You are on page 1of 3

SOMO LA 3: JE, MTU AKIFA ANAKWENDA WAPI?

Kifo ni adui mkubwa wa binadam. Amekua mgeni asiyebisha hodi na hutokea popote na wakati wowote.
Hachagui tajiri wala masikini, msomi na asiyesoma, warefu na wafupi. Kutokana na maumivu makali
yanayoletwa na kifo, Imani nyingi zimeibuka zikiwa na mafundisho mbalimbali juu ya Kifo. Nyingi zikiwa
na lengo la kuwafariji wafiwa, zingine ni kukuza umizimu. Mafundisho makubwa yaliyotawala kwa
sehemu kubwa ni juu ya kutokufa kwa ROHO. Kwamba mtu anapokufa Roho huenda mbinguni kwenye
raha, au Kuzimu kupata adhabu ya milele. Imani nyingine ni ile ya kuzaliwa upya (Reincarnation) kwamba
kama mtu atatenda mema akifa atazaliwa tena akiwa na maisha mazuri katika familia tajiri, au hata ya
Kifalme. Lakini mtu akitenda mabaya atazaliwa akiwa mtu duni au hata kiumbe kingine kama mjusi, chura
nk. Imani nyingine ni ile inayoamini kwamba kifo ni usingizi. Kwamba mtu anapokufa hupumzika kwa
muda hadi Yesu atakaporudi na kuwafufua wapate Kuurithi uzima wa milele, na wengine hukumu ya
jehanam.
Pamoja na Imani zote na zingine sijataja, ni bora kuangalia fundisho la Biblia juu ya hali ya wafu. Wakati
Fulani tunaguswa na misiba mathalan umefiwa na Mke au Mume, mtoto au rafiki wa karibu, ukiwa katika
wakati mgumu Unatarajia walau sauti inayokuhakikishia kwamba Marehem yuko sehem salama, anapata
raha. Lakini je tungependa kusikia faraja ya uongo au ya kweli ambayo ni sawa na maandiko Matakatifu?
Nilihudhuria ibada moja ya mazishi ambayo ilianza kwa muziki wa taratibu. Baada ya kusoma Maandiko
na kuomba Mchungaji alianza kuhubiri. Aliwahakikishia waombolezaji kuwa marehemu alikuwa hajafa
kabisa alikuwa mzima na alikuwa mbele za Mungu. alikuwa akitazama kutoka mbinguni kila kilichokuwa
kinaendelea katika ibada hiyo ya mazishi. Marehem alizaniwa kuwa yuko kwenye hali bora Zaidi ya
maisha.
Kwa kuanza Ufafanuzi wa Biblia kwanza tufaham nini maana ya kifo. Kamusi ya Oxford inaandika End
of something mwisho wa kitu. Ili kupata ufafanuzi mzuri kwanza tujue nini kinamfanya mtu kuwa HAI.
Uhai ni Mwili jumlisha pumzi Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani
pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai. Mwanzo 2:7. Tazama hii UHAI=Mavumbi+Pumzi. KIFO=Mavumbi-
Pumzi ya Uhai.
Imani nyingi hata Wakristo zinafundisha kuwa Kuna Mwili, Kuna pumzi, na nafsi (Roho isiyokufa). Biblia
inaandika akampulizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai Hivyo mtu anapokufa anarudi kuwa
mavumbi. Mwanzo 3:19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika
hiyo ulitwaliwa, kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi Huko mavumbini miili
itapumzika hata Yesu atakaporudi mawinguni. Jifunze mafungu yafuatayo ili kuelewa Hali ya wafu.
hatimaye uwe na tumaini la kweli katika Kristo. Usikubali kudanganyika wakati ukweli huu umewekwa
wazi kabisa, hakuna toharani wala pagatory badala yake mafundisho kama hayo yanatumiwa na ibilisi ili
kupalilia umizimu. Kwamba unaweza kuwasiliana na ndugu aliekufa, au akawatokea wakati Fulani. Hizo
ni Roho zidanganyazo Biblia inasema. Soma 1samweli 28:7-14
Yohana 11:11-14 Yesu alifananisha kifo na usingizi Biblia inafananisha kifo na usingizi Zaidi ya mara
50.
1Thesalonike 4:15, 16 wale waliolala katika Kristo watafufuliwa atakapokuja.
Yohana 5:28, 29 Kuna ufufuo wa aina mbili. Wa uzima na mauti.
Mwanzo2:7 Mungu alimuumba mtu kwa mavumbi ya ardhi na kumpulizia puani pumzi ya uhai, na mtu
akawa nafsi hai. Mungu hakuweka nafsi ndani ya mtu kama walimu na wahubiri wengi wanavyotufundisha.
Muhubiri 12:7 Mwili huyarudia mavumbi na Roho humrudia Mungu. Biblia haisemi nafsi humrudia
Mungu, bali Roho.
Ayubu 27:3 Roho ni sawa na pumzi au uweza wa Mungu uletao uhai.
Zaburi 146:3,4 Pumzi au Roho inapomrudia Mungu, mawazo hupotea
1Timotheo 6:16 Wanadam hawana uzima wa milele, ni Mungu pekee asiyepatikana na mauti.
Rumi 2:7 sisi tunatafuta uzima wa milele. Biblia inalitumia neno Roho mara 1600, lakini hakuna mahali
inaposema roho isiyokufa.
1Korintho 15:51-54 Yesu atakaporudi ndipo tutakapovikwa kutokufa.
Zaburi 115:17 Wafu hawamsifu Mungu.
Matendo 2:34 Daudi hakupanda mbinguni alipokufa, bali anangojea kuja kwa Yesu na ufufuo wa
kwanza.
Muhubiri 9:5 wafu hawajui neno lolote.
Ezekiel 18:4Roho (Mtu) itendayo dhambi itakufa.
Ufunuo 1:17-18 Mimi ni wa Kwanza na wa Mwisho na alie Hai, nami nalikuwa nimekufa natazama ni hai
hata milele na milele nami ninazo funguo za mauti na za kuzimu. Yesu ana funguo za Mauti (Uwezo wa
kuhuisha) kuzimu ni kaburini penye giza na sio motoni. Yesu ni limbuko la waliolala. Atawafufua
wapendwa wetu waliolala siku atakaporudi mawinguni maana ana mamlaka. Alimtoa Lazaro aliyekufa siku
nne. Paulo Mtume wa Kristo anaandika Angalieni nawaambia ninyi siri; hatutalala sote, lakini sote
tutabadilika, kwa dakika moja kufumba na kufumbua wakati wa parapanda ya mwisho. Maana parapanda
italia na wafu watafufuliwa wasiwe na uharibifu nasi tutabadilishwa. 1Wakorintho 15:51-52.

HEALTH TIPS!!!!
AFYA YA INI
Kuna vitu vya pekee sana katika mwili wako kama vile ini: Siyo kwamba ini ni kiungo kikuu tu katika
mwili wa mwanadamu lakini pia lina fanya kazi nyingi kuliko viungo vingine vingi katika mwili. Kuchuja
sumu mwilini, hutoa nyongo inayosaga chakula, kuongoza kemikali mbalimbali mwilini. Uharibufu
wowote ukitokea katika ini hakuna awezaye tena kufanya marekebisho ili ini liweze kuendelea na kazi
yake. Ini hakika ni zawadi ya pekee kutoka kwa Mungu.

KUNA MAMBO MAKUU SITA YANAYOPELEKEA UHARIBIFU WA INI


1. Kulala kwa kuchelewa sana na kuchelewa kuamka asubuhi.
a. Saa 3-5 Usiku ni mda ambao mwili unajisafisha kuondoa sumu na madawa (detoxification) katika
mwili (lymph nodes) muda huu mtu anapaswa kupumzika au kusikiliza muziki wa taratibu kwaya
isiyokuwa na midundo. Kama mda huu mama atakua akihangaika na watoto mara vyombo basi hatua
hii ya kuondoa sumu haitafanyika vizuri na haitakua na matokeo chanya.
b. Saa 5-7 Usiku Sumu inakua ikiondolewa katika Ini. Inafanyika mtu anapokuwa katika usingizi mzito
c. Saa 7-9 Usiku Uondoaji wa sumu unahamia kwenye gall bladder pia hufanyika wakati mtu akiwa
katika usingizi mzito
d. Saa 9-11 Asubuhi Sumu inaondolewa katika mapafu, hivyo mtu anaweza kukohoa au chafya,
mtu haitaji kutumia dawa kwasababu uondoaji wa sumu umefika katika mfumo wa hewa.
e. Saa 11-1 Asubuhi Sumu inaondolewa katika Colon utumbo unakuwa hauna kitu.
f. Saa 1-3 Asubuhi mwili unanyonya virutubisho kutoka utumbo mdogo. Hakikisha unapata
kifungua kinywa cha maana kwaanzia 1230-3000Asubuhi. Kuchelewa kulala na kuchelewa
kuamka inaharibu mpangilio wa uondoaji sumu hivyo Ini linajawa na sumu.
2. Kutokukojoa asubuhi na Kutopata kifungua kinywa
3. Kutumia dawa nyingi za hospitalini marakwamara (Drugs)
4. Kula kupita kiasi {overeating} hii ni njia kuu ya kufanya uharibifu katika ini lako, wewe kula tu kila kitu
unachotamani na utavuna uharibifu wa ini.
5. Kula na kunywa visivyofaa: kuna baadhi ya vitu ambavyo ini lako halipendi hata kukutana navyo mfano
ngano nyeupe, vyakula vya viwandani kama vile juisi na vyakula vyote vitengenezwavyo
viwandani{prossesing food, refined white flour product} na baadhi ya mafuta.
6. Kukosa vyakula vyenye protein pamoja na fati.
7. Kula vyakula vibaya kama vile caffeine, alcohol {pombe kwa aina zake zote} na madawa ya kulevya.
8. Kuvuta hewa yenye sumu huathiri ini moja kwa moja.
Note: jitahidi kuupenda mwili wako kwa kula vyakula na vinywaji vyenye kuujenga mwili wako kwa kuwa
utapata afya njema kumbuka Mungu amekupatia hekalu lake ili kulitunza kwa kula vizuri kwa afya
kushindwa kuutunza mwili wako kwa uzembe ipo siku utadaiwa na yule aliyekupatia.
Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na bbc umebaini kuwa, Homa ya Ini husababishwa na Ngono
isiyosalama ambapo Mwanaume na Mwanamke hulambana sehemu za siri. Ni vyema kushiriki tendo la
ndoa kwa mwenzi mmoja na usafi uwe kipaumbele.
NAMNA YA KUTUNZA INI LAKO
Hakikisha unakula vyakula vyenye potassium kwa wingi kama vile mchele, ndizi, ngano nyeusi,
mbegu mbalimbali kama vile mbegu za maboga, mbegu za matunda mbalimbali, almond na vingine vingi
vinavyofanana na hivyo.
Kunywa maji kwa wingi. Kunywa kidogo kila bada ya muda. Mfano asubuhi unapoamka kunywa
glass mbili za maji, baada ya masaa mawili kunya glass moja kunywa baada saa moja. Hakikisha kila
unapoenda kuoga unakunywa maji glass moja, wakati unapoenda kulala kunywa glass moja ya maji.
Kunywa juisi ya matunda kwa wingi, tengeneza juisi mwenyewe hasa juisi ya carrot na beet.
Jitaidi kutumia mafuta kidogo kwa chakula na jitaidi kutumia alizeti kuwa sehemu kubwa katika
matumizi ya vyakula vyako.
Jitaidi kula matunda ya apples kwa wingi angalau kila siku apple moja.
Tangawizi ni nzuri kwani ina nafasi kubwa ya kulinda ini lako, fanya tangawizi kuwa sehemu ya
kinywaji chako kila siku.
TUMAINI
Ni wale tu wanaosoma neno la Mungu na kusikia sauti ya Mungu ikisema nao ndio wanafunzi wa
kweli. Wanatetemeka wanaposoma neno la Mungu kwa hao ndio wanaoishi ukweli, na ili kuisikia
sauti ya Mungu tunapaswa kumsihi Mungu atuwezeshe na kumkabidhi yeye yale yote
yanayotutenganisha na yeye.

Ubarikiwe sana Rafiki!! Baada ya kusoma mafundisho haya, Je sasa unaamini kwa usahihi hali ya Wafu?
Je ungependa kujifunza Zaidi?. Tafadhali tuandikie tujifunze2017@yahoo.com kwa swali au namna ya
kuboresha huduma zetu. Pia kama kuna mada inakutatitiza usiache kutuandikia.
WITO: Je ungependa kutoa maisha yako kwa YESU ili awe Bwana na Mwokozi wako binafsi? Je una
jambo linalokusumbua, yaweza kuwa ugonjwa, Kazi, Ndoa, Mahusiano, Kipato, Biashara, Hujapata
watoto, na Unataka Mungu akutendee? Tafadhali tuandikie_

Nataka Kujifunza: Jina Kamili________________________________


Nmaba za Simu_____________________________
Maombi au Ushauri: Jina Kamili______________________________
Hitaji lako________________________________
Namba ya simu_____________________________

You might also like