You are on page 1of 8

SEMINA YA UKATILI DHIDI YA WATOTO NA ULINZI

ENEO: MAIN HALL (MH)- 6th/12)2019.

UTANGULIZI

Ufunguzi

Mkuu wa Idara ya sheria aliwatambulisha wageni waalikwa, pia


alimkaribisha Mtendaji Kata ya Bigwa kuwatambulisha viongozi
alioambatana nao.

UZINDUZI

Saa 09:27 asubuhi, Mgeni rasmi,(mlezi wa wanafunzi) alizindua semina


kwa sala, kisha alijitambulisha na kuwashukuru idara ya sheria na
saikolojia. Mgeni rasmi alifafanua maana ya mtoto na kwanini
tunamzungumzia mtoto.

UWASILISHAJI WA MADA

Shehereshaji alimkaribisha mtoa mada wa kwanza kutoka idara ya sheria,


Madam Norga Komba na kuzumgumzia mada ya kwanza iitwayo Sheria za
watoto.

Maana ya mtoto na sheria zinazomlinda mtoto, alifafanua hili kwa kutumia


kesi ya Mwanasheria Mkuu dhidi ya Rebeca Gyumi (2016), pia alieleza juu
ya haki za watoto kupitia Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 kifungu cha 5 na
sheria ya kimataifa. Pia alimkaribisha Madam Ijukaine kuendelea na mada
ya haki za watoto, haki ya elimu, haki ya kuishi, haki ya kulindwa dhidi ya
ukatili na haki ya kusikilizwa.

Maswali; Saa 10:20

(1) Ni adhabu gani hutolewa endapo utamtelekeza mtoto?


(2) Ni kwa namna gani unaweza kumlinda mtoto ambaye wazazi wake
walitengana?
(3) Ni adhabu gani hutolewa kwa mzazi au mtu alietelekeza familia?
Majibu

Swali la 1 na 3; Adhabu itatolewa kutokana na nguvu ya mamlaka. Sheria


ipo kimya sura ya 13 na 26 lakini ni kosa kisheria.

Swali la 4; Mzazi au mlezi waamue nani wakuishi na mtoto au mtoto


mwenyewe aamue nani wakuishi nae lakini haimzuii mzazi ambae
hawaishi pamoja kutokumwangalia watoto, watamlea mtoto kwa nyanja
zote hata kama hawaishi pamoja.

CHAI

Saa 10:46 – 11:32 asubuhi.

UWASILISHAJI MADA NO:2

Mtoa mada wakili wa serikali kesi za jinai Veronica Chacha. Jinsi ya


kumlinda mtoto mahakamani.

- Ulindwaji wa mtoto anapotenda kosa


- Ulindwaji wa mtoto anapotoa ushahidi mahakamani.

Maswali

1. Sheria inasemaje juu ya mtoto kusingiziwa kosa?


2. Inakuwaje kwa watoto wa mtaani wanapofanya makosa na
kupelekwa mahakamani?
3. Mtoto anaruhusiwa kukata rufaa?
4. Sheria inasemaje juu ya mtoto anayefanya makosa siku 7 kabla ya
kufikisha miaka 18?
5. Sheria inasemaje juu ya mtoto anaeshirikiana makosa na mtu
mzima?
6. Umri unatumikaje kama kigezo Cha kujitetea mahakamani?
Majibu

1. Vizuri haifanyi kazi idara moja, kuna polisi wanakamata kisha


wanapeleleza wanapeleka jalada ofisi ya wakili wa serikali, wakilipitia
wakiona kesi imetengenezwa wanalifunga jalada kama wakiona lipo
sawa wanalifungua mahakamani. Kwa hiyo si rahisi kwa mtoto
kusingiziwa kosa kwasababu sio idara moja pekee inayofanya kazi.
2. Afisa ustawi wa jamii atasimama kama mzazi.
3. Anahaki ya kukataa rufaa kama ataona maamuzi yaliyotolewa na
mahakama hayajamridhisha. Mfano maamuzi yametolewa
mwanafunzi wa sekondari apelekwe shule ya maadilisho, anauwezo
wa kukataa rufaa kwasababu shule ya maadilisho anapelekwa
mwanafunzi wa shule ya msingi.
4. Bado ni mtoto kwasababu hajatimiza miaka 18, kwa hiyo atashtakiwa
na kuhukumiwa kama mtoto wa chini ya miaka 18.
5. Kesi itasikilizwa mahakama ya wilaya au mkoa, kwenye adhabu
watatofautiana, mtoto atahukumiwa kama mtoto na mtu mzima
atapewa adhabu kama mtu mzima.
6. Kifungu cha 15 cha Kanuni ya Adhabu; miaka 10 na 11 atapelekwa
mahakamani ikiwa anauelewa wa alichokifanya kwamba ni kosa,
lakini sheria inamtaka mtoto kuanzia miaka 12 ndio apelekwe
mahakamani.

Kazi na majidiliano

Mnamo saa 12:22 mchana, mshehereshaji aliruhusu watu wakae makundi


makundi na kujadili maswali

1. Mtoto ni nani?
2. Haki za mtoto ni vipi?
3. Kwanini haki za mtoto zinavunjwa katika jamii?
4. Kwanini mtoto anatakiwa kulindwa na jamii?
5. Ni zipi faida za kumlinda mtoto dhidi ya vitendo hatarishi?

Uwasilishaji wa kazi za makundi

Mnamo saa 12:52 mchana, makundi yalianza kuwasilisha majibu ya


maswali.

Kundi la kwanza

Walijibu maana ya mtoto kupitia Sheria ya Mtoto Kifungu namba 4(1)

Kundi la pili

Waliwasilisha majibu ya swali la pili juu ya haki za mtoto

- Haki za kusikilizwa
- Haki za kupewa elimu
- Haki ya kupendwa

Kundi la tatu

Waliwasilisha majibu swali la tatu, sababu za kulindwa haki za watoto

- Jamii haina uelewa juu ya haki za watoto


- Sababu za uchumi
- Mila na desturi

Kundi la nne

Wawasilishaji walijibu swali la nne kwanini mtoto anatakiwa kulindwa na


jamii?

- Kumwandaa mtoto aje kuwa raia mwema


- Kumwepusha mtoto dhidi ya ukatili.

Kundi la tano

Makundi mawili yaliwasilisha majibu ya swali la tano,


(a)- Kumsaidia mtoto katika makuzi yake
- Kumjengea jamii bora dhidi ya vitendo hatarishi.

(b)-Kumsaidia mtoto kuwa na mlezi bora.

- Kumtengenezea uwezo wa kujiamini.

MWISHO

Mkuu wa idara ya Sheria alihitimisha semina mnamo saa 13:10 mchana,


kwa kuwashukuru wageni waalikwa na wote waliohudhiria.
SEMINA YA UKATILI DHIDI YA WATOTO NA ULINZI

ENEO: MAIN HALL (MH) – 7th/12/2019

UTANGULIZI

Ufunguzi

Madam Shangwe kutoka idara ya ushauri nasihi alifungua semina mnamo


saa 09:16 asubuhi, kwa kufafanua juu ya ukatili wa watoto na aina zake,
kwa kutoa ripoti ya utafiti juu ya ukatili kwa watoto Morogoro.

Uwasilishaji wa mada

Madam Shangwe kutoka idara ya ushauri nasihi alifungua semina mnamo


saa 09:16 asubuhi, kwa kufafanua juu ya ukatili wa watoto na aina zake,
kwa kutoa ripoti ya utafiti juu ya ukatili kwa watoto Morogoro.

Maswali; saa 10:23 asubuhi

(1) Tofauti kati ya ukatili wa kimwili na kijinsia.


(2) Ni hatua gani zinachukuliwa pale mtoto anapogundulika kufanyiwa
ukatili?
(3) Wanawasaidiaje watoto ambao wapo vijijini?
(4) Kisaikolojia unamsaidiaje mtoto ambae amefanyiwa ukatili na wazazi
wake?

Majibu

(1) Ukatili wa kimwili upo ndani ya ukatili wa kijinsia tofauti ni kwamba


unafanyiwa ndani ya mwili wako na ukatili wa kijinsia unafanyiwa
kitendo cha ukatili kwasababu ya jinsia yako wewe mwanamke au
mwanaume.
(2) Kuna hatua za kufuata, Polisi atatoa kibali cha matibabu, Daktari
atatoa matibabu kisha watampeleka kwa wataalamu wa saikolojia.
(3) Kuna namna nyingi za utoaji taarifa kwenye jamii mfano kuna
Mtendaji, mwenyekiti wa mtaa au Polisi.

MAPUMZIKO

Mnamo saa 10:51 asubuhi

UWASILISHAJI MADA No.2

Kutoka kwa Afisa ustawi wa jamii wa Morogoro mnamo saa 11:34 asubuhi
Bi Judith. Na kuzungumza mada juu ya majukumu ya ustawi wa jamii na
watoto.

- Wanashughulika na maswala ya Day-Care


- Jinsi ya kumchukua mtoto.

Kwa kufafanua Kifungu namba 17(1) na (3) cha Sheria ya Mtoto (2009)

MASWALI; saa 11:55 asubuhi

(1) Ni hatua zipi zinahitajika kuchukuliwa kwa watoto wanaokaa


mazingira ya sehemu za starehe?
(2) Ustawi wa jamii unawasaidiaje watoto wa mtaani?
(3) Kwa nini mifumo ya serikali haifanyi kazi juu ya watoto?

UWASILISHAJI WA MADA No.3

Mnamo saa 12:21 mchana, Mshehereshaji alimkaribisha Afisa wa Polisi ili


kuzungumzia ulinzi juu ya mtoto. Ambapo alishukuru serikali juu ya utendaji
wa maaskari. Pia Afisa Ustawi aliongezea juu ya makosa ya dhamana.

Maswali

1. Ni utaratibu gani unaotumika kumlinda mtu anaetoa taarifa za


ukatili?
MMENGINEYO

Mnamo saa 12:48 mchana, Dr. Lema kwa niaba ya Idara ya Saikolojia,
alisisitiza juu ya kuwa mabalozi wazuri wa kutetea haki za watoto. Pia
alimkaribisha msemaji wa wazazi kutoka Bigwa kwa neno la shukrani kwa
wandaaji wa semina.

MWISHO
Dr. Lema alitoa neno la shukrani kwa uongozi wa chuo na wanafunzi kwa
mchango wao pamoja na watoa mada wote na alisisitiza kuwaombea wote
kwa Mungu. Na semina ilifungwa rasmi mnamo saa 13:07 mchana kwa
siku mbili.

You might also like