You are on page 1of 2

FALSAFA JUU YA MTU ALIYEKUFA KATIKA JUKWAA LA IMANI ZETU

Leo hii kumekuwa na mitazamo ya imani mbalimbali kuhusiana na mtu aliyekufa


na kile kinachoendelea baada ya kifo.
Mitazamo mbalimbali
1. kundi la kwanza huamini kuwa mtu akifa roho yake huchukuliwa na kwenda
kwenye moto wa utakaso “PARGATOR” ikiwa alikuwa mdhambi.
Ndugu zake huomba na kutoa sadaka kwenye misa kisha husamehewa na
kukubaliwa na Mungu kuingia mahali pa raha..

2. Wahindu huamini kuwa mtu akifa roho hutoka na kwenda kwa maji / bwawa/
na endapo ng’ombe akija kuyanywa ndipo hupata mimba na kuzaa ndama
ambaye huendeleza maisha ya mtu aliye kufa.

Eg: hilo ndiyo limezaa tamko la kusema heri kuzaliwa mbwa Ulaya.

3. Waislam – wao huamini kuwa mtu akifa anasikia lakini hushindwa kujieleza
na pia anapokuwa kaburini, malaika mwenye kirungu huja na kumuuliza
maswali na endapo hatojibu maswali hayo ipasavyo atapigwa virungu
mpaka ardhi ya saba.

Uchambuzi wa mada.
Mwanadamu nini?

MWANZO 2:7, Mavumbi + pumzi ya uhai = nafsi hai.

QUR –AN 15:26-29 Tulimuumba, binadamu kwa udongo kasha tukampulizia


pumzi,roho inayotokana na sisi.
Kifo ni nini?
Kwajumla kifo ni kukoma kwa uhai., na uhai huletwa na kuwepo kwa pumzi ya
uhai,hivyo kifo ni kukoma kwa pumzi ya uhai.

MWANZO 7:22 Kila chenye pumzi kikifa.


QUR-AN 7:185 Kila nafsi {roho} itaonja mauti.

Hivyo kuonja mauti kwa nafsi humaanisha kukoma kwa pumzi ya uhai – maana
ni kwa hiyo pumzi ndipo hupatikana nafsi hai.

Wafu wako wapi?

Zaburi 146:4 Mtu hurudia udongo.


Qur an 35:22 Wala hawawi sawa walio hai na wafu,kwa yakini Mungu
humsikilizisha amatakaye; na wewe huwezi kuwasikilizisha waliomo
makaburini.( na hao kama wamekufa,wamo makaburini).
Mkazo wa Biblia:
Mhubiri 3:16-22 Nani ajuaye kuwa roho ya mtu huenda juu naya
mnyama…………..
Matendo 2:34 Daudi hakupanda mbinguni…………

Lini mtu huenda mbinguni?

Yohana 5;28-29 waliyomo makaburini watasikia sauti yake…………


Qur 23:16 kisha hakika ninyi siku ya kiyama mtafufuliwa……………

Je wafu wanaweza kusikia?


Kudai kuwa mtu aliyekufa anaweza kusikia ni sawa na kusema kuwa mtu huyo amerejea
tena kuwa hai, lakini maandiko yanaseama wazi juu ya hali ya mtu aliyekufa.

Mhubiri 9;5 Mawazo yake hupotea…


Ayubu 14;14 Mtu akifa hawezi kuwa hai tena….

Maandiko hayo yanaonesha kuwa kamwe mtu aliyekufa hawezi kusikia,kwakuwa kwanza
mawazo yake {hali ya upambanuzi hupotea},pia sehemu nyingine ya maandiko upande wa
Qur an unaonesha juu ya mtazamo kuhusu kifo….

Qur an 25;47 ..amekufanyieni “usingizi” kama kufa, na mchana uwe ndiko


Kufufuka…
Qur 27;80 Kwa hakika huwezi kuwasikilizisha wafu mwito (wako) wala
kuwasikilizisha viziwi, (hasa) wanapogeuka wanakwenda zao.

Wafu wanaweza kuombwa au kuombewa?


Pamoja na hayo yote tuliyokwisha kuyaona hapo nyuma,pia kumekuwa na dhana
kuwa mtu aliyekufa anaweza kuombewa au kuombwa na hayo yote yakazaa
matokeo Fulani kwake au kwa mtu anayefanya hayo.

Swali la msingi ni je maandiko yanaseamaje?


Marko 12:27 Mungu si Mungu wa wafu bali wa waliohai.
Zaburi 115:17 Si wafu wasifuo, wale washukao katika kimya.
Zaburi 146:1-2 Nitamsifu Mungu ningali hai.

Qur 13:31 Qur an haina kazi ya kusemesha maiti….


Tunaweza kuwaomba wafu?

Qur an 12:106 wengi katika wao hawamuamini Mwenyezimungu …..


Soma ufafanuzi wa aya hiyo
*haya hapo kwetu sisi tunayo,japo tunafuata uislam ila tunatia ushirikina,
tunakwenda kwenye makaburi tukayaambia – Bwana nimesongwa na
ukinifungua nitaleta kwako kombe la harua……., anasikia wapi huyo
maiti? Si bure tu mnabwabwatika? Mwenyezi mungu amesema weee
katika Qur an kuwa wafu hawasii…………………..
yes’ mr Manusu- its just a short presentation on death- Mapima’s

dominicmapima@yahoo.com / its my Email address.

You might also like