You are on page 1of 30

Shukurani

Napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kuniwezesha kuandika maelezo haya, pia


kuwashukuru wanafunzi wenzangu, watu mbalimbali na vyanzo tofautitofauti
ambavyo kwa namna moja au nyengine vimesaidia sana katika kuweza kuandika
makala hii.

Kwa ujumla kuna sababu mbali mbali zilizonipelekea kukuiandika makala hii
inayozungumzia shindiukizo la damu (presha). Baadhi ya sababu hizo ni;

1. Shindikizo la damu ni ugonjwa amabao umekuwa tishishio kwa


watu wa jamii na rika tofauti, lakini bado inaelekea watu
waliowengi bado hawajatanabahi juu ya tishio la shindikizo la
damu kwa maisha yao.
2. Bado hakuna mipango na mikakati mizuri iliyowekwa
kukabiliana ugonjwa huu ambao kila familia inaguswa na athari
zake hivi sasa.
3. Mkazo mkubwa umewekwa namna ya kukabiliana na magongwa
mengine kana Ukimwi na kuyawacha kando maradhi mengine
kama hili la shindikizo la damu hali ya kuwa limekuwa ni janga
kubwa katika kila familia.

Afya yako ndio jambo lenye thamani kubwa kuliko kitu chengine chochote kwani
hakuna maana yeyote ikiwa afya yako ni mbaya (Afya ni kitu muhimu na chenye
thamani kubwa kwa maisha ya mwanadamu). Katika maendeleo ya maisha
mwanadamu, afya ni kitu cha kwanza. Mwanadamu hutoweza kuishi kwa raha ki
familia ikiwa atakuwa anasumbuliwa na maradhi na kuhangaika kutafuta
matibabu.

Pamoja na kuwa uandishi sio fani yangu, lakini kwa kuzingatia kuwa shinikizo la
damu ni janga linalowakabili watu wengi, nimeona ni muhimu kwangu nitoe
mchango wangu ili uwe ni changa moto kwa watu nao waweze kutanabahi juu ya
haja ya kusaidia katika kuelimisha jamii. Pia pamoja na kuwa mimi sio mtaalamu
wa elimu ya afya lakini ni mmoja kati ya wale ambao tayari wanaogelea katika
shinikizo la damu, ni matarajio yangu kuwa makala haya yataamsha ari na kusaidia
japo kidogo katika katika kutoa miongozo kwa wale wenye matatizo ya sindikizo la
damu. Hapa nitazungumzia Presha ya juu, nategemea pia kuizungumzia Presha ya
chini siku zijazo.

Baadhi ya watu wanafikiri wao lazima wapate maradhi fulani. Wapo kwenye
mawazo hayo kwa sababu kwenye koo zao kuna maradhi kama hayo. Kupata au
kutopata maradhi ni suala la wakati, kama bado haujafika utakuawa salama na
utakapofika hutakuwa na namna ya kuyakimbia. Sote tunafahamu suala la urithi
ambalo chembechembe zetu za uhai hurithi kutoka kwa wazee wetu. Urithi huu
huwa na mchango mkubwa katika tabia, maumbile, nguvu na afya. Ukweli kuhusu
afya zetu ni kuwa, kwa kiwango kukubwa kabisa matatizo ya kiafya yanayotupata
huwa ni mchango wetu wenyewe katika miili yetu ambao hutoa ruhusa kwa huo
urithi kufanya kazi.

Ikiwa msomaji utapenda kutoa maoni au mchango wa kuboresha makala haya,


nakuombwa uwasiliane nami moja kwa moja kwa kutumia barua pepe;
mazizini@gmail.com au kwa simu; 008613917111448.

Utangulizi

Kwa kuwa napenda kufanya mazoezi, napenda pia afya yangu iwe nzima kwani
nikiwa na afya mbaya sitaweza kufanya au kufurahia mazoezi. Ni vizuri kuishi
maisha yaliyo huru badala ya kuishi maisha ya kifungo cha dawa na masharti ya
madaktari. Hapa nakusudia kuelezea hali ile ya mtu kulazimika kuwa na ratiba ya
kumeza dawa mara tatu, mbili au moja kila siku ili afanye shughuli zake za maisha.
Vijana wanasema mtu kama huyo haendi bila ya chaji, inabidi utie chaji ndipo
aende. Kila mara inakulazimu kuwa na dawa mfukoni, “ unatembea na betri” na
nyumbani umejaza dawa (umefungua Pharmacy). Dawa anayoitaka mtu basi
anaweza kuipata kwako. Hufika wakati ikabidi daktari akakushauri/akakupangia, “
Usile hichi, punguza hichi, kunywa maji mengi kula matunda kwa wingi ”.n k.
Ikishafika hali hii ya kuishi kwa miiko, raha ya maisha inakuwa haipo tena.

Kabla ya kutafakari tatizo la presha ya damu na uhusiano wake na maisha yetu


nitachukua muda mfupi kujitambulisha kwani kwa kufanya hivi na kila mtu
atajitambua na huenda akaanza kuchukua hatua kuichunga na kuipenda afya yake.

Umri wangu ni miaka 40. Nina urefu wa futi 5 inch 8 (174 cm) na uzito wa kilo 85.
Kwa sababu nilijizoesha kufanya mazoezi, ninapenda kufanya mazoezi kila
nipatapo nafasi. Kama kawaida ya watoto wanavyokuwa, na mimi nilikuwa
nikipenda kucheza mpira, kukimbia, kuruka na mengineyo mengi afanyayo mtoto.
Nilipoanza kusoma sekondari muda wa michezo ukawa haupatikani kikawaida na
idadi ya vijana tuliokuwa pamoja ilipungua. Ilibidi nifanye mazoezi ya peke yangu.
Nikaanza kukimbia joging na kufanya mazoezi ya viungo. Utaratibu huu nilidumu
nao nikiwa high school na hata nilipokwenda chuoni. Siku moja nilikwenda
hospitali kwa matatizo mengine lakini kabla ya matibabu, nesi alinipima presha na
kuniambia ipo juu. Hata hivyo sikushughulika. Nilifanya matibabu ya lile
nililoendea na hakuna jambo lolote lililonitokezea kwenye presha. Kwetu maradhi
ya presha sio mageni, pande zote mbili yapo, na vifo vingi huja kwa sababu ya
maradhi haya.

Nilipomaliza chuo na kuanza kazi, nikiwa na miaka 24 bado nilikuwa nikiendelea


na mazoezi. Ukiacha zoezi la kukimbia na la viungo, nilianza zoezi la baskeli.
Nilikuwa napanda baskeli kutoka mjini na kuelekea mashamba (Mkokotoni,
Matemwe, U/Ukuu, Paje na Fumba), zoezi lilokuwa likinichukua kuanzia dakika 45
mpaka saa 5. Kipindi hichi chote uzito wangu ulikuwa kilo 63.

Miaka mine baadae ( 1998) nilienda kusoma tena. Kutokana na sababu nyingi
sikuwa nikifanya mazoezi. Ndani ya miezi mitatu tu uzito wangu ulipanda na
kufikia kilo 72. Miaka miwili baadae (2000) nilioa, mfumo wa maisha ukabadilika.
Mambo yakawa mengi, muda wa kufanya mazoezi ukapungua na hata wakati kwa
ujumla ukawa hautoshi kwa ule wingi wa mambo.

Miaka tisa baadae nilijikuta nina kilo 84. Nilianza jitihada za kupunguza uzito
wangu. Niliamua kurudia zoezi la baskeli ambapo kila wiki nilifanya mara moja.
Kwa kipindi cha miezi mitatu niliweza kupunguza kilo 3 na kuwa na kilo 81. Wakati
nikiendelea na mazoezi nilipata nafasi ya kwenda kusoma chuoni ( 2009 ). Kama
mjuavyo kabla ya kwenda kusoma nje unapima afya yako, na unapofika pia
unapima tena. Vipimo vyangu havikuwa na matatizo yeyote

Nilipofika chuoni na kufanya vipimo, nikaambiwa presha yangu ipo juu kidogo
(154/97), kama ilivyokuwa miaka 19 ilopita nilipokuwa nakwenda kusoma
sikushtuka kwani niliona ndio kawaida kwa mimi. Nikiwa chuoni ndani ya mwezi
mmoja niliongeza kilo 4 na kuwa na kilo 85. Ilibidi nianze tena jitihada za
kushusha uzito, lakini kwa bahati mbaya nikapata tatizo mguu mmoja na hivyo
kushindwa kufanya mazoezi kwa kipindi cha mwezi mzima. Kilo 4 ziliongezeka
tena na kuwa na kilo 89. Baada ya kupata nafuu, ilibidi nianze na mikakati mipya
iliyonichukua miezi miwili na nusu kuweza kupunguza kilo 4 na kuwa na kilo 85
ambazo ninazo hivi sasa.

Kwa maelezo haya unaweza kupata mambo yafuatayo:-

1. Ninao urithi katika mardhi haya ya presha


2. Mazoezi ndio yaliyokuwa yakinisaidia kuiweka sawa presha
yangu
3. Uzito mkubwa ndio ulolitoa tatizo hili la presha kujulikana
4. Tabia ya kutokuwa makini kwenye afya (kutofanya mazoezi,
kutojua uzito sahihi kiafya, kutushughulika na vipimo) kunatoa
mchango mkubwa katika maradhi mwilini.

Sasa tutafakari tatizo la presha.

Maradhi ya shinikizo la damu ( Presha) sasa yamekuwa tatizo kubwa dunia nzima.
Maradhi haya si mageni kama Ukimwi na kwa kiasi kukubwa watu wameshayazoea
na kuhisi kuwa ni ya kawaida. Kila siku hatari za magonjwa haya zinaongezeka. Si
kwamba zanakuja hatari mpya, bali yanjulikana magonjwa mengine ambayo kwa
kuchelewa au kutoitibu presha basi yanatoke na kushtuwa watu. Hata umefika
wakati mtu mmoja anakuwa na presha, sukari, matatizo ya moyo na matatizo ya
kuona, jambo ambalo linaonaekana kuwa geni na watu hufika kusema “ndio
mwisho wa dunia”. Bila shaka kila lenye mwanzo basi lina mwisho, hili hakuna
asiyejuwa.
Kwa hofu ya maradhi haya, watu hawataki kujua kama na wao tayari
wameshakuwa na presha, jambo linalopelekea kuwa na wagojwa wengi
wanaotembea na maradhi haya (walking booms) bila kujijua na
wanapokujajulikana tayari maradhi yanakuwa yamekuwa makubwa. Kama vile
watu wengine wanavyoogopa kupima ukimwi, pia watu wanaogopa kujua presha ya
damu zao. Utasikia watu wengine hasa vijana wakisema, “presha ni maradhi wa
watu wazima, vijana hawapati” hili si kweli kwani hivi sasa maradhi haya yanzidi
kuteremka kwenye umri mdogo kuliko zamani.
Tafsiri mbaya ya maendeleo ya sayansi na teknolojia yanachangia sana tatizo la
presha kwani mifumo yote ya maisha ya zamani sasa imeachwaa kabisa. Ulaji wa
vyakula halisi na maandalizi yake umewekwa mwisho, shughuli za kuutuma mwili
zimehamia kwenye mashine, miili haipati hata zoezi dogo la kutembea kwa miguu.
Tumebadili utaratibu ulio bora wa maisha kwa utaratibu usio bora.
Watu walio wazima hawazilindi afya zao mpaka wapate maradhi. Na kwa haya
maradhi ya presha wakishakuyapata watakachojitahidi ni kutokula chumvi, kuacha
vyakula vya mafuta labda na kunywa maji, lakini mfumo wa maisha unabaki
uleule. Mambo haya yanafanya maradhi haya kuwa tishio kadri siku
zinavyoendelea.
Umefika wakati tujizatiti kupambana na maradhi haya. Watu wanaoumwa na
maradhi haya ni wengi kwani kuna wanaojulikana na wasiojulikana. Kuna idadi
kubwa ya vijana wanaotembea na maradhi haya. Napendekeza : -
a. Vijana wasiache kufanya mazoezi,
b. Wanafunzi wawe na ratiba maalum ya mazoezi kama walivyo na ratiba za
masomo.
c. Tupime afya zetu na tuvifanyie kazi vipimo tunavyovipata,
d. Tubadili mifumo ya maisha,
e. Tufuatilie maradhi haya kwani ni chanzo kikubwa cha magonjwa mengine
makubwa mwilini.
f. Kwa kuwa chanzo kimoja ni urithi kwa maradhi haya, tuchunguze afya za
watoto wetu.

Yaliyomo

Nini Shinikizo la Damu

Viwango tofauti vya maradhi

Sababu na dalili zake

Vyanzo

Jinsia na umri

Urithi kwenye koo

Asili

Mlo

Mafuta mengi mwilini

Kuzongwa na mawazo

Unywaji pombe

Magonjwa ya figo

Utumiaji mkubwa wa madawa mwilini

Uzazi

Ulaji mkubwa wa vitu vitamu

Dalili
Presha kwa watoto

Maumivu ya kifua

Kuchanganyikiwa

Makelele masikioni

Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida

Kutokwa damu puani

Kuwa mchuvu kila mara

Kutoona vizuri

Kuzongwa na mawazo mengi

Kuwa mkali na hasira nyingi

Mtoto kutocheza kama wenzake

Matibabu

Hudhuria kituo cha afya

Badili mfumo wa maisha

Tumia dawa

Hitimisho

Chakula na maradhi

Ununzi wa vyakula
SHINIKIZO LA DAMU

Fahamu nini Shinikizo la Damu

Shinikizo la damau ni pale pressure ya mtu inapokuwa kubwa kuliko kawaida kwa
kipindi chenye kuendelea. Presha ya kawaida inakuwa haizidi 120 juu (systolic) na
80 chini (diastolic) — huandikwa hivi 120/80 mm Hg (read 120 over 80
millimeters of mercury). Daktari atakupima kila unapokwenda kupata matibabu,
na akiona kila anapokupima presha yako ipo juu, itakuwa unapresha tayari.

Ikiwa tayari umegundulika unapresha, ni lazima uchukue mazingatio makubwa


katika kukabili tatizo. Lazima uchukue njia nzuri na salama hasa ukizingatia
presha ni maradhi yenye kuangamiza. Kuna njia nyingi zitakazokufaa ikiwa ni
pamoja na kubadili utaratibu wa maisha unayoishi na matibabua tofautitofauti kwa
kusaidia kushusha presha yako.

Viwango tofauti vya maradhi.

Presha ya kawaida ni chini ya 120/80. Pale mtu presha yake inapokuwa kati ya
120/80 na 139/89, hali hii ni dalili ya kuwa na shinikizo la damu,
(prehypertension). Kiwango cha kwanza cha shinikizo la damu kinakuwa na
kipimo hichi 140/90 mpaka 159/99, na presha iliyo juu ya kiwango hichi, hiyo
inakuwa kiwango cha pili.

Viwango vya Shinikizo la damu

Presha ya Damu (mm Hg) Kiwango

Chini ya 120/80 Kawaida

120/80 mpaka 139/89 Dalili za Shinikizo la damu


140/90 mpaka 159/99 Kiwango cha kwanza cha
shinikizo la damu

160/100 na zaidi Kiwango cha pili cha shinikizo la


damu

Sababu na dalili zake

Nini sababu za shinikizo la damu?

Takriban asilimia 85% mpaka asilimia 95% ya watu wenye shinikizo la damu
hazijulikani sababu zilizowapelekea maradhi hayo. Hata hivyo vipo vyanzo
ambavyoo hupelekea kuwa sababu za kupata maradhi hayo.

Vyanzo

Jinsia na Umri.

Hatari ya kuwapata maradhi haya huongezeka sambamba na kuongezeka umri.


Tatizo hili hupatikana zaidi kwa wanaume hasa kuanzia miaka 45. Lakini kuanzia
umri wa miaka 45 mpaka 54 , wanaume na wanawake wanakuwa katika hatari ya
kupata maradhi haya.

Baada ya umri wa miaka 54, wanawake wanakuwa katika hatari kubwa zaidi ya
kupata maradhi haya kuliko wanaume. Hapa tunapata funzo kuwa homoni za kike
( estrogen ) ni kinga kubwa kwa maradhi haya. Inafikiriwa kuwa homoni za kike
( estrogen ) zinasaidia kuifanya mishipa ya damu kuwa laini ( flexible). Estrogen
pia hufanya kazi na homoni nyengine na kupunguza hatari ya kupata maradhi haya
kwa wasichana.

Wanaume
Shinikizo la damu huongezeka kadri umri unavyoongezeka. Shinikizo hili huanza
kuwa kubwa kwa wanaume pale wanapovuka miaka 45, japokuwa linaweza kuwa
kubwa chini ya umri huo. Watu wenye asili ya Afrika na Amerika hupata tatizo hili
wakiwa na umri mdogo. Mafut mengi mwilini, urithi kwenye koo pia huharakisha
kujitokeza tatizo hili.
Shinikizo la damu ni hatari kwani watu wengi wanakuwa nalo bila kulijua kwa
miaka mingi. Japokuwa maradhi haya hayakimbiliki, zipo njia nyingi za kukinga na
kutibu kwa kufuata maelekezo.

Urithi kwenye koo.

Watu wenye historia ya maradhi haya ndani ya koo zao, ni rahisi na wao kupata
maradhi haya.

Asili (Ethnicity).

Waafrika waliochanganya na Waamerika na Waamerika asili wamegundulika kuwa


na kiwango kikubwa cha maradhi haya. Na tatizo hili limeonekana kuwa kubwa
kwa watu wenye asili za Afrika.

Mlo (Diet).

Watu wanaotumia chakula chenye chumvi nyingi, hupata maradhi haya haraka.

5. Mafuta mengi mwilini (Obesity).

Obesity ni hali ya kuwa na mafuta zaidi ya kiwango kinachohitajika mwilini. Kuwa


na kiwango cha ziada ya mafuta mwilini ni hatari kuliko kuwa na kansa ya ngozi,
kwani, afya yako inakuwa hatarini kwa kukabiliwa na maradhi ya kisukari na
shinikizo la damu. Kuwa na mafuta mengi mwilini na kuwa na uzito mkubwa ni
mambo mawili yanayofuatana.

Japokuwa zipo hali chache hutokea, mtu akawa na uzito mkubwa lakini hana
mafuta mengi mwilini na mwengine akawa na uzito wa kawaida na akawa na
mafuta mengi mwilini. Lakini hali hizi ni za kipekee.

Madaktari hufanya mahesabu kwa kutumia urefu na uzito wako, hesabu


zinazojulikana “body mass index “(BMI) — kufahamu ikiwa uzito ulionao ni salama
au la. Mtu mzima mwenye BMI 30 au zaidi atakuwa na uzito usio salama. Zaidi ya
BMI 40 ni mbaya sana. Ukishakuwa na BMI zaidi ya 40 utakuwa ukiandamwa na
matatizo makubwa ya afya.

BMI Hali ya uzito


Chini ya 18.5 Uzito mdogo
18.5 — 24.9 Kawaida
25.0 — 29.9 Uzito mkubwa
30.0 na zaidi Obese (mafuta)

Kwa kutumia BMI yako, jinsia na umri wako wataalamu wanaweza kufahamu
wingi wa mafuta mwilini mwako na kuweza kukushauri namnagani ya kubadili
mfumo wa maisha yako upate kuwa na afya njema. Hata hivyo ikiwa una hali ya
kupata ganzi mara kwa mara kwenye miguu au mikono na hasa unapokuwa na
uzito mkubwa inawezekana kabisa ukawa na mafuta mengi mwilini.

Bado makundi mawili ya wataalamu yanapishana katika kiwango halisi cha uzito
wa mtu kwa urefu wake. Tofauti iliyopo ni kilo 6. Lakini mimi na wewe tujue kuwa
kuwa na uzito mkubwa si salama.

Kwa kufuata makundi hayo, mtu mwenye urefu wa cm 174 anatakiwa awe na uzito
wa kilo zisizozidi 63 au 70. Itakapokuwa mtu huyu anakilo 80 au zaidi basi tayari
atakuwa na uzito mkubwa. Uzito huu utampelekea kuwa na hatari ya kupata
maradhi mengi pamoja na shinikizo la damu. Tutizame table hii katika kutuongoza
kwenye uzito ulio salama.

Uzito kwa urefu ulio salama


S/n Urefu katika cms Uzito katika kgs Urefu katika cms Uzito katika kgs

Wanaume Wanawake

1 157.5 53.5 – 57.1 147.5 43.5 – 48.5

2 160.0 54.8 – 60.3 150.0 44.4 – 49.9

3 162.5 56.2 – 61.6 152.5 45.8 – 51.2

4 165.0 57.8 – 63.0 155.0 47.1 – 52.6

5 167.5 59.0 – 64.8 157.5 48.5 – 53.9

6 170.0 60.7 – 66.6 160.0 49.9 – 55.3

7 172.5 62.6 – 68.9 162.5 51.2 – 57.1

8 175.0 64.4 – 70.7 165.0 52.6 – 58.9

9 178.0 66.2 – 72.5 167.5 54.4 – 61.2

10 180.0 68.0 – 74.8 170.0 56.2 – 63.0

11 183.0 69.8 – 77.1 172.5 58.0 – 64.8

12 185.5 71.6 – 79.3 175.0 59.8 – 66.6

13 188.0 73.4 – 81.6 178.0 61.6 – 68.4

14 190.5 75.7 – 83.9 180.0 63.5 – 70.3

15 193.0 98.0 – 86.1 183.0 65.3 – 72.1

Ukishaona una uzito mkubwa halafu mara kwa mara unapata ganzi unapokaa au
kulala ama miguuni au kichwani, kichwa kinakuuma upande mmoja na wakati
mwengine jicho linachezacheza, macho yako yanakuwa mekundu sana usipuuze,
pima presha yako. Dalili hizi ni ufikaji pungufu wa damu katika maeneo husika
kutokana na wembamba wa mishipa yako ya damu.

Kuzongwa na mawazo (Stress).

Inavyoonekana watu wenye mawazo mengi na hasira, wanapata maradhi haya


maramoja.

Kuzongwa na mawazo (Stress) na shinikizo la damu havina uhusiano, lakini


jitihada za kuondoa mawazo kunasaidia kujenga afya yako sambamba na
kupunguza shinikizo la damu.

Kuzongwa na mawazo kunasababisha presh yako kupanda kwa muda ule


ulozongwa tu, hakuna ushahidi wa kuonyesha kuwa presha hiyo itaendelea kubaki
juu hata utakapokuwa katika hali ya kawaida.
Wakati mwingi watu huzongwa na mawazo pale wanapohangaika kutafuta
ufumbuzi wa jambo na kushindwa. Mfano mtu anaumwa anakwenda hospitali
maradhi yake hayagunduliki anahangaika kwa muda mrefu akibadili hospitali na
madaktari lakini hapati mafanikio hata akifika kukata tama , jambo hili huweza
kumfanya akaishi na mawazo muda mrefu.

Lakini mtu huyu ikiwa anafanya mazoezi, anashiriki katika shughuli za kijamii
kama tayari alikuwa na shinikizo la damu basi presha yake itakuwa nafuu na
kutopanda mara kwa mara.

Namna mwili unavyokuwa katika hali ya kuzongwa na mawazo.

Kuzongwa na mawazo tafsiri yake mwilini ni mwili kuwa tayari kupambana.


Wakati unapokuwa umezongwa na mawazo, mwili huzalisha homoni ambayo
hukuandaa ama upigane, ukimbie au ufanye lile ambalo litakuwa suluhisho la
tatizo ulokuwa nalo.

Hali hii ya mwili kujiandaa ilikuwa na manufaa makubwa kwa watu wa kale pale
wamapokutana na wanyama wakali kama simba au hatari nyenginezo. Lakini hata
leo mwili wako unaendelea kufanya kama ulivyokuwa ukifanya kwa watu wa kale
isipokuwa badala ya hatari zile za watu wa kale, sasa utapambana na majanga ya
moto, hatari za kwenye usafiri au mivutano kwenye makundi ya watu.

Ukizingati maisha tunayoishi sasa yote yametawaliwa na mambo yanayoiweka


miilimyetu kuwa tayari kila saa, huhitajiki kupigana wala kukimbia na wakati
huohuo mwili unaendelea na maandalizi kamavile hatari ipo usoni. Hali hii
huongeza presha yako na kusababisha mapigo yako ya moyo kuwa juu na miships
yako ya damu kufanyika membamba.

Uhusiano wa kuzongwa na mawazo na shinikizo la damu bado haufahamiki vizuri.

Bado sababu ya kuwa na uzito mkubwa unaotokana na kula sana, unywaji wa


pombe na kutolala vya kutosha husababisha shinikizo la damu.

7. Unywaji wa pombe

Magonjwa ya figo

Utumiaji mkubwa wa madawa mwilini

Uzazi
Ulaji mkubwa wa vitu vitamu ( sukari nyingi mwilini )

Uchunguzi unaonyesha upo uhusiano kati ya wingi wa sukari na


kuongezeka presha ya damu, lakini bado wataalamu hawajashawishika
na hoja hii.
.Kwanini ulaji mkubwa wa vitu vitamua waweza kukupatia shinikizo la damu?
Ijilikane kuwa sukari (fructose) inauwezo wa kupunguza uzalishaji wa asidi (nitric
oxide) ndani ya mishipa ya damu. "Nitric oxide huifanya mishipa ya damu kuwa
na uwezo wa kupunguza presha ya damu. Sukari (Fructose) hupunguza uzalishaji
wa asidi (nitric oxide) na huifanya mishipa kutoweza kufanya kazi yake vizuri.
Pia sukari (Fructose) huongeza uzalishaji wa asidi (uric acid) ndani ya damu
ambayo inasaidia kuongeza presha ya damu. Sukari huisababisha Figo (kidneys )
kuendelea kuwa na chumvi nyingi ambayo inaweza kuchangia kuongezeka presha
ya damu.
Vipi kuhusu vinywaji vitamu vya viwandani?
Vinyaji vya kiwandani sukari yake ni ya kupangwa. Hapajakuwepo na ushahidi
mkubwa wa kuweza kusema navyo vinaongeza sukari nyingi mwilini kwani si kila
mara watu hutumia vinyaji kutoka viwandani. Bado vyanzo vya maradhi haya
vinabakia vile vile.
Vipi basi kuhusu matunda matamu?
Matunda yanaupa mwili uwezo wa kupambana na maradhi. Matunda yana sukari
ya asili ambayo kiwango chake hakifanani na kile kiwango cha sukari inayotiwa
katika vinywaji vya kiwandani. Mbali na sukari, matunda yanavirutubisho
ambavyo mwili unahita kwa ujenzi na ulinzi. Bado sukari mwilini haijawa chanzo
kwa shinikizo la damu, lakini kumbuka chochote ikiwa kitazidi sana mwilini
kinaleta madhara.
Vipi basi kuhusu asali ?
Asali ni dawa. Kama vile tunda la epo linavyoingia moja kwa moja ndani ya
mishipa ya damu na kufanya kazi, na asali hufanya hivyohivyo. Kula asali
kunasaidia kuijenga upya mishipa yako ya damu ambayo imepata matatizo ya
presha na ikiwa huna presha, kufuata taratibu za kiafya na kula asali kutakupa
kinga nzuri kwenye mishipa yako ya damu.

Dalili za shinikizo la Damu


Watu wenye shinikizo la damu kwa kawaida hawapati dalili zozote mpaka presha
yao inapukuwa juu, au presha hiyo iliyo juu kudumu kwa muda mrefu. Katika hali
hii, uharibifu katika viungo muhimu mwilini hutokea, viungo hivyo ni pamoja na
moyo, ubongo na figo, pia uharibifu huu hufika katika mishipa midogo ya damu
kwenye macho. Ni muhimu kufahamu kuwa, ikiwa hapatakuwepo na matibabu ya
maradhi haya basi madhara makubwa yatatokea.

Fahamu: Watoto nao wanakuwa na maradhi ya presha


Ilivyokuwa chanzo kimojawapo cha presha ni urithi, ni wazi tufahamu kuwa hata
watoto huwa na presha. Jambo linalosaidia katika umri mdogo ni harakati nyingi
ambazo mtoto anakuwa nazo ambapo anapata zoezi la kutosha, anakunywa maji
mengi, kwa vile mwili wake upo katika harakati za makuzi, hawi na uzito mkubwa
wenye kudumu, hazongwi na mawazo yeyote kwani wapo watu wa kumfanyia
karibu mambo yake yote ( chakula, malazi, mavazi na elimu ). Lakini anapoanza
kujitegemea halafu akabeba majukumu (kuoa/kuolewa na mengineyo) na umri
wake kuanza kukaribia/kufika ukingoni mwa ujana (miaka 40/45), tatizo la presha
huanza kujitokeza.

Uharibifu wa mishipa ya damu

Kwa kawaida misipa ya damu ni yenye kupindika, yenye nguvu na inavutika. Ndani
ya mishipa ni laini kiasi damu inapita kwa urahisi kuelekea kwenye viungo. Ikiwa
una shinikizo la damu, presha yako itasababisha

a. Uharibifu wa cells ndani ya mishipa yako utakaopelekea kuifanya


kuwa migumu na kusababisha mishipa kuwa membamba na
kutoruhusu damu ya kutosha kufika katika viungo vyako.

b. Kitendo cha mishipa kuharibika eneo la ndani, husabaisha kufanya


bofu, bofu ambalo likipasuka husababisha kutoka damu ndani kwa
ndani (internal bleeding).

Uharibufu wa moyo

Moyo wako hupeleka damu mwili mzima. Usukumaji wa damu usio wa kawaida
unaharibu moyo katika namna nyingi. Namna hizo ni pamoa na zifuatazo :

a. Misipa ya moyo kuwa membamba na kutopeleka kiwango


kinachohitajika cha damu mwilini.
b. Moyo kutanuka na kuwa mkubwa.

c. Kusimama kwa mapigo ya moyo kunakotokana na misuli ya moyo


wako kuwa dhaifu kwa kazi kubwa ya kusukuma damu.

Uharibifu kwenye ubongo

Kama ulivyo moyo, ubongo nao unategemea damu safi ya kutosha ili ufanye kazi
sawasawa. Shinikizo la Damu husababisha matatizo yafuatayo :

a. Stroke ndogo. Hii hutokea baada ya damu kuganda maeneo ya


ubongo. Matokeo makubwa ni kupata Stroke kubwa.

b. Stroke kubwa. Hii hutoke baada ya kukosekana oxygen na virutubisho


kwenye ubongo ambavyo hupelekea cells za ubongo kufa.

Kujua dalili za stroke ni hatu ya kwanza kuzuia isitokee. Stroke, Kwa jina jengine
"kuathirika kwa ubongo," ina dalaili zifuatazo: -

1. Kuumwa na viungo hasa miguu au mikono. Hali hii hutokea kama mtu
aliyeanguka hali hajaanguka. Watu hufikia hatua ya kuchua viungo
hivyo.
2. Kuwa dhaifu au kukosa hisia usoni, mikononi au miguuni upande mmoja
tu wa mwili.
3. Kupoteza uwezo wa kuona au kutoona vizuri jicho moja au yote mawili.
4. Kutoweza kusema, kusema kwa tabu au kutofahamu
kinachozungumzwa.
5. Kuanza ghafla kuumwa sana na kichwa bila kuwepo na chanzo chochote.
6. Kushindwa kutembea au kutembea kwa kuyumbayumba.

c. Kuchanganyikiwa na kuanza kusema, ovyo kupiga makeele na


mambo mengine yanayohusu fahamu.

d. Kupoteza kumbukumbu na ufahamu.

Uharibifu kwenye figo

Figo huchuja majimaji ya ziada na chochote kisichohitajika kwenye damu —


kitendo kinachotegemea mishipa ya damu iliyo mizima. Shinikizo la damu
huharibu mishippa ya damua inayokwenda kwenye figo na kusababisha maradhi
ya figo. Kuwa na kisukari pamoja na shinikizo la damu hupelekea kuongezeka
haraka uharibifu katika figo kama ifuatavyo:

a. Figo kusimama kufanya kazi.

b. Figo kushindwa kuchuja maji na vitu vingine visivyohitajika kwenye


damu.

c. Mishipa ya damu kufanya mabofu na kuweza kupasuka.

Pamoja na kutokuwepo dalili halisi za maradhi haya, mgonjwa anaweza kutokewa


na mambo yafuatayo kufuatia uharibifu uliokwisha fanyika bila kujulikana mwilini
mwake.

1. Maumivu ya kifua ( kifua kubana )

2. Kuchanyikiwa

3. Makelele masikioni

4. Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida

5. Kutokwa damu puani

6. Kuwa mchovu kila mara

7. Kutoona vizuri kama kawaida yake

8. Kuzongwa na mawazo mengi

9. kuwa mkali na hasira nyingi

10. Kwa watoto, wakati mwengine kutomudu kucheza kama


wenzake.
Matibabu
Nini kifanyike baada ya kuziona dalili za kuwa na presha ?
1. Kuanza kuhudhuria kituo cha afya kwa hatua za matibabu

Jee unautaratibu ulojipangia wa kupima presha yako?

2. Kubadili mfumo wako wa maisha.

Hatua muhimu katika kuzuia na kutibu presha ni kuishi kwa kufuata taratibu za
kiafya. Unaweza kushusha presha yako kwa kubadilika katika hali zifuatazo:

i. Kupunguza uzito ikiwa unauzito mkubwa au mafuta mengi mwilini.

Njia za kupunguza uzito zipo nyingi, lakini hapa nitazitaja 16 ambazo unaweza
kuzitumia katika kupunguza uzito.

1. Kula polepole ( jipangie kula kwa muda usiopungua dakika 20 )

Huu ni utaratibu mzuri wa kupunguza mwili. Unapokula taratibu, mwili hupata


kufanya kazi yake vizuri na kiwango cha chakula kinachotosha kwa mwili kikifika,
basi mwili hukataa kula zaidi. Lakini unapokula haraharaka mwili unashindwa
kufanya kazi yake ya kupima kiwango cha chakula na hivyo kujikuta unakula
mpaka unavimbiwa.

2. Kulala masaa mengi


Kulala saa nyingi kunasaidia kupunguza uzito. Uchunguzi unaonyesha unapolala
muda mrefu mwili wako unaepukana na kuhitaji nguvu nyingi kwa shughuli za kazi
na kufikiri. Kushughulika sana na kazi kunaufanya mwili kuhisi njaa na kuhitaji
chakula sana.

3. Kula mbogamboga kwa wingi hasa wakati wa chakula cha usiku

4. Kutanguliza kitu kabla ya kula

Kutanguliza kitu kabla ya kula chakula kunasaidia kukata njaa na hivyo


kutokufanaya kula chakula kingi. Ni mazoea hasa katika mahoteli makubwa,
huwekwa supu na watu huanza kwa kunywa supu halafu ndio huchukua chakula.
Aghalabu supu hii huwa si ya mafuta.

5. Kula nafaka

Kula vyakula vya nafaka isiyo kobolewa kunasaidia sana kupunguza uzito.
6. Kuacha kunywa chai nzito asubuhi

Kujenga utamadunui wa kutokula mlo mzito asubuhi kunasaidia kupunguza uzito.

7. Kupendelea kutumia matunda ( Jam ) kupaka mikate

Kupendelea kupaka jam au kutumia kiteweo kisichokuwa na mafuta kwa chai, na


kupunguza kupaka siagi nyingi kwenye mikate kunasaidia kupunguza uzito.

8. Punguza kula/kunywa sana vitamu

Kupunguza unywaji mkubwa wa vinywaji vyenye sukari kwa wingi


vilivyotengenezwa viwandani.

9. Acha unywaji wa pombe

10. Kunywa muarubaini

Kunywa chai ya kijani au muarubaini. Chai ya kijani waweza kuipata madukani


hasa kwenye supermarket, au kuchukua majani kidogo ya muarubaini kutia katika
kikombe chenye maji yamoto na kusubiri kiasi cha dakika mbili. Huna haja ya
kuyachemsha pekeyake kama nyungu. Unaweza kujenga mazoea ya kunywa kila
unapopata wasaa.

11. Pendelea kula nyumbani

12. Tafuna ubani

Kula ubani (chewingum) au kula muwa ( umenye na kutafuna mwenyewe )


kunasaidia kuongeza kasi ya usagaji wa chakula mwilini na uunguzaji wa mafuta.

13. Punguza chakula chako

Punguza chakula kwa kutumia sahani ndogo badala ya kutumia sahani kubwa kwa
kulia. Hivyo hivyo unaweza kupunguza hata glasi yako kubwa kwa vinyaji vitamu
hasa vya viwandani.

14. Agizia chakula nusu unapukula hoteli na uanze na supu

Kuwa na utamaduni wa kuagizia chakula nusu unapokula hotelini na pendele


kuanza na kitangulizi.

15. Pendelea kula mbogamboga na samaki badala ya nyama hasa za


wanyama

16. Unguza mafuta mwilini kwa zaidi ya Calories 100 kila siku
Jenga mazoea ya kutembea kwa miguu, kukimbia joging, kushughulikia bustani,
kufagia kiwanja cha nyumbani, kufanya kazi za usafi za ndani ya nyumba kama
kupiga deki, kukosha choo kupanga ukumbi na nyenginezo.

ii. Kuacha kabisa uvutaji wa sigara.

Utafiti wa kiafya unaonyesha kuwa, uvutaji sigara unaathiri moyo na mapafu. Pia
huongeza hatari ya kupata baadhi ya kensa. Kwa sababu hizi ni vizuri kuacha
uvutaji wa sigara.

Kwa vipi uvutaji sigara unaathiri mwili wako?


Uvutaji wa sigara unaingiliana na maradhi mengi makubwa makubwa. Pia
unaonekana kupunguza umri wakao wa kuishi. Baadhi ya madhara ya uvutaji wa
sigara ni pamoja na :

• Kukuongezea uwezekanao wa kupata kansa ya mapafu na kansa nyenginezo.


• Kukupatia shinikizo la damu.
• Kupunguza mwenendo wa damu mwilini.
• Kwa wanawake wajawazito huwasababishia kutokwa na damu na kupata
matatizo ya uzazi
• Kwa wanaume, husababisha tatizo la nguvu za kiume.

Matokeo
Unapovuta sigara, pumzi zako huwa kidogo na mapafu yako hujaa moshi. Uvutaji
sigara huingiza mwilini mwako sumu ya nicotine na tar.

Moshi wa sigara
Moshi wa sigara unakuwa na gesi ya carbon monoxide. Gesi hii huchukua nafasi
na kuingia katika damu yako kama ambavyo oxygen inavyoingia ndani ya damu.
Kumbuka kuwa carbon monoxide ni sumu.

Nicotine
Hii ni dawa inayoongeza presha yako ya damu na mapigo yako ya moyo.
Inapunguza mwendo wa damu kwenye mikono na miguu na pia hupunguza kasi ya
kuyeyusha chakula mwilini.

Tar
Huu ndio ukungu unaobakia katika mapafu yako baada ya kumaliza kuvuta sigara.
Ukungu huu hujijenga hata ukasababisha oxygen kidogo kupita na kuingia katika
mishipa yako ya damu.
Madawa mengine
Moshi wa sigara una zaidi ya madawa 4,000. Baadhi ya hayo ni pamoja na
formaldehyde, arsenic, na lead. Mengi ya haya madawa yaliyomo husababisha
kansa.

Unafahamu kuwa uvutaji wa sigara unatia upofu wa macho ?

Jambo hili si lenye kujulikana sana kwa vavutaji wa sigara na wasiovuta sigara
lakini huu ndio ukweli na wavutaji sigara walifahamu hili ili waweze kuchukua
jitihada za ziada kuepukana na uvutaji wa sigara.

Watu wengi wanafahamu ukohozi, kansa ya mapafu, maradhi ya moyo na stroke ni


magonjwa yanayohusiana karibu na uvutaji sigara. Lakini si wengi wanaofahamu
kuwa uvutaji sigara husababisha upofu wa macho.

Kumekuwa na mjadala unaoendelea namna ya kuongeza elimu kwa wavutaji wa


sigara kuhusu suala la upofu wa macho na uvutaji sigara. Japokuwa kuna
tahadhari katika pakiti ya sigara dunia nzima , Australia ndio nchi ya kwanza na
huenda ndio nchi pekee iliyoweka tahadhari ya kuwa "Uvutaji sigara unasababisha
upofu wa macho".

Hakuna mtu aliyetayari kupoteza uwezo wake wa kuona, labda na jambo hili liwe
kichocheo kwa vavutaji sigara kuacha haraka uvutaji wa sigara.

iii. Kula vyakula kwa maelekezo (kula matunda kwa wingi, mbogamboga, na
kupunguza kula mafuta kwa wingi).

Kula matunda kila siku ni jambo muhimu sana na hapa nitazungumzia tunda moja
kama mtu hapati matunda mchanganyiko basi hili litatosheleza.

Upo usemi “ Epo moja kila siku hukuweka mbali na daktari “

Nafahamu maepo ni ghali kwani ni matunda yanayoletwa kutoka mbali, na


matunda yanayofanana na hayo, ” matofaa” ni ya msimu.

Epo ni chanzo muhumu cha aina ya nyuzinyuzi ( fiber ) zote, zinazoyeyuka na


zisizoyeyuka. Kiasi cha asilimia 80 ya nyuzinyuzi katika epo ni zile zinazo yeyuka
ambazo husaidia kuharibu mfumo wa kujengeka mafuta mwilini yanayotokana na
mafuta tutumiayo ya kupikia ( cholesterol ) ndani ya mishipa ya damu na hivyo
kupunguza kwa kiwango kikubwa maradhi ya moyo na shinikizo la damu.

Nyuzinyuzi zisizoyeyuka zinazopatikana katika epo hukaa kwenya utumbo


mwembamba zikizuia maji na kuyafanya yachanganyike na chakula kwa haraka
kuelekea katika hali ya kuyeyushwa katika mfumo wa uyeyushaji chakula.
Epo lina vitamin C ambayo ni muhimu sana katika mfumo wa ulinzi mwilini. Nusu
ya vitamin C katika epo ipo katika gamba lake. Epo pia lina kiasi kidogo cha
vitamin A, calcium na potassium. Ni tunda tamu na epo lenye ukubwa wa kati
hukupatia karibu asilimia 80 ya nguvu ulilapo.

Mafuta mengi, chumvi nyingi na kula chakula kingi kunaharibu afya yako. Hizi ni
baadhi ya njia za kutumia ili kuepuka utumiaji wa mafuta mengi katika vyakula.
a. Chakula kiandaliwe kwa mafuta ya matunda badala ya samli au mafuta
mengineyo.

b. Acha /punguza kula mikate iliyopikwa na mafuta mengi ( maandazi,chapati) au


kupaka samli katika mikate.

c. Chukua tahadhari ya kutokula nyama nyingi au zenye mafuta mengi pamoja na


kunywa supu kila mara.

d. Pendelea kula vyakula vya kuchemsha, kuokwa, kuchomwa au kukaanga


kidogo.

iv. Kupunguza kiwango cha chumvi katika chakula chako unachokula kwa siku
kufikia 2,300 milligrams (kiasi kijiko kimoja kidogo cha chai) kwa siku au
pungufu zaidi .

Hapa kuna maana zaidi ya kutia chumvi katika chakula. Hapa ni kuondoa chumvi
mezani, kuchukua tahadhari na vyakula vyenye asili ya chumvi ( Ng’onda ).
Ikiwezekana chakula chako kisitiwe chumvi kinapopikwa ili utie mwenyewe.

v. Kufanya mazoezi ( kutembea kwa miguu kiasi cha dakika 30 kila siku).

Mazoezi: Njia isiyotumia dawa kushusha presha ya damu.

Kuwa na shinikizo la damu na kutokuwa na mazoezi ni mambo yanayofatana.

Hatari ya kupata shinikizo la damu huongezeka na umri, lakini kuwa na mazoezi ni


kinga kubwa sana. Na ikiwa tayari ushakuwa na presha ya juu, basi mazoezi
yatasaidia kuifanya isipande mara kwa mara. Huhitajiki sana kuamka kila asubuhi
na kufanya mazoezi makubwa ya kukuchosha bali unahitajika kupata mwendo wa
nusu saa kila siku ikiwa ni zoezi lako.

Unaweza kujipangia utaratibu wa kwenda au kurudi kazini kwa miguu badala ya


kutumia chombo cha usafiri.

Kwa vipi mazoezi yanaweza kushusha presha yako ?


Mahusiano ya presha na mazoezi ni kuwa, unapofanya mazoezi moyo wako
unaimarika. Moyo imara unasukuma damu nyingi bila ya kutumia nguvu kubwa.
Ikiwa miyo wako dhaifu, msukumo wa damu kwenye mishipa hupungua na
kusababisha presha ya damu kupungua.

Kuhakikisha presha iko sawa, unahitaji kuendelea na mazoezi . Kwa kawaida


huchukua mwezi mpaka miezi mitatu kupatikana kwa athari za mazoezi
yenyekuendelea mwilini mwako. Faida za zoezi hubakia muda mrefu kadri
unvyoendelea kufanya mazoezi.

Kiasi gani cha mazoezi unahitaji kufanya ?

Mazoezi ya viungo kama kuinua vitu vizito ni muhimu kimipango kwa kuuweka
mwili katika hali imara, mazoezi haya husaidia sana kuweka presha yako sawa kwa
kule kutumia hewa iliyo ndani ya mapafu yako na kuufanya moyo wako upige
harakaharaka.

Zoezi lolote litakaloongeza mapigo ya moyo na kupumua kwa kutumia hewa


kwenye mapafu linafaa. Kukimbia, kulima, kusafisha sakafu, kufagia kiwanja –
kitendo kitachopelekea utumiaji wa nguvu kinafaa. Mazoezi mengine ni pamoja na
kupanda sehemu za juu kama vilima, kupiga push up, kukimbia jogging, kuruka
kamba, kutembea kwa miguu, kuendesha baskeli na kuogelea.

Lakini zoezi lazima liwe na malengo ya kutimiza si pungufu ya nusu saa kwa zoezi la
taratibu na ikiwa ni la kasi basi unaweza kukisia muda kwa uzoefu. Ni vizuri zoezi liwe
lenye kuendelea sio la kukatisha katisha ili kupata athari za zoezi mwilini.

vi. Acha kunywa pombe.

Pombe na afya yako kiakili

Namna gani pombe inaathiri ubongo na nini athari za kunywa pombe sana.

Kwanza unapaswa ufahamu kuwa Ubongo ndio kiungo kinachoongoza shughuli


zote za viungo vyengine mwilini, kuona, kusikia, kuhisi, kuamua, kupumua. Hivyo
ni kiungo kinachohitaji hifadhi ya nje na ya ndani. Utaona hata namna ubongo
ulivyohifadhiwa na gamba gumu (bufuru la kicha) ili kuupa ulinzi wa hali ya juu.

Kinyume kabisa na watu wanavyofikiria kuwa pombe ni kiburudisho, pombe sio


kiburudisho – inachofanya pombe ni kuufanya ubongo usifanye kazi yake
sawasawa. Wakati kiwango kidogo kinapoingia mwilini kinakufanya ujisikie vizuri,
kadri kiwango kinavyoongezeka mambo huwa kunyumenyume.

Khofu na unyonge
Kwa muda mfupi tu pombe ndio hukuondolea mawazo mazito na hali mabya
ambayo unajisikia. Hii ndio sababu baadhi ya wanywaji hutumia pombe
kujisahaulisha matatizo yao , lakini baadae pombe huyafanya matatizo kuwa
makubwa na ya kudumu. Kumbuka kitendo cha mtu kuwa katika hali ya khofu na
unyonge kinamsababishia mwili wake kuwepo katika hali ya kukabiliana na hatari
ambazo ubongo unafikiri zitatokea. Mapigo ya moyo wa mywaji huongezeka muda
wote akiwa katika hali hii. Hali hii humuweka katika hatari ya kupata shinikizo la
damu.

Ukiacha tatizo la presha, mnywaji pombe ataingia katika matatizo mengine


ambayo ni pamoja na:

Makosa ya jinai na kujiua


Upo uhusianao mkubwa kati ya makosa ya jinai, pombe na watu kujiua wenyewe

Uwezo wa kutokuwa na kumbukumbu


Pombe hupelekea ubongo kutofanya kazi sawasawa na kutokuwa na kumbukumbu.
Baada ya muda mfupi kunywa pombe, uwezo wako wa kukumbuka unapungua.
Kiwango kikubwa hupelekea kupoteza kumbukumbu kwa muda mfupi au kwa
muda mrefu. Kunya pombe kwa siku nyingi huwa na madhara ya muda mrefu.

Pombe huathiri sehemu nyingi za ubongo na kusababisha ukuaji mbaya. Unywaji


wa pombe wa muda mrefu husababisha ubongo kupata tabu kukumbuka mambo
ya zamani na hata ya sasa.

Ni muhimu sana kwa vijana hasa wenye umri wa miaka 18 au 19 kwa sababu bado
ubongo wao unaendelea kukua. Vijana wanaoanza kunywa umri mdogo sana wana
hatari ya kupata maradhi ya akili.

Kunywa Maji
Wingi wa kunywa maji ni kinga ya magonjwa mengi, hata hivyo madaktari
wanasema watu wenye maradhi wanahitaji kunywa lita moja (Glasi 5) zaidi ya watu
wazima, ambao wao lazima wapate si pungufu ya lita mbili (glasi 10) za maji kwa
siku. Hii ndio kusema wagonjwa ni muhimu kwao kupata kiasi cha lita tatu (glasi
15) za maji kila siku.

Unywaji wa maji kwa mtu mwenye afya unategemea mambo mengi kama, hali ya
hewa, kiasi cha kazi azifanyazo, kiasi cha afya yake, ukubwa wa mwili wake, na hata
chakula anchokula. Mahitaji a maji mwilini yanaongezeka kutokana na wingi wa
shunguli azifanyazo na hali ya hewa. Katika hali hiyo, watu wengine watahitaji
marambili ya kiwango cha maji ambacho watu hunywa katika mazingira yao.
Watu wanashauriwa kunywa lita mbili (glasi 10) za maji kwa siku kwa sababu
kiwango chengine wanakipata kwenye maziwa, kahawa, chai, matunda,
mbogamboga na vyakula vinginevyo. Ni vizuri ukafahamu kuwa maji mwilini
hayapatikani kwa kunywa maji yenyewe tu bali ni katika vyakula vinginevyo pia, na
hapa utaona kuwa mwili unahitaji maji mengi kwani ikiwa maji mengine huingia
kwa njia nyinginezo na bado mtu mwenye afya kamili analazimika kunywa lita
mbili za maji, basi aliye na maradhi anahitajika kuongeza lita moja ya ziada.

Jambo moja la kuzingatia ni kuwa, kunywa kahawa nyingi kunasababisha mwili


kupoteza maji kwa kukojoa mara kwa mara. Hata hivyo si kwamba hupelekea
upungufu wa maji mwilini, kwani athari yake ni ndogo mno.

Watu wachache wanafahamu kuwa kunywa maji mengi kusikoendana na kula


chakula kingi kunasaidia kupunguza uzito wa mwili. Mpango wowote wa
kupunguza uzito wa mwili ni vyema uendane na unywaji wa maji mengi kwani
utalijaza tumbo maji na utaongeza kasi ya uyeyushaji wa chakula mwilini.

Kumbuka kuna uzalishwaji mkubwa wa sumu na chumvichumvi mwilini kutoka


katika vyakula tulavyo ambao unahitaji kutolewa nje. Jambo la kushangaza, watu
wengi hubadili kiu kuwa njaa na badala ya kunywa maji hula vyakula kunyume na
mahitaji ya mwili wakati ule.

Sambamba na hili, wale watu waliopoteza maji mengi ikiwa kwa kutapika, au
kuharisha wanahitajika kunywa maji mengi zaidi ili kutoa madini ya sodium
ambayo ni chanzo cha upungufu wa maji mwilini. Kundi la wazee lazima lizingatie
sana unyaji wa maji kwani wazee wengi hawahisi kiu sana kitendo ambacho
kinawaweka katika hali ya kuwa na upungufu wa maji mwilini.
3. Matumizi ya Dawa

Athari za dawa unapozitumia.

Ukihisi dawa unazotumia zinakuletea matatizo, fanya utafiti kuona kama ni hizo
dawa unazotumia au ni kitu chengine. Hii ni muhimu kwa dawa yeyote
utakayotumia, sio kwa dawa za presha tu. Japokuwa maelekezo mengi ya dawa
yatakufahamisha namna inavyofanyakazi mwilini. Hii inamaana kuwa dawa si
hatari kutumia kama inavyoonekana na kusikika na watu wengi, kwani ufanyaji
kazi wa dawa (kama kuumwa na kichwa, kutia usingizi, uchovu, kutaka kutapika,
nk.) hutokea kwenye dawa za uwongo (feki). Hata hivyo, fuata maelekezo ya
daktari na unapoona jambo lolote basi urudi tena kwa daktari wako kwa ushuri na
maelekezo mengine. Hakikisha siku zote unamuona daktari ili akupe maelekezo
kamili kabla ya kubadili mwenendo wa matumizi ya dawa aliokupangia, kuanza
matumizi ya dawa nyengine au kuacha kutumia dawa alokupa. Jenga uhusiano wa
karibu na daktari wako ili upate maelekezo ya mara kwa mara.

Mtazamo wa matibabu ya shinikizo la damu

Shinikozo la damu ni hatari kwa sababu linapelekea kupata stroke, kusimama


kufanyakazi moyo, moyo kushindwa kufanyakazi sawasawa au maradhi ya figo.
Malengo ya tiba kwa shinikizo la damu ni kushusha presha na kuvilinda viungo
muhimu vikiwemo Ubongo, moyo, na figo visiathirike. Inaaminika kuwa matibabu
ya shinikizomla damu yameweza kupunguza stroke (35%-40%), maradhi ya moyo
(20%-25%), na moyo kushindwa kufanya kazi (kwa zaidi ya 50%).
Wagojwa wote wenye presha inayozidi kiwango hichi 120/80 lazima wasisitizwe
kubadili mifumo ya maisha wanayoishi na kuanza maisha mapya ambayo ni
pamoja na kula vyakula kwa utaratibu wa kiafya ( healthier diet ), kuacha uvutaji
wa sigara, na kufanya mazoezi kila siku.
Matumizi ya dawa ni muhumu sana ili kushusha presha iliyo juu ya kiwango hichi
140/90 mmHg.
Kwa wagonjwa wenye Kisukari au maradhi ya figo, mapendekezo kwao ni presha
yao iwe chini ya kiwango hichi 130/80 mmHg.
Matibabu ya shinikizo la damu yanakwenda sambamba na kubadili mfumo wa
maisha na bila shaka matumizi ya dawa.

Unaweza kuishusha presha yako kwa kutumia dawa zilizo nzuri. Dawa inategemea
na mwili wako. Dawa hiyohiyo yaweza kuwa inawafaa sana watu wengine lakini
wewe isikufae, ndio kusema kwa wewe itakuwa si nzuri. Italazimika ubadilishiwe
nyengine.
Uchaguzi wa dawa ya Presha.

Uchaguzi wa dawa ya presha ni jambo gumu. Ni jambo la kujaribu ili kupata dawa
inayokufaa.

Kuna dawa chungunzima za kutibu presha hivi sasa ambazo zina hasara zake na
faida zake katika matumizi. Kwa kutegemea kiwango chako cha presha , daktari
atakupatia aina moja au mbili za dawa kwa matibabu. Kwa mtu yeyote ambae
tayari ana shinikizo la damu au anahatari ya kupata shinikizo la damu, kubadilisha
utaratibu wa maisha kama ambavyo tumeelezea kutasaidia sana. Kabla ya kuanza
matumizi ya dawa ni vizuri kufahamu hali tofauti zilizopo.

Kwa wenye presha ya juu na wale ambao wameanza kupata dalili za kuwa nayo
(120/80 to 139/89)

Ikiwa umeanza kupata dalili za kuwa na presha (prehypertension) au tayari


ushakuwa nayo (hypertension), kubadili mfumo wa maisha kutasaidia sana
kushusha presha yako.

Hata ikiwa daktari atakupa dawa kutibu presha yako, bado atapendelea ubadili
utaratibu wa maisha yako kwani kufanya hivyo kutasaidia kupunguza au kuacha
kabisa kutumia dawa. Mabadiliko haya ya maisha ni pamoja na :

α. Kuacha uvutaji sigara.

β. Kula vyakula kwa utaratibu wa kula matunda, mbogamboga, vyakula vyenye


mafuta kidogo na kuzingatia matumizi ya chumvi.

χ. Kuchunga uzito wako (uzito hufuatana na urefu wako).

e. Kufanya mazoezi kwa dakika 30 kila siku. Hata ikiwa utapumzika pumzika
lakini lengo liwe ni kutimiza muda wa dakika 30.

f. Kuacha kunywa pombe.

Huhitajiki kutumia dawa ikiwa presha yako ndio kwanza inaanza, lakini ikiwa pia
una na kisukari, maradhi ya figo au maradhi a moyo daktari atakupatia dawa ili
kuishusha na kuiweka katika hali ya kawaida.

Watu wenye Presha hatua ya kwanza (140/90 to 159/99)

Katika hali hii utalazimika kutumia dawa na kubadili mfumo wako wa maisha. Kwa
mtumiaji wa mara ya kwanza, daktari atakupa dawa moja tu. Inashauriwa dawa
utakayoanza nayo uendelee nayo. Usibadilishebadilishe dawa. Na wakati mzuri wa
kumeza dawa ni asubuhi (saa 1 – 4). Nyakati hizi maranyingi presha hupanda au
kushuka. Kumbuka presha yako huongozwa na mapigo ya moyo, na ndio sababu
kukawa na mapendekezo kuwa asubuhi ni wakati mzuri wa kumeza dawa za
presha.

1. Jumatatu. Tafiti zimeonyesha maradhi ya moyo


huwashambulia sana wagonjwa siku ya Jumatatu. Na katika siku
hii, karibu mara zote maradhi haya hushambulia kuanzia alfajiri
kubwa (saa 10 usiku) mpaka asubuhi (saa 4 asubuhi). Shambulizi
la presha kwa siku ya Jumatatu mara nyingi huwapata wagonjwa
walio majumbani.

2. Jumamosi. Pia tafiti zimeonyesha maradhi ya moyo


huwashambulia sana wagonjwa siku ya Jumamosi. Imeonekana
wagonjwa huwa na nafuu sana wakati wa mchana, lakini wakati
wa usiku huwa na matatizo. Shambulizi la presha kwa siku ya
Jumamosi mara nyingi huwapata wagonjwa walio Hospitali. Vifo
vingi vya wagonjwa wa presha Hospitalini hutokea Ijumaa
kuamkia Jumamosi na Jumamosi kuamkia Jumapili.

Ufuatiliaji katika matibabu


Baada ya kuanza matumizi ya dawa, nilazima umuone daktari wako angalau kila
mwezi mara moja mpaka presha yako itakapokuwa ya kawaida. Muhimu
kuchunguza kiwango cha potasium katika damu mara moja au mbili kila mwaka
kwani dawa za presha unazotumia ama zitaongeza au kupunguza kiasi
kinachotakiwa mwilini.
Na vilevile ni muhimu kuchunguza figo ikiwa hazijapata matatizo.
Hata baada ya presha kuwa sawasawa, bado utahitajika kuendelea kumuona
daktari kila baada ya miezi mitatu au sita ili kuona kama hakuna maradhi mengine
ya moyo yamejitokeza.

HITIMISHO

a. Chakula na maradhi

Karibu maradhi yote yanayomsumbua mwanaadamu hutokana na chakula, ni


maradhi kidogo tu ndiyo ya kuambukiza. Na maradhi haya nafasi yake kubwa ya
kuyapata ni kwenye kula. Kwani kwenye kula, ama mtu atakula chakula kingi
akaongezeka uzito au akaacha kula kilicho muhimu n k. Ikiwa watu watachunga
taratibu za kula (Usile isipokuwa uwe na njaa, usile mpakaukashiba, ule vyakula
kiafya, unywe maji ya kutosha) basi hata kama kunaurithi kwenye ukoo, maradhi
haya hayatamsumbua. Na kinyume chake, hata kama hakuna urithi kwenye ukoo
wake, ikiwa hachungi taratibu za kula, maradhi haya yatajenga mwilini.

Jifunze namna ya kula kwa manufaa ya afya yako


Kwa mfano, mtu anaamka na anaona siku ni mbaya kwake uanamua kujiliwaza
kwa kula keki. Au hajisikii vizuri, unaamaua kunywa supu. Au, unakula mfuko
mzima wa bisi kwa sababu yuko kwenye burudani (anaatizama sinema/mpira).
Watu wengi hugeuza chakula ni kiliwazo, bila kufahamu wanafanya kwa sababu
gani au bila kufikiria kwanini wanafanya hivyo. Huu ni ulaji usio sababu au kwa
maana nyengine ni ulaji usio na maana yeyote. Na itakapokuwa una uzito mkubwa
na unataka kupunguza uzito wako, mazoea ya kula ovyo yatakuwa ndio adui yako
mkubwa. Kula kuna maana moja tu ya kutupatia nguvu za kuishi, lakini wengi kati
yetu tunakula kwa sababu nyengine.
Ifahamu njaa
Kufahamu ulaji usio na maana au ulaji usio na sababu, ni
vizuri tujue aina za njaa:

• Njaa ya kweli • Njaa ya kutamani


• Inakuja kwa nyakati – Inakuja ghafla
maalum – Inachagua vyakula maalum
• Inapokuja unaweza kula – Huwezi kusubiri
chochote – Huwezi kuacha kula mpaka
umalize
• Inapokuja unaweza – Unajisikia vibaya baada ya
kusubiri kumaliza kula
• Unaposhiba unaacha – Unaongezeka uzito
kula •
• Unajisikia vizuri baada ya
kula
• Mwili hupata nguvu

b. Ununuzi wa chakula
Kutokana na uzito wa tatizo lenyewe la presha, kuna haja ya kuelekezana sio kula
tu bali hata namna ya kununua hivyo vyakula.

Mapendekezo matano kuelekea sokoni kwa ajili ya manunuzi ya vyakula.

1. Fanya maandalizi uendapo sokoni/markiti

Lenga kwenda kununua vyakula halisi ambavyo bado havijatengenezwa kutoka


mashambani. Na ikiwa mazingira hayakupi nafasi ya kupata vyakula kutoka
mashambani, taratibu za kiafya zizingatie kwa chochote utakachokinunua.

Baadhi ya maelekezo kuelekea sokoni :

1. Andaa orodha. Kabla ya kwenda kununua vitu, amua ni vyakula


gani utakuja kula kwa siku inayo/zinazofuata. Si vibaya hata kuamua
na vitafunio gani utatumia. Ukifanya hivi utaokoa muda na pesa
utakapokwenda sokoni.
2. Kula kabla hujenda sokoni . Hili ni jambo muhimu sana kwani
ukienda kununua vitu na njaa, vitu vitamu vitakuvutia machoni
mwako na kukufanya kuwa mbali na mpango wa afya unaoufuata.

2. Kumbuka vyakula muhimu kiafya kwako/jamii

Kupatana sana kunaweza kukutoa katika malengo ya kupata chakula kilicho bora.

3. Nunua vyakula halisi. Vyakula halisi ni vizuri kuliko


vilivyoandaliwa viwandani. Vyakula vya viwandani vinakuwa na
mapungufu katika virutubisho. Vyakula halisi vina harufu nzuri,
rangi nzuri, ladha halisi na kiafya ni vizuri. Ikiwa utanunua vyakula
vya viwandani, chagua vyenye mafuta kidogo na chumvi kidogo.

4. Tumia muda mwingi eneo lenye vyakula halisi.

5. Soma/pata maelezo ya unachokinunua. Vyakula vingi vya


kiwandani hutiwa maelezo kuhusu namna kilivyoandaliwa. Soma
kwa makini/pata maelezo kwa muuzaji ili ununue chakula
kinachokufaa. Fufahamu kama havijakaa sokoni muda mrefu na
kuanza kupoteza ubora wake.

You might also like