You are on page 1of 1

JINSI YA KUTENGENEZA DEODORANT YA ASILI KABISA

DEODORANT ni maalum kwa kuondoa harufu mbaya kwapani,kuondoa


weusi na kuling’arisha kwapa lako.

Zipo aina nyingi za deodorant lakini leo nitakufundisha njia ya kwanza


rahisi ya kutengeneza deodorant yako nyumbani.

MAHITAJI
a) Mafuta ya nazi 6tsp
b) Arrow root powder (unga wa magimbi).1/2 kikombe
c) Baking soda ¼ kikombe
d) Essential oil unayoipenda

JINSI YA KUTENGENEZA
• Chukua baking soda changanya na arrow root koroga vizuri
• Kisha changanya na mafuta ya nazi koroga vizuri,mwisho weka
essential oil koroga vizuri.
• Kama una blaenda yako tumia kusagia vizuri hadi uone deodorant
yako imekuwa nzito kisha weka kwenye kopo lako.
JINSI YA KUTUMIA
• Utakuwa utatoa kidogokidogo unajipaka kwapani kila baada ya
kumaliza kuoga.
• MAFUTA YA ASILI UTAYAPATA MADUKA YA ASILI
• ARROW ROOT UTAYAPATA KWENYE MADUKA YA ASILI AU KAUSHA
MAGIMBI JUANI KISHA UTAYASAGA ILI UPATE UNGA WAKE.

By Paschal James

You might also like