Professional Documents
Culture Documents
MBADALA YA WATOTO
Vijiji vya Watoto vya Kimataifa vya SOS ni Asasi inayojumuisha asasi zaidi ya 130 za kitaifa
duniani kote. Ni Asasi isiyo ya Kiserikali au ya Kidini inayotoa huduma moja kwa moja za
malezi, elimu na afya kwa watoto walio hatarini kupoteza au waliopoteza malezi ya wazazi.
Asasi hii pia inatoa mafunzo ya kujenga uwezo wa walezi wa watoto, familia zao na jamii ili
watoto wapate malezi ya kutosha.
Asasi ya Vijiji vya Watoto vya Kimataifa vya SOS inatetea haki za watoto waliopoteza na walio
hatarini kupoteza malezi ya wazazi. Ilianzishwa mwaka 1949 na shughuli zake zinaongozwa na
msingi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Mtoto.
www.sos-childrensvillages.org
Asasi ya Kimataifa ya Huduma ya Jamii (ISS) inasaidia mtu mmoja mmoja, watoto na familia
zinazokabiliwa na matatizo ya kijamii yanayohusisha nchi mbili au zaidi na yanayotokana na
uhamiaji wa kimataifa au kuondolewa kwenye makazi. Kama asasi isiyotengeneza faida na
iliyoundwa mwaka 1924, asasi hii inafanya kazi katika nchi karibia 140 na inahudumia watu
zaidi ya 50,000 duniani kote.
Asasi ya Kimataifa ya Huduma ya Jamii ina umahiri maalumu kwenye maeneo ya kuasili na,
kwa mapana zaidi, kuzuia kutelekeza na kuweka watoto katika malezi mbadala na kusaidia
familia ambazo watoto wanatoka. Pia inapigania heshima ya watoto walioasiliwa au wanaoishi
katika vituo vya malezi. www.iss-ssi.org
3
YALIYOMO
5 DIBAJI
6 UTANGULIZI
DIBAJI
Mamilioni ya watoto duniani kote hawana, au wako hatarini kupoteza, malezi ya wazazi na
wanakabiliwa na changamoto kubwa katika maisha yao ya kila siku, changamoto ambazo
zinaathiri maisha yao ya utu uzima.
Kupitia kazi yake ya kufuatilia utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za
Mtoto (UNCRC), Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu iligundua kuwa
changamoto nyingi zinazowaathiri watoto na familia zilikuwa hazifahamiki vizuri na kwa hiyo
kutokuingizwa katika sera na utekelezaji wa haki za mtoto.
Kufahamu kwa pengo lililoko kati ya haki za watoto na utekelezaji wake kuliifanya Kamati
mwaka 2005 kuazimisha Siku ya Majadiliano ya Msingi kuhusu watoto waliopoteza malezi ya
wazazi. Kutokana na majadiliano ya siku hiyo, Kamati iliiomba jumuiya ya Kimataifa, wakala
wa Umoja wa Mataifa, Asasi Zisizo za Kiserikali, wataalamu, wanataaluma na vyama vya
weledi kuungana na kutengeneza kanuni za kimataifa ambazo zingetoa mwongozo wa kitaalamu
kwa Nchi na watu wengine wanaohusika na utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa
kuhusu Haki za Mtoto.
Kwa hiyo, Kamati inapokea kwa furaha kukubaliwa kwa Mwongozo wa Malezi Mbadala ya
Watoto na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati wa maazimisho ya miaka 20 ya
Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Mtoto yaliyofanyika Novemba 20, 2009. Ni
matokeo ya mapendekezo yaliyotolewa na Kamati mwaka 2005 na ya miaka mitano ya kufanya
kazi, pamoja na ushirikiano na mazungumzo ya kina.
Napenda kuishukuru serikali ya Brazil kwa juhudi zake za kuwakutanisha Kundi la Marafiki na
kwa kufanya kazi bila kuchoka kuhakikisha kwamba Mwongozo wa Malezi Mbadala ya Watoto
unatambuliwa. Hakika, kazi isingekamilika bila msaada wa Asasi Zisizo za Kiserikali na
washirika wengine muhimu, hususani Asasi yenye makao makuu yake mjini Geneva ambayo
inajihusisha na watoto waliopoteza malezi ya wazazi.
Nina furaha kubwa kuelezea matumaini ya dhati ya Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za
Mtoto kwamba Mwongozo wa Malezi Mbadala ya Watoto utakuwa muhimu katika kutekeleza
Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Mtoto, na naliona chapisho hili kama hatua
muhimu ya awali katika usambazaji wa Mwongozo.
UTANGULIZI
Novemba 20, 2009 wakati wa maazimisho ya miaka ishirini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa
kuhusu Haki za Mtoto, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliutambua rasmi Mwongozo wa
Malezi Mbadala ya Watoto. Sisi, Vijiji vya Watoto vya Kimataifa vya SOS na Asasi ya
Kimataifa ya Huduma ya Jamii, tunaupokea Mwongozo huu mpya wa kimataifa kwa furaha
kubwa. Mwongozo unaweza kuimarisha haki za watoto na kuboresha maisha ya mamilioni ya
watoto, familia zao na jamii duniani kote. Kwa lengo la kusaidia usambazaji na utekelezaji wake,
chapisho hili linatoa matini rasmi ya Mwongozo wa Malezi Mbadala ya Watoto (Mkutano Mkuu
A/RES/64/142) na lina maswali kwa ajili ya kutafakari baadhi ya maeneo ya msingi
yaliyoainishwa kwenye Mwongozo.
USULI
Mwongozo wa Malezi Mbadala ya Watoto ulitokana na kugunduliwa kwa pengo katika
kutekeleza Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Mtoto kwa ajili ya mamilioni ya
watoto duniani ambao hawana, au walio hatarini, kupoteza malezi ya wazazi. Kwa hiyo, jumuiya
ya kimataifa imeungana na kutengeneza Mwongozo wa Malezi Mbadala ya Watoto. Ni matokeo
ya miaka mitano ya ushirikiano na majadiliano kati ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za
Mtoto, serikali zikiongozwa na Brazil, UNICEF, wataalamu na wanataaluma, wawakilishi wa
asasi zisizo za kiserikali, vijana wadogo wenye uzoefu na masuala ya malezi, na wengineo.
KANUNI ZA MSINGI
Mwongozo wa Malezi Mbadala ya Watoto unaonyesha umuhimu wa sera na utekelezaji kuhusu
kanuni mbili za msingi: ulazima na kufaa. Katika kiini cha ulazima tunakuta dhamira ya
kuwasaidia watoto ili wabaki, na watunzwe, na familia zao. Kumwondoa mtoto kutoka kwenye
familia yake iwe kimbilio la mwisho, na kabla uamuzi wa aina hiyo haujachukuliwa, tathmini
shirikishi ya kina inahitajika. Kuhusu kufaa, Mwongozo wa Malezi Mbadala ya Watoto unatoa
aina mbalimbali za malezi mbadala zinazofaa. Kila mtoto anayehitaji malezi mbadala ana
mahitaji maalumu kuhusiana na, kwa mfano, malezi ya muda mfupi au mrefu au kuwaweka
ndugu pamoja. Aina ya malezi inayochaguliwa lazima iendane na mahitaji maalumu ya mtoto.
Utunzaji wa mtoto unapaswa kutathminiwa mara kwa mara ili kuona kama kuna ulazima wa
kuendelea kutoa malezi mbadala kwa mtoto, na kama inafaa kumrudisha kwenye familia yake.
MWONGOZO WA MALEZI
MBADALA YA WATOTO
I. DHUMUNI kiuchumi, kijamii na kitamaduni ya kila
Nchi; na
1 Mwongozo huu unakusudiwa kuboresha (d) Kuongoza sera, maamuzi na shughuli za
utekelezaji wa Mkataba wa Umoja wa wote wanaohusika na ulinzi na ustawi wa
Mataifa kuhusu Haki za Mtoto na kanuni mtoto katika sekta za umma na binafsi,
zingine mahususi za kimataifa kuhusu ulinzi pamoja na asasi za kijamii.
na ustawi wa watoto waliopoteza au walio
hatarini kupoteza malezi ya wazazi. II. KANUNI NA MITAZAMO YA JUMLA
...inatoa utaratibu mpana wa haki ili (i) “Wapweke” kama hawatunzwi na ndugu
kuhakikisha haki za mtoto, kwa kuzingatia au mtu mzima ambaye kisheria au kimila
sio tu malezi na ulinzi, bali pia elimu, afya, ana jukumu la kufanya hivyo; au
utambulisho, imani na kutoingiliwa? (ii) “Wametengwa” kama wametengwa na
mlezi muhimu wa zamani anayetambulika
III. MAWANDA YA MWONGOZO kisheria au kimila, lakini ambaye anatunzwa
na ndugu mwingine.
27 Mwongozo huu unahusu matumizi (b) Malezi mbadala yanaweza kuwa ya aina
yanayofaa na mazingira ya utoaji huduma ya yeyote kati ya hizi:
malezi mbadala rasmi kwa watoto wenye (i) Malezi yasiyo rasmi: utaratibu wowote
umri chini ya miaka 18, isipokuwa, chini ya uliowekwa katika mazingira ya kifamilia,
sheria inayomhusu mtoto, akifikia umri wa ambako mtoto anatunzwa kwa misingi
utu uzima mapema. Mwongozo unahusu pia endelevu au ya kudumu na ndugu au
malezi mbadala yasiyo rasmi kama marafiki (matunzo yasiyo rasmi kutoka kwa
umeonyeshwa kufanya hivyo tu, kwa ndugu) au na watu wengine kwa uwezo wao
kuheshimu nafasi ya familia na jamii na na jitihada za mtoto mwenyewe, wazazi
wajibu wa Nchi wa kuwatunza watoto wake au mtu mwingine bila utaratibu huo
waliopoteza malezi ya wazazi au watoa kuwa umepangwa na mamlaka yeyote ya
huduma wanaotambulika kisheria au wa kiutawala au ya kimahakama au chombo
jadi, kama ilivyoanishwa katika Mkataba wa kinachotambulika kisheria;
Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Mtoto. (ii) Malezi rasmi: malezi yote yanayotolewa
katika mazingira ya kifamilia kwa matakwa
28 Kanuni zilizoko katika Mwongozo huu ya chombo cha kiutawala au mamlaka ya
zinawahusu pia, kadiri inavyofaa, watoto kimahakama, na malezi yote yanayotolewa
wadogo ambao tayari wanapata malezi kwenye vituo, pamoja na vituo binafsi, yawe
mbadala na wanahitaji kuendelea kutunzwa yametokana na hatua za kiutawala au
au kupata msaada kipindi cha mpito baada kimahakama au la.
ya kufikisha umri wa utu uzima chini ya (c) Kuhusu mazingira ambamo malezi
sheria husika. yanatolewa, malezi mbadala yanaweza
kuwa:
29 Kwa madhumuni ya Mwongozo huu, na (i) Malezi kutoka kwa ndugu: malezi rasmi
yenye uelekeo huo, isipokuwa mambo au sio rasmi ya kifamilia kutoka kwa jamaa
maalumu yaliyotajwa katika aya ya 30 hapo wa mtoto au marafiki wa karibu wa familia
chini, tafsiri zifuatazo zitatumika: ambayo mtoto anaifahamu;
(a) Watoto wasiokuwa na malezi ya wazazi: (ii) Malezi kutoka kwa familia nyingine:
ni watoto wote ambao hawalelewi na mazingira ambayo watoto wanawekwa na
angalau mmoja wa wazazi wao, kwa sababu mamlaka husika ili wapate malezi mbadala
yeyote na katika mazingira yeyote yale. kutoka kwenye familia zingine za karibu
Watoto wasiokuwa na malezi ya wazazi ambazo sio familia zao zilizochaguliwa,
wanaoshi nje ya nchi yao au wahanga wa kuthibitishwa, kupitishwa na kusimamiwa ili
mazingira ya dharura wanaweza zitoe malezi hayo;
kutambuliwa kama:
13
lugha na dini yake, mazingira ya kifamilia nchi yake, utamaduni, lugha na dini yake, na
na kijamii, historia ya afya yake na mahitaji mahusiano ya mtoto na ndugu zake, kwa
maalumu. lengo la kuzuia kuwatenganisha.
106 Wakala na vituo vyote viwe na sera na Kumbukumbu hizi zitunzwe muda wote
matamko ya kiutandaji yanayoendana na ambao mtoto atakuwepo kwenye malezi
Mwongozo huu, yanayoonyesha malengo, mbadala na zitumiwe na wataalamu
sera, njia na viwango vinavyotumika waliothibitishwa na wanaohusika na malezi
kuajiri, kufuatilia, kusimamia na kukagua yake.
walezi wenye sifa ili kuhakikisha kwamba
malengo hayo yanafikiwa. 111 Mtoto na wazazi au walezi wanaweza
kupewa kumbukumbu zilizotajwa hapo juu
107 Wakala na vituo vyote vitengeneze kulingana na haki ya mtoto ya kutoingiliwa
kanuni za maadili za wafanyakazi ambazo na usiri, kadiri inavyofaa. Ushauri nasaha
zinaendana na Mwongozo huu, zinazoelezea unaofaa utolewe kabla, wakati na baada ya
kazi za kila mtaalamu, hususani walezi, na kuzipitia kumbukumbu hizo.
zionyeshe utaratibu wa kutoa malalamiko
kuhusu vitendo vya uovu vya mfanyakazi WAKALA, VITUO VYA MALEZI &
yeyote. WALEZI
...inatoa ulinzi wa kutosha ili kuhakikisha 116 Walezi walioajiriwa na wakala na vituo
kuwa malezi katika vituo yanatolewa pale tu vya malezi wapatiwe mafunzo juu ya njia
inapobidi, na kwamba juhudi za watoa nzuri za kukabiliana na changamoto za
huduma kuwaweka watoto katika vituo ili, kitabia, zikiwemo njia za kutatua migogoro
kwa mfano, kujipatia fedha, zinapigwa na za kuzuia vitendo vyenye madhara kwa
marufuku? watu wengine na mtu binafsi.
112 Vituo vyote vya malezi viwe na sera 117 Wakala na vituo vya malezi vihakikishe
nzuri itakayodumisha usiri wa taarifa za kila kwamba, pale inapofaa, walezi
mtoto, sera ambayo walezi wote wanaijua na wanaandaliwa ili wakabiliane na watoto
kuifuata. wenye mahitaji maalumu, hasa wale
wanaoishi na virusi vya Ukimwi au
113 Ni vizuri kwa wakala na vituo vyote vya magonjwa mengine ya kudumu ya kimwili
malezi kuhakikisha kwamba, kabla ya au kiakili na watoto wenye ulemavu.
kuajiri walezi na wafanyakazi wengine
wanaohudumia watoto, kutathmini kwa kina 2 Malezi ya wazazi wasiokuwa wa damu
kufaa na uwezo wao wa kuwatunza watoto.
118 Mamlaka halali au wakala watengeneze
114 Mazingira ya kazi, ikiwemo mishahara mfumo, na watoe mafunzo kwa
ya walezi inayolipwa na wakala na vituo vya wafanyakazi, ili watathmini na kulinganisha
malezi, yatoe motisha, yawe ya kuridhisha mahitaji ya mtoto na uwezo na rasilimali za
na endelevu ili wafanyakazi watekeleze wazazi tarajiwa wasiokuwa wadamu na
majukumu yao kwa kiwango cha juu. kuwaandaa wote wanaohusika na mchakato
wa kumweka mtoto katika malezi hayo.
115 Mafunzo kuhusu haki za watoto
waliopoteza malezi ya wazazi na kuhusu 119 Katika kila eneo, uanishaji wa walezi
madhara wanayoweza kuyapata, hususani wasio wa damu wenye uwezo wa kuwalea
wale wanaoishi katika mazingira magumu, na kuwalinda watoto na kuendeleza
kama katika vituo vya malezi vya dharura au mahusiano na familia, jumuiya na kikundi
nje ya mazingira wanayoishi kila siku cha utamaduni, ufanyike.
yatolewe. Walezi pia wapate mafunzo
kuhusu masuala ya kitamaduni, kijamii, 120 Maandalizi maalumu, msaada na
kijinsia na kidini. Nchi zitoe rasilimali za huduma za ushauri nasaha kwa ajili ya
kutosha na njia za kuwatambua wataalamu walezi hao zitengenezwe na zitolewe kwa
hawa ili watekeleze kanuni hizi. walezi wote mara kwa mara, kabla, wakati
na baada ya kumweka mtoto katika malezi.
watoto waliopoteza malezi ya wazazi ili kumpatia mtoto fursa ya kuwa karibu na
wapate fursa ya kuzifanya sauti zao zisikike mlezi fulani. Walezi wawekwe katika vituo
na kutoa maoni yao katika kutengeneza sera. vya malezi ili watekeleze kikamilifu nia na
malengo ya vituo ya kuhakikisha kwamba
122 Wazazi wasiokuwa wa damu mtoto yuko salama.
wahamasishwe kuanzisha vyama vya walezi
ili waweze kusaidiana katika utendaji na 127 Sheria, sera na kanuni zipige marufuku
kutengeneza sera. ushawishi wa kuwaweka watoto katika vituo
vya malezi unaofanywa na wakala, vituo na
C. Vituo vya malezi mtu binafsi.
123 Vituo vinavyotoa huduma ya malezi D. Ukaguzi na Ufuatiliaji
lazima viwe vidogo na vizingatie haki na
mahitaji ya mtoto, katika mfumo ambao 128 Wakala, vituo na wataalamu wa
unafanana sana na wa kifamilia au huduma ya malezi wawajibike kwa
mazingira ya kikundi kidogo. Lengo lake mamlaka halali ambayo inapaswa
kwa ujumla liwe ni kumpatia mtoto malezi kuhakikisha kwamba, pamoja na mambo
ya muda na kuchangia kikamilifu katika mengine, ukaguzi wa mara kwa mara
kumuunganisha na familia yake, au kama uliopangwa na wa kushtukiza unafanyika,
haiwezekani kufanya hivyo, kumpatia ukihusisha ukaguzi na majadiliano na
malezi mbadala bora kwenye familia wafanyakazi na watoto.
nyingine, kwa kumuasili au kumtoa kafala
kwa mujibu wa sheria ya Kiislam pale 129 Kwa kiwango kinachowezekana na
inapofaa. kinachofaa, ukaguzi uwe na sehemu ya
mafunzo na kujenga uwezo wa walezi.
124 Hatua zichukuliwe, ili pale inapobidi na
inapofaa, mtoto anayehitaji ulinzi na malezi 130 Nchi zihakikishe kwamba mfumo huru
wa ufuatiliaji unakuwepo, kwa kuzingatia
mbadala tu awekwe mahali tofauti na watoto uwezo wa taasisi za kitaifa kukuza na
waliofanya makosa ya jinai. kulinda haki za binadamu (Kanuni za Paris).
Mfumo wa ufuatiliaji ufikiwe kirahisi na
125 Mamlaka halali za kitaifa au za ngazi za watoto, wazazi na watu wenye jukumu la
mitaa zitengeneze utaratibu mzuri wa kulea watoto waliopoteza malezi ya wazazi
mchujo ili kuhakikisha watoto wanawekwa wao. Kazi za mfumo wa ufuatiliaji
katika malezi mbadala kwa utaratibu mzuri. zijumuishe:
(a) Kuzungumza kwa usiri na watoto walio
126 Nchi zihakikishe kwamba vituo vya katika aina zote za malezi mbadala,
malezi vina walezi wa kutosha ili kuwepo kutembelea vituo wanavyoishi na kufanya
uangalizi wa karibu na, inapowezekana, uchunguzi juu ya madai ya uvunjifu wa haki
za binadamu katika vituo hivyo, kwa
33
144 Watoto ambao ni wahanga wa biashara ndugu, mlezi ambaye ni mtu mzima, wakala
haramu ya kusafirisha watu nje ya nchi wa Serikali au wakala aliyethibitishwa au
wasiwekwe rumande au wasiadhibiwe kwa kituo cha malezi katika nchi aliyetoka
kushurutishwa kufanya vitendo haramu. kimekubali na kinaweza kumpatia mtoto
malezi mazuri na ulinzi;
145 Mara tu baada ya mtoto mpweke (c) Kama, kwa sababu zingine, uamuzi wa
kutambuliwa, Nchi zinahimizwa kuteua kumrudisha mtoto hauna manufaa kwa
mtoto, kulingana na tathmini iliyofanywa na
mlezi, au ikibidi, mwakilishi wa shirika
mamlaka halali.
linalohusika na malezi na ustawi wa mtoto
ili awe na mtoto kipindi chote cha mchakato 149 Kwa kuzingatia malengo hayo hapo juu,
wa kuanisha hadhi yake na kufanya ushirikiano kati ya Nchi, mikoa, serikali za
maamuzi. mitaa na asasi za kijamii ukuzwe na
uimarishwe.
146 Mara tu baada ya mtoto mpweke au
aliyetengwa kuwekwa katika sehemu ya 150 Ushirikishaji wa huduma za kibalozi, au
malezi, jitihada zifanyike kutafuta familia inaposhindikana kufanya hivyo, wawakilishi
yake na kuanzisha tena mahusiano kati ya wa kisheria wa nchi aliyozaliwa mtoto
familia na mtoto, kama tu haya yote watafutwe kabla, ikiwa kufanya hivyo kuna
yanafanyika kwa masilahi ya mtoto na kama masilahi kwa mtoto au familia yake.
hayawadhuru wahusika.
151 Wale wanaohusika na ustawi wa mtoto
147 Ili kusaidia kupanga maisha ya baadaye mpweke au aliyetengwa wahakikishe mtoto
ya mtoto mpweke au aliyetengwa kwa na familia yake wanawasiliana mara kwa
namna ambayo inalinda haki zake, mamlaka mara, isipokuwa pale inapokuwa ni kinyume
halali za Nchi na huduma ya jamii zifanye na matakwa ya mtoto au ni dhahiri kwamba
jitihada za kupata nyaraka na taarifa ili ni kinyume na masilahi ya mtoto.
kufanya tathmini ya madhara yanayoweza
kumpata mtoto pamoja na hali ya familia 152 Kumuasili au kumtoa kafala mtoto
yake katika nchi yao. kulingana na sheria ya Kiislamu siyo uamuzi
sahihi kufanyika awali kwa mtoto mpweke
148 Mtoto mpweke au aliyetengwa au aliyetengwa. Nchi zinashauriwa kufanya
hasirudishwe nchini kwake: hivi ikiwa tu jitihada za kufahamu waliko
(a) Kama, baada ya kufanya tathmini ya
wazazi wake, jamaa zake au walezi wa
athari na usalama, kuna kila sababu ya
kuamini kwamba ulinzi na usalama wa kudumu zimeshindikana.
mtoto uko hatarini;
(b) Isipokuwa kama, kabla ya kumrudisha
mtoto, mlezi anayefaa, kama vile mzazi,
37
zao kwa kiwango kinachowezekana kabla ...inatoa ulinzi wa kutosha ili kuhakikisha
ya kuchukua ufumbuzi mwingine wowote kwamba jitihada zote za kuwaunganisha
wa kudumu lisisitizwe. watoto na familia zao zimefanyika, kabla
fumbuzi zingine za kudumu, kama vile
kuasili, hazijatafutwa?
TOVUTI MUHIMU
TOLEO