You are on page 1of 109

KUBALI HIVI SASA

Mwl. Elisha Mwakalinga

1
KUBALI HIVI SASA
Hakimiliki zote zipo chini ya ©Elisha Daudi
Mwakalinga

Simu: +255 653 864 907 (Calls/sms)

+255 768 671 298 (whatsapp)

Barua Pepe: elishadaudi3@gmail.com

emwakalinga@myfaithlife.co.tz

ISBN: 978-9976-5267-3-8

Dar es Salaam, Tanzania

©2022

Haki zote zimehifadhiwa: Hairuhusiwi kuzalisha,


kusambaza, kunakili wala kurekodi kitabu au sehemu ya
kitabu hiki pasipo ruhusa ya maandishi kutoka kwa
Mwandishi

Kimechapwa na
Truth Printing
0764 425 704/0692 637 282
geofreymakula@gmail.com
Dar es Salaam-Tanzania

2
YALIYOMO
SHUKRANI ZA PEKEE ..................................................................... 5
WALENGWA ......................................................................................... 6
UTANGULIZI ..................................................................................... 7
Sura ya Kwanza .............................................................................. 10
KUWA MMOJA WAO ..................................................................... 10
Sura ya Pili ....................................................................................... 26
WEKEZA KWA WATU ................................................................... 26
Sura ya Tatu .................................................................................... 34
JENGA TABIA ................................................................................. 34
Sura ya Nne ..................................................................................... 40
KUBALI KULIPA GHARAMA......................................................... 40
Sura ya Tano ................................................................................... 54
USILISHE NJAA LISHA MAONO ................................................. 54
Sura ya Sita...................................................................................... 69
TENGENEZA MFUMO WAKO WA MAOMBI ............................. 69
Sura ya Saba ................................................................................... 74
WATU WAKUU HUANDALIWA SIRINI ....................................... 74
Sura ya Nane ................................................................................... 86
JIBORESHE ..................................................................................... 86
Sura ya Tisa ..................................................................................... 92
UPINZANI NI SEHEMU YA MAISHA UNAPOINGIA HATUA
NYINGINE ........................................................................................ 92

3
Sura ya Kumi ................................................................................... 96
TUMIA UWEZO WAKO WOTE..................................................... 96
Sura ya Kumi na Moja .................................................................. 101
USIOGOPE CHUKUA HATUA.................................................... 101
IKIWA HAUJAOKOKA NA UNATAKA KUMPA YESU MAISHA
YAKO .............................................................................................. 107

4
SHUKRANI ZA PEKEE
Shukrani zangu za dhati ni kwa Mungu Baba wa
Mbinguni aliyeniwezesha kwa msaada wa Roho
Mtakatifu kukamilisha kazi hii mpaka ikatoka.

Mama yangu mzazi Lucy Kalile, dada zangu


Happy, Mariam na Sifa, Mungu awabariki sana kwa
jinsi mnavyoendelea kuwa Baraka kwa kuniombea,
kunitia moyo na kunishauri. Mungu awazidishie
mema.

Wazazi wangu wa kiroho Mchungaji Ibrahimu na


Omega Munanka, Mungu awabariki kwa malezi yenu
ya kiroho, ushauri, maombi na kunitakia mema.
Mungu awazidishie Baraka katika utumishi wenu.

Marafiki zangu wote kila mtu kwa jina lake,


waliohusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha
kazi hii kutoka, Mungu awabariki sana jamani.
Ninaheshimu mchango wa kila mmoja. Ninawaombea
Baraka tele nan a neema za Mungu kwenye kazi na
utumishi wenu.

Mwisho lakini si kwa umuhimu, ninakushukuru


sana wewe ndugu yangu uliyepata neema ya kusoma
kitabu hiki, ninaomba kisiwe kitabu cha kawaida
kwako. Nguvu za Mungu zikufunike unaposoma na
utakapomaliza Mungu akupe hatua mpya katika Jina
la Yesu.

5
WALENGWA
Walengwa wa kitabu hiki ni watu wote wa kike
na wa kiume ambao wanajua Mungu amewaita
kumtumikia katika nyanja mbalimbali,
watumishi vijana ambao tayari wanaendelea na
huduma, walezi na wazazi ambao wanatamani
vijana wao wafikie ndoto kubwa za kulitumikia
shauri la Mungu. Neno hili limetoka kwa Bwana
nalo ni ajabu machoni petu (Zaburi 118:23)

6
UTANGULIZI
Tangu zamani Mungu amekuwa akiwaita watu
mbalimbali makundi kwa makundi ili wamtumikie
Mungu katika huduma na maeneo mbalimbali. Japo si
wengi wanajua kitu ambacho Mungu ameweka ndani
yao, lakini angalau wanasikia wito wa kutumika. Swali
langu ni hili; Kanisa au jamii imejipangaje kulea,
kutunza na kukuza vipawa hivyo ndani ya watu hasa
vijana? Ni kweli kwamba wana vitu vizuri na vikubwa
ndani yao lakini je! Nani anajali malezi yao ili kesho
waweze kufikia pale walipokusudiwa?

Tuna kundi kubwa la vijana na watumishi


wanaoinuka na vitu vizuri lakini hawadumu, baada ya
muda mchache wanapotea kabisa. Ni ukweli kwamba
hata ukiwa na kitu kizuri namna gani, usipojua
thamani yake, ukakosa muda wa maadalizi na namna
bora ya kukitumia basi kitu hicho hakiwezi kukuletea
manufaa yoyote.

Kitabu cha Luka 12:47-48 anasema hivi “Na


mtumwa yule asiyejua mapenzi ya bwana wake,
asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake,
atapigwa sana” Katika mistari hii amezungumza
mambo matatu; Jambo la kwanza ni kujua mapenzi ya
Mungu, pili ni maandalizi na jambo la tatu ni kutenda
sawasawa na mapenzi/makusudi ya Mungu. Kujua
mapenzi ya Mungu (Kusudi) haitoshi peke yake
kukufanya uyatende kwa ubora kama atakavyo

7
Mungu, unahitaji muda wa kutosha wa maandalizi
ambao ndani yake umebeba kukuandaa kimwili, kiroho
na kiakili kusudi utakapoanza kuyatenda uweze
kutenda kwa ubora mkubwa. Lakini pia muda wa
maandalizi ndio unaotengeneza msuri wako na uimara
wako kiasi ambacho utakapoanza safari uweze
kuendelea vizuri pasipo kuyumbishwa njiani.

Anatuonesha tena kwamba mtumwa yule asiyejua


mapenzi ya bwana wake (kusudi aliloumbiwa kulifanya
akiwa hapa duniani), na asijiweke tayari (Asiye na
muda wa kujiandaa kufanya yote aliyoagizwa) na wala
asitende sawasawa na makusudi hayo, atapigwa sana.
Fahamu kwamba siku ya mwisho utatoa hesabu ya
kazi uliyofanya kulingana na kusudi ulilokuwa
umeumbiwa kufanya hapa duniani. (Tafuta kitabu
changu nilichozungumzia juu ya Kusudi ili uweze
kujenga uelewa wa kutosha)

Ndani ya kitabu hiki Mungu ametuongoza


kukuwekea mambo muhimu yatakayokusaidia hatua
kwa hatua kukua na kutumia kila ulichopewa kwa
ubora na matokeo makubwa.

Kuna watu hawajawahi kuambiwa wanatakiwa


kufanya nini baada ya kuwa wamesikia wito ndani yao,
lakini wakikosea ndipo watu huwasema vibaya na
kuwakatisha tamaa; kitabu hiki ni msaada kwako,
utakapokuwa unaendelea kusoma, kitakuwa kinajibu

8
swali lako moja baada ya jingine na kukuwekea ndani
yako msingi mkubwa kuelekea kwenye ndoto na maono
uliyo nayo.

“Yesu akajibu akamwambia, Kubali hivi sasa;


kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.
Basi akamkubali.” Mathayo 3:15. Mungu
anapokuandaa kwa ajili ya utukufu mkubwa mbele
yako, hauna budi kupitia mchakato ambao utakuwa ni
msingi wa kule unakoelekea. Kimsingi Yohana
hakustahili kumbatiza Yesu, lakini kwa ajili ya
kutimiza maandiko na utukufu mkubwa uliokuwa
mbele yake, alikubali. Kubali hivi sasa maana kesho
yako imebeba utukufu mkubwa.

Maisha ya ukuu yana siri kubwa na


wanaofanikiwa kuzijua siri hizo wanakuwa kwenye
nafasi kubwa ya kufanikisha kila wazo jema ndani yao.
Ndugu msomaji, Mungu akufungue macho uweze
kuziona siri hizo na maisha yako hayatabaki kama
yalivyokuwa katika Jina kuu la Yesu Kristo. Amen!

9
Sura ya Kwanza
KUWA MMOJA WAO

K
atika karne hii tuliyonayo, bado Mungu
anatafuta watu wa kufanya nao kazi, watu
ambao atatukuzwa kwa sababu yao, watu
ambao watamfanya Mungu ajulikane. Macho yake yapo
kila mahali kuangalia watu wa namna hiyo. Najua ni
wengi waliookoka lakini walio tayari kutumika kwa
ajili ya Mungu sio wengi, walio tayari kuyatoa maisha
yao jumla kwa ajili ya Mungu na Ufalme wake hawapo
kila mahali, ni kundi dogo sana.

Elisha anatajwa kuwa na sifa za pekee sana


ambazo kwa nyakati zake zilimfanya atumike kwa
viwango visivyokuwa vya kawaida. Kumbuka kwamba;
sifa hizi au mambo haya hayakumshawishi Mungu ili
amtumie Elisha, bali yalipoonekana kwake yalifanya
atumiwe kwa namna ya pekee sana. Mambo hayo ni
kama yafuatayo;

1. Mtu mtakatifu wa Mungu.

Tunaposoma 2 Wafalme 4:8-9 tunaona jambo hili


kwamba; “Hata ikawa siku moja, Elisha
alikwenda Shunemu; na huko alikutana na
mwanamke mmoja mwenye cheo; naye

10
akamshurutisha aje ale chakula. Ikawa kila
alipopita njia ile, huingia kula chakula. Yule
mwanamke akamwambia mumewe, Tazama,
mimi naona ya kuwa mtu huyu apitaye kwetu
mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu.”

Huyu mama tunayesoma habari zake hapa


hakuwa mtu mwenye dhiki, alikuwa ni mtu mwenye
cheo na tajiri. Kuna kitu anatuonesha alichokuwa
nacho Elisha, kwamba huyu ni mtu mtakatifu wa
Mungu. Elisha alipokuwa Shunemu alipokutana na
huyu mama alimshurutisha aende kwake apate
chakula, na akawa akienda mara kwa mara kupata
chakula akipita njia ile; sasa ajabu ni kwamba yule
mama alikuwa akimdadisi na kumchunguza Elisha
bila yeye kujua, kama ilivyo kawaida ya akina mama
kudadisi na kuchunguza mambo. Baadae anakuja
kumweleza mumewe kwamba mtu anayekuja kula
chakula hapa; “Mimi nimemchunguza na
kumwangalia kwa karibu nimegundua ni mtu
mtakatifu wa Mungu” (Maelezo ya ziada haya ni
yangu), akamwomba wamjengee chumba ili awe
analala hapo.

Je! Watu wanapokutazama wanaona nini?


Wanakuja na jibu la namna hii au kuna namna
nyingine wanaona kwako? Watu wanaweza kukuona
kama mfanyabiashara mashuhuri, mfanyakazi bora au
mtaalamu wa kitu fulani lakini hawapaswi kukosa

11
kuiona sifa hii kwanza kwamba wewe ni mtu mtakatifu
wa Mungu.

Najua tunao wachungaji, wainjilisti, waimbaji


wengi sana na wengine wanaendelea kuchipukia,
watumishi mbalimbali na wakristo kwa majina yao,
lakini je tunao watu watakatifu wa Mungu? Ni swali la
muhimu sana tunalopaswa kujiuliza kila wakati.
Mabadiliko makubwa na uamsho katika kanisa
yanahitaji wapatikane watu watakatifu wa Mungu
watakaoweza kusababaisha uamsho na kufanya
Mungu ajulikane.

Unaweza ukajiita mtu mtakatifu wa Mungu lakini


sifa njema ni vizuri ikatoka kwa watu kuja kwako na
sio itoke kwako mwenyewe (2 Wakorintho 3:1). Kama
huyu mama Mshunemu alipomtazama Elisha na
mwenendo wake siku kwa siku kadiri alivyokuwa
anafika nyumbani kwake, akaseama “Naona ya kuwa
mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu
mtakatifu wa Mungu”

Tunahitaji wanaume na wanawake watakatifu wa


Mungu, katika Kanisa, kwenye jamii, kwenye biashara
na miradi mbalimbali, maofisini na hata kwenye siasa
na Serikali. Tukipata watakatifu wa Mungu Serikalini
watatusaidia kusimamia haki sawasawa na
kumuwakilisha Mungu vizuri kwenye nafasi zao.
Tukipata walimu na wakufunzi watakatifu wa Mungu

12
mashuleni na vyuoni, basi kwa sehemu kubwa
tutaokoa kizazi hiki ambacho wengi maisha yao na
ndoto zao zinaishia njiani. Tunahitaji vijana wenye sifa
hii ya utakatifu wa kweli ili kuleta mabadiliko chanya
katika nyanja zote.

Kama Wakristo waamini, Roho Mtakatifu anakaa


ndani yetu na kazi yake mojawapo ni kutusaidia ili
tuwe watakatifu kama yeye Mungu alivyo Mtakatifu (1
Petro 1:15-16) usitafute kuwa mtakatifu kwa sababu
unataka Mungu akutumie kwa viwango vikubwa, bali
tafuta kuwa mtakafitu kwa sababu Baba yako aliye
mbinguni (MUNGU) ni Mtakatifu. Tutafute kuwa
walimu watakatifu wa Mungu, wachungaji watakatifu
wa Mungu, wainjilisti watakatifu wa Mungu, manabii
watakatifu wa Mungu, waimbaji watakatifu wa
Mungu, wana michezo watakatifu wa Mungu,
wafanyabiashara watakatifu wa Mungu, akina baba na
akina mama watakatifu wa Mungu. Huu ndio wito
mkuu ambao mimi na wewe tusipokuwa nao hatuwezi
kumwona Mungu siku ile.

Ile kwamba Mungu anakutumia kugusa maisha ya


watu haina maana kwamba wewe ni mtakatifu wake,
anafanya tu kwa sababu ya huruma na upendo alionao
kwa watu unaowahudumia lakini si kwamba njia zako
zinamfurahisha. Tafuta utakatifu wa kweli katika njia
zako zote,

13
Mambo yanayosababisha kukosekana kwa
utakatifu wa kweli siku hizi za mwisho.

i. Kukosa nidhamu.

Inahitaji nidhamu ili kuishi maisha matakatifu,


nidhamu katika miili yetu, nidhani katika vinywa
vyetu nini useme na nini usiseme. Paulo anasema
“Bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha;
isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe
niwe mtu wa kukataliwa.” 1Kor 9:27. Tunahitaji
kuwa na nidhamu juu ya nini tunasikia, nini tunaona
na kutazama maana hatuwezi kuwa tunasikia vitu
visivyofaa halafu wakati huo huo masikio yetu yaweze
kuisikia sauti ya Mungu. Watu wengi wanahangaika
kuishi maisha matakatifu kwa sababu macho yao
wameyaruhusu kuangalia visivyofaa kama picha za
utupu, video za ngono na baadae wanajikuta wanaishia
kuanguka kila wakati. Unahitaji nidhamu, kuutesa na
kuutumikisha mwili wako kwa ajili ya Mungu.

Unahitaji nidhamu katika matumizi yako ya


muda, nidham katika kulala; kulala ni kuzuri sana
lakini kulala kulikopitiliza hupelekea umasikini bila
habari, unahitaji nidhamu katika mtindo wako wa
maisha ya kila siku kwa ujumla wake. Maisha
yaliyokosa nidhamu ni maisha yanayoelekea mwisho
mbaya na usio na matumaini yoyote.

14
ii. Kukosa muda na Mungu.

Mara nyingi tunataka mikusanyiko, tuombe


tukiwa wengi maana ndio inanoga, ni kweli na ni nzuri,
lakini je unao muda wako binafsi na Mungu? Sote
tunajua baada ya Musa kukaa siku arobaini mlimani
pamoja na Mungu alishuka uso wake ukiwa
umebadilika, unang’aa hata Israeli wote walishindwa
kumwangalia Uso wake. Yesu masihi alitafuta mahali
pa faragha pasipo na watu akakaa huko kuomba peke
yake (Mathayo 14:23) unapokosa muda wa kukaa na
Mungu unakosa nguvu pia ya kukusaidia kuishi
maisha matakatifu, maana tumeumbwa ili tukae na
Mungu katika uwepo wake, nje ya uwepo wake ni kifo.
Utakatifu nje ya uwepo wa Mungu ni mzigo
usiochukulika. Tafuta na boresha muda wako binafsi
na Mungu ili upate nguvu za kukusaidia kuishi kwa
utakatifu.

2. Mtumishi.

Jambo la pili tunalotazamishwa kwa Elisha ni ile


roho ya kitumishi iliyokuwa ndani yake. Tunaposoma 2
Wafalme 3:11-12 inasema “Lakini Yehoshafati
akasema, Je! Hapana hapa nabii wa BWANA, ili
tumwulize BWANA kwa yeye? Akajibu mtumishi
mmoja wa mfalme wa Israeli, akasema, Yupo
hapa Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa
akimimina maji juu ya mikono yake Eliya.

15
Yehoshafati akasema, Neno la BWANA analo
huyu.” Huyu Elisha hakuwa tu anamimina maji
kwenye mikono ya Eliya, amewahi pia kufanya mambo
makubwa sana ikiwemo kuyapiga maji ya mto wa
Yordani yakagawanyika huku na huku naye akavuka
akiwa mwenyewe (2 Wafalme 2:14), Wana wa Manabii
walipomwambia kwamba nchi inazaa mapooza,
alifanya ule muujiza wa kuyaponya maji (2 Wafalme
2:19-22) Mwanamke mmojawapo wa wana wa manabii
alipompelekea kesi kwamba watoto wake wanataka
kuchukuliwa utumwani ili kulipa deni ambalo mume
wake aliliacha. Elisha alisababisha muujiza kwa yule
mama (2 Wafalme 4:1-7) pamoja na miujiza mingine
mingi aliyofanya, Elisha alikuwa akijulikana kama
mtu aliyekuwa akimimina maji kwenye mikono ya
Eliya.

Roho ya utumishi iliyokuwa ndani yake ilifanya


baadae atumike kwa mambo makubwa sana. Yesu
anasema yeye hakuja kutumikiwa bali kutumika na
kuutoa uhai wake kwa ajili ya wengi (Mathayo 20:28)
roho ya kupenda kutumika ndiyo iliyokosekana katika
kizazi chetu. Kila mtu anataka kuwa mkubwa wa
wengine, kila mtu anataka kuwa juu ya wengine, kisha
atoe amri au maagizo ambayo wengine wayatekeleze
huku yeye yakiwa hayamuhusu. Yesu akawaambia
wanafunzi wake “Bali mtu yeyote anayetaka kuwa
mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu” Mathayo
20:26. Ukitaka kuwa mkubwa kuwa mtumishi kwanza,

16
vivyo hivyo ukitaka kufikia hatma kubwa huna budi
kuvaa roho ya utumishi.

Wafilipi 2:7 “Bali alijifanya kuwa hana


utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana
mfano wa mwanadamu” Roho ya utumishi ndani
yako haiwezi kuambatana na kupenda masifa na
kutaka kujulikana. Siku hizi za mwisho ni kama tupo
kwenye mashindano, kila mtu anataka awe juu,
atokeze na chake au aonekane anajua na wengine
hawajui. Biblia inasema Yesu alijifanya kuwa hana
utukufu, akatwaa namna ya mwanadamu, halafu
anaendelea kusema akajinyenyekeza akawa mtii hata
mauti; alijifanya hajui kitu, alijivika unyenyekevu,
akawa mtii, alipotukanwa hakurudisha tusi,
alipotendewa jambo baya hakurudisha, alikuwa mtii
hata mauti ya msalaba.

Baada ya tendo lile na maisha yale ya


unyenyekevu, kujifanya hana utukufu, kutii hata
mauti ya msalaba, “Mungu alimwadhimisha mno,
akamkirimia Jina lipitalo kila Jina.” (Wafilipi 2:8-
9). Kanuni ya kukusaidia kufikia hatima yako na ndoto
zako kubwa haijabadilika, ni lazima kujivika roho ya
utumishi ndani yako ambayo imebeba unyenyekevu na
utii. Hakuna mkato katika jambo hili, unaweza
ukakwepa kanuni hii lakini hata ungefika wapi kama
hauna roho ya utumishi ndani yako utatofautishwa na
waliyonayo.

17
3. Mpakwa mafuta wa Mungu.

“Kisha akaliokota lile vazi la Eliya


lililomwangukia, akarudi, akasimama katika
ukingo wa Yordani. Akalitwaa lile vazi la Eliya
lililomwangukia, akayapiga maji, akasema, Yuko
wapi BWANA, Mungu wa Eliya? Naye alipoyapiga
maji, yakagawanyika huku na huku, Elisha
akavuka. Na hao wana wa manabii,
waliokuwako Yeriko wakimkabili, walipomwona,
walisema, Roho ya Elya inakaa juu ya Elisha.
Wakaja kuonana naye, wakainama kifudifudi
mbele yake.” 2 Wafalme 2:13-15

Hawa wana wa manabii walikuwa wanafunzi


wazuri na waliyajua maandiko vizuri na walijua vizuri
maana yake nini mtu kuitwa mpakwa mafuta wa
Mungu. Hawakuwa wameona akihubiri mahali,
hawakusubiri waone akitoa ushuhuda ndipo wajue
huyu ni mpakwa mafuta, bali walipoona akigawanya
mto Yordani kwa lile vazi lililomwangukia kama
alivyofanya Eliya waliishia kusema huyu ni mpakwa
mafuta wa Mungu.

Mafuta ya Roho Mtakatifu ni muhimu sana kama


tunataka kulifanya kusudi la Mungu katika huduma
zetu. Biblia inasema katika kitabu cha Matendo ya
Mitume 10:38 kwamba “Habari za Yesu wa
Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa

18
Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko
na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote
walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu
alikuwa pamoja naye.” Tunaweza kuwa na pesa
nyingi, muziki mzuri kwenye makanisa yetu na kila
kitu kinachohitajika, lakini kama tutakosa mafuta ya
Roho Mtakatifu na nguvu zake basi itakuwa ni sawa na
bure. Mafuta ni nguvu za Roho Mtakatifu za
kutusaidia kutimiza kila kusudi lake ndani yetu. Kama
tunaweza kufanya kazi ya Mungu pasipo nguvu za
Mungu ni bora sana kama tukiacha na kutafuta kazi
zingine za kufanya. Tunatakiwa tufike hatua ambayo
hatuwezi kutekeleza chochote katika huduma zetu bila
nguvu za Mungu.

Siku hizi kuna changamoto kubwa ya kujua yapi ni


mafuta halisi ya Roho Mtakatifu ndani ya mtu.
Wengine hudhani ni ule ufasaha wa
kinachozungumzwa/mafundisho (1 Wakorintho 2:1, 4-5)
au hudhani ni zile hisia na kelele za mtumishi au ile
sauti nzito. Mafuta ya Roho Mtakatifu ni nguvu za
Mungu ndani ya mtu. Tunatakiwa kuona nguvu za
Mungu na sio maneno matupu au ufasaha wa jambo.
Siku hizi utakuta vijana wengi wanahangaika
kutengeneza sauti ziwe nzuri,, waimbe kwa ufasaha na
ustadi jambo ambalo sio baya hata kidogo, lakini
usisahau kwamba kinachoweza kubadilisha watu sio
ufasaha wa sauti au maneno katika wimbo
unaoimbwa,bali nguvu za Mungu ndani yako.

19
Osinachi Kalu Okoro Egbu maarufu kama
Sinach mwimbaji wa nyimbo za kuabudu nchini
Nigeria na duniani alipohojiwa kuhusu siri ya sauti
yake alieleza mambo matano kama siri ya watu
kuguswa na kubarikiwa kila anapoimba. Akiendelea
kuzungumza alisema “Watu wanaweza kukumbuka
wimbo ambao umeimba, lakini hawawezi
kusahau mguso na mtembeo wa nguvu za Roho
Mtakatifu ulipokuwa unaimba, hawawezi
kusahau jinsi Roho Mtakatifu alivyosema nao,
hawawezi kusahau jinsi Mungu
alivyowahudumia kila mmoja kwa namna
mbalimbali” Hili ndilo jambo la msingi sana kwa
waimbaji na watumishi wa Mungu.

Yesu alipokea nguvu alipopakwa mafuta (Mdo


10:38), hata alipowaambia mitume wakae Yerusalemu
walipokea nguvu (Mdo 1:8, 2:2-4) Petro alipata ujasiri
na kuanza kuhubiri katika mkutano wake wa kwanza
na jumla ya watu elfu tatu waliokolewa kwa sababu ya
ile nguvu aliyopokea (Mdo 2:14, 38-41)

Hatutakiwi kutosheka kwa sababu tuna vitu vingi


ndani yetu, wala kwamba tunaweza kuhubiri vizuri,
tunatakiwa kujiuliza swali hili wakati wote, je! Nguvu
za Mungu zipo ndani yetu? “Lakini nitakuja kwenu
upesi, nikijaliwa, nami nitafahamu, si neno lao
tu waliojivuna, bali nguvu zao. Maana ufalme wa
Mungu hauwi katika neno, bali katika nguvu.” 1

20
Wakorintho 4:19-20. Nguvu za Mungu bado zipo ndani
yako?

Sababu zinazoonesha kwanini Elisha alipakwa


mafuta.

Kumbuka unapotazama sababu hizi, ndani yako


yawe ni maombi kwa Mungu kwamba kama jinsi
mambo haya yalivyokuwa kwa Elisha yawe na kwenye
maisha yako na kuzidi.

1. Kiu na shauku kubwa.

Ukisoma 2 Wafalme 2:1-10 utaona Eliya


akimjaribu na kumpima Elisha katika kile alichokuwa
anatamani kukipata. Biblia inaeleza kwamba walitoka
Gilgali, Elisha alikataa kumuacha Eliya aende
mwenyewe, wakaenda Betheli pamoja bado Elisha
alimng’ang’ania Eliya, hata aliposhauriwa na wana wa
manabii kwamba Mungu atamchukua Eliya, bado
Elisha hakukubali kumuacha Eliya aende popote peke
yake. Walitoka Betheli kwenda Yeriko wote pamoja,
wakatoka Yeriko kwenda Yordani wote pamoja mguu
kwa mguu na hatua kwa hatua.

Wataalamu wanaeleza kwamba umbali wa kutoka


Gilgali kwenda Betheli ni sawa na maili 15 ambazo ni
sawa na kilomita 24, na umbali wa kutoka Betheli
kwenda Yeriko ni maili 12 sawa na kilomita 19, na
umbali wa kutoka Yeriko kwenda Yordani ni sawa na

21
maili 5 ambazo ni kilomita 8. Sasa jumla ya kutembea
kwao siku ile ilikuwa maili 32 ambazo ni sawa na
kilometa 51.

Tujiulize swali hili pamoja; kwanini Eliya


amzungushe mwenzake umbali wote huu ilhali alikuwa
anajua anachokitaka kwake? Bila shaka kuna jambo
Eliya alitaka kuliona kwa Elisha. Hata kama Biblia
haijasema alikuwa anataka nini, lakini tunaweza
kuona kwamba alitaka kuona uvumilivu, juhudi na
kutokukata tamaa/kuridhika njiani. Baadae tunaona
Elisha akirudi na upako mara dufu uliokuwa juu ya
Eliya.

Una kiu na shauku kiasi gani ya kuona unapakwa


mafuta, unatembea na nguvu za Mungu kwenye
huduma na utumishi uliopewa? Elisha alitafuta upako
huu kwa moyo wake wote, alijidhabihu mpaka akapata
alichokuwa anataka. Kiu yako ya kutaka kutembea na
Mungu, kumtaka Mungu na nguvu zake ipo kwa
kiwango gani? Tafuta kuwa na nguvu za Mungu zaidi
ya unavyotafuta kuwa maarufu, kuwa na fedha nyingi
au kupata mafanikio. Nguvu za Mungu ndani yako
zitayaleta yote hayo.

2. Nia safi.

Sababu nyingine ya Elisha kupakwa mafuta


ilikuwa ni nia safi na njema aliyokuwa nayo ya
kumtumikia Mungu. ukifuatilia toka walipokutana na

22
Eliya kwa mara ya kwanza na kuanza safari pamoja ya
kumtumikia Mungu, jinsi Elisha alivyojitoa (1 Wafalme
19:15-21) mpaka Eliya anaondoka machoni pa Elisha,
nia yake ilikuwa ni Mungu atukuzwe.

Sababu kubwa inayofanya watu wengi wasipokee


mafuta au nguvu za Mungu ni kwa sababu hawana nia
safi mbele za Mungu. Kila wanachofanya wanataka
waonekane wao, Mungu anakosa nafasi, ule moyo na
shauku ya kuona Mungu Mungu anatukuzwa,
anainuliwa na kujulikana umepotea ndani ya wengi,
hii ndio sababu pia tuna watumishi wa kawaida sana
(Ezekieli 9:1-6)

3. Hakuipenda dunia.

Hii ni sababu ya tatu ya Elisha kupakwa mafuta.


Hakuwa na chembe chembe zozote za kuipenda dunia.
Jambo hili tunaliona kwa ukubwa baada ya kukutana
na Naamani na kufanya muujiza ule wa ukoma
aliokuwa nao yule jemedari wa Jeshi la Washami.
Elisha alikataa kupokea chochote, hii inadhihirisha
wazi hakuwa na tamaa ya kupenda fedha lakini pia
alilinda sana mahusiano yake na Mungu na kile
alichopewa kisije kikanajisika kwa sababu ya sadaka.
Hakuwa anatafuta kujinufaisha kwa chochote katika
kazi ya Mungu, lakini Gehazi mtumishi wake kama
ilivyokuwa yeye Elisha kwa Eliya, kwa sababu ya
tamaa na kupenda kujinufaisha kwa kazi ya Mungu

23
alipokea ukoma badala ya mafuta ambayo
angeyapokea toka kwa Elisha.

Gehazi angekuwa na tabia kama alizokuwa nazo


Bwana wake Elisha basi tungeshuhudia mambo
makubwa ambayo angeyafanya kwa mikono yake
baada ya Elisha kuondolewa, lakini tabia yake ya
kuipenda dunia na kupenda pesa ilimfanya aishie
kupokea ukoma badala ya upako. Unaweza ukaingia
kwenye huduma vizuri na moyo mzuri kabisa, lakini
baada ya muda moyo wako ukageukia posho, sadaka na
bahasha unazopewa baada ya kutumika. Tamaa za
namna hii zimeua huduma za watu wengi. Huwezi
kuwa na tamaa za namna hii halafu utarajie upako,
mafuta na nguvu za Mungu, tafuta kimoja na elekeza
kila kitu chako hapo.

Mungu atusaidie sana kizazi cha sasa tupone


kabisa eneo hili. Kazi ya Mungu ibaki kuwa kazi ya
Mungu, ifanyike pasipo tamaa yoyote ile. Tukielekeza
nguvu zetu, kiu na shauku yetu kuutafuta uso wa
Mungu na nguvu zake basi upako huo huo ndio
utakaotutajirisha katika maeneo mengine ya maisha
haya.

Kubali hivi sasa kuwa mmoja wao, kubali kulipa


gharama ya kuutafuta uso wa Mungu na kuwa mtu wa
tofauti atakayetembea na nguvu za Mungu wakati
wote, kubali kuwa mtu mnyenyekevu, mtakatifu na

24
mpakwa mafuta wa Mungu. Wakati ulimwengu
unahangaika na namna yake, wewe baki katika
mambo haya, baada ya muda dunia itajua yuko Mungu
ndani yako na watu wataijia nuru yako.

25
Sura ya Pili

WEKEZA KWA WATU

“Ukiwainua watu, baadae hao watu watakuinua


wewe” Dr. Paul Enenche

M
oja ya mambo yaliyolikumba kanisa, jamii na
mtu mmoja mmoja ni ubinafsi wa kufikiri
ukiwekeza kwa watu basi baadae wanaweza
kukuzidi hivyo unajaribu kuweka wivu. Dr. Paul
Enenche anasema hivi "Ukiwainua watu, baadae watu
hao watakuinua wewe" hivyo hakuna unachopoteza.
Wekeza rasilimali zako kwa watu, muda wako, vipawa
vyako viguse maisha ya watu, haijalishi hata iweje,
huwezi kubaki chini au kuwa mtu wa chini. Kiwango
unachowekeza kwa watu ndio kiwango cha matokeo
utakayokuwa nayo kesho.

Daudi kabla hajawa mfalme, alikuwa na kundi la


watu 400 ambao walikuwa na dhiki, madeni na wale
waliokuwa na Uchungu mioyoni mwao (2Samweli
22:2), aliwekeza kwao na baadae wakawa mashujaa
waliokuja kumsaidia katika vita na kumuokoa
alipokuwa katika hatari ya kuuawa. (2Sam 23:8, 21:15-
17) Wekeza kwa watu, gusa maisha yao, washike
mkono na kuwainua kuelekea katika hatima zao na

26
kwa kufanya hivyo unakuwa umejitengenezea
barabara nzuri ya kuelekea katika mafanikio yako.

Huu ni ukweli usiopingika kwamba kwa kadiri


ambavyo unawainua wengine, ndivyo ambavyo na
wewe unazidi kuinuka na kuwa mahali pa juu zaidi.
Mchungaji na Apostle Samweli Lumbu aliwahi kusema;
“Unapowasaidia wengine kukua na kufikia kiwango
cha juu ndivyo na wewe unavyozidi kuwa juu zaidi”
aliongea hivi kwa sababu anajua faida ya kuwekeza
kwa watu. Akiendelea kuzungumzia jambo hili,
aliongeza kusema; “Watu watakapoona umeinuka na
kuwa mahali pa juu kiasi cha kuwa na ushawishi,
watauliza ulipita mikononi mwa nani?, na mwisho
watajua mchango wako kisha watakuheshimu” Hakuna
haja ya kuanza kuoneana wivu, unataka kuinuka?
Wainue wengine.

Ukiangalia mfano katika kitabu cha 1 Samweli 22:2


anasema, “Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya
dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu
wote wenye uchungu mioyoni mwao,
wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari
wao; nao waliokuwa pamoja naye walipata kama
watu mia nne.” Daudi alipokuwa katika kumkimbia
Sauli ili asiuawe ndipo akaenda katika Pango la
Adulamu, akakaa huko. Biblia inasema walimfuata
watu wenye dhiki, wenye madeni, na wale waliokuwa
na uchungu mioyoni mwao, wapata watu kama mia

27
nne hivi. Kumbuka wakati huo Daudi alikuwa sio
Mfalme bado, lakini kwa kile alichokuwa nacho alianza
kuwekeza kwa hao watu. Kwanza kushughulika na
hali walizokuwa nazo, kisha kuwakusanya wawe kitu
kimoja na kuwa jeshi kubwa na lenye nguvu sana
katika Israeli hakikuwa kitu chepesi. Umewahi kufikiri
kama walikuwa wanakaa pangoni, walikuwa wanakula
nini watu mia nne kila siku? Bila shaka kuna neema ya
Mungu ya ajabu iliyokuwa juu ya Daudi kuwawezesha,
lakini pia hawa watu hawakuwa watu wa kawaida.
Tafiti zinasema, miongoni mwao kulikuwa na askari
wengi wenye uzoefu waliotoroka kutoka makabila ya
mashariki, Benjamini na Yuda ili kuja kujiunga naye.
(I Nyakati 11:10-15)

Hili ndilo jeshi lililowapiga Waamaleki na kuwateka


nyara pamoja na kurudisha vitu vyote vilivyokuwa
vimechukuliwa mateka wakiwemo wake zao. “Naye
Daudi akawapiga tangu ukungu wa jioni hata
jioni ya siku ya pili; hakuna aliyeokoka, ila
vijana mia nne waliopanda ngamia na kukimbia.
Daudi akawapokonya wote waliochukuliwa na
Waamaleki; naye hakupotewa na kitu, mdogo
wala mkubwa, wana wala binti, nyara wala
chochote walichojitwalia hao; Daudi
akavirudisha vyote.”

Walikuwa ni mashujaa sana ambao baadae Daudi


alipokuwa mfalme walipewa nafasi za kuwa wakuu wa

28
vikosi mbalimbali. Angalia “Haya ndiyo majina ya
mashujaa aliokuwa nao Daudi...” 2 Samweli 23:8.
Watu hawa walimsaidia Daudi alipokuwa amechoka
asiweze kuuawa na adui zake, badala yake
wakasimama kupigana kwa ajili ya Daudi. “Basi
kulikuwa na vita tena kati ya Wafilisti na Israeli;
Daudi akashuka mpaka Gobu, na watumishi
wake pamoja naye, akapigana na Wafilisti; naye
Daudi akaishiwa na nguvu. Naye Ishi-benobu,
aliyekuwa mmojawapo wa Warefai, ambaye uzito
wa mkuki wake ulikuwa shekel mia tatu za shaba
kwa uzani, naye amejifungia upanga mpya,
alijaribu kumwua Daudi. Lakini Abishai, mwana
wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti,
akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia,
wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi
kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli.”
2Samweli 21:15-17.

Haikuishia hapo, hata wakati Daudi alipo tamani


maji kwa kiu, licha ya kwamba kisima cha maji
kilikuwa kimezungukwa na majeshi ya Wafilisti,
“Akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya
kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango!
Basi hao watatu wakapenya jeshi la Wafilisti,
wakateka maji kutoka kila kisima cha
Bethlehemu, kilicho karibu na lango,
wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini
Daudi hakukubali kuyanywa, akayamimina

29
mbele za Bwana; akasema, Mungu wangu apishe
mbali, nisifanye hivi; je! Ninywe damu ya watu
hao waliohatarisha nafsi zao? Maana kwa hatari
ya nafsi zao wameyaleta. Kwa hiyo hakukubali
kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale
mashujaa watatu.” 1 Samweli 11:17-19. Unaelewa
maana yake nini? Hawa watu walikuwa tayari
kuhatarisha na kupoteza maisha yao kwa ajili ya
Daudi.

Watu uliowasaidia kuinuka, watasimama kwa ajili


yako siku moja na kukupigania, watazuia mabaya
dhidi yako na kuwa ulinzi kwako dhidi ya hila na
mashambulizi ya wakuchukiao. Watu unaowainua ni
ulinzi wa kesho yako. Inawezekana unajiuliza kwamba
huwezi kuanza kuwekeza kwa watu kwa sababu hauna
kitu, sikia, Daudi alianza akiwa hana kitu kwa namna
ya nje na wakati huo walikuwa wanaishi kwenye
mapango na baadae wakahamia Ikulu. Anzia hapo
ulipo, katika hicho unachofanya au ulichonacho,
msaidie mtu mmoja au wawili. Kama unafanya
biashara, msaidie mtu mmoja ili naye aweze kufikia
ulipo hata kwa kumshauri tu. Watu wengi shida yao
kubwa wanadhani wakimsaidia mtu katika kile
wanachofanya basi baadae atakuwa mpinzani wao,
kitu ambacho si kweli. Ukimsaidia mtu na akafika
mahali pakubwa labda kukuzidi hata wewe, hiyo
haiondoi heshima yako kwamba alitokea kwenye
mikono yako.

30
Kwenye maisha yako jitahidi kuwe na mtu angalau
umemwinua toka chini alipokuwa kufika ulipo au hata
zaidi yako. Danieli aliwainua wenzake na akawaweka
kwenye nafasi za juu. “Tena Danieli akamwomba
mfalme, naye akawaweka Shedraka, na Meshaki,
na Abednego, wawe juu ya mambo yote ya Uliwali
wa Babeli; lakini huyo Danieli alikuwa akiketi
katika lango la mfalme.”

Katika kile unachofanya, inua watu wa aina yako,


wekeza kwao, wengine yaguse maisha yao, hiyo si tu
sadaka bali pia ni uwekezaji kwa ajili ya kesho yako
mwenyewe.

Ninao watu ninaowafahamu ambao wamewekeza


kwa watu kiasi ambacho si kwamba wamekuwa tu
maarufu lakini pia maisha yao yameendelea kuwa ya
baraka mno. Mfano, rafiki yangu Mchungaji na
mwalimu Dickson Cornel Kabigumila, kupitia
programu zake za Retreat zinazofanyika kila mwaka,
amewasaidia vijana wengi kujitambua na kuwa vijana
wa tofauti watakaoacha alama katika kizazi chao,
ameanzisha madarasa kupitia makundi ya whatsapp
kwa ajili ya kuwatengeneza vijana kuwa bora zaidi
ambao mmoja wao ni mimi niliyeandika kitabu hiki;
Joel Nanauka kupitia program za Mentorship, vijana
wengi wananolewa na kuinuliwa kuwa watu wakuu
sana; Mwalimu Christopher Mwakasege, tuseme nini
juu ya huyu baba, amewekeza kwa watu kiasi ambacho

31
huwezi sema mabaya juu yake watu wakanyamaza,
lakini pia ameinua walimu wengi sana wa aina yake
ambao sasa ni ushuhuda unaotembea, ameinua
waombaji wengi sana katika taifa hili, ametengeneza
wachungaji, ameimarisha huduma nyingi kwa kile
anachofanya, amegusa maisha ya watu kwa kiasi
kikubwa; Mchungaji Dr. Eliona Kimaro, Mungu
amempa neema ya ajabu sana huyu baba, hakuna
ubinafsi ndani yake, ameinua watu wengi sana kupitia
mikono yake katika kile anachokifanya, amewasaidia
wengi kujitambua, amewaelekeza na kuwaonyesha njia
ya kupita, amefanyika daraja kubwa sana la kuvusha
vipawa na huduma za vijana wengi kufikia kiwango
cha utukufu ambacho walikusudiwa na Mungu,
amewasaidia vijana kiuchumi na kujitegemea. Ninaye
baba na rafiki yangu mtumishi Paul Mwangosi, katika
huduma yake ya uimbaji, huwezi kuzungumza juu ya
huduma ya kusifu na kuabudu nchini Tanzania bila
kumtaja Paul Mwangosi. Amewasaidia waimbaji wengi
hapa nchini, wengine sasa hivi wamekuwa maarufu
lakini walipita katika mikono yake, amewaelekeza njia,
wengine amewapa nafasi ya kuonesha walichonacho na
sasa wamekuwa watu wakubwa; kwa kile Mungu
alichompa amehusika kupanda moyo wa Ibada katika
taifa hili ambapo kuna vitu tunaviona leo ni matunda
yake, amepanda moyo wa Ibada kwenye makundi
mengi ya kusifu na kuabudu yaliyopo makanisani na

32
binafsi, na wengine wengi ambao nisingweza kuwataja
nikamaliza hapa.

Hauhitaji kuwa na vingi ili kuwekeza katika


maisha ya watu, kugusa maisha yao na kuwashika
mkono kuwainua ili wafikie mahali pao pa ukuu,
unahitaji kuwa na moyo wa upendo ili kuyafanya hayo.
Kiwango cha umbali utakaofika kinategemea sana
watu utakaowekeza kwenye maisha yao leo. Huwezi
kuwa mbinafsi na kutarajia kufika mbali.

33
Sura ya Tatu

JENGA TABIA

N
i dhahiri kwamba kuna vitu vingi kwenye
maisha yako vinategemea tabia yako ili
uvipate, vilevile ili uweze kufikia hatima
njema unahitaji kujenga tabia njema na bora. Samsoni
pamoja na kwamba alikuwa ni mnadhiri wa Mungu na
mtu aliyeitwa na Mungu mwenyewe ili kuja kuwaokoa
Israeli na mkono wa adui zao Wafilisti, bado tabia yake
ya kupenda wanawake ilimwangusha na
kumwangamiza kabla ya wakati wake. Haijalishi una
vipawa vingi na vizuri namna gani kama tabia zako ni
mbovu hautafika mbali, kuwa na vipawa, maono na
ndoto ni jambo moja lakini tabia itaamua umbali
utakaoenda nao katika hivi vyote; lakini pia tabia
itaamua ubakie katika unachofanya kwa ubora na
nguvu ile ile kwa muda gani. Chunguza ndani yako, ni
tabia gani ambayo unaona ni kikwazo kwako? Nenda
nayo mbele za Mungu ili akusaidie kuishinda na
kutengeneza kitu kipya ndani yako.

Kuna tabia unahitaji kuzijenga katika maisha


yako ili zikusaidie kufikia kusudi la Mungu kwako. Ni
rahisi kufika ulipokusudiwa lakini kama tabia fulani

34
hauna ndani yako basi itakuwa vigumu kuendelea
kubakia katika unachofanya kwa moto na upako ule
ule uliokuwa nao mwanzo. "Maana tu kazi yake,
tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo
mema, ambayo tokea awali Mungu aliatengeneza
ili tuenende nayo." Waefeso 2:10

Kuna baadhi ya tabia ambazo unapaswa


kuzitengeneza kama kweli unatamani kuwa mtu
mwenye mguso katika kizazi hiki na kijacho katika kile
utakachoamua kufanya. Baadhi ya tabia hizo ni kama;-

Tabia ya uaminifu.

Kadiri siku zinavyoenda mbele ndivyo uaminifu


unazidi kuwa bidhaa adimu kwa watu wengi, si tu
ambao hawajaokoka lakini pia kwa wapendwa wengi.
Jenga uaminifu hata kama hakuna mtu anayeona
fahamu kwamba yupo Mungu anayeona sirini.
Ukipewa kazi hata kama ni ndogo na haikulipi, fanya
kwa uaminifu mkubwa; ukipewa kitu cha mtu ukitunze
tunza kwa uaminifu. Katika huduma hizi kitu
kitakachokufanya uendelee kubaki katika ubora na
upako ulionao ni tabia ya uaminifu, uaminifu ndani
yake una tabia ya kukufanya uaminike kwa watu.
Kama vijana na watu tuliobeba vitu vikubwa vya
Mungu vitakavyoathiri na kugusa maisha ya watu
hatuna budi kujenga tabia ya uaminifu tangu tukiwa
chini hata tutakapokuwa juu. Wengi najua tunatamani

35
namna Mungu alikuwa akimtumia Paulo na kumwinua
viwango vya utumishi wake kila wakati, lakini
ukifuatilia utaona ni kwa sababu ya uaminifu.
Anasema “Nami namshukuru Kristo Yesu Bwana
wetu, aliyenitia nguvu kwa sababu aliniona kuwa
mwaminifu, akaniweka katika utumishi wake;” 1
Timotheo 1:12. Yesu aliona uaminifu ndani yake ndipo
akamuweka katika utumishi, tunaoona matunda yake
yakizalishwa mpaka kesho. Uaminifu kwa Mungu ni
kigezo kikubwa cha kukuinua na kukuweka katika
nafasi ya juu aliyokusudia kwako. Viwango vingine vya
utumishi vinahitaji uaminifu na viwango vingine vya
upako vinahitaji uaminifu ndani yako. Uaminifu wako
kwa watu na kwa Mungu ni ngazi ya kupandia
kuelekea katika ukuu wako.

Kuwa na subira.

Hii ni aina ya uvumilivu ambao ndani yake una


utulivu. Katika jambo lolote unalolitaka kwenye
maisha yako, ngazi yoyote unayotaka kuifikia, lazima
ujifunze kuwa na saburi ili uweze kufika huko
unakotaka kufika. Daudi anasema katika Zaburi 37:7
kwamba "Ukae kimya mbele za BWANA, Nawe
umngojee kwa saburi;" Saburi itakusaidia kuondoa
mahangaiko ya ndani, haraka zisizo na sababu na
presha ya ndani na nje toka kwa ndugu, rafiki na wale
unaowaamini. Unapokosa jambo hili moyoni mwako
kuna vitu unaweza ukafikiri umepata kumbe

36
umeharibu maana wakati wake ulikuwa bado. Mngoje
Bwana kwa Saburi na utulie mbele zake. Hata
ungefika mahali pa juu pa ukuu sana, kama utakosa
subira basi tutashuhudia ukurupukaji katika
maamuzi, kufanya vitu bila kujipanga na kufanya chini
ya kiwango kwa sababu ndani yako kutakosekana si tu
uvumilivu bali utulivu pia. Kumbuka subira ni
uvumilivu wenye utulivu ndani yake.

Tabia ya unyenyekevu.

D.L. Moody alikuwa na msemo aliopenda


kuutumia unaosema “Faith gets the most, love
works the most, but humility keeps the most”
ikiwa na maana kwamba “Imani hupata zaidi, Upendo
hufanya kazi zaidi, lakini Unyenyekevu hutunza zaidi.”
Unaweza ukafanya mambo yote yanayohitajika ili
wewe kuwa mtu fulani, ukapata kila kitu ulichohitaji
lakini ni tabia ya unyenyekevu tu itaamua ubaki nayo
au la. Biblia inataja habari za Yesu kwamba alijifanya
kuwa hana utukufu, akachukua mfano wa
mwanadamu, akawa mtii hata mauti naam mauti ya
msalaba. Unyenyekevu hauna maana kwamba wewe
hauna ulichonacho, au haujui kufanya kama wengine,
la hasha! Lakini ndani yako unajua yuko Mungu
mwenye vyote, anayeweza kumpa yeyote amtakaye bila
masharti yoyote, kwa hiyo hata hicho ulichonacho
unajua ni upendo na neema yake tu kwamba amekupa
wewe. Hivyo ndani yako hautafuti utukufu wako bali

37
wa Mungu, hautafuti kujulikana wewe katika jambo
ulifanyalo bali Mungu.

Tabia ya unyenyekevu itamfanya Mungu akuinue


zaidi, akutambulishe mahali ambapo ulikuwa
hutambuliki lakini pia tabia hii itakufanya uaminiwe
na kutapata nafasi kwenye mioyo ya watu. Kuna watu
pamoja na vitu vikubwa ndani yao, lakini kuna mahali
hawakubaliki kabisa na hawawezi kupokelewa tena.
Kwa sababu walipokwenda kutumika au kufanya kazi
au kuonesha walichonacho hawakufanya kwa
unyenyekevu. Kama tu Mungu huwapinga wenye
kiburi na kuwapa wanyenyekevu neema, basi uwe na
uhakika watu wake hawawezi kupingana na hili neno.
“Ni rahisi ukafika mbali katika ulichoitiwa ila tabia
itaamua ubaki hapo juu au ushuke chini. Tabia
itakufanya uaminike au usiaminike, itakufanya
ukubalike au usikubalike.”

Tabia ya utakatifu.

Kwanza fahamu kwamba tabia ni maadili ya ndani


ambayo yanajenga mwenendo wa mtu au mtindo wa
maisha ya mtu. Na Utakatifu ni tabia ya Mungu ndani
ya mtu. Sasa tunapoongelea tabia ya utakatifu
tunazungumzia juu ya maadili ya ndani yenye tabia ya
Mungu yanayozalisha/sababisha mwenendo na mtindo
wa maisha ya mtu. Utakatifu ni kuishi sahihi sawa na

38
neno la Mungu, ni kujitenga na uovu na kuamua kuishi
kwa haki.

Matokeo ya Utakatifu ndani ya Mtu.

Tabia hii ya utakatifu inapokuwa ndani yako na


kwenye maisha yako inazalisha mambo yafuatayo
ambayo yatakufanya uwe mtu mwenye nguvu, neema,
mguso na ambaye ni tishio kwa shetani na kazi zake.
Mambo hayo ni kama yafuatayo; Kufa kwa dhambi
kwenye maisha yako (Warumi 6:1), Uwepo wa Mungu
wakati wote (2 Wakorintho 5:8) uwepo wa Mungu ndio
utakuhakikishia ushindi, mpenyo na kufanikiwa;
Utakutoa katika umasikini na kutindikiwa (Zaburi
34:10) utakatifu unazalisha ujasiri na ushujaa ndani
yako (1 Samweli 30:6-8, Joshua 1:3-9); Utapata hekima
itakayokusaidia kujua nini cha kufanya wapi na kwa
wakati gani (Mathayo 7:24-25); utakufanya kuwa bora
kimaadili, yaani mtu asiyelaumika (1 Timotheo 4:12).
Tabia hii ya utakatifu unapaswa kuipalilia kwa sababu
ya faida zake kwako na vitu vilivyo ndani yako.

39
Sura ya Nne

KUBALI KULIPA
GHARAMA

M
oja ya mambo muhimu na yasiyopendwa na
vijana na watu wengi licha ya kwamba wana
ndoto na malengo ya kufika mbali ni kulipa
gharama. Wengi wanatamani kufanikiwa katika
wanachofanya, lakini hawako tayari kulipa gharama za
kufika huko kwa sababu kulipa gharama ni gharama
kuilipa. Uzuri ni kwamba kila unachokitaka kina
gharama zake za kukipata, na kuna vitu huwezi
kuvipata kwenye maisha isipokuwa umelipa gharama
zitakazokuwezesha kupata unachotaka.

Changamoto hii inalikumba kundi kubwa la vijana


wanaotamani kufika mbali kielimu, kiuchumi,
kimahusiano nk, wanatamani kutumia vipawa na
karama katika ubora lakini hawatamani kulipa
gharama. Kulipa gharama ni kuwajibika moja kwa
moja na kile unachotamani kukipata kwa muda na
wakati ambao umejiwekea au Mungu amekusudia
kwako. Ni dhahiri kwamba hakuna kitu kizuri
ambacho utaweza kukipata pasipo kulipa gharama ya
kukipata kitu hicho.

40
Zipo gharama za aina tofauti tofauti ambazo
unapaswa kulipa ili kufikia katika kiwango cha
utukufu ambacho Mungu amekusudia kwa ajili yako
kulingana na ulichopewa. Hapa chini nimekuwekea
baadhi tu ya gharama ambazo ni za muhimu na lazima
kwa mtu yeyote anayetaka kuacha alama duniani na
kuwa baraka kwa kizazi hiki na kijacho.

Jitenge na baadhi ya mambo.

Kuna mambo unayapenda sana lakini mchango


wake juu ya kule unakoelekea ni mdogo sana, ni
mazuri kwa kuyatazama lakini hayakufai wewe kwa
sababu hayakuongezei wala hayakupunguzii kitu,
mambo hayo jitahidi kuyaepuka na kuyaacha kabisa
kwa sababu yatakula muda wako wa muhimu ambao
kimsingi ulipaswa uutumie kwa ajili ya mambo
mengine ya muhimu. Kuna mambo ambayo hayana
shida kufanywa na watu wa rika lako, lakini hayakufai
wewe, kuna mambo unapaswa kutokimbizana nayo
katika kuyafanya kwa sababu yatakuondolea utulivu
ndani yako na msimamo wako wa ndani katika kile
ambacho Mungu ameweka kwako.

Angalia hapa maneno ya Paulo asemavyo; “Vitu


vyote ni halali; bali si vitu vyote vifaavyo. Vitu
vyote ni halali; bali si vitu vyote vijengavyo.” 1
Wakorintho 10:23. Sio tu ni halali, lakini je vinakufaa
wewe, jiulize mambo hayo yanakujenga kuelekea

41
kwenye hatima yako kubwa au yanakubomoa? Kaa
chini jiulize swali hili; katika mambo yote unayofanya,
vitu vyote unavyokimbizana navyo je vinakufaa na
kukujenga? Jiulize marafiki ulionao, je wanakufaa?
Wanakujenga au wanakubomoa? Wanakusaidia kuwa
wewe halisi ambaye Mungu amekusudia uwe au
wanakuondoa katika mpango wa Mungu? hii ndiyo
gharama unayopaswa kuilipa, kukubali kuacha baadhi
ya vitu visivyokufaa na kukujenga ili upate vile
ambavyo Mungu amekusudia kwako.

Kuna tabia unazo lakini hazifai kwa kitu


alichoweka Mungu ndani yako. Kaa na utafakari
mwenyewe ni tabia zipi ambazo unaona ni kikwazo na
zitakuchelewesha kufikia kiwango cha utukufu wa
Mungu kwako? Paulo anasema jambo hili kwamba,
“Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote
kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa
kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa
ajili yake nimepata hasara ya mambo yote
nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo;”
Wafilipi 3:8 kuna mambo kadhaa katika mistari hii
nataka uyaone; Mosi, maono, malengo na shauku yako
ya ndani ndiyo huamua ni vitu gani uambatane navyo
na vitu gani usiambatane navyo. Paulo anaeleza
kwamba uzuri wa kumjua Kristo kwake binafsi
ulimfanya apate hasara ya mambo yote na kuyahesabu
kama si kitu akilinganisha na uzuri wa kumjua Kristo.

42
Jitathmini, ni mambo gani ukiyatazama unaona si
kitu kwa ajili ya kitu ulichonacho ndani? Pili; kile
unachokitaka kwenye maisha kinatakiwa kiwe na
nguvu kuliko kitu kingine chochote kwenye moyo wako,
kisha kikutengenezee nidhamu ya kukaa na kutembea
nacho mpaka umekipata. Uzuri usio na kiasi wa
kumjua Kristo Yesu ulimfanya Paulo aone kila kitu
ambacho hakimuelekezi kumjua huyu Yesu kiwe si
kitu. Usianze kukimbizana na kila kitu, acha vingine
vikupite kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kitu
ambacho Mungu ameweka ndani yako. Kubali hivi sasa
maana mbele kuna utukufu mkubwa sana ambao
Mungu ameandaa kwa ajili yako.

Lakini pia fahamu kwamba, si kila kitu ambacho


unapaswa kuachana nacho basi hakina faida kwako.
Tunapozungumzia suala la kulipa gharama, kuna vitu
ambavyo vilikuwa vinakuingizia faida kubwa lakini si
katika njia iliyo halali, hivyo unapaswa kuachana
navyo. Si hivyo tu kuna vingine vilikuwa vinakuingizia
faida kubwa lakini havina mchango wa kule
unakotakiwa kwenda na kitu ulichonacho ndani yako.
Mfano kuna watu wameacha fani walizosomea na kazi
walizokuwa wanazifanya ili wamtumikie Mungu, si
kwa sababu waliyosomea na kazi walizokuwa
wanafanya si muhimu maana walikuwa wanapata
faida kwazo, lakini wakiangalia faida kubwa iliyomo
katika kumtumikia Mungu na ile nguvu
inayowasukuma ndani yao kuelekea mwelekeo wa

43
kiutumishi wanajikuta wanakiona kila kitu si muhimu
kwa wakati huo. Nina rafiki yangu ambaye aliacha
kazi ya ualimu ili aweze kumtumikia Mungu. Kulipa
gharama kwa kukubali kuachana na baadhi ya mambo
hakuna maana kwamba hayo mambo hayana umuhimu
kwako, la hasha! Ila unaangalia kilichoko ndani yako
na kule unapaswa kuelekea.

Kuna mfano wa Elisha mtumishi wa Mungu


wakati akiitwa kwenda kumtumikia Mungu, hakuwa
mtu ambaye hakuwa na shughuli za kufanya, bali
aliingia gharama ya kuachana na mambo aliyokuwa
anafanya ili aweze kutumika kama ambavyo Mungu
alikusudia kwake.

Tunasoma, “Basi, akaondoka huko, akamkuta


Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akilima,
mwenye jozi za ng’ombe kumi na mbili mbele
yake, na yeye mwenyewe alikuwa na lile la kumi
na mbili. Eliya akapita karibu naye, akatupa
vazi lake juu yake. Naye akawaacha ng’ombe,
akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe ruhusa,
nakuomba, nimbus baba yangu na mama yangu,
kisha mimi nitakufuata. Akamwambia, Enenda,
urudi; ni nini niliyokutendea? Akarudi akiacha
kumfuata, akatwaa lile jozi la ng’ombe,
akawachinja, akatokosa nyama zao kwa ile miti
ya ng’ombe, akawapa watu, wakala. Kisha

44
akainuka, akamfuata Eliya, akamhudumia.”
1Wafalme 19:19-21

Ngoja twende taratibu kidogo; Elisha alikuwa


mkulima kabla hajaitwa kwenye utumishi. Jozi za
ng’ombe kumi na mbili maana yake alikuwa na
ng’ombe ishirini na wanne madume ambao ni kwa ajili
ya kilimo tu. Shambani hakuwa mwenyewe, wale
ambao wamewahi kulima kwa kutumia ng’ombe
watanielewa zaidi, kila jozi ya ng’ombe kikawaida
inatakiwa kusimamiwa na watu wasiopunguo wawili
mpaka watatu, tuchukue watu wawili kwa kila jozi,
maana yake alikuwa na wafanya kazi ishirini na
wanne. Jozi moja ya ng’ombe inaweza kulima hekali
moja mpaka mbili kwa siku (tusiwachoshe ng’ombe),
kila jozi ya ng’ombe ilime hekali moja kwa siku, maana
yake kwa siku zinalimwa hekali kumi na mbili za
shamba. Hekali kumi na mbili zinazolimwa kwa siku,
huyu mtu huwezi kumuweka katika kundi la wakulima
wadogo wadogo, bila shaka Elisha alikuwa mkulima
mkubwa.

Si hapo tu, kama atalima hekali kumi na mbili kila


siku mpaka msimu wa kuandaa mashamba
utakapoisha atakuwa na hekali ngapi? Tuangalie
mazao atakayopata baada ya kulima. Chukulia mfano
kwamba alikuwa akilima mahindi na kila hekali itoe
gunia kumi tu za mahindi, maana yake kwa hekali 12

45
anazolima kwa siku atavuna gunia 120 (Haya ni
mavuno ya shamba alilolima kwa siku moja).

Sasa lilipokuja suala la kumtumikia Mungu ilibidi


kuachana na kilimo ili atoe muda wake wote kwenye
huduma. (Sijakuambia ili utumike vizuri inabidi uache
unachofanya sasa hivi ili uonekane ndio umeacha
baadhi ya mambo kama sehemu ya kulipa gharama, la
hasha!) Angalia vijana waliokosa ajira nyuma yake,
angalia kiwango cha mazao ambayo aliamua kukikosa
kila mwaka, ng’ombe aliwachemsha supu wote
akawapa watu wanywe. Mashamba aliyokuwa analima
inawezekana aliyagawa yote, anaondoka kwenda
kumtumikia Mungu huku nyuma hajaacha chochote
kinachomuhusu isipokuwa wazazi wake. Fikiri mtu wa
namna hii, kiwango chake cha kumtumikia Mungu
kitakuwaje? Unafikiri ni mtu atakayekuwa na utani
kwenye huduma? Fuatilia utumishi wa Elisha utaona
jinsi alivyokuwa anajitoa, alikuwa makini na alijua
kitu anachokifanya. Gharama ya kukubali kuacha
baadhi ya mambo uliyokuwa unayapenda sio ndogo,
inahitaji kujitoa kwelikweli, kujua kwa uhakika ni kitu
gani unachokitaka kwenye maisha na unataka kufika
wapi. Gharama ya kukubali kuacha baadhi ya mambo
si ya watu dhaifu maana watu dhaifu hawawezi
kufanya maamuzi kama hayo, inahitaji watu majasiri
wanaojua kule wanakoelekea na nini wanataka kupata
baada ya muda fulani.

46
Jidhabihu.

Nimetumia neno hili jidhabihu likiwa na maana ya


kujitoa wewe mwenyewe kama sadaka kwa ajili ya kile
unachotaka na kule unakotaka ufike. Hakuna njia ya
mkato, ni lazima ujitoe mwenyewe. Mbegu haiwezi
kuota na kuzaa matunda isipokubali kuzikwa ardhini
na kuoza. Kuna nyakati za kujipoteza ili ujipate zaidi,
kuna nyakati za kukubali kudharauliwa maana wakati
huu sio wakati wa kutafuta heshima kwa watu, ni
wakati wa kujichonga ili uwe wewe halisi. Usitafute
kujitambulisha kwa kila mtu ili wakujue wewe ni nani,
acha kazi zako zitasema wewe ni nani. Kuna watu
hatuwajui, ila tukiona kazi zao tunajua huyu ni fulani,
watu hawa hawakutumia muda wao kujitambulisha na
kutaka wafahamike kwa kila mtu, bali walijitoa kwa
ajili ya kile kilichomo ndani yao na kuhakikisha
kinatoa matokeo mazuri kiasi ambacho kazi zao
zimewatambulisha na kuwapa nafasi.

Kubali hivi sasa kujidhabihu mwenyewe. Kuna


wakati ambao kujidhabihu mwenyewe kunakuhitaji
nguvu nyingi, unatoa nguvu zako mpaka tone la
mwisho, ni wakati ambao unaona kama vile watu
wamekusahau, hawakujui maana hata uliotegemea
pengine wangekusaidia na kukushika mkono
wanakupita kama vile hawakufahamu. Usiwalaumu,
mbegu ikiwa chini ardhini inaweza kukanyagwa na
kila mtu, lakini haitafia hapo maana wakati wake wa

47
kuchipuka hata pangekuwa pagumu namna gani
itachipuka tu na itaota na kuzaa matunda, na wale
ambao waliikanyaga ikiwa ardhini watatamani
matunda yake.

Kujidhabihu mwenyewe kunabeba gharama ya


kuhimili matukano, kuhimili maumivu, kuhimili
kuchekwa na watu, kudharauliwa, kuonekana si kitu,
wakati mwingine watu watakuambia umepotea na
unakoelekea sio kuzuri, wengine watakushauri
kuachana na Mungu ili uendelee na mambo yako kama
wao. Kubali kulipa gharama hizo zote. Kitu chochote
kizuri hakijawahi kupatikana kwa urahisi. Maumivu
unayopitia sasa yasikukatishe tamaa bali yakupe
hamasa ya kuendelea mbele zaidi kuelekea kwenye
ndoto na hatma yako.

Muda.

Hii ni gharama nyingine ambayo unapaswa kuilipa


kama unataka kufikia kiwango fulani cha maisha,
huduma au chochote unachofanya. Muda
umegawanyika katika maeneo mengi sana; Mtu mmoja
alisema “Kile unachokipa muda wako mwingi ndiyo
kina umuhimu zaidi kwako”, kuna vitu ambavyo
kwenye maisha yako vinatakiwa uviongezee muda
kulingana na umuhimu wake na vingine uvipunguzie
muda kama sio kuvinyima kabisa kulingana na
kutokuwa na umuhimu kwako na kule unakotaka

48
kufika au kuwa. Muda wa saa 24 ni mchache sana
kufanya kila kitu, chagua mambo ya msingi ya kuyapa
muda wako kama tu unataka kufikia malengo na
kufanikisha ndoto yako.

Moja ya gharama ambayo vijana na watu wengi


hawapendi kuilipa ni gharama ya muda. Kuna kuku
gani ambaye atataka kutotoa vifaranga vyake kabla ya
siku ishirini na moja? Akijifanya anataka kutotoa
vifaranga kabla ya siku ishirini na moja basi mayai
yatakuwa viza hatapata watoto aliokusudia. Kuna
watu ambao wanatamani vitu vizuri lakini hawako
tayari kujipa muda wa kusubiri, wanataka wapange leo
kesho wapate, waanze biashara leo kesho iwe kubwa
na kesho kutwa wawe matajiri, wanataka waanze
huduma leo na kesho wawe maarufu na kupata maelfu
ya watu bila kupitia mchakato, ni dhahiri kwamba vitu
vingi tunavyovitamani vinahitaji tujipe muda wa
kusubiri ili viweze kutokea na kuwa vile
tulivyokusudia viwe.

Tumia muda wako vizuri ambao Mungu amekupa


kila siku katika kujiongezea thamani katika kile
unachotaka uwe au vile unavyotaka uwe. Mfano, wewe
unataka kuwa mfanya biashara mkubwa, tumia muda
wako kujua kuhusu biashara unayotaka kuanzisha,
jifunze kuhusu masoko, namna ya kupata wateja,
usimamizi na utunzaji wa pesa, vilevile ukitaka kuwa
mtumishi wa Mungu mwenye mguso katika kizazi hiki,

49
tumia muda wako kujifunza kuhusu huduma hiyo,
wekeza katika maombi, mifungo, soma vitabu vya
watumishi mbalimbali, soma neno la Mungu, kaa na
watu ambao wamefanikiwa katika eneo hilo.

Tuna kizazi cha ajabu sana siku hizi ambacho


kimeamua kupoteza muda na si kutumia muda vizuri,
kizazi ambacho kinaongelea watu zaidi kuliko mipango
na mambo yanayoweza kuwasogeza katika hatima zao
kubwa, kizazi cha watu ambao muda wao wote wapo
tayari wautumie kuperuzi mitandaoni huku
wakiangalia vichekesho na si mambo yenye
kuwaongezea vitu kwenye ufahamu wao na kuweka
mchango katika kesho yao njema. Ukweli ni kwamba
kesho bora hujengwa na leo yenye tija. Kile
unachokifanya leo kina mchango mkubwa sana katika
kesho yako. Tumia muda wako vizuri na kwa hekima
sana maana zamani hizi ni za uovu mwingi.

Mungu amempa kila mmoja wetu muda sawasawa


na mwingine, wewe hapo una muda sawa na raisi wa
nchi yako, una muda sawa na tajiri wa kwanza kwenye
nchi yako, una muda sawasawa na yeyote unayemuona
amefanikiwa katika eneo ulilopo. Tofauti yako na mtu
mwingine yeyote ni kwenye matumizi ya muda.
Unaweza ukabadili matokeo kwa kubadili namna
unavyotumia muda wako kila siku.

50
Mipango.

Kuna usemi maarufu unaosema “Ukishindwa


kupanga basi umepanga kushindwa”. Ndoto, maono na
picha kubwa tulizonazo ndani yetu ili tuweze kuzifikia
hatuna budi kuwa na mipango ya namna ya kuifikia.
Mipango huanza na namna unavyopangilia siku moja
moja katika yale unayoyafanya yanayokuelekeza
katika kesho yako bora. Tuna watu wengi mpaka
wamekufa hawajawahi kufikia ndoto zao kwa sababu
walikuwa na ndoto lakini hawakuwa na mipango
namna ya kuzifikia ndoto hizo, hii ni kwa sababu kuwa
na ndoto ni jambo moja lakini kuzifikia ni jambo
lingine. Biblia inasema katika Mithali 19:21 kwamba
“Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri
la BWANA ndilo litakalosimama.”

Katika tafsiri zingine anaposema ‘Mna hila nyingi


moyoni mwa mtu’ anazungumzia juu ya “Mipango”.
Kwa hiyo jukumu la kuandaa mipango ni la muhimu
sana na ni la kwako. Andaa mipango namna ya kufika
katika hatima yako, yatengenezee ratiba na kuyagawa
katika vipindi vya muda mrefu, muda wa kati na
mfupi. Siku isipite hujafanya chochote kuelekea
kwenye ndoto yako kubwa. Yale madogo madogo
utakayokuwa unayafanya kila siku yana mchango
mkubwa sana katika kesho yako.

51
Mwendelezo.

Hii ni gharama nyingine unayopaswa kuwa tayari


kulipa. Wengi tunapenda kufanya vitu na kuishia
njiani, hatuna mwendelezo. Umeanza vizuri baada ya
muda umeacha. Ukienda namna hii sio rahisi kupata
matokeo mazuri.

Watu wote wanaofanikiwa kufikia makusudi ya


Mungu kwenye maisha yao, ukiwauliza watakuambia
namna walivyotembea bila kukwepa kuwa na
mwendelezo katika kile walichokuwa wanafanya, hata
kama ni kwa udogo lakini walikuwa wakifanya mara
kwa mara. Mtumishi wa Mungu Raymond W. Hurn
katika kitabu chake cha “Finding your Ministry”
ameandika kwamba “Hauhitaji kusubiri darasa au
kutambuliwa rasmi, bali fanyia kazi kila siku na
mara kwa mara kile ulichopewa ndani yako
kuelekea katika ukuu wako”

Wale ambao ni walimu au waliopewa kitu cha


kuandika ndani yao watanielewa zaidi hapa. Mwl.
Emmanuel Makwaya aliwahi kuniambia jambo hili
mwaka 2017, kwamba “Kama unataka kuwa
mwandishi mzuri, basi hakikisha kila siku
unaandika kitu”. Haikuwa kitu rahisi kwangu, lakini
niliendelea kufanya hivyo, sasa hivi siwezi jisikia vizuri
siku ikaisha sijaandika.

52
Siku moja nilikuwa naongea na mtu mmoja
ambaye Mungu amemuita eneo la Maombi, hasa
kuombea watumishi na kazi ya Mungu, lakini kwa
sababu ya changamoto za maisha na masuala ya kazi
ameacha wito huo, nikaongea naye kwa kirefu na
kumweleza bila kusita kwamba anatakiwa kusimama
tena na kufanya wajibu huo bila kuangalia mazingira
yanasemaje. Muendelezo unahitaji uvumilivu sana ili
uweze kufikia makusudi ya Mungu kwako.

53
Sura ya Tano

USILISHE NJAA LISHA


MAONO

K
ulisha njaa ni kufanya maamuzi kwa
kuangalia hali yako ya sasa bila kujali kesho
yako itaathiriwa kwa kiasi gani na maamuzi
unayofanya. Tuna watu wengi sana waliopoteza
mwelekeo, wameacha kufanya vitu walivyoitwa na
Mungu kuvifanya, wameyaacha maono wanafanya vitu
vingine kwa sababu tu walikutana na hali
zilizowalazimisha kufanya maamuzi bila kuangalia
matokeo ya maamuzi yale katika kesho yao.

Kuna maamuzi unaweza ukayafanya leo


yakaharibu kesho yako kabisa. Tupo katika siku za
mwisho ambapo Shetani anang’ang’ana kuona
unapoteza mwelekeo na kuwa mtu wa kawaida tofauti
na vile ambavyo Mungu amekusudia uwe,
atakutengenezea mazingira ambayo utaona unaridhika
lakini kesho yako inaharibiwa taratibu. Mfano kuna
vijana ambao wanahangaishwa na kujichua na
kutazama picha za uchi kwenye mitandao; kwa kadiri
ambavyo wanaendelea kufanya hivyo wanaona kama
wanaridhika lakini kesho yao na ndoto zao zinazidi
kufifia na kuharibika. Shetani hawezi kufanya kitu

54
chenye kukufaidisha hata kingeonekana kama
dhahabu, lazima ujifunze kuona kama Mungu aonavyo
ili uweze kuwa salama katika zamani hizi.

Tukimwangalia kijana Yusufu alipokuwa katika


nyumba ya Potifa, tunajua alikuwa na nafasi kubwa,
lakini alijua anakotakiwa kufika na ndoto alizonazo
hakutamani kuona zinaharibiwa na kitu chochote kile.
Mke wa Potifa alipomlazimisha kulala naye mara
kadhaa hakukubali, si kwa sababu nyingine yoyote ila
kwa sababu aliona gharama ya kupoteza alichonacho
kwa sababu ya njaa ya siku moja ni kubwa sana,
aliangalia mahusiano yake na Mungu namna
yangekuwa baada ya jambo lile, aliangalia ndoto zake
zingeharibika kwa kiasi gani akaona bora kukimbia na
kutofanya ubaya ule na mke wa bosi wake. Angalia,
Yusufu akasema “Hakuna mkuu katika nyumba hii
kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu chochote ila
wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya
huu mkubwa nikamkose Mungu?...huyo
mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala
nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi
mwake, akakimbia, akatoka nje.” Mwanzo 39:9-12.
Kuliko kuharibu ndoto zako bora watu wakuite mjinga,
wakuone muoga, hata wakikusema watakavyo ni heri
kwako kwa sababu gharama ya kusemwa vibaya na
kuchekwa ukiwa unalisha maono si kubwa kama
gharama ya kusemwa vibaya na kuchekwa ukiharibu
maono na ndoto zako kwa njaa ya siku moja.

55
Kukubali kulisha maono ni gharama sana, njaa ya
muda mfupi inaweza ikakusahaulisha unakoelekea;
njaa ya siku moja ilimfanya Esau auze haki yake ya
mzaliwa wa kwanza na kujikuta maisha yake
yanakuwa tofauti kabisa na vile Mungu alimkusudia.
Jifunze kutokana na makosa ya watu hawa ili usifanye
kama wao;

ESAU.

Huyu alikuwa mtoto wa mzee Isaka. Yeye na


Yakobo walikuwa mapacha na Esau ndiye aliyekuwa
mkubwa kwa kuzaliwa kwanza. Siku moja Esau
alitoka katika kuwinda wanyama amechoka sana na
njaa kali kiasi cha kufa, haikuwa njaa nyepesi ilikuwa
nzito. Wakati huo Yakobo alikuwa amepika chakula
cha dengu, Esau alipofika akaomba apewe chakula
maana alikuwa anaumwa njaa, Yakobo akamtega
kwamba ili apate chakula amuuzie haki ya mzaliwa wa
kwanza. “Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu
na kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? Yakobo
akamwambia, Uniapie kwanza. Naye
akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya
mzaliwa wa kwanza. Yakobo akampa Esau mkate
na chakula cha dengu, naye akala, akanywa,
kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau
akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.”
Mwanzo 25:32-34

56
Kuna maswali ya kujiuliza katika habari hii; Mosi,
je! Mama yao (Rebeka) hakupika chakula siku hiyo
mpaka Esau aende kumuomba Yakobo chakula chake?
Pili, Esau hakupata kitu kabisa alikokuwa ameenda
kuwinda ili akifika nyumba ajitengenezee apate kula?
Tatu, Kama alipata mawindo, nini kilimfanya
ashindwe kuvumilia kidogo tu ajitengenezee chakula
chake kuliko kuingia kwenye mtego wa hatma yake?
Nne, Hakujua haki ya mzaliwa wa kwanza kwamba
imebeba baraka kiasi akaidharau na kuitoa kwa
chakula cha dengu? Tano, Wazazi wao walikuwa wapi
wakati hii biashara inafanyika iliyoathiri maisha yao
ya baadae? Majibu utakayoyapata katika maswali haya
utagundua Esau alikuwa na shida kubwa maana
aliidharau haki ya mzaliwa wa kwanza. Kudharau
maono, ndoto na vipawa kwa ajili ya chakula cha siku
moja kunaweza kukugharimu maisha yako yote ya
baadae ambayo Mungu alikusudia kwako.

Mazingira haya yaliyotengenezwa hapa


yalimshurutisha Esau kufanya maamuzi ambaye
yaliharibu maisha yake ya baadae kabisa, maana
baraka alizokuwa azipate zilienda zote kwa mdogo
wake Yakobo, lakini pia unaona alikuja kuvurugwa
mpaka ulipofika wakati wake wa kuoa. Biblia inasema
“Esau alipokuwa mwenye miaka arobaini,
akamwoa Yudithi, binti Beeri, Mhiti, na
Basemathi, binti Eloni, Mhiti. Roho zao Isaka na
Rebeka zikajaa uchungu kwa ajili yao.” Mwanzo

57
26:35. Sasa ona, kosa moja limegharimu mpaka maisha
yake ya mahusiano. Alioa wake ambao wazazi wake
hawakupenda, si tu kwamba hawakupenda ila Esau
aliwadharau wazazi wake katika suala la kuoa tofauti
na Yakobo ambaye Biblia inasema “Na ya kuwa
Yakobo amewatii babaye na mamaye...” Mwanzo
28:7

Mtu ambaye maono yake yapo mbioni kuharibiwa


utaona; anakuwa si mwepesi kupokea ushauri hata
kwa wazazi wake au walezi wake, kila akiambiwa
aachane na kitu fulani maana kitamharibia maisha
hayuko tayari kusikiliza maana njaa imekuwa kali
sana kiasi ambacho anaona maono yake, ndoto
alizonazo si kitu tena. Haishii tu kutowasikiliza wazazi
au walezi wake lakini hata wazazi wake wa kiroho
kama vile mchungaji wake naye humpuuza na kuona
hawezi kumshauri lolote katika kile anataka
kukifanya, ukishaona hatua hiyo ujue shimo la
uharibifu haliko mbali sana na wewe.

Usilishe njaa, lisha maono uliyonayo, kubali hivi


sasa kuvumilia maumivu, kubali hivi sasa kuvumilia
njaa, wakati mwingine uhitaji huwa mkubwa kila
unapoangalia huoni kama unaweza kutimiza hilo
hitaji, lakini je unapoangalia na kutaka kufanya
maamuzi hayo, umeangalia usalama wa ndoto zako?
Kama yataharibu ndoto ulizonazo, au maono yaliyo
ndani yako, acha ipite kwa sababu kesho yako ni

58
muhimu kuliko unavyoweza kufikiri. Wakati mwingine
huwa natamani Mungu angemuonesha kila mtu picha
ya maisha yake ya baadae aliyomkusudia, pengine
watu wangeheshimu kile kitu na kuhakikisha
wanatunza kwa namna yoyote ile.

SAMSONI.

Habari za huyu ndugu tunazipata katika kitabu


cha Waamuzi 13 Mungu aliposema na mke wa Manoa
“Malaika wa BWANA akamtokea yule mwanamke,
akamwambia, Tazama, wewe sasa u tasa, huzai;
lakini utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto
mwanamume. Basi sasa, jihadhari, nakuomba,
usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho
najisi; kwani tazama, utachukua mimba, nawe
utamzaa mtoto mwanamume; na wembe usipite
juu ya kichwa chake; maana mtoto huyo atakuwa
mnadhiri wa Mungu tangu tumboni; naye
ataanza kuwaokoa Israeli na mikono ya
Wafilisti.” Waamuzi 13:3-5

Samsoni alizaliwa akiwa mnadhiri wa Mungu,


yaani mtu aliyetengwa kwa ajili ya MUNGU.
Maelekezo na makatazo ambayo Mungu alimpa yule
mama na baadae mume wake kwamba wahakikishe
wembe haupiti kichwani kwake, mwanamke hatumii
kileo, divai wala kujitia najisi kwa kitu chochote,
walihakikisha wanafuata yote. Kipindi chote cha

59
ujauzito yule mama hakunywa divai wala kileo
chochote ili kulinda maono ya Mungu ndani ya mtoto.

Sasa angalia Samsoni mwenyewe alipokuwa


kijana, alikutana na Delila, maneno ya ubembelezi,
kushawishi na kumsumbua viliharibu ndoto ya Mungu
ya kuona taifa la Israeli linaokoka katika mikono ya
Wafilisti. Yule mwanamke akamwambia Samsoni
“Wawezaje kusema, Nakupenda; na moyo wako
haupo pamoja nami? Umenidhihaki mara hizi
tatu, wala hukuniambia asili ya nguvu zako
nyingi. Ikawa, kwa vile alivyomsumbua kwa
maneno yake kila siku, na kumwudhi, roho yake
ikadhikika hata kufa. Ndipo alipomwambia yote
yaliyokuwa moyoni mwake, akamwambia, Wembe
haukupita juu ya kichwa changu kamwe; maana
mimi nimekuwa Mnadhiri wa Mungu, tangu
tumboni mwa mama yangu; nikinyolewa, ndipo
nguvu zangu zitanitoka, nami nitakuwa dhaifu,
nitakuwa kama wanadamu wenzangu.” Waamuzi
16:15-17

Unaweza ukaona ni kitu cha kawaida, lakini


hakikuwa kitu cha kawaida, hapa ndipo ndoto ya
Samsoni iliishia. Yule mwanamke kwa ubembelezi na
maneno yake ambayo yalikuwa yakimchokoza Samsoni
aonekane kama hampendi Delila yalimmaliza kabisa
Samsoni. Samsoni alifanya maamuzi kuepuka ile kero
ya mwanamke alipomwendea kila siku na kumweleza

60
jambo lile lile asijue maamuzi hayo yatamgharimu yeye
mwenyewe, familia yake na taifa zima. Unaweza
ukapiga hesabu ya gharama aliyoingia Mungu mpaka
kuhakikisha anapatikana mtu kama Samsoni halafu
baadae anaishia alipoishia. Umewahi kufikiri jambo
hili?

Kuna wakati unakutana na mazingira fulani


yanakulazimisha kufanya maamuzi ambayo kwa
macho pengine unaona ni sahihi maana yatakuondolea
kero fulani, lakini umeangalia ndoto ulizonazo
zitaharibiwa kwa kiwango gani? Umepima hasara
ambayo Mungu ataipata kwa wewe kuvuruga?
Umeangalia kanisa, jamii na familia yako
wataathirikaje na maamuzi yako? Msichana unasema,
huyu kaka amekuwa akinifuata mara kwa mara
kwahiyo nimeona nimwonee tu huruma. Ni kweli
umeepuka kero ya kusumbuliwa, lakini umeangalia
usalama wa mahusiano yako na Mungu na ndoto zako?

Kubali hivi sasa kijana, baba na mama yangu


kutokulisha njaa ya muda mfupi huku ukiharibu
maono yako ya baadae. Vumilia magumu unayokutana
nayo. Samsoni kwa tabia yake ya kupenda wanawake
ndiyo iliyomponza na kujikuta ameingia katika wakati
mgumu. Wakati mwingine tabia zako zinaweza
kukuharibia kesho yako, tabia zako zinaweza
kuwafukuza watu waliobeba vitu vizuri kwa ajili yako
na maisha yako ya baadae.

61
Baada ya Samsoni kueleza asili ya nguvu zake
Biblia inasema Delila alimuweka katika mapaja yake
mpaka Samsoni akalala usingizi, kisha akawaita
Wafilisti wakamnyoa nywele zake, “Kisha akasema,
Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika
usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama
siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya
kuwa BWANA amemwacha. Wafilisti
wakamkamata, wakamng’oa macho;
wakatelemka naye mpaka Gaza, wakamfunga
kwa vifungo vya shaba; naye alikuwa akisaga
ngano katika gereza.” Waamuzi 16:20-21

Mistari hii inatuonesha jambo la ajabu sana;


Samsoni hakujua kwa tendo lile Mungu alimuacha,
kwa hiyo Wafilisti walipomjia alijua atafanya kama
alivyozoea na kumbe zile nguvu alizokuwa nazo
zilikuwa zimemuacha kabisa, mwisho wa siku
akatobolewa macho na kuishia kusaga ngano gerezani.
Swali langu ni; Je! ni kweli Mungu alikusudia Samsoni
aishie kusaga ngano gerezani? Mtu ambaye aliweza
kuwapiga wafilisti elfu kwa mara moja, leo hii tumkute
mahali pa namna hii? Kuna maamuzi unayafanya leo
yanakula na kuimaliza kesho yako, kuna maamuzi
ukiyafanya leo yatakuachia jeraha na alama ya
kudumu ambayo itazima kabisa ndoto ya Mungu
kwenye maisha yako. Kwa Samsoni nywele zingeweza
kuota lakini macho je? Shetani anaitumia njaa yako ya
siku moja kuiba kesho yako kubwa, anatumia njaa

62
kufisha maono ndani yako, anatumia njaa ya muda
mfupi kukupofusha macho usiweze kabisa kuona na
kufikia kesho njema aliyoikusudia Mungu kwenye
maisha yako.

Kwa njaa ya siku moja ule uwezo wa kuona kesho


yako, uwezo wa kuona maono na kuyafanyia kazi,
uwezo wa kuona vitu ambavyo Mungu ameviandaa
kwa ajili yako unakufa, kinachotokea utakosa
mwelekeo wa maisha, hatua zako zinarudi nyuma
badala ya kwenda mbele. Hapa ndipo Shetani
hupasubiri sana, atakutumia anavyotaka. Wale watu
(Wakuu wa Wafilisti walipokusanyika ili kumtolea
sadaka Dagoni mungu wao, na mioyo yao ilipofurahi
kwa kumshinda Samsoni) wakasema “Mwiteni
Samsoni, ili atufanyie michezo” Waamuzi 16:25.
Mtu uliyeaminiwa na Mungu hupaswi kuishia mahali
pa namna hii.

Je! Kila anayelisha njaa hayapendi maono yake?

Fahamu jambo hili kwamba; si kila anayelisha


njaa basi hapendi maono yake au anapenda kufanya
hivyo, wengine Shetani huwatengenezea mazingira
magumu kiasi wanakuwa hawana namna nyingine ya
kufanaya. Unajikuta katikati ya mtihani mgumu kiasi
kuchagua kati ya A na B ni mtihani mwingine mgumu,
unajikuta umeishia mahali pabaya. Hii ndiyo sababu
unahitaji kukaa vizuri na Mungu ili akusaidie katika

63
kila hatua yako ya maamuzi ili uweze kutimiza kila
ndoto njema iliyo ndani yako.

Mambo ya kukusaidia usilishe njaa.

Kabla ya kufanya maamuzi yoyote, pata muda wa


kuomba ili Mungu akuongoze katika maamuzi
hayo.

Maombi yatakusaidia sana ili uweze kufanya


maamuzi sahihi yatakayolinda kesho yako na kile
ambacho Mungu ameweka ndani yako. Ukifuatilia kwa
ukaribu mifano ya watu niliowataja hapo juu
utagundua hawakupata muda wa kuomba kabla ya
kuamua walichoamua, inawezekana hawakuwa na
nafasi hiyo, lakini nataka nikwambie, Shetani hawezi
kukupa nafasi ili uweze kuomba ikiwa amekusudia
kuvuruga kesho yako, unahitaji kujijengea nidhamu ya
kuomba kabla haujaamua jambo lolote kwenye maisha
yako.

Ngoja nikupe mfano wa mtu mmoja kwenye Biblia


aliyeitwa Balaamu, huyu tunamfahamu tunaposoma
kitabu cha Hesabu kuanzia sura ya 22 hadi 24. Mfalme
wa Moabu alipoona kwamba Israeli wamefika
mipakani mwake aliogopa sana alijua ndiyo mwisho
wao maana alisikia habari za Israeli jinsi
walivyowatendea Waamori, akaona njia pekee na nzuri
ya kuwashinda Israeli ni kuwalaani. Akatuma wazee
wa Moabu na Wamidiani kwa Balaamu, walipofika na

64
kumweleza ujio wao, wakiambatanisha na ahadi ya
Mfalme wao ambayo ilikuwa ni “kumfanyizia heshima
nyingi na kila atakaloliomba kwake atapewa”. Balaamu
akawaambia watu wale akasema, “Kaeni hapa usiku
huu, nami nitawaletea jawabu kama BWANA
atakavyoniambia;” Hesabu 22:8, hii mbinu
ilimuondoa katika mtego mkubwa sana wa Mfalme wa
Moabu. Tunafahamu kwamba baadae alienda lakini
angalia kila hatua yake, ilikuwa kila hatua anaenda ili
asikie Bwana atakalomwambia na msimamo wake
ulikuwa kwamba; SIWEZI KUPITA MPAKA WA
NENO LA BWANA MUNGU WANGU,
KULIPUNGUZA au KULIONGEZA.

Kuna mambo mengi yanaweza kutokea,


ukaahidiwa vitu vizuri baadae, lakini jifunze kabla ya
mambo yote, nenda mbele za Bwana kujihakikishia
usalama wa kesho yako ili akuambie la kufanya,
akufundishe jinsi ya kuamua vyema, akushauri nini
cha kuamua na akuongoze kwa kila hatua yako
unayoiendea.

Fahamu ya kuwa ndoto na maono uliyonayo kwa


Shetani si kitu chema, hivyo atatumia hila
kufisha ulichonacho.

Ufahamu huu utakusaidia sana kuamua vyema.


Usipojua kwamba ndoto na maono uliyonayo ni kitu
cha thamani basi hata namna ya kuyalinda hautayapa

65
uthamani. Kama Eva angejua kwamba Shetani
alikuwa anawinda kesho yao na yetu inawezekana
asingeruhusu kabisa kumpa nafasi ya kumsikiliza au
hata kuzungumza naye. Ukijua ulichonacho kwamba ni
cha thamani na Shetani hataki kifanikiwe basi
utatumia kila njia kujilinda ili usiharibu kabla ya
wakati.

Itambue nafasi ambayo Mungu amekupa katika


ulimwengu wa roho na uiheshimu.

Kutokujua nafasi uliyonayo mbele za Mungu


katika ulimwengu wa roho ni shida nyingine ambayo
itakupelekea kutoiheshimu, maana utaiheshimu vipi
nafasi usiyoijua? Tumeona Esau akimwambia ndugu
yake “Itanifaa nini haki hii ya uzazi? (Mwanzo
25:32) Hakujua kwamba kesho yake, na hatma ya
maisha yake vimefungwa kwenye nafasi iliyoitwa
mzaliwa wa kwanza, akaidharau na baadae alilia kwa
machozi na kujikuta maisha yake yanakosa mwelekeo
mzuri na mwisho hatuoni hata kizazi chake kikitajwa
kwenye Biblia baada yake.

Hakuna nafasi ambayo Mungu anakuweka kwa


bahati mbaya. Kila nafasi unayopewa na kuwekwa ni
kwa kusudi maalumu na katika nafasi hiyo kuna kesho
yako njema.

66
Unapokuwa katikati ya jaribu au changamoto
inayokuhitaji kufanya maamuzi fulani, chunga
sana aina ya maamuzi unayofanya.

Changamoto au jaribu siku zote haliwezi


kukuweka mahali pazuri kimaamuzi, lazima
litakufikisha njia panda na mahali ambapo itakuhitaji
hekima ili uamue sawasawa. Jipe muda wa kutulia
kabla haujaamua chochote, angalia ndoto na maono
yako, angalia mahusiano yako na Mungu, je
havitaathiriwa na maamuzi yako? Kilichomponza
Samsoni ni kutaka kuonekana anampenda sana yule
mwanamke bila kuangalia ndoto na mahusiano yake
na Mungu namna yatakavyoathiriwa na maamuzi
yake. Esau angeweza kujipa muda kidogo ajipikie
mawindo yake, angekula kwa uhuru huku haki yake ya
uzaliwa wa kwanza iliyokuwa imebeba baraka zake
ikiwa salama.

Ningekuwa Samsoni.

Baada ya wakuu wa Wafilisti kufurahi kwa


kumshinda Samsoni, wakaomba Samsoni aletwe
kwenye hiyo karamu ili aweze kucheza mbele yao, naye
Samsoni akaletwa, kisha Samsoni akamuomba kijana
aliyekuwa amemshika mkono amwache ili azipapase
nguzo za jengo lile kusudi ajitegemeze humo. Samsoni
akamwita BWANA na kuomba mbele zake. Maombi
haya nataka uyaangalie vizuri; “Samsoni akamwita

67
BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU,
unikumbuke, nakuomba, ukanitie nguvu,
nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate
kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya
macho yangu mawili” Waamuzi 16:28

Ningekuwa Samsoni nisingeanza kuomba Mungu


anipe nguvu ili nijilipize kisasi kwa adui zangu
walionitoboa macho, ningeanza na toba kwa sababu ya
kulisha njaa na kusahau maono makubwa ya Mungu
ndani yangu. Baada ya toba ningeomba Mungu
anirejeshee macho, kisha anipe nguvu za namna ya
kuwashinda na kutoka mikononi mwao. Utagundua
hata baada ya kurejeshewa nguvu alisukuma lile jengo
likaua watu wengi sana na yeye akafia humo humo.
Inawezekana angekuwa na macho baada ya kusukuma
zile nguzo angekimbia nje ili kujiokoa yeye, au Mungu
angempa njia nyingine ya kufanya. Lakini pia
angeomba sawa na mapenzi ya Mungu inawezekana
asingekufa pamoja na Wafilisti hawa. Hata katika
wakati kama huu, jifunze kunyenyekea kwa Mungu na
kuutafuta uso wake ili yeye ajifunue na kujitukuza
kupitia maisha yako na si kuomba kwa kusukumwa na
hasira au hisia kama Samsoni alivyosema kwa ajili
macho yake mawili.

68
Sura ya Sita

TENGENEZA MFUMO
WAKO WA MAOMBI

T
unapozungumzia mfumo wa maombi,
hatuzungumzii tu habari za kuomba, bali kuwa
na utaratibu maalumu na unaoeleweka wa
kuomba. Mfumo huu wa maombi ndio ngazi ya
kupandia juu, kuvuka vikwazo na dhoruba zinazoweza
kutokea katika maisha yako. Usiombe tu kwa sababu
unahitaji kitu fulani toka kwa Mungu, bali omba kwa
sababu ndio mfumo wako wa maisha ya kila siku.

Biblia inazungumza habari za Danieli kwamba


alipokuwa amewekwa kuwa mkubwa katika Babeli na
kuwa miongoni mwa wale wakubwa watatu. Nao
walipoona kuwa amepata kibali kwa Mfalme Dario kwa
sababu ya roho bora iliyokuwemo ndani yake, ndipo
mawaziri na maamiri walipotafuta sababu ya
kumshitaki katika mambo ya Ufalme ili akionekana na

69
kosa aweze kufukuzwa kazi. Walipokosa sababu ya
kumshitaki wakagundua ni mtu wa maombi sana,
ndipo walipokuja na hoja ya kutunga sheria
itakayoenda kinyume na mfumo wake wa maombi.

Sheria na marufuku hiyo ilikuwa inasema kwamba


“Na kupiga marufuku, ya kwamba mtu yeyote
atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, katika
muda wa siku theathini, ila kwako, Ee mfalme,
atatupwa katika tundu Simba” Danieli 6:7b.
Maandiko haya na sheria hii ikasainiwa na Mfalme
Dario na kuwa sheria halali kwamba ndani ya siku
thelathini asionekane mtu yeyote atakayeomba dua
kwa Mungu au mtu yeyote ila kwa mfalme peke yake.

Watu wasio na mfumo rasmi wa maombi ambao


unaongoza maisha yao ya kila siku, walitii sheria hii na
kuacha kuomba. Watu wasio na utaratibu wa maombi
ni rahisi kwao kukata tamaa ya kuendelea na
msimamo wao kwa Mungu kwa sababu ya maneno ya
watu na sheria kubadilishwa inayokinzana na mfumo
wao wa maombi.

Angalia majibu ya Danieli, “Hata Danieli


alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha
kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake (na
madirisha katika chumba chake yalikuwa
yamefunguliwa kukabili Yerusalemu) akapiga
magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru

70
mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa
akifanya tokea hapo.” Danieli 6:10. Nataka
uyaangalie kwa umakini tena maneno haya ya mwisho,
anayosema “Akapiga magoni mara tatu kila siku,
akasali, akashukuru mbele za Mungu wake kama
alivyokuwa akifanya tokea hapo.”

Katika maneno hayo ya mwisho kuna kitu zaidi


ya kuomba ambacho nataka ukione;

Anatuonesha mfumo wake wa maombi ya kila


siku. Danieli pamoja na nafasi aliyokuwa nayo katika
ufalme wa Dario, bado alitenga muda wa kuomba mara
tatu kila siku mbele za Mungu wake. Hii inatupa mimi
na wewe kujua kwamba, suala la kuwa na mfumo wa
maombi halina kisingizio kwamba hauna muda kwa
sababu una kazi, au biashara au majukumu
yanakubana sana, bali kujenga tabia ya kuwa na
maombi katika muda unaofanana kila siku kulingana
na ratiba uliyonayo.

Mfumo wake wa maombi ulimtengenezea


imani kwamba pamoja na sheria iliyowekwa,
bado heshima na hadhi ya Mungu wake haiwezi
kushindanishwa na mwanadamu awaye yeyote.
Ndio maana huoni akiogopa kuendelea na utaratibu
wake wa maombi kama ambavyo amekuwa akifanya
tokea hapo awali. Swali la kujiuliza, sheria
ikibadilishwa na kutaka asiwepo mtu yeyote

71
atakayeomba kwa Jina la Mungu huyu
tunayemuabudu katika Kristo Yesu, bado utakuwa na
msimamo ule ule wa kuwa na maombi binafsi kwa
Mungu wako na kutokukubali hadhi na heshima ya
Mungu kushindanishwa na wanadamu?

Mfumo wake wa maombi uliimarisha


mahusiano yake na Mungu kiasi ambacho
msimamo aliokuwa nao kwa Mungu
haukubadilishwa kwa kuakuangalia ni watu
wangapi wameamua kuacha kumuabudu Mungu
wake. Kiwango hiki cha mahusiano kilimpa kuendelea
kumshukuru na kumuomba Mungu bila kuacha na
matokeo yake Mungu wake ndiye aliyeshinda. Swali
langu tena kwako msomaji wangu, Je! Sheria
itakapobadilishwa ambayo inawataka asiwepo wa
kuomba kwa Mungu ili vitu vilivyotengenezwa na
wanadamu na visivyo Mungu, ukiangalia kila mahali
hata watu wale ambao uliwaamini nao wameanza
kuabudu hiyo miungu au sanamu, bado utaendelea na
msimamo wako wa kumuamini na kumtegemea
Mungu? Bado utaendelea kuomba kama ulivyokuwa
ukifanya tokea mwanzo? Ninakuombea kwa Mungu
yasiwepo mazingira, nyakati au chochote ambacho
kitazimisha moto wa maombi ndani yako katika Jina la
Yesu.

Ndipo mfalme Dario akasema “Mimi naweka


amri, ya kwamba katika mamlaka yote ya ufalme

72
wangu watu watetemeke na kuogopa mbele za
Mungu wa Danieli; maana yeye ndiye Mungu aliye
hai, adumuye milele, na ufalme wake ni ufalme
usioharibika, na mamlaka yake itadumu hata
mwisho. Yeye huponya na kuokoa, hutenda ishara
na maajabu mbinguni na duniani, ndiye
aliyemponya Danieli na nguvu za simba.” Danieli
6:26-27

Mfumo wako wa maombi utakusaidia kuzalisha


nguvu na imani kubwa kwa Mungu itakayokusaidia
kushinda nguvu za upinzani wowote katika nafasi
uliyopo au ambayo utakuwa nayo. Usienende
kikawaida maana wewe si wa kawaida, tengeneza
mfumo wa maombi utakaokuwa unaomba kila siku,
mifungo ya kila wiki na kila mwezi iwepo. Ili kufikia
maisha yenye ukuu na utukufu mkubwa wa Mungu
huna budi kuzingatia kanuni hii, maana ni ya muhimu
sana kwa mtu yeyote anayetaka kuwa na kesho yenye
mguso katika huduma, biashara, kazi, familia na kila
eneo la maisha yake.

73
Sura ya Saba

WATU WAKUU
HUANDALIWA SIRINI

V
itu vizuri na vikubwa huandaliwa sirini, watoto
hutungwa na kuzaliwa sirini, upasuaji na
kuokoa maisha hufanyika sirini, Yakobo
alifanyika kuwa Israeli alipokuwa sirini na Mungu.
Ukitaka kukwepa mahali pa sirini umetaka kuwa mtu
asiye na matokeo katika kizazi chako.

Ninavutiwa sana na habari za Musa jinsi Mungu


alivyomuandaa toka kuzaliwa kwake, namna
alivyolelewa na kukua hata akawa mtu mzima.
Tunazipata habari hizi tukisoma kitabu cha Kutoka
2:11 kwamba “Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu
mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake,
akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri
anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu
zake. Basi akatazama huko na huko, na alipoona
ya kuwa hapana mtu, akampiga Mmisri yule,
akamficha ndani ya mchanga.”

Hii tabia ya watu kutaka kujulikana na kukimbia


na vitu bila kupata utulivu wa kutosha imewagharimu

74
watu wengi sana wenye vitu vikubwa ndani yao. Musa
alikuwa na kitu sahihi cha Mungu lakini wakati
haukuwa sahihi kwa yeye kuanza kujionesha kwa watu
na kutaka kuwaokoa Israeli. Unapotaka kuchomoka na
kitu katika wakati ambao si wa Mungu, uwe na
uhakika utakiharibu na utashindwa kufika mwisho
mzuri kwa sababu ulikosa muda mzuri wa kuandaliwa.

Baada ya Musa kugundua alilianzisha kabla ya


muda ulioamriwa na mbingu, Farao alitaka kumuua na
asingekimbia kweli angeuawa na wana wa Israeli
wangetolewa Misri lakini si kwa mkono wa Musa bali
kwa mkono wa mtu mwingine. Ingekuwa hasara sana
kwa Mungu, na kwa wana wa Israeli wenyewe. Hii
ndio sababu Mungu ameweka kitabu hiki mikononi
mwako, kwamba ujue habari hizi kabla haujatoka
kwenda kumtumikia Mungu au kutumia hicho
alichokupa Mungu, na kama tayari umeanza
kutumikia shauri la Bwana kwenye maisha yako, basi
kikukumbushe ni mambo gani muhimu unayopaswa
kuyajua huko na namna ya kutembea na uwepo wa
Mungu siku zote anazokupa Mungu.

Toka Musa alipomkimbia Farao alipotaka kumuua


kwenye Kutoka 2:15 na Mungu alipomtokea Musa na
kumweleza kwamba anataka kumtuma kwa Farao
katika Kutoka 3:10 pana tofauti ya miaka arobaini. Hii
miaka arobaini aliitumia kuchunga kondoo za baba
mkwe wake kuhani wa Midiani aliyeitwa Yethro.

75
Miaka arobaini sio miaka aliyopoteza, kwa kawaida
unaweza ukaona Musa alisoma vizuri shule ya
darasani alipokuwa akilelewa na Farao kwa hiyo
kusingekuwa na haja ya yeye kupelekwa tena jangwani
miaka 40, kwanza msomi kwenda kuchunga kondoo
lazima watu waliona anapoteza muda, lakini Mungu
alikuwa anajua ni maandalizi ya namna gani ambayo
Musa aliyahitaji kwa kipindi chote hicho.

Unahitaji kukubali kuandaliwa, kutengenezwa


sirini na kuwa vile Mungu anavyotaka, kupata
ukomavu si tu wa kimwili , lakini pia wa kiroho na
kiakili. Mungu anapotengeneza mazingira ya wewe
kuandaliwa, anatengeneza mazingira ya kule
anakokutuma pia, anaweka utayari kwao ili muda
utakapofika waweze kukupokea na kushirikiana nawe
katika kile ambacho Mungu amekupa. Kabla ya wakati
utakutana na maswali kama “Ni nani aliyekuweka
wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu?” na
Musa akaogopa na kukimbia kwa sababu ndani yake
hakuna maandalizi yoyote ya kukabiliana na
changamoto za namna hiyo. Ukitoka kabla ya wakati,
hautaweza kuvumilia changamoto zitakapojitokeza,
utaogopa na kukimbia na mwisho kile kitu kitapotea
kabisa.

Fikiri kuhusu Yoshua mwana wa Nuni mtumishi


wa Musa; kijana aliyefuatana na Musa karibu kila
mahali akifundishwa njia za Bwana, alijifunza

76
kumsikiliza Mungu na kufuata sauti na maelekezo ya
Mungu. Kuna wakati Mungu alikuwa akimuita Musa
mlimani, anawaacha watu wote kisha anapanda na
Yoshua peke yao kwenda mlimani kwa Mungu, hii
ilikuwa ni ili kumuandaa kuwa kiongozi wa taifa la
Israeli baadae. Angalia “BWANA akamwambia
Musa, Njoo huku juu kwangu mlimani, uwe huku;
nami nitakupa mbao za mawe na ile sheria na
hiyo amri niliyoiandika ili uwafundishe. Musa
akaondoka na Yoshua, mtumishi wake, Musa
akapanda mlimani kwa Mungu. Akawaambia
hao wazee, Tungojeeni hapa, mpaka
tutakaporudi kwenu; na tazameni, Haruni na
Huri wapo pamoja nanyi; kila mtu aliye na neno
na awaendee.” Kutoka 24:12-14. Kwa nafasi
aliyokuwa nayo Musa, ungefikiri asingemuacha Haruni
kwa sababu ya nafasi yake na umuhimu wake, lakini
aliwaacha wote na kumchukua Yoshua mtumishi wake.

Katika kizazi hiki kuna kitu kikubwa


kimekosekana, nacho ni watu wa kuandaa kizazi
kijacho katika nyanja mbalimbali lakini pia watu
wenyewe kukubali kuandaliwa mapema. Tuna vijana
wengi ambao ndani yao wanachemka kweli ila
kumekosekana watu wa kuwaandaa kwa ajili ya kule
ambako Mungu amewakusudia. Mtu mmoja alisema
“success without a successor is a failure.” Musa
alimfundisha Yoshua karibu kila kitu kinachohusu
uongozi.

77
Unahitaji kutulia sirini ili utengenezwe, usikimbie
kimbie tu, kaa utulie mbele za Bwana ili Mungu apate
kuachilia maelekezo yote ya huduma na utumishi
alioweka ndani yako. Katika kipindi chote ambacho
Yoshua alikuwa chini ya Musa haumsikii akichomoka
na kitu chake mwenyewe licha ya kwamba alikuwa
mtu hodari sana wa vita, alisubiri wakati ulioamriwa
kwa ajili yake, na alipotoka alikuwa mtu mkuu sana.

Ukisoma kitabu cha Yoshua 1:2 ni rahisi sana


ukaona kama vile Mungu alipoona Musa amekufa basi
akamchagua mtu yeyote tu aliyeitwa Yoshua ili
kuwachukua wana wa Israeli na kuvuka nao ng’ambo
ya Yordani. Mungu akamwambia Yoshua “Musa
mtumishi wangu amekufa; haya basi, ondoka,
vuka mto huu wa Yordani; wewe na watu hawa
wote, mkaende hata nchi niwapayo wana wa
Israeli.” Kabla ya Mungu kumwambia maneno haya
Yoshua, alikuwa na safari ndefu sana pamoja naye ya
kumuandaa kabla ya hapa. Walishinda na Musa
mlimani, kama Musa alifunga siku arobaini mchana na
usiku, Yoshua naye alifunga siku hizo hizo. Mungu
alipomuita Musa na kuzungumza naye mlimani, kuna
wakati walienda na Yoshua naye akasikiliza maelekezo
yale.

Kuna wakati Mungu aliwatembelea kwenye hema


ya kukutania, Yoshua naye alikuwemo tena upako
unapokuwa mkubwa Musa alimwacha Yoshua humo.

78
Wana wa Israeli walipokosea, Yoshua alikuwa anaona
na hata hatua ambazo Musa alikuwa anazichukua
Yoshua pia alikuwa anaona. Aliandaliwa kwa kipindi
kirefu sana kabla ya kuitwa na kupewa jukumu la
kuwaongoza Israeli. Alijifunza mema na mabaya ya
wana wa Israeli, uzuri na changamoto za safari ile kwa
ukaribu sana.

Jifunze kwa Mifano hii.

Daudi mwana wa Yese.

Siku zote tunapozungumza habari za namna watu


wakuu wanavyoandaliwa sirini, hatuwezi kuacha
kusema habari za Daudi mwana wa Yese. Huyu kijana
Mungu alimuandaa kwa ajili ya kuongoza taifa lake;
Biblia inazisema habari zake kwamba akiwa angali
bado machungani alikuwa;

Hodari wa vita, alijijenga na kujitengeneza kiasi


ambacho simba na dubu walipotaka kushambulia
kondoo wa baba yake, aliwaua kwa mikono yake.

Alikuwa mpiga kinubi maarufu na stadi; sifa hii


ilimpa kazi Ikulu ya Sauli na kuwa mshika silaha za
vita wa Sauli.

Alikuwa ni mtu anenaye kwa burasa; unajua sio


rahisi kumkuta mtu wa namna hii ambaye ni hodari
wa vita na aweze kunena kwa busara.

79
Alikuwa ni mtu mzuri Biblia inasema alikuwa na
umbo la kupendeza, mwekundu na mwenye macho
mazuri. Zaidi ya yote Bwana alikuwa pamoja naye.
Tunasoma “Ndipo akajibu mmoja wa watumishi
wake akasema, Tazama, nimemwona mwana
mmoja wa Yese, Mbethelehemi, aliye stadi wa
kupiga kinubi, tena ni mtu shujaa, hodari wa
vita, anenaye kwa busara, mtu mzuri, ambaye
BWANA yu pamoja naye” 1 Samweli 16:18

Mambo yote haya Daudi alikuwa nayo tayari hata


kabla hajawa mfalme wa Israeli, pengine hata ndoto ya
kuwa mfalme hakuwa nayo. Mchakato wa kuandaliwa
ni wa muhimu zaidi kuliko nafasi yenyewe ya kutimiza
wito wako. Kuna watu mnaweza msijue mlichoitiwa
lakini tayari mpo kwenye mchakato wa kuandaliwa
kuwa watu fulani, ndio maana utashangaa watu
wanasema mbona hatukutarajia mtu huyu ametokea
wapi? Wasijue Mungu alikuficha mahali katika
kukuandaa ili uweze kutokea saa ile.

Mke mzuri ni yule aliyeandaliwa kuwa mke, mume


mzuri ni yule aliyeandaliwa kuwa mume, kiongozi
mzuri ni yule aliyeandaliwa na kupitia mchakato ili
awe kiongozi mzuri na bora, vile vile mtumishi mzuri
ni yule aliyeandaliwa kuwa mtumishi mwaminifu wa
Mungu. Ukiangalia kizazi tulichonacho, utagundua
watu wengi sana hawakupitia mchakato wa
kuandaliwa; iwe kwenye ndoa, kwenye siasa, katika

80
kanisa ndio kuna hatari zaidi kwa sababu watu
hukurupuka hata kabla hawajaiva kuwa vile Mungu
aliwataka wawe. Kubali kuandaliwa ili utumike katika
kiwango ambacho Mungu alikukusudia.

Yothamu.

2 Mambo ya Nyakati 27:6, yeye alijitengenezea njia


yake mbele za Mungu. “Basi Yothamu akawa na
nguvu, kwa kuwa alizitengeneza njia zake mbele
za BWANA, Mungu wake.” Hiki ndicho kilikuwa
chanzo cha nguvu zake na fahari yake kubwa,
alizitengeneza njia zake mbele za Mungu. Wewe na
mimi tunahitaji kuzitengeneza njia zetu mbele za
Bwana kwa kukaa chini na kukubali kujifunza na
kupokea maelekezo yote toka kwake tukiwa sirini.

Mungu anaweza kukuinua toka chini na kesho tu


ukawa juu, lakini anajua akifanya hivyo ni rahisi
kwako kuharibikiwa kuliko kunufaika na hicho kitu.
Wana wa Israeli wangeweza kutoka Misri na kwa siku
chache wakafika Kaanani, lakini Mungu
aliwazungusha kwa njia ya jangwani; unafikiri Mungu
hakuweza kuwasaidia wavuke haraka lile jangwa na
kujikuta wako upande wa pili? Biblia inasema
“Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha
watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa
njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya
karibu; maana Mungu alisema, Wasije

81
wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na
vita, na kurudi Misri; lakini Mungu
akawazungusha hao watu kwa njia ya bara
kando ya Bahari ya Shamu; wana wa Israeli
wakakwea kutoka nchi ya Misri hali wamevaa
silaha.” Kutoka 13:17-18

Mungu anajua, akikuinua leo na kesho ukawa juu,


ni rahisi sana kwako kuikana Imani na kurudi nyuma,
lakini pia anajua hautaweza kuhimili vita na
changamoto zitakazotokea njiani, hii ndio sababu
mtumishi yeyote wa Mungu lazima apitie kipindi cha
kuandaliwa na Mungu mwenyewe, apandishwe milima
na mabonde, aimarishwe kiakili, kiroho, apambane na
mambo makubwa na mazito na ayashinde maana
hatma yake sio ndogo ni kubwa inahitaji ukomavu
katika maeneo yote.

Paulo.

Paulo anasema katika Wafilipi 4:12 “Najua


kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali
yoyote, na katika mambo yoyote, nimefundishwa
kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na
kupungukiwa.” Swali langu kwako msomaji, Paulo
anaposema amefundishwa, unafikiri alifundishwa na
nani? Bila shaka na Mungu. Sasa ona, Mungu anaweza
kukufundisha kuwa na njaa na kupungukiwa, unafikiri
ni shule rahisi? Sio rahisi maana unaweza ukaomba

82
ukijua ni Shetani amesababisha upungukiwe kumbe ni
Mungu na lengo lake sio baya ni zuri kabisa,
anaruhusu upitie kipindi cha njaa na kukosa mahitaji
muhimu ili tu kukuimarisha.

Kubali kupitia hayo yote ili baadae utoke kama


dhahabu. Usiwe kama wale ambao akikosa kidogo tu
anaacha kabisa na huduma, anaacha kumtumikia
Mungu, anaona kama vile Mungu amegeuka adui yake,
sikia mtu wa Mungu kama kweli unataka kufikia
viwango vikubwa vya utukufu wa Mungu hauna budi
kupita shule hiyo maana watu wakuu huandaliwa
sirini.

Wakati mwingine badili maombi, usiombe Mungu


akufanye ujulikane haraka, omba Mungu akufanye vile
alivyokusudia uwe, akutengenezee njia utakayopita ili
uweze kusimama katika kusudi lake. Siku zote
kilichopatikana haraka hupotea bila habari.

Eliya Mtishbi.

Ukisoma kitabu cha 1 Wafalme 17:1 utaona biblia


inasema “Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa
Gileadi, akamwambia ahabu, Kama Bwana,
Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama
mbee zake…” Hii ilikuwa mara ya kwanza Eliya
anatajwa katika Biblia. Katika sura zilizopita hakuna
mahali wanazungumza habari zake, lakini katika sura
hii ametokea na anamwambia Ahabu ujumbe mzito

83
sana. Hatuambiwi baba yake nani, wala mama yake ni
nani, Wala amelelewa katika mji upi; hakuna mahali
wanasema habari hizi lakini tayari ni mtumishi na
nabii wa Mungu aliye hai.

Umewahi kujiuliza Eliya alikuwa wapi kabla ya


hapo? Alikuwa mahali pa siri akiandaliwa na Mungu
mwenyewe, saa aliyotokea kwa Israeli kila mtu alijua
Eliya ametumwa na Mungu. kuna watu (wa kike na wa
kiume) hamjulikani sana, hata mkienda mahali
hakuna mtu anajua kama mpo, usipate shida, saa
inakuja ya kudhihirishwa kwako, watu watajiuliza
ulikuwa wapi siku zote? Ulikuwa mahali pa siri pa
kuandaliwa na Mungu. Mafuta yatakayokuwa juu
yako, upako, uvumilivu, ukomavu na kibali vitakuwa
sio vya kiwango cha kawaida. Kubali kukaa mahali pa
siri uandaliwe.

Kama hauko tayari kukaa sirini, hauko tayari


kutumiwa na Mungu.

Mungu huandaa watu wakuu sirini, watu


watakaopindua ulimwengu, watakaobadili historia za
maisha ya watu, watakaogusa na kubadilisha familia,
jamii na taifa wanaandaliwa mahali pa siri, mahali
ambako si kila mtu anaona. Kubali hivi sasa kutulia na
kumtazamia Mungu mahali pa siri.

Kutaka kumtumikia Mungu bila kupita shule yake


ya mahali pa siri ni sawa na kutaka kulitumikia jeshi

84
bila kupitia mafunzo ya kijeshi. Usiogope kukaa mahali
pa siri. Kuna wakati unataka kusema kilicho ndani
yako na hakuna mtu anataka kusikia hata sauti yako,
usipate shida, wakati unakuja ambapo kila mtu
atatamani kuisikia sauti yako. Unataka kuimba lakini
ni kama watu hawana muda na wewe, una kitu ndani
yako unatamani watu wangekiona ila ni kama vile
haupo maana kila mtu anaendelea na shughuli zake.
Tulia wakati huu wa kuandaliwa, siku zinakuja na
sasa zipo karibu ambapo watu watataka sana
ulichonacho maana kimeandaliwa kwa ajili ya wakati
kama huo.

Usihangaikie umaarufu na kutaka kujulikana,


badala yake kaa kwenye uwepo wa Mungu, vyote
vitakuja vyenyewe wakati utakapofika. Usiumie
kwamba hakuna anayekujua wala anayetambua uwepo
wako, fahamu kwamba Mungu anakujua na anajua
mahali ulipo na unayopitia. Mungu hakumtuma
Malaika kwenda kumtafuta Gideoni, bali alienda moja
kwa moja mahali alipo maana alikuwa anamjua na
anajua atampataje. Mungu anakujua kwa jina lako.
Kubali kupitia mchakato huu wa kuandaliwa sirini,
kuna baraka na utukufu mkubwa mbele yako.

85
Sura ya Nane

JIBORESHE

I
li uweze kufikia malengo yako ya kuwa mtu fulani
au kufikia hatua fulani kihuduma, kielimu au
kibiashara unahitaji kujiboresha kila siku kusudi
uweze kufikia kiwango unachokusudia kufika.

Aposto Shemeji Melayeki aliwahi kusema “Kila


siku ni siku kuu, chora picha” akiwa na maana
kwamba kila siku hakikisha unajiboresha kuelekea
kwenye hatma yako kubwa. Chochote unachotaka
kitokee kesho lazima ukifanyie kazi leo na kila siku.
Kama wewe ni mfanya biashara basi hakikisha kila
siku unapata maarifa sahihi kuhusu biashara

Unayetaka kuwa mwimbaji mkubwa basi kila siku


hakikisha unafanya kitu kuelekea kwenye picha kubwa
unayoiona ndani yako. Fanya mazoezi, andika hata
ubeti mmoja kila siku, kaa na waimbaji
waliokutangulia, waulize maswali na ujifunze kwao.

Unataka kuwa mwandishi mkubwa? Basi tafuta


maarifa kwa waandishi waliokutangulia, jifunze
kuhusu uandishi. Mwalimu Makwaya aliwahi
kuniambia “Kila siku andika kitu, isipite siku
hujaandika chochote” hakuwa anamaanisha niandike
kitu chochote tu hata kama hakina maana, najua

86
unajua kwamba huwezi kutoa kitu usichonacho, kama
alitaka niandike kitu kila siku basi alitaka kila siku
nisome kitu kipya ili nipate kitu cha kuandika kila
siku.

Vivyo hivyo kama unataka kuwa msusi tafuta


kujifunza kuhusu masuala yote yanayohusu ususi,
unataka kuwa mtengenezaji mzuri wa keki basi hauna
budi kujifunza kila siku vitu vipya vitakavyokufanya
uwe bora zaidi. Jiboreshe kila siku.

Jiboreshe kwa kutafuta taarifa sahihi ya vile


unavyotaka kuwa siku za usoni. Watu wote unaowaona
wamefanikiwa, ukiwauliza watakuambia namna
walivyoitumia vizuri kanuni hii ya kujiboresha. Chora
picha ya kule unataka kwenda halafu kila siku koleza
wino hapo. Baada ya miaka miwili au mitano, watu
watakujua kupitia kile ambacho uliamua kujiboresha
kwacho, kila ambacho uliamua kuwekeza muda wako,
nguvu zako, akili yako na hata uwezo wako wote hapo
katika kujiboresha kitaamua aina ya mtu na aina ya
matokeo utakayokuwa nayo.

Ni kweli kwamba iko neema ya Mungu na upako


unaoweza kutusaidia, lakini fahamu kwamba upako
unafanya kazi kulingana na kiwango cha maarifa uliyo
nayo.

Tukiwa chuo cha uongozi cha WOFBI Tz,


nilivutiwa sana na Pastor Chris aliyekuwa mmoja wa

87
walimu, jinsi alivyokuwa akifundisha. Mafundisho
yake, na namna alivyokuwa anafundisha nilikuwa
nikihisi nguvu za Mungu zikitembea ndani yangu,
wakati anaelekea mwisho wa kozi ile tulimuuliza
anatumia jina gani kwenye mitandao ya kijamii ili
tuweze kumfuatilia huko. Tulishangazwa sana na
majibu yake, alituambia hana mtandao wowote
anaotumia zaidi ya whatsapp, tulipoendelea kumuuliza
zaidi alitueleza kwamba hana muda wa kuwa huko
kwa sababu muda mwingi kama sio wote anautumia
kusoma neno, kuomba, kujifunza mambo mbalimbali
kupitia vitabu na kufanya kazi yake ya Uchungaji kwa
bidii zote. Akaongeza kusema; tunachokiona akiwa
anafundisha wala sio upako, ni vile amesoma na
kusoma na kusoma kuhusu kitu alichokuwa
anatufundisha kiasi ambacho kimemfanya amekuwa
bora.

Kiwango cha maarifa uliyonayo kwenye eneo fulani


kitazalisha upako kwenye maisha yako kiasi ambacho
watu watahudumiwa na Mungu kwa upako na maarifa
uliyo nayo. Haijalishi ni kwa uchache kiasi gani,
usiache kujiboresha katika kile unataka utambulike
nacho.

Daudi kabla hajawa Mfalme wa nchi, alikuwa


mchunga kondoo na mpiga kinubi maarufu. Roho ya
BWANA ilipomwacha Sauli, roho mbaya kutoka kwa
BWANA ilianza kumsumbua, Sauli alishauriwa atafute

88
mtu stadi wa kupiga kinubi ili ile roho mbaya
itakapoanza kumsumbua, basi kipigwe kinubi vizuri na
ile roho mbaya itamwacha. Alitafutwa Daudi mwana
wa Yese, angalia maneno haya “Ndipo akajibu
mmoja wa watumishi wake akasema, Tazama,
nimemwona mwana mmoja wa Yese,
Mbethelehemi, aliye stadi wa kupiga kinubi, tena
ni mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye kwa
busara, mtu mzuri, ambaye BWANA yu pamoja
naye” 1 Samweli 16:18

Angalia sifa alizokuwa nazo Daudi; Stadi wa


kupiga kinubi, mtu shujaa, hodari wa vita, anenaye
kwa busara, mtu mzuri, ambaye BWANA alikuwa
pamoja na yeye. Rudi nyuma kidogo kitabu cha 1
Samweli 16:11 anasema “Kisha Samweli
akamwambia Yese, Watoto wako wote wapo hapa?
Naye akasema, Amesalia mdogo wao, na tazama
anawachunga kondoo. Basi Samweli
akamwambia Yese, tuma watu wamlete; kwa
sababu hatutaketi hata atakapokuja huku”

Swali langu ni hili, kwa sifa alizokuwa nazo Daudi


ilikuwa sawa kutokuwepo kwenye dhabihu ile? Jibu
ninalopata ni kwamba mzee Yese pamoja na watoto
wake wakubwa hawakujua kilichokuwa ndani ya
Daudi wala uwezo wake.

89
Alipotumwa achunge kondoo za baba yake,
alitumia muda huo kujinoa na kujiboresha kupiga
kinubi mpaka akawa stadi wa kupiga kinubi. Mfalme
Sauli alipotafuta mpiga kinubi stadi, hakuonekana
mwingine isipokuwa Daudi mwana wa Yese. Muda
aliokuwa machungani, hakuwa anajilaumu kwamba
familia imemuacha au ameonewa, hakuwa analaumu
kwamba hajapelekwa shule kama ndugu zake, alitumia
muda huo kama fursa kujiandaa na kujiboresha mpaka
akafikia kiwango cha ushujaa; walipotokea Simba na
Dubu kutaka kuwararua wanyama wake aligeuka na
kupambana nao hata akawashinda. Alipoenda
kuwatembelea kaka zake walipokuwa vitani na kukuta
Goliathi yule Mfilisti akiyatukana majeshi ya Bwana,
alijitosa katika vita ile na akamshinda Goliathi kwa
Jina la Bwana (1 Samweli 17:31-51)

Daudi ndiye mchunga kondoo pekee aliyekuwa na


ajira Ikulu ya Sauli huku akiwa anaendelea na kazi
yake ya uchungaji. “Basi Daudi alikuwa akienda
kwa Sauli na kurudi ili awalishe kondoo za baba
yake huko Bethlehemu” 1 Samweli 17:15

Usiache kujiboresha, hata kama mazingira yako ni


duni, unahisi umeachwa, watu hawakuheshimu,
hawakupi nafasi; usijali. Tumia nyakati hizo kama
fursa kwako ya kujiboresha ili uwe bora zaidi. Siku
watakayokupa nafasi kidogo, itumie fursa hiyo

90
kuwadhihirishia kwamba unaweza na wala wewe sio
bahati mbaya.

91
Sura ya Tisa

UPINZANI NI SEHEMU
YA MAISHA
UNAPOINGIA HATUA
NYINGINE

F
ahamu jambo hili kwamba; upinzani ni sehemu
ya maisha unapoingia hatua nyingine, inaweza
kuwa katika huduma, elimu, kazi, biashara au
katika ndoa. Barbara Wentroble katika kitabu chake
cha God’s Purpose for your life ameandika hivi; “New
level new devil” akiwa na maana kwamba kila
unapopiga hatua kutoka ulipo kuelekea hatua ya juu
zaidi ya hapo, kuna upinzani utakutana nao ambao
haujawahi kukutana nao au haukuwepo kabisa. Hatua
yoyote ile ina kawaida ya kuja na vikwazo, upinzani na
kila aina ya vizuizi. Mfano mtoto anapotaka kuzaliwa,
licha ya furaha iliyo kubwa kwa mama mzazi, lakini
kuna maumivu mengi anayapitia, uchungu na machozi
kabla ya furaha. Vivyo hivyo mtoto anapoendelea
kukua, anapotoka hatua moja kwenda nyingine pia
huwa sio rahisi kwake, hatua hizo huambatana na

92
maumivu na homa za hapa na pale. Hii ni asili na
kawaida kwa mwanadamu.

Yesu alipokuwa anafanya kazi ya uselemala katika


nyumba ya baba yake, hakuna aliyekuwa anamfuatilia
wala kuuliza/kuhoji chochote kumuhusu, lakini
alipoanza huduma yake akiponya, kuokoa na kutoa
mapepo, walianza kuhoji nguvu alizokuwa nazo na
kwamba anafanya hayo kwa mamlaka ya nani?

Alipoanza kufundisha katika masinagogi


akizunguka huku na huko hali amejaa mafundisho
yenye hekima na ufunuo wa hali ya juu, walianza
kuhoji anayoyasema ameyatoa wapi? (Mathayo 13:54-
56). Alipotoa mapepo na kufanya ishara nyingi katika
watu walisema anatoa pepo kwa Beelzebuli mkuu wa
mapepo. Na wengine walihoji anafanya hayo kwa
mamlaka ya nani? (Luka 11:14-15, 20:1-2). Upinzani
huu uliendelea kwa muda wa miaka mitatu na nusu
aliyotumika alipokuwa hapa duniani.

Petro alipokuwa mtu wa kawaida na mvuvi wa


samaki hakuna aliyekuwa anashida naye, lakini
alipoanza huduma kisha akamponya kiwete katika
mlango ulioitwa Mzuri na kufanya ishara kubwa
katika watu, walimshangaa sana maana
hawakutarajia kuona kitu kama kile kikifanywa na
Petro na Yohana.

93
Walipoendelea kuhubiri huku mafundisho yao
yakibadili maisha ya watu kwa kasi ya ajabu,
Masadukayo wakawatokea na kuwakamata kisha
wakawaweka gerezani hata asubuhi, baadae
wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani
ninyi mmefanya haya? Matendo ya Mitume 3:6-7, 4:3-7.
Maswali ya jinsi hii hayakuwepo Petro alipokuwa
mvuvi wa samaki, yalisubiri atokee katika udhihirisho
kamili wa kile ambacho Mungu amemtuma kwacho
duniani.

Si hao tu, hata Stefano kabla hajaanza kufanya


maajabu na ishara kubwa kwa watu, alikuwa mtu wa
kawaida, Biblia imeanza kumtaja katika sura ya sita
ya kitabu cha Matendo ya mitume ikimtambulisha
kama mtu aliyejaa Imani na Roho Mtakatifu.

Stefano alijaa nguvu kutoka juu, hekima na ufunuo


wa kiungu na alipoanza kutumia vizuri kilicho ndani
yake, ndipo wakuu wa masinagogi walipojadiliana naye
juu ya uwezo anaotumia na kwamba anafanya kwa
mamlaka ya nani. Biblia inasema hawakuweza
kushindana na ile hekima iliyokuwa ndani yake wala
huyo Roho aliyesema naye. Walipoona wameshindwa
kumshtaki, walimtengenezea mazingira ya kumshitaki
kwa uongo, na mwisho wakamkamata na kumpiga kwa
mawe hata akafa. Matendo ya Mitume 6:5, 8-15, 7:59-
60.

94
Ukiwa mtu wa kawaida na katika hatua uliyopo ya
kawaida, hautaona maswali, kuhojiwa au hata
kufuatiliwa na watu, lakini pale utakapochukua hatua
ya kusogea kiwango kingine cha utukufu na kutumia
vipawa na karama zilizo ndani yako vyema, utakutana
na upinzani mkubwa kutoka kwa watu wako wa
karibu, rafiki zako, watu wanaofanya kitu kama cha
kwako, wale uliowaamini wangekuwa mstari wa mbele
kukushika mkono na hata kwa watu usiowajua. Hii ni
kwa sababu mioyo ya watu walio wengi haiko tayari
kupokea mabadiliko na kuruhusu wengine waende juu
zaidi ya pale walipokuwa.

Ndio maana ni muhimu sana kujitathmini na


kuhesabu gharama kabla haujaanza safari yoyote ili
utakapokutana na upinzani uweze kustahimili na
kuwa na sababu inayokufanya usiache kufanya
unachokifanya.

Mungu anapowaandaa watu wake sirini, sababu


mojawapo ni kwamba watakapotokea katika uhalisia
wa kile wanacho kifanya, waweze kushinda upinzani
wote utakaotokea, misukosuko, kusemwa vibaya,
kusingiziwa na hata kutengwa na watu wako wa
karibu.

95
Sura ya Kumi

TUMIA UWEZO WAKO


WOTE

E
sau na Yakobo walipokuwa tumboni mwa
mama yao, Mungu alikuwa amewaweka kama
mataifa mawili makubwa, lakini matokeo yake
tunaona Yakobo peke yake anafikia hatua ya kuwa
taifa huku Esau akishindwa kabisa kufikia ndoto hiyo
(Mwanzo 25:23) Kuishi chini ya kiwango au uwezo
uliozaliwa nao kumewafanya watu wengi sana kuishi
nje ya kusudi la Mungu kwenye maisha yao; badala ya
kuwa vile Mungu alivyokusudia toka mwanzo
unajikuta unaishi kama mtu wa kawaida na asiye na
kitu ndani yake.

Gideoni alikuwa na uwezo mkubwa ndani yake


ambao ulitosha kabisa kulisaidia taifa dhidi ya uonevu
na mateso waliyoyapata kutoka kwa Wamidiani.
BWANA akamwambia “Enenda kwa uwezo wako
huu, ukawaokoe Israeli na mkono wa Midiani”
Waamuzi 6:14, lakini kwa sababu ya kutokujua uwezo
aliokuwa nao alisababisha yeye, familia yake na taifa
zima waishi kama watu duni na wasio na nguvu.
Uwezo uliokuwa ndani ya Gideoni haukuletwa saa ile
na Malaika, ulikuwepo siku zote, lakini

96
haukugundulika wala kutumika ipasavyo na
ukasababisha hasara kubwa sana kwa taifa la Israeli.

Uwezo ulio ndani yako usipogunduliwa, na


kutumiwa vizuri, unaweza ukasababisha hasara kwako
mwenyewe, familia yako, watu ambao Mungu alitaka
wanufaike na ulichonacho mpaka Mungu mwenyewe
anaingia hasara kwa kutokujua kwako.

Fahamu kwamba kila mwanadamu aliyezaliwa na


akawekwa duniani basi kuna kitu Mungu amempa
ndani yake; hata kama kila mtu atakuona wewe ni mtu
wa kawaida, fahamu kwamba unacho kitu tena
kikubwa cha Mungu ambacho dunia inakisubiri toka
kwako.

Kitabu cha Mathayo 25:14-15 anasema hivi


“Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri,
akawaita watumwa wake, akaweka kwao mali
zake. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja
talanta mbili, na mmoja talanta akasafiri”. Kwa
mujibu wa mistari hii, kila mmoja kuna kitu Mungu
ameweka kwenye maisha yake, tena sio kitu cha
kawaida, mwandishi wa kitabu hiki ameita “mali zake”
ni vitu vya thamani na vikubwa Mungu amewekeza
kwenye maisha yako, ni wajibu wako kuvigundua,
kuvitafuta na kuviishi kama ambavyo Mungu
amekusudia kwako.

97
Usifukie talanta na kipawa ambacho Mungu
ameweka kwenye maisha yako kama yule mtumwa
aliyepokea talanta moja akaenda akaichimbia chini
akaificha. Si wingi wa talanta unaoweza kukufanya
uzalishe zaidi, bali uwezo wa kujua kwamba
ulichopewa si kwa ajili yako, hivyo kama utatumia
akili na kwa uaminifu kuzalisha kwa kadiri ya neema
ya Mungu na kusudi lake kwako, utapata matokeo
makubwa. Siku ile hatutatoa hesabu kuangalia wingi
au uchache wa matokeo bali kwa kadiri ya makusudi
ya Mungu na kile alichoweka kwako. Ukipewa vingi
kwako vitatakwa na zaidi.

Tunajua sote kwamba, Elisha mwana wa Shafati,


pamoja na mambo makubwa ambayo aliyafanya,
alishikwa na ugonjwa naye akafa. Kifo chake
kimetofautishwa sana na vifo vya watangulizi wake
kama Ibrahimu, Isaka, Yakobo na baadhi ya wafalme
wa Israeli. Biblia inasema huyu alipokufa, akazikwa,
lakini haisemi akapumzika na baba zake kama
unavyoona kwa watu wengine wanapokufa. Elisha
alipokufa, akazikwa, lakini mifupa yake ilikuwa na
upako ule ule kama aliokuwa nao akiwa hai.

Tunasoma “Elisha akafa, nao wakamzika. Basi


vikosi vya Wamoabi wakaingia katika nchi
mwanzo wa mwaka. Ikawa, walipokuwa
wakimzika mtu, angalia, waliona kikosi;
wakamtupa yule mtu kaburini mwa Elisha; mara

98
yule maiti alipoigusa mifupa ya Elisha,
alifufuka, akasimama kwa miguu yake” 2
Wafalme 13:20-21.

Nataka uone kwamba, toka Elisha alipozikwa


mpaka siku wanamtupa yule maiti kwenye kaburi la
Elisha kulikuwa kumepita siku nyingi kiasi ambacho
tayari mwili wa Elisha ulikuwa umekwishaoza na
mifupa imeanza kuonekana. Kwa sababu kama
ingekuwa ni kipindi kifupi asingetuambia kwamba
alipogusa mifupa ya Elisha.

Sasa angalia; Elisha amekaa kaburini siku za


kutosha lakini bado ule upako uliokuwa juu yake
unaendelea kufanya kazi. Hii inamaanisha hakuwa
ametumia kila kitu alichopewa ndani yake, licha ya
kufanya miujiza mingi kwa watu na kulisaidia taifa la
Israeli kushinda vita nyingi. Ninachotaka kusema ni
kwamba, chochote ambacho Mungu ameweka ndani
yako tumia ipasavyo kwa nguvu na uwezo wako wote
mpaka siku utakayolala tuseme kama Daudi kwamba
baada ya kulitumikia shauri la Mungu, umelala
(Matendo ya Mitume 13:36)

Elisha alilala kaburini na upako wa kuponya


wagonjwa, wewe usilale na vipawa vya kuhudumia
watu, Usilale na mawazo mazuri ya kulivusha taifa,
familia na jamii yako; usilale na mbegu za ukuu ndani
yako; usilale na ubunifu ulionao; usilale na maarifa

99
hayo, wako watu wengi sana wanayasubiri; usilale na
mawazo ya miradi mikubwa ndani yako; Chochote
ambacho Mungu ameweka ndani yako si kwa ajili yako
bali ni kwa ajili ya watu, tumia kwa kadiri ya nguvu
unazojaliwa.

100
Sura ya Kumi na Moja

USIOGOPE CHUKUA
HATUA

H
ili ndilo jambo ninaloweza kukuambia kijana
na mpendwa wangu. Kubali kuchukua hatua
kuelekea kutimiza ndoto na maono katika
maisha yako. Usisubiri mpaka ufunuliwe kila kitu ili
kujua kama upo tayari kuanza kuchukua hatua au la,
wakati mwingine Mungu huachilia picha ya alichoweka
ndani yako kidogo kidogo, na kwa kadiri ambavyo
utaendelea kuchukua hatua ndivyo ambavyo
ataendelea kuachilia zaidi. Hatua ndogo ndogo nyingi
huzaa kitu kikubwa, hatua ndogo ndogo zilizojaa Imani
na uvumilivu huzaa matokeo makubwa sana siku za
usoni. Usiogope kuchukua hatua.

Tuchukue mfano wa Ibrahimu baba yetu wa Imani,


Mungu alimwambia atoke katika Uru wa Wakaldayo
aende mahali pale atakapomwambia, Ibrahimu alianza
kuchukua hatua licha ya kwamba hakujua ni wapi pa
kuelekea lakini alichukua hatua. Biblia inasema “Kwa
Imani Ibrahimu alipoitwa aliitika, atoke aende
mahali pale atakapopapata kuwa urithi; akatoka

101
asijue aendako.” Waebrania 11:8. Neno hili
linatuonesha Ibrahimu alipoitwa na Mungu atoke
katika nyumba ya baba yake alitii ile sauti na
akachukua hatua asijue aendako. Hatua ya kwanza ina
nguvu sana kuamua kesho yako.

Kuna mambo usipochukua hatua ya kwanza


huwezi kuona matokeo yake, kuna vitu usipochukua
hatua vinabaki kama vilivyo au kuharibika kabisa,
kuna nyakati usipochukua hatua hata jina lako
linapotea na kusahaulika kabisa tusijue kama aliwahi
kuwepo mtu kama wewe. Kubali hivi sasa kuchukua
hatua. Kuchukua hatua ni ishara ya utii kwa Mungu.
Kutii hakuangalii wala hakuulizi itakuwaje baadae, ila
unafanya ukiamini aliyesema ni mwaminifu naye
atafanya.

Anza kuchukua hatua kuelekea kesho yako njema,


anza kuchukua hatua kuelekea kutimiza maono na
ndoto kubwa ulizonazo. Hakuna namna tutaona kile
ulichonacho mpaka umechukua hatua, watu wengi
wanakufa na vitu vikubwa ndani yao kwa sababu
waliogopa kuchukua hatua ya kwanza kuelekea
kwenye kesho yao.

Vikwazo vipo, changamoto zipo, magumu yapo na


watu wanaokatisha tamaa pia wapo, lakini hivi vyote
havikuzuii wewe kuchukua hatua ya kwanza.

102
Biblia inatahadharisha juu ya watu waoga kwa
namna ya ajabu sana. Angalia katika kitabu cha
Ufunuo 21:8 anasema “Bali waoga na wasioamini,
na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na
wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo
wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo
moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.” Swali
langu, kwanini waoga waende katika ziwa la moto? Hili
jambo limenipa kutafakari sana kwamba kumbe
Mungu anatazama uwoga kama dhambi. Mtu mwoga
anafananishwa na mzinzi, mwasherati, mwabudu
sanamu na mchawi. Tafsiri isiyo rasmi ya woga ni hali
ya kusitasita kuthubutu kufanya mambo fulani kwa
kuangalia mazingira yanayokuzunguka na kuwa na
mashaka juu ya matokeo yatakayotokea.

Kibiblia woga ni kinyume kabisa cha Imani, ni hali


inayopingana na Imani, kama Biblia inasema Imani ni
kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo na bayana ya
mambo yasiyoonekana, basi woga ni kutokuwa na
uhakika wa mambo unayotarajia wala hauna bayana
yoyote ya mambo yasiyoonekana yatakayotokea.

Katika Waebrania 10:38 Biblia inasema “Lakini


mwenye haki wangu ataishi kwa Imani; Naye
akisita-sita, roho yangu haina furaha naye”
Niliposoma msitari huu nilielewa kwanini waoga
wamefananishwa na wazinzi na wasioamini. Kusita-
sita kuchukua hatua za kufanya kile ambacho Mungu

103
amekupa kufanya kwa kigezo cha kuogopa watu,
Mungu hapendi, kwake hilo jambo analifananisha na
kutoamini.

Tuna watu wengi sana ambao Mungu amewaita


kweli na anataka wafanye kile alichowaitia ila woga
umewakwamisha, wanasita-sita kama vile hawana
uhakika na kile wanataka kufanya. Kuna watu wana
maono mazuri na makubwa ya kibiashara na mitaji ipo
au wanajua namna ya kuipata lakini woga
umewakwamisha. Una maono ya kuwa mtu fulani
baadae na kila ukijiangalia unaona mazingira yote ya
kuwa vile unataka lakini woga unakurudisha nyuma,
matokeo yake umebaki palepale, haujapata faida wewe,
umekosesha ufalme wa Mungu matunda
yaliyokusudiwa kwa hicho ambacho ungefanya lakini
pia umemfanya Mungu asijisikie vizuri kwa woga
wako.

Chukua hatua ya Imani leo, usiseme umechelewa


au utaanzaje, anzia hapo ulipo na ulichonacho mkononi
mwako.

Wakoma wanne.

Unakumbuka habari za wale Wakoma wanne


katika kitabu cha 2 Wafalme 7:3-5? Biblia inasema
“Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma,
penye lango la mji; wakasemezana, Mbona
tunakaa hapa hata tufe? Tukisema, Tutaingia

104
mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi
tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende
tukaliendee jeshi la Washami; wakituua,
tutakufa tu. Basi wakaondoka kabla ya
mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha
Washami; na walipofika mwanzo wa kimo cha
Washami, kumbe! Hapana mtu.” Ukiangalia
mazingira waliyokuwa nayo hawa Wakoma wanne
utaona ni halali kwao kama wasingechukua hatua.
Kwanza sheria ilikuwa haiwaruhusu kuingia mjini, pili
walikuwa ni wakoma wasingeweza kuliendea jeshi
wakabaki salama. Walipoangalia mazingira yao
wakaona wakibaki bila kuchukua hatua watakufa kwa
njaa, hata wakitoka kuingia mjini huko nako kuna njaa
watakufa vilevile kwa njaa au kwa kupigwa mawe,
sehemu pekee iliyokuwa imebaki yenye chakula ni
katika jeshi la Washami. Walishauriana wakachukua
hatua kulielekea jeshi la Washami, walipoanza tu
kuchukua hatua, ndipo Bwana akawasikizisha
Washami kishindo cha miendo ya magari na farasi,
kishindo kikubwa mno. Wale Washami wakakimbia,
wakaacha kila kitu kambini. Wakoma wakachukua
nyara za kuwatosha katika hema ya kwanza na ya pili
wakazificha kwa ajili yao kisha wakaenda kuwaambia
mabawabu wa mji na baadae nchi nzima ilipata
chakula.

Kuna wakati ukichukua hatua, Mungu


anasikizisha kishindo hatua zako, utashangaa ulikuwa

105
unajiuliza utawezaje lakini kwa sababu umechukua
hatua Mungu amekufanikisha kwa namna ambayo
haukutegemea. Kwenye kuchukua hatua kuna mwanzo
mpya, kwenye kuchukua hatua kuna mafanikio,
kwenye kuchukua hatua iko nguvu ya Mungu
inayovunja nguvu za upinzani mwanzoni mwa jambo.
Kuna watu hata ungeomba vipi hautawaona mpaka
umeanza kuchukua hatua, watajitokeza kukushika
mkono kwa namna ambayo haukuwaza. Kila kitu
ukiangalia unaona ni Mungu amekusaidia. Usiogope.
chukua hatua leo.

Fikiri kama hawa wakoma wanne wasingechukua


hatua ya kulifuata jeshi la Washami, inawezekana
mjini kungeendelea kuwa na njaa, na wao wenyewe
inawezekana wangekufa kwa njaa. Hauwezi kujua
hatua yako moja itawasaidia akina nani baadae,
hauwezi kujua utaisaidia familia yako kwa kiwango
gani. Mungu amekuamini kukupa mawazo ya biashara,
miradi, huduma au kipawa hicho, usimuangushe kwa
kubaki navyo ndani kama picha isiyoweza kutokea
katika uhalisia, CHUKUA HATUA LEO.

106
IKIWA HAUJAOKOKA NA UNATAKA KUMPA
YESU MAISHA YAKO

S
ema maneno haya kwa imani; “Asante Bwana
Yesu kwa kazi ya msalaba uliyofanya kwa ajili
yangu, ninaomba uniokoe, ninakiri dhambi
zangu na makosa yangu yote mbele zako, ninakupokea
wewe ili unisafishe kwa damu yako, ninaitambua
nguvu ya Neema, ambayo kwa hiyo ninapata wokovu
na si kwa matendo yangu. Biblia inasema “kwa moyo
mtu huamini hata kupata haki na kwa kinywa hukiri
hata kupata wokovu” (Warumi 10:10) Nami naamini
kwa moyo wangu wote kwamba wewe ni mwana wa
Mungu na ninakiri kwamba ulikufa msalabani kwa
ajili yangu ili niokolewe. Futa dhambi zangu zote na
unisafishe kwa damu yako. Ninakukaribisha ndani ya
moyo wangu uwe Bwana na Mwokozi wa Maisha
yangu, Amen”

IKIWA IMEKIRI MANENO HAYA KWA


IMANI, TAYARI UMEOKOKA, WEWE SI
MWENYE DHAMBI TENA, YESU KRISTO
AMEINGIA NDANI YAKO NA SASA
UMEFANYIKA MTOTO WA MUNGU.
KARIBU KATIKA UFALME WA MUNGU.

107
Mungu akubariki sana.

Unaweza kutushirikisha habari hii ya kumpokea Yesu


kwa sms au kutuandikia kwa barua pepe ili tuendelee
kukuombea. Tumia mawasiliano hapo chini.

Vitabu vingine alivyoandika mwandishi Elisha D.


Mwakalinga.

1. Maombi – Tambua Mambo Muhimu


yatakayokusaidia kujibiwa Maombi yako.
2. Imarisha Imani yako – Ili uweze Kushinda
katika Majaribu Mbalimbali.
3. Neema ya Mungu Ushindi Wangu.

Mawasiliano;

Simu: +255 768671298, +255 653864907

Barua pepe: elishadaudi3@gmail.com,

emwakalinga@myfaithlife.co.tz

©2022

MAREJELEO.

• Maximizing your time by Gospel Orji.


• Why God uses D. L. Mood? By R. A. Torrey
• Kuwa ni Kufanya by Emmanuel Godfrey
Makwaya

108
• Nguzo ya Siku by Apostle Shemeji Melayeki
• The world is waiting for You by Gospel Orji
• Disciplines of Godly Man by R. Kent Hudhes
• Disciplines of Godly Young Man by R. Kent
Hughes
• Finding Your Ministry – A study of the fruit and
gifts of the Spirit by Raymond W. Hurn
• God's Purpose for Your Life – Becoming one of
God's Called, Chosen and Faithful Followers by
Barbara Wentroble

109

You might also like