You are on page 1of 40

(a Bible Centered University)

P.O.BOX 1917 MBEYA TANZANIA

HAMETIKI
Kanuni za Kufasiri Maandiko
Msingi wa Kujenga Watendakazi na Viongozi Watumishi
Wanaojizidisha na wenye Maono ya Kuigusa Dunia Nzima.
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
MADA YA KWANZA
UTANGULIZI WA JUMLA WA HERMENEUTICS
1. UTANGULIZI
Neno Hermeneutics linatokana na neno la Kigiriki. Neno hermeneien. hilo linatokana
na neno Hermes mojawapo ya miungu ya Kigiriki aliyekuwa Talishi (messanger).
Mungu huyo alihusika na kusafirisha na kufasili mawasiliano baina ya miungu

Hivyo neno Harmeneus hutumika kumaanisha kuelezea (to explain )au kufasili
(Translate )

Kamusi ya Encarta Premium inafafanua kuwa Harmeneutics ni Sayansi na mbinu za


kufasili matini (maandiko) hususani Biblia

Kwa hiyo tunaweza kusema kwamba Harmeneutics ni sayansi na sanaa ya mchakato


wa kufasili. Au tunaweza kusema kwamba ni kitendo cha kieksijesia katika mkutadha
wa kawaida.

Kufasili ni sanaa inayojihusisha na kuondoa utofauti kati ya mwandishi wa matini na


msomaji wa matini hiyo ili maana au ujumbe uliokusudiwa na mwandishi uweze
kueleweka kwa msomaji wa matini. Hivyo basi neno Hermeneutics ni sawa na neno
kufasili au kutafsiri.

2. SABABU ZA KUFASILI MAANDIKO


Uwepo wa Pengo kati ya Mwandishi na msomaji
Kama ilivyokishwa elezwa hapo awali kwamba haermneutics hushughurikia pengo
lililopo kati ya mwandishi na msomaji. Pengo hilo linaweza kusabisha msomaji
ashindwe kuelewa maana au ujumbe uliokusudiwa na mwandishi. Baadhi ya mapengo
yaliyopo ni

1. Pengo la utamaduni.
Utamaduni ni jumla ya mfumo mzima wa maisha. Pengo la utamaduni linahusisha
tofauti zilizopo kati ya utamaduni wa mwandishi na utamaduni wa msomaji. Ili
kuondoa pengo hili kanuni za Hermeneutics zinahitajika

2. Pengo la Kihistoria
Pengo la kihistoria linahusiana na tofauti ya muda toka kipindi cha mwandishi hadi
kipindi cha msomaji.

1
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

3. Pengo la Lugha
Hii ni tofauti iliyopo kati ya maandishi halisi (origin manuscript) ya Biblia na
tafsri mbalimbali za Biblia. Biblia iliandikwa kwa lugha za Kiebrania cha kale,
Kialamu na Kigiriki cha kale. Lugha tatu tofauti zenye tofauti ya kisarufi. Hivyo kuna
uhitaji wa kuondoa pengo hilo kupitia kanuni za kufasiri Maandiko.

4. Pengo la kijiografia.
Pengo la kijografia linahusika na utofauti wa maeneo kati ya eneo la mwandishi na
eneo la msomaji. Jiografia ya eneo moja huweza kubadilika kutokana na mabadiliko ya
tabia ya nchi na sura ya nchi na maendeleo ya shughuri za kibinadamu. Hivyo kuna
maeneo mengi ambayo yametajwa katika Biblia leo hii hayapo ama yamebadilishwa
majina, hayaitwi kwa majina ya zamani. Pia tofuati za hali ya hewa na shughuli
mbalimbali za kiuchumi

5. Pengo la kifalsafa
Pengo la kifalsafa linahusu tofauti ya kimtazamo kuhusu ulimwengu na maisha kwa
ujumla kati ya mwandishi na msomaji wa Biblia. Ili kuweza kufasili Maandiko kwa
usahihi inatakiwa kutazama ufanano kati ya mtazamo wa mwandishi na mtazamo wa
msomaji.

6. Kutofautiana Kwa Akili Miongoni Mwa Binadamu


Hii inahusu makuzi ya akili, kwa mfano watu wawili wa taif moja na utamaduni
mmoja wanaweza kushindwa kuwasiliana ikiwa mmoja amesoma na mwingine
hakusoma. Yule aliyesoma atakapotumia lugha ya kitaalamu Yule asiyesoma
hataelewa kilichosemwa na msemaji.
Angalia mfano
2.Petro3:15-16
Nanyi uhesabuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa ni wokovu, kama vile na ndugu yetu
mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima aliyopewa. Vilevile kama katika nyaraka
zake zote pia, akitoa humo habari za mambo hayo ; katika nyaraka hizo yamo mambo
ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara,
huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na Maandiko mengine, kwa uvunjifu wao
wenyewe.

2
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Kutokana na nukuuu hiyo ni wazi kuwa baadhi ya mafundisho ya Paulo ni vigumu
kuyaelewa na kwamba baadhi ya watu wasio na elimu wameyapotosha. Kwa
kutazama usuli wa kifalsafa unaweza kuhitimsha kwamba baadhi ya watu ambao
hawakuwa na elimu ya kutosha walimwelewa visivyo. Hayo ndiyo matokeo ya utofauti
wa akili baina ya wanadamu
Msisitizo
Paulo alimwandikia Timotheo kwamba
Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtendakazi asiye na sababu ya
kutahayari ukilitumia kwa halali neno la kweli. 2Timotheo 2:15

Neno la Kigiriki Orthotomaunta linalotafsiriwa kama ukishika kwa usahihi ambayo


maana yake halisi ni kukata moja kwa moja (cutting straight) neno hilo katika
mkutadha wa Maandiko lina maana ya Ukifasili kwa usahihi.
Lengo lake ni kwamba kila mhudumu wa Injili asiogope na anapaswa kufasili Neno la
Mungu kwa usahihi.

3. MKAZO WA HERMENEUTICS
EKSIJESIA NZURI NDIO MSINGI WA THEOLOGIA
Kwa sababu kila kitu tunachokijua kuhusu Mungu kimefunuliwa kwa upana kupitia
Maandiko Matakatifu, kwa hiyo basi Theolojia yote imejengwa juu ya Fasili ya
Maandiko Matakatifu. Kama tutafasili hovyo Maandiko maana yake ni kwamba
Theolojia itakayojengwa itakuwa potofu na italeta athari hasi katika imani na
mwenendo wa waamini. Hii ni kwa sababu matendo na maneno ni matokeo ya kile
mtu anachoaamini. Hivyo tunapaswa kujihusisha zaidi katika kufasili Maandiko kwa
usahihi ili tuweze kuwa na Theologia sahihi inayoegemea kwenye Biblia. (Bible
centred Theology)

EKSIJESIA NZURI NI MSINGI WA HOTUBA BORA


Kila mhubiri wa Neno la Mungu hawezi kukwepa kazi ya kufasili Maandiko. Ikiwa
mhubiri ameelewa maana ya kifungu isivyo sahihi maana yake ni kwamba hotuba au
mahubiri yake yatakuwa potofu. Atafundisha au kuhubiri kile Maandiko
hayamaanishi. Hivyo tunaweka mkazo kwamba kila mhubiri na mwalimu wa Neno la
Mungu hana budi kuhakikisha anakielewa vyakutosha kifungu au somo analotaka
kuhubiri au kufundisha

3
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
4. SIFA ZA MFASIRI BORA WA MAANDIKO
Kwa hakika si kila mtu anaweza kufasili Maandiko. Mfasiri bora wa Maandiko hana
budi kuwa na sifa kadha wa kadha. Baadhi ya sifa anazotakiwa kuwa nazo mfasili bora
wa Maandiko ni
1. Awe amezaliwa mara ya pili (ameokoka)
mfasili wa Maandiko ni lazima ase amekutana na Yesu katika maisha yake na awe
amempokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake.Kuokoka ndio mwanzo
wa mahusiano na Mungu na ndio mwanzo wa kuweza kupokea mambo ya kiungu.
Mtu yeyote asiyeokoka kwake Biblia ni kitabu kilichofungwa na hawezi kuielewa
Biblia.
Soma 1wakorintho 2:14
Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu;
maana kwake huyo ni upuuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa
yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.

Mfasili bora wa Maandiko ni lazima awe na uwezo wa kupokea mambo ya kiroho toka
kwa Mungu.

2. Awe na shauku ya kuijua kweli.


Mfasili bora wa Maandiko ni lazima awe na shauku ya kulielewa Neno la Mungu na
atafute kulielewa. Atake kuijua kweli ya Neno la Mngu kama inavyofundishwa na
Maandiko Matakatifu. Ni lazima awe tayari kulipa gharama katika kujifunza na
kuweka katika matumizi kile anachojifunza
Watu wengi leo wanapenda kujua kweli ya Neno la Mungu lakini hawako tayari
kuitafuta na pale kweli ya neno la Mungu inapoongea tofauti na wanavyotaka
wanaitupilia mbali

3. Awe mnyenyekevu.
Unyenyekevu ni hali ya kukubaliana na hali ilivyo na kuwa tayari kuchukua hatua.
Mfasili wa Maandiko lazima akubali kunyenyekea mbele za Mungu ili Mungu aweze
kusema nae kupitia Neno lake. Pia anapswa kuwa tayari kujifunza na kuachana na
mtazamo aliokuwa nao kabla ya kuelewa maana ya Maandiko hayo. Lazima aweze
kuchukua hatua sawasawa na Neno la Mungu linavyotaka.
Watu wengi na makanisa mengi leo wamejiundia fasili ya Neno la Mungu na wako
tayari kupinga fasili nyingine yoyote iwapo haiendani na fasili zao bila hata ya
kufanya uchunguzi wa kina.

4
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

4. Bidii na uvumilivu
Wakati mwingine kupata fasili ya Andiko si tukio la mara moja au la muda mfupi.
Inaweza kuchukua muda mrefu na inahitaji kujitoa kikamilifu kufanya uchunguzi na
utafiti. Hivyo mfasili bora wa Maandiko hapaswi kuwa mvivu na mzembe. Ni lazima
awe mchapakazi na asiye kata tama upesi. Hakuna njia ya mkato katika kuyaelewa
Maandiko Matakatifu. Ni lazima kutoa muda kikamilifu kujifunza Neno, kununua
vitabu na vifaa vingine vya kujifunzia na mwisho kuliweka neno katika matendo.

5. Aishi maisha ya maombi


Maombi ni mawasiliano na ushirika kati ya Mungu na mtu. Kwa sababu Roho
Mtakatifu ndiye mwandishi mkuu wa Maandiko yeye anajua alichokiandika na
anaweza kutoa mwanga wa kulielewa neno lake. Mfasili bora wa Maandiko anapaswa
kuomba uongozi wa Roho Mtakatifu katika kazi ya kufasili, anapaswa kuomba karama
ya upambanuzi. Kazi ya kufasili Maandiko si kazi ya kitaaluma ni kazi ya kiroho na
hivyo basi maombi ni muhimu ili kuweza kuwa na ufanisi katika kazi hii.

6. Awe na shirika na Roho Mtakatifu


Kwa sababu mwandishi mkuu wa Biblia ni Roho Mtakatifu na wandishi wa
wanadamu walivuviwa na Roho Mtakatifu walipokuwa wakiandika hivyo basi mfasili
hana budi kuwa na ushirika wa kudumu na Roho Mtakatifu. Anapaswa kumruhusu
Roho Mtakatifu kufanya kazi katika maisha yake. Ni kupitia Roho Mtakatifu akili ya
mfasili itatiwa nuru ili iweze kuelewa na kutendea kazi neno la Mungu.

7. Awe na elimu Mtambuka


Elimu ni ujuzi au maarifa mtu ayapatayo kwa njia anuai. Elimu mtambuka ni maarifa
anuai. Mfasili wa Maandiko anapaswa kuwa na maarifa juu ya mambo kadha wa
kadha yanayohusiana na Biblia kwa namna moja au nyingine. Baadhi ya maarifa
hayo ni

Jografia ya Palestina
i. Uelewa kuhusu jografia ya Palestina itamsaidia mfasili kuelewa baadhi ya
vifungu vya Maandiko.
Mfano Zaburi 133:3
Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni.,,,

5
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Uelewa mzuri kuhusu usemi wa umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni
unategemea namna mtu anavyoielewa Jografia ya Palestina.

ii. Historia ya ulimwengu kwa ujumla wake. Historia ni somo linaloshusiana na


matukio mbalimbali yaliyotukia katika vipindi mbalimbali.
Uelewa wa Historia ya ulimwnegu utamsaidia mfasili kujua namna unabii
ulioandikwa katika Biblia ulivyotimizwa na unavyoendelea kutimizwa.
Pia kutamsaidia mfasili kuelewa athari za mataifa mbalimbali ya ulimwengu kwa
Wayahudi au Israeli.
Mfano unatakiwa kuelewa athari za Hellenism (utamaduni wa wagiriki) kwa
Wayahudi ambazo zinaonekana katika Agano Jipya. Ili uweze kuelewa jambo hili ni
lazima uielewe Historia ya Wayahudi tangu kipindi cha Alexander Mkuu hadi
kipindi cha Dola ya Rumi wakati wa Herode mkuu

Historia ya watu wengi wa kale na sasa ni za thamani sana. Mfano habari za dola ya
Ashuru, Misri, Babeli, Uajemi, Uyunani na dola ya Rumi zinatoa mwanga katika
kuielewa Biblia.
iii. Uelewa wa lugha za Biblia
Lugha imekuwa nyenzo au chombo kikuu cha mawasiliano katika zama zote. Kwa
sababu Biblia iliandikwa kwa lugha zingine zisizo zetu, hivyo mfasili wa Maandiko
anapaswa kuwa na maarifa yahusuyo lugha za asili za Biblia ambazo ni Kiebrania,
Kiaramu na Kigiriki.

iv. Elimu ya mambo ya kale (archeology)


Mfasili anatakiwa kuwa na maarifa kuhusu mambo ya kale (antiquities) mfano
uvumbuzi na sanaa ya nchi za mashariki ya kati (middle East). Maarifa haya yatapanua
uelewa kuhusu Maandiko Matakatifu.

6
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

MADA YA PILI

HISTORIA YA HERMENEUTICS
1. UTANGULIZI
Katika kipengele hiki tutatalii historia ya Harmeneutics. Harmeneutics ina historia
ndefu na inavutia sana. Historia ya Harmeneutics inakupa kuzifahamu na kuzielewa
mbinu za kufasili Maandiko ambazo ziliundwa miaka mingi iliyopita na zinatumika
hadi sasa. Katika kipengere hiki tutajifunza historia ya Hermeneutics kutoka katika
kipindi cha wayahudi wa kale mpaka kipindi cha sasa.

Malengo
Baada ya kujifunza kipengere hiki utaweza
 Kuelezea kila kipindi katika historia ya Hermeneutics
 Kuainisha wanazuoni mbalimbali wa Hermeneutics (hermeneutist)
 Kutathmini mchango wa kila mwanazuoni wa Hermeneutics katika uundaji wa
sheria na kanuni za kufasili Maandiko
 Kuainisha mbinu za hermeneutics zilizotumiwa katika kila kipindi.

1. HERMENEUTICS ZAMA ZA WAYAHUDI WA KALE.


Inaaminika kwamba sayansi na sanaa ya kufasili Maandiko ilianza na Ezra na
Waandishi wengine. Watu hawa walitaka kuwasaidia wayahudi wenzao ambao
walikuwa wamesahau lugha yao ya kiebrania wakiwa Babeli. Watu hawa walitafsiri
Maandiko ya kiebrania kwa lugha ya Kiaramu na fafanuzi yake ili Maandiko yaweze
kueleweka kwa watu wote.
Waandishi waliofuata baada ya Ezra walidai kwamba kila herufi ya Andiko ilikuwa
imevuviwa na hii ilipelekea kutokea kwa kipindi cha maana nyingi ya andiko.
Mfano Rabbi Akiba wa karne ya kwanza baada ya Kristo alidai kwamba uradidi,
usambamba, usawe, tamathali za semi, neno, herufi na hata umbo la herufi lilikuwa na
maana mficho.
Hadi kufiki kipindi cha Yesu Eksijesia ya kiyahudi ilikuwa katika kategoria nne
ambazo ni:-
i. Fasili Halisi (Literal Interpretation),

7
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Fasili halisi pia hujulikana kama Peshati. Fasili hii hufanyika msingi wa kategoria
zingine za fasili na haikuandikwa kwa sababu ilichukuliwa kwamba kila mmoja
alikuwa anaifahamu na haikuwa na mkanganyiko.
Fasili Halisi inadai kwamba andiko linamaanisha kile linachosema isipokuwa kama
imeelezwa vingine.

ii. Fasili ya Kimidrashi


Kanuni za msingi za fasili ya kimidrashi ziliundwa na Rabbi Hilleli. Kanuni hizi
zilisisitiza mlinganisho wa mawazo, maneno, na semi, Mlinganisho huo ulipewa
kipaumbele kuliko andiko moja. Mahusiano ya jumla kati ya kanuni kwa tukio fulani
na umuhimu wa mkutadha katika fasili.
Mlolongo wa fasili iliyopitiliza ulipelekea kuzaliwa kwa
 Kutoa maana ya Andiko, semi na maneno bila kuzingatia mkutadha
 Kuunganisha Maandiko yenye semi na maneno yanayofanana pasipo kujali
kama vinaashiria wazo moja au la.
 Kuweka mkazo zaidi katika sarufi katika fasili

Fasili ya Kimidrashi iliweka mkazo zaidi katika maana mficho na hivyo Eksijesia ya
Kimidrashi ilipoteza maana halisi ya Andiko.

iii. Fasili ya Pehisa (pehser)


Kategoria hii ya fasili ilijulikana sana katika jamii ya kumlani. Fasili hii ilikopa sana
kutoka katika kategoria ya Kimidrashi.
Fasili hii iliweka mkazo (focus)katika matukio kuhusu siku za mwisho (eschatology).
Waanzilishi wa Fasili hii walidai kwamba Maandiko yote yaliyoandikwa na manabii
yalikuwa na maana ya kinabii ambayo ilikuwa inaenda kutimia muda si mrefu katika
jamii yao.

iv. Fasili ya Sitiari


Mbinu hii ilikuwa imejikita kwenye mawazo ya kwamba maana ya kweli ya andiko
ilijificha ndani ya maana halisi (literal meaning). Mbinu hii ilitungwa na wagiriki
walipokuwa wanajaribu kuondoa mkanganyiko kati ya mapokeo ya mafumbo ya dini
zao na falsafa zao. Wayahudi ambao walitaka kushika sheria ya Musa na wakati
huohuo kufuata falsafa za Kigiriki walikutana na mkanganyiko huo na baadhi yao
waliamua kushikilia mbinu ya sitiari katika kufasili Maandiko.

8
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

2. HERMENEUTICS WAKATI WA MABABA WA KANISA


Katika kipindi hiki mbinu ya Fasili ya Sitiari ilikuwa na mashiko sana na
ilitawala katika kanisa.Mbinu hii ilipinga na kukataa maana iliyokusudiwa na
mwandishi kwa kukataa fasili ya Uhalisi
Klemensi wa Aleksandria aliainisha aina tano za milango ya maarifa ya
Maandiko ambazo ni Maana ya
i. Kihistoria,
ii. Kimafundisho
iii. Kinabii
iv. Kifalsafa
v. Kimafumbo
Origen alidai kwamba Andiko lilikuwa na milango mitatu tu ya maarifa,
milango hiyo ni
i. mlango wa uhalisi
ii. mlango wa maadili
iii. Mlango wa sitiari.
Agustino alidai kwamba Maandiko yalikuwa na milango minne ya maarifa
ambayo ni
i. Milango ya kihistoria
ii. Kianalojia
iii. Kietolojia
iv. Kisitiari.
Ikumbukwe kuwa japokuwa Agustino aliziacha kanuni nyingi za kihermeneutcis
alizokuwa ameziunda, bado baadhi ya kanuni hizo zina umuhimu sana kwetu.
Baadhi ya kanuni hizo ambazo zinatumika hadi sasa ni
i. Lazima mfasili awe na imani thabiti katika Yesu Kristo
ii. Maana ya kihistoria na kiuhalisi zinatakiwa kupewa kipaumbele zaidi katika
fasili

iii. Kazi ya mfasili ni kuelewa maana iliyokusudiwa na mwandishi nasikuleta


maana yake katika Andiko.
iv. Kifungu kinatakiwa kusoma katika mkutadha wake na si nje ya vifungu vingine
vinavyokizunguka kifungu hicho.

9
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

3. HERMENEUTICS ZAMA ZA KATI (Medieval )


Neno medieval huhusisha kipindi cha karne za kati katika historia ya ulaya. Ni
kipindi cha historia ambacho kimedumu kwa muda wa karibu millenia moja.
Inakadiliwa kuwa kipindi hiki kilianza na kuanguka kwa dola ya Rumi na kumalizkia
na kipindi cha kisasa (morden period) katika karne ya kumi na sita.
Hiki ni kipindi ambacho kanisa Katoliki lilidai kuwa kanisa la kitafa (state church).
Katika kipindi hiki milango minne ya maarifa ya Maandiko kama yalivyowekwa na
mababa wa kanisa yaliendelea kuwa na mashiko
Aina hizo nne za milango ya maarifa ya fasili iliweka mkazo upekee kati na roho ya
herufi na roho ya andiko.
i. Mlango wa maarifa wa uhalisi (literal) humaanisha kile andiko (matini)
linazungumzia moja kwa moja.
ii. Mlango wa maarifa wa sitiari (alegory) huelezea matini kwa kuzingatia maudhui
ya mafundisho (dogma) ya kanisa. Kwa hiyo kila chembe ya kiuhalisi ilikuwa
na maana ya kisitiari au kimafumbo.
iii. Matumizi ya kiuadilifu wa matini kwa msomaji binafsi ni mlango wa tatu wa
maarifa wa fasili
iv. Mlango wanne wa maana unahusisha maarifa kuhusu siku za mwisho
(eschatological knowledge).
Hermeneutics katika kipindi cha zama za kati kilishuhudia utitiri wa mbinu zisizo
za kiuhalisi za fasili ya Biblia (non literal interpretation).

STEPHEN LONGTON (1150-128)


Stphen Longdon alikuwa ni askofu mkuu wa Centerbury. Mtu huyu ndie aliyeingiza
sura katika Biblia. Stephen alifasili Biblia kwa kuegemea dogma. Yeye alidai kwamba
maana ya kiroho inatakiwa kusisitwa zaidi ya maana ya kiuhalisi. Kwa mujibu wa
Stephen ilikuwa ni muhimu sana kuhubiri kusudi la kanisa na ukuaji wa kanisa

THOMAS AQUINAS
Thomas Aquinas alikuwa ni mwanafalsafa, wa kiitalia na mwanatheologia ambaye
kazi zake zimemfanya kuwa mwanazuoni mashuhuri wa falsafa na mojawapo wa
wanatheologia wakuu wa kanisa Katoliki.
Thomas Aquinas alijifunza Falsafa ya Alistote katika chuo kikuu cha Nepali.
Mafundisho hayo yaliweza kumuathiri na kumfanya aweze kuunda mawzo yake ya
kitheologia na kifalsafa.

10
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Aquinas anatambuliwa kuwa mtu mashuhri sana katika kipindi zama za kati. Thomas
Aquinas aliacha kushadadia mbinu ya fasili ya sitiari na kuanza kutetea mbinu ya
uhalisia na matumizi ya mbinu ya sarufi na historia (usuli) kama msingi wa milango
mingine ya fasili ya Maandiko.
Alisisitiza kwamba msomaji wa Biblia anapaswa kutambua kwamba Biblia ina maana
ya kimafumbo (symbolic meaning) kwa sababu mambo ya kimbingu hayawezi
kuelezwa kwa maneno ya kidunia bila kutumia lugha ya ishara (mafumbo).
Kwa majibu wa Thomas Aquinas mfasili anapaswa kushughulikia maana halisi

NICHOLAS WA LIRA (1270-1349)


Nicholas anatazamwa kama mtu aliyeleta athari kubwa katika taaluma ya
Hermeneutics katika kipindi cha zama za kati. Mbinu yake ya Hermeneutics ilijikita
katika mlango wa Fasili ya uhalisi. Japokuwa aliitambua milango mingine minne
iliyofundishwa na wanazuoni wengine. Yeye alisisitiza kwamba mlango wa fasili wa
uhalisi unapaswa kuwa msingi wa milango mingine ya fasili.

Wanahistoria wengi wanakubaliana kwamba Maandiko ya Nicholas yalimvutia sana


Martn Luther na ndiyo yaliyoweza kuchangia sana katika harakati za matengenezo ya
kanisa.

4. HARMENEUTICS YA WAKATI WA MATENGENEZO YA KANISA


Nikipindi ambacho harakati za mageuzi zilizuka ndani ya kanisa kule Ulaya. Kipindi
hiki kilanza wakati Martn Luther alipobandika hoja (Thesis) 95 katika mlango wa
kanisa kule Wittenbugy Ujeruman. Japokuwa kipindi hiki kina historia ndefu toka kwa
watangulizi wa Matengenezo ya Kanisa mfano John Huss.
Kipindi hiki kimalizikia na patano la Westphalia mnamo mwaka 1648.
Mojawapo ya sababu zilizopelekea kuibuka kwa matengenezo ya kanisa ni kuzaliwa
kwa mwamko wa kujifunza (renaisance). Hivyo tutatalii kwa kifupi kipindi cha
renaissance .

Renaisance (zama za mwamko) ni kipindi cha kihistoria kilichoanza miaka ya 1400 na


kikafatiwa na kipindi cha zama za kati ambacho kinajulikana kwa jina maarufu middle
ages.
Neno Renaisance inatokana na neno la kifarasa lenye maana ya kuzaliwa upya. Sababu
zilizopelekea kipindi hicho kuitwa hivyo ni kwamba wakati huo watu walianza kuwa

11
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
na shauku ya kujifunza kuhusu mambo ya kale. Kwa namna moja au nyingine
walijifunza kuhusu mambo ya Ugiriki ya kale, Rumi ya kale n.k.

Wakati huo wa renaissance kuliibuka wasanii wengi sana wengi wao walikuwa
waandishi, wengine wanafalsafa. Watu walijifunza mambo ya hisabati na sayansi
mbalimbali. Kipindi hiki cha Renaisance kilianzia Italia na kisha muda mfupi kilienea
ulaya nzima. Pia renaissance ilipelekea kuzaliwa kwa falsafa ya ubinadamu
(humanismic philosophy) ambayo iliweka mkazo wa uthamani wa kila mtu.
Wanahumanist wa renaissance waliamini kwamba kulikuwa na uwezekano wa
kuboresha jamii kupitia elimu. Elimu hii ilijikita katika kufundisha kutoka katika
matini za kale na iliweka mkazo katika masomo mbalimbali. Baadhi ya masomo
yaliyohusika ni Ushairi, Historia, Uhutubishaji (rhetoric) na falsafa.
Mmojawapo wa wanazuoni wa ubinadamu (humanistic) wa kipindi hiki ni Erasmus.
Erasmus alianzisha mafunzo ya lugha za Biblia kwa kuandika toleo la Kigiriki la
Agano Jipya. Pia ndugu Reuchlin alitafsiri sarufi ya kiebrania na misamiati (lexicon).
Uvumbuzi wa matini za kale na elimu iliyofuata vilisababisha wanazuoni kutupilia
mbali mbinu ya sitiari ya kufasiri Maandiko. Wanazuoni walianza kuweka mkazo
kwamba maandiko yana mlango mmoja tu wa fasili. Wafasili mashuhuri wa kipindi
cha matengenezo ya Kanisa ni Martn Luther na John Calvin

MARTIN LUTHER
Martin Luther alikuwa mwanatheologia na mwanamangenezo ya kanisa wa Ujerumani.
ushawishi wake ulikuwa mkubwa uliogusa Nyanja zote, kidini, kisiasa, kiuchumi na
kijamii. Luther anatambuliwa kama mtu mashuhuri katika historia ya Ulaya.
Hermeneutics ya Luther inaweza kueleweka kwa kuchunguza mtazamo wake kuhusu
Biblia. Mtazamo wake wa kwanza ni kwamba Biblia haipaswi chukukuliwa au
kutazamwa kama vitabu vingine. Imani na roho ya kuangaziwa ni muhimu kwa
msomaji.
Jambo la pili, Luther alidai kwamba kanisa halitakiwa kuipangia Biblia cha
kufundisha bali Biblia ndiyo inatakiwa kusema nini kanisa lifundishe.
Baada ya hapo Luther alipinga mbinu ya fasili ya sitiari.
Katika fasili Luther alidai kwamba katika kuelewa maana ya Andiko lazima kutokane
na uelewa wa uhalisi wa Maandiko ya Biblia. Aliendelea kusema kwamba msomaji ni
lazima azingatie hali ya kihistoria, sarufi na mkutadha wa aya anayokusudia kuifasili.
Luther alisema kwamba Biblia ni kitabu kilichowazi na kinachoelewa kwa urahisi
(Bible is clear book and simpe to understand).

12
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Baada ya kuachana na mbinu ya sitiari Luther alikumbana na changamoto ya kupata
njia nyingine ya kulifanya Agano la Kale kueleweka kwa Wakristo wa wakati huo.
Maana mpaka kipindi hiki mbinu ya sitiari ilikuwa ni mbinu pekee iliyokuwa
inatumiwa katika kufasili Agano la Kale.
Ili kujaza pengo hilo Luther aliunda kanuni ya Kristolojia (Christological principle).
Kanuni hii baadae ilifanyika kanuni ya Hermeneutics ya Martin Luther.
Kanuni hii ilimsababishia Luther kumwona Yesu katika aya nyingi za Agano la Kale
hususani Zaburi.
Pia kanuni hii ilimwezesha kuonesha umoja wa Biblia bila kusababisha mkangayiko
wa fasili ya Maandiko ya Agano kale.

JOHN CALVIN
John Calvin alikuwa ni mwanatheologia, padre, humanist na mwanamatengenezo ya
kanisa wa kule ufaransa. John Calvin anatambuliwa kama mwanaeksijesia mkuu kama
Luther. Calvin aliiona mbinu ya sitiari kama chombo cha shetani cha kuficha maana
halisi ya Maandiko.
Calvin alianzisha msemo mashuhuri unaodai kwamba “Maandiko Hufasiri Maandiko
(Scripture enterprates Scriptue). Usemi huu unaashiria kwamba Calvin aliweka mkazo
katika kujifunza mkutadha, sarufi, maneno na usambamba wa aya badala ya kuleta
maana katika Maandiko.
Alidai kwamba kazi ya kwanza ya mfasili ni kumwacha mwandishi aseme
alichokusudia kukisema badala ya kuleta kile msomaji anachoona kwamba mwandishi
alitakiwa kukisema. John Calvin hakumwona Yesu katika kila aya ya Maandiko.
Kanuni za Hermeneutcs za John Calvin na Martin Luther ndio kanuni za sasa za
kufasili Maandiko za waprotestanti.

5. KIPINDI CHA KUANGAZIWA (Enlightment Age)


Kipindi cha kuangaziwa pia hujulikana kama kipindi cha kufikiri (reasoning) hii
ilipelekea kuzaliwa kwa uradhinishaji (rationalism), njia ya kifalsafa inayokubali
kwamba kufikiri kama chanzo kikuu cha mamlaka katika kuangalia matendo binafsi
ya mtu. (mfano mtu hutakiwa kufikiri kabla ya kutenda jambo fulani).
Kuangaziwa kulishadadiwa na wanafalsafa kama Thomas Hobbs, (1588-1676)na
Baruch Spinoza (1632-1677) ambao walifundisha kwamba Kufikiri (reasoning) ni njia
pekee ya kuamua kilicho kweli au kisichokweli.

13
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

Pia katika kipindi hiki zilizuka falsafa na nadharia (empiricism) zilizodai kwamba
maarifa ya kweli yanaweza kupatikana kwa milango mitano ya fahamu pekee (five
senses).
Hivyo baadhi ya wananadharia walilitazama kanisa kama kitu kilichokuwa kinyume na
nadharia ya milango mitano ya fahamu. Hii ni kwa sababu kanisa lilijikita katika imani
na ufunuo. Hivyo basi waradhinishaji (rationalist) walianza kulishambulia kanisa na
Biblia kwa ujumla.
Mlengo huu ulizaa Theolojia ya Kiliberal ambayo ilianza katika kipindi cha
Harmeneutics ya kisasa (morden hernmeneutics).

6. HERMENEUTCS BAADA YA MATENGENEZO YA KANISA


Kipindi cha baada ya matengenzo ya kanisa kilianzishwa na kanisa Katoliki na
kilikuwa ni kipindi cha mabishano ya kidini. Baraza la trenti liliketi mara kadhaa kati
ya mwaka 1545 na 1563 ili kutoa matamko (decree) kadhaa ambapo dogma ya Kanisa
la Katoliki ilitangazwa.
Kutokana na hali hiyo Waprotestanti nao waliunda matamko yao, kwa mfano kama
ukiri wa Augsburg, kanuni ya Itifaki (formula of Concord) na ukiri wa Helveti.
Kilikuwa ni kipindi cha mabishano makali sana ya kidini.
Mabishano ya matamko ya Doktrini (mafundisho ya Biblia) yalisababisha kusitishwa
kwa kazi ya Hermenetics. Ni katika kipindi hiki ambapo Hermeneutics iliwekwa chini
ya Dogma ya kanisa. Hermeneutcs haikuwa na thamani tena katika kipindi hiki,
japokuwa kulikwa na watu wachache walioendeleza kazi hiyo kwa sehemu.
Baadhi ya watu hao ni Philip Jakob Spener (1635-1705), August Hermann Fracke
(1663-1752), John Albrechet Bengel (1687-1752)
Watu hao walijulikana kwa jina la wacha Mungu (Pietism) Jakob Spener alitambuliwa
kama kiongozi wa uamsho wa wacha Mungu. Spener aliweza kuhimiza watu kuacha
mabishano yasiyo na tija na kurudi kujifunza neno la Mungu na huduma. Wacha-
Mungu waliweka mkazo katika kujifunza Kiebrania na Kigiriki na matumizi ya
Maandiko katika maisha ya kila siku.

Pia walizingatia njia ya fasiri ya sarufi na kihistoria (grammatical historical


Inenterpretation) wakati wa Kufasili Maandiko.
Pia tunapaswa kutambua kwamba Wacha-Mungu hawakudumu kwa muda mrefu.
Baadae walipuuza mbinu ya fasili ya sarufi na historian na wakategemea kile

14
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
kilichoitwa nuru ya ndani (inward light) na baadae walipelekea kila mtu kufasili
Maandiko kwa mtazamo wake mwenyewe. Wakati mwingine walipuuza Maandiko
na kushikilia hisia zao na mitazamo yao.

15
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
MADA YA TATU
KANUNI ZA KUFASIRI MAANDIKO
1.0. UTANGULIZI
Katika mada hii tutajadili baadhi ya kanuni za msingi za kufasiri Maandiko.Inatarajiwa
kuwa baada ya kuchunguza kanuni hizi kwa kina mwanafunzi atakuwa na uwezo wa
kufasiri Maandiko au Biblia kwa ufasaha na hivyo ataweza kuhubiri Neno la Mungu
kwa usahihi
sawasawa na Biblia inavyosema katika kitabu cha 2Timotheo 2:15
“Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtendakazi asiye na sababu ya
kutahayari. Ukitumia kwa halali neno la kweli"

1. KANUNI YA MKUTADHA
Kanuni ya msingi ya Maandiko ni kanuni ya mkutadha

Dhana ya mkutadha

Kamusi ya Oxford living inafasili neno mkutadha kama,


1. Mazingira au hali ambamo tukio au jambo hutendeka
2. Mazingira ya neno katika tungo au sentensi yenye kuonyesha uhusiano wake na
maneno mengine.
Neno mkutadha Kietimolijia linatokana na neno la Kilatini Contextus lenye maana ya
“fuma pamoja au weka pamoja”.

Neno mkutadha uhusisha uhusiano uliopo baina ya neno na maneno mengine


yanayolizunguka neno hilo, au Uhusiano uliopo kati ya kifungu na vifungu vingine
vinavyokizunguka kifungu hicho.

Katika mawanda mapana neno Mkutadha uhusisha mazingira ya wakati Andiko hilo
lilipoandikwa. Hii uhusisha utamaduni na historia vikiunganishwa pamoja na
mkutadha wa matini yenyewe.

Wazo kuu katika kanuni hii ni kwamba kifungu cha Maandiko kinaweza kueleweka
kwa kuangalia vifungu vilivyokitangulia na vifungu vinavyofuata baada ya kifungu
hicho.

16
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Kutokana na maelezo hayo tunaweza tengeneza kanuni ya mfuatano. Unapotaka
kupata maana ya Msitari chunguza mistari iliyotangulia na mistari inayofuata baada ya
mstari huo.

Mstari au kifungu kilichochukuliwa nje ya mkutadha wake daima kitaleta fasili isiyo
sahihi na kupelekea kuzaliwa kwa fundisho potofu na hatimaye imani potofu.

Mhutasari wa kanuni ya mkutadha


Neno Mstari Aya Kitabu Agano Biblia

 Kanuni ya mkutadha inafanya kazi katika nyanja zote za maisha na si Biblia


pekee.
 Ili uweze kuelewa mada ya mazungumzo ni lazima uelewe mazungumzo hayo
yalikoanzia na yalikoishia. Nje na hapo utazalisha maana ambayo
haikukusudiwa na mzungumzaji.

AINA ZA MIUKUTADHA KATIKA BIBLIA


Kuna aina nne za mikutadha katika Biblia

1. Mkutadha wa Andiko
Kuna aina kuu nne za mikutadha ya Andiko ambayo ni
i. Biblia nzima
ii. Agano Jipya au Agano la Kale
iii. Kitabu
iv. Aya

 Katika kanuni ya Mkutadha wa Andiko tunapata kanuni ya maswali matano


ambayo ni muhimu sana kujiuliza na kujibu ikiwa unataka kupata fasili sahihi ya
Andiko. Maswali hayo ni:-
 Nani? (mzungumzaji/mwandishi)
 Kwa nani ? (Mwandikiwa mahususi wa mwanzo)
 Nini? (mada ya mzungumzo/kinachozungumzwa)
 Kwa nini (sababu iliyopelekea jambo hilo kuzungumzwa/kuandikwa
 Lini? (muda jambo hili lilitokea au kuandikwa)
17
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

Kujibu maswali hayo kunakupa kuelewa mazingira yote kwa ujumla na hivyo
kuweza kufasili andiko kwa usahihi.

2. Mkutadha wa Kihistoria
Aina hii ya mkutadha inahusu uhusiano wa kifungu cha Andiko na historia halisi ya
mazingira kifungu hicho kilimoandikwa. Hapa unachunguza tarehe ya kuandikwa
kitabu na matukio yaliyotukia katika kipindi hicho katika Historia. Pia unachunguza
mwandishi wa kitabu na mazingira yake. Kufahamu hali halisi ya kihistoria ya wakati
huo inakupa kufahamu kwanini mwandishi alisema kile alichokisema na kwa namna
alivyosema.

Kweli kuu ya kanuni hii - ni kwamba Andiko haliwezi kumaanisha kile ambacho
hakikumaanishwa kwa wasomaji au wasikilizaji halisi wa mwanzo (japokuwa inaweza
tokea katika mazingira fulani hasa katika unabii 1Petro 1:10-12

3. Mkutadha wa Kiutamaduni
Kila kifungu fulani cha Maandiko kiliandikwa katika mazingira fulani ya
kiutamaduni. Katika kipindi cha uandishi wa Maandiko kulikuwa na kuhusika
kwa kiasi kikubwa na mambo ya kitamaduni ambapo yalitofautiana eneo na
eneo na kizazi na kizazi.

Mkutadha wa kiutamaduni uhusisha kutambua kile kifungu kilimaanisha kwa watu


walioandikiwa kwanza kwa wakati ule na mahali pale kulingana na utamaduni wao.

Mkutadha wa kiutamaduni uhusisha vitu anuai kama vile siasa, dini, uchumi,
sheria, ujenzi, kilimo, vyakula na mambo mengine mbalimbali ya kijamii.

Historia na utamaduni unaowazunguka waandishi ni muhimu sana katika kusaidia


kuelewa fasili ya Andiko.
Ufahamu wa makundi mbalimbali ya dini ya Kiyahudi wakati wa Yesu, (Maherode,
Mafarisayo, Masadukayo na Wazerote), na serikali iliyotawala Palestina wakati wa
Agano Jipya Huleta uelewa zaidi wa Maandiko.

18
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
4. Mkutadha wa kiuhalisia
Mkutadha wa kiuhalisia uhusisha mtindo wa uandishi wa kitabu au kifungu. Kuna aina
mbalimbali za mitindo ya uandishi iliyotumika katika Uandishi wa Biblia. Kila mtindo
wa uandishi una kanuni zake za ufasili. Hivyo ili uweze kufasili kwa usahihi kifungu
au Andiko ni muhimu ujue mtindo wa uandishi uliotumika.

Uvunjaji wa kanuni ya mkutadha


Watu wengi huvunja kanuni ya mkutadha kwa kuchukua sehemu ya kifungu cha
Andiko na kukipa fasili pasipo kuhusianisha na vifungu vingine. Watu wanaofanya
hivyo mara nyingi hutafuta Maandiko yanayohusiana na mawazo yao ili waweze
kutetea mawazo yao.

Unaweza kuifanya Biblia iseme chochote unachotaka ikiwa utavunja kanuni ya


Mkutadha.
Andiko haliwezi kusema kile ambacho halikusema kwa wasomaji/wasikilizaji wa
kwanza.
Napenda kuwahamasisha wanafunzi wa Chuo hiki kuhakikisha unazingatia mkutadha
ili uweze kufasili na kuhubiri kwa usahihi Neno la Mungu.

Mungu hana kigeugeu wala si Mungu wa machafuko, Mungu anamaanisha kile


alichokisema katika Neno lake.

2. KANUNI YA MTAJO WA KWANZA


Kanuni hii inahusu kutajwa kwa neno, kitu au tukio kwa mara ya kwanza katika
Maandiko. Kutajwa kwa neno, kitu au tukio kwa mara ya kwanza katika Biblia hutoa
msingi wa maana wa neno, kitu au tukio hilo katika maeneo mengine katika Biblia
neno hilo linapotokea.

Kanuni ya mtajo wa kwanza ni kanuni ambapo fasili ya mstari/neno au kifungu


hupatikana kwa kuzingatia namna kitu hicho kilivyotajwa kwa mara ya kwanza katika
Biblia.

Kutajwa kwa kitu mara ya kwanza katika Maandiko hubeba maana thabiti
itakayoendelezwa katika Biblia nzima.

19
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Kwa mfano katika kitabu cha Mwanzao 3:7

“Wakafumbuliwa macho wote wawili, wakajijua kuwa wauchi, wakashona majani ya


mtini, wakajifanyia nguo.”
Katika Andiko hili Adamu na Hawa walitumia majani ya mtini kujaribu kuficha
dhambi yao na utupu wao kwa jitihada zao wenyewe. Majani ya mtini huashiria haki
binafsi, kukataa njia ya Mungu ya kupata haki na kujaribu kujipatia haki binafsi mbele
za Mungu.

Hii ndio maana ya majani ya mtini mahali popote yanapotajwa katika Biblia. Kwa
mfano kwa mara ya mwisho majani ya mtini yametajwa katika Mathayo 21:18-20, na
Marko 11:12-14, na Marko 13:28-29.
Katika Injili ya Mathayo na Marko tunakuta mtini wenye majani bila matunda. Yesu
aliulaani na ukayauka.

Ili kuweza kuelewa jambo hili tunapaswa kukumbuka kanuni ya mtajo wa kwanza na
kurudi katika kitabu cha Mwanzo 3.

Majani ya mtini yanawakilisha, Kukataa kwa mwanadamu njia ya Mungu ya ukombozi


na jinsi mwanadamu anavyoitumia haki binafsi katika kujaribu kujipatia kibali mbele
za Mungu.
Majani ya mtini yanawakilisha haki binafsi ya taifa la Israeli walipomkataa Yesu.
Walimkataa yeye (Yesu) kama Mfalme na hivyo hawakuweza kuukubali mpango wa
wokovu toka dhambini. Walikuwa wakijaribu kuwa wenye haki kwa jitihada zao
wenyewe.

Kanuni ya mtajo wa kwanza inaweza kutazamwa kama:-


 Mwongozo wa jumla
 Kanuni ambayo haiwezi kufanya kazi peke yake, kanuni inayofanya kazi sanjari
na kanuni zingine.
Pia inaweza kutazamwa kama:-
 Ufunuo unaofungua mlango kuingia kwenye kweli
 Lango la kuingilia kwenye kweli, mwongozo wa kuvumbua kweli katika ufunuo
mwendelezo.
 Kiungo cha kwanza cha mnyororo mrefu wa ufunuo

20
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
 Mbegu ambayo inaendelea kukua ndani yake katika mtajo mwendelezo katika
Maandiko.
Kanuni ya matajo wa kwanza inaweza kutumika katika maneno, dhana, mifano, watu,
mahali na dhamira.

3. KANUNI YA MTAJO MWENDELEZO


Ni kanuni ambayo inasema kwamba fasili ya mstari wowote hujengwa na mtajo
mwendelezo wa somo/fundisho hilo katika Biblia.
Kanuni ya mtajo mwendelezo inaitazama Biblia kama kitabu kimoja na inatakiwa
ifasiliwe kwa matazao huo.

Biblia ni kitabu kimoja chenye mwandishi mmoja ambaye ni Mungu.


Ijapokuwa haiwezekani kwa mwanadamu kuandika kitabu kama hicho kwa Mungu
inawezekana kwa sababu anautambua mwisho kutokea mwanzo Isaya 46:9-11.

Kanuni ya mtajo mwendelezo inatambua mbinu au njia ya Mungu ya ufundishaji au


ufunuo. Isaya 28:13
“Kwa sababu hiyo Neno la Bwana kwao litakuwa hivi, amri juu ya amri, amri juu ya
amri, kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni; huku kidogo na huku kidogo ...”

Kanuni ya mtajo mwendelezo inatambua kwamba Mungu amefunua kweli yake kwa
mwanadamu kwa njia ya mwendelezo, amefunua kweli yake hatua kwa hatua.
Hii ina maana kwamba maudhui mengi ya Biblia huanza na mbegu, mbegu hupandwa,
humwagiliwa maji na kukua na kuwa mti mkubwa wenye matunda.

Mbegu ya kweli fulani iliyopandwa katika vitabu vya mwanzo vya Biblia hukua kwa
kadri inavyoendelea kutajwa katika Agano la Kale na Agano Jipya. Maudhui
yaliyoanza katika kitabu cha Mwanzo hukuzwa katika sehemu zingine za Biblia na
kuishia katika kitabu cha ufunuo.

Mfano
 Uzao wa mwanamke akawa ni Kristo na Kanisa lake Wagalatia 3:16, 19, 29.
 Kuumbwa kwa Mbingu na Nchi kunapelekea kuumbwa kwa Mbingu mpya na
Nchi mpya Ufunuo 21:1.

 Mti wa uzima (Mwanzo 3) unatoa njia kwa mti wa uzima Ufunuo 22:2, 14.
21
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

4. KANUNI YA MTAJO KAMILIFU


Kanuni hii inasema kwamba Fasili ya Mstari au kifungu ni lazima izingatie mtajo
kamili au mtajo wote wa ujumbe/somo katika Biblia.
Fundisho la kweli la ki-Biblia huwa na kila kitu ambacho Biblia inazungumza juu
yake.

Ili uweze kuwa na fasili sahihi ni lazima uwe na kila kitu ambacho Mungu amesema
kuhusu jambo hilo.
Unaposoma wazo fulani, tukio fulani au mtu fulani, soma kila Andiko katika Biblia
linalozungumzia jambo hilo au mtu huyo. Matokeo ya usomaji huu hutoa msingi mzuri
ambao kwa usahihi huakisi fundisho zima la Biblia (Bible doctrine).

Hakuna kifungu kinachohusiana na fundisho linalohusika kinachopaswa kuachwa


pasipo kuchunguzwa katika uundaji wa fundisho la ki-Biblia.
Kila kifungu cha Maandiko ni sehemu katika vifungu vyote, katika kujenga, kuelezea
na kujazia vifungu vingine.

Hii ni kusema kwamba vifungu vya Maandiko vinajengana, vinaathiriana,


vinaelezeana na kujazia vifungu vingine vinavyohusiana.

Kanuni ya mtajo kamilifu ni muhimu kwa sababu zifuatazo;

Kanuni ya Mtajo kamilifu ni muhimu kutokana na ukweli wa ufunuo endelevu


 Biblia ni ufunuo toka kwa Mungu. Biblia haikuandikwa kwa siku moja bali
iliandikwa muda wa miaka 1500 na matukio yake yanachukua karibu miaka
4000 tangu wakati wa Ayubu hadi wakati wa mtume Yohana akiwa kisiwa cha
Patimo.
 Kile Biblia nzima inachosema huleta msawazo katika kifungu mahususi
unachokisoma au kujifunza.

Kama kifungu kimoja unachokisoma kinasema kwamba Mungu ni Moto ulao, basi
unaweza kuwa na mtazamo mmoja tu kuhusu Mungu. Waebrania 12:29.
Lakini ukisoma kwa undani utangundua kuwa Mungu wetu ni nuru, pendo, roho n.k.

22
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

Kanuni ya mtajo kamilifu hukuwezesha kusisitiza kile Mungu anachosisitiza.


Kanuni hii inatutaka kuweka mkazo katika maeneo yaliyopewa mkazo na kutoweka
mkazo katika maeneo ambayo hayajapewa mkazo katika Biblia.

Kuna watu ambao wanaweka mkazo katika mambo madogo na kuyapuuza mambo
makubwa. Mafarisayo walikuwa ni sehemu ya watu hawa.
Yesu alisema walichuja mbu na kumeza ngamia. Mathayo 23:24.

Mfano kuna mistari mingi sana katika Biblia inayohusu maombi. Na ndio maana
kanisa la kwanza liliyapa maombi kipaumbele.
Unaweza kushangaa kuona mtu anachukua sehemu ndogo tu ya mafundisho na kuipa
uzito mkubwa na kuifanya msingi katika ushirika na huduma.

BAADHI YA VIKWAZO VYA KUVISHINDA KATIKA KANUNI YA MTAJO


KAMILIFU.
Kununi ya mtajo kamilifu inahitaji kuchunguza vifungu vyote katika Biblia
vinavyozungumzia fundisho fulani unalolishughulikia/kujifunza.
Baadhi ya mafundisho yana rejea chache za mistari katika Biblia, lakini Baadhi ya
mafundisho yana rejea nyingi za mistari katika Biblia.

Baadhi ya mafundisho yenye rejea nyingi ni:-


Maombi, Utakatifu, Ufalme wa Mungu, Haki, Imani, Dhambi, Toba, Wokovu na
Ukombozi.
Baadhi ya mafundisho yenye rejea chache za Maandiko:-
Ubatizo wa wafu na Kutawadha (kuosha) miguu.

MCHAKATO WA KUFUATA KATIKA KUTUMIA KANUNI YA MTAJO


MKAMILIFU
1. Gundua mistari mingine inayohusiana na somo unalolishughulikia (kamusi, na
Itifaki ya Biblia ni zana muhimu katika kipengele hiki)
2. Utazame mstari na kisha jiulize mwenyewe maswali kuhusiana na kila mstari

23
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
 Je! Mstari huu unaongezea nini katika kuelewa dhana hii?
 Je! Ni kipengere gani katika dhana hii ambacho mstari huu unasisitiza?
 Je! Mstari huu unarekebisha mtazamo wangu wa jumla kuhusu somo
hili?

Jambo la msingi na la kuzingatia katika kanuni ya mtajo kamilifu ni kwamba ni lazima


upitie vifungu au mistari yote inayohusiana na kifungu unachokichunguza.

5. KANUNI YA MTAJO MLINGANISHO


Kanuni ya mtajo mlinganisho ni kanuni ambapo mstari au kifungu fulani cha
Maandiko hufasiliwa kwa kulinganisha na kulinganua mistari hiyo na mistari mingine
ya Maandiko.
Mfasili anaposoma neno ni lazima azingatie sehemu zingine za Maandiko zinazotoa
mwanga kuhusu sehemu hiyo anayoisoma.
Katika kanuni hii maneno ya msingi ni kulinganisha na kulinganua.

Kulinganisha uhusisha kuchunguza vifungu vingine vya Maandiko vinavyohusiana na


kifungu unachokishughulikia. Vifungu sambamba, ili kuweza kupata mwanga zaidi
kuhusiana na kifungu hicho.

Kulinganua inahusisha kuchunguza kifungu au vifungu vingine vinavyohusiana na


kifungu hicho lakini kwa mtazamo tofauti.

Katika kanuni ya mtajo mlinganishao wazo kuu ni KUTUMIA MAANDIKO


KUFASILI MAANDIKO (ni kuiruhusu Biblia ijifasili yenyewe).

Mfasili wa kwanza wa Maandiko ni Maandiko yenyewe.

Thomas Watson aliwahi kuandika kwamba. Hakuna kitu kinachoweza kukata almasi
isipokuwa almasi yenyewe. Hakuna kinachoweza kufasili Maandiko isipokuwa
Maandiko yenyewe.

Mfasili bora wa Maandiko ni Maandiko yenyewe

24
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Williamu Curnall aliwahamasisha waamini kulinganisha Andiko na Maandiko.
Alisema kwamba Mafundisho potofu huwa kama mashahidi wawili wa uongo daima,
mashahidi wa uongo huwa hawakubaliani wenyewe kwa wenyewe. Maana hutoa
taarifa zinazokanganya.

Kanuni ya uhakika ya kufasili Maandiko ni Maandiko yenyewe, kwa hiyo


kunapokuwepo na kifungu cha Maandiko ambacho hakiko wazi, kifungu hicho
kinapaswa kusomwa sambamba na vifungu vingine vyenye kuhusiana,
vinavyozungumzia mada sawa na kifungu hicho kwa uwazi.

Kanuni ya mtajo mlinganisho inamwelekeza mwanafunzi kutumia Maandiko katika


kufasili Maandiko.
Kama kifungu hakieleweki, daima kutakuwa na kifungu kingine katika Maandiko
kinachoweza kutumika katika kukieleza kifungu hicho kisicho wazi.

Vifungu tofauti vinavyochangia mawazo sawa pamoja hulinganishwa pamoja. Kifungu


kilicho wazi kinasaidia kuelewa kifungu kisicho wazi.

Uzuri wa kutumia kanuni hii ni kwamba Biblia hujibu maswali yake yenyewe.
Jambo la kuzingatia katika kanuni ya mtajo mlinganisho ni kwamba tunafasili kifungu
kisichowazi kwa kutumia kifungu kilichowazi. (tunafasili kifungu kinachoeleweka kwa
kutumia kifungu kisichoeleweka).

Mfano tazama ubatizo katika Kanisa la kwanza.


Kuna maeneo manne katika Maandiko watu walipojazwa Roho Mtakatifu. Matendo ya
Mitume 2, 8, 10 na 19.

Katika maeneno matatu (3) tunaona wale waliojazwa Roho Mtakatifu walinena kwa
lugha.
1. Mwanzo wa ujazo wa Roho Mtakatifu Mdo 2:4

“Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine kama Roho
alivyowajalia kutamka”.
2. Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu katika nyumba ya Kornelio Mdo 10:46
“Kwa maana waliwasikia wakisema kwa lugha na kumwadhimisha Mungu”.

25
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
3. Kujazwa kwa Roho Mtakatifu wanaume kule Efeso Mdo 19:6
“Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao;
wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri”.

Katika tukio la nne haioneshi kwa uwazi ni ishara gani iliyotokea, japokuwa kwa
hakika kuna kitu cha tofauti kilitokea. Katika tukio hili ni Wasamaria waliojazwa Roho
Mtakatifu. Mdo 8:14-21.
“Hata Simoni alipoona watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya
mitume, akataka kuwapa fedha akisema, Mdo 8:18.

Katika tukio hili, kunena kwa lugha hakutajwi kwa wazi, japokuwa mtu anaweza
kushangaa ni nini Simoni alichokiona? Kwa hakika kuna kitu cha tofauti ambacho
Simoni mchawi alikiona na kikamvutia hadi kutaka kutoa hongo kwa Petro.

Baada ya mtume Petro kumkemea Simoni mchawi kwa maneno yafuatayo.


Huna fungu wala sehemu katika jambo hili ... Mdo 8:21
Neno jambo lililotumika katika kifungu hiki linatokana na neno la Kigriki Logos lenye
maana ya Usemi (Utterance).

Kwa kutumia kanuni ya mtajo mlinganisho na mwongozo wa kufasili kifungu kisicho


wazi kwa kutumia kifungu kilicho wazi tunaweza kuhitimisha kwamba kile Simoni
mchawi alichokiona kinachozungumziwa katika kifungu hiki ni kunena kwa lugha.

Kwa kutumia kanuni ya mtajo mlinganisho hutokeza wazo la kwamba mashahidi


wawili au watatu hujenga msingi wa fundisho la ki-Biblia 2 Wakoritho 13:1
“Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa”

Dini ya Umomoni imehalalisha ubatizo wa wafu kutokana na kifungu kilichopo katika


1 Wakorintho 15:29
Au je! Wenye kubatizwa kwaajili ya wafu watafanyaje kama hawafufuliwi kamwe,
kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?

Je kweli kwamba mtume Paulo anathibitisha kwamba watu walio hai wanaweza
kuwasaidia wafu kwa kubatizwa kwa niaba yao mahali pao?
Jambo hili haliwezi si la kuumiza kichwa kwa sababu kuna shahidi mmoja au mstari
mmoja tu katika Biblia unaozungumzia fundisho hili.

26
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

Je! Mashahidi wenigne wa pili na watatu wako wapi? Kunapoibuka jambo kama hili
katika Biblia lenye utata mashahidi watatu ni:-
1. Agizo la Yesu katika Injili
2. Matumizi (practice) yake katika kanisa la kwanza katika kitabu cha Matendo ya
Mitume
3. Ufahamu wa kitheolojia kama ulivyowekwa wazi katika nyaraka mbalimbali za
mitume

Kama tukitumia kanuni hii katika ubatizo na ushirika mtakatifu ni rahisi kutambua
mashahidi wawili au watatu. Kwa hakika tukitumia kanuni hii katika ibada ya
kuosha/kutawaza miguu na ubatizo kwa ajili ya wafu tutakosa mashahidi
wawili/watatu.

Ibada Agizo la Yesu Matumizi (kutumika Kuwekwa wazi


Ubatizo wa maji Mathayo 28:19 Matendo 2:38-41 Wakolosai 2:12
Ushirika Mtakatifu Luka 22:19 Matendo 2:42 1 Wakorintho 11:23
Kuosha miguu Yohana 13 Hakuna Hakuna
Ubatizo wa wafu Hakuna 1 Wakorintho 15:29 Hakuna
umetajwa tu

Fasili ya Andiko hili haiwezi kuumiza kichwa kwa sababu inaelekea kupingana na
Biblia nzima.
 Biblia inafundisha kwamba kifo ni mwisho Webrania 9:27
“Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa ni hukumu”
 Biblia inafundisha kwamba hakuna nafasi nyingine ya kutengeneza baada ya
kufa
Luka 16:19-31, Ezekieli 18:19-32.
 Biblia inafundisha kwamba hatima yetu ya milele inategemea nini tunafanya
wakati tukiwa hai 1Wakorintho 3:10-15.

Maandiko yanafundisha kwamba Mbingu na Jehanamu ni hali za milele Ufunuo 20:10,


22:5.
Ni muhimu sana kufuatilia kwa umakini kile mtume Paulo anachoongelea katika
kifungu hiki. Ukiusoma kwa umakini mstari huu utagundua kwamba mtume Paulo
hazungumzii kuhusika kwake mwenyewe katika ubatizo wa wafu.
27
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

Katika siku za Paulo kulikuwa na dini za kipagani waliofundisha kuhusu ubatizo wa


wafu, na baadhi yao walikuwa ni wazushi kama vile Marsion.

Katika Korintho kulikuwa na tatizo la wamini katika kuyaacha mafundisho ya dini zao.
Pamoja na kuokoka bado walishikilia mfundisho ya dini zao za kipagani. Waliingia
kanisani pamoja na mafundisho yao.

Hivyo mtume Paulo alitumia kile walichokuwa wanakiamini kuelezea kile


walichokuwa wakikipinga.
Waliamini ubatizo wa wafu lakini hawakuamini ufufuo wa wafu

6. KANUNI YA UCHAGUZI

KANUNI YA UCHAGUZI (Baadhi huiiita Predestination)

Hii inahusish uchaguzi wa Mungu juu ya mtu fulani au taifa fulani kwa kusudi lake.

Aina za uchaguzi

1. Uchaguzi wa muda au kipindi fulan. Mungu huchagua mtu fulani, kundi fulani
au taifa fulani kutimiza kusudi lake mahususi katika kipindi fulani
2. Uchaguzi wa kila mmoja wetu, akiwa na utashi (making free will) na uwezo
wa kufanya uchaguzi utakaoamua hatima yake ya milele

Uchaguzi na ukombozi
1. Uchaguzi ni tendo huru la Mungu. Mungu hakutakiwa kumuokoa yeyote kwa
sababu sisi sote tulikuwa tumepoteza nafasi yetu ya kukubalika mbele za Mungu
2. Kile Mungu anafanya kwetu ni kwa sababu ya neema yake iliyo kuu Rumi (:11,
11:5-6. Kwa hakika hatukustahili kabisa. Ni Mungu ambaye ameamua kutuokoa
kutokana na upendo na neema yake.
3. Uchaguzi (predestination) umejikita katika maarifa (foreknowledge) ya Mungu
juu ya mambo yajayo. 1Petro 1:1-2 Mungu anachagua wale ambao aliwajua tangu
zamani kuwa watamkubali Kristo.

ANGALIZO:-

28
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Hakuna kifungu chochote katika Biblia kinachosema kwamba Mungu
alimchagua mtu fulani kwaajili ya kwenda Jehanam
MUHIMU
Unapochunguza kifungu fulani cha Maandiko
1. Unapaswa kujiuliza swali ikiwa kuna mstari katika kifungu hicho ambao
una muunganiko (connection) na kusudi la Mungu la uchaguzi. Kanuni hii
si lazima ifanye kazi kwa kila mstari na kila kifungu na inafanya kazi kwa
kifungu kile kinachoelezea kweli kuhusu kanuni ya uchaguzi inapokuwa
imehusika.
2. Kanuni ya uchaguzi inakwenda sambamba na kanuni ya Agano. kwa hiyo
kanuni hizi mbili ni lazima zizingatiwe kwa pamoja katika matumizi.

Maandiko
Malaki 1:2-3 “.... Je Esau si ndugu yake Yakobo ? Ila nimempenda Yakobo bali
memchukua Esau
Mwanzo 25:19-34 Hata kabla ya kuzaliwa kwao (Esau na Yakobo) Bwana
alimwambia Rebeka akisema” mataifa mawili yako katika tumbo lake na
kabila mbili za watu na watu hao watafarakana tangu tumboni. Kabila moja
litakuwa hodali kuliko la pili, na mkubwa atamtumikia mdogo.

Ingawa Esau alikuwa mzaliwa wa kwanza Mungu alimchagua Yakobu kuwa


juu ya Esau, kwanini ? Hii ni kwa sababu Mungu anajua Esau namna
atakavyokuwa alijua tabia yake na mwenendo wake utakavyokuwa kwa ujumla
hivyo akaamua kumchagua yakobo badala ya Esau.

Warumi 9:6-24

mistari ya 11 hadi 13 inasema :-

11 Kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema
wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya
matendo bali kwa sababu ya nia yake aitae.

12 Aliambiwa hivi mkubwa atamtumikia mdogo.

29
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
13 Kama ilivyoandikwa nimempenda Yakobo bali Esau nimemchukia.

HITIMISHO

Mungu alimpenda Yakobo na kumchukia Esau kwa sababu alijua (foreknew)


tabia zao na historia za mataifa yao.

7. KANUNI YA AGANO

Dhana ya Agano:-

Agano ni makubaliano maalumu yanayofanywa baina ya pande mbili au zaidi za


watu au makundi ya watu. Katika mkutadha wa KiBilblia neno agano lina
maanisha makubaliano maalumu Mungu aliyofanya na watu makundi ya watu
au mataifa. Katika Biblia tunaona watu wakifanya maagano mbalimbali. mfano
Mwanzo 21:17 Abrahamu na Abimeleki

Mungu huja kwa mwanadamu na kutangaza mapenzi yake na kutaka


mwanadamu aitikie na kutii masharti ya tangazo hilo. Hivyo agano tunaweza
kuliita kwamba ni Mkataba malumu ambao Mungu anauandaa na kuuleta kwa
mwanadamu , mwanadamu anaweza ama kuukubali au kuukataa lakini hawezi
kuubadilisha kwa namna yoyote ile.

Katika Biblia Mungu alifanya Maagano mengi na maagano hayo yanaweza


kugawanywa katika kategoria mbili ambazo ni Maagano yenye masharti na
maagano yasiyo na masharti.

Maagano yenye masharti, Hili ni agano ambalo linamtaka mwanadamu


kutekeleza matakwa (terms) fulani yaliyo kwenye agano hilo ili Mungu aweze
kutekeleza upande wake nay eye.

Aina hiii ya Agano hutumia maneno kama “ Ikiwa, Kama, iwapo na nita, ndipo
n.k

Maagano yasiyo na masharti. Hili ni aina ya agano ambapo Mungu yeyey


mwenyewe anaamua kutimiza ahadi zake zilizoko kwenye agano bila mwitikio
wowote wa mwanadamu au bila mwanadamu kutakiwa kutekeleza masharti
yoyote yale. Mungu anaahidi kutenda pasipo masharti yoyote yale. mfano
Kutoka 6:3-8, Mwanzo 9:11

30
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Sehemu Kuu Mbili katika Maagano Mungu aliyofanya na mwanadamu:-

1. Wokovu, wenye msingi (based on) katika imani


2. Urithi wenye msingi (based on) katika utii.

Vipengere vya Maagano


1. Maneno au ahadi za agano
2. Damu ya Agano
3. Chapa au muhuri wa Agano
4. Wahusika wa Agano

ORODHA YA BAADHI YA MAAGANO MASHUHURI KATIKA BIBLIA

i. Agano la Edeni (agano la masharti) Wakati wa utimilifu au wakati wa bila


dhambi Mwanzo 1:26-30
ii. Agano la Adamu ( agano lisilo la masharti) Wakati au kipindi cha dhamiri)
Mwanzo 3:1-24
iii. Agano la Nuhu (agano lisilo la masharti) Wakati wa madaraka au utawala
wa mwanadamu Mwanzo 8-9
iv. Agano la Ibrahimu (Agano lisilo la Masharti) Wakati wa ahadi au kipindi cha
Mababa/wazee Mwanzo 12:1-3, 15, 17,22
v. Agano la Musa (Agano la Masharti) Wakati au kipindi cha sheria Kutoka
20-40
vi. Agano la Palestina (Agano la Masharti) Wakati wa sheria Kumb 27-30
vii. Agano la Daudi (agano lisilo la Masharti) Wakati wa sheria 2Samweli 7:4-
29, Zaburi 89
viii. Agano Jipya (agano lisilo la masharti) Wakati au kipindi cha Neema au
kanisa Yeremia 31:31-34, Mathayo 26:29, Waebrania 8-9

NAMNA YA KUTUMIA KANUNI YA MAAGANO KATIKA KUFASIRI


MAANDIKO

Unaposoma kifungu cha habari katika Biblia ni muhimu kutambua muundo wa agano
wa Biblia. Unapaswa kutambua agano ambalo lilikuwa likifanya kazi katika kipindi
hicho andiko hilo lilipoandikwa au kutolewa. unahitaji kujua namna agano hilo

31
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
lilivyoathiri maisha ya watu wakati huo. unatakiwa kujua namna agano hilo
lilivyohusiana na maagano mengine . Huu ndio ufungua wa kufungua habari nyingi.

Mambo ya kuzingatia

i. Baini kama habari unayosoma ina lugha ya agano


Si kila andiko laweza kuingia katika kipengere hiki. Inapokuwa hakuna lugha
ya agano kanuni hii ya agano haitumiki

ii. Baini aina ya agano au maagano yanayohusika


kuna matukio machache ambapo maagano zaidi ya moja yanarejelewa
katika kifungu cha maandiko. Mfasiri ni lazima awe mwangalifu kupangilia
kujua maudhui au mafundisho ya kila gano ambalo limerejelewa na kifungu
hicho cha habari. Ezekieli 15:59-62, Warumi 9-11, Wagalatia 3:1-29.

iii. Kubaini kategoria ya agano yaani kutambua kama agano nila masharti au si
la masharti.
iv. Kutambua kama agano hilo limetimizwa katika Agano Jipya. Mfano ahadi
ya Agano la Daudi imetimizwa na Yesu Kristo na katika Kanisa katika
Agano Jipya. 2Samweli 7:14-17, Isaya 9:7, Yeremia 33: 17, Luka 1:32.
v. Kufasiri Agano kwa mtazamo wa msalaba wa Yesu na Agano Jipya.
Maagano yote yana kipengere cha alama (symbol) karibu vipengere vya
kila agano yanaonesha au kuelekeza utimizo wake katika agano jipya.
Mfano , damu ya Agano kwa hakika inaelekeza kwa Yesu Kristo na damu
yake aliyoimwaga pale kalvari.

MATUMIZI YA KANUNI YA AGANO


i. Agano la Edeni
ii. Ufunuo 2:7b
Ufunuo 22:14

Ili uweze kutoa fasili sahihi ya mistari hii ni lazima urejelee kwenye agano la Edeni.
Hii ni kwa sababu chini ya Agano hili mti wa uzima umetajwa kwa mara ya kwanza.
Adamu na Hawa walipoteza haki ya kula matunda ya mti wa uzima
waliposhindwa kutii masharti ya agano la Edeni walipokula matunda ya mti wa ujuzi
wa mema na mabaya ambao walikatazwa wasile. Hivyo hawakushinda kwa sababu
hawakutekeleza amri yake na wakapoteza haki ya mti wa uzima. (mwanzo 2:8-17,
3:22-24.
32
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Mpango wa Mungu utakapokuwa umetimia kikamilifu ushindi utakujua tena juu ya
kile kilichopotea

Agano la Adamu

Warumi 12:20

ili kuweze kutambua matmizi kamili ya mstari huu ni lazima msitari uchunguzwe kwa
nuru ya Agano la Adamu. Baada ya kuingia kwa dhambi katika maisha ya
mwanadamu, Mungu alimwambia nyoka (shetani) Nitaweka uadui kati yako na
huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake, huo utakuponda kichwa na
wewe utauponda kisigino. (mwanzo 3:15).

Mstari wa Warumi unazungumzia kuelekea utimizo wa mwisho wa kinabii wa


Agano la Adamu. Kwa hiyo mstari huu ( Warumi 16:20) unatoa
uhakikisho/uthibitisho wa ahadi ya kwanza ya Kimasihi ya ukombozi.

Agano la Nuhu

Ufunuo 4:3

Mstari huu unapaswa kufasiliwa kwa kuhusishwa na agano la Nuhu. Upinde wa mvua
wa kwanza uliwekwa mawinguni kuwa ukumbusho kwa Mungu na mwanadamu kuwa
Mungu hangeangamiza dunia tena kwa maji. (mwanzo9:17)

Upinde wa mvua katika kiti cha enzi unaonesha kwamba Mungu anatunza mhuri wa
Agano la Nuhu daima mbele zake akithibitisha uaminifu wake kwa ahadi yake.

Agano la Ibrahimu

W agalatia 3:29

Haiwezekani kufasili mstahi huu kwa usahihi pasipo kutazama vitu vinavyohusika
katika Agano la Ibrahimu. kama ilivyoelezwa hapo awali. Ibrahimu alitakiwa kuwa
baba wa vizazi viwili ambavyo ni uzao wa kiroho na uzao wa kimwili ( Mwanzo
13:16, 15:5). Uzao wa kimwili ulihusika na urithi wa nchi, watoto, na milki.(mwanzo
12:1-3, 22:16-18)
33
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Ahadi ya kiroho (uzao wa kiroho) ilihusika na masihi na huduma yake kwa mataifa
yote ya dunia. Ahadi hii inahusisha kuhesabiwa haki kwa imani na kumpokea Roho
Mtakatifu. (wagalatia 3:8). Hivyo basi mstari huu unaeleza kwamba mtu ambaye ni
mali ya Yesu amekuwa uzao wa Ibrahimu na anamahusiano ya kimaagano na
Mungu. akiwa mrithi wa ahadi ya Agano la Ibrahimu kupitia Yesu Kristo.

Agano la Musa
Wakolosai 2:16-17

Ujumbe wa msitari hiyo inaweza kueleweka kwa kuihusianisha mistari hiyo na


Agano la Musa. Chini ya Agano la Musa Waisraeli waliamuliwa kushika au kutunza
siku ya sabato, sikukuu, miezi nyakati za kusanyikona miaka ya yubilei. Mambo ya
Walawi 23,25. Katika walaka kwa Wagalaia mtume Paulo anaeleza kwamba mambo
haya yote yalikuwa katika Agano la Sheria. Kwa Waamini wa Kolosai ambao wao
walikuwa wanaishi katika kipindi cha Agano Jipya , kuendelea kushika mambo haya
ilikuwa ni kurudi tena katika kipindi cha Agano la sheria yaani Agano la Musa.

Agano la Daudi

Luka 1: 32-33.

Mistari hii inapaswa kufasiliwa kwa kuihusianisha na ahadi ya Agano la Daudi.


Ahadi hii ina vitu vinne vya msingi ndani yake. ambavyo ni

 Uzao (Seed)
 Nyumba (House)
 Kiti cha enzi (Throne)
 Kingdom ( Ufalme)

Mistari ya Injili ya Luka iliyotajwa hapo juu ilitabiri kwamba vitu hivi vinne
vingepata utimizo wake katika Bwana wetu Yesu Kristo mwana wa Daudi au wa uzao
wa Daudi.

Agano Jipya

Yeremia 31;31-33

Unabii huu unaweza kueleweka kwa kuuhusianisha na utimizo wake wakati


Masihi (Yesu) alipoanzisha Agano Jipya. Siku ambazo Yeremia alitabiri
zinaonesha kuwa ni siku za Masihi ambazo katika hizo alianzisha Agano Jipya.
34
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)

8. KANUNI YA MAADILI (Moral Principle)

Kanuni ya Maadili ya Fasili ya Maandiko

ni kanuni ya kufasili Maandiko inayomsaidia mfasili kupata ukweli


usiobadilika (time less truth) kutokana na wakati kupita kutoka katika kifungu
cha Maandiko na kutumia katika ulimwengu wetu wa sasa.

A. Wakorintho 10:5-11

Si kila kitu kilichotokea katika kipindi cha agano la kale kimeandikwa kwaajili
yetu katika Biblia. Kwa hakika hakuna historia nzima ya mtu yeyote katika
Biblia. Mungu aliamua kuandika matukio ambayo aliamua yeye kulingana na
kusudi lake takatifu. Lengo lake ni kutusaidia sisi kuingia katika mpango wake
kamilifu kwaajili ya maisha yetu na kututayarisha kuwa tayari wakati Bwana
Yesu atakaporudi.

B. Yohana 21:24-25
Si kila kitu alichokifanya Yesu Kristo akiwa hapa duniani kimeandikwa katika Biblia
yaani katika Agano Jipya. Yale ambayo yameandikwa yametolewa kwetu kwa lengo
la kutufunza sisi njia ya wokovu. Tukitazama matukio mbalimbali ya maisha ya Yesu
yaliyoandikwa katika Biblia tunaweza kupata kanuni ya kweli isiyobadilika
kulingana na wakati kupita. (Timeless Principle).

C. Warumi 15:4
Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa, yaliandikwa ili kutufundisha sisi;
ili kwa saburi na faraja ya Maandiko tupate kuwa na tumaini.

D. 2Timeotheo 3:14-17
Biblia imetolewa kwetu ili kutufanya tuwe na hekima, kukuza imani,
kutufundisha sisi namna ya kuishi na kutuandaa kwaajili ya maisha na
huduma. tunapokea haya kutoka katika Neno tunapochunguza kweli
isiyobadilika kulingana na wakati kupita ambayo inapatikana katika matukio
mbalimbali yaliyoandikwa katika Biblia.

35
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
II. Nini kweli ya Kimaadili au Kanuni ya Kimaadili.

Kamusi zinafasili neno hili “maadili kwa namna mbalimbali kama ifuatavyo

1. Funzo au kanuni iliyomo katika hekaya, hadithi au tukio


2. Ujumbe au funzo lililowasilishwa ili kujifunza kutoka katika hadithi au
tukio.
3. Amri iliyoelezwa kwa usahihi, ukweli wa jumla, au upeo
4. Ni mambo ya kimaadili yanayopatikana katika tukio au hadithi.

Kamusi inaelezea neno Moralize kama kupata maadili kutoka katika kitu
fulani. au kufanya maadili kuakisi kuhusu kitu fulani au kuelejea jambo
fulani kwa mtazamo wa kimaadili.

Wajibu mkuu wa mfasili ni kufungua au kuweka wazi uelewa wa watu ili


kuwasaidia kupata funzo la kiroho kutoka katika matukio mbalimbali katika
Biblia kama yalivyowasilishwa. Kwa mfano unaweza kutazama maisha ya Daudi,
Eliya, Musa, na kupata kanuni ya kweli isiyobadilika kulingana na wakati kupita
inayohusika na mahusiano yetu na Mungu.

III. Sababu za kutumia kanuni ya kimaadili katika kufasili Maandiko

Tunahitaji kutumia kanuni hii katika kufasili Maandiko kwa sababu si kila
kweli isiyobadilika kutokana na wakati kupita imeelezwa kwa uwazi katika
Biblia Mithali 25:2

Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo, bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza


jambo.

Mambo mengi ambayo Biblia inatuambia yamewasilishwa kwa maelezo ya


kweli kwa uwazi,kifupi, mafundisho, na kwa lugha isiyokosea. Japokuwa
mengi ya mambo hayo yaliyowasilishwa yamefungwa kwa kiwango fulani cha
siri na tunatakiwa kuyavumbua kwa kutumia kanuni ya kimaadili.

Je twaweza kujifunza kitu fulani kutoka kwa waamuzi mbalimbali katika Biblia
? au kwa wafalme mbalimbali waliotawala katika Israeli na Yuda ?

36
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
vipi kuhusu mafunzo tunayoyapata kutoka katika maisha ya Ayubu, kitabu
cha Ruthu, na Esta ? Tunaweza kujifunza nini kutokana na kifo cha Sauli
mfalme wa kwanza wa taifa la Israeli? 1Mambo ya Nyakati 10:13-14

Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa Bwana, kwa sababu ya
neno la Bwana asilolishika. Na tena kwa kutaka ushauri kwa mwenye pepo wa
utambuzi, aulize kwake, asiulize kwa Bwana, kwa hiyo akamuua, na ufalme
akamgeuzia Daudi mwana wa Yese.

Katika matukio mengi kweli zitakazokuwa zimepatikana zitatokana na namna


wahusika walivyoishi, walivyoitikia kutokana na mazingira katika maisha yao na
namna walivyohusiana na watu wengine.

kama wahenga wanavyosema, nyuma ya kila tukio la kihistoria katika Maandiko


kuna kuwa na funzo la kimaadili au funzo la kiroho ambalo lina lengo la kufundisha.

Namna kanuni ya kimaadili ya kufasili Maandiko inavyotumika.

A. Kanuni ya Kimaadili ya fasili inaweza kutumika karibu kwa kila kifungu


katika Biblia. Karibu sehemu kuu ya inayotumia kanuni ni katika vifungu
vyenye simulizi (narrative portions) . hii inahusisha vitabu vya kihistoria, na
mifano na matukio ya miujiza ya Yesu.

B. kanuni ya Kimaadili ya Fasili inaweza kufungumanishwa pamoja na kanuni


zingine zote.
Wakati kanuni zingine zote za Fasili zimejikita katika kupata fasili hasa ya
kifungu na maana yake ya kiuhalisia , kanuni ya kimaadili ya fasili inajikita
katika kweli isiyobadilika kutokana na wakati kupita inayopatikana kutokana
na kukielewa kifungu kwa usahihi.

C. kanuni ya kimaadili ya fasili inaweza kunyumbuka kwa kiwango cha


kwamba kweli zaidi ya moja isiyobadilika kutokana na wakati kupita
zinaweaa kupatikana kutoka katika kifungu kimoja.

D. Kanuni ya Kimaadili ya Fasihi ni lazima ikubaliane (isiwe na mgongano) na


matmizi ya kanuni nyingine za hermeneutics na Theolojia ya Biblia.

37
By Rev. Dr. Erick L. Mponzi (Dip. Min, BEDCP, B.Th, M.Min, ThD)
Njia mojawapo za kumsadia mfasili ili kuweza kuelewa kanuni ya kimaadili
ya fasili ni kutumia kiambatisho cha orodha ya sifa za wahusika katika
mada hii. Unapokuwa unasoma kifungu unawza kujiuliza maswali. Je!
kifungu hiki kinatufundisha kitu chochote kuhusina na tahadhari , umakini
au upatikanaji n.k ?

ukatapokuwa umepitia orodha ya sifa za wahusika vutawaona wo katika


utendaji katika simulizi nyingi zilizoandikwa katika Biblia.

38

You might also like