You are on page 1of 5

*Bidii bila akili ni mateso kwa mwili! Tafasiri 11, Kisa cha Esau na Yakobo!

*Denis Mpagaze!*

____________________________

Kwa tafasiri yangu kutoka kwenye Biblia naweza kusema duniani kuna watu wa aina mbili;
watumia nguvu bila akili na watumia akili bila nguvu. Watumia nguvu bila akili wanawakilishwa
na Esau na watumia akili bila nguvu wanawakilishwa na Yakobo. Esau na Yakobo ni watoto
pacha uzao wa Isaka na Rebeka. Esau alikuwa muwindaji na Yakobo mkulima. Siku moja Esau
alikwenda kuwinda akarudi kapa, njaa imemkwida, akakuta dogo anafinya msosi, akamwambia
hebu nipe na mie nifinye. Siunajua tena wakubwa ndo zao kuamrishana hata kwa vitu vya watu.
Yakobo akamwambia sikiliza bro hapa ni nipe nikupe, waswahili wanakwambia ukitaka kula
lazima uliwe. Achia haki yako ya uzao wa kwanza niachie msosi, vingenevyo tembea. Esau
akasema uzao wa kwanza kitu gani bana? We baki na hiyo haki nipe msosi nigonge. Esau akauza
haki yake kwa sahani ya wali wa dengu kama mabinti wajinga wanavyouza usichana wao kwa
chipsi kuku!

Siku ya baraka ilipofika, Esau aliagizwa na baba yake akawinde mnyama aliyenona aje
amtengenezee chakula kitamu ale kisha ambariki. Esau akakubali na kuingia porini huku akijua
kabisa aliishauza baraka zake! Rebeka Mama yake akampanga Yakobo wakamaliza
mchezo.Alimwambia dogo baba yako kamtuma Esau amuandalie msosi mtamu ambariki, sasa
sikiliza ingia zizini fasta, kamata wanambuzi wawili walionona tumuandalie mzee msosi fasta.
Chakula kikaadaliwa, Yakobo akampelekea Mzee, akala na kumtwanga baraka, Esau anarudi
ngoma imeisha. Achaa aangushe kilio. Baba hauna mbaraka uliobaki unibariki na mimi? Hamna
dogo, jiandae tu kuntumikia mdogo wako. Esau akaapa kumuua! Unataka kujua nini
kinaendelea? Tafuta Biblia soma kitabu cha Mwanzo ili mimi niendelee na mambo ya msingi!

*Tafasiri ya Kwanza!*

Esau ni watu wenye harakati za pimbi, muda wote wako busy for nothing, wanapiga kazi nyingi
matokeo hafifu. Joel Nanauka anawaita watu hao nzi. Huwa wanakimbizana na mambo mengi
kila siku ila siku ikiisha hakuna walilofanya. Esau anashinda porini siku nzima anakimbiza
mnyama mmoja na wakati mwingine anarudi kapa na kuombaomba! Kila siku tunakuona
unakwenda kazini lakini ubadaiwa kila wanapouza vyakula na pombe. Lakini Yakobo ni watu
wanaofanya kazi kidogo matokeo makubwa kwa sababu wanatumia akili bila nguvu. Joel
anawaita watu hawa nyuki. Hawaendeshwi na matukio. Wanaamini kuwa hawana muda wa
kufanya kila kitu,wana ujasiri wa kusema hapana kwa mambo ambayo wanaona sio ya muhimu
kwao. Pamoja na Yakobo kuwa mtu wa hemani nyumbani kwake chakula hakikatiki, akihitaji
nyama ni kuingia zizini na kukamata aliyenona bila kutoka jasho. Hawa ndo waajiri. Anapanga
akulipe kiasi gani.Anakuendesha anavyotaka na lazima utii. Esau pamoja na ukubwa wake alitii
maelekezo ya mdogo wake, akaachia haki yake ya uzao wa kwanza! Hardworking without
wisdom is a punishment to your body alisema Dr. Mensa Otabili.

*Tafasiri ya Pili!*

Esau ni wale watu wanaokula na kumaliza kila wanachokipata baada ya kuhenyeka kwa siku
nzima, wanaishi hand to mouth na Yakobo ni wale watu wanaoamini katika kuzalisha ndipo
wale.Akina Esau wakipata mshahara wanakula wote na kurudi kutafuta mwingine. Bila kwenda
porini kuua mnyama pori wanalala njaa. Kila alipoona wanyama wazuri alitamani kuwaua
badala ya kuwafuga. Yakobo alifuga wanyama, walipozaana akala kwa kujinafasi. Esau anaua na
kula anachokipata na wakati Yakobo anazalisha nachokipata na kula baadaye. Akina Jakobo
wanamultiply what they get, akina Esau wanaspend what they get! Esau ni watu wanaoua
wanyama wengi kwa nyakati tofauti, Yakobo ni watu wanaofuga wanyama wengi kwa wakati
mmoja. Esau ni watu wanaoamini katika falsafa ya give me a forest and you will find a desert na
wakati Yakobo ni watu wanaoamini katika falsafa ya give me seed and live me alone you will
find a forest.

*Tafasiri ya Tatu!*

Esau ni watu ambao wako tayari kupoteza vitu vyao vya thamani kwa hitaji la siku moja. Esau
aliuza haki yake ya uzao wa kwanza kwa sahani ya wali. Wanatema big G kwa karanga za
kuonjeshwa. Hawaamini katika mvumilivu hula mbivu. Ni sawa na binti anayepoteza usichana
wake kwa chips kuku! Anavunja ndoa yake kwa utamu wa robo saa. Yakobo ni watu
wanaoutumia ujinga wa watu kama fursa, ni watu wanaishi leo na kesho!Esau aliishi katika
maisha ya ponda mali kufa kwaja ndo maana aliuza future yake; Yakobo aliamini katika kesho
yake ndo maana alinunua future ya kaka yake mjinga ikamtoa maishani! Yakobo ni watu
wanaofikiri mbali zaidi ya mbele maana imeandikwa ukifikiri mwaka mmoja ujao panda mbegu;
ukifikiri miaka kumi ijayo panda mti; kifikiri miaka 100 ijayo elimisha watu. Maana yake ni
kwamba kwa kupanda mbegu utavuna mara moja. Kwa kupanda mti utavuna mara kumi. Kwa
kuelimisha watu utajenga kizazi kinachojitambua. Don’t wait till tomorrow which may be done
today.

*Tafari ya Nne*

Yakobo ni wale watu wanaokipa thamani walichonacho, akina Esau ni wale watu wanaokula
kuku na mayai yake bila kukipa thamani. Biblia inawaita watu wa namna hiyo wavivu. Mithali
12:24 inasema mtu mvivu hapiki mawindo yake; bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
Akiwinda anakula ili kesho arudi tena kuwinda. Muwindaji ni mtu yoyote anayepata kipato na
kula kabla ya kuzalisha; Afrika imejaa wawindaji kwa sababu tukipata madini tunayauza kama
yalivyo, hatuyaprocess! Afrika tunachimba mafuna na kuyauza kama yalivyo bila kujua
tumeuza oili, petrol, gesi, lami, plastiki na vitu kibao, hadi mafuta ya ndege. Una miliki ardhi
lakini umeshindwa kuipa thamani; unaimba vizuri lakini wanakula mapromota wako,ukigundua
unaanza kuwatukana mitandaoni. Hapo Mungu hana cha kufanya zaidi ya kukuhurumia.

*Tafasiri ya Tano*

Esau ni watu matapeli ndiyo maana pamoja na kujua kabisa aliishauza birthright lakini
alipoambiwa na baba yake akawinde alikwenda kuwinda, kwa nini asingesema ukweli tu mshua
ee, nimeuza hii kitu. Ni sawa na wewe, pesa inaingia kwenye account yako kwa bahati mbaya,
unakula zaote unaingia kwenye balaa la kulipa. Hata konda ukisahau chenji hakwambii; na wewe
akisahau kukuuliza nauli humkumbushi. Wewe ni Esau.

*Tafasiri ya Sita*

Haijalishi unampenda Mungu kiasi gani; kama unaishi kwa fikra za Esau lazima uhenyeke hapa
Duniani. Ndo maana unaweza kukuta mpendwa ameokoka vizuri, anampenda Mungu, anatoa
fungu la kumi na sadaka kwa uaminifu lakini kulala njaa kwake ni kawaida, kodi ya nyumba
inamtoa jasho, ada za watoto ameshindwa kulipa, mtoto wake wa kwanza aliacha shule kwa
kukosa ada, mwingine alizalia nyumbani na sasa ameungana na wazazi wake kumtumikia
Mungu kwa nguvu nyingi bila akili. Tatizo siyo kuongeza bidii katika kumtumikia Mungu, tatizo
ni mfumo mliouchagua! Bila kubadilisha namna ya kufikiri subiri kula mema ya nchi huko
Mbinguni.

Nchi nyingi za Afrika zinaoparate katika mfumo wa Kiesau; tuna utajiri lakini tunategemea
kusaidiwa hadi na nchi ndogo kama Singapore isiyokuwa na gold, diamond, land, sisi tuna
mafuta, gold, diamond, animals etc. Sisi tunadestroy, wale wanabuild, tunakula kwanza kabla ya
kuzalisha, wao wanawekeza kwanza kabla ya kula. Wazungu wanasema Africa develops
nothing, destroy everything.

*Tafasiri ya Saba*

Wenye fikra za Kiesau wanamuona Yakobo kama mwizi na wakati wenye akili za Kiyakobo
wanamuita Esau tahira! Ukisikiliza mahubiri yetu yote wanamshambulia sana Yakobo na mama
yake kwamba walimdanganya Mzee Isaka. Ina maana walitaka Esau adhulumu mali aliyouza
kitambo? Kwa sababu Esau hana akili hakuweza kumwambia baba nilishauza haki yangu
kitambo! Pengine baba angejua cha kufanya.

Hivi unadhani Yakobo angekuwa mwizi kama unavyofikiria Mungu angembariki namna ile?
Mungu alimbariki Yakobo kwa sababu ya matumizi mazuri ya akili. Matumizi mazuri ya akili ni
ishara ya kwamba unathamini ulivyopewa na Mungu. Hakuwa na zile tabia za kusema
namuachia Mungu kwa kila kitu; hakuwa na fikra za kwamba kwa akili yangu siwezi kama
wasemavyo wacha Mungu wengi. Yaani Mungu amekupa akili halafu unasema kwa akili zangu
siwezi. Hicho ni kiburi.

*Tafasiri ya Nane*

Afrika siyo maskini kwa bahati mbaya, ni maskini kwa mifumo tuliyoichagua wala siyo kwamba
shetani ana hatimiliki na bara letu. Imagine pamoja na kusali kwetu kote bado maisha
yanatupiga; Japan hawasali lakini wanazidi kupaa. Afrika ni raw materials. Tusipobadilisha
mindset tutaendelea kuhenyeka hapa duniani.Vitabu vitakatifu vinaposema watu wangu
wanaangamia kwa kukosa maarifa ni pamoja na kutembea na Biblia pasipokuelewa kilichomo.

Kwakuwa waafrika wengi ni watu wa imani basi tuwekezeni nguvu katika kuwahubiria maisha
yote, ya duniani na mbinguni; siyo kuwahubiria na kuwatamanisha habari za mbinguni tu!
Mungu amekupa dunia uijenge na siyo kuitelekeza na kuiita takataka, ati vyote vitapita; nani
kakwambia!

*Tafasiri ya Tisa*

Usifanye maamuzi ukiwa na njaa wala usifanye maamuzi ukiwa umechoka maana adui yako
atajua udhaifu wako akuumize utaumia; kama huamini uza simu yako kwa mtu anayejua
unashida uone atakavyokulalia.Kama unaamua kuuza, uza bila kutaja njaa inayokuuzisha!

*Tafasiri ya Kumi*

Mlango mmoja unapofungwa pita dirishani; Esau baada ya kupewa masharti magumu na kaka
yake angejaribu kuingia jikoni kwa mama yake najua angekuta msosi angekula; uchungu wa
mwana aujuaye mzazi.Sema ukiishakuwa na njaa akili haifanyi kazi. Hata sumu kwako ni tamu!

*Tafasiri ya Kumi na Moja*


Habari za don’t worry things will be okay bila kubadili namna ya kufikri utasubiri sana.
Tunaaminishana kwamba kila atoaye hupokea. Utatoa sana hadi utakufa maskini mura. Unajua
kwa nini? Kwa sababu anakubariki kupitia kazi za mikono yako! Swali ni je hiyo mikono yako
inafanya kazi ya nani? Umeajiriwa na mshahara wako ni fixed, Mungu akibariki kazi ya mikono
yako unadhani nani anayekula Baraka zako?

Hata tunapoomba lazima tuwe makini. Unaishi mtaa wa Kanyaga twende,unamuomba Mungu
akuwezeshe kujenga nyumba na wakati huna kiwanja, unajua nini kitatokea? Mungu atashusha
Baraka hizo na kuangalia ni nani katika mtaa wako ulikofanyia maombi anajenga ili ambariki.
Ndo maana unaweza kukuta mtaani kwenu tajiri anaendelea kuwa tajiri. Ni kwa sababu maskini
wote mnambariki kwa maombi yenu kwa sababu hamjui namna ya kuomba.

Hivi umeishasoma kitabu changu kipya cha Maisha ni Kutafuta si Kutafutana? Rusha 5,000 tu
nikurushie kwa Whatsapp! 0753665484! Lakini pia kuna kitabu kingine kipya kinaitwa
Ukombozi wa Fikra za Mwafrika. Bei Moja!

You might also like