH), 2007 na wa kujenga pamoja na Dkt. Zubeida Tumbo-Masaba ( Mtafiti Mwandamizi, Taasisi ya
Uchunguzi wa Kiswahili) na Kate Forester Kibuga pamoja na Karen Walker kwa kusoma
na kuhakiki.

Shukrani za pekee kwa Dkt. Regina Goergen (EvaPlan) siyo tu kwa moyo wake wa
ujasiri katika kuchochea maandalizi ya hivi vijitabu bali pia katika kusambaza wazo
hili, na kuwezesha vijitabu hivi kukubalika katika nchi 17 ulimwenguni. Vijitabu hivi
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) vimekuwa zana mwafaka kwa maana ya njia bora ya kufikisha habari kuhusu ujinsia na
afya ya uzazi kwa vijana.

Tunamshukuru mchoraji wa katuni Nd. David Chikoko kwa mchango wake mkubwa katika
kuchora vielelezo vilivyotumika katika mfululizo huu.

Kwa njia ya pekee tunapenda kuwashukuru Meja Jenerali (mstaafu) Herman Lupogo
(aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa TACAIDS) na Bi Rustica Tembele (TACAIDS) na
Dkt. Catherine Sanga (RCHS) kwa mchango wao endelevu katika kusambaza vijitabu
hivi na bila kusahau mashirika yote yaliyosaidia katika machapisho na usambazaji wa
vijitabu hivi kwa miaka yote hiyo.

ISBN 978 - 9987 - 449 - 60 - 6

Dkt. Axel Doerken


Haki zote za kunakili zimehifadhiwa.
Mkurugenzi GTZ Tanzania.
Yaliyomo:

Utangulizi............................................................................................. v
Je, kuna tofauti gani kati ya neno Virusi vya UKIMWI kwa
kifupi VVU na UKIMWI?.................................................................1
Kinga ya mwili ni nini?........................................................................2
Nini kinatokea wakati Virusi vya UKIMWI (VVU) vinapoingia
mwilini na vinakwenda wapi katika sehemu ya mwili?.................2
Je, inachukua muda gani tangu mtu aambukizwe na VVU hadi
vionekane kwenye damu?..................................................................3
Je, watu wote wenye virusi vya UKIMWI watapata
UKIMWI? Na kama ndiyo, itachukua muda gani?......................3
Je, mtu mwenye kuonekana na afya nzuri, anaweza kuwa na
virusi vya UKIMWI?.........................................................................4
Je, ni tabia zipi zinazochangia kuenea kwa virusi vya
UKIMWI?............................................................................................5
Je, mwanaume akitoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga
shahawa anaweza kuambukizwa yeye au mwanamke na
Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?................................................6
Je, nikijamiiana na mtu mwenye virusi vya UKIMWI
bila kutumia kondomu, nitapata virusi vya UKIMWI na
UKIMWI?............................................................................................6
Je, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI vinaambukiza kwa
kujamiiana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni ?..7
Kunyonyana ulimi kunaweza kuchangia kupata virusi vya
UKIMWI?............................................................................................7
Je, nitaweza kupata virusi vya UKIMWI na UKIMWI
nikijamiiana na msichana au mvulana wa umri mdogo sana?.....8


Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa wanapata
maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?....................9
Je, mtu anaweza kuambukizwa virusi vya UKIMWI na
UKIMWI iwapo atavaliana nguo na mtu mwenye Virusi vya
UKIMWI na UKIMWI?.................................................................. 10
Nikitumia nyembe kali au sindano pamoja na mtu mwenye
Virusi vya UKIMWI ninaweza kupata Virusi vya UKIMWI
na UKIMWI?..................................................................................... 10
Je, ninaweza kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na
UKIMWI kwa kuumwa na mbu?.....................................................11
Je, nikila na mtu mwenye Virusi vya UKIMWI,
nitaambukizwa na virusi vya UKIMWI na UKIMWI?..............11
Je, nikitoa au kupata damu hospitalini, itakuwepo hatari
ya kupata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?............................ 12
Mama mwenye virusi vya UKIMWI na UKIMWI, anaweza
kuzaa mtoto? Na anaweza kumwambukiza mtoto aliye
tumboni au wakati wa kumnyonyesha?........................................ 12
Ni asilimia ipi ya Watanzani ambao wameambukizwa na
Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?.............................................. 13
Hali ya maambukizi ya VVU Tanzania kimkoa............................ 14
Je, nifanye nini ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya
UKIMWI na UKIMWI?.................................................................. 14
Je, ni kweli kwamba kufanya ngono na bikira inaponyesha
maambukizi........................................................................................ 16
Nifanye nini ili kujua kama nina au sina maambukizi ya
Virusi vya UKIMWI?....................................................................... 16
Niende wapi kupima kama nina Virusi vya UKIMWI?............. 17

ii
Je, nikiambukizwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI
nifanye nini?...................................................................................... 18
Je, matokeo ya kupima na kukutwa huna virusi vya Ukimwi
ni yapi?................................................................................................ 19
Je , vipimo vya Virusi vya UKIMWI vinasema ukweli?........... 20
Je,niwasiliane na niishi vipi na watu wanaoishi na virusi vya
UKIMWI na UKIMWI?................................................................. 20
Ni tahadhari gani nichukue ninapomhudumia mgonjwa wa
UKIMWI?.......................................................................................... 21

iii
iv
Utangulizi

Vijana wa enzi hii wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo


za kiafya, kijamii na za kiuchumi. Changamoto nyingi za
kiafya zinaathiri urefu na ubora wa maisha yao ya utu uzima.
Ulimwenguni kote, vijana wengi wako hatarini kushiriki ngono
zisizo salama, ambazo zinaweza kuwaambukiza magonjwa
yatokanayo na kujamiiana. Takwimu za utafiti wa 2003-04
kuhusu vidokezo vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWi
Tanzania (Tanzania HIV/AIDS Indicator Survey) umebaini
kuwa 3.5% ya vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 na 2% ya
vijana wenye umri wa miaka 15-19 kuwa na maabukizo ya VVU.
Utafiti huo pia umebaini kuwa ukosefu wa elimu ya kutosha
juu ya uhusiano wa kimwili na jinsi VVU vinaelezwa kuwa ni
mojawapo ya sababu zinazochangia kuwepo na tatizo hili. Kwa
wale vijana kati ya miaka 15-19, ni wasichana 40% na wavulana
43% ambao wana elimu ya kutosha juu ya VVU, wakati vijana
wenye umri wa miaka 20-24 nusu yao ndiyo wenye elimu sahihi
juu ya VVU.
Kijitabu hiki kimetayarishwa kwa ajili ya kuwapa vijana taarifa
muhimu juu ya VVU na UKIMWI. Bila elimu ya kutosha, vijana
wanapotoshwa kwa urahisi na hawawezi kufanya maamuzi
sahihi. Halafu inakuwa rahisi kwao kupata maambukizo ya VVU
na kuishia kuteseka na madhara yake mengi.
Watu wengi wanafikiria kuwa elimu juu ya mambo haya haswa
katika umri mdogo inahimiza tabia ya kutowajibika, lakini
kumbe hii ni kinyume cha fikra hizo. Uzoefu umeonyesha wazi
kuwa vijana wakipata taarifa huchagua mwenendo salama.
Maswali yaliyomo kwenye kijitabu hiki yalikusanywa kati
ya mwaka 2000 – 2006 kutoka kwa wanafunzi wa shule za
msingi, sekondari na chuo kikuu. Vijana hawa walitokea mikoa
tofauti hapa Tanzania na umri wao ni kati ya miaka 11 hadi
24. Kijitabu hiki kimetayarishwa na jopo la wataalamu wa
fani mbalimbali walio kwenye sayansi ya jamii, afya na elimu.


Vijana walihusishwa katika hatua zote za kukitayarisha. Kwa
njia ya kuchapisha kijitabu hiki, tunategemea tumechangia
kuinua uelewa ambao utawajengea vijana tabia ya kuwajibika
katika maswala ya uhusiano ya kimwili yasiyokuwa na matokeo
mbadala. Kumbuka haya ni juu ya mwili wako na maisha yako
kwa hiyo yathibiti kwa kuyasimamia. Kwa vijana wa Tanzania,
chukueni hii kama changamoto. Taarifa inawezesha. Tumia
uwezo huu kujenga maisha yako ya baadaye. Katika mapambano
dhidi ya maambukizo ya VVU, kila mmoja wetu ana nafasi yake
ya utendaji. Kwa asilimia kubwa VVU haiji kwako bali ni wewe
unaifuata na kujiambukiza. Tunawapa wote changamoto katika
kuwajibika na kuhimili maisha yako.

Dkt. Fatma Mrisho


Mwenyekiti Mtendaji Tume ya Kudhibiti
UKIMWI Tanzania (TACAIDS)

vi
Je, kuna tofauti gani kati ya neno Virusi vya
UKIMWI kwa kifupi VVU na UKIMWI?

Neno VVU ni virusi au vijidudu vinavyosababisha ugonjwa


wa UKIMWI. Neno hili kwa lugha ya Kiingereza ni HIV yaani
“Human Immunodeficiency Virus”. UKIMWI ni kifupi cha
maneno matatu ambayo ni Upungufu wa Kinga Mwilini. Kwa
Kiingereza jina la UKIMWI AIDS ambacho kirefu chake ni
“Acquired Immune Deficiency Syndrome”. Neno UKIMWI
tayari linaonyesha tayari aina ya ugonjwa, ikiimanisha kuwa
mwili umepungua uwezo wake wa kinga kwa maradhi mbalimbali
mwilini. Dalili za upungufu huu ukianza kujitokeza basi maradhi
haya huitwa UKIMWI.
Tofauti kati ya VVU na UKIMWI ni kuwa mtu aliyeambukizwa
VVU bado anaweza kuonekana mzima wa afya. Pamoja na kuwa
virusi hivyo vitaonenekana katika damu yake, ni kwamba virusi
hivyo vitakuwa havijaanza bado kushambulia chembechembe
nyeupe za damu. Kwa upande mwingine kinga ya mwili ya mtu
anayeumwa UKIMWI itakuwa tayari imepungua. Mwili wake


utaanza kuugua magonjwa nyemelezi. Magonjwa nyemelezi
hupata nafasi ya kushambulia mwili huu ambao tayari kinga
imepungua. Watu wnaoumwa UKIMWI wanaweza kupungua
uzito wa mwili, kuharisha au kupata matatizo ya ngozi. Hata
hivyo maradhi haya siyo lazima yatokane na kuwa na VVU. Ili
kuwa na uhakika, onana na mtaalamu yaani dakatari wako.

Kinga ya mwili ni nini?

Kinga ya mwili ni mpangilio wa mwili kujikinga na maradhi. Chem-


bechembe nyeupe zilizopo katika damu ya mwili mzima wa bi-
nadamu zina kazi maalum
katika kuhakikisha kinga
ya mwili ipo. Kama aska-
ri jeshi wanaolinda nchi
yao, chembechembe hizo
kwa pamoja zinalinda
mwili dhidi ya magonjwa.
Hivyo, kama chembeche-
mbe hizo zikishambuliwa,
mwili hauwezi kujikinga
na maradhi au magonjwa.

Nini kinatokea wakati Virusi vya UKIMWI


(VVU) vinapoingia mwilini na vinakwenda wapi
katika sehemu ya mwili?

Virusi hivi vinakaa katika chembechembe nyeupe zilizopo kwenye


majimaji ya mwili wa binadamu hasa kwenye damu, shahawa
na maji maji ya ukeni na maziwa ya mama anayenyonyesha.
Ndani ya chembechembe nyeupe ndiyo mahali virusi vinakaa na
kuendelea kuzaliana. Vikiwa ndani ya chembechembe nyeupe hizi,
virusi huendelea kuzaliana hadi kusababisha chembechembe


nyeupe hizi kupasuka. Virusi hivi hupata nafasi ya kuendelea
kushambulia chembechembe nyingine nyeupe za damu. Kwa
kadri chembechembe nyeupe zilizoshambuliwa zinavyoendelea
kupasuka ni kwa kiwango hicho hicho chembechembe nyeupe
zinaendelea kuharibiwa na kupungua. Matokeo yake ni kupungua
kwa kinga mwilini na mtu kuendelea kudhoofika.

Je, inachukua muda gani tangu mtu aambukizwe


na VVU hadi vionekane kwenye damu?

Inakadiriwa huchukua miezi mitatu tangu kuambukizwa na VVU


hadi virusi hivyo vio-
nekane kwenye damu.
Itakuwa kazi bure ku-
kimbilia kwenda kupi-
ma VVU mara tu baa-
da ya kufanya ngono
isiyo salama. Inabidi
kusubiri miezi mitatu
kabla ya kwenda kwe-
nye Ushauri Nasihi na
Upimaji wa Hiari.

Je, watu wote wenye virusi vya UKIMWI


watapata UKIMWI? Na kama ndiyo, itachukua
muda gani?

Ndiyo, baada ya muda fulani karibia watu wote wenye


maambukizi ya Virusi vya UKIMWI wataanza kuugua UKIMWI.
Lakini muda kati ya kuambukizwa na kuanza kuugua UKIMWI
unatofautiana. Wengine wanaishi muda mrefu. Kwa wastani
watu wazee wazima wanaendelea kuishi miaka kumi kabla ya


kupata dalili za awali. Watoto wanaopata virusi kabla ya umri
wa miaka mitano kwa wastani wanendelea kuishi mwaka moja
hadi mitatu.
Hakuna jibu la ujumla ni miaka mingapi ataishi tena mtu
aliyeambukizwa na virusi vya UKIMWI. Idadi ya miaka ya
kuishi baada ya kuambukizwa inategemea vitu vingi, kinga
asilia inayomkinga mtu, hali ya lishe ya mtu, wakati muafaka na
usahihi katika kutibu magonjwa nyemelezi na wakati muafaka
na usahihi wa kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI
kwa Kiingereza Anti-Retro-Viral drugs (ARVS )

Je, mtu mwenye kuonekana na afya nzuri,


anaweza kuwa na virusi vya UKIMWI?

Ndiyo, mtu anayeonekana na afya nzuri anaweza kuwa na virusi


vya UKIMWI. Katika hatua ya mwanzo baada ya kuambukizwa
mtu anakuwa na virusi vya UKIMWI kwenye damu lakini
haonyeshi dalili zozote za kuumwa. Hatua hii inaweza kuchukua
zaidi ya miaka kumi! Hii ni hatari sana, kwa sababu kama
unajamiiana na mtu mwenye kuonekana na afya nzuri, lakini
ndani ya mwili tayari anavyo virusi vya UKIMWI, anaweza
kukuambukiza.
Njia pekee ya kuwa na uhakika
kama mtu ameambukizwa na
VVU au la ni kwa njia ya kupima
damu katika Vituo maalamu vya
kupima au hosipitalini. Kwa hiyo,
kujamiiana bila kujikinga kwa
kutumia kondomu inawezekana
kuhatarisha maisha yako, hata
kama mpenzi wako ni mtu mwenye
kuonekana na afya nzuri.


Je, ni tabia zipi zinazochangia kuenea kwa
virusi vya UKIMWI?

Virusi vya UKIMWI kwa kiasi kikubwa vinaenea kwa njia ya


kujamiiana. Kama mtu ana wapenzi wengi wa kufanya ngono,
uwezekano wa kupata maambukizi unaongezeka,. Hi ni kwa
sababau kila mpenzi anaweza kuwa chanzo cha maambukizi
endapo watashiriki ngono za aina yeyote (ukeni au sehemu ya
haja kubwa) bila kutumia kondomu.
Pia kuchelewa kutibu magonjwa mengine ya zinaa, inachangia
kuenea kwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kwa mfano, kama
mtu anaugua ugonjwa wa zinaa, vijidudu vya UKIMWI vinaweza
kuingia mwilini kwa urahisi zaidi kwa sababu ya vidonda sehemu
zake za siri.
Mwisho, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na ulevi wa pombe
wa kupindukia yanaweza kuchangia kufanya maamuzi yasiyo
sahihi katika matendo ya ngono.


Je, mwanaume akitoa uume nje ya uke kabla
ya kumwaga shahawa anaweza kuambukizwa
yeye au mwanamke na Virusi vya UKIMWI na
UKIMWI?

Ndiyo, hata akitoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga mbegu


anaweza akaambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Ni hatari kwa mwanamke na pia kwa mwanaume, kwa sababu
vijidudu vimo ndani ya majimaji ukeni na uumeni. Hasa kama
mmoja kati ya wapenzi ana vidonda au michubuko midogo
sehemu za siri, Virusi vya UKIMWI. huingia kwa urahisi.
Kutoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga shahawa siyo njia
salama ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Je, nikijamiiana na mtu mwenye virusi vya


UKIMWI bila kutumia kondomu, nitapata virusi
vya UKIMWI na UKIMWI?

Uwezekano wa kuambukizwa
na Virusi vya UKIMWI na
UKIMWI ukijamiiana na mtu
mwenye virusi vya UKIMWI bila
kutumia kondomu ni mkubwa.
Mpaka leo, kondomu ni njia pekee
ya kuzuia kuambukizwaVirusi
vya UKIMWI na UKIMWI
wakati wa kujamiiana. Kama
kondomu inatumiwa ipasavyo
na kila unapojamiiana na mtu
mwenye virusi vya UKIMWI,
uwezekano wa kuambukizwa ni mdogo sana. Kutumia kondomu
ipasavyo ina maana kutumia kondomu mpya, kuivaa vizuri uumeni
na kuitoa kabla ya uume kulegea.


Je, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI
vinaambukiza kwa kujamiiana kwa njia ya
sehemu ya haja kubwa au mdomoni?

Ndiyo, kuna hatari kubwa ya kuambukizwa Virusi vya UKIMWI


na UKIMWI wakati wa kujamiiana kwa njia ya sehemu ya haja
kubwa au mdomoni.
Ngozi ya ndani ya sehemu ya haja kubwa ni laini sana na
uwezekano wa kupata michubuko wakati wa kujamiiana ni mkubwa,
kwa sababu hakuna majimaji kama ukeni yanoyorahisisha uume
kuingia. Kwahiyo virusi vya UKIMWI ni rahisi sana kuingia
mwilini mwa mwanamke kupitia kwenye michubuko hii..
Pia ngono kwa njia ya mdomoni ( „kula koni, chumvi chumvi ,
kulamba ukeni) hatari sana kama mwanamke ana vidonda au
michubuko mdomoni na mwanaume au vidonda au michubuko
uumeni, wanaweza kuambukizana.
Watu wote wanashauriwa kutumia kondomu ili kuzuia
maambukizi.

Kunyonyana ulimi kunaweza kuchangia kupata


virusi vya UKIMWI?

Uwezekano wa kuambukizwa virusi vya UKIMWI kwa


kunyonyana ndimi ni mdogo sana. Kwa kubadilishana mate
wakati wa kubusiana tu, haiwezekani maambukizi ya virusi vya
UKIMWI kutokea. Lakini kama mmoja kati ya wapenzi ana
vidonda / michubuko mdomoni, uwezekano wa kuambukizana
huongezeka.


Je, nitaweza kupata virusi vya UKIMWI na
UKIMWI nikijamiiana na msichana au mvulana
wa umri mdogo sana?

Ndiyo, utaweza kuvipata virusi vya UKIMWI. Uwezekano


wa kuambukizwa hautegemei umri wa mpenzi wako, lakini
unategemea afya yake! Kama huyu msichana au mvulana tayari
ameshapata virusi vya UKIMWI na unajamiiana naye utaweza
kuambukizwa.
Mara nyingi huwezi kufahamu kama mtu ana virusi vya UKIMWI
au hapana, kwa sababu katika hatua ya mwanzo baada ya
kuambukizwa hakuna dalili zozote za kuugua.
Vilevile ni tabia mbaya sana kushawishi wasichana au wavulana
wadogo kujamiiana. Kwa usalama na faida ya wote, mnashauriwa
kuacha mapenzi na wasichana au wavulana wadogo.

Lakini huyu msichana alikuwa


mdogo sana, na nilifikiri
alikuwa bikira


Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa
wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI
na UKIMWI?

Kuna sababu kuu mbili kwa wana ndoa kupata maambukizi ya


Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Kwanza, inawezekana kuwa mmoja kati yao alikuwa tayari na
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kabla ya siku ya kuoana.
Kwani hata mtu aliyeambukizwa na Virusi vya UKIMWI
anaweza kuonekana mwenye afya nzuri na kuwa navyo mwilini
siku ya harusi. Hii ni pale ambapo awali alifanya ngono na mtu
aliyeambukizwa Virusi ama alivipata kwa kupitia njia nyingine
kwa mfano, njia ya damu isiyo salama..
Kama mtu aliwahi kufanya ngono kabla, njia pekee ya kuhakikisha
kuwa hana virusi kabla ya kufunga ndoa ni kwenda kupima
damu.
Pili, wanandoa hao wanaweza kuambukizwa baada ya kufunga
ndoa, pale ambapo mwenzi mmoja atafanya mapenzi na mtu


mwingine. Kama mmoja wao au wote wawili watafanya ngono
na mpenzi mwingine (mahusiano nje ya ndoa) wanaweza kupata
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Je, mtu anaweza kuambukizwa virusi vya


UKIMWI na UKIMWI iwapo atavaliana nguo na
mtu mwenye Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Hapana, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI hauambukizwi


kwa kuvaliana nguo na mgonjwa, kwa sababu vijidudu vya
UKIMWI vinakufa baada ya muda mfupi vikiwa hewani. Hata
hivyo, kufuatana na kanuni za usafi, ni vizuri zaidi kuvaa nguo
zilizofuliwa na kupigwa pasi.

Nikitumia nyembe kali au sindano pamoja na


mtu mwenye Virusi vya UKIMWI ninaweza
kupata Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Ndiyo, unaweza kuambukizwa ukitumia nyembe kali au sindano


kwa kuchangia pamoja na mtu mwenye virusi vya UKIMWI.
Matumizi ya vyombo vyenye makali, kama sindano, visu au
nyembe yana hatari. Kama baada ya kutumika damu husalia
katika vyombo hivi, na endapo vitatumika bila kutakaswa au
kuchemshwa, matumizi yake yanaweza kusababisha maambukizi
ya magonjwa mbalimbali, pamoja na UKIMWI.
Kwa hiyo ni muhimu sana kutochangia vifaa vyenye makali na
watu wengine au lazima kuvitakasa na kuchemsha kila baada ya
kuvitumia.

10
Je, ninaweza kuambukizwa na Virusi vya
UKIMWI na UKIMWI kwa kuumwa na mbu?

Hapana, mbu na wadudu wengine hawawezi kukuambukiza


virusi vya UKIMWI kutokana na mfumo wa miili yao. Virusi
vya UKIMWI haviwezi kuishi kwenye miili yao, kwa sababu
siyo mazingira vinavyoyapenda. Virusi vya UKIMWI vinajilisha
na kuzaliana katika chembechembe nyeupe za damu, lakini
chembechembe za aina hii hazipo katika mwili wa mbu. Kwa
hiyo, virusi vya UKIMWI vinakufa mara baada ya mbu kufyonza
damu na aking‘ata mtu mwingine baadaye hakuna hatari ya
kuambukizwa.
Thibitisho jingine la ukweli huu ni kwamba sisi sote tungekuwa
tumebeba virusi vya UKIMWI kama mbu angelikuwa
anaambukiza kwa sababu sisi sote tunaishi katika mazingira
yenye mbu na karibu na watu wengine.

Je, nikila na mtu mwenye Virusi vya UKIMWI,


nitaambukizwa na virusi vya UKIMWI na
UKIMWI?

11
Hapana, ukila na mtu mwenyemaambukizi ya Virusi vya UKIMWI
huwezi kuambukizwa Virusi vya UKIMWI wala UKIMWI,
isipokuwa pale ambapo wote wawili mna vidonda mdomoni na
mnachangia kijiko kimoja. Lakini uwezekano huu ni mdogo
sana, kiasi tunachoweza kusema kwamba huwezi kuambukizwa
Virusi vya UKIMWI na UKIMWI ukila sahani moja na mtu
aliyeambukizwa na virusi.
Lakini, kufuatana na kanuni za afya, ni vizuri zaidi kila mtu
atumie vifaa vyake na baada ya kuvitumia avioshe kikamilifu.

Je, nikitoa au kupata damu hospitalini,


itakuwepo hatari ya kupata virusi vya UKIMWI
na UKIMWI?

Katika swali hili lazima tutofautishe kati ya kutoa damu na


kuwekewa damu. Kutoa damu hakuleti hatari, kama mtaalamu
wa afya aliyechoma sindano kwa ajili ya kutoa damu anatumia
sindano na vifaa vilivyochemshwa.
Kwa kawaida hakuna matatizo kuongezwa damu, kwa sababu
damu inapimwa kabla ya kumuongeza mgonjwa hospitalini.
Iwapo damu imepimwa na sindano zilizochemshwa zimetumika
hakuna ubaya wowote katika kuongezwa damu.

Mama mwenye virusi vya UKIMWI na


UKIMWI, anaweza kuzaa mtoto? Na anaweza
kumwambukiza mtoto aliye tumboni au wakati
wa kumnyonyesha?

Ndiyo, mama mwenye virusi vya UKIMWI na UKIMWI anaweza


kubeba mimba kama mwanamke mwingine yeyote. Ila ni muhimu
kukumbuka kwamba kuna uwezekano wa mtoto kuambukizwa na
Virusi vya UKIMWI.

12
Lakini siyo watoto wote waliozaliwa na
mama mwenye maambukizi watabeba
virusi. Kuwa moto ataambukizwa au
Natumaini hataambukizwa itategemea na idadi
sitapata VVU
ya virusi ambavyo viko kwenye damu
ya mama na sababu nyingine. Tafiti
zimeonyesha kwamba watoto wawili
kati ya watoto watatu waliozaliwa
na akina mama wenye maambukizi ya
Virusi huambukizwa na hivyo virusi.
Pamoja na hayo, mama mwenye
virusi vya UKIMWI anaweza kum-
wambukiza mtoto wake wakati wa
kumnyoshesha kwa sababu ya kuwe-
po virusi kwenye maziwa ya mama.
Akina mama walio na maambukizi ya
UKIMWI na UKIMWI wanashauriwa kuacha kuzaa na kutumia
njia za uzazi wa mpango.

Ni asilimia ipi ya Watanzani ambao


wameambukizwa na Virusi vya UKIMWI na
UKIMWI?

Nchini Tanzania ni 7% ya watu wenye umri kati ya miaka 15-49


wana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Hii inamaanisha kuwa
kati ya watu 100 wa umri huu 7 wao wameambukizwa na Virusi
vya UKIMWI.
Kila mkoa una watu walioambukizwa kwa kiwango tofauti, mikoa
mingine ikiwa na kiwango cha juu . Jedwali lilioambatanishwa
hapa linaonyesha Mkoa wa Mbeya, Iringa na Dar es Salaam
kuathirika zaidi na idadi kubwa ya watu waliopima na kuonekana
kuwa na virusi vya UKIMWI.

13
Hali ya maambukizi ya VVU Tanzania kimkoa

Mkoa Asilimia
1. Mbeya 13,5
2. Iringa 13,4
3. Dar es Salaam 10,9
4. Mtwara 7,4
5. Pwani 7,3
6. Kilimanjaro 7,3
7. Mwanza 7,2
8. Tabora 7,2
9. Ruvuma 6,8
10.Shinyanga 6,5
11.Rukwa 6,0
12.Tanga 5,7
13.Morogoro 5,4
14.Arusha 5,3
15.Dodoma 4,9
16.Kagera 3,7
17.Lindi 3,6
18.Mara 3,5
19.Singida 3,2
20.Manyara 2,0
21.Kigoma 2,0
Chanzo: TACAIDS:HIV/AIDS Indicator Survey, Tanzania 2003-2004, Ukurasa 76

Kwa ujumla ni kwamba maambukizi yamezidi mijini au sehemu


zenye biashara. Wengi walioathirika ni vijana.

Je, nifanye nini ili kujikinga na maambukizi ya


virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Hakuna chanjo dhidi ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI


na UKIMWI, Lakini kuna mienendo ya tabia ambayo itaweza

14
mpenzi
Kuwa na
m m o ja Acha
ifu
a mwamin kutembea
ua Zina peku
I una Ac
ha
IMW
UK

kukusaidia kujikinga na maambukizi ya UKIMWI na UKIMWI.


Kutokufanya ngono kabisa ni njia mojawapo ya kujikinga na
maambukizi ya UKIMWI na UKIMWI. Kuwa mwaminifu na
kuwa na mpenzi ambaye hajaambukizwa ni njia nyingine ya
kujikinga. Lakini hii inahitaji wote muwe katika afya nzuri (
bila maambukizi) wakati mnaanza uhusiano wa kujamiiana kwa
mara ya kwanza.
Pia inashauriwa hima kutafuta matibabu ya magonjwa ya ngono
mara pale yatakapojitokeza. Vidonda vinavyosababishwa na
magonjwa ya ngono vinasababisha mwingiliano wa maji maji ya
ukeni, maji maji ya uumeni na damu wakati wa kujamiiana na
kuwezesha Virusi vya UKIMWI kupita kwa urahisi.
Kufuata kanuni za ngono salama ni njia nyingine ya kujikinga
ili usiambukizwe na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Ngono

15
salama kwa upande mwingine ni kitendo cha kukaribiana ambacho
hakitahusisha uume kuingia ukeni au njia ya haja kubwa. Pia
utumiaji wa kondomu kila wakati ngono itahusisha kuingizwa
kwa umme, ukeni au njia ya haja kubwa ni njia nyingine ya
kujikinga

Je, ni kweli kwamba kufanya ngono na bikira


inaponyesha maambukizi?

Hapana, huwezi kupona Virusi vya UKIMWI au UKIMWI kwa


kufanya ngono na bikira. Hakuna tiba ya maambukizi ya Virusi
vya UKIMWI!
Pamoja na hayo, kama utakuwa na maambukizi ya magonjwa ya
ngono, utaweka afya ya huyo bikira katika hatari kama ngono
hiyo itafanyika bila kinga.

Nifanye nini ili kujua kama nina au sina


maambukizi ya Virusi vya UKIMWI?

Ipo njia moja ya kuhakikisha kama umeambukizwa Virusi vya

Twende tukapime

Kituo cha Ushauri na Unasihi

16
UKIMWI na UKIMWI au hapana. Njia hii ni ya kupima damu
yako katika vituo vyenye utaalamu wa upimaji.
Ni muhimu kukumbuka kuwa Virusi vya UKIMWI, vinaonekana
kwenye damu ya binadamu miezi mitatu baada ya kuambukizwa.
Kipindi hiki kati ya kuambukizwa hadi kufikia miezi mitatu kipimo
hiki hakiwezi kuonyesha kama maambukizi ya virusi yapo au
hayapo. Kipindi hiki ni cha hatari sana , kwani aliyeambukizwa
anaweza kuwaambukiza wengine bila kujua.

Niende wapi kupima kama nina Virusi vya


UKIMWI?

Vituo vyenye utaalamu na katika hospitali au Taasisis kama


vile Shirika la Amref au CCBRT wana uwezo wa kutoa ushauri
nasaha na vipimo vya kuaminika. Ushauri nasaha unakusaidia
wewe kuelewa kipimo hicho ni cha nini, ni majibu gani yanayoweza
kupatikana au kutopatikana. Upimaji huu hufanywa kwa siri, ni
wewe tu pekee yako unaweza kupewa majibu. Katika miji mingi,
vituo vya ANGAZA vipo na pia vituo hivi hutoa huduma rafiki
kwa vijana.
Huduma za upimaji hazipatikani kwa urahisi sehemu za vijijini

17
kwa sababu vyombo vinavyotumika katika upimaji ni vya gharama
kubwa na vinahitaji umeme na uangalizi mkubwa. Mpaka sasa
huduma hizi zinapatikana katika hospitali na kwa baadhi ya
mashirika yanayojishughulisha na maambukizi ya Virusi vya
UKIMWI na UKIMWI.
Jambo nzuri ni wewe kuuliza habari zaidi katika kituo cha afya
kilicho karibu nawe.

Je, nikiambukizwa virusi vya UKIMWI na


UKIMWI nifanye nini?

Jambo la msingi ni kutokukata tamaa na kuwa na matumaini.


Mara nyingine inasaidia kama utakuwa na mazungumzo na watu
ambao tayari wanaishi na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI
au marafiki na ndugu unaowaamini. Jaribu kuongea na mwenzi
wako ili kumfahamisha juu ya hali yako ya maambukizi. Yeye pia
anaweza kuwa ameambukizwa na angependa kupima. Ni muhimu

BADILI
TABIA
UKIMWI sina

18
kuzingatia kanuni muhimu za afya nzuri kama vile kula vyakula
vyenye mlo kamili na kujiweka katika hali ya usafi. Kwa mantiki
hiyo hiyo ni lazima kuharakisha kutibu maradhi mengine
yatakayojitokeza. Watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI
wanashauriwa wasitumie pombe wala kuvuta sigara, kwa
sababu vyote hivyo huchangia katika kudhoofisha mwili. Kama
watafanya ngono, ni lazima watumie kondomu ili wasiambukize
wengine.
Aliyeambukizwa, baada ya miaka kinga ya mwili wake itaanza
kupungua na atatakiwa kupata dawa za kupunguza makali ya
UKIMWI (ART).
Kama mtu aliyeambukizwa na virusi vya UKIMWI atazingatia
masharti haya, kuna uwezekano wa kuishi na kufurahia maisha
kwa miaka mingi.

Je, matokeo ya kupima na kukutwa huna virusi vya


Ukimwi ni yapi?
Kwa kawaida mtu anapoamua kwenda kupima mara nyingi
anakuwa na sababu za kumfanya ahisi kuwa au kutokuwa na
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI. Kwa hiyo mtu akipata jibu
kuwa hana maambukizi ya Virusi vya UKIMWI, itabidi ajiulize
huo wasiwasi ulitokea wapi.
Pale mtu anapojua ni kitu gani kilimfanya aende kupima, ni
vyema mtu huyo kukaa mbali / kuacha kurudia hilo jambo au
tabia iliyomweka katika hatari ya kupata maambukizi ya Virusi
vya UKIMWI na UKIMWI. Kwa mfano, kama alifanya ngono na
mtu zaidi ya mmoja na kwa nyakati zote hakutumia kondomu.
Baada ya kupima, mtu huyu anatakiwa aache tabia ya kuwa na
wapenzi wengi na pia awe anatumia kondomu kujikinga dhidi ya
maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Ni muhimu
kuchukua tahadhari zote ili kujikinga na maambukizi ya Virusi
na UKIMWI na UKIMWI.

19
Je , vipimo vya Virusi vya UKIMWI vinasema
ukweli?

Uwezekano wa kupata majibu ya uwongo ni mdogo sana,


isipokuwa tu kama vipimo vitafanyika kipindi chini ya miezi
mitatu baada ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na
UKIMWI kukupata. Hata kama vipimo vilivyofanyika ni vya
kuaminika, itabidi uende kupima mara ya pili, kama una wasiwasi
na matokeo ya hicho kipimo.

Je,niwasiliane na niishi vipi na watu wanaoishi


na virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Mtu anayeishi na virusi vya UKIMWI na UKIMWI anahitaji


ushauri na mara pale atakapohisi unamjali ( unamheshimu)
na kumjali, uzito wa ugonjwa unakuwa mwepesi. Mtu mwenye
UKIMWI ni mgonjwa kama wagonjwa wengine, isipokuwa
anahitaji faraja zaidi kwa sababu
ugonjwa wake hauna tiba.
Matunzo sahihi kwa watu
wanaoishi na Virusi vya UKIMWI
na UKIMWI ni muhimu, Mtu
RAFIKI
ATAENDELEA anayeishi na Virusi vya UKIMWI
MWENUE
UKIMWI KUWA RAFIKI apate lishe bora ili aweze
YANGU
kuimarisha afya yake na awe
msafi wa mwili, nguo, nyumba na
vyakula. Pia apatiwe matibabu
haraka na kwa ukamilifu kwa
maradhi yote yatakayojitokeza
na asaidiwe kufanya kazi nzito.
Mtu anayeishi na Virusi vya
UKIMWI na UKIMWI ana haki
za binadamu kama binadamu

20
wengine. Kumbuka kwamba rafiki au ndugu yako mwenye Virusi
vya UKIMWI na UKIMWI bado ni rafiki au ndugu yako!

Ni tahadhari gani nichukue ninapomhudumia


mgonjwa wa UKIMWI?

Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI mara nyingi huenea sana


kwa njia ya kujamiiana, na hauambukizwi kwa kumhudumia
mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya UKIMWI au UKIMWI.
Hata hivyo ni muhimu kuwa mwangalifu na kuchukua tahadhari
ili kuzuia kuambukizwa.
Ukimtibu vidonda vya mtu aliyeambukizwa na Virusi vya
UKIMWI, ni vyema kuvaa mipira ya mikononi (glavu ) na daima
ni vizuri kufunga kitambaa au plasta mahali penye jeraha. Vifaa
vyenye ncha kali vinavyotumiwa na mtu mwenye maambukizi ya
virusi vya UKIMWI, kwa mfano nyembe, kutunzwa sehemu ya
pekee na visitumiwe na watu wengine.
Hatua hizi ni muhimu na za msingi kwa wahudumu wa watu
wenye virusi vya UKIMWI ili kuzuia yeye au watu wengine
wasipate maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Kama unamtunza
/ unamhudumia mtu aliyeambukizwa na Virusi vya UKIMWI
na huna uhakika au una wasiwasi na tahadhari za kuchukua,
unashauriwa kutafuta msaada kutoka kwa mtoa huduma wa
afya ili akupe maelezo zaidi.

21
Mambo ya Kukumbuka

22

You might also like