Professional Documents
Culture Documents
KUSIFU NA KUABUDU
1|Page
SHUKURANI:
Kwa namna ya pekee kabisa namshukuru Mungu kwa msaada wa Roho Mtakatifu
aliyeniongoza kuandika kitabu hiki. Lakini pia kwa namna ya kipekee ninamshukuru
Mchungaji wangu Rev. Elia Chisawilo kwani amefanyika Baraka na msaada mkubwa sana
kwangu hasa nilipokuwa namfuata kwa maswali mengi yaliyopelekea mimi kuandika na
kukamilika kwa kitabu hiki na hakusita katika kunisikiliza na kunisaidia hata pale
alipokuwa na majukumu mengine ya kazi zake za utumishi aliacha na kunisikiliza. Pia
ninawashukuru baadhi ya wababa wa kanisa la TAG - Mwembe bamia (CMF) ambao kwa
nyakati tofauti waliweza kuchangia kwa mawazo yao nami nikayachukua na kuyafanyia
kazi, bila kusahau viongozi wote wa idara kwa michango yao hasa tulipokuwa katika vikao
vya viongozi walinipelekea kuchukua mawazo yao na kuyaingiza katika kitabu hiki.
Pengine nitakuwa sijawatendea haki wale wote kwa namna moja ama nyingine nilichukua
mawazo yao vikiwemo vyanzo mbalimbali ambavyo niliweza kuvipitia kwa muda wote
niliokuwa nikiandaa kitabu hiki ingawa naweza nisiwe na kumbukumbu ya vyanzo vyote
lakini natambua na kuthamini mchango au mawazo yao na itoshe kwa kusema asante sana
na Mungu awabariki.
Msukumo huu ulitokana na hali halisi ya mazingira niliyokuwa nikikutana nayo kwa
muda mrefu hasa linapokuja suala la kusifu na kuabudu kwa kutokuleta mguso wa ndani na
kukidhi mahitaji ya mtu (yangu) kukutana na Mungu kupitia ibada ya kusifu na kuabudu.
Yawezekana hali hii imekuwa ikiwakuta wakristo wengi na kwa kupitia kitabu hili linaweza
kuleta mabadiliko kwako wewe ambaye unaguswa katika kumtumikia Mungu kama
kiongozi wa sifa na kuabudu.
Naamini Mungu ni mwaminifu na ninaomba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu atusaidie ili
sehemu hii ya kusifu na kuabudu ilete mabadiliko makubwa na uponyaji kwa kanisa la leo
Amen.
2|Page
YALIYOMO:
1. KUSIFU NA KUABUDU NI NINI
2. NANI MWENYE SIFA NA KIONGOZI WA IBADA YA
KUABUDU
3. SIFA BINAFSI ANAZOTAKIWA KUWA NAZO KIONGOZI
WA KUABUDU
4. MOYO WA KUSIFU NA KUABUDU
5. LENGO LA KUABUDU KWETU AU KUSUDI HASA LA
KUABUDU KWETU.
6. TENDO LA KUABUDU KWA ASILI NI LA KIROHO
7. TIMU YA KUABUDU (PRAISE TEAM)
8. JE NI SAWA KIBIBLIA KUTUMIA VYOMBO VYA MUZIKI?
9. KWANINI TUNAABUDU?
10. HITIMISHO
3|Page
SEHEMU 1: KUSIFU NA KUABUDU NI NINI?
Tunapojifunza Somo hili ni vema Tukafahamu kwanza nini maana ya KUSIFU na
KUABUDU.
Kusifu na kuabudu ni tendo la “IMANI” na “Utii” kwa Mungu wetu, na wala hali hii
haitegemei hisia peke yake (Si tendo la kutegemea hisia zetu pekee) kama ambavyo
tungeweza kufikiri. Ndani ya ibada zetu hatuwezi kukwepa kuwa na utaratibu huu wa
kumwabudu Mungu lakini pia hatuwezi kutokuwa na utaratibu wa kuwa na kiongozi au
viongozi wa kusifu na kuabudu, kwani Mungu wetu pia ni Mungu wa utaratibu. Hii
itatuwezesha kuwa na utaratibu mzuri unaolenga kutukutanisha na Mungu na kupokea
kile ambacho tunakiitaji kutoka kwake, ingawa si tu kupokea lakini lazima tuelewe pia
Mungu alituumba ili tumwabudu (Worship).
4|Page
SEHEMU YA 3: SIFA BINAFSI ANAZOTAKIWA KUWA NAZO KIONGOZI WA
KUABUDU
Hatua ya kwanza na ya muhimu sana, kiongozi wa sifa na kuabudu anatakiwa awe
amezaliwa mara ya pili (Kuokoka) na awe na Roho Mtakatifu (Kujazwa na nguvu za
Roho Mtakatifu).
Ni mtu mwenye IBADA(MWABUDU) aliye huru mbele za watu na mnyenyekevu na
mtii mbele za Mungu.
Anatakiwa awe makini Kiroho mwenye Roho wa Mungu ili aweze kuwaleta watu
katika uwepo wa Mungu.
Mwaminifu, kwani kuongoza ibada ya kuabudu mara nyingi hufanywa kwa imani na
utii na siyo kwa hisia.
Ili uishi maisha ya ushindi ni lazima ujue ibilisi ameshashambuliwa na kama utajua
hivyo basi utaelewa unao ushindi kiroho kwa kuwa Yesu Kristo alishakushindia. Hali hii
ni vigumu kuielewa kirahisi kama bado hujampokea Yesu huwezi kuishi na kutembea
katika hali ya ushindi bila kuwa na nguvu za ziada zinazokuonyesha kuwa mshindani
wako alishashindwa. Tunaposifu na kuabudu Mungu hushuka Ebr 2:11-13 hivyo tunatoka
kwenye kushindwa kwetu kwenda kwenye ushindi wa Kristo (1 Kor 15:57)
Hatua ya pili ni wewe kuwa Mwabudu (mtu wa ibada) hali hii itakupa uhuru mbele
za watu, lakini pia itakupelekea kuwa mtu mnyenyekevu na mtii mbele za Mungu. Ni
vizuri sana kiongozi wa sifa na kuabudu ukapenda kuabudu, na hasa ukizoea tabia ya
kuabudu bila kujali uko peke yako au la!
Tabia ya kumwabudu Mungu itakusaidia pale unapokuja katika kipindi cha kusifu
na kuabudu tayari umefungua moyo wako kuruhusu nguvu za Mungu zitembee na
kukutana na watu. Tunaona hali ya kuzoelea kuabudu ndo ilifanya Paulo na Sila kule
gerezani kwa kufunguliwa na hili ni somo kubwa sana kwetu hivi leo. Kwani tunapoingia
katika ibada hii ya kusifu na kaubudu tunatamani Mungu akutane na vifungo mbalimbali
vya watu. Watu wengi wanakuwa kwenye vifungu vya magonjwa, huzuni, njaa, mapepo,
n.k hivyo tunategemea kipindi hiki kilete uponyaji kwa watu hawa na pengine kuliko
hatua nyingine yoyote ya vipindi vya ibada.
6|Page
mwaminifu na kutembea katika tabia ya uaminifu. Wengi wetu tunaishi katika hali ya
uaminifu. Lakini tumeshindwa kutembea katika tabia ya uaminifu
Ili maisha yako yawe katika hali au tabia ya uaminifu lazima ufuate hatua hizi zifuatazo: -
1. Ni wewe na Mungu – Daniel 3;16-18
2. Ni wewe na jamii (watu) Paulo anasema sisi ni barua ya kusomwa na watu wote,
maana yake hapa kuna kuaminiwa, kukubaliwa na kuinuliwa.
3. Ni wewe mwenyewe (binafsi) maana yake dhamira yako ikushuhudie kuwa ndivyo
ulivyo. Yesu anasema yamtokayo mtu ndo yaliyomjaa (1 Samwel 12: 1- 5)
Unapoamua kuishi maisha ya uaminifu Mungu anaachilia Baraka zake – Kumb 28:1-8,
Ayubu 42:10.
Hapa tunaweza kujifunza kitu, kumbe uaminifu wako pia unatokana na unachokikiri –
Isaya 6:8 kwani umejengwa katika hali ya haki na imani yako Zab 34:15
Hivyo basi hili tuwe katika hali ama tabia ya uaminifu tunatakiwa kuwa watu wenye
haki na imani (Rum 10:10) haki na uaminifu hukaa ndani ya moyo wa mtu, na Mungu
anawatafuta wenye haki ili aweze kuwasaidia shida zao. Tunajenga msingi wa haki kwa
kuwa waaminifu ili kufike mbinguni na si kwa ajili ya watu. Lakini ni vizuri tukabeba
tabia za Bwana wetu Yesu Kristo jinsi alivyobeba tabia ya uaminifu kutoka kwa Baba
yake- Kum 7:9.
Hali ya kutunza uaminifu wetu kwa Mungu kutatufanya tulipwe kutokana na tabia
hiyo, kama tunavyoweza kujifunza juu ya mfano wa taranta kwa wale watumishi (math
25.26) mwanzo sura 15 (Agano la Mungu na Ibrahimu).
Daudi anasema neno moja nimelitaka kwa Bwana nalo ndilo nitakalolitafuta, nikae
nyumbani mwa Bwana siku zote za maisha yangu niutazame uzuri wa Bwana, Na
kutafakari hekaluni mwake (Zab 27:4) Ni wazi kwamba Daudi alijua siri ya kukaa
nyumbani mwa Bwana, alitunza uaminifu na kuishi maisha ya uaminifu.
Kuwa rafiki ni kuwa mtu wa watu mvumilivu na ujifunze kubadilika wala usiwe mtu
wa kukwazika mara kwa mara. Hapa uvumilivu kwa kweli unahitajika sana maana ni
sehemu ambayo shetani anatumia sana kuwaangusha watu wengi kwenye makwazo
na hatimaye unatoka kwenye msingi wa Mungu, hivyo uvumilivu ni muhimu sana,
jenga tabia ya kuwa na tahadhali wakati wote kwani makwazo hayana budi kuja au
7|Page
kuwepo ndani ya kanisa na hapo ni vizuri ukaibebeba imani sawa sawa kwani
kinachomfanya Ibrahimu kuwa Karimu wale wageni ni tendo la imani na pengine
alifanya hivyo si kwa sababu alitegemea kupata kitu kutoka kwao la! Bali katika hali
yake ya kutembea katika haki ya Mungu ilimsukuma kuwahudumia bila kujali wana
nini kwa ajili yake. Lakini pia tunaona anapoenda kumtoa Isack mwanae mpendwa
kama alivyoelekezwa na Mungu (mwanzo 22:7) Isack anamuuliza baba yake kuhusu
kondoo wa sadaka, majibu ya Ibrahimu kwa Isack kuwa Mungu atajipatia
mwanakondoo, pengine ni jibu ambalo mimi na wewe hatukulitegemea au na hata
Isack mwenyewe kwani ndani yake kuna imani kubwa.
Ukiwa na mahusiano mazuri na Mungu unajengwa ujasiri wa imani yako hata katika wakati
mgumu unaouendea. Mungu anakuwa na urafiki wa karibu na Ibrahimu kwa sababu
Ibrahim pia alijenga imani kubwa kwake pamoja kwamba alikuwa anaenda kumtoa
mwanae alikuwa anakabiliwa na pengine huzuni kubwa ndani yake, laikini alikumbuka
urafiki wao na Mungu na kuwa hata huyo mtoto ametoka kwake (Mungu) hivyo aliamini
bado Mungu anaweza kumletea tena furaha katika maisha yake.
Kumbuka hapa nazungumzia sifa ya urafiki ulio katika imani. Katika Yakobo 1;5-8,
Biblia inatuambia juu ya kuwa na imani pasipo shaka yoyote, kwani imani ya kusitasita
haitakupa matokeo chanya katika Ukristo wako na hasa ukiwa kiongozi wa sifa na
kuabudu maana utakuwa ni mtu wa kukaribisha makwazo kila wakati hivyo badala ya
kukuinua unazidi kudidimia. Kama Ibrahimu angekuwa mtu wa kusitasita basi hata
Sara Mkewe asingeweza kumzaa Isack, maana mkewe Sara bila shaka jambo hili
lilikuwa gumu moyoni mwake kuzaa katika umri wake.
Hapa tunajifunza jinsi ambayo ukikaa vizuri na Mungu na kujenga imani kwake inaweza
kukuletea matokeo ambayo akili yako haina majibu nayo. Lakini imani hiyo pia itakupa
faraja ambayo hukutegemea.
Imani inaleta ujasiri (Isaya 43:1-2, Isaya 6:8) pia imani uleta Baraka mwanzo 22:17
Sifa nyingine ni kuwa mwana muziki – ni vizuri zaidi kama ukakuwa na uwezo wa
kuimba au kuwa na vionjo vizuri vya kutumia vifaa vya muziki kama utakuwa nauwezo
huo. Kwani tunaamini ukiwa na uwezo wa kupangilia vizuri vyombo vya muziki unaweza
kwa sehemu kubwa kuliweka kusanyiko katika hali nzuri ya mwitikio na hapo ndipo hali ya
kuabudu itakuwa katika mtiririko mzuri usio chosha, hivyo kuwafanya watu wahame
katoka kimwili na kuzama Kiroho zaidi.
Uwe mtu unayejitolea, hapo ni vizuri nieleze kwa kirefu kidogo. kiongozi wa sifa na
kuabudu lazima awe tayari wakati wote kama nilivyokwishaeleza huko nyumba, lakini
tunapenda au tungependa awe ni mtu wa kujitolea kwa Mungu kwanza, kisha familia na
kanisa kwa ujumla, maeneo haya ni muhimu sana kwa kiongozi anayetaka huduma yake
iwe nzuri na inayoleta matunda mema.
8|Page
Uwe ni mtu uliyejiandaa vizuri na mwenye muonekano mzuri katika mavazi yako na
yawe ya heshima na unadhifu yasiyoleta maswali mengi. Na hapa hata katika mitindo
mbalimbali ya mavazi yako pengine hata mifumo ya nywele kwa wale wenye kuwa na
mitindo mbalimbali ukizingatia zaidi eneo la huduma yako kuliko matokeo ya kila
ulichokibeba. Maana tumejikuta waumini wengine wanaamishia mawazo yao kwenye
mtindo wa nywele muda wote wakasahau hasa wanapaswa wamwabudu Mungu. Katika
mavazi uliyovaa yasiwe yenye kuonyesha mazingira yako yote ya mwili au mepesi kupita
ile hali ya kawaida (Trasparent) na kama kweli utakuwa makini zaidi basi wakati unaposifu
ni wakati ambao kama hukujiandaa unaweza kusababisha minong’ono mingi na fujo isiyo
ya lazima kutokana na maandalizi yako hasa kwa upande wa mavazi. Ni eneo ambalo Ibilisi
analitumia sana kuchota akili za watu ili wasimwabudu Mungu mwonekano huo ni kwa
wote yaani kiongozi wa sifa wa kiume na wa kike lakini pia ni kuhakikisha mavazi yako
yanavishikizo imara kabla ya kuingia kwenye huduma. Hii ni kukulinda pia na fedheha
inayoweza kukupata mbele za watu.
9|Page
na hali yako uliyo nayo huku ukiendelea kutafuta fursa zaidi za kuongoza (Zakaria
4:10)
(d) Itikia wito wa Mungu kwa kuwa mwaminifu katika vichache (Luk 16:10)
Biblia inasema “Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo
kubwa pia, na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia”.
Zipo fursa nyingi kutoka kwa Mungu na huja kulingana na mahitaji ya wahusika, hivyo
ni wewe kuona jinsi gani ya kutumia fursa unayoiona mbele yako hata kama si ile
uliyokusudia kwani yawezekana ikawa kipimo kwa ile huduma iliyokusudiwa ndani
yako au uliyokusudia wewe. Na hapa utajikuta wakati mwingine unatakiwa kujifunza
au kufundishwa ili uweze kufikia hatua ya kuongoza math 7:7 “ombeni nanyi
mtapewa tafuteni nanyi mtaona, bisheni nanyi mtafunguliwa”. Ukikubali kuitikia
katika vichache basi Mungu atakupandisha katika vingi pasipo wewe kujua, kwani
Mungu ndiye anaona akutumie wapi na kwa kusudi lipi.
Efeso 1:11 “huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye”. Moyo wa
kitumishi uandaliwe kufanya chochote wakati ufaao na wakati usiofaa, kinachotakiwa
ni ule utayari wako hata pale unapoona si pa kukufaa (yaani pasipo na fursa) au
10 | P a g e
panawepesi au ugumu, penye kuvutia au pasipovutia wewe itikia wito wa Mungu kwa
kuwa na tumani. Ebr 13;21 “Awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema,
mpate kufanya mapenzi yake”.
Kwanza kabisa utambue kuwa wewe kama kiongozi wa sifa na kuabudu lazima
ulilishe kundi au watu, hivyo lazima uchague nyimbo nzuri itakayowawezesha watu
kuingia kwenye kuabudu, na nyimbo hizi ziwe za kuwaunganisha na uwepo wa
Mungu (kukutana na Mungu) maana yake wapate chakula kizuri cha Kiroho kupitia
uimbaji. Na kwa kuwa utakuwa unalipenda kundi lazima utajitoa hasa ili ulitimize
kusudi lako kama mchungaji mwema. Yohana 15:13 Biblia inasema “hakuna aliye na
upendo mkuu kama huu wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake” na Yohana
10;11 inasema “Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo”. Kwa
misingi hiyo utaona unawajibika kuwapa kondoo wako chakula chema na
kitakachowafanya wafurahie kuwa na mtu kama wewe. Ki msingi hapa ndipo sehemu
inayohitaji maandalizi ya hali ya juu kama kweli kama utataka watu wakutane na
uwepo wa Mungu kupitia nyimbo ulizozichagua. Siku zote kondoo atategemea kupata
maelekezo mazuri kutoka kwa mchungaji wake atakayewaelekeza mazingira mazuri
ya kupata kile walichokitegemea (yaani chakula kizuri cha kiroho) tena ukisoma
katika waefeso 3;8 “inasema utajiri wa Kristo usiopimika’ hivyo malisho
wanayotegemea siyo ya kunyang’anyana bali ni yale nyenye utoshelevu katika Kristo
Yesu. Watu wale na wanywe mbele za Mungu kupitia uimbaji kiasi cha kuwatosheleza
na kuua yale mahitaji yao ya kimwili na matatizo mbalimbali, Wanayokuja nayo
kutoka mazizini mwao (nyumbani mwao).
11 | P a g e
Kabla sijamaliza kwenye kipengele hiki nimeona nikuandalie maswali
yatakayokuwezesha pengine kukufungua zaidi na kukuimarisha katika huduma hii ya
kusifu na kuabudu.
1. Je haiba yako ni ipi na pengine ungependa Mungu akutumie katika hali hiyo
uliyonayo au uliyolelewa nayo na pengine iliharibu mahusiano yako na Mungu,
hivyo unaomba Mungu sasa akutayarishe upya uweze kutumika katika huduma hii
ya kumwimbia?
2. Je katika maisha yako ulishawahi kuwa na msukumo wa kumtumikia Mungu
katika huduma hii au kuna sababu nyingine uliyo nayo inayopelekea uanze na
kuchukua hatua ya kumwimbia Mungu kama kiongozi wa sifa na kuabudu?
3. Je maisha yako ya Haki, uaminifu na imani yakoje, unahisi kuna eneo ambalo
halijakaa sawa n a ungependa Mungu akutane nalo ili mwelekeo wako uwe salama
hasa pale unapoamua kuchukua hatua?
4. Je kiroho au maisha ya kiroho ukoje, unafikiri inatosha sasa kumtumikia Mungu au
wakati wako umefika wa kufanya hivyo au bado una mashaka mashaka na
huduma unayoiendea?
5. Je katika sifa nilizokwisha kuzitaja hapo nyumba unaona kabisa unakosa sehemu
ya sifa fulani na ambayo inaweza kuwa kikwazo katika huduma yako na Je
ungependa Mungu afanye nini ili uondokane na tatizo hilo?
Na ni vizuri tulenge kumwinua yeye nakuonyesha ukuu wake ama uweza wake.
Zaburi 48;1 (Bwana ndiye aliye Mkuu, na mwenye kusifiwa sana)
Ili tuelewe namna nzuri ya kuabudu lazima tuangalie mambo yafuatayo: -
(a) Ni hali ya mwonekano wetu wa kawaida na si lazima ufundishwe bali ni silica
tuliyonayo. Mfano mtoto mchanga anasilika ya kutabasamu na kucheka na
wanakuwa huru wanapofanya hivyo bila kufundishwa na mtu yeyote, lakini
unapokuja kwa watu wazima lazima watataka kutoa sauti ili watambulike au
kuonyesha mwitikio juu ya jambo fulani. Kama ilivyo kwa sura zote mbili
12 | P a g e
Mungu ametupa amri, haijalishi unajisikiaje pale anapotaka umwabudu njia ni
moja tu ya kumwabudu kwani huko ndiko tunakwenda kukutana naye.
Utayari wetu wa kumwabudu utupeleka uzimani. tunaona kusitasita kwa
Musa kulifanya akapewa msaidizi wa kuongozana naye pengine Mungu
hakupenda iwe hivyo lakini tunakuwa katika hali kama ya mtoto mchanga
tunaruhusu mambo mengi zaidi kwenye maisha yetu, hasa ya kutufanya
tutabasamu na kuwa na amani.
(c) Picha ya tatu ni kuonyesha thamani ya Mungu kwetu na kwa wengine pia,
kama tujuavyo Mungu wetu ni wa thamani sana na pengine ni vigumu
kuelezea thamani yake (ufunuo 4:11) “umestahili wewe, Bwana wetu na
Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na uweza, kwa kuwa wewe ndiwe
uliyeviumba vitu vyote, na kwa sababu ya mapenzi yako vilikuwako, navyo
vikaumbwa”. Kusifu na kuabudu kunahusiana na yale Mungu aliyoyafanya,
lakini hasa kwenye kuabudu kunamaanisha yeye ni nani.”
Na shauku hii imejengwa katika misingi ya uimbaji. Hivyo Mungu hutupa shauku
kupitia muziki. Kwanini Mungu hutupa shauku kupitia muziki ni kwa sababu: -
1. Kupitia muziki tunaweza kuonyeshwa shauku ya kumwabudu zaidi na
kumdhihirisha zaidi Mungu ndani yetu.
2. Pia uimbaji, hasa tunapotumia vyombo vya muziki vinakuwa na mchango mkubwa
kwa watu kuwafikisha katika uwepo wa Mungu. Miili yetu inakuwa
imeunganishwa tayari na makusudi ya Mungu hivyo kuhama katika hali ya
kawaida na kumwacha Mungu atawale zaidi, na ndipo utaona mabadiliko tofauti
kama tungekuwa tunasikiliza tu maneno ya Mungu.
Ibada ya Kikristo ni zaidi ya kuwa katika hisia fulani au msisimko fulani tu, bali ni
zaidi ya hayo, kwani kuabudu kwetu kumejengwa juu ya mwamba imara wa Kweli juu
ya Mungu ni nani Zab 24:10 “Ni nani mfalme huyu wa utukufu?” 1 falme 8:27 “Tazama
mbingu hazikutoshi wala mbingu za mbingu.”
17 | P a g e
Lazima ujue Mungu ni mwaminifu, mwema, mwenye neema, mwenye huruma
asiyebadilika, wa kushangaza, mwenye nguvu zote, anajua vyote, wa ajabu, mtakatifu,
mwenye rehema, mwenye hekima, kweli na wa milele yupo kila mahali, ni upendo
hakuna aliye kama yeye, Zab 89:6 “maana ni nani katika mbingu awezaye
kulinganishwa na Bwana? Ni nani afananaye na Bwana miongoni mwa malaika?
Matokeo ya kujua majina na sifa za Mungu inatupa kuimarika zaidi katika imani na
kuelekeza mioyo yetu kwa Mungu hivyo kuwa na ibada nzuri ya kumwabudu Mungu
na hasa kutuongezea shauku na hali ya kumjua yeye tunayemwabudu kwa usahihi
zaidi (Yoh 4:22) tunaabudu tukijuacho
Kama haya hayatafanyika basi maana yake tutakuwa tunadhoofisha ule ukuu wa
Mungu na kwa msingi huo dhana ya kuabudu kwetu haitakuwa na maana yoyote.
Ibada ya Sanamu ni kuwa na mawazo ya kumfikiria Mungu yasiyo ya hadhi ya Mungu.
Ili kudumisha dhana ya kuwa Mungu yuko juu ya yote na ameinuliwa sana ni lazima
kujua kwamba Mungu anaweza yote na ni kuabudiwa na kutukuzwa. Na hii si kwamba
tunamfanya yeye kuwa tu mkubwa bali lazima tumuone alivyomkubwa.
Kuabudu ni kuonyesha heshima kwa Yule aliye mkuu kuliko wewe, unapomwona aliye
mkuu kuliko wewe ndipo unaweza kuabudu, kwa kule kuelewa na kumfanya yeye
atawale maisha yako.
Ibada ya kuabudu ya kweli ni muhimu zaidi na ni ya ndani sana pengine zaidi ya kitu
kinachoonekana kwa nje, mfano muziki, mbinu za uongozi, au hata kikundi cha kuabudu.
Na hapa ndipo kiongozi wa sifa au kuabudu lazima awe makini sana na mwangalifu, kwani
18 | P a g e
yawezekana ukawa unashughulika na kulenga katika mambo nje ya kuabudu na kuacha
kushughulika na mambo ya rohoni. Maana yake unaweza kujikuta unalenga katika nyimbo
za kisasa kwa lengo la kuwafurahisha watu ili tu uonekane bora bila kutambua kuwa
kuabudu tunalenga kutatua matatizo ya watu na ndipo Mungu huonekana kwani yeye
hutazama hali ya ndani ya mioyo yetu.
Hivyo maandalizi ya kiongozi wa sifa na kaubudu ni muhimu sana yenye orodha nzuri
za nyimbo na kwa mtiririko ulio bora katika kuabudu. Na maandalizi haya yatakupa nafasi
ya kuomba kwa Mungu na kumuuliza Mungu, juu ya mahitaji yetu ili kupata majibu kwake
ya orodha ya nyimbo utakazotu tumia katika ibada ya kuabudu. Na hii pamoja na kuomba
maombi ya pamoja na kwamba yawezekana nyimbo zikawa za kawaida lakini kitendo
chako cha kumsihi Mungu kitaleta mabadiliko makubwa katika ibada ya kuabudu, kwani
msimamizi mkuu atakuwa ni Mungu mwenyewe. Unaweza kukuta umetumia maneno
machache lakini yenye tija kubwa katika ibada ya kusifu na kuabudu. Watu wengine
hufikiri wingi wa maneno ni “vikorombwezo” vingi ndivyo vinaweza kuleta namna nzuri ya
kumwabudu Mungu na kusahau kuwa mwenye kuabudiwa ni nani, ingawa uelewa juu ya
unayemwabudu ni muhimu sana ili kujiachia kwake (mbele za Mungu).
Kwa kuwa tunakuwa tunalenga kukutana na Mungu katika Ibada ya kuabudu pengine
si vibaya kama utamuuliza mchungaji wako au msimamizi wako juu ya somo la mahubiri, si
kwamba orodha yako ya nyimbo lazima iegemee kwenye mahubiri la hasha, bali inaweza
kuwa njia nzuri ya kupanga orodha yako ya nyimbo pia, na hii hasa tunalenga watu watoke
na kitu pale wanapokuja kwenye ibada badala ya kutoka wakiwa watupu. Watu wanaweza
wasitoke na neno lakini wakatoka na wamejawa na furaha ya kumwabudu Mungu, hivyo
kutoona kama ibada ni kupoteza Muda.
3. Tendo hili la kuendelea kujianchia mbele za Mungu hasa katikati ya wiki kwa ajili ya
maandalizi yako, kutakufanya uwe karibu zaidi na Mungu na pengine Mungu atafunua
moyo wake wote kabla ya Ibada.
20 | P a g e
- Panaweza kufanyika mabadiliko kwenye orodha yako, lakini haina maana kuwa
mawazo ya mwanzo hayakustahili bali kunakuwa na hitaji maalumu pengine kwa
ajili ya watu wewe ni kuendelea na mchakato huo mpaka wakati utakapofika wa
ibada na hili ni eneo la utii ambalo litaleta mafanikio mazuri kwenye suala la ibada.
- Kama una nyimbo za ziada na pengine ungeona uzitumie basi ni vizuri kuzimaliza
mwishoni mwa ibada ingawa bado utapaswa kuzifanyia mazoezi ili ziendane na
nyimbo za awali mpaka zitakapokaa sawa, na wakati wingine Mungu anaweza pia
kurekebisha orodha hiyo wakati unapoimba.
Lakini pia ni vizuri utafute taarifa zao kabla kwa kila mtu atakayetaka kujiunga na
timu ya kuabudu na hapa ni vizuri uzingatie historia yao Kiroho ili kama kuna marekebisho
basi yaweze kufanyika mapema. Na si vibaya kama utawajulisha watu wanaotaka kujiunga
ni kitu gani au sifa zipi wanatakiwa kuwa nazo, kwani si kila mtu mwenye msukumo
anaweza kujiunga na timu hii. Lazima uwaonyesha matarajio yanayotakiwa watakapokuwa
wamejiunga na timu na baada ya mchakato mzima wa kufahamiana vizuri basi ni vema
utaratibu uanze mara moja wa kuanza mazoezi na pengine hata elimu ambayo wengi wao
hawakuwa nayo kuhusu jambo hilo.
Waandaliwe Kiroho na kimwili yaani mwenekano wao katika uvaaji, tabia ili
wanapokuwa katika huduma hii na nje ya huduma wawe ni watu wa mfano wa kuigwa
wakiwa wamevaa Sura nzuri ya Ukristo (yaani wenye mauhusiano mazuri na Mungu).
Kama watakuwepo wenye ujuzi wa kutumia vyombo basi ni vema kama hawapo bado
wanaweza kuandaliwa ili waweze kutumia vyombo vya muziki vizuri na kwa weledi wa
hali ya juu katika kuwaunganisha watu na muziki.
22 | P a g e
B: NAMNA YA KUWAFUNDISHA WANA TIMU AU KIKUNDI CHA KUSIFU NA
KUABUDU (PRAISE TEAM)
Tunaamini ufundishaji wowote una kanuni zake, hivyo hata kufundisha muziki
lazima ufuate kanuni au taratibu za kufundisha muziki, na hasa tungependa kuona kiongozi
wa kikundi cha Kusifu na Kuabudu kwa sehemu kubwa akiwa ni mwalimu na mtaalamu
wa muziki. Na kama hayupo basi wateuliwa wachache ambao watajifunza ili waweze kuja
kuwasaidia kikundi cha kuabudu. Pengine kuwa na wataalam ni vizuri zaidi ili waweze
kutoa maelekezo makini juu ya wakati gani unaofaa kucheza au kutocheza, na kwa weledi
zaidi pia kutoenda nje ya mtiririko wa vyombo. Ni vizuri kuwa na watu tofauti na vyombo
tofauti katika timu ili kuleta radha tofauti tofauti ya muziki na hii inaweza kuleta
muunganiko mzuri sana kati ya wahusika na washirika.
Lakini ni vizuri zaidi kwa kiongozi uliyepewa jukumu hilo la kukifundisha kikundi
cha kuabudu ukakumbuka jinsi Mungu alivyo mwema kwako (kumbuka Bwana ndiye
Mchungaji wangu) wakati unapofundisha. Zaburi 23:1 na katika Zaburi 78:72 tunaona ama
tunasoma Daudi kama mchungaji wa watu, kwa msingi huo Zaburi hizi zinaelezea jinsi
Mungu alivyomtunza na kumchunga Daudi na jinsi ambavyo Daudi alivyochunga watu
wake. Katika kujenga timu nzuri ya kuabudu lazima wawe ni watu wanaofamiana vizuri na
wenye umoja wa hali ya juu nje na ndani ya huduma, hii itajenga umoja mzuri katika
kufanya mazoezi, na umoja huu kama utakuwa wazi sana basi tunategemea kukua na
kujenga kikundi ambacho ni imara katika Kanisa. Lakini umoja wa ‘Kiroho” ni wa muhimu
zaidi na unakamilishwa kwa hatua ya pamoja ya kupata muda wa zaida wa kumwabudu na
kumwomba Mungu pia kusoma Biblia kwa pamoja.
Timu ya kuabudu lazima iwe na mwelekeo mmoja kama ambavyo Farasi ni lazima
wavute kuelekea upande mmoja au jinsi ilivyo kwa mme na mke lazima wafanye kazi kwa
mwelekeo na malengo yanayofanana, vinginevyo hakuna kitakachofanyika. Hivyo
tunaamini kama timu ya kuabudu itafanya kama hii mifano basi tunaamini itakuwa ni timu
bora na yenye nguvu katika kuwainjilisha watu katika huduma hii ya kusifu na kuabudu.
Kama tutachukua mfumo wa Bwana wetu Yesu Kristo basi tunaamini huduma hii
itakuwa yenye Baraka sana katika kuwaimarisha watu na kuvuna roho za watu wengi
ambao bado hawajamjua Mungu, lakini pia italeta uponyaji kwa watu wengi. Soma vifungu
vifuatavyo kukusaidia ni jinsi gani unatakiwa uwe: mark 10:45, wafilipi 2:5 math 20:25, 26
23 | P a g e
(ii) Mahudhurio kwenye mazoezi ni muhimu sana ili kuweza kuwa na
maandalizi mazuri au yaliyoshiba kwa ajili ya ibada.
(iii) Ni vizuri kwa kiongozi wa ibada kuwa na muda wa ziada wa kujiandaa
mwenyewe na mahali pakufanyia mazoezi, hivyo itakulazimu ufike mapema
kabla ya wanatimu ili kufanya maandalizi.
(iv) Mazoezi ni vizuri yakazingatia muda au ratiba mtakayokuwa mmejiwekea
kama kikundi ili kutoingilia ratiba nyingine kwa sehemu husika au ratiba
nyingine za makundi mengine katika Kanisa.
(v) Kiongozi lazima uwe na orodha ya wanakikundi ili kuweza kubaini ambaye
atakuwa hajaudhuria na jambo hili ni jema na la msingi ili kuwasiliana naye
pengine ni mgonjwa au amepata shida hivyo kuona namna ya kumsaidia.
Lakini pia ni taadhali kwa siku ya ibada kwani kama hakuwepo kwenye
mazoezi ni ukweli kwamba mnaweza kupishana katika uimbaji au mpangilio
mliyojiandaa wakati yeye hayupo.
(vi) Lisha kudni lako kwa kuomba kuabudu na kusoma neon la Mungu na
wajulishe matamanio yako kutokana na mazoezi.
(vii) Ni vizuri siku zote ukamaliza mazoezi kwa wakati na ukumbuke
kumshukuru kila mtu (mwanakikundi) kwa ajili ya kuwa mwaminifu
kutenga muda wake kwa ajili ya timu mwisho mmalize kwa kumshukuru
Mungu kwa maombi na kutawanyika.
24 | P a g e
(iii) Mtazamaji ni Mungu Je wewe ungependelea mtazamo upi katika hii?
26 | P a g e
Hivyo kupaa ni ile hali ya utangulizi yaani kuanzisha wimbo na hali ya kuwa angani ni
kule kuimba wimbo na kutua kwa ndege aridhini ni kumalizia wimbo. Kama kiongozi
wa nyimbo za kuabudu atachukua mfano huu na kuufanyia kazi basi unaweza
kupangilia vizuri zaidi na kufikisha zaidi lengo la kuabudu kwa watu.