You are on page 1of 3

Solly & Flory Corporation

www.sollydaddy92@gmail.com
www.hadassah5464@gmailcom
0769 567 263 / 0753 907 403

KIJANA NA UCHUMI
Kwanza kabisa yakupasa utambue kuwa kijana ni mtu wa thamani sana mbele za MUNGU, hii
haimaanishi kuwa wengine sio wa thamani mbele zake, La hasha‼... nimesema hivyo kwa
sababu kuna mambo ambayo yanamfanya kijana kuwa mtu wa kitofauti au mtu wa muhimu
sana. Mmambo hayo ni kama yafuatayo;

 Kijana ni mwenye nguvu (Mithali 20:29)


 Wakati wa ujana ndio wakati wa kujenga msingi wa maisha (Future yako)
 Wakati wa ujana pia ndio wakati sahihi wa kumtumikia MUNGU (Mhubili 12)

Hizo ndizo baadhi ya sababu za kujua kwanini wewe ni muhimu sana na shetani anajua hilo pia
ndio maana wakati wa ujana ni wakati mgumu sana na wenye changamoto nyingi kwa sababu
shetani anahangaika na vijana.

Vijana wengi tumekuwa tukipata shida katika eneo la uchumi na mwisho wa siku tunajikuta
hatuna kitu kabisa, japo kuna roho za umaskini na Ufukara zinazowafuatilia watu wa
MUNGU lakini pia zipo hali nyingine ambazo tunajisababishia sisi wenyewe.

Yapo matatizo yanawapata wengi hasa katika eneo hili la uchumi mwisho wa siku unajikuta
mambo mengi hayaendi na unakata tama na kuhisi huna bahati au umerogwa n.k

Wapo wanaoshindwa kuoa, kujikimu nadani ya familia zao, kupata mahitaji yao ya kila siku,
tatizo kubwa likiwa ni Uchumi mbovu.

Kwanini vijana wengi wanapata pesa na hazikai kwa muda mrefu?


Zipo sababu ambazo haya na hili tatizo limetukumba vijana wengi sana, hasa sisi wanachuo kwa
wale wanaopokea pesa ya kujikimu au kwa jina jingine hujulikana kama Boom... unamkuta
kijana anakuwa na mipango mingi sana na hilo boom, lakini baada ya kupewa pesa hiyo
anashangaa inakaa kwa muda mfupi tu na inakwisha bila kuifanyia kitu chochote.

Solima and Florida Page 1


Sababu zinazosababisha pesa isikae kwa muda mrefu ni kama zifuatazo;

1. Kutokumuheshimu Mungu kwa Mali na Fedha.

Mithali 3:9-10 neno la MUNGU linasema 9Mheshimu Bwana kwa mali yako, Na kwa
malimbuko ya mazao yako yote. 10Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo
yako yatafurika divai mpya. Unapomuheshimu MUNGU kwa mali zako atakujazia zaidi na
zaidi, Embu tafakari hapo wapendwa.

Mathayo 6:19-21, Hagai 1:2-8 maandiko haya yanaongelea swala zima la utoaji wa zaka na
sadaka pamoja na michango mingine ndani ya kanisa n.k… kutoka katika kitabu cha Mathayo 6
kinasema 19Msijiwekee hazina duniani… pia katika msitari wa 33 neno la MUNGU linasema
33
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Malaki 3:8-10 hapa neno linaongelea kuhusu zaka na sadaka, na sio zaka tu ni “zaka kamili”
sio nusu maana kuna watu wanatoa, ndio… lakini sio zaka kamili. Mpendwa wangu unapotoa
zaka isiyo kamili hauna utofauti na yule ambaye hajatoa kabisa hivyo kama umepanga kutoa
zaka nusu ni bora usitoe tu, kumbuka Anania na Saphira (Mdo 5)

2. Kutamani kuishi maisha yanayokuzidi uwezo.

Wapo watu wanaotamani kuishi maisha ghali wakati hali yao ya kiuchumi hairuhusu kabisa.
Kwetu sisi vijana tatizo linakuja pale ambapo fulani au rafiki yako ana simu ya iPhone au
Samsung basi na wewe unataka hiyo iPhone au Samsung wakati hali ya mfuko wako ni
Smart kitochi au Kiswaswadu , kwa hiyo unajikuta unatumia fedha ambazo hukupangilia
kununua simu ya gharama kubwa, mpendwa ridhika na ulichonacho. Waebrania 13:5 neno la
MUNGU linasema 5Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa
kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Na kitabu
cha 1Timotheo 6:6 neno la MUNGU linasema 6Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni
faida kubwa.

3. Matumizi bila malengo au mipango.

Hii nayo ni shida kubwa sana kwa vijana wa sasa, wengi wetu hatutumii pesa kwa malengo au
mipango. Mpendwa unatakiwa kuwa na mipango kwa mfano unaweza ukawa unamuomba mtu
pesa kila siku alafu jibu lake ni “sina”... sio kwamba yeye kila siku hana, Hapana‼.. zipo
lakini zimepangiliwa kwahiyo ya kukupa wewe haipo, au lile fungu alilokuwa amelitenga kwa
ajili ya kukopesha na kusaidia limekwisha. Unaweza ukawa umepokea mshahara au Boom
kwetu sisi wanachuo, ila kama hujapangilia mshahara unaweza ukaisha siku hiyohiyo au
Boom linaweza kuisha siku hiyohiyo kwa vijisababu visivyoeleweka Mara baby amekuja
anataka hiki na kile, mara mmeenda kula bata, mara mmeamua kubadilisha mazingira hata
nyumbani hapalaliki siku hiyo, mambo yanakuwa mengi...alafu pesa zikiisha anaenda kwa
mchungaji kumuomba amuombee kua ana pepo la umaskini linamfuatilia kumbe ni kutofahamu.

Solima and Florida Page 2


4. Kumdhurumu MUNGU

Kumbukumbu la Torati 16:17 neno la MUNGU linasema 17Kila mtu na atoe kama
awezavyo, kwa kadiri ya baraka ya Bwana, Mungu wako, alivyokupa. Je, utoavyo zaka n
asadaka kanisani, michango ya ujenzi, mahubili na effort mbalimbali, ni kama
unavyobarikiwa? Jiulize na ujijibu moyoni mwako.

Kwahiyo kabla ya kuonana na wachungaji na wazee wa kanisa kwa ajili ya kuombewa,


jichunguze kwanza je, katika sababu hizi nilizotaja ipi/zipi zinakuhusu? Na kama zinakuhusu
anza leo kujirekebisha na kama bado utaendelea kuwa na shida dumu katika maombi au
zidisha maombi ikiwezekana onana na wachungaji au wazee wa kanisa ili wapate kukuombea
maana kama nilivyosema hapo juu kuwa pia kuna roho za ufukara na umasikini na madeni
ambazo zinawasumbua watu wa MUNGU.

BWANA AWABARIKI SANA NA AWASIMAMIE KATIKA HILI

Prepared by Mr Solima and Ms Florida

Solly & Flory

©2023

Solima and Florida Page 3

You might also like