You are on page 1of 155

MBINU ZA KUUZA ZAIDI

Siri Za Kuongeza Mauzo Yako Kwa Kutumia


Gharama Ndogo Ndani Ya Muda Mfupi.

Joel Arthur Nanauka


©Januari 2022 Joel Arthur Nanauka

Kitabu hiki kimeandikwa na Joel Arthur Nanauka,


kikiwa ni kitabu cha 18 katika mfululizo wa
Practical Wisdom Series.

Haki zote zimehifadhiwa. Huruhusiwi kunakili,


kudurufu, kusambaza kwa njia ya nakala laini (soft
copy) au kutumia sehemu ya kitabu hiki bila idhini
ya mwandishi. Kufanya hivyo itakuwa ni ukiukwaji
wa haki za mwandishi, na ukiukwaji wa taratibu hii
unaweza kupelekea mashitaka toka kwa waandaaji
wa kazi hii.

Joel Arthur Nanauka


Dar-Es-Salaam, Tanzania. Afrika Mashariki.
Simu: +255 756 094875 / 0745 252 670
Barua pepe: jnanauka@gmail.com
Tovuti: www.joelnanauka.com

Kimesanifiwa na INFINITE PRESS


Contacts +255 757 400 948
Email: praisearnold.pa@gmail.com

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 02


YALIYOMO
Utangulizi: 05

08
Shuhuda

Changamoto 5 Kubwa Za Biashara Nyingi. 15

Sura Ya Kwanza: Makosa 7 Yanayowakosesha 20


Wafanyabiashara Wengi Wateja Na Namna Ya
Kuyaepuka.

Sura Ya Pili: Hatua 7 Za Kufuata Ili Upate Wateja 33


Wengi (Effective Sales Process)

Sura Ya Tatu: Mbinu 5 Kuu za Kuweka Bei Sahihi 54


Itakayofanya Uuze Zaidi

Sura Ya Nne: Njia 8 Za Kumshawishi Mteja Kununua 66


Kupitia Bei Yako

Sura Ya Tano: Formula Ya Siri ya Kumshawishi 86


Mteja Anunue Bidhaa / Huduma yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 03


Sura Ya Sita: Mbinu 9 Bora Zaidi Za Kujitangaza Ili 98
Kuvuta "Attention" ya Bidhaa/Huduma yako Kirahisi.

Sura Ya Saba: Mbinu za Kutumia Mteja Anapokataa 117


Kununua Bidhaa / Huduma Yako (Overcoming Sales
Objections)

Sura Ya Nane: Mbinu 6 Za Kuhakikisha Mteja 130


Ananunua (Closing Techniques)

Hitimisho 140

Kukuhusu Mwandishi 142

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 04


UTANGULIZI

Mwaka 2018 nilitafutwa na kampuni moja kubwa


ambayo ilikuwa inatoa mitaji kwa kampuni zingine 8
zilizoko bara na visiwani kwa ajili ya kuwasaidia
kufanikiwa zaidi katika biashara zao.

Katika historia ya kampuni hizi, zilikuwapo zingine


ambazo walishawahi kuongezewa mitaji mara
kadhaa lakini hazikupata mabadiliko yoyote yale na
kuna zingine ambazo zilikuwa zinajitangaza sana ila
hawakuona mabadiliko yoyote.

Kuna baadhi ya kampuni hizi zilikuwa tayari


zimeanza kupata shida ya kulipa wafanyakazi wao
na wengine walikuwa wanakabiliwa na madeni
makubwa sana ya kibiashara ambayo ilikuwa
inaonekana wazi kabisa kuwa haitawezekana
kuyalipa.

Jukumu langu la kwanza nililopewa ni kufanya


mabadiliko yatakayochukua mwaka mmoja ili

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 05


kuwasaidia kuanza kuinuka tena kibiashara. Baada
ya kuyafanyia uchambuzi na kutengeneza mbinu za
kubadilisha namna wanavyoendesha mambo yao,
nilianza kufanya nao program mara moja.

Ilipofika miezi mitatu, kampuni zote zilizokuwa


kwenye program zilianza kuongeza mauzo yao na
aliyepata chini kabisa ilikuwa ni wale ambao
walipata ongezeko la mauzo kwa 35%.

Ingawa ilikuwa inaonekana kuwa kampuni hizi


zilikuwa zinaelekea kufa, hakuna hata moja ambayo
ilikufa na yote yanaendelea vizuri kwa sasa na
yameendelea kufanikiwa kimauzo na kuongeza
thamani ya mitaji yao.

Siri hizi walizozitumia kuleta mabadiliko katika


biashara zao, unaweza kuzitumia pia kuleta
mabadiliko katika baishara yako pia.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 06


Bila kujali hali ya biashara yako ya sasa, mbinu hizi
ambazo niliendelea kuzifundisha kwa
wafanyabiashara mbalimbali kuanzia wa chini, wa
kati na wa juu, zimewaletea matokeo makubwa
sana.

See You At The Top

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 07


SHUHUDA

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 08


Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 09
Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 10
Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 11
Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 12
Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 13
Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 14
BIASHARA YAKO INAKABILIWA NA
CHANGAMOTO IPI KATI YA HIZI 5?

Kama kuna changamoto yoyote kati ya hizi ambazo


unazipitia kwa sasa, basi unaweza kupata majibu ya
kukusaidia katika kitabu hiki na ukazitatua kwa
haraka.

Changamoto Ya Kwanza: Mauzo yako yameshuka


sana hadi umeanza kushindwa kuendesha biashara
yako.

Kama unafanya biashara na kwa sasa haupati


mauzo ya kutosha kukufanya uweze kugharamia
gharama za msingi za uendeshaji wa biashara yako.

Kama mapato unayopata kwenye biashara


hayakuwezeshi kabisa kulipa gharama za kulipa
pango ya eneo la biashara, hayakuwezeshi tena
kuwa na uwezo wa kuwalipa wafanyakazi wako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 15


Au imekuwa changamoto kwako kulipa watu ambao
unanunua bidhaa kutoka kwao (suppliers), basi
kitabu hiki kitakusaidia kutoka kwenye hizo
changamoto.

Changamoto Ya Pili: Wateja wanasifia bidhaa


zako/huduma Yako ila wanaishia kutoa visingizio na
hawanunui.

Ukweli ni kuwa, inapofika kwenye suala la


ubora/uzuri wa bidhaa au huduma unayoiuza
hakuna ubishi kuwa kila mteja huwa anasifia sana.

Yaani, kila mtu ambaye unamueleza kuhusu bidhaa


au huduma yako huwa haachi kuisifia, ila mwisho
wa siku hanunui.

Yaani anaishia kutoa visingizio mbalimbali vya


kutokununua hadi unashangaa.

Kila siku unajiuliza: Mbona wateja wanasifia sana


bidhaa/huduma yangu ila hawanunui kabisa?.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 16


Kitabu hiki kitakupa mbinu za kuwageuza wateja
wanaosifia, kuanza kuwa wanunuzi wa bidhaa zako.

Changamoto Ya Tatu: Unatumia gharama kubwa


ya matangazo na hauoni ongezeko la mauzo.
Uliamini kuwa ukianza kufanya matangazo kwa
nguvu, basi utaweza kuongeza mauzo yako.

Hata hivyo, pamoja na kuweka bidii na juhudi katika


kutangaza, bado haujaweza kufanikiwa kabisa
kuongeza mauzo.

Yaani uwekezaji wako wa kifedha na muda kwenye


kujitangaza, haujakupa matokeo mazuri.

Ndani ya kitabu hiki, utagundua kosa ambalo


umekuwa unalifanya na itakusaidia kujua mahali pa
kujirekebisha ili matangazo unayoyafanya kwa ajili
ya kujitangaza, yaweze kukuletea matokeo.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 17


Changamoto Ya Nne: Ushindani wa kibiashara
umekuwa mkubwa sana na umeathiri mauzo yako.

Pengine wakati unaanza, ushindani haukuwa


mkubwa kama ulivyo sasa.

Inawezekana watu waliokuwa wanafanya biashara


kama wewe walikuwa wachache au hawakuwepo
kabisa kwenye eneo ulilopo.

Ila kwa sasa kumekuwa na watu wengi wanaofanya


biashara kama ya kwako na imesababisha muanze
kugombania wateja wachache ambao zamani
walikuwa ni wateja wako peke yako.

Kitabu hiki kitakusaidia kujua mbinu za kutumia ili


uweze kuuza zaidi ya washindani wako.

Changamoto Ya Tano: Wateja wanasema wana


watu wengine ambao wanawapatia huduma/bidhaa
nzuri zaidi.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 18


Kila unapojaribu kutafuta wateja ili wanunue
bidhaa/huduma zako, huwa wanakubali kuwa
unachouza ni kizuri na wanakihitaji, ila kisingizio
kikubwa huwa ni kuwa, kuna mtu tayari anawapatia
huduma/bidhaa kama zile ambazo wewe huwa
unauza pia.

Kama kila wakati unapoongea na wateja kuna


ambao mara nyingi wanakuambia, “Ningeweza
kununua, ila tayari kuna mtu ambaye ananipatia
huduma/bidhaa kama hii tayari”

Kwenye kitabu hiki, utajifunza mbinu rahisi ya


kukusaidia kumpata mteja wa namna hii.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 19


SURA YA KWANZA

Makosa 7 Yanayowakosesha
Wafanyabiashara Wengi Wateja Na
Namna Ya Kuyaepuka.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 20


Kwa kila ambaye anasumbuka sana na kuongeza
mauzo yake, huwa kuna makosa ambayo
anayafanya.

Katika tafiti mbalimbali, kumeonekana kuwa kuna


makosa 7 ambayo watu wengi huwa wanayafanya
na yanakwamisha juhudi zao za kutaka kuuza zaidi.
Ukiweza kuyashinda makosa haya, basi
unajiongezea uwezo wako wa kuuza zaidi.

Kosa la Kwanza: “Weak MINDGAME”

Mwandishi nguli wa masuala ya akili na ufahamu ili


kupata mafanikio ya kifedha, T.Harver Eker aliandika
kitabu cha “The Secrets of Millionaires Mind” (Siri
zilizo kwenye akili za mamilionea), anasema kuwa
kwenye maisha hauwezi kuwa zaidi ya vile ambavyo
umejiona.

Kwa maneno mengine ni kuwa uwezo wako wa


kuuza unatokana na vile unavyojiona kwa ndani
kuwa wewe ni mtu unayeweza kuuza sana.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 21


Hii huitwa, “The Law Of Correspondence” ambayo
inaeleza kuwa, unachokipata kwa nje kinaakisi kile
ambacho umekiona kwa ndani yako.

Kama haujawahi kujiona ukiwa unauza sana,


itakuwa ngumu sana kuuza hata kama una bidhaa
au huduma nzuri sana.

Kuna watu wameshaamini kuwa, watu ambao


wanauza zaidi ni wale ambao wamesomea mambo
ya mauzo na masoko, na kwa sababu wao
hawajasomea masomo rasmi kwenye eneo hilo basi
hawawezi kufanikiwa, ukiamini namna hiyo basi
hautaweza kuuza zaidi.

Mipaka unayojiwekea ya kufanya kitu kwenye


Maisha yako, huwa inaitwa “Limiting Belief”. Mfano,
nikikuuliza leo, “Hivi unafikiri uwezo wako mkubwa
kabisa kwa sasa wa kufanya mauzo ni shilingi
ngapi?” - Hebu fikiria na upate jibu lako kabla
haujaendelea.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 22


Umepata shilingi ngapi?

Kwa kiwango chochote kile ambacho umepata, basi


ujue hapo utakuwa umetumia 40% tu ya uwezo
wako wote, yaani kuna 60% haujatumia ambazo
zingeongeza sana mauzo yako.

Hii ni kwa mujibu wa mwandishi wa kitabu cha


“Living With The Seal”, ndugu Jesse Itzler.

Yaani kama wewe umesema mauzo makubwa


kabisa unayoweza kufanya ni 400,000/- kwa mwezi
basi uwezo wako halisi ni kuuza 1,000,000/- kwa
mwezi. Ni mipaka uliyojiwekea ndio inakufanya
ushindwe kufanikiwa zaidi.

Jiambie: “Mimi naweza kuuza zaidi ya vile ambavyo


niliwahi kuuza kabla” .

Kumbuka ujuzi peke yake bila kujiona ukiwa muuzaji


mzuri wa bidhaa/huduma hautakupa matokeo
unayoyataka.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 23


Kosa la Pili: Kushindwa Kujua Wateja
Wako ni Akina Nani Hasa.

Katika watu walioko duniani takribani billioni 7,


unahitaji asilimia ndogo sana ya watu katika hao
kuweza kufanikiwa katika biashara yako.

Hauhitaji kila mtu awe mteja wako, unahitaji watu


wachache katika wengi waliopo wanunue bidhaa
yako. Ukijaribu kumuuzia kila mtu bidhaa yako,
utajikuta haupati mauzo kama ambavyo unatamani.

Watu wengi sana wameshindwa kuuza zaidi kwa


sababu wamekuwa wakitapanya nguvu, muda na
pesa zao kujaribu kumfanya kila mtu awe mteja
wao.

Hapo baadaye tutajifunza namna ya kuchagua


wateja kimkakati, ambao ukiwalenga lazima
watanunua bidhaa yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 24


Kwa watu wengi kutojua aina ya wateja ambao
wanawalenga, wamejikuta wanatumia “platform”
ambazo sio sahihi kwa biashara zao ambazo
wateja wao hawapo kabisa.

Kosa la Tatu: Kuuza Bidhaa/Huduma


Badala Ya Kuuza Faida.

Hivi unajua kuwa watu hawanunui bidhaa yako


unayoiuza? Watu wananunua faida inayotokana na
bidhaa unayoiuza (Rudia tena kusoma na uelewe).

Kwenye kitabu changu cha SAIKOLOJIA YA


MTEJA, nimeeleza kwa undani kuhusiana na vitu 9
ambavyo mteja huwa anavitafuta anapotaka
kununua bidhaa yako.

Watu wengi sana kwa kutokujua hili, wameweka


nguvu kwenye kutangaza vitu ambavyo
haviwasaidii kuuza zaidi.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 25


Usisahau siku zote kuwa "Features Tell, Benefits
Sell", yaani unapoielezea bidhaa yako kwa kutaja
ujazo, mwonekano wake, imezalishwa wapi, rangi
yake n.k hivyo vyote vinasaidia kuitaja bidhaa na
huitwa “features”.

Lakini kama unataka kuuza bidhaa yako, unatakiwa


uwasilishe kuhusu faida (benefits) ambazo bidhaa
yako inatoa, yaani suluhisho ambalo mteja atalipata
kwa kutumia bidhaa yako.

Hii ndio maana kabla haujauza lazima ujiulize, hivi


huduma/bidhaa yangu inatoa suluhisho gani la
kipekee ukilinganisha na wengine? (Unique Value
Proposition).

Usisahau kuwa, hakuna mtu anayependa kuuziwa,


mtu yeyote anayenunua sio kwa sababu anapenda
kununua bali kwa sababu anavutiwa na faida
ambazo atazipata kutokana na kutumia
bidhaa/huduma yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 26


Kumbuka: Watu hawanunui unachouza, wananunua
kile bidhaa yako itakachowafanyia.

Kosa la Nne: Umeshindwa Kujenga


Kuaminika.

Watu wananunua kwako kwa sababu wanakuamini,


hii ndio maana mara nyingi kwenye uuzaji wa
bidhaa huwa wanatafuta watu maarufu wa
kutangaza bidhaa husika, ili kuwaaminisha watu kwa
haraka.

Swali la msingi la kujiuliza ni kuwa, "kwa nini watu


wakuamini wewe kwamba unachosema kuhusu
bidhaa au huduma yako ni kitu cha ukweli? "

Kadiri ambavyo unashindwa kujenga hali ya


kuaminiwa na watu ambao unataka wawe wateja
wako, ndivyo ambavyo itakuwa ngumu kwako
kuuza.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 27


Hata hivyo, watu hawakuamini tu bila kuwa na kitu
au namna ya kujenga kuaminiwa.

Hapo baadaye tutajifunza namna bora ya kujenga


kuaminiwa na wateja wako, kwa namna ambayo
chochote utakachowaambia watakisikiliza na
watafuata ushauri wako.

Kosa la Tano: Kuweka Bei Isiyo Sahihi.

Bei ya bidhaa yako unayouza huwa inajulisha sana


kama utauza sana ama la. Kuna wateja wengi sana
ambao unawapoteza kwa kushindwa kuweka bei
ambayo siyo sahihi.

Kuna wale ambao wanaweka bei ya juu sana kuliko


wateja wako wanavyoweza kumudu, na matokeo
yake wamewakimbiza wateja wao bila wao wenyewe
kujua.

Kuna baadhi ambao wameweka bei ya chini sana


kwenye bidhaa zao inayofanya watu watilie shaka
ubora wa bidhaa ambayo wanaiuza.
Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 28
Kwa namna yoyote ile kati ya hizi mbili, ukikosea
kuweka bei iliyo sahihi basi unakuwa umepoteza
wateja wako bila wewe mwenyewe kujua.

Hapo baadaye tutajifunza mbinu 7 za kuweka bei


sahihi ili kuvutia wateja wako wanunue bidhaa zako.

Kosa la Sita: Unakata Tamaa Mapema.


Kuna wauzaji ambao wamekata tamaa, baada ya


kujaribu kuuza na kushindwa kupata matokeo
ambayo waliyatarajia.

Unachotakiwa kujua ni kuwa kila unapofeli, basi


unakuwa unatengeneza uwezo wa kufanikiwa zaidi
katika kile ambacho unakikusudia.

Mtandao mkubwa wa masuala ya masoko duniani,


Marketing Donuts katika utafiti wake, imeonyesha
kuwa ni 2% tu ya mauzo hufanyika baada ya
kukutana na mtu kwa mara ya kwanza.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 29


Hii inamaana 98% ya mauzo hufanyika baada ya
kujaribu kuuza kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo, cha kushangaza ni kuwa 44% wauzaji


huwa wanakata tamaa baada ya kuambiwa HAPANA
mara ya kwanza.

Yaani walio wengi huwa hawawezi kabisa kuendelea


mbele mara baada ya kukataliwa na mteja kwa
mara ya kwanza.

Wauzaji 22% huwa wanakata tamaa baada ya


kukataliwa mara ya Pili, na wengine 14% Wanakata
tamaa baada ya kukataliwa mara ya tatu.

Wauzaji 12% wanakata tamaa baada ya hapana ya


nne na waliobakia 8% tu ndio huendelea kwenda
hatua ya Tano.

Hata hivyo kuna kundi kubwa sana la wateja huwa


wanafanya maamuzi baada ya kukataa bidhaa mara
ya tano, hivyo kuna kundi dogo la wauzaji ndio

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 30


hufaidika kuwapata kwani wengine wanakuwa
wameshakata tamaa. Inawezekana wewe
umeshafanya kila kitu na ni kama vimekukatisha
tamaa kabisa na hautaki tena kuendelea mbele.

Kumbuka: Mauzo mengi hufanyika baada ya


kukataliwa mara ya kwanza. Hapo baadaye
utajifunza mbinu za kumfanya mteja wako afanye
maamuzi kwa haraka zaidi ili utumie muda mfupi
kumuuzia.

Kosa la Saba: Hauwaoneshi


Watakachokosa Wasiponunua Kwako.

Ni hasara au maumivu gani mteja atayapata kama


atachelewa au hatanunua kutoka kwako?

Usipofanikiwa kumuonyesha mteja kitu ambacho


atakikosa kama asiponunua kwako kwa wakati huo,
basi unakuwa umejitengenezea mazingira ya
kumkosa mteja huyo.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 31


Moja ya jukumu la muuzaji ni “putting your
customer on the fence", yaani unamuweka katika
hali ambayo inamlazimisha kufanya maamuzi ya
haraka kwani asipofanya hivyo kuna kitu atakikosa
kwenye maisha yake.

Kwa mfano: Kuna deadline bei itapanda.

Kumbuka: Hakuna anayetaka kutumia pesa, hivyo


lazima umtengenezee mazingira ya haraka na
ulazima wa kutumia pesa.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 32


SURA YA PILI

Hatua 7 Za Kufuata Ili Upate


Wateja Wengi
(Effective Sales Process).

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 33


Kwa mujibu wa taasisi ya Sales Management
Association, 90% ya makampuni ambayo
yanayofanikiwa katika mauzo huwa wanatumia
mfumo maalumu wa mauzo.

Makampuni haya huwa yanauza 28% zaidi


kulinganisha na mengine ambayo hayatumii mfumo
maalumu.

Yaani kama makampuni yasiyo na mfumo maalumu


yanauza shilingi 1,000,000/- yale yanayofuata
mfumo maalumu wa uuzaji, yanauza 1,280,000/-.

Cha kushangaza ni kuwa ,kwa mujibu wa taasisi ya


Objective Management Group, 68% ya watu
wanaouza duniani huwa hawatumii mfumo
maalumu wa mauzo (Formal Sales Process) na
matokeo yake huwa wanafeli sana.

Je, wewe huwa unatumia mfumo


maalumu wa kuuza?

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 34


Kuuza sio suala la kubahatisha, bali kuna mchakato
ambao ukiufuata utakusaidia kupata mteja yeyote
yule unayemuhitaji kwenye bishara yako.

Mauzo yanaongozwa na kanuni ya kichocheo na


matokeo, yaani kuna vitu ukivifanya basi vitakupa
aina fulani ya matokeo.

Kuna watu wengi kwa kutokujua hili, wamekuwa


wanatumia rasilimali zao za fedha, nguvu na muda
kufanya vitu ambavyo haviwapi wateja na matokeo
yake wanakata tamaa kwa sababu matokeo
hayaendani na nguvu wanayotumia.

Watu wanaouza kwa kutumia mbinu hii


wamefanikiwa sana kuweza kuongeza mauzo yao
kwa muda mfupi. Nawe itakusaidia sana.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 35


Hatua Ya Kwanza: PROSPECTING
(Formula Ya Siri Ya Kuchagua Wateja Sahihi)

Kwenye hatua hii unatakiwa kuchagua aina ya mteja


unayemtaka ambaye tunamuita “Dream Client”,
yaani nikikuuliza ni mtu wa namna gani unamlenga
kama mteja wako, unatakiwa kuwa na vigezo
ambavyo unavitumia kumpata huyo mteja.

Ili kufanikisha hili itabidi utengeneze sifa za mteja


ambaye hasa ndiye unamlenga (Clients Profile).

Hapa lengo kubwa ni kuhakikisha kuwa unamjua


mteja wako vizuri ili usitumie nguvu zako
kuzielekeza kwa watu ambao sio wateja.

Katika hatua hii unapaswa kutengeneza Ideal Client


Profile (ICP) ya wateja wako, ambayo unakuwa
unaeleza vigezo vya wateja unaowalenga.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 36


Mfano: Umri wao, eneo wanalotokea, kipato cha
chini, cha kati au cha juu, unalenga jinsia gani,
bidhaa/huduma yako inalenga watu wanaofanya
kazi za aina gani, kiwango cha elimu yao, maeneo
wanayokaa n.k.

Hii inamaana mtu yeyote ambaye haendani na


vigezo vya ICP yako, hautakiwi kutumia muda wako
mwingi kumuuzia.

Zoezi:
Andika ICP ya wateja ambao unawalenga kuwauzia
bidhaa/huduma yako.

1. .....................................................................................
2. .....................................................................................
3. .....................................................................................
4. .....................................................................................
5. .....................................................................................
6. .....................................................................................
7. ....................................................................................

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 37


VITU 4 VYA KUTUMIA KUMJUA MTEJA ALIYE
TAYARI KUNUNUA.

Sio kila mteja ambaye ana sifa zote ulizoziainisha


kwenye ICP atanunua kwako kwa wakati huo.

Ili kujua yupi ndiye ambaye atanunua kwa haraka na


yupi hatanunua, unatakiwa kutumie vigezo vinne
vifuatavyo:

i. Uhitaji wao: Inawezekana kabisa mteja wako


akawa ana sifa zote sa ICP ambazo umezibainisha.
Ila swali la muhimu ni kuwa, je, ana uhitaji wa hicho
kitu? Ukiona hana uhitaji ina maana endelea
kutafuta mteja mwingine.

ii. Bajeti Yao: Ana uwezo wa kumudu gharama ya


huduma/bidhaa yako? Inawezekana ana sifa zote za
kuwa kwenye ICP yako ila hana bajeti ya kumruhusu
kununua bidhaa / huduma yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 38


iii. Mamlaka ya kufanya maamuzi: Je, mteja
unayetaka kumuuzia ndiye mwenye maamuzi ya
kununua.

Kwa mfano: Unapouza bidhaa za Watoto, mwenye


maamuzi ni mzazi, hivyo unatakiwa kumlenga mzazi
zaidi.

iv. Muda wa Uhitaji (Timing of Need):


Inawezekana ni kweli ana uhitaji, lakini Je uhitaji
wake ni wa wakati huo?

Kwa mfano: Uhitaji wa bidhaa za stationaries kwa


ajili ya shule upo kila wakati, ila mwanzo wa mwaka
shule zinapofunguliwa uhitaji huu huwa ni mkubwa
zaidi.

Mambo haya manne yatakusaidia kuchuja wateja


ambao tayari umewaweka kwenye orodha ya ICP
yako na utaweza kujua yupi na yupi ambaye ndio
wako tayari kununua kwa haraka kuliko wengine, ili
uweke nguvu zako huko.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 39


Hatua ya Pili: ANZA KUWASILIANA NA
WATEJA WAKO.

Baada ya kutumia vigezo ambavyo tumejifunza


hapo juu na kujua mteja ambaye ana uwezekano
mkubwa wa kuja kununua kwako, hatua inayofuata
ni anza kutengeneza mahusiano na wateja wako
watarajiwa.

Mambo mawili muhimu ya kuzingatia unapoanza


kuwasiliana na wateja wako ni:

Anza kujenga mahusiano nao kwanza: Usisahau


kuwa watu wengi hawapendi kuuziwa na mtu
ambaye hawamfahamu kabisa.

Tafuta mbinu ambazo zitakusaidia kuaminika kwa


haraka. Inawezekana kupitia kuonyesha uwezo
wako, uzoefu wako au kutumia watu ambao
ulishawahudumia na wakafurahia huduma yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 40


Hapo baadaye tutajifunza njia rahisi ya kujenga
kuaminika mbele ya mteja wako.

Jambo la pili ni kujiuliza Njia nzuri ya kuwapata


ni Ipi?: Kila mteja ana njia yake nzuri ambayo
unaweza kumpata kwa urahisi.

Wengine ni kwa njia ya simu, wengine ni


kuwatembelea ofisini/nyumbani kwao, wengine ni
kwa matangazo ya redio, vipeperushi, Kupitia
mitandao ya kijamii, Kwa njia ya e-mail.

(Kama utatumia njia hii zingatia kuwa imegundulika


kuwa muda mzuri wa kuwatumia watu email ni saa
2 hadi 4 asubuhi au saa 9 hadi 10 jioni).

Kutegemea na sifa za wateja wako unaweza kutumia


njia tofauti kwa kila mteja, au kutumia njia zaidi ya
moja kwa mteja mmoja.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 41


Hatua ya Tatu: AMUA NANI AWE
MTEJA WAKO.

Sio kila unayewasiliana naye au anayeulizia bidhaa


yako ataweza kuwa mteja wako, wewe ndio
unatakiwa kuamua nani awe mteja wako.

Kumbuka kutumia vile vigezo vinne vya hatua ya


kwanza kupima nani anakufaa na nani ambaye
hatakufaa kabisa kwa wakati huo.

Uzoefu unaonyesha kuwa takribani 50% ya wale


uliowadhania watakuwa wateja wako huwa
hawanunui.

Yaani katika watu 10 ambao mwanzoni walionyesha


kama wanataka kununua kwako, ni wateja 5 tu ndio
ambao wana uhakika wa kuwa wateja kamili.

Jiepushe kutumia muda na rasilimali zako kwa watu


ambao unaona hawafit kwenye profile ya wateja
wako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 42


Hii ndio maana, ni muhimu kutumia muda mwingi
kuzungumza na kumuuliza maswali mengi mteja
wako ili ujue kama anakidhi vigezo vya ICP yako.

Yule ambaye anakidhi vigezo vingi zaidi, ndiye


ambaye anastahili kupata muda wako mwingi na
yule ambaye hakidhi vigezo vingi inamaanisha sio
mteja wako wa haraka na itatakiwa utumie muda
naye kidogo sana.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 43


Hatua ya Nne: JIWEKE KWENYE NAFASI
YA KUAMINIKA.

Usisahau kuwa, watu wako tayari kununua kwa mtu


wanayemwamini zaidi hata kama bidhaa zake ni za
gharama zaidi au hata wakati mwingine zinapokuwa
na ubora mdogo kuliko bidhaa za watu wengine.

Kuna njia nne (04) ambazo unaweza kuzitumia


kujenga hali ya kuaminika zaidi kwa wateja wako:

Onyesha suluhisho ulizonazo kwa ajili ya


wateja wako (Common Problems): Onyesha
kwa waziwazi bidhaa/huduma yako inatatua
changamoto gani. Usielezee tu ubora wa bidhaa
au bei rahisi ya bidhaa yako, elezea changamoto
gani hasa ndio unaitatua. Usisahau kuwa watu
wananunua bidhaa kwa sababu kuna suluhisho
wanalitafuta. Onyesha bila shaka kuwa
bidhaa/huduma yako inaweza kutatua
changamoto hiyo na mifano ya kuwa imewahi
kutatua changamoto hiyo kwa watu wengine
ambao uliwahudumia.
Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 44
Wapatie thamani endelevu (Consitency
Value): Kutegemea na aina ya huduma au
bidhaa unayouza, unaweza kuamua kutoa
thamani endelevu. Kwa mfano, mimi kabla
sijaanza kuandika na kuuza vitabu, nilianza kwa
kuandika kwa uendelevu kwa muda mrefu
kwenye mitandao ya kijamii. Kumbuka kuwa,
wakati mwingine utahitaji kutoa thamani hii
bure kwa watu ili waendelee kukuamini.

Toa Elimu ya jumla kuhusu eneo lako la


huduma: Kama wewe ni muuza vifaa vya
magari, badala ya kila siku kutangaza bei za vifaa
vyako, unaweza kutoa elimu ya vitu vya
kuzingatia ili engine ya gari yako idumu kwa
muda mrefu, kama unauza vyakula vya lishe
unaweza kutoa elimu juu ya aina ya vyakula
vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili, vyakula
vya kuepuka kama unataka kupunguza uzito n.k.
Utakapokuwa ukitoa elimu watu wanaanza
kukuona kama mtaalamu na wataanza kuamini
aina yoyote ya bidhaa/huduma unayouza.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 45


Pia wanapata uhakika kuwa hauuzi kwa sababu
unatafuta pesa bali kwa sababu unajua suluhisho
ambalo watu wanalipata kupitia bidhaa/huduma
yako.

Pata namna ya kuwasiliana na kila mtu


binafsi (Personalized Communication): Tafuta
namna ya kuwasiliana nao kwa majina yao. Kila
mtu huwa anapenda kuona kuwa anatambulika
kibinafsi na huwa anajisikia kuheshimiwa.
Unaweza kufanya kupitia program ya meseji,
unaweza kufanya kupitia emails etc. Ukiweza
kufanya hivi, utasababisha “The Law of
Reciprocity” ifanye kazi, ambayo inasema kuwa
ukimfanyia mtu kitu kizuri naye atalazimika
kutafuta fursa ya kukufanyia kitu kizuri pia. Hapa
inamaanisha, utakapowasiliana naye kibinafsi
naye pia atatafuta namna ya kukufurahisha kwa
kuamua kuwa mteja wako.

Wale ambao hawako tayari kununua, endelea


kuwapatia THAMANI.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 46


Siku wakitaka kununua, jina lako litakuwa la kwanza
kwenye akili yao. Kwa wale utakaoona wanahitaji
bidhaa yako wakati huo, basi endelea na hatua ya
tano.

Hatua ya Tano: WAUZIE WALIO


TAYARI.

Katika hatua nne za kwanza, utakuwa tayari


umeshawajua wateja wako, umeshajua wako wapi
na pia umeshajua mahitaji yao n.k.

Katika hatua hii ndio hasa utakuwa uko tayari


kufanya mauzo kwa wateja wako. Kwa sasa tayari
umeshakuwa mtu wanayekuamini kuwa unaweza
kutatua matatizo yao.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 47


MAMBO 5 YAKUZINGATIA UNAPOWAPA WATEJA
WAKO OFA ILI WAWEZE KUNUNUA
KUTOKA KWAKO.

i. Iendane na uhitaji wao wa wakati huo: Usitoe


ofa ambayo haiko kwenye mahitaji ya wakati huo,
ujumbe wako uwe unajibu mahitaji ya wakati huo.

ii. Ilenge wahusika kabisa: Usiweke ofa ya jumla


jumla kwa tamaa ya kutaka kila mtu. Kujaribu kutoa
ofa ambayo ni ya jumla itakufanya ukose kuvutia
watu ambao ni sahihi kwa haraka.

iii. Ielezee namna inavyojibu maswali/matatizo


yao yanayowasumbua: Ujumbe wako, ulenge
kujibu maswali na kutoa suluhisho la matatizo
ambayo wanakabiliana nayo.

iv. Iweke iendane na bajeti yao: Kupitia ICP yako


utakuwa umeshajua uwezo wa wateja wako, hivyo
inabidi uweke bei inayoendana nao.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 48


Baadaye tutajifunza namna ya kuweka bei sahihi
kwa wateja uliowalenga.

v. Iwekee ubunifu wa package/vifurushi: Hii


inamanisha namna unavyoweza kuweka vifurushi
vya watu kununua haraka, tutajifunza baadaye
namna bora ya kufanya hivyo.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 49


Hatua ya Sita : KABILIANA NA
VIPINGAMIZI VYA KUUZA.
(Deal With Sales Objections)

Kwa kawaida lazima kuna vipingamizi utakutana


navyo mfano: bei kubwa, mimi sio mwenye
maamuzi, ngoja nikafikirie kwanza, niliwahi
kununua kama hii nikapata shida, kuna mwingine
anauza bora kama wewe, sijawahi kukusikia, kwa
sasa sihitaji n.k.

Je, unajibu vipi maswali kama haya?

Katika sura zinazofuata tutajifunza namna ya kujibu


maswali yote haya. Hakikisha unasoma kitabu hiki
hadi mwisho.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 50


Hatua ya Saba : KUENDELEA KUUZA.

Hakikisha umewafikisha wateja wako kwenye


kiwango cha wao kufanya maamuzi wenyewe. Kuna
hatua mbili ambazo unaweza kuzitumia:

Hatua Ya Kwanza: Uza Bidhaa Kwa Walio Tayari


Sasa Hivi: Unaweza kufanya DIRECT SELLING- mfano:
Unamuuliza mteja wako baada ya kumaliza kuongea
naye “ungependa nikupatie ngapi? au “ungependa
nikuletee lini”.

Kwenye hii unauza kwa namna ya fikra kuwa mteja


ameshakubaliana na wewe na anachopaswa
kufanya ni kuchagua tu baadhi ya vipengele vya
utekelezaji, haumpi nafasi mteja wa kusema aidha
anataka au hataki.

Aina nyingine ni INDIRECT SELLING: Hii unampa


nafasi mteja kutafakari na kufanya maamuzi yeye
mwenyewe kwa kumpa fursa ya kuamua.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 51


Kwenye uuzaji wa namna hii unamuuliza maswali
kama “je, umependa bidhaa yangu na inajibu maswali
yako yote?”

Kumbuka unapouza unaweza unaweza kutumia


vigezo kama: Uharaka (Urgency) kwa kumuonyesha
kuwa akishindwa kufanya maamuzi bei itapanda
baada ya muda fulani au kuna ofa fulani kubwa
ataikosa.

Hatua Ya Pili: Tengeneza Plan Ya Kufuatilia


Wasio Tayari Sasa Hivi.

Kuna wale ambao kwa sasa wameshindwa kuwa


wateja wako, usiwapoteze kabisa, jaribu kuangalia ni
namna gani unaweza kuwaweka karibu zaidi.

Unaweza kutumia "Free Trial": Unamwambia mteja


jaribu kwa muda bila kulipia ili ujiridhishe.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 52


Nia kubwa ya hatua hii ya pili ni kuendelea kubakia
katika akili zao siku zote ili wakati wowote wateja
hawa watakapohitaji huduma, uwe katika akili zao
siku zote.

Tafakari
Katika hatua hizi, ni ipi ambayo ulikuwa hauifanyii
kazi vizuri na ungependa kuifanyia kazi kwa haraka?

...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 53


SURA YA TATU

Mbinu 5 Kuu za Kuweka Bei Sahihi


Itakayofanya Uuze Zaidi

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 54


Namna unavyoweka bei kwenye bidhaa/Huduma
yako inaweza ikaamua kama utauza kidogo ama
utauza sana.

Ukikosea kidogo aidha kwa kuweka ya juu sana au


ya chini sana unaweza kukosa kabisa wateja.
Kumbuka kupanga bei ni suala la kisayansi na pia la
kisaikolojia.

Unapofanya biashara usiweke bei yako bila kujua ni


kigezo gani umekitumia kuweka bei.

Kuna mbinu TANO ambazo unaweza kuzitumia ili


kupanga bei ya bidhaa/huduma yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 55


Mbinu ya Kwanza:
PENETRATION PRICING
(Bei ya Kupenyea Kwenye Soko)

Bei hii hutumika kama unataka kuingiza bidhaa


mpya sokoni au kuingia kwenye soko ambalo
haujawahi kuwepo kabisa. Unaweza kuweka bei hii
kwa njia zifuatazo:

Kutumia Break even/production Cost: Hapa


unauza bila faida na bila hasara. Unaweka bei
sawasawa na ile ya gharama za kuzalishia
bidhaa husika. Hapa nia kubwa ni kufanya
bidhaa yako ijulikane kwa haraka kwa kuwa
rahisi kununuliwa sokoni.

Unaweka faida kidogo sana: Hapa unaweka


bei zaidi ya gharama za uzalishaji, ila bei yako
inakuwa ndogo sana ukilinganisha na watu
wengine wanaouza bidhaa kama za kwako
sokoni.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 56


Mara nyingi bei hii sio ya kudumu, unaanza nayo na
kisha baada ya muda baada ya watu kutumia kwa
muda fulani, unaanza kuiongeza bei ya
bidhaa/huduma taratibu taratibu hadi utafika bei ya
kupata faida unayoitaka.

Faida ya kutumia mbinu hii ni kuwa utavutia watu


wengi haraka sana pale ambapo unaanza kuitumia.
Hasara yake ni kuwa utakapoanza kuongeza bei,
kama utaongeza kwa haraka watu watakukimbia
baadaye.

Falsafa ya kutumia bei hii ni kuwa badala ya kuweka


gharama kubwa kwenye matangazo, unaamua ile
faida ndogo unayopata/uliyoipoteza ndio inakuwa
gharama yako ya matangazo kwa kuvutia wateja.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 57


Mbinu Ya Pili: COMPETITIVE PRICING
(Bei ya Ushindani)

Katika mbinu hii ni kuwa, unaweka bei sawasawa na


ile ambayo inatumika na washindani kwenye soko
unaloingia.

Kwenye mbinu hii, itakulazimu kufanya utafiti kwa


wengine wanaouza na kutoa huduma/bidhaa kama
zako na kisha unatumia bei ileile.

Hapa swali kubwa ni sababu gani ambayo itafanya


watu wengine waje kwako na sio kwa wale wengine
ambao bei zenu zinafanana. Hii ina maana lazima
utafute kitu cha kuvutia zaidi ya bei.

Faida kubwa ya kutumia hii ni kuwa unakuwa


umeondoa ushindani wa bei kwenye biashara yako.

Changamoto yake ni kuwa inakubidi kuwa “reactive”,


yaani unakuwa kazi yako ni kuwaiga watu wengine. .

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 58


Na pia unaweza kujikuta unapata hasara kwa kuiga
bei za watu wengine kwa sababu kuna washindani
wako wengine watakuwa wananunua
malighafi/bidhaa kwa bei rahisi hivyo hata wakiuza
bei ndogo bado watapata faida, au wengine
wanazalisha wenyewe au wanatumia malighafi zao
wenyewe n.k.

Ukikutana na washindani wakubwa, wanaweza


wakaendelea kupunguza bei na isiwaathiri na wewe
ukipunguza inakuathiri na mwisho ukashindwa
kufanya biashara kabisa.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 59


Mbinu ya Tatu: VALUE-BASED PRICING
(Inaegemea katika thamani)

Bei hapa inategemea thamani ambayo mteja


anaamini bidhaa/huduma yako inayo. Katika bei hii
kinachoongoza zaidi ni "Perception", Mtazamo wa
mteja wako. Bei hii pia inabebwa na guvu na
ukubwa wa brand yako kwenye soko.

Wakati mwingine sio lazima kiwe kitu tofauti sana


na wengine, haswa inakuwa ni mtazamo wa wateja
kwenye bidhaa/huduma uliyonayo.

Kwa mfano ni watu wachache sana ambao


wanaweza kutofautisha ladha za aina mbalimbali za
maji kama wakiwekewa kwenye glasi.

Hata hivyo, kulingana na “brand” ambazo kampuni


mbalimbali za maji zimejenga sokoni, kuna aina za
brand za maji zinauzwa kwa bei ghali sio kwa
sababu ya ladha yake bali kwa sababu ya brand yao.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 60


Hivyo hata wewe kwenye kutoa huduma/kuuza
bidhaa unaweza kuamua kuuza kulingana na aina
ya brand ambayo umeijengea bidhaa/huduma.

Wakati mwingine, unaweza kutumia bei hii kwa


kuchaji gharama tofauti kwa watu tofautitofauti
kulingana na unavyoona uwezo wao wa
kugharamia.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 61


Mbinu Ya Nne: COST-PLUS PRICING
(Ongeza juu ya bei ya uzalishaji)

Kwenye mbinu hii unapiga mahesabu bei ya


kuzalisha bidhaa yako kisha unaongeza kiasi gani
(Mark Up) kama faida yako juu yake. Kitu cha
kukumbuka hapa, ni kuhakikisha unaweka gharama
zote za uzalishaji uliotumika.

Kuna wafanyabiashara wengi sana ambao huwa


hawajumlishi gharama zote muhimu za uzalishaji
zikiwemo usafiri waliotumia, umeme/maji n.k

Baada ya kujua gharama ya kuzalisha bidhaa yako


(Unit Price), unaweza kupata bei kwa njia mbili:

Moja unaamua kuongeza kiwango maalumu


cha faida yako kwenye kila bidhaa. Mfano:
kweye kila bidhaa unaamua kuongeza faida ya
shilingi 2000 kwa bidhaa zote.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 62


Mbili unaweza kuamua kuweka ongezeko la
asilimia (%) fulani juu ya gharama ya
uzalishaji. Mfano: Unaweza kusema kuwa faida
yako itakuwa 20% ya gharama za
uzalishaji/ununuzi. Hivyo kama
umezalisha/umenunua bidhaa kwa 10,000/- , bei
yako ya kuuzia itakuwa 10,000+ (20%*10,000)=
12,000/-

Unaweza kuamua ni ipi kati ya hizi mbili utaitumia


kulingana na aina yako ya huduma/bidhaa
unayouza.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 63


Mbinu Ya Tano: PRICE SKIMMING
( Unaibadilisha kulingana na Soko)

Hapa unakuwa unabadilisha bei yako kulingana na


soko linavyoenda. Unaweza kuamua kulingana na
miezi, muda wa watu kupokea mshahara, uadimu
wa bidhaa n.k.

Hii inamaanisha unakuwa hauna bei moja ya


kudumu sokoni, yaani unaangalia ni bei ipi ambayo
itakuwa inafaa kwenye soko, hasa baada ya kuwa
umeshalijua soko lako, hauwi na bei moja ya
kudumu.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 64


Tafakari:
Je, kuna mtu/kampuni ambayo inatumia mbinu
yoyote kati ya hizi tano tulizojifunza?

Je, ni mbinu ipi kati ya hizi ambayo unataka kutumia


kuanzia leo?

...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 65


SURA YA NNE

Njia 8 Za Kumshawishi Mteja


Kununua Kupitia Bei Yako

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 66


Kuna njia nyingi unaweza kuzitumia katika
kumshawishi mteja kununua bidhaa/huduma zako.

Katika sura hii tutaangalia namna ambavyo kwa


umaalumu kabisa unaweza kutumia bei kama
sehemu ya kumshawishi mteja wako.

Njia ya kwanza: Kupitia punguzo


maalumu la bei (DISCOUNT)

Hapa unaamua kupunguza bei ya bidhaa au


huduma yako tofauti na bei ya awali ambayo
ilizoeleka.

Njia hii inasaidia kuuza kwa haraka bidhaa zako,


inakusaidia kuuza vitu vilivyokaa muda mrefu sana,
laiki pia inasaidia kuvutia watu ambao wanafanya
maamuzi kwa kuangalia bei tu (price-sensitive
customers).

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 67


Njia hii unaweza kuitumia kwenye maeneo
yafuatayo:

i. Wateja wapya (To new customers): Hapa


unalenga kuvutia wateja wapya, unatoa tangazo
kuwa mteja akija kwako kwa mara ya kwanza basi
utampa punguzo la kiasi fulani.

ii. Weka Deadline (Expiry Dates): Hapa unasema


kuwa nitatoa punguzo la bei kwa muda wa siku tatu
au kuanzia tarehe 2 hadi tarehe 5 saa kumi jioni.

Ukitumia njia hii hakikisha unaitangaza sana ili kila


ambaye anavutiwa na punguzo la bei aweze kuwa
mteja wako.

Kumbuka kuwa punguzo lako halitakiwi kuwa chini


ya gharama za uzalishaji/ununuzi, inaweza kuwa
hivyo tu pale ambapo umeshaona umetengeneza
faida za kutosha na sasa lengo lako ni kumaliza
bidhaa ili uziagize zingine.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 68


Njia ya pili: Vifurushi
(PRODUCT/SERVICE BUNDLES).

Kama umeshawahi kutumia huduma ya mitandao


ya simu, hii ni rahisi sana kuielewa.

Pale wanaposema ukinunua kifurushi cha shilingi


2000 utapata muda wa maongezi, meseji za kutuma
na MB kwa ajili ya mtandao (internet), hiyo huwa ni
mbinu ya kifurushi katika mauzo.

Yaani unaamua kuweka vitu vingi/bidhaa


tofautitofauti kwenye ofa moja ili mtu aone kuwa
anapata vitu vingi kwa wakati mmoja.

Mbinu hii ina faida kadhaa ikiwemo, kuuza bidhaa


ambazo hazitoki sana kwa kuziambatanisha na zile
ambazo zinatoka sana (help to sell unpopular
products).

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 69


Mteja atanunua zaidi kwa sababu anaona anapata
vitu vingi zaidi (consumer will spend more) na pia
inakupunguzia gharama za matangazo kwa sababu
ile ambayo haijulikani sana huwa inapata faida kwa
kuambatanishwa na ile ambayo inajulikana sana.

Kuna namna mbili ambazo unaweza kutengeneza


vifurushi vyako vya mauzo:

A. Pure Bundling
Kwenye njia hii kuna aina mbili unazoweza kufanya:

i. Joint Bundling (Joint product)


Unaweka bidhaa mbili ambazo zinafanana kabisa,
mfano: nguo mbili au machungwa matatu n.k.

ii. Leaders Bundling (Discount to one product if


you buy a leader product)
Hapa unachofanya, ile bidhaa inayopendwa zaidi
unabaki na bei yake ila unaambatanisha na bidhaa
nyingine ambayo haipendwi sana ambayo
unaiwekea punguzo endapo mtu atanunua ile
inayopendwa zaidi (rudia kusoma tena).

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 70


Hapa unamfanya mtu anayenunua ile bidhaa
anayoipenda, hata kama itakuwa ni bei juu kidogo
asione maumivu sana kwani anaona kuna bidhaa
nyingine ameipata kwa bei rahisi.

Wakati huo, wewe kama muuzaji imekusaidia kuuza


ile bidhaa nyingine isiyo maarufu sana.

B. Mixed Bundling (Buy one at high price or two


at a cheaper price)

Hapa unawekewa bidhaa zaidi ya moja zenye bei


tofauti, ila kama ukinunua zote kwa pamoja
unapewa punguzo la bei la jumla.

Kwa mfano: kitabu changu cha TIMIZA MALENGO


YAKO kinauzwa 15,000/- na kitabu changu cha
MBINU ZA KUONGEZA KIPATO CHAKO kinauzwa
10,000/-. Kama ukinunua vitabu hivi kwa nyakati
tofauti vitakugharimu 25,000/-, ila kwa kutumia
mixed bundling naweza kukuambia kuwa kama
utavinunua vyote kwa pamoja, badala ya kulipa
25,000/- utalipa 20,000/-.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 71


Kumbuka. Kwenye mbinu hii “discount” haiko
kwenye kitabu kimojakimoja bali iko kwenye bidhaa
zote kwa pamoja.

Kwenye mbinu hii mtu akiamua kununua


kimojawapo katika viwili unavyomuuzia basi
hatapata kabisa punguzo la bei, hadi anunue vyote
kwa pamoja.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 72


Njia Ya Tatu: BEI ZA MSIMU
(Seasonal Pricing)

Hapa unaamua kuuza kwa kutumia matukio


ambayo yanakupa sababu za kupunguza bei
kwenye msimu husika.

Kwenye mbinu hii unaweza kutumia njia mbili: moja


ni kuamua kujikita kwenye kuongeza mauzo kwa
kulenga “profit margin” yaani unaweka bei ambayo
faida yake ni kubwa sana kwa kila bidhaa na utapata
faida kubwa.

Au unalenga kupata faida ndogondogo ila kwa


kuuza bidhaa nyingi zaidi (Turnover).

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 73


Maeneo 5 ambayo unaweza kutengeneza
bei za msimu.

A. Kwako mwenyewe
Hapa unalenga matukio/tarehe/misimu ambayo
inakuhusu mwenyewe moja kwa moja.

Mfano: Siku yako ya kuzaliwa (Birthday), Siku ya


kumbukumbu ya harusi yako (wedding anniversary),
siku yako ya graduation n.k.

B. Kwa Familia Yako


Hapa unaangalia watu wako wa karibu: Mtoto
kumaliza shule, birthday ya mke/mume, wazazi n.k.)

C. Sikukuu za kitaifa
Unalenga sikukuu za kitaifa ambazo kila mtu
anazijua: Mfano sikukuu za Uhuru, sabasaba,
nanenane n.k.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 74


D. Sikukuu za Kimataifa
Hapa unalenga zile sikukuu ambazo
zinasherehekewa dunia nzima: Mfano Christmass,
Mwaka mpya, Mei Mosi, Idd-elfitr, siku ya mtoto wa
Africa, Siku ya Wanawake duniani n.k.

Hapa kitu cha muhimu ni kuweza kuunganisha


sikukuu husika na bidhaa unayouza.

E. Hobbies Zako
Hapa unaambatanisha punguzo lako la bei na vile
vitu unavyovipenda. Kwa mfano kama wewe ni
mshabiki wa mpira wa miguu na timu yako
imeshinda/imechukua kombe unaweka punguzo la
bei, mwanamuziki unayempenda amechukua tuzo
n.k.

Kwenye bei hizi zote unachofanya ni kuzishusha


kwa muda mfupi kwenye msimu husika, kisha
baada ya hapo unazirudisha kwenye bei yake ya
kawaida.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 75


Njia ya nne : Unganisha na bidhaa
zingine (Brand Association)

Kwenye mbinu hii, unaamua kuambatanisha bidhaa


mbili kwa pamoja ili kumshawishi mteja wako aweze
kununua.

Yaani kuna bidhaa unaiuza kisha unasema mtu


akinunua bidhaa fulani atapata na nyingine ya bure.

Kuna namna mbili za kufanya:

i. Kuambatanisha bidhaa zinazoendana na


bidhaa yako.
Hapa unaamua kuambatanisha bidhaa ambazo
zinaendana, mfano nguo na viatu, au nguo na
urembo n.k.

ii. Ambazo ni tofauti na bidhaa zako


Hapa unaambatanisha na bidhaa unayouza na
bidhaa tofauti kabisa.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 76


Mfano hapo zamani kulikuwa kuna uji unaitwa
YEBOYEBO ambao ulikuwa ukinunua unapewa na
kandambili za plastiki za njano.

Baada ya muda viatu navyo vikaanza kuitwa


yeboyebo. Hivyo nawe unaweza kuamua kutafuta
kitu cha tofauti ukakiambatanisha na bidhaa
ambayo unaiuza.

Kitu cha muhimu hapa ni usiweke kitu ambacho


kitakuharibia bidhaa yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 77


Njia ya Tano: BEI YA CHAMBO
(Bait Pricing)

Umeshwahi kuona watu wakivua Samaki kwa


ndoano? Huwa wanaweka chambo kama mtego
ambaye ndio haswa samaki anamfuata na kisha
anakutana na ndoano na anavuliwa.

i. Pure Bait: Hapa unatangaza kitu kwa bei fulani ila


unauza vichache sana na mtu akija unamuambia
kimepanda kwa bei kidogo.

Yaani mfano unasema - nauza kwa bei ya discount


20% kwa wateja kumi wa kwanza kisha baada ya
hapo wengine wataongezewa bei au unaweza
ukasema idadi fulani ya wateja wa kwanza watapata
bure kisha wanaobakia watatozwa bei ya kawaida.

Hii itasaidia watu wengi kutaka kununua bidhaa


yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 78


ii. Bait and Switch: Hii unatoa bei ya ofa kwa idadi
fulani ya wateja wa kwanza.

Ila kwa sababu siku zote lazima kuna ambao


watakuwa wamekosa, unaandaa mapema bidhaa
mbadala (Substitute/Alternative product) ambayo
utawapendekezea kununua baada ya kukosa
kwenye ile idadi ya kwanza.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 79


Njia ya Sita: BEI YA KISAIKOLOJIA
(Psychological Pricing)

Unajaribu kupata uamuzi wa kihisia (Emotional) wa


mteja wako badala ya kushawishi akili
(Rational/Logical).

Umeshawahi kununua kitu na baadaye ukagundua


haukihitaji/hukitumii? Kwenye manunuzi mara
nyingi watu hawafanyi maamuzi kutumia akili, ila
wanafanya maamuzi zaidi kwa kutumia hisia.

Kwenye mbinu hii unaweza kutumia mbinu tatu:

i. Cheza na Bei unayoweka


Mfano: weka 999 badala ya 1000, au 2999 badala ya
3000. Hii inamfanya mtu afikirie kwenye mia badala
ya elfu, au kwenye elfu mbili badala ya elfu tatu.

Hatafikiria sana tofauti ya shilingi moja bali


saikolojia itamwambia bado hajavuka kwenda elfu
tatu.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 80


ii. Bidhaa moja unauza kwa bei ghali ikiwa peke
yake na kuna mbili zisizo bora bei nafuu kidogo.
Mfano: Nguo moja bora sana kwa 10,000/- au nguo
mbili zisizo na ubora kwa 15,000/-. Hapa kwa mteja
ambaye anapenda bei chee atalazimika kununua
mbili zisizo na ubora hata kama alikuwa hajaweka
bajeti yake.

iii. Kutumia ujazo kulazimisha mtu anunue zaidi


Mfano kwenye chupa za maji, nusu lita anakuambia
ni 500/- halafu lita moja na nusu (1.5ltrs) ni 1,100/-.

Kwa kawaida kama nusu lita inauzwa mia tano, lita


moja na nusu ilitakiwa iuzwe 1,500/- ila mtu
anapokuuzia kwa 1,100/- ; hata kama ulikuwa hauna
mpango wa kununua lita moja na nusu kwa wakati
huo utaona bora kununua hivyo kwani utakuwa
umepata nafuu kwa kiwango kikubwa sana
kulinganisha kama ukinunua nusu lita tu kwa sasa
hivi kisha ununue tena nusu lita baadaye.

Hapa ni kuwa, unakuwa umemlazimisha mtu


kununua zaidi ya alivyopanga.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 81


Njia ya saba: Bei ya Uchokozi
(CAPTIVE PRICING)

Hapa unatumia njia ya “Lock-in contract” kwa


kumfanya mtu aendelee kuwa mteja wako kwa
muda mrefu bila yeye mwenyewe kujua mapema
pale mwanzoni.

Ili kufanikisha hili, unaweza kutumia mbinu ya “Loss


Leader Approach” ambapo unafanya ile bidhaa
ambayo ndio hasa inatakiwa zaidi, unaiuza kwa bei
rahisi na unakuwa haujapata faida kubwa sana ila
bidhaa inayoambatana nayo ndio ambayo
utatengenezea faida kubwa zaidi kadiri siku
zinavyoenda.

Hivyo kwenye njia hii unakuwa na aina mbili za


bidhaa:

Bidhaa mama (Core Product): Hii unaiuza kwa bei


ndogo zaidi.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 82


Bidhaa ambatanishi (Captive Product): Hii ni
bidhaa ambayo ndio unalenga kutengeneza faida
zaidi.

Mfano: Kampuni inayouza mashine za kunyolea za


Gillete hawapati faida zaidi kwenye mashine za
kunyolea bali kwenye zile nyembe ambazo
utalazimika kuendelea kununua.

Mfano mwingine ni unaponunua “Printer”, unaweza


kuipata kwa bei ndogo sana, ila utashangaa
utakapoanza kununua wino ndio gharama ni kubwa
sana, yaani unaweza kujikuta baada ya kununua
wino mara mbili/tatu inalingana kabisa na gharama
ya kununua printer nyingine mpya kabisa.

Hapa jambo la msingi la kujua ni kuwa, faida kubwa


hauipati kwenye ile bidhaa mama, bali kwenye
bidhaa ambayo itaendelea kuhitajika kutumiwa na
bidhaa mama.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 83


Njia Ya Nane: Mjumuisho wa mbinu
mbalimbali

Hapa unaweza kuamua kutumia njia zaidi ya moja


kwa wakati mmoja au ukaamua kuweka program
mbalimbali za kutumia njia mbalimbali kwa nyakati
tofauti.

Kumbuka sio kila wakati kila njia itakupa matokeo


yanayofanana, itahitaji uwe mtu ambaye unafanya
utafiti wako vizuri sana na kufanya maamuzi ya
kimkakati kuhusiana na njia ipi ambayo itakupa
matokeo mazuri unayoyatamani.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 84


Tafakari:
Ndani ya mwezi mmoja ujao ni njia gani tatu kubwa
ambazo unatamani kuanza kuzitumia ili kuongeza
mauzo kwenye bidhaa/huduma ambayo unaiuza.

1. .....................................................................................
2. .....................................................................................
3. .....................................................................................

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 85


SURA YA TANO

Formula Ya Siri ya Kumshawishi Mteja


Anunue Bidhaa/Huduma yako

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 86


Kama unataka kumfanya mteja wako anunue kwa
haraka na asitumie gharama kama kisingizio cha
kutokununua bidhaa yako, basi unatakiwa kutumia
“formula” hii ya siri ili kumshawishi.

Ili kufanikisha kumshawishi ni lazima kuwe na


pande mbili ambazo zimekamilika katika kuitumia
kwa mafanikio:

Upande wa Kwanza: MUONYESHE


FAIDA (Benefit)

Unakumbuka pale mwanzoni tulieleza kuwa,


unapomwambia mteja kuhusu sifa za nje za bidhaa
yako inamsaidia kuijua bidhaa yako, ila
unapomwambia faida ya bidhaa yako, hapa
inamsaidia kuona ulazima na umuhimu wa kutumia
bidhaa yako.

Kuna namna sita (06) ambazo unaweza kuzitumia


kumuonyesha mteja wako faida atakazopata
kutokana na kutumia bidhaa/huduma yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 87


i. Ongezeko la Faida/Increased Profit
Hapa unaonyesha namna ambavyo mteja wako
akitumia bidhaa yako, atapata faida ya kipesa.

Yaani kama hapo zamani alikuwa anapata faida


kidogo, sasa unamuonyesha namna ambavyo kwa
kutumia bidhaa/huduma yako atapata faida kubwa
zaidi.

ii. Urahisi wa kufanya kitu/Ease of use


Hapa unalenga kumuonyesha urahisi uliopo katika
kutumia bidhaa yako ukilinganisha na kama
angetumia bidhaa za mtu mwingine.

Wakati mwingine unaweza ukauza urahisi wa


upatikanaji wa bidhaa yako ukilinganisha na bidhaa
zingine kama ya kwako.

Hapa unamuonyesha kuwa atahitaji kutumia nguvu


kidogo anapotumia bidhaa yako ukilinganisha na
nguvu anazohitaji anapotumia bidhaa zingine.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 88


iii. Kuondokana na maumivu fulani/Pain Relief
Kumuonyesha namna ambavyo bidhaa/huduma
ambayo unampatia itamuondolea aina fulani ya
maumivu.

Tafiti za uuzaji zinaonyesha kuwa mtu ambaye


anataka kuondoa maumivu anakuwa yuko tayari
mara mbili zaidi kununua kuliko yule anayetaka
kupata faida.

Hii ndio maana ukiwa na maumivu ya jino, utajaribu


kila dawa ambayo unapendekezewa kuitumia.
Kutegemea na aina ya bidhaa/huduma unayouza,
hapa inaweza kuwa ni maumivu ya mwili, kihisia,
kisaikolojia kiuchumi au ya kiakili.

iv. Kuokoa pesa/Saving Money


Hapa unamuonyesha mteja kuwa, kwa kutumia
bidhaa yako atakuwa ameokoa kiasi fulani cha
fedha, tofauti na kama angeenda kununua kwa mtu
mwingine au wakati mwingine.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 89


v. Mwendelezo wa huduma baada ya
kununua/Ongoing Support
Hapa unamuonyesha kuwa kama akitumia bidhaa
yako, utaendelea kuwa naye hadi baada ya muda
fulani ukiendelea kumsaidia au kuwa karibu naye.

Hii inatoa uhakika wa mtu kujua kuwa atakuwa


pamoja nawe kwa muda mrefu zaidi kadiri
anavyoendelea kutumia huduma yako.

vi. Matokeo ya Haraka Mfano: Kupungua uzito


Hapa unaonyesha uharaka wa matokeo ambayo
mtu atayapata baada ya kutumia bidhaa/huduma
yako.

Kwa mfano umeona watu wanaouza bidhaa za


kupungua uzito, huwa wanaonyesha picha za
namna watu walivyopungua uzito ndani ya miezi
fulani baada ya kutumia bidhaa.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 90


Upande wa Pili: TUMIA USHAHIDI WA
WATU WALIOFAIDIKA NA BIDHAA YAKO
(Social Proof)

Robert Cialdini, Mwandishi wa kitabu cha Influence:


The Psychology of Persuasion anasema social proof "Is
a psychological phenomenon where people assume the
actions of others in an attempt to reflect correct
behaviour for a given situation".

Hapa anamaanisha kuwa watu wengi wanaamini


kuwa vitendo vya watu wengine vinawakilisha tabia
sahihi zinazotakiwa kufuata katika jambo fulani.

Hii ndio maana watu wakiona watu wanaowaamini


wanafanya jambo fulani, huwa nao wanaamini kuwa
jambo hili linatakiwa kufanyika hivyo.

Kwenye njia hii, kuna aina Sita (06) za “Social Proof”


ambazo unaweza kuanza kuzitumia kama namna ya
kumshawishi mteja wako kununua zaidi:

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 91


i. Mtaalamu/An Expert .
Hapa unatengeneza ushawishi kupitia mtaalamu
wa eneo husika ambaye anaamika tayari. mfano:
Mwalimu akizungumzia kitabu anachotakiwa
kusoma mtoto wako, mzazi yeyote atakuwa tayari
kufanya hivyo.

Au daktari anapoamua kupendekeza aina ya dawa


ya kutumia, au hospitali ya kwenda kutibiwa n.k
wewe kama mgonjwa unamsikiliza sana, ni kwa
sababu ni mtu anayeaminika, mtaalamu wa ngozi
anapozungumzia mafuta mazuri ya kupata n.k.

Hivyo wewe unaweza kuangalia kulingana na aina ya


bidhaa/huduma yako unaweza kumtumia aina gani
ya mtaalamu ili kuongeza ushawishi wa
bidhaa/huduma yako.

ii. Watu maarufu/Celebrity


Umeshawahi kujiuliza kwa nini matangazo mengi ya
bidhaa huwa wanatumia watu maarufu, kwa mfano
PEPSI waliwahi kumtumia Mchezaji maarufu wa
Argentina Lionel Messi,

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 92


Mwimbaji maarufu nchini Tanzania Diamond
Platnumz n.k. Hii ni sawa na kutuma ujumbe kuwa,
kama watu hawa maarufu wanatumia basi wewe
usiwe na shaka.

Kwa upande mwingine inaeleza kuwa nawe


unatakiwa kuungana nao ili nawe pia uwe katika
hadhi yao. Hii ndio maana kuna “brand” nyingi za
nguo wanapozizindua huwa wanatafuta watu
maarufu wa kuzitangaza kwanza.

iii. Mtumiaji/Users
Hapa unatumia watu ambao tayari walishatumia na
kuridhika na huduma yako. Hapa unawaomba wale
ambao wamefurahia huduma yako kueleza aidha
kwa maandishi, sauti au video wakielezea namna
walivyonufaika na huduma yako.

Kusudio kubwa kwenye hili ni kujenga hali ya


kuaminika kwa haraka kupitia watu wengine zaidi ya
wewe mwenyewe, usisahau kuwa watu wanapenda
kununua kwa mtu ambaye anaaminika na watu
wengine pia.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 93


iv. Watu wengi/ Wisdom of the Crowd
Umeshawahi kusikia mtu/kampuni inasema “hadi
sasa tumeshawahudumia watu milioni moja” au
kwenye vitabu unakuta wanaandika juu ya kitabu
“Kitabu hiki kimeshauza nakala zaidi ya milioni tatu”

Au Msanii anaposema “hadi sasa hivi wimbo wangu


wa YouTube umeangaliwa na watu milioni 2” au
“kwenye platform ya Audiomack/Spotify
wameshadowaload watu laki mbili” .

Hii yote inalenga kukuonyesha kuwa hautakiwi kuwa


na mashaka kabisa na bidhaa/huduma ambayo
inatolewa.

Matumizi ya namba huwa ni muhimu sana pia kwa


sababu watu huwa hawapendi kuwa wa kwanza
kutumia bidhaa, wanataka wengine wajaribu
kwanza wao wafuate baadaye baada ya kuwa na
uhakika kabisa.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 94


Hii ndio sababu kubwa pia, kwa nini watu wengi
wanafanya bidii kuwa na wafuasi wengi kwenye
mitandao ya kijamii.

v. Wakiona marafiki zao wanatumia bidhaa


yako/ Wisdom of friends
Ushawishi wa eneo hili unatokana na ukweli kuwa,
watu wako wa karibu pia wanaamini na kutumia
bidhaa au huduma yako.

Mfano: Watu wapoona watu wako wa karibu kama


vile mwenzi wako, watoto wako, marafiki zako n.k.
Watu wakiona watu wa karibu wanazungumzia
vizuri bidhaa/huduma yako inawasaidia
kuwaaminisha kuitumia na wao pia.

Hii ndio maana unapomuuzia mtu, unaweza


kumuomba akutambulishe/kukuunganisha na watu
wake wengine wa karibu ambao anadhani
wangependa kutumia bidhaa/huduma yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 95


vi. Kutambuliwa na mamlaka fulani/Certification

Hapa unaongeza ushawishi wako kwa kufanya


bidhaa au huduma yako itambulike na mamlaka
fulani ambayo yenyewe inaheshimika zaidi katika
eneo husika.

Mfano kwa watu ambao wanauza bidhaa/kutoa


huduma ya chakula wanapotambulika na kuwa na
uthibitisho wa Tanzania Medicines and Medical
Devices Authority (TMDA).

Au kama wewe ni mtoa huduma na unakuwa


unatambulika na umoja wa watoa huduma katika
eneo lako (Associations) n.k.

Kulingana na unachofanya unaweza kulazimika


kusomea “certification” fulani ili kuongeza ushawishi
na uzito katika kile unachokifanya. Hii itakufanya
unapoongea, uonekane kama mtaalamu wa
kiwango cha juu katika eneo lako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 96


Tafakari:
Je, katika njia hizi za kumshawishi mteja kununua
bidhaa/huduma zako, kwa sasa ni mji gani tatu
kubwa ambazo unaweza kuanza kuzitumia
kuongeza ushawishi kwa wateja wako?

1. .....................................................................................
2. .....................................................................................
3. .....................................................................................

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 97


SURA YA SITA

Mbinu 9 Bora Zaidi Za Kujitangaza Ili


Kuvuta "Attention" ya Bidhaa / Huduma
yako Kirahisi.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 98


Kumbuka kuwa, unaweza ukawa na bidhaa nzuri
sana ila kama watu hawaijua, hautaweza kuuza
vizuri. Ni lazima uwe na namna ya kuwafanya watu
waijue na waitake bidhaa yako ili uweze kuiuza.

Katika sura hii utajifunza mbinu tisa ambazo


unaweza kuanza kuzitumia leo ili kufanya
bidhaa/huduma yako ivutie wateja.

Kumbuka, unaweza kutumia moja au zaidi kwa


wakati mmoja kulingana na aina ya kile
unachofanya na matokeo ambayo unayatafuta.

Mbinu Ya Kwanza: Tumia “Contest


Strategy”

Hapa unaamua kufanyisha watu mashindano ya


kupata kitu fulani na kuwapa zawadi wale
watakaoshinda.

Kwenye mbinu hii kuna mambo matatu ya msingi:

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 99


Moja, unawashindanisha watu kupata zawadi ya
unachouza au inayoendana na unachouza:
Yaani, kama unauza nguo, unawashindanisha
watu na wanashinda nguo au unaweza kuamua
kutoa zawadi tofauti na unachouza ila
kinachoendana kidogo na unachouza. Jitahidi
katika kufanya hivi, isihusishe watu kutoa pesa.
Unaweza kutumia njia ya maswali, na
wanaopata majibu sahihi basi wanapata zawadi.

N:B Kwa sababu nia ni kuhusisha watu wengi zaidi,


hakikisha pia maswali yako yanakuwa marahisi sana
ambayo mtu yeyote yule anaamini akishiriki
kuyajibu basi atashinda.

Jambo la pili, Hakikisha umepata coverage


nzuri: Unapotumia njia hii, kumbuka nia yako ni
kuhakikisha kuwa unakuwa na watu wengi sana
wanashiriki kadiri iwezekanavyo. Hivyo ili kupata
faida ya mbinu hii unaweza kuhusisha waandishi
wa habari, watu wenye ushawishi mkubwa
(kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii n.k.)

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 100


Jambo la tatu, unaweza kuwataka watu
wawaambie watu wengine kama sehemu ya
masharti: Mfano, kama unaendesha shindano
hili kwenye akaunti yako ya mitandao ya kijamii
unaweza ukasema “Tag rafiki zako watatu na
niambie bidhaa yangu mpya iliyotoka hivi
karibuni”. Kila anapotag watu maana yake
anakusaidia kuwafanya wakufahamu na
wakufuatilie pia.

Mbinu Ya Pili: Toa Misaada (CSR-


Corporate Social Responsibility)

Hapa unaamua kutoa misaada kutoka kwenye


biashara yako, unaweza kutoa kwenye faida
uliyopata au ukaamua kuwa ni sehemu ya matumizi
yako kama uwekezaji wa kujitangaza.

Unaweza kufanya hili kwa njia mbili kubwa:

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 101


Kwa watu/mtu mwenye Shida
Hapa unaamua kutafuta kundi fulani la watu wenye
shida (kituo cha wazee, kituo cha Watoto, wodi ya
wagonjwa n.k) na unaamua kuwapa msaada fulani,
au unaamua kutafuta mtu mmoja mwenye shida
unamsaidia (Mfano: mlemavu unamsaidia baiskeli,
mgonjwa unamsaidia matibabu n.k.)

Kumbuka watu hupenda kujiambatanisha na watu


wenye huruma, hivyo kwa kufanya hivi utafanya
watu wengi wapende kuwa upande wako na
wapende kufanya biashara na wewe pia kwa sababu
wanajua kuwa wanapofanya biashara na wewe
wanakuwa wanasaidia jamii pia.

Kwa taasisi/jamii fulani


Hapa unaamua kujenga kitu fulani kwa gharama
zako mwenyewe au unatoa sehemu ya msaada kwa
jamii. Mfano: Unaamua kujenga kisima kwa ajili ya
wanakijiji, au unatoa mabati kiasi fulani kwa ajili ya
ujenzi/mifuko idadi fulani ya simenti au madawati
n.k.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 102


Hapa unafanya kitu kitakachoacha alama, na
itasababisha watu wakuseme vizuri na hii inafanya
watu wakuamini na kuwa tayari kufanya biashara na
wewe.

Mbinu Ya Tatu: Mitandao ya Kijamii


(Social Media)

Hapa unatumia mitandao ya kijamii ili kuvuta


“attention” yako vizuri. Baada ya kufanya ile ICP yako
kule mwanzoni, utakuwa umeshajua wateja wako
wengi huwa wanatumia mitandao gani ya kijamii
zaidi.

Mambo makubwa mawili ya kuzingatia unapotumia


mitandao ya kijamii katika kuvuta “attention” ya
wateja wako ni pamoja na mambo yafuatayo:

Jambo la kwanza, jiweke kama mtaalamu/expert


katika eneo lako. Njia rahisi ya kufanya hili ni kutoa
elimu mara kwa mara kuhusiana na kitu
uanchokiuza kabla ya kuanza kuuza.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 103


Kwa mfano kama wewe unauza vyakula vya lishe,
unaweza kutoa ushauri wa namna ya kutengeneza
mlo kamili, vyakula hatarishi, vyakula vizuri vya kula
usiku n.k.

Utakapofanya hivi, watu wengi zaidi watakuwa


wanatembelea akaunti zako kujifunza na
watakapokuwa na shida fulani basi watakuwa tayari
kukuuliza na kuchukua ushauri kutoka kwako.

Jambo la pili, jitahidi kutumia video mara kwa


mara. Utafiti kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii
unaonyesha kuwa takribani 40% ya watumiaji
wanapendelea zaidi kuangalia video kuliko kitu
kingine chochote kile.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 104


Mbinu ya nne: Dhamini Matukio
Mbalimbali (Sponsor Events).

Hapa unachagua matukio kimkakati kwa kuangalia


vitu vikubwa viwili:

Moja ni kuangalia yale ambayo yanaendana na


bidhaa/huduma unayotoa na mbili kwa kuangalia
matukio ambayo yanawafikia aina ya wateja ambao
wewe unawatafuta zaidi.

Kama bidhaa zako zinahusu wanawake unaweza


ukalenga matukio yanayowakusanya wanawake
zaidi , kama vijana unalenga matukio ya vijana n.k.

Kwenye udhamini, unaweza kupata udhamini kwa


njia mbalimbali:

i. Unaweza kupata “Mention”


Hapa unakuwa unatajwa kwa jina na muongozaji
tukio (MC/Moderator) kama mmoja wa watu
mliodhamini tukio husika.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 105


ii. Kuweka bango (Banner)
Hapa unaweka bango linaloonyesha
bidhaa/huduma unayotoa. Kumbuka ni muhimu
kuweka eneo ambalo ni la kimkakati ambalo watu
wataliona kama vile: Geti la Kuingilia, eneo ambalo
watu watapita wakati wa kwenda kuchukua chakula
n.k.

iii. Meza ya kuweka bidhaa


Kwenye hili, unapata meza ya kuweka bidhaa zako
au vipeperushi ambavyo vinaelezea bidhaa au
huduma yako. Kwenye hili, ni muhimu pia kutafuta
sehemu nzuri ya kuweka meza ili iwe rahisi watu
kukuona.

Ukiwa kwenye tukio ambalo unaweka meza


inashauriwa uwahi mapema ili kujua watu
watakuwa wanaingilia na kutokea wapi ili uchague
nafasi nzuri ya kuweka meza yako.

iv. Nafasi ya Kuzungumza


Kwenye hili, unapata fursa ya kuzungumzia
kuhusiana na huduma au bidhaa yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 106


Jambo la kwanza la kuzingatia ni kuwa tumia muda
mfupi kadiri uwezavyo, yaani jitahidi utumie dakika
chini ya zile walizokupa.

Jambo la pili, kwa kutegemea na aina ya tukio


jitahidi uwe umevaa nguo ambayo ina nembo ya
bidhaa/huduma/kampuni yako.

Pia kumbuka kuwa hata kama anayeongea ni


mmoja, kama unaweza kwenda na watu wengine
zaidi ambao watakuwa wamevalia nguo zenye
nembo yako inasaidia sana.

Unaweza pia kushika bidhaa yako mkononi


unapoenda kusimama mbele ya watu. Hii itakuwa
rahisi pale unapoongea kuionyesha bidhaa kwa
washiriki wa tukio husika na wakaiona.

Kumbuka unapoongea mbele za watu mara


nyingine itakuwa wakati wamechoka sana, jitahidi
kuzungumza mambo muhimu tu ya msingi.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 107


Ili kujifunza zaidi nakushauri utembelee Youtube
Channel yangu na utafute video “Siri Tano za Kuwa
Mzungumzaji Mzuri” na pia kitabu changu cha
namna ya kuzungumza kwa ushawishi.

Mbinu ya Tano: Ushirikiano na


wengine (Partnership)

Hapa unashirikiana na mtu ambaye atakuongezea


kuonekana kwako au nguvu ya “brand” yako.
Unaposhirikiana na mtu wa namna hii, kusudi
kubwa ni kutumia ushawishi wao kujitangaza zaidi,
hii inaongeza sana kuonekana kwako (Visibility).

Kwenye kushirikiana na wengine, unaweza kuamua


kufanya tukio la pamoja na wengine au kufanya kitu
kwa makubaliano ya kuambatana.

Kwa mfano: Mfanyabiashara maarufu wa nguo Fred


Ngajiro, VUNJA BEI mara nyingi kila anapofungua
duka pembeni yake kunakuwa na duka la viatu la
rafiki yake FRANK KNOWS.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 108


Kwa sababu bidhaa ambazo wanauza zinaendana
“Complementary Products”, inakuwa rahisi sana
mmoja kujitangaza kupitia mwingine.

Hii inafanya kazi nzuri sana kama mnauza bidhaa


ambazo hazishindani na badala yake zinahitajiana.

Kwa upande mwingine unaweza kuamua kufanya


matangazo ya pamoja yanayohusu bidhaa zenu.
Mfano “Kila unaponunua nguo kwa Vunja Bei, utapata
punguzo la 20% kwa viatu vya Frank Knows”.

Hii inasaidia pia, kama mmoja tayari ni maarufu,


atamsaidia mwingine kujitangaza.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 109


Mbinu Ya Sita: Tumia mbinu ya
“Face Lift”

Unaamua kufanya kitu kinachoonyesha kama vile


biashara yako imeanza upya au imepata mabadiliko
makubwa sana.

Sio lazima yawe mabadiliko makubwa sana,


yanaweza kuwa mabadiliko ya kawaida kama vile:
Kupaka rangi, kuweka mapambo, kuweka mpangilio
upya wa bidhaa zako, ukabadilisha maandishi ya
bango lako n.k.

Mabadiliko haya huwa yanaathari kubwa sana ya


kisaikolojia kwa wateja wako kwa kuwafanya
waanze kuamini kuwa watapata ubora zaidi.

Kila unapofanya mabadiliko haya, hakikisha


unatangaza na pia unatangaza ofa mpya
inayoambatana na mabadiliko ambayo umeyafanya.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 110


Mbinu ya Saba:
Maadhimisho/Anniversary

Hapa unaamua kutumia maadhimisho ya kibiashara


kama sehemu ya kuvutia wateja zaidi. Unaweza
kuangalia maadhimisho ya kutimiza mwezi/mwaka/
miaka fulani na unaalika marafiki zako kwa pamoja.

Unapofanya maadhimisho, unaweza kutumia kama


sababu ya kutoa punguzo la bei n.k na hii itavutia
watu zaidi.

Hakikisha kila unapofanya maadhimisho basi


unayatangaza vizuri ili watu wengi waweze
kufahamu. Unaweza kutengeneza “poster” kupitia
mitandao ya kijamii au unaweza kuweka bango
mbele ya ofisi yako kutoa tangazo linaloonyesha ofa
yako unayotoa.

Unaweza pia kualika mtu fulani maarufu ambaye


utamualika ili kuongeza uzito wa tukio.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 111


Mbinu ya Nane: Tumia ufunguzi rasmi
(Launch Party)

Kwenye mbinu hii, unaamua kutumia siku maalumu


kwa ajili ya uzinduzi wa ofisi yako au
bidhaa/huduma.

Ili kuvutia watu wengi zaidi, unaweza kuamua


kualika watu maarufu ambao watakusaidia pia
kuendelea kutangaza kuelekea siku ya tukio husika.

Waalike watu wenye ushawishi na waombe


wenyewe pia waseme kupitia mitandao yao ya
kijamii kuwa watakuwepo. Hii itasaidia kukutangaza
kwa wafuasi wao.

Kutegemea na mahusiano ulilyonayo, kuna baadhi


ya watu maarufu wengine ili waweze kuja itabidi
uwalipe, kwenye kufanya hivyo inabidi uichukulie
kama ni uwekezaji wako katika kuitangaza
bidhaa/huduma yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 112


Mbinu ya Tisa: Tumia Mabalozi
(Brand Ambassador)

Ripoti ya kampuni ya Nielsen ilionyesha kuwa 84% ya


watu hununua bidhaa/huduma kwa sababu ya
kuiamini (Trust), yaani kabla hawajaweka vigezo vya bei
huwa wanaangalia kama wameiamini au la.

Unaweza kutumia njia nne kuchagua balozi wa


bidhaa/huduma yako:

i. Niche Authority
Inabidi uangalie aina ya watu ambao utawatumia
kutangaza bidhaa zako ili ushawishi wao uendane na
kile wanachotangaza.

Mfano: utakuwa umegundua kuwa wachezaji wa


mpira wanatumika zaidi kutangaza vifaa vya
michezo vya makampuni makubwa kama vile Nike,
Adidas, Puma, Kappa n.k.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 113


Kama unauza bidhaa za mavazi, itatakiwa umtumie
mtu ambaye anasifika kwa kupendeza, ni model,
aliwahi kushinda/kushiriki mashindano ya
ulimbwende n.k.

ii. Peer Advocate


Kwenye kigezo hiki, balozi unayemchagua anatakiwa
aendane kwa namna fulani na wateja unaowalenga.

Kwa mfano: Unaweza kuangalia vigezo vya umri,


eneo wanaloishi, jinsia, walioko kwenye ndoa n.k.

Kwenye kuongeza ushawishi wa kutumia Blue Band


kwenye mkate kwa watoto, huwa wanawatumia
watoto pia. Kwenye kutangaza pedi za akina mama,
hawafanyi wanaume wanafanya wanawake
wenyewe.

Hapa suala la msingi ni kuwa balozi anatakiwa


kuendana kwa sifa na wale ambao anawatangazia
bidhaa/huduma.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 114


iii. Watu maarufu/Celebrity
Hapa unaangalia watu wenye ushawishi mkubwa
kwenye jamii ambao wanaweza kuifanya bidhaa
yako ijulikane kwa haraka.

Moja ya changamoto ya kutumia watu hawa


maarufu ni kuwa, ikitokea wamefanya kitu chenye
kuleta aibu, basi aibu hiyo itaambatana pia na
bidhaa yako.

iv. Wanaopenda bidhaa yako na wako tayari


kuisemea/ Enthusiast
Hawa ni wale ambao wameshawahi kutumia
bidhaa/huduma yako na imewaletea matokeo na
wako tayari kuisemea vizuri.

Hii ni aina nzuri sana ya mabalozi kwa sababu huwa


wanaongea kwa hamasa kubwa.

Umeshawahi kuona watu walioshinda bahati nasibu


wakitumiwa kushawishi wengine waamini katika
bahati nasibu? Wanachofanya hapo ni kuwafanya
wale walioshinda kuwa mabalozi wao.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 115


Tafakari
Je, kulingana na mwenendo wako wa biashara kwa
sasa hivi, ni mbinu gani nne za kuvuta “attention”
ambazo unaweza kuzitumia ili kuongeza mauzo
yako?

...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 116


SURA YA SABA

Mbinu za Kutumia Mteja Anapokataa


Kununua Bidhaa / Huduma Yako
(Overcoming Sales Objections)

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 117


Sales Objection, Ni vile vitu ambavyo mteja
anavitumia kama sababu ya kutonunua bidhaa
yako, yaani visingizio vya kwa nini hawezi kununua
kwa wakati huo.

Inaweza kuwa DIRECT kwa kusema "HAPANA


KABISA" au kutumia INDIRECT kwa kutoa sababu
nyingine.

Sio kila anayeonyesha dalilli ya kutokuwa tayari


kununua bidhaa yako inamaanisha haitaji, wengine
ni kwa sababu ya "Misconception". Hivyo tunasema,
kila objection unayopewa ni fursa ya wewe
kuongeza ushawishi wako.

Bila kujali unafanya bishara gani, utakutana na aina


NNE KUU ZA OBJECTION:

i. Kutohitaji Kwa Wakati Huo (Lack Of Urgency)


Katika hili, mteja anakuonyesha kuwa ameikubali
bidhaa au huduma yako na hana tatizo nayo, kitu
pekee ni kuwa kwa wakati huo hayuko tayari
kuinunua/kuitumia.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 118


Hivyo anakuambia “nitanunua siku nyingine”. Kwenye
hili tutaangalia baadaye namna ya kukabiliana na
jibu kama hili.

ii. Kutohitaji Kabisa (Lack of Need)


Katika hili mteja anaonyesha kuwa hana uhitaji
kabisa na bidhaa/huduma ambayo unaitoa. Hii kwa
muuzaji ni fursa ya kuelezea vizuri kuhusu
umuhimu wa bidhaa/Huduma yako.

Hapa pia ili kujua kwa nini mteja haitaji, unaweza


kuuliza maswali ambayo ni "Open Ended", yaani
maswali yanayotoa fursa kwa mtu kuelezea zaidi
kwa nini ahitaji bidhaa yako.

iii. Kukosa Pesa (Lack of Budget)


Kwenye hili mteja anaweza kukueleza kuwa hana
pesa kabisa au ana pesa ndogo sana ambayo
hauwezi kuwa tayari kufanya naye biashara.

Hapa ina maana kazi kubwa ya muuzaji ni


“Kuposition value” ya anachokiuza.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 119


Swali la tafakari:
Umeshawahi kujiuliza kwa nini watu hawasemei bei
hospitali/duka la madawa?
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................
...............

iv. Kutokukuamini (Lack of Trust)


Hii hutokea pale watu ambapo wanakuwa
hawakuamini wewe, hawaamini bidhaa/huduma
unayotoa au mtu ambaye unaambatana naye
kwenye kufanya hiyo biashara.

Ingawa “objections” ziko nyingi, ila mara nyingi


zitaangukia katika makundi haya manne.

Kutoka na makundi haya, kuna vitu vifuatavyo


ambavyo unatakiwa ujifunze namna ya kuvikabili
unapokuwa unauza:

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 120


Kwa mfano mtu anaweza kusema hana pesa, lakini
kikiwa ni kitu cha muhimu sana kama vile matibabu,
kodi ya nyumba n.k lazima itapatikana.

Hivyo kazi yako kubwa kama muuzaji ni kuhakikisha


kuwa unaonyesha uthamani wa unachokiuza na
kuwa faida atakayopata kwa kununua
bidhaa/kutumia huduma yako ni kubwa sana kuliko
bei anayolipa.

Usiingie katika kutoa majibu kama vile “Na mimi


nimenunua kwa bei ghali”, hii haitakusaidia
kubadilisha mawazo ya mteja wako.

• Ngoja nikaongee na…..(Mke / Mume /


Mzazi / Bosi / Business Partner n.k)

Ukisikia mtu anazungumza hivi maana yake ni kuwa


(a) Hana maamuzi
(b) Anamtumia huyo mtu kama kisingizio.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 121


• Gharama ni kubwa sana
(It's too Expensive)

Tafiti za wanunuzi zinaonyesha kuwa katika wateja


10 ambao utawatafuta, kuna wateja 6 ambao
watatumia kisingizio hiki kutonunua kutoka kwako.

Mteja yeyote ambaye anakuambia kuhusiana na


ukubwa wa gharama, anakuwa anamaanisha
mambo yafuatayo:

(a) Hawana pesa ya kununua .


(b) Hawajaona thamani ya unachouza.
(c) Wanaweza kupata sehemu nyingine kwa bei
rahisi zaidi.

Kazi yako kubwa ni kuyajibu maswali haya ambayo


yanakuwa yamejificha kwa ndani. Kutokuwa na pesa
hutokea kama mtu anaona naweza kuwa na
mbadala.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 122


Inawezekana ikawa ni kweli hana maamuzi au
wakati mwingine anamtumia huyo mwingine kama
kisingizio tu.

Ufanye nini?:

Tafuta kujua kama ni a au b. Kama ni A tafuta


namna ya kujua visingizio ambavyo huyo mwingine
anaweza kuvitumia kwa kumuuliza mteja wako.

Mfano muulize swali hili : unadhani ukiongea naye


nini kinaweza kumzuia kununua kutoka kwangu?
Majibu yake yatakupa mwanga wa kujua mambo ya
msingi ya kuendelea kuyaelezea.

Mbinu nyingine hapa ni kutafuta namna ya kuongea


naye moja kwa moja mtu ambaye anaonekana
amebeba maamuzi ya mteja wako.

Unaweza kumuomba mawasiliano ya huyo mtu au


unaweza pia kuamua kumshawishi amlete kwenye
biashara yako ulipo/wewe uende ukaonane naye.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 123


Hii itasaidia kujibu maswali ya huyo mtu mwenye
maamuzi wewe mwenyewe. Kwa vyovyote
itakavyokuwa, basi tafuta kujua kwa undani sababu
kati ya zile kubwa nne ni ipi inamfanya asinunue ili
ujue namna ya kukabiliana nazo.

• Nahitaji Nikafikirie Kwanza


Mtu wa namna hii usimlazimishe kufanya maamuzi


wakati huo. Mwambie hakuna shida atapata muda
wa kufanya maamuzi, ila tafuta kujua ni kwa nini
anataka muda kufikiria kwanza.

Njia nzuri ya kukabiliana na mtu wa namna hii ni


kuwaonyesha uharaka “Sense of Urgency”-
waonyeshe kitu watakachokosa wasipofanya
maamuzi haraka.

Mfano unamwambia: Ila kumbuka bado siku mbili


ofa itaisha na baada ya hapo bei itapanda au
kumwambia kuwa, kimebakia kimoja tu na ukikikosa
leo basi hautakipata tena.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 124


Kitu kikubwa hapa ni kumfanya mtu afanye
maamuzi bila kuhisi kuwa amelazimishwa lakini
aweke uzito mkubwa.

• Nimeshawahi Kupata Tatizo Na Hii


Huduma/Bidhaa

Hapa mtu anakupa uzoefu mbaya aliowahi kuupata


kwa kutumia bidhaa/huduma kama hiyo. Cha
kwanza kabisa kama bidhaa/huduma ilitolewa na
wewe/kampuni yako anza kwa kuomba samahani.

Kama ni bidhaa/huduma ilitolewa na kampuni


nyingine hapa utatakiwa kutoa pole kwa usumbufu
au hasara ambayo ameipata.

Baada ya kufanya hivyo, kabla ya kuanza kuelezea


unachotaka kumuuzia, tafuta kujua tatizo ambalo
alilipata na onyesha hisia zako za huruma kwake
kwa hasara au madhara aliyoyapata. Jiepushe
kuwasema vibaya watu waliomuhudumia.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 125


Baada ya hapo, onyesha namna ambavyo
unamthibitishia kuwa tatizo ambalo alikutana nalo
halitajirudia tena au namna utakavyolishughulikia
kwa utofauti.

Mfano: unaweza kumpa uhakika kwa kutumia


ushahidi fulani wa watu ambao uliwahudumia huko
nyuma n.k.

Njia nyingine ni kutoa “guarantee” ya kumhakikishia


kuwa hatapoteza: Mfano kama hautapata matokeo
nakurudishia pesa, au kifaa kisipofanya kazi
nitakubadilishia au lipa nusu kisha nenda katumie
baada ya muda fulani ukiridhika utamalizia
iliyobakia.

Kumbuka, mtu anapoelezea tatizo alilowahi kulipata


huko nyuma kwa watoa huduma kama wewe
anamaanisha kuwa amepoteza kuamini (trust), kazi
yako kubwa ni kuhakikisha kuwa unaijenga hiyo
trust kwa wakati huo.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 126


• Tayari Kuna Mtu Ananiuzia/Nina
Mkataba Naye

Mtu akikupa sababu ya namna hii, cha kwanza


heshimu uchaguzi wa mteja wako wa kutumia
watu/kampuni hiyo.

Usiingie kabisa kwenye mtego wa kuanza


kuwaponda wapinzani wako ambao anawatumia
kwa sababu haujui ukaribu wake na wao na
ukifanya hivyo inakuwa umepoteza sifa ya kuwa
“Professional”.

Tafuta kujua ni nani ambaye anamuhudumia kama


inawezekana, kuna wengine watasema na wengine
wanaweza wasiwe huru kusema. Ila wengi huwa
wanakuwa tayari kuzungumzia.

Baada ya hapo, tafuta kujua vigezo na masharti


(Terms & Conditions) ambazo anapewa na
anayemuhudumia kwa sasa.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 127


Unaweza kuangalia bei anazouziwa, muda wa
malipo, ananunua mara ngapi kwa mwaka n.k.

Kumbuka nia kubwa ya maswali haya ni kuangalia


tofauti iliyoko kati yako na ambaye anampatia
huduma kwa sasa ili ujue namna ya kuingia na
kumshawishi ahame kutoka kwa huyo mtu na aanze
kufanya biashara na wewe.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 128


Tafakari:
Je, wateja wako wengi kwa sasa huwa wanatumia
mbinu ipi kukwepa kununua kutoka kwako?
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................

Unapanga kutumia majibu gani katika haya


tuliyojifunza?
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................
...........................................................................................

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 129


SURA YA NANE

Mbinu 6 Za Kuhakikisha Mteja


Ananunua
(Closing Techniques)

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 130


Uwezo wa kufanya “marketing” ni kuwafanya watu
wajue ulichonacho, ila kitu muhimu ni kuweza kuuza
(sales).

Watu wengi wanawekeza katika kuwafanya watu


wajue walichonacho ila huwa wanashindwa
kuwafanya watu watoe pesa na kununua.

Kwenye sura hii, utajifunza mbinu ambazo unaweza


kuzitumia ili kuhakikisha kuwa asilimia kubwa ya
wateja ambao umewafanyia “marketing” wananunua
bidhaa yako .

Mbinu ya kwanza: Onyesha uharaka /


dharura (The Urgency Close)

Mbinu hii ni ile ambayo inalenga kuonyesha kuwa


mtu akishindwa kukipata kwa wakati huo ambao
unamuuzia aidha:
a. Hatakipata tena vita kuwa vimeisha.
b. Atakipata kwa bei kubwa zaidi.
c. Atakipata kwa ugumu zaidi.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 131


Kwenye mbinu hii unaweza kutumia namna kubwa
tatu:

i. Muda maalumu wa ofa (Limited Time offer):


Hapa unamwambia mteja kuwa, ofa yako inaanzia
siku fulani na inaishia siku fulani/muda fulani na
ukiikosa, hautaipata tena.

ii. Mabadiliko ya bei (Price Change Technique):


Hapa unaficha uharaka wako kwenye bei.
Unamwambia mtu kuwa bei ya kitu hiki itapanda
baada ya muda fulani.

iii. Uhaba wa bidhaa (Scarcity Technique):


Hapa unaonyesha kuwa zimebakia bidhaa chache
na hazitapatikana tena au kuna idadi ya watu
maalumu ambao wakishafika hautauza tena au
unamwonyesha kuwa bidhaa zipo ila kuna watu
wengi wanazigombania kuzinunua.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 132


Mbinu ya Pili: Unampa orodha ya
kuchagua (The Option Close)

Kwenye mbinu hii unampa mteja orodha ya


kuchagua kwenye vile ambavyo umemuambia.
Hapa nia ni kumuweka njia panda kuchagua na
kutomruhusu kukaa bila maamuzi.

Mfano:
“Mwaka huu ni muhimu sana usome vitabu vyangu
viwili, kile cha Money Formula kinachofundisha elimu
ya fedha isiyofundishwa shuleni na kile cha mbinu za
kuongeza kipato chako, Je wewe ungependa kukisoma
kipi?” au unamwambia

“Unaweza kuchukua bidhaa moja na ukalipa baada


ya mwezi mmoja au uchukue mbili na ulipe baada ya
miezi mitatu, wewe unachagua kuchukua ipi?”

Hapa ulichofanya ni kuweka nadharia kuwa


ameshafanya maamuzi na ni lazima achague
mojawapo na hana namna ya kuamua kutokununua
kabisa.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 133


Mbinu ya tatu : Unafanya kama
ameshakubali (Assumptive Close)

Hapa ni kama “unaassume” mteja ameshakubali


tayari. Yaani baada ya kuongea naye, swali la
mwisho unalomuuliza ni kama vile tayari
ameshakubali kununua.

Baadhi ya maswali ambayo unaweza kumuuliza ni


kama vile:

"Je, Hii ungependa nikuletee lini?"

“Je, wewe unataka ngapi?”

“Je, hii ungependa tukuletee wapi?”

Kisaikolojia utakapomuuliza mteja kwa namna hii,


na yeye analazimika kufanya “confirmation tendency”
kwa kufanya maamuzi.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 134


Mbinu ya nne: Unampa Mapendekezo
(Suggestive Close)

Kwenye mbinu hii unaongea kama mtaalamu


(expert) unayetoa ushauri kulingana na uzoefu
wako/taaluma yako.

Kwa mfano unamwambia mteja:

“kulingana na changamoto yako, hii ndio


itakufaa zaidi”

“Kulingana na uzito wako, vyakula hivi ndio


vitakufaa zaidi”

“Watu wenye miili kama yako, wanashauriwa


kuvaa viatu vyenye kisigino cha namna hii”

“Kwa umri wako, hii ndio itafaa zaidi”

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 135


Kitu kikubwa cha kuzingatia ni kuwa katika hili,
wewe kama muuzaji unaamua kutoa ushauri
kulingana na utaalamu wako na pia uzoefu wako

Mbinu ya Tano: Ondoa kitu kwenye ofa


yako (Take away closes)

Hapa kama mteja anasema kitu ni ghali sana,


unaondoa baadhi ya bidhaa/kupunguza kitu fulani
kisha unamshushia bei.

Wateja wengi ukiwafanyia hivi, kisaikolojia


watakuwa hawataki kupoteza ulichopunguza na
wanaanza kuona ulichokitoa ni cha muhimu sana
ndio maana unataka kubaki nacho, mwishoni
wataamua kununua tu.

Mfano: Unauza simu, unamwambia hii simu iko na


full package: Ina charger, battery moja ya ziada na
earphone. Unamwambia kuwa ukimpa vitu vyote
unamuuzia 150,000/-.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 136


Kama mteja atasema bei hiyo ni ghali na anasema
kuwa anataka umuuzie kwa 100,000/-.

Unachofanya kama muuzaji, haumkatalii bali


unamwambia kuwa, kwa bei hiyo nitakuuzia simu ila
nitabakia na betri ya ziada na charger pia hautapata.

Kisaikolojia imeonekana kwamba, wateja wengi


sana wakiona unaondoa kitu baada ya kuomba
kupunguziwa bei huwa wanaamini unachotoa ni cha
thamani sana na pia wanaumia kupoteza.

Kwa sababu ya aina hiyo ya maumivu huwa


wanaamua kupanda bei ili wakipate, na hapo
itakusaidia kuwauzia kwa bei nzuri zaidi yenye faida
upande wako.

Ukifanya hivi hata kama hawatafika kwenye bei ya


awali uliyowatajia, ila watakuwa tayari kuongeza
tena kidogo ili wapate vyote.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 137


Mbinu ya sita: Soft Closes

Kwenye kuuza kupitia mbinu hii unajaribu kuuliza


maswali ambayo hayamlazimishi kufanya maamuzi
ya haraka ila yanakusaidia kujua anachowaza.

Mfano:
Kama nikipunguza kwa 20% utakuwa tayari
kununua?

“Kama nikikupa viwili kwa bei hii utakuwa tayari


kununua?”

“Nikikuongezea muda wa kulipa mkopo, Je


utakuwa tayari kuchukua?”

Mbinu hii unaitumia pale ambapo unakuwa hauna


uhakika kuhusiana na utayari na uamuzi wa mteja
kuhusiana na bidhaa yako.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 138


Tafakari:
Je, katika mbinu hizi sita za kufungia mauzo, ni zipi
ambazo unaona kwa aina ya bidhaa/huduma
unayotoa unaweza kuanza kuzitumia kuongeza
wateja zaidi?

1. .....................................................................................
2. ...................................................................................
3. .....................................................................................
4. .....................................................................................

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 139


HITIMISHO

Kwenye kitabu hiki umejifunza mbinu mbalimbali za


uhakika ambazo wauzaji wa bidhaa / huduma
mbalimbali wamekuwa wakizitumia ili kuongeza
mauzo yao.

Kila mahali nilipofundisha mbinu za kuongeza


mauzo, wale ambao waliamua kufanyia kazi
wamepata matokeo makubwa sana.

Kabla haujaweka kitabu hiki chini, pata muda wa


kutafakari na kuamua katika mbinu nyingi sana
ambazo umejifunza kupitia kitabu hiki, ni zipi
ambazo unaweza kuanza kuzitumia kulingana na
aina ya biashara na bidhaa/huduma unayotoa.

Ili kuendelea kupata matokeo makubwa kwenye


eneo la mauzo, nakushauri upate muda wa kufanya
kozi ya mauzo pia online (Wasiliana kwa
WhatsApp kupitia 0762 312 117 au 0742 112 946

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 140


na pia hakikisha unasoma kitabu changu kingine
cha Saikolojia Ya Mteja kupitia mawasiliano
yaliyotolewa kwenye kitabu hiki.

Nakutakia mafanikio makubwa unapoanza kufanyia


kazi uliyojifunza na tafadhali usiache kutuma
ushuhuda wako wa ongezeko la mauzo kwenye
biashara yako kupitia mawasiliano yangu.

See You At The Top

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 141


KUHUSU MWANDISHI

Joel Arthur Nanauka ni mwandishi wa vitabu na


mwalimu katika maeneo ya uongozi, biashara na
kujitambua.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 142


Ni mhitimu wa masomo ya biashara na uongozi
kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam na
Stashahada ya juu ya Diplomasia ya Uchumi kutoka
kituo cha mahusiano ya nje (Centre For Foreign
Relations).

Mwaka 2020 alitajwa katika orodha ya vijana 100


wenye ushawishi zaidi katika bara la Afrika na
pia kijana mwenye ushawishi zaidi Tanzania
katika eneo la ufundishaji watu kujitambua
(Personal Development). Pia aliwahi kutajwa kama
kiongozi bora kijana wa Dunia mwaka 2012,
nchini Taiwani, China.

Amekuwa mkufunzi wa wakurugenzi wa


kampuni binafsi na mashirika ya umma kupitia
taasisi ya wakurugenzi Tanzania (IoDT) katika eneo
la kuendesha mabadiliko katika taasisi (Change
Management )

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 143


Joel ni mwalimu (Certified Trainer) katika eneo la
biashara na ujasirimali anayetambuliwa na
kutumika kufundisha mitaala ya vyuo vikuu vya
Regent na Joseph Business School vyenye makao
yako makuu nchini Marekani.

Pia amekuwa mlezi wa wajasiriamali wa Afrika


kupitia shindano maalumu la Africa
Entrepreneurship Award linalofanyika kila mwaka
chini ya Benki ya BMCE iliyoko nchini Moroco.

Joel alikuwa ni mmoja wa timu maalumu ya


wataalamu walioteuliwa na serikali chini ya
Baraza la Uwezeshaji la Taifa (NEEC) katika
kuandaa muhtasari wa mtaala maalumu wa
ujasiriamali wa Taifa.

Joel Arthur Nanauka amekuwa mkufunzi wa


vyombo vya habari tangu mwaka 2018 kupitia
taasisi ya Tanzania Media Foundation (TMF) katika
eneo la biashara na uongozi.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 144


Amewahi kufanya kazi na Umoja wa Mataifa (UN)
kupitia shirika la UNESCO na baada ya hapo
alianzisha taasisi ya Africa Success Academy
ambayo kwa sasa ndiye mkurugenzi wake.

Joel amemuoa Rachel na wamebarikiwa watoto


watatu wa kike: Joyous, Joyceline na Jonel

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 145


VITABU VINGINE VILIVYOANDIKWA NA
JOEL ARTHUR NANAUKA.

HARDCOPY (Nakala ngumu)

1. Timiza Malengo Yako (Mbinu 60 walizotumia


watu maarufu kufanikiwa)

2. Ishi Ndoto Yako (Siku 30 za kuishi maisha


unayotamani)

3. Tabia 12 Zinazoleta Mafanikio.

4. Ishinde Tabia Ya Kughairisha Mambo.

5. Ongeza Kipato Chako (Maarifa juu ya fedha,


Biashara na uwekezaji)

6. Nguvu Ya Mwanamke.

7. Mbinu Za Kufanikisha Ndoto Katikati Ya


Changamoto.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 146


8. How To Pass Your Exams With Ease.

9. Uzalendo Na Ujenzi Wa Taifa.

10. Ufanisi Kazini

11. Boresha Mahusiano Yako.

12. Money Formula

13. Core Genius

Kupata Hardcopy wasiliana nasi

0745 252 670

0762 312 171

0756 094 875

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 147


eBOOKS / SOFTCOPY (Nakala laini).

1. Money Formula (Elimu ya fedha isiyofundishwa


shuleni)

2. Hatua Sita Za Kujiajri.

3. Muongozo Wa Mafanikio.

4. Core Genius (Jinsi ya kugundua uwezo wako wa


kipekee)

5. Jinsi Ya Kufanikiwa Katikati Ya Nyakati


Ngumu.

6. Saikolojia Ya Mteja

7. Mbinu Za Kujenga Ujasiri Na Kujiamini.

8. Surviving The Crisis.

9. Namna Ya Kuondokana Na Madeni.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 148


10. Uzalendo Na Ujenzi Wa Nchi.

11. Mbinu Za Kuongeza Kipato.

12. Strategy, Siri Za Kupata Matokeo Makubwa


Ndani Ya Mwaka Mmoja.

13. Nifanye Biashara Gani?

14. Marafiki.

15. Ufanisi Kazini.

16. Kiongozi Wa Tofauti.

17. Sayansi Ya Tabia.

18. Mbinu 8 Za Maandalizi Ya Kufaulu Mitihani


Kwa Kiwango Cha Juu.

19. Siri 12 Wanazotumia Wanafunzi Bora Ndani


Ya Chumba Cha Mitihani.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 149


20. Maono.

21. Mafanikio Ya Kifedha Kwa Wanandoa.

22. Kuyaishi Maono Yako.

23. Nguvu Ya Mwanamke.

24. Ishinde Tabia Ya Kughairisha Mambo.

25. Ishi Ndoto Yako.

27. Mbinu Za Kuongeza Kipato Chako.

28. Uzalendo Na Ujenzi Wa Nchi.

29. Pigania Maono Yako.

Kupata eBooks Wasiliana nasi

Whatsapp 0742 112 946

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 150


Kozi Alizoziandaa, Unaweza Kuzisoma Online.

1. Mbinu Za Kuuza Zaidi.

2. Jinsi Ya Kujenga Kipato Cha Uhakika Kwa


Kujiajiri.

3. Jinsi Ya Kuondokana Na Madeni.

Kupata kozi hizi wasiliana nasi

Whatsapp 0762 312 117

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 151


TEMBELEA MITANDAO YA KIJAMII YA
JOEL ARTHUR NANAUKA.

YouTube: Joel Nanauka (Utapata VIDEO nyingi za


kukufundisha mambo mbalimbali)

Instagram: joelnanauka_ (Utapata mafunzo kila siku


yatakayokusaidia kupiga hatua katika maisha)

Facebook: JNanauka (Utapata mafunzo kila siku na


pia shuhuda mbalimbali za watu walionufaika na
mafunzo)

Twitter: jnanauka.

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 152


Unaweza kupata vitabu vingine vilivyoandikwa na
JOEL NANAUKA kutoka TIMIZA MALENGO
BOOKSHOP tunapatikana Njia Panda Chuo Kikuu
Ubungo, wasiliana nasi kwa namba zifuatazo.

Instagram: timizamalengo_bookshop

0745 252 670

0756 094 875

Mbinu Za Kuuza Zaidi | Joel Arthur Nanauka | 153

You might also like