You are on page 1of 20

Dkt.

Dyaboli

JINSI YA
KUMTONGOZA
MWANAMKE YEYOTE
UKAMPATA
Mbinu 7 Rahisi Zilizosaidia Mamilioni ya
Wanaume Duniani Kote

Dkt. Dyaboli

ii
JINSI YA KUMTONGOZA MWANAMKE
YEYOTE UKAMPATA

JINSI YA KUMTONGOZA MWANAMKE YEYOTE


UKAMPATA: Mbinu 7 Rahisi Zilizosaidia Mamilioni ya
Wanaume Duniani Kote
Copyright © 2020 na Dkt. Dyaboli, Mojo

ISBN: 979-8-35480-737-6

OriginalMinds Publishers
P.O.Box 666,
Uhuru Ave,
Mwanza - Tanzania

Haki zote zimehifadhiwa

iii
Dkt. Dyaboli

“Kama una sura mbaya, na pesa pia huna....


Kuwa fundi wa kutongoza!”

- King Solomon

iv
YALIYOMO

Utangulizi

1 Maana ya Kutongoza na Aina za 10


Utongozaji
 Utongozaji ni Sayansi au ni
Sanaa?
 Utongozaji kwa Njia ya Vitendo
 Utongozaji kwa Njia ya Maneno
2 Ubongo wa Mwanamke 21
 Wanawake Hupenda Mwanaume
Aliye na Sifa Zipi?
3 Epuka Makosa Haya 7 Unapokuwa 32
Unamtongoza Mwanamke
4 Mbinu 7 Rahisi za Kumtongoza 46
Mwanamke Yeyote Ukampata
5 Kanuni ya Dhahabu ambayo 63
Haijawahi Kufeli
 Mfanye Atake Kufanya
Unachotaka Afanye

Hitimisho
Vitabu Vingine vya Mwandishi Huyu
Kuhusu Mwandishi

5
Dkt. Dyaboli

Utangulizi

MAPENZI ndio mkanda unaoishikilia dunia


hii. Kwa vyovyote, mkanda huu ukilegea au
ukifyatuka, dunia itadondoka. Mungu
anajua dunia inao wanawake wa kutosha
kwa kila mwanaume kutongoza pindi
anapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Hata hivyo, kutongoza ni jambo ambalo


bado limeendelea kuwa gumu kwa
wanaume wengi, ingawa hawawezi kukiri
waziwazi kwa kuhofia kuushusha uanaume
wao. Mwanaume anaweza kumwona
mwanamke akavutiwa naye sana tu lakini
akakosa ujasiri wa kwenda kuzungumza
naye kumweleza hisia zake.

Wengi siku hizi hukimbilia kuomba namba


za simu ili watongoze kupitia simu. Wapo
ambao hata baada ya kupata namba ya
simu ya mwanamke husika bado

6
JINSI YA KUMTONGOZA MWANAMKE
YEYOTE UKAMPATA
kumshawishi mwanamke huyo linakuwa ni
zoezi gumu. Wengine wakikutana na
vikwazo vichache tu kama mwanamke
kumwambia hapana, au tayari ana mtu, au
hahitaji mahusiano kwa kipindi hicho, basi
tayari wanakata tamaa na kukubali
kushindwa.

Umewahi kujiuliza ni kwanini kuna


mwanaume mtaani kwako au kwenye
kundi lako anapata wanawake wengi
wazuri wakati wewe unahangaika upate
walau mmoja na bado inakuwa ngumu? Na
mara nyingi ukiangalia unaona kabisa huyo
anayepata wanawake wengi ni mtu wa
kawaida tu kama wewe na inawezekana
hata kipato na mwonekano umemzidi!
Tatizo nini basi?

Kujua Jinsi ya Kutongoza ni silaha muhimu


ambayo kila mwanaume anapaswa awe
nayo kwani ina manufaa makubwa
maishani si tu kwenye mapenzi bali
kwenye nyanja zote za maisha; iwe ni
kwenye biashara, siasa, ajira, mahusiano
ya kijamii, na kadhalika.
7
Dkt. Dyaboli

Sehemu ya ubongo wa mwanaume


inayojihusisha na matamanio ya mapenzi
ina ukubwa mara mbili na nusu
ikilinganishwa na ile ya ubongo wa
mwanamke. Hii ni kusema, fikra za
mapenzi hupita mara nyingi zaidi kwenye
ubongo wa mwanaume kwa siku na mara
moja tu kwa siku kwenye ubongo wa
mwanamke katika siku zake za kawaida.
Kwahiyo kutamani wanawake, kutamani
mapenzi, ni asili ya mwanaume. Hata
viongozi wakubwa wa kiroho wamekiri
kwamba hata miujiza haiwezi kuibadili asili.

Naamini sote tumepata kusikia mikasa ya


wanaume waliochukua maamuzi ya kuwa
wananunua tu makahaba, au kubaka ovyo,
na wengine kujitoa uhai baada ya kuwa
wanakataliwa kila mara na wanawake
waliowahusudu. Unaweza kudhani
wanaume hawa walikuwa na changamoto
za akili lakini nakwambia, hawakuwa na
shida. Kama kungekuwa na mto unaoweza
kutibu mapenzi hapa duniani, hakika mto
huo ungekuwa na thamani kubwa kuliko
8
JINSI YA KUMTONGOZA MWANAMKE
YEYOTE UKAMPATA
dhahabu.

Yaani pesa huna, sura huna, hata ukimwi


huna; na uwezo wa kutongoza nao ukose?
Qmmmq! Sasa wewe unawezaje kuwa
mfano wa Mungu?

Inaeleweka vema kwenye idara za


Udodosi wa Akili na Mahusiano ya
Wanadamu kwamba tabia ya mwanadamu
iko kama kahaba; inalala na yeyote
anayeandaa kitanda. Ni kwa namna gani
unaweza kuandaa kitanda hicho, ndicho
ninachokwenda kukufunza ndani ya kitabu
hiki.

9
Dkt. Dyaboli

1.
MAANA YA KUTONGOZA NA
AINA ZA UTONGOZAJI

UTONGOZAJI ni Sayansi ya Akili. Ni


mchezo wa akili wa kuweza kujipatia
unachotaka toka kwa mtu, wakati
mwingine pasipo hata kuomba, na
huweza kutumika kujipatia chochote
maishani ikiwa ni pamoja na mapenzi,
pesa, utiifu, nafasi ya kazi, uaminifu,
wafuasi au kitu kingine chochote.
Huhusisha kupindua uhalisia wa jambo
ili liweze kufanyika kwa manufaa yako.
Tunaweza kusema wanasiasa wakubwa
na wafanyabiashara nguli hasa wa idara
za masoko ni miongoni mwa
10
JINSI YA KUMTONGOZA MWANAMKE
YEYOTE UKAMPATA
watongozaji wazuri zaidi duniani.

Katika muktadha wa kitabu hiki,


kutongoza ni kumshawishi mwanamke
kwa mbinu mbalimbali, wakati mwingine
za ulaghai, ili aweze kukubaliana nawe
na kuanzisha mahusiano ya kimapenzi
na wewe. Ni jambo ambalo linaweza....
kufanyika ghafla tu kwa mwanamke
unayekutana naye kwa mara ya
kwanza, au inaweza kuwa ni
mwanamke ambaye unamfahamu ila
una hisia za mapenzi juu yake kwahiyo
unahitaji kuwasilisha hisia hizo kwake ili
muwe wapenzi.

Kwa maneno mengine, kutongoza ni


kama kujiuza na kuhakikisha unauzika
kwa mwanamke unayemtaka. Ni kama
wewe unakuwa ni bidhaa ambayo kwa
namna yoyote ile inatakiwa iwe vile
ambavyo mteja wako (mwanamke
husika) atavutiwa nayo na kukubali iwe
yake.

11
Dkt. Dyaboli

Ingawa kutoa midokezo au kumfuata


mwanamke moja kwa moja kumwelezea
hisia zako linaweza kuonekana kuwa ni
jambo gumu au la kutia woga,
kutongoza hakupaswi kuwa jambo la
kumtia hofu mwanaume. Linapofanyika
kwa umakini na usahihi kwa
kuzingatia.....................

12
JINSI YA KUMTONGOZA MWANAMKE
YEYOTE UKAMPATA

13
Dkt. Dyaboli

VITABU VINGINE VYA


MWANDISHI HUYU:
ALMASI YA KIJANI: Tiba ya Magonjwa
Yote Duniani. Magonjwa yote duniani
yanatibika na kupona kabisa lakini
ulimwengu wa sayansi hautaki hili liwe
wazi kwasababu magonjwa ni biashara
kubwa inayokiingizia Kiwanda cha Tiba
matrilioni ya dolari kila mwaka. UKIMWI,
Saratani, Shinikizo la Damu, Pumu,
Kisukari, Upungufu wa Nguvu za Kiume,
Siko Seli, n.k., yote yanatibika na kupona
kabisa. Lakini wakikutibu ukapona kabisa
si biashara yao itadorora? Wenyewe wana
kauli-mbiu yao inasema “Huwezi kupata
pesa nyingi toka kwa mgonjwa anayepona;
mfanye aendelee kuwa mgonjwa!”
Kitabu hiki kinakupa tiba mujarabu za
majani, maua, mizizi na magome ya miti
kwa magonjwa yote duniani!

WASOMI WAJINGA (Rais Hana Nguo):


Hii ni tamthiliya ya kisiasa, komedi nyeusi,
inayoangazia changamoto zinazokikumba

14
JINSI YA KUMTONGOZA MWANAMKE
YEYOTE UKAMPATA
kijiji cha Nyinyoro (nchi huru ya kiafrika) na
jinsi viongozi wake wanavyotumika kama
vibaraka wa Watu wa Chaki (Wazungu).
Inajaribu kufichua nani ni nani, kwanini
mambo yanakwenda yanavyokwenda, na
kuangalia uwezekano wa kukikomboa kijiji
toka kwenye meno ya Wanyinyoro walafi
na Watu wa Chaki.
Tembea ujifunze; mpishi bora sio mama
yako! Kuna uovu mkubwa ndani ya kijiji
hiki. Kuna wafu wanakunywa damu za
watu. Halafu ajabu, watoto wanaogopa
giza, wakubwa wanaogopa mwanga.
Waliokula chumvi nyingi matendo yao
hayana ladha.
Mmoja wa wanakijiji anasema ‘Kwakweli
hali ni tete; majalalani sasa mbwa na paka
wanakula hadi viatu! Nani atupe ugali? Kila
kitu kimepanda bei isipokuwa pombe,
sigara na kondom. Watu wanatembea
wamekodoa macho kwasababu njaa
inawafanya washindwe kuona vizuri.
Wanawake wanazidi kuota ndevu na kuwa
na matumbo makubwa kwasababu ya kula
viporo. Wanaume watapata wapi nguvu za
kiume na hali ya maisha ilivyo?’

15
Dkt. Dyaboli
Vilio vimetapakaa. Wanaikumbuka kauli-
mbiu ya kiongozi aliyepita:
‘Usipojikaza Unakazwa!’
GIDI: MTI WA MAARIFA (Jinsi ya Kuuza
Roho Yako kwa Shetani ili Upate
Mafanikio). Hukuumbwa ili uwe masikini.
Kitabu hiki kinatoa mwongozo wa jinsi ya
kufungua Malango ya Kuzimu ili kusaini
mkataba na Mfalme wa Kuzimu upate
mafanikio maishani. Matambiko
yanayoelezwa na Abramelin the Mage
ndani ya kitabu hiki ni ya hatari sana kwa
mtu ambaye ni maamuma kwenye ibada
za kishetani kwani Malango ya Kuzimu
yakishafunguka hakuna kurudi nyuma.
Hata hivyo, kinachomvutia Mfalme wa
Kuzimu sio ujuzi wako wa kumwita kwa
usahihi bali ni utayari wako wa kuikumbata
dhambi na kuieneza. Unaweza kuuliza
‘Kama matambiko hayo ni ya hatari kiasi
unachosema, kwanini unayaandika
yasomwe basi?’ Na mimi nitakuuliza
“Kwanini Mungu aliliweka Tunda la Maarifa
mbele ya macho ya Adam na Hawa?”
Ukijibu swali langu, utakuwa umejibu swali
lako.

16
JINSI YA KUMTONGOZA MWANAMKE
YEYOTE UKAMPATA
Kama umechoka kuwa askari, unaweza
kuamua kuwa Mfalme. Hii ndiyo ramani.
Ave Satanas!
SEXUS: Siri za Ngono Tamu. Watu
wengi wanafikiri kufanya mapenzi ni
kuingiza uume ndani ya uke na kuanza
kushindilia au kukatika mpaka wafike
kileleni. Unakuta mwanaume anashindilia
mpaka mishipa ya shingo inasimama!
Wewe! Hapo unafanya mapenzi au
unafanya mazoezi? Ngono ni sayansi.
Ngono ni sanaa. Ngono ndiyo mchezo
wenye wachezaji na mashabiki wengi zaidi
duniani, lakini bahati mbaya zaidi ya 85%
ya watu hawajui jinsi ya kuucheza kwa
usahihi. Leo wengi wanasingizia vibamia,
mabwawa na upungufu wa nguvu za
kiume. Kila mchezo una siri na kanuni
zake!
Kitabu hiki ni Mwongozo unaokupa siri
kabambe za Kufanya Ngono kwa Usahihi
ili muweze kuridhishana, kupendana
maradufu na kunufaika kihisia, kiakili na
kiroho.
TAFSIRI ZA NDOTO. (Kwa ushirikiano na
Mchungaji Abel Muthembi, Sheikh Umar
17
Dkt. Dyaboli
Al-Majid na Mganga wa Jadi Snubi wa
Mandembo). Kwanini tunapolala huwa
tunaota? Je, ndoto tunazoota huwa
zinajaribu kutwambia nini?
Watu wengi hukumbwa na mabalaa au
kupoteza fursa muhimu kwasababu waliota
ndoto zilizowatahadharisha au kuwapa
mwongozo lakini hawakuchukua hatua
kwasababu hawakuelewa ndoto hizo
zilimaanisha nini. Hii ndiyo sababu imani
na dini zote ulimwenguni zinautambua
umuhimu wa ndoto.
Ndoto zinaweza kukwambia ikiwa kazi
yako, mahusiano yako, afya yako au hata
wapendwa wako, viko hatarini. Zinaweza
kukwambia fanya hiki - ndiyo njia yako ya
mafanikio. Lakini kama hujui jinsi ya
kutafsiri ndoto,...?
Kitabu hiki kinakufundisha jinsi ya
kuzitafsiri ndoto unazoota ili uweze
kuzitumia kwa usalama na mafanikio ya
maisha yako.

UJINGA WA BABA: Riwaya ya Uhalisia


iliyosheheni matukio ya kusisimua na
kustaajabisha.

18
JINSI YA KUMTONGOZA MWANAMKE
YEYOTE UKAMPATA

KUHUSU MWANDISHI
Dkt. Dyaboli ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha
Alexandria, Misri, na ana Shahada za Uzamili
katika Uponyaji wa Asili, Udodosi wa Akili,
Falsafa na Usikirifu. Hupendelea kufanya tafiti za
kina na za muda mrefu ili kupata majibu ya
maswali magumu na ufafanuzi wa mambo
yanayoonekana kutokuwa ya kawaida.

Mwaka 2014 alishiriki kwenye Uchunguzi wa Tiba


za Asili miongoni mwa watu wa kabila la Mano
huko Libya, uchunguzi ulioratibiwa na Ofisi ya
International Health ya Marekani. Mwaka 2015
akiwa nchini Uingereza alipata mwaliko wa
kujumuika na uongozi wa The Satanic Temple
kwaajili ya chakula cha jioni. Walizungumza
mengi. Kati ya mwaka 2015 – 2016 alishiriki
kwenye miradi mitatu ya uponyaji wa asili kwenye
nchi za Afrika Kusini, Mali na Gabon, miradi
ambayo ilikamilika Julai 2016, na mwaka 2017,
yeye na rafiki yake wa siku nyingi, Dkt. Gandhi,
walifanikiwa kuongoza makundi mbalimbali ya
matabibu wa tiba asilia kwenye sherehe za tiba
za jadi nchini Nigeria.

Ameendelea kufanya tafiti mbalimbali


akishirikiana na wataalamu katika nyanja za dini,
usikirifu, elimu ya viumbe kama majini, sayansi,
na uchawi.

19
Dkt. Dyaboli

Email: drdyabolimojo7@gmail.com

WhatsApp: +255 699 321 918

20

You might also like