You are on page 1of 58

TARATIBU ZA KISHERIA

Kitabu hichi kimeandikwa na Joel Nanauka, kikiwa ni kitabu


cha 4 katika
mfululizo wa Practical Wisdom Series
Haki zote zipo chini ya Joel Arthur Nanauka
Haki zote zimehifadhiwa.

Huruhusiwi kunakili, kudurufu au kutumia sehemu ya kitabu


hiki bila idhini ya mwandishi. Kufanya hivyo itakuwa
ni
Ukiukwaji wa haki za mwandishi, na ukiukwaji wa taratibu hii
unaweza kupelekea mashitaka toka kwa waandaaji wa kazi
hii.
Mpangilio wa ndani umefanywa na Andrew Rwela.

2020

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 1


UTANGULIZI

UTANGULIZI
Mungu alipokuleta duniani, alihakikisha kuwa ameweka
uwezo wa kipekee sana ambao mara tu utakapougundua na
kuanza kuufanyia kazi utakuletea matokeo makubwa sana.
Watu wengi, wanazaliwa na hadi wanaondoka duniani
hawajajua uwezo huu wa kipekee uliojificha ndani yao na
matokeo yake wanaishia kuwa watu wa kawaida sana.
 
Moja ya hatari kubwa sana ya kutojua uwezo wako wa
kipekee ni kujikuta unafanya kitu ambacho hukutakiwa
kufanya kabisa. Ni kujikuta unatumia nguvu kubwa kwenye
Maisha yako na huku unapata matokeo kidogo sana.
Ni kujikuta unapata pesa ila haufurahii Maisha.
 
Natamani maarifa haya yangefundishwa katika kila shule
pale ambapo kila mtu anaanza kusoma. Natamani maarifa
haya yangejulikana  kwenye kila ngazi ya familia, kwa kila
mzazi ili amsaidie mtoto wake kujua kitu sahihi cha
kufanya.

Mkononi mwako umeshika kitabu ambacho kitaleta


mapinduzi makubwa kwenye Maisha yako na wale ambao

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 2


UTANGULIZI

wanakuzunguka. Jiandae kuwa wa tofauti baada


ya kumaliza kitabu hiki.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 3


SEHEMU YA KWANZA

Kila Mtu Ni “Genius” Kwenye


Eneo Fulani La Maisha Yake.
Wewe la kwako unalijua?
Albert Einstein aliwahi kusema kuwa “Kila mtu ni Genius.
Lakini kama utamhukumu samaki kwa kushindwa
kupanda juu ya mti, basi samaki ataishi Maisha yake yote
akiamini kwamba hana akili”
(Everyone is a genius but if you judge a fish by its ability to
climb a tree, it will live its whole life believing that it is stupid).

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 4


SEHEMU YA KWANZA

Kila mtu ni “genius” katika eneo  fulani katika maisha yake, 


hakuna mtu ambaye hana uwezo kabisa wa kufika kilele cha
mafanikio  katika maisha yake.

Hii inamaanisha, kama hauwezi kufanya kitu fulani basi


hautaweza kufanya kitu kingine chochote katika Maisha
yako, kuna eneo ambalo ukiligundua na ukaamua kuwekeza
litakufanya uwe wa tofauti sana.
 
Hapa ndio utaelewa kwa nini kuna watu ambao hawakuwa
wanafanya vizuri shuleni lakini kwenye maisha waliamua
kufanya kitu fulani na wakafanikiwa sana. Hii ni kwa sababu
kuna aina za “ugenius” ambazo mfumo wa kawaida wa
shule hauwezi kuzijua na kuzipima.
Tutajifunza Zaidi kuhusu hili hapo mbeleni.
 
Kuna wakati mwingine katika maisha  unakutana na watu
ambao UWEZO wao unaonekana ni mdogo lakini
wamefanikiwa sana katika maisha. Kitu kikubwa na cha
muhimu sio kuwa na uwezo mkubwa zaidi kuliko watu wote,
bali ni kujua eneo ambalo wewe ni Genius na uanze
kuwekeze kwenye eneo hilo kila siku bila
kuchoka.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 5


SEHEMU YA KWANZA

Kila mtu ni “genius” katika eneo  fulani katika maisha yake, 


hakuna mtu ambaye hana uwezo kabisa wa kufika kilele cha
mafanikio  katika maisha yake.

Hii inamaanisha, kama hauwezi kufanya kitu fulani basi


hautaweza kufanya kitu kingine chochote katika Maisha
yako, kuna eneo ambalo ukiligundua na ukaamua kuwekeza
litakufanya uwe wa tofauti sana.
 
Hapa ndio utaelewa kwa nini kuna watu ambao hawakuwa
wanafanya vizuri shuleni lakini kwenye Maisha waliamua
kufanya kitu fulani na wakafanikiwa sana.
Hii ni kwa sababu kuna aina za “ugenius” ambazo mfumo
wa kawaida wa shule hauwezi kuzijua na kuzipima.
Tutajifunza Zaidi kuhusu hili hapo mbeleni.
 
Kuna wakati mwingine katika maisha  unakutana na watu
ambao UWEZO wao unaonekana ni mdogo lakini
wamefanikiwa sana katika maisha.
Kitu kikubwa na cha muhimu sio kuwa na uwezo mkubwa
zaidi kuliko watu wote, bali ni kujua eneo ambalo wewe ni
Genius na uanze kuwekeze kwenye eneo hilo kila siku bila
kuchoka.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 6


SEHEMU YA KWANZA

Moja kati ya fumbo kubwa lililojificha katika safari ya


mafanikio ni kujua UWEZO WA KIPEKEE ULIO NAO (Core
Genius) na kufanya kazi inayoendana na uwezo wako wa
kipekee. (Rudia kusoma tena sentensi hii na hakikisha
umeielewa).
 
Moja ya sababu kubwa ya watu wengi kushindwa
kufanikiwa katika maisha ni kutojua UWEZO WA KIPEKEE
na  kufanya mambo kulingana na UWEZO huo.

Wengi wanajilazimisha kufanya mambo tofauti kabisa na


ambayo walikuwa wanatakiwa kuyafanya sababu hawajui
UWEZO wa kipekee walio nao.

Kuna watu wanatumia nguvu kubwa sana, kwenye kazi,


biashara, masomo n.k  na wanajikuta wanatumia  miaka
mingi sana  kufanya mambo mbalimbali lakini hawapati
matokeo waliyoyatarajia.

Mwisho wa siku wanaanza kuona matokeo ni kidogo sana


ukilinganisha nguvu na muda wanaoutumia katika kufanya
kazi. Moja ya sababu kubwa ya jambo hili ni kutojua UWEZO
wa KIPEKEE WALIO NAO.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 7


SEHEMU YA KWANZA

Core Genius Maana Yake Ninini?


Core Genius inamaanisha ni ile NGUVU YA KIPEKEE ambayo
mtu anayo ndani yake. Ukiijua nguvu hii itakufanya uwe wa
tofauti sana kwenye Maisha.
 
Katika kuelezea tafsiri za nguvu za kipekee alizonazo mtu,
kuna tafsiri tatu kuu zinazoweza kuelezea UWEZO wa
KIPEKEE wa MTU.

1. Moja ni kile kitu kinachokutofautisha kwa urahisi (key


differentiater).

Mfano: Wachezaji wa mpira, hata kama mpo wengi lakini


wewe kuna kitu ambacho kinakutofautisha kabisa na
wengine, Watu wanakiona ni kitu cha tofauti sana
wakikulinganisha na wengine, hata usipokuwepo ni kitu
ambacho watu wanaweza kusema kwamba “wanakimiss’
kwa sababu wewe haupo.

Kwa mchezaji inawezekana ni uwezo wake wa kukimbia


kwa kasi zaidi, kupiga chenga n.k. Hivi watu wanapokumiss
kwenye ofisi, kwenye biashara unayofanya n.k huwa
wanasema wamemiss nini haswa?
CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 8
SEHEMU YA KWANZA

2. Ni Kile kitu kinachokufanya uonekane umekamilika,


unakifanya kwa ukamilifu mkubwa (perfection note)
unakifanya bila dosari yoyote.

Namna nyingine bora ni kuelezea kile kitu ambacho


unapokifanya kinaonekana hakina dosari na kimefanyika
kwa kiwango cha juu sana.
 
Hapa ndio watu wanasema, kama unataka kitu chako
kifanyike kwa kiwango cha juu sana, basi mtafute fulani.

Je, kuna kitu ambacho watu wanatamani wewe ndio ufanye


na sio mtu mwingine?

3. Namna ya tatu ya kuelezea uwezo wako wa kipekee ni


kuangalia jumla ya ujuzi wako, maarifa yako, uzoefu wako,
na uwezo wako wa ndani kipekee. (the combination of your
skills, knowledge, experience, and traits)

Hebu jiulize ukiangalia jumla ya vitu vilivyoelezwa hapo juu,


wewe unajiona unaweza kufanya jambo gani kwa namna ya
tofauti ambalo ni muunganiko wa yote kwa pamoja.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 9


SEHEMU YA KWANZA

Mambo Matatu (03) Ya Kuongoza Tafakari Yako


1. Kitu unachokipenda (Passion)
2. Kitu unachokiweza, una ujuzi au una uzoefu nacho.
3. Kitu ambacho watu wako tayari kukulipa
(kitu gani ambacho watu wako tayari kukulipa).

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 10


SEHEMU YA KWANZA

Kuishi kwenye Core Genius yako, maana yake nini?


Ni pale ambapo, unafanya UNACHOKIPENDA na ambacho
una UWEZO nacho wa kukifanya, na wakati huo huo watu
wako tayari KUKULIPA kwa unachokifanya
 
Nia yako katika maisha inatakiwa kuunganisha maeneo
haya matatu kwa pamoja. Kuna wengi sana ambao hadi leo
wamefanikiwa kuunganisha mawili, lakini ili ufanikiwe ni
lazima uunganishe yote kwa pamoja, UNACHOPENDA,
UNACHOWEZA, NA UNALIPWA KWA HICHO.
 
Sasa tuyaangalie makundi haya matatu na ujiulize na wewe
uko kundi gani, ili ujue namna ya kuhama kutoka kundi moja
kwenda lingine.
 
Kundi la Kwanza: Wanafanya wanachokipenda, wana
ujuzi nacho ila hakiwaingizii pesa kwa sasa.

Kundi hili lina watu ambao tayari wanajua passion yao na


wameshafanya maamuzi ya kuishi kwenye passion zao
tayari. Mara nyingi watu walio katika kundi hili huwa ni
wavumilivu sana na wanaamini kuna siku mambo
yatabadilika na wataanza kuona matunda ya bidii yao.
CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 11
SEHEMU YA KWANZA

Hawa ndio watu wanaoongoza kwa kutoeleweka na watu


wao wa karibu na jamii kwa ujumla.

Watu  walio katika kundi hili, huwa wanaweza kuacha kazi


nzuri au wakaacha kufanya kitu kinachoendana na taaluma
yao na wakaenda kufanya kitu tofauti kabisa.Mara nyingi
watu wengi huwaona wamechanganyikiwa kwa sababu
huwa wanaongoza kwa kuona vitu ambavyo wengine
hawavioni.
 
Kama utajikuta kwenye kundi hili na ukaona kabisa
unachofanya unakipenda sana, na una ujuzi nao wa kutosha
bila shaka kabisa ila hakikulipi. Kuna mambo muhimu
unatakiwa uyawekee mkazo. Cha kwanza ni kuhakikisha
unaongeza ujuzi wako wa kibiashara (Business Skills) hasa
katika eneo la masoko na mauzo (Marketing and Sales).

Watu wengi sana walioko kwenye kundi hili, huwa


wanakuwa na uwezo mzuri, mawazo mazuri na mipango
mizuri, wanachopungukiwa na uwezo wao wa kibiashara 
wa kubadilisha walichonacho kukifanya kuwa pesa. Kama
umejiona uko kwenye kundi hili, hakikisha unatafuta kitabu
changu cha ongeza kipato chako kinachozungumzia
CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 12
SEHEMU YA KWANZA

maarifa juu ya fedha, biashara na uwekezaji kitakusaidia


sana.

Kundi la Pili: Wanachofanya kinawalipa vizuri, wana


ujuzi nacho ila hawakipendi.
 
Kundi la pili ni la wale ambao wanachokifanya kinawalipa na
wanaweza kuendesha maisha yao bila tatizo lolote. Pengine
wamefika sehemu ambayo kipato cha kulipia gharama za
msingi za maisha sio tatizo kabisa. Lakini pia, kitu
walichoamua kufanya wana ujuzi nacho wa kiwango cha
juu.
 
Kundi hili linajumuisha watu ambao walienda shule/vyuo na
kusomea baadhi ya taaluma na wakaanza kuzifanyia kazi.
Wengi wao walitumia miaka kadhaa kupata hizo taaluma na
wana vyeti vinavyoheshimika katika jamii.
 
Kumbuka kuna watu ambao walienda kusoma kozi shuleni
au vyuoni ambazo ukweli hazikuwa machaguo yako.
Wengine walilazimishwa na wazazi wao, wengine ilikuwa ni
ushawishi wa rafiki zao na wengine ndio kozi pekee ambazo
waliweza kusoma kwa sababu maksi zao ndio ziliwaruhusu.
CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 13
SEHEMU YA KWANZA

Watu wa namna hii huwa wanakuwa na furaha ya muda


mfupi pale wanapoanza kazi mwanzoni lakini baada ya
hapo furaha inapotea kwa sababu, furaha ya kweli
inashikiliwa na wewe kufanya kile ambacho unakipenda
kutoka moyoni.

Hivyo hata kama utalipwa vizuri na ni kitu ambacho una


uwezo nacho, ila kama sio kitu ambacho unakipenda kutoka
moyoni basi hauwezi kuwa na furaha ya kudumu.
 
Kama wewe ukijikuta uko kwenye kundi hili ni lazima ukae
chini na utengeneze mpango wa kuhama hapo ulipo ili
uamie kule ambako ungependa kuwepo.
 
Kuna wengine wamejikuta wanataka kutoka kwenye
kuajiriwa ili waweze kwenda kwenye kujiajiri, kama wewe ni
mmoja wao hakikisha unatafuta kitabu changu cha
‘’Kuajiriwa hadi kujiajiri’’ kinachoelezea namna ya kuhama
vizuri kutoka upande mmoja kwenda mwingine kwa
mafanikio makubwa.
 
Ili kuvuka kutoka katika hali hii, ni lazima utengeneze
‘’Profesional Transition Plan ‘(PTP) inayoelezea kwa kutaja
CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 14
SEHEMU YA KWANZA

muda na nyakati mbalimbali ambazo utaamua kujenga


uwezo kwa ajili ya kitu ambacho unadhamiria kukifanya.

Kundi la tatu: Wanapenda kufanya wanachofanya, inawalipa,


ila ujuzi ni mdogo na kama wakiongeza ujuzi basi watalipwa
Zaidi.
 
Hili ni kundi ambalo wameshajua kitu wanachokipenda
kwenye Maisha yao na tayari wameanza kukifanya na
kinawaingizia pesa kwa sasa, ingawa wanajua kabisa kuwa
kama wakiongeza ujuzi zaidi watapata pesa nyingi kuliko
ambazo wanapata kwa sasa hivi.
 
Watu wa namna hii wengi wanadumaa kwa sababu huwa
wanaridhika mapema sana na kidogo walichonacho. Hata
hivyo wakijikagua wanaona kabisa kuwa wana fursa kubwa
ya kuongeza ujuzi wao na kupata matokeo makubwa zaidi.
 
Hebu jiulize katika kile unachokifanya je, Kinachokuzuia
kufanikiwa zaidi ni kukosa ujuzi au kuna kitu kingine? Kama
ni kukosa ujuzi, basi angalia na jikague ni ujuzi wa namna
gani ambao unaukosa na uanze kuufanyia kazi mara moja ili
kuhakikisha kuwa unasonga mbele.
CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 15
SEHEMU YA KWANZA

Hakikisha unajua aina ya ujuzi unaouhitaji na tengeneza


mpango mahsusi wa kujenga ujuzi huo aidha kwa njia ya
kuhudhuria kwenye semina, kusoma vitabu, kupata mentor
wa kukusaidia, kusoma kozi zinazotolewa
mtandaoni n.k.
 
Kumbuka: Kwenye maeneo mbalimbali ya maisha yako,
unaweza kujikuta uko kwenye makundi tofauti tofauti. Lakini
pia haimaanishi ukiwa kwenye kundi moja basi utakaa hapo
kwa kudumu, kuna vitu vikibadilika vinaweza kukutoa kundi
moja na kukupeleka kwenye kundi lingine.
 
Tafakari:
1. Je, kwa sasa katika makundi haya, wewe uko kundi gani?

2. Ni vitu gani ambavyo unatakiwa kuanza kufanya ili


kuhamia katikati ambako utaanza kupata matokeo
makubwa na utakuwa umetengeneza furaha zaidi?
 
3. Kabla haujandelea sehemu inayofuata, tengeneza
mpango wa namna ambavyo utatoka eneo ulilopo sasa
kwenda eneo unalolitamani.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 16


SEHEMU YA PILI

Kuna Aina Ngapi za “Core Genius”


na Nitatumia Vigezo Gani Kujua
ya Kwangu?

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 17


SEHEMU YA PILI

Kwa muda wa miaka mingi sana wataalam wa maswala ya


UBONGO waliamini kuna aina tatu tu za kujifunza :
1. Kuona
2. Kusikia
3. Vitendo
 
Na kwa utafiti ambao ulifanywa hadi wakati huo ulionyesha
kuwa, aina hizi tatu  ndizo zinajulisha uwezo wa mtu wa
kipekee..
 
Hata hivyo, mapinduzi makubwa sana yalitokea pale
ambapo Dr. Howard  Gardner, mwalimu katika chuo kikuu
cha Harvard, nchini marekani alipochapisha kitabu chake
(1983) cha ‘’  Frames Of Minds’’ (Theory of Multiple
Intelligencies ).

Katika utafiti wake aligundua kuwa kuna aina nane za


uwezo wa kipekee ambazo wanadamu wanazo na kuwa
mfumo wa shule umejikita katika kufundisha aina mbili tu.
Hii imesababisha watu wengi sana wafeli kwenye maisha
hasa baada ya kufeli shule kwa sababu waliamini kuwa
hawawezi kufanikiwa tena.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 18


SEHEMU YA PILI

Hii ndio maana, watu waliofanikiwa sana katika biashara


kama vile tajiri mkubwa Gary Vee alipoulizwa kwa nini alifeli
shule, akajibu ‘’I didn’t fail school, but school failed me’’
akimaanisha kuwa hakushindwa masomo ya shuleni bali
mfumo wa shule ulishindwa kutambua uwezo wake.
 
Kwa maoni yangu, hiki ambacho utajifunza katika sehemu
hii ya kitabu kinatakiwa kiwe sehemu ya mtaala wa shule
kila mtu anapoanza. Inatakiwa kufundishwa kwa walimu ili
wawe washauri wazuri kwa wanafunzi hasa katika
kuchagua masomo wanayotaka kusomea.

Inatakiwa wafundishwe wazazi mbalimbali ili wajua namna


ya kuwashauri watoto wao masomo wanayotakiwa
kuyasoma. Hivyo basi kila mtu anaweza kufanikiwa sana
katika maisha yake, kama atagundua uwezo wake wa
kipekee na kuanza kuishi sawasawa na uwezo huo.

Katika kutathmini uwezo wa kipekee wa  mtu, kuna mambo


matatu muhimu ambayo unatakiwa kuyazingatia:

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 19


SEHEMU YA PILI

1. Watu wako tofauti kulingana na walivyo, hakuna  mtu


yeyote anayefanana na mwingine Duniani. Hivyo kila mmoja
ana namna yake ya kuonyesha uwezo wake. Usilazimishe
mguu uishi na ufanye kama mkono.
 
2. Hatufanani namna ya kuchakata taarifa, kila mtu
anachakata taarifa kulingana na uwezo wako wa kipekee
alio nao.
 
3. Elimu yoyote unayoipata inamaana sana au manufaa
sana kama utaweza kuitumia kulingana na uwezo wako wa
kipekee.

KUSUDI KUBWA LA
KUJIFUNZA HIZI AINA NANE NI ILI UWEZE KUWA NA
UWEZO WA KIPEKEE NA KUFANIKIWA,
PIA KUGUNDUA VIPAJI VYA WATU WANAOKUZUNGUKA.
 
Katika kukuza kipaji cha mtu au mtoto unaangalia vitu
anavyovipenda zaidi kisha unaanza kuvijengea uwezo.
Kwenye uwezo wa kipekee,  kuna ile yenye nguvu za ziada.
Ni kama vile ambavyo mtu mwenye mikono miwili lakini
mmoja unakuwa na  nguvu zaidi.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 20


SEHEMU YA PILI

Inawezekana, mtu akawa anaweza kufanya mambo mengi


sana, ila kuna jambo moja ambalo ndio ameumbiwa
kulifanya kwa ufanisi zaidi, ni lazima ulijue na uanze kuliishi.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 21


SEHEMU YA TATU

ZIJUE AINA NANE ZA


‘’CORE GENIUS ‘

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 22


SEHEMU YA TATU

AINA YA KWANZA: Verbal-Linguistic Intelligence ( Word


Smart)

Sifa yao ya kwanza: Ni watu wazuri katika kutumia maneno.

Wanapenda kuandika, kusoma, wanapenda kufundisha


wengine, wanapenda kuelezea mambo kwa kina,
wanapenda kusoma vitabu na makala mbalimbali,
wanapenda kuandika na wanagundua sana makosa ya
maneno yaliyoandikwa.
 
Sifa yao ya pili: Wanapenda kusimulia mambo mbalimbali

Wanapenda stori, wanapenda kuelezea vitu, kila


wanachokiona, kusoma, kusikia na wanapenda kusimulia.
Akihudhuria tukio anapenda kuelezea kila kitu au kama
wewe ulihudhuria wanapenda uwasimulie kila kitu.
Wanapenda maelezo ya kina.
 
Wanapenda kutumia misemo mbalimbali kama methali,
nahau, hadithi au nukuu za watu wengine. Kama ni
mwanafunzi anapenda kuandika notes sana
anapofundishwa. Wanapenda sana lugha za kigeni na hata

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 23


SEHEMU YA TATU

kama anajua maneno machache atajitahidi kuongeaongea.


Wanapenda kukwambia vitabu walivyosoma, magazeti au
website na wanapenda sana kuongea.

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA KWA UFANISI

Mhariri (Editor) Mwandishi (Author) Mwalimu

Mhubiri/Imamu Mwanasiasa Mtangazaji

Mshehereshaji Mwigizaji Mtu


(Mc) wa masoko na
mauzo (Marketing
and Sales)

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 24


SEHEMU YA TATU

Jaribu kufikiria kama una sifa hizo, na je zinaingiliana vipi na


unachokifanya?

Unaweza kuunganisha unachokifanya na huu uwezo wa


kipekee.
 
AINA YA PILI: Logical - Mathematical Intelligence (Number
Smart)

Hawa ni watu wanaopenda sana kujua sababu iliyoko


nyuma ya kila kinachotokea. Mara nyingi wanaongozwa na
AKILI zaidi kuliko HISIA. Kama hawaelewi sababu ya
kufanya kitu fulani basi huwa hawako tayari kabisa
kukifanya.
 
Mara nyingi huwa hawawezi kushawishiwa kwa maneno,
wanahitaji kuona namba zaidi au tafiti mbalimbali
zinasemaje kuhusiana na jambo hilo. Ni watu wanapoenda
“data” zaidi.
 
Utawajuaje watu hawa?

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 25


SEHEMU YA TATU

Wanapenda kufanya hesabu za vitu mbalimbali kwa


kichwa na huwa wanapatia. Huwa ni wepesi wa kujua
hesabu mbalimbali za haraka.
 
Wana mipango mingi sana lakini huwa hawaifanyii kazi
na ni wazuri kwa namba wanajua kuelezea mipango ya
kipesa lakini siyo utekelezaji. Wanapoangalia wazo, huwa
wanajikita katika namba tu (za bidhaa, idadi ya fedha
watakazopata, faida, n.k). Huwa hawaangalii vitu vingine
kabisa.
   
Wanapenda kuweka vitu katika makundi (Wanapenda
kusema aina fulani, kundi fulani, watu wa namna hii n.k).
Huwa wanaamini watu na vitu duniani vimegawanyika
katika makundi mbalimbali yanayofanana.
  
Wanapenda zaidi kutumia namba na data
zinazoambatana na maelezo ya kisayansi.
   
Wengi  wao huwa hawafanyi vitu  hadi watakaporidhika
kuwa kimekuwa kamili kabisa (perfectionist).
  

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 26


SEHEMU YA TATU

Huwa ni watu ambao wanaweza kutumia muda mwingi


wakiwa peke yao na kujiuliza maswali mengi sana.

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA KWA UFANISI

Mwanasayansi Mwanasheria Daktari

Mhasibu Mwanasiasa Mwandishi

Mtafiti IT/mtu Mtaalamu


(Researcher) wa kompyuta wa sera (Policy
Expert)

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 27


SEHEMU YA TATU

AINA YA TATU: Spatial Intelligence - Picture Smart

Hawa ni watu ambao, sehemu yao ya ubongo inayohusiana


na picha na matukio ina nguvu zaidi kuliko eneo lingine
lolote la ubongo wao.
 
Utawajuaje watu hawa?
      
Wanakumbuka  matukio mbalimbali kwa kuona zaidi
kuliko
kusoma
      
Wanakumbuka rangi mbalimbali za nguo za watu,
majengo, magari, n.k
       
Wanaweza kueleze vizuri hadi anayesikiliza akajenga
picha ya wanachoongea
  
Wanapenda kuchora picha mbalimbali hata kama sio
wachoraji wazuri sana
        
Wanapenda kumechisha rangi mfano, mavazi, nyumbani,
simu, n.k
    
CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 28
SEHEMU YA TATU

Wanapenda sana kuona picha, na wanapenda filamu


(movies).
      
Mfano wakienda kwenye harusi, wanaelezea kwa picha
bi harusi alipendeza sana, wataeleza kuhusiana na shela,
viatu, msimamizi wake n.k kisha wataelezea kuhusu
ukumbi ulivyopambwa na wageni walivyotokelezea vizuri
n.k
    
Akianza kukuelekeza mahali anataja kila kitu  ambacho
kitakusaidia kufika unapokwenda. Atataja majengo na
rangi zake, mitindo ya nyumba, aina za maduka n.k
    
Wana kumbukumbu sana na maeneo mbalimbali na
hawapotei kirahisi hata kama walifika mara moja.
       
Huwa wanakumbuka watu hata kama walikutana na
wewe mara moja kwa muda mfupi.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 29


SEHEMU YA TATU

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA KWA UFANISI

Mbunifu Muuzaji Muuzaji


wa mavazi wa nguo wa bidhaa
(Fashion za
Designer) urembo

Mpiga Msanifu Mpambaji


picha majengo (Decorator )
(Professional (Architect)
Photographer)

Mrembaji Mpaka Mwongoza


wa ndani rangi (majengo, Filamu/Muziki
(Interior magari n.k) (Film or Movie
designer) Director)

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 30


SEHEMU YA TATU

AINA YA NNE: Bodily - Kinesthetic Intelligence (Body Smart)

Hawa huwa wapenda zaidi kutumia miili yao na kufurahia


pale nguvu zao zinapohusika katika kufanya mambo
mbalimbali:
 
Utawajuaje watu hawa?
      
Wanapenda kutembeatembea, hawapendi kukaa sehemu
moja. Hata wakiwa ofisini mara nyingi huwa hawatulii.
      
Wanajifunza kirahisi kwa kufanya kwa vitendo kuliko
kusikiliza au kusoma.
      
Wanapenda kuelezea kwa vitendo, wanapenda
kuonyesha ishara au kuonyesha kwa kitendo kitu
kilivyotokea au mtu alivyofanya.
   
Wanapenda kugusa, akiongea na wewe lazima
akuguseguse kila mara. Ukimpa simu aangalie kitu
kimoja lazima aingie kwenye vitu vingine.
      
Wanapenda kuchunguza vitu vinafanyaje kazi,

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 31


SEHEMU YA TATU

hawaridhiki na kuangalia juu juu. Wanapenda kufungua


ndani ya vitu waone vinafanyaje kazi. Kitu kikiharibika huwa
kabla hawajatafuta mtaalamu anataka wajaribu kwanza.
   
Wanaongea kwa kushikashika vitu vinavyowazunguka.
      
Wanapenda michezo, mazoezi, na kama ni watoto basi
wanapenda sana kukimbizana.
       
Wana nguvu sana za kufanya kazi na wako busy sana.
Mara nyingi hawachoki kwa haraka. Wakati kila mtu
amechoka wenyewe huwa bado wana nguvu.

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA KWA UFANISI

Mwanamichezo Mchezaji Fundi


muziki (Dancers) magari

Mwigizaji Mtengeza Zimamoto


mzuri (Actors) vitu vya mikono: (Fire Fighter)
Mfumaji, Mchongaji
(Handcraft)

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 32


SEHEMU YA TATU

Mfanyakazi Kocha Fundi


mbuga za wa timu/daktari wa simu
wanyama mazoezi

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 33


SEHEMU YA TATU

AINA YA TANO: Musical intelligence (music smart)

Hisia zao huguswa kirahisi sana na muziki wa aina


mbalimbali na ni wepesi sana kujua uzuri au ubaya wa
muziki.
 
Utawajuaje watu hawa?
    
Wanasifia sana muziki, hasa tungo mbalimbali.
   
Wana uwezo wa kutunga mashairi ya muziki hata kama
hawana mpango wa kurekodi na kuimba.
  
Wana uwezo wa kutumia vifaa vya mziki.
  
Wanajifunza kwa kusikiliza zaidi kuliko kuongea.
   
Wanajitungia nyimbo zao wenyewe.
   
Wanakumbuka sana mashairi ya nyimbo mbalimbali,
wanaweza kuziimba vizuri. Wanaweza kukariri nyimbo,
au maneno ya nyimbo.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 34


SEHEMU YA TATU

Wanagundua sauti za watu mbalimbali kwa haraka hata


kabla hawajamuona.
       
Ukiongea nae kwa simu atagundua mabadiliko ya sauti.
Kama hauko sawa, una mafua, unaumwa, hauna furaha,
n.k.
    
Wanapenda kuimba imba kila wakati: Wakiwa wanaoga,
wanatembea, n.k hata kama sauti zao sio nzuri sana.
   
Wanapenda kupiga mluzi.
   
Wengine katika kundi hili huwa wana kipaji cha kuimba
kwa umahiri.
       
Wanaweza kirahisi kupiga vyombo vya mziki.
   
Wanajua haraka kuwajua wanaoimba vibaya hata kama
wao sio walimu wa muziki.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 35


SEHEMU YA TATU

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA KWA UFANISI

Mwimbaji / Muandaaji Mtunzi


Mwanamuziki wa muziki wa wimbo
(Music Producers) (Song Compersors)

Mwalimu Promota Muandaaji


wa muziki wa wanamuziki wa matamasha
ya muziki

Muuzaji wa Meneja Mtaalamu


vyombo vya wa wa sauti za vyombo
muziki mwanamuziki vya muziki
(Sound Engineer)

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 36


SEHEMU YA TATU

AINA YA SITA: Naturalist intelligence (Nature Smart)

Kwa asili hawa ni watu ambao wanajali sana mazingira na


huwa wanapenda wanyama na mimea. Huwa kila
wanachokiangalia katika mazingira yao wanakiona ni cha
thamani sana na wanapenda kutunza vitu na kuvikuza pia.
 
Utawajuaje watu  hawa?
      Wakiwa kwenye nyumba/ofisi wanapenda kila kitu
kikae
katika mpangilio wa nyumba, kusiwe na mwingiliano.

Hata kwa vitu vidogovidogo kama viatu, vikombe n.k  huwa


wanakwazika sana visipowekwa mahali panapostahili.
      
Wakiona uchafu kidogo tu huwa inawakera sana, na kila
saa wanataka kusafisha kila mahali.
      
Wao binafsi ni wasafi sana.
       
Wanapenda sana wanyama wakufuga.
      
Wanapenda vitu vya asili kama chakula, nguo, dawa n.k.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 37


SEHEMU YA TATU

Wanapenda sana bustani, maua, miti n.k


Wanapenda kutembelea vivutio vizuri, wanyama, miti, na
milima.
Wanagundua mabadiliko ya hali ya hewa kwa haraka
sana.

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA KWA UFANISI

Mkulima Mtunza Mwalimu


mzuri bustani mzuri wa kufundisha
Wanyama
mf: Mbwa

Mwanasayansi Daktari Kampuni


wa Wanyama/ wa mifugo ya usafi wa
mimea mazingira

Kampuni Muuza Muuza


ya kupendezesha vifaa vya maua
maeneo usafi/Mapamb mbalimbali
(Land Scape and o ya ndani (Flowerist)
Gardening)

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 38


SEHEMU YA TATU

AINA YA SABA:  Intraperson intelligence  (self-smart)

Aina hii ya ugenius imejikita katika mtu kujitambua yeye


mwenyewe na kuwa mtu wa kuangalia ndani yake zaidi
kuliko nje yake.

Watu wa kundi hili wako makini sana na hisia zao na mara


nyingi wako kivyaovyao na wako bize na mambo yao.

Mara nyingi sana sio waongeaji sana na wanapenda


kujifunza kivyaovyao hata kama wangesaidiwa kirahisi na
mtu mwingine.
 
Watu hawa hawapendi kuwa kwenye vikundi na hata
kwenye mazungumzo huwa hawapendi kuchangia.
Wanaamini katika kufanya mambo wenyewewenyewe.
 
Utawajuaje watu hawa ?
·       
Mara nyingi hupenda kufanya kazi peke yao na watu
wengi huwatafsiri kama ni wachoyo.
      
Wanafanya mambo kwa ubora sana, pale wanapokuwa

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 39


SEHEMU YA TATU

wanafanya wenyewe.
Wanapenda sana falsafa mbalimbali. Wakiongea
utawasikia “kulingana na falsafa fulani”
      
Wanapenda sana kuzungumzia vitu vya kufikirika sana
/nadharia ideas n.k.
    
Wanajitambua sana wao wenyewe (udhaifu wao, nguvu
zao n.k ), self awareness yao ni kubwa sana.
       
Wanapenda sana mambo ya saikolojia. 
Wanapenda mambo yao  yakamilike ndio wafanye kitu
(perfectionist).
       
Ukitaka kufanya nao jambo wanauliza maswali mengi 
sana wakati mwingine unaweza kuwaona wasumbufu.
Huwa hawafanyi kitu hadi waone kila kitu kiko
sawasawa, siyo watu wa kujihatarisha (They don’t take
risk).
       
Wanapenda kujiajiri, hawapendi kuajiriwa hawapendi
kuamrishwa, hawapendi kutumwa, hawapendi
kupelekeshwa na maagizo.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 40


SEHEMU YA TATU

Wanapenda kuweka rekodi ya mambo. Wanaandika


tarehe, matukio na kumbukumbu mbalimbali.
      
Wanapenda kukaa peke yao na kutafakari mambo yao
wenyewe, hawapendi kujichanganya sana na watu.
·       
Wanapenda kujifunza kuhusu tabia zao.
   
Wanapenda sana kufikiri na kuja na mawazo mazuri ya
biashara.

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA KWA UFANISI

Mwanasaikolojia Mwanatheolojia/ Mtoa ushauri


Mhubiri mzuri/
Consultants

Mjasiriamali/ Mwanafalsafa Mwandishi


Wanakuwa mzuri wa hadithi
na
mawazo mazuri
ya biashara

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 41


SEHEMU YA TATU

Afisa Mpelelezi Mchambuzi wa


usalama mambo
(Analyst)

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 42


SEHEMU YA TATU

AINA YA NANE: Interperson intelligence  ( People smart)

Katika kundi hili watu wanaoangukia hapa huwa wanapenda


kujichanganya sana na watu. Huwa wana uwezo mkubwa
wa kuhamasisha watu kwenye mambo mbalimbali na sio
watu ambao wanahukumu watu sana. Huwa wanatoa fursa
mpya kwa kila anayekosea. Ni watu ambao ni wepesi wa
kusamehe wanaowakosea pia.
 
Utawajuaje watu hawa?
       
Ni watu ambao wanajali sana hisia za wengine, ukifiwa,
ukiumia n.k. Wanaumia sana na hisia za watu wengine
wanapopata matatizo na kupitia maumivu ya aina
mbalimbali.
       
Wanapenda kuwa sehemu ya matukio mbalimbali kama
vile  harusi, na matamasha. Wako kila mahali na hawaoni
tatizo kutumia muda mwingi kwenye  matukio
mbalimbali.
       
Ni wahudhuriaji wazuri wa semina na kila tukio huwa
hawataki kubaki nyuma.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 43


SEHEMU YA TATU

Wanapenda kufundisha watu. Wakipata maarifa kidogo


huwa wanatafuta sababu ya kuwafundisha wengine.
      
Wanapenda sana marafiki, japo siyo urafiki wa ndani
sana, mara nyingi urafiki wao huwa ni wa juu juu tu.
Huwa wanatengeneza marafiki haraka hata kwa
kulazimisha.
       
Wako kwenye makundi mengi ya whatsapp,
wanachangia kila kundi, wako active kwenye kila mada
na kwenye kila kundi wanajulikana kwa michango yao.
    
Wanahusika sana kwenye mambo ya kijamii, wanajitolea
sana hata kama hawana vingi na ni wagumu kukataa
wanapoombwa kufanya kitu na kwenye makundi mengi
wakiwepo huwa wanapata vyeo kwa haraka.
       
Hata biahara zao wanachanganya biashara na mahitaji
binafsi, na biashara ikafa. (wanashauriwa kuweka
mfumo wa kifedha).

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 44


SEHEMU YA TATU

KAZI WANAZOWEZA KUFANYA KWA UFANISI

Mwanadiplomasia Kiongozi/Meneja Afisa


Ustawi wa jamii

Mtu
Mhudumu
wa mauzo na Mshauri
kwa wateja
masoko

Kocha Kufundisha
Dalali
watoto

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 45


SEHEMU YA TATU

Kumbuka: Katika hali ya kawaida mtu mmoja anaweza


kuonyesha uwezo katika eneo zaidi ya moja ila lazima kuna
eneo mojawapo kati ya haya nane ndilo ambalo litakuwa na
nguvu zaidi na lazima ulitambue

Tafakari

1.   Je, katika maeneo haya manane, ni maeneo gani matatu


ambayo unaona yanaendana sana na wewe?
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………….

2.   Katika maeneo uliyoyataja, Je ni eneo lipi katika hayo


matatu ambayo unaona ndio hasa linaendana na wewe kwa
kiwango cha juu zaidi?
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………….
 
3.   Je, unachofanya sasa hivi kinaendana na sifa za eneo
ambalo linafanana na wewe zaidi?
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………….

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 46


SEHEMU YA TATU

4.   Kama jibu lako kwenye namba 3 hapo juu ni hapana,


unapanga kufanya nini ili uanze kuoanisha uwezo wako na
kile unachokifanya?
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………….
 
5.   Je, kuna mtu unayemfahamu wa karibu yako (mwenzi,
mtoto, Rafiki n.k) ambaye umegundua yuko kundi ojawapo
katika uliyojifunza? Umegundua yuko kundi gani? Unaweza
kumshirikisha ulichojifunza?
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………….

Katika aina hizi nane za Ugenius ambazo mwanadamu


anazo, ni munimu kujua mfumo wetu wa shule huwa
unapima aina mbili tu kuu:

Yaani ile ya kwanza na ile ya pili (Verbal-Linguistic na


Logical-mathematic). Hii ni kwa sababu mfumo wa shule
umeandaliwa kupima ubongo wa kushoto zaidi ambako
ndio aina hizi za ugenius ziko.

Aina 6 za ugenius zilizobakia, ziko upande wa kulia wa

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 47


SEHEMU YA TATU

ubongo na mfumo wa shule haujatengenezwa kuzipima.

Hii maana yake ni nini?

Kama wewe ni genius wa upande wa kulia basi mfumo wa


kawaida wa shule hautakuwa rafiki kwako na utafeli.

Na kwa sababu hiyo utatajwa kama usiye na akili, kumbe


kilichofanyika ni samaki anahukumiwa kwa uwezo wa
kupanda juu ya mti.

Hii ndio maana wale wenye ugenius wa aina 6 zilizobakia,


kama vile wanamichezo, wanamuziki, wachoraji n.k
tulipokuwa nao shuleni walionekana hawana akili, ingawa
wengine walipoamua kuendeleza ugenius wao walifanikiwa
kimaisha.

Mfumo wa shule umetengezwa kuwa rafiki kwa watu


ambao wanajua na wanapenda hesabu na uwezo wa
kuandika na kuzungumza zaidi. Ila wengine wote waliobaki
unawaita hawana akili.

Hii ndio maana mtu akifeli shule anaweza kufaulu kwenye

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 48


SEHEMU YA TATU

maisha kama tu akigundua ugenius wake. Kama wewe ni


mzazi ni muhimu sana kujifunza mapema Genius nature ya
mtoto wako ili umsaidie kusoma taaluma sahihi.
Usilazimishe afanye kitu ambacho sio genius nature yake
kwani atapoteza muda, atakulaumu baadaye na hatafurahia
maisha.

Hii ndio maana lazima kuwe na “alternative paths to


education” Mfumo wa elimu uruhusu kila mwenye ugenius
wake apate nafasi ya kuonwa.

Hata hivyo kwa sababu bado marekebisho haya


hayajafanyika. Ni muhimu kutumia elimu uliyoipata kwenye
kitabu hiki kujikagua na kuwasaidia wengine pia.

Hakikisha unajibu maswali kwa ufasaha kama yalivyoulizwa


hapo mwishoni mwa kitabu hiki.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 49


HITIMISHO

Utakapogundua uwezo wako wa kipekee na kuuoanisha na


kitu unachofanya, hakunashaka utakuwa umeanza safari ya
mafanikio yasiyopingika kabisa.
 
Mara baada ya kumaliza kusoma, jitahidi kuweka katika
matendo yale ambayo umejifunza ili yakuletee matokeo kwa
haraka zaidi. Kumbuka maarifa uliyoyapata kupitia kitabu
hiki yanaweza kuwasaidia watu wanaokuzunguka, watoto
wako au wafanyakazi ambao mko ofisi moja ili kujua kila
mtu anapaswa kufanya nini.
 
Nakushauri ili ufaidike zaidi na ulichojifunza, tafuta mtu
ambaye utajadiliana naye kwa mapana ili ikusaidie kujijua
zaidi.
 
Nakutakia mafanikio makubwa zaidi.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 50


HITIMISHO

TEMBELEA MITANDANO YA KIJAMII YA JOEL NANAUKA

YouTube: Joel Nanaka


(Utapata VIDEO nyingi za kukufundisha mambo mbalimbali)

Instagram: JoelNanauka_
(Utapata mafunzo kila siku yatakayokusaidia)

Facebook: Joel Nanauka Page


(Utapata mafunzo kila siku na pia shuhuda mbalimbali.)

Kupata vitabu vingine vilivyoandikwa na Joel Nanauka


wasiliana na namba zifuatazo:
       
0745 252 670

0756 094 875

0683 052 686

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 51


HITIMISHO

Naamini kitabu hiki kitakuwa kimekusaidia sana katika


kujifunza mambo mbalimbali ambayo yataharakisha safari
yako ya mafanikio.Ninakusihi ufanyie kazi yale uliyojifunza
kwa bidii ili upate matokeo makubwa zaidi.
 
Kumbuka kuwa kuna uwezo mkubwa sana ndani yako na
kama ukiamua kuufanyia kazi basi hakuna kitu ambacho
kitakuzuia.
 
Nakutakia mafanikio katika ndoto yako na usisite
kuwasiliana nasi kwa uhitaji wowote wa ushauri binafsi,
mafunzo kwa wafanyakazi ama ushauri wa kibiashara.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 52


HITIMISHO

VITABU VINGINE VILIVYOANDIKA NA JOEL NANAUKA


      
TIMIZA MALENGO YAKO
(Mbinu 60 walizotumia watu maarufu kufanikiwa)
    
ONGEZA KIPATO CHAKO
(Maarifa juu ya Fedha, Biashara na Uwekezaji)
  
ISHINDE TABIA YA KUGHAIRISHA MAMBO
   
NGUVU YA MWANAMKE
    
ISHI NDOTO YAKO
(Siku 30 za kuishi maisha unayoyatamani)

MONEY FORMULA, Elimu ya Fedha Isiyofundishwa Shuleni

UFANISI KAZINI
  
JINSI YA KUIFANIKISHA NDOTO YAKO KATIKATI YA
CHANGAMOTO
  
TABIA 12 ZINAZOLETA MAFANIKIO
  
CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 53
 
HITIMISHO

UZALENDO NA UJENZI WA NCHI

MUONGOZO WA MAFANIKIO
 

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 54


KUHUSU MWANDISHI

Joel Arthur Nanauka,


Ni mhitimu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam kwenye
shahada ya Biashara na Uongozi (Bcom-Hons) na
stashahada ya juu katika Diplomasia ya Uchumi (Economic
Diplomasi - 5.0 GPA) ambako alitunukiwa kama
mwanafunzi bora katika wahitimu.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 55


KUHUSU MWANDISHI

Aliwahi pia kuwa mwanafunzi bora wa kitaifa mwaka 2002


baada ya kumaliza masomo yake ya kidato cha nne Kibaha
sekondari.

Joel ametajwa na taasisi ya Avance Media yenye makao


yake makuu nchini Ghana kuwa ndiye kijana mwenye
ushawishi zaidi katika eneo la mafunzo ya kujiendeleza
(Personal Development and Academia) kwa mwaka
2019/2020.

Taasisi ya BMCE bank yenye makao yake makuu


Casablanca nchini Morocco na Taasisi ya Graca Machel
Trust (GMT) iliyoko Africa Kusini inamtambua Joel Nanauka
kama mkufunzi mwelekezi (Mentor) katika program zake.

Joel amewahi kuteuliwa na Baraza la Uwezeshaji la Taifa


(NEEC) lililoko chini ya ofisi ya Waziri Mkuu kama mjumbe
kwenye kamati ya wataalamu wa kutengeneza mwongozo
wa mafunzo ya wajasiriamali wa taifa.

Mwaka 2012 alitajwa kuwa kiongozi bora kijana duniani


katika kongamano la viongozi vijana lililohusisha nchi
mbalimbali duniani lililofanyika Taiwani, China.
CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 56
KUHUSU MWANDISHI

Amewahi kufanya kazi na Shirika la Umoja la Mataifa


UNESCO na ni mwandishi wa vitabu zaidi ya 15 kwenye
lugha ya Kiswahili, kiingereza na kifaransa.

Ni mkufunzi na mshauri katika masuala ya biashara,


uongozi na ufanisi kazini kwenye makampuni mbalimbali
ndani na nje ya Tanzania.

Joel amemuoa Rachel na wana watoto wawili wa Kike,


Joyous na Joyceline.

CORE GENIUS, Jinsi Ya Kugundua Uwezo Wako Wa Kipekee | Joel Nanauka | 57

You might also like