You are on page 1of 40

NIAMUE LIPI?

Hakimiliki

Daniel John Seni@2013

Unaruhusiwa kunakili, kutumia na kusambaza maneno yaliyo


katika kitabu hiki bila kuomba kibali kutoka kwa mwandishi.
Lengo la mwandishi si kutumia kitabu hiki kwa mauzo, lakini ni
kuufahamisha umma wa wakristo kuhusu masuala ya kimaadili.

Kwa mara ya kwanza kilipigwa chapa na Shekinah Press-Dar es


salaam

1
YALIYOMO
NIAMUE LIPI? ...................................................................................................4
MAADILI YA KIKRISTO .................................................................................5
Maadili ni nini? ..............................................................................................5
Maadili binafsi................................................................................................7
Maadili ya kijamii ..........................................................................................7
Chanzo cha maadili ya Kikristo...................................................................9
Ufunuo wa Kawaida ...................................................................................10
Ufunuo maalum ...........................................................................................10
Neno lililo hai ...............................................................................................10
Masuala ya Siasa ..........................................................................................13
Kanisa na siasa .............................................................................................14
Hoja za wanaataa kujihusisha na siasa .....................................................15
Hoja kwa wale wanaokubali kujihusisha na siasa. .................................15
Maswali la mjadala: .....................................................................................16
Vita katika agano la kale .............................................................................17
Vita katika agano jipya ...............................................................................17
Kanuni za kutumia kunapotokea vita kati ya wakristo na wasio
wakristo.........................................................................................................17
Swali la mjadala ...........................................................................................18
Umaskini .......................................................................................................18
Rushwa ..........................................................................................................19
Harambee/fund rising................................................................................19
Kuomba msaada kwa wasio wakristo ..................................................21

2
Kutangaza fedha zilizotolewa katika harambee au kama ni msaada
wa mtu.......................................................................................................21
Mhubiri kuomba fedha ili aje kufanya kwenye mkutano .................22
Utasa/Ugumba ............................................................................................23
Chanzo cha utasa/ ugumba .......................................................................24
Kwa wanaume .............................................................................................24
Kwa wanawake ............................................................................................25
Namna ya kushughulikia ugumba/utasa................................................26
Ndoa ya Lameki Mwanzo 4:19-25 .............................................................27
Ndoa ya Ibrahimu Mwanzo 16-17 na 28-30 .............................................27
Talaka ................................................................................................................29
Nini sababu ya talaka?. ...............................................................................29
Mitazamo mbalimbali kuhusu talaka .......................................................32
Nini madhara ya talaka kwa maisha ya wanandoa? ..............................33
Kileo katika maandiko matakatifu ............................................................35
Mkristo na kunywa pombe. ......................................................................36
Misingi ya mkristo kunywa pombe ....................................................37
Misingi ya mkristo kutokunywa pombe ..............................................38

3
NIAMUE LIPI?
Dunia nzima inahangaika siku hizi kuhusu suala la maadili.
Kwa sasa tunazo changamoto mpya ambazo kanisa halijawahi
kuzipitia hata siku moja. Ingawa Neno linasema kwamba mambo
yote yanayotokea yalishawahi kutokea, lakini jinsi yanavyotokea
ni kwa kiwango cha juu sana. Watu wengi hawaelewi waamue lipi
katika maisha yao. Tunashuhudia masuala ya kimaadili ambayo
hatuna hakika kama yanaenda kinyume na mapenzi ya Mungu
ingawa yako katika mjadala mkubwa, na hapa kutoa hitimisho ni
kwenda kinyume na masuala ya kitaaluma yanayofanyiwa utafiti.

Kuna mambo kama vile; uvutaji wa sigara, je Biblia


imekataza kuvuta sigara? Kuna masuala kama vile ndoa za jinsi
moja, je Biblia imekataza? Kuna masuala kama vile unywaji wa
pombe, masuala ya kingono ambayo hayako wazi katika Biblia.
Hapa ndipo sasa tunapohitaji kitu kinachoitwa “kujua maadili ya
kikristo.” Hivi unajua kwamba siku hizi ni jambo la kawaida kwa
mkristo kupokea rushwa? Kwa madai kwamba hiyo ni fedha ya
shukrani au ya maji? Je kubadilika kwa jina ndio kumehalalisha
suala hili? Hivi pia unajua kwamba siku hizi kijana wa
kiume/kike kushiriki ngono na mchumba wake ni jambo la
kawaida sana? Hata hivyo mtu atakuuliza kwani ni dhambi? Si
nitamuoa mwenyewe? Mambo kama haya yanachanganya jamii
kwa ujumla. Tunahitaji kuwa na mwongozo wa kuamua katika
mambo yetu.

4
Kitabu hiki ni mwongozo mfupi wa maadili ya Kikristo
kwa sehemu fulani. Tutaangalia hoja za msingi kwa ujumla halafu
tunaweza kutabanaisha nini tufanye sasa katika maisha yetu ya
kila siku.

MAADILI YA KIKRISTO
Maadili ni nini?
Maadili ni “Ni mpangilio wa kanuni bora zinazotawala
mwenendo wa kundi maalum la watu.1” Fasili hii inamaanisha
kwamba maadili ni:

Kwa mujibu wa maana hii kumbe kila kundi la watu lina


kanuni zake zinazotawala mwenendo mzima wa kundi hilo. Kwa
maana hiyo ni sahihi kusema kuna maadili ya kikristo, maadili ya
kiualimu, maadili ya kiuongozi nk. 2 maadili ni “maelekezo
yanayofaa ambayo hutolewa kupitia wasilisho fulani.” Ukiangalia
vizuri zaidi fasiri hii utagundua kuwa mwandishi anakaza juu ya
maelekezo yanayofaa, kwa maana hiyo yale maelekezo yasiyofaa
hayo siyo maadili.

Watu wengine hutumia neno ‘maadili’ kumaanisha


mafundisho kuhusu ‘ukweli na uongo’ uzuri na wema. Wengine
wanasema kwamba maadili yanahusika na tabia za watu zilizo
nzuri au mbaya.

Kulingana na fasili hii tunaweza kupata maana moja ya maadili


kwamba ni mpangilio wa kanuni bora ambazo zimelenga kutoa

1
Kunhiyop, S.Y. (2008:). African Christian Ethics. Nairobi: Wordalive Publishers
2
Ndallu na wenzake (2014). Kamusi Teule ya Kiswahili Sanifu. NairobiL: EEP

5
maelekezo yanayofaa kwa ajili ya kundi fulani la watu katika jamii
husika.

Maadili ya kikristo ni mpangilio wa kanuni bora ambazo


zimelenga kutoa maelekezo yanayofaa kwa ajili ya wakristo.
Wataalam wengine hudai kuwa Maadili ya Kikristo muhtasari
wake umetolewa na Wakolosai 3:1-6: "Basi mkiwa mmefufuliwa
pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkon wa
kuum wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa
maan mlikufa na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu.
Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa
pamoja naye katika utukufu. Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika
nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani,
ndiyo ibada ya sanamu; kwa ajili ya mambo hayo huja ghadhabu ya
Mungu3.

Huku zaidi ya orodha ya "kufanya" na ya "kutofanya,"


Biblia inatupa maelekezo ya kina juu ya namna tunapaswa kuishi.
Biblia ndio kila kitu tunahitaji kujua kuhusu jinsi ya kuishi maisha
ya Kikristo. Hata hivyo, Biblia haifundishi kila hali ambayo sisi
hukumbana nayo katika maisha yetu. Ni jinsi gani sasa tunaweza
kuamua hali kama hizo ambazo Biblia haiko wazi kihivyo katika
kuamua mambo? Hapa ndipo maamzi ya kikristo yanapokuja sasa
kutumika!

Sayansi hudai maadili ni "seti ya kanuni za maadili, utafiti


wa maadili." Kwa hiyo, maadili ya Kikristo itakuwa kanuni
inayotokana na imani ya Kikristo ambayo sisi hutenda. Wakati
neno la Mungu linaweza kukosa kuangazia kila hali sisi hupitia
3
www.gotquestions.org/Kiswahili/Maadili-ya-Kikristo.html

6
katika maisha yetu, kanuni zake hutupatia viwango vya
kujiendesha katika hali hizo ambapo hamna maelekezo ya wazi.

Kwa mfano, Biblia haisemi chochote kwa wazi kuhusu


matumizi ya dawa za kulevya, lakini kulingana na kanuni sisi
hujifunza kwa njia ya maandiko, tunaweza kujua kwamba ni
makosa. Kwani Biblia inatuambia kwamba mwili ni hekalu la
Roho Mtakatifu na kwamba tunapaswa kumheshimu Mungu nao
(1 Wakorintho 6:19-20).

Tunahitaji kujua wazi kwamba neno la Mungu halitoi kila


hali ambayo sisi tunakumbana nayo katika maisha yetu, Katika
mambo mengi, tunaweza tu kuona ni nini Biblia inasema na
kufuata mwendo sahihi kwa kuzingatia kanuni hizo. Katika
maswali ya kimaadili ambapo maandiko hayatoi mwelekeo wa
wazi, sisi tunapaswa kuangalia kanuni ambayo inaweza kutumika
katika hali hiyo. Tunapaswa kuomba juu ya neno lake, na
kujiachilia sisi wenyewe kwa Roho wake. Roho atatufundisha na
kutuongoza katika Biblia kupata kanuni ambazo sisi tunahitaji
kusimama kwayo ili tuweze kuishi kama iwapasavyo Wakristo.

Maadili binafsi
Haya ni maadili yanayohusu mtu binafsi kwa kile ambacho
anatakiwa kukifanya katika jamii. Inahusu hasa na namna mtu
anavyotakiwa kufanya kwa upande wake yeye kama yeye.

Maadili ya kijamii
Maadili haya yanahusu mwenendo mzima katika jamii.
Katika nchi kama Tanzania mara nyingi mkazo uko katika maadili
ya kijamii kuliko maadili ya kibinafsi. Katika kufunza maadili

7
tunahitaji pia kujua maana ya maneno haya ili ya yatusaidie kujua
zaidi mila na desturi za jamii husika. Mara nyingi jamii zetu
zinaongozwa na maadili ambayo yametawala kama mila na
desturi. Lakini swali la kujiuliza, je mila na desturi hizo ni nzuri?
Tusichanganye maana ya maadili na mila na desturi.

Tamaduni/Utamaduni : Ni desturi fulani za maisha zilizozoelewa


au mila au ustaarabu.

Desturi ni kawaida ambazo jamii fulani inaona kuwa ni za lazima


au ni jambo la kawaida litendwalo na watu kila siku au ni ile hali
ya mazoea. Desturi zinaweza kuwa nzuri au mbaya ili mradi watu
wamezoea hivyo!

Mila ni mambo yanayofanywa kulingana na chanzo na mazoea ya


jamii asili.

Mila na desturi mara nyingi sana zinapingana na maadili ya


kikristo. Wakati mwingine watu unaweza kuwauliza kwa nini
mnafanya hivi? Jibu watakalokwambia ni kwamba kwa sababu
tumekuta wazazi wetu wakifanya hivi, yaani mazoea! Mara nyingi
mazoea yanaenda kinyume na mwenendo wa kikristo. Wakristo
wanaongozwa na neno la Mungu. Lakini hata katika neno la
Mungu wakati mwingine watu wanapofasili tofauti baadhi ya
vifungu vya Biblia wanaibuka na maana mpya na kupelekea kuwa
na maadili tofauti tofauti ya kikristo. Kwa hiyo tunahitaji kujua
maana halisi katika kufasili baadhi ya vifungu vya kibiblia ili
tuweze kufuata kile ambacho Neno la Mungu limeagiza kuhusu
maisha yetu kwa ujumla.

8
Kila jamii ina maadili yake lakini maadili ya kikristo ya
pote! Si kwa watu wa sehemu fulani tu. Kwa mfano hapa
Tanzania tuna makabila zaidi ya 125 lakini ukiangalia kila kabila
lina maadili yake fulani ambayo yanaambatana na mila na desturi
(ndani yake kuna miiko kadha wa kadha) ndani yake lakini
maadili ya kikristo yanahitaji kutumika katika hali zote katika
makabila haya.

Tunahitaji pia kujua kwamba Biblia kama mwongozo wetu


iliandikwa katika utamaduni wa watu fulani, hata hivyo yapo
mambo ya kitamaduni na mambo ambayo Biblia imekaza kama
mwongozo kwa kanisa. Jambo fulani inaweza kuliona jamii totauti
na jinsi Biblia inavyolijadili. Kwa mfano suala la kuacha
mke/mume katika jamii nyingi za kiulimwengu ni jambo la
kawaida kabisa lakini Biblia inalijadili kwa upana zaidi.

Chanzo cha Maadili ya Kikristo


Maadili ya kikristo chanzo chake kikuu Biblia. Biblia ndiyo
kiongozi mkuu katika maadili ya kikristo. Jamii inaweza kuliona
jambo fulani kuwa ni zuri lakini Biblia ikaliona kuwa ni baya. Kwa
mfano suala la kuwa na Boy/Girl Friend na mkawa mnashiriki
kimwili ni suala la kawaida kabisa katika jamii yetu kwa leo lakini
jambo hili kibilia linahesabika kama uasherati! Nadhani katika
jambo hili hakuna mjadala sana kwa sababu hakuna andiko lolote
linashadidia dai kama hilo katika maandiko. Kwa hiyo tunahitaji
kujua Biblia inasema nini hasa katika jambo fulani kuliko
kuangalia jamii inasema nini.

Chanzo cha maadili yote ni Mungu mwenyewe. Kwa hiyo


Mungu ndiye chanzo kikubwa cha maadili. Mungu ameyafunua

9
maadili hayo kupitia ufunuo wake. Tunajua wazi kwamba Mungu
amejifunua kwa mwanadamu kwa namna mbili; ufunuo wa
kawaida/ujumla na ufunuo maalum.

Ufunuo wa Kawaida
Ufunuo wa kawaida ni ule ufunuo ambapo Mungu
amejifunua mwenyewe kupitia asili, historia na dhamira za watu.
Zab. 19:1 inasema Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, na anga
laitangaza kazi ya mikono yake. Soma pia maandiko haya. Zaburi
147:8-9, Mdo 14:15-17, Rum 2:14-15, Rum 1:21. Nadhani baada ya
kusoma mafungu haya umepata kitu pale kwamba Mungu
amejifunua kwa watu kwa namna ya jinsi alivyoumba vitu vyote
duniani na kwa dhamira ndani ya kila mtu. Ni dhahiri kwamba
kila mtu anao ufahamu wa ndani kuhusu Mungu. Hakuna mtu
anayeweza kusema kwamba hakumjua Mungu kwa sababu
Mungu ameweka ufahamu wake ndani yako.

Ufunuo maalum
Mungu amejifunua katika ufunuo huu kwa njia ya Neno.
Kwa nini ni ufunuo maalum ? Kwa sababu ni njia ya pekee kabisa
ambayo Mungu ameitumia ili kujifunua kwa wanadamu, yaani
njia hii inaonyesha suluhisho la dhambi za mwanadamu kwa
kumtuma Yesu KRISTO kama Neno la Mungu halisi yaani lililo
hai na kuwa kuwa mwili (Yn 1:14) “Neno akafanyika mwili,
akakaa kwetu” Ufunuo wa Mungu kwa njia ya Neno
umegawanyika katika aina mbili:

Neno lililo hai


Neno lililo hai ni Yesu KRISTO mwenyewe aliyekuja kwa jinsi
ya Mwili huku akiwa Neno halisi yaani akiwa Mungu. Yohana

10
1:1,14. “hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako
kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu…naye Neno akafanyika
mwili akakaa kwetu”

1.1.Neno kama Biblia. Maandiko yote yameandikwa kwa msaada


wa Roho Mtakatifu (2Petro1:20-21) yaani wanadamu
waliandika yaliyotoka kwa Mungu wakiongozwa na Roho
Mtakatifu (2Tim 3:16).

Katika kutafuta maarifa katika neno la Mungu tunahitaji


kusoma kwa makini, kwa kuzingatia kanuni za kisarufi na
tafsiri ya neno la Mungu kwa wakati huo na wakati wa leo.
Inashauriwa unaporejelea Biblia uwe na usuli wa Biblia nzima.
Huwezi kupata usuli huo bila ya kusoma Biblia nzima.
Inashauriwa kusoma Biblia yote ili kujua jambo fulani katika
maandiko. Kwa mfano ukisoma katika Agano la Kale peke
yake unaweza kujikuta ukakubaliana na hoja kwamba kuoa
wake wengi ni sawa kwa sababu Biblia inasema hivyo jambo
ambalo linatakiwa liangaliwe katika Biblia nzima. Kwa hiyo
kuwa makini kusoma fungu au mstari mmoja katika Biblia na
kutoa mahitimisho yake kwa haraka haraka. Hitimisho lolote
lile linalohusiana na masuala ya kimaadili lazima yafikiwe
kama tu Neno la Mungu limeshadidia suala hilo katika
mawanda yake.

Kila unaposoma neno la Mungu lazima ukusudie kulitii na


wala sio kwa kufuata mawazo yako. Watu wengi sana hufuata
mawazo yao badala ya neno la Mungu. Biblia katika Zaburi
119:11 inasema Moyoni mwako nimeliweka Neno lako nisije
nikakutenda dhambi. Kwenda kinyume na kile ambacho neno la

11
Mungu linasema inaweza kusababisha wewe kutenda dhambi
hivyo unapolisoma uwe na lengo la kutii na kukubali matokeo
yoyote yale yatakayotokea.

Hata hivyo katika kutatua masuala ya kimaadili tunahitaji


kuwa makini zaidi. Kwa mfano katika maadili ya kikristo
kutoa mimba ni kitendo kiovu ambacho ni dhambi kwa mtoaji
lakini je itakuwaje kama ujauzito huo ukiendelea kuwepo
tumboni mwa mama inaweza kupelekea kifo chake? Je atoe
mimba ili kutunza mama au mama afe na mtoto abaki? Haya
ni baadhi tu ya mambo ambayo yanahitaji kujadiliwa kwa
makini sana kabla ya kutolewa maamzi sahihi huku maadili ya
kikristo yakizingatiwa.

12
CHANGAMOTO ZA KIMAADILI ZINAZOKABILI UKRISTO
SIKU HIZI
Kuna changamoto za kimaadili nyingi sana ambazo katika
kitabu hiki hatuwezi kuzijadili kila moja. Ni kweli kwamba katika
Ukristo kila siku changamoto mpya inazaliwa/inajitokeza. Sasa ni
vigumu sana kushughulikia changamoto hizi kwa muda wa siku
nne na hata kama tungepata muda wa kutosha si rahisi sana
kuzimaliza.

Nadhani watu wanaoshughulika na masuala ya ushauri


wanajua ni mambo gani wanapambana nayo kila siku. Unaweza
kushangaa kila siku watu wanakuja kupokea ushauri lakini kila
mtu ana hoja yake ya pekee kabisa. Hivyo basi kwa minajili ya
kozi ya Biblia nimechagua baadhi ya changamoto tu. Zifuatazo ni
changamoto za kimaadili kwa kanisa la leo

Masuala ya Siasa
Hatuwezi kujua zaidi kuhusu masuala ya siasa bila kujua
kuhusu serikali. Serikali ni watu waliochanguliwa kwa ajili ya
kuwaongoza watu wengine. Kunhiyop (khj) 4 anafafanua kuwa
kazi kubwa ya serikali ni kuwaadhibu wale ambao wanavunja
sheria za nchi fulani. Sheria hizo zinakuwa zimeandaliwa kwa ajili
ya kuwaongoza watu wa makundi yote katika nchi. Yaani hakuna
cha dini fulani bali watu wa dini zote huunganishwa na kuwa
wamoja kwa kutii sheria moja. Serikali imetawaliwa na wanasiasa.

4
Khj-kirefu chake ni kama hapo juu au keshatajwa

13
Wanasiasa ndio wanaoshika nchi kwa sasa, bila siasa hakuna
serikali. Sasa kanisa linajikuta likiwa katikati ya siasa na
kushindwa cha kufanya.

Kanisa na siasa
Kanisa wakati mwingine limekuwa katika changamoto
katika siasa. Baadhi ya marais wamekuwa wakitangaza hadharani
upande wa dini wanaoushadidia. Katika historia kwa mfano,
mwaka 1991 raisi wa Zambia Fredrick Chiluba alitangaza kuwa
Zambia ni taifa la Kikristo. 5 Huku akitubu kwa ajili ya uovu
ambao umewahi kufanywa na watu wa taifa la Zambia. Mfano
mwingine ni raisi wa Nigeria, Obasanjo alidai kuokoka baada ya
kufungwa kwa makosa ya kijeshi. Katika kipindi cha uchaguzi
alitangaza kwamba yeye atakuwa raisi wa Kikristo jambo ambalo
lilisababisha wakristo wengi kumpigia kura.

Inawezekana kabisa mchungaji ukawa na kanisa halafu


ukaingia katika siasa? Je kanisa linaweza kutoa mwongozo wa
jinsi ya kuchagua kiongozi anayefaa katika serikali? Nakumbuka
Mwaka 2010 kanisa Katoliki liliandika waraka kwa washirika
wake kuonyesha aina gani ya kiongozi aweze kuchaguliwa. Je
ilikuwa sahihi? Haya ni baadhi ya maswali ya msingi
tunapoendelea kujadili suala la siasa katika maadili ya kikristo.

Katika maandiko serikali imeelezwa katika mazingira


kadha wa kadha. Ukianzia katika agano la Kale wakati wa
utawala wa Wafalme inadhihilisha wazi kwamba Mungu alikubali
tawala za wanadamu katika mazingira hayo.

5
Paul Freston (2001). Evangelicals and Politics in Asia, Africa and Latin America.
Cambridge: Cambridge University press, Uk 158

14
Kuna makundi mawili yanayozungumzia ujihusishaji wa
kanisa katika siasa. Kuna kundi la kwanza linadai kuwa ni kanisa
linapaswa kujihusisha kikamilifu katika siasa na wale wanaokataa
kwamba kanisa halipaswi kujihusisha na siasa.

Hoja za Waonaataa Kujihusisha na Siasa


Wale wanaoshadidia upande huu wanadai kuwa kanisa
limetengwa kabisa na Yesu Kristo na hivyo lenyewe si la
ulimwengu huu. Katika Yohana 17:16 “ninyi si wa ulimwengu
huu.” Warumi 12:2 inasema “wala msiifuatishe namna ya dunia
hii bali mgeuzwe upya nia zenu mpate kujua hakika yaliyo
mapenzi ya Mungu yaliyo mema ya kumpendeza na ukamilifu.”
Pia katika 2Kor 6:17 inasema “tokeni kati yao mkatengwe nao
asema Bwana.” Kulingana na maandiko haya wanaoshadidia
upande huu wanadai kuwa kanisa haliwezi kujihusisha na
mambo ya siasa wala watumishi wake kuhusika katika siasa kwa
sababu wao ni watu tofauti katika ulimwengu huu.

Hoja kwa Wale Wanaokubali Kujihusisha na Siasa.


Wanaoshadidia upande huu wanadai kuwa kila mkristo
lazima awe hai katika mambo ya kiulimwengu. Wanadai kuwa
kanisa haliwezi kukaa nje ya ulimwengu kwa sababu linahitaji
kuonyesha upendo wa Mungu kwa watu wa ulimwengu.
Wanadai kuwa bila kanisa kujihusisha na siasa na pamoja na
serikali wakristo hawawezi kuishawishi jamii kubadilika.kwa
mfano katika Biblia akina Mordekai na Danieli waliweza
kubadilisha serikali zikawa za kumtii Mungu. Kwa upande
mwingine wanakaza kwamba kanisa halingii kichwa kichwa tu

15
katika siasa bali linahusika na mambo ya siasa kwa namna
ifuatayo: -

i. Kuombea serikali na watu wake kwa ujumla


ii. Kuikosoa serikali kama inaenda kinyume na maadili
yanayotakikana
iii. Kushirikiana na serikali katika kuondoa maovu katika nchi

Kambi hii pia ina misingi mingine kutoka katika maandiko ikidai
kwamba:

i. Serikali inaanzia kwa Mungu Mwenyewe. Rom 13:1


ii. Serikali hufanya kazi kwa niaba ya Mungu. Rom 13:4
iii. Serikali ipo kwa ajili ya kuhamasisha mazuri kufanyika.
Rum. 13:4-5.

Kwa minajili ya kozi hii nakubaliana na kambi pili kwamba


kanisa linaweza kujihusisha na siasa. Kanisa lijihusisha katika
siasa ili kupata nafasi katika masuala ya kiuchumi, kijamii na
kiafya. Kama kanisa likipata nafasi kama hizo ndani ya kanisa basi
ufalme wa Mungu hapa duniani utaendelea kuinuliwa zaidi na
zaidi.

Maswali la mjadala:
1. Je mchungaji anaweza kugombea uongozi katika siasa, kwa
mfano ubunge huku akiendelea kuongoza kanisa? Kubali au kataa
kwa hoja kuntu.
2. Tunawezaje kukemea viongozi wanaofanya maovu zaidi katika
nchi zetu zinazoendelea? Je unaweza kumkabili raisi kama
amefanya ubaya?

16
3. Kama tukikubaliana kwamba serikali zote zinatoka kwa
Mungu, je unasema nini kuhusu serikali za kijeshi ambazo wakati
mwingine huua umati wa raia wasio na lawama?
4. Msimamo wako ni upi kuhusu kanisa na siasa? (hakikisha
unatumia maandiko)

VITA NA MAASI
Suala la vita na maasi linahitaji mjadala mkubwa sana. Kuna watu
wengine wanaodai kwamba mkristo haruhusiwi kujihusisha na
vita vya aina yoyote ile isipokuwa vita vya kiroho tu. Lakini
wengine wanadai kwamba wakristo wanaweza kwenda kwenye
vita ili kusaidia kukomboa katika vita.

Vita katika agano la kale


1.1.1.1.Waisrael waliagizwa kuwafukuza Wakanaani kwa vita (
Hes. 33:50-56)
1.1.1.2. Mfalme Sauli aliagizwa kuwaua Waamaleki kwa vita
(Isam.15:2-3)
1.1.1.3. Mungu ni mtu wa vita nk

Vita katika agano jipya


1.1.1.4.Kununua panga. Luka 22:36-38
1.1.1.5.Ufalme wa Yesu sio wa dunia hii ( Yoh. 18:36)

Kanuni za kutumia kunapotokea vita kati ya wakristo na wasio


wakristo
1.1.2. kutafuta suluhu kila inapowezekana. Math 26:52
1.1.3. kuhamasisha haki duniani

17
1.1.4. Kuondoa ukabila ndani ya kanisa (Gal 3:28)
1.1.5. Upendo na msamha kwa maadui

Swali la mjadala
Je mkristo anaweza kwenda katika vita? Kama anaweza
kwenda ni kwa namna gani anaweza akatunza amri
inayosema usiue? Jadili kwa hoja maridhawa.

MASUALA YA KIUCHUMI
Uchumi ni kipengele kingine muhimu katika kanisa la leo. Kuna
mambo mengi yanayohusiana na masuala ya kiuchumi ambayo
yaliyo mengi yanahitaji mwongozo wa kimaadili. Yafutayo ni
baadhi ya mambo hayo: -
Umaskini
Suala la umasikini katika jamii nyingi za kiafrika ni suala
tete. Watu wengi wengi wanahangaika kwa sababu ya maisha
magumu. Wakati mwingine wanakosa hata mavazi, malazi na
hata chakula. Lakini je ni mapenzi ya Mungu watu kuwa maskini
? Nafikiri sio mapenzi ya Mungu bali ni matokeo ya dhambi, na
kwa sababu hiyo Mungu aliamua kuweka utaratibu wa namna ya
kutoka katika hali ya umasikini. Wakati Mungu alipomuumba
mwanadamu alikusudia aishi maisha tele lakini anguko
limesababisha matatizo makubwa sana katika jamii zetu. Lakini
swali la msingi, je kwa nini nchi nyingi za kiafrika ni maskini sana
kuliko za Ulaya ? Je madhara ya anguko yako kwetu tu? Kwa nini
hali ya maisha ni tofauti kiasi hicho ? Je matajiri wamewaibia
maskini mali zao? Je nini maadili ya kikristo katika jambo hili?

18
Je Mungu amepanga umaskini kwa watumishi wake? kwa nini
tunahangaika na umaskini? jadili

Rushwa
Siku hizi watu hujaribu kupunguza ukali wa neno ‘rushwa’
‘hongo’ kwa kusema; zawadi, hongera, maji, chai nk. Watu wengi
hutoa na kupokea rushwa kwa namna tofauti tofauti. Wengine
hudai ni shukrani tu, wengine hudai ni mshahara kwa kazi yangu
na wengine hudai ni haki yangu kupokea rushwa. Ili rushwa iitwe
rushwa mazingira ya utoaji wake yanahitaji yaangaliwe. Kazi ya
rushwa ni kununua haki
Biblia imekataza kupokea rushwa ya aina yoyote ile na kwa
mazingira yoyote yale. (soma mafungu haya Kumb. 10:16-18,
2Nyak 19:7, Mhub. 7:7, Zab 62:10) nk
Swali la mjadala: 1. Je unakubaliana na msemo kwamba
“rushwa haiepukiki katika jamii yetu?”
Tuchukulie unaendesha gari, unasimamishwa na trafiki na gari
lako linaonekana lina kosa dogo tu la rangi kuchubuka. Na
asikari anakuomba faini ya shilingi 30.000/= hapo hapo
anakwambia ‘hebu naomba unipe ya maji nikuache uende na
safari zako, leta 2000/- ‘je utakubali kumpa? Kama utakubali
toa hoja madhubuti na kama hautakubali toa hoja kuntu.

Harambee
Harambee au kwa lugha nyingine ‘changizo’ ina asili yake.
Jamii nyingi za kiafrika zina utamaduni wa kusaidiana kwa
pamoja kama kazi inahitaji watu wengi. Hiyo nayo tunaweza
kusema kuwa ni aina fulani ya harambee. Kila kabila lina aina

19
yake ya kufanya harambee; kwa mfano katika jamii ya wasukuma
kuna maneno maalum yanayotumika kuelezea harambee ya aina
hiyo kwa mfano ‘lubili’ ‘buyobe’ ‘ikhuma lya busiga’ nk. Kwa
Wakulya wanasema’irika.’ Kwa hiyo suala la harambee si suala
geni katika jamii nyingi za kiafrika. Watanzania wana msemo
‘umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu’
Changizo au kufanya kitu katika hali ya umoja ni jambo la
kawaida katika ukristo. Katika biblia kuna sehemu nyingi ambapo
changizo liliweza kufanyika kwa ajili ya kuinua huduma fulani
iendelee kwa nguvu.
a) Musa alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa hema. Kut.
20-34
b) Mfalme Daudi alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa
hekalu. INyak. 28:12, 19. 29:2-9
c) Nehemia alifanya harambee kwa ajili ya kurekebisha mji
wa Yerusalemu. Neh. 1:4-11, 2:1-18; 3:1-5 nk (au soma
kitabu chote cha Nehemia)
d) Ezra alifanya harambee kwa ajili ya ujenzi wa hekalu. Ezra
2:68-69
e) Hagai naye katika huduma yake alifundisha watu kujitoa
kwa ajili ya kazi ya Mungu. Hag. 1:1-14
f) Yesu pia alihudumiwa katika huduma yake na wanawake
kadha wa kadha. Luka 8:1-3
g) Mitume nao walihitaji fedha kwa ajili ya kuendeleza
huduma yao. Mdo. 4:32-5:11
h) Mtume Paul alifanya changizo kwa ajili ya huduma. I Kor
16:1-3, 2Kor 8:1-24
Swali la msingi ni kwamba kwa nini suala hili liko katika maadili ya
kikristo?

20
Kwa kuwa ni muhimu katika huduma ya BWANA kuwa na
changizo la watu wengi, au mtu mmoja/supporter, au kanisa
maalumu linaweza kukusapoti lakini bado kuna mambo ya
kimaadili ambayo yanahitaji kuzingatiwa katika upataji wa
huduma hizo. Mambo yafuatayo yanahitaji kuangaliwa kwa
makini sana katika huduma
Kuomba Msaada kwa Wasio Wakristo
Swali ambalo mara nyingi tunapaswa kujiuliza ni je tunaweza
kwenda kuomba msaada wa kifedha labda kwa ajili ya kujenga
kanisa kwa watu wasio waamini? Je mtu ambaye pengine tunajua
wazi kwamba labda amepata fedha kwa njia ya rushwa/au jambo
lolote lile baya, je tunaweza kuzipokea fedha kama hizo? Je
tunaweza kuwaendea Waislamu matajiri na kuwaomba
wachangie huduma zetu?
Maswali haya yote yanahitaji uchunguzi wa hali ya juu
sana. Wengi wanaoshadidia upande wa kwamba inawezekana
kuchukua fedha kwa wasio waamini wanadai kwamba fedha
walizo nazo watu sio za kwao. Wanatoa mfano wa Ezra na
Nehemia waliopokea msaada wa mfalme wa Babel ambaye
alikuwa mwabudu miungu. Hili ndilo suala la kimaadili katika
harambee!
Kutangaza fedha zilizotolewa katika harambee au kama ni
msaada wa mtu.
Hii inatokea hasa kama katika changizo umeita MC anayejulikana
kabisa. Anahamasisha watu na watu wanatoa fedha nyingi. Je
fedha hizo zitangazwe?

21
Mhubiri kuomba fedha ili aje kufanya kwenye mkutano
Hili nalo siku hizi linasumbua sana jamii za Kikristo. Watumishi
mbalimbali wanaomba fedha kabla ya kufika katika mkutano wa
Injili. Waimbaji wengi wa injili siku hizi bila kuweka chochote
kwenye akaunti yake hawezi kwenda kwenye mkutano wa Injili.
Je hayo ni maadili ya Kikristo. Je ni maadili ya kikristo kutoa
namba zako za akaunti za benki kwa umati wa watu? Je ni sawa
kwa mtu akitaka kuombewa atoe kwanza fedha kwa ajili ya
huduma hiyo? Haya ni baadhi ya maswali ya msingi ambayo
tunahitaji kujiuliza na kuyatolea majibu sahihi.
Watumishi wa Mungu tunahitaji kuwa makini katika
masuala haya ya kimaadili. Lakini kwa ujumla tunaweza kusema
kwamba, mambo yafuatayo katika masuala ya kifedha katika
huduma yanapaswa yafuatwe: -
Angalia nia ya mtoaji ni ipi? Kama ni ya kisiasa zaidi au
anataka kumteka mchungaji/mwinjilisti au anataka kupata sifa
fulani ndani ya kanisa hilo? Usipokee fedha ovyo ovyo maana ni
hatari sana!
Kwa wewe unayepokea lazima uwe mwaminifu na
muwazi. Kama umepewa fedha kwa ajili ya kujenga kanisa
unapaswa kujenga kanisa tu. Kuna wachungaji wengi
wakishapata misaada ya aina hiyo tayari wanaibadilishia
matumizi, wananunua magari nk. Jambo hili ni hatari sana.
Kuwepo na mrejesho kwa kile ulichotumia. Ni vizuri zaidi
kuelezea vizuri kile ambacho umetumia. Ikiwezekana andika kila
kitu, itakusaidia sana maana kuna wafadhili wengine wanataka
kujua kila kitu.
Baada ya kuangalia mambo ambayo ni ya muhimu; epuka mambo
yafuatayo: -

22
• Epuka kupotosha ukweli. Kama una mradi utagharimu
shilingi laki tano sema laki tano.
• Epuka kuwashawishi watu kutoa hata pale wasipotaka
kutoa. Kuna watu makanisani wanatoa vitu huku
wakinugh’nuka mioyoni mwao
• Epuka kuwa ombaomba/ Mungu hasemi kwamba tuombe
kwa watu.

MASUALA YA FAMILIA NA NDOA


Suala la familia na ndoa ni suala ambao linahitaji kujadiliwa kwa
undani zaidi. Ndoa ni taasisi pekee ambayo Mungu huitumia
kuendeleza uumbaji wake hapa duniani. Lakini wakati mwingine
ndoa hizi hizi zinakuwa na changamoto nyingi ambazo
zinapelekea mambo fulani fulani ambayo sio mazuri kutokea
katika maisha ya kila siku. Katika sehemu ya familia na ndoa
tutaangalia masuala ya utasa, mitara, talaka na mahusiano.
Utasa/Ugumba
Utasa katika nchi nyingi za kiafrika ni suala mtambuka. Kwa
maana ya kwamba waafrika wanaamini kwamba watoto ndio
urithi wa pekee kabisa. Sasa inapotokea kwamba kuna tatizo la
utasa mambo haya yanakuwa ni shida kubwa. Watu wengi
wametoa talaka kwa sababu ya kutokupata watoto kwa wake zao
wa kwanza. Watu wengi wanaamini kwamba ndoa bila kuwa na
mtoto bado haijawa ndoa sahihi bali ni ndoa nusu. Tunahitaji
kujifunza na kujua mapenzi ya Mungu nini katika maisha ya ndoa
zetu. Kama tukikaza kwamba lazima tuwe na watoto je
inapotokea hakuna watoto inakuwa ni laana au? Watu wengi

23
wanatembea usiku na mchana kwenda kwa waganga wa kienyeji
kwa ajili ya kutafuta watoto. Lazima tuwe makini katika jambo
hili. Kuna wachungaji wengi ambao wamejikita katika huduma ya
kuombea tu watu wasio na watoto huku wakikaza kwamba mtu
asiyekuwa na watoto ana laana kutoka kwa Mungu na yeye
anaondoa laana hizo.

Chanzo cha utasa/ ugumba


Kabla ya kwenda mbali zaidi hebu tuangalie maana ya utasa na
ugumba. Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu (2004:398)6
tasa ni “kiumbe chochote cha kike kisichoweza kuzaa” kwa hiyo
tunapozungumzia tasa tunamaanisha mwanamke asiyeweza
kuzaa. Neno ‘mgumba7’ maana yake ni “mtu aliyefikia umri wa
kuzaa lakini akawa hajazaa wala kupata au kutia mimba” kwa
hiyo neno ugumba ni kwa watu wote. Sasa tuangalie kwa ufupi
sababu za kuwa mgumba kwa:-

Kwa wanaume
• Uhanithi-huyu ni mwanaume asiyekuwa na nguvu za
kiume kabisa, yaani ni dhaifu. Uume wake hauwezi
kusimama sawasawa na hivyo hawezi kufanya mapenzi na
mke wake. tatizo hili husababishwa na masuala ya
kiafya,kwa mfano kupiga punyeto kwa muda mrefu na
hata masuala ya kisaikolojia. Kama mtu akiwa na tatizo hili
tunawashauri kwenda kupima hospital ili kubaini chanzo
cha tatizo.

6
TUKI (2004). kamusi ya Kiswahili sanifu. Nairobi: Oxford
7
khj

24
Swali: wewe kama mchungaji ukiletewa suala la mtu ni
kuwa hanithi utafanyaje ili uweze kunusuru ndoa yao?
Utawashauri vipi?
• Tatizo katika kutoa mbegu- wanaume wengine hawawezi
kuwapa wake zao uja uzito kwa sababu shahawa/mbezi
zao haziwezi kufikia yai la mtoto. Yaani katika kutoa
mbegu/shahawa hazina spidi ya kufikia yai.
• Kukosekana kwa mbegu katika shahawa-wanaume
wengine hawana mbegu katika shahawa zao. Wanamwaga
shahawa kama kawaida lakini hazina mbegu. Hili nalo ni
tatizo kubwa.
• Kuharibika kwa mbegu za kiume-wakati mwingine mbegu
za kiume zinaharibika na kufa kabisa. Wanaume wengi
wanaopenda kuvaa chupi zinazowabana hupatwa na tatizo
hili mapema sana. Maana kwa kawaida mbegu haziwezi
kukaa katika joto kali.
• Matatizo ya kiroho, wakati mwingine masuala ya kiroho
yanaweza kusababisha kuwa mgumba mwanaume
tafuta sababu za kiroho za ugumba katika maandiko matakatifu
kisha yaelezee kwa undani na chanzo cha matatizo hayo.
Kwa wanawake
Wanawake wengi wanakuwa matasa kwa sababu zifuatazo
• Tatizo la homoni za uzazi
• Tatizo la tumbo la uzazi/hakuna kizazi
• Maambukizi katika uke
• Chango la kike
• Tatizo kiroho

25
Namna ya kushughulikia ugumba/utasa
Kila kundi la watu lina namna yake ya kutatua tatizo hili
kubwa katika jamii. Jamii nyingi zisizoamini hukimbilia
kwa waganga wa kienyeji na kujikuta wanagawa ngono
kwa kudanganywa ili wapate watoto. Wanaume wengine
wanaambiwa mashariti magumu. Kwa mfano jamaa mmoja
alienda kwa mganga wa kienyeji akaambiwa kwamba alale
na mama yake mzazi ndipo kizazi cha mke wake
kitafunguka. Kwa ushauri wangu ni bora:-
• Kumwomba Mungu sana na kutambua nini hasa kusudi la
ndoa katika maisha yenu.
• Kwenda kuwaona wataalamu wa afya ili waone suala hili
kitabibu zaidi. Na kama hakuna tatizo la kitabibu basi ni
vizuri kusubiri mpango wa Mungu
• Kujifunza namna ya kujua siku ambazo mwanamke
anaweza kuchukua mimba au la
• Kujua kusudi la Mungu katika uumbaji. Kila kitu
kinachokuja duniani kinakuwa na kusudi la Mungu katika
maisha ya mwanadamu. Kwa mtu aliyeokoka si jambo la
kulazimisha upate mtoto wakati Mungu hajaamua kufanya
hivyo. Usije ukachanganyikiwa na kuanza kukimbilia
maombezi kila kukicha

Mitara (ndoa za wake wengi

Waafrika wengi hawaoni kwamba ni jambo geni kuingia katika


ndoa za mitara. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mwanaume
wa kiafrika anaweza kuoa mwanamke mwingine wakati wowote
ule bila shida. Hili nalo ni tatizo kwa wakristo wengi. Nakumbuka

26
kanisa moja niliwahi kusali nilipokuwa kijana mdogo lililoitwa
Last Church/Batola mhali (kwa kisukuma) lilikuwa linahalalisha
kabisa kuoa wake zaidi ya mmoja. Mwinjilisti kanisa hilo alikuwa
na wake wawili Ada na Sila. Kuna siku waligombana sana hao
wake zake na kubebeana mapanga na hapo hapo ndipo kikawa
chanzo cha familia yetu kuhama kanisa hilo!!
Mpango wa Mungu haikuwa kwamba mwanadamu aweze kuoa
wake wengi, kwani alipomuumba Adamu alimwomba na Hawa
nao walikuwa wawili tu. Hata hivyo kwa sababu ya anguko la
mwanadamu, kwa sababu ya dhambi mwanadamu alijitwalia
wake zaidi kwa kadri alivyotaka. Hebu tuangalie ndoa za mitara
katika biblia na madhara yake.

Ndoa ya Lameki Mwanzo 4:19-25


Huyu ndiye mtu wa kwanza kabisa kujitwalia wake wawili.
Ukisoma mistari hiyo utaona kwamba huyu jamaa alikuwa roho
ya kisasi kama ya Kaini. Kwa hiyo moja kwa moja makosa yake
yanaelekezwa kwa uasi aliokuwa nao. Matokeo yake yeye
mwenyewe anakiri kwamba anaweza kulipizwa kisasi na Mungu.
Hapa tunaona kwamba madhara yake ilikuwa kwenda kinyume
na Mungu.ukoo wa Kaini mara nyingi imeonekana katika
maandiko kwamba ni ukoo wa kigaidi uliokataa kwenda katika
sheria ya Mungu.

Ndoa ya Ibrahimu Mwanzo 16-17 na 28-30


Ni dhahiri kwamba Ibrahimu alizaliwa katika familia yenye
kushika msimamo wa ndoa za wake wengi(20:12). Katika ndoa
yao Ibrahimu alichelewa sana kupata mtoto wa ahadi, lakini mke

27
wake Sarah,kwa sababu tayari ndani yake yalikuwepo mawazo ya
kuwa na wake wengi kwa mume wake,alimshauri amchukue
Hajiri. Hapa ndipo chanzo cha matatizo ya ndoa hii.

Katika agano jipya hakuna mahali popote ambapo tunakuta kuna


mtu alikuwa na wake zaidi ya mmoja. Lakini tukiangalia
maandiko inaonekana kwamba kuna waliokuwa na wake zaidi ya
mmoja. Hebu soma mafungu haya (I Kor 5:1-9) hapa tunaona
jamaa ambaye alikuwa ni mzinzi kiasi cha kulala na mke wa baba
yake, je wewe unadhani ni mama yake mzazi? Labda nafikiri
kwamba huyu baba yake alikuwa hawara/nyumba ndogo. Sio
hapo ukisoma katika I Tim 3:1ff utaona sifa za asikofu na shemasi
kwamba wawe waume wa mke mmoja. Hii inatudhihilishia
kwamba kulikupo na watu ndani ya kanisa wenye wake zaidi ya
mmoja.
Maandiko hakuna sehemu ambapo yameruhusu mwanaume kuoa
wake wengi au mwanamke aolewe na wanaume wengi,
kinachofanywa na binadamu ni ugumu wa mioyo yao. Wengine
katika kipindi hiki kwa sababu ya changamoto za ndoa wanaamua
kuwa na nyumba ndogo ili kunusuru maisha yao. Hii ni hatari
sana, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na neno la
Mungu.
Kwa kawaida hakuna mtu anayeweza kugawa upendo wake
katika sehemu mbili. Na ndiyo maana ndoa za wake wengi
zinakuwa na matatizo mengi sana. Unakuta wanawake hao
hawaelewani kila siku. Kuna mifano mingi katika agano la kale
ambayo inaonyesha madhara ya ndoa za mitara. Ushauri wangu
ni kwamba ni lazima tufundishe watu wafuate utaratibu wa
Mungu kwamba ndoa ni ya mke mmoja. Hakuna sababu ya kuoa

28
mke wa pili. Na kuoa mke wa pili ni kwenda kinyume na neno la
Mungu.

Swali: je kama kanisani kwako kuna waumini ambao kabla ya


kuokoka walikuwa na wake zaidi ya mmoja, utawashauri
wawaache au utafanyaje? Jadili kwa mapana huku ukizingatia
maadili ya kikiristo ni pamoja na hekima ya Roho Mtakatifu
kufanya kazi

Wewe kama mchungaji umeitwa kwenda kumbatiza mtu aliye na wak


utafanyaje?

Talaka
Suala la talaka ni suala nyeti sana katika kanisa. Watumishi wengi
wanahangaika kutatua masuala yanayohusiana na talaka. Katika
kipindi hiki suala la talaka ni jambo la kawaida miongoni mwa
wapendwa. Hasa kunapokuwa na tatizo ambalo wanandoa
wamekosana na jamii pamoja na kanisa inaliona wazi basi talaka
hutolewa.

Nini sababu ya talaka?


Kwa ujumla kuna sababu nyingi ambazo zinasababisha talaka
kutolewa. Nitajaribu kutaja baadhi ya hayo matatizo kama
ifuatavyo;-
• Kukosekana kwa watoto miongoni mwa wanandoa ni sababu
kwa Waafrika. Na hasa lawama zinapelekwa kwa wanawake

29
• Kusalitiana kimapenzi, yaani kama kuna mmoja anatoka nje
ya ndoa basi yule mwingine anaamua kuachana naye
• Kulazimishwa na wazazi wa upande mmoja kuachana kwa
sababu za kimila na kitamaduni
• Mmojawapo wa wanandoa hao kupatwa na magonjwa ya
kuambukizwa hasa UKIMWI
• Sababu za kiuchumi katika wanandoa. Wengine wanapooana
huonekana wakiwa na mali mara baada ya kuisha mali hizo
huachana mara moja
• Huko Ulaya wengine wanaona kwamba kama mtu
amemchoka mwenzake anaamua kuachana naye tu bila hata
sababu za msingi
• Ugomvi wa mara kwa mara ndani ya nyumba hupekea talaka
kwa wanandoa hao. Ugomvi huo unaweza kusababishwa na
tabia sugu za wanandoa hao kutokubadilika ili kuendana
pamoja.
• Matumizi ya mabavu ndani ya nyumba husababisha talaka
miongoni mwa wanandoa. Kwa mfano kwa waafrika walio
wengi kumpiga mwanamke ni jambo la kawaida sana, lakini
kuna wakati inafikia hali ngumu ndipo mwanamke huamua
kuondoka na kudai talaka. Ni mara chache kukuta familia
mwanaume anapigwa na mwanamke japo kuna familia za
namna hii nyingi.
• Kunyimana kitandani. Nazungumzia hapa ile hali ya
kumnyima mwenzi tendo la unyumba hupelekea talaka
miongoni mwa wanandoa. Hii inatokea pale ambapo
miongoni mwa wanandoa anatoa tendo la ndoa kama silaha

30
ya kumwadhibu mume/mke wake. jambo hili huvunja ndoa
nyingi kila siku.
• Wivu wa kimapenzi huvunja ndoa nyingi, unaweza kukuta
miongoni mwa wanandoa anakuwa na wivu kiasi kwamba
hataki kumwona mwenzi wake anaongea na mtu mwingine.
Mfano unakuta baba akimwona mke wake ana mtu mwingine
wa kiume basi moja kwa moja anasema kwamba huyu
anakutongoza na hivyo kudai talaka kwa haraka sana.
• Ndoa za mitara huvunja ndoa ya kwanza. Mara nyingine kwa
wapenzi ambao hawakukusudia kuwa ndoa yao itakuwa ya
wake wengi wakiona kwamba kuna mwanamke mwingine
ameletwa ndani mara moja hudai talaka.
• Ulevi wa kupindukia, hili mara nyingi linatokea hasa ikiwa
mmojawapo wa wanandoa hao akiwa mlevi kupindukia na
mwingine hana tabia za ulevi ikifikia hatua fulani mmoja
anachoka kumvumilia mwenzake kwa ajili ya ulevi wake basi
huamua kuvunja ndoa
• Maendeleo ya sayansi na teknolojia yanasababisha ndoa
nyingi kuvunjika. Kwa mfano matumizi mabaya ya simu
yanavunja ndoa za watu. Nakumbuka kijana mmoja alikosea
akatuma massage ya mapenzi katika simu ya mke wa mtu,
ujumbe huo ulileta mtafaruku ndani ya ndoa hiyo. Pia
matumizi ya mitandao ya kijamii kama vile facebook na
twitter yanasababisha kuvunjika ndoa. Pale ambapo mmoja
wa wanandoa anasahau ku-log out kama alikuwa ameingia
mtandaoni na mtu mwingine mbaya akiingia kwenye akaunti
yake na kuweka picha mbaya itampa shida kubwa sana.

31
• Watoto wa kambo huvunja baadhi ya ndoa za watu. Hii
inatokea pale ambao mmoja wa wanandoa hao alikuwa na
mtoto wakati wa kuolewa, watoto wa aina hiyo wakati
mwingine huleta matatizo makubwa ya kuchonganisha
wanandoa hao
Hizi ni sababu chache tu miongoni mwa sababu nyingi
zinazosababisha kuvunjika kwa ndoa. Na kumbuka kwamba kila
ndoa ina sababu yake ya pekee ambayo haifanani na nyingine
inayopelekea kuvunjika kwa ndoa hiyo.
Fungu la kwanza ambalo linazungumza juu ya talaka kwa mara
ya kwanza ni katika Kumbukumbu la Torati 24:1-5 mahali ambapo
tunaona kwamba Musa aliwaelekeza watu namna ambavyo
wanaweza kuwapa talaka wake zao. Lakini jambo hili Yesu
alisema kwamba sababu za Musa kuruhusu talaka ilikuwa ni
ugumu wa mioyo ya watu

Mitazamo Mbalimbali Kuhusu Talaka


• Kuna wanaosema hakuna kutoa talaka kabisa katika
maisha ya mwanadamu. Soma Warumi 7:2-3,I kor 7:39, Mal
2:16
• Kuna wanaosema kuwa ni ruksa kutoa talaka lakini usioe
tena. Hawa nao wanasimama na mafungu mbalimbali,
mfano. Math 19:9 wanafafanua kwa namna ya pekee sana
• Kuna wale wanakubali kwamba kama
mwanamke/mwanaume umemkamatisha kwenye uzinzi
unaachana naye mara moja. Nao wanasimama na fungu hili
la Math 19:9 na Kumb 24:1-5 wakifasiri neno OVU kuwa ni
uzinzi

32
Kila kundi la watu wana msimamo wao juu ya suala hili lakini
cha kuzingatia ni kwamba tunahitaji kumwomba Mungu
hekima ya pekee katika kujadili suala la talaka makanisani
huku tukijua mambo yafuatayo: -
• Ndoa ya kikristo imekusudiwa kuwa ni ya milele. Mal 2:16
• Kuna wakati inaweza kutokea talaka. Math 19:8
• Talaka ni hatari sana kwa wanandoa
• Hatuwezi kujumuisha moja kwa moja masuala ya talaka
lazima yaangaliwe kwa undani zaidi
• Kuna matumaini ya ziada baada ya talaka na kuoa tena, kwa
maana ya kwamba hilo si suluhisho la maisha ya
mwanadamu
• Kabla ya kufanya uamuzi wa haraka wa kuvunja ndoa yako,
fikiria. Mara nyingi talaka haimalizi mahangaiko ya maisha.
Badala yake, inatatua tatizo moja, na kutokeza lingine.
Katika kitabu chake, The Good Enough Teen, Dakt. Brad
Sachs anaonya hivi: “Wenzi wa ndoa wanaotalikiana
huwazia kwamba kufanya hivyo kutafaa kabisa, yaani,
talaka yao itawaondolea kabisa huzuni na ugomvi mkali, na
badala yake wapate utulivu mwanana. Lakini kutarajia hilo
ni sawa tu na kutarajia kuwa na ndoa kamilifu,
haiwezekani.” Hivyo, ni muhimu kuwa na habari kamili na
kuona talaka kihalisi.
• Talaka huweka majeraha yasiyokoma mpaka kaburini
Nini madhara ya talaka kwa maisha ya wanandoa?
• Huharibu afya ya kiroho
• Huharibu afya ya kimwili
• Kuchanganyikiwa miongoni mwa wanandoa

33
• Watoto kukosa malezi ya wazazi wote wawili
• Matatizo ya kifedha. Daniella, anayeishi Italia, alikuwa katika
ndoa kwa miaka 12 alipogundua kwamba mume wake
alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi
mwenzake. Daniella anasema hivi: “Nilipogundua jambo
hilo, mwanamke huyo alikuwa na mimba ya miezi sita.”
• Kuna matatizo ya kifedha. hebu ona mfamo huu baada
ya kutengana kwa muda, Daniella aliamua kumtaliki
mume wake. “Nilijaribu kuiokoa ndoa yangu,” anasema,
“lakini mume wangu hakuacha kuwa na uhusiano nje ya
ndoa.” Daniella anahisi kwamba alifanya uamuzi
unaofaa. Lakini anasema hivi: “Mara tu tulipotengana,
hali yangu ya kiuchumi ikawa mbaya. Nyakati nyingine
nilikosa hata mlo wa jioni. Nilikunywa tu maziwa.”8

Swali:1 je kama miongoni mwa washirika wako amepatikana na


ugonjwa wa UKIMWI ilhali mwenzi wake hana, utaamuaje suala la
kuzuia talaka isitolewe?
swali 2. Hebu tuchukulie kwamba umemkamata mume/mke wako ana
kwa ana (ready handed) akiwa katika kifua cha kahaba utavumilia
kuishi naye au utampa talaka?
Swali 3.wewe kama mwanadamu umewahi kufumaniwa? Ulimalizaje
mgogoro huo nyumbani kwako?

MATUMIZI YA VILEO

8
http://www.jw.org/sw/machapisho/magazeti/g201002/mambo-manne-kuhusu-
talaka/

34
Matumizi ya vileo ni jambo la kawaida kwa watu wengi, wakristo
na wasio wakristo. Ni jambo ambalo ni la muda mrefu hata kabla
ya histori ya binadamu kuanza kurekodiwa katika maandishi.
Kinaachofanya unywaji wa pombe/divai uwe ni wa kawaida ni
kwa namna ambavyo inatengenezwa. Pombe/divai nyingi
inatengenezwa kutokana na nafaka, kwa mfano mtama huweza
kutengeneza aina mbalimbali ya vileo. Kwa mfano kwa
wasukuma mtama huweza kutengeneza pombe iitwayo ‘gongo’
au ‘mapuya’ au ‘mataputapu’ nk. Pia nafaka za mahindi
hutengeneza pombe. Lakini zamani za siku hizi nimesikia
kwamba watu hutengeneza hata pombe kwa kutumia kinyesi cha
wanyama na wanadamu. Hii ni katika kuhakikisha kwamba
wanaongeza ukali katika vileo hivyo.
Maendeleo ya viwanda yamehamasisha unywaji wa pombe za
kawaida na pombe kali kwa kutengeneza vileo hivyo kwa njia ya
kisasa kabisa. Hapa Tanzania, kampuni ya bia inatengeneza aina
mbalimbali ya bia kwa mfano Safari lagar, Serengeti larga, tusker
lagar. Bia hizi zote utafiti unaonyesha kwamba sio kali sana.
lakini nimewahi shuhudia mtu amekunywa bia mbili aina ya ‘Ze
bingwa’ na kuishiwa nguvu kabisa. Kuna vinywaji vingine
vinatoka nje ya nchi kama vile whisky ambayo ina 50% ya kileo.
Daniel Jakes nk. Hata konyaji ni kileo kikali sana .

Kileo katika maandiko matakatifu


Kileo kinaonekana kutajwa katika maandiko kwa namna
mbalimbali na kuonyesha umuhimu wake kwa watumiaji.

35
• Divai inatajwa kama dawa ya tumbo kwa anayesumbuliwa
na tumbo na kwa ushauri wa daktari anaweza kutumia. I
Tim 5:23
• Yesu alitengeneza divai kwenye arusi ya kana ya Galilaya
na watu wakanywa na kulewa. Yoh 2:1-11
• Divai inatumika kuponya vidonda/majeraha ya vidonda.
Lk 10:31
• Divai inasaidia kupoteza mawazo ya umasikini. Mith 31:7
• Divai hufurahisha moyo wa mwanadamu. Zaburi 104:15
• Divai ilitumika katika sadaka kwa Bwana. Hes. 15:5-7
Japokuwa divai/pombe imeongelewa kwa mlengo chanya
katika mafungu haya lakini pia tukumbuke kwamba kwa
upande mwingine imeongelewa kwa mlengo hasi. Yaani
kwamba ina madhara kwa maisha ya wanadamu. Mfano
mafungu haya yanaonyesha hivyo, Kumb 21:20 IKor 6:7-9 nk

Mkristo na kunywa pombe.


Swali hili limekuwa ni swali la siku nyingi na kila siku
wakristo wengi wanapingana katika hili. Kwa baadhi ya
madhehebu ya Kikristo yanaruhusu kunywa pombe ila
usilewe tu. Lakini kwa upande mwingine wengine wanasema
kwamba kunywa pombe ni dhambi kubwa mbele za Bwana.
Huku wengine wakidai kwamba kunywa pombe ni tabia
mbaya tu ila siyo dhambi. Hebu tujaribu kuangalia hoja za kila
upande unavyodai.

36
Misingi ya mkristo kunywa pombe
Biblia haikatazi unywaji wa pombe bali inakataza ulevi wa
pombe. Ndiyo maana katika I Tim 3:3 ‘si mtu wa kuzoelea ulevi’
kuzoelea ni kitenzi cha ‘kuzoea’ maana yake kuendekeza tabia
ya kufanya hivyo. Na hapa Paul anatoa sifa za kiongozi wa
kiroho. Kumbe wakiristo wengine wasio viongozi wanaweza
kunywa pombe.
• Biblia imeagiza mkristo aweze kujitawala sio kuacha
kunywa pombe, hivyo basi kama mkristo anaweza
kunywa bia moja na akalala bila kumbughudhi mtu basi
anaweza kunywa ili mradi tu atawale hali yake.
• Biblia inatambua kwamba pombe inaweza kutumika
kama dawa, basi si mbaya kunywa pombe kwa ajili ya
afya9.
• Si kila mtu anayekunywa pombe anakuwa mlevi. Na
biblia imekataza ulevi sio unywaji wa pombe.
• Kukataa kunywa pombe unaweza kujitenga na jamii.
Kwa mfano kuna jamii zingine kama ukienda kwenye
sherehe lazima uzimue kidogo ndipo uonekane
unashirikiana nao.

9 Mtu mmoja anaitwa nabii Tito (Nabii wa pombe- a prophet of beer) ni nabii anayehubiri watu
kunywa pombe akitumia maandiko matakatifu ya Biblia na kudai kuwa Biblia inaruhusu kunywa
pombe.Hufanya mahubiri yake maeneo ya posta mpya hapa jijini Dar es Salaam.
Nabii Titto yeye anadai kuwa ameoteshwa na mungu kuwa watu wanywe pombe kwani ni tiba
sahihi tosha kwa magonjwa mbalimbali na si pombe tu mpaka sigara. Dini yake aliyoianzisha
inarushu watu kuoa wake wengi,kuvuta sigara na kunywa pombe.Huyu ndiye nabii Tito (a
prophet of beer)

37
• Unapokunywa pombe unatuliza akili yako na hivyo
kukufanya siku nyingine ukitaka kufanya kazi ufanye
kwa bidii kubwa
• Suala la kunywa pombe halihusiani na masuala ya uzima
wa milele. Kwa kuwa mtu amempokea Yesu kuwa
Bwana na Mwokozi wa maisha yake basi amehesabiwa
haki na ana uzima wa milele. Hivyo si dhambi kunywa
pombe.

Misingi ya mkristo kutokunywa pombe


• Biblia inaonya juu ya matokeo ya matumizi ya pombe
• Mtu aliyeweka nadhiri haruhusiwi kunywa kileo. Hes 6:2-3
• Makuhani hawakuruhusiwa kunywa vileo. LAW 10:9
• Wafalme hawakupaswa kunywa vileo katika falme zao. MIT
31:4
• Kileo hupotosha watumishi wa Mungu wanaojaribu kunywa.
ISA 28:7
• Si vizuri mtu aliyekusudiwa kuwa mkuu kutumia kileo. LK
1:15
• Kunywa pombe kwa mkristo ni kuonyesha na kuendelea
kuishi maisha ya zamani. 1PET 4:3-4
• Pombe huleta magomvi katika nyumba za watu
• Ulevi huua idadi kubwa ya watu. Nadhani hata wewe
umeshuhudia watu ambao wamekufa kwa sababu ya pombe
• Pombe huvunja ndoa nyingi sana
• Hakuna anayeanza kunywa pombe na kusema kwamba
hatakuwa mlevi bali hustukia mlevi tu

38
• Matokeo ya ulevi ni mabaya mno. Mfano kwa habari ya Lutu
kulala na watoto wke wakati wa ulevi na Nuhu wakati wa
ulevi alilaani mjukuu wake Kanaani.
• Kila mlevi unayemwona alianza kama mnywaji halafu
polepole akawa mlevi mkubwa.
Ushauri Kuhusu Pombe
Ukizingatia vizuri neno la Mungu, hakuna mstari wa Biblia ambao
unazuia moja kwa moja kwa mtu kunywa pombe. Lakin katika
hali ya uzoefu wa kibinadamu na maadili ya kimaadili na kwa
kuwa hoja zinazopinga kunywa pombe ni nyingi sana, kwa
ushauri wangu usijaribu kunywa pombe hata siku moja. Usijaribu
hata kutaka kujua ladha yake ikoje. Achana na misemo ya
wataalam soda ni hatari kuliko bia kwa afya !! Eti uache kunywa
soda ugeukie kunywa bia ni hatari sana.

Mch: Daniel John Seni


S.L.P 32807/senishekinah@gmail.com/ 0769080629
Dar es salaam
Ni mchungaji wa kanisa la Shekinah Presbyterian Church
Tanzania

39

You might also like