You are on page 1of 18

Mhoji: Sawa, naitwa Mwalimu Evodius, leo tupo hapa Makete

Mhojiwa: ndio
Mhoji: na tupo kwenye kata ya Lupalilo yap. Nipo na KI wa kwanza ambaye atajitambulisha
yeye ni nani, anaweza akatuambia cheo chake kama ni mzee maarufu ama kuna
chochote alichonacho kwenye jamii anaweza akatuambia afu basi tuanze mahojiano
yetu, karibu Mzee wangu
Mhojiwa: Asante, Mimi kwa jina naitwa Mathias Chitambi Mwila
Mhoji: sawasawa
Mhojiwa: ni mkazi wa Kijiji cha Lupalilo
Mhoji: mhmmm sawa. Na tumeambiwa kwamba ni mzee maarufu
Mhojiwa: ndio
Mhoji: au Mzee mwenyeji
Mhojiwa: ndiyo
Mhoji: ukiwa mwenyeji ndo umaarufu wenyewe huo sio lazima umaarufu wa kwenye magazeti
au redio
Mhojiwa: ndiyo
Mhoji: sawa, kama nilivyosema ni maswala yanayohusiana na chanjo au Afya kwa ujumla, labda
tukianzia na hilo, unafahamu chanjo zote ambazo zipo kwenye jamii yetu
Mhojiwa: yah nazifahamu ndio
Mhoji: mmhmm
Mhojiwa: kuna chanjo za aina nyingi huaw zinatolewa hapa kijijini, kwamfano kuna chanjo hizi
za watoto ambazo ni Surua, Tetanus, kuna kifua kikuu, kuna kupooza pia kumekuwa
na chanjo hizi za naniii, za ugonjwa wa Covid
Mhoji: Corona
Mhojiwa: Corona eeeh, hizo ndo walikuwa wanazitoa
Mhoji: aah sawa kabisa, kumbe unajua chanjo mbalimbali
Mhojiwa: ndiyo
Mhoji: na Lengo kubwa mzee wangu la chanjo huwa ni nini, kwa uelewa wako wa kawaida
Mhojiwa: katika uelewa wangu mimi
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: Kwa chanjo za hawa watoto hawa wadogo chini umri wa miezi sifuri mpaka miaka
mitano, ni kuzuia, ni kuwakinga ili wasiweze kupata magonjwa ya maambukizi
wakiwa watoto wa changa
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: eeeeh, kwa watu wazima ni kwaajili ya kuzuia magonjwa ya maambukizi
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: kama ilivyotokea hii chanjo ya nanii, ya Corona, ni kama kuzuia
Mhoji: mh kwahiyo ni kama kinga kwa namna moja au nyingine
Mhojiwa: kinga
Mhoji: sawa, na wee mzee wangu umechanja chanjo, kati ya hizo ulizozitaja, kuna chanjo yoyote
ambayo wewe umechanja
Mhojiwa: aaah Mimi nimechanja kujikinga na maambukizi ya Corona
Mhoji: mhmmmm
Mhojiwa: eeeh nimechanja
Mhoji: aaah umechanja chanjo ya Corona
Mhojiwa: ndiyo
Mhoji: na umechanja ile chanjo moja au chanjo mbili
Mhojiwa: chanjo moja
Mhoji: anh sawa, na walikuelezea hospitalini kwamba hii ni chanjo moja
Mhojiwa: ndio
Mhoji: au labda kuna mbili we unataka ipi ama ilikuwepo moja tu hiyo
Mhojiwa: aah kwa wakati huo ilikuwepo ni moja
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: enhee ilikuwepo moja, kwa baadaye zikaja hizi za mbili, kwahiyo mimi nikawa
nimewahi kupata ile ya kwanza kabisa chanjo moja
Mhoji: sawa kabisa, na walikutaarifu kuhusiana na maudhi utakayoyapata baada ya chanjo na
jinsi gani ya kuhimili
Mhojiwa: aaah walinifahamisha kwamba kuna maudhi madogo madogo ambayo unaweza
kuyapata , kwamfano kama
Mhoji: eeeh
Mhojiwa: kuumwa kichwa, au kujisikia kichefuchefu ni swala la kawaida nisiwe na hofu navyo
Mhoji: na ulivyo chanja uliyaona hayo
Mhojiwa: eeh hayo mimi niliyaona
Mhoji: yalikaa kwa kipindi gani
Mhojiwa: aah kama masaa kumi na mbili hivi
Mhoji: eeh baadaye yakaisha
Mhojiwa: baadaye yakaisha, nikawa naendelea vizuri
Mhoji: tulikuwa tunaambiwa wengine wanasema ukichanja unakuwa unaumwa mkono mpaka
leo, wewe mkono wako hauumi
Mhojiwa: aaah mkono wangu mimi upo vizuri tu
Mhoji: eeeh
Mhojiwa: ila nilikuwa napata kichefuchefu na wakati mwingine kichwa kuuma ndo hayo
matatizo madogo madogo ambayo nilikuwa nayapata
Mhoji: sawa kabisa, hasa wewe umechanja, kwenye famiia yako au jamii yako hapa,
wamechanja pia au kuna wengine hawajachanja
Mhojiwa: anhaa mimi kwa familia yangu, wote niliokuwa nao kwenye familia wamepata chanjo
Mhoji: walipata chanjo
Mhojiwa: eeh, Mke wangu na mfanya kazi nilimleta kupata chanjo, ila hao watoto wengine
wanakaa nje
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: sinao hapa
Mhoji: sawa, hapa kwenye jamii yetu hapa, kuna lazima ambao hawakuchanja si ndio, kwa
namna moja au nyingine
Mhojiwa: ndio
Mhoji: na wewe kama mwanakijiji, lazima mnainteract, mnakaa, mnazungumza, unasikia mawili
matatu. Sababu ni zipi kuu zinazosemwa kwa nini wengine hawajachanja ama bado
hawapo tayari kuchanja
Mhojiwa: anhaa kwakweli, kwenye kipindi tunazunguka zunguka, kuna baadhi wengine
walikuwa wanakataa kwamba hizi chanjo ni hatari. Alafu wengine inauwa kizazi sijui
nini nini, basi tulikuwa tunajaribu kufanyaje, kuwaelekeza jinsi ambavyo sisi
wenyewe tumechanja hatuna madhara kama hayo. Kwahiyo tulikuwa tunawashauri
bwana, hii chanjo inasaidia sana, haina madhara kama hivyo mnavofikiria nyinyi,
jitahidini kwenya kufanyaje
Mhoji: kuchanja
Mhojiwa: kuchanja. Kuna wengine tulikuwa tunawaleta mpaka hapa eeh
Mhoji: kwa sababu kuna baadhi wameelewa kuna baadhi hawajaelewa
Mhojiwa: eeeh lakini kwa muda wa katikati hapa, kuna wengi walielewa
Mhoji: wengi wamelewa , lakini bado kuna ambao wapo bado hawajaelewa
Mhojiwa: eeh wamesugu, lakini huwezi kusema wote mia wamechanja, kuna baadhi ambao
Mhoji: eeeh baadhi
Mhojiwa: nimeona hao wahudumu wa Afya hao, sasahivi bado wanazunguka zunguka kwenda
kuwatafuta wale ambao bado hawajachanja
Mhoji: mhmmm sawasawa
Mhojiwa: sasa sielewi kwa sasa wana idadi gani ambao, wanaweza kuwafikia uko, kwa watu
ambao hawakupata wakati huo
Mhoji: sawasawa
Mhojiwa: Ndio
Mhoji: Labda unadhani kuna kakitu gani ambako kangefanyika, watu wangekuwa wana muitikio
mkubwa zaidi
Mhojiwa: aaah sahivi ni kuhamasisha tu, muendeleee kuhamasisha kwenye sehemu za
mikusanyiko, kwenye mikutano humo, mjaribu kuwaelimisha eeeh. Watambue
kwamba wale waliochanja mpaka sasa wapo, na wengine waliokuwa wanasema aah
mpaka nguvu za kiume zinapotea nini, lakini waliochanjwa ndio mashihidi ambao
Mhoji: wanaweza wakasema
Mhojiwa: wakasema eeh, kwamba bwana eeh, mimi nimechanja hakuna madhara, mimi
nimechanja hamna madhara. Kwahiyo wale waliokuwa bado, watakuwa na nguvu ya
kusema ah, ngojea na mimi niende nikananii
Mhoji: sawasawa
Mhojiwa: Ili tu tujitahidi kwenye mikutano, kwenye makundi, tuzidi kuwaelimisha ili waliobaki
waweza , wakachanje
Mhoji: sawa, Na jinsi unavyofahamu
Mhojiwa: mhh
Mhoji: Ugonjwa huu mtu akikuambukiza, utaona dalili gani au kiashiria gani kwamba umepata
kaugonjwa haka
Mhojiwa: aaha inafwatana na ugonjwa ambao utakuwepo
Mhoji: kwamfano Corona
Mhojiwa: kwa Corona, unaweza ukakuta yani, nanii, mafua, kukohoa sana, mwili kupungua
nguvu eeh, Hizo unaweza ukagundua kwamba
Mhoji: sawasawa kwa uchache
Mhojiwa: kwa uchache, unaweza ukagundua kwamba hapa mimi nina shida flani, ngoja niende
hospitalini
Mhoji: sawa kabisa
Mhojiwa: nikapata maelekezo zaidi
Mhoji: anhaaa, na kumbe unatakiwa ukiona hivo uende hospitalini, ndo hatua zilizokuwa
zinachukuliwa
Mhojiwa: hatua, kwa wengine walivokuwa wanaenda hivo, kuna wengine walikuwa wanabaki
majumbani
Mhoji: wakifanya nini, wakipata huduma gani labda
Mhojiwa: Nyumbani kuna wengine walikuwa wanatumia vitu vyao vya kienyeji, majani majani
hayo, sijui wengine wanachukua mananiii, sijui vitunguu swaumu, sijui nini, malimao
sijui wanachanganya afu wanakunywa. Lakini baada ya kuwaelimisha, wengi wao
walivokuwa wanaona hivo, basi walikuwa wanakuja kituoni kuja kupata ushauri zaidi
Mhoji: ok
Mhojiwa: ndio
Mhoji: sawa kabisa, kwa sasahivi mzee wangu wewe na familia yako mnajikinga kwa namna
gani, na mnaamini huu ugonjwa wa Corona kwanza upo ama haupo, na kama upo
mnajikinga kwa kupitia nin
Mhojiwa: kwa sasahivi, sisi pale nyumbani, jinsi ya kuweza kujikinga, yani kifamilia,
nimewahamasisha kwenye familia, tuna ndoo ya maji ya kunawa
Mhoji: enheee
Mhojiwa: tumeweka pale nyumbani, tunapotoka chooni tuna kindoo, afu tumehakikisha maji,
yani maji tunayotumia ni ya kuchemsha. ALafu kila shughuli unayoifanya,
unavyotaka kwenda kuandaa chakula lazima unawe mikono eeh, yani katika shughuli
zote za kiAfya, tunafwata utaratibu ambao upo pale nyumbani, tunanawa, tuwe
tunamazoea ya kunawa, alafu tunapofanya shughuli za nanii za vumbi, kuvaa mask
mdomoni
Mhoji: mmh kuna wengine walikuwa wanasema haya mambo yote unayosema yalikuwa ni
kipindi kile, sahivi watu hawafanyi chochote kuhusiana na kujikinga
Mhojiwa: aaah hata ukipita kwenye vibanda utakutana na ndoo za maji
Mhoji: bado zipo
Mhojiwa: zipo eeh
Mhoji: anhaaa
Mhojiwa: ndoo za maji, sabuni ya maji kwa ujumla
Mhoji: mhmmm sawa kabisa.
Mhojiwa: ndio
Mhoji: Hivi kwenye jamii yetu nani ambaye yupo kwenye hatari zaidi, kundi ambalo lipo
kwenye hatari zaidi kupata maambukizi ya Corona, ugonjwa wa Corona, ni
wanawake, watoto, wazee au ni kundi gani ambalo lipo kwenye hatari
Mhojiwa: mhmmmm kundi ambalo lipo kwenye hatari kupata hali hii zaidi
Mhoji: zaidi
Mhojiwa: zaidi ni hawa wazee walevi
Mhoji: (akicheka) wazee lakini walevi
Mhojiwa: eeh walevi, aah tuseme kundi lote la walevi, sababu wale ukienda, hata sasahivi
kwenye vilabu hivi, wakishalewa, hawana subira. Wanafanya mambo yote ambayo
ya kinyume na ustaarabu wa Afya
Mhoji: tara tara taratibu
Mhojiwa: eeeh ya taratibu, unakuta wakati mwingine wanaenda chooni hawanawi, ni wakati
mwingine wanaweza waka nanii, wakajitawaza kutumia mikono alafu anaenda
kuchora kwenye ukuta na mavi. Kwahiyo wale, ndo wapo kwenye kundi la hatari ya
kupata huo ugonjwa wa Corona
Mhoji: la hatari zaidi
Mhojiwa: eeeh
Mhoji: mhhh na wananchi wanajua haya makundi yapo kwenye hatari, ama inategmeana na
elimu iliyopatikana, ama wewe hii umeipata wapi
Mhojiwa: Hii imetokana na Elimu ambayo wametoa wahudumu kwenye jamii. Eeh wakifika
pale, wanapoenda kunanii, kutoa chanjo, huwa wanatoa na elimu, kwmaba bwana,
kuna moja mbili tatu, kundi lenye hatari sana kupata maambukizo hayo ni kundi hili.
Kwahiyo wamejaribu sana kujikita kwenye vilabu
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: na kusimamia vizuri sana kwenye naniu, eeh, kidogo sahivi uelewa wanao
Mhoji: mhmm je swala la ushirikishwaji lipoje, tumeshirikishwa vipi na jamii yetu au na
viongozi wetu kwenye jamii maswala ya magonjwa, hata ilipokuja ugonjwa wa
Corona, na tulikuwa tunashirikishwa kwa njia zipi
Mhojiwa: anhaaa, tulikuwa tunashirikishwa kwa njia ya vikao.
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: Elimu yani, wanafika pale mnajadiliana, mnaelezana dalili
Mhoji: mara kwa mara, ama kipindi flani
Mhojiwa: kuna kipindi, wameweka utaratibu
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: eeh wameweka utaratibu, wanaweza kukaa baada ya mwezi mmoja, ama baada ya
wiki mbili tatu, wanazunguka. eeh bana kuna moja mbili tatu, tunakuwa
tunakumbushana yale ambayo yapo, ili jamii iwe na kumbukumbu na tatizo hilo
Mhoji: sawasawa , na hizo wanazozitumia kwamfano mikutano, unadhani ni bora, njia bora au
kuna njia zingine ambazo wangezitumia ingekuwa bora zaidi lakini huwa
hawazitumii
Mhojiwa: aah ni kweli, njia ambazo huwa wanazitumia hawa, nani, njia ambazo zinatumika
sana, kwamfano huku kwetu, ni kwenye nanii, kwenye mikutano.
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: Alafu waliwahi kupita kwenye kitongoji
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: eeh alafu waliwahi kupita kwenye jamii wakawa wanaelimisha
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: eeeh kwahiyo ujumbe unaonekana ulishika vizuri kwa , kwa ujumla
Mhoji: sawa, hakuna njia ambayo (simu inaita pembeni) Hakuna njia ambayo katika hizohizo
sehemu haipo, lakini unadhani huwa inatakiwa iwepo na ingekuwepo ingekuwa nzuri
zaidi
Mhojiwa: aaah kwenye nanii, kwenye matangazo, kwa kutumia vipaza sauti
Mhoji: ingesaidia
Mhojiwa: ingesaidia zaidi eeh
Mhoji: kupita huku wanatangaza
Mhojiwa: ndio
Mhoji: anhaaa
Mhojiwa: ingesaidia zaidi
Mhoji: sawasawa, na mara nyingi kwenye ushirikishwaji huwa kuna kamati pia zipo za Afya, pia
sijui za kata , za nini huwa zipo?
Mhojiwa: zipo
Mhoji: unaonaje utendaji kazi wao wanaofanya, ni mzuri ama ingewezekana kukawa na
utaratibu mwingine wa kamati hizo, zifanye kwa namna tofauti
Mhojiwa: aaah mimi kwangu mimi, ninaona ni nzuri, kwasababu kila wakati naona ,wanakaa
wanazungumzia maswala ambayo yapo kijijini, eeeh inafaa
Mhoji: mhmmm kwamfano Wizara ingekuwa na ujumbe wa kiAfya, ilete kwenye kamati hizo ili
waje wawaambie jamii, au wizara ije moja kwa moja kwenye jamii
Mhojiwa: hapana, ilete kwenye kamati hizo, kamati ndo ilete kwenye jamii. KWasbabu
Mhoji: eeeh
Mhojiwa: Jamiii inaa, jamii na hiyo kamati ni watu ambao wanafahamiana. Kwamba kwamba
hutu nikimwendea hivi, uelewa wake upo hivi lakini ukitoka huko moja kwa moja
inakuwa ngumu, kuna wengine huwa wanasikiliza, wanapuuzia. Lakini ukitumia hao
wa hapa, wanaweza wakaeleza na wakaelewa.
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: ndio
Mhoji: sawa kabisa. Na je unaonaje kuhusiana na viongozi mbalimbali kwenye jamii yetu.
Kwamfano kuna wakisiasa, wa kiserikali tunaweza sema, kuna wa kidini,
inawezekana hata kuna wa kimila na viongozi mbalimbali. Kwahiyo wapi ambao
wana ushawishi mkubwa kusema jambo, jamii inafwata na inawasikiliza, ambayo ipo
juu, ambaye akisema watu wanafwata
Mhojiwa: aaha kwangu mimi naona wote wana. Kwasababu ukienda kansani, waumini wale
wanapoenda pale, kwasababu haya matangazo yalifika mpaka sehemu zote, kansani,
wapi wapi, walikuwa wanaeleza, kwamba kuna moja mbili tatu, na ule ujumbe
ulikuwa unapokelewa, na utekelezaji tulikuwa tunauona
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: Kwahiyo idara zote , yani katika idara zote ambazo zilipewa taarifa kufikisha huu
ujumbe, ulifika vizuri sana
Mhoji: mhmmm kwahiyo sasa ni njia zote
Mhojiwa: Njia zote zinakubalika
Mhoji: Viongozi wa kisiasa, viongozi wa kidini, hakuna ambaye yupo juu ya mwenzake
anayesikilizwa zaidi
Mhojiwa: hapana
Mhoji: wote wanasikilizwa sawa tu
Mhojiwa: ndio. Ukienda kansani, kwasababu unapoenda kansani, wakati ule
Mhoji: Kwamfano akisema wa kisiasa na akisema wa kidini, yupi unamuamini zaidi
Mhojiwa: kwa
Mhoji: yani taarifa za kiAfya, ikisemwa kwenye chombo cha kiDini, au viongozi wa kidini na
ikisemwa na kiongozi wa kisiasa, wapi wewe moyo wako au jamii ya hapa sio wewe,
ambao wanasikiliza zaidi na unaamini watafanya hicho kitu
Mhojiwa: sasa, Mimi, kwasababu ukienda Kansani, sio wote wanaoenda kansani, kuna wengine
ujumbe hauwafikii, wa siasa wanawapitia. Sasa unaona hivi vyote kidogo vina
Mhoji: vinachanganyikana
Mhojiwa: vinachanyikana hapo. Ukienda kwenye siasa uko, kuna wengine wanaenda kuna
wengine hawaendi.Sasa huyu anaweza akapata ujumbe kupitia kule, huyu anapata
ujumbe kupitia Kansani. Kwahiyo ukija kunanii, kuweka kwa pamoja, inaonekana
mambo yanaenda vizuri
Mhoji: sawa kabisa. Na je unaonaje utendaji kazi wa wahudumu wa Afya kwenye kata labda, au
kwenye kituo cha Afya , kwenye Dispensari au Hospitali katika mazingira yenu,
wanafanya vya kutosha kiasi ya kwamba, walifanya chanjo ziende vizuri, au
walikuwa ni sehemu ya chanjo isiende vizuri
Mhojiwa: aah mimi niliona wahudumu wa Afya, walikuwa bega kwa bega na wataalamu wa
Afya. Kwasababu wao, wahudumu ndo walikuwa wanawapitisha, watumishi wa
Afya, kwamba bwana, twendeni moja mbili tatu
Mhoji: Ukiongelea hilo, unaongelea hao wahudumu pamoja na hao unaosema wewe madaktari
au manurse pamoja na hao wahudumu, utendaji wao kazi kwa ujumla
Mhojiwa: ulikuwa mzuri sana
Mhoji: okay
Mhojiwa: kwasababu tulikuwa tunaona wanabeba vitendea kazi, wanazunguka navyo
Mhoji: na wamefanya kipindi hicho, ama mpaka sasa
Mhojiwa: mpaka sasa, juzijuzi hapa nimewaona wamebeba mpaka nkasema mnaenda wapi,
tunaelekea huku eeh na carrier ile pale nliona wamebeba wanaelekeza hivi, nikaona
hii kazi bado inaendelea siyo imeishia. Siyo kwamba nazungumza kwa kutaka nanii,
aaah aah, nimewaona mimi, tena niliuliza nyie bado mnaendelea kunaniii, akasema
ndio, nkasema sawa.
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: eeeh
Mhoji: sawa. Na je umbali wa vituo hivi, vipo karibu na wanachi au umbali unaweza ukawa pia
sababu ya watu kuchanja ama kutokuchanja
Mhojiwa: aaah huyo kutokuchanja huyo naona tu ni sababu tu atakuwa ameipenda, lakini
wahudumu mara nyingi huwa wanasafiri
Mhoji: mhmmm wanawafwata watu
Mhojiwa: wanawafwata watu walipo. Wanawafwata watu, wa kule juu kuna kituo kule lakini wa
huku wanajitahidi sana. Ninaona mara nyingi wanaenda na pikipiki
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: eeeh wanazunguka zunguka, wanazunguka zunguka kufanya hizo kazi. Kwahivyo mtu
ambaye hakuchanja mpaka sasa, aah huyo atakuwa tu kwa sababu yeye alipenda
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: pengine yeye imani yake
Mhoji: sawasawa. Kuna wakati mtu yupo tayari kuchanja, lakini kila akifikiria , mambo yaliyopo
kwenye mambo ya Hospitali au kituo cha Afya au Dispensari, Moyo wake unarudi
nyuma kwenye mambo ya kuchanja, akifikiria mambo hayo
Mhojiwa: Sasa inawezekana yule aliyekutana naye siku ile, Elimu ilikuwa pengine haikumkolea
Mhoji: na yeye alikuwa anarashia rashia
Mhojiwa: eeeh sasa kama mtaalamu wa Afya amemuona kama huyu nimemuelekeza kwamba
bhana kuna moja mbili tatu, ameshindwa kunielewa na anataka kuchanja lakini Elimu
yangu bhana sijui ni kitu gani ambacho kimemchanganya, basi anaomba mwingine
aendelee kumuelimisha
Mhoji: sawa kabisa. Na je kwenye jamii yetu hapa , kwasababu ni Mzee wangu unaweza ukawa
unafahamu zaidi kuliko ningeuliza hili swali vijana, kuna mila, desturi au tamaduni
zilizopo hapa kwenye mazingira yetu, ambazo zimekuwa za jadi kabisa, lakini
zimekuwa sehemu ya kusababisha either watu inapotokea chanjo wachanje au
wasichanje
Mhojiwa: eeh hayo yalikuwepo
Mhoji: eeh ningependa kusikia mifano yake vizuri
Mhojiwa: eeh mifano yake, kana kwamba unaona kamtaa kingine kapo kule, si kuna kamsitusitu
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: kamtaa kale kulikuwa kuna watu ambao wana mila
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: umeona eeh, yani hawawezi wakafanya kitu bila kufika maeneo yale kusemelea, lakini
baada ya kutoa elimu yani hata kama hizi chanjo hizi, walikuwa wanakataa, walikuwa
wanazuia. Sasa baada ya kukaa, kujadiliana, kufanya nini, kuwaelimisha wale wazee
wa mila wale, kwakweli hata watoto chanjo walikuwa wanawaleta.
Mhoji: mhmmm ,walikuwa wanashikilia kitu gani, ninataka kujua hilo
Mhojiwa: yani walichokuwa wanashikilia wao, wanasema hizi mila za mababu
Mhoji: ambazo hazitaki nini
Mhojiwa: yani tukichoma sindano huko nyuma tulikuwa hatuchomi sindano
Mhoji: enheee
Mhojiwa: tukichoma sindano tunaweza tukapata madhara
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: watoto wakizaliwa wanatengwa , yani wanalala chini kwenye manyasi uko, Kwahiyo
hizi baada ya kugundua na baada ya kufikisha kwenye ofisi za serikali, wale watu
walikuwa wanaitwa. Wakifika pale wanawaelekeza eeeh, wanaelekezwa
Mhoji: ndo wanakubali
Mhojiwa: wanakubali
Mhoji: sawasawa, Labda kwamfano mila hizi za vyakula, labda mila flani jinsi ya kula au jinsi
ya kusalimiana ambayo lazima mtu huyo ujue umemsalimia mpaka ufanye hivyo,
ama ule chakula mpaka ufanye hivyo, au labda kama ni pombe mpaka mpeane vibuyu
vibuyu, kuna mila za namna hiyo
Mhojiwa: hizo mila zilikuwepo, lakini baadaye tulikuja kuzitokomeza, Viongozi walikuwa
wanakazia. Sababu hawa jamaa, zamani pombe walikuwa wanapokezana mila zao,
hakuna mtu anayekunywa pombe
Mhoji: peke yake
Mhojiwa: peke yake eeh, walikuwa wanapokezana kama kwenye ki kibuyu kinazunguka sehemu
zote walizokaa pale. Lakini baada ya kutokea hili tatizo la Corona, tulilipigania sana
kwamba kila mtu awe ana chombo chake
Mhoji: awe na chombo chake (akitabasamu)
Mhojiwa: eeh cha kunywea pombe
Mhoji: mhhh
Mhojiwa: anaenda pale ,anamiminiwa , anachukua pombe yake anakaa pembeni anakunywa.
Hiyo imesaidia kidogo
Mhoji: anatamani kumpa mwenzake lakini hawezi akikumbuka Corona
Mhojiwa: hawezi eeeh. Sasa hilo limesaidia sana kuvunja ile miko ambayo ilikuwa nayo nyuma,
na kwenda kisasa.
Mhoji: na je mambo ya kusalimiana, kuna mila flani ya kusalimiana huku ambayo labda lazima
watu washikane wafanye nini
Mhojiwa: kweli hiyo mila ilikuwepo. Huku mila kusalimiana mila zao kusalimiana walikuwa
wanakumbatiana
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: eeh walikuwa wanapeana mgongo
Mhoji: wanasema ngolile
Mhojiwa: eeh ngolile sijui nini, kukumbatiana, kupeana mikono hii
Mhoji: (acheka)
Mhojiwa: sasa baadaye tukaanza , wakawa wanawaelimisha, nyinyi mnavopeana mikono,
mnashikana
Mhoji: ndo mnavyo, maambukizi yanavozidi
Mhojiwa: maambukizi ndo yanavozidi, huwezi jua huyu ametoka wapi, na wewe umetoka wapi.
Kwahiyo hii hali siyo nzuri. Kwahiyo jamani tujaribu tu kusalimiana tu kwa
kutamkiana au kupeana habari, habari habari, ugolile golile basi unaenda. Lakini siyo
lazima kukumbatiana, na baadaye kukawa na visheria flani flani, akioneakana mtu
amepeana nanii, anaitwa ofisini.
Mhoji: anhhaaa waliweka sheria
Mhojiwa: enheee, wakifanya hivi labda wanapelekwa ofisini, mpaka sasahivi ime
Mhoji: imepunguwa
Mhojiwa: imepunguwa eeh
Mhoji: Je kuhusuana na mila, tamaduni labda za mwanamke, yeye ni nani, na mwanaume ni nani
, huku inasemaje kwa muda mwingine unasikia huyu ndo mwenye maamuzi ndo
mwenye nini, mwanamke ndo anatakiwa afanye nini, hivo vitu vipo uku
Mhojiwa: aaah hivo vitu vipo
Mhoji: mmhmm
Mhojiwa: hivo vitu vipo
Mhoji: bado mwanaume ana sauti , na wenda ikaathiri pia mambo ya, nenda ukachanje au
usichanje
Mhojiwa:eeeh hizo mila zipo
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: Lakini viongozi wamejaribu kupambana nao, mpaka sahivi elimu ipo
Mhoji: mhhh
Mhojiwa: eeeh, yani kwamfano kama mwanamke amejifungua, unaweza ukakuta mzee pale
nyumbani hakanyagi. Anaenda anahama sehemu nyingine
Mhoji: anahama
Mhojiwa: eeeh unaona eeh, kwahiyo
Mhoji: kwanini ipo hivo
Mhojiwa: yani
Mhoji: kwamba anamuacha kwanza
Mhojiwa: eeh anamuacha
Mhoji: nyumbani kwako inabidi uhame
Mhojiwa: eeh baada ya kuleta vyakula pale anasema mwanamke ajitunze kwanza.
Mhoji: ajitunze mwenyewe
Mhojiwa: sasa tuchakula atatoa wapi huyu, wamejaribu kunanii , viongozi watendaji wamejaribu
kuingilia kati sana baada ya kuona sasa, hata ukuaji wa mtoto
Mhoji: unakuwa wa shida
Mhojiwa: wa shida,
Mhoji: na hiko kipindi mwanaume anakuwa anakaa wapi
Mhojiwa: si anafwata mtu mwingine
Mhoji: mwanamke mwingine
Mhojiwa: eeeh
Mhoji: anaweza akasababisha hata magonjwa sasa
Mhojiwa:eeeh sana tu
Mhoji: Wenyewe huku jambo la kuzaa, ni kama wanaliona ni jambo baya au jambo gani,
kwasababu mpaka kumuacha mke wako
Mhojiwa: eeh bwana, kwa mila za huku, uko nyuma ilikuwa ni shida, ilikuwa ni shida kana
kwamba Mama akijifungua wanamtenga, Mama akiwa mjamzito wakati mwingine
mwanaume anasafiri anaenda kutafuta maisha huko, huku mama yupo peke yake
Mhoji: mhhh
Mhojiwa: sasa ndo maana baada ya kubana, mara nyingi sana watoto walikuwa chini sana uzito,
walikuwa wanaingia kwenye kadi nyekundu
Mhoji: kwashiokor
Mhojiwa: kwashiokor nini eeh, baada ya kunanii, baada ya kuwaelimisha, kuwashawishi, yani
ndo wamejirudi sasa
Mhoji: sawasawa , na huku kuna mambo yale ya tawala ya nini , ya Vijana kuvuka kundi flani
kwenda flani, kufanyiwa mambo ya sherehe flani
Mhojiwa: aaah huku hamna
Mhoji: huku hayapo
Mhojiwa: eeeh kwasahivi hamna
Mhoji: Je kuhusiana na ikitokea jambo jipya, kwa mfano hilo la chanjo labda au ushauri flani wa
kitaalamu mpya, jamii yetu imekuwa ikija mbele kupokea au inarudi kwanza nyuma
ndo baadaye inakuja kupokea na kukubaliana na jambo
Mhojiwa: aaah ni kweli, hawa watu mara nyingi huwa wanapenda kwanza kusikilizia. (akicheka)
Mhoji: kusikilizia
Mhojiwa: eeh kwamba wanajivuta kwanza. Itumike kwanza nguvu, ikishatumika nguvu, pale
ndo unaanza uelewa sasa, hata nikifanya hivi, mimi nitakuwa salama. Lakini hawana
mwili huo wa kusema kwamba hiki kimetokea ,ngojea tupate utaratibu unaokubalika
hamna.
Mhoji: mhhhh
Mhojiwa: eeeh ndiyo
Mhoji: sawa kabisa. Kwahiyo kitu gani kilitakiwa kifanyike kwanza ili watu wawe wanakuwa
mbele, wasisikilizie kwanza
Mhojiwa: elimu
Mhoji: kwa sababu swala la Afya si halitakiwi kusikilizia kwanza
Mhojiwa: eeeh ukiona kama kitu kimetokea, inabidi pale nanii, elimu kwanza.
Mhoji: Elimu ndo msingi
Mhojiwa: eeeh wawakusanye, eeh wawaweke sehemu moja au kwenye mkutano wa hadhara
waitishe pale, waanze kutoa elimu, wakishatoa elimu wale watakaokuwepo wanaanza
kufwata taratibu. Wakishaona kwamba hawa siku mbili tatu hawana kitu, basi sasa
ndo wanaanza kufwata hao wenyewe, naona hata kwenye chanjo hizi
Mhoji: aaah
Mhojiwa:eeeh
Mhoji: (akicheka)
Mhojiwa: si chanjo hizi wakati walienda kwenye mkutano pale, wakananiii, wakaelimisha
elimisha, wanaotaka kunaniii, wakapatika thelathini arobaini wakachoma choma.
Sasa siku ya pili ya tatu, unakuta hawa wanaa kuja hao wenyewe hapa. Kwamba
mbona jamaa
Mhoji: mbona hajafanya chochote
Mhojiwa: eeeh basi wakawa wanajitoa wanakuja
Mhoji: wanaamini sasa
Mhojiwa: eeh kwamba aaah hiki kitu ni kweli
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: ndio
Mhoji: sasa tangu huu ugonjwa umetangazwa na shirika la Dunia la Afya, Je unadhani Tanzania
na Wizara ya Afya imefanya vya kutosha, au ilitakiwa ifanye zaidi kwenye kitu gani
Mhojiwa: aisee naona Idara ya Afya imefanya kazi kubwa sana, ndo maana sahivi kidogo,
kusikia sikia kwamba flani anaumwa, flani anaumwa hicho kitu hakipo kwasababu
Elimu imepita na watu wameipokea vizuri. Ndo maana magonjwa magonjwa hivi,
sahivi yamepungua kwa kasi
Mhoji: sawasawa, na wanatakia sasa wafanye vizuri zaidi kwenye kitu gani
Mhojiwa: sanasana wafwate utaratibu uleule walionaniii, kwamba ukitoka chooni maji ya kuna
yawepo na maji ya sabuni nini, tukifwata taratibu huu, hili tatizo litakuwa hamna
Mhoji: sawasawa. Na we unaamini mzee wangu kwamba Corona bado ipo ama haipo
Mhojiwa: Sababu Corona, naona bado ipo. Hata huku kwetu, hatujawahi kuona kwasasahivi
lakini sehemu zenye watu wengi unaweza ukakuta bado ipo lakini sio kwa kasi sana,
inaweza ikatokea kwa mara chache kwa mtu mmojammoja. Haswa wanaoelewa ni
wale wanaofanyia kwenye Hospitali kubwa, kwamba huyu mgonjwa ana dalili hizi,
huyu ana dalili si ndo yenyewe Corona ama ni kitu kingine. Sababu Corona inaenda
na matatizo mengine, maudhi mengine kwamba kukohoa, nini ,nini
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: ndio
Mhoji: sawasawa. Na kuhusiana na chanjo ya Corona wewe unaiamini
Mhojiwa: aah naiamini
Mhoji: mhmm
Mhojiwa: naiamini ndo maana nkachanja
Mhoji: aah kuna wengine wanasema ukichanja, unaweza ukapata tena maambukizi ya Corona
tena ukishachanja
Mhojiwa: aah inafwatana na nguvu ya mwili, eeh inafwatana na nguvu ya mwili, kana kwamba
kama umechanja, kama ile chanjo haikunanii, unaweza ukapata
Mhoji: mhhh
Mhojiwa:eeeh
Mhoji: lakini unakuwa tofauti kidogo na ambaye hajachanja jinsi inavyoingia
Mhojiwa: mhhhh
Mhoji: sawa, na tofauti na hapo, umeshawahi kuona tofauti na serikali kuna kikundi cha watu au
taasisi inakuja kuhimiza hayahaya mambo ya Corona na Chanjo tofauti na serikali
kwenye jamii yetu hapa imekuwa hivi vikundi ama taasisi zikija
Mhojiwa: mhhh hapa, sababu siwezi nikafahamu zaidi pengine kwenye mashirika kwamfano ya
sumbasisu na hao wenyewe walikuwepo kwenye kushirikiana kuhamasisha. Ila hapo
siwezi nkajua sasa, wanaoelewa zaidi ni wale wataalamu ambao walikuwa wana
Mhoji: aaha nilidhani walikuwa wanapita kwenye majumba yetu huku, na ukiwaona hata taasisi
zingine
Mhojiwa: aaah hapana
Mhoji: sababu wahudumu wa Afya umesema umekuwa ukiwaona, na wengine hawa wakisema
sisi sio serikali
Mhojiwa:aaah hapana sijawaona
Mhoji: sawa, na nanii, kuhusiana na, umeshawahi kusikia hatua mbalimbali ambazo serikali
imewahi kuchukua dhidi ya ugonjwa huu. Hatua, mahimizo, makatazo ama kama
kuna sera, tangia huu ugonjwa uingie, umewahi kusikia hivyo vitu
Mhojiwa: eeeh nimewahi kusikia
Mhoji: kwamfano umesikia nini
Mhojiwa: Nimewahi kusikia kwana kwamba, nimewahi kusikia kwamba watu wasishirikiana
kinywaji, kutumia chombo kimoja, kila mtu awe
Mhoji: na cha kwakwe
Mhojiwa: cha kwake
Mhoji: sawasawa
Mhojiwa: na katazo lingine ambalo lilikuwepo, kwa mtu ambaye hajanawa mkono, asipewe
huduma
Mhoji: mmmhm ambaye hajanawa
Mhojiwa: eeeh mpaka anawe mkono, haswa upande wa vilabu, kwahiyo kulikuwa na ndoo pale
ukinawa, unana wa ukiwa unaingia ndani
Mhoji: sawasawa
Mhojiwa: hapo ndo niliwahi kusikia. Na kwenye maduka nimesikia kwamba mtu asiyetekeleza
kuweka maji tiririka pale, basi biashara inafungwa
Mhoji: aaah sawasawa
Mhojiwa: kwahiyo hayo ndo makatazo tuliyoyasikia
Mhoji: (simu ikiita) La mwisho kabisa, kuna maoni gani yoyote yale ambayo unataka useme,
labda tuyafikishe Wizara ya Afya, ambayo inahusu na mambo ya Afya, ambayo
umekuwa na dukuduku nalo au maoni lakini ulitamani yafike
Mhojiwa: anhaa mimi maoni yangu serikali naomba tu izidi kukazia upande wa Afya kuhusu hii
nanii, kuhusu Corona
Mhoji: Ugonjwa wa
Mhojiwa:Corona
Mhoji: Corona eeh
Mhojiwa: enhee iendelee kuhamasisha kwamba kufwata ule utaratibu ambao serikali
imejiwekea. Afu la pili nilikuwa naomba serikali ijaribu kuangalia watumishi upande
wa Afya
Mhoji: mhmmm
Mhojiwa: sekta ya Afya kuna watumishi wachache sana, Vituo vipo vizuri lakini watumishi
hamna
Mhoji: sawa
Mhojiwa: enhee afu pili serikali iangalie upande wa dawa, unaweza ukafika sehemu kama hapa,
unataka kutibiwa, unaandikiwa lakini dawa hamna
Mhoji: hamna
Mhojiwa: kwahiyo hicho ndo serikali ijaribu kuangalia
Mhoji: sawa kabisa. Asante sana kwa maoni yako mazuri haya
Mhojiwa: sawa nashukuru sana
Mhoji: Aya

You might also like