Professional Documents
Culture Documents
NAJIFAHAMU
NAJIFAHAMU
1
YALIYOMO:
1. UTANGULIZI……………………… 3
SURA YA KWANZA.
1. Mimi ni nani?.......................................4-7
2. Ninajengaje fikra njema niwe mwema…8-12
SURA YA PILI.
SURA YA TATU.
SURA YA NNE.
SURA YA TANO.
2
UTANGULIZI.
3
SURA YA KWANZA
1
MIMI NI NANI?
K
atika kutambua mzizi wa matatizo yetu, na ukweli wa kuyahusu
maisha yetu kujitambua ni moja ya jambo muhimu sana.
Mtu anayejitambua na kufahamu kuwa yeye ni nani na yupo hapa duniani kwa
kusudi gani?, atakuwa na ufahamu wa juu kuhusu maisha yake na ya wengine
na kwa kufahamu hilo atakuwa na uchukuaji mkubwa wa hatua za kimaisha.
4
Kuelekea safari ya kujitambua inahitaji kuacha kuamini watu
wanavyokusema na kukuona, bali inahitaji kujitafuta wewe na kuja ukiwa
wewe na kuiambia dunia niiteni kwa jina hili na nitambueni kwa jina hili,
mimi ni huyu futeni yale yote mliyokuwa mkiinita kuwa mimi ni
mshindwaji, kuwa mimi ni asiyejua kitu, kuwa mimi ni mhangaikaji
tu nisiye na maana, kuwa mimi si lolote wala chochote, waambie
wafute hayo majina na waanze kukuona katika muono mpya na muonekano
mpya wenye nguvu zako na wenye uwezo wako wote.
Kumbuka wewe si mwili huo ulio nao, na wewe si jina hilo unaloitwa, wewe ni
zaidi ya hayo na wewe unatambulika kwa mambo haya matatu muhimu;-
6
Kwahivyo jambo la kwanza na muhimu sana kwenye safari ya kujitambua
unapaswa kukubali na kukili kuwa unao uwezo mkubwa sana wa kufanya
mambo makubwa na inategemea akili yako ina nini?, maswali ya kujiuliza ni
kuwa unaipatia na kuilisha mawazo gani ? mambo ambayo yanatengeneza
msingi wa kuwa wewe.
Ni wakati muafaka sasa kuanza kuipatia akili mambo mazuri kwa maana ya
kuchunga sana taarifa unazozipokea na ambazo mara kwa mara unaulisha
ubongo wako kwakua hizo ndiyo hugeuka kuwa wewe kwa kujionyesha
kwenye hisia zako na matendo yako. Kwamba hisia zako na matendo yako ni
zao la akili (fikra) zako na kama utakuwa mwenye akili njema basi utakuwa na
hisia njema na matendo mema na mwisho kuwa mtu mwema na mwenye
kujitambua.
7
SURA YA KWANZA
2
NINAJENGAJE FIKRA NJEMA ILI NIWE MWEMA?
U
jengaji wa fikra njema (akili) njema ndiyo jambo muhimu la kufanya
kuelekea ujitambuaji wa juu, safari hii inakutaka kuanza kuondoa
fikra mbovu ambazo kwa hakika zimekufanya kuwa mtu wa ajabu
kwenye jamii na kukupatia maisha ya majuto, maisha ya kujitweza, maisha ya
kukosa uthubutu wa kufanya makubwa, maisha ya kuogopa kila kinachotokea
kwenye maisha yako badala ya kukikabili na kujitengenezea maisha bora,
unaishi ukiwa umekufa angali ukiwa unatembea kwakua kila kitu
kinakuchukua wewe na unakwenda kwa kila mwelekeo moja ya jambo baya
sana kwenye maisha ya binadamu.
Katika kufahamu ni kwa namna gani unaweza kujenga fikra njema na zenye
umuhimu sana kwenye maisha yako kukupatia maisha unayoyataka na
mwisho kuwa mtu mwema mwenye kujitambua ni kwa kufanya mambo haya:-
8
1. Jiweke katikati ya makundi ya watu waliofanikiwa zaidi yako, hii
itakutia hamasa, na wivu mzuri, na kukupatia bidii ya kufanya
vizuri zaidi na zaidi.
2. Jitamkie maneno chanya kila siku kuwa utakuwa mtu bora
mwenye uwezo wa juu na mwenye kuutumia uwezo wako wote
kwa ajili ya mafanikio yako.
3. Jiepushe na watu wanaokukatisha tama na waepuke kabisa kwa
kaa nao mbali, na hawa kuwafahamu ni rahisi sana utaona stori
zao ni za kulalamika, kukosoa tu, kuhukumu, na kukatisha tamaa
kwa kila hatua unayotaka kuichukua achana nao hawa
wananyonya uwezo wako wote ni sawa na gari yenye tenki bovu la
mafuta haiwezi kukaa na mafuta kwa ajili ya safari ya mbali.
4. Tafuta mtu wa kukushauri aliyefanikiwa mweke karibu na mtumie
kukushauri.
5. Azimia kuachana na mabaya na uanze kuishi kwenye njia ya
uchanya ama uzuri unaovutia ambao utakuletea watu wazuri na
ambao ulitaka kuwa nao nyakati zote.
6. Azimia kuwatendea wengine kwa uzuri kwa lengo la kuwafanyia
jambo jema na zuri na la heshima bila kutarajia kitu toka kwao.
Anasema siku moja alirudi nyumbani akiwa mwenye uchovu wa hali ya juu
sana kiasi cha kuyakatia tamaa maisha yake na kuona hakuna analoweza
kufanya alikaa chini ndani ya nyumba yake na kujiuliza maswali muhimu na
kujambia kwa mfumo mtazamo chanya juu ya maisha yake kwa kusema
“hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwangu, na hakuna mwenye
dhamana na maisha yangu, yakiwa mabovu kama yalivyo sasa ni mimi
9
mwenyewe , na kama nataka yawe mazuri ni mimi mwenyewe wenye uwezo
wa kuyafanya yawe mazuri” baada ya maneno haya akachukua kikaratasi
akaandika nini anataka kwenye maisha yake anasema kutoka hapo maisha
yake yalianza kubadilika na kuanza kuishi maisha ya mafanikio na sababu ya
kuanza kuishi maisha ya mafanikio ni pale tu alipoamua kuandika mambo
anayoyataka kwenye maisha yake.
Na malengo hayo yanaweza kuwa ya muda mfupi yaani kuanzia mwezi mmoja
mpaka mwaka mmoja, ambayo yaweza kuwa kama
Ama malengo ya muda wa kati yaani kuanzia mwaka mmoja mpaka miaka
mitano na isizidi miaka mitano ambayo yaweza kuwa:-
Ama malengo ya muda mrefu haya ni ya zaidi ya miaka mitano mpaka miaka
kumi na yaweza yakawa:-
11
yako inayotokana na matokeo ya fikra zako juu ya mambo muhimu ya
kijamii kama dini yako, saikolojia yako(tabia zako), falsafa yako(yale
unayoyaamini), na mwisho kuwa na mtazamo utakaotoa matendo na kuwa
wewe.
Kwahivyo unajenga ndani yako kwanza kisha ndani yako inatoka nje na nje
yako inaakisi ndani yako ulivyo juu ya mambo unayoyapenda sana na
ambayo unayafanya kwa urahisi sana hata kama wengine wanasema
hawajui na wamechoka kufanya lakini wewe unafanya tu, na kadili
unavyofanya ndivyo kiwango chako cha furaha na utoshelevu ndivyo
kinavyokuwa na kuwa kikubwa sana na mwisho kuwa wewe na watu
wanasimama kukupigia makofi baada ya kufanya kwa ishara ya
kukuheshimu na kukupongeza.
Mambo hayo yaweza kuwa kuimba kwako, kucheza kwako, kuongea kwako,
kuwashauri wengine, kuchora, kufanya mahesabu, kufundisha, kuwatetea
watu, kuongoza tukio fulani kwa uzuri, kuuza, kuwahudumia wengine,
kupika, kubuni, kusaidia wengine, na n.k hayo ndiyo yanayokutambulisha
kuwa wewe ni nani?
12
SURA YA PILI
1
AINA YA VIPAJI NA NAMNA YA KUFAHAMU KIPAJI CHAKO.
V
ipaji ni moja ya injini iliyowafanikisha wengi baada ya kufahamu
wanakipaji cha aina gani? , na baada ya kufahamu hawakubaki kusema
tu kuwa kipaji hiki kitanivusha bali waliingia kukifanyia kazi zaidi na
zaidi katika kukifanya kianze kuishi na baada ya mazoezi magumu ya bila
kuchoka na ya kila siku mwisho dunia ilikuja kuwatambua kuwa hawa ni watu
wasio kuwa wakawaida na wanapaswa kupewa heshima kwa kazi zao nzuri
zilizotukuka kutokana na vipaji, dunia inashuhudia uharibifu mkubwa wa
vipaji vya maana ambavyo vvipo ndani ya watu na watu hao hawafahamu
kama wanavyo vipaji hivyo na wameishia kuishi maisha ya kawaida na yasiyo
na maana kwa jamii, inasadikika kuwa angali binadamu anapokuwa katika
hali yake ya utoto kiwango chake cha kipaji huwa kipo juu sana zaidi ya
asilimia 98% akiwa kwenye umri wa miaka mitano mpaka kumi , baada ya
kutoka hapo mtoto huanza kupoteza uwezo wa vipaji vyake na mpaka kufika
umri wa miaka kumi na nne anakuwa kapoteza uwezo mkubwa wa vipaji
vyake na kuanza kuishi gizani, na sababu kuu zinazotajwa kuchangia uharibifu
huu mkubwa wa vipaji ni malezi ya wazazi , mazingira anayokulia, aina ya
elimu anayopata, mambo haya hudidimiza kabisa tumaini la mtoto kuishi na
vipaji vyake mwisho wa siku anakuwa dubuwasha ama roboti wa kupangiwa
kila kitu, cha kufanya, namna ya kuwaza, namna ya kufikiri, namna ya kula,
namna ya kuenenda, namna ya kufurahi, namna ya kukasirika n.k.
Benjamin franklini aliwahi kusema kuwa watu wengi sana wanakufa wakiwa
na miaka 25 na wanazikwa wakiwa na miaka 75 , kwamba kwenye maisha
kuna aina tatu ya vifo , moja kifo cha kiroho ambapo mtu anakuwa hana
mahusiano ya moja kwa moja na nguvu tenda yaani Mungu katika kumsaidia
kufanya makubwa hapa duniani , na kifo aina ya pili ni kifo cha uwezo wake
wa kufanya mambo kwa njia ya urahisi sana lakini anachokifanya anakifanya
kwa uzuri na wengine wanampongeza kwa kufanya hicho anachokifanya yaani
kifo cha kipaji chake ingawa unaendelea kupumua lakini unaishi chini ya
uwezo wako, kifo cha aina ya tatu ni kifo cha kimwili ambapo hapa unakufa
mwili wako na kuzikwa kaburini habari lako linakuwa limekwisha kama na
hakuacha alama duniani basi unabaki kuwa umeandikwa majina yako ya
utambulisho hapa duniani kwenye kaburi lako tu.
Kifo aina ya pili yaani kufa kivipaji ni moja ya kifo cha hatari sana kwakua
unaishi duniani bila kuwa na kusudi na moja kwa moja hauwezi kuwa na
furaha, kwakua hakuna hata ndoto moja ulizokuwa nazo iliyowahi kutimizwa
, unaishi kwa kukata tamaa, unateswa na mambo ya kupita kama matatizo,
changamoto na umebaki kuwa bingwa wa kusimulia matatizo yako badala ya
kusimulia na kuhubiri mafanikio yako umekuwa unajulikana kwa majina ya
matatizo mbaya sana.
Ndani yako una uwezo mkubwa sana, kama utakubali leo kuanza kuchukua
hatua kubwa kubwa za kujitafuta ndani yako na uanze kuishi wewe ukiwa na
mwenye kila kinachohitajika kwenye maisha yako, wajapani wanaopatikana
kwenye mji mmoja mzuri sana ujulikanao kwa jina la Okinawa , moja ya sifa
ya mji huu ni kuwa wakazi wa eneo hili wanaishi miaka mingi sana duniani, na
ni moja ya eneo ambalo watu wake wanaishi wakiwa na furaha kwa kipindi
kirefu, nyuso zao zinauchangamfu wa kiwango cha juu, huwezi kukosa kutoka
kwao tabasamu, vicheko, kufanya kazi kwa upamoja, kukaa kwa upamoja na
huku wakicheka, utani wa hapa na pale, ulaji wa vyakula vya asili ambavyo
14
hulima kwenye nyumba zao, na ulaji wa mazao ya ziwa na bahari naaam kwa
uzuri mji huu ulifikia hatua mpaka ya kubadilishwa jina na kuwa mji wa
waishi miaka mingi yaani (longevity) kilichokuja kugundulika kutoka kwa
watu hawa ni kuwa ni miongoni mwa watu wanaishi kwa kusudi yaani Ikigai
neno la kijapani lenye maana ya kuishi ~iki kwa kusudi ~Gai na kupatikana
falsafa ya Ikigai ambayo inawasaidia wajapani wengi kugundua
vipaji vyao na kuviishi kwa kutumia kanuni muhimu nne ambazo
ni
Hii ina maana mambo gani unaweza kuyafanya kwa ajili ya wengine yaani
kufanya kwa ajili ya wengine kujitoa kwa uwezo wako kwa ajili ya wengine
hapa wawajibika kutambua mambo hayo unayoweza kuwafanyia wengine.
Hii ina maana ya mambo ambayo huwa unayafanya ukiwa na furaha sana na
hauchoki kuyafanya hapa wawajibika kuyatambua mambo hayo.
3. Upi ujuzi wako unaokufanya kufanya jambo fulani kwa uzuri zaidi?
Hii ina maana ya kufahamu ujuzi wako na huu waweza kuwa wa kusomea ama
wa kujifunza chini ya mtu mwingine na ukawa na ujuzi huo wa juu na kila
ukifanya wengine wanauliza kwa hamu ya kutaka kujua nani kafanya kitu
hicho na unatajwa kuwa ni wewe.
15
Kurahisisha kujifahamu wewe jiulize maswali hayo na yapatie majibu na
yaandike na ukishayaandika yafanyie kazi kila kukicha na endelea kujiuliza
maswali sahihi na ujiambie ukweli kwa mfano, nini kinanisukuma kuamka
asubuhi na mapema na kitu gani kinanifanya kuchelewa kulala ? kitu hicho
chaweza kuwa kimebeba siri za kufanikiwa kwako na kuanguka kwako gundua
kwa haraka na kama kinakupa mafanikio na furaha endelea kupapalilia
kukifanya na kama kinakupatia maisha ya hovyo anza kuachana nacho mara
moja ili uanze kuishi wewe ujifahamu uzuri wa kuwa wewe.
16
SURA YA PILI
2
NJIA NYINGINE NZURI ZA KUFAHAMU VIPAJI CHAKO.
M
wandishi na mwanasakolojia wa chuo kikuu cha Harvad nchini
marekani miaka ya 90 alianidika kitabu kizuri sana kijulikanacho
kama Frame of Mind ndugu Howard Gardner aliandika
kitabu hicho kuashiria kuwa kuna aina ya uwezo mkubwa sana walionao watu
wa kitofauti tofauti baina ya huyu na yule na si kwamba wote tunapaswa kuwa
na aina moja ya uwezo wa juu yaani uginiasi , kupitia kitabu chake anaibua
aina saba ya uwezo wa juu ambao unawatambulisha watu na huenda na wewe
ukajigundua upo kwenye eneo gani.
Uwezo huu una maana ya kuwa watu wenye uwezo huu wana uwezo wa juu
kuhusiana na masuala ya kimahesabu na wanao ujuzi huu kwa asili ama
kwa kujifunza kwa kiwango juu. Watu wanapatikana kwenye kundi hili ni
pamoja na wanamahesabu wakubwa , wanasayansi , madaktari wakubwa ,
wana anga.
17
iii) Spatial (Uwezo wa juu wa kiubunifu na sanaa)
Uwezo huu una maana ya watu wenye ubunifu wa juu kutokeza mambo
mapya ama kuyatokeza kwa namna yake ya kipekee. na watu kutoka kundi
hili ni pamoja na wasanii wakubwa , wachoraji .
Uwezo huu unawahusu watu wenye uwezo wa kutumia uwezo wa miili yao
kutokeza mambo mazuri na makubwa kwa kutumia mwili tu kama
kukimbia , wacheza mziki ,mafundi ujenzi ,mafundi makanika, mafundi
mbao ,na hata wapishi wakubwa. Watu kutoka kundi hili wanasifa kuu ya
kujifunza kwa kutenda yaani (hand on learning)
Uwezo huu unawahusu watu wenye wenye kuongea sana , ama kuzungumza
kwa umahili na kuwasiliana na wengine kwa urahisi, na watu kutoka kundi
hili ni pamoja na waimbaji wakubwa , wahubiri wakubwa , wahamasishaji
wakubwa ,wanasiasa wakubwa , waigizaji wakubwa , na wauzaji
wakubwa.
18
Baada ya kuwa umeona aina za vipaji kama hivyo hapo juu, sasa nawe
unaweza pia kufahamu aina ya kipaji chako kupitia ama kwa kutumia njia
kama hizi.
b) Baada ya kuwa umeandika majibu yako kwa uzuri jaribu kuwauliza watu
unaofaana nao sana kisha wao wakwambie wanakuonaje na kisha nenda
ulinganishe na majibu yako ambayo ulikuwa wajichunguza na kujifanyia
tathimini juu ya vipaji vyako, kuna namna fulani utaona kuna kufaana
ama kupata wazo jipya juu yaw ewe.
c) Andika kile kilichosemwa na hao wengine juu yako, ili uanze kuyaona
mambo kwa uhalisia na kuanza kujifahamu.
19
d) Mwisho linganisha majibu yako na kile ambacho wengine wamesema na
kisha fuata hatua inayofuata juu ya kuanza kuishi kipaji chako na
kukitendea haki.
20
SURA YA PILI
3
KUFANYIA KAZI KIPAJI NA KUANZA KUISHI WEWE.
H
aitoshi kuwa na kipaji tu, kisha ukafanikiwa na kipaji hicho kuna
hitajika mambo ya kufanya muhimu sana kukifanya kipaji kikusaidie
kutimiza mengi na yenye mafanikio hapa duniani katika safari ya ya
kujitambua na kuanza kuishi uwezo wako ama wewe, mambo hayo ni pamoja
na kuwa tayari umekifahamu kipaji chako na sasa unataka kuanza kufanyia
kazi basi fanya haya kwa uzuri kabisa utaona ukifanikiwa kutokana na kipaji
chako.
21
2) Wacha visingizio.
Wengi ya watu wanaacha kufanyia kazi vipaji vyao kwa kujipa visababu na
visisngizio vingi na wanaweza kuorodesha sababu hata mia za kwanini
hawawezi kufanya jambo fulani na ukizingalia kwa umakini na jicho la
mashaka unaweza kulidhia kabisa kuwa watu hawa wapo sahihi kutokufanyia
kazi lakini ukweli wa mambo ni kuwa hata kama zitakuwepo sababu za msingi
za wewe kutokufanyia kazi kipaji chako nakwambia ziweke pembeni na
ziambie naomba mnisubiri hapa kwanza naenda kufanya kwa namna yoyote
ile, kisha jitose kwenda kufanya, washindi wote waliacha kujionea huruma ,
kujipa sababu zisizo na maana juu ya mambo fulani fulani na waliazimia
kufanyia kazi vipaji vyao iwe jua linawaka ama mvua inanyesha.
Na kwa sababu unao uwezo wa asili anza kufanyia kazi kipaji chako
utajikusanyia mafanikio ya kutosha na mali za kutosha na dhamiria kuwa
hakuna jambo litakuzuia kufanyia kazi kipaji chako, na kama kuna vizuizi njia
za kutatua na kuondoa vikwazo hivyo vitatumika na utafanikiwa.
22
4) Endeleza kipaji chako kwa kuwasaidia na wengine.
23
b) Mshauri (mentor)
Hawa kazi yao kubwa huwa wanafanyaka kazi kukuonyesha njia kule
unakotaka kwenda na njia hiyo yaweza kuwa kifamilia , kiuchumia au hata
kibiashara, mshauri anakupatia ushauri mwanana ambao unatakuwa
unahitaji sana, anakushirikisha taarifa muhimu na yeye hufurahi wewe
unapofanikiwa na huchukia pale unaposhindwa kuchukua hatua muhimu
zinazohitajika ili kukufanya ufanikiwe.
Ili kuwatunza washauri kumbuka haya kwamba wao wapo kwako si kwakua
wanataka uwalipe ama usaidie wenyewe wapo kwako kukutegemeza kiushauri
kwahivyo kuwa makini na uwatunze na tambua mchango wao kwenye maisha
yako.
c) Rafiki (friend)
Hawa ni wale ambao kwa muda mrefu upo nao na kuna aina fulani ya tabia
mnaendana na kwa hakika anakufaa kwa mchango wake wenye tija kwenye
maeneo yako ya kile unachotaka kufanya.
d) Sahibu (comrade)
Hawa ni wale wanakuja kwenye maisha yako kwa sababu maalumu nayo ni
kwa kuunganishwa na adui ambaye ni adui yako lakini na yeye sahibu
amekutwa adui huyo naye ni adui yake kwahivyo anakuja kuunganisha nguvu
kummaliza adui yenu, akimaliza kumuungamiza adui yenu huyo huondoka
kwenye maisha yenu.
24
f) Kocha (coach)
Ni mtu anayejua vipaji vyako ama aina ya uwezo wako fulani ambao wewe
haujaugundua ama hauvijui na yupo tayari kukuambia namna ya kufanya.
g) Mwamini (confidant)
25
SURA YA TATU.
1
JENGA TABIA BORA NAYO ITAKUJENGA KUWA BORA.
K
atika safari ya kujitafuta na kujitambua huwezi kuliacha jambo la
kitabia, tabia ndiyo muhimili wa muhimu katika kuelekea safari yako
ya kujitambua na kuanza kuishi wewe kwa furaha.
Ili kufamu kwanini tabia ni muhimu tufahamu maana yake kuwa tabia ni
pamoja na mambo yote amabayo mtu/kiumbe hufanya kwa kuyarudia rudia
ambayo yanatujenga kwa uzuri ama kwa ubaya na kama ukitaka kuanza
kubadili hatua zako muhimu kimaisha eneo hili ndiyo eneo wa kulipatia uzito
wa juu na kwa umhimu wake unaotakiwa sana.
26
unasikiliza nyimbo za aina ileile iliyojengwa kichwani kwako, mikanda ya
video iliyojengwa kichwani kwako, kukaa na aina ya watu waliojengwa
kichwani kwako na vyote hivi vyaweza kuwa chanya ama hasi ni wewe
unayewajibika kufanya mabadiliko yanayotakiwa.
Milango yetu ya fahamu inaingiza taarifa na hizi taarifa zinajenga picha kwa
matendo ya kurudiwarudiwa na hukaa huko na mwisho hukomaa katika akili
isotambuzi na ikishafika huku hushika nguvu na kufanya vitu viende
vyenyewe na hapo sasa ndiyo yanapotokea matabaka ya watu wenye furaha na
wasio na furaha na wenye mafanikio na wasio na mafanikio ni kutokana na
tabia ambazo huwapatia matokeo ya kimafanikio na kiuduni kwa asilimia 99%
, aliyeduni anatabia duni kwa asiliamia 99% na mwenye mafanikio anazo tabia
za kimafanikio kwa asilimia 99%, kwamba matajiri wameshajingea uwezo wa
kuona utajiri akilini mwao na mambo hayo yanafanyika yenyewe pasipo
kutumia nguvu kwakua yameshakuwa akilini mwao na yanathibitishwa na
matendo yao , hivyo hivyo kwa maskini na wenye hali dhoofu kuwa ndani yao
kunakuwa kumejenga umaskini wa kutisha na kinachoonekana nje yao ni
matokeo ya ndani yao.
Na mwisho jambo hilo hugeuka kuwa tabia ya mtu na litaanza kufanyika bila
yeye kuliwazia ama kulipangia kulifanya na ubongo wake hautakuwa tena kazi
ya kuanza kulifikiria jambo hilo badala yake litajitokeza kwa haraka tu
kichwani na kufanyika.
Sasa katika kutaka kubadili tabia mbaya ni muhimu kubadili mambo mawili
ya juu na na la tatu muhimu kwamba badili kisababishi na kisha badili
mazoea, kwa mfano kama ulizoea kukaa na walalamikaji, wenye kulaumu kila
kitu kinachotokea kwenye maisha yao, basi acha kwenda kukaa nao kaa na
wale wanaokujenga wale wenye mtazamo chanya wenye kuona fursa kwenye
mkingamano wa matatizo na hapo taratibu taratibu jambo hilo litaanza
27
kufutika kichwani kwako kwa kupakiwa jambo jipya mbadala na hilo,
kumbuka kuanza kidogo kidogo bila kuacha kubadili tabia mbaya na mwisho
tabia hizo zitabadilika.
Tunaposema tabia mbaya maana yake halisi ni zile tabia ambazo hazikujengi
badala yake zinakubomoa na kukuacha ukiwa mwenye huzuni kuu, mwenye
kuteseka kihisi, mwenye kubaki na hatia tabia hizo ni kama uvutaji wa sigara,
utumiaji wa madawa ya kulevya, ulevi wa kupindukia na mambo kama hayo.
i) Tabia ya ubinafsi, hali ya uchoyo kufanya mambo kwa ajili yako tu.
ii) Tabia ya kuwa na uoga wa kushindwa.
iii) Tabia ya kutokuweka malengo yanayofikiwa.
iv) Tabia ya kughairisha mambo na ukianza haumalizi unaishia njiani.
v) Tabia ya kutokutaka kujifunza.
vi) Tabia ya kutokutenda yale uliyopanga.
vii) Tabia ya kukosa uvumilivu.
viii) Tabia ya kutokuwa na vipaumbele unafanya lolote lile.
ix) Tabia ya kukata tamaa.
x) Tabia hasi kukaa na watu hasi, kulalamika, kulaumu kwa kila kitu ,
kukosoa kwa kila jambo.
Hizo zinaweza kuwa sehemu ya tabia mbaya na haribifu sana kwenye safari
yako ya kimafanikio na katika kujitambua na kujifahamu wewe ni nani na
uanze kuishi uzuri wa maisha uyatakatayo.
28
kujihusu wewe na ikifuatiwa na nguvu ya matendo makubwa
yanayoyafanya hayo kujidhihiri wazi kwenye maisha yako.
ii) Kukaa na watu chanya , ikiwa ni pamoja wale unaopenda kuwa kama
wao, wale wanaokuhamasisha kufanya makubwa, wale wenye
kuthubutu, wale wenye kutenda kwa vitendo wanayoyasema
midomoni kwao, wale ambao furaha na tabasamu halikauki kwenye
nyuso zao, wale ambao wana nguvu ya kuona kesho kwa kutenda
vyema leo wakijiandalia kesho yao nzuri.
iii) Kuvuta hisia ya mambo mazuri, hii ni tabia nzuri sana na yenye
nguvu sana katika ujenzi wa mambo makubwa akilini kwako, ona
malengo uliyoyaandika yakitimia, ona dunia yenye utele wa kila aina
ya fursa na mawezekano ya kimafanikio, jione ndani yako ukiwa
vizuri na mwenye nguvu za kufanikisha malengo yako.
29
vi) Kuza na kuwa na matarajio bora na chanya kwenye maisha yako ,
ikiwa ni pamoja na yale umepanga kuyatimiza kwenye maisha yako
kubali kuendelea kujiboresha kujikuza na kufanikisha yanayotakiwa
kuza imani yako ya kuyaona yakitimia usiache kufanya kile
unachokiweza kukifanya leo.
30
SURA YA NNE
1
MISONGO MDUDU ANAYEKULA UHAI WA WENGI.
M
isongo limekuwa tatizo kubwa sana kwenye ulimwengu wa sasa na
limetokea kuweka vikwazo kwenye mambo mengi katika safari ya
kujifahamu na kujitambua, kwa sababu unapokuwa katika hali hii
hata uwezo wako wa kufikiri na kufanya maamuzi sahihi hupungua, na kwa
kiwango kikubwa msongo umeharibu sana namna ya watu wanavyoishi na
eneo kubwa panapozalishwa misongo aina mbalimbali ni kutokana na
mahusiano, aina ya kazi wanzofanya watu, aina ya starehe wanazofanya watu
kama ulevi wa vinywaji vikali, namna wanavyofikiri na kuyapatia tafsiri
mambo mbalimbali na kwa kiwango cha juu sana msongo mkubwa sani ni
misongo ya kimawazo inayotokana na mahusiano ya kimapenzi na kifamilia,
na hali hii imetokeza ndoa na mahusino machungu na wengi wanaishi bila
kuwa na furaha, mambo mengi hayakamilishwi, tafiti nyingi zinaonyesha
namna ambavyo mahusiano mengi yamevunjika na kushindwa kudumu na
wengine wamejiua.
32
SURA YA NNE
2
AINA YA MISONGO NA NAMNA YA KUONDOKANA NAYO.
Kwa mfano wanawake kwa sasa kwa kiwango kikubwa na wanaume kwa wingi
wanakabiliwa na zimwi la kushindwa kuhimili usaliti wa kimapenzi ama
kukosa uaminifu wa wenzi wao hali inayopelekea kutokeza maamuzi mabaya
na yanayofanya watu kubaki midomo wazi kwa kile ambacho mtu ameamua
juu ya tukio kama hilo, haishangazi tena kuona mwanaume akipiga
mwanamke msaliti mpaka kumuua na yeye kuishia kujiua ama kufungwa jela
33
kwa miaka mingi na kufia jela hukohuko, ama haishangazi kuona mwanamke
akimwekea sumu mwanaume msaliti kwenye chakula na mwanaume huyo
kula na kufa, na mwanamke huyu kufungwa jela ama kuishi maisha ya hatia
akiwepo hapa duniani hali ni mbaya.
ii. Kuwa na mtazamo chanya kwa kila hali unayoipitia, fikra chanya ni
kuyaona mambo yaliyojitokeza kuna namna fulani yanasababu za
mambo hayo kutokea na kuwa halisia kuwa si mambo ambayo yanaweza
kudumu kwa muda wote na hata kama yametokea kuna namna bora na
nzuri zaidi ya kuyafanya yaishe na kuondoka kwenye maisha yako,
badala ya kubaki ukijilaumu wewe na kulalamika hali ambazo kwa
hakika huwa haziondoi matatizo badala ya kuyaongeza tu.
34
iv. Tumia muda wa kutosha kufanya tathimini kujua wapi umekosea na
nini ufanye kurekebisha ili kosa hilo lisije likajirudia na kukutosa tena
kwenye kuwa na msongo wa kimawazo, kwa mfano umepoteza fedha
zako nyingi na unapofanya tathimini unagundua kuwa haukuwa na
uhifadhi bora wa fedha hizo, kugundua hivyo kunakupatia nafasi ya
kubadili utunzaji wako na kuanza kutunza vizuri ili usije kupoteza tena.
vii. Heshimu hisia za wengine hata kama zipo kinyume nawe, kufanya hivi
kutakupunguzia mawazo mengi yasiyo na maana kwenye maisha yako
kutokana na kuishi na wengine, hakikisha unapendezwa na watu
wengine kwa jinsi walivyo, epuka kushauri bila kuombwa ushauri na
mtu husika, epuka kueleza matatizo yako kwa watu unaojua kabisa
hawana msaada juu ya matatizo hayo, epuka kuwakosoa watu,
kuwalalamikia, kuwalaumu na hata kuwahukumu bali sitawisha sifa
nzuri ya kuwasifia kwakua ndicho kitu unapenda wewe na wao
wanapenda pia.
35
ndoto kubwa na kuwa na mategemeo makubwa ya kimaisha, kuwa na
ndoto kubwa ni kule kuweka malengo na mipango , mikakati, tarehe ya
mwisho ya kuyatimiza hayo na kuanza kufanyia kazi mara moja bila
kukatishwa tama, lakini kuishi na mategemeo makubwa ni kujitwisha
jambo fulani kubwa kisha ukitegemea fulani atatimiza, na asipotimiza
ndiko kuanguka kihisia na kuwa na msongo wa kimawazo acha ishi kwa
malengo ambayo una uhakika nayo kuyatimiza.
ix. Kubali kwamba si wewe tu unayepitia hali mbaya kama hiyo, maisha
hayapo upande wako tu na ugumu hauko upande wako tu , pia kuna
wengine wanapitia hali mbaya na ngumu hata wakati mwingine kuzidi
hata wewe, nakumbuka simulizi la baba yangu alipokuwa akinisimulia
kuwa kuna siku alikuwa nyumbani kwake amekaa ametulizana akiwaza
namna maisha yanavyomwendea kombo, wakati yupo kwenye lindi la
kimawazo mara ghafula alipita mtu anayemfahamu fika na mtu huyu
kwa sasa amekuwa mtu wa makamo kama yeye lakini amechoka sana
mwenye mavazi chakavu, baba yangu katika kumwangalia vizuri
alimfahamu na kumuita jina lake …….fulani…..ndugu yule aliitika na
kuelekea upande alipo baba na wakaanza kusalimiana naye, na
kukumbushana kipindi cha nyuma waliko wahi kukutana
wakatambuana kuwa wote walisoma shule moja ya msingi huko
Buswelu, anasema baada ya kusalimiana pale yule ndugu aliaga na
kuondoka, baba akawaaambia wale waliokuwa karibu yake kuwa
mnayemuona yule bwana tumesoma naye na alikuwa na akili sana
darasani, watu wakashangaa kwa kusema yule haiwezekani bwana kwa
muonekano huo, baba anasema aliacha na kuwaza juu ya ugumu wake
kuwa eti na yeye maisha yanamwendea kombo akabaki na tumaini jema
kuwa kumbe mimi afadhari.
Hii pia inaweza kukujenga na wewe usione kabisa kuwa wewe ndiye
mwenye kupitia maisha magumu peke yako hesabu baraka zako na si
kushindwa kwako, jikusukume zaidi kutengeneza hali bora maisha bora
yanakusubiri ni wewe tu.
36
x. Jipe nafasi ya kufanya yale unayoyapenda sana, haya ni kutia ndani
unayopenda na ukiyafanya unapata furaha yaweza kuwa kusoma vitabu,
kulala, kufundisha , kufanya mazoezi, kufanya matembezi, kuchora,
kuimba, kusikiliza mziki, kucheka na wengine, kuongea na wengine kwa
aina ya kufurahishana na kuelemishana, kuwasiliana na mtu
unayempenda sana na n.k
xi. Fanya kazi kwa bidii, katika kazi ndiko Mungu ndiyo alikokuwa
anakutana na Adamu kwa mjibu wa simulizi la vitabu vitakatifu, na
wewe kupitia kufanya kazi kutakupunguzia kwa kiasi kikubwa sana
kuwa na mawazo hasi ambayo mengi hukuchochea kuwa na msongo wa
kimawazo, jikite kutafuta majibu ya matatizo mbalimbali na huko ndiko
kiwango kikubwa cha msongo wa kimawazo utapotea.
xiii. Kula vyakula bora, kula vyakula bora huupatia mwili wako uwezo wa juu
wa kutatua mengi ya matatizo yanayotokana na namna ya kufikiri na
utajipatia nguvu nyingi za kushinda misongo mingi ya kimawazo.
xiv. Kama unahisia fulani kuhusu, mtu fulani mwambie acha kubaki na hisia
hizo na mwisho kujipa msongo usioa na maana, kama kuna mtu
unampenda sana mwambie nakupenda, hakuna kosa kumwambia mtu
hisia zako, na kwa kufanya hivyo ni kwa kujiponya kwa haraka na
kushinda msongo wa kimawazo.
xv. Fanya yale umesema unataka kufanya, wengi wakuwa wasemaji wazuri
tu na mwisho hawafanyi kinachotakiwa kufanywa na mwisho
wamejikuta wakiwa kwenye msongo wa kimawazo juu ya yale walitaka
kuyafanya kwenye maisha yao, kama umesema nataka kufungua
37
biashara weka mipango na namna ya kukuwezesha kuanzisha biashara
itakupatia wakati mzuri wa kuondokana na msongo wa kimawazo.
38
SURA YA NNE
3
NJIA SALAMA ZA KUKUONDOLEA MISONGO
e) Wacha kutaka kufanya mambo yote kwa wakati mmoja bali jifunze
kujipatia ratiba ya mambo mbalimbali na acha kufanya jambo
ambalo halipo kwenye ratiba yako.
39
SURA YA TANO.
1
MAISHA YA MAFANIKIO NA FURAHA.
M
aana halisi ya kufanikiwa yaweza kuwa kwa njia rahisi tu nayo ni
kupata kile unachotaka iwe kwenye mtazamo chanya ama hasi kama
umepata kile ulichokuwa unataka unakuwa kwenye fanikio fulani la
jambo unalolitaka na hapo hapo utakuwa na nafasi ya kuwa mwenye furaha
kwakua umetimiza jambo ulilokuwa unalitaka.
40
matokeo ya kuishi maisha yasiyo kuwa na furaha, twawajibika kuwa na furaha
na wakati huohuo tukiwa wenye mafanikio.
a) Kukosa vipaumbele.
Huku ni kule kuwa mtu mwenye kufanya kila kinachokuja mbele yako na kwa
kufanya hivyo unakosa umakini kwenye mambo muhimu yanayopaswa
kufanyika kwa umakini, ana kupoteza rasilimali muhimu za kufanyia mambo
muhimu ambayo yangekupatia mafanikio ya haraka, kitendo cha kuwa na
vipaumbele hutia ndani kuwa na nidhamu ya kufanya jambo linalopaswa bila
kuachana nalo na kufanya mengine kisa unafuata ushabiki wa watu wengine
na hisia, mambo yanayokukosesha uwezo wako wa kuyapata mafanikio
unayoyataka.
Mafanikio ya kutafutwa kwa njia fupi huleta madhara mengi kwenye maisha
na hakuna jambo ambalo linaweza kudumu kwa muda mrefu kama
limepatikana kwa njia ya haraka na isiyoeleweka, kwa mfan0 leo ni rahisi
kuwakuta vijana wa makamu na watu wazima wakitafuta mafanikio ya kifedha
kwa kubeti ama kucheza michezo ya kubahatisha, hukuna mafanikio ya
namna hiyo ambapo unaweza kusema umeyapata na kuwa utatudumu nayo,
41
maisha yanataka kujitoa, kufanya kwa viwango vya juu na uwe mtu mwenye
kuwajibika sana.
c) Kukosa kujiamini.
e) Kuendeshwa na uoga.
Uoga imekuwa sumu namba moja inayoua vipaji vya wengi na kuwafanya
watu kuishi maisha ya kawaida kisa tu wameendekeza uoga wa aina yoyote na
kuwafanya washindwe kuamua kutaka kufanya makubwa kwenye maisha na
moja ya uoga mbaya wanaokutana nao watu wengi ni pamoja na uoga wa
kushindwa, uoga wa kujiandaa, uoga wa kutokujua na hawataki kujifunza
anabaki kusema sijui, uoga wa kushindwa, uoga wa kukosolewa, uoga wa
kukataliwa, uoga wa mafanikio, na uoga wa kufanya maamuzi na mwisho
kuishia kufanya maamuzi mabaya kwa kuendeshwa na hisia zaidi ama
ushabiki, n.k
42
na kujaribu huko na kushindwa kwingi ndiyo kunakupatia nafasi kubwa ya
kufanikiwa.
Kila mtu ana aina yake ya uwezo wa kipekee ambao kutokana na uwezo huo
anaweza kujipatia mafanikio kutokana nao, sasa wengi hatutumii vipaji vyetu
na uwezo huu na mwisho tunakufa tukiwa hatujatumia chochote katika
kuifanya dunia kuwa mahali pazuri pa kuishi, kwa asili binadamu waliotumia
uwezo wa juu wa uwezo wao walionao wametumia kwa asilimia 10% mpaka
12% tu na wamefanya makubwa lakini je kama wangeamua kutumia asiliamia
40%? anatufahamisha ndugu Willium James, amua kwa kutumia njia
zilizoanishwa kugundua vipaji vyako na uvitumi kwa juhudi katika kukusaidia
kufanikiwa.
Kujiuliza ama kuuliza maswali sahihi imekuwa njia mama ya watu kujifunza
wasioyajua, na njia hiyo imewaokoa katika kufahamu mengi kuliko wale wasio
uliza maswali wameishia kuwa na ufahamu ule ule walio nao, katika
kuendeleza jambo hili zuri la kuuliza maswali basi tunawajibika pia kujiuliza
maswali sahihi na kuyapatia majibu sahihi mfano wa maswali hayo ni pamoja
na:-
43
LAZIMA , roho ya kimafanikio kwa mujibu wa aliyekuwa
mwenyekiti wa makampuni ya IPP, marehemu Reginald Mengi?
9. Je wajua kwa hakika mzizi wa matatizo yako ama yenu?
10.Je utaachana na ubinafsi na uroho kuyatafuta mafanikio?
44
SURA YA TANO.
2
VIAMBATA VYA MAFANIKIO.
B
aada ya kuona sababu zinazowasababisha wengi kushindwa
kupayapata mafanikio ni muhimu sasa kuona viambata muhimu vya
mtu anayetaka kufanikiwa na kuishi maisha ya furaha.
1. Ona picha kubwa akilini mwako kuhusu maisha yako, ona ukifanikiwa,
ona ukiwa mtu mwenye mafanikio makubwa.
5. Mara zote kuza uwezo wako wa kufikiri na jifunze kufikiri kwa urefu na
kwa ubunifu juu ya kila changamoto.
6. Usingalie kutokuwa na kitu, ona na ishi kwenye dunia yenye kila kitu na
kazi yako ni kwenda kuchukua ama kutafuta na kupata.
45
magumu na ya tabu inaweza kukupati funzo gani kwako juu yao?
ukipata funzo hilo fanyia kazi.
46
~MWISHO~
Ukiwa umesoma sura za kitabu hiki cha “najifahamu furaha ya kuwa
mimi” weka kwenye vitendo angalau hata kwa jambo moja
kubwa ambalo unataka kuriboresha kwenye maisha yako, kila
unapoanguka endelea kujihamasisha kuwa unaweza na
utafanikiwa na mwisho utaondoka duniani ukiwa mtupu na
mwenye furaha kuu na kutokeza kumbukumbu la kukumbukwa
na kila mmoja na hata kusimuliwa kila vizazi ukiwa unaishi hali
ya kuwa mwili wako ukiwa kaburini.
47