You are on page 1of 138

SANAA YA UTONGOZAJI 01

Namna ya Kuwa Mwanaume Mwenye


Mvuto na Ushawishi kwa Mwanamke.

Isaack Nsumba
Hakimiliki
Haki zote zimehifadhiwa. Huruhusiwi kunakili,
kudurufu au kutumia sehemu ya kitabu hiki bila idhini
ya mwandishi. Kufanya hivyo itakuwa ni ukiukwaji wa
haki za mwandishi, na ukiukwaji wa taratibu hii
unaweza kupelekea mashitaka toka kwa waandaaji wa
kazi hii.

Isaack Nsumba
Dar-Es-Salaam, Tanzania. East Africa
Simu: +255 654 722 733
Barua pepe: isaacknsumba@gmail.com
Tovuti: www.isaacknsumba.com
YALIYOMO
Utangulizi 3

Sura ya Kwanza: Maana ya


Kutongoza na Aina za Utongozaj 14

Sura ya Pili: Ijue Saikolojia ya


Mwanamke Wakati Anataka
Mwanaume wa Kuwa Nae 25

Sura ya Tatu: Ijue Kanuni ya


Utongozaji Inayofanya Kazi Zaidi 40

Sura ya Nne: Mbinu za Kumtongoza


Mwanamke Aliye Katika Mahusiano 41

Sura ya Tano: Makosa ya Kuepuka


Wakati Unamtongoza Mwanamke 41

1
Sura Ya Sita: Sababu Zinazopelekea
Hali ya Mwanaume Kukataliwa Mara
kwa Mara 41

Hitimisho 41

Kuhusu Mwandishi 41

2
Utangulizi
Mwaka 1987 Bwana Byron Sengalt
Alifanya Utafiti Uliolenga Kubaini
Sababu Za Wanaume Wengi
Kukataliwa Na Wanawake Na
Wengine Kuwa Na Hofu Kiasi Cha
Kushindwa Kutongoza.

Baada Ya Utafiti Wake Kukamilika


Majibu Ya Utafiti Wake Yalikuwa
Kama Ifuatavyo.

1. Asilimia 85% Ya Wanaume Kuna


Makosa Huwa Wanafanya Wakati Wa
Kumtongoza Mwanamke
Yanayowapelekea Kukataliwa.

3
2. Wanawake Hawawakatai Wanaume
Kwa Sababu Hawawataki, Ila
Wanawakataa Kwa Sababu Ya Bad
Approach Ya Wanaume Wanayoingia
Nayo.

3. Wanaume Wengi Hawajui Mambo


Sahihi Ya Kufanya Wakati Wa
Kumtongoza Mwanamke Na Kwa
Sababu Hawafanyi Mambo Hayo
Wengi Wanaishia Kukataliwa.

4. Kuna Saikolojia ya Mwanamke


Ambayo Kila Mwanaume Anapaswa
Kuijua Kabla Hajamtongoza
Mwanamke Ili Asikatalie Na Ndio

4
Wanaume Wanaoijua Saikolojia Hiyo
Wanapata Wanawake Kirahisi Zaidi Ya
Wanaume Wengine.....

We Mwenywe Ni Shahidi Kuna


Wenzako Hawasumbuki Hata
Wanapotaka Kumpata Mwanamke
mpaka inafika wakati unahisi labda
wanatumia dawa/kimzizi.

Hata Hivyo, Baada Ya Utafiti Wake


Aligundua Kuwa, Njia Rahisi Kabisa Ya
Mwanaume Kuondokana Na Hofu Ya
Kutongoza Na Kujijengea Uwezo Wa
Kumpata Mwanamke Yeyote Yule
Ni....

Kujua Mambo Sahihi Ya Kufanya Ili


Kumshawishi Mwanamke.

5
Na Ndio Maana kupitia kitabu hiki
Nataka Ujifunze Mambo Hayo Ili
Ukawe Mwanaume Mwenye Uwezo
Wa Kumuingia Mwanamke Yeyote
Utakaemtaka.

Je, Upo Tayari Kujifunza Mambo


Hayo?

Kama umejibu NDIO basi KARIBU


SANA, hakikisha unakisoma kitabu
hiki choote mpaka unakimaliza.

Sanaa ya Utongozaji ni moja kati ya


vitabu vyangu vilivyofanya vizuri
sana, kwani vimesaidia maelfu ya
watu waliopata kuvisoma.

6
Hiki ni namba 01, kama hujasoma
Sanaa ya Utongozaji 02 hakikisha
unakisoma ili kikusaidie.

Hii ni kwa sababu ili uweze kujenga


uwezo wa uhakika ni lazima uwe na
mkusanyiko wa maarifa kutoka katika
vitabu vyoote viwili, yaani Sanaa ya
Utongozaji 01 na Sanaa ya
Utongozaji 02.

Kupitia vitabu vyoote viwili utapata


mafundisho katika ukamilifu wake
unayoweza kuyatumia kama silaha
unapotaka kumtongoza mwanamke
yeyote na ukafanikiwa.

Mbinu utakazojifunza katika vitabu


hivi (1&2) zitumie kwa umakini sana

7
kwa sababu zina nguvu kiasi cha
kukufanya uwe Playboy.

Hivyo unapaswa kuwa nazo makini


zisije zikakuletea madhara, kwani
baada ya kuzitumia utagundua kuwa
utakuwa ni mwanaume mwenye
MVUTO na USHAWISHI kwa
wanawake tofauti ulivyokuwa
mwanzo.

Mwanasaikolojia nguli Bwana Lev


Vygotsky alifanya utafiti ili kubaini
aina 70 za hofu zinazowakumba
wanadamu.

Katika utafiti wake alikuja kubaini


kuwa asilimia 80% ya wanaume wana
hofu ya kuzungumza na wanawake
ambayo kitaalamu inafahamika kama

8
Gynophobia na mashaka wakati wa
kutongoza (Seduction Anxiety)

Hii ni sawa na kusema kwamba


wanaume 8 kati ya wanaume 10
(8/10) hawana ujasiri kabisa wa
kuzungumza na wanawake na wana
hofu ya kufanya hivyo.

Alipokuwa akiendelea kufanya utafiti


ili kubaini chanzo cha wanaume kuwa
na hofu hiyo alikuja kupata majibu ya
kushangaza sana ambayo hata wewe
leo yanaweza kukushangaza pia.

Katika utafiti wake alibaini kuwa


wanaume wengi wana hofu na
mashaka ya kutongoza wanawake sio
kwa sababu hawana uwezo wa
kufanya hivyo ila ni kwa sababu

9
hawaijui saikolojia ya mwanamke na
SANAA YA UTONGOZAJI
itakayomsaidia mwanaume kuwa na
ujasiri wa kuzungumza nao.

Kisaikolojia imethibitika kuwa


wanawake ni viumbe wanaopenda
kusikilizwa na kusikiliza hata kama
wao wanaongea au wanaongeleshwa
vitu visivyo na maana yoyote, pamoja
na wanaume wengi kuujua huu ukweli
kuwa haihitaji mambo mazito ili
waweze kuongea na mwanamke
bado idadi ya wanaume wenye uwezo
wa kufanya hivyo imekuwa ndogo
sana.

Tafiti zilizofanywa hivi karibuni


zimebaini kuwa kadri siku zinavyozidi
kwenda ndivyo hofu hii huzidi

10
kuwakumba wanaume wengi na ndio
maana wengi hupendelea kuomba
namba ya simu na sio kuwasilisha
uhitaji wao kupitia mdomo.

Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa


hata baada ya wanaume kupewa
namba bado hofu ya kuwasiliana na
mwanamke huwa palepale kwa
kutokujua namna sahihi ya kuelezea
hisia zao na kuonesha uhitaji.

Hii inatokana na kutokujua au


kutokuwa na cha kuongea na
mwanamke (lack of story and
stucking routine)

Yawezekana hata wewe umewahi


kutamani kukutana na mwanamke
mzungumze ila alipokubali wito wako

11
na mlipokutana maneno ambayo
ulipanga kumwambia yalitoweka na
ujasiri ukapotea kabisa mbele yake.

Au uliomba namba ya simu na mara


baada ya kupewa ulijikuta hauna cha
kumwambia ili kumfanya ajue,
ashawishike na kukukubalia uhitaji
wako.

Kuwasilisha uhitaji wako kwa


mwanamke ni jambo linalohitaji
ufahamu mkubwa kwa sababu lengo
lako ni kugusa hisia zake na
kumfanya akuone wewe unamfaa,
ufahamu huo nimeuita “SANAA YA
UTONGOZAJI”

Lengo la kitabu hiki sio kukufanya


uwe mwanaume wa kila mwanamke,

12
ila kimedhamiria kukujaza ufahamu
utakaokusaidia kutimiza lengo la
kuwasilisha hisia zako kwa
mwanamke na kumvutia mwanamke
unaemtaka.

Kama ukishindwa kufanya hivyo ni


rahisi sana kuingia katika mahusiano
na mwanamke usiyemtaka kwa
sababu tu ulishindwa kumpata yule
umtakae kwa kutokujua namna ya
kuelezea hisia zako kwake.

Kupitia kitabu hiki utajifunza


Saaikolojia ya mwanamke ambayo
kupitia hiyo utaweza kuwa na
ufahamu wa namna gani ya kuwavutia
wanawake na kuwa mwanaume
mwenye ushawishi mbele yao.

13
Sura Ya Kwanza

Maana ya Kutongoza na Aina za


Utongozaji

Kutongoza kunaweza kukawa na


maana na tafsiri nyingi, mwisho
maana na tafsiri hizo lazima zikutane
mahali pamoja na kukubaliana kuwa;
Kutongoza ni kitendo cha kuwasilisha
hisia za uhitaji wa kuanzisha
mahusiano na mtu wa jinsia ya tofauti
na yako ili kumfanya ashawishike
kuwa nawewe.

Yaani Ila kutongoza ni zoezi


linalohisha kumfanya mwanamke
akujue, akupende, akuhitaji, akuamini
na akuone wewe ndo yule

14
mwanaume ambae amekuwa
akitamani siku zoote kuwa nae.

Lengo la uwasilishaji wa hisia hizo za


uhitaji ni kumshawishi unaemtaka na
kumfanya aone kuwa wewe unafaa
kuwa nae na kutokea hapo awe tayari
kuwa nawewe.

Kutongoza ni zaidi ya kumwambia


mwanamke kuwa Nakupenda,
nakuhitaji na nataka nikuoe tujenge
familia

Kutongoza ni Sanaa na Sanaa ni


ufundi wa kufanya jambo fulani katika
namna ya uzuri na mvuto kiasi cha
kumvutia mtu mwingine.

15
Wapo wanaume wengi ambao
wamekosa wanawake sio kwa sababu
wanawake hao hawakuwa sahihi ila
kwa sababu walikosa au kupungukiwa
uwezo wa kushawishi.

Ili kumfanya mwanamke akubali


kuingia katika mahusiano nawewe
anahitaji kupata sababu ya kwanini
afanye hivyo na sababu hiyo
anatakiwa aipate kutoka katika
ushawishi wako.

Kama usipokuwa na uwezo wa


kumshawishi mwanamke kuna hatari
ya kukosa mwanamke unaemtaka na
kuangukia katika mikono ya
mwanamke ambae humtaki ila kwa
sababu amekuja mwenyewe au
umetafutiwa, kuna msemo unasema

16
kuwa usipokuwa na ufahamu wa
namna ya kula unachokitaka basi
utakuwa kati ya watu ambao
wanakula wanachokipata hata kama
hawakitaki

Mtu anaejua namna ya kukipata kile


anachokitaka yupo katika nafasi nzuri
ya kukipata, mtu asiyejua namna ya
kukipata anachokitaka ni vigumu sana
kukipata hata kama alistahiri kukipata.

Kuna mwanamke fulani ni haki yako


kabisa kuwa nae ila kwa sababu
umekosa uwezo wa kumshawishi basi
ni vigumu sana kumpata.

Hii ni kwa sababu hata kama


anakupenda bado atahitaji ushawishi
wako, kwa kufanya hivyo ndivyo

17
hujisikia raha na kuona umemtendea
haki.

Kutongoza kumegawanyika katika


aina mbili, ya kwanza ni WORDILY/
VERBAL SEDUCTION ambapo
inakutaka mwanaume kumueleza
mwanamke kwa maneno juu ya hisia
na uhitaji ulionao wa kuingia katika
mahusiano nae.

Katika aina hii ya utongozaji, kilicho


na umuhimu ni ujasiri wa kuongea na
uwezo wa kuyapangilia maneno ili
kuwasilisha ujumbe wako kwa
mwanamke unaemtaka na wenye
uwezo mzuri wa kufanya hivyo huwa
wanafanikiwa.

18
Aina hii ya utongozaji huweza
kufanyika ana kwa ana au kupitia
simu kwa njia ya meseji au maongezi.

Basi Dina, binti Lea, ambaye Lea alimzalia Yakobo, akatoka


kuwaona binti za nchi. 2 Shekemu, mwana wa Hamori, Mhivi,
mkuu wa nchi, akamwona akamtwaa, akalala naye,
akambikiri. 3 Moyo wake ukaambatana na Dina binti Yakobo,
akampenda huyu msichana, akasema na huyu msichana kwa
maneno mazuri. Mwanzo 34:1-2

Huo ni mfano wa mwanaume


aliyemtongoza mwanamke kupitia
maneno na kufanikisha lengo,
msisitizo haupo kwenye kuzungumza
nae, bali msisitizo upo kwenye
kuzungumza nae kwa maneno
mazuri.

Kisaikolojia wanawake wameumbwa


na shauku ya kusikia maneno mazuri
kutoka kwa wanaume.

19
Hii ndio sababu kwanini mwanamke
anaweza akajikuta ameshawishika
kuwa na mwanaume fulani na asijue
ameingiaje katika mahusiano nae kwa
sababu alipagawa na maneno
aliyokuwa akiambiwa.

Hata baada ya kuanzisha mahusiano,


suala la mawasiliano kwa mwanamke
huwa linapewa kipaumbele zaidi ya
mwanaume, hii ni kwa sababu ya ile
njaa ya kusikia maneno kutoka kwa
mwanaume.

Kwahiyo, ikiwa utatumia njia hii


kumnasa mwanamke unashauriwa
kujua mambo ambayo wanawake
hupendelea zaidi kuyasikia kuwahusu,
mambo hayo ni pamoja na vile
unavyomtazama kipekee, munekano

20
wake jinsi unavyovutia pamoja na vile
unavyotambua thamani ya uwepo
wake katika maisha yako.

Aina ya pili ya utongozaji inaitwa


NON-VERBAL/WORDILY
SEDUCTION, katika aina hii ya
utongozaji mwanaume hulazimika
kuwasilisha uhitaji wake kupitia
vitendo vya wazi (communicating
through acts of services)

Aina hii ya utongozaji imeambatana


na gharama ya muda, fedha pamoja
na utayari, hii ndio aina ambayo
nashauri watu wengi waitumie kwa
sababu imethibitishwa na
wanasaikolojia kuwa hakuna kitu
kinapeleka ujumbe kwa haraka katika

21
ubongo wa mwanadamu kama
matendo anayotendewa.

Hautakiwi kumwambia mtu vile


unamjali na kumthamini anaweza
kuyaona hayo kupitia matendo yako.

Kupitia matendo yako ndipo


mwanamke huweza kujua namna
unavyomjali na kumthamini na ndio
maana ni rahisi sana mwanaume
kumteka mwanamke ambae
ameolewa ikiwa atafanikiwa
kumfanyia yale ambayo hafanyiwi na
mume wake.

Kilicho na umuhimu katika hii aina ya


pili ni kujua matendo ambayo
ukimfanyia mwanamke unaemtaka
yataachilia mguso affection ndani

22
yake na kumfanya akuhitaji au aone
kuwa wewe unamfaa kwa sababu
unajua kugusa hisia zake.

Kumbuka, kutongoza ni zoezi


linalolenga kushawishi, ili uweze
kumshawishi ni lazima uguse katika
vitu anavyovipenda bila yeye
kukwambia.

Hii itakuongezea nafasi credit ndani


ya moyo wake na kumfanya ajue
kuwa unazijua hisia zake vizuri na
unajali mahitaji yake, kwahiyo lengo
sio tu kufanya, bali ni kufanya kilicho
muhimu, katika ubora na kwa wakati
kinapohitajika.

Lakini pia, katika aina hii ya pili


unaweza usimfanyie mambo

23
yatakayomuonesha kwamba wewe
UNAMUHITAJI yeye ila ukafanya
mambo yatakayomfanye YEYE
kukuhitaji WEWE.

Utajifunza hili katika sura zinazofuatia


kwa sehemu, japo nimeweka kwa
mapana zaidi katika Sanaa ya
Utongozaji 02.

Aina hii ya utongozaji ndio yenye


nguvu zaidi kwa sababu yeye ataanza
kushawishika nawewe kabla wewe
hujatamka neno.

24
Sura Ya Pili
Ijue Saikolojia ya Mwanamke Wakati
Anataka Mwanaume wa Kuwa Nae

Miaka ya 70 jopo la wanasayansi


kutoka nchini China na Japan
wakiongozwa na Masao Doi, Takuzo
Aida, Yuen Ren Chao pamoja na Pan
Jianwei walifanya utafiti kwa samaki
wa kike anaeitwa GOLDFISH ili
kubaini ni kitu gani ambacho samaki
huyo anaangalia anapotafuta Goldfish
wa kiume ili waweze kujaamiana.

Katika utafiti wao waliweza kubaini


kuwa Goldfish wa kike anapotafuta
Goldfish wa kiume huangalia Goldfish
mwenye wanawake wengi au

25
aliyezungukwa na wanawake wengi
zaidi kuliko wengine.

Baada ya kugundua hilo ndipo


walipokuja na matokeo ya utafiti wao
ambao waliwasilisha kwa jina la
“TRIANGLE OF HUMAN DEMANDS”
ambapo walielezea aina tatu ya vitu
ambavyo binadamu anavihitaji zaidi.

Kitu cha kwanza: kile ambacho


hawezi kukipata au ambacho
hakipatikani kirahisi.

Binadamu wengi wanapenda vitu


visivyopatikana kirahisi, hii ni kwa
sababu binadamu asipopata
changamoto katika kupata kitu
kiwango chake cha furaha baada ya
kukipata kitu hicho huwa kidogo sana

26
na kuna uwezekano asikipe thamani
inayostahili.

Kwa wanawake hii ipo, wanawake


wengi hawapendi wanaume ambao
wanapatikana kirahisi na ndio maana
mara nyingi mwanamke akijua
unampenda SANAA aanza
kukudharau na kukuchukulia poa.

Kama utakuwa mfuatiliaji utakuja


kugundua kuwa mtaani kwenu, kazini
au chuoni wanaume
wanaoonekanaga kuwa bize na
mambo yao huwa na nafasi kubwa ya
kupata wanawake tofauti na wale
ambao huwa karibu zaidi na
wanawake.

27
Hii ni kwa sababu wanawake
hawapendi au kuvutiwa na wanaume
ambao wanapatikana kirahisi.

Kitu cha pili: kile ambacho wengine


wanakihitaji au kinahitajika zaidi
Most Wanted

Wanawake hawapendi wanaume


ambao hawahitajiki, hii ndio sababu
kwanini wanaume maarufu
wanapendwa sana na wanawake
pamoja na ukweli kwamba wanawake
hao wanajua kuwa hawawezi kuwa
peke yao hata wakipewa nafasi.

Kutokana na utafiti wao walibaini


kuwa asilimia 98.9% ya wanawake
wanavutiwa zaidi na THE MOST
WANTED MEN (wanaume

28
wanaopendwa na wanawake wengi
zaidi ya wanaume wengine)

Mwanamke anajisikia fahari zaidi


akijua kuwa yupo katika mahusiano
na mwanaume ambae anahitajika na
wanawake wengine na ndio maana
mwanaume mwenye wanawake
wengi ni rahisi zaidi kupata
wanawake wengine KIRAHISI kuliko
yule asiye na mwanamke kabisa.

We mwenyewe ni shahidi, umewahi


kuona mwanamke anatongozwa na
mwanaume aliye single anamkatalia
ila akitongozwa na kijana aliye katika
mahusiano na mwanamke mwingine
anakubali.

29
Au, kuna uwezekano wa kijana wa
kiume kuwa na sifa ya kuwa na
wanawake wengi, lakini cha ajabu
pamoja na kuwa na sifa hiyo bado
akiwatongoza wanawake wengine
hawamkatai licha ya ukweli kwamba
wanafahamu kuwa ana wanawake
wengi.

Ili kuthibitisha hili fuatilia wanawake


wengi utakuja kugundua kuwa wapo
tayari wakubali kuwa na mwanaume
ambae ameoa ila sio mwanaume
ambae hana mwanamke.

Hiyo ni kwa sababu ya kitu kinaitwa


DRIVE TO CURIOSITY (kuendeshwa
na udadisi) wanawake wengi
wanajiulizaga kwamba Kwanini huyu
apendwe na wanawake wengi?

30
Jibu linalokuja katika fikra zao ni
kwamba, lazima atakuwa na kitu cha
tofauti ndio maana wanawake
wengine wanavutiwa nae.

Kisaikolojia ipo hivi, kitu


kinachopendwa na wengi huwa
kinaaminika na kuonekana ni kizuri, ni
bora na kinafaa, kwahiyo, mwanamke
anaamini kwamba, mwanaume
anaependwa na wanawake wengi au
yule ambae ana wanawake wengi
ndiye mwanaume anaefaa zaidi.

Mwanamke anapotafuta mwanaume


wa kuwa nae, anatafuta yule ambae
wanawake wengine wanaweza
kumtaka au tayari wameshamtaka, na
hii ndio sababu kwanini ni rahisi

31
mwanaume kumpata rafiki wa
mwanamke wake.

Kwa mujibu wa Asch experiment


iliyofanywa na mwanasaikolojia nguli
Solomon Asch mwaka 1951, katika
utafiti wake aligundua kuwa watu
huamini kupitia watu wengine, kile
kinachoonekana kupendwa na wengi
huwa kinaaminika kwamba ni kizuri,
hii inaitwa informative influence.

Kwa upande mwingine informative


influence ni sawa na kusema kwamba
kuna vitu wala sio vizuri, ila
vinaonekana vizuri kwa watu ikiwa
kuna watu wengine wanavipenda vitu
hivyo na kuviona vizuri

32
Lakini pia tunaweza kusema kwamba,
kuna vitu ni vizuri na ni bora, ila
havionekani kama ni vizuri kwa
sababu bado havijaonekana
vikitumiwa na watu wengine.

Kwahiyo weka akilini mwako kuwa


unatakiwa kumuonesha mwanamke
kwamba kama atakupata wewe basi
amebahatika sana kwa sababu idadi
ya wanawake wengine wanaokuhitaji
wewe ni kubwa sana.

Kitu cha tatu: kile ambacho


wachache tu ndio wana access
nacho.

Moja ya jambo muhimu unalotakiwa


kulijua kuhusu wanawake ni kwamba
Wanawake wanahitaji wanaume

33
ambao sio kila mwanamke anaweza
kuwapata japo wanahitajika zaidi
(Most of women feel attracted to men

be cheaply available)

Hii ndio sababu kwanini mwanamke


anaweza kuvutiwa kirahisi na
mwanaume ambae anajua kuwa
atakuwa pekeake, lakini pia
wanawake wenzake watakuwa
wanamuonea wivu kwa sababu ya
nguvu ya ushindani, Nguvu na uhitaji
na wivu (Power of competition,
Demand and Jealousy)

Mwisho kabisa utafiti wa


wanasayansi hao ulihitimisha kwa
kusema kuwa Mwanamke anahitaji
mwanaume ambae Hawezi kumpata,

34
anayehitajika na wanawake wengi
zaidi pamoja na mwanaume ambae
hapatikani kirahisi.

Hii ni kusema kwamba mwanamke


akikupa namba ya simu saivi na
ukamtafuta muda huohuo kwa
sehemu fulani unakuwa umekosa
kigezo cha kuwa nae.

Hii ina maana kwamba ukimuonesha


mwanamke kuwa hakuna mwanamke
mwingine anaekutaka basi tayari
umekosa nguvu ya kumpata, hii ni
kusema kwamba mwanamke akijua
kuwa hakuna mwingine anaekuhitaji
basi umeshamkosa, Unajua ni
kwanini? Hii ni kwa sababu zifuatazo;

35
1. Wanawake wengi huamini kuwa
mwanaume mzuri ni yule ambae
wanawake wengi wanamtaka,
yawezekana asiwe mzuri mbele ya
macho ya mwanamke huyo, ila kwa
sababu tu wanawake wanaomtaka ni
wengi basi kuanzia hapo nayeye
ataanza kumuona mzuri.

2. Watu wengi huamini kuwa kitu


kinachohitajika zaidi ni kizuri na kina
thamani kubwa, hii ipo hata kwa
wanawake wakati wanaangalia
mwanaume wa kuwa nae, wengi
huangalia idadi ya wanawake
wanaomuhitaji mwanaume huyo na
ndio maana mwanamke yupo tayari
kumuacha mwanaume ambae kwake
yupo pekeake na kwenda kwa

36
mwanaume ambae atakuwa na
mwanamke mwenzake.

3. Wanawake wengi wanaendeshwa


na udadisi (Driven with curiosity)
mwanaume akiwa anasifiwa au
anaonekana kuwavutia wanawake
wengine wanawake huanza kujiuliza
ana kitu gani cha tofauti na wanaume
wengine?

Swali hili linaibua msukumo wa kutaka


kuwa karibu na mwanaume huyo na
kuanzia hapo huanza kujenga
matamanio ya kuwa nae.

4. Moja ya kitu ambacho wanawake


wengi wanakitafuta ndani ya
mwanaume ni uhakika Assuarance
na uhakika huu hakuna namna

37
wanaweza kuupata isipokuwa kwa
kuwaangalia wanawake
wanaomzunguka mwanaume huyo.

Hii tafsiri yake ni kwamba mwanamke


anapomtazama mwanaume mwenye
mwanamke anapata kufahamu kuwa
mwanaume huyu ana uwezo wa
kumridhisha mwanamke, kumhandle
na kumtunza na ndio maana
akapendwa, anapata kujua kuwa
mwanaume huyu ni mwanaume
anaefaa na ndio maana kuna
mwanamke alimkubalia.

Kwahiyo mwanaume unapomtongoza


mwanamke epuka sana kumuonesha
kuwa upo single, hiyo itamfanya
ajiulize maswali mengi kama huyu

38
mwanaume ana kasoro gani mpaka
anakuwa single?

Muhimu; Hakikisha unakisoma kitabu


hiki mpaka mwisho ili uweze kujifunza
makosa ambayo wanaume wengi
wanafanya, na ukijifunza hakikisha
wewe unayaepuka kadri uwezavyo, ili
yasikufelishe kama yalivyowafelisha
wengine.

39
Sura Ya Tatu

Ijue Kanuni ya Utongozaji Inayofanya


Kazi Zaidi

Dan Bilzerian ni miongoni mwa


wanaume maarufu sana duniani, na
umaarufu huo amejipatia kutokana na
uwezo wake mkubwa wa kunasa
wanawake wazuri zaidi duniani, kwa
sasa anajulikana kama Playboy wa
Dunia.

Lengo la sura hii sio kukufanya uwe


playboy ila kuna kitu kizuri cha
kujifunza kutoka kwa Dan ambacho
kimeandikwa pia katika kitabu cha
Dominick Mann kinachoitwa UNLOCK
HER LEGS (Namna ya kumvutia

40
mwanamke bila kutumia nguvu wala
gharama kubwa) na kitu hicho ni
kanuni ambayo mimi nimeipa jina la
“DON’T CHASE, JUST ATTRACT”
(Usifukuzie, Vutia)

Kanuni hii inasema kwamba, kadri


unavyojitahidi kumfuatilia mwanamke
na kumuonesha kuwa unamuhitaji
sana ndivyo unavyozidi kumfanya
apoteze hamasa ya kuwa nawewe na
aanze kukupuuzia (loose interests
and start ignoring you)

We mwenyewe ni shahidi katika hili,


mwanamke ambae umekuwa
ukijitahidi kadri uwezavyo
kumuonesha jinsi unavyomuhitaji na
kumthamini ndiye anaekuumiza na

41
kukupuuzia kana kwamba haoni
juhudi na jitihada zako kwake.

Hii ni kwa sababu wanawake


hawataki wanaume cheap wanahitaji
wanaume ambao wanahitajika zaidi
na hawapatikani kirahisi kama
tulivyoangalia katika sura ya pili.

Kwahiyo kwa mujibu wa kanuni hii


kuna mambo kadhaa ambayo
mwanaume anatakiwa aepuke wakati
anamtongoza mwanamke.

Jambo la kwanza: epuka


kumuonesha kuwa unamuhitaji zaidi

Hii kanuni inasema kwamba kadri


unavyomuonesha kuwa unamuhitaji
ndivyo ambavyo thamani yako kwake

42
inashuka na ukumbuke thamani yako
ikishuka unapoteza mvuto na
ukipoteza mvuto unakosa ushawishi
ndio maana unaweza kujitahidi
kumuonesha kuwa unampenda na
wala asijali kabisa juhudi zako.

Siri ya kuwa na nguvu na mvuto kwa


mwanamke ni kumuonesha kuwa
haumuhitaji kama ambavyo anadhani
na unaweza kufanikiwa katika hili kwa
kumuonesha au kumuaminisha kuwa
una machaguo mengi zaidi (you have
more options) na sio yeye pekeake.

Hii itamfanya ajue kuwa kama


asipokupa nafasi na kukuwahi wewe
basi wengine watamuwahi kwa
kukupa nafasi. (The secret of having

43
power over women is not to show
that you need them)

Akifika hiyo hatua ndani yake


inazaliwa hofu ya kupoteza au kukosa
nafasi ambayo inafahamika kama
F.O.M.O (fear Of missing Out) na hii
itamfanya akupe nafasi haraka
iwezekanavyo ili asije akakukosa
wakakuchukua wengine.

Jambo la Pili: Epuka kumuonesha


kuwa una chaguo moja tu ambalo ni
yeye pekeake.

Katika sura ya pili tuliangalia namna


ambavyo samaki jike aina ya Goldfish
anavyovutiwa na samaki dume
mwenye wanawake wengi ndivyo
ilivyo kwa mwanamke.

44
Mwanamke akijua kuwa hauna
options zaidi yake ni vigumu sana
kumpata, na miongoni mwa kauli
ambazo hutakiwi kabisa kumwambia
ni kauli kama “sina mwingine zaidi
yako, ukinikataa wewe nani
atanitaka” na zingine zinazofanana na
hizo.

Moja ya mbinu ya kufanikiwa katika


hilo ni kutokukubali kuwa hauna
mwanamke mwingine, muoneshe
kuwa kama yeye akikataa unao
uwezo wa kumpata mwingine aliye
bora zaidi.

Hii itamfanya ajue kuwa wewe ni wa


thamani na unahitajika jambo ambalo
linaweza kumshawishi na yeye
kukuhitaji.

45
Jambo la Tatu: Epuka kumuonesha
kuwa wewe unapatikana kirahisi.

Wakati unamtongoza mwanamke


epuka kumfanya akuone wewe ni
Cheap na badala yake jibidiishe
kumfanya ajue akipata nafasi ya
kuwasiliana nawewe au akipata muda
wa kuzungumza nawewe iwe ni
kupitia simu au ana kwa ana basi
anatakiwa kujua kuwa amepata nafasi
ya upendeleo sana.

Inashauriwa kukaa masaa 12 mpaka


46 (siku moja mpaka siku 3) kuanzia
ulipopata namba ya mwanamke
uliyekutana nae kabla ya kuwasiliana
nae kwa mara ya kwanza.

46
Wengi huwa wanafanya kosa la
kutuma meseji au kupiga dakika
chache mara baada ya kupewa
namba, hii inamfanya akutafsiri kuwa
wewe ni cheap na ni mrahisi mbele
yake, kinachotokea anapata nguvu
juu yako jambo ambalo sio sahihi.

Kumbuka kuwa kiasili binadamu


anapenda kukutana na ugumu
utakaomuumiza kichwa na ndio
maana kuna wakati uwezekano wa
kupata kitu fulani kirahisi upo lakini
mtu anatumia njia yenye ugumu
kidogo.

Mwanamke anataka mwanaume


ambae atamsumbuasumbua na
kumfikirisha na sio mwanaume ambae
ni mrahisi.

47
Akikupa namba hakikisha unajifanya
kama umesahau ili ajue kuwa
haumzingatii na kumtilia maanani, hii
itamfanya awe na jukumu la kuitafuta
attention yako na akiipata anajiona
mwenye bahati.

Jambo la Nne: Epuka kumuonesha


kuwa kutokuwepo kwake kuna athari
katika maisha yako.

Kwa mujibu wa hii kanuni inasema


kuwa kadri unavyomuonesha
mwanamke kuwa una furaha hata bila
ya uwepo wake ndivyo unavyozidi
kumfanya akufuatilie na aweke
umakini wake kwako (put her
attention into you) ili apate nafasi ya
kujua ni kitu gani kinachokupa furaha.

48
Ile attention atakayoweka kwako
inalenga kutaka kujua ni kwa namna
gani unampenda na wakati yeye sio
chanzo cha furaha yako kwa sababu
hata asipokuwepo wewe una furaha,
swali hili linaweza kumpa majibu kuwa
yeye kwako sio kipaumbele kwa
sababu una machaguo mengine ndio
maana una furaha.

Hii inaweza kumfanya awe dhaifu na

anajua kuwa kwako hana nafasi


kubwa, akifika hii hatua ni rahisi sasa
wewe kumpata kwa sababu ataona
kama amependelewa kuwa nawewe.

Wanaume wengi wanakosea sana


kuwaambia wanawake maneno kama
“sijalala, sijakula au sijafanya kitu

49
fulani kwa sababu yako” wakiamini
kuwa maneno hayo huashiria upendo
wasijue kuwa maneno hayo hutosha
kumfamya mwanamke awaone wao ni
wadhaifu.

Kumbuka kuwa wanawake


wanavutiwa na wanaume walio imara,
wanaojiamini na wanaume ambao
hawawezi kuendeshwa wala
kuathiriwa kihisia (masculine men)

hii humfanya mwanamke ajione yuko


sehemu salama ikiwa atapata nafasi
ya kuwa na mwanaume huyo.

50
Namna ya Kuitumia Kanuni ya
Chase, Just Attract Kumpata
Mwanamke Unaemtaka

Kwa sababu kanuni inasema


unatakiwa uwekeze nguvu nyingi
kumvutia mwamnamke unaemtaka na
sio kuwekeza nguvu nyingi
kumfukuzia basi kuna mambo
unatakiwa kuyafanya ambayo
yatakusaidia kumfanya avutiwe
nawewe na akivutiwa nawewe ni
rahisi wewe kumshawishi na
kumfanya awe mwenzi wako.

Jambo la Kwanza; Muoneshe kuwa


unahitajika na wengi.

Mfano wa goldfish jike unatuonesha


kwamba wanawake wanahitaji
51
wanaume ambao wanahitajika na
wanawake wengi, njia mojawapo ya
kumvutia mwanamke ni kumfanya
ajue kuwa wewe ni aina ya
mwanaume ambae unahitajika na
wanawake wengi.

Dan Bilzerian anaetajwa kama


mwanaume mwenye mvuto na
ushawishi mkubwa kwa wanawake
alipoulizwa aliwezaje kuwa na uwezo
huo alibainisha kuwa kuna wakati
ilimlazimu kufanya sherehe fupi na
katika sherehe yake huwaalika
wanawake ambao atapiga nao picha
na kisha kupost katika kurasa zake za
mitandao ya kijamii.

Hii iliwafanya wanawake kujawa na


wivu kwa kudhani wanawake walio

52
karibu na Dan kuna kitu wanafaidi,
lakini pia hali hii iliibua udadisi
Curiosity ndani ya wanawake na
kujiuliza Dan alikuwa na kitu gani cha
kipekee kiasi cha kuvutia wanawake
wengi namna hiyo?

Hii ilimtengenezea mazingira ya


kuwavutia wengine na kuwafanya
watamani kuwa karibu nae jambo
ambalo liliwafanya waanze kutafuta
umakini attention wake na baada ya
muda ni wanawake ndio walikuwa
wakimfukuzia Dan na sio Dan
kuwafukuzia wao.

Sisemi ufanye kama Dan, ila nataka


uone namna ambavyo ukifanikiwa
kumfanya mwanamke ajue kuwa

53
wewe ni mwanaume unaeyehitajika
sana The most wanted man
utafanikiwa kumfanya yeye avutiwe
nawewe.

Jambo la Pili; Tumia pre-selection


rule.

Pre-selection inasema kuwa ili uweze


kumpata mwanamke unaemtaka ni
vizuri kutafuta mwanamke ambae
kupitia huyo unaweza kufanikisha
zoezi lako la kumvutia umtakae.

Hii ni kusema kwamba, yawezekana


una rafiki wa kike ambae mmezoeana
nae, unaweza kumtumia huyo kama
sehemu ya kujitangazia ili kumvuta
unaemtaka.

54
Unaweza kulifanikisha hilo kwa
kutumia muda mwingi pamoja nae
huku mkifurahia, unaweza kumjali ili
kumfanya yule umtakae apate wivu
na aanze kukuhitaji wewe.

Mtu mmoja aliwahi kusema kuwa


mwanaume aliye na mpenzi na
akampenda mpenzi wake kwa wazi
anao uwezo wa kupata wapenzi
wengine wengi kwa sababu
watavutiwa na vile mwanaume huyo
anavyompenda mpenzi wake na
kuwafanya wapatwe wivu, kwahiyo
unaweza kumtumia rafiki yako wa
kike kama jukwaa la kujinadi kwa
mwanamke unaemtaka.

Kwa upande mwingine pre-selection


inakutaka uweke ukaribu na rafiki wa

55
mwanamke umtakae na umfanye
rafiki huyo kufurahia zaidi uwepo
wako, unajua nini kitatokea ukifanya
hivyo?

Kama ukiweka ukaribu na rafiki wa


mwanamke unaemtaka na
ukafanikiwa kumfanya afurahie basi
utakuwa kwenye nafasi nzuri ya
kumpata mwanamke umtakae kwa
sababu atavutiwa na kile unafanya
kwa rafiki yake na kujawa wivu ndani
yake.

Utafiti umebaini kuwa hakuna


wanaume wanaopata wanawake
kirahisi kama wale ambao wana
marafiki wa kike ambao wanafurahia
urafiki huo au wenye wapenzi
wanaofurahi na kupendeza,

56
Hii ni kwa sababu wanawake
wanapenda wanaume wenye uwezo
mkubwa wa kuwapa furaha,
ikionekana mwanaume anaweza
kumpa furaha mwanamke wake ni
rahisi sana mwanaume huyo kuvutia
wanawake wengine.

Jambo la Tatu; Kuwa Mwanaume wa


Thamani (Be Prize, Be Alpha Male)

Umeshawahi kujiuliza ni kwa nini kuna


wanaume wanakimbiliwa zaidi na
wanawake kuliko wanaume wengine?

Hii ni kwa sababu wanaume hao wana


thamani fulani inayowafanya
wanawake wavutiwe na hadhi
Status fulani za wanaume hao, hii
mana yake ni kwamba mwanamke

57
anavutiwa zaidi na hadhi aliyonayo
mwanaume.

Hadhi inatokana na mwanaume


kufanya mambo fulani yanayokubalika
katika jamii na ndio maana waigizaji,
wacheza mpira, wachekeshaji,
waimbaji na watu wanaofanana na
hao huwavutia wanawake kirahisi
zaidi kuliko wengine.

Kama una kipaji au uwezo wowote


unaokufanya ufanye jambo fulani
katika ubora wa hali ya juu utumie
uwezo huo unaweza kukuongezea
thamani kiasi cha kumfanya
mwanamke akuhitaji.

Unachotakiwa kukumbuka ni kwamba


lengo la kutongoza ni kujiuza na

58
kuhakikisha unauzika kwa mwanamke
unaemtaka na ili uweze kufanikiwa
katika hilo lazima uwe vile ambavyo
yeye atavutiwa nawewe.

Hakikisha kadri uwezavyo unakuwa


mwanaume mpambanaji na mwenye
matokeo katika mapambano yako,
jitengeneze na kujijenga kiuchumi
kwa kufanya shughuli
zitakazokuingizia kipato na kuboresha
maisha yako.

Suala la wewe ni nani na una nini lina


nguvu sana wakati mwanamke
anafikiria kukukubalia wewe, ndio
maana inaonekana kama wanaume
waliopiga hatua katika maisha
hukimbiliwa zaidi na wanawake
wengi.

59
Wanachofuata kwao ni ile fahari
ambayo mwanamke anakuwa nayo
pale wengine wanapojua kuwa
anatoka na mwanaume fulani, hisia
hizo zinaitwa “pride of ownership”

Wanaume wengi kwa kulijua hili,


wamejikuta katika namna ambayo
inawalazimu kuwa waongo kwa
kujinadi mbele ya wanawake ili
kupandisha hadhi status zao.

Wengi wameazima magari, wengine


wameazima mpaka nguo, simu,
vyumba (maghetto) na hata kudiriki
kupiga picha maeneo yanayovutia
zaidi ili tu kuonesha kwamba wao ni
wanaume wa hadhi ya juu high class
men

60
Sikushauri wewe kufanya hivyo kwani
utajitengenezea utumwa mbaya
endapo kile ulichojinadi ni kinyume na
uhalisia wa maisha yako jinsi ulivyo.

Lakini pia utapoteza point mwanamke


akigundua kuwa unafanya yoote hayo
ili kumvutia yeye, kuwa aina ya
wanaume ambao hawafanyi mambo ili
kumplease mwanamke (bad guys &
Jerks).

61
Sura Ya Nne

Mbinu za Kumtongoza Mwanamke


Aliye Katika Mahusiano

Baada ya kuamka asubuhi na kufanya


maombi ya kumshukuru Mungu kisha
kusoma kurasa kadhaa za kitabu
kama ilivyo kawaida yangu kila
ninapoamka.

Niliamua kuingia katika moja ya


mtandao wa kijamii na nikakuta
ujumbe unasema “A good woman is
not easy to find nowdays, you have
to steal her from hands of a careless
man”

62
Tafsiri yake ni kwamba, kwa zama
tulizonazo hivi sasa ni vigumu sana
kumpata mwanamke bora, ili kumpata
unatakiwa kumuiba kutoka katika
mikono ya mwanaume asiyemjali wala
kumthamini (anaemchukulia poapoa)

Kuna wakati ambapo, mwanamke


unaemtaka anakuwa tayari yupo
katika mahusiano na mwanaume
mwingine ambae hamjali wala
kumthamini mwanamke huyo.

Kuna kitu kinaitwa LOVE SHIFTING


hiki ni kitendo cha hisia za kimapenzi
kuhama kutoka kwa mtu mmoja
kwenda kwa mtu mwingine.

Yawezekana mwanamke huyo kwa


sasa ni kweli kabisa hakupendi na

63
anampenda mwanaume wake licha ya
ukweli kwamba ananyanyasika,
anatumika na kupuuzwa.

Ila kupitia hiki unachoenda kujifunza


katika sura hii itakuwa rahisi kwako
kumvutia na kufanya upendo alionao
kwa mtu wake uhamie kwako.

1. Tumia udhaifu wa mwenzi wake

Inapotokea mwanamke unaemtaka


yupo katika mahusiano na mwanaume
mwingine, epuka kosa la kuanza
kumpondea mwanaume wake na
badala yake tafuta kuujua udhaifu wa
mwenzi wake na uutumie kama mtaji.

Kwa mfano mwanamke anapenda


mwanaume atakaewasiliana nae na

64
kumpa zawadi mara kwa mara na
kumfanya ajisikie vizuri na kufurahia
ila mwanaume wake huwa hafanyi
hivyo, kwako hiyo ni nafasi nzuri
ambayo ukiitumia inaweza kukusaidia
sana.

Unapomfanyia yale anayotamani


kufanyiwa na mwenzi wake alafu
hafanyiwi kuna mambo kadhaa
yanazaliwa ndani yake.

Kwanza anaanza kukuona wewe ni


bora kuliko mtu wake, lakini pia
anaanza kukuona kama mtu unaezijua
hisia zake zaidi ya mwenzi wake, kila
mwanamke anapenda kuwa na
mwanaume ambae mwanaume huyo
anajua namna ya kumfanya
mwanamke afurahi na kuridhika.

65
Point ya msingi hapa ni kuangalia yale
mambo ambayo anamiss kutoka kwa
mwenzi wako na ukiyajua hakikisha
kwako anayapata.

Na ili uweze kulifanikisha hili


utalazimika kutumia muda mwingi
kumjua na kujua anamiss nini kwa mtu
wake, ila epuka suala la kuwa na
urafiki nae.

Muulize maswali kama unadhani


mwanaume wako anatakiwa
kukupendaje ili ufurahie penzi lake
yale atakayokwambia yatumie
kuyafanya wewe.

66
2. Zungumza Lugha yake ya upendo
(Speak her Love Languge)

Love language ni yale mambo


ambayo mtu akifanyiwa anatafsiri
kama anapendwa, kila mwanamke
ana lugha yake ya upendo.

Yawezekana mwenzi wake haijui ila


hakikisha wewe unaijua na kila
unalomfanyia liwe linaendana na
lugha yake ya upendo.

Njia rahisi kabisa ya wewe


kulifanikisha hili ni kuzijua lugha zote
tano na uzitumie kwake moja baada
ya nyingine, utakayoona imemgusa
zaidi ya zingine hiyo ndiyo lugha
yake.

67
Kama unahitaji kuzijua lugha hizo
nashauri usome kitabu changu
kinachoitwa LUGHA TANO ZA
UPENDO kitakachokusaidia sana
kama kilivyowasaidia wengine wengi
waliopata nafasi ya kukisoma.

Bi muhimu kujua kuwa, mapenzi


yamejaa ushindani, ili kujihakikishia
ushindi ni lazima uwe mbunifu zaidi
ya wengine.

3. Jaza Tenki lake la Upendo


(Fill her love tank)

Mwanaume unapoanza kumtongoza


mwanamke, yeye anakuwa hana hisia
kabisa juu yako wala mawazo
kukuhusu.

68
Unatakiwa kufahamu kwamba, huwa
inakuwa vigumu sana kwa mwanamke
kukukubali ikiwa hana msukumo
wowote kutokea ndani yake wa
kukukubalia wewe.

Kwahiyo, hakikisha kila unalofanya


linalenga kujaza tenki lake la hisia
zake juu yako, tenki hili kuna mahali
likifika ataamua kuwa nawewe.

Njia rahisi ya kulijaza ni kuyafanya


mambo niliyokufundisha katika
namba moja na namba mbili (rejea
ukayasome tena.

69
4. Tumia mbinu chambo
(Bait Techinique)

Baada ya kumfanyia mambo


uliyojifunza katika namba 1, 2 na
namba 3 na kujiridisha kwamba
mambo hayo yalikuwa yakimgusa na
anayapenda na kuyafurahia
ukimfanyia baada ya muda fulani
unatakiwa kupunguza kuyafanya au
kuacha.

Kufanya hivyo utakuwa


umemtengenezea uhitaji wa yale
uliyokuwa ukimfanyia na hivi sasa
umeacha.

Atajikuta anayamiss yale mambo yote


kutoka kwako na kila

70
anapoyakumbuka anaanza kukufikiria
wewe.

Ndani yake itazaliwa shauku ya


kuendelea kuyapata mambo hayo
kutoka kwako, shauku hii itaambatana
na hisia za yeye kutamani kuwa
karibu yako zaidi akiamini kwamba
atafurahi zaidi ya mwanzo.
Ndipo ataanza kuitafuta attention
yako wakati huo wewe ni kama hauna
mpango nae na hii itamfanya ahisi
labda kuna mwanamke mwingine
unamfanyia jambo litakalomfanya
awe na wivu juu yako.

Akifika hii hatua ni rahisi kwako


kumpata kwa sababu anakuwa
ameshawishika vya kutosha.

71
Muhimu; mambo haya yamefanyiwa
kazi na wengi na kuonekana kuleta
matokeo, ili uweze kupata matokeo
nawewe utalazimika kuyafanya kwa
muda kwani kadri unavyozidi
kuyafanya ndivyo
yanavyokutengenezea mazingira ya
wewe kufanikisha lengo lako.

72
Sura ya Tano

Makosa ya Kuepuka Wakati


Unamtongoza Mwanamke

Wakati mwingine ugumu unaokutana


nao katika kumtongoza mwanamke
sio kwa sababu hakutaki, ila ni kwa
sababu kuna makosa ambayo
unafanya yanayosababisha ashindwe
kuvutiwa na wewe.

Hakikisha makosa haya unayaepuka


kwa gharama yoyote ile.

Kosa la Kwanza: hali ya kumfanya


awe rafiki yako au kukubali wewe
kuwa rafiki yake

73
mwanamke akikufanya wewe kama
rafiki yake ni vigumu sana kugeuka na
kuwa mpenzi.

Urafiki kati ya mwanamke na


mwanaume humfanya mwanamke
kujihisi huru kuelezea hisia zake na
ndio maana anaweza akawa
anakuelezea jinsi ambavyo anakutana
na migogoro katika mahusiano na
mwanaume wake.

Lakini pia fahamu kuwa wanawake


kwa asili hutafuta kitu kilicho mbali na
ambacho hawana na ndio maana ni
rahisi kwa mwanamke kuingia katika
mahusiano na mwanaume asiyemjua
na kukuacha wewe ambae umekuwa
rafiki au karibu yake kwa muda fulani.

74
Mwanamke akikuweka katika ukanda
wa urafiki Friendhship Zone huwa
inakuwaga vigumu sana kukukubalia
endapo utamtongoza.

Hii inatokana na ukweli kwamba


akikuweka katika friendship zone
anaanza kukuona kama nice guy,
mwanaume usiyeweza kumhandle, na
ataanza kukutumia.

Kosa la Pili: kuwekeza kwajili yake au


kujitoa zaidi kwake.

Nadhani umewahi kusikia wanaume


walioachwa na wanawake
waliowasomesha mpaka wakafika
hatua ya kuhitimu.

75
Kinachomfanya mwanamke amuache
mwanaume pamoja na gharama
nyingi ambazo mwanaume ameingia
ni kwa sababu kadri mwanaume
anavyowekeza zaidi kwa mwanamke
ndivyo ambavyo anazidi kupoteza
mvuto mbele ya macho ya
mwanamke huyo.

Kuwekeza ni aina mojawapo ya


utongozaji kati ya zile mbili
tulizoangalia katika sura ya kwanza,
lakini unashauriwa usiwekeze katika
kiwango cha kumfanya mwanamke
ahisi unataka kumnunua, kumteka
kwa yale unayomfanyia au unafanya
kwa sababu ya udhaifu ulionao.

Sababu ya pili ni kwamba wanawake


wengi hawapendi kuwa watumwa au

76
watu wanaotumikia kifungo fulani,
unapowekeza zaidi kwa mwanamke
inamfanya aone kama unataka
kumtawala jambo ambalo litamnyima
uhuru.

Sababu ya tatu, wanawake wengi


wanamtafsiri mwanaume anaejitoa
sana kwao kama mwanaume
asiyejiamini na ndio maana anatumia
fedha na mali alizonazo kumteka
mwanamke.

Ni vizuri kukumbuka kuwa,


mwanamke yeyote anavutiwa zaidi na
mwanaume anaejiamini na ndio
maana mwanamke anaweza
kumuacha mwanaume mwenye fedha
na kumfuata asiye na kitu kwa sababu
tu mwanaume huyo anajiamini.

77
Kosa la Tatu: kumuonesha kuwa
yeye ndiye chaguo lako la mwisho.

Wanawake hawataki kabisa kujisikia


wako katika mahusiano na
mwanaume ambae hana uwezo wa
kupata mwanamke mwingine, hii
inamfanya mwanamke afikirie kuwa
upo nae kwa sababu hauna mwingine
(Only option), wanawake wanapenda
kujua kuwa miongoni mwa machaguo
mengi uliyonayo umemuona yeye
anafaa (The best option).

Hii inampa kujidai na kujiona ni


mwanamke wa tofauti, wa thamani na
mwenye bahati hata kukupata wewe,
kwahiyo, usifanye kosa la
kumuaminisha kuwa yeye ndiye
chaguo lako la mwisho hata kama

78
ukweli uko hivyo kwamba hauna
chaguo jingine zaidi yake.

Kosa la Nne: kumuonesha kuwa kuna


uwezekano wa wewe kuwa na
mwanamke mwingine mara baada ya
kuwa nayeye.

Katika aina 70 za hofu zinazomkabili


mwanadamu, kuna aina tatu za hofu
zinamkabili zaidi mwanadamu
mwenye jinsia ya kike.

Aina ya kwanza inaitwa Anglophobia,


hii ni hofu ya kukutana na maumivu,
mwanamke hayupo tayari kufanya
jambo ambalo kabla hajalifanya atajua
kuwa kuna uwezekano wa kukutana
na maumivu.

79
Kwahiyo wakati unamtongoza epuka
kumfanya ajue kuwa kuna uwezekano
wa kumuumiza mbeleni kwa sababu
akijua hivyo hawezi kukubali ili
asikutane na maumivu.

Aina ya pili ya hofu inayowakumba


wanawake zaidi inaitwa
chronophobia, aina hii ya hofu
humfanya mwanamke awe na hofu ya
kukutana na mabaya, mabaya hayo
yanaweza kuwa ni mateso na stress
za mapenzi utakazomsababishia, aina
hii ya hofu wakati mwingine
inafahamika kama Assumed Danger
(hatari za kufikirika)

Hakikisha katika kila utakalofanya


lengo lako liwe ni kumuhakikishia

80
Amani, utulivu na usalama kwa muda
wote atakaokuwa na wewe.

Aina ya tatu ya hofu inayowakumba


wanawake inaitwa Autophobia, hii ni
ile hali ya kuogopa kutelekezwa au
kuachwa solemba, wakati
unamtongoza mwanamke unatakiwa
kumfanya ajue kuwa wewe na yeye
mtakuwa pamoja katika nyakati zote,

Ndio maana kumtongoza mwanamke


ni pamoja na kumfany AKUAMINI.

Ni kweli unatakiwa kumuonesha kuwa


una machaguo mengi na unaweza
kumpata mwanamke mwingine lakini
pia mfanye ajihisi yuko kama atakuwa
nawewe basi atakuwa sehemu

81
salama, mpe uhakika wa ulinzi wa
hisia zake.

Akijua kuwa kuna uwezekano wa


kumtelekeza mbeleni labda baada ya
wewe kufanikiwa ni vigumu sana
kukupa wewe nafasi.

Kosa la Tano: kumuonesha kuwa


kipaumbele chako kikubwa ni SEX na
sio UHUSIANO.

Wanawake wote wana hofu ya


kuchezewa na kuachwa,
unapomtongoza epuka suala la
kumuonesha kwamba lengo kuu
ulilonalo ni kufanya nae ngono.

Ile hofu ya kuachwa baada ya


kufanya nae inaweza kumfanya

82
akukatalie ili kuepuka maumivu
atakayokutana nayo mbeleni endapo
atakukubalia na kukuruhusu mfanye
sex.

Usiwe aina ya mwanaume ambae,


mara zote unapowasiliana na
mwanamke unagusia sana suala la
sex, hii itamtengezea mazingira ya
kukuona kama mwanaume ambae
kwake hauna lengo jingine isipokuwa
kusex nae.

83
Sura Ya Sita

Sababu Zinazopelekea Hali ya


Mwanaume Kukataliwa Mara kwa
Mara
Kupitia utafiti uliofanywa na Chuo
kikuu cha Harvard kitengo cha
saikolojia ya binadamu (Human
Psychology) umeonesha kuwa
binadamu yeyote kwa sehemu kubwa
anaumia zaidi endapo akikataliwa.

Kiuhalisia hakuna mtu anaependa


kukataliwa kwani kunaweza kumfanya
ajione ni mtu asiyefaa kitu.

Yawezekana suala la kukataliwa


limekuwa likikusumbua mara kwa

84
mara kila unapoamua kumtongoza
mwanamke, yaani kila mwanamke
unaemtongoza anaishia kukukataa.

Yawezekana kukataliwa huko


kunatokea moja kwa moja au katika
namna isiyo ya moja kwa moya, kuna
mambo kadhaa yanaweza
kusababisha hali ya namna hiyo.

Kukataliwa kwa namna ya moja kwa


moja ni pale anapokwambia
sikupendi, sikutaki, sina hisia
nawewe, hujanivutia

Na kukataliwa kwa namna isiyo ya


moja kwa moja ni pale unapopewa
majibu kama siwamini wanaume, nina
mtu, sihitaji mwanaume kwa sasa

85
Bila kujali ni jibu gani amekupa, huko
koote ni kukataliwa. Zipo sababu
kadhaa zinzoweza kupelekea hali ya
kukataliwa mara kwa mara.

Sababu ya Kwanza; kushindwa


kushawishi.

Unapomtongoza mwanamke
unatakiwa kujua kuwa unahusika na
hisia zake, lengo ni kumfanya akuone
wewe unamfaa hivyo ni lazima uwe
na uwezo mkubwa wa kumshawishi.

Kuna wakati unaweza kukataliwa sio


kwa sababu nyingine, ila ni kwa
sababu uwezo wako wa kumshawishi
mwanamke ni mdogo kiasi cha
kumfanya akukubalie.

86
The principle of seducing and build
wealth are the same, people who
succeed at these games understand
how to attract and not to chase

Haya ni maneno ya Dan Bilzerian


yenye maana kwamba Kanuni za
kibiashara na kupata mwenzi
zinafanana, watu wanaofanikiwa ni
wale wenye uwezo mzuri wa
kushawishi (kuvutia upande wao).

Njia rahisi ya kukabiliana na


changamoto ya kukataliwa
inayotokana na kukosa uwezo wa
kushawishi ni wewe kujenga uwezo
huo, uwezo wa kushawishi ndio
utamfanya mwanamke afike hatua ya
kuona kwamba anakuhitaji hata kama
hapo mwanzoni alikuwa anakukatalia.

87
Sababu ya Pili; makosa unayofanya
wakati wa utongozaji.

katika sura iliyopita umejifunza


makosa ambayo unatakiwa
kuyaepuka wakati unamtongoza
mwanamke.

Kuna uwezekano mkubwa wa


mwanamke zaidi ya mmoja kukukataa
kwa sababu unayarudia makosa kwa
kila mwanamke unaemtongoza,

Kama umegundua kuwa kuna makosa


ulifanya au umekuwa ukifanya
unatakiwa kuyaorodhesha kwa
kujiuliza je ni makosa gani huwa
unafanya ambayo yamekuathiri?

88
Ukiyabaini hakikisha kuanzia hapo
haufanyi makosa tena ili usiendelee
kukataliwa.

Sababu ya Tatu; kutongoza


wanawake ambao
wanekwishachukuliwa (Seducing
Ready Taken Women)

kuna wakati unaweza kukataliwa kwa


sababu unatongoza wanawake
ambao tayari wapo katika mahusiano
na wanaume wengine.

Lakini hata hivyo, shuhuda nyingi


zinaonesha kwamba upo uwezekano
wa mwanaume kumpata mwanamke
ambae tayari yupo katika mahusiano
na mwanaume mwingine.

89
Hili linawezekana endapo utakuwa na
uwezo mkubwa wa kushawishi
pamoja na kutumia mbinu za
kumtongoza mwanamke aliye katika
mhusiano ulizojifunza katika sura ya
nne (rudi ukazisome tena)

Usije ukaliamini jibu la mwanamke na


nitakwambia kwanini.

Nilipokuwa Nasoma Masoko Na


Mauzo (Sales and Marketing)
Nilifundishwa Kitu Kimoja Na Mwalimu
Wangu.

Aliniambia Kwamba Isaack, When a


Customer Reject Your Product,
Knows That He/She Has Not Reject
Your Product As It Is, But Your Offer

90
Alimaanisha Kwamba, Pale Mteja
Atakapoikataa Bidha Yako, Hajaikataa
Bidhaa Kama Bidhaa Ila Amekataa Ofa
Yako, Yaaani Namna Ulivyotaka
Kumuuzia Hiyo Bidhaa.

Baada Ya Miaka Mingi Kupita,


Nimejifunza Kitu Kimoja Kikubwa
Sana, Nimejifunza Kwamba Kanuni Za
Masoko Na Mauzo Ni Sawa Na
Kanuni Za Utongozaji.

Ndio Maana Dan Bilzerian Ambae Ni


Mmoja Kati Ya Watongozaji Mahiri
Aliwahi Kusema Hivi👇

Laws of Seduction and That of


Making Money through Business Are
the Same Yaani Kanuni Za
Utengenezaji Wa Fedha Kupitia

91
Biashara Hazitofautiani Na Kanuni Za
Utongozaji.

Hii Ni Kwa Sababu Kwenye Biashara


UNAUZA BIDHAA YAK
Kuifanya Ikubaliwe Lakini Kwenye
Kutongoza UNAJIUZA WEWE Ili
Kumfanya Unaemtongoza Akukubalie.

Zoezi ni Lilelile Linahusu Uuzaji na


Kanuni Zake Ni Zilezile.

Kwahiyo, Usije Ukaliamini Jibu la


Mwanamke, Na Nitakwambia Kwanini

Unapomuuzia Mteja Kitu Anaweza


Kukataa, Sio Kwa Sababu Hakitaki, Ila
Kwa Sababu Hajashawishika

92
Kwahiyo, Majibu Yake Yooote Ya
Sina Hela, Bei Yako Kubwa, Nitakuja
Wakati Mwingine, Ngoja Nikafikirie

Hayo Yoote Yanamaanisha Kuwa


Hujanishawishi Vya Kutosha Kiasi
Cha Mimi Kukupa Hela Yangu

Ndio Maana Mteja Anaweza Akaacha


Kununua Bidhaa Kwako Akaenda
Kununua Kwa Massawe. hiyo Yoote
Huthibitisha Kwamba Wewe
Ulishindwa KUMSHAWISHI.

Hiyoo Ni Kwenye Kuuza Bidhaa, Na


Kwenye Kumtongoza Mwanamke Iko
Hivyohivyo, Usije Ukaliamini Jibu
Lake na Ukakata Tamaa.

93
Anaweza Kukambia Nina Mtu, Sihitaji
Kuwa Na Mahusiano Kwa Sasa,
Naomba Tubaki Kuwa Marafiki,
Siwaamini Wanaume N.k.

Majibu Yake Yoote Yanayoonesha


Kutokukubaliana Nawewe
Yanamaanisha Kitu Kimoja Tu!

Kitu Chenyewe Ni Hiki


Yanamaanisha Kuwa,
“Hujanishawishi Vya Kutosha Kiasi
Cha Mimi Kukubali Kuwa Mpenzi
Wako”

Kwahiyo, Unatakiwa Kujua Kwamba


Hajakukataa Wewe, Ila Ameikataa
Approach (Mbinu) Uliyotumia Na
Namna Ulivyomuingia.

94
Ndio Maana Ni Vizuri Sana Kujifunza
Namna Gani Unaweza Kuwa ni
Mwanaume na USHAWISHI Kwa
Mwanamke na kwa sababu tayari
unasoma kitabu hiki nakushauri
usome na namba mbili yake, yaani
Sanaa ya Utongozaji 02.

Sababu ya Nne; kutokuwa na vigezo


(Being Disqualified)

Kila mwanamke ana vigezo vya


mwanaume anaemtaka, na kabla
hajakubali kuwa na mwanaume lazima
kwanza achunguze kama mwanaume
huyo ametimiza vigezo
vinavyohitajika.

Vigezo hivyo ndivyo ambavyo


mwanamke huvitumia ili kujua kama

95
unamfaa au haumfai, ikionekana
hujatimiza vigezo anavyovitaka huwa
inakuwa vigumu sana kwa yeye
kukubali ombi lako.

Au, inawezekana mwanaume akawa


amepungukiwa vigezo fulani kama
vile muonekano, ila akawa na kitu cha
tofauti kidogo kinachoweza
kumsaidia.

Kitu hicho yawezekana ni fedha,


cheo, umarufu, kipaji au chochote
chenye nguvu ya kumshawishi
mwanamke na kukufanya ukubalike
katika macho ya watu.

Ndio maana, baadhi ya wanaume


wanapogundua kuwa kuna vigezo

96
wamepungukiwa hulazimika kutumia
mbinu mbadala ili kutimiza lengo.

Sababu ya Tano; Udhaifu fulani


(certain weakness)

kuna wakati ambapo mwanaume


anakataliwa kwa sababu ya udhaifu
alionao, changamoto ni kwamba
huwa ni vigumu kuambiwa moja kwa
moja sababu inayomfanya akataliwe
ila akambiwa sababu nyingine kama
vile nina mtu au sipo tayari kwa
sasa Yote ni katika namna ya
kuhakikisha anakataa ombi la
mwanaume.

Hii haina maana kwamba, mwanaume


mwenye udhaifu fulani hawezi kupata
mwanamke, ila upo uwezekano

97
mkubwa wa yeye kukataliwa kwa
sababu ya udhaifu huo endapo
atatongoza wanawake ambao
hawapo tayari kuwa na mwanaume
mwenye aina fulani ya udhaifu.

Lakini, unapopata mwanamke licha ya


udhaifu fulani ulionao labda ulemavu
au wowote ambao umewafanya
wengine wakukatae ni muhimu kujua
kwamba huo alionao kwako ni upendo
wa dhati na ndio maana amekubali
kuwa nawewe.

Sababu ya Sita; Roho ya Kukataliwa


(Rejection Spirit)

Kuna wakati ambapo shida inaweza


isiwe kutokuwa na vigezo, wala
inaweza isiwe unatongoza wanawake

98
walio katika mahusiano au una
udhaifu fulani ila shida ikawa ni roho
ya kukataliwa inakusumbua.

Mara nyingi mtu mwenye roho ya


kukataliwa huwa anandamwa na hali
ya kukokukubalika mbele za watu, kila
anachofanya hakipokelewi vyema na
jamii.

Hii inaweza kutokea katika maeneo


mengine ya maisha mpaka katika
eneo la kutafuta mwanamke wa kuwa
nae.

Upo uwezekano ukawa na elimu


nzuri, kazi, fedha, cheo na maisha
mazuri kabisa na bado ukakataliwa na
wanawake.

99
Ukiona hivyo ujue unahitaji
kulishughulikia jambo hili mapema.

Roho ya kukataliwa huwa


inaambatana na roho ya uharibifu,
unaweza ukapata mwanamke lakini
usidumu nae kwa muda mrefu
kutokana na hiyo roho, yaani kila
ukianzisha mahusiano wanawake
wanakukimbia baada ya muda.

Tatizo la aina hii linaweza


kushughulikiwa kiroho zaidi kulingana
na dini ya mtu, uzuri ni kwamba mara
utakapoanza kulishughulikia kwa
kumaanisha utaanza kuona
mabadiliko makubwa sana
yatakayotokea katika maisha yako.

100
Lakini njia ya uhakika zaidi ni kutafuta
chumvi ya mawe, kisha weka katika
ndoo na maji na uende ukaoge maji
hayo huku ukijitamkia maneno kama
nitavutia, sitakataliwa, nitapendwa,
nitakubalika, nitaheshimika na kuwa
mtu mkuu

Baada ya kumaliza kufanya hivyo,


hakikisha unavaa vizuri, kula vizuri,
fanya mazoezi, nukia, piga picha
nzuri, tumia vitu viz .. Yaani
jipende.

Hii ni kwa sababu kwa mujibu wa


kanuni ya kuvutia (law of attraction)
inasema tunavutia aina ya watu katika
maisha kulingana na namna
tunavyoishi maisha yetu, lakini pia

101
watu wengine hutufanyia sawasawa
na vile tunavyojifanyia sisi.

Hivyo, ukijipenda, ukajijali, ukajikubali


ni rshisi sana kuvutia upendo na
kukubalika kutoka kwa watu wengine.

Kutongoza ni zoezi endelevu, hivyo


sio zoezi la siku moja, mbili au wiki hii
ni kwa sababu lengo lako ni kujenga
Imani ndani ya mwanamke unaemtaka
na kuuteka utayari wake.

Unachotakiwa kujua ni kwamba


mambo madogo madogo
unayomfanyia kila siku yana athari
ambazo zitaonekana baada ya muda
fulani, hii ni kwa sababu ya kanuni ya
Brailfold inayoitwa Aggregation of
Marginal Gain (kukusanya faida
ndogndogo mara kwa mara)
102
Kanuni hii inasema ikiwa utawekeza
juhudi zako kufanya jambo fulani japo
kwa udogo ila katika namna endelevu
basi baada ya muda kuna uwezekano
wa kufanikiwa katika jambo
unalolifanya.

Yawezekana asikuelewe leo, lakini


kama hautaacha wala kukata tamaa
kuna siku atauona upendo wako na
kutokea hapo ataanza kukuhitaji.

Usisahau kwamba, Hiki kitabu


unachosoma sasa ni namba moja, ili
kujihakikishia kuwa unakuwa na
maarifa ya kutosha kuhusu saikolojia
ya wanawake na namna ya kuwa
mwanaume mwenye mvuto na
ushawishi basi hakikisha unasoma
namba mbili pia.

103
Visome vyoote viwili kisha kisha weka
katika matendo yoote utakayoona
yanakuhusu mara baada ya kuvisoma
vitabu hivi, natamani kusikia shuhuda
kutoka kwako vile kinaenda
kukusaidia, usiache kutendea kazi kile
ulichojifunza na usiache kunipa
mrejesho wa matokeo utakayoyapata.

104
Hitimisho

Kijana mmoja wa Kifaransa baada ya


kutongoza wanawake na
KUKATALIWA MARA KWA MARA,
alikwenda kwa mtaalamu Casanova,
enhee ikawaje👇

Casanova ni miongoni mwa TOP FIVE


SEDUCERS (Watongozaji Mahiri) na ni
mtu ambae amekuwa akifundisha
mbinu za kutongoza.

Alipofika ofisini akionesha kukata


tamaa akamuuliza "What Should i do
to make women attracted to me" (nini
naweza kufanya ili wanawake
wavutiwe namimi)

105
Casanova akamwambia "Bro, Make
Sure You Build a Beautifull Garden
and Butterfly will come for it"
alipomaliza kusema hayo akaendelea
na shughuli zake.

Alimaanisha nini, alichomaaanisha ni


hiki hapa, "Bwana Mdogo, Hakikisha
unaunda Bustani Nzuri na Vipepeo
watakuja kwaajili ya hiyo bustani"

Casanova akaona bwana mdogo


hajaelewa, akaongeza kusema "Focus
on building yourself to become a
HIGH VALUE MAN, any woman is
loving to be in touch with HIGH value
MAN"

Akajizungusha katika kiti chake then


akavuta chupa ya wine akapiga funda

106
moja akaendelea kusema "The Best
Investment you can make is in
yourself first"

Yule kijana akawa kama amewashiwa


taa gizani, amekutana na kitu
hajawahi kuambiwa, akakubaliana na
Casanova kuwa kuanzia hapo
atabadilisha vipaumbele vyake tofauti
na mwanzo.

Ushauri wa buure kwa vijana wa


kiume; Kama unahitaji vipepeo, basi
usipoteze muda kuwafukuzia
vipepeo, poteza muda wako mwingi
kutengeneza bustani nzuri na vipepeo
watakuja wenyewe.

Kila mwanamke anapenda kuwa na


mwanaume mwenye hadhi ya juu, so

107
badala ya kuendelea kusumbuka na
wanawake sumbuka kuwa
mwanaume mwenye hadhi ya juu
(High Class Man)

Wanawake ni kama vipepeo, kila


kipepeo hupenda na huvutika kukaa
katika bustani yenye maua mazuri na
yanayovutia ndani yake, so na wa
wanawake wanapenda vitu vizuri.

Usiwe aina ya mwanaume ambae


unataka mwanamke adate nawewe
kwa kukuonea huruma, mfanye aone
na ajue kuwa kuna sababu ya yeye
kudate na mwanaume kama wewe.

Kama ukiruka STAGE ya kujijenga,


kujitengeneza na kujiongezea
THAMANI, nipo hapa kukwambia

108
kuwa wanawake watakuruka pia,
trust me or not.

Kila mwanamke unaemuona


anamtaka mwanaume ambae
mwanamke atajivunia kuwa nae, fika
level ambayo mwanamke wako
ajivunie kuwa nawewe.

Na uzuri ni kwamba, kadri thamani


yako inavoongezeka ndivyo
unavyozidi kupunguza matumizi ya
nguvu katika kumpata mwanamke,
nina ushuhuda katika hili.

Sikiliza Master, You will loose time


and alot of money by chasing women,
but youll never loose women by
become a HIGH VALUE MAN.

109
Unaweza kupoteza fedha nyingi na
muda kuwafukuzia wanawake, ila
huwezi kukosa mwanamke endapo
utakuwa mwanaume mwenye
THAMANI.

So, focus on building yourself chief,


pigania ndoto zako, jiongezee
thamani mwanangu, tafuta fedha
mkaka, boresha maisha yako mzee,
wekeza sana then booom.

The more your life become well, more


you become attractive to ladies
(maisha yako yanavyozidi kuwa bora,
ndivyo mvuto wako kwa wanawake
unaongezeka)

Kipaumbele chako cha kwanza kama


mwanaume kinatakiwa kiwe ni

110
KUTENGENEZA FEDHA NYINGI
ikiwezekana uajiri vijana wenzako, na
ninaamini unaweza kamanda.

Tafuta fedha kwa hasira kama


unavyolitafutaga bao la tatu (hahaha),
kamia kusaka mpunga kama
unavyokamiaga kitandani ukiwa na
pisi iliyokusumbuaga (hahaha)

Sure mzee, mi nakwambia coz haya


mambo nimeyashuhudia, hakuna
mwanamke anamtaka mwanaume wa
kawaida, add your value mwanangu
ninaekukubali sana.

Fika hatua ambayo ukimtongoza


mwanamke awe anajua kabisa
kwamba haujaenda kwake kwa

111
sababu umekosa wengine au ye ndo
kimbilio la mwisho.

Kadri ambavyo thamani yako


inavoongezeka ndivyo unavyokuwa
na machaguo mengi ya wanawake,
your value increases OPTIONS.

So, nguvu unayoweka kuwatafuta


ihamishie kama ilivyo kwenye
kutafuta life, kumake more money na
kuboresha maisha yako yawe bora
zaidi ya yalivyokuwa jana na juzi.

Na kama leo kuna mwanamke


anakuchukulia poa kwa sababu bado
ni KABWELA, huna HELA, maisha
yako ni magumu basi👇

112
Zikusanye dharau zake zoote
uzimeze kama zilivyo then zikutie
MIHASIRA ya kupambana kinouma ili
upate FEDHA na HADHI anayoitaka,
alafu👇

Ukiipata hakikisha haudate nayeye,


nenda kachomoke na pisi moja kali
inayomjua Mungu, ambayo haina
mbambamba na inayokuelewa then
ishi nayo hiyo.
By the way, kama unahitaji
kutengeneza fedha ili kuyaboresha
maisha yako na haujui pakuanzia.

Nashauri usome kitabu changu


kinachoitwa MONEY PASSCODE
akitakachokusaidia kujua Siri
Zitakazokusaidia Kupata Mafanikio
Ta Kifedha.

113
Tumia namba 0654722733
kuwasiliana nami kupitia whatsapp na
utajipatia kitabu ukiwa sehemu
yoyote duniani.

114
Orodha ya Vitabu Vya Isaack
Nsumba

1. Sanaa Ya Utongozaji 01 |
Kinafundisha Namna Ya Kuwa
Mwanaume Mwenye Mvuto na
Ushawishi Kwa Mwanamke.

2. Sanaa Ya Utongozaji 02 |
Kinafundisha Namna Ya Kuwa
Mwanaume Mwenye Mvuto na
Ushawishi Kwa Mwanamke.

3. Money Passcode | Kinafundisha


Siri Zitakazokusaidia Kupata
Mafanikio ya Kifedha.

4. Biashara Mtandaoni | Kinafundisha


Muongozo Utakaokusaidia
Kujitengenezea Kipato Kupitia
Mtandao.

115
5. Huyu Ndiye | Kinafundisha
Muongozo Utakaokusaidia
Kumtambua Mwenzi Sahihi.

6. Muache Aende | Kinafundisha


Mbinu Za Kutumia Ili Kumsahau Mtu
Anaekuumiza, Asiyekupenda Wala
Kukuthamini.

7. Lugha Tano Za Msamaha |


Kinafundisha Namna Ya Kuomba
Msamaha Unaoponya Majeraha ya
Mwenzi wako na Kukufanya
Usamehewe.

8. Usimuache Aende Zake |


Kinafundisha Namna Ya Kumtunza Na
Kumlinda Mwenzi Wako Pamoja Na
Kudumisha Uhusiano Wenu.

116
9. The Golden Woman | Kinafundisha
Tabia Zinazomvutia Mwanaume Kwa
Mwanamke Na Namna Ya Kuwa
Mwanamke Wa Tofauti.

10. Mwanamke Mashine |


Knafundisha Uwezo Wa Kipekee Ulio
Ndani Ya Mwanamke Na Namna Ya
Kuutumia Ili Kuleta Mafanikio.

11. Emotional Muscles | Kinafundisha


Namna Ya Kukabiliana Na Hisia Kama
Vile Wivu, Hasira, Huzuni Pamoja Na
Hofu.

12. Boresha Mahusiano Yako |


Kinafundisha Mambo Ya Kufanya Ili
Uwe Na Mahusiano Bora Na
Utayoyafurahia.

117
13. Sanaa Ya Mawasiliao Katika
Mahusiano | Kinafundisha Namna Ya
Kuwasiliana Kwa Ufanisi Pamoja Na
Kutatua Changamoto Za
Kimawasiliano.

14. Maisha Ni Kusudi | Kinafundisha


Namna Ya Kuligundua Na Kuliishi
Kusudi La Kuumbwa Na Kuwepo
Kwako Dunaini.

15. Sanaa Ya Kutoa Na Kupokea


Katika Mahusiano | Kinafundisha
Namna A Kutoa Katika njia Inayogusa
Moyo wa Mpokeaji, Na Kupokea
Katika Namna Inayogusa Moyo wa
Mtoaji.

118
16. Dhihirisha Uanaume Wako |
Kinafundisha Namna Ya Kuwa Vile
Impasavyo Mwanaume Kuwa.

17. Mwongozo Wa Usomaji Wa


Vitabu | Kinafundisha Namna
Unavyoweza Kuwa Msomaji Mzuri Wa
Vitabu Na Nwenye Mafanikio Katika
Usomaji.

18. Namna Ya Kuuteka Moyo Wa


Mwanaume | Jinsi Ya Kumpata
Mwanaume Umtakae Au Kumteka
Mwanaume Uliyenae.

19. Hatua Za Kufuata Ili Kurudiana Na


Ex Wako | Kinafundisha Hatua Kwa
Hatua na Namna Unavyoweza
Kumrudisha Ex Wako Pamoja na
Kufufua Penzi Lililokufa Au Kupooza.

119
20. Shule Ya Biashara | Siri
Zitakzokusaidia Kufanikiwa Katika
Biashara Yako, Namna ya Kuisimamia
na Kuikuza.

NB: Vitabu vyote vimeandikwa kwa


lugha ya Kiswahili na unaweza
kuvipata kupitia namba 0654722733
(TUMA UJUMBE WHATSAPP).

120
Tembelea Mitandao Ya Kijamii Ya
Isaack Nsumba Ili Kujifunza Zaidi

Youtube: Isaack Nsumba


(Utapata VIDEO Nyingi Za
Kukufundisha Mambo Mbalimbali)

Instagram: Isaack Nsumba


(Utapata Mafunzo Kila Siku
Yatakayokusaidia)

Facebook: Isaack Nsumba


(Utapata Mafunzo Kila Siku Na Pia
Shuhuda Mbalimbali)

Twitter: Isaack Nsumba


(Utapata Mafunzo Kila Siku
Yatakayokusaidia)

121
Tiktok: Isaack Nsumba
(Utapata Video Fupifupi Kila Siku
Zenye Uwezo Wa Kukuongezea
Ufahamu Zaidi)

122
Kuhusu Mwandishi
Isaack Nsumba, ni mwandishi wa
vitabu, Makala na Muandaaji wa
Maudui (Content Creator) lakini pia ni
mwalimu mbobevu (An Expert
Teacher) katika masuala yoote
yanayohusu Mahusiano, Uchumba,
Ndoa, Malezi, Uchumi pamoja na
Uongozi.
Kitaaluma Isaaack ni muhitimu wa
masomo ya Sanaa na Elimu (Bachelor
of Arts with Education) kutoka Chuo
kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAINT
AUGUSTINE UNIVERSITY OF
TANZANIA).
Mwaka 2022 alitajwa kama
mwandishi bora chipukizi (The Best
Young Author) na kutunukiwa tuzo ya

123
mwandishi bora chipukizi Tanzania
(The Best Young Author Award in
Tanzania)
Isaack ni Mkurugenzi (Chief Executive
Officer) na mwanzilishi wa taasisi ya
Wisdom For Winning inayohusika na
utoaji wa elimu ya kujitambua, Elimu
ya Mahusiano, Uchumba, Ndoa,
Malezi, Uchumi pamoja na Uongozi
ambayo ndiyo anayoiongoza kwa
sasa.
Kwahiyo, ukiwa unamuhitaji kwaajili
ya semina za vijana, wanawake au
wanaume, semina uongozi, semina za
uchumi, fedha na biashara pamoja na
makongamano yoote ya kanisani
unaweza kuwasiliana na namba
zilizopo katika kitabu hiki kwa kutuma
kupitia whatsapp.

124
Shuhuda Za Watu Walisoma Sanaa
Ya Utongozaji 02 Na Namna
Kilivyowasaidia

125
126
127
128
129
130
131
132
133
134
135

You might also like