You are on page 1of 14

Huduma ni msaada anaopatiwa mtu.

Huduma ya kwanza, ni msaada anaopewa mtu aliyepata jeraha


au aliyepata janga kabla ya kumpeleka hospitali.
Au
Huduma ya kwanza ni msaada wowote anaopewa mhanga ili
kupunguza maumivu baada ya janga alilolipata kabla ya
kupelekwa hospitalini kwenda kupata huduma zaidi.
Umuhimu wa huduma ya kwanza .
 Kuokoa maisha.
 Kupunguza maumivu.
 Kumpa matumaini mhanga.
 Kumsaidia daktari kupata taarifa kamili ya mgonjwa
uliyempeleka.
Sifa za mtu anayetoa huduma ya kwanza.
*Awe jasiri
*Awe mkarimu.
Sanduku la huduma ya kwanza ,ni kisanduku kidogo ambacho
ndani kinawekwa madawa na vifaa vingine kwa ajili ya huduma
ya kwanza na kisanduku kiwe ni chenye kubebeka kwa urahisi.
Vifaa vinavyowekwa kwenye sanduku la huduma ya kwanza
Mkasi,hutumika kukata vitu mbalimbali kama pamba na
bandeji.
Mpira wa mikono(gloves), huvaliwa mikononi na mtoa huduma
ya kwanza ili kuepuka migusano ya ngozi na damu.
Plasta ,hutumika kufunga majeraha baada ya kuweka Dawa na
pamba .
Bandeji,hutumika kufungia majeraha baada ya kusafisha na
kuweka dawa.
Yuso,hutumika kuoshea vidonda au majeraha mbalimbali.
Iyodini,hutumika kupaka kwenye vidonda kipya ili kukausha au
kuzuia damu isitoke.
Panadol,hutumika kumpa mgonjwa ameze ili kupunguza
maumivu.
Matukio ambayo yanaweza kutolewa huduma ya kwanza
1.Mtu aliyezama maji
Mtu aliyezama maji anakuwa na maji mengi kwenye mapafu na
hivyo anashindwa kupumua.Hivyo anahitaji huduma ya
kulazimisha maji yatoke haraka ili aweze kupumua.
Kama mtu aliyezama hajazirai mwokoaji ni lazima awe
mwangalifu sana kwa sababu mtu anayezama anatapatapa na
anaweza kumzamisha mwokoaji kwa kumng'ang'ania kwa
nguvu zote,kwani mwokoaji hapaswi kumgusa anaezamana
anatakiwa atumie kipande cha mti,nguo,au kamba kumvuta
aliyezama.
Namna/Jinsi ya kumhudumia mtu aliyezama maji.
(a)Mtoe ndani ya maji haraka iwezekanavyo.
(b)Mlaze chali na kisha anza kumsaidia kupumua kwa kuvuta
pumzk kwa nguvu ukitumia mdomo kwa mdomo.
(c)Akiwa amelala chali jaribu kugandamiza tumbo lake taratibu
kwa kuelekea ndani,nje Mara nyingi .
(d)Rudia kumlaza chali mhanga na kisha anza kumsaidia
kupumua kwa kuvuta pumzi kwa nguvu ukitumia mdomo kwa
mdomo ,kisha mgandamize tumbo lake taratibu kuelekea
ndani,nje Mara nyingi halafu mwinue haraka ili kumtapisha maji
yaliyokatika mapafu.Endelea kufanya hivyo Mara Tatu au nne.
(f)mpeleke hospitali haraka.
2.Mtu anayetapika na kuharisha .
Ugonjwa wa kuharisha / kutapika hupunguza kwa kiasi kikubwa
maji katika mwili.Sababu zinazompelekea mtu kutapika au
kuharisha ni kama vile kunywa sumu,kula chakula
kichafu,kunywa maji au kinywaji kichafu.
Jinsi ya kumhudumia mtuanayetapika na kuharisha.
(a)Kumnywesha maji ya matunda kwa wingi.
(b)kumnywesha maji ya madafu.
(c)kumnywesha maji maalumu yaliyochanganywa na chumvi na
sukari.
(d)Mgonjwa apelekwe hospitali haraka.
3.Mtu aliyevunjika mfupa.
Mtu anaweza kupata jeraha la kuvunjika mfupa kutokana na
sababu mbalimbali kama vile;
@Ajali ya kuanguka.
(b)kugongwa wakati wa michezo.
(c)magari kugongana au kupinduka.
Mtu aliyevunjika mfupa anaweza kutambulika iwapo
atashindwa kutumia kiungo kilichopata ajali ,kwani sehemu
iliyoumia huwa na maumivu makali.
Kuna mivunjiko ya aina mbalimbali.
(A)Mvunjiko wa mfupa kwa ndani.
Mfupa huvunjika vipande viwili bila mfupa kutokeza nje ya
ngozi kwani Mara nyingi nje huonekana uvimbe tu.
(B)Mvunjiko wenye jeraha.
Mvunjiko wa jeraha unakuwa wa aina mbili yaani ,
*Mfupa huvunjika vipande viwili ambavyo huchoma kwenye
mnofu na kufanya jeraha bila kutokeza nje ya ngozi.
*mchoro hapa
*mfupa huvunjika vipande viwili na kutokeza nje ya ngozi.
Jeraha huonekana katika sehemu inayozunguka Mvunjiko kwa
ndani na nje ya ngozi.
Mchoro hapa.
(C)Mvunjiko wa kupinda bila ya kukatika vipande viwili.
Mfupa huvunjika bila ya kukatika kabisa vipande viwili kwani
Mvunjiko huo hufanana na kijiti kibichi ambacho kikipindwa
huweza kuvunjika bila kukatika kabisa.
Jinsi ya kumhudumia mtu aliyevunjika mfupa.
(a)Kabla ya kutoa huduma yoyote zuia damu inayotoka.
(b)Mhudumie mgonjwa hapo hapo alipopatia ajali,kama jeraha
linaonekana kwenye Mvunjiko lifunike kwa hali ya usafi na
wala usijaribu kurudishia mfupa katika hali yake ya asili.
(c)Tengeneza kwa uangalifu sehemu ya mwili iliyovunjika kwa
kuifunga kwa magango(mbao) safi na imara.
(d)Iwapo mgonjwa amepata mshtuko,mpatie huduma ya kwanza
kwa ajili ya mshtuko.
(e)Funga sehemu ya mwili kwa gango(mbao)gumu imara na
jepesi.Gango liwe na urefu wa kutosha kutegemeza sehemu yote
ya mwili yenye mfupa uliovunjika na Fanya yafuatayo_
*Funika ngozi katika sehemu ya mwili iliyovunjika kwa
kutumia pedi za pamba ,kitambaa au nyasi laini kwani
humsaidia kuzuia sehemu iliyovunjika kuumizwa na magango
pamoja ba bandeji.
*Yakiwa yanahitajika magango mawili hakikisha yamelingana
kwa hali zote ,kisha weka kila gango kando ya
Mvunjiko,mfano_
a) Iwapo ni Mvunjiko wa mfupa ya kiganja ,weka na kisha
funga magango kutoka ncha za vidole vya mkono mpaka
kwenye kiwiko cha mkono na tegemeza mkono kwenye
mbeleko.
4.Kutokwa na damu puani
Kutokwa na damu puani husababishwa na kupasuka na kwa
mishipa ya damu puani.Mishipa hii inaweza kupasuka baada ya
kushindwa kuhimili msukumo wa damu au kuumizwa.

JINSI YA KUMPATIA HUDUMA YA KWANZA MTU


ANAYETOKA DAMU PUANI
a) Mketishe mgonjwa hali kichwa chake kimeinamishwa

mbele kidogo.
b) Mwambie mgonjwa abane pua kwa dakika tano kwenye

kiungo chenye sehemu ngumu na laini.


c) Mwambie atumie mdomo kutoa hewa na kuvuta hewa .
d) Lowanisha kitambaa safi katika maji baridi na
umwekee kitambaa hicho kwenye paji la uso wake.
e) Damu ikiacha kutoka ,mwambie avute hewa kwa
kutuki pua kwani itamsaidia kuondoa bonge lolote la
damu puani.
f) Iwapo damu inaendelea kutoka mpeleke mgonjwa
haraka hospitalini kwa matibabu zaidi.
5.kuzirai
Ni hali ya mtu kupotewa na fahamu.kuzirai kunaweza
kusababishwa na mambo kama yafuatayo:
a) maumivu makali ya mwili.
b) ulegevu wa moyo.
c) Habari za ghafla zilizo njema au mbaya.
d) kuona au kusikia mambo ya kuogofya.
e) uchovu kutokana na kusimama au kuketi kwa muda mrefu
mahali penye hewa nzito isiyo safi.
f) Kutokwa na damu kwa wingi.
g) Ugonjwa wa kisukari.
Jinsi ya kumpa huduma ya kwanza mtu aliyezirai.

a) Mlaze chali mgonjwa.


b) Legeza nguo zake shingoni,kifuani na kiunoni.
c) Mpatie mgonjwa hewa nyingi safi kwa kufungua
madirisha na milango. Kama mgonjwa yupo nje zuia watu
wasimzingire ili apate hewa safi ya kutosha.
d) Mpepee ili kumpatia hewa nyingi zaidi.
e) Mvutishe pumzi kwa taratibu.
f) kama anavuta pumzi kwa kelele,mgeuze aliyezimia na
kumuweka katika hali ya kifudifudi kidogo.
g) Usimlishe au kumnywesha kitu chochote akiwa katika
hali ya kuzimia.
Katika matukio haya kuna mbinu mbalimbali za kutumia
kufundishia mada ya huduma ya kwanza nazo ni kama
zifuatazo:
_Onesho mbinu,mbinu hii yampasa mwalimu kuandaa vifaa
kufanya vitendo na kuwashirikisha wanafunzi ,kisha wanafunzi
kurudia kufanya kama mwalimu alivyowaelekeza.
_Alika mgeni,mbinu hii mwalimu humualika mgeni kutoka
sehemu nyingine au aliye na uwezo na maarifa ya kufundisha
mada iliyoandaliwa .
-MASWALI NA MAJIBU: Mbinu hii mwalimu huuliza
maswali kuhusu kile alichokifundisha na kuwapa wanafunzi
shughuli ya kufanya au kazi ya kufanya.

Tumetumia mbinu ya igizo dhima katika tendo la ufundishaji na


ujifunzaji kwa kufundisha tukio la utoaji wa huduma ya kwanza
kwa mtu aliyevunjika mkono.

MBINU:Igizo dhima hii huonesha vitendo tunavyopaswa


kuvitumia katika mazingira ya tukio kwa ufasaha zaidi ili
kumpunguzia mgonjwa maumivu na kuendeleza maisha ya
mhanga.
ZANA:Bandeji, mbao, kitambaa, kamba.
Hatua ya kufuata wakati wa kutumia mbinu ya Igizo dhima
katika kutoa huduma ya kwanza kwa mtu
i. Kuuliza wanafunzi ntrini maana ya huduma ya kwanza.
Huduma ya kwanza ni msaada wowote anaopewa mhanga ili
kupunguza maumivu baada ya janga alilolipata kabla ya
kupelekwa hospitalini kwenda kupata huduma zaidi.
ii. Kuongoza wanafunzi kuorodhesha vifaa vinavyotumika
kumhudumia mtu aliyevunjika mfupa .
Bandeji, mbao, kitambaa, kamba.
iii. Kuongoza wanafunzi kuonyesha igizo dhima kwa kufuata
hatua za kumpa huduma ya kwanza mtu aliyevunjika
mfupa.
HATUA
 Kuchunguza na kugundua sehemu iliyovunjika .
 Kuzungusha kitambaa katika eneo linalozunguka mfupa
uliovunjika.
 Kuweka mbao mbili pembezoni mwa sehemu iliyovunjika.
 Tumia bandeji kufunga hizo mbao mbili .
 Kisha pitisha kamba mkononi hadi shingoni
iv. Mpeleke mgonjwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

b)Tumia mifano ya kutosha kufafanua dhana ya viumbe hai.


VIUMBE HAI ni vitu vilivyo hai kama vile binadamu,
wanyama ,mimea na bacteria. Na pia Viumbe hai vimeundwa
na chembe hai ndogondogo sana zinazoitwa seli.

Katika uundaji huo wa viumbe hai tuone mfululizo mzuri wa


muundo wa kiumbe hai ambayo ni
Seli_ Tishu _ Ogani _ Mfumo_ Kiumbe halisi.
-SELI ni kiini cha msingi wa uhai wa kiumbe
-Tishu ni seli zilizojiunga kufanya kazi moja au zaidi ,mfano
mshipa wa damu .
-Ogani ni tishu zilizounganika kwa pamoja ili kufanya kazi
moja au zaid. mfano; moyo ,mapafu, figo ,ini na kongosho.
-Mfumo ni ogani zilizoungana kwa kufanya kazi moja au zaidi
kwa kutegemeana.
-Kiumbe ni matokeo ya mifumo inayoshirikiana na
kutegemeana.
SIFA ZA VIUMBE HAI
 Kukua
 Kujongea
 Kula
 Kuzaliana
 Kupumua
 Kutoa takamwili
 Huhitaji chakula

Makundi ya viumbe hai


 Protista
 Fungi au kuvu, mfano uyoga
 Animalia au wanyama ,mfano binadamu
 Plantae au mimea
 Monera

AINA YA VIUMBE HAI


a) Mimea
b )Wanyama

MIMEA
Mimea imegawanyika katika makundi mawili, makundi hayo ni
mimea inayotoa maua na mimea isiyotoa maua. Mimea inayotoa
maua imegawanywa katika makundi mawili, makundi hayo ni
1)Mimea aina ya Monokotiledoni
Mimea aina ya monokotiledoni vena za majani yake ni
sambamba, ina mizizi ya nyuzinyuzi ambayo imejitokeza
kwenye kitako cha shina, haina mzizi mkuu na mbegu zake ina
kotiledoni moja. Mfano wa mimea hiyo ni mahindi,
mtama ,uwele na mpunga.
2)Mimea aina ya Daikotiledoni
Mimea aina ya daikotiledoni imegawanyika katika jamii ya
mikunde na isiyo ya mikunde, Mimea jamii ya mikunde mizizi
yake ina vinundu na pia husaidia kurutubisha udongo, mfano:
karanga ,mkunde na mharagwe.Na pia mimea isiyo ya mikunde
mizizi yake haina vinundu, mfano: mwembe na mpera.
SEHEMU ZA MBEGU
Mbegu ina sehemu kuu tatu
 Gamba au testi (sehemu ya nje ya mbegu)
 Kiinitete (mmea mchanga)
 Ghalambegu au kotiledoni (sehemu ya kuhifadhia chakula
kwa ajili ya mmea mchanga).

Sehemu za nje za ua:


 Kikonyo(kinaungana na tawi la mmea au shina na ua).
 Sepali(hushikilia ua na huhifadhi ua cha nga)
 Petali(huvutia wadudu)
Sehemu za ndani za ua:
 Stameni(sehemu ya kiume ya ua inayotoa poleni au
chavua).
 Stigma( hupokea poleni)
 Ovari(hupevuka na kuwa tunda)
 Staili(hupitisha poleni hadi kwenye ovari)
Sehemu za kike za ua huitwa PISTILI-(Stigma, Staili na ovari)
na sehemu za kiume za ua zinaitwa TASMENI (Kichavuo na
filamenti).

UCHAVUSHAJI ni tendo la kusafirishwa kwa chavua kutoka


kwenye chavulio hadi kwenye stigma.
Njia za uchavushaji
 Uchavushaji pekee(chavua hutoka kwenye chavulio ya ua
na kutua kwenye stigma ya ua hilohilo).Vitu vinavyosaida
uchavushaji huu ni ndege na wadudu.Mfano wa mimea ni
boga na haragwe.
 Uchavushaji mtambuko(chavua hutoka kwenye chavulio
za ua na kutua kwenye stigma za ua jingine la mmea wa
jamii hiyohiyo).Vitu vinavyosaidia uchavushaji huu ni
wadudu na upepo. Mfano wa mimea ni mahindi.
Chakula cha mimea hutengenezwa katika majani ,kitendo cha
kusafirisha chakula kutoka kwenye majani hadi kwenye mizizi
kinaitwa translokesheni.Mishipa inayosafirisha chakula katika
mmea inaitwa floemu na mishipa inayosafirisha maji na chumvi
za madini toka kwenye udongo kupitia kwenye miziz ya mimea
huitwa zailemu.
Tabia za mmea katika kuitikia vichocheo
 JIOTROPIZIMU(mizizi hukua kuelekea chini na shina
kuelekea juu)
 FOTOTROPIZIMU(shina hukua kuelekea nishati ya
mwanga iliko)
 HAIDROTROPIZIMU(mizizi hukua kuelekea maji yaliko)

WANYAMA
Wanyama wamegawanyika katika makundi mawili nayo ni
 Protozoa -wenye chembe hai (seli)moja tu mfano:Amiba na
Paramesiam.
 Metazoa –wenye chembehai zaidi ya moja
mfano:binadamu.
Wanyama wamegawanyika katika aina mbili nazo ni
 Wenye uti wa mgongo
 Wasio na uti wa mgongo

Wanyama wenye uti wa mgongo wapo katika makundi matano


nayo ni kama ifuatavyo
 Samaki mfano dagaa na sangara
 Amfibia mfano chura na chura magamba
 Reptilia mfano nyoka na kenge
 Ndege mfano bata na kuku
 Mamalia mfano binadamu na ng’ombe

Wanyama wasio na uti wa mgongo wamegawanyika katika


jamii zifuatazo
 Amiba na Paramesiamu
 Athropoda mfano Inzi-miguu sita
Buibui-miguu nane
Jongoo-miguu zaidi ya nane
 Mollusca mfano konokono
 Annelida -mminyoo bapa mfano tegu
-minyoo duara mfano Askari na safura
-minyoo yenye miili iliyogawanyika
mfano minyoo ya ardhini
 Echinodemata

You might also like