You are on page 1of 160

KUTAMBUA MAMLAKA

YA

BIBLIA
Na
Roy C. Deaver

Hakimiliki na:
BIBLICAL NOTES PUBLISHING
Haki Zote Zimelindwa

HAKIUZWI
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi kuiga au kunakili
au kupiga chapa au kukitoa kitabu hiki au sehemu yake
kwa njia yoyote ile bila idhini ya maandishi kutoka
kwa Publishing Designs, Inc., isipokuwa kwa kunukuu
pekee.
DIBAJI

K
wenye dibaji ya toleo la mwaka 1997 la kazi
hii, tulirejea ukweli kwamba maandishi mengi
yaliandaliwa kwa ajili ya mihadhara na pia
yalitumika mwaka 1971 kwenye mihadhara ya Biblia
katika Shule Kuu ya Dini, Memphis, Tennessee. Ujumbe
mkuu wa mihadhara hiyo ulikuwa “Uvuvio na Mamlaka
ya Biblia”. Mihadhara yote iliyowasilishwa ilichapwa
katika mfumo wa kitabu, lakini katika uandishi huu,
kitabu hiki hakipatikani tena. Ulikuwa ni mhadhara
mzuri sana na kitabu ni kizuri sana.
Kichwa cha habari niliyochopewa kilikuwa: “Kuimarisha
Mamlaka ya Biblia”. Katika kuweka tayari vifaa
vya kufundishia vitakavyotumika katika darasa la
Hermeneutics la Shule ya Mafunzo ya Wahubiri ya
Brown Trail, ndipo nikabadilisha kichwa cha habari
cha kitabu na kuwa “Kuyatambua Mamlaka ya Biblia.”
Hata hivyo ni sahihi kusema kuwa mwanadamu hawezi
kuanzisha mamlaka ya Biblia. Ni jukumu letu kugundua
hayo mamlaka (kwa kuzingatia mtazamo na mwenendo
unaotakiwa), kuyaheshimu na kuongozwa nayo.
Darasa la Hermeneutics (kanuni za kutafasiri Biblia, au
Jinsi ya Kujifunza Biblia) ni sehemu muhimu sana katika
maisha na kazi za watu wote ambao wanatamani kujua
na kufundisha kile ambacho Mungu anataka tufanye. Ni
lazima tukusudie kuwa na mamlaka ya Biblia kwa kile
tunachofanya.

- iii -
Hili ni toleo jipya na liliokuzwa la Kuyatambua Mamlaka
ya Biblia. Kazi hii toka imechapishwa ni mwaka mmoja
sasa, na watu wengi sana wameendelea kukiagiza. Tuna
furaha sana kwa hili. Ni kwa sababu ya maombi maalumu
kutoka kwa William S. Cline, Mhariri wa Wakifu wa
Firm, ndipo tumeweza kuandaa vifaa vitakavyotumika
katika masomo ya Biblia. Kitabu hiki kina jumla ya
sura kumi na tatu na orodha ya maswali ya kujifunza
yanafuata kwa kila sura. Tunapenda kuwatia moyo
walimu na wanafunzi kujifunza haya yaliyoandikwa kwa
makini sana, kwa kufikiri, kwa maombi, daima ukiweka
akilini mwako umakini na umuhimu wa suala lenyewe.
Ni lazima tuelewe jinsi Mungu anavyotoa Mamlaka.
Baraka za Mungu ziwe pamoja nasi kadri tunavyojitahidi
sana kuwa wanafunzi wazuri wa neno Lake.

Ni wako katika Ufalme,

Roy Deaver

- iv -
TABARUKU
Kwa Dr. Thomas B. Warren
(Ni mtu ambaye hana haja ya kukisoma) – Rafiki
Mpendwa na Askari wa Yesu, tukiwa pamoja kwa miaka
mingi, mingi sana ya ajabu.

-v-
- vi -
YALIYOMO
SOMO LA KWANZA
I. UTANGULIZI 1
SOMO LA PILI
II. FUNDISHO LA BIBLIA JUU YA UVUVIO
(Sehemu ya Kwanza) 9
SOMO LA TATU
III. FUNDISHO LA BIBLIA JUU YA UVUVIO
(Sehemu ya Pili) 17
SOMO LA NNE
IV. NI LAZIMA TUTAMBUE KWAMBA AGANO
JIPYA HUWEKA KIELELEZO KITAKATIFU 25
SOMO LA TANO
V. MAANA YA IMANI YA BIBLIA 35
SOMO LA SITA
VI. JE INAWEZEKANA SISI KUFAHAMU? 45
SOMO LA SABA
VII. KAULI YA MSINGI 57
VIII. TOFAUTI MUHIMU (Sehemu ya Kwanza) 59
SOMO LA NANE
IX. TOFAUTI MUHIMU (Sehemu ya Pili) 69
SOMO LA TISA
X. TENDO NA MAJUKUMU 77

- vii -
XI. MUNGU HATAVUMILIA KILE AMBACHO 78
HAKIKUAMRIWA
XII. NI LAZIMA TUBAKI KATIKA KILELE CHA
MLIMA WA MAMLAKA YA BIBLIA 79
XIII. TUNAPASWA KUJUA JINSI AMBAVYO
MUNGU HARUHUSU 80
XIV. LAKINI VIPI KUHUSU UKIMYA WA
MAANDIKO? 81
SOMO LA KUMI
XV. MAMALAKA YANATHIBITISHWA KWA
MFANO 87
SOMO LA KUMI NA MOJA
XVI. MAMLAKA YANATHIBITISHWA KWA
KUDOKEZA 97
XVII. MAMLAKA YANATHIBITISHWA KWA
KAULI YA MOJA KWA MOJA 100
SOMO LA KUMI NA MBILI
XVIII. MAMLAKA YA BIBILIA
YANATHIBITISHWA KWA MANUFAA
BINAFSI 105
SOMO LA KUMI NA TATU
XIX. JE MAMLAKA YANANUKULIWA NA
KAMUSI? 115
KIAMBATISHO A 130
KIAMBATISHO B 141
KIAMBATISHO C 144

- viii -
SOMO LA KWANZA

1. UTANGULIZI

1
-1-
K
atika somo letu la KUTAMBUA MAMLAKA
YA BIBLIA tunashughulika katika misingi
ya kauli tatu muhimu: (1) Mungu YUPO, (2)
Biblia ni Neno la Mungu, na (3) Mungu alitupatia Biblia
kutuongoza katika maisha haya na kutupeleka mbinguni
baada ya maisha haya yatakapokwisha. Kauli zote hizi
tatu zinaweza kuthibitishwa, lakini hii haipo katika
mawanda ya somo hili kuonesha huo uthibitisho. Kwa
sasa tutashughulikia zaidi kauli namba 3. Biblia mara
kwa mara huzungumzia juu ya asili yake ya miujiza –
UVUVIO WAKE – na namna nzuri ya kuitumia ili iwe
Maandiko yaliyovuviwa. Kwa wazee wa Efeso Paulo
alisema: “Sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno
la neema yake, linaloweza kuwajenga na kuwapa ninyi
urithi miongoni mwa wote ambao wametakaswa.”
(Matendo 20:32).
Kama hivi ndivyo na tunasadiki kwa uthabiti kabisa
kwamba ndivyo, basi ni dhahiri tutakuwa tunaguswa
kuhusu vile Biblia inavyotoa mamlaka.
1. Wakolosai 3:17 inaunganisha, “Lo lote mfanyalo,
ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika Jina
la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba katika Yeye”.
“Katika jina la Bwana” humaanisha kwa mamlaka ya
Bwana, kama Bwana alivyoamuru. (Matendo 4:7-10)
Wakristo wanalazimika (na wana fursa) ya “kutembea
kwa imani” (2 Kor. 5:7). Kipimo ambacho mkristo
anaongozwa nacho ni kipimo cha imani. Katika Warumi
10:17 Paulo anasema kwamba “Basi, imani chanzo
chake nikusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo.” Ni

-2-
dhahiri kwamba, mkristo huenenda kwa kusikia neno la
Mungu. Kama imani huja kwa kusikia neno la Mungu
basi pale pasipokuwa na neno la Mungu hapawezi kuwa
na imani. Na pale pasipo na imani hakuna kumpendeza
Mungu. (Waebrania 11:6). Ni lazima tuguswe na kuhusu
mamlaka ya Biblia na jinsi ya KUYATAMBUA mamlaka
ya Biblia.
Ni kazi yangu kujifunza na wewe wakati huu juu ya
suala la Kuyatambua mamlaka ya Biblia. Ni jukumu
langu kuelezea, kufafanua, kuthibitisha, namna Mungu
anavyoamuru. Ni lazima nioneshe kwa uwazi, kwa
kukazia, kwa maelezo rahisi, kwa usahihi, na kimaandiko
namna ambavyo mamlaka ya Biblia yanavyothibitishwa.
2. Naomba nipendekeze kwamba suala hili ni la muhimu
sana. Tusipojua namna Mungu (au Biblia) inavyoamuru,
hatuwezi kuwa na uhakika kuhusu kitu chochote
tunachofanya au kusema katika muktadha wa dini. Kijana
mmoja alikuwa anahubiri kwa ajili ya kanisa la Bwana
huko magharibi mwa Forth Worth. Alikuwa ameonesha
shauku ya kufundisha pamoja nasi katika Chuo cha

ajili ya usaili. Nilimdokezea kwamba kuna uvumi


umeenea kuwa hana uhakika kuwa matumizi ya ala za
muziki kwenye ibada ya kikristo ni dhambi. Tulijadili

Ni wazi kwamba alikuwa anaelekea kutetea matumizi


ya ala za muziki katika ibada. Hatimaye nikamwambia:
“Ukiacha mambo mengine, uko radhi kukubali kwamba
hakuna mamlaka yanayoamuru matumizi ya vyombo vya

-3-
muziki kwenye Idada ya Kikristo?” Akajibu: “Ndugu
Deaver, sina uhakika juu ya namna Mungu anavyotoa
mamlaka”. Jibu langu lilikuwa: “Kama ndio hivyo hakika
hatuwezi tukakutumia. Maana kama hujui jinsi Mungu
anavyotoa mamlaka, basi huwezi kuwa na uhakika juu ya
kitu chochote.” Haikuchukua muda huyu kijana akawa
kwenye mstari wa dhehebu "Kanisa la Kikristo".
3. Habili alitoa sadaka ya mnyama, na hii ilimpendeza

alivyoelekezwa. Ibrahimu alijenga madhabahu na mahali


hapo akamwabudu Yehova. Musa alijenga hema kama
alivyooneshwa mlimani. Wana wa Israeli wa Agano la Kale
walimkaribia Mungu kupitia makuhani wa kabila la Lawi.

kwenda Yerusalemu kumwabudu Mungu mara tatu kwa


mwaka. Daudi aliamuru matumizi ya muziki wa ala katika
kumwabudu Mungu. Katika nyakati za Agano la Kale
kulikuwa na desturi za ndoa za mitara na uchomaji wa ubani.
Kama alivyofanya Abeli, ni lazima nami nitoe kafara ya
mnyama ili nimpendeze Mungu? Kama Nuhu, ni lazima
nijenge safina? Kama Ibrahimu, na mimi nimwabudu
Mungu katika madhabahu ya kidunia kwa kutoa kafara
za wanyama? Kama Musa, ni lazima nijenge hema? Ni
lazima nimwendee Mungu kupitia Kuhani wa kabila la
Lawi? Ili ibada yangu ikubaliwe na Mungu, ni lazima
niende Yerusalemu mara tatu kwa mwaka? Kama
alivyofanya Daudi, je na mimi naweza kutumia vifaa vya
muziki katika kumwabudu Mungu? Je, na mimi niwe na
ndoa za mitala?

-4-
Kama alivyofanya Abeli, je ni lazima nitoe sadaka ya
kuteketeza ili nimpendeze Mungu? Kama Nuhu, je

nitengeneze madhabahu ya kidua na nimtolee Mungu


sadaka za kutekeza katika hiyo? Kama Musa na mimi leo

kupitia kuhani wa kabila la Lawi? Ili nimuabudu Mungu


kwa namna inayokubalika, je napaswa kwenda Yerusalem
mara tatu kwa mwaka? Je naweza kama Daudi, kutumia
ala za muziki katika kumuabudu Mungu? Je naweza
kushiriki katika tabia ya kuoa wake wengi? Je nitakuwa
nipo sahihi nikimchomea Yehova ubani?
Kama naweza kufanya vitu hivi na kama ni lazima
nivifanye – nawezaje kujua kwamba naweza na ninawezaje
kujua kwamba ni lazima? Kama siwezi kufanya vitu hivi
na kama sio lazima nifanye vitu hivi – nitajuaje kwamba
si lazima Je, Daudi au Musa au Ibrahimu au Yakobo
waliwahi kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi? Je,
Daudi au Ibrahimu, au Musa waliwahi kushiriki Meza
ya Bwana katika siku ya kwanza ya juma?
4. Alhamisi moja usiku, Bwana alikutana na wanafunzi
wake, akashiriki Sikukuu ya Pasaka, akaanzisha
Meza ya Bwana, na akawanawisha wanafunzi miguu.
Kuhusiana na kuwanawisha wanafunzi wake miguu,
Bwana alisema, “Kwa hiyo, ikiwa Mimi niliye Bwana
wenu na Mwalimu wenu nimewanawisha ninyi miguu,
pia hamna budi kunawishana miguu ninyi kwa ninyi.
Mimi nimewawekea kielelezo kwamba imewapasa
kutenda kama vile nilivyowatendea ninyi.” (Yohana

-5-
13:14,15). Kama Wakristo, tunashiriki Meza ya Bwana.
Hatuadhimishi sikukuu ya Pasaka, na katika ibada yetu
hatunawishani miguu. Kati ya mambo haya matatu,
tunaamuaje kwamba tunawajibika kutunza moja tu?
5. Zaidi ya hapo, wakati Meza ya bwana inaanzishwa
Bwana na wanafunzi wake walikuwa “orofani.” Wakati
Paulo anakutana na ndugu wa Troas ili “kumega mkate”
walikuwa “wamekusanyika pamoja” katika “chumba cha
orofani” na kulikuwa kuna “mianga mingi.”
Ili na sisi tuweze kufuata maandiko katika kushiriki Meza ya
Bwana, ni lazima tuifanyie kwenye “chumba cha orofani”?
Ni lazima kuwepo na “mianga mingi”? Tunaamuaje?
6. Katika Warumi 16:16, Paulo anasema: “Salimianeni
kwa busu takatifu.” Ili na sisi tuweze kumpendeza
Mungu ni lazima tusalimiane kwa busu takatifu? Kama
ni hapana, kwa nini? Na kama ndiyo kwa nini hatufanyi
hivyo? Vyovyote vile, je tunaamuaje?
Ni lazima idhihirike kuwa, ni muhimu sana kwetu,
kutafakari kwa makini sana na kwa maombi katika suala
la namna ya kuyatambua mamlaka ya Biblia.

-6-
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Jadili Yeremia 6:16-19

2. Je wanadamu “wanathibitisha” mamlaka ya Biblia?


Angalia Dibaji. Jukumu letu ni nini? Angalia Dibaji.

3. Nini maana ya “Hermeneutics”? Angalia Dibaji

4. Tunafanyia kazi misingi ya kauli tatu muhimu. Ni


zipi hizi?

5. Kariri Matendo 20:32

6. Kulingana na Wakolosai 3:17 tunapaswa kufanya vitu


vyote kwa namna gani?

7. Ni somo gani kuu tunalojifunza katika 2Wakorintho 5:7?

Ni somo gani kuu tunalojifunza katika Warumi 10: 17?

-7-
Ni somo gani kuu tunalojifunza katika Waebrania
11:6?

8. Jaza: Kama hatujui namna Mungu anavyotoa


mamlaka, basi ……………………

9. Ni lazima nitoe sadaka ya kuteketeza ya wanyama?


Ni lazima tujenge safina? Ni lazima tujenge hema? Ni
lazima kumwendea Mungu kupitia kuhani wa kabila
la Lawi? Ni lazima twende Yerusalemu kuabudu?

10. Je, Daudi au Musa au Abrahamu au Yakobo waliwahi


kubatizwa kwa ajili ya ondoleo la dhambi?

11. Ni lazima Wakristo waadhimishe sikukuu ya Pasaka?

12. Ni lazima Wakristo washiriki Meza ya Bwana katika


“chumba cha orofani”?

13. Ili kumpendeza Mungu ni lazima tusalimiane kwa


“busu takatifu”?

14. Ni muhimu sana kwetu kutafakari kwa makini na kwa


maombi juu ya suala gani?

-8-
SOMO LA PILI

2. FUNDISHO LA BIBLIA
KUHUSU UVUVIO
(Sehemu ya Kwanza)

2
-9-
UTANGULIZI

K
atika 2 Timotheo 3:16, 17 Paulo anathibitisha
uvuvio wa maandiko (Kila andiko, lililovuviwa
na Mungu…..) hii inarejelea juu ya matumizi
ya maandiko yaliyovuviwa (“….lafaa kwa mafundisho,
kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na
kuwafundisha katika haki…..”) na inaonesha matokeo ya
uvuvio huu na matumizi yake (“…ili mtu wa Mungu awe
kamili, amekamilishwa apate kutenda kila kazi njema.”).
Kuna mafungu mengi sana yanayoonesha dai la Biblia
kuwa imevuviwa na Mungu. Lakini Biblia ina maana
gani kuweka dai hili? Maana ya “uvuvio” ni nini kama
neno linavyotumika kwenye Biblia?
Ni muhimu sana kuwa makini katika kujibu swali hili.
“Uvuvio” ni istilahi ambayo kwa sasa inatumika katika
dhana tofauti tofauti. Mwanausasa wa cheo cha juu
anadai kuamini katika Mungu. Lakini haamini katika
Mungu wa kwenye Biblia, Anadai kuamini Kristo, lakini
haamini katika Kristo wa kwenye Biblia. Vivyo hivyo
anadai kuamini katika uvuvio wa kwenye Biblia lakini
hamaanishi kwa “uvuvio” ambao Biblia inafundisha.
Anaamini kwamba maandiko ya Paulo yalikuwa
yamevuviwa kwa maana ile ile kama yalivyo maandiko
ya Shakespeare, Milton, Tennyson, na Poe. Wala hasiti
kuchambua uzuri wa kitabu cha Warumi kwa misingi ya
kwamba “Paulo siku hiyo alikuwa anajisikia vizuri!”
Nadharia nyingi za uongo zinasumbua ulimwengu wetu.
Hebu tuangalie chache tu.

- 10 -
(1) Kuna baadhi ya watu ambao wanadai kwamba hakuna
kitu chochote cha maana kuhusiana na Biblia. Kwao
Biblia ni kitabu tu kama vitabu vingine – kitabu kizuri
pengine lakini ni kitabu kilichoandikwa ya mwanadamu.
(2) Usasa unadai kwamba Biblia ni mkusanyiko wa
kumbukumbu zilizopita za wanadamu waliowahi kuishi
zamani, zilikusanywa pamoja na kuhaririwa na Goerge –
George Redactor, ni hivyo tu! (3) Baadhi wanasema kuwa
Biblia imevuviwa kimiujiza katika baadhi ya sehemu au
kwa kiwango fulani au kwa kiasi fulani tu. Sasa tunauliza:
katika maeneo gani? kwa kipimo gani? kwa kiasi gani?
nani anayeamua? Hii inapinga waziwazi uvuvio wa
Biblia. (4) Baadhi wanashikilia wazo la kwamba Mungu
(kwa namna fulani) aliwapa watu mahususi mawazo
yasiyokuwa na mipaka na akawaruhusu hawa watu
kuweka “mawazo hayo kwa maneno yao wenyewe.” Sasa
tunauliza Biblia inasemaje kuhusiana na uvuvio wake?

AHADI NA UTIMILIFU
Bwana aliahidi kutoa uvuvio wa kimiujiza. Bwana
alisema: “…..nanyi mtaburutwa mbele ya watawala na
wafalme kwa ajili Yangu, ili kuwa ushuhuda kwao na
mbele ya watu wa Mataifa. Lakini watakapowapeleka,

mtapewa la kusema wakati huo. Kwa sababu si ninyi


mtakaokuwa mkinena, bali ni Roho wa Baba yenu
atakayekuwa akinena kupitia kwenu” (Math. 10:18-
20). Akaendelea kusema: “Atakapokuja huyo Roho
wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye
hatanena kwa ajili Yake mwenyewe, bali atanena yale

- 11 -
yote atakayoyasikia, naye atawaonesha mambo yajayo.
Atanitukuza Mimi, kwa maana atayachukua yaliyo
Yangu na kuwajulisha ninyi.” (Yohana 16:13,14)
Bwana alitimiza ahadi yake. Siku ya Pentekoste ya
Matendo 2, watu awa hawa ambao walipewa ahadi “…
Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kunena
kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia” (mstari
wa 4). Katika mstari wa 39 Petro alisema: “Kwa kuwa
ahadi hii ni kwa ajili yenu na watoto wenu na kwa wale
wote walio mbali na kila mtu ambaye Bwana Mungu wetu
atamwita amjie.’’ Andiko hili ni mfano mzuri wa uvuvio
wa kimiujiza ambao Petro aliuzungumza. Umuhimu wake
kwa hakika unahusisha wokovu wa Wamataifa. Lakini
bado Petro yeye mwenyewe kwa wakati huo, hakuamini
kuwa injili ilikuwa ni kwa ajili ya Wamataifa pia. Katika
Matendo ya Mitume sura ya 10, Mungu alilazimika
kufanya miujiza mara tatu ili kumwezesha Petro aelewe
kuwa alipaswa kuhubiri injili kwa Wamataifa. Hivyo
Mungu alimsaidia kuelewa maana ya kile alicho kihubiri
takribani miaka kumi kabla! Ni Petro ambaye baadae
alitangaza uwezo mtakatifu wa Mungu “…umetupatia
mambo yote tunayohitaji kwa ajili ya uzima na uchaji wa
Mungu….” Paulo anafafanua suala hili: “Ndugu zangu,
nataka mjue kwamba Injili niliyowahubiria haikutokana
na wanadamu. Kwa maana mimi sikuipokea hiyo Injili
kutoka kwa mwanadamu, wala sikufundishwa na mtu,
bali niliipata kwa ufunuo kutoka kwa Yesu Kristo.”
(Wagalatia 1:11-12). Kwa uwazi kabisa, waandishi wa
Agano Jipya wanathibitisha kwamba Bwana alitimiza
ahadi yake.

- 12 -
MUNGU NA MAMLAKA
Mamlaka yote ya asili yako ndani ya Mungu Baba.
“Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi”
(Mwanzo 1:1). “Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, na
mikono yake iliumba nchi kavu” (Zab. 95:5). Na ni “…
Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari
na vitu vyote vilivyomo” (Matendo 14:15). Ni “Mungu
aliyeumba dunia na vyote vilivyomo ndani yake, Yeye
ndiye Bwana wa mbingu na nchi, hakai katika mahekalu
yaliyojengwa kwa mikono ya wanadamu.” (Matendo
17:24). Ni Muumba wetu na mhuishaji wetu. Ni kupitia
yeye ndipo tunaweza kutembea na kuwa watu. Kwa
sababu yeye yupo hivyo alivyo, mamlaka yote ya asili-
na chanzo chake yanatoka kwake.

MWANA NA MAMLAKA
Vitabu vya Mathayo, Marko, Luka, na Yohana
viliandikwa ili kuwashawishi watu waamini kuwa
Yesu wa Nazareti ndiye Kristo, mwana wa Mungu
anayeishi – Masihi ambaye ujumbe wa Agano la Kale
ulimzungumzia. Mungu alisema kwamba Yesu alikuwa
ni Mwana wake. Yesu alidai kwamba Mungu alikuwa ni
Baba yake. Waandishi hawa walitoa ushahidi usiopingika
kuthibitisha madai yake. “Basi yule jemadari na wale
waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu walipoona
lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia,
wakaogopa wakasema, “Hakika huyu alikuwa ni Mwana
wa Mungu!”(Math.27:54)

- 13 -
Lakini kuna nini cha muhimu sana kuhusiana na ukweli
huu? Kwanini kuthibisha kuwa ni Mwana wa Mungu?
Jibu ni: Alikuwa (na yupo) katika nafasi ya kuwa
mrithi wa mamlaka yote kutoka kwa Baba. Alikutana na
wanafunzi wake katika mlima Galilaya na kwa kujiamini
akatamka “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na
duniani” (Mathayo 28:18). Mungu alitoa mamlaka kwa
Mwana – mamlaka ya kushughulikia dhambi za
wanadamu.

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 14 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Ni hoja gani tatu za msingi zinazopatikana katika


2Timotheo 2:16, 17?

2. Nini anachofikiria mwanausasa pale anapozungumza


juu ya “uvuvio”?

3. Ni zipi dhana potofu, angalau nne, kuhusu “uvuvio”?

4. Mathayo 10:18-20 na Yohana 16:13,14 zinaonesha


wazo gani la msingi kuhusu uvuvio?

5. Kulingana na Matendo 2:4, Bwana alifanya nini?

6. Fafanua jinsi Matendo 2:4 inavyoonyesha kwa namna


ya pekee uvuvio wa kimiujiza aliousema Petro.

7. Kwa kuhusianisha na Matendo 2:39 Mungu alifanya


nini katika Matendo 10?

- 15 -
8. Katika 2Petro 1:3, Petro alitangaza nini?

9. Kwa mtazamo wa Wagalatia 1:11,12, ni kwa jinsi


gani ujumbe mtakatifu ulimjia Paulo?

10. Ni hoja gani inayojengwa waziwazi kwa kuzingatia


Mwanzo 1:1; Zaburi 95:5; Matendo 14:15 na Matendo
17:24?

11. Mathayo, Marko, Luka, na Yohana viliandikwa kwa


makusudi gani mahususi?

12. Liwali alisema nini kuhusu Bwana (Mathayo 27:54)?

13. Kuna umuhimu gani juu ya ukweli kwamba Yesu ni


Mwana wa Mungu?

14. Madai gani makubwa aliyodai Bwana kama


ilivyooneshwa katika Mathayo 28:18?

- 16 -
SOMO LA TATU

3. FUNDISHO LA BIBLIA
KUHUSU UVUVIO
(Sehemu ya Pili)

3
- 17 -
MITUME NA MAMLAKA

B
wana alijua kwamba maisha yake ulimwenguni
yangekuwa ni mafupi, lakini ujumbe wake
kwa mataifa ungeendelea. Aliita, akachagua,
akafundisha, akalea, akatoa mafunzo, na kuendeleza
kikundi kidogo cha watu ambao katika mabega yao,
aliweka jukumu la kupeleka habari ya injili ulimwenguni
mwote. Aliahidi kuwa pamoja nao katika kazi yao, na
alikuwa pamoja nao. Kitabu cha Matendo ya Mitume ni
habari takatifu ya jinsi Bwana alivyotembea nao katika
kupeleka injili kwa kila kiumbe ulimwenguni mwote
(Mk. 16:19, 20). Walihubiri injili kwa uvuvio wa miujiza,
neno lao lilithibitishwa kwa matendo ya miujiza.
Hawa watu walidumisha uhusiano wa pekee na Kristo,
Mfalme. Kimsingi, walikuwa ni “mabalozi” wa Mfalme.
Paulo anasema, “Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Kristo…”
(2 Kor. 5:20). Neno ‘mabalozi’ kama lilivyotumika
hapa huhusisha “ubalozi ” mtakatifu na huu “ubalozi”
mtakatifu ni lazima utakuwa umehusisha mamlaka
maalumu. Mitume walikuwa ni wawakilishi rasmi wenye
mamlaka ya Mfalme. Mfalme alitawala akiwa mbinguni,
lakini alikuwa na ubalozi miongoni mwa watu–mitume
ambao aliwapa mamlaka kufunga na kufungua duniani
yale yaliyo fungwa na kufunguliwa mbinguni.

KARAMA YA UNABII
Katika kanisa la awali, kulikuwa na karama za kimiujiza–
karama za kiroho. Watu wa kipindi hicho hawakuwa na
Agano Jipya lililokamilika katika mfumo wa maandishi,
lakini kulikuwa na uhitaji mkubwa wa uongozi na

- 18 -
maelekezo matakatifu. Ili kukidhi haya mahitaji, Mungu
aliweka karama za pekee katika kanisa la awali. Mjadala
wa pekee kuhusiana na karama hizi za kiroho unapatikana
katika 1 Wakorintho, sura za 12, 13 na 14. Katika sura
ya 12, Paulo anajadili karama tisa za miujiza. Kwa
kuzingatia Matendo 8:14-21 tunasema kwa kujiamini
kwamba ni Mitume pekee ndio wangeweza kutoa miujiza
ya Roho Mtakatifu kwa kuweka mikono yao juu ya mtu
mwingine. Ushahidi wa wazi ni kwamba ni mitume tu
waliokuwa na hizi karama tisa za miujiza na kwamba ni
mitume tu –kulingana hitaji walioweza kutoa vipawa hivi
vya kiroho.
Moja ya karama muhimu sana za roho ilikuwa ni karama ya
Roho Mtakatifu. Katika 1 Wakorintho 14 Paulo anasisitiza
ukuu wa karama ya unabii. Ni muhimu kuielewa karama
hii. “Kutoa unabii” hakuna maana ya “kutabiri mambo
yajayo.” Maana yake hujumuisha kipengele hiki cha
mambo yajayo, lakini maana yake ni zaidi ya hapa. Neno
unabii maana yake ya moja kwa moja ni “kusema kwa ajili
ya, au niaba ya.” Manabii (wa Agano la Kale au wa Agano
Jipya) walisema kwa niaba ya Mungu. Mungu alizungumza
kupitia wao. Katika Kutoka 7:1 Mungu alimwambia Musa:
“…huyo ndugu yako, Haruni, atakuwa nabii wako. Musa
angeweza kuzungumza kupitia Haruni. Hii ndio maana ya
neno hili. Manabii wakati mwingine walishughulika na
mambo ya zamani; na wakati mwingine walishughulika
na mambo ya wakati uliopo (kwa wakati huo); na wakati
mwingine walishughulika na mambo ya wakati ujao.
Lakini walikuwa ni Manabii kwa sababu Mungu alisema
kupitia wao.

- 19 -
Kwa hiyo, karama ya unabii, ni mamlaka yaliyomo katika
kila neno kwenye Biblia. Kila neno (kila neno halisi) ni
neno liliotokana na miujiza ya karama ya unabii. Iwapo
Luka ni miongoni mwa waandishi wa Agano Jipya, na
ikiwa Luka hakuwa mmoja wa mitume, hivyo Luka
alikuwa ni nabii katika kanisa la awali – ambaye kupitia
yeye Mungu alifunua mapenzi yake.
Ni lazima isisitizwe kwamba hakuna unabii bila (1) ufunuo
wa moja kwa moja, pamoja na (2) uvuvio wa kimiujiza.
Mungu alifunua, kisha mtu ambaye alipata huo ufunuo
alizungumza au aliandika ujumbe uliofunuliwa kwake.
Uzungumzaji au uandikaji ulifanywa chini ya uvuvio.
Kulikuwa na walimu waliovuviwa wakati wa kanisa
la awali lakini hawakuwa sawa na manabii. Walimu
walishughulika na ujumbe uliofunuliwa kwa manabii.
Andiko muhimu linalothibitisha hilo ni 1Wakorintho
14:30 – “Lakini mwingine aliyeketi akifunuliwa neno,
yule wa kwanza na anyamaze.”

MAANDIKO YA KUFAA
Moja kati ya maandiko ambayo yako wazi na rahisi juu
ya uvuvio wa Biblia ni 1 Wakorintho 2, mstari wa 9 -13.
Katika mstari wa sita Paulo anarejelea “mambo” fulani
ambayo Mungu amewaandalia wale wanaompenda.
Katika mstari wa 10 anasema: “Lakini Mungu
ametufunulia sisi kwa Roho…” Katika mstari wa 12
Paulo anasema: “Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia,
bali roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua
tuliyokirimiwa na Mungu.” Zingatia: Mungu kupitia
Roho alifunua “mambo.” Ufunuo ulikuja kwa watu

- 20 -
waliomo kwenye neno “sisi.” Mimi na wewe hatumo
kwenye neno “sisi”. Hatupati ufunuo wa moja kwa
moja. Swali sasa: Ni kwa jinsi gani ujumbe uliovuviwa
hutoka kwa wale waliohusishwa kwenye neno “sisi”
na kuja kwa wengine tuliosalia? Jibu: Paulo anasema –
“Nayo twayanena si kwa maneno yanayofundishwa kwa
hekima ya kibinadamu, bali yanayo fundishwa na Roho,
tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa manemo ya rohoni”
mstari wa 13). Hii inafanya suala hili liwe wazi vya
kutosha! Mungu alifunua mambo kwa watu fulani (watu
wenye karama ya unabii), ambao baadae waliyanena
na waliyaandika kwa maneno yaliyochaguliwa na roho
Mtakatifu. Hii ni fasili ya Biblia juu ya uvuvio: Huu
ni ukusanyaji mzuri sana wa mambo yaliyofunuliwa,
yaliyofundishwa kwa maneno yaliyochaguliwa na Roho
Mtakatifu.
Uthibitisho na ufafanuzi mzuri unaofanana na huo
hupatikana katika Waefeso 3:1-5. Mungu kupitia Roho
Mtakatifu alimfunulia Paulo siri, kwa kutumia maneno,
ili kumsaidia Paulo kuelewa siri hizo. Paulo aliandika
(kwa maneno) siri ambazo Mungu alimfunulia kwa ajili
ya Waefeso (na wengine), ili kuwasaidia kusoma na
kuelewa uelewa wa Paulo wa siri za Mungu – injili ya
Kristo.

HITIMISHO
Mpendwa wangu, hili ndilo fundisho la Biblia kuhusu
uvuvio. Inatakiwa tukumbuke kwamba uvuvio wa
kimiujiza huhusiana na maneno halisi ya kitabu cha
Mungu – maneno ya Kiebrania katika Agano la Kale

- 21 -
na maneno ya Kiyunani katika Agano Jipya. Wafasiri
au wakalimani hawavuviwi, lakini maneno hayo
halisi yametoka kwa Mungu. Ni maneno yale yale
yaliyochaguliwa na Roho Mtakatifu. Yana maanisha kile
alichotoa Mungu yamaanishe; Na yananena kile
Mungu alichotaka yanene.
Mungu alitoa mamlaka kwa Mwana. Mwana
akatoa mamlaka kwa mitume. Mitume (na wengine
waliowekewa mikono na mitume) walikuwa na karama
ya unabii. Karama ya unabii ilikuwa ni njia ambayo
kwayo Mungu alifunua ujumbe wake. Wale walioupata
ufunuo waliusema na waliuandika “…si kwa maneno
yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu bali
yanaoyofundishwa na Roho.” Walijumuisha “mambo ya
kiroho” – mambo yaliyofunuliwa kwa maneno ya kiroho
– maneno yaliyochaguliwa na Roho Mtakatifu.
Shukrani kwa Mungu kwa ajili ya neno lake lililovuviwa,
lisilopotoka, lisilo na makosa na linalojitosheleza!

- 22 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Ili kupeleka injili ulimwenguni kote, Bwana alifanya


nini?

2. Umuhimu wa Marko 16:19,20 ni nini?

3. Mitume walikuwa “mabalozi” wa Mfalme. Umuhimu


wa ukweli huu ni nini?

4. 1Wakorintho sura ya 12, 13, na 14 ni mjadala mzuri


wa nini?

5. Kipimo cha miujiza ya Roho Mtakatifu (karama ya


roho) kingeweza kupewa kwa mtu mwingine kwa
njia gani?

6. Mitume wanahusianaje na “karama za roho”?

7. Katika 1Wakorintho 14, Paulo anajadili nini?

- 23 -
8. Maana ya “unabii” ni nini?

9. Ni kwa jinsi gani karama ya “unabii” inahusiana na


mamlaka ya Biblia?

10. Ieleweke kwamba hakuna unabii bila nini?

11. Je“Manabii” katika kanisa la awali walikuwa sawa


na “walimu waliovuviwa”?

12. Tafadhali andika muhtasari wa 1Wakorintho 2: 9-13.

13. Tafadhali andika muhtasari wa Waefeso 3: 1-5

14. Uvuvio wa kimiujiza kwa umahususi huhusiana na


neno gani?

15. Tafadhali andika muhtasari wa fundisho la Biblia


kuhusu Uvuvio.

- 24 -
SOMO LA NNE

4. NI LAZIMA
TUTAMBUE KWAMBA
AGANO JIPYA
HUWEKA KIELELEZO
KITAKATIFU

4
- 25 -
MJADALA

K
ama ilivyoandikwa katika Mwanzo 6, Mungu
alimwagiza Nuhu kuhusiana na ujenzi wa safina.
“Uovu wa mwanadamu uliongezeka duniani”
na Mungu akaamua kumwangamiza mwanadamu na
wanyama na mimea na ndege wa angani. “Lakini Nuhu
alipata rehema machoni pa Bwana.” Kwa kutazamia kuja
kwa gharika, Mungu alimkabidhi Nuhu majukumu ya
kujenga safina. Safina ilikuwa ni kwa ajili ya kuwahifadhi
wenye haki, Mungu alitoa maelekezo juu ya vifaa
vitakavyotumika kujengea safina, na akaorodhesha vipimo
vyake. Kwa hiyo Mungu alimpatia Nuhu kielelezo mahsusi
cha namna Safina itakavyojengwa. Katika Mwanzo 6:22,
maandiko matakatifu yanasema: “Ndivyo alivyofanya
Nuhu, sawasawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo
ndivyo alivyofanya.”
Katika Kutoka 25, Mungu alimwelekeza Musa kujenga
hema takatifu. Mlolongo wa maelekezo ya jinsi ya
kujenga yalitolewa kwa Musa. Musa alionywa na
Mungu: “Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama
mfano wake ulioonyeshwa mlimani” (Kutoka 25:40).
Katika Waebrania 8:5 Roho Mtakatifu hurejelea maonyo
ya Mungu kwa Musa, “…alipokuwa tayari kuifanya ile
hema, maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa
mfano ule ulioonyeshwa katika mlima.” Katika kutoka
40:16 andiko linasema: “Musa akafanya hayo yote, kama
BWANA alivyoagiza ndivyo alivyofanya.”
Kama Mungu alivyompa Nuhu kielelezo cha kujenga safina,
na kama pia Mungu alivyompa Musa kielelezo cha kujenga

- 26 -
hema, vivyo hivyo Mungu amempa mwanadamu kielelezo
kwa ajili ya kujenga maisha yake. Mungu ametoa kielelezo
juu ya tabia ya Kikristo (tabia na matendo) na kielelezo kwa
kanisa (taasisi, jina, ibada, malengo ya wokovu, utume).

kielelezo, na pia kama vile Musa alivyowajibika kujenga


hema kulingana na kielelezo, ndivyo na sisi tunavyowajibika
kujenga kulingana na kielelezo kitakatifu.
Mungu, ambaye alimuumba mwanadamu na ambaye
anamjua mwanadamu vizuri, na ambaye anajua kitu
ambacho ni bora kwa mwanadamu, siku zote amejiwekea
haki ya kumwongoza mwanadamu. Na kitabu kitakatifu
ambacho kupitia kwacho anatafuta kumwongoza
mwanadamu sasa ni Agano Jipya la Bwana na mwokozi
wetu Yesu Kristo. Agano Jipya ni kielelezo.
Kielelezo ni kitu kinachofaa kuigwa na ni kitu
kinachokusudiwa kuigwa. Ni usanifu, mwongozo, kitu
cha kuigwa. Mungu alipompa Nuhu kielelezo kwa ajili ya

alielewa vizuri kwamba Mungu alipompa kielelezo kwa ajili


ya kujenga hema, alikuwa hatoi maoni au mapendekezo.
Kuna ndugu fulani (pengine watu “wasiosadikika”
lingekuwa neno zuri) miongoni mwetu ambao wanapinga
kabisa kwamba Agano Jipya ni kielelezo chetu. Tafakari
yafuatayo kutoka kwa Victor L. Hunter, “Some Thoughts on
Theology and Mission,” Mission Magazine, March, 1972:
“Tatizo la theolojia ya urejeshwaji hujikita katika kauli
kwamba utume wa kanisa ni kuunda kanisa la kweli ambalo
kwalo kielelezo cha maisha ya kanisa ni sawa kabisa na

- 27 -
yale ya ulimwengu wa karne ya kwanza. Hujikita katika
dhana kwamba kuna kielelezo katika Agano Jipya ambacho
kanisa linatakiwa kukiiga kwa kila kizazi. Theolojia ya
namna hii inafanya utume wa kanisa kuwa wa kibinafsi na
wenye mtazamo wa kale kuliko kuwa wa kuangalia mbele
na yenye mtazamo wa maisha ya baadae.”
Inatakiwa ieleweke kuwa mtazamo ulioshuhudiwa katika
nukuu ya hapo juu (Mtazamo wa Mission Magazine)
ndio tabia halisi ya Kanisa la Kikristo (Wanafunzi wa
Yesu). Katika ukosoaji wa Ndugu J.D . Thomas We Be
Brethrean, Dr. A.T DeGroot anasema: “Katika kitabu
kizima kuna dhana imejengwa kwamba Agano Jipya ni
njia au kibebeo cha kielelezo cha maelekezo ya kanisa”
(Alfread T. DeGroot, The Restoration Principle, St. Louis,
Misouri, The Bethany Press, ukurasa 159). DeGroot
anaendelea kusema: “Kutokana na uzoefu wa Wanafunzi
wa Kristo na Kanisa la Kristo, tunaweza tukahitimisha
kwamba kwa umahususi zaidi, kadri madai ya urejeshwaji
yalivyofasiliwa katika mtazamo wa kiuongozi, kitaasisi na
muundo wa tabia na taratibu za kidini ndivyo imekuwa
na mafanikio madogo kama nguvu itendayo kazi katika
ulimwengu wa Kikristo” (ukurasa 160).
Hebu ieleweke hapa kwamba muundo wa Agano Jipya
uko ndani ya ukweli kwamba hilo ni Agano Jipya la
Bwana. Katika Mathayo 28:28 Bwana alisema: “Kwa
maana hii ndiyo damu yangu ya Agano, imwagikayo
kwa ajili ya wengi kwa ondoleo la dhambi.” Katika
Waebrania 9:15 tuna: “Na kwa sababu hii ni mjumbe
wa agano jipya…” Paulo anatangaza: “Ndugu zangu,

- 28 -
nanena kwa jinsi ya kibinadamu. Lijapokuwa ni agano
la mwanadamu, hata hivyo likiisha kuthibitika, hakuna
mtu alibatilishaye, wala kuliongeza neno” (Wagalatia
3:15). Kauli hii ni jambo la kuchukuliwa kwa umakini.
Haiwezi kubadilishwa inapokuwa imethibitishwa.
Haitakiwi kupuuzwa. Masharti yake ni lazima yazin-
gatiwe. Agano la Bwana (au mapenzi yake) huhusiana
na baraka za ajabu na faida ambazo hutolewa kwa watu
fulani pale ambapo watu hawa wanakidhi vigezo fulani.

Ukweli kwamba Agano Jipya liliwekwa ili kuwa kielelezo


chetu umesisitizwa katika maandiko kadhaa: (1) “Kila
apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo,
yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisho
hayo, huyo hana Baba na Mwana pia” (2 Yohana 9). (2)
“Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa
mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu
mpate kujifunza kutopita yale yaliyoandikwa…. ” (1 Kor.
4:6). (3) “Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi
yeye aliyewaita katika neema ya Kristo. Na kugeukia injili
ya namna nyingine: Wala si nyingine; lakini wapo watu
wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo. Lakini
ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri nyinyi
injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri na alaaniwe.”
(Wagalatia 1:6-8). (4) “Namshuhudia kila mtu
ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki. Mtu yeyote
akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yali-
yoandikwa katika kitabu hiki; na mtu yeyote akiondoa
lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu
atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na
katika ule mji mtakatifu,

- 29 -
ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.”
(Ufunuo 22:18,19).
Mungu anatarajia kuona tunatembea na kuishi
kulingana na kielelezo kitakatifu. Bwana alisema: “…
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi”
(Math. 28:20). Katika Waefeso 5:11 Paulo anasema:
“…bali msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza
bali myakemee.” Yohana anasema: “Mtu akija kwenu
naye haleti mafundisho hayo, msimkaribishe nyumbani
mwenu, wala msimpe salamu; maana yeye ampaye
salamu azishiriki kazi zake mwovu” (2 Yohana 10).
Katika hotuba kuu tatu ambazo zinaunda kitabu cha
Kumbukumbu la Torati, Musa aliwassitizia Waisraeli wa
Agano la Kale kwamba ni kwa sababu Mungu aliwapenda
ndio maana aliwapa sheria yake si kwa sababu aliwachukia;
na kwamba upendo wao kwa Mungu ungesababisha wao
kuitii sheria ya Mungu. Vivyo hivyo, ni kwa sababu ya
Upendo wa Mungu kwetu ndio maana akatupatia Agano
Jipya na upendo wetu kwake utatusukuma kutii hilo
Agano Jipya. Bwana alisema: “Mkinipenda, mtazishika
amri zangu” (Yohana 14:15). Akaendelea kusema:

(Yohana 15:14). Yohana anasema: “Kwa maana huku


ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake,
wala amri zake si nzito.” (1 Yohana 5:3).
Mungu atusaidie kutambua kadri tunavyojifunza na
kutambua ukweli kwamba Agano Jipya ni kielelezo , na
Mungu atusaidie tuishi kulingana na kielelezo. Amina.

- 30 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Jadili jukumu ambayo Mungu alimpatia Nuhu


(Mwanzo 6), na jinsi Nuhu alivyoitikia.

2. Jadili jukumu ambayo Mungu alimpatia Musa


(Kutoka 25), na jinsi Musa alivyoitikia.

3. Kulingana na Agano Jipya, ni kielelezo gani


ambacho Mungu ametupatia?

4. Jukumu letu ni nini kuhusiana na kielelezo


kitakatifu?

5. Nini maana ya “kielelezo”?

6. Ni nini mtazamo wa watu wengi miongoni mwetu


kuhusiana na dhana ya “kielelezo”?

- 31 -
7. Kwa muktadha wa sasa, ni nini umuhimu wa
Mathayo 26:28; Waebrania 9:15; Wagalatia 3:15?

8. Ni nini umuhimu wa 2 Yohana 9; 1 Wakorintho


4:6; Wagalatia 1:6-8; Ufunuo 22:18,19?

9. Kulingana na Mathayo 28:20, Waefeso 5:11, na 2


Yohana 10, Mungu anatarajia nini kutoka kwetu?

10. Katika hotuba tatu kuu (katika kitabu cha


Kumbukumbu la Torati) Musa alikuwa anasisitiza
kitu gani kwa wana wa Israeli?

11. Kwa nini Mungu aliwapa wanadamu Agano


Jipya? Upendo wetu kwake utatuongoza kufanya
nini?

12. Tafadhali kariri Yohana 14:15 na Yohana 15:14 na


1 Yohana 5:3.

- 32 -
NUKUU MUHIMU
KUTOKA KWA G.K.
WALLACE

K
anisa linaweza kurejeshwa kwa kuchukua Biblia
na kuifuata kama mwongozo wake. Kanisa
linaweza kuwa leo kama lilivyokuwa wakati
uliopita kwa kufuata kielelezo cha mitume. Agano Jipya
linafunua kielelezo cha ibada na kielelezo cha mafundisho
ambacho hakiwezi wala hakitakiwi kupuuzwa. Hebu
tutafute kundi la watu wanaojiita Wakristo (Mdo.11:26).
Hebu tutafute kundi la watu ambao wanaheshimu
mpangilio wa Agano Jipya wa kanisa, wanaohubiri
mafundisho ya kweli, wanaoabudu kulingana na Biblia
inavyoelekeza, na kuishi na kuabudu kulingana na
Biblia inavyoelekeza. “Injili ni uweza wa Mungu uletao
wokovu” (Warumi 1:16). Neno injili hubeba ujumbe
wote na kamili wa Kristo katika nyakati hizi. Injili ni
njia ya Mungu; kwa hiyo tuitafute, na tutembee katika
hiyo. Kama hatutatembea katika njia sahihi, tutatembea
katika ukingo na kuangukia katika shimo refu lisilokuwa
na mwisho.

- 33 -
SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 34 -
SOMO LA TANO

5. MAANA YA IMANI
YA KIBIBLIA

5
- 35 -
Swali: Maana ya Kibiblia ya neno imani ni nini? Je
imani humaanisha kuwa na mashaka au kutokuwa na
uhakika? Je humaanisha kukubaliana na wazo bila kuwa
na ushahidi? Je ni kutokuwa na ufahamu?
Jibu:Imani yenye manufaa (imani ambayo humpa mtu
baraka na rehema za Mungu) humaanisha kusikiliza neno
la Mungu, kufuata kielelezo kitakatifu, kufanya kile Mungu
alichoagiza, kwa kuwa Mungu kasema kifanye, kwa
namna ambayo Mungu ameelekeza, kama Mungu ametoa
kielelezo mahususi, na kwa kusudi ambalo Mungu ametaka
ulifanye. Imani haimaanishi kuwa na mashaka au kutokuwa
na uhakika. Haimaanishi kukubaliana na wazo au mtazamo
bila kuwa na ushahidi. Sio kutokuwa na ufahamu.
Katika Waebrania 11:1 Paulo anasema: “Imani ni
kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, bayana ya
mambo yasiyoonekana.” Andiko hili linarejelea mambo
yatarajiwayo. “Mambo” ni yale yaliyo ndani ya pazia
(Waebrania 6:19). – mbingu yenyewe, yote ambayo ni
mbingu, na yote ambayo ni ya mbingu. Kwamba ambayo
yatatufunga kwa usalama kwa hayo yaliyomo kwenye
pazia ndilo tumaini letu, “tulilonalo kama nanga ya roho,
yenye salama yenye nguvu” (Waebrania 6:16). Tumaini
letu ni zao la, na lililozungukwa na imani yetu. Imani
yetu ni zao la neno la Mungu. “Basi imani chanzo chake
ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo” (Rum.
10:17). Kwa hiyo ni dhahiri, pale ambapo hakuna neno
la Mungu hapawezi kuwa na imani.
Lakini imani yangu ambayo huja kwa kusikia neno
la Mungu, imejikita kwa nguvu juu ya ushahidi

- 36 -
unaojitosheleza na wenye ushawishi mkubwa kwamba
Biblia ni kile ambacho inadai kuwa ndicho – neno la
Mungu aliye hai lililovuviwa, lisilokuwa na mashaka,
lisilokuwa na makosa na linalojitosheleza. Ukweli
huu (huu wa kudai hivyo ulivyo) unapokuwa
unapothibitishwa, wenyewe na katika maeneo mengi
huwa ushahidi wangu. Na ninakubali mafundisho mengi
si katika msingi mwingine isipokuwa tu kama Biblia
isemavyo. Neno linakuwa ni “ngao” yangu (Efe.
6:16). Tunaitetea imani na imani inatutetea. Imani
yangu sio imani ya bila ushahidi. Ni imani inayojikita
katika ushahidi unaojitosheleza na wenye ushawishi
mkubwa. Mambo, tumaini, imani, neno, ushahidi.
Neno “imani” mara nyingi linatumiwa kinyume na
matumizi ya Biblia ya neno hili. Ndugu mmoja alisema,
“Hakuna namna ya kuthibitisha kwamba Mungu yupo.
Tunalazimishwa kukubali wazo kwamba Mungu yupo
kwa imani.” Mwingine akasema, “Hoja hizi zitakupeleka
kwenye jambo hili…lakini kuanzia hapo unatakiwa
usonge mbele kwa misingi ya imani.” Hawa ndugu wote
walikuwa wanasisitiza juu ya wazo kwamba, ushahidi
utamsogeza mtu mbele kidogo lakini kuanzia hapo mtu
atatakiwa asonge mbele kwa kukubaliana na jambo
bila kuwepo na ushahidi. Na kutumia neno “imani”
kwa maana ya kwamba kusonga mbele pasipokuwa na
ushahidi, ni kulitumia neno hili kinyume na matumizi ya
Biblia.
Watu wengine wana hatia ya kutumia vibaya neno “imani.”
Ndugu mmoja katika kusisitiza kwamba hatuwezi kujua

- 37 -
bali tunaweza kukisia, anadai kwamba mtu mwenye
imani anafanya mambo “kana kwamba anajua.”
Tungependa kuuliza swali; Kama mtu wa imani anatenda
kama vile anajua, Kwa nini huyu mtu wa imani asiwe
mnafiki? Na kwa nini huyu mtu wa imani asiwe
agnostiki? Nukuu zifuatazo zinatoka kwa watu
ninaowapenda na ninaowaheshimu – watu wenye elimu
zao kubwa, watu wanaompenda Mungu na neno lake,
watu ambao ni marafiki wa mwandishi wa kitabu hiki.
Ninaorodhesha hapa kauli zao si kwa kuwafedhehesha
bali kwa kutaka kuthibitisha hoja kwamba wengi
wanatumia neno “imani” kwa maana ambayo ni kinyume
na maandiko. Zingatia kwa makini: “Kama ilivyoelezwa
mwanzo, hakuna ushahidi wa kutosha mahali popote pale
kuweza kuthibitisha uwepo wa Mungu, lakini kuna
ushahidi wa kutosha kuthibitisha dhana au imani
kwamba Mungu yupo.” “Uchaguzi huu au msimamo huu
ni suala la hisia binafsi, hakika, kwa sababu linavuka
mipaka ya uhalisia, na kitu ambacho kinaweza
kuthibitishwa waziwazi na kwa hiyo ni ’mruko wa imani
tu!’” “Kwa hiyo ni vema kuchukua mruko mfupi wa
imani inayotakiwa katika imani ya Kikristo, kuliko
kuchukua mruko mrefu wa imani inayotakiwa katika
upagani. Ushahidi kamili usiokuwa na shaka mara
nyingi haiwezekani kuupata, lakini imani thabiti inaweza
kuelezeka.” “Wanaoamini katika nadharia ya mgeuko,
wana imani nami pia nina imani. Ninaamini kwamba
imani yangu ni imani sahihi zaidi.” Matumizi ya namna
hii ya neno “imani” ni hatari na yanasikitisha kwa kweli!
Maana ya “imani” katika Biblia ni nini? Neno hili
linatumiwaje? Imani (kwa maana ya Kibiblia), Je

- 38 -
humaanisha “mambo ya kukisia” Je ni sawa na neno
lisilohakikishwa? Je inakuwepo tu pasipo ushahidi? “Kwa
imani Habili alimtolea Mungu dhabihu iliyo bora kuliko
Kaini…” (Waebrania 11:4). “Kwa imani…Nuhu alijenga
safinakuokoa nyumba yake…” (Waebrania 11:7). “Kwa
imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende mahali pale
atakapopapata kuwa urithi…” (Waebrania 11:8). “Lakini
kwa kuiona ahadi ya Mungu, hakusita kwa kutokuamini,
bali alitiwa nguvu kwa imani akimtukuza Mungu, huku
akijua hakika Mungu anaweza kufanya yale aliyoahidi”
(Warumi 4:20,21). Maneno “kwa imani” yana maana gani
katika kauli hizi? Je Habili, Nuhu na Ibrahimu walikuwa
wanakisia? Je, walikuwa wanafanya waliyoagizwa kwa
kukisia tu? Je walikuwa wanatenda pasipo ushahidi?
Biblia inasema: “Basi imani chanzo chake ni kusikia, na
kusikia huja kwa neno la Kristo” (Warumi 10:17). Kwa
hiyo imani ya kwenye Biblia inahusisha: (1) ukweli wa
uwepo wa Mungu (2) ukweli wa uwepo wa mwanadamu
(3) uwezo wa Mungu wa kumfunulia mwanadamu (4)
uwezo wa mwanadamu kumsikiliza Mungu (5) ushuhuda
wa Mungu kwa mwanadamu (6) na mwitikio sahihi wa
mwanadamu kwa ushuhuda.
Tunasisitiza tena kwamba “imani” – kwa maana ya Biblia
ni kutenda kama Mungu alivyoagiza. Hakuna imani ya
Kibiblia ambayo haina ushuhuda kutoka kwa Mungu.
Imani haimaanishi kukosekana kwa ushahidi. Ukweli
ni kwamba imani inahitaji kuwepo na ushahidi, na
hakuwezi kuwa na imani pale pasipo na ushahidi. Mungu
anahitaji tuwe na ushahidi. Uwepo wa Biblia yenyewe

- 39 -
ni ushahidi. Yohana anasema: “Lakini hizi zimeandikwa
ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana
wa Mungu; na kwa kuamini muwe na uzima kwa jina
lake” (Yohana 20:31).
Hatuwezi tukakosoa tabia ya Tomaso (Yohana 20:24,25).
Bali tunaheshimu sana tabia yake. Tabia yake ilikuwa ni:
“Bila ushahidi, sitaweza kuamini. Nipatie ushahidi nami
nitaamini.” Bwana alimpatia Tomaso ushahidi. Tomaso
alipoona ushahidi akasema: “Bwana wangu na Mungu
wangu.” Dkt. Luka mwanasayansi pekee aliyefunzwa
miongoni mwa waandishi wa Agano Jipya, alifanya
uchunguzi wa suala zima na akaandika kama ifuatavyo: “Kwa
kuwa, watu wengi wametafuta ili kuandika habari za mambo
yaliyotukia katikati yetu, kama vile yalivyokabidhiwa kwetu
na wale ambao walikuwa mashahidi walioona na watumishi
wa Bwana, mimi nami baada ya kuchunguza kila kitu kwa
uangalifu kuanzia mwanzo, niliamua kukuandikia habari

ukweli kuhusu yale uliyofundishwa” (Luka 1:1-4).


Imani kwa namna yoyote ile haimaanishi kukosekana
kwa vitu tunavyoweza kuviona kwa macho. Wakati
mwingine imani hutofautishwa na kuona vitu (kama
ilivyo katika 2 Kor. 5:7), lakini kunaweza kuwa na imani
pale tunapoweza kuona. Bwana alimwambia Tomaso:
“…Wewe kwa kuwa umeniona, umesadiki..” (Yohana
20:29). Wasamaria wengi walimwamini Yesu kwa
sababu ya neno lake (Yohana 4:41). Ukweli kwamba
walikuwa wanamwona hakukuhusisha imani yao kwake.
Kuna imani pale ambapo huwezi ukaona kitu. Bwana

- 40 -
akamwambia Thomaso: “…wa heri wale wasioona,
wakasadiki.”
Wala imani haimaanishi kutokuwepo kwa maarifa.
Inapaswa tupaze sauti kwamba imani ya Biblia
iliyothibitishwa haiondoi kukosa maarifa. Paulo
alisema: “Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua
ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa
mbali na Bwana”. (2 Kor. 5:6) Paulo alijuaje? “Maana
twaenenda kwa imani, si kwa kuona” (2 Kor. 5:7). Haya
ndio maarifa ambayo ni zao la imani. Wasamaria wengi
walioamini katika Bwana walimwambia mwanamke:
“Sasa tunaamini wala si kwa maneno yako tu; maana
sisi tumesikia wenyewe, tena twajua hakika huyu ndiye
mwokozi wa ulimwengu.” (Yohana 4:42). Walisema,
“Tunaamini” na “Tunajua.” Imani haiondoi maarifa wala
maarifa hayaondoi imani. Petro alimwambia Yesu: “Nasi
tumesadiki, tena tumejua kuwa wewe ndiye Mtakatifu wa
Mungu” (Yohana 6:69). (Katika Agano Jipya la Kiyunani
vitenzi vyote viwili [“kuamini” na “kujua”] ni vitenzi
vya hali timilifu. Nguvu ya ukweli huu ni kwamba, kwa
tafsiri ya moja kwa moja Petro anasema: “Tumeamini,
sasa tunaamini, na tutaendelea kuamini; tumejua, sasa
tunajua, na tutaendelea kujua.” Kuamini na kujua ni
vitu vinavyokwenda pamoja.) Paulo anasema: “….kwa
maana namjua yeye niliyemwamini…” (2 Tim.1:12).
Mungu atusaidie tuwe makini katika usemi wetu. Tukusudie
kwa upya kwamba tutaanza kutumia maneno ya kwenye
Biblia kwa jinsi yalivyotumika kwenye Biblia. “Mtu
akisema, na aseme kama mausia ya Mungu…” (1 Pet. 4:11).

- 41 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Imani yenye manufaa humaanisha nini?

2. Je imani ya Biblia ina maana ya mashaka au kutokuwa


na uhakika?

3. Kwa kuzingatia Waebrania 11: 1, tafakari kwa makini


uhusiano uliopo kati ya maneno “mambo,” “tumaini,”
“imani,” “neno” na “ushahidi.”

4. Imani yangu, ambayo huja kwa kusikia neno la


Mungu imejengwa kwenye nini?

5. Biblia inadai kuwa ni nini?

6. Pale ambapo ukweli kwamba neno la Mungu


limethibitishwa, basi neno lenyewe linakuwa nini?

7. Je, imani ya Kikristo ni “imani isiyokuwa na


ushahidi?”

8. Kutumia neno “imani” kwa maana ya kusonga mbele


bila kuwa na ushahidi ni sawa na kufanya nini?

9. Je ni sawa (yaani, sawasawa na maandiko) kutumia


neno “imani” kumaanisha “makisio?” ni sawa
kuzunguma juu ya “mruko wa imani?”

- 42 -
10. Kwa kuzingatia Warumi 4:20,21 imani ya Ibrahimu
ilikuwa ni kazi ya kukisia?

11. Je, Habili, Nuhu, na Ibrahimu walikuwa wanatenda


kutokana na makisio?

12. Kulingana na Warumi 10:17, imani ya Biblia angalau


inahusisha mambo sita. Ni yapi hayo?

13. Ukweli wa uwepo wa Bibilia huthibitisha ukweli


kuhusu nini?

14. Kariri Yohana 20:30, 31

15. Elezea juu ya tabia ya kupendeza ya Tomaso.

16. Elezea kauli ya Luka katika Luka 1:1-4.

17. Je, inawezekana kuwepo na “imani” pale unapoweza


“kuona” kitu?

18. Je “imani” humaanisha kukosekana kwa ushahidi?

19. Je “imani” humaanisha kukosekana kwa maarifa?

20. Je “imani” huondoa “maarifa?” Je “maarifa” huondoa


“imani?”

21. Ni kwa jinsi gani tunatakiwa tuwe makini katika


kutumia maneno ya kwenye Biblia?

- 43 -
SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 44 -
SOMO LA SITA

6. JE KUNA
UWEZEKANO WA SISI
KUFAHAMU?

6
- 45 -
Swali: Katika masuala ya kiroho, je tunaweza kufahamu?
Je tunaweza kujua kwamba Biblia ni neno la Mungu?
Tunaweza kuelewa kwamba sisi ni Wakristo? Je kufahamu
huondoa imani?
Jibu: Hakika, inawezekana sisi kufahamu. Tunaweza
kufahamu kwamba Mungu yupo. Tunaweza tukafahamu
kwamba Biblia ni neno la Mungu. Tunaweza kufahamu
kwamba sisi ni watoto wa Mungu. Kufahamu hakuondoi
imani, na wala imani haindoi ufahamu.

TATIZO
Neno la Kiyunani “ginosko” linalomaanisha
“ninafahamu.” Kiambishi “a-“ (alpha ya Kiyunani) kina
dhana hasi. Hivyo, “aginosko” humaanisha “kutokujua.”
Neno hili ndicho chanzo cha neno la Kiingereza
“agnostic.” Agnostiki ni mtu ambaye anadai kuwa
hakuna ushahidi wa kuhalalisha hitimisho. “Muagnostiki
ni mtu anayedai kwamba hakuna mtu ambaye anaweza
kujua Mungu yupo au kuna ulimwengu wa kiroho. Neno
hili lina asili ya Kiyunani, likiwa na maana ya kutokujua.
Muagnostiki hasemi kwamba hakuna Mungu. Anasema
tu kwamba hawezi kujua. Imani kwamba mtu anatakiwa
akubali kile tu ambacho kinaweza kufahamika kwa
kupitia uzoefu halisi huitwa Uagnostiki”. (World Book,
ukurasa wa 85).
Inasikitisha sana kwamba kuna ndugu miongoni mwetu,
ambao wanafundisha kwamba haiwezekani sisi kujua
kwamba Mungu yupo, na kwamba Biblia ni neno la
Mungu. Tafakari haya yafuatayo:

- 46 -
1. “Ndio, hatuwezi kujua kwamba Mungu yupo. Hakuna
namna tunayoweza kuthibitisha kwamba Mungu
yupo. Tunalazimika kukubali wazo la kwamba Mungu
yupo kwa njia ya imani.”
2. “Mjadala huu utakupeleka kwenye hoja hii…
lakini kuanzia hapo itakubidi usonge mbele kwa
kutumia imani. Hakuna namna kwa kweli ya kuweza
kufahamu.”
3. “Hata hivyo, imani ya namna yoyote ile imejikita
katika uwezekano…mambo ya kufikirika kabisa, ni
dhana tu ya kinadharia.”
4. “Mtu wa imani hufanya mambo ‘kana kwamba’
alikuwa anafahamu…Watu wote wanaishi maisha
yao kwa kufuata imani, kitu kinachowafanya waone
ni kiwango cha juu cha uwezekano.”
5. “Kama ilivyoelezwa mwanzo, hakuna ushahidi wa
kutosha mahali popote pale kuweza kuthibitisha
uwepo wa Mungu, lakini kuna ushahidi wa kutosha
kuthibitisha dhana au imani kwamba Mungu yupo.”
6. “Uchaguzi huu au msimamo huu ni suala la hisia
binafsi, hakika, kwa sababu linavuka mipaka ya
uhalisia, na kitu ambacho kinaweza kuthibitishwa
waziwazi na kwa hiyo ni ’mruko wa imani tu!’”
7. “Kwa hiyo ni vema kuchukua mruko mfupi wa
imani inayotakiwa katika imani ya Kikristo, kuliko
kuchukua mruko mrefu wa imani inayotakiwa katika
upagani. Ushahidi kamili usiokuwa na shaka mara
nyingi haiwezekani kuupata, lakini imani thabiti
inaweza kuelezeka.”

- 47 -
8. Mwamgeuko, ana imani, nami pia nina imani.
Ninaamini kwamba imani yangu ni imani sahihi
zaidi.”
9. “…Hakuwezi kuwa na imani ya kweli bila ukweli,
ushahidi na maarifa…hata hivyo hawathibitishi
kwamba hoja imekubaliwa.”
10. Mwandishi mmoja anazungumzia “Nyanja mbili
za ukweli – wa kimwili na metafizikia.” Anasema
kwamba katika uwanja wa kuonekana kwa vitu
halisi, kunaweza kuwa na maarifa fulani lakini
“….hata hivyo mambo ya kufikirika hayawezekani
katika uwanja wa metafizikia.” Ni kutokana na hoja
hii ndipo anasema “kiwango fulani cha kuthibitika,
ambacho kinaweza kupelekea kiwango kikubwa cha
uwezekano. ” Anaendela kusema: “Ikiwa Ukristo na
mafundisho yake yote yanaweza kuthibitishwa, basi
kusingekuwa na haja ya kuwa na imani.”

MAANA YA MAARIFA
Tunaweza kufahamu kwamba Mungu yupo? Tunaweza
kufahamu kwamba Biblia ni neno la Mungu? Swali la
msingi lililopo kwenye maswali haya ni: Je, tunaweza
kujua kitu chochote kile? Na je kama tunaweza kujua
chochote, je tunaweza kujua kama Mungu yupo? Kujibu
swali hili ni lazima tujue “kufahamu” maana yake ni nini.
(Maswali mengine ya kufurahisha: Hivi inawezekana
mtu kuwa na maarifa juu ya maana ya “kufahamu?” Hivi
inawezekana mtu kufahamu kwamba haiwezekani mtu
kufahamu?)

- 48 -
Jibu kwa swali hili (Je tunaweza kufahamu kitu chochote?)
huhusisha uwanja wa taaluma unaoitwa “epistemolojia.”
“Epistemolojia” ni uwanja wa taaluma unajihusisha na
chanzo, asili, mbinu na mipaka ya maarifa. Epistemolojia,
au nadharia ya maarifa ni tawi la falsafa linaloshughulika
na asili na mawanda ya maarifa, madhanio na misingi
yake, na mategemeo ya jumla ya madai yake juu ya
maarifa”. (Saikolopedia ya Falsafa, Juzuu ya 3, ukurasa
wa 8). Mwanadamu anapata maarifa kupitia njia mbili.
Tunapata kufahamu (kujifunza) kwa kupitia uzoefu
na tunapata kufahamu (kujifunza) kwa kutafakari. Au
tunapata kufahamu kwa miguso ya hisia, na tunapata
kufahamu kwa kufikiri. Lengo langu sio kuleta mjadala
juu ya namna “hisia” inavyohusiana na “Epistemolojia,”
lakini kwa kusisitiza hilo tunapata kufahamu kwa njia za
msingi mbili. Maarifa ambayo huja kwa kupitia mguso
wa hisia au uzoefu halisi huwekwa ya uga Sayansi.
Maarifa ambayo huja kwa njia ya kutafakari huwekwa
uga wa Falsafa. Maarifa ambayo huja kupitia uzoefu,
yanaweza: kihisabati, kifizikia, kibiolojia au kijamii.
Ikiwa kutafakari kunahusiana na ulimwengu, basi
huwekwa chini ya uga wa metafizikia. Ikiwa kutafakari
kunahusiana na mwenendo, basi huwekwa chini ya uga
wa maadili. Ikiwa kutafakari kunahusiana na urembo
basi, huwekwa chini ya uga wa ujumi. Ikiwa kutafakari
ni kujenga hoja kwa usahihi, basi huwekwa chini ya uga
wa mantiki.

- 49 -
USHAHIDI KWAMBA TUNAWEZA
KUFAHAMU
Wanafalsafa Jarabati wanasisitiza kuwa maarifa
ya kweli hupatikana kwa msaada wa kuhisi vitu
vinavyoshikika. Wanafalsafa wa Maisha wanasisitiza
kwamba, haiwezekani mtu kufahamu kitu chochote.
Tunasisitiza katika hoja hii kwamba, ingawa kuna maarifa
yanayopatikana kutokana na vitu vinavyoshikika, pia ni
kweli kwamba kuna maarifa yanayotokana na kutafakari.
Tunasisitiza kwamba inawezekana mtu kufahamu na
kujua kwamba anajua kwa kufanya kazi (kwa bidii)
kutokana na matakwa ya kanuni za ujengaji hoja kwa
usahihi.
Inafahamika kuwa 7 mara 7 jibu lake ni 49. “49” ni
hitimisho lililofikiwa baada ya kutafakari. Lakini
inawezekana sisi kufahamu (na kufahamu kwamba
tunafahamu) kwamba 7 mara 7 jibu ni 49. Vilevile
mtu akiweka sarafu kwenye bahasha, halafu akaiweka
bahasha sandukuni – tunaweza kujua sarafu ilipo.
Tunaweza kujua kwamba ipo sandukuni, na ufahamu
huu tunakuwa nao kwa kutafakari, sio kwa kuhisi. Ikiwa
wanadamu wote ni viumbe wanaokufa, na kama Socrates
alikuwa ni mwanadamu, kwa hiyo tunafahamu kwamba
Socrates alikuwa ni kiumbe anayekufa. Nilisema kitu
hiki kwa wanafunzi wangu: “Kama ni kweli kwamba
alama ya lafudhi inaweza kukaa kwenye silabi tatu
za mwisho katika neno la Kiyunani, na kama ni kweli
kwamba lafudhi ya “sakamfleksi” inaweza kukaa kwenye
silabi mbili za mwisho katika neno la Kiyunani, na ikiwa

- 50 -
ni kweli kwamba lafudhi ya “grevu” inaweza kukaa
kwenye silabi ya mwisho tu ya neno la Kiyunani – kwa
hiyo ni kweli kwamba silabi ya tatu ya neno la Kiyunani
linakuwa na alama ya lafudhi. Na unaweza ukafahamu
hili, na unaweza ukafahamu kwamba unafahamu.”
Sheria ya mantiki inasema kuwa “tunatakiwa kuthibitisha
hitimisho kwa ushahidi.” Ushahidi unaofaa hakika
unahitaji hitimisho fulani. Hatuzungumzi juu ya makisio.
Hatuzungumzi juu ya kuhisi au kubuni au uwezekano.
Tunazungumza juu ya hitimisho linalohitaji ushahidi
mkononi. Na hilo hitimisho linalohitaji ushahidi ni suala
la maarifa. Ni maarifa sawa kama tunavyozungumzia
suala la utambuzi wa hisia.
Ni aina hii ya maarifa tuliyonayo akilini pale tunaposisitiza
kwamba Mungu yupo, kwamba Yesu ni Mwana wa
Mungu, na kwamba Biblia ni neno la Mungu. Ni aina
hii ya maarifa ambayo husukumwa na kuchunguza
ukweli: haiwezekani kuwa na athari bila kuwepo sababu,
haiwezekani kuwepo na sheria bila kuwepo mtoa sheria,
haiwezekani kuwepo picha bila kuwepo mchoraji, hakuna
shairi bila mshairi, hakuna usanifu bila msanifu, hakuna
mawazo bila kuwepo na muwazaji, hakuna uhandisi bila
kuwepo mhandisi, hakuna kemia bila kuwepo mkemia
na hakuna hisabati bila kuwepo mwanahisabati. Sio
lengo la sehemu hii ya kitabu hiki kujadili kwa kina
namna tunavyoweza kufahamu kwamba Mungu yupo
bali ni kusema kwa msisitizo kwamba ni ukweli kwamba
tunaweza kufahamu kwamba Mungu yupo.

- 51 -
MAFUNDISHO YA WAZI YA BIBLIA
Pengine inatakiwa ifahamike kwamba, kwa wale
wanaopenda, kuamini, na kuiheshimu Biblia, kutakuwa
hakuna tatizo kwenye hoja hii. Maana Biblia imekuwa
ikisisitiza mara zote kwamba tunaweza na ni lazima
tumfahamu Mungu.
Tafakari yafuatayo:
1. Bwana alisema: “Nao uzima wa milele ndio huu,
wakujue Wewe uliye Mungu wa pekee, wa kweli na
Yesu Kristo uliyemtuma” (Yohana 17:3); “Mtu ye
yote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua
kama mafundisho Yangu yanatoka kwa Mungu au
ninanena kwa ajili yangu mwenyewe” (Yohana 7:17);
“Ndipo mtaijua kweli nayo kweli itawaweka huru”
(Yohana 8:32).
2. Petro alisema: “Tumeamini na kujua kwamba wewe
ndiwe Mtakatifu wa Mungu.”
3. Luka mwanasayansi msomi alisema: “…mimi nami
baada ya kuchunguza kila kitu kwa uangalifu kuanzia
mwanzo, niliamua kukuandikia habari za mambo
hayo ewe mtukufu Theofilo, ili upate kujua ule ukweli
kuhusu yale uliyofundishwa” (Luka 1:3,4).
4. Paulo alisema: “Kwa maana twajua kwamba kama
hema yetu ya dunia tunayoishi ikiharibiwa, tunalo
jengo kutoka kwa Mungu, nyumba isiyojengwa kwa
mikono ya wanadamu” (2 Kor.5:1).
5. Paulo akaendelea kusema: “Kwa hiyo siku zote tunalo
tumaini, hata ingawa tunajua kwamba wakati tukiwa
katika mwili huu, tuko mbali na Bwana, kwa maana

- 52 -
twaenenda kwa imani wala si kwa kuona. Naam,
tunalo tumaini na ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili
huu na kwenda kukaa na Bwana.” (2 Kor.5:6-8)
6. “…Hii ndiyo sababu ninateseka namna hii, lakini sioni
haya kwa maana ninamjua Yeye niliyemwamini na
kusadiki ya kuwa anaweza kukilinda kile nilichokiweka
amana kwake hadi siku ile” (2Tim. 1:12)
7. Wasamaria walimwambia yule mwanamke: “Sasa
tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu,
bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua
hakika kweli ya kwamba huyu ndiye Kristo, Mwokozi
wa ulimwengu.” (Yohana 4:42).
8. Yohana alisema: “Nimewaandikia ninyi akina baba,
kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo…”
(1Yohana 2:13,14); “Na katika hili twajua ya kuwa
tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake” (1 Yohana
2:3); “Kama mkijua ya kwamba yeye ni mwenye
haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na
yeye” (1 Yohana 2:29). Kimsingi, katika kitabu cha
Waraka wa Kwanza wa Yohana, mwandishi anatumia
neno “kujua” mara ishirini na nne. Wale wanaosisitiza
kwamba hatuwezi “kujua” inatakiwa wafanye bidii
katika kusoma kwa makini maandishi ya Yohana.

HITIMISHO
Wapendwa, tulitaka kusisitiza juu ya madai yanayotolewa
kwamba eti hatuwezi kujua kwamba Mungu yupo, na
kwamba Biblia ni neno la Mungu – kwamba hatuwezi
kuthibitisha kuwa Mungu yupo, na kwamba Biblia
ni neno la Mungu – ni madai ambayo hayana ukweli

- 53 -
wowote. Kuna maarifa yanayopatikana kutokana na
vitu vya kuonekana, na kuna maarifa yanayopatikana
kwa njia ya kutafakari. Na hayo maarifa yanayopatikana
kwa njia ya kutafakari (ikiwa huko kutafakari kunafuata
njia sahihi ya kujenga hoja) yanakuwa ni kweli, na ya
thamani, na yenye mamlaka kama ambavyo maarifa
yapatikanayo kwa njia ya hisia za utambuzi. Mtu yeyote
aliyewahi kupata jibu ambalo si sahihi kwenye mahesabu
ya aljebra anajua kwamba inawezekana mtu kukosea –
yaani kupata jibu ambalo sio sahihi. Na inawezekana mtu
kuthibitisha na kujua jibu sahihi lilikuwa ni lipi.
Hoja inayoongelewa hapa ni hoja yenye umuhimu
mkubwa sana. Mungu atusaidie ili wote tuwasaidie
wapendwa wetu na dunia kwa ujumla kujua kwamba
tunaweza kuthibitisha kuwa Mungu yupo, kuwa Yesu ni
Mwana wa Mungu, na kwamba Biblia ni neno la Mungu.
“Nawaandikia mambo haya ninyi mnaoliamini Jina la
Mwana wa Mungu ili mpate kujua ya kuwa mnao uzima
wa milele…Nasi kama tunajua ya kuwa atusikia, lo lote
tuombalo, tunajua ya kwamba tumekwisha kupata zile
haja tulizomwomba…Sisi twajua kuwa tu watoto wa
Mungu na ya kwamba ulimwengu wote uko chini ya
utawala wa yule mwovu.Nasi twajua ya kwamba Mwana
wa Mungu amekuja, naye ametupa sisi akili ili tupate
kumjua Yeye aliye Kweli. Nasi tumo ndani Yake Yeye
aliye Kweli, yaani, ndani ya Yesu Kristo Mwanawe. Yeye
ndiye Mungu wa kweli na uzima wa milele” (1 Yohana
5:13, 15, 19,20)

- 54 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Kama ilivyoonyeshwa mwanzo kwenye maswali na


majibu, malengo ya sura hii ni nini?

2. Tafakari kwa makini: agnostiki ni mtu wa aina gani?

3. Kama ilivyoonyeshwa kwenye nukuu kumi, wapend-


wa wengi wanafundisha kwamba haiwezekani sisi
KUJUA vitu gani muhimu?

4. Ikiwa mtu anadai kwamba hatuwezi KUJUA vitu hivi


muhimu, anakuwa yupo katika nafasi gani?

5. Hivi inaleta maana mtu kudai kwamba ANAJUA


kwamba mwanadamu hawezi KUJUA kitu chochote?

6. Inawezekana sisi KUJUA kile kinachomaanishwa na


KUJUA?

7. Ni nini maana ya neno “epistemolojia”?

8. Mwanadamu anapata maarifa kwa njia gani mbili


muhimu?

9. Msimamo wa Wanafalsafa Jarabati ni upi?

10. Msimamo wa Wanafalsafa wa Maisha ni upi?

- 55 -
11. Katika somo letu, “49” inawakilisha hitimisho la
namna gani?

12. Ikiwa mtu ataweka sarafu kwenye bahasha na kisha


akaiweka bahasha kwenye sanduku, je ninaweza ku-
jua kwamba bahasha imo kwenye sanduku?

13. Je inawezekana sisi kujua kwamba Socrate alikuwa ni


kiumbe anayekufa?

14. Tafadhali, kariri “sheria ya mantiki.”

15. Hitimisho LINALOTAKIWA kuwa na USHAHIDI ni


nini?

16. Chunguza kwa makini: Yohana 17:3; Yohana 7:17;


Yohana 8:32; Yohana 6:69; Luka 1:1-4; 2 Wakorintho
5:1; 2 Wakorintho 5:6-8; 2 Timotheo 1:12; Yohana
4:42; 1 Yohana 2:13, 14; 1 Yohana 2:3; 1 Yohana 2:29

17. . Mungu atusaidie ili wote tuwasaidie wapendwa


wetu na dunia kwa ujumla KUJUA kwamba tunawe-
za KUTHIBITISHA kuwa _______,______ kwamba
___ ni ______wa Mungu, na kwamba _______ ni
_____ la Mungu.

- 56 -
SOMO LA SABA

7. KAULI YA MSINGI

7
- 57 -
T
umeshaona kwamba ni jukumu la Mkristo
“kuenenda kwa imani.” Tumeona kwamba imani
huja kwa kusikia neno la Mungu. Tumeweka
msisitizo katika hoja kwamba pale pasipokuwepo neno
la Mungu hakuwezi kuwepo na imani. Na bila imani
haiwezekani kumpendeza Mungu. Katika 1 Wakorintho
4:6, Paulo anasema: “Basi ndugu zangu, mambo haya
nimeyafanya kuwa mfano wa mimi binafsi na Apolo
kwa faida yenu, ili muweze kujifunza kutoka kwetu
maana ya ule usemi usemao, “Msivuke zaidi ya yale
yaliyoandikwa.” Hivyo hamtajivunia mtu fulani na
kumdharau mwingine.” Katika Wagalatia 1:6-9 Paulo
anasema: “Nashangaa kwamba mnamwacha upesi
hivyo Yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo na kuifuata
injili nyingine, ambayo kwa kweli si injili nyingine
kamwe, ila kwa dhahiri kuna watu wanaowachanganya
na wanaotaka kuipotosha Injili ya Kristo. Lakini hata
ikiwa sisi au malaika atokaye mbinguni akihubiri injili
nyingine tofauti na ile tuliyowahubiria sisi, basi huyo
mtu na alaaniwe! Kama vile tulivyokwisha kusema
kabla, sasa nasema tena, ikiwa mtu ye yote atawahubiria
injili kinyume na ile mliyoipokea na alaaniwe milele!”
Katika Ufunuo 22:18,19 Bwana alisema: “Namwonya
kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki: Mtu
ye yote akiongeza chochote, Mungu atamwongezea
mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Kama mtu ye
yote akipunguza cho chote katika maneno ya unabii wa
kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika
ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu, ambao
habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.” Ni dhahiri

- 58 -
kwamba hukumu ya Mungu ipo kwa mtu yeyote na wote
watakaoongeza, watakaopunguza, watakaobadilisha,
watakaopuuzia, au watakaojaribu kufanya mabadiliko
katika neno lake.
Kutokana na mafungu haya, tunatengeneza kauli ambayo
haiwezi kupingwa: Maandiko yanafundisha kwamba
katika kazi ya Kikristo na ibada tunapaswa kufanya yale
tu ambayo yameamuliwa na Mungu. Matokeo ya kauli hii
ni kusema: Inawezekana kwa mwanadamu kuyakinisha
yale yaliyoamriwa na neno la Mungu. Na kwa kuongezea
hapo ni kusema: Inawezekana kwa mwanadamu kufanya
kazi za Kikristo na kuabudu yale tu yaliyoamriwa na
neno la Mungu.
Agano Jipya mara zote husisitiza kwamba tunatakiwa
kusikiliza sauti ya Mungu, vile anavyoongea nasi kupitia
Mwana wake. Tunamsikia Mwana wake kwa kusikiliza
neno lake. Kila kitu ambacho Mkristo anafanya ni lazima
kiwe kimeamriwa na Agano Jipya. Hatutakiwi kuongeza
zaidi ya mafundisho yake. Hatutakiwi kuyapunguza.
Hatutakiwi kuyabadilisha. Hatutakiwi kuhukumu kile
ambacho Mungu ameruhusu. Hatutakiwi kukiuka sheria
ambazo Mungu kaziweka. Hatutakiwi kutunga sheria
ambazo Mungu hajaziweka.

VII. TOFAUTI MUHIMU (Sehemu ya Kwanza)


Katika “kuenenda sawa na neno la kweli” – katika
kujitahidi kuelewa suala la kutambua mamlaka ya Biblia,
kuna tofauti fulani muhimu zinazotakiwa kueleweka na
kuheshimika.

- 59 -
1. Agano la Kale/Jipya. Tunatakiwa tuelewe kwa
usahihi tofauti iliyopo kati ya Agano la Kale na Agano
Jipya. Biblia yenyewe inaweka wazi tofauti kati
ya Agano la Kale na Agano Jipya. Katika Mathayo
26:28 Bwana alisema: “Kwa maana hii ndio damu
yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi kwa
ondoleo la dhambi.” Katika Waebrania 9:15 inasema:
“Kwa sababu hii Kristo ni mjumbe wa agano jipya, ili
kwamba wale walioitwa waweze kupokea ile ahadi
ya urithi wa milele, Yeye alikufa awe ukombozi wao
kutoka katika dhambi walizozitenda chini ya agano la
kwanza.” Na katika mistari ya 16 na 17 ya Waebrania
9 inasema: “Kwa habari ya wosia, ni muhimu
kuthibitisha kifo cha yule aliyeufanya, kwa sababu
wosia huwa na nguvu tu wakati mtu akishakufa,
kamwe hauwezi kutumika wakati yule aliyeuandika
bado yungali hai.” Katika Waebrania 8:8 Paulo
anamnukuu Mungu akisema, “Siku zinakuja, asema
Bwana, nitakapofanya agano jipya na nyumba
ya Israeli na nyumba ya Yuda…” Halafu kwenye
mstari wa 13 Paulo anasema: “Kwa kuliita agano
hili “Jipya” Mungu amelifanya lile agano la kwanza
kuwa kuukuu, lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu
na kuchakaa kikaribu na kutoweka.”
Zaidi ni muhimu kutambua kwamba Mungu
amejishughulisha na mwanadamu katika mifumo
mitatu tofauti ya kidini, na kwamba tunaishi katika
mfumo wa tatu wa dini. Ni ukweli kwamba Biblia
inaweka mifumo mitatu tofauti ya kidini. Kuwa na
maarifa ya ukweli huu ni muhimu sana katika kuielewa
Biblia. Katika kurejelea hii mifumo ya kidini tunatumia

- 60 -
neno “vipindi vya dini.” Kulikuwa na kipindi cha dini
cha wazee. Kulingana na kumbukumbu za Agano
la Kale kipindi hiki hujumuisha matukio kuanzia
kipindi cha Adam hadi wakati wa kutoa sheria ya
Musa. Kulikuwa na kipindi cha dini ya Kiyahudi.
Kipindi hiki hujumuisha matukio kuanzia wakati wa
kutoa sheria kwenye mlima Sinai hadi kipindi cha
msalaba. Kuna Ukristo. Kipindi hiki huanzia wakati
wa Pentekoste ya Matendo 2 hadi siku ya Kuja
Bwana mara ya pili. Kipindi hiki ni wakati ambapo
tunatakiwa kumsikia Kristo akizungumza nasi kupitia
Agano Jipya.
2. Imani/Maoni. Ni muhimu sana kutofautisha
waziwazi kati ya imani na maoni, kati ya imani na
akili ya kibinadamu. Najua kwamba Biblia inasema
Nikodemu alikwenda kwa Bwana wakati wa usiku.
Ninaamini kwamba Nikodemu alikwenda kwa
Bwana wakati wa usiku. Biblia haituambii kwa nini
Nikodemu alikwenda kwa Bwana wakati wa usiku,
na kwa hiyo chochote tutakachosema kuhusiana
na hili itakuwa ni maoni tu. Sitakuwa na haki ya
kumlazimisha mtu mwingine kukubali maoni yangu,
na wala yeye hatakuwa na haki ya kunilazimisha mimi
kukubali maoni yake. Hakuwezi kuwapo na umoja
katika suala la maoni, na wala Biblia hailazimishi
kuwepo na umoja katika suala la maoni.
Walipokuwa wakitafakari juu ya safari ya pili ya utume,
Barnaba alitaka kumchukua Yohana Marko, na Paulo
alikuwa anapingana kabisa na wazo la kumchukua
Yohana Marko (Matendo 15:36-41). Kukatokea
“ukinzani mkali” baina yao. Wakagawanyika na

- 61 -
kila mtu akaenda njia yake. Ninapata furaha kubwa
kutokana na ukweli kwamba Mungu anaweza
kutumia udhaifu wa wanadamu kutimiza kazi kubwa.
Kwa sababu ya huu ukinzani, sasa tuna safari mbili
za utume badala ya moja, na sasa tuna watenda kazi
wanne badala ya wawili au watatu. Ninaridhika sana
katika somo kwamba kama wahubiri wawili wazuri
kabisa ambao kanisa liliwahi kuwa nao wamekinzana
vikali katika maoni ya kibinadamu, hata sisi siku zote
tutakuwa na kutofautiana katika maoni ya kibinadamu.
Na wala Biblia hailazimishi kuwepo na umoja katika
suala la maoni.
3. Muda mfupi/Kudumu. Lazima tuwe na uwezo wa
kutofautisha kati ya muda mfupi na wa kudumu.
Kulikuwa na mitume katika kanisa la awali – watu
ambao Mungu aliwaahidi miujiza ya Roho Mtakatifu,
na watu ambao Mungu aliwatimizia ahadi yake.
Kuna watu ambao walikuwa na karama za roho, na
ambao walipewa nguvu na uwezo wa kutoa karama
za miujiza kwa watu wengine. Kulikuwa na watu
wengine katika kanisa la awali waliokuwa na karama
fulani za miujiza. Kulikuwa na watu ambao mitume
waliwawekea mikono, na wakatoa miujiza ya kiroho.
Hakika, ni kweli kwamba sasa tunaona faida ya kazi
na mafundisho ya mitume, na kwamba bado yana
ushawishi mkubwa katika kanisa la Bwana wetu.
Lakini, ukweli unabaki kwamba hatuna mitume
walio hai wenye nguvu za miujiza katika kanisa letu
leo. Pia ni kweli kwamba hakuna mtu kanisani leo
ambaye ana nguvu za kufanya miujiza. Mitume walio
hai, miujiza, karama za roho – vitu hivi vilikuwa vya

- 62 -
lazima katika kanisa changa, lakini vilikuwa vya
muda mfupi tu katika asili na tabia; havikukusudiwa
kuwa sehemu ya Ukristo wa kudumu.
Kulikuwa hakuna neno la Mungu lililotimilika katika
maandishi wakati wa kanisa la awali. Kulikuwa
na uhitaji mkubwa wa mwongozo na maelekezo
matakatifu. Kwa hiyo Mungu aliwaweka manabii
katika kanisa la awali, na kupitia hawa alifunua
ujumbe wake. Kulikuwa kuna “nabii” katika kanisa
la awali na kulikuwepo kupata ufunuo wa moja
kwa moja kutoka kwa Mungu. Lakini hakuna nabii
anayeishi katika kanisa la leo, na hakuna vitu kama
mtu kupokea ufunuo wa moja kwa moja kutoka kwa
Mungu..
Katika siku ya Pentekoste ya Matendo 2, Mungu
aliweka wazi kwamba alitaka ujumbe wa injili
uhubiriwe kwa Kiyahudi. Kimsingi, katika mstari
wa 39, Petro kwa uvuvio alitangaza kuwa ujumbe
wa injili ulikuwa kwa ajili ya wamataifa pia. Lakini
Petro yeye mwenyewe hakujua maana kamili ya kile
Mungu alichosema kupitia yeye. Ni baada ya takribani
miaka kumi baadaye ndipo Mungu akafanya miujiza
ili kumshawishi Petro kuwa injili ilikuwa ni kwa
ajili ya Wamataifa na Wayahudi pia. Hii ilihusisha
uongokaji wa Kornelio na nyumba yake yote ambapo
Mungu aliowaonesha waziwazi Wamataifa na
Wayahudi kwamba injili ya Kristo ilikuwa ni kwa
ajili ya Wamataifa na Wayahudi. Katika kipindi cha
kuanzia miaka baada ya Pentekoste hadi kuongoka
kwa Kornelio na nyumba yake, kanisa lilikuwa
limekataa kuhubiri injili kwa Wamataifa. Kwa hakika,

- 63 -
hakukuwa na dhambi kukataa. Hoja yetu hapa ni
kwamba kukataa huku kulikuwa ni kwa muda mfupi,
na wala haikuwa sehemu ya Ukristo wa kudumu.
Hatufikii hitimisho hili bila kuwa na mantiki bali kwa
kuzingatia mafundisho ya jumla ya Biblia kuhusiana
na masuala haya. Kama ningekuwa namwambia mtu:
Ni jukumu lako “kutafuta kwa bidii zote karama za
kiroho” na kutoa nukuu katika 1 Wakorintho 14:1
kama uthibitisho, nitakuwa ninatenda na kufundisha
kinyume na mafundisho ya Biblia, hata kama
maneno haya yanapatikana katika 1 Wakorintho 14:1.
Tunatakiwa kutofautisha kati ya mambo ya muda
mfupi na yale ya kudumu.

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 64 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Tumeshaelewa kweli gani nne za msingi?

2. Tafadhali kariri 1 Wakorintho 4:6

3. Elezea umuhimu wa Wagalatia 1:6-9

4. Tafadhali kariri KAULI YA MSINGI

5. “Matokeo” ya kauli hii huweza kuwa?

6. Na kuongezea katika kauli hii inaweza kuwa nini?

7. Tunatakiwa kusikiliza sauti ya ________,


anayezungumza nasi kupitia______. Mwana
huzungumza nasi kupitia________, ______.
Kila kitu anachofanya Mkristo ni lazima kiwe
_______________ kwa njia ya________.

- 65 -
8. Hatutakiwi kuruhusu kile ambacho Mungu ________
hatutakiwi________kile ambacho Mungu ameruhusu.

9. Hatutakiwi __________sheria ambazo Mungu


___________; hatutakiwi __________ sheria ambazo
Mungu ______________.

10. Mathayo 26:28, Waebrania 9:16, 17, Waebrania 10:9,


na Webrania 8:8-13 huonesha waziwazi kwamba
tunatakiwa tuelewe hoja gani?

11. Mungu amejishughulisha na mwanadamu katika


__________________tofauti ya kidini. Tunaishi katika
kipindi cha mfumo wa ____________________.

12. Katika kurejelea “mifumo ” hii tunatumia neno gani?

13. Kipindi cha “Ukristo” huanzia wapi hadi wapi?

14. Pia tunatakiwa tuwe waangalifu katika kutofautisha


kati ya __________na _______.

- 66 -
15. Je biblia inatulazimisha kuwa na umoja katika
masuala ya “maoni?”

16. Tumesisitiza hoja gani kuhusiana na Barnaba na Paulo?

17. Pia tunatakiwa tuwe na uwezo kwa kutofautisha kati


ya ____________na ________.

18. Mitume hai, miujiza, karama za kiroho, mambo haya


yalikuwa ni ya________________kwa asili na tabia;
kamwe hayakukusudiwa kuwa sehemu ______ya Ukristo.

19. Leo hakuna ___________wanaoishi kanisani, na


hakuna mafunuo ya ____________ kwa mwanadamu
kutoka kwa Mungu.

20. Itakuwa ni sawa kwa Wakristo leo kukataa kuhubiri


injili kwa Wamataifa?

21. Kwa masuala yote ya Biblia tunatakiwa kutafakari kwa


makini juu ya _______________ya _____________
____________juu ya masuala haya.

- 67 -
SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 68 -
SOMO LA NANE

IX. TOFAUTI MUHIMU


(Sehemu ya Pili)

8
- 69 -
4. MAZINGIRA/MASHARTI. Katika kujitahidi
kujifunza kuhusu majukumu, wajibu na tabia zetu
tunapaswa kutofautisha kwa wazi kati ya mazingira na
masharti. Matendo 16:13-15 inaonesha mazungumzo
kati ya Lidia na nyumba yake. Mazungumzo yalikuwa:
“Siku ya Sabato tukaenda nje ya lango la mji kando
ya mto, mahali ambapo tulitarajia tungepata mahali
pa kufanyia maombi. Tukaketi, tukaanza kuongea
na baadhi ya wanawake waliokuwa wamekusanyika
huko. Mmoja wa wale wanawake waliotusikiliza
aliitwa Lidia, mfanya biashara wa nguo za zambarau,
mwenyeji wa mji wa Thiatira, aliyekuwa mcha Mungu.
Bwana akaufungua moyo wake akaupokea ujumbe wa
Paulo. Basi alipokwisha kubatizwa yeye na watu wa
nyumbani mwake, alitukaribisha nyumbani mwake
akisema, “Kama mmeona kweli mimi nimemwamini
Bwana, karibuni mkae nyumbani mwangu.’’ Naye
akatushawishi.” Siku ya Sabato, mahali pakufanyia
maombi, kukaa chini, kukutana kwa wanawake – haya
yalikuwa ni mazingira. Kuhubiri, kusikiliza, kuamini,
kubatizwa – hizi zilikuwa ni masharti. Mazingira
hubadilika; masharti hayabadiliki.
Matendo 16 pia huonesha kubadilika kwa askari wa
gereza pamoja na nyumba yake na kumfuata Kristo.
Kufungwa kwa Paulo na Sila, kusali na kuimba usiku
wa manane, wafungwa kusikiliza, tetemeko kubwa
la ardhi, kuta kutetemeko, milango kufunguliwa,
mikono kufunguliwa – haya yalikuwa ni mazingira.
Kuhubiri, kusikiliza, kuamini, ubatizo – haya
yalikuwa ni masharti, yalikuwa msingi wa wokovu
wa askari wa gereza. Tunasisitiza kwamba sio vigumu

- 70 -
kutofautisha kati ya mazingira na masharti, na katika
hili akili ya kuzaliwa inaweza kutumika.
5. TUKIO/LAZIMA.Vilevile ni lazima tuweze
kutofautisha kati ya tukio na ulazima. Tunajua
kwamba katika eneo hili huwa kuna kuchanganya na
suala la hali ya mambo na mazingira. Katika baadhi
ya mambo tukio linaweza kuhusishwa na mazingira
lakini “lazima” haiwezi kuwa hali.
Katika Matendo 16:10 tunaona wito mkuu wa kwenda
Makedonia. Mungu aliweka wazi kwamba alitaka
Paulo kuhubiri injili huko Makedonia. Luka anasema:
“Baada ya Paulo kuona maono haya, mara tulijiandaa
kuondoka kwenda Makedonia tukiwa tumesadiki kwa
sababu tuliona kwa hakika kwamba Mungu ametuita
kuhubiri habari njema huko. Tukasafirikwa njia ya
bahari kutoka Troa na kwenda moja kwa moja mpaka
Samothrake, kesho yake tukafika Neapoli. Kutoka
huko tukasafirihadi Filipi, mji mkuu wa Makedonia
sehemu walipokuwa wanakaa Warumi, nasi tukakaa
kwenye mji huo kwa siku kadhaa.” Katika Safari ya
Kwenda Makedonia, Paulo na wenzake walichagua
kusafirikwa kutumia mashua. Wangeweza kutumia
njia za nchi kavu. Kitu cha lazima kilikuwa ni kwenda
Makedonia. Kusafirikwa kutumia mashua kulikuwa
ni tukio tu.
Kulingana na Matendo 20:7-9 ndugu wa Troa
walikutana ghorofa ya tatu kwa ajili ya kuabudu.
Ukweli kwamba sehemu ya kukutania ilikuwa ni
ghorofa ya tatu hakumaanishi kwamba ndiyo ibada
inayokubaliwa. Wangeweza kufanyia ibada katika

- 71 -
ghorofa ya kwanza, au ghorofa ya pili, au ghorofa ya
tano. Kitu cha lazima kilikuwa ni kumwabudu Mungu
kama alivyoagiza. Suala la tukio lilikuwa ni ghorofa
ya tatu.
6. NJIA/KANUNI. Tunapaswa kutofautisha kati ya njia
na kanuni. Wakati mwingine tunakuwa tunajihusisha
zaidi na njia kiasi cha kushindwa kuiona kanuni.
1 Wakorintho 14:26-40 ni sehemu ya mjadala
mkubwa wa Paulo juu ya “Karama za Roho,” na
ambapo mjadala umeanzia katika sura ya 12 mstari
wa 1. Kujaribu kujifunza 1 Wakorintho 14:26-40 bila
kuzingatia muktadha husika, kumesababisha matokeo
ya kusikitisha sana miongoni mwa wapendwa wetu.
Kimsingi watu wengi wamekuwa wakinukuu mstari
wa 34 bila kujua kile kilichoandikwa mstari wa 26.
Katika mistari hii Paulo anazungumzia mkutano
maalumu wa wapendwa huko Korintho. Ulikuwa
ni mkutano mahususi kwa ajili ya kupokea karama
za roho; ulikuwa ni mkutano kwa ajili yao tu. Paulo
anatoa maelekezo mahususi kuhusiana na wale
watakaokuwa wanatumia karama ya kunena kwa
lugha, kuhusu wale ambao watakuwa wanafasiri
lugha, kuhusu wale ambao wangeweza kuwa na
karama ya unabii, na kuhusu mwenendo wa wake za
manabii. Kwa kuzingatia mkutano huu, Paulo anataja
kwa uwazi kabisa masharti mawili ambayo kwayo
watu waliambiwa kuwa kimya; lakini pia anatoa
maelekezo: “Mwanamke na anyamaze kanisani….”
Paulo anafafanua: (1) hawajaruhusiwa kuzungumza;
(2) ni aibu mwanamke kuzungumza kanisani.

- 72 -
Lakini sasa hivi, katika mkusanyiko wetu wa
kawaida, wanawake wanaruhusiwa na wanahimizwa
kuimba. Wanapoimba wanakuwa wanazungumza.
Na wanapozungumza wanapokuwa wanaimba,
wanafundisha. Wanawake wanaruhusiwa “kuja
mbele,” kusimama mbele ya watu na kukiri imani
yao kwa Kristo ili waweze kubatizwa. Wanaruhusiwa
kuungama dhambi zao ili waweze kusamehewa.
Haya yote hufanyika na wala hakuna dhambi na
wala aibu. Kwa uhalisia mikutano yetu sio mikutano
inayozungumziwa katika 1 Wakorintho 14:26-40.
Je hii ina maana kwamba 1 Wakorintho 14:26-
40 haitumiki katika kanisa la leo? Haimaanishi
hivi kabisa. Kanuni zilizowekwa zitadumu kama
zilivyokuwa; njia (mazingira, masharti) ambamo
Paulo aliweka hizi kanuni hazipo katika ulimwengu
wa leo. Kanuni takatifu za kudumu ni: (1) vitu vyote
vifanyike kwa kusudi la kujenga; (2) Mungu sio
Mungu wa machafuko, bali wa amani; (3) wote wawe
watiifu; (4) mambo yote yafanyike kwa heshima na
kwa mpangilio.
7. DESTURI/SHERIA. Pia tunapaswa tuwe makini kati
ya kutofautisha desturi za wanadamu na sheria takatifu.
Naamini hii ndio njia ya kuelewa 1 Wakorintho 11:2-
16. Mengi yaliyosemwa katika mistari hii huhusiana
na desturi zilizokuwepo Korintho, juu ya wanawake
kuvaa utaji. Nashawishika kuamini kwamba Paulo,
katika mistari hii, hafundishi kwamba wanawake
Wakristo, muda wote na sehemu zote ni lazima wavae
utaji. Paulo katika mistari hii kwa kuzingatia desturi
husika, anasisitiza kanuni fulani muhimu ambazo

- 73 -
zinadumu sasa kama ilivyokuwa hapo mwanzo.
Kutokana na mistari hii tunajifunza: (1) Kichwa cha
Kristo ni Mungu; kichwa cha kila mwanaume ni
Kristo; kichwa cha kila mwanamke ni mwanaume;
(2) Mwanaume hatakiwi kufanya jambo lolote
ambalo litamkosea heshima Kristo; (3) Mwanamke
hatakiwi kufanya kitu chochote ambacho kitamkosea
heshima mwanaume; anatakiwa adumishe tabia
ya heshima na kujinyenyekeza; (4) Ni sahihi na ni
vema kuzishikilia desturi ambazo ni nzuri, hatupaswi
kuwahukumu watu wengine kwa kukiuka hizi desturi;
(5) Hatupaswi kuleta malaumu kanisani kwa kukiuka
desturi ambazo ni nzuri (6) Hatutakiwi kuvaa mavazi
ambayo yatatufanya tuonekane kama watu wachafu;
(7) Hatupaswi kuvaa mavazi ambayo tutakuwa
tunamkufuru Mungu na malaika (waliopo wakati
wa ibada); (8) Mavazi yetu yanapaswa yaonyeshe
heshima na usafi wetu. Tazama kiambatisho A.

- 74 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Tunapaswa kuwa makini katika kutofautisha kati ya


___________ na _________.

2. Siku ya sabato, mahali pa kufanyikia maombi, kukaa


chini, mkutano wa wanawake haya yote yalikuwa ni
nini?

3. Kuhubiri, kusikiliza, kuamini, ubatizo – haya


yalikuwa ni nini?

4. Kwa kurejelea kuongoka kwa askari wa gereza na


familia yake, jadili mazingira yake.

5. Kwa kurejelea kuongoka kwa askari wa gereza na


familia yake, jadili masharti yake.

6. Tunapaswa kuweza kutofautisha kati ya ___________


na _________.

7. Katika baadhi ya mambo tukio linaweza kuhusishwa


na _________ na katika mambo mengine lazima
______________.

8. Rejea Paulo kwenda Makedonia, kitu cha lazima


kilikuwa ni nini? Na tukio lilikuwa ni nini?

- 75 -
9. Kwa kuzingatia ibada iliyotajwa katika Matendo
20:7-9, kitu cha lazima kilikuwa ni nini? Na tukio
lilikuwa ni nini?

10. Tunapaswa kutofautisha kati ya ___________ na


_________.

11. 1 Wakorintho 14:26-40 ipo katikati ya mjadala wa


Paulo kuhusu kitu gani?

12. Ni mkutano wa aina gani ambao Paulo anajadili katika


1 Wakorintho 14:26-40 ?

13. Je mikutano yetu ya ibada ya kila siku hufanana na


mikutano hii?

14. ______________ zilizowekwa katika 1 Wakorintho


14:26-40 zinadumu kama ilivyokuwa mwanzo;
____________ ambamo Paulo ameziweka hizi kanuni
_______ katika ulimwengu wa leo.

15. Orodhesha kanuni kuu nne zilizowekwa katika 1


Wakorintho 14:26-40.

16. Tunapaswa kuwa makini katika kutofautisha kati ya


______________ za wanadamu na _____________
takatifu.

17. Kanuni nane takatifu zililizowekwa katika 1


Wakorintho 11:2-16 ni zipi?

- 76 -
SOMO LA TISA

X. TENDO NA
MAJUKUMU

9
- 77 -
T
unapotafakari juu ya “mamlaka ya Biblia” wakati
huu, akilini tunakuwa na mamlaka ya kimaandiko
yanayoongoza matendo yetu na tabia zetu kama
Wakristo. Matendo yetu ni matokeo ya tabia zetu; matendo
yetu hukua kutokana na majukumu yetu. Majukumu yetu
kama watoto wa Mungu, huhusiana na hoja moja ya
msingi; uokoaji wa roho. Huu ndio utume Mungu
alioutoa kwa kanisa lake – uokoaji wa roho za watu.
Hili jukumu la msingi la kuokoa roho hujumuisha
majukumu mengine ya jumla ya (1) kupeleka injili
ulimwenguni, (2) kuwasaidia wahitaji, na (3) kujenga
maadili ya kanisa. Kutekeleza majukumu haya ya jumla,
huhusisha kazi nyingi mahususi.
Ni lazima tuyatimize majukumu haya, kama tunataka
kumpendeza Mungu – hatuna uchaguzi. Lakini, kwa
kuangalia namna ambavyo tunaweza kuyatekeleza
majukumu haya, kuna maeneo ambayo tunaweza kufanya
uchaguzi.
Lakini, ni kwa jinsi gani mamlaka ya Biblia yanathibitishwa
kwa kuzingatia kile ambacho ni wajibu wetu ? Ni kwa
jinsi gani mamlaka huthibitishwa kwa kuangalia namna
tunavyopaswa kuyatekeleza majukumu haya?

XI. MUNGU HATAVUMILIA KILE AMBACHO


HAKIKURUHUSIWA
Chochote kinachotolewa kama ibada kwa Mungu,
ambacho hakijaamriwa na Agano Jipya, hakitakubalika
machoni pake. Ukweli kwamba kitu hicho
KIMEKUSUDIWA kuwa ibada kwa Mungu, haimaanishi

- 78 -
kwamba kitampendeza Mungu. Ibada ya Kaini (Mwanzo
4:2-5) haikukubalika machoni pa Mungu. Mungu kupitia
Malaki, alitafuta kuwarekebisha kuhusiana na jitihada
zao katika kufanya ibada. Mungu aliwaelezea kwamba
sadaka zao hazikukubalika machoni pake. Kimsingi
Mungu alisema: “…Jaribuni kuvitoa kwa mtawala
wenu!...” (Malaki 1:8). Bwana alitumia unabii wa Isaya
kwa Mafarisayo na Waandishi, akisema, “Nao waniabudu
bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya
wanadamu” (Mathayo 15:9).
Biblia mara nyingi hutumia neno “geni” kwa maana
ya “haikubaliki kwa sababu haijaamriwa.” Nadabu na
Abihu “….wakatoa moto wa kigeni mbele ya Bwana,
ambao yeye hakuwaagiza” (Lawi 10:1). “Kisha moto
ukatoka hapo mbele za Bwana, nao ukawala, nao wakafa
mbele za Bwana” (Lawi 10:2). Mfalme Suleimani alioa
“mwanamke wa kigeni” ambaye Mungu hakuruhusu
amwoe. Dhambi kama hii lilikuwa ni tatizo kubwa sana
katika kipindi cha Nehemia (Neh. 13:27). Sodoma na
Gomora na miji iliyoizunguka “wakaenda kufuata mambo
ya mwili yasiyo ya asili” (Yuda 7). Tumeonywa juu ya
“kuchukuliwa na mafundisho ya kigeni” (Waebrania
13:9).

XII. NI LAZIMA TUBAKI KATIKA KILELE


CHA MAMLAKA YA BIBLIA
Kanisa la Bwana limekuwa likipata mapigo ya
matatizo ya (1) ukatazaji na (2) Ulegezaji. Ukatazaji ni
kutengeneza sheria ambazo Mungu hakuweka. Ulegezaji
hupuuzia sheria ambazo Mungu ameziweka. Ukatazaji

- 79 -
huchukulia mambo ya maoni kana kwamba ni mambo
ya imani. Uliberali huchukulia mambo ya imani kama
vile ni mambo ya maoni. Ukatazaji hutafuta kufunga
pale ambapo Mungu hakufunga. Ulegezaji hutafuta
kulegeza pale ambapo Mungu amefunga. Mara nyingi
watu wanapojaribu kutoka katika hali hii ya ukatazaji
wanajikuta wapo katika hali ya Ulegezaji. Tunatakiwa
kuhakikisha kuwa tunakuwa makini kubaki katika kilele
cha mamlaka ya Biblia. Tuhakikishe kwamba hatuangukii
upande wowote kutoka kileleni – kuna kifo na uharibifu
katika pande zote!

XIII. TUNAPASWA KUJUA JINSI AMBAVYO


MUNGU HARUHUSU
Lakini, ili tuweze kubaki katika kilele cha mamlaka
ya Biblia tunapaswa kujua (1) JINSI MUNGU
ASIVYORUHUSU NA, tunapaswa tujue, (2) JINSI
MUNGU ANAVYORUHUSU. Hebu tuangalie
angalau JINSI MUNGU ASIVYORUHUSU. Ni lazima
nijikumbushe wakati wote kwamba Mungu haruhusu:
1. Kwa kuangalia vile ninavyovipenda na
nisivyovipenda;
2. Kwa kuangalia kile kinachonifurahisha;
3. Kwa kuangalia hitimisho lenye makosa ninaloweza
kufikia
4. Kwa kuangalia maoni yangu au maoni ya watu
wengine;
5. Kwa kuangalia kile ambacho ni maarufu sana;

- 80 -
6. Kwa kuangalia kile ambacho kinaweza kuwa
muafaka katika mhadhara wa mtu fulani;
7. Kwa kuangalia mtu fulani anayefahamika
au anayeheshimika katika jamii au kile
anachofundisha;
8. Kwa kuangalia tamaduni za wanadamu;
9. Kwa kuangalia uwezo wa mtu kutoweza “kuona
hatari yoyote katika hiyo”;
10. Kwa kuangalia desturi zilizodumu kwa muda
mrefu;
11. Kwa kuangalia ukimya wa maandiko.

XIV. LAKINI VIPI KUHUSU UKIMYA WA


MAANDIKO
Watu wengi sasa wanasema kuwa ala za muziki katika
ibada ya Kikristo zimeruhusiwa kwa ukimya wa
maandiko. Wanasema hivi kwa kumaanisha kwamba,
Agano Jipya halisemi chochote kuhusu hili, na kwa
hiyo zimerusuhusiwa kutumika katika ibada ya Kikristo.
Inashangaza sana kuona kwamba watu hawa hawa
wanaosema kwamba ala za muziki zimerusuhusiwa
katika ibada ya Kikristo kwa sababu maandiko yapo
kimya, pia wanasema sio lazima kitu kiruhusiwe ndipo
kimpendeze Mungu, na hivyo kinaweza kuruhusiwa
kutokana na ukimya wa Maandiko!
Dhana hii ya mamlaka ya Biblia ni kinyume kabisa na
kanuni ya msingi ya mamlaka ambayo tumekwishajifunza.
Biblia huruhusu kwa KILE INACHOSEMA – NA SIO

- 81 -
KILE AMBACHO HAISEMI! Biblia haisemi chochote
kuhusu kuhesabu rozari katika ibada ya Kikristo, lakini
ukweli huu haumaanishi kuruhusu kuhesabu rozari
katika ibada ya Kikristo. Ikiwa kila kitu ambacho Biblia
imenyamaza basi kinawekwa kwenye ibada ya Kikristo,
na ikiwa kuhesabu rozari ni kitu ambacho Biblia
imenyamaza; kwa hiyo kuhesabu rozari ni kitu ambacho
kinaweza kujumuishwa katika ibada ya Kikristo! Hoja
ya kipuuzi kiasi gani! Halafu hii ndio hoja ambayo
watu wengine wanaisimamia wanaposema kwamba ala
za muziki zimeruhusiwa kwa ukimya wa Maandiko.
Maandiko yanasema kwamba Bwana mwenyewe
asingefanya kazi kama kuhani baada ya mfumo wa sheria
ya Musa. Kwa nini? Kwa sababu hakukuwa na mamlaka
kwa ajili ya hilo! Zingatia hili andiko: “Maana ni dhahiri
kwamba Bwana wetu alitoka Yuda, kabila ambayo MUSA
HAKUNENA LO LOTE juu yake katika mambo ya
ukuhani” (Waebrania 7:14).
Akiwa Yeriko, Bwana aliwafundisha Israeli mafundisho
makuu na ya kushangaza; moja wapo lilikuwa ni umuhimu
wa ukimya wa Maandiko. Mungu aliruhusu “kelele za
kupaza sauti” mahususi. Yoshua yeye alitaka watu wapige
kelele kwa namna tofauti tofauti, katika wakati ambao sio
sahihi, na sehemu ambayo sio sahihi. Kwa hiyo Yoshua
alifafanua jambo lenyewe. Bwana alisema: (1) baada
ya kusonga mbele katika siku ya sita, na (2) baada ya
kusonga mbele siku ya saba, na (3) baada ya makuhani
kubeba sanduku la agano na tarumbeta saba, na (4) baada
ya makuhani kupiga tarumbeta na watu kusikia sauti
ya tarumbeta. NDIPO watu wangeweza kupiga kelele

- 82 -
kuu. Yoshua alisisitiza kulingana na majukumu yaliyopo
mambo ambayo hayakuruhusiwa ni (1) kupiga kelele
nyakati fulani, (2) au kusikika sauti wakati fulani, (3) au
kutoa sauti ya aina yoyote ile. Yoshua alisema: “Msipige
kelele wala sauti zenu zisisikiwe, wala neno lolote
lisitoke kinywani mwenu, hata siku ile nitakapowaamuru
kupiga kelele, ndipo mtakapopiga kelele” (Yoshua 6:10).
Ni somo gani ambalo Mungu na Yoshua waliwafundisha
Israeli kuhusu ukimya wa ufunuo wa Mungu? Mungu
alisema, na Yoshua akalifafanua vizuri.
Kumbukumbu zinasema: “Wakati baragumu zilipopigwa,
watu walipiga kelele, kwa sauti ya baragumu, wakati
watu walipopaza sauti, ukuta ukaanguka, hivyo kila mtu
akasonga mbele moja kwa moja kutokea pale alipokuwa
kutokea kila upande na kuuteka mji” (Yosh. 6:20).
Kwa kuzingatia jukumu lililokuwa mbele ya Wana wa
Israeli (kupaza sauti) kungekuwa na ubaya gani kama
wangepaza sauti muda mwingine wowote ule wakati wa
kusonga mbele? Kungekuwa na kosa gani endapo hata
wangetoa sauti yoyote hata wakati ambao ulikuwa ni
wa kupaza sauti? Jibu: Wangekuwa wanafanya jambo
ambalo halikuruhusiwa na mamlaka takatifu. Wangekuwa
wanafuata ukengeufu wao na hisia zao tu, na sio KILE
AMBACHO MUNGU AMEKWISHASEMA!

- 83 -
MSWALI YA KUJIFUNZA

1. Akilini tunakuwa na mamlaka ya kimaandiko


yanayoongoza ______ yetu na _______ zetu.

2. Matendo yetu ni matokeo ya _________ zetu; matendo


yetu hukua kutokana na ____________ yetu.

3. MAJUKUMU yetu huhusiana na hoja gani ya msingi?

4. Kwa kuhusiana na JUKUMU LETU LA MSINGI,


tuna MAJUKUMU YA JUMLA mengine matatu. Ni
yapi hayo?

5. Kutekeleza majukumu haya ya jumla kunahusisha


________________ nyingi.

6. Kwa kuangalia namna tunavyotekeleza majukumu


haya, kuna maeneo ya _______.

7. Mungu hatavumilia kitu gani?

- 84 -
8. Kweli au Si kweli. Kuwa na NIA ya kufanya ibada
kwa Mungu ni uthibitisho kwamba ibada yako
imekubaliwa mbele za Mungu.

9. Tunajenga hoja gani tunaponukuu Mwanzo 4:2-5;


Malaki 1:8 na Mathayo 15:9?

10. Maana ya “geni” ni nini?

11. Kanisa limekumbwa na matatizo gani mawili ya


msingi?

12. Elezea juu ya asili ya “ukatazaji” dhidi ya asili ya


“Ulegezaji”

13. Kwa kuzingatia haya tunatakiwa tuamue nini?

14. Kwa kurejelea JINSI AMBAVYO MNGU


HARUHUSU, tulitaja hoja kumi na moja. Tafadhali
elezea kila hoja.

15. Ni kitu gani ambacho watu wanabishana kuhusu


“Ukimya wa Maandiko?”

16. Dhana hii (mamlaka kwa kunyamaza) ni kinyume na


nini?

- 85 -
17. Je Biblia inazungumzia kuhusu habari ya kuhesabu
rozari wakati wa ibada?

18. Je, “ukimya” huu unaruhusu kuhesabu rozari wakati


wa ibada?

19. Tafakari na jadili umuhimu wa Waebrania 7:14 na


Bwana kuweza kuhudumu kama kuhani (kwa mujibu
wa sheria za Musa).

20. Pamoja na mambo mengi, ni somo gani kubwa ambalo


Mungu alilitoa kwa Waisiraeli pale Yeriko?

21. Kuhusu “kupaza sauti” kwa Waisraeli, Yoshua


alikuwa anaangalia kitu gani zaidi?

22. Yoshua alifafanua kwamba kuruhusu “kupiga kelele”


HAKUKUJUMUISHA angalau vitu vitatu. Ni vitu
gani hivyo?

23. Kungekuwa na ubaya gani kama wangepiga kelele


muda mwingine wowote ule wakati wa kusonga
mbele? Kungekuwa na kosa gani endapo hata
wangetoa sauti yoyote hata wakati ambao ulikuwa ni
wa kupiga kelele?

- 86 -
SOMO LA KUMI

XV. MAMLAKA
YANATHIBITISHWA
KWA MFANO

10
- 87 -
1. Neno “mfano” kwa mujibu wa kamusi, ni “kitu ambacho
kinatakiwa kufuatwa au kuigwa: ni kielelezo.”
Tumetaja fasili hii ili kuonesha kwamba “mfano”
unatakiwa ufuatwe au uigwe. Mfano “unashurutisha.”
Kwa miaka mingi swali hili limekuwa likiulizwa: “Ni
wakati gani ambapo mifano inakuwa inashurutisha?”
Kwa maoni yangu swali hili sio sahihi. Ni dhahiri
kwamba, kama ni mfano, unashurutisha na kama
haushurutishi basi huo sio mfano.
Swali lingeweza kuwa: Ni wakati gani ambapo Biblia
inahesabu tendo fulani kuwa ni mfano? “Lakini”
unaweza kuuliza, “hivi ndugu Thomas Warren, si ana
kitabu kizuri kabisa kinachoitwa ‘Wakati ambapo
Mfano Hushurutisha?’’ Ndio, anacho. “Hajui kuwa
swali hili sio sahihi?” Ndiyo, anajua! Anajua vizuri
kuliko mtu yeyote. “Sasa kwa nini anatumia jina hili?”
Kwa sababu swali hili kila mtu alikuwa analiuliza, na
aliweka neno MFANO katika alama za nukuu kwa
umakini kabisa.
2. Kwa hoja hii natakiwa kufafanua maana ambayo
natumia neno “kushurutisha” kwa kuhusiana na
mifano. Akilini mwangu nina wazo kwamba (1) vitu
fulani vinashurutisha (na kwa hiyo ni mifano) kwa
maana kwamba ni lazima vifanyike (hivi vinatakiwa;
hakina kuchagua – ukweli huu unafafanuliwa vizuri
kwa kuzingatia mafundisho ya Biblia juu ya suala
hili) na (2) vitu fulani vinashurutisha (na kwa hiyo
ni mifano) kwa maana kwamba vinaweza kufanyika
(Hivi vimeruhusiwa; vinaweza kufanyika, lakini
vinaweza kuachwa bila kufanyika).

- 88 -
3. Kwa mfano, nimeamriwa kuazimisha Meza ya
Bwana, 1 Kor. 11:24, 25. Nimeelekezwa (kwa
mwongozo na mfano) kuiazimisha siku ya kwanza
ya kila juma, Matendo 20:7; 1 Kor. 16:2. Hakuna
uchaguzi hapa. Nimeamriwa kwa mfano kushiriki
meza ya Bwana katika “chumba cha ghorofani”
kikiwa na “taa nyingi.” Hili linashurutisha ikiwa
tu nimerushusiwa kulifanya. Ni hiari. Nimejifunza
kutoka katika maandiko mengine kwamba eneo sio
kitu cha muhimu, na kwa hiyo, nikahitimisha kuwa
“chumba cha ghorofani” ni suala la hiari.
4. Zaidi, nimeamriwa kutoa kadri nilivyobarikiwa. Hili
ni suala la lazima. Sitakiwi kuacha kutoa wakati
nimebarikiwa. Lakini, katika 2 Wakorintho 8:1-5,
ninafundishwa kwa mifano kwamba ninaweza kuzidi
kutoa kadri ninavyobarikiwa. Ndugu wa Makedonia
walitoa “zaidi ya uwezo wao.” Je Paulo aliwaonyesha
hawa ndugu kama mfano, kwa ndugu wa Korintho?
Je huu ni mfano kwangu? Tendo hili linanishurutisha?
Kama ni hivyo, linanishurutisha kwa namna gani? Je
linanifundisha kuwa kila siku ya Bwana ni lazima
nitoe zaidi ya uwezo wangu? Au linanifundisha kuwa
ninaweza kutoa zaidi ya uwezo wangu? Ni kwa jinsi
gani mfano huu unaenda na amri?
5. Kama Agano Jipya linasema “kwenda” ndilo jambo la
lazima na kwamba njia ni uchaguzi, na kama Agano
Jipya linaonyesha Paulo alisafiri kwa merikebu,
kwa hiyo naweza kuhitimisha kuwa, Paulo kusafiri
kwa merikebu ni mfano kwangu (inanishurutisha)
kwa maana kwamba naweza kusafiri kwa merikebu.
Lakini ninaweza kusafiri kwa ndege.

- 89 -
6. Kwa kuzingatia 1 Timotheo 1:3 naamini kwamba
inashurutisha, (kwa maana kwamba umeruhusiwa,
na kwa hiyo unaweza kuigwa) na mhubiri wa injili
kufanya kazi kwenye kanisa ambapo kuna wazee.
Lakini pia ninaamini (1) kanisa likiwa na wazee tu
linaweza kuendelea kuwepo; (2) kwamba mhubiri wa
injili anaweza kufanya kazi kwenye kanisa ambalo
halina wazee wa kanisa; na (3) washiriki ambao
hawana wazee wa kanisa au mchungaji wanaweza
kuendelea kuwepo.
7. Kwa kuzingatia Matendo 11:29,30, naamini kwamba
inashurutisha, (kwa maana kwamba mfano huo
umeruhusiwa, na kwa hiyo unaweza kuigwa) kwa
washiriki kuchagua watu wawili na kutoka kwenda
kupeleka baraka kwa watu wengine.
Ikiwa mfano unashurutisha kwa maana kwamba ni
lazima ufanyike, au kwa maana kwamba unaweza
kufanyika, inatakiwa iangaliwe kwa kutazama
mafundisho ya Biblia yanasema nini kuhusiana
na hoja hii. Pia tunapaswa kuwa makini na mifano
isiyofaa. Mungu ameonesha kwa ajili ya kutufundisha
MAMBO AMBAYO HATUTAKIWI KUFANYA
NA MAMBO TUNAYOTAKIWA KUFANYA.
Thayer, akifafanua neno TUPOS anasema, “mifano
ya kugeuza mawazo, ni kielelezo ya maonyo kwa
wengine.” Ananukuu 1 Wakorintho 10:6, 11 (ukurasa
632 wa kitabu chake). Thayer anaendelea kusema: “…
matukio ya kuanguka yanachukua nafasi ya maonyo
kwa watu wengine.”

- 90 -
8. Ukweli pekee kwamba Biblia imeonyesha tendo
fulani, sio lazima iwe na maana kwamba Biblia
kuonesha tendo hilo ilikusudia liwe mfano. Ni
muhimu sana kutafakari juu ya “matendo yaliyopewa
uzito.” Agano Jipya linazungumza kuhusu….
(1) Matendo ambayo yalikuwa ni dhambi. Yuda
alimsaliti Bwana, Math. 26:47-49. Anania na
Safira walisema uongo mbele ya Roho Mtakatifu,
Matendo 5:1-11. Petro alisujudu mbele ya watunga
sheria wa kibinadamu, Wagalatia 2:11-14.
(2) Matendo yaliyokuwa sahihi wakati yalipofanywa,
lakini ambayo yangekuwa sio sahihi ikiwa
tutayafanya hayo matendo leo. Kanisa la awali
kwa takribani miaka 10, lilikuwa limekataa
kuhubiri injili kwa Wamataifa. Paulo (Matendo
21) alikuwa anafanya mambo kuonesha kwamba
alikuwa anatembea katika njia sahihi, “kushika
sheria.”
(3) Matendo ambayo yalikuwa ya muda mfupi na ya
lazima. Wakristo wa awali waliambiwa “kutafuta
kwa bidii karama za roho,” lakini karama za roho
zilikuwa ni za muda mfupi. Mitume walithibitisha
neno kwa ishara, lakini miujiza ilikuwa ni ya
muda tu.
(4) Matendo ambayo yalikuwa ni ya muda mfupi
na hiari. Paulo alimtahiri Timotheo “…kwa
ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa
maana wote walijua kwamba baba yake alikuwa
ni Myunani,” Matendo 16:3. Mitume walikuwa
wanahubiri kila siku hekaluni, Matendo 5:42.

- 91 -
(5) Matendo ambayo yalikuwa ni ya kudumu lakini
ya hiari. Ndugu wa Makedonia “walitoa zaidi ya
uwezo wao” 2 Wakorintho 8:3. Hii haikutakiwa
kufanyika, lakini iliruhusiwa kufanyika na kanuni
yao ya kwenda “maili nyingine zaidi” ni sehemu
ya kudumu ya Ukristo.
(6) Matendo ambayo yalikuwa ni ya kudumu na ya
lazima. Wakristo wa awali walitakiwa kutoa
walichonacho. Walitakiwa kuiazimisha meza ya
Bwana.
Ni dhahiri kwamba, matendo yale tu ambayo
yalikuwa ni ya hiari na/au ya kudumu na
ya lazima na ya kudumu ndiyo tunaweza
kuyahusisha na Ukristo wa leo. Tunapopata
sababu ya tendo lililofanyika katika Agano Jipya
(1) ambalo limeshuhudiwa kuwa ni sahihi, (2)
ambalo ama lilikuwa ni la hiari au lazima na (3)
ambalo linahusiana na kipengele cha kudumu
cha Ukristo – hivyo tuna mamlaka ya kuiga
tendo hilo. (ZINGATIO BINAFSI: Makala hii
“matendo yaliyoainishwa” ilitokana na uchunguzi
niliovutiwa nao nikiwa na Dkt. Thomas B. Warren,
miaka mingi iliyopita, uzoefu wangu kuhusu hili
ni kwamba umuhimu wa hoja hii hautambuliwi).
Pengine inatakiwa ioneshwe kuwa mfano
haubagui. Mfano unaoruhusu kusafiri kwa boti,
lakini haubagui kusafiri kwa gari. Matendo 20:7
inaruhusu kushiriki Meza ya Bwana katika siku
ya kwanza ya juma. Hoja kwamba ni dhambi
kushiriki Meza ya Bwana siku ya alhamisi usiku,

- 92 -
ni kwa sababu hakuna mamlaka juu ya jambo
hilo. Maandiko mengi yanaonyesha wajibu wetu
wa kuimba wakati wa Ibada ya Kikristo. Jambo
linalofanya uimbaji kwa kutumia ala za muziki
ni makosa, ni ukweli kwamba hakuna mamlaka
juu ya kufanya jambo hilo. Kanuni takatifu ya
“kuenenda kwa imani” inahusisha kuheshimu
ukimya wa Maandiko. Angalia Kiambatanisho B
na Kiambatanisho C.
Kuamua kwamba kitendo ni mfano kunahitaji; (1)
matumizi sahihi ya kanuni za sayansi ya kufasili
Biblia, (2) matumizi ya kanuni za MANTIKI, na
(3) kuangalia UJUMLA wa mafundisho ya Biblia
kuhusiana na mada inayojadiliwa.

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 93 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Mamlaka ya Biblia huthibitishwa na _____________.

2. Maana ya “mfano” ni nini?

3. Mtu anapouliza: “Ni wakati gani ambapo mfano


unashurutisha?” je hili ni swali sahihi?

4. Swali sahihi ni nini?

5. Jadili maana mbili tofauti ambazo tunazitumia kwa


neno “shurutisha”

6. Kushiriki meza ya Bwana katika siku ya kwanza ya


kila juma ni “lazima” kwa maana ipi?

7. Kushiriki meza ya Bwana kwenye chumba cha


ghorofa ni “lazima” kwa maana ipi?

8. Kutoa kadiri nilivyofanikiwa ni suala la LAZIMA.


Lakini kwa kuzingatia 2 Wakorintho 8:1-5, je ni
sahihi kutoa zaidi ya nilivyofanikiwa? Mfano huu
unahusianaje na “amri?”

9. Paulo kusafiri kwa Merikebu, ni mfano kwangu kwa


maana gani?

- 94 -
10. Je 1 Timotheo 1:3 inatoa mamlaka kwa wahubiri wa
injili kwenye kanisa ambalo lina wazee wa kanisa?
Ni kwa maana gani fungu hili “linashurutisha?” Je,
ni sawa kulingana na maandiko mhubiri kufanya kazi
kwenye kanisa ambalo halina wazee?

11. Je ni sahihi washiriki kuchagua watu wawili ili


kuunganisha nguvu ya kuwafikia wengine? Je ni
sahihi kwa washiriki kutumia mfumo wa posta
kuwafikia wengine?

12. Je tunajuaje kwamba mfano unashurutisha kwa


maana kwamba ni LAZIMA ufanyike, au kwa maana
kwamba UNAWEZA kufanyika?

13. Katika waraka wetu tuliangalia “matendo


yaliyoainishwa”. Hakikisha, unajifunza, unajadili,
unaelewa aina sita tofauti za matendo.

14. Ni vitu gani vinavyotakiwa viwe kweli ili kwamba


sisi tujue kwamba tuna mamlaka ya kuiga matendo
yaliyoandikwa kwenye Biblia?

15. Tumesema kwamba “mfano” haubagui . Tafadhali


fafanua hili.

16. Ili kujua kwamba tendo lililofanyika linahusisha


mfano kunahitajika nini?

- 95 -
SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 96 -
SOMO LA
KUMI NA MOJA

M
amlaka haitegemei kwa sababu nimeyasoma,
bali ni kutokana na ukweli kwamba Mungu
ameyaandika; sio kwa sababu nilitafakari kwa
usahihi, bali ni kwa sababu Mungu alidokeza hivyo.

XVI. MAMLAKA YAMETHIBITISHWA KWA


KUMAANISHA
Mara nyingi watu wanazungumza juu ya “dokezo,” lakini
“dokezo” huhusiana na “kumaanisha.” Ufahamu huhusika
na kufikirikwa usahihi, lakini kufikirikwa usahihi(katika
muktadha huu) kulingana na kile Mungu alichomaanisha.
Kila kitu ambacho Biblia inafundisha, hufundisha ama
kwa wazi au kwa kudokeza. Na kile inachokifundisha
kwa kudokeza ni cha kweli, kinashurutisha, chenye
mamlaka kama kile inachofundisha kwa wazi. Tunatakiwa
kufikirikwa usahihi kulingana na kile ambacho Mungu
anamaanisha kwenye matamko yake ya wazi. Na
mamlaka yanakuwapo sio kwa sababu nimeyasoma, bali
ni kutokana na ukweli kwamba Mungu ameyaandika; sio
kwa sababu nilitafakari kwa usahihi, bali ni kwa sababu
MUNGU ALIMAANISHA HICHO!
Kuna tofauti kubwa sana kati ya “ufahamu” na “makisio.”
Vitu vingi vinaitwa “dokezo” ambavyo hata sio “dokezo”
lakini ni makisio tu. Matendo 16:15 inasema kwamba
Lidia na nyumba yake walibatizwa. Mara nyingi

- 97 -
inadaiwa kuwa, kwa hiyo Lidia alikuwa ameolewa,
kwamba alikuwa na watoto, na kwamba baadhi ya hawa
watoto walikuwa ni watoto wachanga, na kwa hiyo
imeruhusiwa na maandiko kubatiza watoto wachanga.
Hapa kuna kiwango kikubwa cha “makisio” lakini sio
“dokezo.” Kuhusiana na hili hebu ieleweke kwamba sio
lazima kuzungumza juu ya ufahamu “wa lazima.” Kama
ni “dokezo” basi ni “lazima.” Na kama si “lazima” basi
sio dokezo. Mantiki ni “sayansi ya kufikia dokezo halali.”
Pale ambapo tendo, ukweli, au fundisho LINADAI taarifa
za Kibiblia bila kutajwa kwa umahususi, hivyo hilo tendo,
huo ukweli, au hilo fundisho ni suala la KUMAANISHA.
Kwa mfano, nimepewa mamlaka kufundisha kwamba
baada ya Sauli wa Taso kuwa Mkristo, aliungama dhambi
zake. Lakini hatuna tamko la wazi linaloonyesha kwamba
aliungama dhambi zake. Tunajenga hoja kama ifuatavyo:
Ikiwa (A) ni kweli kwamba hakuna mtu anayeweza
kuwa Mkristo bila kuungama dhambi zake; na ikiwa
(B) ni kweli kwamba Sauli wa Taso alikuwa Mkristo;
hivyo, (C) ni kweli kwamba Sauli wa Taso, alipotaka
kuwa Mkristo, aliungama dhambi zake. Tunakubaliana
na (A) na tunaweza kutoa uthibitisho, Tunakubaliana na
(B) na tunaweza kutoa uthibitisho. Hii inaweza kutupatia
ukweli tunapounganisha (A) na (B). Kwa hiyo, (C) – ni
kweli kwamba Sauli wa Taso, alipotaka kuwa Mkristo,
aliungama dhambi zake. Lakini ukweli huu hufundishwa
kwa KUDOKEZWA, sio kwa WAZI.
Jiometri inapowekwa kwa WAZI ukweli kwamba “kitu
chochote kizima ni jumla ya sehemu zake,” hivyo jiometri

- 98 -
imewekwa kwa KUDOKEZA (1) kwamba kitu chochote
kizima ni kikubwa kuliko sehemu zake, na (2) sehemu ya
kitu chochote ni ndogo kuliko kitu kizima kinachohusiana
nacho. Na hiki kinachofundishwa hapa kwa KUDOKEZA
ni cha kweli kama kitu ambacho kingefundishwa kwa
WAZI. Ndivyo ilivyo hata katika neno la Mungu. Katika
kushughulika na “dokezo” tunashughulika na kumaanisha.
Biblia inatoa mamlaka kwa KUDOKEZA.
Hebu turudi tena kwenye darasa la Jiometri. Tuchukulie
kwamba tunajishughulisha na umbo la kijiometri, umbo
ambalo ni mraba, na upande mmoja una urefu wa inchi
6. Hebu tuangalie huu ukweli kama hoja tofauti. (A)
tunajishughulisha na umbo la kijiometri. (B) Umbo hili ni
mraba. (C) Upande mmoja wa umbo hili ni inchi 6. Kwa
kuwa tunaelewa haya mambo matatu, tunajua mambo gani
mengine KWA SABABU TUNAJUA HAYA MAMBO
MATATU? Au, swali hilo hilo kwa namna tofauti,
“Ni nini maana ya haya mambo matatu?” Ni vitu gani
VINADOKEZWA na SENTENSI VIUNGO zilizoundwa
na VIUNGO (A) na (B) na (C)? Tunajua (D) kwamba
kuna pande zingine tatu ambazo kila upande una inchi
sita. Tunajua (E) mzingo wa umbo hili ni inchi ishirini
na nne. Tunajua (F) eneo la umbo hili ni inchi za mraba
sitini na sita. Na tunajua (G) kwamba kuna pembe mraba
nne katika umbo hili. SENTENSI VIUNGO zilizoundwa
na VIUNGO A na B na C humaanisha (D) na (E) na (F)
na (G). Hiki ni kielelezo cha MDOKEZO. Kwamba kile
tunachofahamu kwa MDOKEZO kinakuwa ni kweli,
chenye mamlaka kama kilivyo tunachofahamu kwa
WAZI. (katika hali hii ni kile tulichopewa)

- 99 -
XVII. MAMLAKA YAMETHIBITISHWA KWA
KAULI YA MOJA KWA MOJA
Sio sahihi kabisa kwa mtu kusema: “Mfano uliothibitishwa,
ufahamu wa lazima, na amri.” Tatizo langu lipo kwenye
neno “amri.” Haitoshi kukidhi hali nzima. Badala yake,
“amri” ni sehemu ya eneo kubwa la kujifunza ambapo
katika kujifunza hilo, hapa tunatumia maneno ya “kauli
ya moja kwa moja.”
Katika suala la kujifunza mamlaka ya Biblia ni muhimu
sana kuweka msisitizo katika eneo la “kauli ya moja
kwa moja.” Baadhi ya kauli za moja kwa moja ni amri,
lakini kauli nyingi za moja kwa moja sio amri. Hizi kauli
za moja kwa moja zinaweza kuainishwa katika msingi
wa HALI, na katika msingi wa ASILI ZAKE. Uainisho
huu haukufanywa bila hoja ya msingi, bali umefanywa
kwa msingi wa Agano Jipya la Kiyunani. Ni suala tu
la kutambua kile tulichonacho katika Agano Jipya la
Kiyunani. Sarufi ya Agano Jipya la Kiyunani ina hali
nne: hali ya kuarifu, hali ya kuamuru, dhamira tegemezi
na hali ya uchaguzi. Kimsingi hali humaanisha: uhusiano
wa TENDO unaoneshwa na kitenzi katika ulimwengu
wa UHALISIA. Kama tendo ni HALISI basi hali ni ya
kuarifu. Kama tendo ni UWEZEKANO WA KUTOKEA,
basi hali ama ni ya kuamuru, au dhamira tegemezi, au ya
uchaguzi.
Kauli katika hali ya KUARIFU inaweza kuwa: (1) katika
hali ya kutangaza, kama katika Marko 16:16; au (2) ya
kuuliza, kama ilivyo katika Warumi 6:1. Kauli katika
DHAMIRA TEGEMEZI inaweza kuwa (1) ya kuonya,

- 100 -
kama ilivyo katika Waebrania 6:1; (2) masharti, kama
ilivyo katika Wakolosai 3:1 (kuna aina mbalimbali za
masharti); (3) makatazo, (4) ya kufanya shauri, au (5)
hitimisho. Kauli katika hali ya KUAMURU inaweza
kuwa: (1) lazima (amri), kama ilivyo katika matendo
16:31; (2) lazima-ya kuruhusu, kama ilivyo katika
Matendo 2:38; au (3) makatazo. Kauli katika hali ya
UCHAGUZI huonesha matakwa au matamanio, kama
ilivyo katika Warumi 6:2 (“Mungu amekataza,” kwa
kawaida: haiwezi kuwa hivyo!). Kauli hii katika hali
ya uchaguzi inanipa mamlaka ya kufundisha kwamba
hatutakiwi kufundisha kwamba tunatakiwa kuendelea
katika dhambi ili neema izidi.
Hii hutupatia kauli saba tofauti. Kauli ya “lazima” (amri)
ni MOJA tu kati ya hizi KUMI NA MOJA. Kwa hiyo,
neno “amri” huhusiana na eneo ambamo kuna aina tofauti
KUMI NA MOJA za matamko, kwa hiyo linakuwa ni
tamko moja tu kati ya MATAMKO KUMI NA MOJA!
Sina haki ya kupuuzia haya kumi na moja mengine.
Ni kweli kwamba kuna “matamko ya moja kwa moja”
mengine mengi kwenye Biblia ambayo hatuyaangalii
ili kuthibitisha mamlaka ya Biblia kuhusiana na wajibu
wetu. Lakini, ukweli unabaki kwamba, kuna matamko
ya moja kwa moja yanayoweka mamlaka ya Biblia. Ni
dhahiri kwamba sijaruhusiwa kufundisha kuwa mtu
ambaye Bwana alimponya, alizaliwa na dhambi, eti kwa
sababu, Wayahudi walisema hivyo (Yohana 9:34).

- 101 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Mamlaka yanathibitiswa na_____________.

2. “Dokezo” huhusiana na nini?

3. Kila kitu ambacho Biblia inafundisha, hufundisha


ama kwa ____________ au kwa___________.

4. Tunajihusisha na kufikiri ______________ kwa


kuzingatia kile ambacho Mungu ___________ katika
kauli zake za wazi.

5. Mamlaka yaliyomo kwenye kile ambacho


KINAMAANISHWA katika kauli za Mungu za
WAZI yamejikita katika ukweli gani?

6. Jadili na fafanua tofauti kati ya “dokezo” na “makisio.”

7. Mantiki ni nini?

8. Je nimeruhusiwa kufundisha kuwa Paulo wa Taso


aliungama dhambi zake pale alipotaka kuwa Mkristo?

9. Toa hoja zilizojengwa hapa kwa kumbukumbu zako.

10. Kuungama kwa Sauli ni suala la nini?

- 102 -
11. Usemi “Kitu kizima chochote kile ni jumla ya sehemu
zake,” hutuambia kitu kingine kipi kwa KUDOKEZA?

12. TUNAJUA nini kutokana na sababu kwamba


TUNAJUA kuwa tunajishughulisha na umbo la
kijiometri, ambalo ni mraba, ambalo kila upande ni
inchi 6?

13. Mamlaka huthibitishwa na _____________.

14. Kwa muktadha huu, neno “amri” linajitosheleza


kukidhi hali yote?

15. “Amri” ni sehemu ya eneo kubwa la kujifunza


tunaloliitaji?

16. “Matamko ya moja kwa moja” yameainishwa katika


msingi gani?

17. Uainisho huu hufanywa kwa kuzingatia nini?

18. Sarufi ya Agano Jipya la Kiyunani ina hali nne. Ni


zipi hizo?

19. Maana ya msingi ya HALI ni nini?

20. Tendo lina weza kuwa _________ au ni _______.

21. Ikiwa tendo ni HALISI, hivyo hali ni nini?

- 103 -
22. Ikiwa tendo lina UWEZEKANO WA KUTOKEA,
hivyo HALI inaweza kuwa nini?

23. Kauli katika HALI YA KUARIFU inaweza


kuwa (kama ilivyo kwa asili yake) nini?

24. Kauli katika DHAMIRA TEGEMEZI inaweza


kuwa (kama ilivyo kwa asili yake) nini?

25. Kauli katika HALI YA KUAMURU inaweza


kuwa (kama ilivyo kwa asili yake) nini?

26. Kauli katika HALI YA UCHAGUZI inaweza


kuwa (kama ilivyo kwa asili yake) nini?

27. Hii inatupatia jumla ya aina ngapi za kauli?

28. Kauli ya “lazima” (amri) ni nini?

29. Kwa hiyo, neno “amri” ni kauli moja tu kati ya kauli


ngapi?

30. Tafadhali rejea tena “kauli ya moja kwa moja –


ilivyoainishwa kama HALI, na kama ASILI.”

- 104 -
SOMO LA
KUMI NA MBILI

XVIII. MAMLAKA
YA BIBLIA
YAMETHIBITISHWA
KWA KUFANYA JAMBO
LINALOFAA

12
- 105 -
K
atika kutekeleza majukumu yetu kuna eneo la
kufanya jambo linalofaa. Kila jukumu ambalo
Mungu ameshawahi kutoa, limehusisha kufanya
jambo linalofaa. Kwa kuhusianisha na majukumu ambayo
Mungu alishawahi kutoa, inawezekana kweli kabisa
(kuhusiana na kutekeleza majukumu) Mungu alisema
NAMNA ya kuyatekeleza, na hapo hapo HAKUSEMA
NAMNA ya kuyatekeleza.
Jambo linalofaa huhusisha hekima za kibinadamu. Ikiwa
Mungu anaainisha Majukumu, lakini hajatoa maelekezo
ya namna ya kuyatekeleza, basi tumeruhusiwa kuhusisha
hekima za kibinadamu. Katika majukumu ya kuongoza
washiriki, wazee wa kanisa ndio wenye mamlaka katika
eneo la kufanya jambo linalofaa.
Manufaa binafsi ni yale ambayo yanahimiza. Hakuna
manufaa binafsi pale ambapo hakuna faida. Ndivyo
ilivyo katika majukumu ya kanisa la mahali, jambo lenye
manufaa ni lile ambalo linaendana na maandiko, ambalo
lina faida ya asili, na ambalo linaweza kuchaguliwa na
wazee wa kanisa katika kutekeleza jukumu lolote lile
la kanisa – jukumu hilo ni lazima liwe limetokana na
mifano iliyothibitishwa, kwa mdokezo, au kauli ya moja
kwa moja.
Inatakiwa pia tuelewe kwamba HAKUNA MANUFAA
BINAFSI pale ambapo HAKUNA JUKUMU. Sina
nia ya kulithibitisha hili kwa hiyo kwa haraka haraka
tutaita “jambo la manufaa.” Kushindwa kutambua
na kuuheshimu ukweli huu, kulitengeneza matatizo
makubwa katika Harakati za mwanzo za Urejeshwaji.

- 106 -
Pia inatakiwa isisitizwe kuwa tunapothibitisha kwamba
kitu fulani ni cha manufaa – kulingana na fasili ya
Biblia ya manufaa – kwa hiyo tunakuwa tunathibitisha
kwamba hicho kitu kina mamlaka matakatifu, na kwa
hiyo linakuwa ni suala la imani, kama kweli ni “jambo la
manufaa,” basi linakuwa suala la imani.
Pengine umakini unapaswa uwekwe kwenye suala
la “mambo ya hiari” katika uhusiano wa “mambo ya
manufaa.” Tofauti, kama ipo, ni nini? Katika kutekeleza
majukumu tuliyopewa kuna “mambo ya hiari” na kuna
“mambo ya manufaa.” Tafakari juu ya majukumu yetu
kupata sehemu ya kukutania. Jukumu hili linafanya
SEHEMU ya kukutania kuwa LAZIMA. Sehemu
ya kukutania ni MUHIMU. Kuhusiana na sehemu
ya kukutania kunaweza kuwa na uchaguzi wa aina
nne: kununua jengo, kukodisha jengo, kujenga jengo,
kukutana nyumbani. Jambo la manufaa linaweza kuwa
ni kukodisha jengo. Katika mazingira tofauti, jambo
la manufaa linaweza kuwa ni kujenga jengo. Ni wazi
kwamba kitu hicho hicho kinaweza kuwa cha hiari na
cha manufaa kwa wakati huo huo. Sio mambo yote ya
hiari yanaweza kuwa ya manufaa, lakini mambo yote
ya manufaa ni ya hiari. Lakini katika jambo la manufaa,
kuna faida ya asili ndani yake.
Ni lazima tuoneshe tofauti kwa ufupi kati ya “jambo
la manufaa” (msaada) na “nyongeza.” Kitu chochote
ambacho hakikuruhusiwa na Maandiko, lakini
kinatumika, ni nyongeza. Msaada wa kweli, yaani jambo
la manufaa, limeruhusiwa na maandiko.

- 107 -
Mungu ametupatia jukumu la “enendeni.” Tunaweza
kwenda kwa KUTEMBEA kwa miguu, na tunaweza
KUENDESHA CHOMBO. Kutembea na kuendesha
chombo ni njia mbili tofauti za kuenenda. Njia hizi zina
uhusiano wa moja kwa moja na jukumu la “Enendeni”.
Lakini hazihusiana. Kutembea sio msaada – sio jambo
la manufaa, na kuendesha sio jambo la manufaa kwa
kutembea. Fimbo ya kutembelea, inahusiana na kutembea,
inaweza kuwa ni jambo la manufaa, ni msaada.
Ni sawa na suala la utambuzi, tunatambua kwa KUSIKIA
na tunatambua kwa KUTAZAMA. Kusikia sio jambo la
manufaa kwa kuona, na kuona sio jambo la manufaa kwa
kusikia. Hizi ni njia mbili tofauti za utambuzi. Hivi ni
“viungo.” Miwani ya macho inaweza kuwa ni jambo la
manufaa (msaada) kwa kuona, na kifaa cha kusikilizia
kinaweza kuwa jambo la manufaa (msaada) kwa kusikia.
Kwa suala la kufanya muziki – hii inaweza kufanyika
kwa kuimba; inaweza kufanyika kwa kutumia ala za
muziki. Kuimba na kupiga ala za muziki kuna uhusiano.
Iwe ni kuimba au kupiga ala za muziki, kimoja kinaweza
kufanyika bila kingine. Kuimba sio msaada kwa kupiga
ala za muziki, na kupiga ala za muziki sio msaada kwa
kuimba. Kitabu cha nyimbo ni msaada kwa kuimba.
Kuwa na mtu anayeongoza watu kuimba ni “msaada”
na jambo la manufaa. Tunapotumia kitabu cha nyimbo
katika kuimba, tunakuwa TUNAIMBA TU. HATUIMBI
NA KUFANYA KITU KINGINE TOFAUTI.
Matumizi ya jambo la manufaa ni mapana sana. Huu ndio
msingi ambapo tunalinda (1) majengo yetu ya kanisa, (2)

- 108 -
visima vyetu vya ubatizo, (3) mafundisho yetu katika
madarasa ya Biblia, (4) shule za uimbaji, (5) vitabu vyetu
vya nyimbo, (6) viongozi wetu wa nyimbo, (7) kuimba
wimbo wa kualikwa, (8) kutumia vikombe vya jumuia,
(9) vikapu vya kuekea changizo, (10) mtu kuongoza
kundi katika maombi, (11) mbao zetu za kuandikia, (12)
mfumo wa kuongea na umma (13) na kadhalika.
Wapendwa fulani wameshikilia msimamo sana
katika mtazamo wao juu ya suala la jambo linalofaa.
Wanalitambua na kuliheshimu katika baadhi ya maeneo,
lakini wanashindwa kulitambua na kuliheshimu katika
maeneo mengine. Wanajua kwamba jengo la kanisa ni
jambo la manufaa, ni jukumu walilopewa kulijenga,
lakini wanashindwa kutambua kuwa darasa la Biblia
ni jambo la manufaa, linalohusiana na jukumu la
kujifunza, kukua, kulisha kondoo na kuwatii wazee.
Wanakubali kwamba shule ya kuimba ni jambo la
manufaa, linalohusiana na jukumu la kuimba, lakini
wanashindwa kutambua kwamba darasa la Biblia ni
jambo la manufaa linalohusiana na jukumu la kufundisha.
L.W. Hayhurst alipoacha msimamo wa kupinga-Jumapili
alisema: “Nimeamua kwamba nitakapojenga jengo la
kanisa nitafanya kitu kile kile kwa kuzingatia kanuni
wanazozifuata pale wanapokuwa na darasa la Biblia.
Nitawezaje kufanya kitu kile kile wanachofanya wao,
halafu kuwahukumu kwa kile wanachofanya? ”
Ni kanuni ya msingi ya kufasili Biblia kwamba kama
na wakati ambapo Mungu ameainisha NAMNA ya
kutekeleza jukumu lolote lile, hiyo NAMNA inakuwa

- 109 -
ni ya lazima kama lilivyo jukumu lenyewe; lakini kama
na wakati Mungu HAONYESHI NAMNA, basi njia na
mbinu huachwa chini ya hekima za kibinadamu, katika
suala la kufanya jambo lenye manufaa .

CHATI
! YA MAMLAKA

&*5'! *)'5'! -.!+<B:GD:E:!


"#$%#!
&#'(&'$')&*!
+,*!!
-."'/*$0! -.!6:! 1.!+<<H>E:!
;<:=>?<!
4.!+<IGJ:!

8.!":K@:=B>!
1.+#(0+23*!
1.!(@:A>=:!
BCDCACE>! L.!+:B:EI!

M.!"N>K@I!
4.!+*#5'!6*!
"07*!+,*!
4.!6:! O.!6:!+<?:GJ:!K@:<=>!
"07*! ;<:A<=<! P.!+:B:EI!

Q.!5:E>A:!
8.!6:!
8.!7*"90!5*! -R.!5:E>A:S>G:JI=<@<K<!
"*$#/**!! <F@:D<E>!
--.!":B:A:G>I!
!

- 110 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Mamlaka ya Biblia yanathibitishwa na nini?

2. Kwa kuhusianisha kila jukumu ambalo Mungu


alishawahi kutoa kwa mwanadamu, kuna eneo la ____.

3. “ Jambo la Manufaa ” linahusisha nini cha lazima?

4. Kuhusiana na jukumu la washiriki, ni nani ambaye


anafanyaka kazi katika eneo la jambo la manufaa –
mwenye mamlaka ya kufanya na kutekeleza maamuzi?

5. “Jambo la Manufaa ” ni yale ambayo _________.


Hakuna “ jambo la manufaa ” pale pasipo na ________.

6. Jifunze kwa makini fasili ya “ jambo la manufaa ”


(kwa kuhusianisha na kanisa la mahali pamoja).

7. Inatakiwa tuzingatie hoja gani muhimu (kuhusiana na


jambo la manufaa)?

- 111 -
8. Tunapothibitisha kwamba kitu fulani kweli ni
cha “manufaa” kwa wakati huo huo tunakuwa
tunathibitisha nini?

9. Je kuna tofauti kati ya “mambo ya hiari” na “mambo


ya manufaa?”

10. Tafadhali fafanua, “Sio mambo yote ya hiari ni ya


manufaa, lakini mambo yote ya manufaa ni ya hiari.”

11. Lakini katika mambo ya manufaa kuna kitu gani cha


asili?

12. Msaada wa kweli (jambo la manufaa) _________ na


Maandiko.

13. Kitu chochote ambacho HAKIJAIDHINISHWA na


Maandiko, lakini ambacho kinatumika, ni nini?

14. Jadili: kwenda, kutembea, kuendesha, na fimbo ya


kutembelea.

- 112 -
15. Jadili: utambuzi, kusikia, kutazama, miwani ya
macho, na vifaa vya kusikilizia.

16. “Kutengeneza muziki” kunaweza kufanywa kwa


kutumia nini?

17. Kuimba na kupiga ala za muziki ni njia mbili tofauti


za kufanya nini?

18. Kuimba sio ___________ kwa kupiga vyombo


vya muziki, na kupiga vyombo vya muziki sio
____________ kwa kuimba.

19. Kitabu cha nyimbo (kinapotumika katika ibada yetu)


ni nini?

20. Kwa kiwango ambacho Mungu anaainisha NAMNA


ya kufanya jambo, hali inakuwaje?

21. Ikiwa Mungu anatoa jukumu lakini HAAINISHI


NAMNA ya kuyafanya, hali inakuwaje?

- 113 -
SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 114 -
SOMO LA
KUMI NA TATU

XIX. JE MAMLAKA
INAAMULIWA NA
KAMUSI?

13
- 115 -
SWALI
“Mamlaka ya Biblia inaweza kuamuliwa kwa kutumia
kamusi? Ninaambatisha makala kwa ajili ya jarida,
nikiomba kwamba uipitie, kama inawezekana, na iwe
mapema kadri iwezekanavyo.”

JIBU
Mbele yangu nina makala ya jarida la Kanisa, nikiombwa
kwamba niweze kuipitia. Kwa kutambua (1) umuhimu
wa mada ambayo makala inaishughulikia, na (2) hatari
iliyopo katika mtazamo ulioonyeshwa na mapendekezo
yaliyofanywa, ninaendelea kuvuta umakini kwenye
makala hii. Nitanukuu kila aya ya makala, na nitatoa
maoni muafaka.

AYA YA KWANZA
Inaonekana siku hizi kuna maandishi mengi sana
kuhusiana na suala la Mamlaka ya Biblia kwa ajili ya
desturi ndani ya kanisa. Kwa kuwa ni vizuri kwamba
wengi wanapenda kufanya yale ambayo ni sahihi
machoni pa Mungu, suala la “mamlaka” siku zote huwa
haliko wazi sana.
1. Ndio mengi yameandikwa kuhusiana na mamlaka
ya Biblia. Kuna wapendwa wengi wenye uwezo,
waaminifu, wanaojituma, waliojitolea ambao
wamedhamiria kushikilia “mstari wa ukweli” na
kupinga makosa yote. Hawa wanaonesha na kusisitiza
kile ambacho Biblia inasema kuhusiana na mamlaka
ya Biblia (na kuhusiana na mada yoyote ile ya Biblia).
Kwa upande mwingine kuna wengine wanaoandika

- 116 -
kutokana na mtazamo kwamba “Wala haijalishi…
sio ya muhimu sana hata hivyo.” Baadhi (kimsingi
ni wengi) wanasisitiza dhana kwamba sio lazima
kuwa na mamlaka ya Biblia kwa kile tunachofanya na
tunachosema katika suala la kidini.Baadhi wanajaribu
hata “kuthibitisha” kwa kutumia Maaandiko kwamba
Mungu wala hahitaji tuwe na mamlaka ya Biblia kwa
kila kitu. Na wengine wanasema kwamba mamlaka
ya Biblia inaweza kuthibitishwa kwa misingi kwamba
“Biblia haisemi kitu chochote”! Angalia kwa makini
hoja ya ajabu na inayojipinga yenyewe kwamba Biblia
inatoa mamlaka kwa kutokuwepo kwa mamlaka ya
Biblia!
2. Sio tu ni “vizuri” kwa sisi kufanya yale yanayopendeza
machoni pa Mungu; ni LAZIMA KABISA kama
tunataka kumpendeza Mungu katika maisha haya, na
kuishi pamoja naye milele, pale ambapo maisha haya

kama jambo halijaruhusiwa na neno la Mungu, basi


halitampendeza Mungu (Waebrania 11:6).
3. Mtunzi wa makala anasema: “…suala la ‘mamlaka’
siku zote huwa haliko wazi sana”. Hili sikubaliani
nalo kabisa. Ikiwa suala la mamlaka ya Biblia haliko
wazi, basi hakuna kitu kwenye Biblia ambacho kipo
wazi. Siku moja, nilipokuwa nikimfanyia usaili
mtu mmoja kwa ajili ya kuajiriwa katika chuo cha
Kikristo, nilimuuliza swali kuhusiana na matumizi ya
ala za muziki katika ibada ya Kikristo: “Uko tayari
kutambua na kukubali kwamba hakuna mamlaka

- 117 -
ya Biblia kwa ajili ya hilo?” Akajibu: “Ndugu
Deaver, sina uhakika na jinsi ambavyo Mungu
anatoa Mamlaka.” Jibu langu kwake: “Kama ndio
hivyo kwa kweli hatuwezi tukakuajiri, kwa sababu
kutokana na hivyo, huwezi kuwa na uhakika na
KITU CHOCHOTE!”. Kama “suala la mamlaka”
haliko wazi akilini mwa mwandishi wa makala haya,
basi hana uhakika kabisa kuhusiana na (1) namna
ambavyo mtu anakuwa Mkristo, (2) namna ambavyo
mtu humwabudu Mungu kwa kukubaliwa, au (3)
majukumu yetu, wajibu wetu na matumaini yetu
kama Wakristo. Katika mazingira haya anaiweka roho
yake hatarini, na pia anaweka hatarini roho za wale
wanaosikiliza kile anachofundisha. Mwanafunzi wa
Biblia haachi kujifunza hadi pale atakapoelewa namna
ambavyo Mungu hutoa mamlaka. Na pale ambapo hili
limewekwa sawa kulingana na Maandiko, linakuwa
limewekwa sawa daima – kama ilivyo katika Marko
16:16.
4. Tunasisitiza tena kwamba kanuni ya msingi ya
Biblia ni rahisi, na iko wazi kwa mtu yeyote na watu
wote wanaotamani kwa dhati kufahamu suala hili.
Wakolosai 3:17 inaunganisha: “Na kila mfanyalo,
kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la
Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.”
“Katika jina la Bwana” humaanisha “kwa mamlaka
ya Bwana” (yaani, kama Mungu alivyotoa mamlaka
[Matendo 4:7-10]). Tumepewa jukumu (na fursa) la
“kutembea kwa imani” (2 Wakorintho 5:7). Kipimo
kitakatifu cha kiroho ambacho kinamwongoza Mkristo

- 118 -
(na ambacho kwacho watu wote wanaojali majukumu
wanatiishwa) ni kipimo cha imani. Paulo anasema:
“Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja
kwa neno la Kristo ” (Warumi 10:17). Ikiwa imani
huja kwa kusikia neno la Mungu, ni wazi kwamba
pale ambapo hakuna neno la Mungu basi, HAPAWEZI
KUWA NA IMANI! Na, kumbukumbu zinaonyesha
kwamba bila imani haiwezekani kumpendeza
Mungu (Waebrania 11:6). Kuna maandiko mengi
yanayofafanua kwamba MUNGU HAVUMILII
MATENDO AMBAYO HAYAJARUHUSIWA AU
MAFUNDISHO AMBAYO HAYAJARUHUSIWA.
5. Ni dhahiri kwamba hatuna muda au nafasi ya kujadili
kwa kina suala la NAMNA MUNGU ANAVYOTOA
MAMLAKA, lakini sisi sote tunaweza kujikumbusha
mstari. (1) Mamlaka ya Biblia yanathibitishwa kwa
“mfano.” Tunatakiwa tujifunze kwa makini (na
kujifunza kujibu) swali muhimu: Ni wakati gani
ambapo tendo huhusisha mfano? (2) Mamlaka ya
Biblia yanathibitishwa kwa kudokeza. Hii inahusisha
kufikiri kwetu kwa usahihi, kwa kile Mungu
alichomaanisha kwa kauli yake ya wazi. (3) Mamlaka
ya Biblia yanathibitishwa kwa kauli ya moja kwa
moja. Nimeruhusiwa kufundisha kuwa mtu anatakiwa
abatizwe ili aweze kuokolewa, kutokana na tamko la
moja kwa moja katika Marko 16:16. (4) Mungu hutoa
mamlaka kwa “ kufanya jambo la manufaa .” Kila
jukumu ambalo Mungu alishawahi kutoa huhusisha
eneo la manufaa binafsi. Lakini ikiwa “jambo la

- 119 -
manufaa” (kulingana na fasili ya kimaandiko ya
“jambo lenye manufaa”), basi limeruhusiwa na
linatokana na suala la imani.
Narudia kusisitiza kwamba huu ni uainisho tu.
Sikusema kwamba suala la Mamlaka ya Biblia ni
“rahisi.” Ninacho sisitiza ni kwamba suala lenyewe
lipo wazi katika Maandiko bila mjadala wowote.

AYA YA PILI
Neno “mamlaka” linapochunguzwa, kuna baadhi ya
mambo ya kuvutia yanayoibuka kama vile; maoni,
nguvu, kauli la kuhitimisha, maamuzi yaliyochukuliwa
kama matokeo, ushuhuda, na ushawishi (Webster – Toleo
la 7 la Wanafunzi).
1. Hili tamko (na utaratibu huu) umenishitua kwa kweli!
Mwandishi wa makala hii anaona suala la Mamlaka ya
Biblia “haliko wazi siku zote.” Sasa atawezaje kujaribu
kufanya suala hili kuwa “wazi kabisa”? Anatafuta
maana kwenye kamusi ya Kiingereza! Utataka kujua
iwapo “kunyunyiziwa maji” ni “ubatizo.” Utafanya
nini? Utatafuta kwenye kamusi! Unataka kujua iwapo
“Jumapili” ni “Sabato” au la. Utafanya nini? Utatafuta
kweye kamusi! Mtu yeyote duniani anayejua kitu
chochote kuhusiana na Kutambua Mamlaka ya Biblia,
na ambaye anajua asili na makusudi ya kamusi,
anajua kwamba huu sio utaratibu sahihi. Muundo na
makusudi ya kamusi ni kuniambia jinsi ambavyo neno
limekua likitumiwa wakati ambapo kamusi ilikuwa
ikiandaliwa. Na kusudi hili linaweza kuwa msaada

- 120 -
mkubwa sana katika kujifunza kwangu Biblia. Lakini,
ukweli unabaki kwamba matumizi ya sasa ya neno
hili (au hata historia ya matumizi yake) hakuhakikishi
kwamba hivi ndivyo hili neno linatumika kwenye
Biblia. Sio sahihi kwa taratibu za kimaandiko, kujaribu
kutafuta maana yake kwenye kamusi. Kimsingi, kwa
kuzingatia uzito wenyewe wa mada inayojadiliwa,
kuangalia maana kwenye kamusi, kunaonesha jinsi
gani mwandishi wa makala haya alivyolichukulia
suala hili kirahisi. Ni mwangalifu katika kuchagua
maneno fulani anayokubaliana nayo, lakini hatuambii
kamusi inasema nini. Anaonekana kuyaonesha
maneno hayo kama “maoni,” “nguvu,” “kauli zenye
kuhitimisha,” “maamuzi yaliyochukuliwa kama
matokeo,” “ushuhuda,” na “ushawishi wa Kibiblia”
yanaweza kuwa sawa katika maana na “mamlaka ya
Biblia.” Hebu piga picha: majukumu yaliyotolewa na
Mungu yapewe mamlaka na “maoni ya Biblia?” au na
“ushawishi wa Biblia?”

AYA YA TATU
Endapo tutatumia hayo maneno hapo juu na
kuyahusianisha na Biblia, tunapata virai kama, Maoni
ya Kibiblia, tamko la hitimisho la Kibiblia, maamuzi
ya Kibiblia, ushuhuda wa Kibiblia, na ushawishi wa
Kibiblia.
1. Ndio, inaweza kuwa rahisi kufuata kamusi na kuja
na maneno haya. Lakini kwa namna gani katika
Dunia ya Mungu inaweza kuthibitishwa kwamba
haya maneno (Maoni ya Kibiblia, tamko la hitimisho

- 121 -
la Kibiblia, maamuzi ya Kibiblia, ushuhuda wa
Kibiblia, na ushawishi wa Kibiblia.) yana maana
zaidi (yako wazi) zaidi ya neno “mamlaka ya Biblia?”
Ninafahamu maana ya swali hili “Je Biblia inaipatia
mamlaka?” lakini maneno “maoni ya Kibiblia,”
“tamko la hitimisho la Kibiblia,” kiasi fulani hayatoi
maana halisi. Ni kwa jinsi gani desturi na tamaduni
zipewe mamlaka na “maoni ya Kibiblia?” Ni kwa
jinsi gani desturi na tamaduni zipewe mamlaka na
“ushawishi wa Kibiblia?”
2. Mara ya kwanza nilipoona makala hii niliyoipitia,
niligundua papo hapo kwamba ni Mradi wa Tulsa na
fikra za Walegezaji. Mpaka sasa bado nafikiri hivyo.
Mtu yuko tayari kuweka dhana kuwa kuna viwango
tofauti vya mamlaka ya Biblia – kama “U” kubwa (U)
shirika na “u” ndogo (u)shirika. Tutarajie kuona kitu
kuhusu (1) mamlaka kwa misingi ya maoni ya Biblia
(2) mamlaka kwa misingi ya tamko la hitimisho la
Kibiblia, (3) mamlaka kwa misingi ya maamuzi ya
Kibiblia, (4) mamlaka kutokana misingi ya ushuhuda
wa Kibiblia, (5) mamlaka kwa misingi ya ushawishi
wa Kibiblia. Kutakuwa na viwango tofauti vya
umuhimu kuhusiana na mada hii inayojadiliwa,
lakini kunaweza kusiwe na SABABU ambayo
itasababisha KUMFUKUZA MTU USHIRIKA!
Lakini, ukweli wenye nguvu na wa wazi usioweza
kubadilika ni ama kitu kimepewa mamlaka na
Biblia au hakikupewa mamlaka na Biblia, na kama
hakikuidhinishwa na Biblia halafu tunakifundisha,
tunakuwa TUNAFANYA DHAMBI.

- 122 -
AYA YA NNE
Kwa upande wangu, hivi virai ni rahisi sana kuvifanyia
kazi kuliko “Mamlaka ya Biblia” kwa sababu vinaeleweka
kwa wazi. Sasa ninapokuwa ninauliza juu ya desturi,
ninaweza kuuliza, “Je hayo ni maoni ya Kibiblia?” au
“Kuna ushawishi wa Kibiblia kwa ajili ya hiyo desturi?”
au “Kuna tamko la hitimisho la Kibiblia?” au “Kuna
ushuhuda wa Kibiblia?” au “Maoni ya Biblia ni nini?”
1. Mimi naona utaratibu wa hapo juu ni hatari sana, upo
nje kabisa ya hoja, na haukamilishi kitu chochote kile.
“Maamuzi ya Kibiblia humaanisha nini?” Mwandishi
anatumia maneno haya kumaanisha “Mamlaka
ya Biblia.” Kwa hiyo, bado ana tatizo la “Ni kwa
namna gani Biblia hutoa mamlaka?” Ni kwa namna
gani Biblia inaweka “Maamuzi ya Kibiblia?” Kama
anajaribu kutafuta kujua “Maoni ya Biblia” ili aweze
kujua mamlaka, bado anatakiwa kushughulika na
suala la “Ni kwa jinsi gani Biblia hutoa mamlaka?”
Badala ya kufafanua, ukungu unakuwa mwingi kiasi
kwamba mwandishi hawezi kuona swali halisi!
2. Kwa nini asiulize tu, “Je Biblia imeidhinisha?”
Au, tunaweza kufundisha hili “katika jina la
Bwana?” Je, Bwana kupitia neno lake
anaidhinisha hii desturi au hili fundisho? Halafu,
anaweza kwenda kwa umahususi zaidi na
kuuliza: (1) Je, hili limeidhinishwa kwa mifano
iliyothibitishwa? (2) je, hili limeidhinishwa kwa
“mdokezo?” (3) je, limeidhinishwa kwa “kauli
ya moja kwa moja?” (4) je, limeruhusiwa kama

- 123 -
“jambo lenye manufaa?” Ikiwa jibu la maswali haya
ni hapana, basi HALIJAIDHINISHWA NA BIBLIA.
3. Ningependa kukoleza wino kwenye kile ambacho
mwandishi anaweza kuwa nacho akilini,
anapotafakari dhana kwamba KITU FULANI
kinaweza kuidhinishwa kwa misingi ya “ushawishi
wa Kibiblia” au “Maoni ya Biblia.”

AYA YA TANO
Vipengele hivi mbalimbali vinafanya iwe rahisi kutafuta
majibu ya maswali yangu. Kwa nini? Kwa sababu
kunavunja hisia zangu binafsi juu ya neno “mamlaka.”
Fasili ya mamlaka ni pana sana kiasi kwamba inaacha
maeneo mengi sana ili akili yangu ijaze “nafasi
zilizoachwa wazi” kadri inavyokidhi matakwa yangu.
1. Kwa miaka mingi nimekuwa nikipata fursa ya
kufundisha (sehemu ya kozi katika Mantiki) “Falsafa
ya Lugha.” Sehemu muhimu kabisa katika kozi
hii ni kipengele ambacho tunashughulika nacho
“utata.” Tunasoma “utata” sio kwa kujifunza jinsi ya
kuutengeneza, bali ni kuugundua na kutambua aina ya
utata uliopo kwenye maandishi, hii yote ni kwa sababu

kwamba utata ni ushahidi wa kuelewa sana, lakini hiyo


sio sababu kabisa. Ni jukumu la msemaji (sawa na
jukumu la mwandishi) kujitahidi ili aeleweke.
2. Aya hiyo hapo juu ni kielelezo kikubwa sana cha utata.
Ni dhahiri kwamba mwandishi anajaribu kusema
kitu fulani bila kukisema. “Muda mwingine kusema

- 124 -
waziwazi ndio kueleweka.” Anamaanisha nini
kusema hisia zangu binafsi juu ya neno “mamlaka.”
Je, hii ndio hisia binafsi? Au ni kinyume chake? Je
ni majivuno kutumia hata neno “mamlaka?” Ina
maana gani kusema “fasili ya mamlaka ni pana
sana…?” Je hivi ni vizuri? au vibaya? Nilidhani
mwandishi ameshasistiza kwamba kwa “kusoma”
amekuja na “fasili” ambayo anaikubali, na kwa hiyo
angeanza kushughulika na fasili mpya. Anamaanisha
nini anaposema “…inaacha maeneo mengi sana ili
akili yangu ijaze “nafasi zilizoachwa wazi” kadri
inavyokidhi matakwa yangu?” Kwa hili kunakuwa na

3. Zingatia kwa makini anaposema “makundi vya


mamlaka.” Hili linathibitisha kile nilichokisema hapo
awali kwamba “Mtu tayari amejenga dhana kuna
viwango tofauti vya mamlaka ya Biblia.” Mamlaka
ya Biblia ni Mamlaka ya Biblia- rahisi, wazi,
imajitosheleza na inaleta maana. Hakuna “vipengele”
vya mamlaka ya Biblia (kama ambavyo mwandishi
wa makala haya anavyotumia hili neno). Hakuna
viwango mbalimbali vya mamlaka ya Biblia.

AYA YA SITA
Kwa kulizingatia hili, sasa ninaamini kwamba nina
nyenzo bora ya kuchunguza maandiko kwa ajili ya
maelekezo ya Mungu kwa ajili ya matendo yangu na
imani. Mungu atubariki sote kadri tunavyojitahidi
kufanya mapenzi yake siku zote.

- 125 -
1. Aya hii inaonyesha hamasa nzuri kwa ajili ya kusoma,
kujifunza, na kulielewa neno la Mungu. Angalau
inaonyesha umuhimu wa kusoma na kujifunza neno la
Mungu. Ninaamini na ninaomba kwa bidii ili kwamba
mwandishi kwa uaminifu kabisa, atake kufanye kile
ambacho ni sahihi, kwamba atake kufanya kile tu
ambacho kina mamlaka ya Biblia.
2. Ngoja nisistize tu ninapomalizia haya maandishi
kwamba simfahamu mwandishi wa makala hii. Wala
jina lake halikuoneshwa. Kwa hiyo ni dhahiri kwamba,
maoni haya sio jitihada zangu binafsi kutoa hukumu au
hata kuhoji nia ya mtu husika ninayemfahamu. Mimi
najishughulisha na makala yenyewe, na ushawishi
inayowezakuwa nayo kwenye eneo inamotoka. Ni
makala ya hatari sana. Pia, ninashawishika kuhusika
na mtua aliyeandika makala hii, na ningependa
kumsaidia kwa namna yoyote ile ambayo ningeweza.
Ndugu, Mungu atusaidie kila mtu ili kutambua
umuhimu wa mamlaka ya Biblia – kuelewa kwamba
kila kitu tunachofanya ni lazima kifanyike “katika
jina la Bwana.” Hebu tujitafakari upya kuweka
msisitizo katika suala la namna ambavyo Biblia
inatoa mamlaka.
Ni lazima TUFIKIRI kama washauri wa Mungu (hii
ni kama ambavyo Biblia inatufundisha kufikiri). Ni
lazima TUZUNGUMZE kama washauri wa Mungu
(zungumza kulingana na mafundisho ya Biblia).
Ni lazima TUABUDU kama ambavyo Biblia
inatufundisha kuabudu. Ni lazima TUTENDE na

- 126 -
TUISHI kama ambavyo Biblia inatufundisha jinsi
ya kutenda na kuishi. Na hivi vitu vinaamuliwa kwa
kusoma Biblia ( zaidi hasa Agano Jipya) kwa juhudi,
kwa umakini na kwa maombi. Na masuala haya
yanaamuliwa na kile ambacho BIBLIA inasema na
sio kile ambacho KAMUSI inasema.

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 127 -
MASWALI YA KUJIFUNZA

1. Swali la msingi katika somo hili ni nini?

2. Mwandishi wa “aya ya kwanza” ana mtazamo gani


kuhusu Mamlaka ya Biblia?

3. Ndugu wengi wamedhamiria kufanya nini?

4. Kwenye #1 tumetaja maoni yenye makosa juu ya


mamlaka ya Biblia. Maoni haya ni yapi?

5. Ni lazima tusisitize ukweli gani wa msingi?

6. Mtu ambaye “suala la mamlaka” haliko wazi,


hawezi kuwa na uhakika kabisa kuhusiana na
______________, namna ambavyo ____________
Mungu kwa kukubaliwa,; au majukumu yetu, wajibu
wetu na matumaini yetu kama ________.

7. Tutatakiwa tujifunze na kufahamu suala gani la msingi?

8. Umuhimu wa Wakolosai 3:17 ni nini?

9. Tunajifunza nini kutokana na Matendo 4:7-10 (kama


inavyohusiana na somo hili)?

10. Tunajifunza nini kutoka 2 Wakorintho 5:7?

- 128 -
11. Tunajifunza nini kutoka Warumi 10:17?

12. Tunajifunza nini kutoka Waebrania 11:6?

13. Mungu havumilii nini?

14. Orodhesha hoja nne zilizoorodheshwa kwenye


“orodha za msingi” za mamlaka ya Biblia.

15. Mwandishi wa makala anajaribu kujifunza maana ya


mamlaka ya Biblia kwa kwenda kwenye chanzo kipi?

16. Muundo na makusudi ya kamusi ni nini?

17. Inawezekana kweli desturi zetu na mitazamo yetu


imeidhinishwa na “maoni ya Kibiblia?”

18. Tulisema kwamba mtu tayari amekwisha jenga dhana


gani kuhusiana na mamlaka ya Kibiblia?

19. Ukweli wa wazi na wenye nguvu ni nini?

20. Mwishowe ni swali gani rahisi linaloweza kuulizwa?

21. Msemaji (au mwandishi) ana majukumu gani?

22. Mwandishi wa makala, hususa ni katika aya ya tano,


anatupatia kielelezo gani chenye nguvu?

23. Inatakiwa tujitathmini upya kufanya nini?

- 129 -
KIAMBATISHO A
WANAWAKE WAKRISTO NA
POCHI NYEKUNDU
(Kutoka Wakorintho 11:2-16)
Katika mafungu haya, Paulo –
I. Anawasifia ndugu wa Korintho kwa uaminifu wao
kwa mambo aliyowafundisha (“Ninawasifu kwa
kuwa mnanikumbuka katika kila jambo na kwa
kushika mafundisho niliyowapa”). Mstari wa 2;
II. Anasisitiza juu ya uongozi ulioanzishwa na Mungu
(“Lakini napenda mfahamu kwamba kichwa cha kila
mwanaume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni
mwanaume, nacho kichwa cha Kristo ni Mungu”).
Mstari wa 3;
III. Anaonesha madhara ambayo mwanaume atayapata,
ikiwa ataomba au kutoa unabii mbele za watu, huku
kichwa kikiwa kimefunikwa (“Kila mwanaume
anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa
chake, anakiaibisha kichwa chake”). Mstari wa 4;
IV. Anaonesha madhara ambayo mwanamke atayapata,
ikiwa ataomba au kutoa unabii mbele za watu,
huku kichwa kikiwa hakijafunikwa (“Lakini kila
mwanamke anayeomba au kutoa unabii pasipo

- 130 -
kufunika kichwa chake, anakiaibisha kichwa chake,
kwani ni sawa na yeye aliyenyoa nywele”). mstari 5;
V. Anatoa maelekezo yenye msisitizo kwamba
mwanamke anatakiwa kufunika kichwa chake
(“Kama mwanamke hatajifunika kichwa chake, basi
inampasa kunyoa nywele zake. Lakini kama ni aibu
kwa mwanamke kunyoa nywele zake, basi afunike
kichwa chake”), mstari wa 6;
VI. Anafafanua kwa nini mwanaume anatakiwa
kutofunika kichwa chake na mwanamke kufunika
kichwa chake (“Mwanaume haimpasi kufunika
kichwa chake kwa kuwa yeye ni mfano wa Mungu na
utukufu wa Mungu, lakini mwanamke ni utukufu wa
mwanaume”), mstari wa 7
VII. Anafafanua kwa kina kwa nini mwanamke ana
jukumu la kuonesha utukufu wa mwanaume (“Kwa
maana mwanaume hakutoka katika mwanamke, bali
mwanamke alitoka kwa mwanaume. Wala mwanaume
hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke
kwa ajili ya mwanaume. Kwa sababu hii na kwa
sababu ya malaika, mwanamke inampasa awe na
ishara ya mamlaka iliyo juu yake”), mstari wa 8-10;
VIII. Anafafanua kwamba katika uhusiano wao na
Bwana, katika ushirika wao na yeye, mwanaume
na mwanamke wanafanana kabisa (“Lakini katika
Bwana, mwanamke hajitegemei pasipo mwanaume
na mwanaume hajitegemei pasipo mwanamke.
Kama vile mwanamke alivyoumbwa kutoka kwa
mwanaume, vivyo hivyo mwanaume huzaliwa na

- 131 -
mwanamke. Lakini vitu vyote vyatoka kwa Mungu”),
mstari wa 11, 12;
IX. Huingia akilini mwao kama jambo zuri kuthibitisha
maelekezo waliyopewa (“Hukumuni ninyi wenyewe:
Je, inafaa kwa mwanamke kumwomba Mungu
bila kufunika kichwa chake? Je, maumbile ya asili
hayatufundishi kuwa ni aibu kwa mwanaume kuwa
na nywele ndefu? Lakini mwanamke akiwa na nywele
ndefu ni utukufu kwake. Kwa maana mwanamke
amepewa nywele ndefu ili kumfunika”), mstari wa
13-15;
X. Anasisitiza kuwa licha ya ukinzani wa mtu yeyote
yule kwenda kinyume chake, desturi za wanawake
kutofunika vichwa vyao, haziruhusiwi (“Lakini
mtu ye yote akitaka kuleta fitina, sisi hatuna desturi
kama hiyo, wala makanisa ya Mungu") mstari wa 16.

Hali ya Korintho ilikuwaje?


1. KUFUNDISHA. Kufundisha katika mikutano ya
kawaida ya ibada ni aina ya kufundisha ambayo
inahusisha mamlaka, ikiwa ni pamoja na mamlaka
kuhusu wanaume (Tito 2:15). Kuna aina ya
kufundisha ambayo mwanamke Mkristo ameamriwa
kufanya (Tito 2:3,4) na kuna aina ya kufundisha
ambayo amekatazwa kufanya (1 Tim. 1:12). Aina
ya kufundisha ambayo amekatazwa kufanya ni
ile ambayo inahusisha kutekeleza mamlaka juu
ya wanaume. Mamlaka au utawala huo unaweza

- 132 -
kuhusika katika kuhutubia watu katika mkutano wa
kawaida wa ibada. Kwa hiyo kakatazwa kufanya aina
hii ya kufundisha.
2. KUOMBA. Kuna aina ya kuomba ambayo mwanamke
mkristo ameruhusiwa kufanya (1 Wathes. 5:17).
Kuna aina ya kuomba ambayo mwanamke Mkristo
amekatazwa kufanya (1 Tim. 2:8). Aina ya kuomba
ambayo amekatazwa kufanya ni kule ambako
kungeweza kuhusisha kuwa na mamlaka juu ya
mwanaume. Kuomba au (kuongoza maombi) katika
mikutano ya kawaida ya ibada kungeweza kuhusisha
mamlaka juu ya wanaume. Aina hii ya kuomba
mwanamke Mkristo amekatazwa kufanya.
3. KUTOA UNABII. “Unabii” ni karama ya roho
kabisa (1 Kor. 12:1, 10). Hakuna unabii bila ufunuo
wa moja kwa moja kutoka kwa Mungu (1 Kor.
14:30). “Unabii” ulikuwa ni kipawa cha ajabu
ambacho kwacho Mungu alidhihirisha matakwa
yake. Huhusisha mamlaka takatifu katika kila neno
kwenye Agano Jipya. Kwa kuwa “kutoa unabii” na
“kuomba” huhusiana kwa karibu katika 1 Kor. 11:4, 5
na kwa kuwa unabii ni karama ya roho, inawezekana
kuwa “kuomba” kunakozungumziwa hapa kulikuwa
kunahusisha karama za roho za miujiza. Maombi
halisi ya Wakristo wa awali yalikuwa ni kama zao la
karama za roho. Kimsingi, karama za miujiza za roho
pengine zilikuwa zinahusika katika kila hatua ya kazi
ya Kikristo na ibada (Rum. 12:6-8)

- 133 -
4. MIKUSANYIKO MAALUMU. Mistari ya (4,5)
inaonyesha waziwazi kwamba baadhi ya wanawake
kanisani huko Korintho walikuwa katika nafasi ya
kufanyia kazi karama ya maombi na unabii. Lakini
“unabii” ulikuwa ni karama ya roho kutoka kwa Mungu
kwa ajili ya kuliadilisha kanisa (1 Kor. 14:4,22).
Lakini mwanamke mkristo asingeweza kufanyia kazi
karama yake ya maombi na unabii katika kusanyiko
la kawaida la ibada, kwa kufanya hivyo wangekuwa
wanachukua mamlaka ambayo walikatazwa kufanya.
Kwa hiyo kulilazimika kuwepo kusanyiko lingine
ambalo wangeweza kutumia karama zao – mikutano
ya wanawake wakristo (pengine na watoto). Hawa
wanawake wakristo wangeweza kujengwa kimaadili,
na kwa hiyo wangechangia kujenga maadili ya kanisa
zima.
5. TATIZO. Kule Korintho kulikuwa na tatizo gani
(kwa kuzingatia mistari inayojadiliwa)? Baadhi
ya wanawake Wakristo waliokuwa na karama ya
kuomba na unabii walikuwa wanaonekana katika
mikutano hii maalumu (ya wanawake na watoto)
bila kufunika vichwa. Huu ungekuwa sio mfano
mzuri: Huu usingekuwa ushawishi mzuri kwa
wanawake wengine. Hawakuwa wamenyoa nywele
zao; waliacha tu kufunika nywele zao. Kwa kuwa
wanaume wasingeweza kuonekana kwenye mikutano
hii, pengine kulichangia kutofunika nywele zao. Kwa
kutazama hali nzima ilivyokuwa Korintho, na kwa
kuangalia umuhimu wa kufunika nywele, ingekuwa
ni vigumu kukubali mtazamo kwamba wanawake

- 134 -
Wakristo wa Korintho wangeweza hata kufikiri
kuacha kufunika vichwa vyao kwenye mikutano
ambayo wanaume wangekuwapo. Katika Saiklopidia
ya Biblia ya Toleo la Kimataifa(uk.3043) kuna maoni
ya kuvutia. “Katika nyakati za ‘Agano Jipya zamani,
miongoni mwa Wayunani na Warumi, wanawake
wenye heshima walivaa kwa kufunika vichwa mbele
ya umma, na kuonekana mbele za watu bila kufunika
kichwa lilikuwa ni kosa kubwa; Taso, mji wa nyumbani
wa Mtume Paulo, ni mji ambao ulikuwa una sheria
kali kuhusiana na suala hili. Kwa hiyo maelekezo ya
Mtume. Paulo katika 1 kor. 11:2-16, msingi wake ni
utaratibu wa kijamii wa wakati huo.”

Maelekezo ya Paulo yalikuwa ni nini?


Paulo alikuwa anasisitiza kwamba mwanamke Mkristo
wa Korintho, hakutakiwa kuonekana mitaani au katika
mikusanyiko maalumu bila kufunika kichwa. Kufunika
kichwa kwa WAKATI HUO na katika ENEO HILO –
Ilikuwa ni DESTURI ambayo ilikuwa ni nzuri tu. Kukiuka
desturi hii kule Korintho ingeleta madhara makubwa.
Paulo anasisitiza kwamba wanawake Wakristo wa
Korintho, hawakutakiwa kuonekana bila kufunika
vichwa vyao. Alitoa hoja tano:
1. Huko kungeonyesha kushindwa kutambua na
kuheshimu ukuu -- uongozi wa mwanaume;
2. Huko kungekuwa ni kushindwa kutambua na
kuheshimu ukweli halisi wa uumbaji – ukweli
unaoonesha usaidizi wa mwanamke;

- 135 -
3. Huko kungekuwa ni kushindwa kuonesha heshima
inayostahili kwa malaika, waliopo katika kusanyiko
la ibada ya Kikristo.
4. Huko kungekuwa ni kushindwa kutambua wa maadili
yao;
5. Huko kungekuwa ni kinyume na desturi za kanisa na
mafundisho mahususi ya Paulo.

Vipi kuhusu kufunika kichwa huko Korintho?


Haya ndiyo makusudi matatu ya msingi ya kuvaa nguo:
kujisitiri, kuwa huru, mapambo. Mtu mwenye “akili
timamu” huvaa kwa staha (Marko 5:15). Mkisto hataweza
kuvaa kwa makusudi, mtindo ambao utachochea tamaa
kwa watu wengine. Mwanamke Mkristo atavaa kwa
namna ambayo atajilinda dhidi ya macho ya tamaa ya
wanaume wenye dhambi. Mkristo hatavaa kwa mtindo
ambao utaleta fedheha katika kanisa la Bwana, tunavaa ili
tuweze kupata joto au ubaridi, kulinda miili yetu. Kuvaa
kusiwe kwa mapambo sana. Mkristo ataepuka mapambo
kupita kiasi.
Mara nyingi nguo huhusisha suala la ishara. Kitu fulani
huvaliwa kama ishara – kuvuta umakini juu ya tukio
fulani, kwa kumbukumbu ya mtu fulani au tukio, kutoa
taarifa, kuonesha mtazamo fulani.
Pengine sababu hizi zote zilihusishwa kwa wanawake wa
Korintho kufunika vichwa katika nyakati za Paulo.
Korintho ulikuwa ni mji wa anasa. Ulikuwa ni mji
unaoharibu maadili. Katika mji huu kulikuwa kuna hekalu

- 136 -
la Aphrodite Pandemos ambalo lilikuwa na wahudumu
wa kike elfu moja waliojitoa katika huduma zake.
Hawa hawakuwa kitu kingine bali ni Malaya. Waliweza
kutambuliwa kwa wazi kwa kuonekana hadharani bila
kufunika vichwa vyao. Na inatakiwa ikumbukwe kuwa
adhabu ya umalaya ilikuwa ni kunyoa vichwa vyao.
Kwa mwanamke Mkristo, kupita katika mitaa ya Korintho
bila kufunika kichwa kungemfanya atambulike kama
malaya wa kawaida wa Aphrodite Pandemos. Suala hili
lingeleta aibu na fedheha kwa kanisa.
Zaidi, kufunika kichwa kwa wanawake wa Korintho
kunaashiria ukweli kwamba mwanamke anatambua na
kuheshimu kanuni ya kujinyenyekeza kwa mwanaume.
Kushindwa kufunika kichwa, kungeonesha kushindwa
kutambua kanuni hii, na kungekuwa na fedheha kanisani.
Mwanamke wa Korintho kufunika kichwa, kulimaanisha:
1. Kwamba alikuwa anajali staha, na alitaka aangaliwe
kama mwanamke safi. Hakutaka atambuliwe kama
malaya wa kawaida wa Pandemos;
2. Kwamba alitambua na aliheshimu kanuni takatifu ya
kwamba mwanamke yupo chini ya mwanaume, na
huu ndio uhusiano mtakatifu ulioanzishwa;
3. Kwamba alitamani kuona yuko sawa kwa haki ya
asili, tamaduni zenye maana, hakutamani kuwa
chukizo kwa watu wengine bila sababu ya msingi
4. Kwamba hakutaka kuleta fedheha katika kanisa la
Bwana.

- 137 -
5. Kwamba hakutaka kuwa chukizo kwa Mungu na
malaika zake.

Kufunika kichwa NDWLNDPMLZDFort Worth


7H[DV86$ – 1969!
Lakini kwa siku zetu na utamaduni wetu:
1. Wanawake kwa kawaida au kwa desturi hawafu-
niki kichwa;
2. Kufunika kichwa kunaweza kusimaanishe suala la
mwanamke kuwa safi na mwenye staha;
3. Kutofunika kichwa hakumtambulishi mwanamke
moja kwa moja kuwa ni malaya wa kawaida;
4. Kufunika kichwa hakuwezi kumaanisha moja kwa
moja kwamba mvaaji anatambua na anaheshimu
kanuni ya kuwa chini ya mwanaume;
5. Kufunika kichwa kusingemaanisha moja kwa
moja kwamba mvaaji hakutamani kuwa chukizo
kwa wengine;
6. Kufunika kichwa kusingemaanisha kwamba mva-
aji hakutaka kuleta fedheha katika kanisa la Bwa-
na;
7. Kufunika kichwa kusingemaanisha kwamba mva-
aji hakutaka kuwa chukizo kwa Mungu au kwa
malaika zake.

Vipi kuhusu Kofia?


Inatakiwa izingatiwe kwamba 1 Wakorintho 11:2-16
hujadili wanawake ambao hawakufunika vichwa vyao.
Hakuna kitu kinachozungumziwa kuhusu kofia. Kabla
- 138 -
kusudi hilo hilo lilohusishwa na utaji, linaweza

siwezi nikasema moja kwa moja kwamba ni mwanamke

anatambua na kuheshimu kanuni takatifu za kuwa

kwamba mvaaji hatamani kuwachukiza wengine kwa

kwamba mvaaji hataki kuleta fedheha katika kanisa la

chukizo kwa Mungu na malaika zake.

Je, haya maandiko hayana umuhimu kwetu?


Yanayo. Kanuni takatifu zilizofundishwa hapa zinatumika
sasa kama ilivyokuwa kipindi hicho ambapo Paulo
aliandika haya maandiko. Tatizo ni kwamba kila mara
tunakwama kwenye vielelezo na mazingira ambamo
kanuni hufundishwa hadi tunashindwa kuona kanuni
zenyewe, kanuni zinashurutisha, desturi hazishurutishi.
Hebu tujifunze:
1. Kwamba kichwa cha Kristo ni Mungu; kichwa cha
kila mwanaume ni Kristo; kichwa cha mwanamke ni
mwanaume;
2. Kwa mwanaume hatakiwi kufanya kitu ambacho
kitamkosea Kristo heshima; kwamba mwanaume

- 139 -
anatakiwa siku zote kuleta heshima kwa Kristo, kwa
maneno, matendo na maisha.
3. Kwamba mwanamke hatakiwi kufanya kitu chochote
ambacho kitamkosea heshima mwanaume; kwamba
anatakiwa kushikilia tabia ya heshima na kujishusha;
4. Ni vizuri na sahihi kuzingatia desturi ambazo ni nzuri,
na kwamba hatutakiwi kuwahukumu wengine kwa
kuvunja hizi desturi.
5. Kwamba hatutakiwi kuleta fedheha kanisani kwa
kukiuka desturi ambazo ni nzuri;
6. Kwamba hatutakiwi kuvaa kwa mtindo ambao
tutatambuliwa kama watu tusio safi;
7. Kwamba hatutakiwi kuvaa kwa mtindo ambao utaleta
chukizo kwa Mungu au kwa malaika zake (waliopo
wakati wa ibada).
8. Uvaaji wetu ni lazima uonyeshe suala la usafi na
staha.
Kama muda utajirudia tena ambapo wanawake wasio
safi wa Fort Worth wanaojitambulisha kwa kubeba pochi
nyekundu kwenye mkono wao wa kulia, ningepinga
vikali kwa kuzingatia 1 Wakorintho 11: 2-16 kwamba
ingekuwa ni dhambi kwa mwanamke Mkristo wa eneo
hilo kubeba pochi nyekundu kwenye mkono wake wa
kulia.

- 140 -
KIAMBATISHO B
BARUA NAMBA MOJA
Ndugu mpendwa …..:
Nimesoma barua yako, na nina furaha ya pekee kusikia
kutoka kwako. Furaha – lakini pia huzuni. Nimehuzunishwa
kwamba umepata kiharusi, lakini nina furaha kwamba
bado unafanya kazi katika huduma ya Bwana.
Ni leo hii (Katika darasa langu la Biblia katika chuo
cha Biblia cha Tennesee) nilikuwa nashughulika na hoja
uliyokuwa unauliza.
Ndio, ulikumbuka kwa usahihi. Nilisisitiza na ninaendelea
kusisitiza kwamba “amri” haibagui, na kwamba “mfano”
hauweki kando. Kama amri inaweka kando basi mfano
pia unaweza kuweka kando. Kama mfano hauweki kando
basi amri pia haiweki.
Mhubiri wa shule ya wapinga-Jumapili, amepata mfano wa
kufundisha katika kusanyiko, na anasema hii ndio njia pekee
inavyotakiwa kufanyika. Mhubiri mpinga-ushirikiano
anaona kile anachofikiri ni mfano kwa kanisa kupeleka
moja kwa moja kwa mhubiri, na anasema kwamba hii ndio
njia pekee inavyoweza kufanyika (suala la uinjilisti).
Kuna maswali mawili: (1) hii ndio njia pekee ambayo
Mungu anatoa mamlaka kwa mfano? (2) Je mfano
hubagua? Au je huidhinisha kile ambacho kimeonyeshwa
kwa mfano?

- 141 -
Nimepewa mamlaka (kwa mfano) kusafirikwa kutumia
mtumbwi, lakini ni dhahiri kwamba ninaweza kusafirikwa
kutumia gari. Kanisa linaweza kuchagua watu wawili
kuunda njia moja ya kupeleka baraka kwa wengine, lakini
kanisa linaweza pia kutumia huduma za posta kupeleka
baraka kwa wengine. Matendo 11:29,30.
Nimeamriwa kutoa siku ya kwanza ya kila juma. Lakini
ninaamini (kwa kuzingatia Wagal. 6:10) kwamba
tunaweza kutoa siku ya Jumatano usiku, kukiwa na
mahitaji maalumu. Kama ndio hivyo amri haibagui.
Fikiria kama Mungu angetuamuru “tuimbe” katika Waefe.
5:19 na “tutumie vyombo vya muziki” katika Wakol. 3:16,
basi ingekuwa ni dhahiri kwamba “kuimba” hakukuweka
kando “kutumia vyombo vya muziki.” Kimsingi katika
Agano la Kale, Waisraeli waliambiwa kuimba na kutumia
vyombo vya muziki. Kwa Waisraeli ambao waliamuriwa
kuimba hakukuweka kando kutumia vyombo vya muziki.
Mungu alipomuelekeza Nuhu kuhusiana na ujenzi wa
Safina,aliainisha kwamba ilitakiwa kujengwa kwa mti wa
mvinje. Je, “mvinje” uliweka kando msonobari? Mungu
alipomuamuru Nuhu kutumia mti wa “mvinje”, Je, kulikuwa
na umuhimu wa Mungu kumwambia Nuhu asitumiemti wa
msonobari au asitumie mti wa mwembe? Hapana. Mungu
hakuorodhesha aina yote ya miti Nuhu hakutakiwa kutumia.
Amri iliamuru nini? Iliruhusu “mti wa mvinje” tu. Je,
Nuhu angeweza kutumia msonobari? Hakika hapana. Kwa
nini? Hakukuwa na mamlaka kwa ajili ya hilo.
Mama anamtuma mwanawe dukani. Anamwelekeza
akanunue pakiti moja ya maziwa, na mkate mmoja.

- 142 -
Mtoto anarudi nyumbani na; (1) pakiti moja ya maziwa,
(2) mkate mmoja (3) kilo moja ya maharage, (4) pipi nne
(5) nusu kilo ya viazi, na (6) mfuko wa sukari.
Mtoto hakuwa mtiifu kwa maelekezo aliyopewa. Mama
hakusema: usinunue hiki na kile. Aliidhinisha kile
kilichopaswa kununuliwa. Mtoto alinunua vitu ambavyo
hakuruhusiwa kununua.
Tunafundishwa kwa amri na mifano kwamba tunatakiwa
kushiriki meza ya Bwana katika siku ya kwanza ya kila
juma. Je tunaweza kushiriki meza ya Bwana siku ya
Alhamisi usiku? Hakika hapana! Kwa nini hapana! Kwa
sababu HAKUNA IDHINI YA KUFANYA HIVYO.
Je amri (au mfano) unaweka kando Alhamisi usiku?
Hapana. Unafanya nini sasa? Huidhinisha kushiriki siku
ya kwanza ya juma.
Ndivyo ilivyo sawa na amri ya kuimba. Kuimba
hakubagui kucheza. Kuna idhinisha kuimba. Sasa kuna
ubaya gani na kucheza? Hakuna mamlaka kwa ajili ya
hilo. Sababu ya kuweka kando ni ukosefu wa mamlaka.
Kanuni ya msingi kabisa ya Kibiblia ni: Tunatembea
kwa imani. Imani huja kwa kusikia neno la Mungu. Pale
ambapo hapana neno la Mungu hakuna imani. Na bila imani
haiwezekani kumpendeza Mungu. Kanuni ya kutembea
kwa imani hujumuisha kuheshimu ukimya wa Maandiko.
Mungu aendelee kuwa pamoja nawe na akubariki katika
huduma yake.
Ni wako katika Ufalme,
Roy Deaver

- 143 -
KIAMBATISHO C
BARUA NAMBA MBILI
Ndugu mpendwa …:
Asante sana kwa barua yako ya Julai 25, 1975.
Nimependezwa na maoni yako kuhusiana na KANUNI
ZA UREJESHAJI.
Nilisisitiza katika makala ambayo umerejelea kwamba “…
mfano hauweki kando.” Ninaamini hili ni sahihi. Mfano
unaidhinisha kile kilichotolewa mfano, lakini hivi ndivyo
ninaweza kusema kuhusu hili. Mfano wenyewe hauweki
kando. Mfano wa mtu kusafiri kwa kutumia mtumbwi
huidhinisha mtu kusafiri kwa mtumbwi, lakini hauweki
kando kusafiri kwa kutumia gari au ndege. Mfano wa
kushiriki meza ya Bwana kwenye ghorofa ya tatu, hauweki
kando kushiriki kwetu kwenye ghorofa ya kwanza. Mfano
katika (2 Kor. 8:1-5) ambao Paulo aliutoa kwa ajili ya
ndugu wa Korintho hakika unaidhinisha wapendwa wa
Korintho (na sisi) kutoa zaidi ya uwezo wao. Hata hivyo hii
haimaanishi kwamba tutakuwa tunafanya dhambi tukitoa
kulingana na uwezo wetu (au kulingana na tulivyobarikiwa).
Kwa kuzingatia meza ya Bwana, nilisema: “Hoja
inayofanya iwe dhambi kushiriki meza ya Bwana Alhamisi
usiku ni kutokana na ukweli kwamba hakuna mamlaka
kwa ajili ya hilo.” Nikaendelea kusema: “Maandiko
mengi yanaonyesha wajibu wetu kuimba katika ibada ya
Kikristo. Kitu kinachofanya ionekane kuwa ni dhambi

- 144 -
kutumia ala za muziki ni kutokana na ukweli kwamba
hakuna mamlaka kwa ajili ya hilo. Kanuni takatifu ya
kutembea kwa imani hujumuisha kuheshimu ukimya wa
Maandiko.” Hakuwezi kuwepo na imani pale ambapo
hakuna neno la Mungu.
Kama suala ni kwamba tuna mfano wa watu wanaoshiriki
meza ya Bwana katika ghorofa ya tatu, na kama suala
ni kwamba tunaweza kushiriki meza ya Bwana kwenye
ghorofa ya kwanza kwa mujibu wa maandiko, basi
itakuwa inamaanisha kwamba (kuhusiana na sehemu)
mfano hauweki kando.
Kama suala ni kwamba tuna mfano wa watu waliosafiri
kwa mtumbwi, na kama kimaandiko tunaweza kusafiri
kwa kutumia gari – itakuwa inamaanisha kwamba mifano
haibagui.
Kama suala ni kwamba wapendwa wa Makedonia
walitoa zaidi ya uwezo wao, na kwa mujibu wa maandiko
tunaweza kutoa kulingana na uwezo wetu, basi itakuwa
ina maana kuwa mfano (Paulo alinukuu kwa ajili ya
wapendwa wa Korintho na sisi) haubagui.
Ulisema kuwa mpingaji anaweza kuuliza swali: “Kwa
kuwa Agano Jipya linaidhinisha kusafiri kwa mtumbwi,
lakini haliweki kando kusafiri kwa gari, huoni kwamba
kuruhusu Meza ya Bwana kufanyika siku ya kwanza
ya juma, ni kuruhusu kushiriki siku ya Alhamisi usiku?
Kama hatuna idhini kwa ajili ya Alhamisi usiku, tunapata
wapi idhini ya kusafiri kwa gari? Kama kimoja huwekwa
kando, kwa nini isiwe kingine? Nitafurahi kusikia maoni
yako kuhusiana na hoja hii.”

- 145 -
Nimependezwa sana na umakini wako katika swali hili.
Ni swali zuri sana na ambalo linatakiwa kujibiwa kwa
umakini.
Ninaona katika maandiko wapendwa wanasafiri kwa
kusudi kubwa la utume kwa kutumia mashua (Mdo.
13:4; Mdo. 27:16), na ikiwa pia nitagundua kwamba
walisafiri kwa kutembea (Mdo. 18:22; Mdo, 20:13), basi
ni lazima nihitimishe kuwa Bwana hakukusudia kuweka au
kuidhinisha njia mahususi ya kusafiria. Ni lazima nihitimishe
kuwa namna ya kusafiri imeachwa bila kuainishwa.
Katika maandiko ninaona kwamba wapendwa walishiriki
Meza ya Bwana kwenye ghorofa ya tatu (Mdo. 20:7-9),
na kama nikikuta katika maandiko kwamba wapendwa
walishiriki Meza ya Bwana katika sehemu tofauti na
ghorofa ya tatu (1 Kor. 11:17 ), basi najua kwamba Bwana
hakukusudia kuweka au kuidhinisha sehemu maalumu.
Bwana mwenyewe alisisitiza katika Yohana 4:20-24
kwamba kukubalika kwa ibada hakuamuliwi na eneo.
Ikiwa nitapata katika maandiko kwamba wapendwa
walishiriki Meza ya Bwana katika siku ya kwanza ya
juma, na ikiwa nitapata katika maandiko kwamba,
wapendwa walishiriki Meza ya Bwana Jumatano usiku,
basi nitalazimika kuhitimisha kuwa Bwana hakukusudia
kuweka au kuidhinisha muda maalumu kwa ajili ya
kushiriki. Lakini sipati ushahidi wowote kwamba
wapendwa walishiriki Meza ya Bwana Jumatano usiku.
Ninapata ushahidi wa kutosha na usiopingika kwamba
iliadhimishwa na inapaswa kuadhimishwa kila siku ya
kwanza ya juma.

- 146 -
Kabla ya Alhamisi usiku (katika uhusiano na siku ya
kwanza) inaweza kufananishwa na gari (katika uhusiano
na mtumbwi) ni lazima nipate kitu kinachohusiana na
siku ya kwanza kinachofananishwa na kutembea katika
uhusiano wake na mtumbwi, lakini siwezi kupata kitu
hicho. Kuna mamlaka ya wazi kwa ajili ya gari. Kuna
ushahidi wa kutosha kabisa kwamba Mungu hakukusudia
kuweka au kuidhinisha njia mahususi ya kusafiri. Kuna
ushahidi wa kutosha kwamba Bwana alikusudia kuweka
au kuidhinisha muda fulani mahususi (kuhusiana na siku)
kwa ajili ya kushiriki Meza ya Bwana.

UKWELI
(1) Bwana alisema “enendeni.” (2) Wapendwa wakaenda
kwa mashua. (3) Wapendwa wakaenda kwa kutembea

HITIMISHO
Ni lazima nihitimishe kutokana na ukweli huu kwamba
(1) Ni lazima niende; (2) ninaweza kwenda kwa mtumbwi
(3) Ninaweza kwenda kwa kutembea; (4) Namna ya
kwenda, kwa hiyo haijaainishwa, ninaweza kwenda kwa
kutumia njia yeyote ile, hiyo iko sawa.

UKWELI
(1) Tumeamriwa kutoa kama tulivyobarikiwa.
(2) Wapendwa wa Makedonia walitoa zaidi ya uwezo
wao.

- 147 -
HITIMISHO
Kutokana na ukweli huu ni lazima nihitimishe:
(1) Nimepewa jukumu la kutoa; (2) Ni lazima nitoe
angalau kama nilivyobarikiwa; (3) Ninaweza kutoa zaidi
ya nilivyobarikiwa.

UKWELI:
(1) Wapendwa walipewa jukumu la kushiriki Meza ya
Bwana. (2) Walishiriki meza ya Bwana katika siku ya
kwanza ya Juma. (3) Tuna maelekezo maalumu kwamba
Meza ya Bwana inatakiwa kushiriki meza ya Bwana kila
siku ya kwanza ya juma (Mdo. 20:7 pamoja na 1 Kor. 16:2).
(4) Hatuna mamlaka ya kushiriki Meza ya Bwana katika
muda mwingine tofauti isipokuwa siku ya kwanza ya juma.

HITIMISHO
Kutokana na ukweli huu ni lazima nihitimishe: (1) Ni
lazima tushiriki Meza ya Bwana; (2) Ni lazima tushiriki
Meza ya Bwana siku ya kwanza ya juma; (3) Ni lazima
tushiriki Meza ya Bwana kila siku ya kwanza ya juma;
(4) Tunatakiwa tushiriki Meza ya Bwana katika siku ya
kwanza ya juma tu.
Ngoja nisisitize tena, hoja inayofanya iwe dhambi
kushiriki Meza ya Bwana siku ya Alhamisi usiku, ni
kutokana na ukweli kwamba hakuna mamlaka kwa ajili
ya hilo – sio wazo kwamba mfano hubagua.
Asante tena kwa barua yako. Ni matumaini na maombi
yangu ya dhati kwamba fikra hizi zitakuwa za manufaa
kwako kwa ajili ya kujifunza na kufundisha.

- 148 -
Mungu aendelee kuwa pamoja nawe na akubariki katika
huduma yake.
Ni wako katika Ufalme,
Roy Deaver

SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 149 -
SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 150 -
SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 151 -
SEHEMU YA KUANDIKIA VITINI

- 152 -

You might also like