You are on page 1of 86

KITABU CHA

Wachungaji & wazee


Kwa ajili ya

HUDUMA ZA WATOTO

“Waacheni watoto wadogo waje kwangu…”

KIMEANDALIWA NA
Idara ya Huduma za Watoto na
Taasisi ya Wachungaji ya Halmashauri Kuu ya
Kanisa la Waadventista wa Sabato
Kwa Kushirikiana na Idara ya Huduma za Watoto NTUC
Kimetafsiriwa na Moseti Chacha
moseti.chachc@gmail.com
YALIYOMO
Dibaji……………………………………………………….…………….… 4
Utangulizi………………………………………………………………….. 5
Sura ya 1
Filosofia ya Huduma za Watoto………………………………………….. 6
Sura ya 2
Utume wa Huduma za Watoto………………………………………….... 9
Sura ya 3
Huduma ya Yesu kwa Watoto…………………………………….………10
sura ya 4
Mashauri ya Ellen G. White juu ya Huduma za Watoto………..……….. 12
Sura ya 5
Historia Fupi ya Huduma za Watoto……………………..……………… 13
Sura ya 6
Maelezo ya kazi ya Mratibu wa Huduma za Watoto…………………… 16
Sura ya 7
Uratibu wa Kamati ya Huduma za Watoto………………………………19
Sura ya 8
Tabia Nane za Huduma za Watoto zenye Afya katika Kanisa…...…….. 22
Kuwezesha Uongozi…………..…………………………….…… 22
Huduma inayoongozwa kwa karama……………..…….………. 23
Hali ya kiroho yenye msisimko…..……………………….……… 45
Miundo inayotenda kazi………………………..………….…….. 52
Huduma za Ibada zinazovutia………………………………...…. 53
Vikundi vidogo vya ujumla……………………………………..… 54
Uinjilisti uliojikita katika mahitaji………………………………… 56
Mahusiano ya upendo…………………………………………… 59

Sura ya 9
Miongozo ya Ubatizo na Mapendekezo ya Watoto…………….....……60
Sura ya 10
Matamko ya Konferensi Kuu kuhusu Watoto…………………………..64
Matamko juu ya Ustawi na Thamani ya Watoto…………...……64
Matamko juu ya Unyanyasaji wa Watoto………………………. 65
Sura ya 11
Programuu za Huduma kwa Watoto kwa ajili ya Kanisa mahalia…..…69
Programu Zinazo Wafikia Watoto Ndani ya Kanisa………….... 70
Shule ya Sabato ya Watoto……………………...……… 70
Kanisa la Watoto…………………………………………. 71
Mkutano wa Maombi wa Watoto…………………….… 70
Darasa la Ubatizo la Watoto………………………….…. 71
Kwaya ya Watoto…………………………….………….. 72
Sabato ya Watoto……………………………………….. 72
Mkutano wa Watoto………………………………....…. 73
Mkutano wa Watoto wa Uinjilisti………………………. 73
Chama ya Wahubiri Wadogo…………………………….74
Kongamano la Muziki la Watoto…………………..…… 74
Kambi la Watoto la Uoto wa Asili………………………. 74
Programu Zinazo Wafikia Watoto Wapya…………………….. 75
Shule ya Biblia wakati wa likizo……………………….... 75
Chama cha Biblia cha Mtaa……………………………... 75
Vikundi vya Michezo……………………………….…… 76
Sanaa Mwisho wa Juma………………………………… 76
Karibu Mtoto………………………………………….… 76
Huduma ya Maktaba Inayohama………………..……… 77
Mafunzo ya Biblia Majira ya Joto……….....……………. 77
Sura ya 12
Nyenzo
zinazopendekezwa………………………………………………………79
Vitabu……………………………………….….…………………79
Magazeti………………………………….…….……………….. 80
Tovuti……………………………………….….………………... 80
Hitimisho……………………………………………..…………………. 82
DIBAJI

A
gizo la Kristo la Kulisha Kondoo (Yohana 21:5) na kuruhusu watoto
waje Kwake (Marko 10:13, 14) linatoa mamlaka kwa kanisa kufanya
uinjilisti kwa watoto na kusimamia malezi yao ya kiroho. Kitengo
cha Huduma za Watoto katika kanisa la Waadventista wa Sabato
kimejitoa kikamilifu katika kutoa nyenzo, kuwezesha na kuratibu upanuzi na
uimarishaji wa malezi ya kiroho kwa watoto katika kanisa, ili kuwaleta katika
uhusiano wenye upendo, wa kutumika na Yesu na kujikabidhi kwa kwa dhati
katika kanisa la Waadventista Wasabato.
Kitabu hiki ni mwongozo kwa wachungaji, wazee wa makanisa, viongozi
wa watoto wa kujitolea, wazazi na wengine katika makanisa mahalia ambao
wanatamani kuelewa na kujifunza jinsi ya kuratibu huduma mpya za watoto
au kutia nguvu huduma zilizopo tayari. Toleo hili dogo linatoa falsafa na
utume wa Huduma za Watoto, likifuatiwa na mapendekezo ya programu
kwa ajili ya watoto zinazoweza kujaribiwa katika kanisa mahalia. Pia
linajaribu kufanyia kazi tabia nane za kanisa lenye ustawi kama
ilivyopendekezwa na Christian Schwarz, kwa Huduma za Watoto zenye
ustawi, na kwa jinsi hiyo kutoa mtazamo uliokamilika wa Huduma za Watoto
unaopaswa kutenda kazi ndani ya huduma zote za kanisa.
Wachungaji na wazee watagundua kuwa kitabu hiki ni rahisi kutumiwa na
kuwekwa katika iutendaji wanapojihusisha katika malezi ya hali za kiroho za
watoto ndani ya kanisa. Katika ulimwengu wa leo ambapo watoto
wamejawa na mawazo na maadili yanayokinzana na yale ya Kanisa la
Waadventista, ni muhimu kwamba kila kanisa mahalia na kiongozi wake
kutafuta njia za kuwasaidia watoto wetu katika kufanya maamuzi yaliyo
sahihi kuhusu Imani yao.
Chama cha Wachungaji cha Halmashauri Kuu kinayo furaha kuunga
mkono Idara ya Huduma za Watoto ya Halmashauri Kuu ili kuchapisha
kijitabu cha maelezo ya Huduma za Watoto kwa Wachungaji na Wazee. Hii
na iwe nyenzo ya kumwezesha kila kiongozi wa kanisa na mshiriki
anayetamani kulea watoto kuelekea katika uhusiano wenye upendo, na wa
kumtumikia Yesu, na kujenga wanafunzi wadogo wa Kristo waliojikabidhi
kwa Kanisa la leo na la kesho. Hebu na tukumbuke, kujenga kanisa la kesho
kunaanzia kwa watoto wa leo.
James A. Cress, Mkurugenzi. Shirikisho la Wachungaji. Halmashauri
Kuu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato. Silver Spring, Maryland
UTANGULIZI

W
engi wetu tunaamini kwamba watoto ndio kesho yetu. Watoto
ndio kanisa la baadae. Kwa hiyo, Kanisa, wazazi, na waalimu
wana jukumu la kuwafundisha kuwa washiriki na viongozi wa
baadae walio imara. Hata hivyo, tunasubiri tu siku za zijazo? Vipi kuhusu
wakati uliopo sasa? Je, tusingeanza mafunzo yetu sasa badala ya kubonyeza
kitufe cha subiri kwa watoto wetu?
Hata hivyo, utafiti unaonyesha uharaka wa kuwekeza muda, nguvu, na
fedha zetu kwa watoto sasa hivi badala ya wakati fulani huko mbeleni.
Utafiti wa hivi karibuni wa George Barna1 unaripoti kwamba asilimia 32 ya
wale waliofanya uamuzi wa kumkubali Yesu walifanya hivyo katika umri kati
ya miaka 5 na 12; asilimia 4 ya wale walio na umri kati ya 13 -18; na asilimia 6
kwa watu wa miaka 19 au zaidi. Kwa maneno mengine, kama watu
hawamkubali Yesu kama Mwokozi wao kabla hawajafikia umri wa
kupevuka, uwezekano wa kumkubali baadae ni mdogo sana.
Umuhimu wa kuwahusisha watoto katika mchakato huu wa kufaya
maamuzi katika miaka yao ya awali ni muhimu katika kujenga kanisa imara
leo. Tunaamini kwamba kujenga kanisa la kesho kunaanza na watoto wa leo!
Kwa hiyo, inaanzia kwa watoto katika makanisa mahalia. Inaanza na kila
kanisa kuwa na mratibu wa Huduma za Watoto ambaye atasimamia
programu zitakazowasaidia watoto kukua katika uhusiano wao na Yesu.
Kwa kuongezea, mchungaji na wazee wa kanisa ni watu muhimu ambao
wanaweza kusaidia, kutegemeza na kutia hamasa viongozi wa watoto
katika kukuza karama zao na muda wao ili kuendeleza Imani ya watoto
ndani ya kanisa. Kwa hiyo, mwongozo huu unatumika kama kiongozi kwa
Wachungaji na wazee katika kuelewa utume na jukumu la mratibu wa
Huduma za Watoto katika kanisa lao mahalia. Mwongozo huu una mawazo,
mapendekezo, na nyenzo zinazoweza kutumika katika kutekeleza
programu na shughuli za watoto.

1
Barna George. Transforming Children into Spiritual Champions. Ventura, California: Regal
Books, 2003
Sura ya 1
FALSAFA ya
HUDUMA ZA
WATOTO

H
uduma za Watoto hutafuta kuendeleza Imani ya watoto wenye
umri kati ya kuzaliwa na miaka kumi na nne. Pamoja na Shule ya
Sabato ambayo inatoa elimu ya dini kwa watoto mara moja kwa
juma, Huduma za Watoto hutafuta kutoa huduma kadhaa ambazo
zitawaongoza watoto kwa Yesu na kuwafanya kuwa wanafunzi katika
kutembea naye kila siku.
Biblia imeweka wazi sana kwamba watoto ni wa pekee kwa Mungu. Kama
utachunguza kile Biblia inachosema kuhusu watoto, utagundua sehemu
kubwa ya taswira kadhaa:2
Watoto ni zawadi kutoka kwa Mungu. Anawapa wazazi watoto kama
ishara ya upendo na utimilifu binafsi (Kum. 7:13; Zab. 127:3).
Watoto ni wa kutamaniwa. Kutoka katika uumbaji, Mungu ametuagiza
kuzaa watoto (Mwa. 9:7; Kum. 6:3).
Watoto huleta furaha na mibaraka kwa watu wazima. Mungu anatoa
faida nyingi kwa wazazi kupitia malezi ya watoto wao (Hes. 5:28; Kum
28:4, 11).
Watoto wanapaswa kufundishwa jinsi ya kuanzisha uhusiano na Mungu.
Moja kati ya changamoto zetu kuu ni kuhamisha Imani zetu na uelewa
wetu wa Mungu kwa watoto wetu (Kut. 12:26, 37; Kum. 6:1-7; Mit. 22:6).
Watoto ni wa thamani sana kwa Mungu kiasi kwamba anatuamuru
tuwalinde. Wazazi wanapaswa kuhakikisha usalama wa kiroho na wa
kimwili wa watoto wao (1 Sam. 20:42; Ezra 8:21).
Mungu anawapenda watoto kiasi cha kuhakikisha wanapata nidhamu.
(Mit. 3:11-12; 13:24; 19:18; Efe.6:4).
Mungu anafurahia asili na haiba ya watoto na anawaambia watu wazima
wajifunze kutoka kwao. Maandiko yanatambulisha tabia kama uwazi,

2
Barna George. Transforming Children into Spiritual Champions. Ventura, California: Regal
Books, 2003
unyenyekevu, urahisi, na Imani kama viwango vinavyopatikana kwa
watoto, na Mungu anathamini tabia hizi (Mat. 18:3; 19:14; Flp. 2:15).
Kama watoto wana thamani kiasi hiki kwa Mungu, basi wanapaswa
kuwa na thamani kwetu pia.
Utume Mkuu wa Yesu ni kwamba: “Enendeni mkawafanye mtaifa yote
kuwa wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana na la
Roho Mtakatifu.” (Mathayo 28:19). Hakika, hii inajumuisha kuwafanya
watoto kuwa wanafunzi na kuwaongoza kujitoa kwa dhati kwa Yesu.
Sura ya 2
UTUME
wa HUDUMA
ZA WATOTO

U
tume wa Huduma za Watoto ni kulea watoo ili wawe na uhusiano
wa upendo, na wa kumtumikia Yesu. Tunatafuta kutimiza utume
huu kwa kuendelezea:

Huduma zinazohusiana na Neema, ambazo kwazo watoto wote watapata


uzoefu wa upendo wa Yesu usio na masharti, watapata uhakika wa ukubali
na msamaha, hatimaye wafanye agano Naye.

Huduma jumuishi, ambazo kupitia huduma hizi, wale wanaojitolea


kuhudumia na watoto wanaohudumiwa watathaminiwa na kushirikishwa
bila kujali rangi yao, kabila, lugha, jinsia, umri, uwezo wala hali ya uchumi-
jamii wa wahusika.

Huduma za Uongozi, ambazo kwazo wale wanaojitolea watawezeshwa,


kufundishwa na kushehenezwa kwa ajili ya kuhudumia watoto kwa namna
iliyo bora.

Huduma zinazohusishwa na utendaji, ambazo kwazo watoto wanapewa


nafasi ya kuhudumia watu wa kwenye mitaa au miji yao kwa vitendo, hivyo,
kuanzisha mpangilio wa kuwafikia wengine katika jamii, huduma
itakayoendelezwa maisha yao yote.

Huduma za Ushirika, ambazo kwazo idara inafanya kazi pamoja na huduma


zingine, kama vile huduma za familia, Shule ya Sabato, uwakili, na zingine ili
kuendeleza malengo shirikishi.
Huduma salama, ambazo makanisa yetu:

a) huchagua wanaojitolea wenye chimbuko imara la hali ya kiroho na


maadili; na
b) kuchukua njia za usalama za kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji
wa kimwili, kihisia, na kiroho, na kanisa kutoka kwenye wajibu wake

Huduma za uijilisti, ambazo kwazo watoto ambao hawajakumbatiwa na


kanisa wataoneshwa upendo wa Yesu kupitia programu za kuifikia jamii
kama vile: Shule za Biblia wakati wa likizo, Kitengo cha watoto cha Shule ya
Sabato, Klabu ya Biblia katika ujirani, na vipindi vya saa za Hadithi.
Sura ya 3
HUDUMA
Ya YESU
kwa WATOTO

W
akati wote wa huduma yake hapa duniani, Yesu alitenga muda
kuhudumia watoto. Kalamu ya Maandiko pamoja na uvuvio
vilidhihirisha wazi wazi thamani aliyoiweka kwa watoto.
Huduma yake ilijumuisha yafuatayo:

1. Aliwabariki watoto na kuwaombea. Wakati wakina mama walipoleta


watoto wao kwa Yesu, wanafunzi walijaribu kuwafukuza. Hata hivyo,
badala yake Yesu aliwakemea. Kisha akaweka mikono yake juu ya
watoto, akawabariki, na akawaombea (Mathayo 19:14)

2. Aliwatambua watoto. Yesu alitamka kwa uhakika kwamba ufalme wa


mbinguni ni wa watoto wadogo pia. Hata hivyo, mtu yeyote
asiyeupokea ufalme wa mbinguni kama mtoto mdogo hatauingia kabisa
(Marko 10:15). Hapa anatambulisha kigezo muhimu ili kuingia ufalme wa
Mungu ni kuwa na imani na unyenyekevu kama mtoto.
Katika tukio jingine Yesu alipoulizwa na wanafunzi wake kwamba nani
atakayekuwa mkuu katika ufalme wa mbinguni, akamweka mtoto
mdogo kati yao, “akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa
kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.” (Mathayo
18:3). Hapa tena, Yesu anatilia mkazo umuhimu wa kujifunza kutoka kwa
mtoto. Anataja moja ya tabia hizi katika Mat 18:4: “Basi, ye yote
ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu
katika ufalme wa mbinguni.”

3. Alifanya urafiki na watoto. Alifurahia mambo madogo waliyofanya na


hata maua waliyomletea. E. G. White anaandika kwamba: “Kadri watoto
walivyokusanya maua ya porini kwa wingi, na kujikusanya ili kumpatia
maua hayo kama sadaka zao, aliyapokea kwa furaha, na kutabasamu na
kudhihirisha furaha yake katika kuona aina nyinigi za maua.” Upward
Look, uk. 57.

4. Alishirikiana na watoto. Yesu hakuwaangalia tu watoto wakicheza, bali


aliungana nao katika shughuli zao. Tena E. G. White anaandika kwamba:
“Kristo aliwatazama watoto wakiwa katika michezo yao, mara nyingi
alidhihirisha ukubali wake walipopata ushindi dhidi ya kitu walichokuwa
wameamua kufanya. Aliwaimbia watoto kwa maneno matamu yenye
Baraka. Alifahamu kwamba walimpenda. Hakuwahi kukunja sura mbele
yao. Alishiriki furaha na huzuni zao za kitoto. Mara nyingi alikusanya
maua, na baada ya kuonyesha watoto uzuri wake aliwaachia kama
zawadi. Ndiye aliyeumba maua, na alifurahia kuwaonesha uzuri wake.”
– Upward Look, uk. 57.
Sura ya 4
MASHAURI YA ELLEN
WHITE JUU Ya HUDUMA
kwa WATOTO

E
llen G. White amepokea wahyi kwa wingi kutoka kwa Mungu kuhusu
umuhimu wa watoto na haja ya kuwafundisha wakiwa bado wadogo
kumkubali Yesu kama Mwokozi wao. Anatetea huduma kwa watoto,
na haya ni baadhi ya mashauri yake:

“Hakuna jinsi nyingine yoyote ya kuweka umuhimu kwenye mafunzo ya


watoto kuliko katika ngazi ya awali. Masomo ambayo mtoto anajifunza
katika kipindi cha miaka saba ya kwanza katika maisha yanachukua sehemu
kubwa katika kuunda tabia yake kuliko yote anayojifunza katika miaka
inayofuata.” – Child Guidance, uk. 193

“Bado ni kweli kwamba watoto wanaguswa zaidi kwa mafundisho ya injili;


mioyo yao inakuwa wazi kwa mivuto ya kimbingu, na wanakuwa imara
katika kutunza masomo waliyopokea. Watoto wadogo wanaweza kuwa
Wakristo, wakiwa na uzoefu kulingana na umri wao. Wanahitaji kuelimishwa
katika mambo ya kiroho, na wazazi wanapaswa kuwapatia kila nafasi, ili
kwamba waweze kuunda tabia inayoendana na kufanana na tabia ya
Kristo.” – Desire of Ages, uk. 515.

“Watoto wa miaka nane, kumi au kumi na mbili wana umri unaofaa


kufundishwa juu ya somo la dini ya binafsi. Usiwafundishe watoto wako kwa
kuelekeza wakati fulani ujao ambapo watakuwa wakubwa wa kutosha
kuweza kuungama na kuamini ukweli. Kama wakielekezwa vyema, watoto
wadogo sana wanaweza wakawa na mitazamo sahihi juu ya hali yao kama
wenye dhambi, na njia ya wokovu kupitia Kristo.” – Testimonies, vol. 1, uk
400.
“Yesu aliona wanaume na wanawake ambao wanapaswa kuwa warithi wa
neema Yake na wafuasi wa ufalme Wake ndani ya watoto ambao walikutana
naye, na baadhi yao aliona kuwa wangekuwa wafia dini kwa sababu yake.
Alifahamu kwamba watoto hawa wangemsikiliza na kumkubali kama
Mkombozi wao kwa utayari zaidi kuliko watu wazima, ambao wengi wao
walikuwa wamejawa na mambo ya kidunia na wenye mioyo migumu. Katika
kufundisha, alijishusha na kuwa sawa nao. Yeye, Mkuu wa Mbinguni, alijibu
maswali yao na kurahisisha masomo yake yaliyokuwa muhimu ili kuweza
kufikia uelewa wao wa kitoto.” – Evangelism, 579.

“Katika mandhari za mwisho za historia ya dunia, wengi wa hawa watoto na


vijana watawashangaza watu kwa ushuhuda wao wa ukweli, ambao
utatolewa kwa namna iliyo rahisi sana, lakini kwa roho na uweza mkuu.
Wamefundishwa hofu ya Bwana, na mioyo yao imelainishwa kwa kujifunza
Biblia kwa umakini na kwa maombi. Katika siku za usoni, watoto wengi
watapewa uwezo wa Roho wa Mungu, na watafanya kazi katika
kuutangaza ukweli kwa dunia, ambapo kwa wakati huo washiriki wa kanisa
walio wakubwa hawataweza kuifanya kazi hiyo kwa namna iliyo bora zaidi.”
Counsels to Teachers, u. 166, 167.

“Wale wanaompenda Mungu wanapaswa kuhisi kuvutiwa sana na watoto


na vijana. Mungu anaweza kufunua ukweli wake na wokovu kupitia kwao.
Yesu anawaita wale walio wadogo wanaomwamini kama kondoo katika zizi
lake. Ana upendo maalum na mvuto kwa watoto . . . zawadi ya pekee
ambayo watoto wanaweza wakampatia Yesu, ni upya wa utoto wao.” RC
373.6

“Yesu alipowaambia wanafunzi wake wasiwazuie watoto kuja kwake,


alikuwa akizungumza na wafuasi wake walio katika vizazi vyote, -- vongozi
wa kanisa, wachungaji, wasaidizi, na Wakristo wote. Yesu anawavuta
watoto kwake, na anatuagiza, tusiwazuie; kana kwamba anasema,
watakuja kama msipowazuia.” – Desire of Ages, uk. 517.
Sura ya 5
HISTORIA FUPI
Ya HUDUMA ZA
WATOTO

KAZI KATIKA MIAKA YA 1800


Pamoja na kwamba ni kweli kuwa Huduma za Watoto hazikuwa chini ya
idara kamili ya Halmashauri Kuu hadi mwaka 1995, Kanisa la Waadventista
wa Sabato kwa muda mrefu lilitambua umuhimu wa kuhudumia watoto
hata katika miaka ya 1800. Kazi kwa ajili ya watoto ilianza mwaka 1863
wakati Adelia Patten alipoandika mfuatano wa masomo ya watoto ya miaka
miwili. Kuanzia 1864 hadi 1888 masomo ya watoto yalichapishwa katika
kijitabu cha Youth instructor, idadi kubwa ya mafunzo hayo ilijikita katika
historia ya kibiblia na hadithi za Biblia. Mwaka 1869 G. H. Bell aliandika
mfuatano wa masomo kwa ajili ya watoto.

KAZI MWANZONI MWA MIAKA YA 1900

Mwaka 1890 kijitabu cha “Our little Friend” kilianza kubeba masomo ya
Shule ya Sabato kwa ajili ya watoto walio katika ngazi ya msingi na awali,
kilichokuwepo kwa miaka sitini na saba. Mwaka 1957, hicho kitabu kilianza
kuwa na masomo ya Shule ya Sabato kwa ajili ya watoto wachanga pamoja
na wale wa madarasa ya awali. Masomo ya Shule ya Sabato kwa ajili ya
Watoto wa shule za msingi yalitokea katika chapisho jipya liitwalo, Primary
Treasure mwaka 1957. Lesoni za Shule ya Sabato kwa ajili ya umri wa shule
ya msingi na wa kati zilianzishwa Australia mwaka 1911 – 1913, na muda sio
mrefu lesoni zaidi zilizalishwa kwa ajili ya watoto wa ulimwengu wa
wanaozungumza Kiingereza uliobaki. Kuanzia mwaka 1933 hadi 1936
mfuatano wa matoleo matano yaliyoitwa Bible Stories for the Cradle Roll
yalitokea. Nyenzo zingine za mitaala ya watoto zilitokea kila baada ya kipindi
fulani, kutoka katika Idara ya Shule ya Sabato ya Halmashauri Kuu na kutoka
kwa waalimu walio hai wenye shauku pamoja na wafanyakazi katika shule
ya Sabato mahalia duniani kote.
Miaka ya 1960 watu kadhaa walichukua nafasi ya utendaji katika Idara ya
Huduma za Watoto: Curtis Barger, Tom Ashlock, na Ben Leibelt. Tom
Ashlock alihusika kuunda program mpya ya Shule ya Biblia wakati wa likizo,
pamoja na kazi zake za uandishi zikiwekwa katika Little Friend na Primary
Treasure.

KAZI YA WATOTO CHINI YA HUDUMA ZA KANISA

Pamoja na kwamba kulikuwa hakuna idara rasmi kwa ajili ya watoto, lakini
katika mkutano wa Halmashauri Kuu wa 1985 uliofanyika huko New Orleans,
Idara ya Huduma za Kanisa iliundwa, ambayo iliundwa kwa kama
muunganiko wa idara nne: Shule ya Sabato/Shughuli za Walei, Uwakili na
Maendeleo, Vijana, na Huduma za Kaya na Familia. Idara hii inajumuisha
huduma na msaada kwa kazi ya Huduma za Watoto, lakini hadi mkutano wa
Dunia wa Mashauri, mwaka 1987 ndipo Huduma za watoto zilipojitokeza
kama idara mpya ndani ya Idara ya Huduma za Kanisa.
Idara hii, kwa kushirikiana na Review and Herald na Shirika la uchapishaji
la Pasific Press zilizalisha Lesoni ya Shule ya Sabato kwa ajili ya watoto. Hii
ilijumuisha Lesoni ya Shule ya Sabato ya Chekechea, Lesoni ya Msingi ya Shule
ya Sabato, Lesoni ya vijana wadogo ya Shule ya Sabato, na Lesoni ya Vijana wa
Awali ya Shule ya Sabato (sasa hivi Mahusiano) pamoja na somo la Utume
(toleo la watoto). Idara pia ilizalisha program za msaada kwa ajili ya viongozi
wa shule ya Sabato ya watoto wachanga, msingi, na vijana wadogo/vijana
wa awali.
Kuanzia 1985 – 1990, idara ya Huduma za Watoto ilipokea msukumo wake
kutoka kwenye njozi na msukumo aliokuwa nao Helen Craig, mkurugenzi
msaidizi wa Shule ya Sabato ya Watoto aliyepita, Shule ya Biblia wakati wa
Likizo, na Uinjilisti wa Watoto. Kuanzia 1990 – 1995, Virginia Smith aliongoza
kazi kwa ajili ya Huduma za watoto kama moja ya huduma zinazounga
mkono Idara ya Huduma za Kanisa.

KUTOKEA KWA IDARA

Mkutano wa Konferensi Kuu mwaka 1995 huko Ultrecht uliasisi kipindi cha
mageuzi katika Huduma za watoto. Julai 4, 1995, A. H. Tolhurst alipendekeza
mada kwamba Idara ya Huduma za Watoto ianzishwe kama Idara tofauti na
idara zingine za kanisa. Iliungwa mkono na kupigiwa kura, na Huduma za
Watoto ikawa idara mpya kanisani, idara pekee kuanzishwa katika kikao cha
mkutano wa Halmashuri Kuu.
Mwaka 2000 mtaala mpya wa watoto uliandikwa kwa ajili ya kanisa
ulimwenguni. Huu ulikuwa matokeo ya tafakuri ya ubunifu na tathmini
iliyofanywa na watu wengi kutoka kwenye divisheni zote ulimwenguni.
Ikifahamika kama ‘Kiungo cha Neema’ (GraceLink), mtaala huu mpya
unakazia dhana nne za msingi katika Imani ya Kikristo:

1. Neema, Nafasi ya Mungu katika mpango wa wokovu;


2. Ibada, mwitikio wetu katika ari ya Mungu ya kuokoa;
3. Jamii, jinsi neema ya Mungu inavyotulazimisha kuishi pamoja kwa amani
kama familia ya Mungu; na
4. Huduma, mwitikio wetu kwa upendo wa Mungu tunapojitoa katika
kuvuta nafsi za wengine na kuwahudumia.

Leo hii, idara ya huduma za Watoto imekuwa ni utume wa ulimwengu


mzima ikijumuisha kila divisheni ulimwenguni ikiwa na mkurugenzi wa
kusimamia kazi ya malezi na mafunzo ya kiroho kwa ajili ya watoto.
Sura ya 6
MAELEZO YA KAZI
Ya MRATIBU wa
HUDUMA ZA WATOTO

MAJUKUMU YA MRATIBU WA HUDUMA ZA WATOTO


NI KAMA IFUATAVYO:

1. Kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Idara ya watoto.


2. Kufanyia kazi mtaala wa ‘Kiungo cha Neema’ (GraceLink) na kutoa
mafunzo kwa viongozi na waalimu akitumia mtaala huo.
3. Kupanga na kufanyia kazi kalenda ya programu za mwaka mzima kwa
ajili ya watoto ambayo itawavuta kwa Kristo na kuwapatia ushirika
katika shughuli za kanisa.
4. Kutengeneza bajeti ya kutekeleza programu na shughuli zote kwa ajili ya
watoto.
5. Kutumika kama mwakilishi wa matakwa na mahitaji ya watoto kwa:
a. Baraza la Kanisa – kwa kutoa taarifa kwa wajumbe wa baraza la
kanisa kuhusu changamoto na mafanikio, kwa kutoa ripoti ya
matokeo kama hayo ya mchanganuo wa mahitaji ya watoto na kwa
kusimamia fedha kwa ajili ya programu za watoto.
b. Mchungaji – kwa kufanya kazi pamoja ili kufanya Nyanja mbalimbali
za uhai wa kanisa ziwe rafiki kwa watoto na kuleta maana kwao.
c. Viongozi wa shughuli za watoto – kwa kuwaunga mkono na kuwatia
moyo.
6. Kuchukua hatua zinazoeleweka katika kudumisha viwango vya ubora
wa kimaadili katika uongozi wa watoto kwa kuchuja viongozi wa
kujitolea na waalimu.
7. Kudumisha mawasiliano na wazazi na viongozi wa shughuli za watoto,
kuwapa taarifa kuhusu warsha, mikutano, makambi, na nyenzo zingine
na kuwatia moyo wanapokua katika kuwaelewa watoto.
8. Kutafuta fursa za kuwa pamoja na watoto ili kudumisha mawasiliana na
jinsi wanavyofikiria na mahitaji yao.
9. Kufanya kazi na mchungaji katika matukio yanayojumuisha watoto,
kama vile:
a. Kuweka wakfu watoto
b. Ubatizo
c. Kisa kwa watoto wakati wa ibada kuu
d. Mashemasi wadogo
10. Kuandaa ripoti za takwimu kwa ajili ya mkurugenzi wa konferensi.
Sura ya 7
URATIBU Wa
KAMATI Ya HUDUMA
ZA WATOTO

K
anuni ya kanisa inapendekeza kwamba baraza la kanisa lisaidie
kutengeneza kamati ya Huduma za watoto baada ya kuchagua mtu
atakayetumika kama Mratibu wa Idara ya Huduma za Watoto.
Mratibu atafanya kazi pamoja na baraza ili kuchagua watu wengine
watakaotenda kazi katika kamati yake.

UCHAGUZI WA WAJUMBE WA KAMATI

Mratibu wa Huduma za watoto anaanza kupangilia orodha hii kwa


kufuata hatua hizi:
Anachagua watu wenye uwezo kwa ajili ya kamati ya Huduma za
watoto. Kamati itajumuisha:
Mratibu wa Huduma za watoto (Mwenyekiti)
Viongozi wa vyombo vingine vya watoto
Watu wengine wenye kuvutiwa na kuwa na hisia kali na huduma za
watoto.
Idadi ya kawaida ya wajumbe wa kamati inayopendekezwa ni 5 – 10.
Peleka kwenye baraza la kanisa majina ya wajumbe wa kamati
waliopendekezwa ili wapitishwe.

MAJUKUMU YA KAMATI

Kamati ina majukumu yafuatayo:


Kutengeneza tamko fupi la utume.
Kuchanganua mahitaji ya watoto ndani ya kanisa na katika jamii.
Kuunda mpango wa jumla.
Kupanga kalenda ya mwaka ya programu kwa ajili ya watoto.
Kuratibu kalenda ya huduma za watoto pamoja na idara zingine za
kanisa
Kutengeneza bajeti kwa ajili program zilizopangwa.
Kushirikisha baraza la kanisa katika bajeti na mipango yenu na kuomba
fungu la fedha.
Tunza kumbukumbu sahihi za watoto walioshiriki katika shughuli
zilizofadhiliwa na kanisa na kuzikabidhi kwa karani wa kanisa.
Kuwawezesha na kuwategemeza viongozi wa programu.

KUFANYA UTAFITI WA MCHANGANUO WA MAHITAJI

Ni muhimu sana kufanya utafiti wa mchanganuo wa mahitaji ya familia na


watoto wao ndani ya kanisa lako na jamii. Matokeo yatatumika kumsaidia
Mratibu wa Huduma za watoto na kamati katika kuunda mtaala, kuratibu
shughuli, kutoa mafunzo kwa waalimu, na kuweka malengo. Tengeneza
fomu ndogo ya utafiti ambayo washiriki wa kanisa na wazazi katika jamii
yako wanaweza kujaza kwa dakika 3 -5. Mfano ufuatao unaweza ukatumika,
lakini marekebisho yanaweza kuhitajika ili kujumuisha maswali
yanayoendana na familia katika jamii husika.

Huduma za Watoto
UTAFITI WA MCHANGANUO WA MAHITAJI
Ili tuweze kukuhudumia wewe na watoto wako kwa ubora zaidi,
tumepanga utafiti huu. Tafadhali chukua dakika kadhaa kujibu maswali
yafuatayo. Matokeo ya utafiti huu yatatumika kutusaidia katika kuratibu
programu, kutengeneza nyenzo, na kupanga malengo kwa ajili ya huduma
yetu yote kwa watoto.
1. Una watoto wangapi? ___________________________________
2. Watoto wako wana umri gani? ____________________________
3. Una mtoto mwenye mahitaji maalum? Ndiyo Hapana
Umri: _________
4. Ni programu za aina gani ungependa tutengeneze kwa ajili ya watoto
wako? (Weka alama kadiri unavyoona inafaa.)
mikutano ya faragha siku ya kazi za ustadi
mradi wa utoaji wa huduma kwaya
mapishi huduma ya wanasesere
maonyesho ya afya jaribio/mchezo wa Biblia
kambi la porini mandari (pikniki)
kikundi cha maombi chama cha kuhubiri
Mengineyo: ___________________________________________________
_____________________________________________________________
5. Ungependa turatibu programu za aina gani kwa ajili ya wazazi?
______________________________________________________________
______________________________________________________________
6. Kama ungetakiwa kuchagua program 3 zinazohitajika zaidi, ungechagua
zipi?
1) ___________________________________________________________
2) ___________________________________________________________
3) ___________________________________________________________
Sura ya 8
TABIA NANE za IDARA
ya HUDUMA za
WATOTO yenye AFYA
katika KANISA MAHALIA

C
Hristian Schwartz anonesha katika kitabu chake cha Natural Church
Development kwamba, kila kanisa linalositawi na kukua lina tabia
nane. Tabia hizi pia zinaweza zikawakilishwa katika Huduma za
watoto ili kwamba ziweze kudumisha idara inayositawi na kukua katika
kanisa mahalia. Tabia hizi nane ni:
Kuwezesha Uongozi
Huduma inayoongozwa kwa kipawa
Hali ya kiroho yenye hisia kali
Miundo inayotenda kazi
Huduma za Ibada zinazovutia
Vikundi vidogo vya ujumla
Uinjilisti uliojikita katika mahitaji
Mahusiano ya upendo

1. KUWEZESHA UONGOZI
Viongozi makini wanatilia mkazo katika kuwawezesha Wakristo wengine
kwa ajili ya huduma. Wanatoa nyenzo, wanaunga mkono, na wanatia
hamasa mtu mmoja mmoja ili wawe kile Mungu anachowataka wawe. Kwa
hiyo idara ya Huduma za watoto inawezaje kulisaidia kanisa mahalia katika
kuwezesha uongozi katikati ya washiriki wake? Hii inaweza kufanyika kupitia
programu za mara kwa mara za kufundisha uongozi ili kuwezesha watu
wenye uwezo wa stadi za uongozi kuwa viongozi na waalimu wa watoto.
Zaidi ya hayo, kutekeleza program ya wanasihi yenye matokeo bora pia
kunasaidia kuwezesha watu wenye uwezo ambao wanataka kufanya kazi
kwa ajili ya watoto.

A. KUTHIBITISHA UONGOZI

Kuratibu Huduma za watoto kwa ajili ya kanisa mahalia kunajumuisha


kutoa mafunzo kwa waalimu na wasaidizi. Programu ya Kuthibisha Huduma
za Watoto ya Halmashauri Kuu na Divisheni ya Amerika Kaskazini (NAD)
inaweza ikatumika katika mafunzo hayo mara kwa mara. Jumla ya kozi tisa
zinaunda ngazi ya msingi ya mafunzo ya uongozi ya Halmashauri Kuu. Kozi
hizi zinaweza zikafundishwa na mkurugenzi wa Huduma za Watoto wa
Konferensi au kiongozi mwingine aliyefuzu katika semina kwenye
makongamano ya wakufunzi, mafunzo ya uongozi, au majuma ya
kuthibitisha uongozi. Inaweza ikachukua miezi kadhaa hadi mwaka kuweza
kukamilisha kozi zote tisa, mwisho wake cheti cha uthibitisho kitatolewa
kutoka Idara ya Huduma za watoto ya Halmashauri Kuu kwa kila aliyeshiriki.
Ufuatao ni ufupisho wa maelezo ya kozi hizi za uthibisho. Maelezo ya kina
kuhusu kozi hizi na muhtasari wa hotuba zake yanaweza yakapatikana
kutoka kwenye Idara ya Huduma za Watoto ya Halmashauri Kuu.

Kuelewa ‘Kiungo cha Neema’ (GraceLink)


Kupitia mtaala wa ‘Kiungo cha Neema’, kujifunza jinsi neema, ibada, jamii,
na huduma vilivyoingizwa kwenye masomo ya Biblia, na kuelewa mtazamo
mpya katika kuufundisha mtaala huo.

Kujifunza kwa Vitendo


Gundua njia bora na za kuvutia za kufundisha watoto wa umri wowote kwa
kuwahusisha katika vitendo badala ya hotuba.

Kukuza Imani ya Watoto


Gundua jinsi watoto wanavyokuza imani yao na kujifunza kuwaongoza
kupitia hatua za makuzi ya Imani kuelekea katika uhusiano wa kujitoa
kikamilifu kwa Yesu Kristo.

Nidhamu Chanya ya Darasa


Jifunze baadhi ya dhana za kumudu darasa kwa neema na uimara kadiri
unavyowezesha kujifunza kwa vitendo katika masomo yako.

Kulea Watoto Kumcha Mungu


Wasaidie wazazi wajifunze njia makini za kulea watoto wao katika kumcha
Mungu kwa kufanya ibada iwe ni mtindo wa maisha.

Kulinda Watoto dhidi ya Unyanyasaji (Kuwachuja waliojitolea)


Walinde watoto katika kanisa lako kwa kuanzisha mchakato makini wa
kuwachuja wanaojitolea. Jifunze jinsi ya kuanzisha fomu za kujiunga kwa
wale wanaojitolea bila kufedhehesha viongozi wa muda mrefu.

Usalama na Huduma za Dharura kwa ajili ya Watoto


Hakikisha kuna usalama wa watoto katika shughuli zilizofadhiliwa na kanisa
kwa kutekeleza mchakato utakaowalinda dhidi ya madhara yoyote ya
kimwili, hatari, ajali, na majanga mengine yasiyotabirika.

Kuelewa Maendeleo ya Mtoto: Kuzaliwa hadi kupevuka


Gundua tabia za ukuaji wa watoto wenye umri wa miaka 0 – 14, jinsi
wanavyojifunza, na njia bora ya kuwafundisha. Elewa mahitaji, uwezo, na
changamoto za watoto ambao hawajapevuka. Jifunze vidokezo vya
kiutendaji vya kuwafanya waendelee kuunganika kwenye kundi wakati uo
huo wakiunnganika na Yesu.

Kuelewa jinsi Watoto Wanavyojifunza


Elewa jinsi watoto wanavyojifunza kupitia mitindo yao mbalimbali ya
kujifunza na jaribu kutimiza mahitaji ya kila aina ya mwanafunzi. Gundua siri
za kutengeneza mpango kazi wenye mafanikio.

B. KUSIMAMIA WALIOJITOLEA

Jambo la msingi linalowavunja moyo waratibu wengi wa huduma za


watoto ni kutafuta, kutoa mafunzo, na kuwatia hamasa wale wanaojitolea.
Inaweza kuwa vigumu kupata watu wa kujitolea walio sahihi. Wale walio
tayari mara nyingi huwa hawana ujuzi. Na wale walio na ujuzi mara nyingi
huwa hawako tayari. Tunawezaje kupata msaada tunaohitaji ili kwamba
tuweze kufundisha mtu mmoja mmoja kwa ajili ya uongozi wa siku zijazo?
Mtu anayejitolea ni nani?
Mtu ambaye sio lazima afanye lakini hata hivyo anafanya!
Hauwezi kuwafukuza kazi.
Lakini wanaweza wakaacha kazi wakati wowote wakitaka.
Kielelezo chenye matokeo ya juu cha Kuongoza Wanaojitolea

1. Kudahili

4. Kuongoza Kizidishi cha Huduma 2. Kuchuja

3. Kuwezesha

Muundo huu umeundwa na majukumu manne:


1. Kudahili
2. Kuchuja
3. Kuwezesha
4. Kuongoza
Majukumu yote manne yatakapofuatwa kwa makini, huduma yako itazidi
mara dufu. Kutakuwa na watu zaidi wanaojitolea kuwa viongozi na
wanajengwa ili kuwa viongozi wa baadaye.

Kielelezo cha Uongozi kwa Wanaojitolea


Kuna mitazamo kadhaa katika kuongoza wanaojitolea. Lakini kutumia
mtazamo wenye mguso mkubwa kuna matokeo yaliyo bora zaidi kwa ajili
ya mafanikio katika Huduma za watoto kama tunataka kujenga viongozi wa
baadaye. Hebu tuangalie vielelezo viitano vya uongozi kama ilivyoonyeshwa
katika mchoro hapa chini. Msitari wa kuelekea juu unawakilisha faida kwa
wanaojitolea na unaokwenda kulia unawakilisha faida kwa kanisa.
Aina za Vielelezo

Mtazamo dhaifu: Mchungaji anafanya kila kitu.


Alama: Aliyejitolea 0; Kanisa 0

Mtazamo wa mtoa msaada: wanaojitolea wanaombwa kusaidia;


Wanatumika na kunyonywa
Alama: aliyejitolea 0; kanisa 10

Mtazamo wa kuhisi vyema: waliojitolea hutumika wanapotaka


Alama: aliyejitolea 10; kanisa 0

Mtazamo wa msaidizi: tofauti ya daraja kati ya viongozi na


waliojitolea; hakuna nguvu katika kutia
hamasa, kutoa mafunzo kwa ajili ya
uongozi.
Alama: aliyejitolea 5; kanisa 5

Mtazamo wenye mguso


Wa juu : Kujitoa kwa kanisa zima katika
kuchagua na kuwafundisha
waliojitolea; kujenga timu ili kufikia
malengo ya ufalme.
Alama: aliyejitolea 10; kanisa 10

Kuwapa nyenzo waliojitolea


Tunawawezesha waliojitolea kwa kuwapatia:
Maelezo ya huduma
Vifaa muhimu
Rasilimali: za kibinadamu, kifedha, maandishi
Mafunzo: semina, maonesho, mifano ya kuigwa/washauri
Msaada, tathmmini, kuimarisha

Maelezo yanayohusu Huduma yanasema:


Cheo au nafasi/huduma
Orodha ya mambo muhimu ya kufanya
Orodha ya mafunzo muhimu yanayohitajika
Ujuzi zaidi ulio muhimu kwa ajili ya kazi
Mafunzo zaidi kwa ajili ya huduma

Kwa nini mafunzo hushindwa?


Tunapuuzia kutoa fomu ya maombi ya usajili ili kupata ahadi ya
kushiriki mafunzo.
Mafunzo hayahusiani na dhana husika
Taarifa pekee
Kukosekana kwa mawasiliano
Hakuna mrejesho pande zote mbili
Mambo yasiyo na maana
Mzungumzaji havutii

Jinsi ya kufanya mafunzo yawe na uhusiano?


Mwite kila mtu kwa jina lake; changamsha chumba na muwe na
wakati mzuri.
Kila mtu avutiwe na mwenzake; shirikishaneni furaha na mashaka
pamoja.
Muwe kundi la kusaidiana; ombeni pamoja
Mara moja moja mtoke na kula pamoja kwenye meza moja
Tumia ucheshi; panga mambo ya kushtukiza

Kuvutia watu kwa ajili ya mafunzo


Mafunzo hayo yapatie jina la mkutano wa timu ya uongozi
Dai orodha ya mahudhurio
Shughulika na masuala
Sikiliza uzoefu unaoelezwa na waliojitolea
Mruhusu kila mmoja achangie
Imarisha na na toa mrejesho
Usitawale mazungumzo
Usipoteze muda wao

Mafunzo ya Yehoshafati
Tafakari kwa makini kile unachofanya
Kazi yako ni kwa ajili ya Mungu
Mungu yupo pamoja nawe
Hofu ya Mungu na iwe juu yako
Hakuna uonevu, wala upendeleo, au rushwa
Tumika kwa uaminifu, kwa moyo wote

Wanaoongoza katika wale waliojitolea


Mahitaji ya msingi
Toa maono
Elezea maana ya utume wenu
Kuwa mshauri (ushauri wa binafsi/usimamizi)
Mwanafunzi (toa uongozi wa kiroho)

Viongozi wenye matokeo yanayotarajiwa . . .


Weka injili katika utendaji – mimina upendo
Sikiliza sauti ya Mungu
Chukulia Biblia kuwa mamlaka kamili
Tegemea maombi
Weka maisha yao yote katika uwiano
Huduma inayozidi
Siku zote muwe viongozi washauri/wa kuigwa
Zidisha majukumu kwa kuyaongeza
Tayarisha mtu atakayechukua nafasi yako
tia moyo ukuaji wao binafsi
waombe waungane nawe
kabidhi majukumu yako pole pole

Kanuni za Mguso wa Juu


Mtu anayejitolea ni mtoto wa Mungu
Uongozi wa kanisa unapaswa kufanyia kazi uwakili wa wanadamu pia
Tambua thamani iliyokuzwa ya mtu aliyejitolea
Wanaojitolea ni wabia wenye uwezo
Kazi za muhimu za kiongozi ni kusajili, kuchuja, kutoa mafunzo na
kufanya kuwa wanafunzi

C. JINSI WACHUNGAJI NA WAZEE WANAVYOWEZA KUWEZESHA


VIONGOZI WA WATOTO
Toa nafasi kwa viongozi wa watoto ili waratibu ibada ya watoto katika
siku zilizo maalum.
Husisha viongozi wa watoto katika kamati za mipango mahali ambapo
wanaweza wakajifunza stadi za uongozi.
Tegemeza program za Huduma za Watoto kwa kusaidia katika maeneo
ya uwasilishaji, usafiri, kutangaza matukio
Watie moyo kujaribu mawazo mapya.
Toa bajeti kwa ajili yao katika kuongoza program za watoto
Chagua watu wenye uwezo kuingia katika kamati ya Huduma za Watoto.

2. HUDUMA YENYE MWELEKEO WA KARAMA

Mungu ametupatia kila mmoja wetu karama na talanta. Wakati sio kila
mtu ana karama ya kufundisha na kufanya kazi na watoto, bado kuna wale
walio na ari kwa ajili yao. Ni wajibu wa kanisa kutafuta watu wa aina hiyo
wenye uwezo ambao wana karama hizi na kuwaelekeza kwenye Huduma
za Watoto.
Wakati wachungaji na wazee wanatafuta watu walio na karama na talanta
kwa ajili ya kufanya kazi na watoto, lazima pia wachuje wale wanaojitolea ili
kuhakikisha usalama wa watoto. Ni lazima watoto walindwe dhidi ya watu
ambao wanaweza kuwaumiza kimwili, kihisia, na kiroho. Huduma
inayoongozwa na karama inahusisha kazi kama kusajili, kuchuja, na
kuongoza waliojitolea.

A. KUSAJILI WANAOJITOLEA
Kusajili wanaojitolea kamwe sio kazi rahisi, lakini ni kazi ya muhimu kwa
Huduma za watoto. Watoto wanahitaji uangalizi zaidi, msaada, na uongozi
kutoka kwa watu wazima katika programu zote za watoto. Kwa hiyo, kusajili
wanaojitolea kunatakiwa kuwa ni mchakato unaoendelea kadri mratibu na
kamati ya huduma za watoto wanapotafuta watu wengine
wakuwawezesha kwa ajili ya huduma.

Vigezo katika Kuchagua Wanaojitolea


Chagua watu ambao wana tabia hizi:
Anaonyesha upendo na kujitoa kikamilifu kwa Mungu na kwa kanisa
Ana maadili ya hali ya juu
Ana uwezo na uzoefu wa uongozi
Ana upendo kwa watoto

Majukumu ya Msajili
Anatafuta wanaojitolea wakati wote
Ana faili la wanaofaa kujitolea
Ana majukumu kwa kila kazi
Ana akiba ya fomu za usajili wa huduma

Hatua katika Kuchagua Wanaojitolea


Omba kuhusu watu unaohitaji.
Shirikisha watu wengine maono yako.
Tangaza hitaji la watu wa kujitolea kwa kutumia moja ya njia hizi:
Matangazo kwenye vipeperushi au mimbarani
Mialiko ya kwenye simu
Aliyejitolea kupendekeza mwingine atakayejitolea
Kupitia kamati cha uchaguzi ya kanisa
Mwaliko wa ana kwa ana
Tambua nafasi zinazohitajika kwa ajili wanaojitolea.
Mwalimu
Mratibu wa sanaa
Kiongozi wa muziki
Msimuliaji wa hadithi
Mratibu wa wanasesere
Mratibu wa timu
Amua muda wa kutoa huduma kwa kila nafasi
Toa maelezo ya kazi ambayo yanaeleza mategemeo na wajibu.
Fanya kazi ya kutafuta wanaojitolea iwe ni mchakato endelevu.

Kama mtupa mshale


ANAYEJERUHI KILA MTU
Ndivyo alivyo yeye
ANAYEMWAJIRI MPUMBAVU
Au anayewaajiri WAPITAO

B. KUCHUJA WANAOJITOLEA
Kwa nini kuchuja wanaojitolea?
Ili kugundua wale Mungu aliowaita kwa ajili ya utume
Kuoanisha karama ya mtu na huduma
Kupima mvuto wao
Kulinda watoto
Kulinda kanisa dhidi ya madeni
Kuanzisha upatanifu wa dondoo

Nani anayefanya mchujo?


Mratibu wa Huduma za Watoto
Kiongozi wa idara
Kamati ya mchujo ya kanisa
Mratibu wa Huduma za watoto
Anapokea fomu za usajili
Anahusiana na kiongozi wa idara
Kamati ya mchujo
Inafanya uchunguzi wa maisha ya nyuma na udahili
Kanuni saba
Kuitwa katika huduma
Tabia – mchujo wa Mungu
Kemia – mtazamo, utayari
Ushindani – mafunzo, uzoefu
Usawa/upatanifu
Kujitoa kwa dhati
Hali – kiakili, kimwili, kiroho
Wanajitolea kwa dhati wanashirikiana na Daudi kusema: “sitamtolea
Bwana, Mungu wangu sadaka za kuteketezzwa nisizozigharimia.” 2
Samweli 24:24.
“Mtabiri aliye bora wa mambo ya mbeleni ni matendo ya nyuma.”
“Anayejitolea akishindwa, kosa linamrudia msajili/mchujaji wala sio yule
anayejitolea.”

C. MIONGOZO YA WAADVENTISTA YA USIMAMIZI WA BIMA KATIKA


KUCHUJA WANAOJITOLEA
Mfano wa miongozo iliyotolewa na Shirika la Waadventista la kukabiliana
na hatari kwa ajili ya waratibu wa Huduma za watoto na viongozi wengine.
Unaweza ukaitumia unapochuja wanaojitolea, na kwa sehemu zingine
unaweza ukazitumia kadiri zitakavyotimiza mahitaji yako. Mfano wa fomu
ya usajili wa wanaojitolea na fomu ya wadhamini pia zimejumuishwa.
SHIRIKA LA WAADVENTISTA LA KUSIMAMIA HATARI
Shirika la huduma ya kukabiliana na hatari la kanisa la Waadventista Wabato duniani

Watoto watasimamiwa na mtu (watu) mzima wakati wote. Program za


watoto zitaendeshwa katika mfumo usio na manyanyaso,au usumbufu
wakati wote.

Kulinda Huduma za watoto


Uongozi wa Waliojitolea – matendo bora
Mkazo kwenye utume
Siku zote utume uwe ndio mkazo wako
Utume usukumwe na kuelekeza wanaojitolea
Utume ulenge kwenye utendaji wa wanaojitolea na sera kwa ujumla
Kuwaondoa wanaojitolea kuendane na kutegemeza utume

NAFASI KWA UTENDAJI BORA KATIKA HUDUMA ZA WATOTO


“Kanisa mahalia linapaswa kuchukua hatua zinazoeleweka ili kulinda watoto
wanaoshiriki katika shughuli zinazofadhiliwa na kanisa kwa kuchagua watu
walio na historia nzuri kiroho na kimaadili kama viongozi na washiriki katika
programu za watoto.” Kanuni ya kanisa toleo – 2000 uk.120
MAKANISA HAYAKO SALAMA
Jumuia ya Imani
Kutokuelewa dhana kuhusu manyanyaso ya watoto
Kukosekana kwa njia za usalama ili kulinda watoto
Nafasi mbali mbali za kufanya kazi na watoto
Kuwafikia watoto kwa urahisi bila kufikia viwango vya mchujo
Hitaji la wakati wote kwa ajili ya wanaojitolea kwa ajili ya kufanya kazi na
watoto na idara ya vijana

WAJIBU WA MFUMO
Wajibu wa kulinda watoto wote kutoka kwenye hatari
Ushiriki salama katika shughuli za kanisa au za shule
Kwamba shughuli zote zinasimamiwa na mwajiriwa au mtu anayejitolea
aliyepitia mafunzo
Matengenezo sahihi ya vifaa ili kupunguza nafasi ya hatari
Wajibu wa kufanyia kazi malezi yanayoleta maana kwa wafanyakazi
inaweza ikajumuisha:
Uchaguzi wa makini wa waajiriwa na wanaojitolea
Mafuzo sahihi kwa wafanyakazi na wanaojitolea
Usimamizi sahihi wa wafanyakazi na wanaojitolea
Tendo linalofaa ambapo ni lazima kuondoa wafanyakazi
Wajibu wa kutoa taarifa ya matukio yote ya unyanyasaji wa mtoto
kulingana na sheria
WAJIBU KWA WATOTO & WATU WAZIMA
Watu wazima wanaofahamika kuwahi kufanya matendo ya unyanyasaji
kwa watoto hapo kabla au utendaji mwingine usiofaa hawataruhusiwa
kushiriki katika program zinazofadhiliwa na kanisa katika huduma za
watoto
Hatua zinazofaa zitachukuliwa kuepuka kuwahisi watu wazima
wanaohusika na uzimamizi kupitia matumizi ya njia zifuatazo za usalama
Kanuni ya miezi sita itatumika katika kuwafahamu zaidi watu wapya
wanaojitolea
Kanuni ya watu wazima wawili itatumika katika shughuli zote
zinazofadhiliwa na kanisa
Lazima kwa wale wanaojitolea wote kushiriki katika program ya
uelewa wa unyanyasaji wa watoto kila mwaka
Kila dai linalotolewa dhidi ya mtu mzima aliyejitolea kuhusu utendaji
usiofaa litachunguzwa kwa makini na kanisa na njia sahihi za
marekebisho zitachukuliwa.
Kama mashtaka yatatolewa dhidi ya mtu mzima kuhusu utendaji usiofaa
kwa mtoto tutaheshimu haki za mtu huyo na kushughulikia masuala yote
yanayohusu suala hilo kwa siri
Tuna wajibu wa kufanya shughuli zetu kwa uwiano na ushauri wa
Mathayo 7:12

KANUNI YA MIEZI SITA & UCHAGUZI WA WANAOJITOLEA


Weka kanuni ya utendaji ambayo inasema kwamba hakuna mtu yeyote
atakayechukuliwa kwa nafasi ya uongozi wa kujitolea katika programu za
huduma za watoto zinazofadhiliwa na kanisa hadi amekuwa mshiriki wa
kanisa kwa zaidi ya miezi (6) sita
Watake wanaojitolea wote kujaza fomu ya taarifa kuhusu Huduma ya
kujitolea ili kuchukuliwa kama mteule katika huduma ya kujitolea katika
kanisa lako
Chagua kamati ndogo (washiriki 3 – 5) ya tathmini ya huduma ya kujitolea
ili kufanyia kazi tathmini ya wateule wote wa kujitolea katika programu za
huduma ya watoto
Amua ngazi sahihi katika kuchuja wanaojitolea inayohitajika kwa ajili ya
nafasi zote za kujitolea zinazohusu programu za huduma za watoto
Endesha mchujo wa ngazi ya msingi kwa ajili ya watu wazima wote
waliojitolea ambayo itahusisha vipengele vifuatavyoc:
Kusailiwa na kiongozi wa idara ya huduma za watoto kwa kila
aliyeomba kujitolea kwa mfano, kiongozi wa Idara ya Shule ya Sabato,
mkurugenzi wa Watafutanjia, mkurugenzi wa Wavumbuzi nk…
Ukamilishaji wa fomu ya taarifa ya huduma ya kujitolea na kusainiwa na
mtu mzima anayejitolea
Taarifa zote zinazopokelewa na fomu ya taarifa za huduma ya kujitolea
zitatunzwa na kanisa mahalia kwa hali ya usiri na kufungiwa katika faili
lililofungwa.

NGAZI ZA MCHUJO WA HUDUMA YA KUJITOLEA


NGAZI YA MSINGI – Wanaojitolea Wote
Usaili binafsi wa maombi ya kujitolea
Kujaza fomu ya taarifa ya huduma ya kujitolea pamoja na sahihi
Alama za udhamini binafsi kutoka kwenye kamati ya mchujo
NGAZI YA KATI – Wanaojitolea wenye uwezo mkubwa wa maingiliano na
watoto pamoja na kuhusika katika shughuli nje ya maeneo ya kazi
Mambo yote ya mchujo ngazi ya msingi pamoja na
Kutembelea nyumbani na kutazama
Kuchunguza historia ya makosa ya jinai na kupata uhakika katika ofisi ya
msajili wa makosa ya kingono – hii inaweza ikahitaji alama za vidole na
ruhusa ya maandishi ya anayeomba ili kupata ruhusa ya kuona taarifa hizi
kutoka kwenye vyombo vya dola
NGAZI YA UPEO MPANA – Wanaojitolea walio na uhusiano wa ana kwa ana na
watoto kwa mfano ndugu mkubwa msaidizi anayeishi nyumbani au nje ya
nyumbani nk.
Mambo yote ya mchujo wa ngazi ya msingi na ya kati, pamoja na
Uchunguzi wa historia ya kijasusi
Uchunguzi wa unyanyasaji wa watoto
Tathmini ya akili
Mchujo makini wa wanaojitolea unahitaji kutambua utume wa taasisi na shughuli
zingine za wanajitolea zilizo za muhimu ili kukamilisha utume huo. Wabunifu wa
mchujo makini lazima pia watambue utayari wa wanaojitolea katika kuachia
sehemu ya ufaragha wao kwa ajili ya mema. Mchujo lazima ufanyike kwa usahihi
kiasi cha kuwa na mguso katika unyanyasaji wa watoto, lakini usiingilie ufaragha
wa wanaojitolea zaidi ya inavyohitajika kwa ajili ya usalama wa watoto
wanaofanya kazi nao. Kila taasisi inayohudumia vijana inapaswa kuelewa
kwamba hata wanaojitolea waliochujwa vizuri bado wanaweza kuwa hatari kwa
watoto wanaofanya nao kazi.
Chanzo: The National Assembly of Nationa Volunteer Health & Social Welfare Organizations – National
Collaboration for Youth – Screening Guide for volunteers

NYENZO KWA AJILI YA HUDUMA YA KUJITOLEA


Taarifa za huduma ya kujitolea kwa ajili ya Huduma ya watoto (Muundo wa
Kanisa)
Sera ya usalama wa watoto na mwongozo wa mchakato (Muundo wa
kanisa)
Fomu ya wafanyakazi wa huduma kujitolea ya Huduma ya Watoto –
Divisheni ya Amerika Kaskazini – Idara ya Huduma za Watoto
HUDUMA YA KUJALI – KUPUNGUZA VIZUIZI ILI KUPATA USHIRIKIANO
Siku zote weka MKAZO wako katika Utume wako
Alika watu kuomba nafasi ya kujitolea katika programu yako ya huduma za
watoto na uendeshe mafunzo-elekezi ili programu yako iweze kupata watu
wanaovutiwa katika huduma yako
Yesu alithamini kwa upeo mkubwa zoezi la kuwalinda watoto (Mathayo
18:1-6), ni kwa sababu hii zoezi hili la kuwalinda watoto ni kigezo muhimu
katika Huduma za Watoto, na hivyo watu wazima wanatazamiwa kuwa na
mwenendo ulio sawa sawa na kanumi za Biblia muda wote katika namna
wanavyoingiliana na watoto katika kanisa lako.
Ili kuweka mfano, viongozi wote wa huduma za watoto hawana budi
kushiriki katika program ya mchujo hata kama wamekuwa wakijitolea kwa
miaka mingi katika kanisa lako.
Epuka kuingia katika malumbano marefu kuhusu sababu kubwa
zinazolazimu kuchuja wanaojitolea katika kanisa lako. Maswali kama hayo
yashughulikiwe katika vikao vya faragha vinavyohusisha mhusika
anayeuliza mwenyewe na uongozi.
Pitia kwa uangalifu taarifa zilizopo kwenye fomu ya kila mwombaji wa
kujitolea ili kujiridhisha kwamba zimejazwa ipasavyo na kuthibitishwa kwa
sahihi ya mwombaji.
Ikiwa kuna fomu ambayo haijajazwa vizuri, mkaribishe mhusika ili
aikamilishe na kuikabidhi. Panapokuwa na kipingamizi kwa swali lolote
katika fomu, basi lishughulikiwe kwa pamoja na mhusika ili kumpatia nafsi
ya kushiriki kwenye mchujo. Hii itaakisi weledi katika zoezi zima huku
ukilenga katika utume wako.
Usiendeshe zoezi la mchujo kwa njia za mkato. Wale wote wanaojitolea
lazima watimize matakwa ya ngazi ya msingi ya mchujo.
Ikiwa mwombaji ataendelea kukataa kushirikiana katika hatua zilizowekwa
za mchakato wa mchujo, basi asiruhusiwe kutumika katika nafasi ya
kujitolea inayowahusisha watoto
VIGEZO MUHIMU VYA MAFUNZO KWA WANAOJITOLEA
Elimu kuhusu utume wa program ya Huduma za Watoto
Uelewa wa matazamio, mwenendo kimaadili na kanuni zitakazofuatwa
katika program kuhusiana na muingiliano na watoto.
Kutambua uwepo wa elimu kuhusu kunyanyaswa kwa watoto (kimwili, na
kingono) na hatua ambazo kanisa lako limechukua ili kuzuia uwezekano wa
kutokea unyanyasaji katika program yako.
Elimu yenye mguso mzuri na mbaya na mafunzo kuhusu jinsi ya kuthibitisha
watoto kwa namna iliyo nzuri.
Elimu ya jinsi ya kuamua ngazi iliyo sahihi ya usimamizi katika kuendesha
program yao kwa jinsi iliyo salama muda wote.
Kuweka wazi kwamba kushindwa kukubaliana na mwenendo na maadili
ambayo yamewekwa na kanuni kunaweza kuwa na matokeo ya
kusimamishwa katika zoezi zima la kujitolea katika program.
Tumia washiriki wenye taaluma (Waalimu, Madaktari, wanasheria,
wafanyakazi wa jamii n.k.) katika familia yako ya kanisani na uwaalike
wakusaidie kutenda kazi katika kuwapatia mafunzo wanaojitolea ili kuleta
kuaminika na msaada katika juhudi zako za ulinzi wa watoto
Shirika la uangalizi wa Bima linatoa miongozo hii na fomu hizi ili kusaidia
maendeleo ya programu za usalama na uangalizi wa hatari. Shirika la
Waadventista wa Sabato la usimamizi wa Bima haliwajibiki katika uongozi wa
shughuli zilizowekewa bima ya usalama. Dhima ya ukomo kwa upande wa Shirika
la Waadventista la uangalizi wa hatari inakanushwa hapa

TAMKO LA KUSUDI NA SERA YA HUDUMA ZA WATOTO


KUHUSU ANAYEJITOLEA
(TAMKO LA KUSUDI)
Makutano pamoja na wafanyakazi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato la
__________________________ wamejitoa katika kuhakikisha kuna mazingira
salama ya kusaidia watoto kujifunza upendo na kumfuata Yesu Kristo. Kwa
wakati huu, ongezeko la majeraha ya janga la unyanyasaji wa kimwili na wa
kingono linalosumbua watoto limeteka usikivu wa taifa letu, jamii yetu na
kanisa letu. Makanisa yenye Programu kwa ajili ya watoto sio kwamba yana
kinga dhidi ya wale wanaonyanyasa watoto.
Kwa hiyo, Kanisa la Waadventista wa Sabato la _____________________
linaamini kwamba ni muhimu kuchukua hatua za kuhakikisha kwamba kanisa
na programu zake, kwa uwezo wake zinakuwa salama na kutoa uzoefu wa
furaha kwa watoto na vijana.
Sera zifuatazo zimesimikwa na kuakisi ahadi yetu ya kutoa ulinzi kwa watoto
wote wanapohudhuria shughuli au programu zozote zinazofadhiliwa na kanisa
katika kanisa la _________________________
(TAMKO LA SERA)
I. Mtu anayejitolea kufanya kazi na watoto na vijana anapaswa:
a) Kuwa mshiriki hai wa kanisa angalau kwa miezi sita (6), isipokuwa kama
upekee umetolewa na kamati ya tathmini ya huduma za kujitolea na
kuthibitishwa na baraza la kanisa.
b) Lazima ajaze na kutia sahihi fomu ya taarifa ya Huduma za kujitolea na
kuiwakilisha kwenye kamati ya tathmini ya huduma za kujitolea kwa ajili
ya kuchujwa na kupitishwa.
c) Wote wanaoomba kujitolea watawakilisha udhamini binafsi ambao
utapitiwa na kamati ya tathmini ya huduma za kujitolea.
d) Wote wanaojitolea wanategemewa kutegemeza na kukubaliana na
masharti ya utendaji kazi yaliyowekwa kwa ajili ya huduma ya kujitolea
katika kanisa la Waadventista wa Sabato la_______________________

II. Wafanya kazi wote wanaokutana na watoto lazima washike sheria ya


“watu wawili” ambayo ina maana kwamba wafanya kazi lazima waepuke
kuwa peke yao na watoto nyakati zote.
III. Programu zote za watoto na vijana lazima zitoe angalau watu wazima
wawili ili kusimamia shughuli za watoto na vijana.
IV. Watu wazima waliotendewa unyanyasaji wa kimwili au wa kingono wakiwa
watoto wanahitaji upendo na kukubaliwa na familia ya kanisa. Mtu aliye na
historia ya aina hiyo lazima azungumze na mmoja kati ya wachungaji na
kueleza hitaji lake kufanya kazi na watoto na vijana, katika mahojiano ya
siri, kabla ya kupata kibali cha kufanya kazi katika maeneo hayo
V. Watu ambao wametenda unyanyasaji wa kimwili au kingono na wale walio
katika uchunguzi, wawe wamehukumiwa au la, hawapaswi kufanya kazi
katika shughuli au programu zozote zinazofadhiliwa na kanisa
zinazohusisha wanafunzi, watoto au vijana.
VI. Nafasi za mafunzo katika kuzuia na kutambua unyanyasaji wa watoto
yatatolewa na idara mbalimbali za kanisa letu. Wafanya kazi katika maeneo
haya wanategemewa kushiriki katika mfunzo hayo
VII. Wafanya kazi lazima watoe taarifa haraka kwa mchungaji au kwa uongozi
wa kanisa tabia yoyote au matukio yoyote yanayoashiria unyanyasaji au
yasiyofaa. Taarifa inapotolewa, hatua zinazofaa zitachukuliwa. Hatua hizi
zinaweza zikajumuisha miongozo na sera zifuatazo za ofisi za Konferensi
ya ____________________________________ itifaki za utendaji kazi
zilizowekwa na kanisa hili kulingana na sheria za taifa na za makosa ya jinai.
VIII. Miongozo itatolewa kwa ajili ya wanaojitolea kufanya kazi na watoto na
vijana kwa kila anayejitolea.

Imepigiwa kura na baraza la kanisa la: ________________________________


Tarehe _______________________________
KUTAMBUA CHANZO:
Kanisa la Waadventista Wasabato Azure Hills na Konferensi ya Kusinimashariki mwa California

Shirika la uangalizi wa hatari linatoa miongozo hii na fomu hizi ili kusaidia maendeleo
ya programu za usalama na uangalizi wa hatari. Shirika la Waadventista la uangalizi
wa Hatari haliwajibiki katika uongozi wa shughuli zilizowekewa bima ya usalama.
Dhima ya ukomo kwa upande wa Shirika la Waadventista la uangalizi wa hatari
inakanushwa hapa
SERA NA TARATIBU ZA ULINZI WA WATOTO KATIKA
KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO
(MUUNDO WA MATENDO BORA)
UTUME: Utume wetu ni kutoa mazingira yaliyo salama, ya kiroho na yasiyo na
unyanyasaji kwa kila mtoto anayeshiriki programu na shughuli za Kanisa la
Waadventista wa Sabato la ___________________________
MALENGO: Ni lengo letu kuzuia kila aina ya unyanyasaji wa watoto, kimwili,
kihisia au kingono na kulinda waajiriwa wetu na watu wetu wanaojitolea dhidi
ya mashtaka ya uongo kuhusu matendo kama hayo.
TAFSIRI:
Mtoto – shule ya awali hadi shule ya msingi
Mtoto mkubwa – vijana wadogo hadi vijana waliopevuka
Unyanyasaji wa watoto – ni tendo lolote kwa mtoto linalotishia usalama wa
mtoto au linaloacha maisha yake yakiwa na makovu ya kimwili au kihisia. Ni
pamoja na matendo yote yasiyofaa kimwili, kingono au mawasiliano ya mtu
mzima yoyote kupitia matumizi ya mamlaka juu ya mtoto. Unyanyasaji pia
unaweza ukatokea kati ya watoto wawili. Hata kama ni kutokana na
kutokuelewa kwa mtoto, kutokuwa na hatia au hofu zinazoweza kuchangia ni
njia za unyanyasaji.
Unyanyasaji wa kimwili – ni jeraha lolote kwa mtoto ambalo limesababishwa
na njia zozote za ajali, pamoja na majeraha yanayoonekana kuhitilafiana na
maelezo ya jeraha hilo.
Unyanyasaji wa kihisia – ni mawasiliano yoyote ya mdomo yanayomuathiri
mtoto, kama vile kumshusha hadhi, kumdhalilisha, kumuita majina yasiyofaa,
maneno ya kumdharau, lugha ya kikatili au lugha chafu, nk.
Unyanyasaji wa kingono – kuvunja ufaragha wa jinsia ya mtoto iwe kwa
kumshika, kumsisimua kwa macho au kwa maneno. Inajumuisha kushika
sehemu zozote za binafsi za mtoto, kuingiza vitu mdomoni, sehemu za siri
au/na kinyume na maumbile, kumuambia au kumwomba mtoto kuwezesha
kujichua, kuonyesha sehemu za siri kwa mtoto, kumruhusu mtoto kushuhudia
au kuangalia namna yoyote ya shughuli za kingono, kuonyesha picha za ngono,
nk…
UTARATIBU:
Wafanyakazi wote na wale waliojitolea kufanya kazi na watoto, lazima
wajaze fomu ya wafanyakazi wa Huduma za Watoto. Hakuna mabadiliko
yanayoruhusiwa katika fomu hii bila ruhusa ya baraza la kanisa kwa ushauri
wa kisheria.
Wafanyakazi wote na wote wanaojitolea, wanakubali kufuata sera na
utaratibu wa ulinzi kwa watoto wa Konferensi ya ____________________
Washiriki wapya wanaotamani kufanya kazii na watoto na vijana lazima
wawe washiriki hai wa kainsa mahalia angalau kwa miezi sita (6) kabla
hawajaruhusiwa kufanya kazi na watoto.
Watu wazima watasiamia programu na shughuli za watoto nyakati zote. Hii
ina maana kwamba siku zote kutakuwa na angalau watu wazima wawili (2)
wanaosimamia tukio lolote ili kuepuka hali zifuatazo:
Wafanyakazi wataepuka kuwa wenyewe na watoto nyakati zote. Hii
itawalinda wote mtoto na mtu mzima kutoka kwenye hatari au
mashtaka yoyote.
Mtoto hatasaidiwa kutumia maliwato isipokuwa kuna mtu mzima wa
pili karibu na eneo hilo anayeelewa sababu ya msaada huo
Hakuna mtoto atakayeadhibiwa isipokuwa kwa kukutana na mtu
mzima mwingine ambaye anaelewa hali inayohitaji adhabu. Adhabu
zozote kali zinazuiliwa vikali.
Hakuna “mtoto” (kwa maana iliyotajwa hapo juu) atakayeachiwa kwenda
maliwatoni isipokuwa mzazi, mlezi au watu wazima wawili wakimsindikiza
Inashauriwa kwamba shughuli au programu zozote za watoto kufanyika
kwenye madarasa au ofisi zenye madirisha kwa ajili ya uangalizi rahisi.
Vyumba vyote vinapaswa kufungwa wakati wote.
Kila shughuli au programu inayofadhiliwa na kanisa inayohusisha watoto
wa umri mdogo inayofanyika nje ya kanisa lazima iwe na ukubali wa
viongozi wa kanisa.
Baraza la kanisa lazima lipitishe shughuli au safari zozote za usiku kabla
hazijafanyika. Watoto wote wa umri mdogo wanaoshiriki katika shughuli
hizi lazima wawe na ruhusa iliyosainiwa na mzazi kwa ajili ya kila safari
pamoja na barua ya dharura ya afya. Wazazi na/au waleziwatapewa taarifa
ya watu wazima ambao watahusika katika shughuli au safari hiyo.
Tabia yoyote inayoonekana kuwa ya kinyanyasaji au isiyofaa itaripotiwa
kwa kiongozi wa kanisa au mchungaji kwa ajili ya uchunguzi.
Washiriki wanaofahamu mtu yeyote aliyehukumiwa, aliyekiri bila kubisha,
au kuamuliwa kwamba alitenda unyanyasaji wa kimwili au kingono na
anashiriki ibada mara kwa mara, wanapaswa kumshauri mchungaji juu ya
taarifa hii. Uongozi wa kanisa utahusika kutoa uangalizi zaidi kwa mtu huyo
anaposhiriki katika matukio ya kanisa.
Watu ambao wamewahi kuhukumiwa au kukiri au kuashiria kuwa
wamewahi kuhusika kwa namna moja au nyingine katika unyanyasaji wa
kimwili au kingono wasiruhusiwe kushiriki katika kujitoela katika Idara ya
Huduma za Watoto inayofadhiliwa na kanisa lolote, au vijana wadogo na
wakubwa, au program ya raia wa daraja ya juu au shughuli nyingine zozote.
Imepigiwa kura na baraza la kanisa la: ___________________________
Tarehe: ___________________________
CHANZO
Kanisa la Waadventista Wasabato Beltsville na Konferensi ya Potomac

Shirika la uangalizi wa hatari linatoa miongozo hii na fomu hizi ili kusaidia maendeleo
ya programu za usalama na uangalizi wa hatari. Shirika la Waadventista la uangalizi
wa Hatari haliwajibiki katika uongozi wa shughuli zilizowekewa bima ya usalama.
Dhima ya ukomo kwa upande wa Shirika la Waadventista la uangalizi wa hatari
inakanushwa hapa

ADVENTIST RISK MANAGEMENT, INC.


Kutoa Ufumbuzi … Kupunguza Hatari
SAMPULI YA FOMU YA MAOMBI YA
HUDUMA YA KUJITOLEA

Jina: ___________________________________________Jinsia: _________


Anwani:_______________________________________________________
______________________________________________________________
Simu: _________________________________________________________
Barua pepe: ___________________________________________________
Namba ya leseni ya udereva: ______________________________________
Namba ya mfuko wa hifadhi ya jamii: _______________________________
Kazi: _________________________________________________________
Mwajiri: _______________________________________________________
Tarehe ya kuzaliwa: _____________________________________________
Hali ya Ndoa: __________________________________________________
Jina la mwenzi: _________________________________________________
Majina ya watoto na umri: ________________________________________
______________________________________________________________
Nafasi inayohitajika: _____________________________________________
Programu ya watoto: ____________________________________________
Ngazi ya umri: __________________________________________________
Uzoefu wa huduma nyingine (Programu, Ngazi ya umri, nafasi)
______________________________________________________________
______________________________________________________________
Ushirika wa kanisa: ______________________________________________
Anwani ya kanisa lako: ___________________________________________
Umekuwa ukishiriki katika kanisa hili kwa muda gani? __________________
Tarehe ya usharika: ______________________________________________
______________________________________________________________
Andika tamko fupi la kile unachoamini katika Ukristo: _________________
______________________________________________________________
______________________________________________________________
______________________________________________________________
Tafadhali weka udhamini wa watu wawili wasiokuwa familia (watu hao
wanapaswa kuwa nje ya kanisa):
Jina: __________________________________________________________
Anwani: _______________________________________________________
______________________________________________________________
Simu: _________________________________________________________
Jina: __________________________________________________________
Anwani: _______________________________________________________
______________________________________________________________
Simu: _________________________________________________________

Umewahi kukamatwa na polisi, kupelekwa mahakamani, kuhukumiwa kwa


kosa la jinai? ___________________________________________________
Kama ndiyo tafadhali elezea: ______________________________________
______________________________________________________________
______________________________________________________________
______________________________________________________________

Ninahakikisha kwa ufahamu wangu kwamba taarifa nilizotoa katika fomu hii
ni sahihi. Ninaruhusu udhamini au kanisa liloorodheshwa kwenye fomu hii
kutoa taarifa yoyote kuhusu tabia yangu na uwezo wangu wa kufanya kazi na
watoto. Kwa hayo ninaachilia taasisi yoyote au mtu yoyote kutoka kwenye
deni litakalosababishwa na mimi.

Sahihi: _______________________________ Tarehe: _________________


MFANO WA FOMU YA UDHAMINI

Jina la mwimbaji: _______________________________________________


Anwani: _______________________________________________________
______________________________________________________________
Umemfahamu mwombaji kwa muda gani na kwa upeo gani? ___________
______________________________________________________________
______________________________________________________________
Toa maoni kuhusu historia ya familia ya mwombaji. ___________________
______________________________________________________________
______________________________________________________________
Toa maoni yako kuhusu tabia na utu wa mwombaji. ____________________
______________________________________________________________
______________________________________________________________
Toma maoni yako kuhusu safari ya kiroho ya mwombaji. ________________
______________________________________________________________
______________________________________________________________
Kutokana na ukadiriaji wako, mwombaji anafaa jinsi gani kufanya kazi na
watoto? _______________________________________________________
______________________________________________________________
______________________________________________________________
Unaweza ukampendekeza mwombaji huyu? _________________________

Bila shaka kwa mashaka kidogo Hapana kabisa

Jina la mdhamini: _______________________________________________


Anuani: _______________________________________________________
______________________________________________________________
Kanisa: ________________________________________________________
Cheo au kazi: ___________________________________________________

Sahihi ya mdhamini: ________________________ Tarehe: ______________

D. JINSI WACHUNGAJI NA WAZEE WANAVYOWEZA KUSAIDIA KUCHUJA


WANAOJITOLEA
Chagua kamati ya mchujo
Toa msaada katika kuchuja waliojitolea
Pitia udhamini wa waliojitolea
Toa msaada kwenye maamuzi ya kamati ya mchujo

3. HALI YA KIROHO YENYE MSISIMKO

Lengo kuu la programu za watoto ni kulea watoto katika kukua kwao


kiroho jinsi wanavyoendeleza uhusiano wa upendo na kutumika pamoja na
Yesu. Kuendeleza hali ya kiroho ni kazi ya wote kanisa na familia. Katika
kanisa, Shule za Sabato za Watoto zinaratibiwa ili kutoa elimu ya kidini kwa
watoto kusoma Biblia na kuhusika katika shughuli zitakazowaongoza
kuamua kumfuata Yesu kama rafiki na Mwokozi wao. Ni muhimu kwamba
wachungaji na wazee wawatie moyo familia ili kuwekeza katika masomo ya
Biblia kwa ajili ya watoto wao.

A. MTAALA WA KIUNGO CHA NEEMA (GRACELINK)

Mwaka 2000, mtaala mpya wa Shule ya Sabato unaoitwa ‘Kiungo cha


Neema’ (GraceLink) ulianzishwa kwa ajili ya kanisa la watoto ulimwenguni.
Masomo haya ya Biblia yanafundisha dhana ya neema, yakitumia njia ya
kujifunza kwa vitendo njia inayohusisha watoto kupitia uzoefu wa somo la
Biblia, na kulifanyia kazi katika maisha yao. Changamoto kubwa inayokumba
makanisa mahalia ni namna ya kuwapa mafunzo waalimu wa Shule ya
Sabato ya watoto juu ya jinsi ya kuuzoea mtaala huu mpya hata kama
yawezekana hawahusiki moja kwa moja katika kuufundisha. Chunguza
kurasa zifuatazo ambazo zitakupatia taswira ya ‘Kiungo cha Neema’.
HISTORIA YA KIUNGO CHA NEEMA

Mtaala mpya wa Shule ya Sabato kwa ajili ya watoto ni matokeo ya utafiti


makini wa soko uliofanyika kati ya
viongozi wa watoto katika nchi ya
Marekani na Kanada (1995), ambayo
baadaye ilithibitishwa kwa utafiti katika
sehemu zingine za dunia. Viongozi hawa
walituambia wanataka mtaala wa
“Kiadventista” hasa, uliojikita katika
mafundisho ya Biblia. Walitaka hasa
masomo ambayo yatawahusisha watoto
kivitendo katika mchakato wa kujifunza,
masomo yatakayoleta dhana ya neema,
na kuongoza katika kuwa na uhusiano
binafsi na Kristo.
Wakati viongozi wa Kanisa walipogundua elimu ya dini inayoongezeka
katika idadi kubwa ya watoto wa Kiadventista ilikuwa imewekwa mikononi
mwa wachapishaji wa vifaa vya Waadventista, walipiga kura kutafuta
rasilimali zinazohitajika ili kuanzisha kitu kipya. Mwaka 1996, Kamati ya
Mtaala ya Halmashauri Kuu ilikubali ombi la mtaala mpya.
Mtaala wa “miaka kumi na mbili” kwa watoto wenye umri wa kuanzia
kuzaliwa hadi miaka 14 una masomo 624. Kuanzishwa kwa mtaala wa msingi
na mahitaji yake kulikabidhiwa kwa Kituo cha John Hancock kwa ajili ya
Huduma ya Vijana katika chuo cha La Sierra, ukisimamiwa na Dk. Bailey
Gullespie na Stuart Tyner. Idara ya Shule ya Sabato ya Halmashauri Kuu,
chini ya uongozi wa Dk. Patricia Habada, ilitambua na kusimamia wataalamu
waliokuwa wakiwakilisha divisheni zote ulimwenguni katika kuandika
masomo mapya na shughuli za programu. Review and Herald pamoja na
taasisi ya Uchapishaji ya Pasifiki walijitoa kikamilifu katika rasilimali zao ili
kuzalisha kazi mpya ya sanaa yenye rangi nne kwa ajili ya kila ngazi ya umri,
ambpo waliyatoa masomo hayo kwa divisheni zote bila gharama.
Kizazi kipya cha Waadventista sasa kina nafasi ya kukazia katika nyanja
nne za uzoefu wa Ukristo unaokua – Neema, Ibada, Huduma na Jamii.
Watoto watatiwa changamoto kila wakati kufanyia kazi mafundisho ya
Biblia katika maisha yao ya kila siku. Waalimu na wazazi wanaweza wakawa
na ujasiri kwamba watoto watafurahia masomo tofauti ya Waadventista wa
Sabato katika mazingira chanya, ya kuhusisha kila mmoja na yanayotia moyo
usharikia hai kama washiriki wa kanisa na raia wema wa dunia.

Utume wa mtaala wa ‘Kiungo cha Neema’ ni:


Kusaidia watoto wafurahie kupata uzoefu wa neema ya Mungu na kuitikia
kwa
Kuonyesha upendo kwa Mungu (ibada)
Kuonyesha upendo kwa familia na marafiki (jamii)
Kuhudumia wengine katika dunia yao (huduma) kama washiriki hai wa
familia ya Mungu sasa na siku zote.
Malengo ya ‘Kiungo cha Neema’ ni:
Kulea uhusiano binafsi na Yesu Kristo
Kuingiza mafundisho ya neema
Kujenga watoto katika Neno la Mungu
Kuingiza wajibu wa kimaadili
Kukaribisha utofauti
Kuhusisha watoto katika Huduma isiyo ya ubinafsi
Kuamsha ushuhuda wa asili wa ushindi
Kukuza hali ya kujitambua kama wana na binti za Mungu

FALSAFA
Nguvu nne za msukumo wa kukua kwa uzoefu wa Ukristo zinatoa msingi
wa ‘Kiungo cha Neema’. Misukumo hii ni:

Neema: Yesu ananipenda. Amechukua hatua ya kulipa gharama ya dhambi


zangu na kunipatia uzima wa milele kama mtoto Wake, na uwezo kamili wa
kukua na kuwa kama Yeye.

Ibada: Ninampenda Yesu. Ninaweka maisha yangu kwake nikishurkuru kwa


kile alichofanya kwa ajili yangu. Siombi tu na kumwabudu, lakini pia ninatii
amri zake kwa sababu ninafahamu anajua kile kilicho bora kwa ajili yangu.

Jamii: Yesu anakupenda pia. Furaha ya kweli inatoka katika kuhudumia


wengine, na katika kupeleka habari njema za upendo wa Yesu kwa dunia
nzima.
MIZUNGUKO YA DIVISHENI

AWALI: Mtaala wa darasa la awali unajumuisha mzunguko wa miaka miwili


unapendekezwa kwa watoto wenye umri wa kuanzia kuzaliwa hadi miaka
miwili. Hii inaleta uwezekano wa kujirudia rudia. Hata hivyo, kulingana na
mabadiliko yaliyotokana na ukuaji wa uelewa, somo moja litamaanisha kitu
tofauti kabisa kwa watoto wa umri wa miezi 22 kuliko katika miezi 2. Badala
ya kujifunza kisa kipya kila juma, wale wa darasa la awali watajifunza kisa
kimoja kwa mwezi.

CHEKECHEA: Watoto wa chekechea pia wana masomo ya mzunguko wa


miaka miwili yanayopendekezwa kutumiwa kwa watoto wenye umri wa
miaka 3 hadi 5. Mara nyingine tena, wale wa miaka 5 hawatajali kusikia tena
kisa walichojifunza wakiwa na miaka 3.

MSINGI: Ngazi ya shule ya msingi ina mzunguko wa miaka minne, Ngazi hii
inapendekezwa kwa watoto wenye umri miaka 6 hadi 10. Wazazi
wanategemewa kujifunza na watoto walio wadogo. Baadhi ya maswali ya
kujifunza kila siku yatakuwa magumu kwa watoto wadogo na yanaweza
kuondolewa na wazazi. Kwa sababu ule muda wa Shule ya Sabato
umejengeka katika shughuli za vitendo, basi kila mmoja darasani anahusika.

VIJANA WADOGO: Ngazi ya vijana wadogo pia ina mzunguko wa miaka


minne. Inapendekezwa kwamba makanisa yapitie kwa uangalifu na
kukamilisha mzunguko wote wa miaka minne iwe kwamba ngazi hii ya
vijana wadogo itagawanywa katika makundi mawili – vijana wadogo na
vijana wa kati (waliopevuka)* au iwe kwamba vijana wadogo na vijana wa
kati watakutana pamoja.

*Imani ya ya wakati uliopo ni kifaa kingine maalum kwa ajili ya vijana wa kati (Umri miaka 12 -14)
wanapokutana tofauti na vijana wa wadogo.

MUUNDO WA SHULE YA SABATO

A. Ingiza lesoni siku ya Sabato. Watoto wanapitia na kufanyia kazi kanuni


walizojifunza katikati ya juma kwa msaada wa wazazi wao na miongozo
yao ya kujifunza Biblia. Kwa njia hii, masomo waliojifunza katika Shule ya
Sabato yanakuwa sehemu ya muhimu katika uzoefu wa kukua kwa imani
ya mtoto. Mafungu ya kukariri, ambayo pia wanajifunza katika Shule ya
Sabato, yanapitiwa na kutiliwa mkazo katika juma linalofuata,
yakiunganishwa katika akili ya mtoto na shughuli za kufurahisha za
kujifunza ambazo wameshazoea.
B. Tilia mkazo wakati wa Shule ya Sabato katika ujumbe mmoja. Kila
ujumbe unahusiana na moja kati ya nguvu zile nne za msukumo wa
kukua kwa uzoefu wa imani: neema (Mungu ananipenda), ibada
(ninampenda Mungu), jamii (tunapendana), na huduma (Mungu
anakupenda pia).
C. Mfikie kila mtoto kwa njia anayojifunza zaidi. Kila mpangilio wa
kufundisha umejengeka katika mtiririko wa kujifunza kwa asili. Kwa
kufuata mtiririko huu, wanafunzi wataunganishwa na ujumbe wa juma
kwa njia ambayo itavuta usikivu na mawazo ya kila mmoja.
D. Wape wanafunzi uzoefu wa kujifunza kwa vitendo ili kuwapa utayari
wa kuweza kutafakari kwa kina kweli zilitolewa. Uzoefu huu unapaswa
kufuatiwa na vipindi vya kuuliza maswali ambayo yatawaongoza katika
kutafakari kile walichojifunza, kutafsiri uzoefu, na kufanyia kazi taarifa
hiyo katika maisha yao.
E. Husisha mfanyakazi wa Shule ya Sabato ya watu wazima kwa namna
mpya isiyomfanya akabakia pale kwa kudumu
mtu mzima mmoja anaweza akaoongoza Shule ya sabato ndogo.
Shule ya Sabato kubwa inaweza ikaongozwa na kiongozi/mwalimu
mmoja, pamoja na watu wazima wengine wanaojitolea ili kuwezesha
mahusiano ya kikundi kidogo.

JUMLA YA SAA ZA KUJIFUNZA NA MTIRIRIKO WA ASILI WA KUJIFUNZA

Pamoja na ‘Kiungo cha Neema, saa nzima ya shule ya Sabato inatolewa


kwa ajili ya somo. Vipengele vine vinajumuisha
1. Shughuli za kujiweka tayari;
2. Somo la Biblia;
3. Kuweka somo katika utendaji na
4. Kushirikishana somo.

Shughuli za kujiweka tayari. Shughuli hizi zimetayarishwa ili kuwapatia


watoto uzoefu wa kujihusisha.
Wanaingiza dhana ya somo kwa njia ya ubunifu na ya kufurahisha,
ikiwasaidia kuunganisha mawazo ya mtoto na hisia pamoja kwenye dhana
ya somo. Angalau shughuli 2 - 3 zinapendekezwa kwa ajili ya kila somo.
Kuuliza maswali. Baada ya kila shughuli watoto wanapatiwa nafasi ya
kusema jinsi shughuli hiyo ilivyowafanya wajisikie na kuwaruhusu kupata
maana ya kiroho kutoka kwenye shughuli hiyo na kwenye kisa cha Biblia
kilichobeba shughuli hiyo.
Viongozi na waalimu wanapaswa kuuliza maswali matatu ya muhimu
katika kipindi cha maswali:
Kutafakari – unajisikiaje kuhusu kile tulichofanya?
Kutafsiri – ina maana gani kwako?
Utendaji – unakwenda kufanya nini kuhusu hilo?
Somo la Biblia. Hii ni nafasi kwa ajili ya watoto kuangalia somo na
kulichunguza kuona kile Mungu anachojaribu kuwaambia. Kisha
wanajifunza kufanyia kazi somo katika maisha yao ya kila siku.
Kushirikisha somo. Huu ni wakati kwa watoto kuitikia somo. Wanaweza
kujipanga kuitikia kama kundi, ili wafundishe watu wengine kile
walichojifunza, au fanya kitu kushirikisha watu wengine fungu la kukariri.
MCHORO WA MZUNGUKO WA KUJIFUNZA

4
1

B. KUWAKUZA KIROHO VIONGOZI WA WATOTO


Pamoja na kuwasaidia watoto kukuza hali zao za kiroho, wachungaji na
wazee wanashika nafasi ya muhimu katika kulea na kuwa mfano kwa
viongozi wa watoto katika makuzi yao ya kiroho. Kuwa mfano wa kiroho
kwa viongozi vijana wasio kuwa na uzoefu mkubwa kunazaa matunda
mengi baadaye. Kanisa litakuwa na viongozi imara wa kiroho katika
miaka inayokuja. Kanisa linalositawi linatengenezwa.
Kwa nini uwe mlezi na mfano wa kuigwa (Mshauri/Mnasihi)?
Viongozi vijana wasiokuwa na uzoefu wa kutosha wanahitaji mshauri

Sababu za kuwa Mshauri


Maadili yanafundishwa kwa wale wanaoshauriwa
Inaendeleza stadi za uongozi
Inatengeneza nafasi ya kushirikishana imani
Inajenga kujiamini kwa anayeshauriwa
Inaruhusu mashauri juu ya masuala ya maisha
Inatoa mfano wa huduma na uwakili
Inaondoa ubinafsi kwa mshauri
Inafungua akili kwa ajili ya uwezekano mpana
Inavutia anayeshauriwa kuanzisha maisha ya maombi binafsi

Kuwa Mfano wa kuiga/Mshauri Kunakuza Karama za Roho


Mtazame anayeshauriwa ili kutambua karama maalum za roho
Toa nafasi kwa anayeshauriwa kutumia karama hizo
Mtie moyo anayeshauriwa kutumia karama za roho kwa ajili ya
huduma

Nani Anaweza kuwa Mfano wa kuigwa/Mshauri?


Mtu yoyote mwenye nia anaweza …
Kuwa mhanga
Kushirikiana na wenzake hata na muda wake
Kuwa na upendo
Kutokuhukumu na kuwa mtegemezi
Kuwa kocha
Wachungaji na wazee wanaweza kuwa.

Mawazo ya kusaidia kuanza


Omba kwa ajili ya huduma hii
Kuwa rafiki wa vijana na watoto
Watie moyo kwa kuwathibitisha – kwa majina yao
Muombe Mungu akupatie mshauri kijana

Wezesha na Toa Mafunzo


Wapatie vitu wanavyoweza kusoma ili wakue kiroho
Onyesha mfano kwa kufanya shughuli hiyo
Waruhusu wajaribu, wakishirikiana nawe
Waruhusu wajaaribu wenyewe
Wape uhakika na kuwapatia pendekezo moja au mawili
Wapeleke katika matukio ya kujifunza

C. JINSI WACHUNGAJI NA WAZEE WANAVYOLEA HALI YA KIROHO YA


HISIA KALI
Himiza familia kuwa na ibada za familia mara kwa mara na kujifunza
lesoni ya Shule ya Sabato pamoja na watoto wao.
Tangaza umuhimu wa kuwekeza fedha ili kununua masomo ya Biblia
kwa ajili ya watoto
Himiza wazazi kununua vitabu vizuri vya Kiadventista kwa ajili ya
watoto wao
Saidia kufundisha somo moja au mawili katika mgawanyiko wa
watoto wakati Fulani.

4. MIFUMO INAYOTENDA KAZI

Kanisa linalositawi linatenda kazi ndani ya mifumo ya kanisa la ulimwengu.


Kulingana na muundo wa taasisi yetu, kanisa mahalia lina jukumu na
kuwajibika kwenye konferensi, na konferensi kwa unioni, na unioni kwa
divisheni, na divisheni kwa Halmashauri Kuu. Uhusiano huu unatenda kazi
pande zote. Taasisi ya juu inawezesha konferensi kwa mafunzo na rasilimali.

A. KUFANYA KAZI NA KONFERENSI

Huduma za Watoto zinatenda kazi ndani ya muundo wa mfumo wa kanisa.


Kwa hivyo, mratibu wa Huduma za Watoto anafanya kazi na mkurugenzi wa
Huduma za Watoto wa Konferensi, akitenda majukumu yafuatayo:

Anamwalika mkurugenzi wa Huduma za Watoto wa konferensi aje


kuendesha mafunzo kwa ajili ya waalimu.
Anashauriana na mkurugenzi wa konferensi kwa mawazo na
mapendekezo katika kutengeneza program
Anatuma taarifa za shughuli za kila robo kwa mkurugenzi wa huduma za
watoto
Anahudhuria program za mafunzo ya huduma zilizoratibiwa na
mkurugenzi wa huduma za watoto
Anamwalika mkurugenzi wa Huduma za Watoto ili azungumze katika
programu kubwa za watoto.

B. KILE WACHUNGAJI WA WAZEE WANACHOWEZA KUFANYA ILI


KUTEGEMEZA MIUNDO YA KANISA
Kuchagua mratibu wa Huduma za Watoto ili kuratibu programu za
malezi kwa ajili ya watoto kanisani kwako
Toa taarifa kwa konferensi juu ya jina, anuani, na namba ya
mawasiliano ya mratibu wa Huduma za Watoto
Unga mkono programu za Huduma za watoto katika konferensi
nzima kwa kumtuma mratibu na watoto kama washiriki kwenye
matukio haya ya mafunzo

5. HUDUMA ZA IBADA ZA KUVUTIA

Tabia ya tano ya kanisa lenye afya ni uratibu wa ibada zinazovutia kwa kila
umri. Kanisa zima litajawa na msisimko wa uhai, na furaha pale washiriki
watakapojihisi kuthaminiwa na kuhusishwa. Mratibu wa Huduma za Watoto
anafanya kazi na mchungaji ili kupanga ibada ambazo zitatimiza mahitaji ya
watoto kanisani.

A. PROGRAMU ZA IBADA MAALUM KWA WATOTO


Kanisa lililo rafiki kwa watoto – hubiri, nyimbo, viti vya kanisa na vifaa
vingine viwe vinavyowafaa watoto
Sabato ya Watoto – sabato ya tatu ya Oktoba inasherehekewa na
kanisa la ulimwengu, ambapo watoto wanashiriki katika huduma ya
ibada au wanasimamia huduma yote ya ibada
Kanisa la Watoto – ibada ya kanisa lililojitenga kwa ajili ya watoto
katika eneo tofauti, ambayo inaweza kufanyika mara mbili kwa
mwezi.
Kisa cha watoto katika huduma ya ibada kanisani
B. KILE WACHUNGAJI NA WAZEE WANACHOWEZA
KUFANYA KUVUTIA IBADA
Tazama kanisa kwa macho ya mtoto
Jifunze kuwafahamu watoto kwa majina yao
Andaa mahubiri yanayohusisha watoto kwa kujibizana na kushiriki
Weka jitihada katika kuleta huduma mpya kwa watoto
Ingiza nyimbo 1 - 2 za watoto kwenye huduma ya ibada
Husisha watoto kwenye ibada, kama vile kuomba, kusoma neno, au
kukusanya sadaka.

6. VIKUNDI VIDOGO VILIVYO KAMILI

Vikundi vidogo vya watoto ni njia nyingine ya kukuza maendeleo ya kiroho


ya watoto. Kama ilivyo kwa vikosi vidogo vya watu wazima, vikundi vidogo
vya watoto pia vitakutana mara moja kwa juma katika maeneo
yaliyochaguliwa katika ujirani wa nyumba za watoto.

Watoto wanakutana kwa ajili ya maombi, kujifunza Biblia, na kujumuika


pamoja. Vikundi hivi vidogo vinaunda msingi wa kuifikia jamii ya watoto
wasio wa kanisani pale wanapoalikwa kuunganika katika shughuli hiyo.
Mratibu wa Huduma za Watoto asipuuze thamani ya vikundi hivi vidogo, na
anapaswa kuhimiza kupangwa kwa vikundi hivi.

Leo, vikundi vidogo vya watoto vimeongeza malengo zaidi ya yale ya kulea
ukuaji wa kiroho. Vikundi vidogo vinaweza vikahudumu kama vikundi vya
kutoa huduma kwa watoto ambaao wanateseka katika maumivu. Ni
kukutana kwa mioyo ambapo watoto wanapewa malezi ya kihisia kadiri
wanavyoongozwa kwa Yesu.

A. AINA YA VIKUNDI VIDOGO KWA AJILI YA WATOTO

Utume wa Watoto
Anzisha programu ya watoto katika Utume
Shule au kanisa linaweza kuwa sehemu ambapo watoto watakutanika
na wazazai wao ili kwa pamoja wafundishwe jinsi ya kuwa mitume.
Wazazi wanapata mafunzo tofauti juu ya jinsi ya kuwafanya watoto wao
kuwa wanafunzi wakati watoto wanajifunza jinsi ya kufanya kazi pamoja
na wazazi wao kama timu.
Wazazi na watoto wanazungumza, wanaulizana maswali, na wanakuwa
na masomo ya Biblia (www.kid-center.org)

Kikundi cha Maombi cha Watoto


Watoto wanakutanika katikati ya juma kwa ajili ya maombi
Wanaombea wagonjwa, marafiki zao, na mahitaji yao binafsi
Wanajifunza kumtukuza Mungu kwa ajili ya maombi yaliyojibiwa.
Kwa kawaida kipindi huanza na fungu fupi kutoka kwenye Biblia

Upinde wa Mvua
Hiki ni kikundi cha kutoa msaada kwa watoto wanaoumia na
kusononeka, kwa sababu ya kifo cha mpendwa, kutalakiana kwa wazazi,
walio na mzazi au ndugu aliye na ugonjwa mbaya, au maumivu mengine.
Watoto wanakutanika mara moja kwa juma pamoja na mratibu wa
Upinde wa Mvua wakati wanaposhirikishana hisia, hofu na maumivu
yao.
Wanajihushisha katika shughuli iliyo ya kiuponyaji, kama vile kutoa hisia
zao, kuziandika au kuchora na kupaka rangi
Watoto wanajifunza kwamba matukio haya yanatokea sio kwa sababu
wana hatia, lakini badala yake ni mambo yaliyo nje ya uwezo wao.
Watoto wanajifunza kwamba mambo ya kutia huzuni yatapita na
mwisho wake kuna upinde. Maisha bado yana thamani, hasa pale
wanapokuwa na Yesu kama kiongozi na rafiki. www.rainbows.com

B. KILE WACHUNGAJI NA WAZEE WANACHOWEZA KUFANYA KWA AJILI


YA VIKUNDI VIDOGO
Kutoa bajeti ya kuendesha programu ya Upinde au vikundi vingine
vyenye programu za kutoa msaada.
Kupeleka watu kwa ajili ya mafunzo ya Upinde
Kusaidia viongozi wa watoto wanaoendesha vikundi hivi vidogo
Kushiriki mara moja moja katika vikundi vidogo vya watoto
7. UINJILISTI ULIOJIKITA KATIKA MAHITAJI

Agizo la Yesu la kupeleka injili “kwa kila kabila, lugha na jamaa” alilowapa
wanafunzi wake bila shaka linajumuisha kupeleka injili kwa watoto pia. Ellen
White anatukumbusha kwamba:

“Yesu alipowaambia wanafunzi wasiwazuie watoto kuja kwake alikuwa


akiwaambia wafuasi wake katika vizazi vyote, - kwa viongozi wa kanisa,
wachungaji, wasaidizi, na wakristo wote. Yesu anawavuta watoto, na
anatuagiza, “msiwazuie” ni kama angesema, watakuja kama hamtawazuia.”
– Evangelism, p. 580.

Tafiti za hivi karibuni pia zinaunga mkono dhana hii kwamba watoto chini
ya umri wa miaka 14 ni rahisi sana kukubali injili. Kwa hivyo, kanisa
linahitajika kuteka nafasii hii ili kuwafikia na kwa nguvu kuwashirikisha injili
watoto ambao hawajawahi kusikia kuhusu Yesu. Kristo alionna umuhimu wa
kuwafikia watoto:

“Miongoni mwa watoto walioletwa kukutana naye, Yesu aliona wanaume na


wanawake ambao wanapaswa kuwa warithi wa neema yake na walio chini ya
ufalme wake, na baadhi ambao wangekuwa wafia dini kwa ajili yake.
Alifahamu kwamba watoto hawa wangemsikiliza na kumkubali kama
Mkombozi wao kwa utayari zaidi kuliko watu wazima, ambao wengi wao
walikuwa wamejawa na mambo ya kidunia na wenye mioyo migumu. Katika
kufundisha, alijishusha akawa sawa nao. Yeye, Mkuu wa Mbinguni, alijibu
maswali yao na kurahisisha masomo yake yaliyokuwa muhimu ili kuweza
kufikia uelewa wao wa kitoto.” Evangelism, uk. 579.

Kwa hiyo agizo liko wazi na tunahitaji kuingia kazini katika kupanga
programu za kuifikia jamii nyingi kadiri akili zetu za kibunifu zinavyoweza
kuzalisha. Kumbuka, lengo la mwisho la kuwafikia watoto ni kuwasaidia
kumfahamu Yesu ili kwamba wajenge uhusiano wa upendo Naye.

A. AINA ZA UINJILISTI

Uinjilisti wa Watoto Wahubiri


Mtiririko huu wa uinjilisti unadumu kwa jioni saba pamoja na watoto
wakihubiri ujumbe kila jioni. Kimsingi mikutano hii ya kiuinjilisti inapangwa
kwa ajili ya watoto, ikiwa na lengo la kuwafanya watoto wawafikie watoto.
Hata hivyo, inawezekana pia kuwa na mfuatano wa watoto wakihubiri ili
kuwafikia watu wazima pia.
Wazungumzaji hawa wa jioni ni watoto wahubiri ambao wamepitia
mafunzo na wamechaguliwa kushiriki. Watoto wengine pia wanashiriki
katika kuleta mazungumzo rahisi juu ya afya, wimbo mkuu wa ibada, na
kukaribisha watu mlangoni.

Uinjilisti wa Urafiki
Mtazamo huu umegundulika kuwa ni moja kati ya njia zenye matokeo
sahihi katika kufanya uinjilisti kwa watoto. Watoto wote wana marafiki na
rafiki anapowaalika kuja kanisani, kuna uwezekano mkubwa wa wao
kwenda kuliko wanapoalikwa na mtu wasiyemfahamu. Uhusiano ni muhimu
katika maisha ya watoto.
Watoto wanafundishwa stadi za jinsi ya kufanya marafiki na jinsi ya kualika
marifiki.

Stadi za Urafiki. Kufundisha watoto stadi za kutengeneza marafiki na


kuwatunza kuna thamani kubwa katika uinjilisti wa urafiki.
Jinsi ya kusalimia mtu – mshike mkono mgeni au rafiki na useme: “Habari
za asubuhi. Karibu kwenye Shule yetu ya Sabato (au kambi/chama cha
Biblia). Tunafurahi sana umekuja.”
Jinsi ya kukaa na mtu – mwonyeshe rafiki yako kiti na keti chini naye.
Kama kuna marafiki wawili au zaidi waliowatembelea, waonyeshe viti.
Kisha wajulishe kwamba utakuja kuketi nao ukisha maliza kualika
marafiki wengine ambao wanaweza kuja.
Jinsi ya kumtambulisha rafiki – mruhusu mtoto aliyekuja na rafiki
asimame na kumtambulisha. Mtoto anaweza kusema, “Nina furaha sana
kumtambulisha rafiki yangu mzuri (au mwana-darasa, jirani), Tony
Bacchus. Kisha amgeukie Tony na anaweza kusema, “asante kwa kuja
Tony. Karibu tena.”
Jinsi ya kufanya marafiki – watoto wanaweza wakajifunza kuchukua
hatua ya kuwafanya wengine kuwa marafiki katika mtaa wao, shuleni
kwao, au katika mkutano wa watu wazima. Biblia inatutia moyo kufanya
hivyo katika Mithali 18:24: “Mtu aliye na marafiki lazima ajionyeshe kuwa
rafiki; na kuna rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.”
Msalimie mtoto mwingine na ujitambulishe ukisema, “Mambo! Mimi ni
Jeff. Nipo darasa la tano.”
Uliza jina la rafiki mwingine ukisema. “Jina lako ni nani? Unaishi wapi?
Unasoma wapi?
Pata taarifa za mawasiliano kwa mfano, “Kwa hiyo huwa unakuja katika
kituo hiki cha jamii mara ngapi? Nitawezaje kukuona tena? Una namba
ya simu? Anwani?

Kadi za mwaliko. Weka tayari kadi kwa ajili ya watoto kuzitoa ili kudumisha
mawasiliano na marafiki hawa wapya. Wahimize pia kuandika na kuzichora
pia. Wapatie kadi za kuwaalika marafiki katika programu maalum kama vile
kambi la siku moja, Shule ya Biblia Wakati wa Likizo au kongamano la
uimbaji.

Kuwa na kitabu cha Kumbukumbu. Hakikisha majina ya marafiki wa watoto


wako na watu waliokutana nao yanaorodheshwa kwenye kitabu cha
kumbukumbu. Kitabu hiki cha kumbukumbu ni muhimu kwa ajili ya
programu na shughuli zitakazofuata pamoja na kutembelea

Fuatilia. Ni muhimu kuwe na ufuatiliaji imara wa watoto wale waliohudhuria


programu moja au mbili za kanisa. Wapange watoto ambao wameleta
marafiki zao kwenye vikundi na waambie wawatembelee marafiki hawa
wapya. Tengeneza shughuli zingine za kufurahisha za kuwavuta ndani.

Kipindi cha kushirikishana Somo la Biblia Kila siku la ‘Kiungo cha Neema’
Wahimize watoto kuweka kwenye vitendo sehemu ya kujifunza ya Kiungo
cha Neema, “Wakishirikiana ujumbe” na marafiki zao. Kila juma wanapaswa
kushiriki ujumbe na mtu fulani kupitia mradi au huduma maalum.

B. JINSI WACHUNGAJI NA WAZEE WANAVYOWEZA KUSAIDIA KATIKA


UINJILISTI WA WATOTO
Andika makala ya taarifa za shughuli za uinjilisti wa kuifikia jamii.
Weka kwenye ratiba ya kanisa juma la uinjilisti.
Ruhusu watoto waliohusika katika uinjilisti kutoa ushuhuda.
Unga mkono watoto na viongozi wao kwa kuhudhuria baadhi ya
mikutano yao.
Toa bajeti kwa ajili ya uinjilisti wa watoto.
8. MAHUSIANO YA UPENDO
Watoto huimba moja kati ya nyimbo zao wanazopenda, “Anipenda ni
kweli Mungu anena hili … Yesu mwokozi, ananipenda …” upendo wa Yesu
ndio msingi wa injili na watoto, wanaitikia kwa namna iliyo chanya kwa
upendo wa aina hiyo unapoonyeshwa kwa uhalisia. Kwa hivyo, upendo
lazima utawale katika huduma yetu kwa watoto. Lazima tuwapende
watoto. Lazima tuwe na hisia kali kwa ajili ya watoto.

A. KUTOA VIELELEZO VYA MAHUSIANO YA UPENDO


Wahakikishie watoto na wazazi wao mbele ya halaiki.
Waalimu na viongozi wa watoto waonyeshe upendo na kujaliana.
Wasahihishe watoto kwa uvumilivu na uwe tayari kuwapatia nafasi
ya pili.
Kumbuka siku zao za kuzaliwa.
Toa muda maalum kwa watoto kwa ajili ya kushiriki karama na
talanta zao

B. KILE WACHUNGAJI NA WAZEE WANACHOWEZA KUFANYA ILI KUWA


KIELELEZO CHA UPENDO KWA WATOTO
Weka ratiba ya kisa cha watoto wakati wa ibada.
Kusanya “sadaka ya mwana-kondoo” maalum kwa ajili ya miradi ya
watoto.
Kuwe na makala ya watoto maalum katika programu na mahubiri ya
kanisa.
Ruhusu watoto washiriki kanisani, kama vile kutumika kama
mashemasi wadogo, wasalimiaji na wakaribishaji; kukusanya sadaka,
au kutoa muziki maalum.
Sura ya 9
MIONGOZOya UBATIZO
na MAPENDEKEZO
KWA AJILI YA WATOTO

N
i mwitikio gani tunaowapatia watoto wanapoomba kubatizwa?
Tunaanzaje kuwaanda kukubali neema ya Mungu na kutembea
kikamilifu katika mwangaza wake? Wanapaswa kuwauliza nini
kabla ya ubatizo? Ni umri gani ulio bora kwa ajili ya kubatizwa? Hatupaswi
kusita kwa muda mrefu, maana uamuzi wa mtoto unaweza ukafifia. Kama
tusipoitikia uamuzi wao wa kusisimua wa kumfuata Yesu na kubatizwa,
tunaweza tukapoteza nafasi ya dhahabu ya kufanya hivyo baadae.
Kufanya uamuzi wa kumfuata Yesu ni hatua muhimu kuelekea katika
kukua kiroho. Kanuni ya Kanisa, uk. 29 inakubali kwa kusema:

“Ubatizo ni uhusiano wa kiroho. Unaweza ukaingiwa na wale tu walio


ongoka. Ni kwa njia hii pekee usafi na ubora wa hali ya kiroho ya kanisa
unavyoweza kudumishwa. Ni wajibu wa kila mchungaji kuagiza wale
wanaokubali kanuni za ukweli, kwamba wanaweza wakaingia kanisani
katika msingi imara wa kiroho. Wakati hakuna umri ulioanishwa kwa ajili
ya ubatizo, inashauriwa kwamba watoto wadogo wanaoonyesha tamanio
la kubatizwa watiwe moyo na kuingizwa katika programu ya mafunzo ili
iwangoze katika kubatizwa.”
Ellen G. White pia anatambua kwamba watoto huwa wanafanya maamuzi
imara kwa ajili ya ubatizo. Analishauri kanisa katika Testimonies, vol 1. Uk.
400 kwamba:
“Watoto wa miaka minane, kumi au kumi na mbili, ni wakubwa wa
kutosha kuanzishiwa somo la dini ya binafsi. Usiwafundishe watoto wako
ukimaanisha wakati Fulani huko mbeleni ambapo watakuwa wakubwa
kiasi cha kutosha kuungama na kuamini ukweli. Kama wakielekezwa
vyema, watoto wadogo sana wanaweza wakawa na mitizamo sahihi ya
hali yao kama wenye dhambi, na njia ya wokovu kupitia kwa Kristo.”
UHAKIKISHO WA IMANI

Mtoto anapofanya uamuzi wa kuwa mfuasi wa Kristo, mratibu wa


Huduma za Watoto anapaswa kutia moyo uongozi wa kanisa katika
kuandaa huduma ya Uhakikisho wa Imani kwa ajili ya mtoto huyo. Sherehe
hiyo inasaidia kuhakikisha uamuzi wa mtoto na kumfanya atambue kwamba
kusanyiko lote linafurahi pamoja naye kwa kufanya agano la namna hiyo.

SOMO LA BIBLIA LA KUJIFUNZA UBATIZO

Chagua na utumie mwongozo wa kujifunza ubatizo au nyenzo nyingine ya


Biblia inayofaa kwa ajili ya watoto ambayo imepitishwa na Kanisa la
Waadventista wa Sabato. Miongozo ya kujifunza ifuatayo inapendekezwa
kwa ajili ya matumizi ya watoto:
Bible Treasure (Hazina ya Biblia), kimehaririwa na Aileen Sox. Nampa,
Idaho: Pasific Press Publishing Association, 2004.
ChristWise (Kama Kristo): Mwongozo wa uanafunzi kwa ajili ya vijana
wadogo, na Troy Fitzgeald. Hagerstown, MD: Review and Herald
Publishing Association, 2002.
ChristWise (Kama Kristo): Mwongozo wa uanafuzi kwa ajili ya Vijana
wakubwa, na Troy Fitzgerald. Hagerstown, MD: Review and Herald
Publishing Association, 2002.
Its My Choice (Ni Uchaguzi Wangu), na Steve Case. Hagerstown, MD:
Review and Herald Publishing Association, 1996.

VIAPO VYA UBATIZO

Baada ya mtoto kukamilisha mosomo ya kujifunza Biblia na amekuwa


tayari kuwa mshiriki wa kanisa, ombi lake la kubatizwa linapaswa kupelekwa
kwenye baraza la kanisa. Siku ya ubatizo wakati ambapo mtoto ataulizwa
hadharani, muombe mchungaji atumie “Viapo vya Ubatizo
Vilivyorahisishwa” na Steve Case. Hii ni rahisi kwa mtoto kuelewa viapo
hivyo anapofanya agano.

UHAKIKISHO WA IMANI
(Mfano wa Tukio hili)

…………………………………………………………………………….........
Wimbo:
Mruhusu mtoto achague wimbo anaoufahamu vyema.
Sio lazima wimbo wa kwenye kitabu cha nyimbo, unaweza
kuwa wimbo wa Shule ya Sabato.
Utangulizi:
Mtoto akae kiti cha mbele kabisa kabla ya tukio hili.
Mchungaji au rafiki katika imani ambaye anamfahamu
vyema mtoto anaweza akamtambulisha kwa washiriki.
Toa historia fupi ya ni lini, wapi na kipi kilichosukuma
uamuzi huo.
Weka mkazo kwenye maoni kuhusu huyo mtoto. Unaweza
ukasema: “ninapenda kumtambulisha kwenu Bryan hapa
kanisani. Mwezi uliopita katika Mkutano wa Watoto Bryan
alifanya uamuzi. Aliamua kumfanya Yesu kuwa rafiki yake
na anataka kuwa mmoja wa watoto wake.”

Uhakikisho:
Uhakikisho huo unapaswa kusomwa au kukaririwa na
mtoto mbele ya washiriki.

Kwa mfano: “Kwa sababu ninafahamu kwamba Mungu


ananipenda ninachagua kuishi maisha yangu kama mmoja
wa watoto Wake, kwa sababu Yesu alikufa kwa ajili yangu
ninataka kumfurahisha kwa jinsi ninavyoishi.

Rafiki wa Imani
Anatambulishwa:
Elezea wajibu wake.
Kwa mfano: “Kuwa na rafiki wa kukuunga mkono
kunaweza kukaleta maana ya kufanikiwa au kushindwa.
Biblia inasema kwamba, “kama mmoja akianguka, rafiki
yake anaweza akamwinua. Lakini ole wake mtu Yule
aangukaye na hakuna wa kumwinua!” (Mhubiri 4:10).
Bryan amechagua mwalimu wake wa Shule ya Sabato,
Bwana Jerry Page, awe rafiki yake wa Imani. Rafiki wa
Imani ni mtu atakayemtia moyo katika nyanja zote za
maisha yake, lakini muhimu zaidi, katika safari yake ya
kiroho pamoja na Yesu.
Rafiki wa imani anasoma agano lake kwa mtoto.
Kwa mfano: “Kama rafiki yako wa imani, ninaahidi
kukuunga mkono na kukujali. Kama wewe, ninaweza
nikatenda makosa, lakini ninafahamu kwamba Mungu
ananisamehe. Ninataka ufahamu kwamba unaweza ukaja
kuzungumza nami wakati wowote. Ninataka kuwa rafiki
yako.”

Mwitikio wa
Washiriki:
Ruhusu washiriki wahusike katika tukio hili kwa
kunyoosha mikono yao na kusimama kama ishara ya
kuunga mkono.
Kwa mfano: “Bryan, kuna watu wengine wengi hapa
ambao wanafahamu kwamba wangependa kuwa
marafiki zako wa imani. Wale kati yenu walio washiriki
ambao wangependa kuwa “rafiki” kwa Bryan tafadhali
msimame? Wale walio tayari kumtia moyo na kumuunga
mkono kwa upendo; wale wanaotaka kuweka agano la
kuwa chanya na kutomkosoa au kumhukumu, lakini kuwa
rafiki, tafadhali simameni sasa.”

Ombi:
Mchungaji anatoa ombi fupi.

Shikaneni
Mikono:
Mpatie mtoto kadi ya uhakikisho wa imani.

VIAPO VYA UBATIZO VILIVYO RAHISISHWA

Viapo vya ubatizo

1. Ninaamini katika Mungu Baba, Mwana wake, Yesu Kristo; na Roho


Mtakatifu.
2. Ninakubali kifo cha Yesu kwa ajili ya kulipa dhambi zangu.
3. Ninakubali moyo mpya ninaopatiwa na Yesu badala ya moyo wangu
wenye dhambi.
4. Ninaamini kwamba Yesu yupo mbinguni kama rafiki yangu mpendwa na
kwamba ananipatia Roho Mtakatifu ili niweze kumtii.
5. Ninaamini Mungu alinipatia Biblia kama mwongozo wangu wa muhimu.
6. Kwa Mungu kuishi ndani yangu, ninataka kutii Amri Kumi ambazo
zinajumuisha utunzaji wa siku ya saba ya juma kama Sabato.
7. Ninataka kusaidia watu wengi kadri niwezavyo ili wawe tayari kwa ajili
ya ujio wa pili wa Yesu.
8. Ninaamini Mungu anawapa watu wake vipawa maalum, na kwamba
Roho ya Unabii inatolewa kwa watu wake waliochaguliwa.
9. Ninataka kulisaidia kanisa la Mungu kwa mguso, nguvu na fedha zangu.
10. Ninataka kuutunza vyema mwili wangu kwa sababu Roho Mtakatifu
anaishi ndani yake sasa.
11. Kwa uwezo wa Mungu, ninataka kutii kanuni za msingi za Kanisa la
Waadventista Wasabato.
12. Ninataka kubatizwa na kuwaonyesha watu kwamba mimi ni Mkristo.
13. Ninataka kuwa mshiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, na
ninaamini kanisa hili lina ujumbe maalum kwa ajili ya ulimwengu.

Imetolewa kutoka katika It’s my Choice (Ni uchaguzi wangu), na Steve Case. Hagerstown, MD: Review
and Herald Publishing Association, 1996. Sura ya 10
Sura ya 10
MATAMKO YA
HALAMASHAURI
KUU kuhusu
WATOTO

TAMKO JUU YA USTAWI NA THAMANI YA WATOTO


Waadventista Wasabato wanathibitisha haki ya kila mtoto kuwa na
mazingira ya nyumbani yaliyo imara na yenye furaha, na uhuru na msaada
wanaohitaji ili kukua na kuwa kama Mungu alivyodhamiria awe. Mwaka
1989, mkutano mkuu wa Halmashauri Kuu ulitambua umuhimu wa msingi
wa watoto kwa kukublai “Mapatano kuhusu Haki za Watoto.” Kwa kuwiana
na kanuni hizi, na kufikiria thamani Yesu aliyowapatia watoto aliposema,
“Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana
walio mfano wa hao, ufalme wa mbinguni ni wao” (Mathayo 19:14),
tunatafuta kuwasaidia watoto wanaoteseka kutokana na mivuto hii hatari:

Umasikini - umasikini unaathiri maendeleo ya watoto, kwa kuwanyang’anya


mahitaji muhimu kama chakula, mavazi na malazi na kwa namna moja au
nyingine ukiathiri afya na elimu yao.

Kukosa Elimu – kukosa elimu kunafanya iwe vigumu kwa wazazi kupata ujira
wao au kuitunza familia au kumfanya mtoto afikie upeo wa uwezo wake.

Huduma duni ya afya – mamilioni ya watoto hawapati huduma ya afya kwa


sababu wanakosa bima, au wanaishi maeneo yasiyokuwa na huduma ya
afya.

Unyanyasaji na kutokulindwa – watoto wanaharibiwa na kunyanyaswa pale


wanapotumika kama wafanyakazi kwa bei ndogo, kazi za jasho,
mapambano ya kivita, na starehe potovu za kingono za watu wazima, na
wanapoachwa kutazama mambo yaliyokithiri ya kingono katika vyombo vya
habari au kwenye mitandao.
Ukatili – kila mwaka watoto wengi wanakufa vifo vya kikatili. Sehemu
kubwa ya watu wanaoteseka katika mapambano ya kivita ni wanawake na
watoto. Watoto wanabeba makovu makubwa ya kimwili na kisaikolojia,
hata baada ya mapigano kusitishwa.
Kwa kuitikia masuala na mahitaji yaliyotajwa hapo juu, Waadventista wa
Sabato wanasimamia haki za watoto zifuatazo:
1. Haki ya kuwa na mahali pa kuishi penye upendo na utulivu ambapo pana
usalama na hapana unyanyasaji.
2. Haki ya kupata chakula cha kutosha, mavazi na malazi
3. Haki ya kupata huduma ya afya iliyo sahihi na bora
4. Haki ya kupata elimu inayowaanda watoto kwa ajili ya kuchukua nafasi
chanya katika jamii kwa kuendeleza vipawa vyao binafsi na kuwapatia
uwezo wa kuingiza kipato.
5. Haki ya kupata elimu ya kidini na kimaadili nyumbani na kanisani.
6. Haki ya kutokubaguliwa na kunyanyaswa.
7. Haki ya kuwa na utu, kuheshimiwa, na kuendeleza kujiamini kwao.

TAMKO KUHUSU UNYANYASAJI WA KINGONO KWA WATOTO


Unyanyasaji wa kingono hutokea pale mtu aliye na umri mkubwa zaidi au
mwenye nguvu zaidi ya mtoto anapotumia nguvu, mamlaka au cheo chake
alichoaminiwa kwacho kumhusisha mtoto katika tabia au jambo la kingono.
Ngono kati ya wana-ndugu, ni njia ya kipekee ya unyanyasaji wa kingono
kwa watoto, na inatambulika kama jambo lolote la kingono kati ya mtoto na
mzazi au ndugu, ndugu wa ukoo au mzazi wa kambo.
Wanyanyasaji wa kingono wanaweza kuwa wanaume au wanawake na
wanaweza kuwa wa umri wowote, taifa lolote au kutoka kwenye jamii
yoyote. Wanaweza kuwa wanaume walio-oa watoto, wenye kazi za
kuheshimika, na watendaji wazuri kanisani. Ni kawaida kwa wakosaji
kupinga vikali tabia yao ya unyanyasaji, na kukataa kuona matendo yao
kuwa ni matatizo, na kuhalalisha tabia yao au kulaumu kitu au mtu
mwingine. Wakati ni kweli kwamba wanyanyasaji wengi huonyesha
kutojiamini kwa hali ya juu, matatizo haya kamwe hayapaswi kukubaliwa
kama kisingizio cha kumfanyia mtoto unyanyasaji wa kingono. Mamlaka
nyingi zinakubali kwamba tatizo hasa katika unyanyasaji wa kingono kwa
watoto linahusika zaidi na tamaa ya mamlaka au kumiliki kuliko tamaa ya
ngono.
Mungu alipoumba familia ya wanadamu, alianza na ndoa kati ya
mwanaume na mwanamke iliyojengeka katika upendo na kuaminiana.
Uhusiano huu bado umeundwa ili kutoa msingi wa familia tulivu, yenye
furaha ambayo inalinda na kusimamia utu, thamani, na heshima ya kila
mwanafamilia. Kila mtoto, awe wa kiume au wa kike, anapaswa
kuhakikishiwa kuwa yeye ni zawadi kutoka kwa Mungu. Wazazi wanapewa
nafasi na wajibu wa kuwalea, kuwalinda na kuwajali kimwili watoto
waliopatiwa na Mungu. Watoto wanapawa kuheshimu, na kuwaamini
wazazi wao na wanafamilia wengine bila hatari ya kunyanyaswa.
Biblia inahukumu unyanyasaji wa kingono kwa watoto kwa maneno
makali kadiri iwezekanavyo. Inatazama kila jaribio la kuchanganya, kuzuia
kuondoa, au kuhafifisha mipaka binafsi, ya vizazi au ya kijinsia kwa kupitia
matendo ya unyanyasaji wa kingono kuwa ni matendo ya usaliti na uvunjaji
wa utu wa kutisha. Biblia inakataa dhahiri matumizi mabaya ya nguvu,
mamlaka na wajibu kwa sababu hivi vinagusa pale ulipo moyo na hisia za
ndani kabisa za mhanga kumhusu yeye mwenyewe, kuhusu wengine na
kumhusu Mungu na inavunja vunja uwezo wake wa kupenda na kuamini.
Yesu alitumia lugha ngumu katika kukataza matendo ya yeyote ambaye
kupitia neno au tendo, atamsababisha mtoto kuanguka.
Jamii ya Wakristo Waadventista haina kinga dhidi ya unyanyasaji wa
kingono kwa watoto. Tunaamini kwamba itikadi za imani ya Kiadventista
zinatutaka tuhusike kikamilifu katika kuzuia mambo hayo. Pia tuna agano la
kuwasaidia kiroho wanaonyanyaswa na wanyanyasaji pamoja na familia zao
katika kupata uponyaji na mchakato wa kupona, na kuwafanya wataalam
waliopo kanisani na viongozi walei kuwajibika kwa kuhakikisha mwenendo
wao unastahili kama watu walio katika nafasi za kuaminiwa kama viongozi
wa kiroho.

KAMA KANISA TUNAAMINI KUWA IMANI YETU IMETUITA ILI:


1. Kutetea kanuni za Kristo kwa ajili ya mahusiano ya kifamilia ambayo
yanatambua kujiheshimu, utu na usafi wa watoto kama haki ya lazima ya
kimbingu.
2. Kuwezesha mazingira ambayo watoto walionyanyaswa wanaweza
wakajiona salama pale wanapotoa taarifa kuhusu kunyanyaswa
kingono, na wanaweza kuhisi kwamba mtu fulani anaweza
akawasikiliza.
3. Kuwa na taarifa za kina kuhusu unyanyasaji wa kingono na athari yake
katika jamii ya kanisa letu.
4. Kusaidia wachungaji wa viongozi walei kutambua vidokezo vya kuashiria
unyanyasaji wa kingono kwa mtoto na kufahamu jinsi ya kuitikia kwa
ufasaha pale unyanyasaji unapohisiwa au mtoto anapotoa taarifa
kwamba ananyanyaswa kingono.
5. Kuunda mahusiano rejea pamoja na wataalamu wa ushauri nasaha na
taasisi zinazoshughulikia unyanyasaji wa kingono, ambao wanaweza
kwa utaalamu wao kusaidia mhanga aliyenyanyaswa pamoja na familia
yao.
6. Kutengeneza miongozo/sera katika ngazi sahihi ili kuwasaidia viongozi
wa watoto katika:
a. Kujaribu kushughulikia kwa usawa watu walioshitakiwa kwamba
wamewanyanyasa watoto kingono.
b. Kuwawajibisha wanyanyasaji kulingana na matendo yao na kutoa
adhabu inayofaa.
7. Kuunga mkono kuelimishwa na kusitawishwa kwa familia na
wanafamilia kwa:
a. Kuondoa imani za kidini na kitamaduni zinazoshikiliwa na
zinazoweza kutumika kuhalalisha au kufunika unyanyasaji wa
kingono kwa watoto.
b. Kujenga hali nzuri ya kujithamini kwa kila mtoto ambayo inamsaidia
kujiheshimu yeye na wengine.
8. Kutoa msaada wa kujali na huduma ya ukombozi uliojengeka katika
imani ndani ya jamii ya kanisa kwa ajili ya wahanga wa unyanyasaji na
wanyanyasaji wakati mkiwasaidia kufikia mtandao wa rasilimali za
kitaalamu katika jamii.
9. Kunga mkono mafunzo kwa ajili ya wataalamu zaidi wa familia ili
kuwezesha uponyaji na mchakato wa uponaji wa walionyanyaswa na
wanyanyasaji.
………………………………………………………………………………….
Tamko hilo hapo juu lina taarifa zilizoelezewa katika mafungu yafuatayo ya maandiko:
Mwa 1:26; 2:18 -25; Law 18:20; 2 Sam 13:1 -22; Mat 18:6-9; 1 Kor 5:1-5; Efe 6:1-4; Kol 3:18-21; 1 Tim 5:5-8.
………………………………………………………………………………………………………………
Tamko hili lilipigiwa kura wakati wa Mkutano wa Majira ya Hari wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya
kanisa la Waadventista wa Sabato tarehe 1 Aprili, 1997, huko Loma Linda, California.
Sura ya 11
PROGRAMU ZA
HUDUMA ZA WATOTO
Kwa ajili ya
KANISA MAHALIA

UMUHIMU WA HUDUMA ZA WATOTO KATIKA KANISA MAHALIA

Kila kanisa mahalia linapaswa kuwa na programu ya huduma za watoto,


bila kujali uchache wa watoto wanaohudhuria. Programu ya namna hii
inaweza kutoa malezi kwa watoto na kuwahusisha katika jamii ya
wanaoamini kanisani, kwa ajili ya kuwaongoza kufanya uamuzi wa kumfuata
Yesu Kristo. Wachungaji, wazee na kamati ya uchaguzi wanapaswa kuweka
kipaumbele katika kutafuta viongozi wenye mapenzi ya kufanya kazi na
watoto, iwe wanalipwa kama wafanyakazi au wamejitolea.

KUPANGA PRGRAMU ZA HUDUMA KWA WATOTO

Makanisa makubwa yenye watoto wengi yanaweza yakaajiri mchungaji


wa watoto au kiongozi ili kuendesha programu ya huduma kwa watoto.
Katika makanisa madogo ambapo kuna watoto wachache zaidi, mratibu wa
huduma za watoto anaweza kuchaguliwa kwa ajili ya jukumu hili. Wakati
mwingine kiongozi wa Shule ya Sabato huchaguliwa kupanga programu
kwa ajili ya watoto wa kanisa husika.
Kanuni ya Kanisa inapendekeza kwamba mratibu wa huduma za watoto
achaguliwe kuingia kutumika katika baraza la kanisa au baraza la mashauri.
Hii inasaidia sana ili mratibu aweze kufanya kazi pamoja na mchungaji na
kanisa kwa ajili ya watoto katika kupanga programu zote ambazo zitatukuza
badala ya kuleta mashindano na wengine.
PROGRAMU NA SHUGHULI ZA WATOTO
Ni muhimu tupange programu bora kwa ajili ya watoto. Hata hivyo,
tunahitaji kukumbuka kwamba programu ni nyenzo kwa ajili ya kuujenga
mwili wa Kristo. Siku zote tusipoteze mwelekeo utume wetu katika huduma
za watoto: kulea watoto kuwa na uhusiano wa upendo na wa kumtumikia
Yesu. Kila programu tunayotoa inahitaji kuwaongoza watoto katika njia hiyo
ya imani.
Usipange zaidi ya inavyohitajika! Anza na kidogo lakini chenye maana
badala ya kuanza na mengi yaliyo ya kawaida. Ni muhimu kuimarisha
programu zilizopo na kuongeza zingine kadri hitaji linavyojitokeza,
ukikumbuka akilini uwepo wa fedha kwa ajili ya msaada na wanaojitolea.
Hatuhitaji kuwa na programu zote za makanisa mengine. Chagua tu zile
programu ambazo unaweza ukafanya, ukikumbuka kwamba kadiri
programu za huduma kwa watoto zinavyotolewa na kutangazwa na kanisa
kwa wingi, ni kwa jinsi iyo hiyo kanisa linavyovutia familia, na kusanyiko
litakua. Sura hii inachunguza baadhi ya programu za kuwafikia watoto.
Inatoa mawazo na kutia moyo huduma fulani. Lakini chagua kwa makini.

PROGRAMU ZINAZOWAFIKIA WATOTO NDANI YA KANISA


SHULE YA SABATO YA WATOTO

Kusudi: kutoa elimu ya dini kwa watoto ambayo itawasaidia kujenga


uhusiano na Yesu. Huu ni wakati ambao watoto hujifunza maandiko,
hujumuika pamoja, na inahusika na huduma ya kuwa wafuasi waaminifu wa
Yesu Kristo.

Maelezo: jumla ya saa moja ya prgoramu ya Shule ya Sabato iliyojikita katika


masomo ya Biblia ya kila juma. Watoto wanahusishwa katika kujifunza kwa
vitendo na kushiriki katika shughuli mbalimbali zinazokidhi mtindo wao wa
kujifunza.

Mambo ya kipekee: hii ni huduma pekee inayowafikia watoto


Waadventista. Inatoa nafasi kubwa ya kujifunza Biblia pamoja na watoto na
kuwasaidia kuyaweka masomo haya katika maisha yao ya kila siku.
Wakurugenzi wa Huduma za Watoto wanahitaji kuhakikisha kwamba
makanisa yote yenye watoto yawe na Shule ya Sabato kwa ajili ya watoto
kulingana na umri wao.

Nyenzo: Children’s Ministries; Ideas and Techniques that work


(AdventistSource); Nyenzo za Mtaala wa Kiungo cha Neema kwa waalimu
(Review and Herald).

KANISA LA WATOTO

Kusudi: kuwapatia watoto nafasi ya kuabudu katika mpangilio wa umri wao,


kujifunza kulingana na ngazi yao ya uelewa, na kushiriki katika ibada.

Maelezo: kanisa la watoto ni huduma ya kanisa kwa ajili ya watoto. Inaaza


wakati ile ya watu wazima inapoanza. Kanisa la watoto linapangwa
kulingana na mahitaji ya kila kanisa, ikifanyika mara moja kwa mwezi hadi
mara mbili kwa mwezi. Kanisa la watoto linahitajika zaidi na watoto wa
miaka 2-8, ambao wanapata shida kukaa kwa muda mrefu.
Watoto umri wa vijana wadogo wanahitaji kanisa lao la vijana wadogo, au
wanaweza kuhudhuria ibada ya kawaida. Kanisa la watoto linakuwa na
vielelezo vya ibada ya kawaida kama vile nyimbo za sifa, maombi,
kushirikiana au kutoa ushududa, kujifunza neno, hubiri la watoto, na
maigizo au vichekesho vinavyoendana na Neno katika maisha ya kila siku.

Nyenzo: 101 Ideas for Children’s Church na Jolene Roehlkepartain


(AdventistSource); Childeren’s Church: Responding to God’s Love
(AdventistSource); Children’s Sermons: Using the 5 to tell God’s Story, by
Philip D. Schroeder (Shirika la Uchapaji la Abingdon).

MKUTANO WA MAOMBI WA WATOTO

Kusudi: Kuhusisha watoto katika uzoefu wa maombi wenye maana.

Maelezo: Inahusisha mazungumzo mafupi kuhusu maandiko ili kuimarisha


imani za watoto katika kuelewa maombi. Ni pamoja na nyimbo, maombi na
shughuli fulani au stadi za kazi. Watoto pia wanaweza wakakutana katika
nyumba mojawapo badala ya kanisani.

Mambo ya kipekee: Inawapatia watoto nafasi ya kipekee kwa ajili ya kukua


kiroho na kujumuika pamoja na watoto wengine.
Nyenzo: Forever Stories Funpack (Review and Herald); 52 Ways to Teach
Children to Pray (Rainbow books); 100 crative Prayer Ideas fo Kids na Karen
Holford (Pasific Press); vitabu vya maombi vya watoto; juma la maombi ya
watoto (Adventist Review).

DARASA LA UBATIZO LA WATOTO

Kusudi: kuandaa watoto ambao wameonyesha tamaa ya kubatizwa.

Maelezo: watoto wanajifunza misingi ya imani ya Ukristo na Kanisa la


Waadventista wa Sabato ili kuelewa uhusiano wao na wajibu wao kwa
Mungu na kwa jumuia ya waumini.

Mambo ya kipekee: masomo ya ubatizo ya watoto yanatolewa katika ngazi


ya uelewa wa watoto. Wanaweza wakachukua muda mrefu kadiri
watakavyo katika kujiandaa kwa ubatizo.

Nyenzo: “It’s my Choice” Mwongozo wa Ubatizo na Steve Case (Review and


Herald); Christwise: Discipleship Guide for Juniors na Troy Fitsgerald (Review
and Herald); Christwise: Descipleship Guide for teens na Troy Fitzgerald
(Review and Herald).

KWAYA YA WATOTO

Kusudi: Kuwapatia watoto uzoefu wa kuabudu kupitia muziki na


kuwafundisha kuimba katika kuelewa muziki kama huduma ya kuifika jamii.

Maelezo: kikundi cha muziki kwa ajili ya watoto ambacho kinaimba hasa
kanisani lakini pia katika jamii. Unaweza ukawa ni mradi wa muda mfupi au
muda mrefu kwa ajili ya maandalizi ya kambi la vijana, makambi, au Sabato
ya watoto. Watoto katika jamii wanaweza kualikwa kujiunga na kwaya hiyo
na wazazi wao wakaalikwa kuja kutazama wakiimba, na mahusiano
kujengwa ambayo yanaweza kuwa ushuhuda mkubwa.

Mambo ya kipekee: huduma hii inaleta pamoja shule ya kanisa, shule ya


umma na watoto wa jamii. Inatoa nafasi kubwa ya kufundisha watoto
muziki mzuri na kuleta mvuto katika aina ya muziki wanaopenda.
SABATO YA WATOTO

Kusudi: kuwapatia watoto nafasi ya kutumia karama na talanta zao kwa


kushiriki katika huduma ya ibada.

Maelezo: hii ni programu maalum ya kila mwaka katika kila Sabato ya tatu
ya Oktoba, ili kukuza uelewa wa mahitaji ya watoto na wajibu wetu kama
kanisa kuyatimiza mahitaji yao. Watoto wanashiriki katika huduma ya ibada,
wakipewa kazi kama vile kuomba, kusoma Maandiko, wimbo mkuu wa
ibada, kuhubiri, kukusanya sadaka, na muziki maalum.

Nyenzo: Open your Heart, Open Hands, 2003 (Huduma za Watoto Divisheni
ya Marekani); Stand Up! Stand Out! 2004 (Huduma za watoto Divisheni ya
Marekani).

MKUTANO WA WATOTO

Kusudi: Kutoa uinjilisti wa kiroho na malezi kwa ajili ya watoto katika


mikutano ya muundo wa kambi.

Maelezo: watoto hukusanyika kwa siku 2-3 kwenye eneo la kambi au kituo
cha mikutano kwa ajili ya shughuli za kushirikishana kivitendo ambazo
zinaunga mkono kukua kiroho, kimwili, kijamii na kiakili. Mada maalum
zinachaguliwa na programmu inapangwa kulingana na mada hizi. Programu
zinaweza zikajumuisha uwakili, historia ya kanisa, uzoefu wa ki-Biblia, na
mashujaa wa kwenye Biblia.

Mambo ya kipekee: Inatoa namna ya kuandaa programu kwa ajili ya siku za


juma pamoja na Programu za Sabato. Watoto pia hupatiwa nafasi ya
kuendeleza stadi zao za uongozi, za kiroho, kimwili na kijamii.

Nyenzo: My Place in Space (Idara ya Huduma za Watoto Halmashaur Kuu);


Jesus, then and Now (AdventistSource).

MKUTANO WA WATOTO WA UINJILISTI

Kusudi: Kusaidia watoto kuweka agano kwa Yesu, na kuelewa mpango wa


wokovu na misingi ya imani ya Waadventista wa Sabato.

Maelezo: Mtiririko wa mikutano kwa ajili ya watoto ambayo inatoa kweli


kulingana na umri wakati wazazi wakishiriki mikutano ya uinjilisti ya watu
wazima. Programu zinajumuisha visa vya Biblia na mafundisho, mafungu ya
kukariri, nyimbo, maombi, shughuli mbalimbali na sanaa.

Mambo ya kipekee: Inatoa somo la kina kuhusu mpango wa wokovu na


imani mbalimbali za Waadventista wa Sabato katika ngazi ya watoto.

Nyenzo: Bible Treasures na Aileen Sox (Pasific Press); Forever Stories


Funpack – ages 4-11 (Review and Herald); The Underground Adventure
(Divisheni ya Pasifiki kusini).

CHAMA CHA WAHUBIRI WADOGO

Kusudi: kuwapa mafunzo watoto ambao wana karama ya kuhubiri Neno la


Mungu.

Maelezo: watoto, ambao wanavutiwa na kuhubiri, wanajiunga na chama


hiki ambacho hukutana mara 1 au 2 kwa juma. Wanapata mafunzo ya
kuandaa, kuwasilisha, pamoja na stadi zingine za kuzungumza katika halaiki.
Baada ya miezi kadhaa ya kujifunza, wahubiri hawa watoto wanapewa
nafasi ya kufanya kwa vitendo stadi hizi katika matukio halisi kama vile
huduma ya ibada, mikutano ya uinjilisti, kanisa la watoto na kadhalika.

Mambo ya kipekee: watoto wanafata nafasi ya kupewa mafunzo kama


wahubiri wadogo pale wanapovutiwa na kuwa na karama ya kuhubiri. Pia
kuna nafasi ya kujumuika na kufanya kazi na wenzao katika uzoefu mkuu wa
kiroho.

Nyenzo: Young Preachers Club imetolewa na idara ya Huduma za Watoto,


Divisheni ya Amerika ya kati.

KONGAMANO LA MUZIKI LA WATOTO

Kusudi: kuwapatia watoto nafasi ya kutumia talanta zao za muziki katika


nyanja za uimbaji, upigaji wa vyombo, uigizaji wa muziki, nk.

Maelezo: watoto wanakusanyika kwa siku nzima ya kongamano la muziki.


Programu zinajumuisha maonyesho mafupi ya vyombo vya muziki, uigizaji,
mapambio, n.k. Ikifuatiwa na watoto kupiga muziki. Watoto wa kwenye
jamii wanaweza kualikwa kujumuika katika kongamano.
KAMBI LA WATOTO LA UOTO WA ASILI

Kusudi: ni kuwavutia watoto na kuwaongoza katika kufurahia sehemu ya


dunia yenye uoto wa asili unaofurahisha na kutia nguvu.

Maelezo: kutoka kwenda kwenye kambi au sehemu Fulani kwenye uoto wa


asili kwa siku kadhaa ambapo watoto hushiriki katika shughuli za uoto wa
asili ambazo zitawainua, zitawatia hamasa na kuwavutia kumshukuru
Mungu Muumbaji.

Mambo ya kipekee: watoto wanapata nafasi ya kuchunguza ulimwengu wa


asili kupitia shughuli ya kufurahisha, michezo, maonyesho ya video, na
kujifunza uoto wa asili. Huu ni wakati mzuri kwa kundi la watoto mbalimbali
na urafiki.

Nyenzo: Sharing Nature with Children I and II imetolewa na Joseph Cornell


(Dawn Publication); A Family Guide to Sabbath Nature Activities imetolewa
na Eileen Lantry (Pasific Press); Four Seasons . . . Five Senses; 52 Weeks with
Nature imetolewa na Thais Randall Baer (Pasific Press).

PROGRAMU ZINGINE

Kongamano la afya la watoto; kambi la uwakili; kambi la Biblia la watoto;


madarasa ya Biblia ya kila juma kwa watoto ambao hawasomi katika shule
za Kiadventista; juma la maombi; kisa cha watoto wakati wa ibada; makundi
madogo ya watoto.

PROGRAMU ZINAZOWAFIKIA WATOTO WAPYA


SHULE YA BIBLIA WAKATI WA LIKIZO

Kusudi: kuwafikia watoto katika jamii na kuwaongoza kwa Yesu.

Maelezo: shule ya Biblia wakati wa likizo (VBS) ni programu maarufu ya


kuifikia jamii. Kwa ujumla huwa inafanyika wakati wa likizo kwa siku 5-10.
Inaweza ikaanza asubuhi kuanzia saa 3:00 hadi saa 12:00 mchana au muda
mwingine wowote unaoendana na mahitaji ya jamii. Programu hii
inajumuisha kipindi kizuri sana, visa vya Biblia, sanaa, na michezo. Vijana
wanaweza wakapata na msaada mkubwa hapa.
Mambo ya kipekee: watoto wa ndani ya kanisa wanapata nafasi ya
kukutana na watoto wa kwenye jamii, na wanajifunza jinsi ya kuwa marafiki
wa wageni hawa.

Nyenzo: Friends Forever (AdventSource); Jesus’ Kids in the Kitchen


(AdventSource); Creation Station (Review and Herald); Lava Lava Island
(Group Publishers)

CHAMA CHA BIBLIA CHA MTAA

Kusudi: Ni kuendelea kuwa njia ya ufuatiliaji wa Shule ya Biblia Wakati wa


Likizo.

Maelezo: Hii ni programu ya saa 1 - 2 ya visa vya Biblia, nyimbo, sanaa, na


michezo ambayo inaweza ikafanyika nyumbani, kwenye egesho la magari,
au uwani. Familia ya mshiriki aliyejitolea inaweza kusimamia chama cha
Biblia na kuwaalika watoto ambao walihudhuria kwenye Shule ya Biblia
wakati wa Likizo pamoja na wale ambao hawakudhuria.

Mambo ya kipekee: Ni mradi mzuri wa familia wa kuwafikia wale watoto


waliohudhuria Shule ya Biblia wakati wa Likizo. Kuwaalika katika hiyo
nyumba kwa ajili ya chama hicho na kuwatia moyo kuwaalika rafiki zao
katika jamii waje kujiunga pia.

Nyenzo: Forever Stories Funpack (Review and Herald); My Bible Friends na


Donna Williams (Konferensi ya Florida).

VIKUNDI VYA MICHEZO

Kusudi: Kuwafikia wakina mama vijana katika jamii na kuwatambulisha kwa


Mungu.

Maelezo: Wakina mama walio na watoto wadogo wanaalikwa kuleta


watoto wao kanisani kwa ajili ya kufurahi, michezo na kujumuika pamoja.
Watapata nafasi ya kukutana na wamama wengine vijana wa kanisani, hivyo
kuwapatia nafasi ya kujenga urafiki ili kuwa na mtandao wa pamoja.
Programu hii inaweza kufanywa mara mbili kwa juma katika chumba
kikubwa ambapo kuna nafasi ya magari ya kuchezea, bembea ndogo, na
shughuli zingine. Wapatie wamama na watoto wao vinywaji. Na baada ya
muda, wanaweza kualikwa kwenye masomo ya malezi, vikundi vidogo, nk.
Nyenzo: Mother of Preschoolers (MOPS)(Group Publishers).

SANAA MWISHO WA JUMA

Kusudi: Kuwahusisha watoto katika shughuli za kufurahisha kwa kujifunza


na kutengeneza vitu mbalimbali vya sanaa.

Maelezo: Watoto ndani ya jamii wanaalikwa kushiriki katika shughuli za


kufurahisha za kubuni na kutengeneza vitu vya sanaa. Programu hii inaweza
kufanywa Jumapili asubuhi kuanzia saa 3:00 hadi saa 12:00 mchana au muda
wowote unaofaa kwa wazazi kuleta watoto wao. Kufahamiana na watoto
pamoja na wazazi wao ni muhimu katika kuunda mahusiano bora.

Mambo ya pekee: Watoto wanapatiwa nafasi ya kujifunza sanaa mpya na


kujenga marafiki wapya ni nafasi nyingine ya kuwafahamu wazazi katika
jamii.

Nyenzo: Encyclopedia of BibleCrafts for Children (Group Publishing); Bible


story Crafts and Projects Children Love (Group Publishing); Creative Can – do
Crafts imetolewa na Lois Keffer (Group Publishing).

KARIBU MTOTO

Kusudi: Kufahamiana na wamama wapya mtaani na kuwasaidia katika miezi


yao ya awali ya kuwa mama.

Maelezo: Wanawake wa kanisani wanakutana pamojaa na kuwatembelea


kina mama ambao wamejifungua. Wanaweza kuwa marafiki, ndugu, au
majirani wa wanawake wa kanisani. Wanapeleka chakula, zawadi kwa ajili
ya mtoto, na nyenzo kwa ajili ya matunzo ya mtoto ili mama huyu asome.

Mambo ya kipekee: Hii ni programu bora zaidi ya kuifikia jamii kwa maana
kina mama waliojifungua wanahitaji kutiwa moyo na kusaidiwa katika miezi
yao ya mwanzo. Urafiki mzuri unaweza kuanzishwa utakaowezesha
kupatikana kwa nafasi zingine za kushuhudia.

Nyenzo: Welcome Baby Program imetolewa na Kay Kuzma (AdventSource).


MAKTABA INAYOHAMA

Kusudi: Kuwafikia watoto katika jamii ya vijijini na kuwatambulisha kwa


Yesu kupitia vitabu na hadithi.

Maelezo: Kila juma gari la maktaba inayohama linasafiri katika miji maalum
ya vijijini ili kuwapatia watoto pale vitabu na nyenzo zingine za visa vya
Biblia. Kila mtoto anaweza kuazima kitabu kimoja au viwili kwa juma moja
na atavirudisha kwa ajili ya kupewa vitabu vingine gari litakaporudi juma
linalofuata. Maktaba hii inayo hama pia inatoa maonyesho ya wanasesere,
kisa cha Biblia na nyimbo za watoto kwa takribani dakika 45.

Mambo ya kipekee: Hii ni programu inayofaa katika kuwafikia watoto katika


miji na vijiji ambao hawana nafasi ya kupata vitabu na nyenzo mbali mbali.
Inafungua njia ya kukutana na mahitaji ya watoto pamoja na kuwapatia
nafasi ya kujifunza kuhusu Biblia na injili. Kwa sehemu nyingi, wazazi pia
huvutiwa na maktaba hii inayotembea.

Nyenzo: Children Stories imechapishwa na Pasific Press na Review and


Herald.

MAFUNZO YA BIBLIA MAJIRA YA JOTO

Kusudi: Kutoa nafasi kwa watoto kwa ajili ya masomo mahsusi ya Biblia.

Maelezo: Mkazo unakuwa katika kujifunza kwa vitendo katika maeneo


maalum kulingana na mada za Biblia. Visa vya Biblia hupewa uhalisia katika
maisha halisi jinsi masomo ya Biblia yanavyofunuliwa.

Mambo ya kipekee: Watoto hupitia uzoefu wa masomo ya Biblia katika hali


halisi ya maisha. Wanakaa ufukweni na kupitia uzoefu wa bahari au ziwa
husika; wanatembelea chumba cha mahakama ili kujifunza haki ya Mungu;
wanatembea katika shamba la ngano na kuchunguza mfano wa ngano na
magugu. Watoto wanatengeneza mradi wa programu za kujifunza Biblia,
kama vile kuunda makumbusho ya Uumbaji baada ya kujifunza Mwanzo.
Makumbusho hayo yanakuwa na mabaki ya viumba, mifupa, na mifano ya
wanyama wa kale.
PROGRAMU ZINGINE

Huduma ya wanasesere; saa ya hadithi kwa jamii; programu za kwenye


redio, n.k.
Sura ya 12
NYENZO
ZINAZOPENDEKEZWA

VITABU
Allen, Steve. Growing a Healthy Children Ministry. Cincinnati, Ohio: Standard
Publishing, 2002.
Barna George. Transforming Children Into spiritual Champions. Ventura,
California: Regal books, 2003.
Bowdon, Boyce. The Child – Friendly Church; 15 Models of Ministry with
Children. Nashville, Tennessee: Abingdon press, 1999.
Calkins, Jack. Grace Is for Kids. Lincoln, Nebraska: AdventSource, 1997.
Chromey, Rick. Children’s Ministry Guide for Smaller Churches. Loveland,
Colorado: Group Publishing, Inc. 1995.
Craig, Jutila. Leadership Essentials for Children’s Ministry. Loveland,
Colorado, Group Publishing, 2002.
Dallow, Gill. Touching the Future. Oxford, England: the Bible Reading
Fellowship, 2002.
Frank, Penny. Leading Children. Nottingham, England: St. John’s Extension
Studies and Children Ministriy, 2001
Habenicht, Donna. How to Help your Child Really Love Jesus. Hagerstown,
Maryland: Review and Herald Publishing Association, 1994.
Habenicht, Donna. 10 Christian Values every kid should know. Hagerstown,
Maryland: Review and Herald Publishing Association, 2004.
Holford, Karen. 100 Creative Prayer Ideas for kids. Nampa, Idaho: Pasific
Press Publishing Association, 2003.
Hopkins, Gary and Joyce W. Hopp. It takes a Church: Every Member Guide to
Keeping Young People Safe and Saved. Nampa, Idaho: Pasific Press
Publishing Association, 2002.
Introducing GraceLink; A New Curriculum for Children’s; Sabbath Schools.
Silver Spring, Maryland: General Conference Sabbath School Department,
1999.
Irwin, Bernadine L. A Child shall Lead them: Releasing the Power of Children
as Ministers. Loma Linda, California: Millenia Publising Co.,2000.
Maspeaker, Barbara. Quick Access Ideas for Children Ministry. Lincoln,
Nebraska: AdventSource.
Robinson, Robert J. 52 Easy Program Ideas for Kindergaten Sabbath School,
Year B. Lincoln, Nebraska: AdventSource, 2003
Roehlkepartain, Jolene, ed. Children Ministry that works. Loveland,
Colorado: Group Publishing, Inc., 1991.
Tetz, Myrna and Gary Hopkins, com. We Can Keep Them in the Church.
Nampa, Idaho: Pasific Press Publishing Association, 2004.
Yount, Christine. Recruit and Nurture Awsome Volunteers for Children’s
Ministry. Loveland, Colorado: Group Publishing Inc., 1998.

MAGAZETI

Children’s Ministry. Loveland, CO: Group Publishing Inc.


Kid’s Ministry Ideas. Hagerstown, MD: Review and Herald Publishing
Association.
Evangelizing Today’s Children. Warrenton, MO: Child Evangelism Fellowship,
Inc.

TOVUTI

www.childrensministries.gc.adventis.org: Hii ni tovuti ya idara ya Huduma


za Watoto Halmashauri Kuu. Lengo lake ni kuhudumia wale wanaofanya
kazi na watoto kwa kuwapatia mawazo, nyenzo, na taarifa ambazo ni
msaada kwa viongozi na waalimu wa watoto. Pia kuna sehemu maalum kwa
ajili ya watoto na masomo ya asubuhi, shughuli na mawazo ya sanaa kwa
ajili ya watoto.

www.childmin.com: Hii ni tovuti ya Idara ya Huduma za Watoto ya Divisheni


ya Amerika ya kaskazini. Utume wake ni kuunga mkono na kusaidia wale
wanaofanya kazi na watoto katika makusanyiko.

www.KidsBibleinfo.com: Hii ni tovuti maalum kwa ajili ya watoto, wenye


umri wa miaka 6 hadi 12, ili kwamba waweze kujifunza kweli za ajabu za
Biblia katika mifumo iliyo rahisi kusoma na yenye kuvutia. Tovuti hii
imetengenezwa na mada za Biblia, visa, michezo, na mtiririko wa masomo
ya Biblia.
www.hikidz.org: Hii ni tovuti ya kuvutia sana kwa watoto umri wa miaka 6-
12. Ndani yake kuna visa, kuchunguza Biblia, uoto wa asili, kompyuta,
michezo, kumfahamu Mungu na mengi zaidi. Lengo lake ni kutoa dunia
salama kwa ajili watoto mahali ambapo wanaweza wakapafurahia,
wakagundua taarifa mpya za kuvutia kuhusu dunia, maisha, maadili ya
muhimu, n.k. pamoja na Ukristo. Tovuti hii pia inalenga kubadilika badilika,
kuwa kwa ajili ya kila mtu, kuwa fasaha katika Biblia, kutokulenga dhehebu
Fulani, fasaha kwenye Biblia, inayopatikana kwa urahisi na tamaduni zote na
inawafaa watoto wote bila kujali wanatoka wapi.

www.4kids.ag.org: Hii ni tovuti ya Taasisi ya Taifa ya Huduma za Watoto,


ambayo ipo ili kuhudumia makanisa mahalia, wachungaji wake, na walei
katika kutafuta kwao huduma bora kwa ajili ya watoto wa kanisa lao na jamii
zao. Inalenga kuunganisha sehemu nyingi za Huduma Kwa watoto katika
kanisa mahalia na inapambana kusaidia kanisa mahalia kukua kwa kuvutia,
kuwafikia, na kuwanidhamisha watoto na familia zao.

www.kidology.org: Tovuti hii inalenga kuwawezesha na kuwatia moyo wale


wanaohudumia watoto kwa kutoa mafunzo ya vitendo, nyenzo za kiubunifu
za ufundishaji, na mashauri binafsi.

www.rainbows.com: Tovuti hii inatoa nyenzo bora sana, vidokezo, makala,


na mawazo juu ya kuwasaidia watoto kuchukuliana na huzuni na maumivu.
HITIMISHO

H
uduma za Watoto zinapaswa kuwa sehemu muhimu ya Kanisa
lolote la Waadventista Wasabato. Wewe kama mchungaji, mzee
wa kanisa, unaweza ukachukua nafasi kubwa katika kuwasaidia
watoto kukuza uhusiano wa upendo na kumtuikia Yesu. Unaweza ukatoa
nafasi za kuwafundisha na kuwashauri watoto kama viongozi wa leo na
kesho. Unaweza ukavutia kusanyiko lako kuwa na njozi ya kuongoza na
kulea watoto katika safari ya kiroho. Unga mkono programu zao, na
uwahusishe katika nyanja zote za maisha ya kanisa. Kumbuka, kujenga
kanisa la kesho kunaanzia kwa watoto wa leo!

You might also like