You are on page 1of 87

MBINU ZA KUMLEA MTOTO

MBINU
ZA
KUMLEA
MTOTO

Mwl. Joyce Z. Mgaya 1


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Kimesanifiwa na kupigwa chapa na:


Ebeligisha Tanzania Co Ltd
P.o.Box 10434
Mwanza -Tanzania
Simu:+255(0)754334614,+ 255(0)693423632
Email: ebeligishatanzania@gmail.com

Mwandishi:
Mwl. Joyce Z. Mgaya
Musoma - Mara- Tanzania
Simu:+255(0)714270442,+ 255(0)759196115
Toleo la kwanza © 2021
ISBN: 978 - 9976 - 5706 -5-9
Na: Mwl. Joyce Z. Mgaya
Haki zote zimehifadhiwa, hairuhusiwi kuiga, kunakili,
kupiga chapa au kutoa kitabu hiki kwa jinsi yoyote bila
idhini ya mwandishi.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 2


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

YALIYOMO
SHUKRANI...........................................................................4
UTANGULIZI........................................................................6
SURA YA 1............................................................................8
UMUHIMU WA KULEA WATOTO KATIKA NJIA
IWAPASAYO....................................................................8
SURA YA 2..........................................................................32
KUMULEA MTOTO NI AGIZO LA MUNGU...............32
SURA YA 3..........................................................................43
KUMJUA MUNGU WA KWELI NA UWEZA WAKE.. 43
SURA YA 4.........................................................................54
KUTAMBUA UTHAMANI WA MTOTO......................54
SURA YA 5..........................................................................65
UTII KWA MUNGU NA WAZAZI.................................65
SURA YA 6..........................................................................76
FAIDA ZA MTOTO ALIYEZALIWA NA KULELEWA
KATIKA KUMCHA MUNGU NA KUMUABUDU
MUNGU NA WALA SI MIUNGU..................................76
VITABU VYA REJEA.........................................................88

Mwl. Joyce Z. Mgaya 3


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

SHUKRANI

K wa namna ya kipekee, napenda kutoa shukrani kwa


Mungu, muumba Mbingu na Nchi, aliyeniwezesha
kuandika kitabu hiki pindi nilipopata wazo juu ya kitabu
hiki miaka mitano iliyopita. Pia namshukuru mume
wangu kipenzi, Mchungaji Julius Mgaya Kituti na
watoto wetu kwa namna walivyonitia moyo na
kuniombea ili kutimiza kusudi hili.
Napenda kumshukuru Mkurugenzi wa kampuni ya
Ebeligisha Tanzania ya Mwanza, Paschal M. Francis;
kwa kuhariri, kukichapa na kunitia moyo ili nisonge
mbele katika uandishi wa vitabu.
Kwa moyo wa shukrani namshukuru Askofu Sephania
Lulegeya na familia yake ambaye kwa sasa ametangulia
mbele za haki, na viongozi wote wa jimbo la Musoma
kwa maombi yao.
Nawashukuru pia Rebeka Musa, Mkurugenzi wa W.W.I
na Renatus Karanga, Katibu wa C.W.T Jimbo la
Musoma kwa maombi yao na kunitia moyo kuendelea
kukiandika kitabu hiki.
Kipekee kabisa namshukuru Mratibu Mkuu wa mafunzo
na malezi ya watoto kitaifa, Elias Ntilabigwa wa makao
makuu Dodoma, kwa kuniongezea maarifa ya namna ya
kulea na kusimamia watoto niliposhiriki mafunzo
aliyoyaratibu Mwanza.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 4


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Nawashukuru pia viongozi na washirika wa kanisa


tunaloliongoza ambao mara zote wapo kunitia moyo,
kunishauri na kuniombea ili niweze kutimiza huduma
aliyoiweka Mungu ndani yangu.
Ninao wengi wa kuwashukuru lakini itoshe tu kusema
nawashukuru wote, hata kama sijawataja majina, na
nathamini sana michango yenu.
Asanteni sana na Mungu awabariki. Amina!

UTANGULIZI

K atika ulimwengu wa sasa watu wamesahau


kabisa umuhimu wa kulea watoto katika njia
Mwl. Joyce Z. Mgaya 5
MBINU ZA KUMLEA MTOTO

ipasayo; wamesahau kabisa kuwa kila mzazi mkristo


anayemwamini Mungu katika Roho na kweli anao
wajibu wa kumlea mtoto wake katika njia impasayo.
Tunapaswa kujua ni muhimu na lazima kwa mzazi,
mlezi na walimu wa watoto makanisani, kujua
kwamba tunao wajibu mkubwa wa kuwalea watoto
vizuri katika njia iwapasayo, kama neno la Mungu
linavyotuagiza katika kitabu cha (Mithali 22.6).
“Mlee mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha,
hata atakapokuwa mzee”.
Kitabu hiki kinazungumzia umuhimu wa kulea
maana kama tunavyojua watoto ni warithi wa taifa,
warithi wa ulimwengu, na warithi katika kazi ya
Mungu.
Serikali ya Tanzania inawajali watoto, kwani
inaweka jitihada za kuwalea watoto na kuwatunza.
Ndiyo sababu tunaona kuna vituo vya watoto
yatima, shule, hospitali, n.k; hivi vyote ni njia za
kuwalea watoto kwa kuwa inajua umuhimu wa
watoto na kwamba ni warithi wa kesho katika taifa.
Hivyo basi wazazi tunaomcha Mungu, kanisa, na
watumishi wa Mungu tunapaswa kuujua umuhimu
huu wa kuwalea watoto vizuri kwa kuwa tunajua
kabisa kwamba wao ni warithi wa mali zetu, tabia
zetu, mienendo yetu, huduma zetu, utumishi
tunaoufanya mbele za Mungu.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 6


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Mungu hakutuumba tuishi tu bali alituumba na


kutupatia neema ya wokovu ili tumtumikie. Hivyo
katika wokovu tulio nao tunapaswa kumwabudu na
kumtumikia Mungu pamoja na watoto wetu, kwa
kujua kuwa tu warithi pamoja na watoto wetu.
Musa akamwambia Farao hawataacha kitu hata
ukwato maana hawajui atakachokihitaji Bwana (Kut
10:8-9, 24-26)

SURA YA 1

UMUHIMU WA KULEA WATOTO KATIKA NJIA


IWAPASAYO.

1. NINI MAANA YA MALEZI AU KULEA?

Mwl. Joyce Z. Mgaya 7


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

(a) Malezi au kulea ni tendo ama matendo


yanayofanywa na wazazi, walezi, na jamii, kwa
mtoto kwa lengo la kumwangalia, kumkuza,
kumlinda, kumwendeleza na kumwongoza mtoto
katika maeneo yafuatayo; ambayo ni kumlea mtoto:
i). Kimwili
ii). Kiakili
iii). Kijamii
iv). Kihisia
v). Kimaadili na
vi). Kiroho
ili mtoto aweze kuishi na kukua vizuri na
kukubalika katika familia yake, jamii na taifa pia.
Ni lazima mtoto alelewe vizuri katika maeneo hayo
sawasawa na neno la Mungu katika (Luka 2:52)
“Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na
kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu”.

(b) Katika kitabu hiki tunajifunza na kuona jinsi


Bwana Yesu alivyoweza kukua na kuendelea vizuri
kwa sababu alilelewa vizuri na Yusufu pamoja na
Mariamu mama yake.
Hawa wazazi au walezi wa Yesu Kristo walimlea
Yesu vizuri na kumwangalia kwa bidii; hata wakati
fulani aliwapotea wazazi wake akabaki hekaluni
akiwa mdogo, walirudi kumfuata. Hiyo ilikuwa ni
ishara ya uangalizi.
Kwa namna nyingine tunaweza kusema kulea, ama
malezi ni uangalizi wa karibu sana kwa mtoto.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 8


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

(c). Hali kadhalika Biblia inatueleza wazi kuwa


Yusufu hakuwa Baba mzazi wa Yesu Kristo, tena
walipokuwa katika harakati za uchumba, ndipo
Yusufu alipogundua kuwa mchumba wake ana
ujauzito, naye akaazimu kumwacha kwa siri, neno
linasema kwa sababu alikuwa mtu wa haki.
Hivyo hakutaka kumwaibisha mchumba wake,
lakini pia alipokuwa katika kufikiri kumwacha
ndipo Malaika wa Bwana alipomtokea na
kumjulisha mpango wa Mungu.
(Mathayo 1:20) “Basi alipokuwa akifikiri hayo,
tazama malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto,
akisema, Yusufu mwana wa Daudi usihofu
kumchukua Mariamu mkeo, maana mimba yake ni
kwa uwezo wa Roho Mtakatifu”.
Haya yote yalitokea baada ya Mungu kuona kuwa
hawa watu wawili wana sifa za kumlea huyo mtoto
ambaye alihitaji kwa kupitia wao afike duniani
kuwaokoa watu; mimi, wewe na watoto wetu.

i). Binti Mariamu alikuwa na sifa ya kuishi maisha


matakatifu, aliutunza ubinti wake hivyo alikuwa na
uwezo mzuri wa kumlea mtoto katika maadili mema
na kumfanya aendelee kukua katika utakatifu kama
jinsi mtoto mwenyewe alivyozaliwa katika
utakatifu.

ii). Pia bila kumsahau kijana Yusufu jinsi alivyo


kuwa mtu wa haki, hii inaonesha kuwa naye katika
haki yake alimwendeleza mtoto kukua na kuwa mtu

Mwl. Joyce Z. Mgaya 9


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

mwenye haki vilevile, kama ilivyompasa kuwa mtu


wa haki.

(d) UMUHIMU

(i). Hivyo basi katika hatua za awali za malezi ya


watoto ushiriki makini wa wazazi au walezi katika
maeneo mbalimbali ni muhimu na ni lazima kwa
ajili ya makuzi mazuri ya watoto; kama
inavyofanyika katika vituo vya kulelea watoto
mashuleni, makanisani, n.k.
Kulitambua hili ni swala la msingi kabisa la
kuwalea watoto vizuri bila ubaguzi wa kijinsia,
rangi, kabila, n. k.
Ni vyema mtoto akalelewa vizuri kimwili, kiakili,
kimaadili, kijamii, na kiroho zaidi maana huyu
mtoto akilelewa kiroho pia atajifunza, kuwa na
maadili mema.

(ii). Hili jambo la kuwalea watoto vizuri ipasavyo


halijaanza katika wakati huu tulio nao bali lilianza
tokea mwanzo; yaani tokea Agano la Kale.
Mungu alihitaji watoto walelewe vizuri na
wasikizishwe maneno ya Kimungu; maana Mungu
alijua wakiyashika maneno yake watatenda vyema
tu. Ukisoma katika kitabu cha (Kumbukumbu la
Torati 6: 1-2, 25) utaona;
“Na hii ndiyo sheria na amri, na hukumu
alizoziamuru Bwana Mungu wenu, mfundishwe
mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia

Mwl. Joyce Z. Mgaya 10


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kuimiliki, upate kumcha Bwana Mungu wako,


kushika amri zake zote, na sheria zake,
ninazokuamuru, wewe na mwanao na mwana wa
mwanao siku zote za maisha yako, tena siku zako
ziongezwe”. “ .. tena itakuwa haki kwetu,
tukitunza kufanya maagizo haya yote mbele ya
Bwana, Mungu wetu kama alivyotuagiza.”

(iii). Haya ni maneno ya Mungu kupitia kinywa cha


Musa ili kuwafikia wana wa Israeli na wana wao.
Kwa wakati ule maneno haya yalikuwa ni agizo na
amri na sheria.
Ina maana gani kusema ilikuwa ni agizo ama amri
na sheria?
Ni kwamba agizo au amri au sheria, ikiisha
kuamriwa au kupitishwa ni kutenda, tena mtu
aliyeonekana anakwenda kinyume na amri au sheria
yoyote iliyowekwa aliadhibiwa.

(iv).Wakati mwingine naweza kusema pia kuwa


katika Agano la Kale, walionekana kupewa maagizo
na jukumu la kuwalea watoto wao vizuri ilikuwa ni
taifa moja la Israeli, ambao walikuwa ndio taifa la
Mungu.
Lakini sasa wakati huu tulionao ama baada tu ya
Yesu kuja ulimwengu wote tulipewa agizo ama
maagizo.

(v). Basi baada ya kusema hayo, shauku yangu ni


kwamba na wakati huu tulionao bado tuna nafasi

Mwl. Joyce Z. Mgaya 11


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kubwa ya kuchukua jukumu la kuwalea watoto wetu


vizuri; Kimwili, Kijamii na Kiroho ili nao
wakaendelea vizuri kabisa na kuvifikia viwango vile
anavyohitaji Mungu.
(Mithali 23:24) “Baba yake mwenye haki
atashangilia. Naye amzaaye mtoto mwenye hekima
atamfurahia”.
Ndugu msomaji wa kitabu hiki Mungu anatuonesha
ama kutufundisha kuwa mtu aliye na mtoto mwenye
haki atashangilia, Na pia aliye na mtoto mwenye
hekima atamfurahia. Hapo utajifunza na kuona kuwa
mtoto mwenye haki ni wa thamani sana na mtoto
mwenye hekima anahitajika ili mzazi awe na furaha.
Sasa wapatikanaje hawa watoto?
Watapatikana kwa njia ya malezi bora
yanayohitajika kwa mtoto na mtoto ayapate kwa
wakati sahihi.

2. MALEZI YANAANZIA WAPI?

(a). Katika kipengele hiki tuangalie kwa makini


kuwa malezi yanapaswa kuanzaia wapi.
Hapa ndiyo sehemu nyeti kabisa ama ya kwanza na
ya muhimu kabisa ambayo watu wameisahau na
baadaye kuyageuza malezi kuanzia pale ambapo
palihitaji mwendelezo lakini baadaye ndipo pakawa
mwanzo.
Kwa kusema hivyo niingie moja kwa moja kwamba
malezi bora na ya msingi kabisa huanzia tumboni
pale tu mama anapojitambua kwamba ameshika

Mwl. Joyce Z. Mgaya 12


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

ujauzito hapo ndipo malezi yanapaswa kuanza hapo


kwa ushirikiano wa baba na mama, kwa pamoja na
jamii pia,
Mama anapojua kuwa ni mjamzito moja kwa moja
anapaswa kuchukua hatua na kufuata taratibu za
kiafya na kuwasikiliza wataalamu wa kiafya na
kufuata maelekezo ambayo yatakuwa ndiyo mwanzo
mzuri wa kumsaidia, kuanza kuyachochea malezi na
makuzi ya mtoto anapokuwa tumboni. Malezi
ambayo yatamwendeleza mtoto kukua, kimwili,
kiakili, kijamii, kimaono, kihisia na kimaadili na
kufikia hatua ya kiroho vizuri zaidi.
Kumbuka mtoto anapokuwa tumboni huwa ni
chombo tupu kinacho hitaji kuwekwa tayari kwa
ajili ya kujazwa vitu viwe vizuri au vibaya.
Kama nilivyokwisha kusema mama anapokuwa
mjamzito anapaswa kwenda katika vituo vya afya na
kupewa maelekezo ambayo yatampatia msaada
ambao pia utamsaidia, kuanza au kuwa na hatua ya
mwanzo wa kumlea mtoto vizuri kuanzia tumboni.
Kwa mfano: Wamama au mama anapokuwa
mjamzito huelekezwa aina ya vyakula ambavyo
vitampa sapoti ya kumkuza mtoto aliye tumboni na
kumsaidia na kuimarisha afya ya mama na mtoto na
ambavyo havina madhara kwa mtoto, pia kutoa
ushauri, kwa walezi wote.
Mfano: Mama apewe muda wa kupumzika na
mambo mengine yatakayoimarisha afya yake.
Lakini vivyo hivyo hata katika habari ya kiroho,
malezi huanzia tumboni. Mama yake Samsoni

Mwl. Joyce Z. Mgaya 13


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

alipewa maagizo na Mungu juu ya ujauzito wa


mtoto Samsoni, jinsi atakavyozaliwa na
atakavyolelewa na ni vitu gani mama yake
hakutakiwa kuvitumia.
(Waamuzi 13:3-4) “Malaika wa Bwana akamtokea
yule mwanamke, akamwambia, Tazama, wewe
sasa u tasa, huzai; lakini utachukua mimba nawe
utamzaa mtoto mwanaume, Basi sasa jihadhari,
nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile
kitu kilicho najisi.”
Hii pia inaonesha kuwa Mungu anaijua vizuri hatua
hii ya mwanzo kabisa kuwa ni sehemu ambayo
ikikosewa italeta shida baadae, lakini pia ikipatiwa
nafasi nzuri italeta manufaa mazuri baadae.
Kwa hiyo tunapaswa kujifunza zaidi katika malezi
lakini tukifuata hatua hii ya mwanzo kabisa na kwa
kuongozwa na neno la Mungu, kuwa kuangalia
watumishi, wa Mungu, waliongozwa na Mungu
katika hatua ya malezi ya mwanzo na wakawalea
watoto vizuri, ambao baadae, walikuwa ni msaada
katika maeneo ambayo Mungu alihitaji wawepo.
Kama vile Yusufu na Mariamu mkewe ambao
walimtii Mungu, na kufuata maagizo katika kumlea
Yesu Kristo mkombozi wa ulimwengu (Mathayo
1:18-24).
Lakini pia Zakaria na Elizabethi, ambao walikuwa
wamekwisha kuwa wazee kabisa na kukata tamaa ya
kuzaa lakini Bwana aliwatokea, kwa ajili ya kuwapa
maelekezo ya kile kitakachozaliwa.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 14


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

(Luka 1:5-7) “Zamani za Herode, mfalme wa


Uyahudi, palikuwa na kuhani mmoja, jina lake
Zakaria, wa zamu ya Abiya, na mkewe alikuwa
mmojawapo wa uzao wa Haruni, jina lake
Elizabeti. Na wote wawili walikuwa wenye haki
mbele za Mungu, wakiendelea katika amri zote za
Bwana, na maagizo yake bila lawama. Nao
walikuwa hawana mtoto, maana Elizabeti alikuwa
tasa, na wote wawili ni wazee sana”.

Hapo tunajifunza na kuona kuwa kabla ya hatua za


mwanzo Mungu, huwa anawahitaji wazazi ama
walezi wenye sifa ambazo zitawasaidia, kuwapa
nafasi nzuri ya kuwalea watoto. Hawa watu
tuliowaona hapo juu na kuangalia habari zao kwa
ufupi; moja kabisa walikuwa na sifa za kuwa watu
wa haki na wenye kuishi maisha matakatifu, maana
pasipo maisha matakatifu na yenye haki hauwezi
kulea watoto kama ipasavyo.
Maana yake ni nini kusema hayo?
Unaona hapo ilifika wakati Mungu alihitaji
wasinywe vileo vyovyote, ili kusudi watoto
wasinajisiwe, maana wao ni maalumu kwa kazi ya
Mungu.
Hivyo tunajifunza kuwa umuhimu mkubwa
ulikuwepo wa wazazi hawa kuwa na ushirikiano wa
karibu maana wote walikuwa na haki.
Tunaweza kujifunza hapa moja kwa moja na kuona
kuwa ukosekanaji wa watoto, walio lelewa vizuri
katika maadili mema, yanayojumuisha maeneo yote

Mwl. Joyce Z. Mgaya 15


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

yanayohusu ukuaji wa mtoto kuanzia mwanzo,


kumbe pia inaweza kuwa ni wazazi walezi.
Wakipatikana wazazi watakao kubali kujifunza,
kufuata kanuni na taratibu zote za kitaalamu kiafya
kimaadili na kiroho tunaweza kukisaidia kikazi
tulichonacho katika swala la mlezi tokea mwanzo
kwa ushirikiano wa kutosha toka kwa wazazi,
walezi, jamii na kufikia ngazi ya taifa.
Katika ulimwengu huu kuna mambo ambayo
tunaweza kujifunza na yakakusaidia pia kutupigisha
hatua fulani.
Kwa mfano: Ulimwengu usema, “Ukiona vyaelea
vyaundwa”.Lakini pia Bwana Yesu alipokuwa
katika mafundisho yake alikuwa na maneno ya
kuwafanya watu wachangamke. Muda mwingine,
alisema katika (Mathayo 7:24-28) “Basi kila
asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya,
atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga
nyumba yake juu ya mwamba; Mvua ikanyesha
mafuriko yakaja, pepo zikavuma zikaipiga nyumba
ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa
juu ya mwamba. Na kila asikiaye maneno yangu
asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu,
aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua
ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma,
zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake
likawa kubwa.”
Tunajifunza ili vielee ni lazima viundwe na ili
viundwe lazima kusikiliza maneno ya Mungu ndipo
tutajenga vitu imara.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 16


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Kwa hiyo ili kuhakikisha kuwa mtoto anapata


malezi mazuri tangu anapokuwa tumboni, wazazi na
walezi hawana budi kuzingatia mambo muhimu.
Katika ile hatua ya kwanza kabisa mama
anapotambua kuwa yeye ni mja mzito, wazazi wote
wawili wanapaswa,
kuonesha mambo fuatayo kama vile:-
i).Ushirikiano
ii).Upendo
iii).Kutoa huduma zinazostahili kwa mama
mjamzito; Kama vile kupelekwa kwenye vituo vya
afya kwa ushirikiano wa baba na mama. Mama
mjamzito apewe tiba na ushauri wa kitaalamu zaidi.
Mama apewe muda wa kupumzika, kuepukana na
mambo ya mila, desturi na tamaduni za ajabu kwa
mama mjamzito zitakazopelekea kiumbe ama roho
ambayo iko tumboni isikue vizuri.
Bila kusahau mama mjamzito au wazazi walezi wote
wawe watu wa ibada, wampende Mungu na
wahudhurie katika nyumba za ibada, wahakikishe
wanafanya mambo yanayompendeza Mungu wajue
kuwa kuna vitu anavyorithi mtoto katika hatua hii ya
mwanzo.
Wazazi wasiwe watu wa kuzoelea ulevi, matusi,
wasiwe watu wenye kauli chafu,
Ndio sababu wenzetu katika Biblia walizuiliwa
kutumia vileo ambavyo vitamkosesha mtoto Baraka.
Sasa hata sisi kwa wakati huu tunao uwezo wa
kujizuia, kwa sababu hatujui atakayezaliwa kwetu ni

Mwl. Joyce Z. Mgaya 17


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

mtu wa namna gani; ili na sisi tusiwakoseshe watoto


na Mungu, na pengine kuzuilia baraka zao.
Mungu wetu humjui mwanadamu, tokea mwanzo
angalipo tumboni na kabla hajatoka.
(Yeremia 1:4-5) “Neno la Bwana lilinijia,
kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo
nalikujua, na kabla hujatoka tumboni
nalikutakasa; nimekuweka, kuwa nabii wa
mataifa.”
Kwa hiyo Mungu humjua mtu tokea mbali tena, na
kumuwazia mawazo mema kuliko sisi tunavyoweza
kujiwazia, au kuwawazia wengine.
Kwa hiyo unapaswa kujua hayo na kuyazingatia
kama mzazi ama mlezi.
(Yeremia 29.11) “Maana nayajua mawazo ninayo
wawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani
wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku
zenu za mwisho”.
Katika hili andiko utaona Mungu anaposema
anatuwazia mema siyo sisi peke yetu ni sisi pamoja
na watoto wetu maana anatujua sisi zaidi pengine
tunavyojijua sisi. Na ukisoma katika kitabu cha
Samweli kinamuelezea mwanamke, Hana, jinsi
alivyokuwa ni mwanamke mwenye roho ya uchungu
na machozi mengi kwa sababu ya kukosa mtoto,
naye akamuomba Mungu ampe mtoto.
Biblia inaeleza jinsi alivyomwekea Bwana nadhiri
ya huyo mtoto atakapompata hii pia ilimpelekea,
aweze kumlea mtoto huyo vizuri hata ulipofika
wakati wa kumuachisha maziwa na kumpeleka

Mwl. Joyce Z. Mgaya 18


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

nyumbani mwa Mungu kama ilivyokuwa ahadi


yake, ama nadhiri yake.
(ISamweli 1.10-11) “Naye huyo mwanamke
alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamwomba
Bwana akalia sana. Akaweka nadhiri, akasema,
Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia
teso la mjakazi wako, na kunikumbuka wala
usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi
mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapo
mpa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake,
wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe”.
Hili halikuwa swala rahisi sana kama tunavyoweza
kudhani, najua kabisa kuwa, hili jambo lilimpa
mama huyu kazi kwa sababu aliahidi kumpa Bwana
huyo mtoto, sasa basi alikuwa na wajibu wa kumlea
vizuri.
Na kama inavyojieleza katika Biblia, ndivyo alivyo
fanya mwanamke Hana, na kumpa Bwana huyo
mtoto ambaye alikuwa mkombozi wa Israeli wakati
huo ambapo sauti ya Mungu ilikuwa imekoma kwa
watu wake lakini kwa kupitia mtoto Samweli
ikasikika tena.
(1Samweli 3:1) “Basi mtoto Samweli akamtumikia
Bwana mbele za Eli. Na neno la Bwana ilikuwa
adimu siku zile; hapakuwa na mafunuo dhahiri.”
E. BAADA YA KUZALIWA MTOTO.
Baada ya mtoto kuzaliwa wazazi au walezi hawana
budi kuendelea na wajibu wao wa kulea mtoto
mwenye umri wa miezi 0 - 6 kwa kufuata kanuni
zile za mwanzo, ambazo ni za kumlea mtoto:

Mwl. Joyce Z. Mgaya 19


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

i) Kimwili
ii) Kiakili
iii) Kihisia
(iv) Kimaadili
v) Kijamii na
vi) Kiroho au dini.
ili mtoto aweze kuishi, kukua vizuri na kukubalika
na jamii na katika maeneo yote anayotarajia
kukabiliana nayo maana anapokua huyu mtoto,
anatarajiwa kuwa atakua na kuongezeka kimwili,
kiakili na hata kufika umri wa kuanza shule; ambayo
ni maeneo atakayoanza kukabiliana nayo.
Akiwa peke yake lakini yatakuwa na mwendelezo
mzuri ama yatamfaa mtoto ikiwa amewekewa
msingi mzuri unaoweza kumpa kujitegemea katika
hatua ya mwanzo.
Kwa hiyo baada ya kuzaliwa mtoto tunapaswa
kutumia mbinu mbalimbali ambazo zitamsaidia
mtoto kuendelea kukua vizuri.
A. MTOTO ANAKUAJE KIMWILI?.
Mtoto hukua kimwili, kwa kuongezeka kimaumbile
ambako kunaambatana na mabadiliko katika urefu,
uzito, upana na kukua kwa ubongo, kulingana na
umri wa mtoto. Ili mtoto aendelee kukua kimwili,
anahitaji huduma muhimu kama vile: chakula
kilicho na mchanganyiko wa virutubisho vyote na
vyenye kutosheleza mahitaji ya mwili wa mtoto
kulingana na umri wake, huduma za afya, upendo,
mafunzo ya awali, ulinzi, usalama, na mazingira safi
na salama.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 20


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Haya ni mambo ambayo huonekena kuwa ya


kawaida sana ambayo pengine hayawezi
kuzingatiwa na kuangaliwa katika maendeleo ya
ukuaji wa mtoto kimwili. Lakini tunapaswa
kukumbuka kuwa Bwana wetu Yesu Kristo
alizaliwa katika mwili na wazazi wake
walimwangalia maendeleo yake ya ukuaji kimwili
na kufuata kanuni na taratibu walizopewa na Mungu
kwa kuongozwa na Roho na kuhakikisha mtoto
anakua vizuri kimwili na kuongezeka, hadi kufika
wakati wa Bwana aliohitaji mtoto Yesu afanye
alichokusudiwa.
(Mathayo 2:13) “Na hao walipokwisha kwenda
zao, tazama, Malaika wa Bwana alimtokea Yusufu
katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto
na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata
nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta
mtoto amwangamize”.
Hapo utajifunza na kuona Mungu alikuwa
anaangalia uthamani wa mtoto huyu katika ukuaji,
maana mtoto alipokuwa katika kukua na
kuongezeka kimwili, ndipo adui alipokuwa katika
mpango wa kumuangamiza mtoto apotee kabisa
kimwili. Kwa hiyo Mungu akawapa wazazi akili na
maarifa ya kumlea na kumtunza mtoto ili aendelee
vizuri, kukua kimwili na kuongezeka hadi hali ya
kiroho.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 21


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Ili mtoto akue kimwili anahitaji huduma nzuri


ambazo ni lishe, afya, kuoneshwa upendo, na
kuwekewa ulinzi wa kutosha.
Hivyo, hata sisi katika nyakati hizi tulizonazo bado
tunayo nafasi ya kuwalea watoto kwa kuongozwa na
Neno la Mungu kama tunavyojifunza.
B.UKUAJI WA MTOTO KIAKILI.
Mtoto pia hukua na kuongezeka kiakili. Kukua na
kuongezeka kiakili ni kuongezeka ufahamu, uwezo
wa kufikiri, kutafakari na kutatua matatizo yake
kulingana na umri. Ukuaji na maendeleo ya mtoto
kiakili unahusisha pia mabadiliko ya mtoto kitabia,
usikivu,ubunifu, udadisi na jinsi mtoto anavyopokea
na kutafsiri mambo mbalimbali katika mazingira
yanayomzunguka.
Ukuaji wa ubongo wa mtoto unaanza tangu mimba
inapotungwa, imedhihirika kitaalam kuwa ubongo
wa mtoto hukua kwa kiwango cha asilimia 80 katika
kipindi cha ujauzito hadi miaka 3 ya mwanzo wa
maisha yake. Hivyo kuna uhusiano mkubwa kati ya
mama mjamzito na ukuaji wa ubongo na akili ya
mtoto.
Kwa hiyo ni muhimu mama mjamzito apate huduma
zote muhimu, kama zile nilizoelezea katika
kipengele cha malezi yanaanzia wapi, maana katika
hatua hii inahitaji utulivu wa kutosha katika familia
ili mama aweze kulea kile ambacho kiko tumboni
vizuri kwa ushirikiano, pia mama apunguziwe kazi
nzito ambazo zinaweza kuathiri ukuaji wa ubongo
na kuongezeka kiakili. Mama mjamzito apewe lishe

Mwl. Joyce Z. Mgaya 22


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

nzuri. Asile vyakula vitakavyomsababishia mtoto


aliye tumboni madhara, ya akili yanayosababishwa
na ubongo.
(Waamuzi 13:4) “Basi sasa, jihadhari, nakuomba
usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho
najisi”.
Pia mama mjamzito aepukane na mambo mabaya
yasiyompa Mungu utukufu maana katika
utengenezaji wa akili ama ubongo kuna vitu mtoto
atarithi kutoka kwa mama zaidi. Kwa mfano, Mama
asiwe mtu wa matusi, mwizi, muongo, mzushi, na
pia wazazi wote wawili wasiwe watu wa kupenda
ugomvi ili badala yake wawe watu wenye kumcha
Mungu. Hii pia itasaidia huyo mtoto atakayezaliwa
ama anayetarajia kuzaliwa kukua vizuri kiakili.
Na mambo mengine mengi kama hayo yasiwepo. Ili
kusaidia ukuaji wa mtoto kiakili na kufanya ubongo
wake kuwa vizuri zaidi, wazazi wote wawe watu
wenye busara na hekima.
Pia kuna hatua ya ukuaji wa mtoto kiakili baada ya
kuzaliwa mara tu mtoto anapozaliwa huanza
kujifunza juu ya mazingira anamoishi kwa kutumia
milango yake ya fahamu ambayo ni: Kuona,
Kunusa, Kusikia, Kuonja na Kugusa.
Kwa hiyo katika hatua hizi tunapaswa pia kuweka
mazingira vizuri mtoto, anapokuwa amefika umri
wa kuona na kutambua vitu awekewe picha nzuri
katika Televisheni zetu majumbani, wasione picha
mbaya ambazo zitamfanya atakapokua na yeye
afuate matendo mabaya.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 23


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Na katika kunusa pia mtoto asipelekwe kwenye


majumba mabaya kama vile kwenye baa na
vilabuni. Wazazi na walezi wasiwe walevi, mtoto
akizoelea zile harufu anaweza kumsababishia kuwa
mlevi baadae.
Na katika kusikia nimeelezea kwenye hatua ya
ujauzito, mtoto anapaswa kusikia vitu kwenye
masiko yake kama vile nyimbo nzuri, maneno
mazuri, lugha zenye matamshi mazuri na vitu
vingine ambavyo havitamsababishia mtoto madhara
katika maendeleo ya ukuaji wake wa kiakili.
Pia kwenye kuonja mtoto ni mtu ambaye anapenda
kujaribu kila kitu kwa hiyo anapofika katika umri
wa kuweza kuchukua kitu na kuonja basi asiwekewe
karibu vitu ambavyo ni hatari; mfano;
Dawa, sumu za kuua wadudu n.k. Vivyo hivyo
katika kugusa mtoto akae mbali na moto, maji ya
moto na vitu vyenye ncha kali maana anaweza
akagusa na vikamletea madhara makubwa katika
maisha yake. Kwa hiyo katika hatua hizi mbili za
mwisho kuonja na kugusa mtoto apewe vitu vizuri
vya kuchezea, ambavyo havitamwathiri mtoto katika
ukuaji wake wote na pengine kumsababishia
ulemavu.

C. UKUAJI NA MAENDELEO YA MTOTO


KIHISIA NA KIMAADILI.

Hisia ni nini?

Mwl. Joyce Z. Mgaya 24


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Hisia ni hali inayojitokeza baada ya mtu kukabiliwa


na aina fulani ya tukio au kwa kupata habari au
taarifa. Hisia hizo hujidhirisha kwa njia ya hasira,
chuki, furaha au upendo, kwa kusema hivyo naweza
kusema kuwa mtoto nae huwa anapata hisi au huwa
na hisia.
Kwa hiyo wazazi na walezi wanapaswa kulitambua
hilo kuwa mtoto nae huwa anahisi na tunapaswa
kujua, ukuaji wa hisia kwa mtoto ni hali
inayomwezesha mtoto kuelewa hisia zake na
kujifunza namna ya kudhibiti. Hisia anazoonesha
mtoto zina umuhimu wa pekee katika kukua na
kuendeleza tabia na utu wake.
Hivyo wazazi na walezi wanapaswa kuwa na
mwitikio chanya na hisia hizo ili kumwezesha mtoto
kuzionesha kuzielewa na kudhibiti hisia hizo. Mtoto
anaweza kuonesha hisia hizo kutokana na sababu
mbalimbali; Kwa mfano mtoto anapokatazwa
kuchezea maji machafu, kwa hasira atalia
kwasababu haelewi kwa nini asiendelee na mchezo
wake. Pia anaweza kuonesha hisia ya furaha
anapofanyiwa mambo mazuri; kwa mfano
anapotimiziwa mahitaji yake.
Maadili ni nini?.
Maadili ni uwezo wa mtu kutambua na kutenda
ipasavyo katika jamii anamoishi.
Hivyo mtoto anapaswa kukua na kulelewa vizuri
katika ukuaji na maendeleo ya mtoto kimadili.
Mtoto anapozaliwa hajui mema wala mabaya, bali
anajenga maadili kutokana na kufundishwa na kuiga

Mwl. Joyce Z. Mgaya 25


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

mienendo ya watu wengine anao ishi nao. Matendo


yanayooneshwa na watu walio karibu na mtoto
yamvute zaidi na kuigwa kuliko maneno au amri
anazopewa mtoto katika kumjengea tabia na utu
wake, kwa mfano. Mzazi au mlezi anapoonesha
hasira kwa kukaripia, kutukana au kumpiga mtoto
anapokosea. Mtoto atajifunza katika hali hiyo kuwa,
ndiyo njia sahihi ya kutatua tatizo linapojitokeza,
mtoto anajifunza kuwa mvumilivu, kutumia busara
na kuwa mwema, kwa wengine iwapo mzazi au
mlezi atakuwa mvumilivu na kumwelekeza mtoto
anapokosea kwa upole na utaratibu.
Wazazi walezi na jamii kwa ujumla watambue kuwa
ukuaji na maendeleo ya mtoto kihisia na kimaadili
unajengeka kutokana na mifano, watakayoonesha
wazazi au walezi kwa matendo mazuri
atakayofanyiwa mtoto katika umri wake pia.
MATENDO YA MTOTO NA NAMNA YA
KUENDELEA KUYACHOCHEA.

UMRI MATENDO YA HATUA ZA


MTOTO UCHANGAMSHI
Analia akiwa na njaa; Aonyeshwe upendo
kama amechoka au ana
maumivu.
Ajengewe imani na
Anafurahi au hali ya usalama
Miezi kutabasamu. kwa kuitikiwa hisia
zake.
0-6 Mfano:

Mwl. Joyce Z. Mgaya 26


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kumnyonyesha,
kucheza naye na
kuimba.
Anafurahi na
kutabasamu mahitaji Kumwangalia
yake yakitimizwa. mtoto unapoongea
naye.
Anajisikia salama au
kupendwa Kuongea na mtoto
anapobebwa au kwa tabasamu,
kukumbatiwa. akumbatiwe na
kubebwa.

Anamwamini mama Asiachwe peke


au mlezi aliyemzoea. yake kwa muda
mrefu.
Anashituka anaposikia
mshindo au kelele kali. Apewe vifaa vya
michezo.

Miezi Kama
Anamkubali mtu ilivyoainishwa
aliyemzoea. hapo juu pamoja
7 - 12 na:
Anaogopa kutengana
na mama au mlezi. Kumzoeza kuwa na
mahusiano na watu
Anatabasamu na wengine zaidi ya
anacheza bila mama.
wasiwasi akiwa yupo
karibu na mtu Kumwimbia mtoto.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 27


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

aliyemzoea.
Kuongea naye.
Anaonyesha wasiwasi
au uoga wa kuanguka Kucheza naye.
toka sehemu za juu.

Anakasirika
anaponyang’anywa
kitu alichoshika.

Mwaka
Anaonyesha upendo. Kama
1-2 ilivyoainishwa
Uoga kwa mtu hapo juu pamoja
asiyemzoea hupungua. na:

Anashtuka na kuogopa Kumsikiliza na


iwapo atatishwa kwa kumpa maelekezo.
maneno au kitu.
Kumsimulia hadithi
Huona aibu kwa zenye kuonyesha
wageni ujasiri.

Ana hasira za haraka Kutosimulia hadithi


zinajitokeza kwa au kumwonyesha
kununa, kujitupa chini, vitu vya kumtia
kugalagala, kujipiga hofu au wasiwasi.
kichwa, kumpiga au
kumtupia kitu mtu. Kumhimiza mtoto
mwenye aibu
kujieleza kwa

Mwl. Joyce Z. Mgaya 28


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

uhuru na njia
mbalimbali.

Miaka
Anaonyesha huruma. Kama
3-4 ilivyoainishwa
Anapenda kusifiwa. hapo juu pamoja
na:
Ana uwezo wa
kudhibiti hisia hasi. Apewe nafasi ya
kucheza na
kupumzika

Aendelee
kusaidiwa
kuzionyesha na
kuzielewa hisia
zake

Aelekezwe njia
mbalimbali za
kudhibiti hisia zake
kwa mfano kuimba,
kuchezea, vifaa vya
michezo, kuchora.

Miaka Anazielewa hisia zake Kama


na ana uwezo wa ilivyoainishwa
5-6 kudhibiti hisia hizo. hapo juu pamoja
na:

Mwl. Joyce Z. Mgaya 29


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Aelekezwe kwa
upendo umuhimu
wa kupendana
kusuluhisha
migongano kwa
njia ya kuzungumza
na kusameheana.

Alindwe na hofu
zinazojitokeza

Afundishwe
taratibu za
kushirikiana na
watu wengine.

Anajiamini. Kama
Miaka ilivyoainishwa
Mbishi. hapo juu pamoja
7-8 Anaweza kuelezea na:
hisia na mahitaji yake.
Aelekezwe
Anaweza kusema kudhibiti hisia
uongo akitishwa zake.

Hizo ni sehemu mojawapo za muhimu ambazo


tukizingatia vizuri katika hatua za mwanzo tutakuwa
tumeweka msingi mzuri utakaoendeleza, mambo
mengine, ya malezi kwa ujumla.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 30


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

SURA YA 2

KUMLEA MTOTO NI AGIZO LA MUNGU.

S wala la kuwalea watoto ni agizo la Mungu.


Tokea mwanzo Mungu alitaka watoto walelewe
vizuri.
Mungu alihitaji watoto wafundishwa mambo ya
kawaida yanayohusu maisha ya kila siku ya
mwanadamu.
Lakini pia alihitaji wafundishwe neno na kuzishika
sheria, na amri zake, Ndiyo sababu hata Mungu
alipokuwa akizungumza na Musa, akimpa maagizo
kwa ajili ya wana wa Israeli, kuhusu kumcha Mungu
na kumtumikia wasiache kuwaambia watoto na
watoto wa watoto wao.
(Kumbukumbu 6:1-2) “Na hii ndio sheria, na
amri na hukumu, alizoziamuru Bwana, Mungu
wenu mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile
mnayoivukia kumiliki, upate kumcha Bwana,
Mungu wako, kushika amri zake zote, na sheria
zake, ninazokuamuaru, wewe na mwanao, na
mwana wa mwano, siku zote za maisha yako, tena
siku zako ziongezwe”.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 31


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Hapa utaangalia swala ama jambo hili la kulea


watoto wetu vizuri, linakubalika kabisa mbele za
Mungu, tena ni wajibu wetu. Hawa walikuwa na
ahadi ya kuvuka, kwenda kuimiliki nchi, lakini sisi
tuna ahadi ya kuurithi uzima wa milele pamoja na
watoto wetu. Kwahiyo hata sisi bado tunao wajibu
wa kulea, kuwafundisha watoto, wetu na watoto wao
ili waweze kuzishika amri za Mungu na sheria yake
kama neno linavyo tuagiza.
Na pia tunajifunza kumbe tukifanya hivyo katika
maisha yetu yote ambayo Mungu ametupatia, hapa
duniani, pia atatuongezea siku, zingine, kwasababu
tumewajibika.
A.KUMJUA MUNGU.
Ni muhimu na vyema kabisa kwa mzazi anayemcha
Mungu, katika roho na kweli kumfundisha mwanae
kumjua huyo Mungu tena Mungu wa kweli na,
kumwabudu au kumcha.
Katika habari hii ya kumjua Mungu na kumcha,
tunaweza kuwafundisha watoto wetu tokea mwanzo,
tangu tumboni, kama nilivo elezea katika sura ya
kwanza kwa sababu mtoto anapokuwa tumboni,
huwa yuko katika hali ya roho japo anapozaliwa
huwa tunamuona yuko katika mwili. Lakini
anapokuwa tumboni anatenda kazi katika roho zaidi
hivyo akianza kufundishwa kuanzia tumboni
anaelewa japo hiyo inakuwa ni kiroho zaidi lakini
ndivyo ilivyo. Nimeelezea kuwa mtoto ana weza
akarithi tabia za mzazi kuanzia tumboni ndiyo

Mwl. Joyce Z. Mgaya 32


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

sababu wale watoto ambao Mungu alikuwa


amekusudia kuwatumia Mungu alitoa maagizo kwa
wazazi wao hata pengine walipo kuwa hawajatunga
mimba kama vile Yohana, Samsoni huwa ni watu
ambao kuzaliwa kwako Mungu alishuka moja kwa
moja kusema na wazazi.
(Waamuzi 13:3-4) “Malaika wa Bwana
akamtokea yule mwanamke, akamwambia,
Tazama wewe sasa utasa, huzai; lakini utachukua
mimba, nawe utamzaa mtoto mwanaume. Basi
sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala
kileo wala usile kitu kilicho najisi.”
Ukisoma (Luka 1:5-7) utaona vilivyo habari za
Yohana mbatizaji; Mungu alivyoagiza malaika
wake, katika maandalizi ya kuzaliwa huyo mtoto.
Kwa hiyo napenda kuelezea zaidi hapa ili tuone
umuhimu wa kutambua kuwa mtoto anaweza
fundishwa kumjua Mungu toka tumboni maana
maandiko yanathibitisha. Nimeelezea kuwa mtoto
anapokuwa tumboni anatenda kazi katika roho, zaidi
japo anapozaliwa huonekana katika umbo la mwili,
ukisoma kitabu cha Luka utaona katika habari za
kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo na Yohana
mbatizaji. Mariamu alipotokewa na Malaika
aliyekuwa ameongozwa na Mungu kuleta habari. Na
baada ya Malaika kuondoka Mariamu alienda
mpaka kwa Elizabethi na alipofika kwa Elizabethi
kitoto kichanga kiliruka katika tumbo; hii
inamaanisha kuwa roho hizi mbili ziliwasiliana.
Ukiangalia ni kwamba hata huwa wanawake

Mwl. Joyce Z. Mgaya 33


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

walikuwa hawajasimuliana chochote ila katika


salamu tu, zile roho zikaanza kupeana heshima mara
moja na mtu kujawa na Roho papo hapo.

(Luka 1:41) “Ikawa Elisabeti aliposikia kule


kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga
kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa
na Roho Mtakatifu”. Kwa hiyo kusema hivyo kuna
uwezekano mkubwa wa kulea na kufundisha mtoto
tangu angali tumboni hadi anapofikia umri wa
kuzaliwa.
Na baada ya mtoto kuzaliwa aendelezewe malezi
hayo hayo kisibadilike kitu hadi pale mtoto
anapofika umri wa kuanzia kuwa na uelewa ama
ufahamu zaidi ambapo ni kuanzia miaka 9-17
Huu ni umri mtoto anapofikia hapo ikiwa hakupata
malezi yoyote tokea mwanzo ya kusikia neno la
Mungu.
Inahitajika njia ya kumsaidia haraka iwezekanavyo
ili angalau kuanzia hapo na kuendelea aweze
kunusuliwa roho yake. Lakini pia mtoto mwenye
umri huu ikiwa alipata malezi mema baada ya
kuzaliwa miezi 0 hadi miaka 8, atakuwa na
maendeleo mazuri na kuendelea kukua na kulelewa
na kufundishwa vizuri.
Katika agano la kale mambo yalifanywa kuwa sheria
zaidi, hata watoto ambao hawakufundishwa vizuri,
kumcha Mungu wakaenda kinyume waliadhibiwa
hata kufa. Mungu hakuangalia kuwa hawa ni wa
nani wala wa nani hata kama alikuwa wa Kuhani.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 34


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Kama hakufundishwa vizuri katika kumcha Mungu


waliadhibiwa.

Ukisoma pia katika kitabu cha Samweli.Watoto wa


kuhani Eli walipokwenda kinyume katika kumcha
Mungu waliadhibiwa na kufa. Hata sasa tuna kazi ya
kuwafundisha watoto katika kumcha Mungu ili
kusudi wasije, kufa kiroho na hatimaye kumkosa
Mungu na kutoingia katika mbingu zake takatifu.
B) TUWAFUNDISHE WATOTO KUMJUA
MUNGU KATIKA NJIA SAHIHI.
Tunaweza kuwafundisha watoto kumjua Mungu katika
njia mbalimbali, kwa mfano:
Kumjua Mungu wa kweli.
Mungu wa kweli ni nani?
(i). Mungu wa kweli ni Mungu muumbaji.
(ii).Ni Mungu aliyeziumba mbingu na nchi.
(iii). Ni Mungu aliyeumba vitu vyote.
(a). Ametuumba sisi wanadamu.
(b). Ameumba dunia na vyote vilivyomo
(c).Ameumba vinavyoonekana na visivyoonekana
Mwanzo 1:1 Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu
na nchi. Watoto wafundishwe kwa kuoneshwa vitu
halisi, kama vile miti, maji au bahari, ziwa na picha
zinazo onesha vitu alivyo viumba Mungu.
Na pia aonyeshwe mistari inayothibitisha maandiko.
Mtoto asimuliwe habari ya Mungu kwa namna ya
hadithi nzuri yenye kumsisimua kuhusu kumcha
Mungu, mfano habari ya Ayubu jinsi alivyo kuwa

Mwl. Joyce Z. Mgaya 35


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

mcha Mungu. Alivyokuwa mtu wa haki aliyemcha


Mungu na kuepukana na uovu.
Asimuliwe kwa kina kulingana na umri wake, penye
kuonyesha furaha mzazi mlezi afurahi, penye
kusikitisha mzazi mlezi au mtu anayesimulia naye
aoneshe kusikitika.
Mambo kama hayo yatamsababisha mtoto awe na
hamu au shauku ya kujifunza na kufundishwa
kumjua Mungu na kuwa Mungu anahitaji nini kwetu
na kwao pia. Na pia wataona kuwa kuna sababu ya
kumcha Mungu na kuwa mwenye haki kuna faida
gani. Maana utakapomwelezea mtoto jinsi Ayubu
alivyokuwa mwenye haki utamfafanulia nini maana
ya kuwa mwenye haki mbele za Mungu na faida
zake.
Mtoto afundishwe na kuonyeshwa mistari ya
kukariri ya muhimu juu ya somo alilofundishwa.
Mfano; Mtoto amefundishwa kuhusu kumjua
Mungu ni nani, na alitoka wapi, na alianza kuwepo
wakati gani. Ni vizuri mzazi mlezi amueleze mtoto,
kwa neno maana kama tunavyoamini neno lina
nguvu. Mfano; Mtoto aambiwe Mungu wetu ni
Mungu wa kweli alikuwepo tokea mwanzo kabla ya
vitu vyote kuwako na vitu vyote. Hivi vilifanywa
kwa yeye Mungu, pasipo yeye kisingefanyika kitu
chochote.
(Yoh 1:1-3)
Mtoto afundishwe na kuelekezwa kuwa Biblia
humuelezea Mungu, kuwa hana mwanzo wala
mwisho, ni wa milele. Uwepo wake unatokana na

Mwl. Joyce Z. Mgaya 36


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

yeye mwenye mzazi, mlezi katika kipindi cha dini


shule, nyumbani, maeneo yoyote yale utakayopata
fursa ya kuzungumza na watoto, usiache
kuwafundisha mambo ya muhimu, kulingana na
umri wake.
Mtoto afundishwe na kuambiwa Mungu
tunayemzungumzia na kufundisha habari zake
hakuna nyakati wala wakati ambao hajawahi
kuwepo; yeye yupo nyakati zote anafanya kazi ama
anatenda kazi yake wakati wote.
(Waebrania 1:10-12) “Na tena wewe, Bwana,
hapo mwanzo uliitia misingi ya nchi, na mbingu ni
kazi ya mikono yako; Hizo zitaharibika bali wewe
unadumu; nazo zote zitachakaa kama nguo. Na
kama mavazi utazizinga, nazo zitabadilika lakini
wewe u yeye yule, Na miaka yako haitakoma”.
(Zaburi 102:25-28)
Haya maandiko yatakuwa uthibitisho au nguzo ya
kile ulichokifundisha kwa mtoto, kwa sehemu mtoto
ambaye amekuwa akiamini na kufahamu ataelewa
zaidi, lakini katika Zaburi maneno hayo yanafanana
lakini isipokuwa mstari wa 28 unaelezea kuwa;
(Zaburi 102:28) “Wana wa watumishi wako
watakaa na wazao wao wataimarishwa mbele
zako.”
Wana wa watumishi ni akina nani?
Wana wa watumishi ni watoto wetu sisi tunaomcha
Mungu.
Hii pia inaelezea ili wana wa watumishi wakae na
wazao kuimarisha ni pale watakapokuwa

Mwl. Joyce Z. Mgaya 37


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

wamelelewa vizuri na kufundishwa kumjua Mungu


na kumcha. Ndipo hayo yote yatakapo timia ama
kuthibitika kwao.
d. Mtoto anapaswa kufundishwa kuwa Mungu ni
Mungu anayefanya kazi zake kwa utaratibu.
Mungu wetu hakurupuki, Mungu wetu si mganga,
wa kienyeji mpaka aotee, sio mpiga bao la mtoto
afundishwe ili naye anakua ajue Mungu hufanya
kazi kwa utaratibu na anahitaji watu wafanye kazi
katika utaratibu vile vile.
Tuwaelekeze, kuwafundisha na kuwaonyesha katika
kitabu cha Mwanzo ambapo ndiyo mwanzo wa kazi
za Mungu na katika utaratibu wake.
(Mwanzo 1:1-31)
Tufundishe katika sehemu ya kwanza. Kumbuka
jinsi Mungu alivyofanya kazi ya uumbaji wa mbingu
na nchi kwa utaratibu
(1). Siku ya kwanza - Alitenga Mchana na Usiku.
(2). Siku ya pili - Akatenga anga na maji.
(3). Siku ya tatu - Ardhi na mimea.
(4). Siku ya nne - Jua na mwezi
(5). Siku ya tano - Viumbe vya baharini na vya
anga
(6). Siku ya sita - Wanyama wa kufugwa wanaoishi
katika nchi na hatimaye mtu.
(7). Na siku ya saba - Mungu alimaliza kazi yake
yote aliyoifanya. Akastarehe siku ya saba maana
yake akapumzika siku hiyo na kuibariki kazi zote za
mikono yake.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 38


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Kwa hiyo tunapojifunza na kufundisha katika


taratibu za Mungu za kazi na ibada tunapaswa
kuangalia mambo ya msingi ambayo yanaweza
kuwapoteza watoto wetu, na hata watu wengi ambao
hawajahamasika kiroho.
Mfano; Katika hii siku ya saba ya mapumziko ya
Mungu ni lazima tuijue vizuri na kuwafundisha
watoto na wengine waelewe ni kwa nini Mungu
alipumzika, na kwa nini anahitaji pumziko la
mwanadamu, na siku ya ibada.
Tuwafundishe kuwa Mungu wetu alifanya kazi na
kupumzika si kwa sababu alikuwa amechoka, bali
kwa sababu alikuwa amekwisha ifanya kazi nayo
ikafanyika vizuri kwa hiyo alihitaji kupumzika.
Tuone kuwa pumziko la Mungu ni tofauti kabisa na
la watu. Watu wengi wanajua kupumzika ni
kuchoka, na wengine hupumzika sababu ni wavivu,
kwa hiyo tuone na kuwaonyesha wengine kuwa
pumziko la Mungu ni la tofauti kabisa na la watu
wavivu na watu wengine.
Pia tuielezee siku ya saba kadri ya uongozi wa Roho
Mtakatifu na kwa mafundisho ya watumishi wake.
Siku ya saba.
Siku ya saba ni siku ambayo Mungu alimaliza kazi
akaitenga siku hiyo kuwa siku yake ya kupumzika.
Kwa hiyo siku ya saba ni siku ya pumziko ni siku ya
kuonyesha ushirika pamoja nae, hii pia haijalishi
kwa siku zingine hatupaswi kufanya ushirika nae ila
ni kwa sababu yeye mwenyewe aliiteuwa siku hii na
kuibariki na kuifanya kuwa takatifu na maalumu

Mwl. Joyce Z. Mgaya 39


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kwa kupumzika na kumbukumbu ya kumaliza kazi


yake ya uumbaji na kuonyesha maana ya sabato
kuwa ni pumziko au kuacha na sabato ya kila juma
ili kuwa ni siku ya saba ya juma iliyowekwa wakfu
kwa sheria ya Musa kama siku ya kuacha kazi zote
za kawaida kujitoa kupumzika na kumuabudu
Mungu.
(Kutoka 20:8-11) “Ikumbuke siku ya sabato
uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako
yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA,
Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote,
wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala
mtumwa wao, wala mjakazi wako, wala mnyama
wako wa kufuga, wala mgeni aliye chini ya
malango yao. Maana, kwa siku sita BWANA
alifanya mbingu, na nchi,na bahari, na vyote
vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo
BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.”
(Kutoka 16:23-30),
(Kutoka 31:12-14),
(Kumbukumbu 5: 12-13)
Sheria katika Agano la Kale ilikuwa ni kivuli cha
Agano Jipya. Kwa hiyo tunapaswa kujifunza
kwamba kwa sasa tupo katika kipindi cha neema.
Na ukisoma hayo maandiko yote yanaelezea maana
ya sabato, kwa hiyo utaendelea kujifunza.
Lakini hata hivyo tunapojifunza na kufundisha
katika siku hii ya sbato, ni lazima pia kuyakataa
matumizi mabaya yanayohusu siku hii ya
mapumziko yanayotumiwa vibaya na watu.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 40


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Nikujuze tu mtumishi wa Mungu, unapokuwa katika


kufundisha kuwa ni kwa nini siku hii ya saba ni siku
ya mapumziko ni siku inayotupatia nafasi ya
kuthibitisha kuwa imani yetu, na furaha yetu,
upendo wetu ni katika Bwana na siyo katika
ulimwengu au ubinafsi wetu au mali, kazi zetu,
starehe zetu, na hata kufanya uharibifu.
Lakini sisi wakristo katika Agano Jipya tunaitumia
siku ya kwanza ya juma; yaani Jumapili kuungana
na waamini wengine kuabudu Mungu.
Roho Mtakatifu alishuka siku ya Jumapili; tukio hilo
pia limepelekea wakristo katika Agano Jipya
kuitenga siku hiyo kwa ajili ya kuabudu na
kukumbuka ufufuo wa Yesu Kristo na kushuka huko
kwa Roho Mtakatifu.
(Mdo 2:1-4), (1 Kor 16:2), (Mathayo 28:1)
Haya maandiko yote yanaelezea yaliyofanyika
katika siku ya kwanza ya juma.
Zaidi ya hayo tunapojifunza juu ya Mungu kumaliza
kazi yake Biblia inaelezea kuwa Mungu alipumzika
baada ya kumaliza kazi ya uumbaji tu lakini kazi
zingine kama kuabudu kutumikia na kumtolea hizo
bado zilikuwa zinaendelea, AMEEN!

Mwl. Joyce Z. Mgaya 41


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

SURA YA 3

KUMJUA MUNGU WA KWELI NA UWEZA


WAKE.
A. Ni kwa nini kuwafundisha watoto kumjua Mungu
wa kweli na uweza wake?
Tunapaswa na ni muhimu kuwafundisha watoto
kuhusu kumjua Mungu wa kweli na uweza wake;
maana tukilifanya hilo hakika:
(i). Nafsi za watoto zitakaa salama.
(ii). Watajiamini kwa habari ya Mungu na kufanya
vizuri katika maisha yao na popote watakapokuwa.
Tukiangalia katika maandiko yanayowaelezea
watoto ambao wanaitwa vijana sasa baada ya
kulelewa vizuri katika hatua ya mwanzo na baadaye
kufika ujana.
(2Wafalme 5:2-3) “Na Washami walikuwa
wametoka vikosi, wakamchukua mfungwa mmoja
kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye
akamhudumia mkewe Naamani.
Akamwambia bibi yake, laiti Bwana wangu
angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria!
Maana angemponya ukoma wake”.
Ni kwanini huyu binti alikuwa na ujasiri wa
kumwambia mke wa bosi wake. Tena jemedari wa
vita, kuwa kuna mtumishi wa Mungu huko,
anayeponya, bila kuogopa.
Ni kwa sababu, huyo binti hakuwa na hofu wala
wasiwasi alijua jemedali ambaye ni bosi wake

Mwl. Joyce Z. Mgaya 42


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

akienda kule, anakopatikana Mungu wa kweli


atapona, maana upo uweza wake ule mkuu.
Pia wapo wengine kama Danieli, Shedraka,
Meshaki na Abednego.Habari zao ziko katika kitabu
cha Danieli.
(Danieli 3:8-30), (Dan 6:10-28)
Hawa vijana waliweza kusimamia imani
iliyowapelekea kushinda, kuabudu miungu
iliyokuwa imesimamishwa ya mfalme ni kwa
sababu walijua Mungu waliyenaye wanayemwabudu
ni wa kweli, ni zaidi ya miungu, anao uweza mkuu
wa kuwaokoa katika hali yoyote ile.
Kwa hiyo wao pia hawakusita wala kuogopa mfalme
pamoja na amri zake zote alizokuwa ameziweka.
ukisoma (Danieli 3:16-18)
“Ndipo Shadrack, Meshaki na Abednego,
wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee
Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno
hili. Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia
aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye
atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme. Bali kama
sihivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali
kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo
sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.”
Kwa hiyo hapo utaona uamuzi wa hawa vijana sio
wa kawaida tu ni kwasababu walikuwa na uakika
juu ya Mungu wao.
Bila kusahau habari za malkia Esta. Aliyelelewa
vizuri na mjomba wake Modekai, Biblia
inamuelezea modekai kuwa alikuwa ni mjomba wa

Mwl. Joyce Z. Mgaya 43


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Esta kwa hiyo alikua ni mzazi mlezi wa binti huyu


Esta na inaelezeka na kuonekana kuwa alimlea
vizuri juu ya kumjua Mungu pia hakuishia kumlea
kimwili tu, alimlea na kiroho pia.
Na hata wakati wake ulipotimia wa kuolewa alipata
kibali mbele ya mfalme cha kuwa malaika, kwa hiyo
hii inaonyesha kuwa alikuwa binti mzuri na
aliyelelewa vizuri.
Kwa hiyo ni kuwa uangalizi na kwa kulelewa vizuri
kwa Esta, kulikuwa na msaada mkubwa juu ya
Wayahudi katika wakati ule yalipo tokea mambo
magumu juu ya Wayahudi katika utawala wa
mfalme Ahasuero, Esta alipewa habari juu ya
mambo yaliyowapata ndugu zake, kwa mara ya
kwanza aliogopa sana, lakini kwa sababu alikuwa
anamjua Mungu wa kweli anayepaswa kuabudiwa
aliyekuwa akimwabudu, akiwa kwa mjomba wake.
Akachukua jukumu la kumwomba Mungu juu ya
yale yaliyo wapata nduguze, hali akijua Mungu anao
uwezo wa kuwaokoa Wayahudi na mkono wa
Hamani katika utawala wa mfalme Ahasuero.
(Esta 4:15-16) “Basi Esta akawatuma ili wamjibu
Mordekai, Uende uwakusanye Wayahudi wote
waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili
yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu,
usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu
tutafunga vile vile ; kasha nitaingia kwa mfalme,
kinyume cha sharia; name nikiangamia, na
niangamie.”

Mwl. Joyce Z. Mgaya 44


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Tunawafundisha watoto na kuwalea katika kumjua


Mungu wa kweli na uweza wake, hali tukijua kuwa
hata Serikali yetu ya Tanzania inatambua mtoto
kama taifa la kesho, hivyo tunapaswa kujua hawa
watoto ni watumishi wa kesho, ama wa baadae, kwa
hiyo wasipofundishwa vizuri wanaweza wasifanye
vizuri katika maisha yao ya baadae katika kumjua
Mungu. Kuna mambo mengi ya kuwafundisha
watoto, ambayo pia yanaweza kuwapa fursa kama
vile:-
A. UAMINIFU
Ili mtu amjue Mungu na afanye vizuri pia kuna
umuhimu wa kuwa mwaminifu hivyo ni jambo la
msingi sana mtoto kufundishwa kuhusu uaminifu.
Tunamwona kijana Yusufu alikuwa anamjua Mungu
lakini pia alikuwa mwaminifu.
(Mwanzo 39:1, 21)
Huo uaminifu wa Yusufu ulionesha jinsi
anavyomjua Mungu, kwa hiyo alisimama vizuri na
kulitetea jina la Bwana kwasababu alikuwa
mwaminifu.
Lakini sasa hivi katika nyakati tulizo nazo vijana
waaminifu ni wachache. Vijana wana mambo ya
ajabu wanaishi na wamama kama wake zao. Maisha
yao ni mabaya yameharibika, hawana sifa za kuwa
waaminifu, Hali kadhalika mabinti nao hivyo
wanatembea na kufanya zinaa na wababa ambao ni
baba zao, maadili yameporomoka, watu wamekosa
kiasi wameacha kuwa waaminifu mbele za Mungu,
kwa sababu wazazi walezi wameacha wajibu wa

Mwl. Joyce Z. Mgaya 45


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kulea na kufundisha badala yake tumeacha dunia


ndio inayofundisha. Maigizo ya mapenzi ndio
yamejaa, filamu za ajabu na mambo mengine mengi
ambayo Mungu hayapendi na amesema katika neno
lake tusiipende dunia na mambo yaliyomo, na tena
tusifuatishe namna ya dunia hii.
(Warumi 12:2) “Wala msifuatishe namna ya dunia
hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu,
mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo
mema ya kumpendeza, na ukamilifu”.
Pia mtu hawezi kufanya mapenzi ya Mungu na
kuwa mkamilifu bila kulelewa na kufundishwa
vizuri. Kwa hiyo kuna sababu nyingi mno za kulea
na kufundisha juu ya uaminifu.
(Kutoka 12: 36) “Bwana akawajalia kupendelewa
na Wamisri hata wakapewa kila walichokitaka,
nao wakawateka Wamisri nyara”.
Ni kwa sababu Musa alimjua Mungu na
akawafundisha wana Waisraeli, nao wakafanya
kama walivyofundishwa, hadi kufikia wakati wa
kupata wokovu wa kutoka Misri kwa kishindo, neno
linaeleza kuwa Bwana akawajalia kupendelewa na
wamisri. Walipendelewa na Wamisri sababu
walimjua Mungu wao na kutenda mambo yake
katika uaminifu. Kwa hiyo katika kumjua Mungu
wa kweli na kuwa waaminifu, ni muhimu sana
kuanzia kwetu sisi wazazi walezi.
Neno la Mungu linasema malimbuko yakiwa safi
kadhalika na dongo lote pia, hii ina maana kubwa
sana, kwa wazazi na walezi wakiwa vizuri katika

Mwl. Joyce Z. Mgaya 46


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kumjua Mungu na kuwa waaminifu, basi watoto


wetu nao pia watakuwa waaminifu katika swala
zima la kumjua Mungu na kuabudu katika uaminifu.
(Warumi 11:16) “Tena malimbuko yakiwa
matakatifu kadhalika na donge lote na shina
likiwa takatifu matawi, nayo kadhalika na donge
lote; na shina likiwa takatifu, matawi nayo
kadhalika.”.
Katika hili andiko mtu wa Mungu atajifunza na
kuona, kwa sisi wazazi ni malimbiko ya familia zetu
kwa hiyo tukifanya mambo yasiyo mpendeza
Mungu, wala yasiyopasa kuwa wakamilifu watoto
wetu vivyo hivyo watakavyo enenda.
Leo katika dunia hii tunayoishi mambo haya yapo
na yanaonekana. Unakuta katika familia baba ni
mlevi, mama mlevi, mtoto mlevi, mjukuu mlevi,
vivyo hivyo hata kitukuu kitalewa maana hapa
malimbuko yameharibika, na hata katika swala la
zinaa vilevile ni hayo, na kuabudu Mungu ndiyo
kabisa. Kwa hiyo, unakuta dunia inalia na
kuomboleza, inawayawaya. Dunia inakosa watu wa
kuiendeleza, maana sio wote wameharibiwa. Kumbe
wakipatikana wazazi wenye mtazamo chanya
wataokoa kizazi hiki na kuliponya taifa maana
watafundisha na watoto kumjua Mungu kumcha,
kuishi maisha matakatifu, na ya uaminifu.
B. KUMTUMAINI BWANA
Katika kumjua Mungu pia, kuna kumtumaini. Kama
vile mtoto anavyomjua mzazi wake na kumtumainia
kuwa anaweza kumsaidia kwa lolote analolihitaji.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 47


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Kwa hiyo tunapowafundisha watoto kumjua Mungu


pia katika maisha yao yote ya kila siku hapa duniani
Mungu aliowapa na kuwajalia kuishi tusiache
kuwafundisha kumtumaini Bwana, hii itasaidia.
Wazazi na walezi wengine wanapokuwa
wamefanikiwa kupata mali, kwa sehemu
huwatumainisha watoto katika mali, kumbe ni kosa,
lililo kubwa katika yote ni kumcha Mungu na
kumtumaini.
(Mithali 3:5-6) “Mtumaini Bwana kwa moyo wako
wote, wala usitegemee akili zako mwenyewe; katika
njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito
yako”.

Watoto wanapaswa kufundishwa kumtegemea


Bwana. Watoto wenye umri wa kufanya kazi,
wafundishwe kazi lakini katika kazi zao, wasiache
kutegemea, kumtumainia Bwana maana yeye ndie
anaye nyoosha mapito na njia zetu zote.
Katika nyakati hizi tulizo nazo watu wameacha na
kusahau kuwafundisha watoto katika kumtumainia
Bwana kuwa Mungu ndiye atoae baraka.
Hii imepelekea vijana wengi kuharibikiwa,
wanafikia umri wa ujana kutoka utotoni.
Wanapoanza kuona umuhimu wa kutafuta maisha,
yaani kujitegemea; wengine hutoroka nyumbani
pasipo kuaga na kibaya zaidi hawajui
wanakokwenda na hufikiri kuwa hii pengine ndiyo
njia sahihi ya kujitegemeza kimaisha.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 48


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Imewapelekea vijana wengi kuingia katika mambo


magumu, wengine wakidanganywa na waganga wa
kienyeji kuwa kutafuta maisha bila madawa
haiwezekani.
Kwa njia hii vijana wengine wamewaua wazazi,
ndugu, na jamaa zao wa karibu wakidanganywa
kuwa ndiyo njia sahihi ya kutafuta mali; kitu
ambacho si kweli.
Na mabinti wengi wameharibika kwa kujiuza; kwa
kufanya miili yao kuwa biashara kwani hawaoni
chakufanya; jambo ambalo ni hatari sana.
Kwa hiyo, wazazi na walezi wanaomcha Mungu
wanapaswa kuyaangalia mambo kama haya na
kuwasaidia watoto wao kwa kuwalea vizuri, ili
wajue kumtegemea Mungu katika kila hatua.
Neno la Mungu linasema, katika (Zaburi 33:16)
“Hapana mfalme aokoaye kwa wingi wa uwezo
wala shujaa haokoki kwa wingi wa nguvu”.
Hii ina maana kuwa unaweza kuwa na uwezo
mkubwa, nguvu nyingi lakini haya yote hayawezi
kukuokoa pasipo kumtumaini Bwana. Ukimtumaini
Bwana pia utapata hekima na maarifa ya kuendesha
maisha au mambo yako.
Kwa hiyo wazazi na walezi wawafundishe watoto
kumtegemea Mungu.
(Yeremia 9:23-24) “Bwana asema, hivi mwenye
hekima asijisifu kwa sababu ya hekima yake, wala
mwenye nguvu asijisifu kwa sababu ya nguvu
zake, wala tajiri asijisifu kwa sababu ya utajiri
wake; bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya

Mwl. Joyce Z. Mgaya 49


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kwamba ananifahamu mimi na kunijua ya kuwa


mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu, na
haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na
mambo hayo, asema BWANA”.
Ukimjua Bwana utamtumaini na kujisifu katika
yeye, na ndio furaha ya Bwana. Kumtumaini Bwana
na kumjua huleta furaha kubwa sana katika maisha
ya mtu Isaka na Daudi walipomjua Bwana na
kumtumainia alifanya mambo makubwa sana, pia
kumjua Bwana na kumtumaini kulimpa Daudi
ujasiri, hata alipo sikia ndugu zake Israeli,
wanasumbuliwa na Goriath, Daudi alisikia wivu wa
kimungu ndani yake, hali kadhalika alijua
ukimtumaini Bwana hakuna kinachoshindikana.
Kwa hiyo ni vyema kabisa mtoto afundishwe
kumtegemea Mungu na siyo elimu wala mali zake.
(1Samwel 17:26, 37) “Daudi akaongea na watu
waliosimama karibu, akisema, je! Atafanyiwaje
yeye atakayemuua Mfilisti huyo na kuwaondolea
Israeli aibu hii?. Maana Mfilisti huyu
asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya
Mungu aliye hai? “ Daudi akasema, BWANA
aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya
dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu.
Sauli akamwambia Daudi, Enenda na BWANA
atakuwa pamoja nawe”.
Haya ni maneno ya Daudi ya kuonesha kuwa
anamtumaini Bwana vilivyo, kwa sababu watoto
wakimtumaini Bwana watakuwa vizuri katika
maisha yao yawe ni ya kiroho au ya kimwili, jambo

Mwl. Joyce Z. Mgaya 50


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

lililo kuu ni kumtumaini Bwana. Mtu anaweza


kusomesha mtoto kwa gharama kubwa na bila
kumtegemea Mungu na kutumaini fedha ila mtoto
asifike popote, jinsi pengine ambavyo mzazi ama
mlezi walivyotarajia lakini mwingine akatumia
gharama kidogo kwa kumtumaini Mungu na
akafanya vizuri. Kwa hiyo swala la msingi ni
kumtumaini Mungu, Daudi hakutumaini wala
mavazi ya vita maana Israeli walienda na hayo
mavazi lakini bado walipigwa na kukimbia.
Kitu chochote kinachopfanyika vizuri lazima uwe na
matumaini ndani yake.
Hata mkulima anapoona majira na msimu wa kilimo
huanza kuyaweka matumaini yake kwamba atalima
na kufanikiwa.
Mfano; Isaka alikuwa na matumaini katika kilimo
naye Bwana akambariki katika kilimo, katika
kipimo kimoja akavuna vipimo mia,
Ukisoma katika kitabu cha mwanzo utaona,
(Mwanzo 26:12)
Kwa hiyo ukimtumaini Mungu na kuwafundisha
watoto kumtumaini, kazi ya Mungu itakuwa kubwa
na itasonga mbele.
Mtu anayetumaini jambo fulani ni vigumu kumtoa,
katika tumanini lake ndiyo sababu ukiangalia
maswala ya imani mtu akisha kuamini jambo, katika
imani yake liwe baya au laa! ni vigumu kumgeuza,
hadi neema ya Mungu itokee. Paulo kabla ya
kuokoka alikuwa mtu wa dini, lakini katika dini

Mwl. Joyce Z. Mgaya 51


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

yake bado aliamini vibaya aliendelea kumkosea


Mungu akiwa na dini.
(Mdo 9:1)
Kwa hiyo watoto wakilelewa vibaya wataendelea
kumkosea Mungu japo wako ndani ya dini. Kwa
mambo kama nilivyo tangulia kusema hapo awali
kama vile kujiuza, hadi leo tuna vijana wa kiume ni
mashoga ni kwa sababu wamelelewa vibaya na
kufundishwa vibaya. Kwa hiyo nakuomba tu mzazi
mlezi Mungu akupe neema upya ya kulea na
kufundisha vizuri, Barikiwa na Mungu.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 52


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

SURA YA 4

KUTAMBUA UTHAMANI WA MTOTO.

T unapaswa kutambua uthamani wa mtoto na


kuonesha uthamani wake, kama vile vitu vya
thamani, vinavyoweza kuoneshwa thamani na
kutunzwa sababu ni vya thamani. Basi tujue kuwa
mtoto ni wa thamani, anapaswa kuoneshwa
uthamani wake na kutunzwa, kama vile vitu vya
thamani vinavyo tunzwa.
Watoto ni wa thamani maana ni zawadi tunayopewa
na Mungu kutoka kwake moja kwa moja.
Zawadi zingine tunazozipata kutokana na elimu
zetu, japokuwa nazo ni zawadi toka kwa Mungu, ila
mtoto hata kama hauna elimu wala pesa Mungu
anakupa, kwa hiyo ni zawadi ya pekee sana ambayo
inahitaji kuoneshwa uthamani kuliko vitu vyote.
Watu wengine wameacha kuonesha uthamani wa
watoto badala yake wamevipa vitu uthamani katika
nafasi ya kwanza, kama vile pesa, magari, utajiri
wao, ndio vitu walivyo viona vya thamani.
Lakini ukisoma neno la Mungu utaona kuna watu
waliokosa watoto, na walikuwa na mali za kutosha
lakini, hakuona kuwa ni vya thamani kwao.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 53


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

(Mwanzo 13:1-2)
Abramu akapanda kutoka Misri yeye na mkewe na
kila alichokuwa nacho, na Lutu pamoja naye mpaka
kusini 2) Naye Abramu alikuwa ni tajiri sana kwa
mifugo, kwa fedha, na kwa dhahabu. Ni nini kusudi
la hili andiko ni kwamba nataka nikuoneshe mtu na
Mungu kuwa mtoto ni wa thamani kubwa Abraham
hakuona kama vitu alivyo navyo ni vya thamani
bado alikuwa na uhitaji wa mtoto.
(Mwanzo 15:2-3) “Abramu akasema, Ee Bwana
MUNGU, utanipa nini, nami naenenda zangu hali
sina mtoto, na atakayemiliki nyumba yangu ni
huyu Eliezeri, Mdameski? Abramu akasema,
Tazama, hukunipa uzao, na mtu aliyezaliwa
nyumbani mwangu ndie mrithi wangu”.
Hii inadhihirisha na kuonesha mtu wa Mungu,
mtumishi wa Mungu kuwa vitu si vya thamani
kuliko mtoto, maana hata mali tunazozitafuta ni kwa
jili ya Mungu na watoto wetu maana ndio warithi
Abramu alisema hili na ndivyo ilivyo watoto ni
warithi wetu na mali zetu, warithi katika huduma
zetu na pia ni warirhi wa taifa. Kanisa taifa haiwezi
kuendelea bila ya watu wa kuendeleza na watu hao
ni watoto wetu.
Inasikitisha na kushangaza kuna watu ambao
wanawatoa watoto wao kafara kwa ajili ya kupata
mali, je? Hizo mali ni kwa ajili ya nani sasa?.
Na pia inapokuwa wa mama, mabinti wanao zaa na
kutupa watoto wao chooni.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 54


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Kwa sababu ambazo wanazijua wao wenyewe,


wengine ndio kabisa wanafunga na kuzaa kabla ya
wakati; siyo kwamba ni wagonjwa, au kwa sababu
zinazoeleweka bali ni kwa maamuzi pengine
hawataki usumbufu kuchafuliwa; na hiyo
haimpendezi Mungu.
Lakini wapo wanawake ambao walikuwa hawazai,
wakamlilia Mungu kwa uchungu ambao ni pamoja
na mwanamke. Hana, mwanamke huyu alipokuwa
amekoswa zawadi hii ya mtoto hakuwa na furaha
maishani mwake siku zote, hadi pale Bwana alipo
kuwa amemtimizia haja ya moyo wake.
(1Samweli 1:10-11) “Naye huyo mwanamke
alikuwa na uchungu rohoni mwake, akamuomba
Bwana akalia sana, Akaweka nadhiri, akasema,
Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia
teso la mjakazi wako, na kunikumbuka wala
usinisahau mimi mjakazi wako, kunipa mimi
mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi
nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za
maisha yake wala wembe hautamfikilia kichwani
kamwe”.
Kwa hiyo mwanamke huyu aliona umuhimu wa
mtoto na kuhitaji kuwa na mtoto naye si kwamba
hakuwa na mali, walikuwa nazo tena mumewe
alimpenda na kumhudumia kama mama mwenye
mtoto, lakini hakuridhika hadi alipompata mtoto.
1Samweli 2:1 “Naye Hana akaomba, akasema
Bwana pembe yangu imetukuka katika Bwana,
kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu”.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 55


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Kwa kuwa naufurahia wokovu wako.


Haya yalikuwa maombi ya furaha ya Hana baada ya
kupata kitu cha thamani ambacho alikuwa
anakihitaji, watu wengi leo huweka nadhiri za
kuhitaji magari, pesa, mali, n.k. na baada ya kupewa
pengine hawawi tena na maombi ya shukrani maana
wakiisha pata kile wanachokihitaji na kuviona ni
vya thamani.
Basi tunapaswa kuona sana uthamani wa watoto
tuliopewa na Mungu ili tuwalee vizuri ni pale
ambapo tutatambua uthamani wao. Nimetanguliza
kusema kama tunayo weza kuvipa vitu heshima mali
zetu zawadi tulizo pewa na ndugu zetu kwa sababu
tumetambua ni vya thamani, basi tutambue kuwa
watoto ni wa thamani sana maana ni zawadi
tuliopewa na Mungu mwenyewe.
YESU KRISTO AUTAMBUA UTHAMANI WA
WATOTO.
(Marko 10:13-16) “Basi wakamletea watoto
wadogo ili uwaguse; wanafunzi wake
wakawakemea. Ila Yesu alipoona alichukizwa
sana, akawaambia, waacheni watoto wadogo waje
kwangu, msiwazuie, kwa maana watoto kama
hawa ufalme wa mbinguni ni wao”.
Katika andiko hilo hapo juu utaona Yesu akaendelea
kuelezea kuwa usipoukubali ufalme wa mbinguni
kama mtoto, huwezi kuingia kamwe; ni kwa sababu
alitambua uthamani wa mtoto, kisha akawakumbatia
na kuwabariki.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 56


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Yesu atambua uthamani wa mtoto kwa sababu hata


ndani ya makanisa pengine watoto ni wengi kuliko
watu wazima.
Pia watoto wanaweza kuja kwa kristo kwa wepesi
bila kujali mazingira yakoje kuliko mtu mzima.
Yesu aliona umuhimu wa mtoto, ndani ya kanisa
sababu mtoto anayepata mafundisho ya awali ya
kiroho na kutiliwa mkazo.
Mtoto huyo huwa na maendeleo mazuri sana katika
maisha yake anapoendelea mbele.
Naomba nitoe ushuhuda kuhusu mimi mwenyewe.
Nilizaliwa katika familia iliyo kuwa na dini ya
Anglikani, Kwahiyo katika utoto wangu nilikuwa ni
kisali hapo nilikuwa nikihudhuria ibada na shule ya
jumapili kanisani hapo na katika siku za sikukuu,
tulipewa chai hivi vitu vilinifanya kuona kuwa
kumbe tunatambuliwa uthamani wetu. Nilihudhuria
mikesha na kuona mikanda ya Yesu alivyoteswa na
kusulubiwa. Hii pia ilinifanya nilipokuwa nikirudi
nyumbani nikaanza kuwauliza wazazi wangu
maswali mengi juu ya Mungu.
Sijui ndiyo bahati mbaya kwamba wazazi wangu
walikuwa wanaabudu, kama kawaida ya wanaekimu
walikuwa hawana majibu ya msingi juu ya maswali
yangu. Niseme ni kwamba pengine walikuwa
hawajui neno la Mungu, vizuri.
Maana maswali yangu yalikuwa hivi
(i). Mungu ni nani?
(ii). Mungu yuko wapi?.
(iii). Alifanyaje akaumba mlima ninayoiona?

Mwl. Joyce Z. Mgaya 57


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

(iv)Je! Haya mawe madogo ndiyo hukua na kuwa


makubwa?.
(v) Je, wao wazazi wangu walizaliwa na nani?
Hadi wamefika hapo walipo na hivyo ndivyo,
walinijibu kiasi ambacho sikuridhika. Baba akasema
toka nitakuchapa; zaidi ya yote, mama yangu
aliniambia Mungu na malaika wako juu wananiona
na kunicheka nilitazama juu ya dari nikitarajia
kuwaona sikuwaona.
Nimeeleza hivi mpendwa wangu msomaji wa kitabu
hiki kutaka kuonesha kutambua uthamani wa mtoto
pengine katika maswali yake itamsaidia kukua
vizuri.
Yesu alitambua akiwawekea watoto mikono na
kuwabariki atakuwa amewapandia mbegu ya
wokovu, kwa hiyo kumsikiliza mtoto ni
kumuonesha Yesu pia alilitambua hili kwamba ili
uokoke na kubadilisha lazima ufanane na mtoto
mchanga ili pia uwe mnyenyekevu lazima uwe kama
mtoto, maana mtoto huwa ni mnyenyekevu.
Hata anapokosea hunyenyea tu anapoonywa ama
kuchapwa na mzazi mlezi wake hunyenyekea tu. Na
mtoto anawahi kusamehe, kwa hiyo watoto ni wa
thamani sana, Yesu limtolea mifano mingi.
(Mathayo 18: 3-5) “Akasema, Amini, nawaambia,
msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia
kamwe katika ufalme wa mbinguni”.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 58


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Basi yeyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama


mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme
wa mbinguni.
Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa
huyu kwa jina langu, amenipokea mimi”.
Kwa hiyo tunapotambua uthamani wa mtoto na
kuwa na mbinu mbalimbali kuwalea, tutakuwa
tumetambua uthamani wa Yesu kwetu, kuwa ndiye
mwenye kutupatia watoto katika kutambua uthamani
wa mtoto pia mtoto apewe UHURU.
Mtoto apewe uhuru kulingana na umri alionao,
mfano; miaka 15-17 ni mtoto anayeanza kutambua
zaidi. Kwa hiyo anaweza kupewa nafasi au uhuru
kiasi katika jambo linalomhusu mtoto, kuna mambo
yanayo husu mtoto mfano; Elimu maana hata neno
linasisitiza juu elimu (Mithali 4:13) kwa hiyo mtoto
anaposoma na kuendelea kusoma miaka (15-17),
kuna wakati utafika atakuwa na maamuzi ya
kuchagua anachohitaji kusomea, kwa hiyo mzazi
anayo nafasi ya kumweleza, kumshauri mtoto.
Wazazi wengi hawajui kutumia eneo la kumpa
mtoto uhuru sina maana kwamba mtoto apewe
uhuru uliopitiliza kwa mfano; Mtoto mdogo
mwenye umri kuanzia miaka mitano 5-8 apewe
nafasi ya kucheza, kupumzika, hiyo ni sehemu ya
uhuru kwake asizuiliwe mtoto. Lakini pia mtoto
aelekezwe na kuadhibiwa anapokosea, mtoto
asiache kuelekezwa na kuadhibiwa, huo utakuwa
uhuru uliopitiliza.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 59


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

(Mithali 13:24) “Yeye asiyetumia fimbo yake


humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye
humrudi mapema”.
Kumnyima mtoto wako fimbo ni kumpa mtoto
uhuru usiofaa kitu, ambao utampoteza katika
maandiko haya tunajifunza kuwa mtoto ni lazima
aelekezwe, simaanishi kuwa mtoto apigwe sana,
ama asiadhibiwe kabisa, hapana Biblia inaelezea
kuwa ujinga umefungwa ndani ya moyo wa mtoto
na fimbo ya adhabu ndio itakayomfukuzia mbali huo
ujinga. Lakini hii haina maana sasa kuwa mtoto
apewe adhabu kiasi kwamba mtoto akose uhuru wa
kuongea hapana.
(Mithali 22:15) “Ujinga umefungwa ndani ya
moyo wa mtoto; lakini fimbo ya adhabu itaifukuzia
mbali”.
Kuna wazazi ama walezi ambao wameitumia fimbo
kama mwamuzi wa watoto, na kuwa madikteta
katika familia, wamefanya watoto kukosa uhuru na
kujiamini, watoto wengi waliokosa uhuru kwa
wazazi hawezi kufanya hata vizuri shuleni hata
katika kazi anazopewa na watu afanye atakuwa mtu
wa mashaka hofu na wasiwasi nyingi sababu
amelelewa kwa kubanwa sana. Watoto wa namna hii
pia wakipata nafasi hufanya mambo mabaya.
Pengine ambayo yatawaharibia maisha kumnyima
uhuru mtoto wako kupita kawaida. Pia ni moja wapo
ya kutotambua uthamani wake kwako ni kweli
kwamba fimbo inaweza kusaidia kumuonya mtoto
lakini siyo asilimia mia watoto wengine kwa

Mwl. Joyce Z. Mgaya 60


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kupewa uhuru kwao inaweza kuwasaidia kutatua


matatizo yao pasipo fimbo kwa hiyo fimbo isiwe
ndio mtatuzi wa matatizo ya watoto.
Lakini kuna wazazi ambao hawana habari na mtoto
kumuonya, kumrudi na kumsaidia kwa namna
yoyote ile hayo nayo ni makosa.
(Mithali 19:18) “Mrudi mwanao, kwa maana liko
tumaini wala usiikaze nafsi yako kwa kuangamia
kwake”
Kwa hiyo tujapo wapa uhuru ili wasishindwe katika
kukaa katika ujasiri pia ni lazima kuwarudi. watoto.
Maana ni agizo la Mungu katika maandiko
matakatifu ili usikae katika kuangamia.
Hapa sasa ndipo utaona umuhimu katika huu umri
wa kuanzia miaka 15 – 17 maana wako katika hatua
ngumu ambayo wanakaribia kuingia utu uzima, kwa
hiyo wasipoelekezwa katika uhuru wao wanaweza
kuharibikiwa.
Zaidi kwa hiyo nikuombe tu mpendwa mzazi
uzingatie yafuatayo ili kumuonyesha uthamani
wake.
MTOTO PIA HUONESHWA UTHAMANI KWA
KUPENDWA.
Watoto wathaminiwe na kupendwa tukifanya hivi
tutakuwa tumeonyesha uthamani wa watoto.
Wazazi na walezi wengi hufanya makosa katika
familia kwa kuonyesha upendo kwa ubaguzi kwa
watoto wao waliowazaa wenyewe hayo ni makosa
tena wengine wakidai kuwa hiyo ni maandiko kuna
mambo ambayo Mungu aliyafanya mwenyewe kwa

Mwl. Joyce Z. Mgaya 61


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kusudi lake ili kufundisha wanadamu kwa hiyo


hatuwezi kujifunza katika makosa; mfano, Isaka na
watoto wake.
Je! wewe unapofanya hivyo huo ubaguzi Mungu
anasema kuhusu hao watoto wako. Mungu alisema
na Isaka na Rebeka katika habari ya watoto wao.
(Mwanzo 25:23) “Bwana akamwambia, mataifa
mawili yako tumboni mwako, na kabila mbili za
watu watafarakana tangu tumboni mwako. Kabila
moja litakuwa hodari kuliko la pili, na mkubwa
atamtumikia mdogo”
Kwa hiyo haya yalikuwa ni makusudi ya Mungu
mwenyewe ila na sisi sasa tunapaswa kufanya yaliyo
makusudi ya Mungu kwetu katika kuweka watoto.
Kumlea mtoto kwa ubaguzi huleta madhara
makubwa duniani katika familia au jamii zingine
watoto wamekuwa hawaelewani watoto wa tumbo
moja wanauana kwa wivu kumekewepo na roho ya
Kaini na Habili mwingine hataki mwenzake
afanikiwe mtu anadiliki kuumua ndugu yake ii apate
mali hayo ni makosa makubwa sana pengine
yanayosababishwa na wazazi, walezi, kweli wazazi
wakikataa hizo roho mbaya za shetani ndani ya
mioyo yao na kuwalea watoto katika upendo na
kuonyesha uthamani wao wote wataleana na
kufaana zaidi.
Katika mataifa mengine kila mtoto ni wathamani
kwa kipaji alichompa Mungu lakini katika taifa letu
watoto wanaoonekana ni wa thamani na wenye
kipaji cha elimu hayo ni makosa na mapokeo ya

Mwl. Joyce Z. Mgaya 62


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

awali tuliyoyapokea tunapaswa kutambua kuwa


mtoto yeyote ni wathamini awe na kiapaji cha
ukulima, biashara, muziki, ufundi hivyo vyote ni
vya thamani maana bila chakula kutoka kwa
mkulima, mfanya biashara atakitoa wapi? Na bila
mfanya biashara mfanya kazi atakinunua wapi?
Kwa hiyo tutambue hilo kwa watoto wote ni sawa
na vipaji vyao vyote wamepewa na Mungu tuvijali,
tuvithamini na kuviendeleza.
Niliwahi kusikia katika familia moja alikuwepo
mtoto anasoma na akawa ndiyo amefika kidato cha
nne, mitihani imefika kabisa alipokuwa katika hizo
harakati akakutana na fomu huko shule za kujiunga
na mziki, mtoto huyo aliambia wazazi wake kuwa
yeye ya elimu hayawezi na hata hapo amefika kwa
kujisukuma tu, kwa hiyo yeye ameamua kwenda
kujiunga na fomu ya mziki, mapambo na kufundisha
shoo na mapambo wazazi wake walikataa lakini
mwisho walikubaliana nae akaenda na akafanya
vizuri na kwendelea, kwahiyo anashughulika na
muziki na mambo na maisha yanaenda vizuri,
Kwa hiyo tuviangalie vipaji vya watoto kuwa
makini hivyo tutakuwa tumeonesha uthamini wao
nakuwalea katika upendo na wakafika salama.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 63


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

SURA YA 5

UTII KWA MUNGU NA WAZAZI.

N i jambo mojawapo la muhimu na la busara


kabisa mtoto kufundishwa kumtii Mungu, maana
tangu mwanzo wa historia ya mwanadamu
alipoumbwa, alipimwa utii wake na Mungu
kutokana na maagizo waliopewa kupitia neno la
Mungu. Kwa hiyo tunapaswa kuwalea na
kuwafundisha katika utii.
UTII KWA MUNGU
(a). Utii ni uadilifu toka kwa Mungu.
(b) Kuwa mtii ni kuishi katika ahadi ya Mungu.
(c). Kuwa mtii ni kuendelea kupokea baraka za
Mungu.
(d). Kuwa mtii ni kudumisha na kujenga uhusiano
na Mungu.
Tangu mwanzo wanadamu wanapimwa na Mungu
kutokana na maagizo anayowapa kutokana na neno
lake maishani mwao kwa njia ya imani na utii
yanaonyeshwa kama kanuni inaongozwa katika
uhusiano wa Adamu na Mungu katika Edeni.
Adamu alionywa kwamba atakufa kama akiyaasi
mapenzi ya Mungu au maagizo ya Mungu na kula
kutokana katika mti wa ujuzi wa mema na mabaya,
kwa kuwa adamu alikuwa hajaona kifo cha
mwanadamu alitakiwa kuamini na kutii kwa kufuata
neno alilosema Mungu.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 64


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Adamu alipewa agizo kama kipimo cha uadilifu


Agizo liliwekwa mbele yake kuwa uchunguzi na
makusudi kabisa kuamini na kutii, au kutoamini na
kutotii mapenzi ya Mungu muumbaji wake, kwa
kadri ambavyo Adamu angeliamini neno la Mungu
na kulitii, angeliendelea katika uzima wa milele na
katika ushirika wa baraka za Mungu.
Mwanzo 3:6 “Mwanamke alipoona yakuwa ule utii
wafaa kwa chakula wapendeza macho nao ni mti
wa kutamanika kwa maarifa basi alitwaa katika
yake akala, akampa na mumewe naye akala”.
Kwa hiyo katika eneo hili la utii kwa Mungu
tunapaswa kujifunza kufundisha kuelekeza watoto
kwamba utii ni sehemu moja wapo inayomfurahisha
Mungu. Mtu kimtii Mungu hatakosa baraka za
Mungu, kumbe tunaweza kuwafundisha kabisa
watoto, kuwa kutotii ni uasi.
Adamu na Hawa waliasi amri ya Mungu kwa
kuacha kutii maagizo ya Mungu, badala yake kaitii
sauti ya nyoka, ambaye ni shetani.
Tufundishe na kuonyesha agizo maalum ambalo
Mungu alichohitaji, kwa mwanadamu ni utii,
mwanadamu, hakuruhusiwa kula matunda kutoka
kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya.
Matokeo ya kutotii agizo hili yalielekezwa ama
yalisababishwa na shetani au Ibilisi ambaye ni adui
mkuu wa Mungu hakutaka mwanadamu amtii
Mungu, kwa hiyo alimjia Hawa kama nyoka
mwelevu kujaribu kumfanya asitii agizo ambalo
Mungu likuwa amempa, Alishawishiwa Hawa

Mwl. Joyce Z. Mgaya 65


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kutomtii Mungu kwa kula kutoka katika mti


aliokatazwa. Naye Hawa akamshawishi Adamu
naye akala. Kwa hiyo kutotii huku kunaitwa dhambi.
(Mwanzo 3:16) Kwa hiyo mtoto afundishwe kuwa
mojawapo ya dhambi aliyoifanya mwanadamu ni
kutotii, kuliamini neno la Mungu, kuamini kwamba
kwa namna fulani Mungu hamanishi hasa kile,
anachokisema kuhusu wokovu, haki, dhambi, na
hukumu na kifo. Uongo wa shetani zaidi ni kwamba
kukoswa toba na dhambi za makusudi kabisa dhidi
ya Mungu siyo lazima vilete kutengwa na Mungu
milele.
Shetani alisababisha kuanguka kwa mwanadamu
kwa njia ya udanganyifu. Hii ndio mojawapo ya njia
zake katika kuwaongoza watu mbali na njia ya
Mungu na kweli, ili kusudi watu waendelee kutomtii
Mungu hata leo, shetani hudanganya na kupotosha
macho, akili za wasioamini wa ulimwengu huu ili
wasiweze kuelewa Injili. Na kwa njia ya uongo wa
shetani wengine ndani ya kanisa wanaamini
kwamba wanaweza kuishi maisha machafu na bado
waurithi ufalme wa milele. Udanganyifu ndio njia
kuu ya shetani kuongoza wengi katika uasi dhidi ya
Mungu. (2The 2:8-12), (Ufunuo 20:8)
Katika maandiko haya utaona kazi ya shetani kuwa
ni uongo madanganyo, udhalimu na kuendelea
kuwapoteza waliopotea ambao wengi wao wanazo
dini lakini wanaamini katika, uongo na kujifurahisha
katika udhalimu. Katika hili mtu wa Mungu
inatakiwa Wakristo wote, lazima kadri ya uwezo

Mwl. Joyce Z. Mgaya 66


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

wao na kujiandaa kupambana, katika mapambano


yanayoendelea ya kufa na kupona dhidi ya uongo
wa shetani, katika maisha yao wenyewe na
makanisani, shuleni, na katika maeneo yote na
kuhakiki roho za watu pamoja na watoto
zinanusurika na roho ya uasi.
Vipo vitu ambavyo vinaendelea ulimwenguni
ambavyo ni uasi lakini wanadamu hawavioni, kuwa
ni uasi na kutomtii Mungu. Kama vile mavazi
yanayotia aibu. Katika familia nyingi leo ukiingia
baba, mama, mtoto, utawatofautisha labda kwa
maziwa na nywele ndo utajua. Huyu ni mwanamke
na huyu ni mwanaume,
Haya ni mambo ambayo yako hadi kwa watu wanao
mcha Mungu siyo wa mataifa tu.
Lakini kumbuka neno la Mungu linaelekeza katika
mavazi kujipamba n.k.
(1Timotheo 2:9) “Vivyo hivyo wanawake na
wajipambe kwa mavazi ya kujistiri, pamoja na
adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka
nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo
za thamani ”.
Katika maeneo kama haya wasiofundisha watoto na
kusaidiwa ni mojawapo ya maeneo yanafanywa leo
watoto washindwe kumtii Mungu na na maagizo
yake wtoto wameacha kufuata maagizo ya kumtii
Mungu badala yake wanatii ulimwengu,
hawamtafuti Mungu wanafuata mitandao na
utandawazi. Kuiga mambo mabaya, mavazi mabaya
ya mataifa mengine ambao wao katika nchi zao

Mwl. Joyce Z. Mgaya 67


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

wamevaa kwasababu maalumu; pengine kama vile


joto katika mabara mengine. Kwa hiyo
inawapelekea kuvaa nguo nyepesi, fupi, n.k. au
pengine ni tamaduni za watu fulani, Unapaswa pia
kama mzazi, mlezi kuzijua pia tamaduni zako yaani
mila za kwenu na za watu au mataifa na makabila
mengine ili uweze kumsaidia mtoto aishi vizuri na
asimkosee Mungu. Zile tamaduni na mila zilizo
njema basi afundishwe mtoto na zilizo mbaya
azuiliwe mfano; Salamu ziko za aina nyingi au
mbalimbali na lengo la salamu ni kuonyesha
heshima. Mtoto anapoamkia huonyesha heshima
katika hili mtoto anaweza kufundishwa kwamba
Mungu wetu pia huamkiwa kwa njia ya maombi
alfajiri pamoja na kumshukuru kuonyesha shukrani
kwamba ametulinda na kuonyesha utii kwamba
katika kila jambo tunamtanguliza Mungu.
Lakini hizo salamu kama vile kumkumbatia na
kupiga busu, haya ni mambo ambayo pengine ni ya
mataifa mengine na tamaduni zingine. Tunaweza
kuona katika hizo salam kama haziko vizuri na
tukawazuia ili kusudi wasimkosee Mungu wabaki
katika utii.
Hata katika agano la kale Mungu alihitaji watu
wamtii na kutembea katika njia zake. Alisema na
watumishi wake na watumishi wake walisema na
watu wakae juu ya maagizo yake ili watembee na
kumtii katika hayo.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 68


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

(Kumbukumbu 13:4) “Tembeeni kwa kumfuata


BWANA Mungu wenu; mcheni na kushika
maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi
mtumikieni na kushikamana naye.”
Mungu alihitaji watu watembee kwa kufuata
maagizo yake, kushikamana naye. Hii ni njia
mojawapo ya utii kwa Mungu, maana mtu anaye
mtii Mungu lazima atatembea katika njia zake.
Kwa hiyo swala la utii ni la msingi mtu wa Mungu
mtoto wako akiweza kutembea katika utii ataziona
baraka za Mungu.
Utajifunza juu ya watu waliomtii Mungu, na
wakawafundisha watoto wao utii kwa Mungu na
watoto hao wakapata baraka za kipekee toka kwa
Mungu.
ISAKA KUBARIKIWA NA MUNGU.
Isaka alibarikiwa na Mungu kutokana na utii
aliokuwa nao baba yake naye akaurithi utii.
Ibrahimu alikuwa mtu mtii kwa Mungu kwa
viwango vya juu sana hadi Mungu anamhakikishia
kuwa hakika nimejua unanipenda.
Kumbe unaweza kujifunza kuwa kumtii Mungu ni
njia ya kuonyesha kuwa unampenda Mungu. Kwa
hiyo kumbe utii ni upendo maana ukimpenda mtu
utamtii, ukimpenda Mungu utamtii kwa kufuata
maagizo yake.
(Mwanzo12:1-3,7) “Bwana akamwambia Abramu,
toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako na
nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi
nitakayokuonyesha”.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 69


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

(Mwanzo 13:14-18,15) na (Mwa17:1-8,15-22)


(Mwanzo 22:15-18)
Ilimbidi Isaka ajifunze kuishi kwa ahadi za Mungu,
kama alivyofanya baba yake.
Hapo utaona sehemu ya muhimu ya ahadi na agano
ilikuwa ni ule uhusiano wa binafsi na Mungu
alioelezwa katika maneno “Nitakuwa pamoja
nawe” (Mwanzo 26:24). Haikutosha Isaka kuwa na
Ibrahimu kama baba yake, ila ilimpasa pia
kuzipokea ahadi za Mungu kwa Imani. Hapo tu
ndipo Bwana angeweza kusema “Mimi ni pamoja
nawe nami nitakubariki na kuzidisha uzao wako”
Ilimpasa Isaka kuwa mtiifu ili kuendelea kupokea
baraka za agano vivyo hivyo, sisi na watoto wetu
tunapaswa kuwa watiifu kwa Mungu ili kuendelea
kupokea baraka za Mungu katika maisha yetu yote;
Haitoshi kuishi kwa kutegemea baraka za wazazi au
za watu wengine bali kwa uhusiano binafsi na
Mungu katika maisha yetu.
UTII KWA WAZAZI
Utii kwa wazazi wetu na walezi ni muhimu maana
ni agizo na ni amri.
Kwa hiyo tunapoacha pia kujifunza kufundisha
kuhusu utii kwa wazazi tunakuwa tumeyaacha
maagizo na amri za Mungu.
Kutoka 20:12 “Waheshimu baba yako na mama
yako, siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi
upewayo na Bwana Mungu wako”.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 70


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Hapo utajifunza na kuona kutii wazazi kumbe ni


kuheshimu. Ili pia tufanikiwe na kuwa na siku
nyingi za kuishi ni pale atakapo watii wazazi.
Kumbukumbu la Torati 5:16, Efeso 6:1-3
Haya ni maneno ya Mungu yanayo husiana na utii
kwa wazazi na kuwa heshimu, lakini pia Waefeso,
mtume Paulo anaelezea pia tuwalee watoto wetu
katika Bwana, Hii ni zaidi sana kwa watu
wanaomcha Mungu ni vema wkajitahidi
wasiwachoshe watoto wao.
Kolosai 3:20-21 “Ninyi watoto watiini wazazi wenu
katika mambo yote, maana jambo hili lapendeza
katika Bwana, (12) Ninyi akina baba,
msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata
tama”.
Hapo tunaona na kujifunza kwa watu ambao
wanaweza kuwafunza watoto ni wazazi.
Ili wapate kuwatii, neno la Mungu linaelezea kuwa
tusiwachokoze watoto wasije wakakata tamaa,
Hivyo basi tukifundisha watoto vizuri watuheshimu,
na pia hawatakata tamaa katika maisha yao yote ya
kiroho au ya kimwili.
KUTOTII WAZAZI HULETA LAANA
Torati 27:16 “Na alaaniwe amdharauye baba yake
na mama yake na watu wote waseme Amina”.
Hapa pia utaona juu ya mtoto asiyetii atapata laana.
Kuna mambo yanayotokea ambayo pengine
huwafanya watoto wapate laana kwa hiyo wazazi
Wanapaswa kuyaepuka mambo kama vile ulevi na
zinaa za ajabu.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 71


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Nuhu alipolewa mtoto wake mmoja alimuona na


kumcheka, na alipolevuka katika ulevi wake akatoa
laana.
Mwanzo 9:25 “Akasema na alaaniwe Kanaani,
atakuwa mtumwa kabisa kwa ndugu zake”.
Ukiangalia laana hii haikuwa ya busara kabisa,
ndani yake kulikuwa na uonevu japo mtoto alikosa.
Aliyesababisha kosa ni Nuhu mwenyewe kwa hapo
ndiyo linakuja andiko la Kolosai 3:21
“Ninyi akina baba msiwachokoze watoto wenu
wasije wakakata tamaa.”. Kwa hiyo mzazi au mlezi
unapaswa kuwa mtu wa staha unayeishi na
kujiheshimu ili kuepusha laana sizizo na sababu
katika nyumba yako. Katika ulimwengu huu wa
sasa kuna wazazi wengi ambao wameleta laana juu
ya watoto wao, kwa kutojiheshimu wenyewe.
Unakuta baba na mama wote ni ulevi, watu
wanaopenda zinaa, uasherati. Hadi unakuta heshima
yao kwa watoto wao inaondoka. Kwa hiyo mambo
kama hayo wazazi wanapaswa kuepukana nayo
haraka ili kuwapa watoto furaha ama kuwa na
furaha na wazazi wao.
JUKUMU LA MZAZ/WAZAZI WALEZI
1).Kuwapenda watoto na kuwathamini
- Mzazi au mlezi anapaswa kuonyesha upendo wa
dhati kwa watoto wake.
- Mzazi atamke maneno yanayoonyesha unamjali na
kumpenda.
- Na wala siyo maneno mabaya yaliyojaa laana

Mwl. Joyce Z. Mgaya 72


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

-Mwonyeshe kwa vitendo kwamba unapenda na


mtendee matendo mema.
-Uwe na muda wa kuongea naye, muda wa
kumsikiliza /na kumuelekeza ambayo atakayo fanya
ya kuonesha kumtii Mungu na kuonesha heshima
kwenu wazazi.
-Na pia uwe na mda wa kushiriki michezo yake n.k
-Fuatilia njia zake, pamoja na masomo yake.
-Hakikisha mtoto anakula chakula na mahitaji
muhimu.
(2)Kuwafundisha watoto mambo yapasayo kuyajua
Kufanya.
Torati 6:6-7 “Na maneno haya ninayo kuamuru
leo yatakuwa katika moyo wako 7) Nawe
uwafundishe watoto wako kwa bidii, na kuyanena
uketipo katika nyumba yako na utembeapo njiani
na ulalapo na uondokapo”.
Mfundishe kumjua Mungu, maombi neno, ibada n.k.
Mfundishe maadili mema.
Mtoto afundishwe kufanya kazi aina zote kwa umri
wake.
Hakikisha unampeleka shuleni.
Mtoto akikosea muonye ikibidi mpe adhabu,
Adhabu iendane na umri wake na kosa na pia
iendane na haki za binadamu.
Nimeelezea katika kipengele cha kuutambua
uthamani wa mtoto.
Mithali 22:15, Mithali 23:13
iii). Kuwaombea watoto bila kukoma.
Luka 23:27-29

Mwl. Joyce Z. Mgaya 73


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Maombolezo2:19
Kumbuka kuna vita kali kati ya shetani na
mwanamke pamoja na uzao wake
Mwanzo 3:14-15, Ufu 12:17
Watoto watajwe kwa majina yao kila siku mbele za
Mungu, waombewe bila kukoma, usikubali
kunyamaza mpaka warudishwe. Yeremia 31:15
BARIKIWA na MUNGU!!!.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 74


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

SURA YA 6

FAIDA ZA MTOTO ALIYEZALIWA NA


KULELEWA KATIKA KUMCHA MUNGU NA
KUMUABUDU MUNGU NA WALA SI MIUNGU.

K una faida kubwa kwa mtu anayezaliwa, kuishi


katika kumcha Mungu na kumwabudu Mungu na
wala si miungu.
Kumwabudu Mungu ni faida maana ni agizo la
Mungu tokea mwanzo Mungu wetu alihitaji
kuabudiwa. Si hivyo tu tunamjua Mungu kuwa ni
Mungu wa kuabudiwa. Kwa hiyo mtoto anayelelewa
katika kumcha Mungu na kumwabudu anayo faida
maana atakuwa anatembea katika agizo la Mungu.
Zaburi 103:17 “Bali fadhili za Bwana, zina
wamchao, tangu milele hata milele, na haki yake
ina wana wa wana”.
Katika kumcha Bwana kuna fadhili zinazo kaa tangu
milele na milele kuna haki ambayo itakuwa ndani ya
wana kwa sababu ya kumcha Bwana.
Kutoka 20:6 “Nami nawarehemu maelfu elfu
wanipendao, na kuzishika amri zangu”
Amri ambazo ni pamoja na kumcha na kumwabudu
maana ili kuwa si halisi na wala si rahisi mtu
kumcha Mungu pasipo kumpenda na kuzishika amri
zake. Hata hivyo mtu aliyezaliwa na kulelewa katika
kumcha Bwana na kumwabudu anayo faida maana
na kumcha Bwana ni chanzo cha hekima na maarifa

Mwl. Joyce Z. Mgaya 75


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

kwahiyo huyo mtu atakuwa tokea mwanzo wake,


akiwa na maarifa na hekima.
Mithali 1:7 “Kumcha Bwana ni chanzo cha
maarifa, bali wapumbavu haidharau hekima na
adabu”.
Tunasababu za msingi za kuwalea watoto katika
kumcha ili wapate faida katika maisha yao.
Ili pia wawe wenye akili njema lazima kumcha
Mungu.
Zaburi 111:10 “Kumcha Bwana ndio mwanzo wa
hekima wote wafanyao hayo wana akili njema”.
Katika vipengele hivi ulivyoviona utaona kabisa
faida ya kumcha Mungu kwa sababu ni:-
Agizo na amri.
Katika kumcha Bwana kuna fadhili.
Kuna haki.
Kuna rehema.
Kuna maarifa na hekima.
Kuna akili njema.
Tukiendelea mbele na kuziona faida za kumcha
Bwana mwandishi katika zaburi anaelezea kuwa ana
heri mtu yule amchaye Bwana anaye pendenzwa na
maagizo yake.
Utajifunza kuwa unaheri katika kumcha Bwana
anaelezea na kusema aweke mtu huyo pia utakuwa
hodari sababu amemcha Bwana.
Zaburi 112:1-2 “Haleluya, Heri mtu yule amchaye
Bwana, Ampendezwaye sana na maagizo yake (2)
wazao wake watakuwa hodari duniani, kizazi cha
mwenye adili kitabalikiwa”.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 76


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Kwa hiyo kumcha Bwana pia ni kuwa mtu mwenye


adili na kizazi chake kitabarikiwa.
Pia tukiwazaa watoto na kuwalea katika kumcha
Bwana watakuwa watu wenye adili na vizazi vyao
baadae vitabarikiwa.
Mtoto aliyezaliwa na kulelewa katika kumcha
Mungu atatengana na uovu, na huo ndio ufahamu.
Kwa hiyo tunawajibu wa kulea na kufundisha
watoto katika kumcha Mungu ili wawe na hekima
na watengane na uovu.
AGANO LA KALE
Katika agano la kale kumcha Mungu na kumwabudu
ili kuwa ni sheria na amri pia ilikuwa ni agano watu
walimwabudu Mungu kwa uzuri na utakatifu na
kutetemekewa.
Zaburi 96: 9. Zaburi 29:2
“Mwabudu Bwana, kwa uzuri wa utakatifu,
tetemekeni mbele zake nchi yote”. Kumwabudu
Mungu kwa uzuri na utakatifu na kwa kutetemeka ni
faida pia.
Kwa hiyo katika agano hilo watu walifanya hivyo
kumwabudu Mungu na walitenga maeneo na
kujenga madhabahu za kuabudu, na kutoa sadaka
zao hapo katika madhabahu walizozijenga.
1Samweli 1:3 ‘Na mtu huyo alikuwa akikwea
kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka ili
kuabudu na kumtolea Bwana wa majeshi dhabihu
katika shilo.”
Hizi ni habari za mtu mmoja aliye julikana kwa jina
la Elikana yeye na nyumba yake alikuwa na

Mwl. Joyce Z. Mgaya 77


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

utaratibu wa kukwea mwaka kwa mwaka, kwenda


kuabudu huko shilo na kumtolea Bwana dhabihu.
Pia alipokuwa katika kutoa dhabihu hakujitolea
pekee yake aliwatolea watoto wake pia, Hii ilikuwa
na maana kwamba, alikuwa anawalea na
kuwafundisha kumwabudu Mungu pamoja na
matoleo.
Hivyo ni muhimu kumfundisha mtoto kumcha
Mungu na kumwabudu Mungu pamoja na sadaka
hiyo ni njia ya kukamilisha Ibada, kwa hiyo
anapaswa kujua ili ukamilishe Ibada lazima utomlee
Mungu unayemwabudu matoleo au dhabihu.
Katika agano hili la kale, Mungu aliweka agano la
tohara. Kwa hiyo kila mtu mme alitahiliwa kama
Ishara ya agano waliloliweka na Mungu wao na
agano hili halikuanzia kwa Musa bali lilianzia kwa
Ibrahimu, Ibrahimu mwenyewe alitahiliwa akiwa na
umri mkubwa pamoja na mwanaye Ishimaeli,
Mwanza 17:26 “Siku ile ile akatahiliwa Ibrahimu
na Ishmaeli mwanawe”.
Mwanzo 17:9“Mungu akamwambia Ibrahimu,
Nawe ulishika agano langu, wewe na uzao wako
kwa vizazi vyako baada yako. Hili ndilo agano
langu utakaolishika kati ya mimi na wewe na uzao
wako baada yako kila mwanaume wa kwenu
atatahiriwa”.
Hili lililokuwa agano la Ibrahimu toka kwa Mungu
ama uthibitisho wa kuwa anamcha Mungu na
kumuabudu. Na likafanywa na kila mtu mme
aliyekuwa katika nyumba ya Ibrahimu.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 78


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Lakini Musa na Yoshua pia Mungu alifanya nao


agano, Hata alipofika ule wakati ambao Musa
alikuwa amemkosea Mungu, na Mungu
akamwambia yeye hatavuka ile nchi apate kuimiliki,
aliwakumbusha wana wa Israeli kulishika agano la
Bwana.
Torati 4:24 “Jihadhari nafsi zenu, msije
mkalisahau agano la Bwana Mungu wenu
alilolifanya nanyi mkijifanyia sanamu za
kuchonga, mfano; wa umbo la kitu chochote
alichokatazwa na Bwana Mungu wenu”.
Hata wakati ule wana waIsraeli watu wazima
walipofia jangwani watoto wao, walifanywa tohara
kwanza ndio wakavua kuwamiliki nchi maana ni
agano. Pia katika agano jipya Mungu
anadhithibitisha hili.
Mdo 7:8 “Akampa agano la tohara basi Ibrahimu
akamzaa Isaka akamtahili siku ya nane, Isaka
akamzaa Yakobo, Yakobo akaazaa wale kumi na
wawili wazee wetu”.
Utaona anatuthibitisha kwa sisi tumwabudu Mungu.
(Kumb 2:28), (Fip 3:3)
Anasema pia katika wakati ule tohara ilifanyika
katika mwili yaani tohara ya nje, tena kwa mikono.
Lakini agano letu la sasa tohara ni ya moyoni katika
roho. (Rum 2:29)
Katika maandiko haya ya agano jipya utaona kuwa
kumbe tukiokoka na kumcha Mungu katika roho,
tukimwamini Yesu Kristo tutakuwa tumeisha pata
agano la tohara ya Mungu kwa njia ya Yesu kristo.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 79


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Kolosai2:11 “Katika yeye nimetahiliwa kuwa


tohara isiyofanyika kwa mikono kwa kuwa mwili
wa nyama, kwa tohara ya Kristo”.
Mpendwa mteule wa Mungu na msomaji wa kitabu
hiki nafikiri nimejaribu kuelezea mengi katika eneo
hili la kumcha Mungu na kumwabudu na
kumuonyesha kwa ufupi kwamba swala la kumcha
Mungu na kumwabudu halijaibuka tu sasa hivi.
Tumeona lilianza tokea mwanzo yaani katika agano
la kale, wenzetu pia walimwabudu Mungu na
wakapata faida katika kumcha Mungu na wakapata
faida katika kumcha Mungu na kumwabudu hadi
Mungu akaona umuhimu wa kuweka agano na watu
wake tumeona kwanza kabisa aliweka na baba yetu
Ibrahimu mzee wa imani lakini pia aliweka na Musa
pamoja na Yoshua ukisoma katika vitabu vya Agano
la Kale kama (Mwa 17:26), (Mwa17:9-10), (Kumb
4:24) na vingine vingi utaona mambo kama haya,
lakini tumeona kumbe hata katika agano jipya
hatujasahaulika Mungu bado alitupatia agano naye
kwa njia ya kipekee mno ambayo pia tumeisoma
katika (Mdo 7:8) ambapo hapo anaendelea
kudhihirisha kuwa yeye ndiye mwenye kumpa
Ibrahimu agano hili lakini katika (Kolosai 2: 11).
Hapa pia utaona kwamba na sisi tunayo tohara
isiyofanywa kwa mikono kwa kuvua mwili wa
nyama, bali ni kwa tohara ya Kristo Yesu,
aliyesulubiwa na kufa msalabani, kwa hiyo
tunaweza kujifunza na kuona kwamba kufa kwa
Yesu kristo msalabani ni njia ya agano kwetu.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 80


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Baada ya kusema haya nataka pia nikuonyeshe


kwamba kumcha Mungu na kuabudu pia ni lazima
kulijua neno.
NENO LA MUNGU.
Katika maandiko matakatifu, Neno la Mungu
hautambuliwa kama ni chakula cha kiroho. Pia neno
la Mungu ni maziwa, Petro akiwaaandikia wakristo
waliohitaji kukua kiroho alisema kama watoto
wachanga waliozaliwa sasa yatamani maziwa ya
akili yasiyoghoshiwa. Ili kwa hayo mpate kuukulia
wokovu.
1Petro 2:2. Kwa hiyo kwa wazazi Wakristo
waliokoka na kumpa Yesu maisha yao, waliokomaa
kiroho ambao neno la Mungu ni chakula chao.
Wakipatikana na kusimama vizuri watawasaidia
watoto na watu wengine pia.
Ukisoma katika Waebrania utaona mtume Paulo ana
waandikia kwamba.
“Kwa maana iwapasapo kuwa wahitimu (maana
wakati mwingi umepita) mnahitaji kufundishwa na
mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu
nanyi, na mmekuwa na hitaji maziwa wala si
chakula kigumu” (Ebr 5.12)
Kwa hiyo utaona kuwa kumbe kuna wakati ambao
tunahitajika kuwa waalimu, na kumbe bado
tunahitaji kufundishwa na mtu. Kumbe na sisi
wenyewe tunakuwa bado tunahitaji maziwa na si
chakula kigumu, Hivyo itakuwa ni hatari katika
maisha yetu ya kiroho pamoja na watoto wetu.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 81


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Kwa kuona hivyo tunapaswa kutambua tunao


wajibu wa kuwa imara katika neno sisi kama wazazi
walezi ili tuweze kulea watoto wetu vizuri, katika
kumcha Mungu na kumwabudu.
Hitaji kubwa pia leo katika kanisa niseme kwamba
ni kuwa na wakristo walio na ufahamu kidogo wa
neno la Mungu kwa sababu wakristo hawa wa leo
hawasomi neno; hawana hamu na shauku ya kusoma
neno na si kwamba hawana Biblia hapa wengine
wanazo zaidi hata ya mbili. Mwingine hana kabisa si
kwamba hana uwezo wa kununua Biblia ila ni
kwasababu hana hamu wala shauku ya kusoma
Biblia na hao walionazo huzifunua siku za jumapili
katika Ibada pekee hii siku moja haiwezi kufanya
wewe kulisoma neno na kulielewa na kuwafundisha
watoto wako na kuwasaidia wengine, kwa hiyo
jambo la muhimu kwa mkristo awe mtu wa kupenda
kusoma neno la Mungu.
Hapo ndipo atakapoweza kuwalea watoto wake na
kuwasaidia na kufikia kuziona faida.
HASARA ZA KUABUDU MIUNGU NA WALA SI
MUNGU.
Kuna hasara kubwa zinazowapata watu, wanao
abudu miungu na kuacha kuabudu Mungu wa kweli
na aliye hai.
Tokea mwanzo Mungu alipomuumba mwanadamu
Mungu alihitajia abudiwe yeye peke yake, lakini
mwanadamu aliposhindwa kumwabudu Mungu,
alipata hasara katika maisha yake, Mungu
alimtupilia mbali katika utumwa lakini bado

Mwl. Joyce Z. Mgaya 82


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

aliposikia kilio chao katika utumwa ule na


kuwarudisha ten, aliwapa maagizo ya kumwabudu
yeye peke yake na wala si miungu mingine.
Kutoka 20:1-3 “Mungu akanena na Musa
maneno haya yote akasema mimi ni Bwana,
Mungu wako niliyekutoa katika nchi ya misri
katika nyumba ya utumwa. Usiwe na miungu
mingine ila mimi”.
Hii mistari inatuonyesha jinsi Mungu ambayo
hakuhitaji watu waabudu miungu, na kwahiyo mtu
aliyeacha amri hii na kuabudu miungu mingine
alipata hasara katika maisha yake na nyumba yake.
Lakini pia yapo maandiko mengine yana endelea
kuthibitisha na kuonya ambavyo Mungu alitoa agizo
hili la kutoabudu miungu.
Torati 6:14 “Msifuate miungu mingine katika
miungu ya mataifa inayowazunguka”.
Kwa hiyo katika haya pia tunaweza kujifunza na
kuwafundisha watoto wetu kuwa Mungu wetu ndiye
Mungu anayestahili kuabudiwa na si miungu maana
tukiabudu miungu tutapata hasara katika maisha
yetu ambazo moja wapo ya hasara hizo ni;
(i) Hasira ya Mungu kuwaka juu yetu. Kuwakiwa
na hasira ya Mungu ni hasara kubwa sana na watu
wa Mungu walipokuwa wakimkosea Mungu kwa
kumwabudu na kufuata miungu hasira ya Mungu
iliwaka juu yao na hata kuangamizwa.
Torati 6:16 “Kwani Bwana, Mungu wako aliye
katikati yako ni Mungu mwenye wivu, isije

Mwl. Joyce Z. Mgaya 83


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

ikawaka juu yako hasira ya Bwana, Mungu wako


akakuangamiza kutoka katika uso wan chi”.
(ii). Ni kutembea katika laana ya Mungu. Watu
walipo muacha Mungu na kufuata miungu
walitembea katika laana za Mungu. Mungu
amenena katika maandiko yake matakatifu katika:-
Torati 4:19,24-26 “Mungu akawaambia wana wa
Israeli kwamba tena msije mkainua macho yenu
juu na kuliona jua, nyota na mwezi
mkashawishika kuviabudu na kuvitumia”. Na pia
anasema kwa kuwa yeye ni Bwana ni moto ulao na
mwenye wivu, kwa hiyo utakapozaa wana wa wana
na mkisha kuwa katika nchi siku nyingi mkajiharibu
na kufanya sanamu ya kuchonga kwa umbo la kitu
chochote, mkafanya uovu machoni pake na kumtia
hasara. Anasema kuwa mbingu na nchi vitashuhudia
kwamba karibu mtaangamia na kushindwa kuivukia
nchi tunayo itarajia kuivukia.
Kuna hasara ya kuaibishwa na Bwana kwa wale
wote wanao abudu sanamu
(Zaburi 97:7) Katika hii mtu wa Mungu anapaswa
kujifunza kwamba Mungu wetu hapendezwi na watu
wanao abudu miungu wala sanamu maana watapata
hasara kubwa zaidi ya zote ambao ni kukosa uzima
wa milele, huo ndio wito wetu mkuu kwa Mungu,
mengine yote ni maangalizo ya kutufanya tufike.
Lakini yeye Mungu ameendelea katika agano jipya
na kusema inawapasa wamuabuduo halisi
wamuabudu katika roho na kweli.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 84


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

Yohana 4:23 “Lakini saa inakuja nayo saa ipo


ambapo waabudu halisi watamwabudu Baba
katika roho na kwetu kwa maana Baba awatafuta
watu kama hao wamuabudu.”.
Haya ni maneno ya Bwana wetu Yesu kristo
aliyozungumza na mwanamke Msamaria katika
kisima cha Yakobo, tena alizungumza naye na
kumuonyesha kwamba wanaabudu wasicho kijua,
kwa hiyo kumbe kuabudu muingu ni hasara kubwa
kwasababu mtu huabudu asichokijua.
Na kama nilivyokwisha kusema kwamba watu
katika agano la kale waliweka hadi agano la tohara
kwa ajili ya kuabudu, vivyo hivyo na sisi katika
agano jipya ipo tohara ya Yesu ambayo
inatuunganisha na Mungu wetu kwani
tunapomwamini Yesu tunakuwa na tohara ya Yesu
Filp 3:3 “Maana sisi tu tohara tumwabuduo
Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya kriso
Yesu, wala hatuutumainii mwili.”
Hivyo basi katika hayo yote tunapaswa kuona amri
hii ni ya kumlea au kuwalea watoto wetu vizuri
katika Bwana na kuwafundisha kuyashika yote
yaliyo mema bila kusahau kuwafundisha kumcha
Mungu na kuabudu ipasavyo, ili kuyafikia mema, na
kuepuka hasara zitokanazo na kuabudu miungu na
kumuacha Mungu.Tusisahau kutoa muda wetu
kuzungumza na watoto wetu, kutoka na maeneo
yote ambayo tumejifunza kuwalea maana katika
kitabu hiki kwa mtu ambaye atafanikiwa kukipata na
kukisoma najua mpendwa mteule wa Mungu

Mwl. Joyce Z. Mgaya 85


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

utakuwa na hatua kubwa katika kulea mtoto wako


na watoto wengine, Na kwa wakristo utakapokisoma
kitabu na kuchukua hatua za kufundishaji na
kuyatendea kazi masomo haya na kufundisha watoto
wako, utayaona mabadiliko makubwa sana.
HITIMISHO
Nashauri utenge muda wa mazungumzo na maswali
baada ya mafundisho ili kuona kwamba yale
unayofundisha anayaelewa na kuyatendea kazi.
Utakapofanya mambo kama haya pia utaona
kwamba yale uliyojifunza yana faida au
kujifurahisha tu.
ANGALIZO.
Kwa wazazi/mzazi mlezi wakati wote unapoona
mtoto amegeuka au tabia yake ina kuudhi muone
adui yako shetani ndani ya mtoto na kamwe
usimuchukie mtoto, Anayetafutwa hapo ni wewe na
uzao wako.
Pambana na shetani au roho za shetani ndani ya
mtoto na kamwe usikubali kumsukuma mtoto kwa
shetani. Kipindi hicho unatakiwa kuonyesha upendo
wa karibu na wa dhati kwa mtoto.
Mueleze kwa upole na upendo, usipambane naye
kimabavu utampoteza mtoto achukuliwe na shetani
(wajuaje neema na rehema za Mungu juu ya mtoto)
kumbuka habari ya mwana mpotevu
(Luka 15:11-24)

Mungu akubariki sana msomaji wa kitabu hiki.


AMENI!!!

Mwl. Joyce Z. Mgaya 86


MBINU ZA KUMLEA MTOTO

VITABU VYA REJEA

Askofu Mabula Kitula (2008). Umezaliwa kukua;


Kanuni za kukua kiroho: Inland publishers, Mwanza
-Tanzania.
Bible society of Tanzania and Kenya (1997), Biblia,
maandiko Matakatifu: Bible society of Kenya and
Tanzania.
E. A. G. T (2016) Mtaala wa kwanza wa kufundisha
watoto; Chipukizi wa injili: Kamati ya Taifa ya
Kurugenzi ya watoto (CWI) - Tanzania.
Idara ya Ustawi wa jamii (2020). Mafunzo ya malezi
ya watoto katika vituo vya kulelea watoto wadogo –
Mwanza- Tanzania.
Paschal Francis (2019). Wajue Maadui wa Hatima
Yako: Paschal Francis Publishers, Mwanza -
Tanzania,
Pastor. Aldrof. Pangalas (2020) Jinsi ya kuishi na
Mwenzako kisaikolojia. Ebeligisha Tanzania,
Mwanza - Tanzania.

Mwl. Joyce Z. Mgaya 87

You might also like