You are on page 1of 71

P.O.

BOX 1917 MBEYA TANZANIA


E-mail. elamseminary@gmail.com. TEL. 0762532121

Luka 10:2

Kuwaanda Watendakazi Kwaajili Ya Mavuno Ya Nyakati


Za Mwisho
Msingi wa Kujenga Watendakazi na Viongozi
Watumishi Wanaojizidisha na wenye Maono ya
Kuigusa Dunia Nzima.

SAFARI
YA
MSAFIRI

Kimetungwa na

John Bunyan

2
DIBAJI

SAFARI YA MSAFIRI ni kitabu kimojawapo cha vitabu mashuhuri na


kipendwacho sana katika ulimwengu. Kina msaada kwa Mkristo wa kisasa kama
kilivyokuwa msaada kwa Jihn Bunyan alipokiandika yapata miaka mia tatu
iliyopita.

Hiki si kitabu kinachohusu wakati fulani au mahali. Ni picha ya maarifa ya


Wakristo wa zamani zote na katika kila nchi. Hadithi hii inasimulia magumu na
furaha aliyonayo Mkristo asafiripo kutoka Mji wa Uharibifu (yaani ulimwengu
huu) kwenda Mji wa Mbinguni. Tunapokisoma tunashiriki taabu za Msafiri
anapojitahidi kulipitia Ziwa la Kukatisha Tamaa, lenye matope mengi huku
akichukua mzigo mzito wa dhambi. Tunashangilia pamoja naye katika uhuru wake
wakati mzigo unapovingirika kutoka mgongoni mwake mbele ya msalaba.
Tunatetemeka pamojna naye anapopitia Bonde la uvuli wa Mauti na anapokuwa
katika mamlaka ya jitu ovu Kukata-Tamaa. Tunayo matumaini pamoja naye
auonapo Mji wa Mbinguni, na hatimaye twashangilia anapokuwa amekwisha
uvuka mto na kuuingia huo mji mzuri.

3
MSAFIRI AUACHA ULIMWENGU HUU

Maendeleo yake

Hapo nilipokuwa nikitembea katika bara la ulimwengu huu, nilifikia pango, hapo
nilijilaza na kulala usingizi; na katika kulala kwangu nikaota ndoto. Katika kuota
kwangu nilimwona mtu mwenye nguo zilizoraruka-raruka, jina lake Msafiri;
alionekana kuwa mtu takaye kuanza safari. Naye alikuwa na kitabu mikononi
mwake. Alikuwa na mzigo mkubwa mgongoni mwake, nao ni mzito sana
(Zab 38:4). Nilimwona akifungua kile kitabu kukisoma. Na alipokuwa katika
kukisoma kitabu hicho alitetemeka na kulia, “Nifanye nini mimi”? (Mdo 16:30).

Basi aliingia tena nyumbani mwake, huku akifadhaika zaidi. Akawaambia mkewe
na watoto: “Ninafadhaika sana kwa sababu nimeambiwa katika Maandiko kwamba
mji wetu huu utateketezwa kwa moto kutoka mbinguni.
Tutaangamia sote tusipotafuta njia ya kujiokoa.

Mkewe na watoto walishangazwa na kuingiwa na hofu, maana walimwona kuwa


amerukwa na akili. Walimwambia aende kulala; lakini hakulala usingizi, ila
alidumu usiku kucha akipiga kite na kulia. Asubuhi yake aliona hali yake inazidi
kuwa mbaya , akajaribu kusema na mkewe na watoto kama kwanza, lakini wao
walimjibu kwa ufedhuli pengine walimcheka na pengine walimwacha tu
wasimwangalie.

Kwa muda wa siku kadha alitembea peke yake mashambani. Mara nyingine alisali
na mara nyingine alisoma kitabu chake; lakini alisumbuka kila mara. Katika
kukisoma kitabu chake alisononeka mno na kulia, “Nifanye nini nipate kuokoka”?
Akatazama huku na huko, kana kwamba anataka kukimbia, lakini hakujua
akimbilie wapi.

4
MSAFIRI AKUTANA NA MWINJILISTI

Kisha nilimwona mtu jina lake Mwinjilisti akimjia Msafiri na kumwuliza, “Je,
unalilia nini?” Akajibu, “Bwana mkubwa, kwa kusoma kitabu hiki nimepata kujua
kwamba imenipasa kufa na baada ya hayo sina budi kuhukumiwa, nami sitaki
kufa na siwezi kuthubutu kukutana na hukumu hiyo”.

Kisha Mwinjilisti akasema, “kwa nini hutaki kufa, hali kuna maovu mengi katika
maisha haya?” Msafiri akajibu, “kwa sababu naogopa kuwa mzigo huu nilio nao
mgongoni utanizamisha chini mno kuliko kaburi. Kweli bwana, mimi sipendi kufa
na kwenda hukumuni.”

Kisha Mwinjilisti akasema, “Iwapo hii ndiyo, hali yako, mbona wabaki kusimama
hapa?” Akajibu, “Kwa sababu sijui niende wapi.” Ndipo Mwinjilisti akampa
Msafiri gombo la chuo. Ndani yake liliandikwa, “Ikimbie ghadhabu itakayokua”
(Mt 3:7). Akiisha kulisoma gombo la chuo, akamtazama sana Mwinjilisti, na
kusema “Nikimbilie wapi?

Msafiri akutana na Mwinjilisti

Mwinjilisti akaonyesha kwa kidole chake eneo pana la nchi na kusema, “Je,
wauona ule mlango mdogo mwembamba?” (Mt 7:13-14). Msafiri hakuweza

5
kuuona mlango huo, walakini alifikiri aliweza kuuona mwangaza tu. Kisha
Mwinjilisti akasema, “Kaza macho yako kwenye mwangaza huo, nawe nenda moja
kwa moja kuuelekea na hatimaye utaliona lango. Ukiligonga hilo lango, mtu
atatokea na kukuambia yakupasayo kufanya.”

Basi nikaona katika ndoto yangu kwamba Msafiri huyo kwa utii alianza kukimbia.
Kabla hajafika mbali mkewe na watoto walianza kumwita ili awarudie (Lk 14:26).
Lakini Msafiri hakutaka kuwasikiliza, naye akakimbia huku akipiga kelele,
“Uzima! Uzima! Uzima! wa milele!” Hakugeuka nyuma, bali aliendelea kupiga
mbio nje ya mji ule, kuelekea katikati ya uwanda.

MSHUPAVU NA MSIKIVU WANAMFUATA

Mshupavu na
Msikivu
wanamfuata

Jirani zake
walipomwangalia
akikimbia, baadhi
yao walimcheka na wengine walijaribu kumtisha. Wengine wakamwita arudi. Kati
ya hao walikuwapo wawili waliokaza nia kumshika na kumrudisha nyumbani kwa
nguvu. Majina yao ni Mshupavu na Msikivu.

Msafiri alikuwa amekwisha kwenda kitambo wakati Mshupavu na Msikivu


walipomfikia. Akawauliza, “Kwa nini mmekuja?” Wakamjibu, Tumekuja
kukushawishi urudi pamoja nasi”. “Hilo haliwezekani”, alijibu Msafiri. “Ninyi
mnaishi katika mji wa uharibifu ambamo nilizaliwa na mimi pia. Mtakufa humo na
kuzama chini kuliko kaburi mpaka mahali pawakapo moto wa milele. Njoni jirani
zangu wema, ili tufuatane. “Nini!” alijibu Mshupavu. “Tuwaache nyumba rafiki
zetu wote na starehe zote tufuatane nawe?”

6
“Ndiyo”, alisema Msafiri; “kwa sababu hayo yote hayawezi kufananishwa hata
kidogo na hayo ninayoyatazamia. Na iwapo mna nia kwenda nami, mtayapata hayo
yote.”

“Je, ni mambo gani unayoyatafuta hali unaucha nyuma ulimwengu, ili uweze
kuyapata?” aliuliza Mshupavu.

“Nautafuta urithi usio haribika, usio na uchafu, usionyauka, (1 Pet 1:4). Urithi huo
uko mbinguni, nao ni salama na tayari kupewa kwa wakati wake wale wautafutao
kwa bidii. Waweza kusoma mwenyewe katika kitabu changu.”

“Lo! Kitabu chako na kipotelee mbali”, alijibu Mshupavu. Je, utarudi pamoja nasi
au sivyo?” alimaliza. “La hasha, sitarudi nyuma hata kidogo”, alijibu Msafiri.

Ndipo Mshupavu alimgeukia Msikivu: “Ee bwana, njoo twende nyumbani peke
yetu. Huyu mpumbavu amejaa ujinga mtupu.” “Usimcheke”, alijibu Msikivu
“Ikiwa ayasemayo ni ya kweli, yeye atakuwa heri kuliko sisi. Nafikiri nitafuatana
naye.

“Loo! Mpumbavu mwingine zaidi”, Mshupavu alishangaa na kughadhabika. “Ni


vema kama ungerudi nami. Nani ajuaye mahali atakapokufikisha mkichaa huyu?
Twende usiwe mpumbavu!”

Akimgeukia Msafiri, Msikuvu aliuliza: Je, rafiki unajua njia iendayo mahali
upatafutapo?” “Ndipo Mwinjilisti aliniambia kwamba kuna lango dogo chini ya
uwanda, na kwamba nikilifikia na kugonga mtu atatokea na kuniambia yanipasayo
kufanya.” Msikivu akajibu, “Vema, twende nitafuatana nawe.” Lakini Mshupavu
alikataa, akasema: “Mimi siwezi kuwa mwenzi wa watu wapumbavu na wajinga
kama hawa.” Baada ya Mshupavu kugeuka na kuwaacha, Msikivu na Msafiri
waliongea walipokuwa wakitembea uwandani.

“Ebu, Msafiri, niambie zaidi habari za mambo hayo ya huko tuendako”, alisema
Msikivu.

7
“Ni rahisi kwangu kuyawaza kuliko kuyasimulia. Lakini kwa vile wataka kuyajua
nitakusomea habari zake katika kitabu changu,”

“Ndipo, pasipo shaka, alijibu Msafiri. Maana kitabu kimeandikwa na yeye


asiyeweza kusema uongo ( Tit 1:2).
“Vema kweli kabisa. Ni mambo gani hayo?” Aliuliza Msikivu.

“Upo ufalme usio na mwisho, na uzima wa milele tutakaopewa ili tuweze kuishi
katika ufalme huo milele” (Yn 10:27-29).
“Kuna zaidi?” Aliuliza Msikivu.
“Ndiyo, alijibu Msafiri. Tutapewa taji za utukufu na mavazi yatakayotufanya
tung’ae kama jua” (2 Tim 4:8; Mt 13:43).
“Hayo ni mema sana; je, kuna zaidi tena?” aliuliza Msikivu.
“Hapatakuwa na kilio kabisa, wala majonzi yawayo yote, kwa kuwa yeye mwenye
mahali hapo atayafuta machozi yote katika macho yetu,” alijibu Msafiri;
(Ufu 7:16-17; 21:4).

“Lakini twawezaje kuyafurahia hayo yote?” aliuliza Msikivu.


“Bwana Mtawala wa nchi hiyo, amekwisha yaandika hayo katika kitabu hiki
(Isa 55: 1-2). Iwapo tunataka kweli kumpokea Yeye, atutapa yote bure,” alijibu
Msafiri.

“Vema Msafiri mwema, ninafurahi kusikia mintaarafu hiyo yote. Haya na tukaze
mwendo.”
“Lakini siwezi kwenda upesi nitakavyo kwa sababu ninao mzigo huu mgongoni,”
alijibu Msafiri.

ZIWA LA KUKATISHA TAMAA

Basi niliona katika ndoto yangu, ya kwamba hao wawili walilifikia bwawa lenye
matope sana katikati ya huo uwanda. Kwa sababu hawakuiangalia njia sawa sawa,
wote wawili walitumbukia kwa ghafula, wakaanguka matopeni. Jina la bwawa hilo
lilikuwa Ziwa la Kukatisha Tamaa. Wakagaagaa kitambo na wakafunikwa na

8
matope pote mwilini. Msafiri alianza kuzama matopeni kwa sababu ya ule mzigo
mgongoni mwake.

Ziwa la Kukatisha Tamaa

Msikivu alikasirika na kusema, “Hii ndiyo furaha uliyokuwa ukinipasha habari


zake? Iwapo tunapata mashaka kama haya mwanzoni, tuna matumaini gani kabla
ya kumaliza safari yetu? Nikijaliwa kutoka ziwani humu mzima, utaweza
kuendelea na safari peke yako.”

Kisha Msikivu akakazana kwa nguvu na mwishowe akajitoa katika matope kwa
upande wa nyuma walikoingilia. Naye akaenda zake, na Msafiri hakumwona tena.
Hivyo Msafiri aliachwa peke yake akigaagaa katika ziwa la Kukatisha Tamaa.
Akazidi kujitahidi upate kuufikia upande wa pili wa ziwa uliokuwa karibu zaidi na
lango lile dogo. Lakini hakuweza kutoka mle ziwani kwa sababu ya ule mzigo
mgongoni mwake.

MSAADA ANAMFIKIA MSAFIRI

Ndipo nikaona katika ndoto yangu kwamba mtu aitwaye Msaada alimjia Msafiri na
kumwulia anafanya nini pale.

Msafiri akajibu, “Bwana mkubwa, mimi niliambiwa na mtu aitwaye Mwinjilisti


kuifuata njia hii. Aliniambia kuliendea lango lile kule ili nipate kuokoka na hasira
inayokuja. Basi nilipokuwa nikienda kule nilitumbukia ziwani humu.

9
“Lakini kwa nini hukutazama! Kwani kuna ngazi za mawe zilizowekwa katika
tope; kama ungezitumia ungalivuka salama mahali hapa.”

“Nilikuwa katika haraka ili niweze kulifikia lile lango,” alisema Msafiri. “Kwa
hiyo nilichukua njia ya mkato, nami nikatumbukia humu ziwani,” Msafiri
alijieleza.

Msaada unafikia Msafiri

Kisha Msaada akasema, “Lete mkono wako. Ndipo akamtoa nje na kumwambia
aendelee na safari yake.

MSAFIRI AENDA KWENYE KIJIJI ADILI, AKUTANA NA BWANA


HEKIMA-YA- DUNIA.

Basi Msafiri alipokuwa akitembea peke yake alimwona mtu akimjia akipitia
kondeni kuja kumlaki. Jina lake mtu huyo lilikuwa Bwana Hekima-ya-dunia, naye
akiishi katika mji uitwao Shauri-la-mwili. Huu ulikuwa mji mkubwa sana, si mbali
na mji ule alikotoka Msafiri. Mtu huyo alikwisha sikia habari za Msafiri.

Unakwenda wapi na mzigo huo? Aliuliza Bwana Hekima-ya-dunia


“Ninakwenda kwenye lango lile kule, alijibu Msafiri.
“Nimembiwa huko nitautua mzigo wangu mzito.”
“Je, utasikia kama nikikupa ushauri?” aliuliza Bwana Hekima-ya- dunia.
“Kama ni ushauri bora, ndiyo,” alijibu Msafiri; kwa sababu nahitaji msaada.”

“Nitakushauri kuutua mzigo wako upesi. Hutatulia moyoni mwako kamwe mpaka
hapo utakapoutua, wala huwezi kuzifurahia baraka ulizojaliwa na Mungu, alisema
Bwana Hekima-ya-dunia

10
“Hayo ndiyo ninayoyatafuta.” Lakini siwezi kuutua mzigo huu kwa haraka peke
yangu, na wala hakuna mtu katika nchi yetu anayeweza kunitua. Ndiyo maana
ninakwenda njia hii, kama nilivyokuambia, ili nipate kuondolewa mbali mzigo
huu,” alisema Msafiri.

“Ni nani aliyekuambia uende njia hii?” aliuliza Bwana Hekima-ya-dunia.


“Mtu aitwaye Mwinjilisti, alijibu Msafiri.
“Lakini hakukupa shauri jema,” alisema Bwana Hekima-ya-dunia. Utaona ya kuwa
hii ni njia ya hatari na taabu. Naona ya kuwa umekwisha pata taabu tayari. Uchafu
wa matope ya Ziwa la Kukatisha Tamaa unao katika nguo zako. Bwawa hilo ni
mwanzo tu wa taabu zako. Utaona uchovu na maumivu, njaa, kuwa uchi, hatari ya
kuuliwa na simba, giza, na mwishowe mauti. Kwa nini mtu pasipo kufikiri ajitupe
katika mambo kama hayo kwa kumsikiliza mgeni?”

“Lakini mzigo huu nilionao mgongoni ni wa kuogofya kwangu kuliko mambo


hayo yote uliyoyataja,” alisema Msafiri. “Sijali ni mambo gani nitakayoyakuta
njiani mradi nikiondolewa mzigo huu”

Msafiri katika njia isiyo sawa

“Ulipataje kujua habari za mzigo huu?” aliuliza Bwana Hekima-ya-dunia.


“Nilizipata kwa kusoma kitabu hiki nilicho nacho mkononi,” alijibu Msafiri.
“Ndivyo nilivyodhani,” alinung’unika Bwana Hekima-ya-dunia. “Jambo hilo hilo
limewapata watu wengine wanyonge. Lakini kwa nini unajaribu kujiweka huru

11
kutokana na mzigo wako kwa njia hii ambayo imejaa hatari nyingi. Kama
ungenisikiliza ningalikuonyesha jinsi ya kukipata kile ukitakacho bila hatari
zozote. Badala yake ungaliupata usalama, urafiki na raha msatarehe.”
“Tafadhali niambie niwezavyo kuyapata hayo,” alisema Msafiri.

“Katika kijiji kiitwacho Shauri-la-mwili anakaa mtu jina lake Haki”, alieleza
Bwana Hekima-ya-dunia. “Yeye anaweza kuwasaidia watu kuitua mizigo kama hii
toka mabegani mwao. Najua amefanya mema kadha wa kadha kwa njia hii.
Nyumba yake haipo mbali, na waweza kwenda huko na kuondolewa mzigo wako.
Kama hutaki kurudi huko ulikokaa kwanza waweza kumtuma mtu kuwaita mkeo
na watoto. Maisha yako yatakuwa na furaha sana kwa sababu utaishi karibu na
majirani wema. Tazama, njia ni ile, kupitia kile kilima kule.”

MSAFIRI KATIKA NJIA ISIYO SAWA

Msafiri hakujua la kufanya. Hatimaye alifikiri kuwa huenda aliyoambiwa yakawa


kweli; basi ni vema alifuate shauri alilopewa na mtu yule. Hivyo aliiacha njia yake
na kwenda nyumbani kwa Bwana Haki ili kuomba msaada. Lakini alipofika karibu
na kilima ambacho ingempasa kukipitia, aliogopa kuendelea mbele. Kilima
kilionekana ni kirefu mno na miamba ilikuwa kama inainama upande juu ya njia.
Msafiri aliogopa, huenda ikamwangukia kichwani. Sasa mzigo wake ulikuwa
mzito zaidi kuliko mwanzoni.

Kisha miali ya moto ikatoka kilimani, naye Msafiri aliogopa asije akateketea
(Kut 19:16, 18). Akaogopa sana akaanza kujuta kwa vile alilifuata shauri la Bwana
Hekima-ya-dunia.
Kisha alimwona Mwinjilisti akimjia, naye akaanza kutahayari sana.

“Unafanya nini hapa Msafiri?” Aliuliza Mwinjilisti. Lakini maskini, Msafiri


hakuwa na la kusema. “Wewe siye niliyekuona unalia nje ya Mji wa Uharibifu?”
“Naam, ni mimi,” alijibu Msafiri.
“Je, mimi sikukuonyesha njia ya kwenda hadi penye lango dogo? Mbona basi
umegeuka na kuiacha njia ile mara hii? Hivi sasa humo katika njia ile”, alimaliza
Mwinjilisti.

12
Kisha Msafiri akasema, “Nilikutana na mwungwana mmoja aliyeniambia kwamba
humo kijijini ningeweza kumwona mtu ambaye angeniondolea mzigo wangu. Basi
nilipofika hapa na kuona hali ya njia, nikasimama kwa vile niliogopa kilima
kisiniangukie. Sasa sijui la kufanya.”

“Basi simama kidogo,” alisema Mwinjilisti; “nami nitakuonyesha maneno ya


Mungu.” Msafiri aliposimama huku akitetemeka, Mwinjilisti akasoma hivi,
angalieni msimkatae yeye anenaye. Maana ikiwa hawakuokoka wale waliomkataa
yeye aliyejiepusha na yeye atuonyaye kutoka mbinguni” (Ebr 12:25). “Lakini
mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha
naye.” (Ebr 10:38). Naye akayaeleza maneno hayo hivi, “wewe ndiye mtu huyo
unayejitia katika mashaka hayo. Umeanza kulikataa shauri lake aliye juu sana, na
kuiacha njia ya amani.”

Ndipo Msafiri alianguka miguuni pake akilia, “Ole wangu, maana nimeangamia!”
Mwinjilisti alipoona hivi, alimshika mkono akasema, “Kila dhambi na kila neno la
kufuru watasamehewa wanadamu (Mt 12:31). Usiwe asiyeamini, (Yn 20:27).
Kisha Msafiri akajiona hajambo kidogo, na Mwinjilisti akaendelea kusema,
“Sikiliza hayo nitakayokuambia. Mtu Yule aliyekudanganya anaitwa kwa haki
Bwana Hekima-ya-dunia, kwa sababu anayafuata mafundishao ya dunia tu
(1 Yn 4:5). Anayapenda mafundisho hayo kwa sababu yanamwepusha na msalaba
(Gal 6:12). Basi pana mambo katika mashauri ya mtu huyu ambayo imekupasa
kuyachukia na kuyapa kisogo.
“Kwanza, alikugeuza kuiacha njia ya haki, nawe ulimsilikiza; Bwana asema,
“Mlango ni mwembamba na njia imesongwa iendayo uzimani, nao waionao ni
wachache” (Mt 7:14).

“Pili alijaribu kukugeuza uupe kisogo msalaba, ingawa huwezi kuupata uzima bila
huo msalaba. Mfalme wa Utukufu amekuambia kuwa yeye aipendaye nafsi yake
ataiangamiza (Yn 12:25).

“Tatu alikuongoza katika njia iendayo mautini. Alikuwa akikupeleka kwa Bwana
haki ambaye hangeweza kamwe kukuondolea mzigo wako. Huwezi kuhesabiwa

13
haki kwa matendo ya sheria; maana kwa matendo ya sheria hakuna mwenye mwili
anayeweza kuwekwa huru na mzigo wake” (Rum 3:20).

Baada ya hayo Mwinjilisti akatoa kilio akielekea mbinguni kuonyesha kuwa


alikuwa amesema kweli. Basi moto ukatoka mlimani nao wakasikia maneno haya,
“Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana! Kwa
maana imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu asiyedumu kati yote yaliyoandikwa
katika kitabu cha torati, ayafanye” (Gal 3:10)

Msafiri alikuwa akilia kwa uchungu na akawa na haya sana kwamba alikuwa
ameiacha njia ya haki. “Je, naweza kurudi na kuliendea lile lango ndogo? Najuta
sana kwamba nilimsikiliza mtu huyo. Lakini je, dhambi yangu itasamehewa?”

“Dhambi yako ni kubwa sana,” alisema Mwinjilisti; hata hivyo mtu huyo pale
langoni atakupokea. Uwe mwangalifu tu, ili usiiache njia mara ya pili.” Kisha
Mwinjilisti akatabasamu na kumbusu walipokuwa wakiagana.

MSAFIRI AINGIA NDANI YA LANGO

Msafiri akashika njia upesi. Hakusema na mtu awaye yote njiani mpaka alipofikia
lango. Juu ya lango yaliandikwa maneno haya, “Bisheni; nanyi mtafunguliwa”
(Mt 7:7). Basi Msafiri akabisha mara tatu. Hatimaye mtu mmoja, jina lake Nia
Njema, akaja langoni na kumwuliza yeye ni nani, ametoka wapi na kisha anataka
nini.

14
Msafiri aingia ndani ya lango

“Mimi ni maskini mwenye mzigo wa dhambi,” akajibu Msafiri; ninatoka katika


Mji wa Uharibifu, nami nauendea Mlima Sayuni ili nipate okolewa na hasira
zitakazokuja. Nimeambiwa kuwa hii ndiyo njia. Je, utaniruhusu niingie ndani?
Ni Njema akalifungua lango akasema, “Mimi ni radhi kwa moyo wangu wote.”

Lakini hapo Msafiri alipokuwa anataka kuingia ndani, huyo mwenzake akamvuta
kwa nguvu. “Mbona wanivuta hivyo?” akauliza Msafiri. Nia Njema akamwambia
kuwa hapo punde mbali na lango pana ngome imara. Hapo Shetani na wasaidizi
wake hujaribu kuwapiga mishale wote wafikao langoni, akitaka kuwaua kabla ya
hawajaingia.

Alipokwisha ingia ndani, huyo mngoja mlango alimwuliza habari za safari yake;
na Msafiri akasimulia yote yaliyompata. Akamaliza kusema, “Aha! Wewe ni
mwema jinsi gani kwa kuniruhusu niingie!
“Hatumkatazi mtu yeyote,” akasema Nia Njema; haidhuru amefanya nini kabla ya
kufika hapa. “Hawatupwi nje kamwe” (Yn 6:37). Basi fuatana nami na
nitakuonyesha njia ikupasayo kuiendea.

“Lakini je huko mbele njia haikupinda au kupotoka hata mtu mgeni kuweza
kuikosa na kupotea?” akauliza Msafiri. “Ziko njia kadha wa kadha ambazo
zashikamana na njia hiyo, lakini zinapotoka-potoka, kisha ni pana. Kwa hivi
utapata kujua njia iliyo sawa na ile isiyo sawa. Njia iliyo sawa tu ndiyo iliyonyoka
na tena ni nyembamba.”

Kisha Msafiri aliomba iwapo huyo mwenzake asingeweza kumsaidia kuutua mzigo
wake. Lakini aliambiwa awe radhi kuuchukua mpaka atakapofika mahali ambapo
mzigo utaanguka wenyewe kutoka mgongoni mwake. Ndipo Msafiri alijiweka
tayari kuendelea na safari. Nia Njema akamwambia kuwa akiisha kwenda mbali
kidogo atafika nyumbani kwa Mkalimani. Hapo agonge mlango, naye ataonyeshwa
mambo ya ajabu.

15
NYUMBANI KWA MKALIMANI

Baada ya Msafiri kuagana na rafiki yake, aliendelea mpaka kufikia nyumbani kwa
Mkalimani. Akagonga mlango mara tatu. Hatimaye mtu akafika mlangoni na
kuuliza ni nani aliyegonga mlango. “Mimi ni Msafiri. “Je, naweza kusema na
bwana mwenye nyumba hii?” alijibu. Alipofika huyo mwenye nyumba, Msafiri
akamwomba amwonyeshe baadhi ya mambo ya ajabu ambayo yatamsaidia katika
safari yake.

CHUMBA CHENYE MAVUMBI


Mkalimani alipokwisha kumleta Msafiri ndani, alimwongoza mpaka kwenye
chumba kikubwa. Chumba hicho kilijaa mavumbi kwa sababu hakikupata
kufagiliwa kamwe. Ndipo Mkalimani alimwita mtu akifagie, nao walivuta pumzi
kwa shida, kwa sababu ya mavumbi. Kisha Mkalimani alimwambia msichana
aliyesimama karibu kukinyunyiza chumba kwa maji. Hivyo ikawa rahishi
kukifagia pasipo mavumbi mengi. “Maana yake ni nini?” akauliza Msafiri.
Mkalimani akajibu, “Chumba hiki ni mfano wa moyo wa binadamu. Uchafu ni
tabia yake na dhambi ya asili, na uovu wake wa ndani ambao wamfanya mtu asiwe
safi. Yule aliyeanza kufagia ni mfano wa sheria katika Torati; lakini msichana
alieyaleta maji ni mfano wa Injili. Kama vile huyo wa kwanza asivyoweza
kukisafisha chumba kwa sababu vumbi lilikuwa juu, ndivyo sheria inavyoweza
kuionyesha dhambi moyoni, lakini haina nguvu ya kutakasa roho (Rum 7:4).
Lakini kama vile maji yalivyopunguza vumbi, ndivyo kwa nguvu za Injili, dhambi
hushindwa. Roho hupata kutakaswa na ikiwa yenye kufaa kuwa maskani ya
Mfalme wa Utukufu (Efe 5:26).

SHAUKU NA SABURI

Kisha niliona katika ndoto yangu huyo Mkalimani akimwongoza Msafiri mpaka
katika chumba kidogo ambamo watoto wawili walikuwa wameketi. Mmoja wao
aliyeitwa Saburi alionekana mwenye furaha na kuridhika; lakini huyo wa pili
aliyeitwa Shauku alionekana asiyeridhika kabisa. Mkalimani akaeleza jinsi mtu
fulani alivyokuwa amewaahidia hao watoto kwamba watapata zawadi mwanzoni

16
mwa mwaka ufuatao. Saburi alikuwa radhi kungoja, lakini Shauku alitaka kupata
zawadi yake wakati ule ule.

Ndipo walimwona mtu akimletea Shauku mfuko uliojaa tunu. Hii ilimfurahisha
sana Shauku, naye akamcheka Saburi kwa vile alivyokuwa radhi kungoja. Lakini
baada ya muda mfupi alikuwa amevitapanya vyote na wala hakubakiwa na kitu, ila
vitambaa vilivyoraruka-raruka.

Basi Mkalimani akamwambia Msafiri, “Huyo Shauku ni mfano wa wale


wanaoyajali mambo ya dunia hii. Saburi ni mfano wa wale wanaoyajali mambo ya
ulimwengu ujao. Watu wa dunia wataka kuyafurahia mambo ya ulimwengu huu
hivi sasa. Hawataki kungoja mpaka ulimwengu ujao. Wanaiamini methali ile
isemayo, “Ndege aliye mkononi ni bora kuliko wawili walioko angani.”
Hawaiamini Biblia isemavyo mintarafu nzuri wa ulimwengu ujao ukiona jinsi
alivyotumia upesi vyote na asibakiwe na kitu. Ndivyo itakvyokuwa kwa watu wa
namna hiyo mwishoni mwa dunia hii.

Kisha Msafiri akasema, “Naona ya kuwa huyo Saburi ana busara kwa sababu
anavingojea vitu bora kupita vyote na atavifurahia vitu vyake wakati mwenzake
hana chochote” (Lk 16:25).

“Naam, na zaidi ya yote, utukufu ujao hautachakaa kamwe. Shauku hakuwa na


sababu yoyote ya kumcheka Saburi, kwa sababu Saburi amevipata mwishowe vitu
vyake bora.”

“Kweli naona, “alisema Msafiri; “kwamba ni bora kutovitaka vitu vilivyopo sasa,
ni vema kuvingojea vile vya baadaye.”
“Ndivyo,” alijibu Mkalimani; “kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali
vile visivyoonekana ni vya milele” (2 Kor 4:18).

MOTO WA NEEMA

Kisha nikaona katika ndoto yangu ya kuwa huyo Mkalimani alimshika mkono
Msafiri na kumwonyesha moto uliokuwa unawaka karibu na ukuta. Mtu mmoja

17
alikuwa akiuzima huo moto kwa kuumwagia maji. Lakini kadiri alivyoumwagia
maji mengi ndivyo moto ulivyozidi kutoa ndimi na kuwaka.

“Hii ina maana gani?” “Huyu ni Kristo, ambaye kwa neema yake huifuliza kazi
iliyokwisha anzishwa ndani ya moyo wa mtu. Hivyo haidhuru Shetani afanye nini,
roho za watu wake hudumu zimejaa neema (2 Kor 12:9). Mtu yule asimamaye
nyumba ya ukuta atufundisha kwamba ni vigumu kwa hao wanaojaribiwa
kuifahamu kazi hii ya neema inavyoendeshwa rohoni.

Moto wa Neema

NDOTO YA SIKU YA HUKUMU

Baada ya hayo Mkalimani alimwongoza Msafiri mpaka kwenye chumba ambacho


kwanza mtu alikuwa akiamka toka kitandani. Alipokuwa akivaa nguo zake
alitetemeka sana akasema, “Nilikuwa nikilala niliota naona mbingu zikiwa nyeusi
sana. Ngurumo na umeme zilinifanya niogope sana. Nikasikia sauti kubwa ya
parapanda na kumwona mtu akiketi katika mawingu akihudumiwa na maelfu ya
malaika. Kisha nilisikia sauti kuu ikisema, “Amkeni, enyi wafu, na njoni
mhukumiwe!” Kisha miamba ikapasuka, makaburi yakafunuka na wafu wakatoka.
Baadhi yao walijawa na furaha na wengine walijaribu kujificha, chini ya mlima.
Mimi pia nilijaribu kujificha, lakini sikuweza kwa sababu mtu Yule aliyeketi juu
ya mawingu alinikazia macho. Nikazikumbuka dhambi zangu zote, na moyo
wangu uliniambia nilivyo kwenye hatia (Rum 2:15-16). Kisha nikaamka.”

18
“Kwa nini uliogopa sana?” aliuliza Msafiri.
“Kwa sababu nilifikiri siku ya hukumu imekwisha fika, nami sikuwa tayari bado,”
alijibu mtu huyo.
Alipokuwa akiagana nao, Mkalimani alimwambia Msafiri ayakumbuke mambo
hayo. Ndipo Msafiri akendelea na safari yake.

MSAFIRI NAUFKIKA MSALABA NA ANAONDOLEWA MZIGO WAKE

Njia hiyo aliyoifuata Msafiri iliitwa Wokovu, na kila upande kulikuwa na ukuta.
Alijaribu kukimbia asiweze kwa ajili ya ule mzigo mgongoni mwake.

Aliharakisha sana mpaka alipokifikia kilele ambacho juu yake palikuwa na kaburi.
Basi hivyo nikaona katika ndoto yangu kwamba mara tu Msafiri alipoufikia
msalaba, mzigo wake ulifunguka ukaanguka kutoka mabegani mwake na
kuvingirika mpaka chini ya kilima na kutumbukia ndani ya kaburi nisiweze kuuona
tena.

Msafiri anaufikia Msalaba

Ndipo Msafiri alifurahi kuondolewa mzigo wake na akasema kwa moyo wa furaha,
“Yeye amenipa furaha na uzima kwa kifo chake.” Kisha akasimama kimya
kitambo akiangalia na kusatajabu. Alishangazwa sana kwamba kwa kuuangalia tu
msalaba aliondolewa mzigo wake.

19
Basi ikatukia hapo alipokuwa akiangali na kulia, aliwafikia watu watatu. Kila
mmoja alivaa nguo za kumetameta. Kisha wakamsalimu, “amani iwe nawe” na
mmoja wao akasema, “Dhambi zako zimesamehewa” (Mk 2:5). Wa pili akamvua
Msafiri nguo zake zilizoraruka-raruka na kumvalisha vazi jipya (Zek 3:4). Wa tatu
akamtia alama katika kipaji cha uso wake (Efe 1:13) na kumpa gombo la chuo
lililotiwa muhuri. Akamwagiza Msafiri kwamba aliangalie gombo hilo
anapoendelea na safari. Kisha akalionyesha penye lango hapo atakapoufikia Mji
wa Mbinguni. Kisha hao watu wakaenda zao, lakini Msafiri aliruka-ruka kwa
furaha. Akaendele mbele akiimba hivi:
Umebarikiwa msalaba! Limebarikiwa kaburi!
Abarikiwe zaidi ya yote Mtu Yule aliyetiwa fedheha
Kwa ajili yangu.

MSAFARI ANAWAFIKIA MJINGA, MVIVU NA MFIDHULI

Kisha nikaona katika ndoto yangu kwamba huyo Msafiri alipokuwa akiendelea
mbele, aliwafikia watu watatu. Hao walikuwa wamelala usingizi mzito hali
wamefungwa pamoja kwa pingu za chuma miguuni. Majina yao yalikuwa Mjinga,
Mvivu na Mfidhuli. Msafiri akajaribu kuwaamsha ili wasaidie kuziondoa hizo
pingu. Akawaambia kama iwapo huyo ambaye huzunguka-zunguka kama simba
angurumaye akifika na kuwakuta vile, hapana budi angeweza kuwameza
(1 Pet 5:8).

Aliposema nao hivyo wakafumbua macho na kumtazama mjinga akasema, Mimi


sioni hatari.” Mvivu akasema “Ngoja nilale kidogo.” Naye Mfidhuli akasema,
“Kila mtu aangalie mambo yake mwenyewe.” Basi wakajinyosha ili kulala tena, na
Msafiri akaendelea na safari yake. Lakini aliudhika alipofikiri jinsi watu walio
hatarini namna hiyo hawakutaka msaada wake!.

20
Msafiri awafikia watu watatu

DESTURI NA MNAFIKI
Msafiri alipokuwa akiyatafari hayo akawaona wawili walioitwa Desturi na
Mnafiki, wakipanda ukutani. Alipowakaribia, Msafiri akawauliza walikuwa
wametoka wapi wa walikuwa wakienda wapi.

“Tulizaliwa katika nchi iitwayo Kiburi, nasi twauendea Mlima Sayuni kutafuta
umaarufu na utajiri,” walimjibu.
“Basi mbona hamkuingia kwa hilo lango lililopo pale mwanzoni mwa njia?
Aliuliza Msafiri. “Je, hamjui ya kuwa imeandikwa, “Yeye asiyeingia mlangoni
katika zizi … lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi?”
(Yn 10:1).

Wakamjibu, ilikuwa ni mbali mno kwetu kulipita lango; hivyo watu kutoka Mji
wetu huitumia njia ya mkato kwa kuupanda ukuta kama tulivyofanya sisi.”

21
Desturi na Mnafiri wanapanda ukuta

“Lakini hapana shaka tunamtenda dhambi Bwana iwapo hatuifuati njia


aliyotuonyesha,” akasema Msafiri. Hao wawili wakamwambia kwamba hawakuwa
na haja ya kujiudhi kwa ajili ya hilo. Jambo walilolifanya lilikuwa ni desturi kwa
miaka zaidi ya elfu moja, na kwa vyovyote iwapo walikuwamo katika njia ile ile,
inadhuru nini waliingiaje. Je, inamaanisha kuwa hali yake ni bora kuliko wao?

Msafiri akajibu, “Mimi ninakwenda kwa kuifuata kanuni ya Bwana wangu, lakini
ninyi mwaenda kwa kuzifuata fikira fidhuli za tamaa zenu wenyewe. Mmekwisha
hesabiwa kama wevi na huyo Bwana wa njia. Mmeingia peke yenu bila uongozi
wake, na mn atoka peke yenu bila rehema zake.”

“Lakini twaweza kuzishika sheria kama wewe unavyozishika,” walijibu. “Hatuoni


unatofautina namna gani na sisi isipokuwa ni hilo koti ulilo nalo mgongoni.
Tunadhani ulipewa na rafiki fulani ili kuficha aibu yako.

“Kwa matendo ya sheria hamtaokolewa,” alisema Msafiri, (Gal 2:16); “kwa


sababu hamkuingia kwa mlango wa zizi la kondoo (Yn 10:1). “Naam, koti hilo
nilipewa kwa wema wa Bwana wa mahali pale ninapopaendea kwa sabau sikuwa
na kitu hapo mwanzoni ila nguo zilizoruraka-raruka. Ninajituliza moyo
ninapofikiri kuwa nitakapofika penye lango la mji, Bwana atanitambua kwa sababu
ya koti hili ninalolivaa ambalo alinipa. Ninayo pia alama juu ya kipaji cha uso

22
wangu. Huenda ninyi hamkuiona. Nao walinipa gombo la chuo ili kunifariji na
kumpa mtu aliye lango la mbinguni.”

Watu hao hawakumjibu, ila walitazamana na kucheka. Kisha nikaona kuwa


Msafiri aliwatangulia huku akilisoma gombo lake.

MSAFIRI APANDA KILIMA CHA MASHAKA

Wote waliendelea mpaka walipofika chini ya kilima kilichoitwa Kilima cha


Mashaka. Hapo palikuwa na njia mbili, mbali na hiyo njia ya kunyooka iliyotoka
pale langoni. Njia moja ilikuwa imezunguka kwa upande wa kulia, na ya pili
upande wa kushoto, chini ya kile kilima. Lakini njia nyembamba ikaenda moja
kwa moja kuelekea kilimani. Msafiri akajiburudisha kwa kunywa maji katika
chemchemi ya maji baridi aliyoiona karibu na chini ya kilima, kisha akaanza
kukikwea kile kilima.

Hao watu wawili walipofikia kilima wakaona jinsi kilivyoinuka kwa ghafula; kwa
hiyo walikata shauri kuifuata njia nzuri iliyokizunguka kile kilima. Walikuwa na
hakika kwamba watakutana na Msafiri tena upande wa pili wa kilima. Mmoja
alishika njia iliyoitwa Hatari, iliyompeleka mpaka kwenye msitu mnene na
alipotelea huko. Yule wa pili alishika njia iliyotiwa Uharibifu, nayo ilimpeleka
mapka kwenye milima yenye miamba, na huko alijikwaa akaanguka asiweze
kuamka tena, akafa.

Kisha nikaangalia kuona jinsi Msafiri atakavyokwea kile kilima. Kwa ghafula
aliacha kukimbia na akaanza kutembea. Lakini baadaye ilikuwa vigumu hata
kutembea. Akaanza kukipanda kilima kwa kutambaa kwa mikono na magoti,
maana kile kilima kiliinuka kwa ghafula sana.

Karibu kama katikati ya njia kukiendea hicho kilima palikuwa mahali penye kivuli.
Bwana wa kilima ndiye aliyekifanya kiwe hivyo ili wasafiri waliochoka wapate
kupumzika. Basi hapo Msafiri alipoketi ili kupumzika alilitoa gombo lake na
akasoma maneno ya faraja. Nayo yalikuwa ya faraja mno na kwa uchovu aliokuwa

23
nao ulimfanya akalala usingizi mzito hata lile gombo likamdondoka. “Ewe mvivu
mwendee chungu, zitafakari njia zake ukapate hekima” Mit 6:6.

MWOGA NA MASHAKA

Kulikuwa karibu kumekuchwa Msafiri alipoamka kwa ghafula. Akaanza kwa


haraka na kwa nguvu kukikwea kile kilima.

Msafiri alipokwisha kufika kileleni, aliwaona watu wawili wakikimbia kumlaki.


“Je, kuna nini?” aliuliza Msafiri. “Mbona mwakimbia katika njia isiyo sahihi!
akamaliza.
Mmoja wao jina lake Mwoga, akajibu kwamba walikuwa njiani kuuendea Mji wa
Sayuni. Lakini kila walipoendelea mbele ndivyo walivyokuta na hatari; kwa hiyo
walikuwa wanarudi nyuma. Ndipo akajibu Mashaka; “kwani hapo mbele yetu
kidogo palikuwa na simba wawili wakali, nasi tulikuwa na hakika kwamba
tukiwakaribia tu hapana shaka wangeturarua.”

Ndipo Msafiri akasema, “Mwanitia hofu hata mimi, lakini nikimbilie wapi nipate
kuwa salama? Nikiirudia tena nchi yangu nina hakika nitaangamia huko. Lakini
kama nikiufika Mji wa Mbinguni nitakuwa salama. Yanipasa kuendelea na safari.
Nikirudi nyuma ni kufa tu. Nikiendelea mbele ipo hofu ya mauti, lakini mbele yake
ni uzima wa milele. Basi nitaendelea mbele,” alimaliza.

Hivyo Mashaka na Mwoga wakakimbia kukitelemka kilima, na Msafiri akaendelea


na safari yake. Akayafikiri tena hayo aliyoambiwa na hao wawili, akalitafuta
gombo lake. Lakini hakuweza kuliona! Akaingiwa na wasiwasi sana asijue la
kufanya. Akapiga magoti na kumwomba Mungu amsamehe kwa ajili ya kitendo
chake cha kipumbavu (1 The 5:6-8). Kisha akarudi nyuma kulifatuta gombo lake.
Katika kurudi hivyo njiani mwote alikuwa na majonzi kupita kiasi.

Akaangalia huku na huko njiani ili kulitafuta gombo ambalo ilikuwa ni faraja yake
mara nyingi safarini.
Alipofika mahali pale penye kivuli aliketi chini akalia kwa muda kitambo.
Baadaye akiangalia chini aliliona lile gombo na kwa upesi akaliokota. Akawa na

24
furaha sana! Akamshukuru Mungu kwa kumwonyesha lilipokuwa. Akaanza safari
yake tena hali mwenye machozi ya furaha. Akakwea sehemu iliyobaki ya kilima
kwa haraka sana. Lakini kabla hajafika kileleni jua lilikuwa limekuchwa. Ndipo
alipokumbuka jinsi Mwoga na Mashaka walivyoingiwa na hofu kwa ajili ya simba.
Akafikiri jinsi wanyama hawa wanavyotangatanga usiku. Alishangaa iwapo
atakutana nao atawezaje kuokoka wasimle.

MSAFIRI ALIFIKIA JUMBA ZURI

Akiwa na mawazo hayo yasiyofurahisha moyoni mwake, akatazama mbele yake


akaona jumba la kupendeza sana, liliiitwa “Uzuri”.

Basi nikaona katika ndoto yangu ya kuwa huyo Msafiri alifanya haraka akiongeza
hatua zake ili akapate kulala katika jumba hilo. Lakini kabla hajaendelea mbali
sana aliingia njia nyembamba na akawaona simba wawili njiani. Akaogopa (maana
hakuweza kuona kwamba simba hao walikuwa wamefungwa kwa minyororo).
Akataka kurudi nyuma kama Mashaka na Mwoga walivyofanya, maana alifikiri
kwa vyovyote angekufa. Lakini mlinga lango ambaye jina lake lilikuwa Mkeshaji,
alimwona akisimama kama atakaye kurudi nyuma. Akampigia makelele akisema
“Je, nguvu zako ni chache?” (Mk 4:40). Usiogope hao simba wamefungwa.
Wamewekwa hapo ili kuwajaribu hao wenye imani na kuwatambua hao
wasiokuwa nayo. Pita katikati ya njia na hakuna litakalokupata.

Ndipo nikaona ya kuwa alikwenda mbele, huku akitetemeka kwa ajili ya hofu ya
simba. Lakini aliyafuata maagizo ya huyo mlinda mlango. Simba wakanguruma,
lakini hawakumdhuru. Kisha akapiga makofi kwa furaha. Akaendelea mbele
mpaka akasimama mbele ya mlango. Kisha Msafiri akauliza, “Bwana mkubwa,
naweza kupata mahali pa kulala usiku huu?” Mngoja mlango akamwuliza, “jina
lako ni nani, nawe umefikaje hapa usiku? Jua limekwisha kuchwa.”

Msafiri akajibu, “Jina langu sasa ni Mkristo, lakini hapo kwanza niliitwa Mbaya
Msafiri. Ningefika mapema, lakini kwa ujinga wangu nililala kivulini kando ya
kilima. Kisha nilipofika kileleni, sikuliona gombo langu. Ikanipasa kurudi na
kulitafuta, nami ndiyo kwanza nimekuja.”

25
“Vema,” akasema mlinda mlango; “nitamwita mmoja wa wanawake watumishi wa
nyumba hii. Kama atayapendelea hayo usemayo kutokana na sheria za nyumba hii,
atakukaribisha ndani pamoja na wengine wa jamaa hiyo.” Hivyo Mkeshaji akapiga
kengele na mwanamke jina lake Hiari akatokea nje mlangoni. Akauliza, “kuna
nini?” Mkeshaji akajibu, “Mtu huyo yumo njiani kuuendea Mlima Sayuni. Lakini
kwa sababu ni usiku sasa na tena amechoka sana, ameomba kupata mahali pa
kulala.”

Hiari akamwuliza maswali machache na kisha akawaita mabibi watatu zaidi wa


jamaa ile, nao ni Busara, Mtawa na Upendo. Wakamwongoza mpaka ndani.
Nyumba hii ilijengwa na Bwana wa Kilima hiki kwa ajili ya wenye kuhitaji na
wasafiri kama wewe.” Mkristo akawafuata mpaka ndani kabisa. Wakaongea huku
chakula kikiwa kinatayarishwa.

“Njoo, Mkristo mwema”, akasema Mtawa; “twende tuyaongelee yote yaliyokupata


safarini. Huenda tukasaidiwa sisi sote.” “Nitafurahi kuwasimulia,” akajibu
Mkristo. Akawasimulia yote kuhusu safari yake mpaka kuwasili hapo.
“Nini kinachokufanya kutaka kuuendea Mlima Sayuni?” Aliuiliza Busara.
“Ninatumaini kumwona akiwa hai Yeye alikufa msalabani kwa ajili yangu.”
Akajibu Mkristo. “Huko ninatumaini kuokolewa kutoka yote yanayonisumbua hivi
sasa. Watu wasema, “hakuna mauti huko” (Ufu 21:4). Huko nitaishi na watu
niwapendao hasa. Maana kusema kweli ninampenda kwa sababu aliniondolea
mzigo wangu, nami nimechoka na ugonjwa uliomo moyoni mwangu, ningependa
kuwapo pale ambapo sitakufa tena kamwe. Nataka kuishi pamoja na hao ambao
wataimba daima. “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu.”

Kisha Upendo akasema, “Mbona hukuileta jamaa yako pamoja nawe?”


Mkristo akalia na kusema, “Aa! Ningalipenda sana, lakini wao hawakupenda
kabisa nisafiri. Niliwaambia kuwa Mungu alinifunulia kwamba mji wetu
utaharibiwa. Lakini nikawa kama afanyaye dhihaka machoni pao, na
hawakunisadiki” (Mwa 19:14).
“Lakini walikuwa na udhuru gani hata wasifike?”

26
“Mke wangu aliogopa kuachana na ulimwengu ule, nao watoto wangu walikuwa
wakiyafuata mambo ya kupendeza ya ujana. Basi kwa mambo haya na haya
waliniacha kutangatanga njiani peke yangu.”

Sasa nikaona katika ndoto yangu ya kuwa waliketi pamoja na kuongea mpaka
chakula kilipokuwa tayari. Kisha wakaketi ili kula. Mazunguzo yao yote
walipokuwa mezani yalikuwa mintaarafu Bwana wa Kilima. Waliongea pia
kuhusu aliyoyafanya na kwa nini aliyafanya, na kwa nini alijenga nyumba hiyo.
Kutokana na hayo waliyoyasema nilihisi ya kuwa huyo alikuwa shujaa mkuu.
Alikuwa amepigana na kumwua huyo aliyekuwa na nguvu za mauti (Ebr 2:14-15);
lakini alijihatarisha sana mwenyewe. Hayo yalinifanya nimpende zaidi.
Wakaongeza kusema kuwa aliuweka kando utukufu wake mwenyewe ili apate
kuyafanya hayo kwa ajili ya hao maskini wanadamu. Nao walipata kumsikia huyo
Mwana wa Mfalme akisema kwamba hangependa kuukaa Mlima Sayuni peke
yake. Wakasema pia kwamba aliwafanya wasafiri wengi wawe wakuu, ingawaje
kwa asili walizaliwa kuwa waombaji (1 Sam 2:8; Zab 113:7).

CHUMBA CHA AMANI

Waliendelea kuongea hadi usiku wa manane. Kisha wakajiweka mikononi mwa


Mungu awalinde usiku. Wakamchukua Mkristo orofani ambako dirisha lake
lilikuwa wazi kuelekea mawio ya jua. Chumba hicho kiliitwa Amani. Akalala
humo mpaka asubuhi.

MKRISTO AKAA KUTWA KATIKA JUMBA

Asubuhi yake Mkristo alikuwa tayari kuendelea na safari yake. Lakini


walimwambia kuwa hataondoka mpaka wamtembeze kwanza humo ndani ya
jumba.

Basi kwanza walimwingiza katika chumba kimoja ambamo walimwonyesha


Maandiko ya zamani sana. Katika hayo akasoma kwamba huyo Bwana wa Kilima
alikuwa Mwana wa Mzee wa siku. Mlikuwa pia na maelezo ya matendo
aliyoyatenda katika huduma yake. Kisha wakamsomea baadhi ya matendo yenye

27
sifa ambayo baadhi ya watumishi wake waliyafanya (Ebr 11:33-34). Kisha
wakamsomea tena mahali palipoonyesha jinsi Bwana wao alivyo tayari kumpokea
yeyote kwa upendo wake ijapokuwa huko nyuma alimpinga Yeye kwa matendo
yake.

Kisha wakamleta katika chumba walikomwonyesha kila namna ya silaha. Bwana


aliziweka hizo tayari kwa ajili ya wasafiri. Palikuwapo panga, ngao, chepeo na
viatu ambavyo havitachakaa. Kulikuwa na silaha nyingi zaidi hata asiweze
kuzihesabu. Wakamwonyesha pia baadhi ya silaha ambazo watumishi wake
walizitumia kufanya mambo ya ajabu. Akaiona fimbo ya Musa, mtungi wa
Gideoni, kombeo la Daudi na vitu vingine vingi. Mkristo akapendezwa sana.

MILIMA YA KUPENDEZA

Siku ya pili wakamchukua mpaka juu ya paa la nyumba ili kumwonyesha Milima
ya Kupendeza. Akaangalia kusini, naye akaona kwa mbali sana nchi nzuri yenye
milima ya kupendeza, na yenye misitu upande mmoja na mashamba yenye
matunda upande mwingine. Akauliza jina la nchi hiyo. Wakamjibu kuwa yaitwa
Nchi ya Imanueli, na kwamba njia ya msafiri yapitia nchini humo. “Utakapofika
huko utaweza kuliona lango la Mji wa Mbinguni,” wakamaliza.

MKRISTO AENDELEA NA SAFARI YAKE.

Mkristo alitaka kuanza safari yake tena. Lakini kwanza hao rafiki zake watatu
walimpa silaha zote atakazohitaji kuzitumia atakapokutana na adui njiani.
Wakafuatana naye mpaka langoni. Hapo Mkristo alimwuliza bawabu kwamba
amewaona wasafiri wowote wakipita.

28
Rafiki zake walimpa silaha zote.

Bawabu akajibu, “Naam, nilimwona mtu aitwaye Mwaminifu.”


“Ehe,” akasema Mkristo; “namfahamu mtu huyo. Alikuwa jirani yangu. Je,
wadhani kwa sasa yuko mbali sana?”
“Kwa sasa hivi bila shaka amekwisha kupita kilima,” akajibu.
“Vema,” akasema Mkristo; “Bwana akae nawe akuongezee mibaraka kwa fadhili
ulizonitendea.”

Ndipo Mkristo akashika njia, lakini hao mabibi Busara, Mtawa na Upendo
walitaka kwenda pamoja naye mpaka chini ya kilima. Kisha Mkristo akasema,
“Kama ilivyokuwa vigumu kukipanda kilima, naona pia kuwa ni hatari
kukitelemka.”

“Naam,” akasema Busara; “ni vigumu kwa mtu kuliteremkia hilo bonde la
Unyenyekevu, kama ufanyavyo, naye, asiteleze. Ndiyo sababu tumefuatana nawe.”
Hivyo akaanza kuteremka kwa uangalifu, lakini hata hivyo akateleza mara mbili
hivi. Kisha nikaona hapo Mkristo alipofika chini ya kilima. Hao rafiki zake
walimpa chakula, naye akaendelea mbele. Hatimaye alilifikia Bonde la
Unyenyekevu.

29
MKRISTO APIGANA NA APOLIONI

Lakini wakati huo alipokuwa katika Bonde la Unyenyekevu, maskini Mkristo


alikuwa amekwenda muda mfupi tu, akamwona adui mbaya aliyeitwa apolioni
(Ufu 9:11), akija kumkabili. Ndipo Mkristo alianza kuogopa. Basi alifikiri afanyeje
– arudi nyuma au asimame na kumgojea. Lakini alikumbuka hakuwa na kinga
mgongoni mwake, basi alikaza nia kusimama pale pale.

Ndipo akenda mbele na huyo Shetani aliyeitwa Apolioni akakutana naye. Huyo
jitu alikuwa wa kutisha sana, yaani huyo Shetani. Alifunikwa na magamba mwilini
kama samaki na alikuwa na mabawa, ila sura yake ilikuwa kama joka. Kinywani
mwake ulitoka moto na moshi. Alipomfikia Mkristo, alimtazama kwa dharau na
kumwuliza, “Watoka wapi, nawe waenda wapi?”

Mimi natoka katika Mji wa Uharibifu, ambapo ni mahali pa uovu wote. Nami
nauendea Mji wa Sayuni.
“Naona ya kuwa wewe ni mmojawapo wa raia zangu. Mimi ni mkuu wa miungu
ya nchi ile, akasema Apolioni.
“Ni kweli nilizaliwa katika nchi ile yako, lakini utumishi wako ulikuwa mgumu na
mshahara ulikuwa ni mdogo sana mtu asiweze kuishi; “kwa maana mshahara wa
dhambi ni mauti,” alimaliza Mkristo (Rum 6:23).

Hapana mkuu yeyote atakayekubali kuwapoteza raia zake hivi, alisema Apolioni.
“Wala mimi sitakupoteza wewe. Lakini kwa vile unanung’unika mintarafu
utumishi na mshahara wako, uwe radhi kurudi, nami nitakulipa zaidi.”

“Lakini nimekwisha jiweka kwa mwingine, ndiye Mfalme wa wakuu, nawezaje


kukurudia wewe?”
“Wewe umefanya hivi kama methali isemayo, “Kuuacha ubaya na kuingia ubaya
zaidi.” Lakini ni kawaida kwa wale waliojiita watumishi wake, baada ya muda
kitambo kuponyoka na kunirudia mimi. Ukifanya hivyo yote yatakuwa sawa,”

Lakini Mkristo akajibu, “Ewe Apolioni mwenye kuharibu! Kusema kweli napenda
kumtumikia huyo Mfalme katika utawala wake, shirika lake na nchi yake zaidi ya

30
nchi yako. Usijaribu kunishawishi tena. Mimi ni mtumishi wake, nami nitamfuata
Yeye.”
Fikiri tena kwa ungalifu mintarafu mambo ambayo yaelekea yatakupata njiani.
Wajua kwamba wengi miongoni mwa watumishi wake wana shida kubwa kwa
sababu ya kuniasi na kuziacha njia zangu. Ni wangapi miongoni mwao wameuawa
kwa vifo vya aibu? Mbali ya hayo, unafikiri utumishi wake ni bora kuliko wangu
ingawaje hafiki kamwe kumwokoa yeyote anayemtumikia? Lakini kwangu mimi,
kama ulimwengu wote ujuavyo, ni mara ngapi nimewasaidia wale ambao
wamenitumikia kwa uaminifu? Nimewaokoa kwa nguvu, au kwa kusema uongo,
au kwa hila. Hivyo basi, nitakuokoa wewe,” akamaliza Apolioni.

“Yaonekana kana kwamba anachelewa kuwasaidia, lakini ni kwa sababu anapima


upendo wao kwake,” alijibu Mkristo. Hawatazamii wokovu hivi sasa, maana
wanaungojea utukufu wao. Wataupata hapo Mkuu wao atakapotokea katika
utukufu wake mwingi pamoja na malaika zake.”

Kisha Apolioni akasema, “Wewe umekwisha kuwa mkosaji usiye mwaminifu


katika utumushi wako kwake, nawe wawezaje kutazamia mashahara kwake?”
“Hiyo ni kweli,” alisema Mkristo; lakini Mkuu nimtumikiaye na kumheshimu ni
mwenye huruma na tayari kusamehe. Nimekwisha pata msamaha kwake.”

Ndipo Apolioni akakasirika mno, akasema, “Mimi ni adui wa Mkuu huyo.


Namchukia Yeye mwenyewe. Nazichukia amri zake na watu wake. Basi nimekuja
kupigana nawe.”
Kisha Mkristo akasema, “Apolioni jihadhari unalofanya, maana mimi nimo katika
njia ya Mfalme, ndiyo njia ya utakatifu. Kwa hiyo tunza nafsi yako.”

Ndipo Apolioni akasimama na kupanua miguu yake, huku akiziba njia yote, “Mimi
siogopi jambo hili,” akasema jiweke tayari kufa; maana naapa kwamba
hutaendelea mbele. Nitakuua hapa hapa.” Akiisha kusema hayo akamtupia Mkristo
mshale wa moto. Lakini alikuwa na ngao mkononi mwake akaukinga mshale
usimpate. Ndipo akaufuata upanga; maana aliona ya kuwa ni wakati wa kuanza
mapigano. Apolioni alikuwa akiipiga mishale mingi sana kwa upesi sana.
Ijapokuwa Mkristo alifanya kila alivyoweza kuiepuka, alijeruhiwa kichwani,
mkononi na miguuni. Hayo yalimfaya Mkristo arudi nyuma kidogo, lakini

31
alipigana kwa uthabiti kama alivyoweza. Vita hii kali ilidumu kiasi cha nusu siku,
na kwa sababu ya majeraha yake, Mkristo alipungukiwa na nguvu.

Kisha Apolioni alipopata nafasi hiyo, alimkaribia Mkristo na kumpiga mweleka


mpaka chini. Hivyo upanga wake Mkristo ukamponyoka. Ndipo Apolioni
akasema, “Sasa nimekupata hasa.”

Msafiri apigana na Apolioni

Basi ndipo alizidi kumfinya ili afe, mpaka Mkristo alifikiri kwamba atakufa.
Lakini kama Mungu alivyopenda, hapo Apolioni alipokuwa tayari kumpiga pigo la
mwisho ili kummaliza, Mkristo akaunyosha mkono wake na kuushia upanga wake.
Akaushika na kusema, “Usifurahi juu yangu, Ee adui yangu; niangukapo,
nitasimama tena” (Mik 7:8). Aliposema hayo Mkristo alimpiga Apolioni pigo la
kumfisha. Pigo hilo lilimfanya aanguke kama aliyekufa. Mkristo alipoona vile
akamwendea tena na kusema. “Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na
zaidi ya kushinda, kwa Yeye aliyetupenda” (Rum 8:37). Baada ya hayo Apolioni
akayanyoosha mabawa yake akaenda zake; Mkristo asimwone tena.

Hapana mtu awezaye kuielewa vita hii isipokuwa aliyeiona kwa macho yake na
kusikia kwa masikio kama nilivyosikia jinsi huyo Apolioni alivyopiga kelele na
ngurumo ya kutisha. Hali kadhalika naye Mkristo alivyougua moyoni mwake. Ni
hapo tu alipoona kuwa amemjeruhi Apolioni kwa upanga wake mkali kuwili,
32
ndipo alipotabasamu na kutazama juu. Vita vile vilikuwa ni jambo la kutisha
ambalo mfano wake sijapata kuuona kamwe.

Basi vita vilipokwisha, Mkristo akasema. “Nitamshukuru Yeye aliyeniokoa kutoka


kinywa cha simba, kwake Yeye aliyenisaidia kumshinda Apolioni.” Naye kweli
akatoa shukrani.

Kisha ukamfikia mkono wenye majani ya mti wa uzima. Mkristo akayachukua


majani na kuyabandika juu ya majeraha yake, nayo yakapona mara. Ndipo aliketi
kula chakula alichopewa kabla ya vita. Hicho kilimburudisha, akaendelea na safari
yake akiwa na upanga wake mkononi. Lakini hakumwona Apolioni tena katika
bonde lile.

BONDE LA UVULI WA MAUTI

Basi mwishoni mwa bonde hili kulikuwa na bonde lingine lililoitwa Bonde la
Uvuli wa mauti. Njia ya kuuendea mji wa mbinguni ilipita katika bonde hilo.
Mkristo alikutana na taabu huko kuliko zile taabu alizozipata na Apolioni.

Kisha niliona katika ndoto yangu hapo Mkirsto alipoufikia ukingo wa bonde,
alikutana na watu wawili. Nao walikuwa wanafanya haraka wakirudi nyuma
alikotokea Mkristo. “Mnakwenda wapi? Akauliza Mkristo.
“Nyuma, nyuma! Yafaa nawe pia arudi nyuma kama wataka kuishi na kuwa na
amani,” walimjibu. “Kwani kuna nini?” Akauliza Mkristo. “Kuna nini!
Wakamjibu hao wawili; “sisi tulikuwa tukiifuata njia hiyo uifuatayo wewe, nasi
tulikwenda kama tulivyoweza. Kama tungaliendelea mbele zaidi, tusingeweza
kurudi tena na kukuonya wewe, ni mahali pa kutisha sana.”

Kisha Mkirsto akasema, “walakini hii ni njia yangu ya kuuendea mji wa


mbinguni.” “Waweza kwenda, lakini sisi hatuachagui kuendelea mbele,”
walisema. Basi wakaachana.
Mkristo akaendelea kimya kimya akiwa na upanga upande wa kulia kulikuwa na
handaki lenye kina sana; ambamo vipofu wamewaongoza vipofu wenzao kwa
miaka mingi. Kwa upande wa kushoto kulikuwa na bwawa la hatari. Nayo njia

33
ilikuwa nyembamba kupita kiasi. Mkristo aliona vigumu kuifuata njia bila hatari
ya kuangukia upande huu au ule. Kulikuwa na giza nene hata hakuweza kuona
akanyage wapi. Karibu katikati ya bonde niliona kuwa njia ilipita karibu na
Jehanamu. Ndipo Mkristo akishangaa afanyeje, maana miali ya moto na moshi
pamoja na sauti za kutisha vilitoka mara kwa mara. Mkristo akalazimika kuutia
upanga alani na kutumia silaha nyingine iliyoitwa Maombi Yote (Efe 6:18). Basi
akalia, “Ee Bwana, nakuomba sana, uniokoe nafsi yangu (Zab. 116:4).

Alivyozidi kuendelea mbele, miali ya moto ilizidi kumfikia na akazidi kuzisikia


sauti za kutisha. Pengine alifikiri atararuliwa vipande-vipande. Mara nyingine
alifikiri kurudi nyuma, kisha tena akafikiri amekwisha fika nusu ya bonde.
Akakumbuka jinsi alivyoshinda hatari nyingi na akafahamu kwamba hatari za
kurudi nyuma zingezidi kuliko zile atakazozikuta akiendelea mbele. Basi alikaza
nia kuendelea mbele, naye akalia, “Mimi nitakwenda kwa nguvu za Bwana.”

Mara kwa mara Mkristo alitatanika sana hata asiitambue hata sauti yake
mwenyewe. Mmojawapo wa hao mashetani akaenda nyuma yake na
kumnong’oneza masikioni, huku akimtia fikira nyingi mbaya. Alidhani fikira hizo
zatoka moyoni mwake mwenyewe. Mambo haya yakamsumbua Mkristo kuliko
yote mengine yaliyompata huko nyuma yaani kufikiri kuwa angemtukana Yeye
ambaye anampenda sana.

Alipokuwa amesafiri muda kitambo, Mkristo alidhani aliisikia sauti ya mtu


ikisema, “Nijapopita kati ya bonde la Uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa
maana Wewe upo pamoja nami” (Zab 23:4). Ndipo akafurahi sana, na sababu za
kufurahi zilikuwa tatu.

Kwanza, alijua kuwa mtu mmoja aliye mchaji wa Mungu alikuwapo pia katika lile
bonde. Pili, alifahamu kuwa Mungu alikuwa pamoja naye gizani, ingawaje hakuwa
akimwona (Ay 9:11). Tatu, alitumaini atamfikia mtu Yule na kusafiri pamoja naye.

Basi kulipopambazuka, Mkristo alitazama nyuma; si kwa sababu walitaka kurudi,


bali alitaka kuona kwa nuru ya mchana ni hatari zipi alizokuwa amezipata wakati
wa giza. Mkristo aliamshwa moyo namna gani akashukuru kwa kuokolewa katika
hatari zote za njiani. Ingawa hapo mwanzoni aliziogopa, sasa aliziona hatari hizo

34
waziwazi kwa sababu ya nuru ya mchana. Jua nalo lilipochomoza lilimsadia
Mkristo kwa sababu sehemu ya pili ya hilo bonde ilikuwa ya hatari kuliko sehemu
ya kwanza. Kutoka hapo aliposimama, hata mwisho wa bonde, njia yote ilikuwa
imejaa mitego, mitambo na nyavu. Ilijaa pia mashimo marefu mno, hivyo kama
kungalikuwa giza kama hapo mwanzo, haikosi angeliangukia tu.

MKRISTO AMKUTA RAFIKI

Mkristo alifika mwisho wa bonde na akakuta mahali palipoinuka, napo paliinuliwa


hivyo kusudi ili wasafiri waweze kuiona hiyo nchi iliyo mbele yao. Hapo juu
Mkristo akatazama mbele akamwona mtu jina lake Mwaminifu. Ndipo akapaza
sauti, akaita, “Ningoje, nami nitafuatana nawe.”

Kwa upesi Mkristo akamfikia Mwaminifu, nao wakaendelea mbele pamoja, huku
wakiyaongelea hayo yote yaliyowapata humo njiani.
“Ulikaa katika Mji wa Uharibifu kwa muda gani kabla hujaanza safari hii?”
akauliza Mkristo.
“Mpaka niliposhindwa kuendelea kukaa,” alijibu Mwaminifu. “Palikuwa na
maneno mengi mara baada ya kuondoka kwako kwamba mji wetu utateketezwa
kabisa kwa moto kutoka mbinguni.”

“Nini? Jirani zako waliongea hayo?” aliuliza Mkristo.


“Naam,” alijibu Mwaminifu; lakini kwa kweli sidhani kuwa walisadiki; maana
niliwasikia baadhi yao wakicheka hapo walipokuongelea wewe na “safari yako ya
bure” maana ndivyo walivyoiita safari yako. Lakini mimi nilisadiki, na hata sasa
nasadiki, kwamba mwisho wa mji wetu utakuwa ni kuteketezwa kwa moto na
kiberiti. Kwa hiyo nimejiokoa.”

“Je, ulipata habari zozote za jirani yetu Msikivu?” Akauliza Mkristo.


“Ndiyo,” akasema Mwaminifu; “tangu aliporudi amefanyiwa dhihaka na
kudharauliwa na watu wote. Tena ni shida kwamba mtu yeyote atampa kazi.
Nilikutana naye mara moja barabarani, lakini alikwenda upande wa pili wa
barabara kana kwamba alikuwa na haya; kwa hiyo sikusema naye. Hapo mwanzo

35
nilikuwa na matumaini mema juu yake, lakini sasa naogopa kwamba atapotea
katika maangamizi ya mji.”

MASIMULIZI YA MWAMINIFU

“Vema, jirani yangu Mwaminifu, twende, tuache kumwongelea yeye, na


tuyaongelee sasa mambo yanayotuhusu sisi wenyewe. Niambie ni mambo gani
yaliyokupata njiani?” Aliuliza Mkristo.
“Mimi niliepuka hilo bwawa ulimoanguka wewe, nikalifikia lango bila hatari
yoyote,” alisema Mwaminifu. “Nilikutana na mwanamke mmoja jina lake
Mwasherati aliyetaka kunidhuru.”
“Ilikuwa vizuri ulimwepuka. Je, alikufanyiaje wewe?” Akauliza Mkristo.
“Huwezi kufahamu jinsi mwanamke huyo alivyokuwa na maneno ya kupendeza,
naye alijaribu kunivuta nigeuke kando ili nifuatane naye, huku akiniahidia anasa za
kila namna,” alieleza Mwaminifu.
“Hakukuahidia maridhisho ya dhamiri njema?” Aliuliza Mkristo.

“Wajua maana yangu ni Uradhi wa mambo yote ya tamaa za mwili,” alisema


Mwaminifu.
“Namshukuru Mungu umemwepuka. “Anayechukiwa na Bwana atatumbukia
ndani ya shimo” (Mit 22:14).” Mkristo alisema.
“Mimi sijui kama nilimwepuka kabisa au sivyo,” alijibu Mwaminifu.
“Kwa nini, natumaini hukuyakubali matakwa yake?” Aliuliza Mkristo.
“La, alijibu Mwaminifu; “sikukubali kujinajisi nafsi yangu. Nililikumbuka andiko
la kale nililoliona lisemalo “Hatua zake zinashikamana na kuzimu” (Mit 5:5). Basi
niliyafumba macho yangu nisije kuvutwa na uzuri wake (Ay 31:1). Kisha
alinilaani, nami nikaendelea na safari yangu.” “Je, ulikutana na mtu yeyote
njiani?” aliuliza Mkristo.

ADAMU WA KWANZA

“Nilipofika chini ya kilima kiitwacho Shida, nilimkuta mzee mwanamume


aliyeniuliza mimi ni nami na nilikuwa naenda wapi. Akasema, “Unaonekana kuwa

36
u mtu mwaminifu. Je, utaridhika kukaa nami kwa mshahara nitakaokupa?” Kisha
nikamwuliza jina lake na anakokaa. Akasema jina lake ni Adamu wa Kwanza,
naye aliishi katika mji uitwao Udanganyifu (Efe 4:22). Akaniambia kuwa kazi
yake ni kupendeza na mshahara wake ni kwamba mwishowe ningekuwa mrithi
wake. Aliniambia kuwa nyumbani mwake mlikuwa na mambo yote ya
kufurahisha ya ulimwengu ule. Akasema tena kuwa alikuwa na mabinti watatu:
Tamaa ya Mwili, Tamaa ya Macho na Kiburi cha Uzima (1 Yn 2:16); na kwamba
ningeweza kumwoa mmoja wao kama ningelitaka. Kisha nilimwuliza alitaka nikae
naye kwa muda gani, naye akanijibu kuwa muda wote atakapokuwa hai
mwenyewe.”

“Vema, ulipatanaje na huyo mzee?” Akauliza Mkristo. “Hapo kwanza nilifikiri


ningeweza kufuatana naye kwa sababu niliyaona maneno yake kuwa ni sawa.
Lakini nilipokuwa nikieongea naye, nilikitazama kipaji cha uso wake, nami
nikaona yameandikwa maneno haya, “Mvue mtu wa kale na vitendo vyake.” Kisha
nikachomwa sana moyoni mwangu kwamba kila alilosema na kusifia kiasi gani,
hapo atakaponileta nyumbani kwake tu angeniuza kuwa mtumwa. Kwa hiyo
nilimwambia anyamaze kwa maana singetaka kuukaribia mlango wa nyumba yake.
Kisha alinishutumu na kuniambia angemtuma mtu kunifuata ili kuifanya njia
yangu kuwa uchungu nafsini mwangu. Kwa hiyo nikageuka na kumwacha. Kisha
akanishika na kunivutia nyumba kwa nguvu, hata nilidhani kuwa alikuwa
amechukua sehemu fulani ya mwili wangu ili imwandame yeye. Ndipo nikalia
nikasema “Ole wangu, maskini mimi” (Rum 7:24).” Alieleza Mwaminifu.

MWAMINIFU NA MUSA

“Basi nikaendelea kukwea kile kilima,” akaendelea kusimulia Mwaminifu.


“Nilipokuwa nimekwisha kukikwea kilima kama nusu yake, nikaangalia nyuma,
nami nikamwona mtu ananikimbilia nyuma yangu. Akanikuta karibu na mahali
penye kivuli.

“Ni papo hapo nilipoketi ili kupumzika, lakini nikalala usingizi na kupotewa na
gombo langu, akasema Mkristo.

37
“Lakini ndugu mwema, ngoja nikuambie,” aliendelea Mwaminifu. “Mara mtu
huyo aliponikuta, alinipiga na kunibwaga chini, nami nikalala kama aliyekufa.
Lakini nilipopata fahamu, nilimwuliza kwa nini alinitendea vile. Akaniambia ni
kwa sababu nilijiweka kwa siri upende wa Adamu wa Kwanza. Ndipo akanipiga
tena konde la kufisha kifuani, hata nikalala miguuni pake kama aliyekufa. Hivyo
nilipopata fahamu tena nikamlilia anihurumie. Lakini akasema, “Mimi sijui jinsi ya
kukurehemu.” Ndipo alinipiga tena na kuniagusha chini. Hapana shaka
angenimaliza kabisa, lakini mtu mmoja akafika na kumwambia aniache.”
“Mtu huyo aliyemwamrisha mtesi wako akuache alikuwa nani?” Aliuliza Mkristo.
“Hapo mwanzo mimi sikumtambua, lakini alipokuwa akipita, niliyaona matundu
mikononi mwake na ubavuni. “Ndipo nilitambua ya kuwa ni Bwana wetu.” Alijibu
Mwaminifu.

“Mtu aliyekuwa anakupiga ni Musa,” alisema Mkristo. “Yeye hamhurumii mtu


yeyote, wala hajui kuwahurumia hao wanaoivunja torati yake.”
“Najua hayo vizuri kabisa,” alijibu Mwaminifu. “Hiyo haikuwa mara ya kwanza
kukutana naye.”
“Lakini wewe hukuiona hiyo nyumba iliyojengwa pale juu ya kilima?” aliuliza
Mkristo.
“Naam, niliiona, na hao Simba pia; lakini nafikiri walikuwa wamelala, maana
ilikuwa yapata saa sita za usiku. Kwa vile nilikuwa na wakati wa kutosha
nilimpitia huyo Bawabu, kisha nikakiteremka kilima”, alijibu Mwaminifu.

“Laiti ungelifika hapo penye nyumba, maana wangekuonyesha vitu vya shani
ambavyo hungevisahau kamwe maishani mwako,” alisema Mkristo. “Lakini
niambie ulikutana na yeyote katika lile bonde la unyenyekevu?”

ASIYERIDHIKA

Mwaminifu alijibu swali aliloulizwa. “Naam, nilimkuta mtu jina lake Asiyeridhika,
aliyenitaka nirudi nyuma pamoja naye. Sababu yake ilikuwa ati kwamba hilo
bonde halimpatii mtu heshima kwa lolote. Aliniambia pia kwamba marafiki zangu
wote kama vile Kaburi, Mfidhuli, Mwenye Kujikinai na Utukufu wa Dunia
watachukizwa sana nikijifanya mpumbavu kiasi hiki kwa ujaribu kulipitia hilo
bonde gumu.”

38
“Nawe, Je, ulimjibuje?” Aliuliza Mkristo.
“Nilimwambia kuwa hawa walikuwa wa mbari yangu, lakini tangu nilipopata
kuwa msafiri wamenikataa. Nilimwambia tena kwamba kabla ya heshima huja
unyenyekevu, na roho yenye kiburi kabla ya kosa. Kwa hiyo ningependelea
kulipitia bonde hilo na kupata heshima ambayo wenye hekima wanaitafuta”.
Alijibu Mwaminifu. “Je, ulikutana na kitu kingine zaidi katika bonde hilo?”
aliuliza Mkristo.
“Naam,” alijibu Mwaminifu; “nilikutana na mtu mwingine jina lake Aibu; lakini
nilidhani jina hilo sio sahihi.”
“Alikuambiaje?” Aliuliza Mkristo.
“Alisema kwamba ni jambo la kuhuzunisha, tena la aibu mtu kujali dini. Alisema
kuwa dhamiri yenye huruma haimfai mtu. Tena akaongeza kuwa ni wachache tu
wenye enzi, nguvu, matajiri, au wenye hekima wangekubali shauri langu. Akasema
kuwa ilikuwa ni fedheha kuomba msamaha kwa jirani yangu kwa ajili ya makosa
au kuyasahihisha iwapo nimemdanganya yeyote”. Alieleza Mwaminifu.

“Nawe ulimwambiaje?” akuliza Mkristo.


Sikujua la kusema hapo mwanzoni,” alijibu mwaminifu; Kisha nikafikiri kuwa
lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu (Lk 16:15); nami
nikazidi kufikiri kuwa huyo Aibu ananiambia jinsi wanadamu walivyo, lakini
haniambii lolote jinsi Mungu alivyo. Nikazidi kufikiri pia kwamba siku ya hukumu
hatutahukumiwa kulingana na wanavyofikiri wanadamu. Tutahukumiwa kufuatana
na hekima pamoja na sheria zake Aliye juu. Kwa hiyo asemayo Mungu ni bora
kuliko yote, ingawaje watu wote waliojifanya wapumbavu kwa ajili ya ufalme wa
mbinguni ndio wenye hekima kuliko wote, na mtu maskini anayempenda Kristo, ni
tajiri mno kuliko mtu mkubwa zaidi ulimwenguni anayemchukia Yeye. Kwa hiyo
nilimfukuza Aibu aende zake. Alikuwa adui wa wokovu wangu.”

Kisha Mkristo akasema, “Nafurahi ndugu yangu kwamba ulisimama kiume kwa
ushujaa mbele ya mtu huyu mwovu. Mimi pia ninakubali ulivyosema kuwa ana
jina lisilo sahihi, maana haoni aibu kufuata njiani na kutufanya tuone haya kwa
ajili ya yote yaliyo mema. Lakini na tuendelee kumpinga.”

“Nadhani inatupasa kuomba msaada juu ya huyo kwa mmoja anayetutaka tuwe
mashujaa duniani kwa ajili ya kweli,” alisema Mwaminifu.

39
“Ndiyo,” akajibu Mkristo. Lakini je, ulikutana na mtu mwingine tena pale
bondeni?”
“La, hasha,” alijibu mwaminifu “maana nilikuwa na mwanga wa jua njiani mwote,
na vile vile katika Bonde la Uvuli wa Mauti.”

WASAFIRI HAWAPATANI NA POROJO

Basi nikaona katika ndoto yangu kwamba hapo walipokuwa wakitembea na


kuendelea mbele, walimkuta mtu jina lake Porojo, nao wakasafiri pamoja.
“Haya twende zetu,” alisema Mwaminifu; “twende tuutumie wakati wetu kwa
kuzungumza mambo ya manufaa.”

“Nafurahi kuwa nimekutana nanyi,” akajibu Porojo; “maana kusema kweli ni


wachache tu wapendao kuutumia wakati jinsi hii wanaposafiri. Hupenda zaidi
kuzungumzia mambo yasiyo na faida. Ni jambo gani lipendezalo na la manufaa
kama kuyazungumzia mambo ya Mungu? Maana kwa kufanya hivyo, mtu aweza
kupata ujuzi wa vitu viovu kama vile ujalivu wa vitu vya mbinguni. Kwa njia hii
watu waweza kujifunza kuwa kuzaliwa upya ni jambo la lazima, na kwamba
matendo yetu mema hayatoshi ili kuupata wokovu, na ya kuwa twaihitaji haki ya
Kristo. Mbali ya hayo, mtu atajifunza kwa mazungumzo ili kujua maana ya
kutubu, kuamini, kusali, kuteswa na mambo kama haya. Tena kwa mazungumzo
atajifunza ahadi kubwa za Mungu na jinsi ya kuwafunza wajinga pia.”

“Haya yote ni kweli,” alisema Mwaminifu. “Nami nafurahia kuyasikia.


“Inasikitisha,” alisema Porojo; “kwamba ni wachache sana wanaofahamu haja
kubwa ya imani na kazi ya neema katika roho zao ili kuupata uzima wa milele.
Kwa ujinga wanaishi kwa matendo ya sheria ambayo kwayo hapana mtu awezaye
kuuingia ufalme wa mbinguni.”

“Vema basi; alisema Mwaminifu. “Ni jambo gani tutakalolizungumza?”


“Lolote ulitakalo,” alijibu Porojo. “Nitazungumza mintarafu jambo lolote kama ni
la kutufaidia.”
Ndipo Mwaminifu aliongeza hatua ili kutembea pamoja na Mkristo, huku akisema,
“Hapana shaka mtu huyo ni msafiri bora sana.”

40
Hapo Mkristo alitabasamu na kusema, “Mtu huyu anatudanganya kwa ulimi wake.
Jina lake ni Porojo, nami nashangaa kwamba humfahamu, maana anaishi mjini
mwetu.”
“Vema; anaonekana kuwa mtu mwema.” Alisisitiza Mwaminifu.”
“Ndivyo anavyoonekana kwa hao wasiomfahamu,” alisema Mkristo. “Mtu huyu
apenda kushirikiana na wowote, na atajiunga na mazungumzo yoyote yale. Kama
vile aongeavyo nawe sasa, ndivyo atakavyoongea hapa anapokutana na wauza
pombe. Kwa jinsi anavyozidi kulewa, ndivyo anavyozidi kuongea. Dini haina
nafasi moyoni mwake au nyumbani mwake, wala katika maisha yake. Yote aliyo
nayo ni katika ulimi wake na dini yake ni kupiga makelele kwa huo.”

“Ndivyo usemavyo”! akasema Mwaminifu kwa mshangao. “Basi nimedanganywa


na mtu huyu.”
“Umedanganywa?” Mkristo aliuliza. “Hapana shaka na hilo. Yeye huzungumza
habari za sala, toba, imani na kuzaliwa upya, lakini yote ayajuayo mintarafu ya
hayo ni mazungumzo tu. Nimekuwa pamoja na jamaa yake ndani ya nyumba yake
hamna dini, hamna sala wala dalili yoyote ya kuzitubia dhambi. Yeye ni aibu na
fedheha ya dini kwao wote wanaomfahamu (Rum. 2:24). Kwa upande wangu
naamini kwamba kwa ajili ya maisha yake maovu amewakosesha wengi na
kuwaangusha. Naye atakuwa sababu ya maanguko ya wengi zaidi.”

“Vema,” Mwaminifu alisema; “mimi naona kwamba kusema na kutenda ni mambo


mawili tofauti. Nami nitaiangalia zaidi hiyo tofauti.”
“Ni mambo mawili tofauti,” Mkristo alieleza; “kweli, nayo ni tofauti kama vile
roho na mwili. Sehemu muhimu ya dini ni matendo. Huyo Porojo hayajui hayo.
Anadhani kusikia na kusema kwatosha kumfanya mtu kuwa Mkristo wa kweli.
Anajidanganya roho yake mwenyewe. Siku ya hukumu watu watahukumiwa
kufuatana na matendo yao.
Hawataulizwa, “Je, uliamini?” Swali litakuwa, “Mlikuwa watendaji au wenye
kuzungumza tu?” Si kwamba kazi iwayo yote isiyotokana na imani itakubaliwa.
Lakini nataka kukuonyesha jinsi maungamo ya huyo Porojo yatakavyokuwa kazi
bure katika siku hiyo.”

“Nifanyeje, ili kuachana naye?” aliuliza Mwaminifu.

41
“Nitakushauri,” alimjibu Mkristo; “naye hatapenda kufuatana nawe, isipokuwa
Mungu atamgusa moyo wake na kuugeuza. Zungumza naye kwa makini sana
mintarafu nguvu ya dini. Akiisha kukubali mwulize wazi wazi kwamba
ameyaweka hayo moyoni mwake, nyumbani mwake na katika mwenendo wake.”
Ndipo Mwaminifu alisogea kando apate kufuatana na Porojo, akasema,
“Nimeamua tuyazungumzie mambo haya: Neema ya Mungu iokoayo yajionyesha
namna gani inapokuwa moyoni mwa mtu?”
“Vema, ni swali zuri sana. Nami ni tayari kukujibu,” alisema Mkristo. “Kwanza,
hiyo neema ya Mungu ikiwamo moyoni inasababisha kuikemea dhambi kwa
makelele makuu. Pili …..”
“Ngoja kwanza, twende tukifikiri habari za kila jambo moja moja. Nadhani
ingekuwa bora kusema neema hujionyesha kwa kule kuifanya roho iichukie
dhambi,” akasema Mwaminifu.

“Kwani kuna tofauti gani kati ya kuzililia dhambi kwa suti kuu na kuzichukia?”
aliuliza Porojo.
“Aha, pana tofauti sana. Mimi nimewasikia wengi wakizililia dhambi kwa sauti
kuu wanapohubiri, ambao waweza kuzikubali mioyoni mwao na maishani mwao.
Huyo mwanamke aliyetaka kumkosesha Yusufu alipiga kelele kwa sauti kuu kana
kwamba alikuwa mtakatifu sana (Mwa 39:15). Lakini kwa kweli alitaka kutenda
dhambi. Watu wengine wazililia dhambi kama vile mama amkemeavyo mtoto
wake huku akimtukana na baadaye humkumbatia na kumbusu-busu. Lakini ni
jambo gani la pili ambalo lingeshuhudia kuwa neema ilikuwa inafanya kazi
moyoni?” aliuliza Mwaminifu.

“Naona ni kuzijua sana siri za hiyo Injili,” alisema Porojo.


“Lakini ufahamu mkubwa unaweza kupatikana katika siri za Injili na hata hivyo
kusiwe na kazi ya hiyo neema moyoni,” alisema Mwaminifu. “Kristo alipouliza,
“Je, mmeelewa na hayo niliyowatendea?” aliongeza, “Mkiyajua hayo, heri ninyi
mkiyatenda” (Yn 13:17). Uheri haupo katika kuyajua bali katika kuyatenda. Kujua
kwawapendeza wenye maneno mengi na wenye majisifu. Kutenda ndiko
kumpenezako Mungu. “Je, ungependa kuniambia dalili nyingine jinsi neema ya
Mungu inavyojionyesha ilipo?”
“La. Sitaki tena,” alijibu Porojo”maana naona hatutaridhiana.”

42
“Basi iwapo wewe hutaki, utaniruhuhusu mimi? Kazi ya neema rohoni
inajionyesha kwake aliye nayo na tena kwa hao wanaoingojea. Kwake aliye nayo,
humpa thibitisho la hatia ya dhambi. Inamwonyesha tabia yake ya asili na dhambi
ya kutoamini itakayompatia adhabu ya milele ikiwa hapati rehema mkononi mwa
Mungu kwa njia ya imani katika Yesu Kristo. Neema hiyo hufanya kazi ndani yake
na humfanya kusikitika na kutahayari kwa ajili ya dhambi. Naye anajua kwamba ni
lazima kumwendea Kristo, Mwokozi wa ulimwengu kama anataka kuupata uzima
huo. Basi kwa kadiri ya imani yake kwa Mwokozi wake kwamba ni imara au
dhaifu, ndivyo itakavyokuwa furaha yake na amani. Ndivyo litakavyokuwa pendo
lake kwa huo utakatifu. Ndivyo na tamaa zake zilivyo, huku akitamani kumjua
Yeye zaidi, na kumtumikia katika ulimwengu huu.”

Kwa wengine neema inajionyesha kwa kuikiri kwao imani katika Kristo na kwa
maisha yanayolingana na kukiri huko. Tena inajionyesha kwa maisha ya utakatifu
moyoni na maishani, si kwa mazungumzo tu kama afanyavyo mnafiki au mwenye
maneno mengi.”
“Sasa kama hutakaidi, nataka kukuuliza swali lingine,” alisema Mwaminifu.
“Mimi sikaidi,” alijibu Porojo. “Swali lako ni lipi?” dini yako ni ya maneno na
katika ulimi, na wala si katika tendo la kweli?” Mwaminifu aliuliza.

Kisha Porojo akaanza kupotewa na raha, lakini baadaye akajibu, “Mimi


sikutazamia mazungumzo ya namna hii.
Mimi si tayari kutoa jibu kwa maswali kama haya. Ebu niambie, kwa nini
waniuliza? “Kusema kweli yote,” alisema Mwaminifu, “nimesikia kwamba wewe
u mtu ambaye dini yako ni ya maneno tu. Mwenendo wako waonyesha kuwa
huyaamini usemayo. Watu wasema ya kuwa wewe ni aibu kwa Wakristo fedheha
kwa wale wote wanaokuamini wewe.”

BWANA POROJO AONDOKA

“Basi wewe kwa vile ulivyokuwa tayari kuziamini habari hizi na kuhukumu kwa
upesi sana, hufai kwa mazungumzo. Basi kwa heri,” alimaliza Bwana Porojo.
Ndipo akaenda zake. Kisha Mkristo akamkaribia Mwaminifu akasema,
”Nilikuambia yatakayokuwa. Aona ni vema kukuacha wewe kuliko kuyabadili
maisha yake. Ametupungiza udhia kwa kuondoka kwake.” “Lakini mimi nafurahi

43
kwamba tulizungumza naye machache,” alisema Mwaminifu. “Huenda akayafikiri
tena.”

“Ulifanya vema kuzungumza naye wazi wazi. Siku hizi ni shida kumwona mtu
atakayesema na watu kwa uaminifu. Ndiyo sababu mambo ya dini yaonekana
mabaya kwa watu wengi. Lakini hawa wapumbavu wenye maneno mengi
wapokewa katika ushirika wa Wakristo, nao ulimwengu hauwezi kufahamu. Ni
aibu kwa Ukristo na huzuni kwa hao walio wanyofu. Laiti watu wote
wangewatendea hao kama ulivyofanya,” alimaliza Mkristo.

MWINJILISTI AKUTANA NA WASAFIRI

Hivyo wakaendelea mbele wakizunguza na hata kuifanya hiyo njia kuwa nyepesi
vile ambavyo bila mazungumzo wangeiona kuwa ni ya kuchosha. Basi
walipokuwa karibu kulipita hilo pori Mwinjilisti akatokea na kuwasalimu. Mkristo
na Mwaminifu walifurahi sana kumwona. Wakamsimlia mambo yote yaliyowapata
njiani na jinsi walivyofika hapo kwa shida.

“Nafurahi,” alisema Mwinjilisti; “si kwa sababu mlikutana na majaribu, bali kwa
sababu mmekuwa washindi na kwamba mmedumu katika njia hii. Endeleeni kwa
uthabiti kwa maana mnao uwezo wa mbinguni na wa dunia upande wenu.”

Kisha Mkristo akamshukuru huyo Mwinjilisti kwa ajili ya maneno ya faraja


aliyowapa. Akaomba iwapo Mwinjilisti angewaambia habari za mambo ambayo
yangeweza kuwapata na jinsi watakavyoweza kuyapinga na kuyashinda.

“Wanangu,” akasema Mwinjilisti, “mmesikia kwamba imewapasa kuingia katika


ufalme wa mbinguni kwa njia ya dhiki nyingi. Karibu sasa mtaingia mjini. Humo
mmoja wenu au nyote wawili itawapasa kutia muhuri ushuhuda mlio nao kwa
damu. Lakini muwe waaminifu hata kufa, naye Mfalme atawapa taji ya uzima.”

44
WASAFIRI WATAABIKA PENYE SOKO LA UBATILI

Kisha nikaona katika ndoto yangu kwamba walipokwisha toka katika hilo pori,
waliuona mji mbele yao, jina la mji huo lilikuwa Ubatili (Zab 62:9). Mjini humo
mlikuwa na soko lililoitwa Soko la Ubatili. Hapo zamani sana Shetani alipoona
kuwa njia ya wasafiri ilipitia mjini humo, alijenga soko. Ndani yake aina
mbalimbali za vitu vya kudunia vinauzwa kwa kwa mwaka mzima. Hivyo katika
soko hili vyauzwa vitu kama vile nyumba, ardhi, bidhaa , uchumi, heshima, tamaa,
vyeo, nchi, falme, raha, furaha za kila namna na uovu wa kila namna.

Wasafiri penye Soko Ubatili

Iliwapaswa wasafiri kulipitia soko hilo. Mara tu walipoingia, watu walianza


kuwazunguka kwa sababu mbalimbali.

Lakini wasafiri hawa wahakuviangalia sembuse kuvitazama vitu vilivyouzwa. Mtu


yeyote alipowavuta kununua kitu walisema sala hii: “Unigeuze macho yangu
nisitazame visivyofaa” (Zab 119:37). Baadhi ya wauzaji huko sokoni walisema,
“hao walikuwa wapumbavu, na wengine kwamba wana wazimu (Ayu 12:4; 1 Kor
4:9).” Wengine waliwadhihaki na wengine wakawahimiza wenzao ili wawapige
mno; na machafuko yalizuka pale sokoni hata pakawa hapana amani.

45
KUKAMATWA NA KUTIWA KUZIMBANI

Ndipo Mkuu wa Tamasha alisikia habari hizo akawatuma baadhi ya rafiki zake wa
kuaminika ili kuachukua watu hao na kuwahoji. Lakini hao waliochaguliwa
kuwahoji waliamini kuwa watu hao ni wenda wazimu. Au tena walifikiri kuwa
watu hao walifika ili kuleta fujo hapo sokoni. Kwa hiyo walikamatwa na kupigwa
pamoja na kupakwa matope mwilini. Kisha wakatiwa katika kizimba cha chuma ili
kwamba waweze kuonekana na kudhihakiwa na wote waliokuwapo mnadani.

Wasafiri walikaa kizimbani kwa muda wakichekwa na kuonewa hasira. Lakini


wasafiri walivumilia, wakirudisha maneno mazuri kwa hayo mabaya
waliyonenewa, na vitendo vyema badala ya vile viovu. Kisha waliletwa tena mbele
ya wenye kuwahoji. Wakawapiga bila huruma na kuwafunga kwa minyororo.
Wakazazungusha huku na huko pale sokoni ili wawe kielelezo na kitisho kwa
wengine.

Lakini Mkristo na Mwaminifu walitenda kwa akili sana. Wakaipokea aibu kwa
upole mno na uvumilivu hata wachache pale sokoni kweli wakavutwa upande wao.
Hili liliwachukiza zaidi hao wengine. Basi wakajaribu kuwaogofya kwa
kuwaambia kuwa watauawa. Wakawatia tena kizimbani na kuifunga miguu yao
katika mkatale. Ndipo waliyakumbuka hayo waliyokuwa wameambiwa na
Mwinjilisti. Wakafarijiana wao kwa sababu walijua kwamba huyo ayakayekufa
ndiye atakayekuwa na hali njema zaidi. Hivyo kila mmoja wao alitamani moyoni
awe ndiye atakayekufa.

HUKUMU

Kisha katika wakati wa kufaa waliletwa ili wahukumiwe. Mashahidi watatu –


Husuda, Imani-Mbovu na Mkatili na wakawashitaki hao wawili. Waamuzi
walikuwa Bwana Kipofu, Bwana Hana-Wema, Bwana Uovu, Bwana Mpenda-
Shauku, Bwana Mponda-Mali, Bwana kichwa-Ngumu, Bwana Uadui, Bwana
Mwongo, Bwana Mkalili, Bwana Mchukia-Nuru na Bwana Mwenye-Chuki. Wote
wakaamua kuwa Mwaminifu alikuwa na hatia na kwamba alistahili kufa.

46
MWAMINIFU AUAWA KISHAHIDI

Kwa hiyo wakamtoa nje ili kumtendea kama ilivyokuwa desturi yao. Kwanza
walimpiga na kisha wakamkata-kata kwa visu. Baada ya hayo walimtupia mawe na
kumjeruhi kwa moto hali wamemfunga penye nguzo. Hivi ndivyo Mwaminifu
alivyoufikia mwisho wa maishia yake.

Basi niliona kwamba nyuma ya mkutano kulisimama gari na farasi wakimngojea


huyo Mwaminifu. Wakamchukua mawinguni kwa gari hilo pamoja na sauti ya
parapanda mpaka kwenye lango la Mbinguni. Mkristo alirudishwa gerezani, lakini
Yeye aamuruye mambo yote alimfanya atoroke kutoka mikono ya adui zake.

MWENYE-TUMAINI ANAJIUNGA NA MKRISTO.


Kisha nikaona katika ndoto yangu ya kwamba Mkristo hakuendelea na safari peke
yake. Mmoja jina lake Mwenye-Tumaini, aliyasikia maneno ya Mwaminifu na
Mkristo. Aliangalia sana jinsi walivyovumilia katika mateso, na sasa alijiunga na
Mkristo. Hivi ndivyo mmoja alivyokufa ili kuishuhudia kweli, na mwingine
anainuka kutoka mavumbi yake ili kuwa mwenzake Mkristo katika safari yake.
Mwenye-Tumaini alisema, “pia alikuwa na hakika walikuwa watu wengi zaidi
mjini ambao watafuata baadaye.”

47
Mwenye-Tumaini anajiunga na Mkristo

Hivyo nikaona ya kwamba wakiisha kutoka pale penye mnada walimkuta mtu jina
lake Mpenda-Faida. Alikuwa anatoka katika mji uitwao Usemi-Mzuri. Aliwaambia
kwamba alikuwa nao jamaa wengi matajiri katika mji huo. Mintarafa mambo ya
dini aliwaeleza akisema, “tunatofautiana katika mambo ya dini na watu wengine
kwa vipengele vidogo viwili: kwanza, sisi hatushindani kamwe na tabia zisizo
saidia kitu. Pili, tu wenye bidii siku zote dini inapopendwa vema.” Mpenda-Faida
akaendelea kuwaeleza kwamba ikiwa watakubali kusafiri pamoja naye watamwona
kuwa mtu mwema sana.

Mkristo akajibu, “kama utafuatana nasi itakupasa kusafiri katika majira mema ya
mwaka na majira mabaya. Imekupasa pia kuikiri dini hapo inapokataliwa kama
vile unavyokiri pale inapopendwa vema. Inakupasa pia kusimama karibu nayo
hapo inapofungwa kwa minyororo na hali kadhalika inapotembea njiani na
kusifiwa na watu.

“Haya niache nichague nitakalo, lakini niruhusu nifuatane nanyi,” akasema


Mpemda-Faida.
“La, huwezi kufuatana nasi isipokuwa umefanya kama tufanyavyo sisi,” alijibu
Mkristo.
Kisha Mpenda-Faida akasema, “Mimi sitaacha kamwe na fikira zangu za zamani,
maana hazimdhuru mtu, kisha zina faida. Kama hamnikubali nifuatane nanyi
nitakwenda peke yangu mpaka nitakapokutana na wengine watakokubaliana
nami.”

MARAFIKI WATATU NA MPENDA-FAIDA

Basi niliona katika ndoto yangu kwamba Mkristo na Mwenye-Tumaini


walimwacha mtu huyo, wakamtamgulia mbele yake. Ndipo walipoangalia nyuma
wakawaona watu watatu wakijiunga na huyo Mpenda-Faida. Majina yao yalikuwa:
Bwana Okoa-Yote, Bwana Mshika-Dunia na Bwana Mpenda-Mali. Huyu Bwana
Mpenda-Faida aliwafahamu kwa sababu walikuwa wanafunzi pamoja katika Shule
ya Mwalimu Mkaza-Mno. Mwalimu huyo aliwafundisha jinsi ya kuyapata

48
waliyoyataka ama kwa nguvu au kwa kubembeleza, kwa kusema uongo au hata
kwa kujifanya ni watu wa dini.

Basi walipokwisha amkiana Mpenda-Mali akamwuliza Mpenda-Faida, “Ni kina


nani watu hao walio mbele yetu?” Mpenda-Faida alijibu, “Hao ni watu watoka
nchi ya mbali, na kutokana na namna yao walivyo waenda kuhiji.” “Lakini kwa
nini hawakutungojea,” aliuliza Mpenda-Mali; “na tungeliweza kufuatana nao,
maana sote twaenda kuhiji.”

“Ni kweli usemayo,” alijibu Mpenda-Faida. “lakini watu hao ni washupavu sana,
nao wanayatia maanani maazimio yao wenyewe hata hawapendi mashauri ya
wengine. Ijapokuwa mtu ni mchaji Mungu, kama hakubaliani nao katika mambo
yote, watamsukumia mbali asifuatane nao. Wao wanaamini katika kuyashikilia
maazimio yao ijapokuwa watu wengine wanawapinga. Lakini mimi naifuata dini tu
mradi naweza kupata faida ndani yake.”

Walipokuwa wakiendelea mbele walikaza mwendo na kuwafikia Mkristo na


Mwenye-Tumaini. Ndipo Mpenda-Faida akawauliza swali: “Mwaonaje iwapo mtu
fulani anayo biashara duni katika ulimwengu huu, lakini akaambiwa biashara yake
ingeongezeka tu ikiwa atakuwa mshika dini sana. Je, haitakuwa sawa kwake
kufanya hivyo ili apate hiyo faida, na wakati huo huo akawa bado ni mtu
mwema?”

Mkristo alijibu akisema, “Hata mtoto mchanga katika mambo ya dini aweza
kuyajibu maswali kama haya. Si vizuri kwa watu kumfuata Kristo ili kuipata
mikate aliyowapa (Yn 6:26-27). Kwa hiyo vibaya zaidi namna gani kumfanya
Kristo na dini kana kwamba ni njia ya kuupata na kuufurahia ulimwengu?
Wapagani, wanafiki na mashetani ndio wanaofikiri kama hivyo. Nami nafikiri
kuwa mtu anayeishika dini ili kuupata ulimwengu, ataitupa dini yake kwa urahisi
kwa ajili ya ulimwengu, kama Yuda alivyofanya.”

Ndipo watu hao wakasimama na kuangaliana wao kwa wao, lakini hawakuweza
kumjibu Mkristo. Mwenye-Tumaini na Mkristo wakendelea mbele wakiwaacha
Mpenda-Faida na Rafiki zake nyuma. Na Mkristo akasema, “Ikiwa watu hawa

49
hawawezi kustahimili maswali ya binadamu mwenzao, watawezaje kustahimili
yale watakayoulizwa mbele ya kiti cha hukumu ya Mungu?”

DEMA NA CHIMBO LA FEDHA

Kisha Mkristo na Mwenye-Tumaini wakaendelea tena mbele. Wakaenda mpaka


walipofika uwanda mpana ulioitwa Raha.

Dema na chimbo la fedha.

Waliupita uwanda huo bila shida. Kwa upande wa pili wa uwanda kulikuwa na
kilima kidogo kilichoitwa Faida-Mbaya ambapo palikuwa na chimbo la fedha.
Kisha nikaona katika ndoto yangu ya kuwa mbali kidogo na hiyo njia karibu na
hilo chimbo la fedha alisimama Dema (2 Tim 4:10). Huyo akawaita Mkristo na
mwenzake, akasema, “Geukeni upande huu nami nitawaonyesha kitu.” Lakini wao
hawakumsikiliza, wala hawakukubali kugeuka na kumtazama.

“Ninayo haki kwamba Mpenda-Faida na wenzake wafikapo hapa hawakosi


watageuka na kwenda huko kuangalia,” alisema Mwenye-Tumaini.
“Hapana shaka, maana fikira zao huwaongoza hivyo. Nami nafikiri watakufa huko
huko,” akaongeza Mkristo.

NGUZO YA CHUMVI

Ndipo nikaona ya kwamba upande wa pili wa uwanda huu wasafiri waliifikia


nguzo ya zamani karibu na njia. Wote wawili walishangaa kwa ajili ya umbo la
ajabu la nguzo, maana ilionekana kama mwanamke. Kisha Mwenye-Tumaini

50
aliona Maandiko juu ya kichwa chake, yameandikwa hivi: “Mkumbukeni mkewe
Lutu.” Ndipo wakakumbuka kuwa nguzo hii ya chumvi ilikuwa ndiyo ile ya
mkewe Lutu. Wakakumbuka kwamba alipata kugeuzwa kuwa nguzo ya chumvi
kwa sababu alitazama nyumba hali mwenye moyo wa choyo wakati alipokuwa
akikimbia kutoka mji wa Sodoma (Mwa 19:26).

Nguzo ya Chumvi

Kisha niliona kuwa waliendelea mbele hata wakaufikia mto wa kupendeza, ambao
Mfalme Daudi aliuita “Mto wa Mungu” (Zab 65:9), lakini Yohana aliuita “Mto wa
Maji ya Uzima” (Ufu 22:1). Wakaendelea mbele wenye furaha sana katika hiyo
njia iliyouambaa huo mto. Wakanywa pia maji ya huo mto ambayo yaliburudisha
roho zao zilizochoka. Kandokando ya mto upande huu na upande ule kulikuwa na
miti mikubwa iliyokuwa na matunda ya kila aina. Kila upande wa huo mto
kulikuwa na konde lenye majani na maua mazuri. Walikaa katika shamba
mojawapo kwa siku chache, maana hapa waliweza kujinyosha na kulala salama
salimini (Zab 23:2-3).

JITU KUKATA-TAMAA AWACHUKUA WASAFIRI MPAKA KWENYE


NGOME WASIWASI.

Kisha nikaona katika ndoto yangu kwamba hapo walipokuwa wakiendelea mbele,
njia iliuacha huo mto. Walisikitika kuuacha huo mto lakini hawakuthubutu kuiacha
hiyo njia. Kisha hiyo njia ilikuwa si nzuri, ilikuwa inaparuza, nao wakafa moyo na
wakatamani njia iliyo nzuri zaidi.

51
Basi kitambo kidogo tu mbele yao kwa upande wa kushoto wa njia kulikuwa na
madaraja machache yaliyoelekea kwenye konde liitwalo Njia-ya-kando ya shamba.
Kisha Mkristo akayapanda madaraja na akakiona kinjia kikiongoza karibu na njia
yao kwa upande wa pili wa boma, “Njoo, Mwenye-Tumaini. Twende tuvuke,”
akasema Mkristo.

“Lakini itakuwaje iwapo njia hiyo itatukosesha?” aliuliza Mwenye-Tumaini.


“Haielekei itakuwa hivyo,” alijibu Mkristo. “Tazama, yaenda sambamba na njia hii
tunayoipitia.”
Hivyo Mwenye-Tumaini alisadikishwa na mwenzake akamfuata. Wakakiona kinjia
hicho kuwa rahisi sana kukifuata. Walipotazama mbele walimwona mtu
akitembea. Jina lake huyo mtu lilikuwa Matumaini-ya-Bure. Basi walimwita na
wakamwuliza, “njia hiyo ilikwenda mpaka wapi?”

“Inakwenda mpaka Mji wa Mbinguni,” alijibu.


“Waona.” Alisema Mkristo. “Mimi sikukuambia hivyo? Tuko salama.
Lakini walipokuwa wakimfuata usiku uliingia na kukawa giza sana. Hawakuweza
kumwona mtu huyo aliyewatangulia. Matumaini-ya-Bure aliendelea mbele lakini
hakuweza kuiona hiyo njia mbele yake. Akaanguka katika shimo refu na
kuangamia pale pale.

Ndipo ikaanza kunyesha mvua na kulikuwa na radi pamoja na ngurumo kwa jinsi
ya kutisha, na maji yakaifunika njia. Kisha Mwenye-Tumaini akasema kwa
masikitiko, “Aha, ni afadhali ningeliishika njia yangu.”
“Nani angedhani kwamba njia hii ingetupeleka kwingineko?” alisema Mkristo.
“Mimi niliogopa tangu mwanzo,” akasema Mwenye-Tumaini. “Ningelisema wazi
wazi kama hungekuwa mkubwa wangu.”
“Tafadhali nisamehe, sikukusudi maovu,” alisema Mkristo. “Twende tujaribu
kurudi nyuma tena.”

Kwa wakati huu kurudi nyuma kulikuwa na hatari sana. Wakajaribu kurudi nyuma,
lakini kulikuwa na giza, na hayo maji yakaongezeka mno hata hawakuweza
kuyafikia madaraja usiku ule. Mwishowe walikiona kibanda kidogo wakaingia
ndani yake, na kwa vile walikuwa wamechoka sana wakashikwa na usingizi
wakalala

52
JITU KUKATA-TAMAA

Basi si mbali sana na mahali walipokuwa wamelala palikuwa na jengo imara


ililoitwa Ngome-Wasiwasi. Lilikuwa mali ya Jitu katili aliyeitwa Kukata-Tamaa.
Mapema sana asubuhi, hilo jitu Kukata-Tamaa lilikuwa likitembea huku na huko
katika mashamba yake. Likawaona Mkristo na Mwenye-Tumaini hali wamelala.
Likawaamsha kwa sauti ya ukali na ya kikatili. Likwauliza wao ni akina nani na
tena wanafanya nini katika hozi yake. Wakaliambia wao ni wasafiri na ya kwamba
walikuwa wamepotea. Ndipo Jitu Kukata-Tamaa likasema, “Mmeruka mpaka kwa
kutembea katika mashamba yangu na kulala katika hozi yangu. Kwa hiyo
imewapasa mnifuatae.”

Hivyo walilazimishwa kwenda kwa sababu hilo Jitu lilikuwa la kutisha na lenye
nguvu kuliko wao. Nao hawakuwa na la kusema kwa sababu walijua kuwa
wamekosa.

NDANI YA NGOME-WASIWASI

Ndipo Jitu likawasukumiza mbele yake. Likawatia katika ngome ndani ya chumba
chenye giza sana, kichafu, nacho kilikuwa na harufu mbaya. Wakalala huko kwa
siku nne bila chakula chochote wala maji ya kunywa. Hapakuwa na mwanga na
hakuna mtu yeyote aliyewauliza hali zao. Basi huyo Mkristo alikuwa ana majonzi
juu ya majonzi. Ilikuwa ni hiyo haraka yake iliyowaletea mashaka haya.

Hilo Jitu Kukata-Tamaa lilikuwa na mkewe aliyeitwa Kutoamini-Nafsi. Basi


lilipokwenda kulala lilimwambia mkewe hayo liliyofanya. Nalo likamtaka mkewe
ampe shauri litakavyowatendea hao wafungwa. Yeye akamwambia atakapoamka
awapige pasipo kuwahurumia. Hivyo asubuhi jitu lilichukua rungu kubwa sana
likawaendea na kuwakaripia sana. Kisha likawapiga hata wasiweze kujitetea.
Hawakuweza hata kujigeuza hapo sakafuni walipolala. Kisha likawaacha
wakisononeka. Basi walidumu mchana wote wakisononeka na kulia.

Asubuhi yake liliwaendea kama lilivyofanya hapo kwanza. Likaona ya kuwa


walikuwa wameumia sana kwa hayo mapigo liliyowapiga. Likawaambia kwamba

53
hawatatoka kamwe mahali hapo. Kwa hiyo njia ya pekee kwao ilikuwa ni kujiua
kwa kisu, au kujinyonga au kula sumu. “Maana mwapenda kuishi kwa sababu
gani,” lilisema, “ambapo maisha yenu yamejaa maumivu?”

Hao wawili wakaliomba lile Jitu Kukata-Tamaa liwaachilie waende zao.


Waliposema hayo Jitu likawaendea huku limekunja uso. Hapana shaka
lingeliwaua Jitu lenyewe, lakini lilishikwa na kifafa, likaanguka chini. Kwa muda
halikuweza kuitumia mikono yake na hivyo likawaacha.

“Ndugu, tutafanyaje?” aliuliza Mkristo. “Maisha yetu hapa ni yenye taabu, sijui
kama ni vizuri kuishi hali hii au kuyaondoa maisha yangu mwenyewe. Roho yangu
yachagua kufa kuliko kuishi. Ni heri kuwamo kaburini kuliko chumba hiki cha
kutisha. Je, tutalifuata shauri la hilo jitu?”

“Hali yetu hivi sasa ni ya kutisha,” alijibu Mwenye-Tumaini. “Kifo kingenifaa


zaidi kuliko kuishi hivi siku zote. Lakini na tufikiri habari za maneno ya Bwana
mintarafu hiyo nchi tunayoiendea. Amesema hivi, “Usiue.” Iwapo hatungemwua
mtu mwingine sembuse kujiua nafsi zetu. Mbali ya hayo, yeye amuuaye mtu
mwingine ameuua mwili wake tu. Lakini iwapo mtu anajiua mwenyewe anaua
mwili na roho mara moja. Nawe ndugu yangu waongea habari za kupumzika
kaburini, lakini umesahau kule kuzimu. Kwani huko ndiko waendako wauaji
wote, maana kila mauuaji hana uzima wa milele” (1 Yn 3:15).

“Na tukumbuke pia kwamba hilo jitu Kutaka-Tamaa halinazo sheria zote mikononi
mwake. Watu wengine walikamatwa na lenyewe, lakini waliokoka kutoka mikono
yake. Ni nani ajuaye, yumkini huyo Mungu, aliyeuumba ulimwenguu, atamfanya
Jitu Kukata-Tamaa afe? Au pengine huenda likasahau kutufungia mlango! Au
huenda likashikwa tena na kifafa mbele yetu hata lisiweze kuitumia mikono yake
na miguu? Na tuwe na saburi, tukavumilie kwa muda. Wakati utafika
tutakapokuwa huru. Lakini tusijiue wenyewe.”

Kwa maneno hayo Mwenye-Tumaini alimtia moyo nduguye. Hivyo wakaendelea


kukaa gizani pamoja siku ile katika hali yao ya huzuni isiyo na furaha. Sasa karibu
ni jioni hilo Jitu likateremka tena chumbani humo ili kuona kama wafungwa wake
wanayashika mashauri yake. Lakini lilipowafikia liliwakuta wangali hai.
Likawaghadhaibikia sana na kukasirika. Likawaambia kwamba ingekuwa heri
kama wasingalizaliwa.

54
Basi hao wawili walitetemeka sana, nao wakongea iwapo wangeyashika mashauri
ya Jitu au sivyo. Huyo Mkristo alionekana tena kama alitaka kuyafuata. Lakini
Mwenye-Tumaini alisema, “Ndugu yangu, unakumbuka vile ambavyo umekuwa
shujaa hata hivi sasa. Shetani hakuweza kukushinda, wala hayo yote uliyoyaona,
kuyasikia na kukutana katika Bonde la Uvuli-wa-Mauti. Nawe sasa u mwoga?
Mimi nipo pamoja nawe hapa, mtu aliye mnyonge kuliko wewe. Jitu amenijeruhi
na kuninyima chakula na maji. Lakini na tuvumilie zaidi kidogo. Kumbuka pale
penye Soko la Ubatili hukuuogopa mnyororo, kizimba, wala kifo.”

Asubuhi yake Jitu liliwaendea tena. Kisha likawachukua mpaka kwenye uwanja
wa ngome, nalo likawaonyesha mifupa na mafuvu kama mkewe alivyosema.
“Hawa walikuwa wasafiri kama ninyi,” alisema; “na walipita katika mashamba
yangu kama ninyi mlivyofanya.”
“Nami nilipopenda niliwararua vipande-vipande, na ndivyo nitakavyowatenda
ninyi.” Ndipo lilipowapiga na kuwarusha chumbani.

Jitu Kukata-Tamaa

Basi ulipoingia usiku Jitu lilistaajabu kwa nini mapigo yake wala mashauri yake
hayakuweza kuwamaliza. Kwa ajili ya hayo mkewe alijibu, “Naona wanayo
matumaini ya kwamba mtu fulani atakuja na kuwafungulia. Au huenda wanazo

55
funguo ambazo kwazo watumaini kujiokoa.” “Nitawapekua-pekua asubuhi,”
likasema Jitu.

UFUNGUO WA AHADI

Basi usiku ule panapo usiku wa manane, walianza kusali, nao waliendelea kusali
mpaka karibu na kucha. Basi ilikuwa majira kidogo tu kabla ya kucha huyo
Mkristo akaanza kusema kama mtu aliyeshangaa. “Jinsi nilivyo mpumbavu,”
alisema; “kulala katika chumba cha kuchukiza ambapo nigeweza kuwa huru.
Ninao ufunguo mfukoni uitwao Ahadi. Nina hakika utafungua kufuli lolote katika
ngome hii.”

Ufunguo wa ahadi

Kisha Mwenye-Tumaini akasema, “Hizo ni habari njema. Toa huo ufunguo ili
tujaribu.” Ndipo Mkristo akautoa ufunguo humo mfukoni na akaanza kujaribu
kuufungua huo mlango. Mara alipougeuza huo ufunguo kwenye kufuli, mlango
ukafunguka, nao wakatoka nje. Kisha wakaufungua mlango wa kutokea kwenye
uwanja wa ngome. Baada ya hayo wakauendea mlango wa chuma. Kufuli la
mlango huu lilikuwa gumu sana, lakini hata hivyo lilifunguka. Ndipo walilisukuma
lango ili watoke nje upesi. Lakini lango lilifanya kelele nyingi hata kuliamsha hilo
Jitu Kutaka-Tamaa. Liliamka upesi ili kuwakamata wafungwa wake, lakini
lilishikwa na ugonjwa wake wa kifafa lisiweze kuwafuatia.

Basi wakaendelea mpaka kuifikia tena Njia kuu ya Mfalme na hivyo wakawa
salama. Kisha wakaandika tangazo karibu na madaraja ili kuwaonya wasafiri.
Wengi waliofuata baadaye waliyosoma yaliyoandikwa wakaokoka na hatari.

56
WASAFIRI WANAKAA NA WACHUNGAJI

Basi wakendelea mbele hata wakaifika milima ya kupendeza. Hivyo wakaipanda


hiyo milima ili kuziona bustani, miti na chemchemi za maji. Wakanywa maji huko
na kula matunda ya miti, wakaburudika.

Basi juu ya milima kulikuwa na Wachungaji waliokuwa wakilisha kondoo wao


karibu na njia. “Milima hii ya kupendeza ni ya nani? Waliuliza hao wasafiri. “Nao
hao kondoo ni wa nani?”
“Milimi hii yaitwa nchi ya Imanueli, na hawa kondoo ni wake pia,” wakajibu
Wachungaji.
“Naam, mwaenda katika njia iliyo sawa,” wakajibu Wachugaji.

Kisha nikaona katika ndoto yangu kwamba Wachungaji hao waliwauliza maswali
hao wasafiri. Walipoyasikia majibu yao waliwaangalia kwa mapenzi wakasema,
“Karibuni hapa penye Milima ya Kupendeza.”

Wakawachukua wasafiri mahemani kwao na kuwapa chakula. Wakasema kuwa


wangependa wasafiri kukaa nao kwa muda mchache ili wapate kujuana nao.
Waliwataka pia wapate kuyafurahia mambo mema ya Milima ya Kupendeza.
Hivyo wakakaa na Wachungaji siku chache.

Kabla hawajaendelea na safari yao Wachungaji waliwataka wasafiri kutazama


kwenye darubini huko wakielekea lango la Mji wa Mbinguni. Huko wakaona
sehemu ya utukufu wa mahali walipokuwa wakipaendea. Ndipo mmoja wa
Wachungaji akawapa hati ya njia. Mchungaji mwingine akawaambia wajihadhari
na huyo Mbembelezi. Mwingine aliwaambia wahakikishe kwamba hawatalala
katika Nchi-ya-kupendeza-mno. Na mwingine aliwatakia safari njema. Basi
nikaamka! Kisha nikalala na kuota tena, nikawaona wasafiri wale wale
wakiteremka hiyo milima kuelekea mjini.

WASAFIRI WANAKUTANA NA ASIYEJUA-KITU MBEMBELEZI NA


MKANA MUNGU.

ASIYEJUA-KITU

Kisha wakamkuta mtu jina lake Asiyejua-Kitu. Alikuwa akitembea katika njia
ndogo iliyopotoka, nayo ilikutana na ile ya wasafiri. Basi Mkristo akamwuliza
alikotoka na anakokwenda.

57
“Bwana mkubwa,” alijibu, “Mimi nilizaliwa katika nchi iitwayo Majivuno, nami
nauendea Mji wa Mbinguni.” “Lakini wafikiri utaingiaje hapo langoni?” aliuliza
Mkristo. “Inawezekana ukakutana na matatizo huko.”
“Nitaingia kama watu wema wengine waingiavyo,” alijibu Asiyejua-Kitu.

“Lakini una nini cha kuonyesha hapo langoni hili wakufungulie?” aliuliza Mkristo.
“Nayajua mapenzi ya Bwana wangu.” Alisema Asiyejua-Kitu. “Nami ninayo
dhamiri njema. Nalipa madeni yangu, nasali, nafunga, natoa zaka za mapato yangu
na kutoa sadaka. Nimetoka nchi yangu ili niende huko niendako.”

“Lakini hukuingia kwa lile lango dogo jembamba lililopo mwanzoni mwa njia hii.
Uliingia kwa njia ile ndogo iliyopotoka. Kwa hiyo na hofu kwamba haidhuru
unavyojihesabia mwenyewe hutaweza kuingia huo mjini,” alijibu Mkristo.

“Mabwama zangu,” alisema Asiyejua-Kitu; “ninyi mnafuata dini ya nchi yenu,


nami nitafuata dini ya nchi yangu. Natumaini nitakuwa salama. Kwa habari za
lango unalolisema, watu wote wanajua li mbali sana na nchi yetu. Sidhani kwamba
yupo mtu aijuaye walau njia ya kuliendea. Lakini hii haidhuru. Tunayo njia ndogo
yenye majani mabichi, nayo nzuri ya kupendeza iteremkayo kutoka nchi yetu.”

Basi Mkristo alipoona kwamba mtu huyo anajivuna mno, alimnong,oneza


Mwenye-Matumaini akisema, “Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye
(Mit 26:12). Tuzungumze naye zaidi? Au tumwache ayafikiri hayo ambayo
amekwisha yasikia, na baadaye tusimame na kumngojea?”

Basi wakaendelea mbele na Asiyejua-Kitu akifuata. Wakaenda kitambo kidogo


mpaka wakaiona njia ngeni. Sasa hawakujua wafuate njia ipi, kwa sababu zote
mbili zilikuwa za kunyoka. Basi walipokuwa wakifikiri waifuate njia ipi, mtu
mwenye mavazi meupe aliwafikia, akawauliza kwa nini walisimama hapo.
Wakamjibu, “Tunaendea Mji wa Mbinguni, lakini hatujui njia ipi ya kuifuata.”
“Nituatenai,” alisema mtu huyo. “Nami naenda huko huko.”

MBEMBELEZI NA WAVU WAKE

Basi wakamfuata. Lakini kidogo kidogo ile njia iliongoza mbali na huo mji
waliokuwa wakiuendea. Wakaendelea kumfuata. Lakini baadaye kidogo, kabla
hawajaelewa aliyokuwa akiyafanya huyo mtu, akawaingiza katika wavu. Wote
wawili walikuwamo wavuni hata hawakuweza kujitaoa. Kisha nguo ile nyeupe
aliyokuwa ameivaa huyo mtu ikaanguka kutoka mgongoni mwake.

58
“Sasa naelewa kuwa nimekosa,” alisema Mkristo, “Wachungaji walituambia
tujihadhari na huyo Mbembelezi. Tumetambua usemi wa mwenye hekima kuwa ni
kweli hata sasa, “Mwenye kujipendekeza kwa jirani yake, hutandika wavu ili
kuitega miguu yake” (Mit 29:5).
“Pamoja na hayo Wachungaji walitupa hati ya njia kutuelekeza habari za njia
yenyewe, lakini tulisahahu kuisoma,” alisema Mwenye-Tumaini.

Basi hivi wakalala wavuni huku wakijililia. Hatimaye wakamwona mtu mwenye
mwanga umeremetao akiwajia, akiwa na mjeledi mikononi mwake. Akauliza
walikotoka, tena wanafanya nini mahali pale. Wakamwambia kuwa mtu mwenye
mavazi meupe ndiye aliyewaongoza vibaya.

Wasafiri wanadanganywa na Mbembelezi

“Ni huyo Mbembelezi, nabii wa uongo,” alisema huyo mtu. “Alijigeuza


mwenyewe awe mfano wa malaika wa nuru! (2 Kor 11:13-14).” Ndipo akaukata
huo wavu na kuwaacha watoke nje. Kisha akawaongoza nyuma walikotoka mpaka
pale walipoiacha njia yao ili kumfuata Mbembelezi. “Mlilala wapi usiku?”
aliwauliza. “Tulikaribishwa na Wachungaji katika Milima ya Kupendeza,”
walijibu.
“Kwa nini hamkuisoma hiyo hati mliyopewa? Aliwauliza tena wakajibu kwamba
“walisahahu.”
“Hao Wachungaji hawakuaambieni kujihadhari na huyo Mbembelezi?”
“Naam, lakini hatukudhani kuwa mtu huyo mwenye kusema maneno ya kusisimua
aliweza kuwa Mbembelezi (Rum 16:17-18).

59
Ndipo niliona katika ndoto yangu ya kuwa aliwaambia walale chini. Kisha
aliwapiga sana ili kuwafunza njia njema ambayo ingewapasa kuiendea. Naye
alipokuwa akiwapiga alisema, “Wote niwapendao mimi nawakemea, na kuwarudi,
basi uwe na bidii, ukatubu (Ufu 3:19).”

Kisha aliwaambia waende zao mbele na kwamba wayashike maagizo mengine


waliyopewa na Wachungaji. Basi wakamshukuru kwa hisani yake, nao
wakaendelea mbele katika njia iliyowapasa, huku wakiimba.

MKANA – MUNGU

Baadaye punde kidogo walimwona mtu akija na mwishowe akawafikia. Jina lake
aliitwa Mkana-Mungu, naye aliwauliza, “mnakwenda wapi?
“Tunauendea Mlima Sayuni,” walijibu. Ndipo Mkana-Mungu alianza kucheka
sana. “Ninyi ni wapumbavu kiasi gani,” alisema. “Mnajitia katika safari yenye
taabu na mwishoni hamtajipatia chochote. Hakuna mahali kama hapo
mnapopawaza katika ulimwengu huu mzima.”

“Lakini patakuwapo katika ulimwengu ujao,” alijibu Mkristo. “Mimi nilipokuwa


kwetu niliyasikia hayo unayoniambia. Ndiyo maana nilitoka. Nimekuwa
nikiutafuta mji huo kwa muda wa miaka ishirini. Lakini sijauona mji huo hata hivi
sasa.”

“Sisi wawili tumesikia na kusadiki kwamba mahali hapo papo, na paweza


kupatikana,” alisema Mkristo.
“Kama nisingeliamini toka kwetu, nisingefika umbali huu kupatafuta. Na iwapo
kuna mahali kama hapo ningepaona, maana nemetembea umbali zaidi kuliko ninyi.
Kwa hiyo narudi,” akamaliza Mkana-Mungu.
“Je, ni kweli hayo aliyosema huyu?” aliuliza Mkristo. “Angalia”, akasema
Mwenye-Tumaini. “Yeye ni mmojawapo wa wabembelezi. Nini! Hakuna Mlima
Sayuni? Hatukuliona lango la mji hapo tulipokuwa kwenye Milima ya Kupendeza?
Tena, haitupasi sasa kuenenda kwa imani? Twende zetu; mtu Yule mwenye
mjeledi asije akatupta tena.”

“Ndugu yangu,” akasema Mkristo. “Mimi sikuionea shaka kweli ya imani yetu,
nilitaka kukuhakikisha. Mintarafu mtu huyu, ninajua kuwa kapofushwa na mungu
wa ulimwengu huu. Twende tuendelee mbele, hali tunajua tunaiamini hiyo kweli.”

60
Basi wakageuka na kumwacha mtu huyo. Naye akaenda zake hali anacheka.

WASAFIRI WANAPITA NCHI YA KUDANGANYA MOYO

Kisha nikaona katika ndoto yangu ya kwamba waliendelea mbele mpaka waliifikia
nchi moja. Hali ya hewa ya hapo iliwafanya wageni kushikwa na usingizi. Huyo
Mwenye-Tumaini alijiona mzito na mwenye kushikwa na usingizi sana, hata
nashindwa kuyafumbua macho yangu ila kwa shida. Twende tulale hapa kidogo.”

“La,” akasema Mkristo; “kama tukilala hatutaamka kamwe.”


“Ndugu yangu, kwa nini? Usingizi ni mtamu kwa mwenye kufanyakazi. Tutapata
kuburudika tukilala kidogo.”
“Je, hukumbuki? Mmoja wa wachungaji alisema kwamba tusilale katika Nchi-ya-
Kudanganya-moyo. Kwa sababu hiyo, “tusilale usingizi kama wengine, bali
tukeshe, na kuwa na kiasi,” (1 The 5:6).
“Nimekosa,” akasema Mwenye-Tumaini. “Kama ningelikuwa peke yangu
ningelikuwa nikilala, nami ningelikuwamo katika hatari ya mauti.”
“Basi sasa na tuzungumze ili tusishikwe na usingizi,” alisema Mkristo.
Ndipo Mkristo akaanza kusema, “Ulipataje kufikiri hapo mwanzo kufanya vile
ufanyavyo sasa?”

HADITHI YA MWENYE-TUMAINI

“Kwa muda mrefu nilizifurahia mali za dunia. Kisha nilikusikia wewe na


mpendwa wetu Mwaminifu mkisema kwamba mwisho wa mambo hayo ni mauti
(Rum 6:21-23). Kwa kuwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi
(Efe 5:6). Ndipo nilizikumbuka dhambi zangu hapo nilipofikiri kuwa itanipasa
kufika hukumuni upesi.”

“Basi ulifanya nini baadaye?” akauliza Mkristo.


“Niliona kwamba sina budi kujaribu kuishi maisha mema, la sivyo nilikuwa na
hakika ningelikataliwa milele. Basi niliziacha dhambi zangu na nikajitenga pia na
rafiki zangu wenye dhambi. Nikajibidiisha kuzishika kanuni za dini kama vile
kusali, kusoma na kuzililia dhambi zangu. Nami nilifanya mambo mengine mengi,
mno ambayo siwezi kuyataja hapa. Lakini hasa niliposikia usema kama huu:
Matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa unajisi” (Isa 64:6);
“Mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria” (Gal 2:16);

61
“mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, sisi tu watumwa wasio na
faida” (Lk 17:10).

“Kisha nikaanza kufikiri kama hivi: “alisema Mwenye-Tuamini. “Iwapo matendo


yetu yote ya haki ni kama nguo iliyotiwa unajisi, na tena iwapo kwa matendo ya
sheria hapana mwanadamu atakayehesabiwa haki, na kwamba baada ya kuyafanya
yote tuliyoagizwa, hata hivyo tumekuwa watumwa wasio na faida; basi ni ujinga
kufikiri kwamba mtu anaweza kuingia mbinguni kwa kuishika sheria.”

“Kisha nikafikiri habari za mtu mwenye deni la shilingi mia maoja dukani. Lakini
baadaye akawa analipa kila mara kwa bidhaa achukuazo dukani humo, badala ya
kukopa. Hata hivyo deni lake la kwanza lingalipo vitabuni! Mwenye duka anaweza
kumpeleka mahakamani mpaka atakapolipa.”
“Je, hayo yahusiana nawe namna gani?” aliuliza Mkristo.
“Nilitambua kwamba kwa dhambi zangu nilikuwa na deni kubwa kwa Mungu.
Ijapokuwa nabadili hali sasa hata hivyo deni langu la kwanza halijalipwa. Sasa
nitawezaje kuokoka na adhabu ya milele inipasayo kwa sababu ya dhambi zangu?
Tena kulikuwa na jambo jingine lililonisumbua pia. Niliiona dhoruba mpya
ikijichanganya na hayo mema niyafanyayo. Nilifanya dhambi kubwa katika siku
moja itoshayo kunipeleka jehanum kana kwamba sikufanya dhambi kabla ya
hayo,” akamaliza Mwenye-Tumaini.

“Basi ulifanyaje?” akauliza Mkristo.


“Mimi sikujua la kufanya mpaka nilipoongea na huyo Mwaminifu. Aliniambia
kuwa imenipasa kuitafuta haki yake mtu ambaye hakutenda dhambi kamwe,”
alijibu Mwenye-Tuamini.
“Nawe, je uliona ya kuwa kulikuwa na mtu wa namna hiyo?” akauliza Mkristo.
“Aliniambia kwamba mtu hyo ni Bwana Yesu Kristo; anayeketi sasa katika mkono
wa kuume wa Aliye Juu sana (Ebr 10:12). Nikamwuliza jinsi gani haki ya mtu
huyo inavyoweza kumpatia haki mtu mwingine mbele za Mungu. Akaniambia
kuwa Yeye alikuwa Mungu mweza vyote, na ya kwamba alikufa, si kwa ajili yake
mwenyewe, bali kwa ajili yangu. Akaongeza kwamba matendo mema ya Kristo na
stahili zake zitahesabiwa kuwa zangu kama nikimwamini Yeye,” alijibu Mwenye-
Tumaini.
“Kisha ulifanya nini?” aliuliza Mkristo.
“Nilifikiri kwamba Yeye hatapenda kuniokoa,” alijibu Mwenye-Tumaini.
“Kisha huyo Mwaminifu alikuambiaje?” aliuliza Mkristo.

“Aliniambia niende kwake nikaangalie. Ksiha nilisema hainipasi, maana ni


ufidhuli. Lakini akasema sivyo, maana niliitwa niende (Mt 11:28). Kisha

62
nikamwuliza nifanye nini nitakapomwendea. Akasema kuwa sina budi kumwomba
Baba kwa moyo wangu amfunue Yeye kwangu. Nikamwambia kuwa mimi sikujua
la kusema hapo nitakapomwendea. Akanifundisha kusema maneno kama haya: Ee
Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Unijalie na kumwamini Yesu Kristo.
Najua kwamba pasipo haki yake nitapotea kabisa. Bwana nimesikia pia kwamba
Wewe u Mungu mwenye rehema. Wewe umeamuru Mwanao Yesu kristo awe
Mwokozi wa ulimwengu. Wewe Baba unapenda kumpeleka Yeye Kwangu,
mwenye dhambi kama mimi. Nami ni mwenye dhambi sana. Bwana, ongeza
neema yako kwa kuiokoa roho yangu kwa ajili ya Mwanao, Yesu Kristo, Amini.”

“Je, ulifanya kama ulivyoambiwa?” aliuliza Mkristo.


“Naam, nilifanya si mara moja, au mbili; bali nilifanya tena na tena,” alijibu
Mwenye-Tumaini.
“Naye alifunuliwa kwako?” aliuliza Mkristo.
“Mimi sikumwona kwa macho ya mwilini, bali kwa macho ya rohoni. Siku moja
nilielewa ubaya wa dhambi zangu kwamba sikustahili kwa lolote ila jehanamu.
Kwa ghafula nilidhani nilimwona Bwana Yesu Kristo akiniangalia kutoka
mbinguni, huku akisema “Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka” (Mdo 16:31).
Nikalia, na juu ya hayo; nikauliza, “Bwana, mtu mwenye dhambi nyingi kama
mimi naweza kukubaliwa na kuokolewa nawe?” Nami nikamsikia akisema,
“Yeyote ajaye kwangu sitamutupa nje kamwe” (Yn 6:37). “Kristo Yesu alikuja
ulimwenguni awaokoe wenye dhambi” (1 Tim 1:15). “Kristo Yesu ni mwisho wa
sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki” (Rum 10:4). “Alitolewa kwa ajili ya
makoza yetu, na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki” (Rum 4:25).”

“Kisha moyo wangu ukajaa furaha,” aliendelea Mwenye-Tumaini. “Macho yangu


yalijaa machozi, nao moyo wangu ulifurika upendo kwa ajili ya Bwana Yesu.
nikatamani sana kufanya jambo lolote kwa heshima na utukufu wa jina la Bwana
Yesu Kristo.

ASIYEJUA-KITU AFUATA

Kisha nikaona katika ndoto yangu kwamba huyo Mwenye-Tumaini aliangalia


nyumba na akamwona Asiyejua-Kitu akiwafuata. Ndipo nao walimngojea. “Vikoje
sasa kati ya roho yako na Mungu?” aliuliza Mkristo. Mwenye-Tumaini aliangalia
nyuma na kumwona Asiyejua-Kitu.
“Natumaini yote ni salama,” alijibu Asiyejua-Kitu. “Kwa sababu siku zote nimejaa
mawazo mema yanayonifariji ninapotembea.”

63
“Mawazo gani? Ebu tuambie,” aliuliza Mkristo.
“Mimi hufikiri habari za Mungu na mbinguni,” alijibu Asiyejua-Kitu.
“Ndivyo wawazavyo hata hao mashetani na hao waliopewa adhabu ya milele,”
alisema Mkristo.
“Lakini mimi nayafikiri na kuyaamini,” alijibu Asiyejua-Kitu.
“Ndivyo wanavyoyatamani wengine, wasipate kamwe kuyafikia,” (Mit 13:4).
“Lakini mimi nayafikiri na kuviacha vyote.
“Lakini kwa nini unafikiri umeviacha vyote kwa ajili ya Mungu na mbinguni?”
aliuliza Mkristo.
“Moyo wangu huniambia hivyo,” alijibu Asiyejua-Kitu.
“Mwenye-hekima akasema, “Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga”
(Mit 28:26), akajibu Mkristo.
“Hayo yaunena moyo mbaya, alisema Asiyejua-Kitu “moyo wangu ni mwema.”

“Isipokuwa neno la Mungu hutuambia juu ya mambo haya, ushuhuda mwingine


haufai kitu,” alisema Mkristo.
“Neno la Mungu husema hivi mintarafu mioyo yetu, “Hakuna mwenye haki hata
mmoja…hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja” (Rum 3:10, 12). Lasema pia
kwamba “Kila kusudi analowaza mwanadamu moyoni mwake ni baya tu siku
zote” (Mwa 6:5). Tena, “Mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana
wake” (Mwa 8:21).”
“Mimi sitaamini kamwe kwamba moyo wangu ni mbaya jinsi hiyo,” alisema
Asiyejua-Kitu. “Neno la Mungu hupasisha hukumu pia juu ya tabia zetu. Lasema
njia za binadamu ni njia zilizopotoka, zisizo njema bali ni mbaya (125:5). Mungu
anatujua sisi vizuri kuliko tunavyoweza kujijua wenyewe. Anaweza kuiona dhambi
ndani yetu ambapo sisi hatuioni dhambi yoyote. Hapo tunapofikiri haki yetu yote
ni kama nguo iliyotiwa unajisi, tunajua kuwa hatuwezi kusimama mbele za Mungu
huku tukijitumainia hata katika matendo yetu yaliyo bora,” alieleza Mkristo.

“Wewe wadhani mimi ni mpumbavu jinsi hiyo hata nifikiri kwamba Mungu
hawezi kuona mbali zaidi ya mimi?” alisema Asiyejua-Kitu. “Au wadhani kwamba
ningeweza kumwendea Mungu kwa njia ya matendo mema? Najua yanipasa
kumwamini Kristo.”
“Jinsi gani wafikiri kuwa yakupasa kumwamini Kristo hali huoni kwamba
unamhitaji?” aliuliza Mkristo.

64
UJINGA WA SIYEJUA-KITU

“Naamini kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya wenye dhambi. Naamini kwamba
nitahesabiwa haki na Mungu kwa sababu anaupokea utii wangu kwa hiyo sheria.
Kwa njia ya mema yake Kristo, huyafanya matendo yangu ya dini kukubaliwa na
Baba yake, na hivyo ninahesabiwa haki.” Alisema asiyejua-Kitu.

“Imani ya namna hiyo haionyeshwi katika neno la Mungu,” alisema Mkristo. “Ni
imani ya uongo. Inakuhesabia haki kwa sababu ya haki yako mwenyewe badala ya
hiyo haki ya Kristo. Imani hii ya kupotosha, nayo itakuleta kwenye ghadhabu ya
Mungu. Imani ya kweli inaifanya roho iliyopotea kuikimbilia haki ya Kristo.
Hivyo ndani ya haki ya Kristo mtu anapokelewa na Mungu, naye huwa huru mbali
na hukumu.”

“Nini! Wanitaka mimi kuyaamini hayo aliyoyafanya Kristo katika nafsi yake
pasipo mimi?” Aliuliza Asiyejua-Kitu. “Hayo yangetufanya tuishi kama
tupendavyo. Maana ingedhuru nini jinsi tunavyoishi kama tunaweza kuhesabiwa
haki kutokana na hayo kwa njia ya haki ya nafsi yake Kristo tutakapoiamini?”
“Jina lako ni Asiyejua-Kitu, na kweli ndivyo ulivyo,” alisema Mkristo. “Wewe
hujui kitu juu ya imani iokoayo katika haki hii ya Kristo inavyofanya kazi moyoni.
Inauvuta moyo kumwelekea Mungu katika Kristo, ili ulipende Jina lake, Neno
lake, Njia zake na watu wake. Si kama unavyofikiri wewe katika kutokujua
kwako.”

“Mwulize iwapo Kristo alipata kufunuliwa kwake kutoka mbinguni ingawa siku
moja,” alisema Mwenye-Tumaini.
‘Kristo amefichika katika Mungu hata hawezi kutambulikana na yeyote isipokuwa
Mungu Baba anamfunua kwake.”
“Hiyo ni imani yako, lakini siyo yangu,” alisema Asiyejua-Kitu. “Sioni shaka
maana naona kwamba imani yangu ni njema kama yako.”
“Maskini, Asiyejua-Kitu, mimi naona hujui jinsi imani inavyofanya kazi. Amka
upate kuiona hali yako nyonge, nawe umkimbilie Bwana Yesu Kristo. Kwa njia ya
haki yake utapata kuokolewa na hukumu ya milele.”

“Ninyi mna haraka sana,” alisema Asiyejua-Kitu. “Mimi siwezi kufuatana nanyi.
Haya tangulieni mbele, mimi sina budi kubaki nyuma kwa muda.”
Basi ndipo nikaona katika ndoto yangu hao wawili wakitangulia mbele, naye
Asiyejua-Kitu akawafuata nyuma poleple.

65
WASAFIRI WANAIFIKIA NCHI YA BEULA NA MTO WA MAUTI

Walipokwisha kuipita Nchi ya Kudanganya Moyo, ndipo waliingia nchi ya Beula.


Njia waliyokuwa wakiifuata iliongoza moja kwa moja katikati ya nchi hiyo.
Walifurahi mno huko. Upepo ulikuwa mzuri na wa kupendeza na palikuwa na
chakula tele.

Katika nchi hiyo jua lilitoa mwanga wake mchana na usiku. Hilo Jitu Kukata
Tamaa halikuweza kuwafikia hapa. Kutoka hapo waliweza kuuona mji waliokuwa
wakiuendea. Nao ulikuwa umejengwa kwa lulu na vito vya thamani, na njia zake
zilikuwa za dhahabu tupu.

Kisha nikaona kwamba hapo walipokuwa wakienda mbele walikutana na watu


wawili wenye mavazi yang’aayo kama dhahabu. Nyuso zao pia ziling’aa kama
mwanga wa jua. Ndipo watu hao wakauliza maswali na kisha wakasema “Bado
mnayo mambo mawili tu mtakayokutana nayo, na kisha mtaingia mjini.”

Mkristo na mwenzake wakawaomba watu hao wafuatane nao. Hao wakakubali.


“Lakini imewapasa kulipata jambo hili kwa njia ya imani yenu wenyewe,”
walisema wale watu.

Zaidi ya hayo niliona pia ya kuwa kati ya hapo waliposimama na lile lango
palikuwa na mto. Hapakuwa na daraja la kuuvukia, nao mto ulikuwa na kina sana.
Walipokuwa wakiutazama huo mto hao wasafiri hawakujua la kufanya. Lakini hao
wawili waliofuatana nao walisema, “Imewapasa kuuvuka mto huu, la sivyo
hamtaweza kulifikia lango.”

Ndipo huyo Mkristo alikata tamaa zaidi kuliko Mwenye-Tumaini. Wakaangalia


huku na huko, lakini hawakuona njia ya kuuepuka huo mto. Kisha wakawauliza
hao watu iwapo hayo maji yana kina sawasawa kila mahali. Wakasema kwamba
yalikuwa sawa au si sawa kutegemea na jinsi watakavyomwamini huyo Mfalme.

NDANI YA MTO WA MAUTI

Basi wakajitia majini na Mkristo alianza kuzama. Akalia na kuita hivi, “Nitazama
katika maji mengi; gharika zako zote na mawimbi yako yote yamepita juu yangu”
(Zab 42:7).
Kisha Mwenye-Tumaini akamwambia, “Uwe na moyo mkuu, ndugu yangu.
Nimepata pa kukanyaga napo ni pazuri.”

66
Ndipo Mkristo alisema, “Aha, rafiki yangu, huzuni za mauti zimenizunguka; mimi
sitaiona hiyo nchi imiminikayo maziwa na asali.”

Baada ya hayo kulikuwa na giza kuu kumzunguka Mkristo, hata hakuweza kuona
mbele. Tena wakati huu alionekana kupotewa na fahamu zake, na maneno yote
aliyoyasema yalionyesha kuwa alikuwa na hofu. Alifikiri kuwa atakufa humo
mtoni asiweze kamwe kulifikia lango. Aliudhika pia kwa ajili ya dhambi zake.

Kwa hiyo Mwenye-Tumaini aliona vigumu kukishika kichwa cha mwenzake


kisizame majini. Akajaribu kumtia moyo, akisema, “Ndugu, mimi naliona hilo
lango na watu wanatungoja ili kutukaribisha.”

Wasafiri wanauvuka mto kwa shida

Mkristo akajibu, “Ni wewe wakungojeaye. Umekuwa mwenye matumaini tangu


hapo nilipokujua.”
“Hata na wewe pia, Mkristo,” alijibu Mwenye-Tumaini. “Aa, ndugu, hakika yake
kama ningelikuwa mwema angelifika sasa kunisaidia. Lakini ni kwa sababu ya
dhambi zangu amenitia mategoni na meniacha pia,”alisema Mkristo.
“Taabu hizi zinaokupata humu majini hazimaanishi kuwa Mungu amekuacha,”
alijibu Mwenye-Tumaini.
“Zinaletwa ili kujaribu kuona kama utakumbuka wema wake ambao umeupokea
tangu hapo, na kwamba utamtegemea Yeye katika taabu zako.” Kisha akaongeza,
Uwe na moyo mkuu, Yesu Kristo akuponya.”

67
Baada ya hapo Mkristo akapasa sauti, “Aha! Namwona tena, naye aniambia hivi
“Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito
haitakugharikisha, (Isa 43:2).”

Ndipo wote wawili wakajitia nguvu na huyo adui naye akanyamaza kimya kama
jiwe, hata walipofika ng,ambo ya pili. Mara Mkristo alipofika ng,ambo alipata
mahali pa kusimama na sehemu iliyobaki ya mto haikuwa na maji mengi. Basi
hivyo wakavuka.

Basi ukingoni mwa mto wakawaona tena watu wale wenye mavazi ya kung’aa, nao
walikuwa wakiwangojea. Ndipo wakawasalimu, wakisema, “Sisi tu roho
watumikao, tukitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu (Ebr 1:14).

WASAFIRI WAUINGIA MJI WA MBINGUNI

Basi huo mji ulikuwapo juu ya kilima kirefu sana. Lakini hao wasafiri walikipanda
kilima kwa urahisi kwa vile hao watu wawili waliwaongoza kwa kuwashika
mikono. Wakaona kwamba walikuwa wameyaacha mavazi yao ya zamani mle
mle mtoni, ijapokuwa walikuwa wameyavaa walipoingia majini; walipotoka
walikuwa hawanayo.

Kwa hiyo walikikwea kilima kwa urahisi na kwa upesi. Wakafarijika kwa sababu
walikuwa wameuvuka salama huo mto, na sasa walikuwa na wenzao wenye fahari
kama hawa kuwasaidia.

Wakawauliza hao wenye kung’aa nintarafu utukufu wa mahali hapo. Hao wakajibu
kuwa uzuri na utukufu wa mji huo hausemeki kwa maneno.
“Huo ni Mlima Sayuni, Yerusalemu wa mbinguni; na majeshi ya malaika elfu
nyingi, na roho za watu wenye haki waliokamilika (Ebr 12:22-23),”
waliwaambia.

“Mtakapowasili huko mtapokea mavazi meupe, nanyi mtatembea na kuzungumza


na huyo Mfalme kila siku, hata siku zote za milele (Ufu 3:4-5; 22:5). Hamtayaona
tena mambo kama hayo mliyoyaona duniani, kama vile huzuni, magonjwa, taabu
na mauti. “Maana mambo ya kwanza hayatakumbukwa” (Isa 65:16-17).
“Je, tutafanya nini mahali hapo patakatifu?” wakauliza.
“Huko mtapata faraja badala ya taabu, na furaha badala ya huzuni yenu yote.
Mtayavuna mliyoyapanda, ndiyo matunda ya maombi yenu yote, machozi na
mateso mliyoyapata njiani kwa ajili ya huyo Mfalme (Gal 6:7-8). Mahali hapo

68
mtazivaa taji zenu na kumwona daima huyo Mmoja Mtakatifu. Huko mtamwona
kama alivyo (1 Yn 3:2).”

“Tena huko mtamtumikia sikuzote kwa kumsifu, kuimba na kumshukuru.


Mtamtumikia Mmoja ambaye mlijaribu kumtumikia mlipokuwa duniani ambapo
ilikuwa vigumu kwa sababu ya unyonge wa miili yenu. Huko mtafurahi pamoja na
rafiki zenu tena. Hapo atakapokuja katika mawingu pamoja na sauti ya parapanda,
mtafuatana naye ( 1 The. 4:16-17). Hapo atakapoketi katika kiti cha hukumu, nanyi
mtaketi karibu naye (Yud 1:14-15; 1 Kor 6:2-3).

Tena atakaporejea mjini, nanyi mtakuwa pamoja naye milele.” Kisha wakatokea
baadhi ya wapiga baragumu wa huyo Mfalme ili kuwalaki, nao wamevaa mavazi
meupe yang’aayo. Hao wapiga baragumu wakawaonyesha Mkristo na mwenzake
kwa muziki wao na kwa namna walivyotazama na kutenda, ili kuonyesha jinsi
walivyo karibishwa vizuri katika jamii yao.

Wapigao baragumu wanawalaki Wasafiri

Basi ilionekana kwa hao wawili kwamba walifika mbinguni kabla hawajingia
huko. Malaika waliwazunguka pande zote huku wakiimba kwa sauti tamu. Sasa
waliweza kuuona huo mji na kuzisikia kengele zikilia ili kuwakaribisha. Lakini
zaidi ya hayo yote walikuwa na mawazo yenye kuwafurahisha sana walipofikiri
jinsi watakavyoishi na jamii kama hii milele na milele. Hapana ulimi uwezao
kunena, wala hapana kalamu iwezayo kuandika mintarafu furaha timilifu
waliyokuwa nayo! Hivyo wakalifikia hilo lango.
Basi hapo juu ya lango paliandikwa maneno haya kwa harufi za dhahabu, “Heri
wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini
kwa milango yake” (Ufu 22:14).

69
Kisha nikaona katika ndoto yangu kwamba walipiga hodi langoni kama
walivyoambiwa na wale wenye kung’aa. Basi hapo kila mmoja wao alilitoa gombo
la chuo walilopokea mwanzoni mwa safari. Magombo hayo yakapelekwa kwa
Mfalme. Alipokwisha kuyasoma, ndipo aliwaamuru kulifungua hilo lango.

Ndipo niliona katika ndoto yangu kwamba hao watu wawili, Mkristo na Mwenye-
Tumaini waliliingia hilo lango. Nao walipokuwa wakiingia tu wakabadilika.
Walikuwa na mavazi yaliyong’aa kama dhahabu, nao walipewa vinubi pamoja na
taji, na kengele zote mjini zilipigwa kwa ajili ya furaha. Nikawasikia hao wawili
nao wakiimba kwa sauti kuu, “Baraka na heshima na utukufu na uweza una …
Yeye Mwana Kondoo, hata milele na milele” (Ufu 5:13).

Wasafiri wanavikwa Taji

Basi hapo hayo malango yalipofunguliwa ili wasafiri waingie nilichungulia ndani
nyuma yao, nami nikauona huo mji uking’aa kama jua. Njia zake zilikuwa za
dhahabu, nazo zimejaa watu wengi waliokuwa wakimsifu Mungu. Tena kulikuwa
na viumbe vilivyokuwa na mabawa, navyo vikisema, “Mtakatifu, Mtakatifu,
Mtakatifu ni Bwana.” Kisha baada ya hayo wakayafunga malango.

YALIYOMPATA ASIYEJUA-KITU

Basi hapo nilipokuwa nikifikiri mintarafu hayo yote, nilitazama nyuma nikamwona
Asiyejua-Kitu akifika ukingoni mwa huo mto. Lakini aliuvuka bila taabu yoyote
kama hao wengine walivyopita. Kwa kuwa ilitukia kwamba mahali hapo palikuwa
na mtu jina lake Tumaini-la-Bure, ndiye aliyemvusha kwa mashua yake. Asiyejua-
Kitu akakikwea hicho kilima kama walivyofanya wengine, japo yeye alikuwa

70
peke yake. Ndipo mtu alichungulia juu ya lango akauliza, “Wewe watoka wapi”
nawe wataka nini?”

Basi akajibu, “Mimi nimekula na kunywa mbele ya Mfalme, naye amewafundisha


watu katika njia za mji wetu.”

Ndipo walimtaka alitoe gombo lake ili wakamwonyeshe Mfalme. Naye akapapasa-
pasa mifukoni asione kitu. Hivyo wakamwabia Mfalme. Lakini Mfalme
hakukubali kuja kumwona. Akawaamuru hao wawili wenye kung’aa waende
wamkamate na kumfunga. Basi wakamnyanyua juu kwa juu mpaka penye mlango
chini ya kile kilima, wakamwingiza ndani.

Ndipo nilipoona ya kuwa palikuwa na njia iendayo hata kuzimu, kutoka pale penye
lango la mbinguni, pamoja na hiyo itokayo katika Mji wa Uharibifu.

Basi nikaamka na kumbe ni ndoto!

71

You might also like