You are on page 1of 11

JE?

WAZIJUA FAIDA ZA KUSHANGAZA ZA KUTUMIA ZA KUTUMIA UNGA


WA MBEGU ZA PARACHICHI?
SI WAKATI WA KUTUPA MBEGU ZA PARACHICHI TENA.

Kimeandaliwa na:

JOSHUA JOSEPH NAMFUA M.A


Simu: +255719202720/+255758840486
Email: joshuanamfua@yahoo.com

1
Yaliyomo:
1.0 UTANGULIZI: ...................................................................................... 3

2.0 FAIDA ZA UNGA WA MBEGU ZA PARACHICHI ..................................... 4

2.1 HUTIBU: ............................................................................................. 4

2.1.1 SHINIKIZO LA DAMU LA CHINI .......................................................... 4

2.1.2 HUPUNGUZA UKALI WA MARADHI YA MOYO ...................................... 6

2.1.3 KUKUZA NA KUIMARISHA KINGA YA MWILI ........................................ 6

2.1.4 HUBORESHA MFUMO WA MMENGENYO WA CHAKULA ...................... 7

2.1.5 HUUA NA KUZUIA UZALISHAJI WA VIJIDUDU VIENEZAVYO SARATANI.


................................................................................................................ 7

2.1.6 KUPUNGUZA UNENE......................................................................... 7

2.1.7 HURUTUBISHA NGOZI NA KUIFANYA IWE NA MUONEKANO MZURI ..... 7

2.1.8 HUPUNGUZA MAUMIVU YA MIFUPA NA MISULI .................................. 8

3.0 KIJIKO KIMOJA TU CHA UNGA WA MBEGU ZA PARACHICHI HUWA NA


VIRUTUBISHO VIFUATAVYO:.................................................................... 8

4.0 MAANDALIZI NA MATUMIZI ................................................................ 9

5.0 MATUMIZI: ......................................................................................... 9

HITIMISHO: ........................................................................................... 10

MAPITIO (REFERENCE) .......................................................................... 11

2
1.0 UTANGULIZI:

Parachichi kama tunda limekuwepo kwa miaka mingi duniani likijulikana kwa

faida zake mbali mbali na taaluma za kitabibu zimelitumia kwa njia mbali mbali

kutibu maradhi ya: mmengenyo wa chakula, urutubishaji wa nywele na ngozi,

kupunguza makali ya kuungua na mengineyo mengi. Pia kihistoria mbegu zake

zimetumika kutengenezea wino wa kuandikia( je watu hawa walijua faida zake

kiafya?) je? Wajua mbegu yake huwa na 18% ya matunda mengineyo? (tafiti).

Kula vipande viwili hadi vitatu vya parachichi ka siku kutasaidia kujenga kinga

ya mwili na kujiepusha na kumuona daktari kila wakati kwa maradhi madogo

madogo. Lakini je? Wajua unga wa mbegu za parachichi ni kirutubisho yakinifu

na tena tiba kwa maradhi makubwa yanayokabili binadamu? Mara nyingi

tumekuwa tukitupa wala si kuzipanda mbegu za parachichi na kuziacha

zikizagaa na kujiotea kwa shida sana. Lakini baada ya chapisho hili litabadilisha

mtazamo na fikira namna tunavyolitumia tunda na mbegu za parachichi. Najua

unajiuliza maswali kadha wa kadha akilini kama: kivipi hutibu? Na je nitaingiza

tunda zima katika mlo? Vipi kuhusu uchungu? Naandaaje na natumia kwa

kiwango gani? Na maswali mengine mengi ambayo hata mimi nimewahi

kujiuliza. Chapisho hili ltaangazia faida za unga wa mbegu za parachichi,

maandalizi na matumizi.

3
2.0 FAIDA ZA UNGA WA MBEGU ZA PARACHICHI
Chuo kikuu cha Pennsylvania katika kitengo cha tafiti hivi karibuni

wameanzisha uchunguzi juu ya faida za mbegu za parachichi katika

kurutubisha na kutibu mifumo ya mwili na kugundua kuwa asilimia 70% ya

faida za parachichi hutoka katika mbegu. Tafiti juu ya mfumo wa mwili na

matibabu zimeonesha mbegu za parachichi zina faida zifuatazo:

2.1 HUTIBU:
1. SHINIKIZO LA CHINI LA DAMU

2. HUPUNGUZA UKALI WA MARADHI YA MOYO

3. KUKUZA NA KUIMARISHA KINGA YA MWILI.

4. HUBORESHA MFUMO WA MMENGENYO WA CHAKULA

5. HUUA NA KUZUIA UZALISHAJI WA VIJIDUDU VIENEZAVYO SARATANI.

6. KUPUNGUZA UNENE

7. HURUTUBISHA NGOZI NA KUIFANYA IWE NA MUONEKANO MZURI

8. MAUMIVU YA MIFUPA NA MISULI

2.1.1 SHINIKIZO LA DAMU LA CHINI


Matumizi ya unga wa mbegu ya parachichi hutibu shinikizo la chini la damu

kama itatumiwa kikamilifu na kama mfumo wa maisha. Mhusika anatakiwa

kuchota vijiko viwili vya chai vya unga wa mbegu ya parachichi na kuchanganya

na maji moto ya kikombe kimoja cha chai, ongeza asali vijiko viwili vya mezani.

Tumia mara tatu kwa siku.

Dalili zake:

4
Zipo dalili chache zinazoweza kukujulisha mapema juu ya tatizo hili. Yaweza

kuwa ni maumivu ya kichwa, kizunguzungu, kutokuwa na uwezo wa kufikiri au

matatizo ya usagaji chakula tumboni. Kunaweza kukawa na nguvu kidogo tu au

hali ya kuhisi kizunguzungu kila unapoinuka wakati ukiwa umekaa au umelala

mahali flani. Kupoteza fahamu, macho kufifia na kuona maruweruwe, mapigo

ya moyo kwenda kwa haraka na kupoteza maneno wakati unapozungumza au

kigugumizi.

Visababishi:

Nguvu ya msukumo inayotumika kusafirisha huwa ni kidogo mno, maana yake

ni kuwa damu haina uwezo wa kusafiri vizuri pote mwilini kama inavyotakiwa.

Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu unaweza kuondoa maisha ya mtu kabisa;

lakini shinikizo la la damu laweza kuwa ni ugonjwa ambao kwa kawaida mtu

anaweza akawa nao lakini akaishi tu. Ikiwa kipimo cha ugonjwa wa shinikizo la

damu kitaonesha kiwango cha 110/70 hadi 140/90, basi kiwango hicho huwa

ni cha kawaida kwa mtu mwenye afya bora na mara nyingi hoonekana kama

mbaraka pekee.

Hata hivyo hali ya shinikizo la juu la damu huonekana kuwa tatizo iwapo

mtiririko wa damu sehemu za ubongo utapungua na kufikia kiwango ambacho

humfanya mgonjwa ahisi kizunguzungu na kupoteza maneno wakati wa

kuongea.

Ugonjwa huu husababishwa na mambo yafuatayo:

5
1. Magonjwa sugu mwilini

2. Matumizi ta dawa na kidonge yanapozidi nguvu

3. Magonjwa ya figo

4. Upungufu wa damu

5. Kushuka kwa kisukari kweye damu

6. Mizio ya chakula

7. Utapia mlo

8. Kuharibika kwa neva za fahamu kutokana na tatizo la kisukari.

2.1.2 HUPUNGUZA UKALI WA MARADHI YA MOYO


Daktari mashuri kutokea Amerika Dk. Tom Wu aliyewahikushinda tuzo ya

umoja wa mataifa ya madaktari mashuhuri Zaidi duniani na kupewa tuzo

nyingine kama mchangiaji mkuu kitaaluma na kinyenzo na jamii ya saratani ya

marekani alisema: mgonjwa yoyote wa matatizo ya moyo anatakiwa kula

parachichi ikihusisha na mbegu yake hivyo unga wa mbegu ya parachichi ni

muhimu sana kutumika kama kiungo tiba katika chai, maji ya matunda (juisi)

na vimiminika vingine

2.1.3 KUKUZA NA KUIMARISHA KINGA YA MWILI


Utumiaji wa unga wa mbegu za parachichi husaidia uzalishwaji wa seli nyeupe

za damu zihusikazo katika kuukinga mwili dhidi ya bakteria na virusi

vinavyonyemelea na kudhohofisha mwili.

6
2.1.4 HUBORESHA MFUMO WA MMENGENYO WA CHAKULA
Katika America ya kusini mbegu za parachichi zimekuwa zikitumika kutibu

magonjwa mbali ya tumbo ikiwemo mfumo wa umengenyaji chakula, (dysentery)

ugonjwa ushambuliao utumbo mwembamba na kusababisha kuhara na hutumika pia kupunguza

makali ya vidonda vya tumbo.

Vitamini C na E zipatikanazo katika mbegu za parachichi husaidia kurutubisha mfumo wa utendaji

kazi wa tumbo na pia matumizi ya vimiminika vilivyochanganywa na unga wa mbegu za

parachichi husaidia kupunguza unene au fat kwa kiwango cha hali ya juu ikiambatanishwa na

mazoezi.

2.1.5 HUUA NA KUZUIA UZALISHAJI WA VIJIDUDU VIENEZAVYO


SARATANI.
Utafiti uliofanywa katika chuo kikuu cha Antioquia, Medellin, Colombia Novemba,2013 ulionyesha

kuwa matumizi ya mbegu ya parachichi yanachangia kujiharibu zenyewe seli zichangiazo

saratani ya damu (leukemia) na kuziacha seli za mwili zenye afya na uthabiti.

2.1.6 KUPUNGUZA UNENE


Unene kuzidi kiwango ni changamoto kubwa hasa katika dunia ya leo hasa kwa jamii zetu za

kiafrika na husababisha matatizo lukuki. Kuwa makini na mazoezi na mifumo ya ulaji

kutaboreshwa Zaidi na kutumia unga wa mbegu za parachichi kama mfumo wa maisha.

2.1.7 HURUTUBISHA NGOZI NA KUIFANYA IWE NA MUONEKANO MZURI


Tumekuwa mashahidi wa kuziona bidhaa za parachichi madukani kwa ajili ya urembo wa nywele

na ngozi. Je? Tumewahi kujua kuwa unga wa mbegu za maparachichi hutumika kusafisha na

kurutubisha ngozi. Kivipi?

Bidhaa yoyote ya kusafishia ngozi( skin cleanser za aina yoyote) zaweza changanywa na unga

wa parachichi vijiko viwili hadi vitatu na kusugulia uso na sehemu za mwili kwa dakika tano mpaka

7
saba na safisha kwa maji tayari uso na ngozi itakuwa safi na ni hatua za kukomesha matatizo ya

ngozi. Urutubishaji huu wa ngozi haufanyiki nje tu ila san asana huanzia ndani kwa kutumia

(kunywa unga wa mbegu za parachichi)

2.1.8 HUPUNGUZA MAUMIVU YA MIFUPA NA MISULI


(Inflammation) ni kitendo cha sehemu za mwili kuuma, kupata joto, kuweka wekundu, kuchubuka

kama matokeo ya kupata jeraha au msuguano. Hivyo mambo yote haya hutokea katika wili hasa

katika mifupa, misuli na viungo vingine mwilini. Unga wa mbegu za parachichi husaidia sana

kuleta ahueni na baadae kuponya kabisa maumivu haya.

3.0 KIJIKO KIMOJA TU CHA UNGA WA MBEGU ZA PARACHICHI HUWA NA


VIRUTUBISHO VIFUATAVYO:
RDA- ni neno lakitaalamu limaanishalo kiwango cha kila siku cha matumizi.

Vitamini K: 26% RDA

Folate: 20% of the RDA.

Vitamini C: 17% of the RDA.

Potassium: 14% of the RDA.

Vitamini B5: 14% of the RDA.

Vitamini B6: 13% of the RDA.

Vitamini E: 10% of the RDA.

Hivyo kuwa pia na Magnesium, Manganese, Copper, Iron, Zinc,

Phosphorous, Vitamin A, B1 (Thiamine), B2 (Riboflavin) na B3 (Niacin).

8
4.0 MAANDALIZI NA MATUMIZI
1. Kata parachichi wakati wa matimizi na tenga tunda au matunda pembeni

2. Safisha na ondoa ganda la juu kwenye mbegu kwa kutumia kisu

3. Tunatumia kikwaruzio kwangua na weka kwenye chombo

4. Baada ya kupata unga huo anika ndani au sehemu isiyo na mwanga wa

moja kwa moja wa jua kwa siku sita kuhakiki umekauka kasha

changanya na viungo vingine kuongeza ubora, ladha na mvuto; weka

vipande vya Mdalasini, karafuu, mbegu za iliki, mchaichai na tangawizi.

5. Twaga kwenye kinu au peleka mashineni kwa ajili ya kusagwa kupata

unga halisi. ( kumbuka kwenda mashineni na mahindi walau kilo tano

kwa ajili ya kusafisha mashine baada ya kusaga na unga huo utumike

kupikia uji ni muhimu san asana kiafya.

5.0 MATUMIZI:
CHAI: weka vijiko viwili vya mezani na kijiko kimoja cha asali (kama ipo) kwenye

kikombe na kutumia mara tatu kwa siku. Hivyo ndivyo hutibu yoote

yaliyodadavuliwa hapo juu.

UREMBO WA NGOZI WA NJE: changanya na rojo la sehemu iliwayo na sugua

usoni na sehemu za mwili kwa dakika sita mpaka saba kasha nawa na maji ya

9
uvuguvugu husaidia kulainisha, kusafisha, kuondoa na kuzuia chunusi. Unga

huu waweza changanya pia na scrub zozote toka dukani.

HITIMISHO:
Ni kwa ufupi tu namna ambavyo mbegu za parachichi zaweza tumika kama tiba

na kinga katika miili yetu. Faida zinginezo ni kwa mifugo pia hasa wale

wanaokamua ngombe maziwa waweza katakata vipande vidogo vidogo na

kuchanganya kwenye pumba na kushuhudia miujiza ya maziwa na afya tele kwa

mifugo. Hivyo panda miparachichi tangu sasa kuboresha afya ya kizazi hiki na

cha baadae maana si tunda tu peke yake ila mizizi na majani yake ni dawa pia

na mti wake hutumika kwa mbao na kumi hivyo ni frusa nyeti ya kiuchumi.

10
MAPITIO (REFERENCE)
Wright, C.I. et al. Herbal medicines as diuretics: A review of the scientific

evidence. Journal of Ethnopharmacology, v.114, p.1- 31, 2007. Available from:

http://www.sciencedirect.com/science/article/pii/s0378874107003662>

.Accessed: March 8, 2016. doi: 10.1016/j.jep.2007.07.023.

Grant, W.C (1960) influence of avocado on serum cholesterol. Proceeding of the

society for experimental biology and medicine, 104, 45-47. Available from:

http://dx.doi.org/10.3181/00379727-104-25722. Accessed: March 11, 2016.

Pieterse, E., Jerling, J.C., Oothuizen, W., Kruger, H.S., Hanecom, S.M., Smuts,

C.M., et al. (2005) Substitution of high monounsaturated fatty acid avocado for

mixed dietary fats during an energy restricted diet: Effect of weight loss, serum

lipids, fibrinogen and vascular funiction. Nutrition, 21, 67-75. Available from:

http://dx.doi.org/10.1016/j.nut.2004.09.010 Accessed: May 4, 2016

Imafidon, K.E., Amaechina, F.C. (2010) Effects of aqueous seed extract of percea

Americana mill (avocado) on blood pressure and lipid profile in hypertensive

Rats. Advance in biological research, 4, 116-121.

11

You might also like