You are on page 1of 52

DAWA YA KUACHA KUACHA KUKOJOA.

Chukuwa nusu ya kilomoja ya ndevu za mahindi mabichi ambayo hayajakauka kisha yachemshe
kwenye maji lita mbili na nusu (2.5) kwa muda wa dakika kumi alafu utakunywa kutwa mara
tatu kwa muda wa siku tano yaani asubuhi, mchana na jioni. Ukiwa unaendelea kutumia dawa
chukuwa kamba za mti wa passion (mpesheni) kisha funga kiunoni wakati wa kulala utafanya
hivyo kwa muda huo ambao unatumia dawa yako. Yaani siku tano.

Hio ni njia ya kwanza. Njia ya pili sanasana kwa wanawake ni unatakiwa kupanda juu ya mti
kwenye kima ambacho unaogopa kuwa hata ukianguka unaweza kuumia. Sasa ukifika kwenye
hiko kima kojoa kisha uangalie huo mkojo. Hii itakupelekea wewe kuogopa ukiuona ule mkojo
na itakujenegea wakati ukiwa umelala usiku ukitaka kukojoa utashtuka na hutakojoa kitandani
bali kwenye mahala husika.

MAAJABU YA ASALI NA MDALASINI

Mdalasini unatakiwa kuwa kwenywe hali ya unga. Kwa mchanganyiko wa asali na mdalasini
huwa unatibu maaradhi takribani ishirini na moja (21). Unachotakiwa kufanya ni kupata asali
mbichi yenye ujazo wa lita moja, weka kwenye chombo kikavu inaweza kuwa kama bakuli au
dishi. Chukua mdalasini kwenye kijiko kikubwa cha kulea chakula mara mbili kisha changanya
kwenye asali. Changanya mchanganyo wako mpaka uwe mzito na uhakikishe kuwa asali na
mdalasini umechanganyika vizuri. Ili dawa ifanye kazi vizuri. Weka kwa muda wa masaa kumi
na mbili (12). Ndipo utaanza kuitumia. Ukishapata mchanganyiko wako vizuri usiutumie hivi

Jinsi ya kuitumia

Chukuwa maji ya moto weka kwenye biliani (glass) au kikombe kidogo mpaka juu lakini
usijaze sana maana baadaye utakuja kuweka mchanganyiko waka wa asali na mdalasini.
Ukishaweka maji yako kwanye kikombe au glass yako kisha weka ule mchanganyiko waka wa
asali na mdalasini vijiko viwili cha kula. Changanya maji ya moto na mchanganyiko waka wa
asali na mdalasini vizuri. Kisha acha itulie na kupoa maana kuna maji ya moto (45-50 nyuzi joto)
utaacha kwa dakika tano ili uchanganyike kwenye glass yako. Kwa mchanganyo huu utakunywa
asubuhi kabala ya kula chochote na baada ya saa moja utaanza kula kama chai yako au chakula
kingingine kwa glass moja. Na utakunywa tena usiku muda wa kwenda kulala. Fanya hivi kwa
muda wa wiki moja na maradhi yako yatakuwa yameshaondoka yote.

Maradhi ambayo yanatubu kwa mchanganyiko waka wa asali na mdalasini;

1. Hutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume


2. Kukosa la hamu ya kula
3. Hupunguza makali ya vidonda vya tumbo
4. Tatizo la mafua makali kwa haraka kabaisa hupona kwa masaa machache
5. Hupunguza tatizo la cholestro (rehemu) mwilini ambayo hupatikana kwa kula nyama
6. Ugumba amabo husababishwa na hali ya maisha
7. Ugonjwa wa moyo
8. Kusumubuliwa na chunusi (lakini sio kwa kunywa bali ni kwa ule mchanganyiko wako
wa asali na mdalasini kabla hujaweka kwenye maji chukuwa kiasi kidogo weka mkononi
kisha paka sehemu yenye chunusi kama mafuta. Ukishapaka baada ya nusu saa moja
unaweza kucuhukua maji ya uvuguvugu na kunawa hiyo sehemu uliyopaka
mchanganyiko wako. Fanya hivi kwa muda wa siku tano tatizo litakuwa limepungua
limmetoka.
9. Pia kwa watu ambayo wanasumbuliwa na meno. Chukuwa kiasi kidogo cha
mchanganyiko waka wa asali na mdalasini kabla hujaweka maji na dondoshea kwenye
lile tundu la jino. Fanya hivi kwa muda wa siku tano tatizo litakuwa limepungua
limmetoka.
10. Husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni. Hapa utakunywa mchanganyiko waka wa
asali na mdalasini utakunywa glass moja asubuhi na jioni. Kwa muda wa siku tano tatizo
litakuwa klimeisha kabisa.
11. Husaidia kuboresha kinga mwili (CD4) maana kuna wengine kinga zao za mwili
zimeshuka au kupunguwa kwa magonjwa mabalimbali au ni asali yake.
12. Husaidia kupunguza uzito kwa wale wenye uzito mkubwa kupita kiasi.
13. Husadia kuondoa mchafuko wa tumbo.
14. Humsaidia mtu mwenye ugonjwa wa viungo, kuna watu wengine viungo vimeparalaizi
kuna watu wanajinsia uchomvu.
DAWA INAYOTIBU MARADHI MIA MOJA 100

Vitu vya kuchanganya dawa:

1. Asali mbichi kikombe kimoja


2. Unga wa mbegu ya parachichi. Chukua mbegu ya parachichi safisha (chuna ganda la nje)
saga vizuri na chekecha kisa pata unga wake.
DAWA YA KIFUA SUGU

Chukua vitunguu vyenye afya yaani vikubwa na vizuri kadhaa kisha vimenye kisha vikatekate
kwa namna yoyote ile ila viwe vidogo-dogo kisha visage kwenye blenda au kwenye kinu na
hakikisha vinasagikika na kuwa laini kabisa. Chukuwa asali mbichi kabisa na sio asali ya
kupikwa kwa rangi yoyote ile. Chukua kijiko cha vitunguu vya kusagwa na kijiko kimoja vya
asali baadaye koroga mchanganyiko wako wa asali na vitunguu vilivyo sagwa.

Matumizi

Mgonjywa anywe kijiko kimoja asubuhi, machana na jioni. Kwa muda wa siku tatu. Zingatia
uwiano wa asali na vitunguu.

ANGALIZO: Kama utakuwa umetingwa (huna muda) sana na shughuli kwa nyakati za mchana,
jitahidi kwa muda wa asubuhi na jioni kutumia dawa yako. Utakuwa umepona kabisa

Na kama ni kwa mtoto mdogo mpatie kijiko kidogo kwa muda ule ule kama hapo juu.

DAWA YA MACHO

Kuna tatizo la macho na wengine huvaaa mewani. Ila kwa mchanganyiko wa karoti tatu,
kitunguu, tango na nyanya unaweza kutengeza dawa mzuri kwa matatizo ya macho. Ila karoti
inabidi ziwe nyingi kuliko vitungu vingine kwa namna nyingine karoti zizidi. Usimenye
chochote kile.

Jinsi ya kutengenza: Kata vitu vyako kwa usafi wa hali ya juu kisa saga kwenye bleanda wa
twanga kwenye kinu kilicho safi. Hapo utapata chuisi nzuri isiyokuwa na maji.

Matumizi. Mgonjwa atakunywa glass moja kutwa mara tatu yaani asubuhi, mchana na usiku kwa
muda wa siku ishirini na moaj tu. Ila hawa ni kwa wale wenye matatizo ya muda mrefu.

Ila kama ni wenye matatizo ya muda mchache tumia vivyo hivyo kwa muda wa wiki mbili tatizo
lako litakuwa limekwisha kabisa.

ONYO: usiongeze kitu chochote kile ili kuleta ladha.

MAGONJWA MENGINE (32): Pumu, muasho, kukosa choo, hisafisha figo, muasho mwilini,
tatizo la moyo.
.

DAWA YA KUSAFISHA FIGO.

Tiba hii itaenda kusaidia kuiweka figo katika mazingira salama kabisa. Na kuifanya figo kufanya
kazi yaker kwa ufanisi wa hali ya juu.

Kufeli kwa fgo na maradhi mbalimbali

Sababu za kufeli kwa figo

Maji lita moja

Mbegu za mlonge

Mane mane sawa na ubani ila inakuwa katika rangi nyekundu

Machungwa na asali ya nyuki mbichi.

Chukua maganda ya tango yakaushe na utayasaga na kupata unga wa mbegu za mlonge pia
pataungwa wa mane mane pata unga wa maganda ya machungwa.

Chukua unaga manga

DAWA YA KUTIBU BUSHA

FAIDA 11 ZA MCHAICHAI

1. Hungeza CD4
2. Huzuzia kuharisha
3. Huundoa tatizo la saratani pia ni kama kinga na pia hutumika kama kiga kwa saratani
4. Kwa mama mjazito kujifungua salama
5. Hupunguza uzito
6. Hushusha HBP
7. Kusafisha damu ini, na figo

Chukua maji lita tatu na majani kilo utachemsha kwa dakika kumi tano na utakunywa kwa muda
wa wiki moja ila kama ni utatumia kama tiba kunywa kukikombe kimoja kama chai kwa kila
siku. Utakunywa kutwa mara tatu.

DAWA YA KUTIBU BAWASIRI


Nini maana ya bawasiri; bawasiri ni hali ambayo mtu hupata kwa kutokwa kwa uvime wa nyama
kwenye sehemu ya haja kubwa. Hii kwa jina lingine hufaamika kama Nkulo.

MAHITAJI

Pata juisi ya alovera, (chukua majani ya mti wa alovera saga kwenye blenda au twanga kwenye
lakini kumbuka ni chungu sana, usiweke maji kisha chuja msago wako kisha utapatta juisi). Pia
tengeneza juisi yoyote ya matunda yoyote sharti iwe imetengezwa nyumbani yaani si ile ya
dukani. Vile vile tenga asali.

Dawa ya kwanza changanya juisi ya alovera na juisi ya matunda, kwa kuweka nusu glasi ya juisi
ya matunda, na nusu nyingine weka juisi ya alovera na kisha koroga vizuri ili juisi ichanganyike.
Na mgonjwa wa bawasili atakunywa kutwa mara mbili kwa muda wa siku ishirini na moja (21),
kwa uwezo wa Mungu utapona. Vilevile chukuwa maji ya alovera kisha paka kwenye ule
uvimbe wako (mgonjwa), utapakaza kutwa mara tatu. NB usifute baadaya kupaka.

Dawa ya pili, chukua nusu lita ya asali na nusu lita ya habbat soda kisha changanya kisha
kunywa kijiko kimoja asubuhi na jioni kwa siku kumi na nne (14) kisha kunywa maji ya kutosha
sana.

JE UNA MINYOO?/DALILI ZA MINYOO/ATHALI ZA MINYOO/MADHARA YA


MINYOO/TIBA YA MINYOO/KUJIKINGA NA MINYO

DALILI ZA MINYOO/ATHALI

ATHALI ZA MINYOO

TIBA YA MINYOO/KUJIKINGA NA MINYO.

Twanga mbegu za paipai

TIBA YA GESI TUMBONI UHAKIKA 100% - ( dawa 1 ya gesi tumboni / kujaa gesi tumboni )
2020.

Katakata limao au ndimu kwa muundo wowote ule kisha weka weka kwenye susufuria na weka
maji ya kadri kisha katakata vipANDE VYA TANGAWIZI. Kisha changanya kwenye sufuria la
ndimu na maji. Chemsha ndani ya dakika tano (5). Itakuwa teyari. Mbali na kutumiwa na mtu
mwenye gesi vilevile hata kwa mwanamke mwenye hedhi pia hutumika kama ni tiba.

Jinsi ya kutumia: unachotakiwa kufanya ni kuchuja vizuri na kuweka kwenye kikombe cha chai
au glasi, changanya na asali kijiko kimoja mpaka viwili kisha koroga vizuri kabisa kwa ajili ya
matumizi. Pia husaidia kuondoa kitambi na mafuta yasio na lazima mwilini.

DAWA INAYOTIBU MARADHI


Kwa mchanganyiko wa Habbat Soda na Asali huwa inatibu maradhi yote isipokuwa uzee na
kifo. Unachotakiwa kufanya ni kupat unga au poda mara nyingi habbat soda huwa katika mfumo
wa chenga chenga au mbegu (black seeds). Sasa saga habbat soda mpaka ilainika kama
poda/unga.

Uwiano wake ni kijiko kimoja cha unga wa habbat soda na kijiko kimoja cha asali. Au asali
kikombe kikombe kimoja cha asali na kikombe kimoja cha unga wa habbat soda, huo ndo
uwianon wako wa dawa.

Jinsi ya kutumia, baaada ya kupata mchanganyo wako, tumia kijiko kidogo mara pengi huwa ni
kijiko cha chai au tumia nusu kijiko cha chakula. Kutwa mara tatu na utatumia dozi hii kabla ya
kula. Na utakula dawa hii na utakaa saa moja ndo ule chako. Pia wengine wanaamua kutengeza
mafuta na ukunywa hayo mafuta kijiko kimoja na utakuwa umepona na maradhi yako yote.

FAIDA ZA MAFUTA YA MNYONYO

Mbegu za mnyonyo zikamue vizuri na upate mafuta ya mnyonyo.

Faida za mafuta ya mnoyonyo ni kama yafuatayo:

1. Husaidia ukuaji wa nywele, kuna watu wanapata kipara kila siku. Paka mafuata ya
mnyonyo kabla kulala
2. Husaidia usingizi kwa mtu amabaye anapata shida kupata usingizi. Jinsi ya kuyumia haya
mafuta haya. Paka mafuta kidogo kwenye kope zako.
3. Kukuza nywele na huondoa hali ya kipilipili na kutokatika kwa nywele na kuzifanya
nywele zako kuwa nyeusi.
4. Husaidia kutibia maradhi yoyoyote ya ngozi, kama vile mba, mapunye,
5. Husaidia kwa watoto wanaolia usiku au hata mchana. Kwa kumpaka na kwa kumchuwa
mwilini mwake baadaya kuoga
6. Pia huua minyoo yote tumboni. Jinsi ya kutumia kwa mtu mkubwa tumia vijiko viwili
vya chakula.
Miaka, 1-7 kijiko kimoja kidogo
Miaka 8-12 vijiko viwili vya chai
Miaka 13-17 kijiko cha chakula kimoja
Miaka 18 – na kuendelea vijiko viwili vya chakula.

FIGO

Kazi za figo;

1. Kuosha damu kwa kuondoa uchafu amabo tunapata kwenye chakula na kupeleka kuptia
mkojo
2. Kutengeza damu.
3. Kucontrol blood pressure
Maradhi ya figo.

Homa ya kutapika, kifua kubana, maji kuzidi mwilini, Kuhjarisha kufura kwa miguu, uso au
kifua na kupugua kwa damu hadi 3 na hupelekea figo kufanya kazi.

Lakini dalili hizi zimeganyika katika sehemu tano na kuna nyingine huwa ni zaidi kwa hatua
ya kwanza mpaka ya tatu huwezi kuona kwa macho. Lakini kwa hatua ya nne mpaka tano
huwa dalili zake huwa zakawaida sana kama kufura kwa uso, kifua au miguu. Kwa hatua ya
mwisho, mwili huwa unajaribu kujisaidia wenyewe hii itapelekea uso hutoa vitu ambavyo
huwa ni kama unga usoni.

Pia mkojo hutoka damu, povu kwa ajili ya kuwa na

Sababu

Umri wa mtu. Sana sana kuepelekea figo kufanya kazi ni mtu kufikisha miaka ya 45 na
kuendelea. Amabyo huchangia na mtindo wa maisha ambayo tunayoyaishi majumbani.

Kuwa na blood pressure kwa muda wa mrefu

Kunywa dawa za dukani hupelekea figo kushindwa kufanya kazi. Pia zile dawa za uchungu
sana kwa mda mrefu pia hata zile za parecetamol ukinywa kwa mrefu hupelekea figo
shindwa kufanya kazi.

Urithi,

Jitibu Magonjwa 300 Kwa Kutumia Mti wa Mlonge

July 24, 2016 3 comments

Mlonge au moringa oleifera kwa kiingereza umekuwa ukijulikana kama mti wa miujiza kwa
karne nyingi katika baadhi ya nchi za Afrika, Asia na katika nchi za Caribbean. Mti huu
umeripotiwa kutibu zaidi ya magonjwa 300 ikiwemo magonjwa mbalimbali sugu.

Karibu kila sehemu ya mti huu hutumika kama dawa. Majani ya mlonge yanaweza
kutafunwa mabichi, yaliyochemshwa kama mboga au yaliyokaushwa na kusagwa kuwa
unga. Unga wa mlonge unaweza kuhifadhiwa kwa miezi kadhaa bila kupoteza ubora na faida
zake za kiafya.
Mbegu za mlonge zimekuwa dili kubwa duniani kwa sasa, zinahitajika kwa kiasi kikubwa
katika nchi ya Marekani na China na kwa mujibu wa taarifa ni kuwa zinauzwa mpaka 45000
ya Tanzania kwa gramu 500. Walikuja pia wachina kuzinunua kwa wingi na walikuwepo
hapa bei ya mbegu za mlonge ilifika mpaka 11000 kwa kg kwa bei ya jumla yaani kwa
anayechukua kg 100 au 500 au 1000 na kwenda juu. Taarifa zisizo rasmi zinadai wachinja
hawa walikimbia nchini baada ya serikali kuanza kufuatilia na kuwakamata wakwepaji kodi
bandarini. Isingekuwa hivi mpaka leo mlonge ungekuwa umeshatowka wote Tanzania.

Faida za mlonge zimeandikwa na majarida ya afya na lishe kadhaa duniani. Kile ulikuwa
hujui ni kuwa viwanda na makampuni mengi ya dawa za hospitalini yamekuwa yakitumia
virutubishi vilivyomo kwenye mti huu kutengenezea madawa kwa ajioli ya binadamu na
wanyama.

Mlonge una:

Kalsiumu mara 17 zaidi ya ile ya maziwa ya ng’ombe

Potasiamu mara 15 zaidi ya ile ya kwenye ndizi

Una vitamini A mara 10 zaidi ya ile ya kwenye karoti

Una protini nyingi mara 9 zaidi ya ile ya kwenye mtindi

Una klorpfiti (kemikali ya rangi ya kijani ipatikanayo katika mimea) mara 4 zaidi ya ile ya
kwenye nyasi au majani ya ngano (wheatgrass)

Una madini chuma mara 25 zaidi ya yale ya kwenye Spinach


Una vitamini A mpaka Z

Una omega 3, 6 na 9

Una asidi amino zile muhimu zinazohitajika na mwili

Una kiasi cha kutosha cha madini ya zinc ambayo ni madini muhimu katika kuongeza
homoni za kiume na nguvu za kiume kwa ujumla

Mlonge ndicho chakula chenye afya zaidi juu ya ardhi:

Mlonge una jumla ya virutubishi 92, mmea au mti mwingine wenye virutubishi vingi basda
ya mlonge una virutubishi 28. Mlonge una vionsa suku 46 na viondoa uvimbe mbalimbali
mwilini 36, una asidi amino 18 na asidi amino muhimu zaidi 9 ambazo miili yetu haina
uwezo wa kuzitengeneza.

Unga wa majani ya mlonge unao uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 300 mwilini,
magonjwa hayo ni pamoja na :

1. HUko Afrika magharibi madaktari hutumia mlonge kutibu kisukari.

2. HUko India mlonge hutumika kutibu shinikizo la juu la damu

3. HUtibu matatizo u maumivu ya mishipa

4. Hutuliza mapigo ya juu ya moyo


5. Hutibu kansa

6. Pumu

7. Hutuliza wasiwasi

8. Kikohozi

9. Maumivu ya kichwa

10. Inazuia na kushusha ile lehemu hata ile ya juu zaidi

11. Inapunguza mafuta tumboni

12. Inaweza sawa homoni

13. Inatibu maumivu wakati wa hedhi

14. Unasafisha ini

15. Inasafisha mkojo na kibofu cha mkojo

16. Inarekebisha matatizo kwenye tezi

17. Unatibu kipindupindu na kuharisha


18. Kifua kikuu

19. Kichwa kizito

20. Uchovu

21. Mzio

22. Vidonda vya tumbo

23. Maambukizi kwenye ngozi

24. Maumivu mbalimbali mwilini

25. Huondoa madoa doa meusi kwenye ngozi

26. Husafisha damu

27. Hutibu matatizo kwenye koo

28. Huondoa makohozi mazito kooni

29. Huondoa taka na msongamano kifuani


30. Hutibu kipindipindu

31. Huondoa moto wa jicho au uvimbe kwenye jicho

32. Hutibu maambukizi kwenye macho na kwenye masikio

33. Unatibu homa

34. Maumivu kwenye maungio

35. Huondoa chunusi

36. Hutibu matatizo karibu yote ya ngozi na kinga ya mwili

37. Matatizo kwenye mfumo wa upumuaji

38. Inatibu kiseyeye

39. Huongeza uwingi wa mbegu za kiume na nguvu kwa ujumla

40. Inatibu minyoo

41. Huongeza maziwa kwa wingi kwa mama anayenyonyesha

42. Huondoa uvimbe kwenye utumbo mpana


43. Inatibu ugonjwa wa kuvimba mwili

44. Inatibu kuhara damu

45. Inatibu kisonono

46. Unatibu tatizo la kukosa usingizi

47. Unatibu homa ya manjano

48. Unatibu malaria

49. Unatibu U.T.I na matatizo mengine kwenye mfumo wa mkojo

50. Unasaidia pia kujenga na kuimarisha misuli

51. Unatibu magonjwa ya mifupa

Mlonge uansafisha mwili wako wote, unasafisha ini, figo, moyo, macho, unaimarisha meno,
ngozi na nywele. Wakati unatumia mlonge unakufanya ujisikie vizuri, ujisikie mpya na
mwenye nguvu. Watu wengi wanaotumia mlonge huwa ni wenye afya nzuri hata kwa
muonekano tu hata wanapokuwa na umri mkubwa zaidi ya miaka 90.

Majani ya mti wa mlonge pia yanaweza kutumika kutengeneza biogas. Hutumika pia kama
chakala cha wanyama kama sungura , mbuzi, ng’mbe. Mbwa n.k. Sungura wanaonekana
kupenda zaidi mlonge kuliko wanyama wote.
Bamia Hii Hii Unayoijua..Pambana na Magonjwa Yafuatayo kwa Kutumia Bamia..!!!

October 19, 2020 Afya, Makala ya Leo No comments

watu wengi tumekua hatutumii bamia either kwa radha yake au tu kasumba ya kuona Bamia
ni MBOGA ya walala hoi !!!.

Leo Naomba ufahama Bamia kama moja ya Mboga za majani ndio MBOGA yenye uwezo
wakusaidia afya zetu ,,,Bamia ina unatajiri wa nutrients mbali mbali ,, nutrients izo ni

1)- Calories - 30 calories

2)-Vitamin C- 21 Milligrams

3)-Carbohydrates - 7.6 Grams

4)-Fatty - 0.1 grams

5)-Magnesium - 16 milligrams

6)-Diatery Fibers - 3 grams .

Kutokana na kua nautajiri huo mkubwa,, Tafiti zimethibitisha kua BAMIA ni kiboko ya
Magonjwa yafuayo

- Diabetes ( kisukari)

-Asthima ( inayoanza na iliyokwisha kuathiri)

-Cholesterol

-Kidney Disease (Magonjwa ya figo)

Ulcers (Vidonda vya tumbo ).

-Mimba ,,husaidia mtoto kukua akiwa na Afya njema na aliyekamilika .


-Anemia

-Matatizo ya kutoona Vizuri .

-Pia Bamia huongeza nguvu ktk mfumo wa mwili wa kinga ktk kupambana na magonjwa .

- Kuondoa Maumivu wakati wakutoa haja kubwa

-Kuimarisha Mifupa lege lege .

NAMENGINEYO MENGI AMBAYO SIJAYAANDIKA ,, .

Watu wazaman walifanikiwa kuishi miaka mingi kwa kutumia vitu km ivi...

FAHAMU Njia 16 za Kuondoa Sumu Mbalimbali Mwilini...!!!

October 19, 2020 Afya, Makala ya Leo No comments

Mwili unaweza kupatwa na sumu au takataka zisizohitajika na mwili kwa namna mbili, ama
kupitia mazingira tunayoishi (viwanda, migodi nk) au kupitia vyakula na vinywaji ambavyo
tunatumia kila siku. Sumu au taka pia zinaweza kuingia mwilini kupitia dawa mbalimbali
hasa za kizungu tunazotumia kujitibia magonjwa mbalimbali.

Mwili huzalisha hizi sumu au takataka (free radicals) kila mara kunapofanyika mmeng’enyo
wa chakula mwilini mwako.

Njia 16 za kuondoa sumu mbalimbali mwilini

1. Fanya mlo wako mmoja wa siku kuwa ni matunda pekee


Amua moja ya mlo wako kwa siku uwe ni matunda pekee bila chakula kingine zaidi.
Unaweza kuamua ama chakula cha asubuhi au cha jioni kuwa ni matunda pekee, ndiyo
kwenye sahani yako unajaza matunda tu mbalimbali sahani ijae na ule hayo tu kama ndiyo
mlo wako ukimaliza unaweza kunywa juisi ya matunda au maji pekee.

2. Kula vyakula vya asili zaidi kuliko vya viwandani

Kama unataka kuepuka sumu au takataka nyingine kirahisi kuingia katika mwili wako basi
pendelea zaidi kula vyakula vya asili vinavyopikwa nyumbani kuliko kula vya kwenye
makopo au vya dukani au vya kwenye migahawa (fast foods).

3. Fanya masaji

Kwa bahati mbaya waTanzania wengi hawajuwi kuwa masaji ni sehemu ya tiba au ni dawa
pia kwa magonjwa mengine mengi mwilini. Wengi tunaichukulia masaji kama kitu cha
starehe tu (relaxation) lakini unaweza kutumia masaji kama njia mojawapo ya kuondoa sumu
mwilini na utafanikiwa kwa muda mfupi sana.

4. Kunywa maji mengi kila siku

Sababu kubwa ya watu wengi kutengeneza sumu au taka mwilini mwao ni kutokunywa maji
mengi kila siku. Maji ni uhai, bila kunywa maji mengi kila siku ni sawa na kwenda dukani
bila hela mfukoni. Haijalishi upo mazingira gani kama ni ya baridi au ni ya joto ni LAZIMA
UNYWE MAJI YA KUTOSHA KILA SIKU IENDAYO KWA MUNGU.

Unahitaji maji glasi 8 mpaka 10 kila siku. Watu wengi wanahangaika namna ya kuondoa
sumu kusafisha miili yao bila kujua kuwa maji pekee ya kunywa yanatosha kwa kazi hiyo.
Kumbuka asilimia 94 ya damu yako ni maji, asilimia 85 za ubongo wako ni maji, hivyo ili
kusafisha damu na mwili kwa ujumla ni lazima unywe maji ya kutosha kila siku.
5. Acha chai ya rangi na Kahawa

Kama tayari imethibitika una sumu au takataka nyingi mwilini nakushauri uache kunywa
chai ya rangi na kahawa. Badala yake hamia kutumia chai yenye tangawizi au mdalasini au
mchaichai. Chai ya rangi na kahawa vina kaffeina ambayo kwanza huyasukuma maji nje ya
mwili kwa haraka na kuuacha mwili bila kuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya kazi zake.
Kaffeina pia ni madawa ya kulevya kundi la madawa yanayosisimua mwili (stimulants
drugs).

6. Fanya mazoezi ya viungo

Inashangaza sana kuona waTanzania wengi hawaoni umhimu wa kufanya mazoezi ya


viungo. Mazoezi ya viungo ni jambo la lazima kama ilivyo chakula. Iwe unaumwa au
huumwi, iwe una uzito kuzidi au una uzito wa kawaida hakikisha unapata muda wa kufanya
mazoezi.

Mazoezi yanakusaidia kukufanya ujisikie vizuri na hivyo kukuondolea mfadhaiko au stress


kirahisi zaidi, sambamba na hilo mazoezi ni dawa tosha na nzuri ya kuondoa sumu mwilini
haraka zaidi. Hakikisha jasho linakutoka la kutosha na iwe ni jambo la kila mara na siyo
unaenda jumamosi na jumapili (weekend) tu, hiyo haitoshi, fanya mazoezi mara 4 mpaka
mara 5 kwa wiki.

7. Kula zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi (faiba)

Umesikia mara nyingi kwamba unahitaji kula zaidi vyakula vyenye nyuzinyuzi kwa ajili ya
kuwa na afya bora, mmeng’enyo wa chakula wenye afya na hata kukusaidia kupunguza
uzito. Kile ulikuwa hujuwi pengine mpaka sasa ni kuwa vyakula hivi vyenye nyuzinyuzi ni
vizuri pia katika kusafisha mwili na kuondoa sumu au takataka mbalimbali.

Vyakula vyenye nyuzinyuzi nyingi ni pamoja na parachichi, ndizi, peazi, karoti, pilipili hoho,
mchele wa brown (ule wanashauriwa watu wa kisukari wautumie), maharage meusi, njegele,
tende, viazi vitamu, tufaa (apple), machungwa, ugali wa dona pia mkate wa unga wa ngano
ambao haujakobolewa.

8. Funga kula

Ndiyo, kama ulikuwa hujuwi namna nyingine rahisi ya kuondoa au kupunguza sumu mwilini
ni kufunga kula kabisa kutwa nzima. Ukifunga kula mwili unalazimika kuvitumia vile
vilivyomo ndani yake bila kushughulika kuvisaga vingine vipya unavyokula. Kunapokuwa
hakuna shughuli ya kuvisaga na kumeng’enya chakula kipya mwilini ndipo mwili unaweza
kuondoa sumu na taka nyingine kirahisi zaidi.

Amua kufunga kula kabisa kwa wiki mara 2 hata 3 ili kuondoa au kupunguza sumu, hii
inaweza kuwa pia ni njia mojawapo ya kufanya maombi na kujiweka karibu na muumba
wako.

9. Pata usingizi wa kutosha kila siku

Moja ya vitu vinaweza kukupelekea kuwa na sumu mwilini au takataka nyingi ni pamoja na
kutokulala muda wa kutosha kila siku. Usingizi haukopwi na huwezi kuwa na ufanisi katika
kazi zako kama hupati usingizi wa kutosha kila siku.

Usingizi siyo jambo la starehe tu, ni sehemu mhimu sana katika afya yako ya kila siku. Bila
kupata usingizi wa kutosha unaweza kuwa karibu na matatizo kama kuongezeka uzito,
kushuka kwa kinga ya mwili na nguvu zako za mwili kwa zinaweza kushuka.

Unapopata muda wa kutosha wa kulala masaa 7 mpaka 8 kwa siku unaupa mwili wako nafasi
ya kutosha ya kupumzika na kujiripea upya na hivyo ndivyo sumu na takataka nyingine
zinavyoweza kukutoka kirahisi. Ingia kulala mapema walau saa tatu usiku ingia kulala siyo
unakaa unaangalia tamthiliya au mpira mpaka saa sita za usiku!
10. Epuka mazingira hatarishi kwa sumu

Kuna mazingira yanajulikana wazi kuwa ni vyanzo vya sumu mwilini. Maeneo ya migodi ya
madini, maeneo yenye viwanda vingi, maduka yanayouza dawa za kilimo nk

Maeneo haya yanafaa kukaa mbali na makazi ya binadamu kwa usalama wa afya zetu.

11. Tumia mtindi

Moja ya njia nyingine ya kuondoa sumu na takataka nyingine ni kutumia vyakula vyenye
bakteria wazuri (probiotics). Mtindi ndicho chakula pekee kinajulikana kuwa na bakteria
hawa wazuri kwa ajili ya tumbo lako. Pata mtindi kikombe kimoja kila siku na utabaki na
mwili msafi muda wote. TUmia mtindi wa nyumbani ndiyo mzuri zaidi ingawa hata wa
dukani nakuruhusu utumie hasa ule ambao haujaongezwa kingine chochote ndani yake
(flavors and additives).

12. Epuka vyakula vilivyokobolewa

Ili kuwa na mwili msafi kabisa epuka kula mkate mweupe, sukari na vyakula vinavyopikwa
katikati ya mafuta mengi kama vile chipsi, maandazi na vingine vyote vinavyochomwa
katikati ya mafuta mengi.

Mkate upo mkate mweusi (brown bread), sukari ipo asali mbichi, vyakula vinavyopikwa
katikati ya mafuta mengi unaweza kuamua kuwa unavioka (bake) au uvichemshe (boiling).
Uchaguzi ni wako.

13. Ondoa mfadhaiko (stress)


Kile tayari unajuwa ni kuwa mfadhaiko au stress ni jambo baya kwa afya yako. Kile
unatakiwa kujua kuanzia sasa ni kuwa ili kubaki na afya bora kabisa yenye TBS basi ukae
mbali na stress. Kama utaruhusu stress kutawala maisha yako basi ujuwe mwili wako
hauwezi kufanya kazi zake vizuri ikiwemo ya kuondoa taka au sumu mbalimbali mwilini.

Stress peke yake inaweza kupelekea magonjwa mbalimbali mwilini zaidi ya 50. Unapokuwa
na mfadhaiko mwili wako hauwezi kutoa taka nje kirahisi na kinga yako ya mwili inashuka
matokeo yake unakuwa karibu na magonjwa mengine mengi.

Watu wengine wenye uelewa mdogo wakiwa na stress hukimbilia kutumia vilevi wakidhani
zitapungua kumbe ndiyo wanazidi kuongeza tatizo bila kujua. Vitu viwili vinaondoa stress
bila kulazimika kutumia njia mbaya kwa afya yako ni mazoezi ya viungo na tendo la ndoa.
Siku nyingine ukijiona umefadhaishwa sana nenda kafanye mazoezi ya kufa mtu
ikiwezekana baadaye tafuta mtu shiriki tendo la ndoa.

14. Tumia dawa za asili badala ya zile za kizungu

Dawa nyingi za hospitali huwa zina matokeo chanya (positive) na matokeo hasi (negative)
pia ambayo ndiyo matokeo mabaya. Kama unalazimika kutumia antibiotic kila mara au
unameza dawa za kuondoa maumivu kila mara unaweza kuwa unaongeza sumu na taka
mwilini bila kujua na bila sababu yoyote ya lazima.

Kuepuka hilo jaribu kutumia mitishamba au mimea ya asili kwa baadhi ya magonjwa
ambayo si lazima uende hospitali. Siyo mafua tu mtu ameenda kuchoma sindano!

15. Acha vilevi

Moja ya vitu vinavyoweza kuleta sumu au taka mwilini moja kwa moja ni vilevi. Vilevi
kama pombe, madawa ya kulevya, sigara, bangi na vinginevyo ni vitu vinavyopelekea mwili
kuwa na taka moja kwa moja.
Namna pekee ya kuondoa sumu kutokana na vilevi ni kuviacha hivyo vilevi, ndiyo kuviacha.
Usitegemee asubuhi utumie dawa kuondoa sumu mwilini halafu jioni ukanywe pombe au
ukavute sigara utegemee tu ile dawa uliyotumia asubuhi kwamba itafanya kazi, hapana
unajidanganya, dawa ni kuacha vilevi moja kwa moja.

Vingine vya kuacha kama tayari imegundulika una sumu nyingi mwilini ni pamoja na
vinywaji baridi vyote, juisi zote za dukani, chai ya rangi na kahawa.

16. Tumia vifuatavyo kuondoa sumu zaidi

Vifuatavyo vinaondoa sumu kirahisi zaidi mwilini; kitunguu swaumu, unga wa majani ya
mlonge na mbegu zake na mbegu za maboga au unga wake. Kitunguu swaumu Mlonge
Mbegu za maboga.

IFAHAMU Kazi ya Ganda la Chungwa Kwenye Mwili Wako..!!!

October 07, 2020 Afya, Makala ya Leo No comments

Baadhi ya watu wamekuwa wakisumbuliwa na weusi sehemu za makwapa, hali ambayo


huwakwaza hasa zaidia kinadada na kujikuta wakishindwa kuvaa baadhi ya mavazi hasa yale
yenye mikono mifupi kwa kuhofia hali hiyo.

Leo nimekuletea hii mbinu ya kutumia ganda la chungwa kumaliza weusi wa sehemu za
kwapani.

Unachotakiwa kufanya ni kukamua maji ya ganda la chungwa (yale ambayo yakiingia


machoni huuma) weka maji hayo kwenye kikombe kisha changanya na asali kijiko kimoja
kidogo kisha paka mchanganyiko huo sehemu iliyoathirika. Fanya zoezi hili kwa wiki mbili
ili kupata matokeo mazuri.

Matumizi ya Limao Kusafisha Uke ni Hatari Kiafya

October 06, 2020 Afya No comments


Kwa mujibu wa Dkt. Fatima Abdulahi, Daktari Bingwa wa Wanawake katika Hospitali ya
Marie Stopes mjini Abuja amesema, kisayansi kila kiungo katika mwili wa binadamu kina
kemikali kama vile Tindikali na Alkalini kwa kiwango kinachohitajika mwilini

Maji ya limao yanasadikiwa kuwa na kiwango cha juu cha Tindikali ambacho ni cha pili kwa
ukubwa cha 14/1/14, wakati uke wa mwanamke una kiwango cha kati ya 3.8 / 14 na 4.5 / 14
cha Tindikali

Kuna baadhi ya wanawake wanaodaiwa kutumia Limao kujisafisha lakini wataalamu


wanasema ni hatari kufanya hivyo kwasababu maji ya limao yana ukakasi wa hali ya juu
ambao unabadilisha mfumo wa asilia ya uke

Matumizi ya ndimu kusafisha uke yanaweza kusababisha kusambaa kwa magonjwa katika
eneo hilo ikiwemo kuathiri shingo ya uzazi hali ambayo inaweza kusababisha Saratani ya
Shingo ya kizazi

Wanasayansi wanashauri uangalifu uzingatiwe wakati wa kujisafisha ili kujiepusha kupata


michumbuko ambayo hupelekea mwanamke kupata maradhi.

Zifahamu Faida 6 za Juisi ya Tangawizi, Halafu Nenda Kajaribu Uone Ajabu Yake..!!!

September 30, 2020 Afya, Makala ya Leo No comments

Tangawizi ni kati ya viungo mahili vinavyochochea ladha nzuri katika vyakula vya aina
mbalimbali na hivyo kuwavutia walaji kula chakula husika.
Tangawizi pia inapowekwa kwenye vyakula vigumu kama nyama huifanya ilainike na hivyo
kuweza kuiva kwa haraka zaidi.

Leo nataka kukueleza msomaji wangu kuhusu hizi faida nyingine za kutumia juisi ya
tangawizi kama ifuatavyo:-

1. Hutumika kama kituliza maumivu.

2. Husaidia kuboresha mmeng'enyo wa chakula tumboni

3. Huthibiti shinikizo la damu

4. Huboresha afya ya kinywa

5. Hukinga matatizo ya ngozi hasa chunusi

7. Husaidia kukuza nywele (kulinda afya ya nywele).

Utafiti: Usile Chakula Usiku Baada ya Saa Mbili, Mwisho Saa Kumi na Moja Jioni

September 11, 2020 Afya No comments

Tafiti mbalimbali zimekuwa zikitoka kila siku, hivi karibuni umetoka utafiti mpya ukieleza
kwamba kuna hatari kubwa kwa mtu akila chakula kigumu usiku kwanzia saa mbili usiku.

Mtu anaweza kupata mshutuko wa moyo,shinikizo la damu ama strock.

Je Ushawahi Kufahamu Kuwa Mende Ni Lishe Bora Kwako?


September 11, 2020 Afya 1 comment

Je Ushawahi Kufahamu Kuwa Mende Ni Lishe Bora Kwako?

Je umewahi kufikiria kuwa mdudu mende anaweza kuwa mtaji wa kibiashara?

Ingawa jamii inawachukulia mende kama wadudu wachafu, Rwehura Daniel ni kijana wa
kitanzania, ameweza kutumia ubunifu wake na kuanza kufuga na kuwauza mende, ambao
wataalamu wa lishe wanasema kwamba wadudu hao wana kiwango kikubwa cha protein ambayo
ni muhimu kwa binadamu na wanyama.

Jinsi ya Kuongeza Uzito au Unene Bila Kudhuru Mwili Wako

September 11, 2020 Afya No comments

Jinsi ya Kuongeza Uzito au Unene Bila Kudhuru Mwili Wako

Kuna wakati mtu unajiona wazi kuwa uzito wako upo chini na pengine ungehitaji ungeongezeka
kidogo uzito na unene wako kwa ujumla.

Tuachane na wale wanaotaka kuongeza sehemu za kukalia na mapaja kwanza, nitaleta dawa kwa
ajili hiyo siku nyingine. Nazungumzia mtu anayetaka kuongezeka uzito na unene wa mwili kwa
ujumla.

Hivyo kama shida yako ni namna gani unaweza kuongeza uzito na unene wa mwili wako bila
madhara yoyote mabaya basi soma pole pole mpaka mwisho hii makala.

Hii makala pia ni msaada kwa wale wanaotaka kuongeza misuli ya miili yao na kuonekana
wenye kupendeza zaidi.

Nini maana ya kuwa na uzito pungufu?

Kuwa na uzito pungufu ni kuwa na BMI (Body Mass Index) chini ya 18.5. Huu ni uzito ambao
mwili hauwezi kuhimili kuwa na afya nzuri.
Wakati kuwa na BMI ya zaidi ya 25 ni uzito ulio juu na zaidi ya 30 ni uzito uliozidi zaidi au
unaweza kusema ni utipwatipwa.

BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita. Mfano mimi
nina uzito wa kg 80 na urefu wa mita 1.84 ili kupata BMI yangu nazidisha 1.84 mara 1.84 =
3.3856 kisha nagawa na uzito wangu, hivyo kg 80/3.3856 unapata BMI ya 23.62 ambayo ni ya
kawaida (normal).

Hata hivyo kuna udhaifu juu ya mzani wa BMI kwakuwa wenyewe unaangalia tu uwiano wa
uzito na urefu bila kuangalia uwingi wa misuli mtu anaweza kuwa nayo.

Baadhi ya watu ni wembamba sana na bado wana afya nzuri tu. Kuwa na uzito pungufu kwa
mjibu wa BMI siyo lazima mara zote imaanishe una afya mbovu.

Kuwa na uzito pungufu ni jambo la kawaida sana kwa wasichana na wanawake.

Nini madhara ya kuwa na uzito pungufu?

Kuwa na uzito pungufu inaweza kuwa ni jambo baya kwa afya yako kama ilivyo kwakuwa na
uzito uliozidi.

Kwa mjibu wa utafiti mmoja, kuwa na uzito pungufu kulihusishwa na hatari ya zaidi ya asilimia
140 ya vifo vya ujanani kwa wanaume na asilimia 100 kwa wanawake.

Katika utafiti huu kuwa na uzito uliozidi kulihusianishwa na asilimia 50 tu ya vifo vya mapema,
hii inamaanisha kuwa na uzito pungufu ni hatari zaidi kwa afya yako kuliko kuwa na uzito
mkubwa.
Utafiti mwingine ulionyesha kuwa na ongezeko la hatari ya vifo vya mapema kwa wanaume
zaidi walio na uzito pungufu na siyo kwa wanawake, hii inaonyesha kuwa chini ya uzito pungufu
ni hatari zaidi kwa wanaume kuliko kwa wanawake.

Kuwa na uzito pungufu pia kunaweza kuwa sababu ya kushuka kwa kinga ya mwili, kuongezeka
kwa maambukizi, magonjwa ya mifupa na mipasuko ya mifupa, na kusababisha matatizo ya
ugumba na uzazi kwa ujumla.

Watu wenye uzito pungufu pia wanaweza kupatwa na tatizo la kupotelewa na mishipa na kuwa
na hatari kubwa ya kupatwa na ukichaa.

Kinachosababisha mtu kuwa na uzito pungufu

Zipo sababu nyingi zinazoweza kupelekea ukapungua uzito.

Hizi ni mojawapo ya sababu hizo:

Matatizo kwenye tezi ya Thyroid: Ikitokea tezi hii inafanya kazi sana kuliko kawaida basi
kunatokea mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi sana kuliko kawaida na matokeo
yake ni kupungua kwa uzito.

Kisukari: Hasa kisukari aina ya kwanza

Maambukizi: ya magonjwa kama kifua kikuu nk

Kushuka kwa kinga ya mwili

Saratani

Kupoteza hamu ya kula


Ikiwa unajiona una uzito pungufu ni vizuri kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi ili kubaini
nini inaweza kuwa ndiyo sababu hasa ya tatizo kwa upande wako.

Ni mhimu kuonana na daktari ana kwa ana hasa kama imekutokea kushuka uzito wako kwa
ghafla kwa kiasi kikubwa bila kuwa umefanya lolote la kupunguza uzito.

Jinsi ya kuongeza uzito au unene bila kudhuru mwili wako

Kama unataka kuongeza uzito na unene basi ni mhimu kwamba unafanya jambo hili kwa njia
salama ambazo hazitakuletea madhara baadaye.

Kunywa soda, kula maandazi au chipsi za vibandani ni vitu vinaweza kukuongezea uzito na
unene kwa haraka lakini wakati huo huo vinaweza kuharibu afya yako.

Kama uzito wako upo chini ni mhimu kuzingatia umhimu wa kuongeza uzito sambamba na
misuli na siyo kuongezeka uzito pamoja na tumbo au kitambi.

Wapo watu wengi tu wenye uzito sawa na bado wanaugua kisukari aina ya pili, ugonjwa wa
moyo na matatizo mengine ya kiafya yanayohusiana na uzito kuwa juu.

Hivyo ni mhimu kwamba bado unaendelea kula vyakula vyenye afya na kuishi maisha yenye
afya kila siku.

Tuangalie sasa njia za kuongeza uzito na unene kwa haraka bila kuharibu afya yako:

1. Kula zaidi
Jambo la mhimu unaloweza kulifanya ili kuongeza uzito ni kula zaidi ya unavyohitaji mwili
wako. Bila hivi ni vigumu kuongezeka uzito.

Kama ulikuwa unakula mara 2 au 3 kwa siku sasa anza kula mpaka mara 5 kwa siku. Muda wote
tumbo liwe limejaa. Siyo kiasi cha kuwa kero lakini kuwa makini.

2. Kula zaidi vyakula vyenye protini

Lishe moja mhimu zaidi katika kuongeza uzito ni ile yenye protini kwa wingi ndani yake.

Mishipa inatengenezwa na protini na bila kuwa na protini ya kutosha sehemu kubwa ya nishati
ya mwili huishia kuwa mafuta.

Tafiti zinaonyesha kuwa wakati unaongeza kiasi cha chakula unachokula, lishe yenye protini
nyingi kile kiasi kinachozidi huweza kubadilishwa na kuwa misuli ya mwili.

Hata hivyo elewa hili tena, chakula chohcote chenye protini nyingi huwa na uwezo wa
kukupunguzia njaa au hamu ya kutaka kula chakula.

Hili linaweza kukuletea shida tena kuendelea kula zaidi kama moja ya mahitaji mhimu ili
kuongeza uzito na unene kwa ujumla.

Hivyo wakati ukiendelea na lishe yenye protini ni mhimu pia kuongeza mbinu za kuongeza njaa
ili uendelee kula zaidi.
Vyakula vyenye protini kwa wingi vinajumuisha nyama, maharage, mayai (mayai ya kienyeji)
maziwa freshi, karanga, mbegu za maboga (kama unahitaji mbegu za maboga zilizokaangwa
tayari kwa matumizi niachie ujumbe WhatsApp +255769142586), samaki, korosho nk.

Hivyo protini ni mhimu ili kutengeneza misuli na mishipa kwa ujumla, kula protini ya kutosha ni
mhimu ili kuongezeka uzito unaobaki kama misuli na siyo mafuta.

3. Kula zaidi wanga na mafuta

Kula kwa wingi vyakula vyenye wanga na mafuta kama shida yako ni kuongezeka uzito na
unene. Ni vizuri katika mlo ule vya kutosha vyakula vyenye wanga, mafuta na protini kwa
matokeo mazuri zaidi.

Vyakula vyenye wanga kwa wingi ni pamoja na viazi vitamu, ugali wa dona, wali, mkate,
chapati, maandazi, tambi (pasta), maembe, viazi mviringo (chipsi), ndizi, tende, pizza, nk.

Mafuta mazuri yanapatikana katika parachichi na mafuta yake, mafuta ya zeituni, siagi ya
karanga, mayai, mafuta ya samaki, mafuta ya nazi, mafuta ya mawese, ufuta na mafuta yake nk

Hakikisha unakula mara 3 mpaka 5 kila siku mlo wa aina hii.

4. Kula vyakula vyenye nguvu zaidi

Ugali wa dona
Ni mhimu tena kula vyakula vya asili zaidi na vyenye nguvu zaidi. Kama ni ugali kula ugali wa
dona na si sembe, kama ni mkate kula mkate wa unga wa ngano ambayo haijakobolewa.

Kwa kifupi tu usile vyakula vilivyokobolewa au vya madukani kama unataka kuongezeka uzito
na unene kwa njia salama kwa afya yako.

Pia ongeza viungo zaidi kwenye hivyo vyakula ili kuongeza hamu ya kutaka kula zaidi. Ongeza
iliki au mdalasini na viungo vingine vitakavyokufanya upende kula zaidi hicho chakula.

Kula zaidi vyakula hivi kwa kupata nguvu zaidi; lozi, jozi, korosho, karanga, tende, zabibu kavu,
maziwa freshi, mtindi, mafuta ya zeituni, parachichi, nyama ya kuku wa kienyeji, nyama ya
ng’ombe, nyama ya nguruwe, nyama ya mbuzi, viazi, viazi vitamu, siagi ya karanga nk

Vingi ya hivi vyakula vina kawaida ya kukupotezea njaa na hamu ya kula hivyo itakulazimu
wakati mwingine kujilazimisha tu ili ule zaidi kwa siku.

Pia siyo wazo zuri kula sana mboga za majani kama shida yako ni kuongeza uzito hii ni kwa
sababu zitaziba nafasi inayohitajika kukaliwa na vyakula hivi vyenye nguvu zaidi. Pia matunda
iwe kidogo labda tunda moja tu hasa parachichi au ndizi moja tu basi.

5. Nyanyua vitu vizito

Ili kujihakikishia kuwa hicho kiasi cha chakula ulichoongeza kula kinakwenda kwenye misuli na
si kukuletea mafuta na pengine tumbo au kitambi ni mhimu ufanye mazoezi ya kunyanyua vitu
vizito.
Nenda gym na unyanyuwe vyuma mara 3 mpaka 4 kwa wiki, anza na uzito mdogo na uongeze
uzito kidogo kidogo kadri unavyoendelea.

Kama shepu yako ipo nje kabisa yaani haieleweki ni vizuri ukafanya mazoezi hayo ukiwa na
mwalimu wa kukuelekeza kwa matokeo mazuri zaidi.

Ni vizuri pia kuonana na daktari kama una tatizo lolote la uti wa mgongo au mifupa kwa ujumla
kwa ushauri mzuri zaidi kabla hujaanza mazoezi haya.

Mambo mengine 10 mhimu zaidi

Pamoja na mbinu tano hizo hapo juu, ni mhimu kuzingatia yafuatayo kwa matokeo mazuri zaidi
na ya haraka:

1. Usinywe maji kabla ya chakula. Kunywa maji kabla ya kula kutafanya tumbo lako liwe
limejaa na hivyo kuziba nafasi ya chakula ambacho ndiyo mhimu kwa ajili ya kalori
zinazohitajika ili uongezeke.

2. Pata usingizi wa kutosha kila siku. Kupata usingizi wa kutosha na mtulivu kila siku ni mhimu
ili uweze kunenepa na kuongeza uzito na kukua kwa misuli, tena ukiweza lala nyakati za mchana
masaa mawili.

3. Kula mboga za majani mwishoni. Kama unapokula utakuwa na mboga za majani pia basi hizi
ule mwishoni baada ya kuwa umekula protini, wanga na mafuta na hii inaenda pia kwa matunda.

4. Acha sigara. Wavutaji wengi huwa na uzito pungufu, acha kuvuta sigara pia bangi na tumbaku
yoyote. Mara nyingi ukiacha tu kuvuta utaona afya yako inaimarika na kuongezeka sana
5. Ridhika. Kama unataka kunenepa na kuongezeka uzito basi uwe mtu wa kuridhika.

Nikuambie tu maisha ndiyo haya haya na furaha ya kweli haipo kwenye mali, usisubiri mpaka
uwe tajiri ndiyo uwe na furaha, kila siku ukiamka salama shukuru Mungu ni neema tu na zawadi
umeamka salama.

Kumbuka tulikuja watupu na hakuna tutakachoondoka nacho.

Kuongezeka uzito linaweza kuwa siyo jambo rahisi kwa wengine

Hii inaweza kuwa ni kwa sababu baadhi ya watu miili yao inaweza kuwa imejiwekea kikomo
fulani cha uzito wa kuubeba ambapo hujisikia vizuri zaidi katika uzito huo kuliko zaidi.

Utakapojaribu kwenda juu au chini kidogo ya kiwango hicho cha uzito ambao mwili wako
umejiamulia utaona tu njaa yako inapunguzwa au kuongezwa pia mfumo wako wa mmeng’enyo
wa chakula nao utawekwa sawa ili kusiwepo na kuongezeka wala kupungua kwa mwili wako.

Utakapojaribu kula zaidi tegemea mwili wako kukupunguzia hamu ya kutaka kula na kuongeza
nguvu katika mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, hili hufanywa na ubongo wenyewe
ukisaidiwa na homoni ijulikanayo kama ‘leptin’.

Kwahiyo tegemea kazi hii kuwa siyo rahisi kwa baadhi ya watu na hivyo ni mhimu kujilazimisha
zaidi ili kufikia lengo lako.

Mwisho wa siku jambo hili linahitaji muda na siyo jambo la siku 2 au 3 hata hivyo ukiwa na nia
hakuna linaloshindikana.
Ukitaka kuwa mwanaume wa shoka, epuka kula vyakula hivi

September 11, 2020 Afya No comments

Katika makala hii hii utajifunza vyakula mbalimbali ambavyo wanaume hawatakiwi kula ili
kubaki na afya bora wakati wote. Kuna vingine unaweza kuwa unavitumia kila siku bila
mwenyewe kujuwa.

Punguza kula vyakula feki kuzuia kupoteza nywele

Moja ya matatizo makubwa upande wa urembo kwa wanaume ni kupoteza nywele (upala).
Lakini kama unatafuta kitu cha kukilaumu dhidi ya tatizo lako la kunyonyoka nywele basi ni
hiyo sahani yako ya chipsi unayokula kila siku. Vyakula feki (junk foods) ni hivyo vinapatikana
kwenye fast foods na takeaway centers nyingi hasa mijini kadharika vyakula vile vyote vya
kwenye maboksi.

Vyakula hivi feki vina kiasi kingi mno cha lehemu (cholesterol) na lehemu hii hupelekea kile
huitwa kwa kitaalamu kama ‘pregnenolone’ na kupelekea kiasi kikubwa cha
‘dihydrotestosterone’ (DHT) na hatimaye kupotea kwa nywele kichwani a.k.a upara.

Kunyonyoka kwa nywele kunaweza kuwa ni jambo la kurithi (genetics) lakini vile vile aina ya
chakula unachokula kinaweza kuwa kinahusika moja kwa moja.

Punguza kunywa pombe

Wanaume wengi wanaokunywa bia kupita kiasi huwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na
tatizo la kuota matiti kama wamama tatizo lijulikanalo kwa kitaalamu kama ‘gynecomastia’.

Kwenye bia au pombe mara nyingi hakuna lishe ya moja kwa moja na hivyo hukufanya ujisikie
njaa au hata kuongzeka kwa njaa zaidi na ndiyo sababu unaambiwa kama huna uhakika utakula
wapi ni bora usinywe pombe ili kulinda afya yako.
Kwenye bia kuna kitu kama homoni ya oestrogen ya kupandikizwa na hivyo unywaji pombe
kupita kiasi kuna uhusiano wa moja kwa moja na matokeo ya wanaume kuwa na matiti kama
wanawake.

Acha kutumia mafuta ya mboga mboga kuepuka saratani ya tezi dume

Mafuta yatokanayo na mboga mboga au mimea yamekuwa yakipigiwa debe kwa miaka mingi na
watu wanaojihusisha na lishe na wale wenye hasira sana na mafuta yatokanayo na wanyama.
Hata hivyo leo nakujulisha mafuta hayo si salama sana kutumika na mwanaume kila siku. Hili
limekuja hasa kutokana na kuongezeka kwa magonjwa ya moyo na lehemu na watu
walazishwawa kutumia mafuta ya namna hiyo.

Lakini mafuta haya ya mboga mboga ndiyo kitu kibovu kabisa unatakiwa kukiepuka ili usipatwe
na saratani ya tezi dume. Linapokuja suala la kujilinda saratani ya tezi dume basi mafuta yenye
omega 3 ndiyo suluhisho la kudumu na siyo omega 6 kama ilivyo kwenye vyakula vingi vya
kwenye makopo, mafuta ya alizeti, maharage ya soya, mafuta ya canola na mafuta ya corn na
mengine yote yenye omega 6.

Popcorn

Popcorn au bisi ni chakula kingine mwanaume hatakiwi kula, hupikwa kwa kutumia mafuta
yasiyo na afya, sodiamu nyingi na ni chanzo cha baadhi ya kansa. Kuna kitu kinaitwa ‘Diacetyl’
kinachopatikana kwenye popcorn ambacho kinahusika na kusababisha kansa na kuna kingine
kiitwacho ‘Perfluorochemicals’ ambacho huathiri tezi ya thyroid na ugonjwa wakati huo huo
husababisha ugonjwa wa kupungukiwa umakini ujulikanao kwa kiingereza kama ‘Attention-
deficit/hyperactivity disorder (ADHD)‘.Ni vizuri kuacha kula popcorn.

Mkate mweupe

Mkate mweupe una wanga mwingi zaidi usio na faida. Kwenye hatua za kutengeneza mkate
mweupe vitamini zote za kundi B hupotea, hupotea pia nyuzinyuzi (fiber). Siyo hivyo tu mkate
mweupe umesemekana kuwa ni sababu ya ugonjwa wa kisukari na kuongeza uzito zaidi mwilini
wakati huo huo ukisababisha tatizo la kufunga choo au kupata choo kigumu sana.
Vingine vinavyofanana na na hilo ni ugali wa sembe, tambi nyeupe, chai ya rangi na kahawa.
Kula mkate ambao ngano yake haikukobolewa (brown bread), kula ugali wa dona na chai
unaweza kutumia tangawizi au mdalasini badala ya majani ya chai.

Chumvi ya mezani

Chumvi ya mezani ile ya unga nyeupe haifai kwa mwanaume. Kila mmoja amesikia chumvi hii
husababisha shinikizo la juu la damu na pamoja na hayo bado sehemu kubwa ya watu wanatumia
chumvi hii.

Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini, madini na hupitishwa katika joto la nyuzi
joto. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha
kemikali kama vile ‘aluminium silicate’ huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki
katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu.
Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu
(Alzheimer).

Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijapita kiwandani (unrefined sea salt) ndiyo nzuri
zaidi kwa afya ya mwanaume.

Faida saba(7) zitokanazo na juisi ya ukwaju

September 11, 2020 Afya No comments

Juisi ya ukwaju ina umuhumi sana katika miili yetu, pia tunda la ukwaju ni tunda lenye faida
nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Tunda hili huweza kutumika kutengeneza juisi ambayo
matumizi yake yana faida kubwa sana katika afya ya mwili wa mwanadamu.

Zifuatazo ndizo faida zitokanazo na juisi ya ukwaju;

1. Chanzo kizuri cha viuasumu mwilini ‘antioxidants’ ambavyo huzuia Saratani (cancer) kwa
mtumiaji
2. Chanzo cha Vitamini B na C vile vile “carotentes”

3. Hushusha joto la mwili na kuondosha homa, hasa homa ya malaria na homa ya matumbo

4. Huulinda mwili dhidi ya mafua na kero za mafua kooni

5. Husaidia myeyusho na mmengenyo wa chakula na kuondosha kuvimbiwa

6. Husaidia kutibu matatizo ya nyongo (bile disorders)

7. Husaidia kurahisisha choo (laxative)

8.Husaidia kupunguza wingi wa lehemu (cholesterol) na hivyo kuimarisha moyo

9.Husaidia ngozi kuwa nyororo, vile vile husaidia ngozi inayopona baada ya kuungua au yenye
vidond

10.Husaidia kuua minyoo tumboni (kwa watoto wadogo)

Hizi Ndiyo Faida Kumi (10) Za Kula Ukwaju!

Unatakiwa ujaribu kuweka ukwaju karibu katika kila mlo wako kwa kila siku kwasababu ukwaju
una faida nyingi kiafya ambazo hakika zitakufanya uwe na afya njema au kukuimarisha afya
yako kiujumla.

Acha Kuteseka na Maumivu ya Jino Tumia Mbinu Hii..!!!

September 04, 2020 Afya No comments


Maumivu ya meno huwa makali sana na huweza kukusababisha hata kushindwa kufanya kazi
nyingine endapo yatakuwa ya muda mrefu.

Mbaya zaidi unaweza usilale kabisa endapo utapatwa na maumivu ya jino usiku kama hauna
uvumilivu unaweza kutoka usiku huo huo na kukimbia hospitali kwenda kung'oa.

Hata hivyo, hapa ninayo orodha za vyakula na viungo ambavyo huweza kusaidia kupambana na
matatizo ya meno.

Jino linalouma au fizi zilizovimba: Ponda ponda tangawizi mbichi kisha itie chumvi. Weka
kwenye jino linalouma au fizi ilipovimba.

Saga majani makavu ya 'mint' kutengeneza unga wake, kisha tia chumvi na weka kwenye jino
linalouma.

Saga karafuu kuwa unga. Weka kiasi cha unga huo kwenye jino linalouma. Pia kama una mafuta
ya karafuu, chukua nyuzi za pamba (cotton wool) chovya kwenye mafuta hayo na weka pamba
hiyo kwenye jino linalouma.

Tiba hizi tunazo majumbani kwetu tunamoishi lakini tumekuwa hatujui kuwa ni tiba, badala
yake huwa tunakimbilia kung'oa meno yanayouma.

Tabia Hizi 5 Zitakufanya Uwe na Maisha Mafupi Sana Hapa Duniani..!!!

September 04, 2020 Afya, maisha 1 comment

Kwa kawaida maisha ya kibinadamu mwisho wake huwa ni kufa, hivyo kila mwenye pumzi hii
leo mwisho wa maisha yake huishia kaburini.
Hata hivyo, kumekuwepo na viashiria fulani fulani ambavyo huweza kuashiria baadhi ya
makundi fulani ya watu huenda wanaweza kuwa na muda mfupi wa kuishi duniani kutokana na
sababu tofauti tofauti.

Miongoni mwa dalili ambazo huweza kuashiria mhusika anaweza kuwa na maisha mafupi
duniani ni pamoja na hizi zifuatazo.

1. Watu wenye kupenda maisha ya anasa na starehe

Watu wa aina hii huwa katika hatari ya kupoteza maisha haraka hata kabla ya siku zao kutokana
na kuwa na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya zinaa.

2. Wavutaji wa sigara.

Watu wanaovuta sigara huwa katika hatari ya kuishi maisha mafupi zaidi kuliko wale ambao
hawatumii sigara kwani watu wa aina hii huwa katika hatari ya kukumbwa na saratani ambayo
huweza kukatisha uhai wa mhusika hata kabla ya siku zake.

3. Kushinda umekaa siku nzima

Wale ambao huwa miili yao haina mazoezi kabisa nao huwa katika hatari ya kupoteza maisha
mapema kutokana na kushambuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu,
kisukari nk.

4. Unywaji wa pombe

Watumiaji wa vileo na huwa katika hatari ya kupoteza maisha yao mapema kutokana na mambo
mawili makuu

a) Kupata ajali kutokana na kutumia vyombo vya moto wakati wakiwa wamelewa na baadaye
kujikuta wanapoteza maisha.
b) Ugomvi ambao huweza kuibuka kutokana na mihemko ya vilevi wanavyokuwa wamekunywa
na kuweza kusababisha ugomvi mkubwa. Mfano kupigana na chupa na baadaye kupoteza uhai.

5. Ulaji wa vyakula vya viwandani

Kuna wale ambao mara nyingi wamekuwa wakila vyakula vya makopo ambavyo vinapotumiwa
mara kwa kwa mara huweza kuwa na madhara kadhaa likiwemo tatizo la saratani. Hivyo kundi
hili nalo linaweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kabla ya siku zao.

Saratani ya Matiti..Vijue Viashiria Muhimu Kuhusu Ugonjwa Huo....

September 04, 2020 Afya No comments

Saratani ya Matiti ni ugonjwa maarufu sana katika kuwapata Wanawake japokuwa unaweza
kutokea kwa Wanaume ila ni nadra sana ikilinganishwa na Wanawake

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), inakadiriwa kuwa vifo 42,260 (Wanawake
41,760 na Wanaume 500) vinatokea kwasababu ya Ugonjwa huo kila mwaka na 62% ya
Wanawake wanafariki kutokana na kushindwa kupima afya zao mara kwa mara

Idadi kubwa ya Wanawake hawajui viashiria vya mwanzo vya Saratani ya Matiti na kwa mujibu
wa gazeti la Independent, 42% wanajua ni mabadiliko gani ya kuangalia kwenye matiti yao,
huku robo ya Wanawake wakidhani kiashiria pekee ni uvimbe

Wanawake wanashauriwa kukagua matiti yao kila baada ya mwaka na kuangalia viashiria
vifuatavyo; Uvimbe, Badiliko la Umbo au Muundo wa titi, Kutokwa na vipele vidogo au Ngozi
kukakamaa na Chuchu kutoa majimaji

Aidha, viashiria vingine ni Ngozi kutokurudi katika hali ya kawaida baada ya


kubonyezwa/kugandamizwa, Maumivu ya mara kwa mara, Mabadiliko katika mguso wa Ngozi,
Kuvimba maeneo ya kwapa na Mabadiliko katika muonekano wa Chuchu(Kuingia ndani au
kuchomoza)

Inashauriwa unapoona dalili kama hizi, ni vizuri kumuona daktari atakayefanya uchunguzi zaidi
na baadaye kukupeleka kwa bingwa wa magonjwa hayo kwa ushauri na tiba zaidi.

NTACT US

FAHAMU Njia Sita za Asili za Kuongeza Nguvu za Kiume ..!!!

September 01, 2020 Afya, Makala ya Leo No comments

Upungufu wa nguvu za kiume umekua tatizo kubwa sana kwa watu wengi. Tatizo hili
limewakumba wanaume wengi walio katika ndoa na hata wale ambao bado hawajaoa.

Watu wengi wamekuwa wakisumbuka kutafuta utatuzi kwani tatizo hili huwafanya kuwa na
wasiwasi wa maisha. Ndoa nyingi zimevunjika na mahusiano kuharibika kwa sababu ya tatizo
hili.

Kwa wanaume wenye umri mkubwa, upungufu wa nguvu za kiume unaweza usiwe ni tatizo
kwani mwili unakuwa umechoka.

Hizi hapa ni baadhi ya njia zitakazokusaidia kurudisha nguvu za kiume zilizokuwa zimepotea.

Jitahidi kutumia vinywaji na vyakula visivyokuwa na sukari nyingi.

Epuka vinywaji vyote vyenye sukari nyingi kwani ni adui mkubwa sana wa afya yako hasa
wakati unataka kurudisha nguvu za kiume. Kula vyakula asili na nafaka ambayo haijakobolewa,
kula matunda kwa wingi pamoja na mboga za majani. Utafurahia maisha ya kula vyakula asili na
utakuwa imara katika tendo la ndoa.

Epuka unywaji wa Pombe.

Tafiti zinaonesha kwamba pombe inakupa hamu au shauku ya kufanya tendo la ndoa lakini
inakunyima uwezo wa kufanya tendo hilo, kwani hupunguza kiwango cha maji mwilini.

Fanya mazoezi ya viungo.

Watu wengi wamelemewa na magonjwa kwa sababu tu mwili haupati damu ya kutosha kwenda
sehemu mbali mbali kama vile ubongo, ini na figo ambazo ndio sehemu zenye kuufanya mwili
wako ufanye kazi katika uhalisia wake. Uume ili usimame kwa uimara, unatakiwa upate damu ya
kutosha.

Kufanya mazoezi hupunguza kuwango cha mafuta katika mishipa ya damu na kuiwezesha
kupeleka damu ya kutosha katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo uume.

Rudisha Virutubisho ambavyo vimepotea mwilini mwako.

Hakikisha mwili wako unaupa madini ya msingi kama zinki, chuma, selenium, manganese na
vitamin nyingi, kwani madini haya ndiyo yanafanya mwili wako ufanye kazi katika kiwango
stahiki. Madni haya huwezesha viendesha shughuli za mwili yani enzymes kufanya kazi katika
kiwango kizuri na kuimarisha mwili wako. Madini haya hupatikana katika mboga, samaki na
matunda ya aina mbalimbali.

Kunywa maji ya kutosha kila siku.

Kunywa maji ya kutosha kila siku, usingoje mpaka kiu ikupate. Mtu mzima anapaswa kunywa
maji glass 8 mpaka 10 kwa siku. Maji husaidia kuongeza kiwango cha damu na kuondoa sumu
mbalimbali mwilini.
Epukana na msongo wa mawazo.

ufanyaji wa tendo la ndoa huwa unahusisha mambo mengi. Unaweza ukawa umekamilika kiafya
lakini ukashindwa kufanya mapenzi kwa kuwa una msongo wa mawazo. Hakikisha kabla ya
kwenda faragha na mpenzi wako, unaituliza akili na usiwaze mambo mengine nje ya tendo
linaloenda kufanyika. Hii itakupa muda mzuri wa ubongo wako kupeleka damu ya kutosha
katika uume.

JE Umeshawahi Sikia Kauli ya Kubemenda Mtoto...? Huu Hapa Ukweli Kuhusu Kubemenda

August 30, 2020 Afya No comments

Kumbemenda mtoto ni mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama


anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwenzi wake hasa kipindi mtoto bado ni
mchanga na ananyonyeshwa.

Hii ni dhana iliyopo katika jamii mbalimbali, na inadhaniwa hutokea kwa sababu mtoto
kunyonya maziwa yenye mbegu za kiume zilizoingia kwenye maziwa baada ya kufanya
mapenzi.

Je, kuna ukweli wowote?

Hapana. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa!

kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto
kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la
uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa. dhana ya
kuwa shahawa huingia kwenye maziwa na kumuathiri mtoto sio sahihi.

Ni baada ya muda gani mwanamke aliyejifungua anaweza kufanya mapenzi?


unaweza kuanza kufanya mapenzi tena baada ya maji maji yenye damu ya uke (lochia) kuacha
kutoka ambayo ni kama wiki 3 mpaka 4 baada ya kujifungua, na wewe kujisikia vizuri na kuwa
tayari kushiriki katika mapenzi. pia, mnaweza kusubiri mpaka wiki 6 zipite toka ulivyojifungua.

Je, kuna athari yoyote ya kufanya mapenzi baada ya kujifungua?

Kufanya mapenzi baada ya kujifungua hakuwezi kuleta madhara kwa mtoto endapo hamna
maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu). ikiwa mwanaume ana vvu anaweza
kumuambukiza mama na kisha mtoto kuambukizwa kupitia maziwa ya mama.

Ikiwa mnafanya mapenzi kabla ya damu damu ya ukeni kukata, maambukizi ya bakteria
yanaweza kutokea kwenye tumbo la uzazi (endometritis). pia kuna uwezekano wa mama kupata
ujauzito miezi 6 ya kwanza ya kunyonyesha.

Nini kinasababisha afya ya mtoto kuzorota?

Kama tulivyoona, kufanya mapenzi hakusababishi mtoto kubemendwa. afya ya mtoto inaweza
kuzorota kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo;

Kukosa maziwa ya mama ya kutosha

Mtoto kushindwa kunyonya vizuri

Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na
viritubisho vya kutosha.

Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.

Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.

Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).

Kufanya mapenzi na mwenzi wako hakusababishi mtoto kubemendwa. Baada ya kujifungua


mtoto hutegemea kupata lishe bora kutoka kwenye maziwa ya mama, hivyo nyonyesha mtoto
wako vizuri. ukiona ukuaji wake unazorota, onana na daktari.

Kwa Nini Watu Wengi Wanaanguka Bafuni na Kupata Stroke Mara Nyingi
August 18, 2020 Afya No comments

Imetokea mara nyingi kusikia kuwa jamaa kaanguka bafuni na kufariki au kupata stroke au
hajitambui na wala haongei!

Ukiwa unapresha na ukaingia bafuni kuoga, unapoanza kichwani kujimwagia maji ni hatari
kwani mwili wote na viungo upata mawasiliano kwa kuongozwa na sehemu maalum kichwani
iitwayo control centre, hii ina idara nyingi kwa kazi husika kiasi kwamba mwili na viungo vyake
uendeshwa kwa ustadi mkubwa kama Mungu mmoja wa pekee alivyoumba na kukadiria.

Maji yakimwagiwa kichwani yanastua sehemu muhimu zikiwemo za mfumo wa moyo na


fahamu ghafla kiasi kwamba uwiano ukikosa kati ya moyo na fahamu inatokea mtu kuzirai na
hatimaye stroke inatokea.

Ushauri anza kujimwagia kiunoni na kushuka chini kwenye miguu na kisha kifunoni hadi
kifuani na kumalizia kichwani na hii inaweka uwiano sawa kati ya mwili na ubongo kupokea
maji mwilini.

Je Unasumbuliwa na Tatizo la Nguvu za Kiume?

February 06, 2018 Afya No comments

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na maumbile madogo ya uume limekuwa kwa lika zote
Tiba sahihi ya matatizo haya

Chanzo chake na visababisho vyake

DALILI: mwili kuchoka maumivu ya mgongo na kiuno kutopata choo vizuli kinakuwa kigumu
kama cha mbuzi
RADI: hutibu matatizo kwa mda mfupi na inakufanya uchelewe kufika kileleni kwa dakika (30)
kwa tendo(1) utaludia Mara (4) bila kuchoka pia uongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa
maradufu

BOMBA; dawa ya kupunguza matiti makubwa unene na kitambi

ITUJA; dawa inatibu michilizi mwilini inaongeza makalio hips miguu saizi uipendayo

HUDUMA HIZI NA ZINGINE UTAZIPATA POPOTE TANZANIA MUONE DR LAJABU


AU PIGA SIM 0711494261 au 0783823120.

SUA yagundua mwarobaini tatizo la nguvu za kiume na Mvurugiko wa Mzunguko wa Hedhi

July 20, 2018 Afya No comments

Chuo cha Kilimo SUA Kimefanya utafiti na kubaini kuwa mbegu za matunda zinaweza kutibu
matatizo ya nguvu za kiume na mzunguko wa hedhi uliovurugika kwa mwanamke.

Katika miaka ya karibuni wanaume wengi wamekuwa wakisumbuliwa na tatizo la kukosa nguvu
za kiume na kusaka tiba bila mafanikio huku wengine wakikimbilia kwa waganga wa kienyeji.

Hivyo wanafunzi wa SUA wakachukua fursa hiyo kuja na mbinu mbadala ya kukomesha tatizo
hilo ambapo wamegundua kwamba mbegu za matunda kama tikitikimaji, maboga, alizeti, papai
na matunda mengine zinaweza kutibu matatizo hayo.

Stewart Mwanyika ambaye ni Mtafiti Mwandamizi kutoka SUA amesema kiasili mbegu zina
kiasi kikubwa cha madini ya zinki ambayo yanachangia kutengeneza homoni na chembechembe
zinazohusika na utendaji bora wa via vya uzazi hasa vya mwanaume.

Hivyo ameshauri watu kutumia mbegu hizo mara kwa mara iwe tiba ya kudumu kwani madini
ya zinki yanatengeneza haraka chembechembe nyeupe za damu ambazo ni kinga ya mwili na seli
nyingine zinazohusika na via vya uzazi.
”Ukila matunda kama tikitimaji usitupe mbegu, tafuna meza na kama harufu inakukera unaweza
kuzitoa na kuzikausha kisha oka ili kuongeza ladha kisha tafuna, mbegu za papai pia ukiweza
kuzila ni vizuri lakini zina uchungu, ila kwa mbegu za alizeti na maboga kuzikaanga kisha
unatafuna unameza”

Faham Usiyoyajua Juu ya Uwezo wa Hali ya Juu wa Mbegu za Maboga Katika Kutibu
Magonjwa Haya 10..!!!

March 07, 2017 Afya No comments

ULAJI wa maboga ni muhimu lakini ni Watanzania wachache wanaojua faida ya boga na mbegu
zake. Mbegu za maboga zimesheheni protini na madini kadhaa kama vile chuma, kopa,
maginizia, manganizi na zinki, mbegu za maboga zinakuwa mbegu bora na muhimu kutafuna
kila wakati baada ya kuzikaanga au zikiwa mbichi au kama zimepikwa na boga lenyewe kwani
imethibitika pasipo na shaka kuwa mbegu za maboga zina faida lukuki kiafya na zina uwezo wa
kukuepusha na magonjwa hatari zaidi ya 10.

KIBOFU CHA MKOJO

Mbegu za maboga zimekuwa zikitumika kuimarisha afya ya wanaume kutokana na kuwa na


kiasi kingi sana cha madini aina ya Zinc ambayo ni muhimu sana kwa afya ya kibofu cha mkojo
Urinery Bladder. Mbegu za maboga pamoja na mafuta yake, yote kwa pamoja hutoa kinga
kwenye kibofu kupatwa na matatizo ya kiafya, yakiwemo yale ya saratani ya kibofu.

KINGA YA MWILI

Mbegu za maboga zenye kiasi kingi cha madini ya Zinc yana faida nyingi mwilini, ikiwemo
kuimarisha kinga ya mwili, kuboresha ukuaji na uundaji wa chembechembe hai za mwili,
kuboresha usingizi, kuboresha ladha mdomoni na harufu, huboresha afya ya macho na ngozi,
hurekebisha kwenye damu sukari na huboresha nguvu za kiume pia huongeza uwezo wa kufikiri.
Upungufu wa madini ya Zinc mwilini una uhusiano mkubwa sana na matatizo ya kuzaa watoto
njiti, mwanamke au mwanaume kuota chunusi nyingi mwilini, watoto kuwa na uwezo mdogo wa
kuelewa wanachofundishwa darasani kimasomo na matatizo mengine mengi ya kimwili na
kiakili.

MAFUTA YA OMEGA -3

Omega-3 ni moja kati ya mafuta muhimu sana mwilini. Jamii ya karanga pamoja na mbegu za
maboga ni miongoni mwa mbegu zenye kiasi kingi cha mafuta aina hii. Hivyo ulaji wa mbegu za
maboga utakuwezesha kupata kirutubisho hiki muhimu katika mwili wako na kukupa faida za
mafuta haya ambazo ni nyingi.

UGONJWA WA MOYO

Mbegu za maboga zina kiasi kingi cha madini aina ya maginizia Magnesium ambayo huboresha
utendaji kazi wa viungo vya mwili. Huimarisha usukumaji wa damu kwenye moyo, huimarisha
ukuaji wa mifupa na meno, huifanya mishipa ya damu kupitisha damu kwa urahisi na hufanya
upatikanaji wa haja kubwa kuwa laini.

KINGA DHIDI YA SARATANI

Imethibitika kwamba watu ambao hula mlo wenye kiasi kingi cha mbegu za maboga
wamegundulika kuwa na hatari ndogo sana ya kupatwa na saratani za tumbo, matiti, mapafu na
kibofu, hivyo unapokula mbegu hizi husaidia mambo hayo na mengine mengi.

UGONJWA WA KISUKARI

Utafiti uliofanywa kwa kuwalisha wanyama mbegu za maboga, umeonesha kuwa ulaji wa
mbegu za maboga, husaidia kurekebisha kiwango cha Insulin mwilini na hivyo kumuepusha mtu
kupatwa na ugonjwa hatari wa kisukari.
MATATIZO YA UKOMO WA HEDHI

Mara nyingi akina mama watu wazima ambao wamefikia ukomo wa hedhi, hupatwa na matatizo
mbalimbali yanayosababishwa na hali hiyo. Hata hivyo, wataalamu wamegundua kwamba ulaji
wa mbegu umeonesha kuwa mbegu za maboga zina uwezo wa kurekebisha hali hiyo na kuondoa
kabisa matatizo ya kiafya yatokanayo na ukomo wa hedhi.

AFYA YA MOYO NA MAINI

Mbegu za maboga, ambazo zina kiasi kingi cha mafuta mazuri, kamba lishe Fibre na virutubisho
vinavyoimarisha

kinga ya mwili Antioxidants, zimeonekana kuwa bora pia kwa afya ya moyo na ini, huweza
kumpatia mlaji kinga dhidi ya matatizo ya kiafya katika moyo na ini.

DAWA YA USINGIZI

Mbegu za maboga zimegundulika pia kuwa na kirutubisho kinachozalisha homoni’ za usingizi.


Ulaji wa mbegu za maboga saa chache kabla ya kupanda kitandani, hasa ukila pamoja na tunda
lolote, kunasaidia kupata usingizi mzuri mwororo.

DAWA YA UVIMBE

Wataalamu wamethibitisha kwamba mbegu za maboga zina mafuta yenye uwezo wa kutoa kinga
dhidi ya magonjwa ya uvimbe Inflamatory Diseases sawa na dawa aina ya Indomethacin lakini
mbegu hizi hazina madhara kama ilivyo kwa hiyo dawa, ndiyo maana tunahimiza kutumia
mbegu za maboga ambazo huwa ni dawa asili.

JINSI YA KULA MBEGU ZA MABOGA


Ili kupata faida zake zote, zikiwemo zile za mafuta yake, inashauriwa kula mbegu hizo zikiwa
kavu, bila kuzikaanga japokuwa zilizokaangwa bila kuunguzwa nazo siyo mbaya. USHAURI
Hakikisha pia unapata mbegu zilizohifadhiwa vizuri ambazo hazijaoza wala kuwa na fangasi.
Iwapo utapenda kuzikaanga, basi hakikisha unazikaanga kwa muda usiozidi dakika 15, unaweza
pia kuongeza chumvi kidogo kupata ladha, lakini za kukaanga zitakuwa hazina mafuta mengi
kama zile kavu.

Vijana Wengi zaidi Tanzania Hatarini Kupata Ugonjwa wa Kiharusi

October 03, 2019 Afya, Mapenzi 1 comment

Idadi ya vijana na watu wazima wenye umri chini ya miaka 45 wanaopata ugonjwa wa kiharusi
imezidi kuongezeka, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi
Shirikishi Muhimbili (Muhas).

Matokeo ya utafiti huo uliofanywa kati ya Juni 2018 na Januari 2019 yaliwasilishwa juzi kwenye
Mkutano wa Saba wa Sayansi chuoni hapo. Utafiti huo ulitokana na wagonjwa waliopatiwa
matibabu katika kituo cha tiba kilicho ndani ya Muhas.

Ilibainika kuwa wagonjwa 123 kati ya 369 waliobainika kuwa na kiharusi ni vijana na watu
wazima wenye umri chini ya miaka 45; na wengine 246 ni watu wazima wenye umri zaidi ya
miaka 45 pamoja na wazee.

Kiongozi wa utafiti huo, Dkt. Sarah Matuja alieleza kuwa ugonjwa wa kiharusi huaminika kuwa
unawapata zaidi wazee lakini utafiti huo umeonesha kuwa vijana wengi pia wako hatarini.

Alisema kuwa chanzo kikuu cha kiharusi kinaaminika kuwa ni shinikizo la damu (blood
pressure), na kwamba wagonjwa wengi waliotibiwa katika kituo hicho walikuwa na shinikizo la
damu.
Aidha, alisema kuwa vijana wengi waliokutwa na shinikizo la damu hawakuwa wanajua kama
wana tatizo hilo hadi walipopima wakati huo wakiwa na kiharusi, tofauti na wazee ambao mara
nyingi hupata vipimo vya shinikizo la damu.

Wataalam wa tiba wameeleza kuwa vitu vinavyowafanya vijana kuwa katika hatari zaidi ya
kupata kiharusi ni ulevi wa pombe, Virusi Vya Ukimwi, ugonjwa wa moyo na mengine.

Kwa mujibu wa Dkt. Matuja, kiharusi kinaweza kudhibitiwa kwa kuhakikisha hauna uzito kupita
kiasi, hauna shinikizo la juu la damu na kufanya mazoezi mara kwa mara.

Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa kuna ongezeko kubwa la kiharusi kwa vijana na
watu wazima, ambapo mtu mmoja kati ya sita wanaopata kiharusi ni kijana/mtu mzima mwenye
umri kati ya miaka 18 hadi 50.

Faida 48 za juice ya tangawizi

1. Kuondoa sumu mwilini kwa haraka sana.


2. Kuua bacteria wa aina nyingi sana mwilini hata wale wanaoitwa songolela wa
mwilinin hata wale juu ya ngozi
3. Kuondoa uvimbe mwilini
4. Huondoa maumivu mbalimbali mwilini kwa anayehisi maumivu ya mwili akitumia
hii juisi(sharubati) ya tangawizi au kwa kuamua kutafuna.
5. Kusafisha mapafu
6. Kuondoa maumivu ya koo
7. Kuondoa virusi vya homa mbalimbaali katika mwili wa binadamu hata homa ya
baridi
8. Huondoa saratani ya saratani ya tenzi dume. Tangawizi huua kimeng’enya chakula
cha kansa cha seli cha tenzi dume kiitwacho, Five-Lo enzymes na seli hizo za kansa
hufa kwa masaa mawili hadi manne bila hich kimeng’enya.
9. Kutibu kansa kinachosabisha na choo kigumu cha muda mrefu
10. Ina kiini lishe ambacho ni muhimu kinachosaidia kuzuia kuongezeka kwa seli za
kansa ya kongosho kiitwacho kama Gingerroll
11. Dawa mzuri ya Kansa ya damu, kama unadalili ya kupata kansa ya damu basi
unashauriwa kutumia juisi ya tangawizi au kwa kutafuna kipande cha tangawizi.
12. Pia ni dawa nzuri ya kansa ya mapafu, Lungcancer
13. Kuzuia kuzalisha kwa backteria ambaye husabisha vidonda vya tumbo mwilini. Pia
hutibu kuingulia na kansa mbalimbali za tumbo.
14. Huzuia na kusaidia sana kansa ya titi
15. Hutibu kansa ya kwenye kizazi na kansa ya kwenye mirija ya uzazi
16. Huongeza msukumo wa damu mwilini
17. Kuzuia shambulio la moyo
18. Kuzia damu kuganda
19. Kususha cholesterol (rehemu) mwilini au kurahisisha kwa mafuta yalio ganda
mwilini.
20. Kusafisha utumbo mpana
21. Husaidia kufisha damu
22. Hupunguza mshtukoo kwenye utumbo mpana na kunguruma.
23. Husaidia kwa watu walikakamaa mishipa
24. Hutibu shinikizo la damu la juu (kupanda kwa shinikizo la damu)
25. Kuondoa gesi tumboni
26. Kusaidia mmeng’enyo wa chakula
27. Huzuia kutapika
28. Kutibubu homa ya kichwa
29. Kuimarisha afya ya figo
30. Kuondoa kichefuchefu
31. Kusaidia kweneye mfumo wa upumuaji
32. Kutibu maumivu tumbo kwa mwenye hedhi
33. Kupunguza uchomvu
34. Kuna madini magnesium kwa kuongeza kinga ya mwili
35. Kusaidia kuongeza
36. Kulinda kuta za moyo na

Pata kilo moja ya tangawizi katakata ila usimenye bali kusafishi kwa kuosha kwa maji kisha
weka kwenye blenda au twanga kwenye kinu hakikisha inakuwa laini kabisa. Kisha fanya au
tengeza juisi yake kisha weka kwenye glasi kisha kunywa asubuhi na jioni kwa muda wa siku
ishirini na moja (21).

You might also like