You are on page 1of 22

CEO_CRYPTO25

CRYPTO
NI
MCHONGO
Mwandishi

@CEO CRYPTO

Phonenumber
+255625761850

@CEO_CRYPTO25 X (formerly Twitter)

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

Kwenye ulimwengu wa crypto nina safari ndefu sana na kuna mengi


ambayo nimejifunza na kuyajua nikiwa ndani ya huu ulimwengu wa
crypto kwangu naamini ilikuwa moja ya hatua muhimu na kubwa
maishani kwangu.

Natamani kila nilichojifunza na kukipata kwenye huu ulimwengu wa


crypto na wewe ukipate pia au ukifahamu pia inaweza kusiwe na vingi
ambavyo unaweza kuvipata ndani ya hiki kitabu ila naamini hutotoka bure
ndani ya hiki kitabu lazima kuna kitu kipya utajifunza.

Kwakuwa maarifa mengi ya crypto yapo kwenye mfumo wa lugha za


kigeni hasa kiingereza kitu ambacho kinasababisha watumiaji wengi wa
lugha ya Kiswahili kukosa taarifa na maarifa sahihi ya cryptocurrency
kwa ujumla hii ndo sababu iliyonituma kuandika hiki kitabu cha
CRYPTO NI MCHONGO nimeandika kwaajili yako mswahili
mwenzangu kwa lugha rahisi kabisa ya Kiswahili.

Naamini lazima utaelewa tu kuhusu cryptocurrency kwa ujumla na


mambo yake yote yaliyomo kwenye cryptocurrency.

Kwasababu nimejitahidi kufanya tafiti mbalimbali pamoja na uzoefu


wangu ambao niliokuwa kwenye sekta hii ya sarafu za kimtandao
(Cryptocurrency).

Soma hiki kitabu hadi mwisho kimeandikwa kwaajili yako wewe tu. Na
naamini aliyekupa hajakuuzia hiki kitabu nimekitoa Bure kabisa kwaajili
yako wewe. Ni bure kwahiyo na wewe utakitoa Bure kwa wengine ili
elimu ifike mbali zaidi na usisahau kuwapa hiki kitabu rafiki zako angalau
wawili.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

Maarifa ya Ndani
1. Maana ya Cryptocurrency (Sarafu Mtandao)

2. Mfumo wa Blockchain

3. Sarafu ya Bitcoin

4. Kutambua Fursa za Cryptocurrency


-ajira za cryptocurrency
-kutengeneza hela bila kufanya chochote
-kushikilia sarafu mtandao (hold coins)
-Kutengeneza hela kwenye crypto bila mtaji wowote

5. Kutambua masoko ya Cryptocurrency


-Soko la kubadili sarafu mtandao (Crypto Exchange)
-Mkoba wa sarafu mtandao (Crypto Wallet)

6. Namna ya kutambua eneo lako


-Kujenga profile yako binafsi
-Namna ya kukuza portfolio yako
-Namna bora ya kuwekeza kwenye crypto

7. Trading za Cryptocurrency
-Jinsi ya kulinda mtaji (Risk Management)
-Jinsi ya kumiliki hisia zako (Emotional control)
-Uchambuzi wa mifumo (Technical analysis)
-Uchambuzi wa Taarifa (Fundamental analysis)

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

1. Maana ya Cryptocurrency (Sarafu Mtandaoni)


Cryptocurrecy ni neno la kiingereza lakini kwenye Kiswahili ambacho sio
fasaha linatambulika kama Sarafu za kimtandao au sarafu za kidijitali sio
tafsiri sahihi ya neno ila angalau inatupa mwanga wa kujua cryptocurrecy ni
nini?

Kama nilivyotoa tafsiri isiyo rasmi ya cryptocurrency kuwa ni sarafu za


kimtandao au kidijitali na nikisema sarafu namaanisha ni fedha kwahiyo
vilevile tunaweza tukaziita ni fedha za kimtandao yani ni fedha ambazo ili
uzitumie lazima uwe na kifaa chenye mtandao na hizi sio kama fedha zetu za
kawaida tunazotumia kila siku hizi Crypto zipo kwenye mfumo mwingine
kabisa ambao unajiendesha wenyewe.

Cryptocurrency au sarafu mtandao ni fedha ambazo zipo kwenye mfumo wa


kimtandao ambao ni mfumo ambao unajiendesha wenyewe na hauwezi
kuingiliwa na mtu yeyote.

Sarafu mtandao zipo aina nyingi sana duniani ni zaidi ya aina 1000 za sarafu
na sarafu ya kwanza kabisa kuundwa inaitwa Bitcoin na ndo sarafu yenye
watumiaji wengi zaidi duniani kuliko yoyote ile iliyopo ulimwenguni.

Kitu kingine cha kumkumbuka ni kuwa Cryptocurrency zipo kwa matumizi


tofauti tofauti zipo za kwaajili ya michezo, huduma za hospitali, malipo
madogo madogo, elimu na mengine mengi ila zote lengo kuu nikufanya
malipo ya huduma zitolewazo kwenye hayo maeneo mengineyo ambayo
yanahitaji matumizi ya cryptocurrency.

Cryptocurrency (sarafu mtandao) zinasimama kama mbadala sahihi wa


matumizi ya kifedha kuendana na mabadiliko ya teknolojia yanayoendelea
kufanyika katika kipindi hiki Sarafu mtandao inabaki kuwa ni njia sahihi ya
kuenda kwenye mifumo yetu ya kifedha na kiuchumi kwakuwa sarafu
mtandao (cryptocurrency) zimeundwa kuwa wazi.

Kuna namna tunaweza sema kuwa sarafu mtandao (cryptocurrency) ni fedha


zetu kwa wakati mfupi ujao ni hakika sio muda tutahama kwenye mfumo
wetu wa sasa wa kifedha na kuhamia kwenye sarafu mtandao
(cryptocurrency) sababu zipo nyingi ila kubwa zaidi ni ukuaji wa hili soko
kwa kasi kubwa sana yani miaka kwa miaka soko linakuwa kubwa sana.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

SIFA ZA SARAFU MTANDAO (CRYPTOCURRENCY)

1. Urahisi wa kufanya malipo popote.

2. Unaweza ukazimiliki zikiwa na thamani ndogo lakini zikapanda.

3. Usalama mkubwa sio rahisi kudukuwa.

4. Urahisi wa kutunza bila gharama au makato yoyote.

5. Urahisi wa kutuma cryptocurrency kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

6. Zinajiendesha zenyewe kwenye mifumo ya kompyuta.

7. Unaweza kutuma miamala bila kujulikana wewe ni nani au unamtumia nani


(Confidential)

Kuna Sifa nyingi za Sarafu mtandao (Cryptocurrency) hizo baadhi ya sifa zake ila zipo
nyingi unaweza kuongeza nyingine kwa kutembelea kwenye mitandao na kusoma nyinginezo.

Kumbuka sarafu mtandao(Cryptocurrency) zina makundi mengi ila unaweza kuzitofautisha kwa
aina mbili.

Token hizi ni sarafu mtandao (cryptocurrency) ambazo hazina Network zake za Blockchain
zinatumia network za wengine ambazo zinatumika zimetengenezwa ndani ya hizo network.

Coin hizi ni sarafu mtandao (cryptocurrency) ambazo zina Network zake zenyewe yani zina
Blockchain zake mfano BNB, BITCOIN, ETHEREUM, SOLANA na nyinginezo

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

2. Mfumo wa Blockchain
Blockchain nadhani hili neno inawezekana umewahi kuliona au kulisikia sehemu yoyote ile
kama ilivyo maneno mengi yanayotumika kwenye ulimwengu huu wa sarafu mtandao
(Cryptocurrency) bado hayana misamiati sanifu ya kiswahili.

Blockchain ni daftari la kidijitali la kutunza taarifa za miamala ya sarafu mtandao


(Cryptocurrency) hili daftari linatunza taarifa za miamala kwenye kompyuta tofauti tofauti
duniani hauwezi kufuta au kubadilisha taarifa yoyote iliyoko ndani ya daftari hili.

Teknolojia ya Blockchain inajieleza kama teknolojia iliyoundwa kwenye mnyororo yan hata
neno lenyewe Block (tofali) na Chain (mnyororo) na tunaposema mnyororo haimaniishi
minyororo ya baiskeli au ya mbwa hapana maana ni ile ile kuunganisha ila sio na mnyororo
unaoshikika huu ni mnyororo unaomaanisha network kwahiyo block zinasimama kama
kompyuta na chain inasimama kama uunganishaji wa kompyuta kwenye mfumo wa Blockchain
na cryptocurrency kwa ujumla.

Na ninapo sema daftari simaanishi lile daftari tunaloandikia notes za kiswahili au geography
hapana hili ni daftari ambalo limeundwa kwa lugha za kompyuta (coding) kwahiyo hili lipo
ndani ya mifumo ya kompyuta na limeundwa kama daftari la wazi unaweza kusoma taarifa zake
lakini huwezi badilisha chochote unachokiona kwasababu taarifa zipo kwenye kompyuta nyingi
ili ubadilishe taarifa lazima uwe na kompyuta zote.

Na hapo ndipo usalama wa sarafu mtandao (cryptocurrency) ulipo kwakuwa hakuna


atakayeweza badilisha taarifa yoyote nakufanya wizi wowote mana wezi wote wa kimtandao au
wadukuzi huwa wanabadilisha taarifa au kumbukumbu zilizotunzwa na kuhamisha fedha au
kuiba.
Na vilevile ni rahisi unaweza kuona taarifa za miamala yako pia kwakuwa taarifa zinatunzwa
humo mtumaji na mpokeaji wote wanauwezo wa kuona taarifa ya miamala kwahiyo ni rahisi
kuona kama miamala yako imefika au haijafika.

Kupitia mfumo huu hakuna miamala unaoweza kurudishwa ukitumwa au kutuma mara mbili
miamala na ni ngumu kukosea kwasababu kila mtu ana utambulisho wa kutuma hela yani
ADDRESS hizi ndio hutumika kupokelewa miamala yako kwahiyo kama utatumia ADDRESS
sahihi muamala wako utafika bila shida yoyote.

Kwenye Blockchain kuna kitu muhimu zaidi kinaitwa Network hizi ndio zinakamilisha miamala
yote Kulingana na sarafu mtandao (cryptocurrency) husika kama mwanzo tulivyoambiana
kuhusu Coin na Token kama umesahau rejea kwenye ukurasa wa pili.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

Ndani ya mfumo wa blockchain kuna networks (uunganishaji) mbalimbali ambazo zinafanya


kazi ya kutunza na kulinda cryptocurrency, networks kwasasa zipo nyingi ila kuna baadhi
ambazo ni maarufu zaidi

 Tron (TRC20)

 Binance smartchain (Bep20)

 Solana

 Btc

 Erc20

 AVALANCHE

 POLYGON

Hizo ni baadhi ya Networks maarufu zaidi duniani kitu muhimu cha kukumbuka ni kama
unatuma sarafu mtandao (cryptocurrency) kwenda kwa mtu yeyote hakikisha huyo mtu
anakutumia ADDRESS yake sahihi ya hiyo Sarafu mtandao (crypto) na usisahau kumuuliza aina
ya network anayotumia ni muhimu.
Ikitokea umekosea aina network na ukatuma hizo hazitofika zinapoenda na hauwezi kuzirudisha
kwako zinabaki katikati tu kwahiyo itakuwa umepoteza hizo sarafu mtandao (crypto) ni muhimu
kujihakikishia kwenye hii hatua muhimu ili usije ukapoteza.

Blockchain ndio muhimili mkuu wa sarafu mtandao (cryptocurrency) hakuna crypto bila
Blockchain ndio eneo muhimu zaidi kwenye cryptocurrency ukitaka kuelewa soko la crypto
vizuri elewa zaidi kuhusu blockchain.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

3. SARAFU YA BITCOIN

Bitcoin ni sarafu ya kwanza kabisa kwenye soko la sarafu mtandao (cryptocurrency) historia
yake rasmi ilianza 2009 ndio kwa mara ya kwanza bitcoin iliingia sokoni lakini kuanzia 2008
neno bitcoin lilianza kutambulika ulimwenguni baada ya kutolewa waraka kuihusu na mtu au
kikundi ambacho kinajulikana kama Satoshi Nakamoto haijulikani mpaka leo kuwa Satoshi
Nakamoto ni mtu au kikundi cha watu.
Mana hajawahi kuonekana wala kutambulika mpaka sasa amebaki kuwa mtu au watu
wasiojulikana tu lakini walichokifanya kimejulikana na kimekuwa kikubwa mno.

Bitcoin inasimama kama alama kuu na nguzo kuu ya soko la sarafu mtandao (cryptocurrency)
kwasababu ya kuaminika kwake na ukuaji wake unavyoenda kwa kasi kadiri miaka inavyozidi
kwenda nayo inazidi kukua na kujiimarisha zaidi.

Itakumbukwa katika historia ya Bitcoin na soko la sarafu mtandao kwa ujumla kuwa bidhaa ya
kwanza kufanyiwa malipo na bitcoin ilikuwa ni pizza, alikuwa ni bwana Laszlo Hanyenc
ambaye kwa mara kwanza mwaka 2010 alinunua Pizza mbili za Papa John’s alitumia bitcoin elfu
kumi (10000) kupata hizo Pizza mbili hii ndio ilikuwa safari ya kupata thamani kwa bitcoin.
Na njia ya kufungulia thamani kwa soko zima la sarafu mtandao (cryptocurrency) ulimwenguni
na ndio ukuaji wa bitcoin ulipoanza mpaka sasa kwa kutumia Bitcoin mbili (2) unaweza kununua
Pizza za Papa john’s Elfu kumi (10000) huo ni ukuaji sana.

Kwa upekee kabisa Bitcoin zinatakuwa na idadi maalumu ambayo haitoongozeka tena yani idadi
yenye ukomo na idadi ya Bitcoin zote ambazo zitakuwa ulimwenguni ni million 21 tu
hazitoongezeka tena kwa namna hiyo jitahidi umiliki bitcoin zako kabla hazijaisha utazinunua
kwa gharama kubwa huo ni ushauri kidogo.
Na bitcoin zinatoka kwa awamu zinatolewa taratibu ili kuingia sokoni na huu mfumo unaitwa
Minning (uchimbaji) na uchimbaji sio uchimbaji wa kwenye udongo au ardhini hapana ni
uchimbaji ambao unatumia kompyuta na hapa ni kujitolea kompyuta yako kusaidia ufanyikaji wa
miamala ya Bitcoin na utapata gawio kila baada ya dakika kumi huo ndo uchimbaji sasa wa
Bitcoin.
Kwa namna hii ya Bitcoin million 21 kutolewa taratibu ni kuhakikisha uhakika wa thamani ya
Bitcoin itaendelea kuwa juu kwasababu uhitaji unakuwa juu na upatikanaji ni mdogo hapa hata
ukirudi kwenye elimu ya biashara itakupa majibu kabisa kuwa bei lazima itakuwa juu.

Lengo kuu ni kuhakikisha hata ukinunua Bitcoin leo basi hata ikipita miaka mia idadi ya bitcoin
ulizokuwa nazo zitaendana na thamani ya hali ya maisha kwa kipindi hiko husika.
Ebu chukulia mfano upewe million mia leo ikipita miaka mia hiyo million mia itaweza kununua
vitu sawa na wakati huu jibu ni hapana lazima miaka ikipita hiyo million mia inaweza ikawa hela
pipi tu, sasa hiki ndiko kilichokuja kubadilishwa na bitcoin ili hata ikipita miaka mia uweze
kutumia bitcoin yako kwa thamani sawa na wakati uliokuwepo wakati huo.

Na huu mfumo umegawanyika katika vipindi vya miaka 4 kila baada ya miaka 4 basi idadi ya
gawio ambalo wanalipata wachimbaji wa Bitcoin linapungua kwa kugawa mara mbili na hii
ilianza kuanzia mwaka 2012 ambapo idadi ya Bitcoin imekuwa ikipungua kila baada ya miaka 4

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

na hii imekuwa ikiongeza thamani ya bitcoin hiki kitu kinaitwa Bitcoin Halving kinafanyika kila
baada ya miaka 4.

Na katika kila mwaka ambao bitcoin halving inafanyika basi soko la sarafu mtandao
(cryptocurrency) hupanda mara dufu katika miaka miwili ya kwanza baada ya Bitcoin Halving
historia imekuwa hivyo wakati wote.
Na vilevile bei ya juu ya Bitcoin kwenye kila msimu wa Bitcoin Halving huwa ikivuka ya msimu
wa halving uliopita basi huwa hairudi tena kwenye hiyo bei hii yote ni kwasababu ya upunguzaji
wa gawio na uhitaji unakuwa mkubwa sana na upatikanaji ni mdogo sana kwahiyo lazima bei
iwe kubwa sana.

Hivi ndivyo zilivyofanyika na zitakavyoendelea kufanyika

Kipindi cha miaka minne (4) Idadi ya Bitcoin za gawio


2009 - 2011 50
2012 - 2015 25
2016 - 2019 12.5
2020 - 2023 6.25
2024 - 2027 3.125
2028 - 2031 1.562

Hayo ndiyo magawiwo yanavyokuwa kwenye Bitcoin halving zikifanyika na unaona kila baada
ya miaka minne basi nusu ya idadi inapungua na inafanya thamani ya bitcoin kupanda zaidi na
zaidi.

Ni muhimu kufanyika kwa Bitcoin halving mana katika historia kwenye hiyo miaka minne ya
halving basi miaka miwili ya kwanza huwa ni ya soko kupanda na miaka miwili ya mwisho ni ya
soko kushuka hivyo ndio imekuwa kwa halving zote zilizopita.

Kuna umuhimu wa kujua kuwa soko la sarafu mtandao ni soko ambalo ni la kushuka na kupanda
ni muhimu kufanya tafiti zako binafsi kabla ya kuingiza fedha zako kwenye sarafu mtandao hilo
ni muhimu zaidi.

Bitcoin inabaki kuwa ni mfano sahihi wa sarafu mtandao (cryptocurrency) kwa jinsi inavyokuwa
na inavyozidi kuwa na wawekezaji wengi ambao wanamiliki Bitcoin, ni matajiri wengi wakubwa
wameweka fedha zao ndani ya Bitcoin.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

4.Kutambua Fursa Za Cryptocurrency


Kwenye soko la sarafu mtandao (cryptocurrency) kuna fursa nyingi ndani yake hii ni kama ilivyo
kwenye masoko yetu tu ya kawaida mtaani huwa yamebeba fursa nyingi sana ndani yake hivyo
hivyo kwenye ulimwenguni wa sarafu mtandao (cryptocurrency) kuna fursa nyingi pia.

Ningependa kukupa fursa kadhaa zilizopo kwenye sarafu mtandao (cryptocurrency) hapa
nitakupa kadhaa lakini naomba kama unasoma hiki kitabu kikuongoze kutafuta fursa nyingine
zaidi kwasababu zipo nyingi sana jitahidi kusoma mtandaoni na kujifunza kwa watu wengine
waliofanikiwa kwenye sekta hii.

Naomba nikupe fursa kadhaa ninazoona ukizitilia maanani lazima utaona crypto ni mchongo
kabisa wa kukutoa kwenye msoto au sehemu moja kwenda nyingine na hilo ndo lengo langu
kukusanua wewe ambaye bado huna taarifa na hili au umekwama na hujui wapi utajikomboa
labda hiki kitabu kinaweza kukupa kitu.

-Ajira Za Sarafu Mtandao (cryptocurrency)


Ndio kama ulivyosoma hapo juu ajira za sarafu mtandao soko hili pia linatoa ajira yani unaweza
kupata kazi na kuajiriwa kabisa huku ukilipwa mshahara wako swali utajiuliza hizo ajira ziko
wapi na nitapeleka wapi CV zangu niajiriwe au nifanye interview mimi. Sasa kama lengo la
sarafu lilivyo kuwa ni mtandaoni basi na ajira zipo mtandaoni pia.

Ndio ajira za sarafu mtandaoni zipo mtandaoni pia na una jukumu la kuzitafuta zipo zinazohitaji
ujuzi mkubwa, wakati na hata mdogo ila kikubwa uwe mwanafamilia wa crypto mfano wewe
hapo software developer nikikuambia kule upwork kuna makampuni mengi yanakutafuta
uwafanyie kazi tena wanakulipa kwa saa utaamini.

Ajira zipo nyingi za crypto cha msingi tembelea kwenye website mbalimbali za project za crypto
au kwenye site za freelancing kama upwork na nyinginezo kuna ajira za muda na full time na
kazi unafanya ukiwa ndani kwako kitandani na mkeo au mumeo, hivi wewe ukiambia uongoze
group la telegram hiyo kazi itakushinda najua ni hapana utaweza kabisa na unatamani kuniambia
hiyo kazi ipo wapi nianze.

Na mimi nakujibu hizo kazi zipo mtandaoni anza kusoma mtandaoni utaziona tuma maombi
subiri majibu kuna kazi watu wanalipwa dollar 20 kwa saa alafu ni kazi tu ya kupost content
kwenye mitandao ya kijamii, kwahiyo hizo account zako za mitandao ya kijamii zina followers
kibao ni dili hilo ukiamua kutafutia ajira.
Nakupa sehemu kadhaa unaweza pata ajira hata kama sio za crypto kwa ujuzi wako wowote
ingia upwork, fiver, guru au nenda google search Freelancing sites utaziona nyingi tu na kuna
kazi nyingi sana humo fanya hivyo utanishukuru baadae.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

-Kutengeneza hela bila kufanya chochote


Kichwa habari kimekuvuruga si ndio ila ndo hivyo yani kutengeneza hela bila kufanya chochote
inashangaza kabisa lakini kwenye crypto inawezekana kabisa mtu wangu ila kabla hatujaendelea
hivi chochote kwako inamaanisha nini? Kwangu chochote inamaanisha kitu tofauti na kazi ya
kutumia nguvu au akili nyingi ili upate kitu sijui nimekosea lakini ndo nilivyomaanisha.

Hata kama nitakuwa nimekosea kwa maana yako ila ni sahihi usikate tamaa ni kweli kuingiza
hela bila kufanya chochote. Ila kitu pekee muhimu utakachohitaji ni hela ili uingize hela bila
kufanya chochote kile swali utajiuliza ni nawezaje kuingiza hela bila kufanya chochote nikiwa
na hela majibu nitakupa hapa.

Ni hivi kwenye crypto kuna sehemu unaweza ukaweka hela zako halafu ukawa unapata faida
bila ya wewe kufanya lolote mfano Binance wanayohuduma yao ya Binance saving unafanya
saving ya mahela yako kwa mfumo wa crypto halafu unakuwa unapata returns zako kila siku
maokoto ya bure kabisa hayo.

Ila hizo huduma zipo sehemu nyingi pia ukiacha Binance vilevile kuna kufanya Staking nako
unapata maokoto bure bila kufanya chochote ni wewe ku stake tu mahela yako halafu unalala
unapata hela zako.

Haraka ni hivyo ila mfano kwa watumiaji wa Binance kuna pale Binance earn ni unajichagulia tu
huduma ipi ya maokoto ya bure unahitaji ni wewe tu halafu unapata zako hela huku umelala
zako muhimu uwe na hela tu.

Nadhani huduma za Staking na Saving ni huduma za kupata hela bila kufanya chochote zaidi ya
kuwa na hela wewe pia halafu unapata hela ukiwa umelala zako tu yani unakuwa tajiri ukiwa
umelala zako ni raha ilioje aseee.

Jambo kubwa ni ujifunze tu na upate maarifa sahihi ya wapi unaweza fanya hivyo vitu
kwasababu pamoja na yote hayo kuna wizi na mambo mengi ambayo hayafai yanatokea ila
niamini mimi kama utasaka maarifa sahihi hakuna kitu unaweza poteza au tapeli atakayekushika
ila ukiingia bila dira niamini mimi lazima utasema crypto ni wizi ni muhimu sana kutafuta
maarifa sahihi.

Najua kuna unaweza kujiambia mwenyewe moyoni mbona kasema hatufanyi chochote halafu
ghafla kasema tu stake na tufanye saving, ndugu yangu ndo hivyo sasa hela itakujaje bila kupata
njia za hela sahihi lakini ukifanya hivyo vitu unapata maokoto tu hata soko likishuka maokoto
utaokota tu ndo mana nikakwambia fanya hivyo, na naamini utafanya hivyo pia asante sana
tukutane kileleni kwenye mafanikio.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

-Kushikilia sarafu mtandao (crypto hold)


Naam kama nilivyosema hapo juu kushikilia sarafu mtandao tafsiri zangu sio fasaha ila nahitaji
tu uelewe kitu mtu wangu, hapo juu unaweza sema kushikilia au kumiliki sarafu mtandao labda
hapo kuna kamaana umekapata kichwani kwako kwanini hii ni fursa.

Nadhani hii ni moja fursa ambayo ni rahisi zaidi kwenye crypto kwasababu inachohitaji kikubwa
ni uvumilivu lakini huo uvumilivu wako unaweza ukalipwa pa kubwa sana mpaka ushangae
wewe na kwenye huu ulimwengu wa crypto wengi sana wanafanya holding za sarafu mbalimbali
kwasababu ya faida tu unayoweza tengeneza.

Inakuwa hivi itakuhitaji ufanye utafiti wako kwenye sarafu unayoona unaweza kuinunua na
kuifanyia holding, utafiti ni muhimu ili ujue kama ni sehemu sahihi unayoweza kuweka hela
zako kwasababu holding inahusisha manunuzi unanunua sarafu kwaajili ya kuiweka kipindi
kirefu au kifupi ila ukiwa na mategemeo ya hiyo sarafu ipande bei mara dufu na ile uliyonunulia.

Ili ukiuza upate faida, na zipo sarafu ziliwapa watu faida hadi ya mara elfu moja ya thamani
waliyonunulia ndio ndo mana nakwambia hii ni fursa kubwa sana ila inahitaji uvumilivu sana
kwasababu soko la crypto ni la kupanda na kushuka uvumilivu ni muhimu kwenye holding.

Kufanya holding unaweza anza na kiasi chochote kile yani na hakuna ukomo wa faida
utakayopata yan kwa haraka haraka kufanya holding ni sawa na kununua kiwanja porini halafu
huko porini kuwe mjini yani kukue si lazima thamani ya kiwanja chako itapanda hivyo ndo sawa
na kufanya holding.

Ingawa huku kuna tofauti kidogo kwamba kuna kushuka thamani pia ila raha ni kwamba hata
thamani ikishuka idadi ya sarafu zako itakuwa vilevile ingawa thamani yake itakuwa ndio
imeshuka Kulingana na mwanzo wakati unanunua, na ndivyo ikipanda utakuwa na idadi ile ile
ya crypto ila thamani yake imepanda.

Na kuna baadhi ya maneno yaliwahi semwa huko nyuma kuwa ukitaka kuwa millionea basi
wewe hold crypto, ni kweli crypto holding ina hela sana kama tu uvumilivu utakuwa na wewe ila
ni elimu sahihi ya crypto kama itakuwa na wewe pia.

Ulimwengu wa crypto ni mpya sasa ni muhimu utafute maarifa sahihi hiki kitabu kitakupa
mwanga ila ni jukumu lako kusaka nuru kamili ili ufanikiwe zaidi na maarifa yako kwa watu na
mitandao wewe itumie tu vizuri utaniambia tu.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

-Kutengeneza hela kwenye crypto bila mtaji wowote


Nadhani hii itakuwa sehemu pendwa kwa watu wengi kwasababu ya hali na uchumi wetu au tu
kutokana na imani zetu tunaona kuweka hela sehemu yoyote kuna ugumu bora nipambane na
vya bure na ulimwengu wa crypto haujawahi kuwa na uchoyo hata kidogo kuna maeneo ya bure
ya kupiga hela bila mtaji wowote ule ni wewe na uwezo wako tu.

Upo makini na mimi kama ndio basi hakika nafurahia nia yako ya kupenda kujifunza na mimi
nitakupa machimbo manne ya kupiga hela bila ya mtaji wowote ule kwenye crypto soma hapo
chini nitaanza moja mpaka nne.

1. Ushirikishaji wa marafiki (referral)


Hapa makampuni mengi ya crypto yanakuhitaji wewe mwenye uwezo wa kuweza
kushirikishwa watu na marafiki kujiunga na kampuni zao inaweza ikawa soko la crypto au
kampuni inayohusiana na maswala ya crypto. Na hapa utapata kitu kinaitwa referral bonus
endapo utamuunga mtu kwenye kampuni husika.
Mfano Binance ambayo mimi niko nayo ukimuunga mtu na akajiunga vizuri kila akitrade
iwe spot au future wewe unapata 41% ya alicho trade, yani unapata hela mwingine ndio ana
trade huko. Na hii sio Binance tu zipo sehemu nyingi zinatoa bonus tofauti kwahiyo kama
huna mtaji ila una watu basi utapata hela tu.

2. Ualimu wa crypto (Mentor au Teacher)


Hapa ni lazima uwe umesoma na wewe na una maarifa ya kutosha ambayo utayatumia
kuwafundisha wengine halafu watakulipa au unatengeneza kozi au vitabu unauza unapata
hela ukiwa na mtaji sifuri kabisa, na hii mfano mimi nafundisha crypto na mimi kwangu
nafundisha kwa 50,000 sizidishi wala sipunguzi hapo ila hiyo ni mimi ambaye kwangu hii
elimu naitoa bure tu.
Ila wewe unaweza ukawa mwalimu ukafundisha kwa ada labda ya 250,000 unafundisha
vizuri kabisa unapata wanafunzi wengi hapo kwa shilingi sifuri umepata laki 2 na 50, ila
hapa ukitaka uwe vizuri ni lazima uwe na elimu ya kutosha sana.

3. Shiriki mashindano ya crypto


Ndio kuna mashindano mengi ya crypto huwa yanawekwa na kampuni ambazo hazina longo
longo kwahiyo kupata walichokuahidi ni uhakika kabisa bila matatizo yoyote yale. Sasa
wewe unaweza ukawa unatafuta hayo mashindano unashiriki unashinda walichokuahidi
unaweza ukawa unapata hela pia kupitia humo.
Ni rahisi sana kupata hayo mashindano na kushiriki wewe hakikisha tu ni mwanafamilia wa
crypto hilo tu basi.

4. Zawadi za crypto (Airdrops)


Hizi ni zawadi amabazo huwa zinatolewa labda coin ikiwa inaanzishwa kabla haijaingia
sokoni au coin inatarajia kuingia kwenye soko flani basi wanatoa hizo zawadi za crypto
zinaitwa Airdrops kuna watu wamepata hela nyingi kupitia Airdrops ila kikubwa ni lazima
uwe na elimu sahihi kuzihusu kwasababu zinahitaji kuzifanyia utafiti sana ila zina maokoto
sana nazo bila hela unapata maokoto.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

5. KUTAMBUA MASOKO YA CRYPTOCURRENCY

Crypto au sarafu mtandao ni kama maana yake nilivyoielezea mwanzoni kabisa kuwa hauwezi
kuzishika kwa mikono au kuziweka kwenye kibubu kwahiyo kuna mahali zinakuwepo zinauzwa
au unaweza kuuza pia hayo ndio yanaitwa masoko ya kubadilisha crypto (crypto exchange) na
zipo nyingi tu duniani, vilevile unahitaji mkoba wa kubebea crypto zako huo unaitwa mkoba wa
crypto (Crypto wallet) wacha tuanze kutambua

-Soko la kubadili sarafu mtandao (crypto exchange)


Ndio soko ni kabisa ila hili soko ni kwaajili ya bidhaa ambayo ni crypto na ndio maana linaitwa
soko la kubadili sarafu mtandao hapa ndio unaweza ukabadili sarafu flani kuwa sarafu flani, au
unaweza ukaona sarafu flani imeshuka ukainunua ili uuze baadae au vilevile unakuta sarafu flani
unayomiliki imepanda kwahiyo unaingia kuiuza ili upate maokoto.
Masoko yapo mengi sana amabayo ndani yake yana aina nyingi za sarafu mtandao mfano wa
masoko ni kama Binance, Bitget, Bybit, Kucoin na Mexc na mengine mengi sana ambayo
yanatoa huduma za sarafu mtandao.

Ila soko kubwa lenye watumiaji wengi wakati naandika hiki kitabu ni Binance ni soko kubwa
ambalo hata mimi natumia na nakushauri wewe kama huna account huko Binance basi fungua
account huko ila ukijiunga naomba pale kwenye referral ID weka hii namba 460338511 ili tuwe
pamoja kwenye safari yako.
Na kama utajisajili Binance na utakubwa na changamoto yoyote basi namba yangu ipo kwenye
kava mwanzoni kabisa nitafute nitakusaidia kukamilisha kuwa na account yako ya Binance.

Ni muhimu lakini ukitaka kuwa na account kwenye haya masoko inabidi uwe na kitambulisho
kinachotambulika na serikali kama NIDA au Passport ya kusafiria au Leseni ya udereva au
Kitambulisho cha mpiga kura uwe angalau una kimojawapo kati ya hivyo ili uweze kufanya
uhakika na ukamilishe usajili wa Account yako hii ni kwa Exchange zote zinahitaji ufanye
Verification ili wakujue mteja wao.

-Mkoba wa crypto (crypto wallet)


Huu ni mkoba ambao ni wa kidigitali kwahiyo ni mifumo imeundwa ya kikompyuta kwaajili ya
kutunza na kuhifadhia crypto zako hii mikoba (wallet) huwa haina kazi sana ni wewe
kudownload app halisi ya mkoba (wallet) husika alafu utafungua account yako huku hakuna
kuweka taarifa zozote ila kitu muhimu ni kukumbuka maneno 12 ambayo unapewa hayo maneno
unahitajika kuyatunza sehemu salama sana mana ndio njia pekee ya kuingia kwenye account
yako ukapoteza hayo maneno basi na account ndio imepotea.
Na hizi wallet zipo nyingi ila maarufu zaidi ni Metamask na Trustwallet na zinapatikana kote
playstore na App store wewe ni kudownload na kufungua account yako pamoja kukumbuka
kuyahifadhi maneno uliyopewa kwa umakini.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

6. NAMNA KUTAMBUA ENEO LAKO


Huko juu nimeongea mengi sana ila kunamna unahitaji kujua sehemu gani unaweza kukaa au
unaweza kufanya ili iwe rahisi kwako kujiongezea maokoto au kutambulika kuwa unafanya kitu
gani? Kwenye ulimwengu huu wa crypto na mimi nitakupa namna kadhaa ambazo zitakufanya
ujue ni wapi linaweza kuwa eneo lako zaidi la kulifanya kwenye crypto.

-Kujenga Profile yako binafsi


Ni muhimu sana kuwa profile inayoeleweka yaani utambulike unafanya nini hasa kama utahitaji
kuwa na ajira kwenye crypto au kuwa mwalimu wa crypto lazima ujenge profile yako hii
unaweza kufanya kwa namna mbalimbali ila namna nzuri zaidi ni kwa kujitengenezea jina
kwenye mtandao share madini yako, jitambulishe wewe ni nani kwa namna hiyo ukitaka kujua
hili tembelea account yangu ya twitter (X) ukifika tu lazima utajua mimi na deal na crypto.

Hivyo ndivyo unatengeneza profile yako hapo lazima kikitokea kitu chochote au swala lolote
kuhusu crypto jicho litakuwa kwako soma sana na toa madini kwa watu utakuwa bora zaidi na
utakuza profile yako kwa asilimia kubwa sana kama unaanza fanya hivyo kuna siku utaona
majibu yake.

-Namna ya kukuza Portfolio yako


Portfolio namaanisha kile kibunda chako utakachokuwa nacho kwenye wallet au exchange
utakikuzaje bila kutengeneza hasara mana kwenye crypto kuna hasara pia Ukiachana na faida.
Mara zote tunza ukipata faida itunze kwa kutumia stable coin hizi zile coin ambazo hazishuki
wala hazipandi zinaenda sawa na dola tumia hizi kuhifadhia faida zako.

Usikubali kuwekeza kwa kuambiwa na mtu kuwa nunua hizi coin bila ya kufanya uchunguzi
wako binafsi mara zote jihakikishie mwenyewe ili ujue kama ni sahihi au hapana, hata mimi
wakati naanza nilipoteza sana hela kwa kusikiliza watu jitahidi kujihakikishia mwenyewe na
hapo ndio umuhimu wa kupata elimu sahihi ulipo.

Usiwe na tamaa najua hela hazitoshi kuna namna coin ikiripuka kuna faida unapata ila hakikisha
inakutosha usiwe na tamaa ya kupata zaidi rizika na ulichopata ukishikilia sana unaweza
kupoteza.

Tumia hela nyingi kwa kununua coin chache ulizozifanyia utafiti kabisa na umeona zitafanya
vizuri kuliko ile unatumia hela nyingi kununua ma crypto mengi sana alafu mwisho siku
zinazofanya vizuri ni chache kuliko zilizofanya vibaya sasa ukiwa na chache zenye uhakika
ukaziwekea hela nyingi una uhakika wa faida kubwa hata kama moja au mbili zikifanya vibaya.

Amini kwenye ambacho unafanya tu na usiwe na wasiwasi kama una uhakika unachofanya
unakielewa vizuri sana.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

-Namna bora ya kuwekeza kwenye Crypto


Nakuona upo makini kusoma hiki kipengele ni kweli inakubidi uwe makini lakini sidhani kama
utahitaji kuwa makini sana kama umenielewa vizuri huko tangu naanza ila kama hujanielewa
vizuri naomba uwe makini sana hapa kwasababu ni eneo muhimu sana kwako ili uelewe vizuri
kuhusu crypto.

Namna bora kuwekeza kwenye crypto cha kwanza ni ujue crypto ni nini ili usije ukanasa kwenye
mitego ya wezi wa mtandao ambao wanatumia jina crypto kuibia watu na ili crypto ni nini
nimekuelezea mwanzoni ushauri mdogo tu jitahidi uwe na mtu unayemuamini awe mentor wako
atakusaidia kwenye vitu vidogo vidogo vya kuijua crypto.

Cha pili uwekezaji wa crypto ni lazima uwekeze ukijua soko la crypto ni la kupata na kushuka
kwahiyo uwe tayari kwa matokeo yote hayo na ndio mana sio vizuri unakopa hela halafu ndio
unaenda kununua crypto hapo unacheza na tukio hatari sana inakubidi uwe makini sana mtu
wangu.

Cha tatu kama wewe ni kijana huna kazi unaweza jifunza futures trading ingawa ina ugumu kiasi
ila ukiwa vizuri huwezi kukosa hata dola 10 hadi 20 kwa mtaji wa kawaida tu kama dola 100, ni
ushauri tu muhimu ni kujifunza utapata sehemu ya kusimama.

Na kama wewe ni mtu wa kazi upo bize sana wekeza kwa kuhold tu crypto kwasababu ya ubize
wako na una kipato cha mshahara basi holding itakufaa zaidi, nao ni ushauri tu ila unaweza
chambua zaidi ni sehemu gani itakufaa zaidi.

Ila kama una hela nyingi sana wewe ni upo vizuri sana basi nakushauri ufanye saving au staking
utapiga hela nyingi za bure kama zile za kwenye BOND za mabenki mbalimbali ambayo huwa
yanauza BOND.

Ila ili uwe muwekezaji mzuri kwenye cryptocurrency basi ni lazima ukubali kujifunza na
uendelee kupata maarifa kila siku na usijitenge na online hata kidogo kuna vingi utapata na
utajifunza na vita kusogeza kwenye uwezo wako wa elimu ya crypto, ila asikuambie mtu yeyote
kuwa hiki kitu ni kibaya na wewe ukasema ni kibaya bila kufanya upembuzi yakinifu.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

7. TRADING ZA CRYPTOCURRENCY

Crypto ni ndio zimeaanza kuingia lakini tayari zina aina nyingi za trading na watu wengi
wanazitumia hizo kufanya biashara mbalimbali za crypto na mimi sehemu hii nilitamani nikupe
aina mbili tu ya Trade maarufu kwenye crypto na zinatumika sana na watu wengi na sio nyingine
ni Spot trade na Futures trade aina nyingine ya trade ingia google search utaziona usipoona
nitafute nitakwambia leo wacha nikupe taarifa kuhusu hizo mbili.

Futures Trade
Hii ni trade ya crypto inayopendwa zaidi na vijana wapenda maokoto ila ni moja ya trade ngumu
sana na trade inayoweza kukutajirisha na kukufirisi pia, ni ngumu lakini sio kwamba
haiwezekani inawezekana kula sana matunda na futures trading ukiwa na elimu sahihi ya kuingia
kwenye soko.

Hapa futures trading ni trade ambayo wewe ukiingia kwenye trade hauingii na crypto ila
unaingia na mkataba kwahiyo kama utajichanganya ukaenda tofauti na ulichosema kitatokea una
uwezekano wa kupoteza hela kiasi au zote kabisa na ndio mana inaonekana kama trade ngumu
ya crypto.

Hapa futures kwa vile ni kununua mkataba basi unaweza kutengeneza hela soko likipanda na
likishuka pia ni vile wewe kupitia Uchambuzi wako wa soko utakupa majibu gani ambayo
utayanunulia mkataba husika.

Kama ukiona soko litashuka na ukanunua mkataba wa kushuka na soko likishuka kweli basi
utatengeneza hela Kulingana na mtaji wako uliyonunulia mkataba lakini likienda tofauti na
ulichosema basi tambua tu hapo utaingiza hasara Kulingana na mtaji uliyonunulia mkataba hiki
kikombe ndo kinanyweka hivyo yani.

Kuna kitu inaitwa liquidation price sasa hii bei ambayo kwenye mkataba huwa inawekwa kuwa
endapo soko litaenda tofauti na ulichosema halafu ikafikia hii bei basi hiyo trade itaishia hapo na
watachukua hela zote zilizoko futures trade na ukisikia kuchoma account ndo huko sasa.

Spot Trade
Kama jina lake lilivyo Spot ni kweli kwani trade ambayo wanunuzi (buyer) na wauzaji (seller)
mnakutana na kufanya biashara yani mfano wewe unataka kununua crypto flani na unaitaka kwa
bei flani unaingia spot trade unachagua crypto husika halafu unaweza ofa yako kuwa utainunua
kwa sh ngapi Ikitokea ofa yako imepata mtu basi unauziwa au kama unauza wewe basi
itanunuliwa ni rahisi sana yani

Hapa tunasema ni rahisi kwa kuwa hauwezi kupoteza hela zako hata kama soko likishuka
kwasababu kitakachotokea ni thamani itapungua tu ila crypto zako zitakuwepo kwa idadi ile ile
ukiwa account za Exchange utapaona hapo Spot trade kwasababu ndio crypto huwa zinakaa hapo
zikiwa kwa exchange.
Kasoro ya hapa ni kwamba kutengeneza faida ni kwa kupanda kwa soko tu yan bei ikipanda ndio
unapiga hela, likishuka ni hasara kwako pia ingawa hupotezi crypto zako hata kama bei yake
itafika sifuri.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

-Jinsi ya kulinda Mtaji (Risk Management)


Hiyo tafsiri yangu najua sio sahihi sana ila ndicho nilichomaanisha yani namna za kulinda mtaji
wako kwenye trade nimeanza na hili kwasababu watu wengi hili huliweka la mwisho kabisa
wakati ndio jambo la kwanza muhimu sana hasa baada ya kujua zile aina za trade basi lazima
tujue namna za kulinda mali zetu mana tushakubaliana soko la crypto ni la kupanda na kushuka
pia.

Kuna mambo kufanya ili ujilinde na ulinde mtaji wako kwasababu fanya ufanyavyo ni muhimu
kulinda mtaji na hili ni maalumu kwa wale wanaopenda Futures trade wa spot hii sio sana kwenu
ila futures naomba mnisikilize kwa makini. Fanya haya ili ulinde mtaji

i) Tumia asilimia ndogo ya mtaji


Wewe una trade futures au unayetarajia kutrade futures trade ni muhimu kujua kuwa
unahitaji kutumia sehemu ndogo tu ya mtaji ndo iwe ya kuingia nayo sokoni kama una mtaji
mkubwa sana tumia 1% mpaka 5% ila kwa mitaji yetu hii midogo nashauri utumie 10%
mpaka 20% tu ya mtaji wako na uwe vizuri sana ukitumia asilimia hizi. Hii itakusaidia
liquidation price kuwa mbali sana hata soko likikugeuka utakuwa salama.

ii) Fanya utafiti mzuri kabla ya trade


Ni muhimu kufanya utafiti wako ukichambua na coin husika unayotaka kuitrade au
kuiwekeza kwasababu itakusaidia kutambua unaenda kuingia kwenye soko la namna gani hii
itakufanya iwe rahisi sana kujua utrade vipi crypto husika, huu utafiti utaufanya kwa
kutembelea online huko kama google na maeneo mengine kama Twitter (X)

iii) Tumia stop loss


Ukifungua trade hasa trade za future Kumbuka kuweka stop loss hii itakusaidia kuzuia
kupoteza sana pale ambapo soko limeenda tofauti na wewe ulichokiona sokoni kwa wakati
huo na mara zote weka stop loss kwenye kiasi ambacho upo radhi kukipoteza na acha kabisa
tabia ya kusogeza stop loss hii itakusaidia kwenye trade wewe trade kama roboti yani.

iv) Acha kuweka leverage kubwa


Vijana wa mjini wanasema mtaji sisimizi leverage tembo, wenyewe wanamaanisha
wanaweka mtaji mdogo halafu leverage kubwa sasa hizo leverage kubwa sasa hiyo tabia sio
nzuri kabisa kuweka hizo leverage tembo hii ni kwa wale wanaotrade futures trade weka
leverage ya wastani tu ili iwe rahisi kuweza kwenda sawa na soko linavyoenda kuliko kuwa
na leverage kubwa.
Itakufanya upoteze haraka sana pale soko linapogeuka tofauti na aliyeweka leverage wastani
kuna muda ukiwaza faida kubwa ndio hasara kubwa inakuja mbele.

v) Kuwa na njia ya kutokea kwenye trade


Ukifanya Uchambuzi wako hakikisha unakuwa na njia ya kutoka sokoni hapa namaanisha ni
sehemu ambayo utachukulia faida yako, usiwe na tamaa inabidi ujue utatokea wapi kabla
hata hujaingia sokoni ni muhimu sana hilo pia, kwasababu kukaa sana kwenye faida ndio
kwenye hasara panakaribia yani.
Hizi ndio njia ninazotumia mimi na natamani nawewe utumie kwenye trade zako au uziboreshe
zaidi zikusaidie zaidi kwenye trade zako naamini unaweza kufanya hivyo.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

-Jinsi ya kumiliki hisia zako (Emotional Control)


Hisia zipo kila sehemu sio tu kwenye mapenzi hata kwenye trade za crypto inakuhitaji kujua
jinsi ya kumiliki hisia zako hili tatizo la traders wengi na wawekezaji wengi wa crypto
wanashindwa kumiliki hisia zao wanaendeshwa na mihemko na wanajikuta wanakula hasara tu.

Fikiria kuna ule wakati unaona soko linashuka halafu unaona bora ufunge tu ghafla umefunga
unaona soko linapanda tena unatamani unaingia tena linapanda kidogo halafu linashuka
unajikuta tena kwenye hasara unafunga tena unajikuta huo ndo mchezo wako mwisho unaishiwa
kabisa.

Hiyo ni kwasababu unashindwa kumiliki hisia zako binafsi unayumbishwa na mihemko hapo ni
ngumu kutoboa kwenye crypto kwasababu utapoteza taratibu mpaka zitaisha hela zote yani na
Kumbuka soko la crypto au trading liko hivi wewe ukipoteza ujue kuna mwenzako kapata na
wewe ukipata jua kuna mwenzako kapoteza ipo hivyo yani. Epuka haya ili umiliki hisia zako.

- Usitrade unachofikiria au kuamini


Soko sio akili yako au moyo wako au mali mpaka liende kama unavyofikiria wewe trade
unachokiona sio unachofikiria hii itakusaidia

- Usiogope kupoteza nafasi ya kuingia sokoni


Kwenye soko la crypto kuna nafasi nyingi tu ukikosa hii utapata hii usilazimishie kuingia
kwenye eneo ambalo sio sahihi hakikisha umeona entry nzuri kabisa ndio uingie sokoni sasa.

- Usiwe mtu wa kuangalia Angalia trade


Ukifungua trade yako ambayo una uhakika nayo hauna haja ya kila muda kutazama kama
umebandika maharage vile wewe fungua trade acha mengine yaende kama ilivyo au watumishi
wanasema acha mungu akupiganie sasa.

- Ukipata hasara husi trade tena


Ndio ukipoteza tu usirudi sokoni ikiwezekana pumzika hata siku mbili au tatu ukiangalia
ulipokosea halafu jifunze tena halafu futa kosa ndio urudi tena sokoni usilazmishe kurudi sokoni
muda tu ukipoteza kuwa mtulivu tu kwanza.

- Usiwe na kujiamini sana


Hii hata mimi ilishawahi kuniponza nilikuwa najiamini sana sasa ukijiamini sana ni rahisi
kupoteza hisia zako unazomiliki ukaanza kusukumwa na kujiamini kwako mwisho wa siku ni
kilio tu umepoteza soko halitaki ulijue sana na vilevile hakikisha nawewe lisikujue sana kiufupi
msijuane.
Mambo ya hisia hay mara nyingi yapo kwenye namna ambavyo tunafikiri na tunavyoshauriana
sisi kwa sisi ila ni muhimu kumiliki hisia zako.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

-Uchambuzi wa mifumo (Technical analysis)


Sijui nimetafsiri sahihi yote kwa yote kwa natumaini umenielewa nilichomaanisha ila kama
hujanielewa basi anza kujifunza kuhusu uchambuzi wa masoko ya crypto utakutana na kitu hiki
au kama ushawahi kuona mtu ana ma graph hivi yana rangi tofauti basi hapo jamaa ndio unakuta
anafanya Uchambuzi wa mifumo.

Kuna wale ambao tumesoma vitabu vingi hasa kitabu maarufu kwa traders wengi candlestick
bible yote ni kwaajili ya kujifunza Uchambuzi wa mifumo (Technical analysis) hujakosea
nadhani hii ni namna bora zaidi ya kuchambua soko la crypto.

Ila mimi ningetamani kwa kiasi niweze kusema mbinu zangu kadhaa kwenye kufanya
Uchambuzi wa mifumo (Technical Analysis) kama inavyojulikana Uchambuzi huu unahusisha
muda na candlestick hivi ni vile vinavyopanda na kushuka mara nyingi utaona vina rangi
nyekundu na kijani ndo hivyo. Sasa wacha tuambiane tunafanyaje Uchambuzi wa mifumo
(Technical Analysis) kuna namna ya kuzingatia vitu hivi

Usitumie mbinu nyingi za kutafsiri soko – ndio zitakuchanganya kutumia mbinu nyingi unaweza
changanya na Usione kitu sahihi kwenye Uchambuzi wako wa soko jitahidi kutumia mbinu mbili
hadi tatu tu ambazo zitakupa majibu ukiona hazikupi achana na hiyo pair tafuta nyingine.

Hakikisha unaangalia muda na umbo lililotokea – kama nilivyosema kuwa muda ni kitu muhimu
kwenye Uchambuzi wa mifumo jitahidi kuhusianisha muda na matukio yaliyotokea hasa wakati
wa nyuma.

Wakati wote hakikisha hutumii hisia kuchambua – utajiuliza kwanini hii ni sawa nakusema trade
unachokiona sio unachofikiria wewe kwasababu soko litakuonesha kitu basi trade hiko kitu sio
unachofikiria kwa akili yako.

Hakikisha umeona uelekeo wa soko – hii ni muhimu kwasababu unahitaji kujua soko linaelekea
wapi linapanda au linashuka kama soko lipo katikati halishuki wala kupanda hakika usiingie
sokoni subiri uone uelekeo wa soko.

Fanya Uchambuzi wa soko angalau masaa manne kabla ya kuingia sokoni – ni muhimu sana
kuzingatia hili chambua soko muda mrefu ili ujipe muda sahihi wa kuingia sokoni kuliko
kufanya analysis ya chapu halafu unaingia sokoni hakika hutoona soko vizuri linavyoenda
mwisho wa siku utaingia kwa pupa tu na unaweza kupoteza.

Uchambuzi wa mifumo una mbinu nyingi za kuchambua jitahidi kuzisoma na kutafuta mbinu
kadhaa ambazo utakuwa unazitumia wewe usijaribu kutumia kila kitu utachanganyikiwa na
hutoona mafanikio ya unachofanya.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

-Uchambuzi wa taarifa (Fundamental Analysis)


Kwenye aina za uchambuzi kuna uchambuzi huu pia uchambuzi wa taarifa ni moja ya
uchambuzi muhimu sana kwani unahusisha mambo ambayo ni taarifa ambazo zinaweza kubadili
uelekeo wa soko. Hizi taarifa mara nyingi zinaweza kuwa za matukio au maneno ya watu wenye
nguvu duniani.

Ni muhimu kufuatilia taarifa hizi pia kwasababu ni moja ya taarifa zinazoweza kubadilisha
uelekeo wa soko hata kama uchambuzi wako wa mifumo (Technical analysis) yako hiko vizuri
kiasi gani taarifa moja tu inaweza kubadilisha kila kitu kwenye soko.

Uchambuzi wa namna hii unaufanyikaje huu ni aina ya uchambuzi ambao utakuhitaji uwe
mdadisi na mfuatiliaji sana wa maswala ya crypto na vilevile uwe unafuatilia sana watu
wakubwa walioko kwenye ulimwengu wa crypto maana hao wanaweza kubadilisha uelekeo wa
soko wakisema neno moja tu yani.

Utapata wapi taarifa hizo naam hii ni muhimu sana kujua kwenye crypto ni tofauti na soko kama
forex wao kule taarifa zina ratiba kabisa ila huku kwenye cryptocurrency ni lazima uwe
mfuatiliaji ndio utapata hizo taarifa ila jitahidi uwe mtumiaji wa mtandao wa twitter (X) huko
kuna taarifa nyingi sana ambazo zinatolewa au utazipata kiurahisi.
Sehemu nyingine ni kutembelea kwenye tovuti zinazotoa habari za crypto nako utakuta taarifa
mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia kwenye trade zako.

Kitu muhimu cha kukumbuka ni kuwa sio kila taarifa huwa inaweza kukusaidia kwenye trade ni
jukumu lako kujua taarifa ipi inaweza kukuletea matokeo kwenye trade kwasababu sio zote
zinabadilisha uelekeo wa soko nyingine zinatokea na soko linabaki kama hakijatokea kitu vile
linakuwa vilevile.

Uchambuzi wa taarifa mara nyingi kwenye crypto huwa unakuwa mgumu kwasababu hakuna
ratiba maalumu ya taarifa zake kwasababu soko la crypto ni soko huru kwahiyo yeyote yule
mwenye ushawishi kwa watu anaweza akabadilisha uelekeo wa soko ilimradi tu watu wengi
wakimsikiliza kama inavyojulikana soko la crypto halipo kwenye chombo chochote la
kuliendesha jitahidi uwe makini tu.

Wakati wote tilia shaka chochote unachohisi kinaweza kuwa na matatizo na kuwa makini sana
kwenye maaamuzi yako sokoni hasa yanayohusisha taarifa hii itakujenga kuwa bora zaidi na
zaidi kwenye maswala ya uchambuzi wa taarifa, na ni muhimu kujifunza na kupata elimu sahihi
kuhusu uchambuzi wa taarifa kwenye crypto kwasababu ni moja aina ngumu ya uchambuzi
kama hutokuwa makini.
Tenga muda wako ingia youtube, google na kwenye hizi AI zitakusaidia kupata elimu sahihi
ukishindwa kabisa tafuta mwalimu mlipe akufundishe usitafute wa bure hutopata unachokihitaji
walimu wote wazuri wanalipwa.

CRYPTO NI MCHONGO
CEO_CRYPTO25

MANENO MUHIMU
Tangu naanza kuandika hiki kitabu nia yangu kubwa ilikuwa ni kukupa taarifa na vitu ambavyo
huvijui au unavijua nimekukumbusha tu kama unasoma hiki kitabu na wewe ni mwanafamilia
wa crypto basi hongera sana na umechagua njia salama usikate tamaa endelea kupambana tu
tufikishe elimu mbali sana. Ila kama sio mwanafamilia wa crypto basi ombi langu kubwa jifunze
tu crypto halafu endelea na ishu zako mana bora ujue kitu kuliko usijue kitu bila sababu.

Kitu pekee bora kwenye maisha ni kujifunza vitu vipya najua kuna wakati ulijiuliza mtu wa
kwanza kutumia nazi aliitumiaje mimi na wewe hatujui ila unaweza kuta aliichemsha na
maganda yake au jiulize ubunifu wote uliofanyika duniani watu wangeamua wasiendeleze leo si
tungekuwa hakuna kitu chochote kizuri au cha thamani.

Nafikiri ni vizuri kwako pia kuanza kuendeleza ubunifu wa Satoshi Nakamoto ili baadae
wajukuu na vitukuu huko mbele wafurahie ulichokifanya babu yao au bibi yao, mimi binafsi
sijisifii ila ni mtu ninayependa kujifunza nafikiri nimefanya vitu vingi mno ili mradi tu nisipitwe
na sio vibaya kwasababu kila sehemu niliyokuwepo ili nisaidia kujifunza.

Nitakuomba kitu najua mpaka unafika hapa basi umesoma kila nilichokiandika huko juu ombi
langu kwako chukua muda wako anza kujifunza cryptocurrency tafuta haya maarifa popote
utakapoyaona na nakuahidi baadae itakuwa ni moja kitu cha thamani ambacho una miliki na
utafika mbali.

Nilivyoandika hapo ni sehemu ndogo ya vitu vingi ambavyo vipo kwenye soko la crypto
vilivyopo ni vingi sana ila nilivyokuambia ni kidogo tu kati ya vingi sana ambavyo vipo kwenye
soko la crypto vingi zaidi ni jukumu lako kuvitafuta na kujifunza ili view urithi kwa kizazi
chako.

Ujumbe wangu kwako wewe kama umesoma hiki kitabu basi wewe ni mtu wa thamani sana na
mtu muhimu sana kupata hizi taarifa muhimu na kama ulivyosoma wewe usiache wewe tu ndio
ujue hili sambaza huu upendo kwa ndugu, jamaa na marafiki zako nao wao wapate taarifa hizi
muhimu.

Kwasababu kuna umuhimu kwenye kujifunza na hii elimu tunahitaji sana ili tusiwe nyuma kama
ulimwengu unavyoamini kuwa sisi tuko nyuma sana ila tuanze kuwaonyesha kuwa na sisi hatuko
nyuma kabisa.

Na naweza kukuahidi kama utaamua kutiliia maanani crypto labda inaweza kuwa njia ya kutokea
kwenye maisha binafsi nimewaona wengi wametoka kupitia crypto usikae kinyonge jifunze
crypto fanya crypto kuwa mtu wa crypto fanya chochote kile ili uwe ndani ya crypto kwasababu
crypto ni maisha yajayo na ni muhimu kuanza kujifunza sasa.
Asante sana kwa muda wako na wakati naamini kuna kitu umejifunza au umekipata tukutane
kwenye mafanikio.

CRYPTO NI MCHONGO

You might also like