You are on page 1of 24

MTOTO NA

HAKI ZAKE

SHERIA KATIKA LUGHA RAHISI

KIMETOLEWA NA CHAMA CHA WANASHERIA


TANZANIA BARA (TANGANYIKA LAW
SOCIETY) KWA UFADHILI WA TAASISI YA
LEGAL SERVICE FACILITY (LSF)

JANUARI, 2016
MTOTO NA
HAKI ZAKE

SHERIA KATIKA
LUGHA RAHISI

KIMETOLEWA NA CHAMA CHA WANASHERIA


TANZANIA BARA (TANGANYIKA LAW SOCIETY)
KWA UFADHILI WA TAASISI YA LEGAL SERVICE
FACILITY (LSF)

JANUARI, 2016
KIMEANDALIWA NA:
Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara (Tanganyika Law Society)
Kiwanja Na. 391, Mtaa wa Chato
Regent Estate, S.L.P 2148
Dar es Salaam, Tanzania.
Simu +255 22 2775313 / +255 22 5500002
Nukushi +255 22 2775314
Barua Pepe info@tls.or.tz
Tovuti www.tls.or.tz

© Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara, 2016

Waandishi Kimeandikwa na kuhaririwa


• Kaleb Gamaya, chini ya usimamizi wa;
• Mackphason Buberwa Kamati ya Msaada wa Sheria
• Stephen Msechu • Anna Kulaya-Mwenyekiti
• Celina Kibasa • Butamo Philip
• John Mwang’ombola • Daniel Lema
• Alphonce Gura • Donesta Byarugaba
• Judith Kapinga • Fulgence Massawe
• Maria Matui
Wahariri
• Magdalena A. Mlolere, Kamati ya Utafiti na
• Stephen Msechu Machapisho
• Prof. Cyriacus Binamungu
• Dr. Alex Makuklilo
• Dr. Lilian Mongela
• Dr. Ally Possi
• Madeline Kimei
• Daniel Welwel

ii | Mtoto na Haki Zake


Yaliyomo

SHUKRANI ............................................................................... iv
Maana ya Mtoto ......................................................................... 1
Mkataba wa Kimataifa wa Haki za
Mtoto wa mwaka 1989 .............................................................. 1
Mkataba wa Kiafrika wa Haki na Ustawi wa
Mtoto wa mwaka 1990 .............................................................. 3
Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 ................................................ 4
Wajibu wa Mtoto ........................................................................ 5
Wajibu wa Mzazi au Mlezi Kulinda Haki za Mtoto .................... 6
Wajibu wa Jamii ......................................................................... 7
Sheria ya Mtoto na Ajira kwa Watoto ......................................... 7
Mahakama ya Watoto ................................................................. 8
Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 ................................................. 9
Cheti cha Mtoto cha kuzaliwa .................................................... 10
Mtoto aliye kwenye mgogoro na Sheria ....................................... 10
Makosa Ambayo Mtoto Anaweza Kufanya .................................. 11
Ulinzi wa Mtoto na Maslahi Yake Katika Mfumo wa
Haki Jinai .................................................................................... 12
Uthibitisho wa Nasaba ya Mtoto na Matokeo yake...................... 15
Kwanini Uthibitisho wa Nasaba? ................................................. 15

Mtoto na Haki Zake | iii


SHUKRANI
Kamati ya Msaada wa Sheria ya Chama Cha Wanasheria Tanzania
Bara inatoa shukrani za pekee kwa wadau mbalimbali kutoka
mashirika ya kutoa msaada wa kisheria kwa ushauri wao maridhawa
katika kuandaa kijarida hiki cha Mtoto na Haki Zake .

Pili, Shukrani ziende kwa Taasisi ya Legal Service Facility (LSF) kwa
ufadhili na ushauri wa kipekee katika kuandaa kijarida hiki.

Pia Kamati inatoa shukrani za dhati kwa Baraza la Uongozi la Chama


cha Wanasheria chini ya Rais Charles Rwechungura na Sekretariat ya
Chama chini ya Kaleb Gamaya kwa rasilimali na ushirikiano waliotoa
katika kukamilisha kazi hii muhimu kwa taifa letu inayolenga kukuza
uelewa wa sheria miongoni mwa wananchi.

iv | Mtoto na Haki Zake


Maana ya Mtoto
Kwa mujibu wa Sheria ya mtoto ya mwaka 2009 na Mkataba
wa Kimataifa wa Haki za Mtoto wa mwaka 1989, mtoto ni kila
banadamu aliye chini ya umri wa miaka 18.
Sababu za kuwa na ulinzi wa haki za mtoto ni pamoja na;
➣ Watoto ni binadamu, wana haki sawa;
➣ Watoto hawana sauti ya kujisemea au hawana uwezo wa
kupigania haki zao wenyewe;
➣ Kuwepo kwa wimbi kubwa la ukiukwaji wa haki za watoto
mfano ukatili dhidi ya mtoto, utesaji na ubakaji.

Mkataba wa Kimataifa wa Haki za


Mtoto wa mwaka 1989
Huu ndio mkataba mkuu unaoshughulikia haki za watoto duniani
kote. Mkataba huu ulipitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Novemba 1989 na kuanza kufanya kazi tarehe 2 Septemba 1980.
Tanzania imeukubali Mkataba huu tarehe 10 Julai 1991.

Haki za mtoto zinazolindwa na mkataba huu


Kwa ujumla, haki za mtoto zinazolindwa na mkataba huu zinaweza
kugawanywa katika makundi makuu manne:-
(i) Haki ya kuishi kwenye mazingira mazuri ikiwemo kupata lishe
bora;
(ii) Haki ya kuendelea, kukua ikiwemo haki ya kupata elimu, haki
ya kucheza;
(iii) Haki ya kulindwa na wazazi/walezi/jamii au serikali dhidi ya
madhara;
(iv) Haki ya kushiriki katika masuala yanayomgusa.

Unyonyaji wa Mtoto
Hili ni tatizo kubwa duniani kote ambalo mkataba huu unataka

Mtoto na Haki Zake | 1


kulitokomeza. Unyonyaji wa watoto mara nyingi unakuwa katika
maeneo makuu mawili ambayo ni (i) unyonyaji wa kiuchumi (ii)
unyonyaji wa kimapenzi

(i) Unyonyaji wa Kiuchumi


Mara nyingi unyonyaji huu kutokea kwa kutumia watoto kibiashara,
kuwafanyisha kazi za nyumbani , mashambani , migodini, sehemu
za kuuza vileo, migahawani, hotelini . Ajira kwa watoto daima
huambatana na:-
➣ Ujira mdogo au kutolipwa ujira kabisa;
➣ Masaa marefu ya kufanya kazi;
➣ Kazi za hatari kwenye hali mbaya kiafya;
➣ Kupewa vitisho vya kupigwa na mwajiri.

Unyonyaji wa kiuchumi mara nyingi unasabishwa na umaskini wa


wazazi wa mtoto na hususan pale inapokosekana huduma za kijamii
kwa watoto kama vile elimu, chakula na afya.

(ii) Unyonyaji wa Kimapenzi


Huu unajumuisha kutumia watoto kufanya ngono kwa ajili ya utalii,
umalaya wa watoto, watoto kupigwa picha za ngono na kusafirisha
watoto kwenda sehemu (nchi) nyingine kwa ajili ya kufanya biashara
ya ngono. Vyanzo vya unyonyaji huu ni vingi na vinatofautiana.
Katika mazingira ya Tanzania, chanzo cha tatizo hili ni tamaa ya
kujipatia pesa kwa kupitia watoto, utandawazi, umaskini na ubaguzi
dhidi ya wanawake.

(iii) Aina nyingine za Unyonyaji


Japokuwa unyonyaji wa kimapenzi na kiuchumi ndio aina kuu
mbili za unyonyaji dhidi ya watoto, mkataba huu pia unazitaka nchi
wanachama kumlinda mtoto dhidi ya aina nyingine zote za unyonyaji
ambazo zinaathiri ustawi wa mtoto.

2 | Mtoto na Haki Zake


Mkataba wa Kiafrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto wa
mwaka 1990
Mkataba huu ulipitishwa na wakuu wa nchi na serikali za Umoja
wa Nchi huru za Afrika (sasa hivi unajulikana kama Umoja wa
Afrika) Julai 1990. Mkataba huu umeanza kufanya kazi tarehe 29
Novemba 1999. Hadi Agosti 2004, nchi 35 kati ya nchi 53 za Afrika
zimeuridhia, Tanzania imesaini mkataba huu tarehe 3/10/1998 na
kuuridhia tarehe 16/03/2003.

Mambo Muhimu juu ya Haki za Mtoto kwa Mujibu wa Mkataba


huu
Kwa ujumla, mambo muhimu yaliyoainishwa ndani ya mkataba huu
ni;-
➣ Kanuni za msingi: haki za kiafrika ndani ya mkataba huu
zimejengwa katika kanuni kuu nne kama ilivyo kwa Mkataba
wa Kimataifa wa Haki za Mtoto wa mwaka 1989. Kanuni hizo
ni:- maslahi makuu ya mtoto, kutobaguliwa, ushiriki na kukua
na kudumu kwa mtoto.
➣ Haki za kiuchumi, kijamii na kiutamaduni nazo zinatambuliwa
sawa na haki za kiraia na kisiasa.
➣ Haki za kuwalinda mtoto kuzingatia utamaduni, historia, mila
na desturi za kiafrika na pia kulinda umoja na mshikamano
wa Afrika. Dibaji ya mkataba huu inazitaka nchi za kiafrika
kuangalia utamaduni, historia na maadili ya kiafrika katika
kutelekeza majukumu yao chini ya mkataba huu.
Mila na tamaduni potofu: Mila na tamaduni potofu za kiafrika
zinazoathiri ustawi, utu na maendeleo ya mtoto hasa zile zinazohusu
afya na maisha ya mtoto zimepigwa marufuku na Mkataba huu. Hii
ndiyo mojawapo ya sifa kuu za Mkataba wa haki za mtoto wa kiafrika.

Baadhi ya Sheria Zinazolinda Haki za Mtoto Tanzania


Kuna sheria nyingi ambazo zinalinda haki za mtoto nchini Tanzania.
Baadhi ya sheria hizi ni:-

Mtoto na Haki Zake | 3


Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009
Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009 inashughulikia haki
za watoto Tanzania. Sheria hii inajumuisha mambo mbalimbali
ya kukuza, kulinda, na kuhifadhi ustawi wa mtoto; masharti ya
unajibishaji wa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa; masuala ya kulea,
kuasili na uangalizi. Pia inatoa maelekezo na masharti yanayohusu
mtoto anapokuwa katika mgogoro na sheria. Sheria hii inatumika
kutetea masuala yote ya kuboresha, kulinda na kuhifadhi ustawi wa
mtoto pamoja na haki zake.

Kwa mujibu wa sheria hii mtoto ni mtu yeyote mwenye umri chini
ya miaka kumi na nane. Sheria hii inafanunua zaidi kuwa mtoto ni
pamoja na mtoto yatima, mtoto aliye katika mazingira magumu,
mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa, mtoto wa kuasiliwa, na mtoto
anayelelewa katika vituo vya kulelea watoto.

Haki za Mtoto kwa Mujibu wa Sheria ya Mtoto


➣ Haki ya kuishi
➣ Haki ya kupumzika
➣ Haki ya kuheshimiwa na kuthaminiwa
➣ Haki ya kutokubaguliwa
➣ Haki ya jina na utaifa
➣ Haki ya kuishi na wazazi wake
➣ Haki ya kupata huduma bora za elimu, malazi matibabu kwa
ajili ya ustawi wake
➣ Haki ya kushiriki michezo na shughuli za kiutamaduni
➣ Haki ya huduma za pekee kwa walemavu
➣ Haki ya kunufaika na kutumia kwa uangalifu mali za wazazi
wake
➣ Haki ya kutoa maoni, mawazo kusikilizwa na kutoa maamuzi
ya ustawi wake
➣ Haki ya kutoajiriwa katika ajira zenye madhara
➣ Haki ya kulindwa dhidi kudhalilishwa kijinsia.

4 | Mtoto na Haki Zake


Wajibu wa Mtoto
Wajibu wa Jumla wa Mtoto
Pamoja na haki za mtoto pia anawajibika katika maeneo yafuatayo;-
➣ Kufanya kazi kwa ajili ya mshikamo wa familia;
➣ Kuwaheshimu wazazi, walezi, wakubwa wake wote na
atawasaidia pale inapohitajika;
➣ Kuhudumia jamii yake na taifa lake kwa uwezo wake wote
kimwili na kiakili kadiri ya umri na uwezo wake;
➣ Kutunza na kuimarisha mshikamo wa jamii na taifa;
➣ Kutunza kuimarisha mambo mema ya utamaduni wa jamii na
taifa kwa ujumla katika uhusiano na wanajamii au taifa.
➣ Mtoto yeyote aliyepata mafunzo ya ufundi anawajibu wa
kufuatilia kwa makini na kukubali kwa uaminifu, mafunzo
aliyopewa na Mwalimu kwa kuhudhuria mafunzo na kuzuia
uharibifu wowote wa makusudi na kutoharibu mali za mtoa
mafunzo.

Wajibu wa Mzazi au Mlezi kutunza mtoto


Chini ya Sheria ya Mtoto (2009) mzazi, mlezi, ndugu au mtu au
taasisi yeyote inayomlea mtoto ni wajibu wa kumtunza mtoto kwa
kumpatia mtoto haki na mahitaji yafuatao:
➣ Chakula
➣ Makazi
➣ Mavazi
➣ Matibabu ikiwa ni pamoja na kupata chanjo stahiki na kwa
wakati
➣ Elimu na malezi bora
➣ Uhuru
➣ Haki ya kucheza na kupumzika

Mtoto na Haki Zake | 5


Wajibu wa Mzazi au Mlezi Kulinda Haki za Mtoto
Kila mzazi ana kazi na wajibu, uwe wa kisheria, kisera, kimkakati,
kimpango, kimalezi au vinginevyo kumwangalia mtoto wake kwa
kufanya yafuatayo:
➣ Kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya kiubaguzi, unyanyaswaji,
kuwekwa katika Mazingira magumu na hatarishi ya kiroho au
kimwili.
➣ Kutoa malezi, ulinzi, msaada na matunzo ya mtoto ili
kuhakikisha ustawi na makuzi bora ya mtoto.
➣ Kuhakikisha kuwa pale mzazi asipokuwepo basi mtoto yuko
chini ya uangalizi wa mtu mwenye uwezo wa kumlea.
➣ Kutunza na kuhifadhi desturi mustakabali wa jamii na taifa.
➣ Kutunza na kuhifadhi mila sahihi za jamii na taifa lake kwa
ujumla kama ilivyo kwa wanajamii na Watanzania wengine.

6 | Mtoto na Haki Zake


Wajibu wa Jamii
Sheria imeipa jamii jukumu la kutoa taarifa pale ambapo mwanajamii
ana taarifa au ushahidi kuwa haki za mtoto zinavunjwa na mzazi,
mlezi, ndugu au mtu yeyote katika jamii.
➣ Mtu yeyote hapaswi kumbagua mtoto kwa kuzingatia jinsi,
utaifa, umri, dini, lugha, siasa, ulemavu, afya, desturi, uzawa,
mazingira aliyokulia, kiuchumi, kuwa mkimbizi na mengineyo.
➣ Mtu yeyote hapaswi kumnyima mtoto haki ya jina, uraia na
haki ya kuwajua wazazi wake wa kumzaa na ndugu zake.
➣ Mtu yeyote hapaswi kumnyima mtoto haki ya kuishi na wazazi
wake, walezi au familia na kukua katika mazingira salama na ya
amani.

Sheria ya Mtoto na Ajira kwa Watoto


Chini ya sheria hii mtoto mwenye umri wa kuanzia miaka 14 na
zaidi ana haki ya kufanya kazi nyepesi na kupata malipo stahiki.
Ieleweke kuwa, kazi nyepesi ni zile ambazo haziathiri afya ya mtoto,
hazikwamishi maendeleo yake kielimu au makuzi yake.Kazi yoyote
itahesabiwa kuwa ya kinyonyaji endapo itakuwa na viashiria au
mambo yafuatayo:
➣ Inayoathiri afya na ukuaji wa mtoto.
➣ Inayozidi masaa sita kwa siku.
➣ Isiyoendana na umri wake.
➣ Isiyompa mshara wa kujitosheleza.
➣ Mtoto hatoajiriwa au kuhusishwa na mikataba ya kazi
inayomtaka mtoto kufanya kazi usiku.

Pia Mtoto ana haki ya kupokea malipo ya mshahara kulingana na kazi


aliyofanya. Sheria imetoa adhabu mbalimbali kwa wale watakaovunja
haki za mtoto mfano :
➣ Mtu yeyote atayemsababishia au kumpeleka mtoto kupata
mateso atakuwa ametenda kosa na atatiwa hatiani na kulipa
faini isiyozidi milioni tano au kifungo kisichozidi miezi sita au
vyote kwa pamoja.
Mtoto na Haki Zake | 7
➣ Mmiliki au mpangaji yeyote anayeendesha au anayesimamia
baa, kumbi za muziki au kumbi za starehe endapo akimruhusu
mtoto kuingia maeneo hayo atakuwa ametenda kosa na
atatatiwa hatiani na atapaswa kulipa faini isiyopungua shilingi
milioni moja na isiyozidi milioni tano za kitanzania au kifungo
kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja.

Mahakama ya Watoto
Mahakama ya Watoto imeanzishwa Kisheria ili kuhakikisha mashauri
yote yanayohusu watoto yanasikilizwa na kuamuliwa kwa kuzingatia
taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto. Hivyo;
➣ Mahakama ya Watoto itasikiliza na kuamua mashauri ya jinai
dhidi ya mtoto.
➣ Maombi yanayayohusu matunzo ya mtoto.
➣ Mahakama ya Watoto itaongozwa na Hakimu Mkazi.
➣ Mashauri yataendeshwa kwa faragha.
➣ Ni haki ya mzazi, mlezi au ndugu kuwepo; Ofisa wa Ustawi wa
Jamii atakuwepo wakati wa kuendesha mashauri.
➣ Mtoto atakuwa na haki ya kuwa na ndugu wa karibu au
kuwakilishwa na Wakili.
➣ Haki ya kukata rufaa itafafanuliwa kwa mtoto ili aielewe.
➣ Mtoto atakuwa na haki ya kutoa ufafanuzi na maoni.
➣ Uwepo wa Afisa Ustawi wa Jamii unahitajika katika Mashauri
yote yamhusuyo mtoto.

Angalizo: Shauri la mtoto isipokuwa shauri la mauaji litasikilizwa


mara moja kwa muda wa siku moja na kutolewa uamuzi siku hiyo
hiyo au ndani ya muda mwafaka ambao utazingatia maslahi ya mtoto.

Sheria ya Makosa ya Kujamiiana ya mwaka 1998


Kwa ujumla, sheria hii inamlinda mtoto dhidi ya unyonyaji wa
kimapenzi, udhalilishaji wa kijinsia kama vile ubakaji, ulawiti, uwekaji
kinyumba wa watoto na ukeketaji wa watoto wa kike. Adhabu kali
zimewekwa na sheria hii kwa makosa yaliyoanishwa ndani yake.

8 | Mtoto na Haki Zake


Sheria ya Elimu ya mwaka 1978
Sheria hii, pamoja na mengineyo, inaeleza kuwa ni wajibu wa mzazi/
mlezi kumpeleka mtoto yeyote wa kike au wa kiume mwenye umri
wa miaka saba shule ya msingi. Elimu ya msingi ni lazima kwa kila
mtoto nchini Tanzania.

Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971


Sheria hii inaelezea kuwa ni wajibu wa baba kuwatunza watoto wake
kwa kuwapatia elimu, matibabu, malazi na mavazi. Hata hivyo
pale ambapo baba atakuwa ni mgonjwa,au mama anaingiza kipato
atakuwa na wajibu wa kuwatunza watoto kwa kuwapatia mahitaji yao
ya muhimu.
Pia inatamka kuwa ni kosa la kisheria kumuozesha mtoto wa kike
aliye chini ya umri wa miaka 16. Iwapo mtoto wa chini ya miaka 14
ataozeshwa basi ni lazima kuwepo na kibali cha mahakama. Mtoto wa
umri wa miaka 15 anaweza kuozeshwa tu pale ambapo kuna idhini ya
wazazi au walezi wake.
Pamoja na masharti hayo ya kisheria kuruhusu mtoto kuolewa akiwa
na umri wa miaka 15 ni mojawapo ya mapungufu ya sheria. Hii, kwa
sababu inakinzana na sheria za kimataifa na hata sheria ya makosa
ya kujamiana inayomlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ngono katika
umri wa chini ya miaka 18.
Pale ambapo msaidizi wa kisheria ataona kuna matukio ya kuwaozesha
watoto wa kike atapaswa kutoa taarifa polisi , Dawati la Jinsia na
Watoto au awashauri wazazi/ walezi wa mtoto athari za kumuoza
mtoto wa kike katika umri mdogo ikiwa ni pamoja na kumnyima
haki ya elimu, matatizo anayoweza kupata iwapo atapata ujauzito
ikiwa ni pamoja na kifo wakati wa kujifungua.

Mtoto na Haki Zake | 9


Cheti cha Mtoto cha kuzaliwa
Sheria inamtaka kila mzazi kuhakikisha mtoto ana cheti cha kuzaliwa.
Cheti cha kuzaliwa ni haki kwa mtoto anayezaliwa. Wazazi wana
wajibu wa kufuatilia cheti cha kuzaliwa. Cheti cha kuzaliwa kinaweza
kufuatiliwa kuanzia katika hospitali aliyojifungulia mama na kupewa
hati ya usajili wa mtoto ambayo ataweza kuitumia katika kupata cheti
cha kuzaliwa kutoka katika ofisi ya msajili wa vizazi na vifo (RITA)
ambazo zitakuwa katika ofisi ya wilaya ya mahali hapo. Huduma ya
kusajili mtoto aliyezaliwa ni bure, na kupata cheti cha kuzaliwa ni
shilingi 3,500 kwa watoto chini ya umri wa miaka 5.
Umuhimu wa cheti cha kuzaliwa ni:-
➣ Cheti cha kuzaliwa kinamsaidia mtoto kuandikishwa shule bila
usumbufu
➣ Utambulisho wa utaifa wa mtoto
➣ Cheti kinaonyesha wazazi wa mtoto

Mtoto aliye kwenye mgogoro na Sheria


Mtoto aliye kwenye mgogoro na sheria ni yule ambaye amefanya
vitendo ambavyo ni makosa ya jinai chini ya Sheria ya kanuni za
makosa ya jinai kama vile kuiba, kutukana, kudhuru mwili, na
kadhalika. Makosa hayo pia yanaweza kuwa yale ambayo hayaendani
na maadili ya jamii husika.

Uhamasishaji wa Maslahi na Ustawi wa Mtoto Aliye kwenye


mgogoro na Sheria
Mfumo wa sheria ya haki jinai unatakiwa kulinda na kuhamasisha
ustawi wa mtoto na kuhakikisha kwamba haki muhimu za mtoto
aliye kwenye mgogoro na sheria zinalindwa.

Mfumo na sheria za haki jinai unatakiwa kuwa wa usawa kwa mtoto


na kuhakikisha mtoto anakuwepo kwenye hatua zote za ufikiaji haki,

10 | Mtoto na Haki Zake


ikiwa ni pamoja na kuhudhuria mahakamani. Lakini pia ratiba za
mahakama ya watoto zinatakiwa zizingatie kumpatia mtoto nafasi ya
kuhudhuria shuleni.

Msaidizi wakisheria anaweza kutoa taarifa kwa Afisa wa Ustawi wa


jamii kama mtoto huyo amechanganywa na watu wazima kwenye
kesi yake, na kesi hiyo inasikilizwa katika mahakama ya wazi. Endapo
ana taarifa juu ya kuwepo mahabusu /rumande kwa mtoto aliye
katika mgogoro wa sharia ambaye amechanganywa na watu wazima
basi anapaswa kutoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Kituo ili jitihada
za makusudi zichukuliwe ili kumtoa mtoto huyo na watuhumiwa
ambao ni watu wazima. Endapo msaidizi wa kisheria anajua wazazi/
walezi wa mtoto na anazo taarifa juu ya mtoto kukamatwa na polisi
basi anaweza kuwasiliana na wazazi/ walezi wa mtoto ili waweze
kumuwekea dhamana.

Makosa Ambayo Mtoto Anaweza Kufanya


Watoto wengi wanaofanya makosa ya kuvunja sheria ni wale ambao
wanaishi kwenye mazingira magumu na hatarishi mfano mitaani.
Makosa mengi ambayo watoto wanafanya ni:: kubaka au kulawiti
watoto wenzao, wizi, kudhuru mwili, kuvunja na kuiba, kuwapa
ujauzito wanafunzi wenzao.
Angalizo: Mtoto ambaye anafanya makosa haya lakini ana umri
chini ya miaka 10 hawezi kushitakiwa chini ya sheria ya kanuni za
adhabu, wala hatakiwi kukamatwa na polisi lakini anaweza kuonywa,
kushauriwa na kuwa chini ya uangalizi wa afisa ustawi wa jamii.
Vitendo ambavyo mtoto anafanyiwa

Lakini pia mtoto anaweza kufanyiwa vitendo kama: kutelekezwa


au kutopatiwa matunzo na wazazi/walezi, kupigwa, kubakwa,
kulawitiwa, na kupewa ujauzito. Watoto wanahitaji ulinzi kwani
vitendo hivi vingi huanzia majumbani. Ni muhimu wazazi kujua
kuwa vitendo hivi wanavyofanyiwa watoto ni uvunjaji wa sheria.

Mtoto na Haki Zake | 11


Wapi pa Kupata Nafuu?

Kesi au masuala yote yanayohusu watoto yanahusu pia jamii yote,


jeshi la polisi, madaktari, serikali za mitaa, na maafisa wa ustawi wa
jamii katika kila serikali za mitaa.

Mahakama ya watoto itahusika katika mambo yote yanayohusu


watoto. Ikiwa mtoto amefanyiwa vitendo vilivyotajwa hapo juu,
wazazi/mwanajamii anaweza kutoa taarifa katika serikali ya mtaa,
ambayo kwa kushirikiana na afisa ustawi wa jamii, wana wajibu wa
kufuatilia ulinzi na ustawi wa mtoto huyo aliyedhurika. Ikihitajika
kwenda mahakamani, afisa ustawi ana wajibu wa kupeleka maombi
mahakamani juu ya nafuu ya au ulinzi wa mtoto huyo.
Angalizo: Serikali ya mtaa ina wajibu kutokana na sheria ya mtoto,
kuwatafutia na kuwapa hifadhi watoto ambao wametelekezwa au
kukosa makazi.Pia ina wajibu, kwa kushirikiana na afisa ustawi wa
jamii, kuwatafuta wazazi waliotelekeza watoto na kuwarudisha, au
kutoa amri ya matunzo.

Ulinzi wa Mtoto na Maslahi Yake Katika Mfumo wa


Haki Jinai
Mfumo wa haki jinai wa mtoto unaanzia pale atakapokamatwa na
kupelekwa kituo cha polisi, Upelelezi, kufikishwa katika mahakama
hadi maamuzi. Katika mfumo wote huu, watakaohusika ni mzazi/
mlezi, askari polisi, afisa ustawi wa jamii na Mahakama yenyewe.

Wajibu wa Mzazi

➣ Mzazi/mlezi/mtu mwenye jukumu la uangalizi wa mtoto ana


wajibu wa kuhakikisha mtoto anaendelea kupata mahitaji yake
muhimu kama vile kwenda shule.
➣ Ana wajibu kisheria wa kuhudhuria mahakamani wakati wote
shauri linapoendelea.

12 | Mtoto na Haki Zake


Wajibu wa Askari polisi
➣ Askari polisi ana wajibu wa kuwasiliana na afisa ustawi wa jamii
wa eneo hilo juu ya mtoto yeyote aliyekamatwa na kurekodi
taarifa za familia ya mtoto huyo.
➣ Ana wajibu wa kumruhusu mtoto huyo kuwa nje ya mahabusu
kwa udhamini wa mzazi/mlezi au ndugu, au bila dhamana
yoyote.
➣ Askari Polisi ana wajibu wa kumtenganisha mtoto rumande
tofauti na watu wazima
Wajibu wa Afisa wa ustawi wa Jamii
➣ Afisa ustawi wa jamii ana wajibu wa kufuatilia kituoni kuona
kama kuna watoto watuhumiwa.
➣ Ana wajibu wa kuwasiliana na Askari polisi juu ya shauri lolote
linalomuhusu mtuhumiwa ambaye ni mtoto.
➣ Pia ana wajibu wa kulinda maslahi ya mtoto katika mfumo huo
wote na kuhakikisha haki zake zinazingatiwa.

Mtoto na Haki Zake | 13


Malezi ya Kambo na Kuasili Mtoto
Malezi ya kambo: Ni malezi anayopatiwa mtoto na taasisi au mtu
wa kawaida ambaye si mzazi wa mtoto. Maombi ya kutoa malezi ya
kambo hupelekwa kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii kupitia Afisa
Ustawi wa jamii aliyepo ndani ya wilaya yako.

Kuasili mtoto

Ni kitendo cha kisheria kwa aidha mtu mmoja au mke na mume


kumchukua mtoto asiyekuwa wake kwa kumzaa na kumfanya awe
wake/wao kwa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria.

Sheria ya Mtoto inaongelea kuhusu Malezi ya Kambo na Kuasili kwa


kutaja nani anaweza kuasili. Mtu anayeruhusiwa kuasili ni;-

➣ Mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka 21.

➣ Awe ni mtu mwenye maadili na utu na anaweza kuwa mlezi wa


kambo kwa mtoto, na kwamba.

➣ Mtu huyo si mzazi wa mtoto lakini amehiari na ana uwezo wa


kutunza mtoto.

Maombi yote ya kuasili yawasilishwe Mahakama Kuu na katika


kuasili mtoto ambaye mtu anayeomba ana nasaba naye, maombi
yatapelekwa Mahakama ya Hakimu Mkazi au Mahakama ya Wilaya.

Sheria ya mtoto imeweka hitaji la kuridhia kwa wazazi, walezi au ndugu


za mtoto napale ambapo ndugu, mzazi au mlezi walimnyanyasa mtoto
basi hakutakuwa na haja ya kupata ridhaa yao au pale ambapo wazazi,
ndugu, mlezi hawajulikani walipo au hawana uwezo wa kuridhia basi
hakutakuwa na haja yakupata ridhaa.

14 | Mtoto na Haki Zake


Uthibitisho wa Nasaba ya Mtoto na Matokeo yake
Maana ya nasaba: Ni mfanano wa kijinsi, yaani viambata katika mwili.
Mfanano huo unaweza kuwa katika asilimia chache lakini ndio unaothibitisha
undugu.
Kwanini Uthibitisho wa Nasaba?
Sheria inatambua matatizo yaliyopo katika jamii ikiwemo ulaghai katika ndoa,
matatizo ya kubadilishiwa mtoto hospitalini, matatizo katika mirathi
kwa baadhi ya ndugu kukana nasaba za watoto wa ndugu za marehemu
ili mradi wawanyime urithi. Kwa kujielekeza katika matatizo kama haya,
ilionekana ni vyema suala la uthibitisho wa nasaba liainishwe katika Sheria
ya mtoto. Hata hivyo, masuala ya kupima nasaba kwa kufanya ‘DNA test’
katika ngazi ya mahakama yatafanywa kwa ruhusa ya Mahakama Kuu tu. Hali
kadhalika, sheria ya upimaji wa nasaba na kanuni zake zinaelekeza kuwa; ikiwa
wahusika yaani baba na mama, mbele ya Afisa Ustawi au polisi wamekubaliana
kufanya uthibitisho wa nasaba kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, basi afisa huyo
ataijulisha mamlaka hiyo ya upimaji. Vinginevyo, nje ya utaratibu huo, ni
Mahakama Kuu peke yake ndiyo yenye kutoa idhini ya upimaji iwapo
suala hilo litakuwa limefikishwa katika ngazi yoyote ya mahakama.

Endapo itatokea mojawapo wa wazazi wanataka kutumia njia hii


ili kuthibitisha nasaba ya mtoto msaidizi wa kisheria atapaswa
awashauri waende kwa Afisa ustawi wa Jamii au wakili ambaye
atapeleka maombi yao kwa Mkemia Mkuu wa serikali.

Mtoto na Haki Zake | 15


16 | Mtoto na Haki Zake
Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara
Kiwanja Na. 391, Mtaa wa Chato
Regent Estate, S.L.P 2148
Dar es Salaam, Tanzania.
Simu: +255 22 2775313 /+255 22 5500002
Nukushi: +255 22 2775314
Barua Pepe: info@tls.or.tz
18 | Mtoto na Haki Zake Tovuti: www.tls.or.tz

You might also like