You are on page 1of 84

1

2
“Ikiwa upo kwenye mitandao ya Kijamii na hujifunzi, hucheki,
huhamasiki na hujengi mtandao na watu, basi unaitumia vibaya.”
~Germany Kent

CHUO KIKUU
CHA
GOOGLE, LINKEDIN
NA
YOUTUBE
MAMBO 10 MUHIMU AMBAYO HUJAWAHI
KUAMBIWA KUHUSU MITANDAO YA KIJAMII

EDIUS KATAMUGORA

3
CHUO KIKUU
CHA
GOOGLE, LINKEDIN
NA
YOUTUBE

4
SHUKURANI

Kuwa na hisia za kutoa shukrani bila kuitoa ni


saw ana kuandika sms bila kuituma, kwa msingi
huu nimshukuru Mungu aliyenijalia kipaji hiki
cha uandishi na afya njema ya kuendelea
kupumua hewa safi ya oksijeni.

Nipende kuwashukuru ndugu zangu Kenneth


Mbakiza na Khalifa Said kwa kubuni jarada hili
zuri mno kwa ajili ya kitabu hiki. Unaweza
kuwasiliana nao kupitia namba hizi kwa
huduma zao za graphics designing:
• Kenneth Mbakiza - +255 622 588 707
• Khalifa Said - +255 653 118 448
Mwisho nikushukuru wewe kwa kuchagua
kusoma kitabu hiki. Yote yakishasemwa,
naomba usome vitabu vyangu kama

5
Natamani kusoma vitabu na Yusufu Nina
Ndoto na vingine vilivyopo nyuma ya kitabu
hiki.

6
UTANGULIZI
Je umewahi kutamani kuwa mtu wa hamasa
mtandaoni? Kama jibu ni ndiyo kitabu hiki ni
kwa ajili yako? Je unafahamu kwamba kupitia
mitandao ya kijamii unaweza kujifunza mambo
mengi zaidi ya darasani? Wakati naandika
utangulizi huu nilikua nachati na rafiki yangu
mmoja ambaye tumejuana siku za hivi karibuni
mtandaoni, akaniambia yeye anafahamu lugha
ya Kifaransa nikamuuliza ulisoma shuleni,
akanijibu, “Nimesoma vitabu na kujifunza
mtandaoni,” Mitandao ni vyuo vikuu ambavyo
wengi hawajavifahamu. Kama bado hauamini
katika hayo soma kitabu hiki mpaka mwisho.

Kitabu hiki ni kwa yeyote anayetaka kuuza au


kutambulisha huduma au hata kipaji chake
kupitia mitandao ya kijamii, kama ukiyafuata
yaliyoandikwa humu katika vitendo kuna

7
mabadiliko makubwa utayaona katika maisha
yako.

Kitabu hiki hakijaandikwa kwa watumiaji wa


google, LinkedIn na YouTube tu, kuna vingi
nimezungumzia mitandao mingine kama
WhatsApp na Facebook.

Tupo katika zama ambazo kati ya watu 5


unaokutana nao 3 wanamiliki simu zenye
intaneti, ni wakati sasa wa kuitumia mitandao
ipasavyo.

Kisome kitabu hiki na kiwe kama Biblia au


Kuruani ya kutumia mitandao ya kijamii na
nitafurahi endapo utanipa mrejesho baada ya
kitabu hiki kupitia mawasiliano yangu yaliyoko
mwishoni mwa kitabu. Usisite kuwasiliana

8
nami mara huhitajipo msaada kuhusu kitabu
hiki.

Mwisho ni vyema kabisa unapomaliza kusoma


kitabu hiki ukawarushia wengine nao wafaidike
kwani Wakenya wanao msemo usemao,
“Ukitaka kwenda haraka nenda peke yako,
ukitaka kufika mbali nenda na wenzako.”
Ni matumaini yangu kitabu hiki kitakuwa cha
msaada kwako wewe pamoja na marafiki zako.

Nakutakia safari njema ya mabadiliko katika


matumizi yako ya mitandao ya kijamii, binafsi
naamini, safari ya hatua elfu moja, huanza na
hatua moja.
Edius Katamugora
(Kijana wa Maarifa)
22/4/2020

9
TAARIFA MUHIMU
MWANDISHI WA KITABU HIKI
AMECHAGULIWA KUWANIA TUZO
ZA WAANDISHI BORA WA VYUO
VIKUU.

ANAOMBA UMPIGIE KURA KWA


KULIKE PICHA YAKE ILIYOPO
INSTAGRAM TAYARI UTAKUWA
UMEMPIGIA KURA.
ILI KUFANYA HIVYO BOFYA LINK
IFUATAYO HAPA CHINI:

https://www.instagram.com/p/B-
rlirXATeg/?igshid=pmz7cwp549lx

10
1. YAH: GOOGLE, LINKEDIN NA
YOUTUBE NI VYUO VIKUU. ADA
NI BANDO LAKO
Ukisoma kitabu changu cha PUMBA ZA
EDIUS {MAMBO MUHIMU
TUNAYOYACHUKULIA POA
MAISHANI} utakutana na maneno niliyoanza
nayo hapo juu. Maneno hayo niliwahi
kuyaandika facebook ingawa wengi
hawakunielewa.

Kwanza niweke hili wazi mimi nimekuwa


mtumiaji mzuri wa intaneti toka mwaka 2010
hivyo hadi leo hii nimetimiza miaka zaidi ya
kumi nikitumia intaneti, jambo la kushangaza
zaidi ni kwamba faida au matumizi sahihi ya
intaneti nimekuja kuyafahamu mwaka 2016
miaka 6 baada ya kuanza kutumia intaneti.

11
Toka hapo nimekuwa muumini mzuri wa
kuwahasa watu watumie intaneti kwa matumizi
sahihi ingawa bado wengi hawajajua matumizi
yake, wanakuwa kama mimi siku za mwanzo.
Imani yangu kubwa huwa inakwenda na
msemo huu wa kiingereza kuhusu intaneti,
“The Internet is the future,” ni kimaanisha
kwamba intaneti ni wakati ujao au wakati ujao
umebebwa na intaneti.

Jambo la muhimu kufanya hapo ni wewe


kuununua wakati ujao na si kusubiri wakati huo
ufike ndipo ushtuke, utakuwa umeachwa
mbali.

Nimesema kwamba google, linkedIn na


YouTube ni vyuo vikuu kwasababu sehemu
hizo ukizitumia vizuri unaweza kumshinda

12
mwanafunzi anayekaa darasani akisubiri
profesa aje kumfundisha.

Tuanze na Google:
“Google kila kitu. Namaanisha kila kitu.
Google ndoto zako, google matatizo yako.
Usiulize swali kabla haujaligoogle, utapata
jibu au utapata swali bora zaidi,” anasema
Austin Kleon mwandishi wa vitabu.

Msemo huo wa Austin umeshakuwa kama


mwongozo kwenye maisha yangu nikikutana
na kitu ambacho sikijui au kinanitatiza naanzia
google kwanza. Swali la kukuuliza ewe msomaji
wewe google huwa unakwenda kutafuta nini?

Kwiukweli nimejifunza mengi kupitia google,


watu wengi huwa naanza kuwaeleza vitu vingi

13
na naona wananishangaa lakini vyote hivyo
huwa navitoa google. Nikupe mfano tu
nimejifunza namna ya kutangaza matangazo ya
Facebook na Instagram kwa kutumia google.

Kupitia google nimejifunza ujuzi huo ambao


unalipa kw asana katika zama hizi. Mpaka leo
najifunza Copywriting ambao ni ujuzi wa
kuandika matangazo, nimejifunza mauzo
kupitia google, vitu vingi ambavyo darasani
ninashindwa kuvielewa huwa naamini kwamba
walimu zaidi ya kumi wa google watanipa njia
fupi ya kuelewa mambo hayo n ani kweli
nimekuwa nikielewa mambo hayo.

Mimi binafsi uandishi wangu ulianzia katika


kuandika blogu, ndipo baadae nikahamia huku
kwenye vitabu na kuandika makala gazetini.
Kuanzia kufungua blogu hadi kuiendesha
14
vyote nilijifunzia google. Unaweza kutazama
kazi zangu kupitia www.bideism.blogspot.com

Leo nikushauri kitu rafiki yangu kama unataka


kujifunza mambo mengi au jambo fulani
hakikisha unaitumia google ipasavyo. Google
isiwe sehemu ya kupakua miziki au kuangalia
skendo za wasanii, kumbuka hawa
hawakusaidii kupeleka mkono kinywani,
kutimiza ndoto zako au kuilisha familia yako.

LINKEDIN
“LinkedIn leo ni kama Facebook 2012.”
~ Gary Vee
Siku ya kwanza kuandika kuhusu LinkedIN
nilishangaa kuona watu wengi hawaujui
mtandao huo. Kiufupi LinkedIn ni mtandao
wa kijamii kama zilivyo WhatsApp, Twitter,
15
Tiktok na Instagram. Kutojulikana kwa
LinkedIn ni kwamba huo ni mtandao wa watu
wenye kazi (professions) mbalimbali. Ni
mtandao wa wabobezi kwenye sekta
mbalimbali. LinkedIn hakuna vichekesho
huko.

Kama Gary Vee anavyosema sasa hivi mtandao


huo ni kama ilivyokuwa facebook 2012 mwaka
huo facebook ilikuwa na watumiaji wachache.
Kama unakumbuka nimesema mwanzo
nilijiunga na facebook 2010 wakati huo hata ile
sehemu ya ‘people you may know’ nilikuwa
simfahamu mtu hata mmoja, marafiki zangu
niliofungua nao akaunti siku hiyo ndiyo watu
pekee niliokuwa nawafahamu, urafiki wa muda
huo ukawa tu wa kuomba bila hata kumfahamu
mtu.

16
Leo hii ni kinyume, ukijiunga tu na facebook
wataanza kukuonesha watu walio kwenye
mawasiliano yako kwanza. Leo karibia kila mtu
yumo facebook.

LinkedIn ni mtandao mzuri kama unahitaji


kuikuza taaluma yako, huko utakutana na
wabobezi katika sekta yako ambao
watakushirikisha mambo mbalimbali
waliyojifunza makazini. Sikuhizi akaunti ya
LinkedIn pia zinatumiwa na mabosi kuangalia
uwezo wa mtu pale anapoomba kazi, yaani
akaunti yako inaweza kutumika kama CV.

Kitu kingine bora ambacho nimekiona cha


utofauti huko LinkedIn ni kwamba huwa
kampuni kubwa zinatangaza nafasi za kazi.
Mpaka kampuni ziuamini mtandao huo kama

17
sehemu ya kutafuta watu wa kuwapa kazi basi
ujue kwamba mtandao huo sio wa kitoto.

Kama bado ujajiunga na mtandao huo fanya


hivyo haraka sana ujikonekti na watu
waliobobea kwenye kazi unayoyatamani kuja
kuifanya au unayoifanya.
YOUTUBE
Kama ilivyo google YouTube pia ni injini
ambayo unaweza kutafuta mambo mbalimbali
na ukajifunza pia.
Mtandao wa Youtube unao walimu wengi
ambao wanapatikana toka kila kona ya dunia.
Mambo mengi ambayo mwalimu wako wa
darasani anakufundisha na unaona ni magumu
kupitia YouTube unaweza kupata mwalimu
atakayekufundisha kwa njia nyepesi na
ukaelewa kwa haraka.
18
YouTube pia kuna kozi nyingi ambazo
hufundishwa kwa njia ya video ukiweza
kujifunza kozi mojawapo na kuijua ipasavyo
wewe utakuwa haukamatiki, yaani kila mtu
atatamani kufanya kazi na wewe.
Hapo nyumba nilitamani kuanza kutengeneza
video za YouTube kwa ajili ya chaneli yetu
iitwayo LISILOWEZEKANA
LINAWEZEKANA. Rafiki yangu mmoja
aitwaye Edward alinipa mwongozo wa namna
ya kuanza kisha akanimbia tafuta video
nyingine YouTube ujifunze, kilichobaki ni
historia. Leo hii naweza kuediti video hizo kwa
ubora na nimeweza kuwafikia watu wengi mno.
Kitu ambacho kabla nilitamani kwenda
kumlipa mtu anifundishe kupitia Youtube
nimeweza kujifunza tena ndani ya muda mfupi.
Edward niliyemzungumzia hapo juu yeye ni
graphics designer mzuri sana nilipomuuliza
19
alijifunzia wapi ujuzi huo aliniambia kwamba
alijifunza kupitia video za Youtube. Unaweza
kuona kwamba Youtube ni darasa tosha.

ADA YA YOUTUBE, LINKEDIN NA


GOOGLE
Kama vilivyo vyuo vikuu vingine ambapo
unahitaji kulipa ada, ada ya mitandao hiyo ni
bando ambazo huwa unanunua. Kazi ni kwako
kutumia bando unalonunua kutazama umbea,
mambo yasiyo ya maana na mengineyo au
kujifunza kupitia mitandao hiyo.

Jambo jingine ambalo naweza kuongeza hapa


ni kwamba kila unaponunua vocha na kuweka
MB katika simu yako mitandao ya simu
inafaidika, je wewe unafaidika vipi na vocha
uliyonunua? Jibu zuri la swali hilo ni kuitumia
20
mitandao niliyoitaja hapo juu kama sehemu ya
kujifunza kila mara. Hakikisha kabla
haujaambiwa “Mpendwa mteja kifurushi chako
cha MB ….. kinakaribia kuisha,” kuna kitu
umejifunza au kufaidika nacho kwenye
kifurushi hicho.

21
2. KUWA NA WAFUASI WENGI
MTANDAONI HAIMAANISHI
KWAMBA UNAWEZA KUUZA AU UNA
HAMASA KUBWA KWAO
Kitu kikubwa ambacho watu wengi wanalilia
mara nyingi mtandaoni ni kuwa na followers
wengi.
Kuwa na followers wengi hakuna maana
yoyote kama hauwezi kuwabadili hao followers
kuwa wateja wa kazi zao.
Ukweli lazima usemwe, Likes haziliwi,
kuonekana maarufu mtandaoni wakati hauna
pesa mfukoni ni upuuzi.
Watu wengi wana wafuasi wengi mitandaoni
lakini wanashindwa kuwabadili kuwa wateja wa
kazi zao.
Umewahi kusikia mtu aliyekuwa na wafuasi
milioni 2.6 instagram na akashindwa kuuza
22
tisheti 36? Ndiyo wafuasi milioni 2.6 wala
sijakosea.
Arianna Renee aliyekuwa na wafuasi milioni 2.6
instagram anayetumia jina la @arii alishindwa
kuuza brand yake ya Tisheti inayojulikana kama
ERA kwa wafuasi wake hao mamilioni.
Unaweza kujiuliza mtu huyo alishindwaje
kuuza Tisheti hizo chache wakati ana wafuasi
wengi. Jibu ni moja hakuwa mtu anayetoa
thamani (value) kwa watu wake.
Ukitaka kuwa na wateja kupitia mitandao ya
kijamii toa thamani hata ukiwa na watu 1000
wanaoamini kwenye thamani unayoitoa tayari
wewe ni tajiri. Sikuzote unapokuwa unataka
kuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao
kumbuka watu wanakufuata kwa ajili ya
thamani unayoitoa.

23
3. MAUDHUI NI MFALME
Katika kipindi hiki tulichomo ambacho kila
mtu anamiliki simu janja (smart phone) ni
muhimu kukumbuka hili Maudhui ni Mfalme.
Maudhui ndiyo pesa.
Kwa wastani mtu mmoja hutumia karibia saa 5
mtandaoni watu hawa huwa wanatafuta
maudhui yaliyobora. Mtu mwenye maudhui
bora ndiye anayepewa jicho kubwa mtandaoni.
Ili upewe jicho kubwa mtandaoni maudhui
(content) yako yanahitaji kuwa ya kipekee.
Ukiwa na maudhui ya kutoa kwa watu wengine
tambua kwamba watu wakijua unakoyatoa
watakimbilia huko.
Amini pia kwenye unachokifanya, kifanye na
watu wanaopenda kitu unachokifanya
watajileta kwako.

24
Nitakupa mfano mdogo nilianzisha kuandika
misemo niliyoipa PUMBA ZA EDIUS katika
mtandao wa facebook mwanzoni watu
hawakunielewa nikapata vipingamizi vingi
kwamba nakosea. Baadaye nikaamua
kutengeneza kitabu, kitabu hicho kwa muda wa
wiki mbili kimewafikia zaidi ya watu elfu 30.
Tena kwasababu nilikuwa natoa kitabu hicho
bure baadhi ya walioomba kitabu hicho ni wale
ambao walinibeza wakisema nakosea. Pointi ya
kuchukua hap ani kwamba amini kwenye kile
unachokifanya.
Jambo jingine la kufahamu kuhusu maudhui ni
kwamba kadri unavyoendelea kuposti ndivyo
watu wanazidi kuvutiwa na wewe ndivyo watu
wanazidi kukufahamu. Usitegemee kuposti kit
umara tat una uache eti watu watajua unafanya
nini, hilo halihitaji miujiza. Miujiza
unaitengeneza kwa kuposti mara nyingi kadri
uwezavyo kama upo kwenye mashindano
25
ukilala wenzako wanaamka. Ukiacha kuposti
watu wanakimbilia kutazama wengine.
Waingereza wanasema, “Consistency is the
key,” yaani kuendelea kufanya kitu bila kuacha
ndiyo ufunguo.

Mambo Muhimu ya kufahamu hapa:


Maudhui ni mfalme, watu wanatafuta
maudhui bora.
Roma haikujengwa kwa siku moja. Kadri
unavyoweka maudhui yako mtandaoni
ndivyo watu wanavyozidi kukufahamu au
kuvutiwa na wewe.

26
4. WHATSAPP NI DUKA
WANALOLITUMIA WACHACHE
Pamoja na kuchelewa kuifahamu na kuitumia
vizuri WhatsApp business mimi ni
mmojawapo wa waliofanya biashara kupitia
whatsapp ya kawaida. Nimeuza vitabu,
masweta, tisheti nimetangaza biashara za watu
na wamepata wateja.
Siku si nyingi zilizopita tuliunda kundi la
whatsapp liitwalo DREAM TEAM katika
kundi hilo tunatangaza biashara ya mtu mmoja
kila siku kwenye kundi kupitia status, hii
imetuwezesha kuwafikia wateja wengi ambao
hata kabla hatukuwahi kutarajia.
Inawezekana unaona sehemu ya status kama
sehemu ya kuposti memes na vichekesho
wenzako wanaona sehemu ya kutangaza
biashara. Amka sasa usisubiri upate fremu
ndipo uanzishe biashara yako nawafahamu
27
wengi ambao kupitia biashara zao
wanazozifanyia nyumbani kwao wameweza
kukuza brand zao kupita mitandao ya kijamii na
kuwafikia watu wengi.
Huwa nashangaa mtu ana views zaidi ya 200
kwenye status za whatsapp na analia njaa.
Kama wewe ni mmojawapo unafanya makosa
makubwa. Kati ya hao watu 200 ukipata walau
wateja kumi wa biashara yako hauwezi kulilia
njaa. Amka sasa anza kufikiria whatsapp kwa
picha ya tofauti. “Ukibadili unavyofikiri
unabadili unavyozalisha,” anasema Askofu
Joel Osteen. Badili leo unavyofikiri kuhusu
Whatsapp.
Nafurahi kuona leo baadhi ya watu wanaweza
kuwa na madarasa katika makundi ya whatsapp
ili mtu ajiunge na makundi hayo na kupata
elimu ya watu hao kuna kiasi anabidi kuchangia
ilia pate huduma hizo. Jiulize wewe unajua nini

28
ambacho unaweza kukifanya kama darasa
mtandaoni?

29
TAARIFA MUHIMU
MWANDISHI WA KITABU HIKI
AMECHAGULIWA KUWANIA TUZO
ZA WAANDISHI BORA WA VYUO
VIKUU.

ANAOMBA UMPIGIE KURA KWA


KULIKE PICHA YAKE ILIYOPO
INSTAGRAM TAYARI UTAKUWA
UMEMPIGIA KURA.
ILI KUFANYA HIVYO BOFYA LINK
IFUATAYO HAPA CHINI:

https://www.instagram.com/p/B-
rlirXATeg/?igshid=pmz7cwp549lx

30
5. Mashabiki 1000 wa Ukweli
Dhana hii ya mashabiki 1000 wa ukweli
inatokana na makala iliyoandikwa na Kevin
Kelly mwaka 2008
Hii ni kwa waandishi, wanamuziki, mabloga,
wanotengeneza video za Youtube, na wote
wanaotengeneza kitu chochote. Ukweli ni
kwamba hauhitaji kuwa na mjomba
atayekukopesha ili uanzishe biashara. Hauhitaji
kuwa na wafuasi milioni ili kuanzisha baishara.

Ukweli ni kwamba unahitaji mashabiki 1000 wa


ukweli. Kelly anasema, ukitaka kutengeneza
kipato unahitaji kutafuta watu 1000
wataopenda kununua bidhaa yako au kitu
unachozalisha. Kama utaweza kufanya hivyo,
utaweza kutengeneza pes ana kuishi maisha
yako yote bila wasiwasi.

31
Kama ukiamua kutengeneza shabiki mmoja
kila siku itakuchukua miaka 3. Kitu cha
kuzingatia hapa ni kuwa na mawasiliano
endelevu kila mara.

Mashabiki wa ukweli si sawa na masahabiki wa


kawaida hawa watakuwa tayari kununua bidhaa
zako, kama ni msanii hawatakosa shoo zako,
watakuwa tayari kukutangaza ili wengine
wakujue. Kimsingi mashabiki wa ukweli
huwaambii kitu kuhusu wewe.
Nafikiri umewahi kumsikia mtu akimtetea
msanii fulani kana kwamba anamlipa. Huyo ni
shabiki wa kweli.
Kuanzia leo fokasi yako kubwa iwe ni
kuwapata hao mashabiki 1000 wa ukweli na si
mashabiki tu.

32
6. JINSI YA KUUZA NA
KUTENGENEZA BRAND YAKO KWA
KUTUMIA MITANDAO YA KIJAMII
Zama zimebadilika, mambo yamebadilika.
Ujio wa intaneti umefanya mapinduzi
makubwa katika biashara hasa kwa karne
hii ya ishirini na moja. Utangazaji wa
biashara kupitia magazeti na televisheni
kwa kiasi kikubwa hauna nguvu tena kama
ilivyokuwa hapo zamani.

Mitandao ya kijamii imeteka kwa kiasi kikubwa


biashara nyingi hii ni kwasababu watu wengi
wanatumia mitandao ya kijamii. Na moja wapo
33
ya kanuni za kufanya mauzo ni kuwafata wateja
mahali walipo. Wateja wengi wapo kwenye
mitandao ya kijamii hivyo ni wajibu wako
kuwafata huko.

Wakati watu wengine wanajiunga na mitandao


ya kijamii ili waweke picha zao na maandishi ya
kuchekesha kusudi wapate like kuna watu
wengine wametengeneza pesa kubwa kupitia
mitandao ya kijamii. Je wewe umewahi kufikiri
kutengeneza pesa kupitia mitandao ya kijamii?
FAIDA ZA KUTUMIA MITANDAO YA
KIJAMII
1. Ni rahisi sana kujifunza hivyo mtu yeyote
anaweza kujifunza na kuanza kuitumia
mitandao ya kijamii kikamilifu.
2. Ni gharama ndogo ya kujitangaza kwa wateja
ukilinganisha na magazeti na TV.
3. Mitandao ya kijamii hujenga uaminifu. Watu
wanapenda kufanya biashara na mtu
wanayemfahamu. Hivyo ni rahisi kupata wateja
wanaokufatilia kwenye mitandao yako.
34
4. Unaweza kuwasiliana na wateja wako moja
kwa moja.
5. Mitandao ya kijamii itakusaidia kupata
wasomaji wa blogu au website yako kama
unamiliki blogu au website.
6. Mitandao ya kijamii itakusaidia kujua na
kufanya uchunguzi wa soko. Utajua watu
wanataka nini na hawataki nini.
7. Inakuongezea uthamani. Ukiweza kuwa mtu
anayeweka mambo ya maana kwenye mitandao
yako, thamani yako itapanda.
8. Watu watakutafuta na kufanya kazi na wewe.
Ukitengeneza jina lako vizuri katika mitandao
ya kijamii watu wakubwa watahitaji kufanya
kazi na wewe. Mimi ni shuhuda wa hili, baada
ya kuanza kuandika Makala mbalimbali katika
blogu yangu ya BIDEISM nimekuwa
nikitafutwa na watu mbalimbali ili tufanye kazi
pamoja.
9. Itakufungulia connection mpya. Ukiweza
kujibrand vizuri utaweza kufanya kazi na

35
kupata connection kubwa ambazo hata kabla
ulikuwa huzitarajii.

JINSI YA KUTENGENEZA BRAND


YAKO MTANDAONI.
1. Hakikisha unaandika mambo yanayowagusa
watu mara nyingi uwezavyo. Kuna watu wengi
wanatafuta namna ya kutatua matatizo yao. Ni
jukumu lako kuwaonesha namna gani
wanaweza kuyatatua. Hii itakuchukua muda
watu kuanza kukuelewa na muda mfupi ambao
utakuchukua ni miezi 6. Watu mara nyingi sio
rahisi kukuelewa lakini kadri unavyoendelea
watakuelewa. Hivyo usikate tamaa.
2. Angalia wenzako wanafanya nini katika
mitandao yao ya kijamii. Ukiona kuna mtu
anafanya kitu ambacho ulikua ukitamani
kukifanya mtafute na ikiwezakana omba
ushauri kwake akupe njia yeye anawezaje.
Kama yeye ameweza unaweza pia. Kama mimi
nimeweza, wewe pia unaweza.

36
3. Kuwa mtu wa watu. Ukiwajali watu
watakujali pia. Unahitaji kuwa mtu wa watu
katika mitandao ya kijamii. Wajibu watu kwa
heshima, tumia maneno kama; kaka au dada
yanasidia sana. Asikwambie mtu watu
wanapendwa kuheshimiwa. Ukiwapa heshima
watakuja kwako.

4. Uonesha ujuzi wako:


Kuna watu wengi wana ujuzi lakini kwenye
mitandao yao ya kijamii hawoneshi ujuzi huo.
Wanafanana na yule mtu aliyepewa talanta
akaificha. Usikubali kuwa na ujuzi halafu
kwenye mitandao yako ya kijamii hauuoneshi.
Ujuzi wako ni pesa uliyoikalia.

JINSI YA KUJITANGAZA KUPITIA


MITANDAO YA KIJAMII
Takwimu zifuatazo zinaonesha matumizi ya
mitandao ya kijamii nchini Tanzania toka
Machi 2017 hadi mwezi Machi 2018:
37
MTANDAO ASILIMIA YA
WATUMIAJI
Facebook 59.98%
Youtube 17.36%
Pinterest 12.67%
Twitter 5.97%
Instagram 2.27%
Google+ 0.67%

Ukichunguza kwa ukaribu unaweza kujua ni


mtandao upi ambao una watumiaji wengi.
Unahitaji pia kujua wateja wako wanatumia
mtandao upi na inakupasa ujiunge pia na
mtandao huu. Kumbuka biashara huenda kule
wateja waliko. Kama wateja wako
wanapatikana WhatsApp hakikisha umejiunga
Na WhatsApp pia.

38
MAMBO YA KUFAHAMU KABLA
KUANZA KUTUMIA MITANDAO YA
KIJAMII KUJITANGAZA:
· MALENGO:
Unahitaji kuanza kwa kuandika malengo yako
kwanini unataka kutumia mitandao ya kijamii
kujibrand na kufanya biashara. Hatupangi
kushindwa tunashindwa kupanga, watu wengi
hawapangi ndiyo maana malengo yao
hayatimii.

· Jua ni wapi wateja wako. Ukijua watu gani


watakua wateja wako utakua umejiweka
kwenye wakati mzuri. Je ni vijana? wazee Au
wanafunzi, wazazi, kutaja wachache.

· Ni wapi wanapatikana.
Ukijua ni mitandao gani wateja wako
wanapatikana hakikisha unawafata huku. Hapo
utakuwa umelishika soko lako.

39
MAMBO YA KUZINGATIA:
1. Uaminifu.
Kama hautakuwa mwaminifu katika kazi zako
ni bora usifanye biashara kupitia mitandao ya
kijamii. Uaminifu ni nguzo kubwa katika
kufanya biashara kupitia mitandao.

2. Kanuni ya 7/1
Kama katika post unazoziweka katika
mitandao yako ya kijamii hakikisha post 6
zinazungumzia au kuelezea bidhaa zako na
ujuzi wako na post moja ambayo ni ya saba
ndiyo iwe tangazo la bidhaa yako. Ukiwa mtu
wa kutangaza bidhaa tu utawaboa watu na
wataacha kukufatilia. Weka vitu vingi
vinavyowaelimisha na ndipo uweke matangazo
ya bidhaa zako.

3. Kuwa muwazi.
Ukionekana kwenye mitandao ya kijamii
onekena kama mtaalamu. Usionekane kama

40
watu wengine. Kumbuka watu wanhukumu
kava ya kitabu na ni kilicho ndani ya kitabu.
4. Unahitaji kuwa mbunifu. Usifanye mambo
kwa mazoea, kila siku jiulize swali ili:
nitafanyaje kwa ubora Zaidi ya jana? Hilo ni
swali unalopaswa kujiuliza kila siku.

UZUSHI KUHUSU MITANDAO YA


KIJAMII
Kuna uzushi mwingi utausikia lakini na
kuahakikishia kwamba mitandao ya kijamii ni
chaguo jema kama utakua kweli umeamua
kijutanua kibiashara.
Uzushi kwamba mitandao ya kijamii ni ya
watoto:
Utasikia kuwa mitandao ya kijamii inatumiwa
na watoto lakini jambo hilo sio la kweli kabisa.
Takwimu zinaonesha kuwa watu wenye umri
wa kuanzia miaka 35 ndiyo wamekuwa
watumiaji wakubwa wa mtandao wa Facebook,
umri kuanzia miaka 24 hadi 34 huongezeka
mara mbili kila baada ya miezi sita. Watu wengi
41
wanaotumia mtandao wa Twitter wana umri
wa miaka 35-49. Watumiaji wa mtandao wa
LinkedIn wanao wastani wa umri wa miaka 41.

Uzushi kuwa unahitaji utaalamu wa


teknolojia kutumia mitandao ya kijamii:
Kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii
hauhitaji kuijua sana teknolojia ndipo uanze
kuitumia. Kanuni ya 80/20 inasema 80% ya
unachokiweka mtandaoni ni kile unachokitoa
na 20% ni ujuzi wa teknolojia. Hivyo usiogope
kuhusu teknolojia.

42
7. The Internet Is The Future
Jumanne ya tarehe 22 Julai mwaka 2019 nilipata
fursa ya kufundisha somo linaloitwa
INTERNET IS THE FUTURE katika kundi
la whatsapp lijulikanalo kama CYM
International

Yafuatayo ni baadhi ya yale niliyoyafundisha.


Nimechagua somo la intaneti kwa sababu kuu
moja. Imebeba maisha yetu makubwa lakini
bado hatujashutka. Bado tumelala. Kama kuna
walioamka katika matumizi ya intaneti ni
wachache.

Pointi ya kwanza kabisa ya kuanza nayo


darasani.

*Kama haupo kwenye intaneti, hauishi, kama


biashara yako haipo kwenye intaneti haiishi.
Imekufa.*

43
Njia nzuri ya kuwa kwenye sehemu nzuri ya
kuununua wakati ujao(buying the future) ni
kuwa kwenye intaneti.Nimekua nikiwaambia
watu, na nimeandika sana. Badala ya kuitumia
intaneti yenyewe inatutumia.

Nilisoma Twitter wakati fulani zaidi ya asilimia


80 ya watu hutumia intaneti vibaya huku
asilimia 20 tu ndio hufaidika tu.

Intaneti haikuwekwa itutumie bali


tuitumie, habari mbaya ni kwamba watu
wengi inawatumia.

Kuna faida nyingi za kutumia intaneti:

Mfano, kupakua vitabu vya kusoma, kama


unapenda kujifunza kwa video unaweza ingia
youtube. Kikubwa zaidi kuna online Courses
nyingi zinatolewa watu watu wengi hatujui,
Kama nilivyotangulia kusema leo kama

44
biashara yako unayoifanya haipo mtandaoni
biashara hiyo haipo. It doesn't exist.

Tumeshuhudia makampuni mengi makubwa


ambayo yamekuja miaka ya hivi karibuni, lakini
yamekuwa makampuni tajiri sana duniani na
yamegusa maisha ya watu.

Kuanzia
AMAZON
FACEBOOK
ALIBABA
KIKUU
YOUTUBE
UBER
TAXIFY.
NETFLIX

Leo hii watu wengi wanatumia intaneti.


Baishara nyingi zipo mtandaoni. Watu wengi
wanashinda kwenye intaneti. Huko ndipo
macho ya watu yalikohamia.
45
Kuna msemo usemao, "Biashara huenda
kule macho yanapokwenda."

Kama macho yapo kwenye mtandao hatuna


budi sisi wafanya biashara tuwe kwenye
mitandao pia.

Kama watu wanajua unachokifanya kwenye


mitandao watakua tayari kuwaambia wengine
kuhusu wewe. Nzuri zaidi unaweza fikia watu
wengi zaidi. Nafikiri umewahi ona kwenye
matangazo wanasema "Na mikoani tunatuma."

Kwenye mitandao ya kijamii kama unafanya


biashara kwanza lazima ujue wateja wako
wanapendelea nini. Sio wewe unapendelea nini
(mtandao). Kwa mfano kama ni mwandishi ni
rahisi sana kupata wateja wa kazi zako kama
unatumia:

46
Facebook Twitter na Linkedin. Anayeuza
bidhaa ni rahisi sana Instagram kuliko Twitter.

Njia ya kwanza ya muhimu ni kujua wateja


wako wanapenda nini.

Hapa whatsapp ni rahisi kuwa na darasa kuliko


insta au kwingineko. Mfano:

Kama ni mwandishi ni rahisi sana kuwapata


wasomaji Facebook na whatsapp kuliko
Instagram ambapo watu wengi huangalia
picha.

Watumiaji wengi wa insta huwa hawasomi


captions.

Sasa unawatekaje watu wakujue.?

Kwenye mitandaoni kila kitu ni Kujulikana


watu wengi wakikujua umetusua. Kama
hawakujui hakuna jipya utakalopata.
47
Kitu kimoja muhimu kwenye social medias:

*Content Content Content content*

Kwa kiswahili tunasema Maudhui.

Maudhui yako lazima yawe yameshiba. Kama


unauza viatu, je wewe ni mkali wa fashion?

Kama unachora, je una michora ya kuwavutia


watu?

Watu wengi hawatengenezi *content bora*


wanakimbilia kuuza.

Nitoe mfano tu. Mange Kimambi ni content


creator wa kujua watu kiundani hivyo hivyo
watu wa shilawadu.

Millard ni content creator wa habari na


matukio.
48
Joti ni content creator wa vichekesho.

Wewe ni content creator wa nini??

Kuna watu wanajiuliza, labda mimi nauza Asali.


Natengenezaje maudhui?

The best way ni kuwafundisha watu.

Mimi naandika makala zangu bure kwenye


mitandao hapo kuna watu nawafanya
wanakuwa wafuatiliaji wangu wa kila siku.
Hawa baadaye huwa wateja wa kazi zangu.

Unawafundishaje?

Kwa mfano muuzaji wa asali.

Wafundishe watu umuhimu wa kutumia asali.


Ni mambo gani watakosa kama hawatumii
asali, n.k
49
Toa elimu ya bure kuhusu bidhaa yako.

*Kosa la watu wengi wanatoa matangazo ya


bidhaa tu bila kutoa maelezo kama hayo*

Au unauza nguo, suruali za kadeti.

Watolee watu sababu za kuvaa kadeti za Geep,


au Zara badala ya kuvaa Polo. Ni mfano tu.
Lakini inakuonesha ni kiasi gani kwenye
mambo ya fashion umeiva.

Watu huwa wanawafuatilia wale


walioiva/waliobobea katika masuala
wanayoyafanya.

*People will follow you in your area of


competence.*

Watu wanaohusika na mambo ya branding


kwenye mitandao. Unaweza kupata watu wa
50
kuaminika wanaokufuatilia kwa kipindi cha
miezi 6 mfululizo. Haiji kwa usiku mmoja.

Kila kitu kina gharama. "Hauwezi kuwapa


mimba wanawake 9 ukategemea
wajifungue ndani ya mwezi mmoja."
(Warren Buffet)

Leo hii kila mtu anapost kwenye mitandao ya


kijamii. Kila sekunde, kila dakika, kuna content
mpya hutengenezwa.

Lazima utengeneze njia ya kuonekana. Kama


huonekani hauwezi kupata fan base ya uhakika.

So you need tu post at least ten pieces of


contents daily Kama haufanyi hivyo wenzako
na wanafanya na wanateka watu. Ipo wazi kuwa
kila mtu anataka kuonekana lakini
wanaonekana wale wanaokimbia na muda na
wanaopost sana. Nikupe Assignment ndogo,

51
hebu kaangalie Millard Ayo kwa siku anapost
mara ngapi.

Wakati unapost hivi vitu kumi hakikisha vina


uzito. Usifanye kwasababu Edius kasema eti
nionekane. Watu wanafuata vitu bora na si bora
vitu.

Wanaofanya kwa ubora ndiyo wanaoshinda.


Be different
Be exceptional. Usifanye kama mtu fulani
anavyofanya. Tafuta vyako na stick kwa vyako,
wanaopenda vitu kama hivyo watakuja. Dunia
hii ina watu wengi kila mmoja anaweza fikia
watu wake na maisha yakaenda.

"The internet is a copy machine" (Kevin


Kelly)

Chochote unachoweka kwenye mitandao


kinaweza kuwa kopidi na kusambazwa mara
nyingi. So be careful with what you post. Je
52
unapost vitu ambavyo mzazi wako au bosi
wako akiviona hata ona haya ya kukufahamu.

Before you post anything ask yourself this


question "I am posting this so what?"

Ukiona unapata majibu yasiyoeleweka please


usiposti.

Nimalizie kwa kusema kwamba "Mambo


madogo yakifanyika kwa muda mrefu
huwa makubwa."

Anza kidogo kidogo utafika pakubwa. Hakuna


njia nyingine ya kuanza nia kuanza kuanzia
sasa.

53
TAARIFA MUHIMU
MWANDISHI WA KITABU HIKI
AMECHAGULIWA KUWANIA TUZO
ZA WAANDISHI BORA WA VYUO
VIKUU.

ANAOMBA UMPIGIE KURA KWA


KULIKE PICHA YAKE ILIYOPO
INSTAGRAM TAYARI UTAKUWA
UMEMPIGIA KURA.
ILI KUFANYA HIVYO BOFYA LINK
IFUATAYO HAPA CHINI:

https://www.instagram.com/p/B-
rlirXATeg/?igshid=pmz7cwp549lx

54
8. ENDELEENI KUSEMA FACEBOOK
NI YA WATOTO

Nilitamani kuandika makala hii nyuma kidogo


lakini sikupata muda lakini nafikiri leo ndiyo
siku Mungu alipanga iruke hewani, kwa maana
binadamu tunapanga na Mungu anapanga.

Tuyaache hayo, twende kazi...

Siku nyuma kidogo nimekuwa nikiwauliza


watu maswali haya:

55
1. Unatumia facebook?
2. Au ntauliza facebook unatumia jina gani?

Majibu ambayo huwa nayapata huwa


yananiacha mdomo wazi.
Utasikia mtu anasema, "Facebook ni ya
watoto." au "facebook hainogi."
Aliyenifurahisha zaidi alisema, "Niliacha
kutumia facebook baada ya kugundua hata ma
house girl wamejaa huko."

"It's ok, it's ok" (In Pierre's voice)

Unasema Facebook ni ya watoto lakini bado


haujaona umuhimu wake. Binafsi nimekuwa
nikifuatilia mambo mengi kuhusu mitandao ya
kijamii. Natumia muda mwingi kuielewa na
kuisoma kwa makini.

56
Jibu ninalokupa leo ni kwamba facebook sio
ya watoto. (Naomba uwatag wote waliowahi
kukuambia majibu kama hayo hapa.)

Kama facebook ni ya watoto kina Strive


Masiyiwa wasingejisumbua kuja huku
kuandika mambo mengi kuhusu biashara.

Huyu mzee ukimfuatilia huwa hajibu


comments Instagram lakini huku Facebook
anajibu kila comment anayoona inafaa. Bado
unasema huku kumejaa watoto?

Biashara nyingi unazoona zimekua ni


kutokana na wateja kutoka huku facebook.
Binafsi nimetengeneza fan base kubwa
facebook kuliko kwingine.

Endeleeni kusema facebook ni ya watoto.

Je unayajua haya?

57
Leo hii kama facebook ingekuwa nchi,
ingekuwa nchi ya kwanza duniani kwa kuwa
na idadi ya watu wengi. Facebook
inawatumiaji bilioni 2.38 kwa mwezi, wakati
nchi ya China yenye watu wengi inakadiriwa
kuwa na watu bilioni 1.4

Watu milioni 1.56 huingia katika account zao


kila siku. Huku ongezeko likiwa asilimia 8 kila
mwaka.

58
Watu wengi wanaotumia mtandao huu ni
kuanzia miaka 25-34, ambao ni asilimia 29.7
ya watumiaji.

Kila sekunde profiles tano mpya hufunguliwa.

76% ya watumiaji ni jinsia ya kike ya 100% ya


wanawake na 66% ya watumiaji ni wa
kiume wakitoka katika asilimia 100 ya
wanaume.

Watu wengi huwa online kuanzia saa saba


mchana hadi saa tisa alasiri. Ukipost sa 7 watu
wengi wataona kuliki ukipost saa 8.(chanzo
Forbes)

Siku za Alhamisi na Ijumaa watumiaji huwa ni


wengi mno, ongezeko likiwa asilimia 18.

Kila siku picha milioni 300 huwekwa kwenye


mtandao wa Facebook.

59
Wastani wa kila mtu kutumia facebook ni
dakika 20.

Kila sekunde 60 kwenye facebook comments


510000 huandikwa na status 293000 huwa
zinakuwa updated na picha 136000 huwekwa
facebook (Chanzo: The social Skinny)

Asilimia 50% ya vijana wenye umri kuanzia


miaka 18-24 huwa wanaingia Facebook mara
tu waamkapo. (Chanzo: The social Skinny)

42% ya wafanyabiashara wanasema facebook


ni ya muhimu sana katika biashara zao.
Bado unaichukulia poa facebook?

Kupitia facebook nimepata marafiki wengu,


wateja wengi na nimejifunza vingi. Facebook
ni darasa tosha la maisha, (Kwa watu serious
lakini).

60
Kupitia facebook unaweza kutangaza biashara
yako kwa bei rahisi, hata kwa kupitia ukurasa
wako na bado ukapata wateja. Leo hii
kutangaza kupitia redio, Magazeti na
televisheni ni mambo yaliyopitwa na wakati.
Kwa kutumia dola moja kwa siku unaweza
kuwafikia zaidi ya watu 5000 kwa kutangaza
biashara yako na ukapata wateja. Jambo
jingine matangazo ya facebook yanakufanya
uwafikie wateja wa mbali zaidi bila ukomo.
Waliokuwa mnasema facebook ni ya watoto,
mnakwama wapi?

Sehemu nyingine ambayo nakushauri ujiunge


ni Twitter, kama hauna account kuwa nayo
sasa utajifunza mengi. Unaweza kunifollow
pia kupitia @katamugora

Rudi facebook kumenoga.

61
9. UNAWAJUA KIZAZI Y?
Inawezekana ni neno geni kusomeka au
kusikika masikioni mwako lakini ni vyema
uwafahamu watu hawa. Kwa jina jingine
wanafahamika kama kizazi za milenia kingereza
chake kikiwa Generation Y (Gen Y). Hawa ni
watu waliozaliwa kuanzia miaka ya 1982 hadi
kufikia mwaka 1994. Hawa ni watu muhimu
sana kwa sababu jinsi wanavyounhanishana na
kuwasiliana imeleta mabadiliko makubwa
katika ufanyaji wa biashara.
Kama unaanda mpango biashara ambao
haujalenga kizazi hicho jiandae kupata tabu
sana. Serikali pia inahitaji kuwapa jicho la tatu
watu hawa.
Kama umewafahamu je, unajua tabia zao?
Twende sasa nikupe tabia za kizazi hiki cha
milenia.
Moja, ifikapo mwaka 2025 asilimia 75 ya kizazi
Y ndio watakuwa watendaji kazi, ndio
62
watakuwa wameajiriwa au wamejiajiri. Hawa
ndio watakuwa wameshika mzunguko wa
fedha, ndiyo maana nikasema kuwa na mpango
biashara bila kuwatizama wao jiandalie kifo cha
biashara yako.
Kizazi cha milenia kinatizama TV kwa kutumia
kifaa cha kielectronic zaidi ya kimoja.( Kuna
haja ya kuwa na online TVs kwa wamiliki wa
vituo vya television). Hawatizami TV san ana
hawasomi sana lakini wanasikiliza zaidi kile
marafiki zao wanachokisema.
Kizazi za milenia huwaamini zaidi watu wa
mbali na walipo zaidi ya marafiki wa karibu na
hata familia. Hawa wanaweza kununua kitu
kwa kutizama ni nani kakitumia ambaye ni mtu
maarufu.
Wanaweza kufuata(kufolo) brand mtandaoni
Mara tatu zaidi kuliko kumfuata mtu wa karibu
wa kwenye familia yao. (Ukiwa na brand
iliyosimama watakufuata tu)
63
Asilimia 66 yao wataingia kwenye duka fulani
kununua bidhaa kama watamwona rafiki yao
akiwa humo. (Watanunua bidhaa kama
wataona rafiki yao akitumia bidhaa hiyo)
Kizazi za milenia huamini kuwa watumiaji
wenzao wa bidhaa wanajali zaidi ya
mfanyabiashara anayeuza bidhaa, hivyo
huweka maoni yao mtandaoni kuhusu bidhaa
hiyo. (Kuna wakati kampuni ya Tigo ilianzisha
kampeni ya JAZA UJAZWE. Hawa ndio
walikuwa watu waliokataa kampeni hiyo kupitia
mtandaoni hivyo haikudumu)
Wanatumia sana Facebook na Instagram zaidi
ya watu wengine.
Kizazi Y hupenda “Uzoefu” kwanza
wanapenda wakitumie kitu kwanza ndipo
watakaposema wanakipenda ama hawakipendi.
Ni watu wa kidunia sana kwasababu teknolojia
imekuwa sehemu ya maisha yao.

64
Utauzaje kwa kizazi hiki? Wataalamu wanaodili
na kizazi hiki, yaani kizazi Y wanatoa vigezo
muhimu ili watu hawa wawe wateja wako.
• Gharama ndogo
• Ubora
• Huduma ya haraka (fast service)
• Uzoefu “experience”
Kizazi Y wapo konektedi sana mtandaoni zaidi
ya vizazi vilivyowahi kuwepo au wazazi wao.
Kwa kutumia intaneti wanaweza kujifunza
chochote saa 24 kwa siku.

Jambo la kuzingatia hap ani kwamba ili Kizazi


Y kiwe soko lako hauna budi kuwa
mwanamitandao, lazima uwe na kurasa kama
za facebook na Instagram.

65
WAFAHAMU PIA KIZAZI Z
Hawa walizaliwa kati ya mwaka 1995-2004.
Usichokijua ni kwamba watu hawa
wanakamilisha asilimia 18 ya watu wa dunia
nzima. Waitwa Generation Z.
Ingawa bado ni wadogo bado wanauwezo wa
kupata teknolojia na vifaa kama simu, iPods,
tablets na kompyuta na teknolojia hii ndiyo
inatoa taswira ya maisha yao.
Hawa ndio kizazi cha digitali. Wamekulia katika
kizazi cha usawa, wanaamini kwamba
wanaume na wanawake wote ni sawa.

Ukiongelea kizazi Y unaiongelea kompyuta.


Hawa ni kizazi cha kidigitali. Mawasiliano yao
yote hufanyika kwenye intaneti.
Shida kubwa waliyonayo kizazi hiki ni kwamba
hawawezi kumudu vyema mawasiliano ya ana
kwa ana. Kwenye akili yao wanajua kwamba
66
mawasiliano hayo hawayahitaji. Kwasababu
hawajawahi kuijua dunia bila intaneti. (Nafikiri
ni hawa hawa ambao bando zikipandishwa bei
wanakuwa wakwanza kulalamika mtandaoni).
Wanapenda spidi na kuridhishwa haraka sana.
Kila kitu wanachokitaka au wanachotaka
kujifahamu wanaweza kukipata papo hapo.
Hivyo, hawana uvumilivu na wanapenda
matokeo ya haraka.
Kizazi Z pia wanaamini kwamba hawapaswi
kukufahamu wao kama wao au marafiki zako.
Wanaweza kuanzisha mahusiano kwenye
intaneti au mitandao ya kijamii.
Wanaunda makundi kwenye mitandao ya
kijamii na kushirikiana bila hata kufahamiana
wao kwa wao yaani hawajawahi kukutana.
Kizazi Z wanahitaji nini na wanatarajia nini
toka kwako? Hivi ni baadhi ya vitu
vitakavyokusaidia ili kuwafanya wawe wateja
wako:
67
• Kununua vitu mtandaoni na kupakua
(Online shopping & downloading)
• Spidi na suluhisho katika mauzo ambavyo
hutoa majibu na kumwezesha mtu
kununua kwa haraka.
• Uwezo wa kupata huduma kutoka kwako
bila wewe kuwabughudhi au kuwapigia
simu.
• Uwezo wa kubofya mtandaoni na kuweza
kulipia haraka kabla hawajaenda kwenye
kununua kitu kingine.
• Kwa kampuni za mazingira na
zinazotengeneza bidhaa za kimazingira.
Kizazi Y ndicho kizazi kinachohitaji
uelewa mkubwa kuhusu hayo mambo hivi
sasa.
• Mawasiliano ya kielektroniki: Kwasababu
wamekua na sim una wanatumia muda
wao kutuma meseji na kujamiiana
mitandaoni, wanategemea marafiki zao,
familia zao na wafanyabiashara
68
kuwasiliana nao mtandaoni. Ili uweze
kuuza kwa hawa watu wasiliana nao kwa
barua pepe, meseji za kawaida n ahata
kwenye mitandao.
• Ucheshi: Mtandao wa kijamii wa Habbo
wa nchini Australia ambao uliwalenga
watu wenye umri kuanzia miaka 8 hadi 12
kwenye kizazi chao kijacho uliwahi
kufanya uchunguzi na waligundua
kwamba walipouliza, “Unapendelea
matangazo gani?” asilimia 46 ya kizazi Z
walisema, “Matangazo yanayonifanya nicheke
au kufurahi.”
Ukiweza kujua kizazi gani wanatabia zipi na
wanapenda nini ni rahisi kuwafikia haraka
sana na kuwafanya wawe wateja wako wa
kudumu.

69
10. EPUKA KUSHIKA SIMU YAKO
MARA TU UNAPOAMKA

Kama kuna tabia ambayo tunapaswa kuanza


kuijenga ni kuamka na kufanya mambo yako
kabla ya kushika simu.

Simu hizi ni nzuri lakini tabia ya kuamka na


kutizama mtandaoni kuna nini imekuwa
ikitugharimu sana.
70
Kwa mfano ukiamka na mood ya kutosha
ukashika simu yako na kukuta habari mbaya
tayari siku yako itakuwa imeharibika kwa kiasi
fulani.

Au ukiamka na nguvu ukashika simu yako na


kukuta ujumbe wakukuhuzunisha nguvu zako
mara moja zitakwisha. Hata kama una mipango
mingi kwa ajili ya siku husika lazima mipango
yako ivurugike.

71
Hakikisha walau dakika 30 za kwanza baada ya
kuamka haushiki simu na unajiweka bize na
mambo ya msingi.

Ukiifanya hiyo iwe tabia yako itakufanya ufanye


mambo mengi kwa weledi mkubwa na
uzalishaji utakuwa mkubwa.

Asubuhi kabla ya kushika simu yako kuna


mambo mengi ya kufanya; kusali, kufanya
mazoezi ya viungo, kujisomea kitabu, kufanyia
mazoezi kipaji chako, kupata kifungua kinywa,
na kutafakari. Kutaja machache.

Ifanye asubuhi yako kuwa njema kwa kuepuka


habari mbaya. Kumbuka, "Maisha huanza
asubuhi," kama anavyosema Pastor Joel
Osteen.

Kama maisha huanza asubuhi kwanini huanze


kwa kupoteza thamani ya maisha kila
kunapokucha?
72
Njia nyepesi ya kuamka na kutoshika simu ni
kuweka simu yako katika flight mode muda
unapokwenda kulala, hata kama unasoma
kitabu chako kupitia nakala tete hautakuwa na
muda wa kusumbuliwa na mtu kupitia ujumbe
mfupi(sms) au kupigiwa simu au ujumbe wa
whatsapp na mitandao mingineyo.

Mara nyingi pia mitandao ya kijamii imekuwa


ikila muda wetu mwingi wa asubuhi. Hilo sio
jambo jema.

Ukiwa mtumiaji mkubwa wa mitandao ya


kijamii kwa muda mwingi unakuwa kama mlevi
wa pombe au mvutaji sigara. Kuna kemikali
inayoitwa Dopamine ambayo huzalishwa na
ubongo.

Kemikali hiyo hukufanya mtu ujisikie vibaya


kama haujaingia mtandaoni. Unakuwa mlevi

73
wa mitandao. Mitandao ya kijamii haikujengwa
ili sisi tuwe walevi wake.

Ugonjwa ambao watu wengi wanao unaitwa


FOMO(Fear Of Missing Out) kwa kiswahili
tunaweza kusema ugonjwa wa kutaka kila kitu
kisipite bila wewe kujijua, kama asemavyo
Austin Kleon mwandishi wa vitabu. Huo ni
ugonjwa unaowatafuna watu wengi.

Dawa ya ugonjwa huo inaitwa JOMO (Joy Of


Missing Out) yaani furaha ya kukosa baadhi ya
74
vitu. Sio kila kitu kinachowekwa mtandaoni
lazima ukione au ukisome. Niliwahi kusema
siku za nyuma, "Mitandaoni kuna mambo
mengi, chambua ni yapi uchukue
(yanayokuhusu na ya muhimu) na mengine
yaache kama yalivyo"

Mitandao haikujengwa ili itutumie, iliwekwa ili


tuitumie lakini maajabu ni kwamba sasa
inatutumia. Inasikitisha sana.

Jaribu kupunguza matumizi mengi ya mitandao


ya kijamii. Ifanye asubuhi yako kuwa njema
kwa kutoamkia mtandaoni. Fanya mambo ya
msingi kwanza unapoamka. Yaliyopo
mtandaoni yatabaki kuwapo na hakuna litakalo
kupita.

75
TAARIFA MUHIMU
MWANDISHI WA KITABU HIKI
AMECHAGULIWA KUWANIA TUZO
ZA WAANDISHI BORA WA VYUO
VIKUU.

ANAOMBA UMPIGIE KURA KWA


KULIKE PICHA YAKE ILIYOPO
INSTAGRAM TAYARI UTAKUWA
UMEMPIGIA KURA.
ILI KUFANYA HIVYO BOFYA LINK
IFUATAYO HAPA CHINI:

https://www.instagram.com/p/B-
rlirXATeg/?igshid=pmz7cwp549lx

76
KUHUSU MTUNZI

Edius Katamugora ni msomi katika tasnia


ya uhandisi ujenzi (Civil Engineering). Ni
mwandishi pia katika gazeti la JAMHURI
linalotoka kila Jumanne ya wiki makala zake
hupatikana ukurasa wa 6. Hadi leo hii
ameandika vitabu 8 na hiki kikiwemo.

77
Mwandishi amekuwa mkereketwa wa
mabadiliko ya watu katika jamii hivyo
kupitia maandiko yake maisha ya watu wengi
yamebadilika.

Vitabu vingine alivyoandika ni:


1. Barabara ya mafanikio
2. Namna ya Kuwa Mtaalamu Ukiwa
Bado Unasoma (How to Become An
Expert While at School)

78
3. Kijana wa Maarifa
4. Kijana Jithamini (Ameshirikishwa
pamoja na waandishi wengine)
79
5. YUSUFU NINA NDOTO

6. PUMBA ZA EDIUS (MAMBO


MUHIMU TUNAYOYACHUKULIA
POA MAISHANI)

80
KITABU HICHO HAPO JUU
KINAPATIKANA BURE

7. Natamani Kuanza Kusoma Vitabu

81
82
Mawasiliano:
EDIUS KATAMUGORA
0764145476
0758594893 (WhatsApp).
ekatamugora@gmail.com

Mitandao ya Kijamii ya Mwandishi


Blog: Www.bideism.blogspot.com
Facebook: Edius Katamugora
Facebook Page: Edius Katamugora Page
Twitter: @katamugora

Instagram:@ediuskatamugora

LinkedIn: Edius Katamugora

83
OMBI

UKIMALIZA KUSOMA KITABU


HIKI TAFADHALI KITUME KWA
WATU WENGINE WAJIFUNZE
ZAIDI.

PLEASE SHARE! SHARING IS


CARING

MWISHO

84

You might also like