You are on page 1of 3

SAIKOLOJIA YA MWANAMKE

Maelezo haya yanatoa mafunzo kuhusu tabia na akili ya mwanamke wakati anapoingia katika mapenzi
na mwanaume. Na hasa mwanamke anapokuwa mrembo, fahamu atakujaribu bila hata ya yeye
mwenyewe kujifahamu. Ukiweza kufaulu kwenye majaribu hayo, she feels like wow na anaanza kupenda
na kukupa heshima. Lakini ukishindwa kukabiliana na majaribio hayo kinachotokea ni kwamba wewe
mwanaume unakua chini yake na yeye mwanamke anakuwa juu. Na hayo ndio matakwa ya mwanamke
kwa uhalisia.

SAIKOLOJIA 01 : UPENDO NA UHITAJI


Mwanamke huwa na kawaida ya kuangalia uhitaji wa mwanaume. Anapenda kufahamu ni kwa kiasi gani
mwanaume huyu ananipenda na kwa kiasi gani ananihitaji kiasi ya kuwa anashindwa kunikosa.
Anapofahamu ya kuwa wewe unahitaji sana kutoka kwake, huanza kutumia udhaifu huo kukamilisha
matakwa yake binafsi kama vile kufanya vitu kwa uhuru n.k. Hivyo huanza kuchukua mamlaka tataribu
na kujaribu kukudhibiti kupitia huo upendo unao-muonesha. Ili kufaulu hapa unatakiwa kuonesha ya
kwamba unamjali lakini na unampenda lakini ujaribu kumfanya akubali ya kuwa sio muhitaji sana kwake.
Kwa mfano kama umetaka kitu kutoka kwake na yeye amekunyima usioneshe kuwa ulikuwa unahitaji
sana. Nyamaza kimya na wala usirudie kumuomba kila wakati kitu hicho. Ukifanya hivyo, mwanamke
hufikria wewe hauna thamani. Lakini unapo onesha ya kwamba huna haja naye sana, kile ulichokitaka
utapewa kwa upendo zaidi kuliko kama ungeliendelea kusisitiza. Ukitaka kitu kutoka mwanamke jifanye
kama huna haja nacho, atakupa zaidi ya ulivyotaka.

SAIKOLOJIA 02: KUSOMA MAZINGIRA.


Mwanamke huwa na kawaida ya kukusoma tabia zako wewe mwanaume pale munapokuwa katika
mahusiano. Wakati unahitaji mapenzi na kutimiza hisia zako, yeye huangalia kwenye tabia zako, jinsi
ulivyo, mkarimu, mkatili, mwenye hasira, mpole n.k Yote hayo humsaidia kukufahamu wewe na kuanza
kutumia sehemu yenye udhaifu kama ushindi kwake. Hii ni kwasababu mwanamke anapenda sana
uhuru wake lakini wakati huo huo anahitaji upendo pia. Kwa mfano, siku za mwanzo mwanzo kwenye
ndoa na mahusiano anaweza kutoka bila ya kupata ruhusa, anakuangalia jee utafanyaje? Utakemea au
utanyamaza kimya au utachukulia ni jambo la kawaida tu. Hapo huangalia jinsi utavopokea,
anapofahamu ya kuwa kitu fulani hakijakukera na wala hukuonesha hisia yoyote katika jambo
anaendelea kufanya kitu hicho kwa mara nyingine mpaka anathibitisha ya kuwa hujali kwenye hilo. Sasa
siku ambayo utahitaji kumzuia, ndipo hapo ugomvi unaanza. Ili kufaulu hapa, kama kitu chochote
hujapenda kutoka kwake ni bora uwe muwazi tokea mwanzo. Watu wengi huharibu hapa, kwasababu
mwanamke unampenda sana na labda unahisi kama utaongea chochote anaweza kukuacha unaamua
kukaa kimya, fahamu ya kuwa unampa uhuru amabo utakuharimu baadae. Unaposema kitu fulani
hukipendi tokea mwanzo mwanamke anatengeza heshima anajua ya kuwa unampenda lakini wakati huo
huo unamfanya afahamu ya kuwa maisha yako yana thamani zaidi kuliko mahusiano.

SAIKOLOJIA 03: VICE VERSA


Hii ni tabia nyengine ya mwanamke, anaposema kitu fulani atafanya aidha kwa kumuomba au kwa
kutaka mwenye, fahamu kuwa kwa 90% hatofanya kitu hicho. Usitie tamaa kabisa kama atafanya,
chukulia kama vile hajawahi kukuahidi chochote. Na anaposema kitu fulani hatofanya basi kwa 75%
atafanya kitu hicho. Hivyo zikitokezea hali kama hizi usikurupuke wewe mchukulie kama alivyo. Hii ni
kwasabau akili ya mwanamke inapoingia kwenye huwa kama mtoto.

SAIKOLOJIA 04: KUDEKA AU KUJIBEBISHA


Mwanamke hupenda sana kudeka au wanaita kujibebisha, hii ndio asili ya mwanamke na kama
utamuona mwanamke hana tabia hiyo aidha ameshaumizwa sana au amerithi tabia za kiume. Hivyo
anapojibebisha unatakiwa kuenda nae vizuri. Wanaume wengi pia huharibu hapa, wanapomuona
mwanamke anajidekeza wao hukemea tabia hiyo. Kitendo hiki kwa 60% kinapunguza mapenzi kutoka
kwake mwanamke. Kauli kama “hemu, niache nipo busy” utazisikia kutoka kwa mwanaume.

SAIKOLOJIA 05: MAAMUZI


Hii ni sehemu muhimu sana ambayo mwanaume unatakiwa kufaulu. Mwanamke huwa na kawaida ya
kuangalia uamuzi wako. Kwa mfano, tuchukulie mkeo anakwambia baba fulani leo nahitaji ubakie
nyumbani usiende kazini. Huenda hapo hakusema hivyo kwasababu ana hamu na wewe, pengine
alikuwa anaangalia utachukua uamuzi gani? Ukikubali haraka na mara moja itakuwa umempa thamani
na hiyo itamfanya yeye kupoteza mvuto kwako, Ukikataa moja kwa moja unatengeneza picha ya
kutomjali. Sasa unafanyaje? Unatakiwa usikubali lakini utafute sababu au sharti. Kwa mfano, unaweza
kusema hivi, sawa ukitaka nibakie basi nipige busu au nikumbatie. Mwanaume wa design hizi anavutia
sana kwa mwanamke yoyote yule.

SAIKOLOJIA 06: KUEPUKA AU KUPUNGUZA UPENDO


Mwanamke pia anakuwa na tabia ya kukuepuka au kuonesha hakupendi tena au kuonesha upendo wake
umepungua, na hii inatokea baada ya kuishi nae kwa muda mrefu. Ingawa kwa uhalisia anakuwa
anakupenda tena sana lakini hufanya hivyo ili kujua udhaifu wako. Kuangalia jee kwa kutumia silaha hiyo
anaweza kukuburuza. Kwasababu matakwa makubwa ya mwanamke ni kumuendesha mwanaume vile
anavyotaka yeye. Sasa ili kufaulu jaribio hili, usikurupuke isipokuwa muoneshe wewe upo sawa na hali
yoyote hile hata kama kumkosa ikibidi. Wapo wanaume wengine katika hali kama hiyo, huanza kuzalisha
mashaka kwenye uhusiano na kummuliza mwanamke unanipenda au kwanini umepungua upendo
wako. Unapofanya hivyo tu, kaka unafeli.

SAIKOLOJIA 07: HOFU YA KUACHWA.


Mwanamke anapojihakikishia ya kuwa anampenda mtu fulani inakuwa ni kweli kabisa tofauti na
mwanaume. Ndio maana mwanamke hawezi kugawa penzi lake, hata kama atakuwa na wanaume 2 au
zaidi ya hapo, kuna mmoja anampenda kweli na wengine waliobakia anawadanganya. Sasa, mwanamke
huogopa sana kuachwa na mtu anaempenda kwa dhati, jambo hilo humtia hofu sana. Hivyo epuka tabia
za kutania kuwa unataka kumuacha mwenza wako. Kwani kufanya hivyo, hupelekea kupunguza mapenzi
ya mwanamke na kumfanya ajenge chuki taratibu dhidi yako.

SAIKOLOJIA 08 : KUWEKA REFRENCE


Sijapata kuona sehemu ambayo wanawake wapo vyema kama hapa. Wapo vizuri sana kwenye kuhifadhi
mambo. Wewe unaweza kupandisha hasira na kuongea mbovu vya kutosha halafu baada ya muda
ukasahau na ukasamehe pia. Lakini mwanamke chochote utachokisema yeye hunakili na kukiweka
akilini. Na sio hapo tu, bali hutengeneza tafsiri. Hivyo ni jambo zuri kama ukipandisha hasira kubakia
kimya na kutoa maamuzi baadae. Lakini pia unapoweka ahadi kwa mwanamke jikubalishe ya kuwa
utatimiza ahadi yako. kwasababu hata iweje ujue mwanamke kitu hicho atakuwa na kumbukumbu
nacho. Ni bora usi-ahidi kama huwezi kutekeleza, kwanini? Kwasababu kwa kitu kidogo kama hiko tu,
kwa mwanamke kumtia uchungu sana mpaka pale utakapotimiza.

SAIKOLOJIA 09: HAKUBALI KUSHINDWA


Wanawake wana kitu kinaitwa “Complex Superiority Psychology”. Kisaikolojia hali hii inamfanya mtu
kujiona yeye yupo sahihi zaidi au anaweza kufanya kitu kwa ufanisi zaidi kuliko mwengine. Hivyo kwa
mwanamke ni bora afe lakini anapoamua kusimamisha misimamo yake huonesha yupo bora sana.

You might also like