You are on page 1of 122

ROHO AKIFA NDANI

YANGU KWA SHERIA


TORATI HUADHIBIWA
KWA NEEMA

BY APOSTLE: MOSES DISMAS MNDIMA


ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI


HUADHIBIWA KWA NEEMA

BY APOSTLE: MOSES DISMAS MNDIMA

P.O.BOX 33375

DAR ES SALAAM

SIMU 0622-147368/0719-776484

E-MAIL: mosesnyaky@gmail.com

ii
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI


HUADHIBIWA KWA NEEMA

P.O.BOX 33375

DAR ES SALAAM

SIMU 0622-147368/0719-776484

E-MAIL: mosesnyaky@gmail.com

TOLEO LA KWANZA – 2021

ISBN 978-9976-5229-0-7

Haki zote zimehifadhiwa, airuhusiwi kunakiri, kuchapisha, wala


kutafsiri kipengele chochote katika kitabu hiki kwa kutumia kifaa
chochote cha kieletroniki, kutoa nakala pasipo idhini ya mwandishi wa
kitabu hiki. Kitabu hiki ni mali halali ya Mtume Moses Dismas Mndima
(Apostle Mndima) wa kanisa la Huduma ya Mlima wa Utukufu, kwa
unakiri wa kitabu hiki, wasiliana na mwandishi wa kitabu hiki kwa
mawasiliano hayo hapo juu.

iii
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

SHUKRANI
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mungu Baba wa Bwana wangu
Yesu Kristo, kwa Neema zake nyingi kwangu alizozizidisha kupita
kimo cha mawingu na nyota za angani; na kwa Roho wake Mtakatifu
Mwalimu wangu, kwa kunifundisha na kuniongoza toka kuanza hadi
kukamilika kwa uandishi wa kitabu hiki.
Pili, napenda pia kumshukuru Mtumishi wa Mungu, Mtume na Nabii
Agness Gervas Mgonde, kiongozi mkuu wa Huduma ya Mlima wa
Utukufu, kwa msaada wa ushauri na ushirikiano wake wa hali na mali
aliouonyesha kwangu kipindi chote cha uandishi na ukamilishaji wa
uandishi wa kitabu hiki, Mungu akubariki sana Mama; hakika sina cha
kukulipa, ila Mungu mwenyewe atakulipa kwa Baraka zake za rohoni
kwa kipimo cha kusukwasukwa hadi kumwagika.
Nawashukuru pia watumishi wote mlioshiriki kwa namna yeyote
katika uandishi wa kitabu hiki, siwezi kuwataja majina wote kutokana
na wingi wa idadi yenu, lakini Roho wa Bwana mwenyewe atawataja
kila kisomwapo kitabu hiki, na Mungu wa Mbinguni atawakumbuka
na kuwazidisha. Na mwisho, ila sio kwa umuhimu; napenda kutumia
nafasi hii adimu na adhim, kuishukuru familia yangu kwa msaada na
mchango wao kwangu dhidi ya uandishi wa kitabu hiki, lakini zaidi
niwashukuru kwa kunivumilia sana kwa kipindi chote walichonihitaji
bila mafanikio, kutokana na Muda wangu mwingi kutumika katika kazi
ya uandishi wa kitabu hiki. Ahsante familia yangu, haswa Mke wangu
kipenzi, Protasia S Komba; Mungu awabariki na kuwatunza.

iv
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

YALIYOMO
SHUKRANI……………………………………………………………………………………..……...…iv
UTANGULIZI……………………………………………………………..…………………………...…vi
SURA YA 1: ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA…………………..……....….1
ROHO NI NANI………………………………………………………………………………….....…10
ROHO ILIYOKUFA NDANI YA MTU KWA SHERIA……………………………………....13
SURA YA 2: MPANGO WA MUNGU KUUMBA MTU KWA SURA YAKE….....…16
MUNGU AUMBA MTU………………………………………………………………………...….16
SURA YA 3:ASILI YA TORATI NA KAZI YAKE………………………………….……….......31
ASILI YA TORATI…………………………………………………………………..……………….....31
SURA YA 4: MAUTI NA CHANZO CHA KUFA KWA ROHO NDANI YAKO......…41
MAUTI NI NINI………………………………………………………………………………….…....41
NGUVU YA MAUTI……………………………………………………………………..……..…….45
KWANINI TUNKUFA…………………………………………………………………………...…...57
SURA YA 5: FALSAFA ZA UHAI WA MUNGU NDANI YA MTU……………….....…63
FALSAFA NI NINI………………………………………………………………………………...…..63
SURA YA 6:KUSULIBIWA KWA SHERIA YA MAUTI MSALABANI……….….....…70
SURA YA 7: ROHO UHUISHWA KWA NEEMA……………………………………...……76
USHINDI WA VITA VYA KIROHO DHIDI YA UHAI WA MTU……………….......….87
ROHO UHUISHWA KWA NEEMA…………………………………………………….....…...96
KAZI YA NEEMA KWENYE UHUISHO……………………………………………….......….98
HITIMISHO……………………………………………………………………………………….…..112
SALA YA TOBA…………………………………………………………………………..……....….114

SALAMU ZA MWANDISHI……………………………………………………………..……….115

v
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

UTANGULIZI
Somo hili ni hatua muhimu sana, yenye elimu kwa ajili ya mabadiliko
ya maisha yako halisi ya kiroho, yatakayotumika kubadilisha hali yako
ya maisha yako halisi ya kimwili, na kukupa aina mpya ya maisha yasio
ya asili yako kimwili kutoka rohoni mwako, ili kujenga ushuhuda wa
nguvu ya msalaba, na kifo cha Kristo Yesu kwa ajili yako. 3Yoh 1:2
inasema ‘’Mpenzi, naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na
afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
Kwa kuwa Kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu, ili kwamba; tukiwa
wafu kwa habari ya dhambi zetu, tuwe hai kwa habari ya haki yake.
Maana imeandikwa ‘’Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika
mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi; tuwe hai
kwa mambo ya haki, na kwa kupigwa kwake mliponywa (1Petr 2:24).
Kitabu hiki kimeandikwa kwa msaada wa Roho Mtakatifu, ili kutoa
mwanya mpana na njia nyofu ya watu wa Mungu kuusogelea upendo
wa Baba yao (MUNGU) kama wana halisi wa Baba; kwa kutusaidia
kutambua nafasi ya Mungu (BABA) kwenye maisha yetu, yeye akiwa
kama Baba yetu halisi, na kutambua nafasi yetu kwake sisi kama
watoto wake.
Katika kitabu hiki, tutajifunza na kujikumbusha mambo ya msingi ya
kiroho yatakayotuunganisha kwa maungamo thabiti mbele za Mungu
Baba yetu, ili tupate kibali cha kukisogelea tena kiti chake cha Neema
na kupata Rehema. Kitabu kimebeba mambo makuu matatu ya
msingi, ambayo ni Uumbaji, Anguko, Wokovu

vi
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

SURA YA KWANZA: ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA


SHERIA

ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA


Tunaposema kwamba! “roho akifa ndani yangu au ndani ya mtu kwa
sheria” tunamaanisha kwamba! Mtu ni nafsi hai katika mwili,maana
yake ni kwamba! Uhai uliopo kwa mtu huyo unampa haki ya kuishi
milele bila kufa, yaani hakutakiwa kufa (Kuwa na ukomo wa muda wa
kuishi) na uhai wenyeweumefichwa katika asili na lengola kuumbwa
kwake ambalo ni kutenda matendo mema aliyoyatengeneza Mungu
(Pasipo sheria), ili tuyaishi kwa sheria, kwa maana pasipo ile sheria
inayomkataza Adamu kwa kusema ‘’usile tunda la mti wa ujuzi wa
mema na mabaya’’ basi tusingalikuwa na ujuzi wa kutambua hayo
matendo mema ambayo tuliumbwa ili tupate kuenenda katika hayo.
Efeso 2:10 imeandikwahivi ‘’Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika
Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu
aliyatengeneza ili tuenende nayo.’’
Na katika kutenda matendo hayo mema, ndipo tunapokea nguvu ya
Mungu ya kutawala na kuishi maisha ya milele
Sasa ili mtu aweze kutenda hayo matendo mema, na kuishi milele,
yaani asiwe na ukomo wa muda wa huo uhai ndani yake; Mungu
alimuwekea mtu sheria za kuishi. Kwa hiyo; inapotokea roho ya mtu
akifa ndani yake, ujue wazi, ni dhahiri kwamba! Yeye mwenye roho
hiyo (Huyo mtu), amepoteza sifa yake mbele za Mungu ya kuishi
milele kutokana na kuivunja ile sheria ya kuishi (ametenda dhambi).
Kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti ‘’Rum 2:23’’. Imeandikwa
Tunapozungumza kwa habari ya kufa kwa roho ya mtu ndani yake,
hatumaanishi habari ya roho hiyo kuachana na mwili (Kufariki
dunia); Bali tunazungumzia kuondolewa kwa ule uhai wa uhusiano
kati ya mtu na Mungu (Kufa kiroho) yaani, kukosekana kwa ushirika
wa kiroho kati ya Mtu na Mungu kwa sababu ya kuivunja ile sheria

1
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ya uzima (Mtu kutenda dhambi). Katika kitabu cha Mwanzo 2:7,


Mungu anamuwekea Adamu sheria ya uzima (sheria ya kuishi), na
Mungu anasema hivi ‘’Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema
na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo,
utakufa hakika’’
Sheria hii, ilikuwa inasimamia mpango madhubuti wa Mungu kwa
Adamu, ili Adamu aendelee kuishi maisha ya milele kwa makusudi
ya kuitawala dunia milele, lakini Adamu aliivunja sheria hii; na hapo
ndipo mauti ilipoingilia kati uhai wake na kuukatisha uhai huo, kwa
sababu hiyo; ule mpango wa Mungu wa kutaka Adamu aishi milele
na kutawala milele uliishia hapo kwa agano hilo la kwanza. Ebra 9:15
inasema hivi ‘’Na kwa sababu hii ni mjumbe wa agano jipya’’ hapo
anaposema ‘’kwa sababu hii’’ anatafsiri tendo lililokwisha kutendeka,
ambalo katika hilo tendo, lile agano la kwanza limevunjika, na tendo
hilo ni lile kosa la Adamu wa kwanza lililosababisha mauti ipate njia
ya kuingia Duniani.
Baada ya hilo kosa la Adamu wa kwanza (Mtu wa udongo), ndipo
Mungu akamuandaa mjumbe wa agano jipya la mauti ambaye ni
Adamu wa pili (Kristo Yesu) ambaye ni Mtu wa Roho,ili katika mauti
yake Msalabani, mauti ya kwanza (Kuvunjika kwa uhusiano wa kiroho
kati ya mtu na Mungu wake), yaadhibiwe kwa kukomboa makosa ya
kwanza, (Agano la kale).
Ndio maana maandiko matakatifu yanaendelea kusema kwenye Ebr
9:15 kwamba; ‘’Ili mauti ikiisha kufanyika kwa kukomboa makosa
yaliyokuwa chini ya agano la kwanza, hao walioitwa waipokee ahadi
ya urithi wa milele’’.
Kwa hiyo tunaona; kutokana na lile kosa lililopelekea kuvunjika kwa
agano lile la kwanza, limebadili msimamo wa Mungu juu ya haki ya
uhai wa mtu, hapo kwanza; mtu alitakiwa kuishi milele kama sehemu
ya haki yake ya msingi toka kwa Mungu. Lakini sasa,maisha ya milele
sio haki ya mtu tena, bali ni ahadiya Mungu mwenyewe kwa wale
watu walioitwa kuipokea ahadi hiyo.Kwa kuwa agano la kwanza

2
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

lilipovunjika, lilimtenga mtu na Mungu wake; kwa hiyo mahusiano ya


uhai na utawala kati ya mtu na Munguyakaharibiwakabisa kutokana
na lile kosa (Kutenda dhambi).
Mwa 3:8 imeandikwa hivi ‘’Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu,
akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe
wakajificha kati ya miti ya bustani ili Bwana Mungu asiwaone. Kile
kitendo cha kujificha, ndio utengano halisi kati ya mtu na Mungu
kiroho; na utengano huu ulimsababishia Adamu na mkewe kuondoka
kwenye ile nafasi (Position) ya utawala. Mungu alimuumba mtu Kama
kiti chake cha utawala, ili Mungu atawale kupitia mtu, anasema ‘’Na
tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu’’ Mwa 1:26.
Hilo neno ‘’Kwa mfano wetu na sura yetu’’halibebi kabisa maana ya
kuwa Mungu yupo kama sisi, bali linaeleza kusudi halisi la kuumbwa
kwetu. Na katika kuumbwa kwetu, tumebeba kusudi kuu moja tu la
msingi kabisa, na kusudi hilo ni kumuwakilisha Mungu duniani katika
mwili.
Mungu yeye ndiye aliyeumba dunia (Mbingu na nchi) na kila kitu
kilichopo ndani yake kinachoonekana na kile kisichoonekana; yeye
ndiye Mmiliki na mtawala wa vyote, lakini yeye ni Roho, na dunia ni
mwili; kwa hiyo ili Mungu aliye Roho, aweze kupata kuitawala Dunia
iliyo ya asili ya mwili, ilibidi Mungu aumbe mtu mwenye asili ya mwili
ili Mungu aliye Roho apate kuitawala dunia kapitia mwili wa mtu.
Ndio maana Mungu anasema ‘’Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa
sura yetu’’ ili nini? Ili apate kutawala
Mungu anapozungumza neno ’Kwa mfano wetu’’ na ‘’Kwa sura yetu’’
anazungumzia vitu viwili vikubwa tofauti kabisa.Ambavyo ni:
i. ‘’Kwa mfano wetu’’

Mungu Anaposematufanye mtu ‘’Kwa mfano wetu’’lile neno


’’mfano’’ linawakilisha neno ‘’Kama’’ Kwa hiyo, anaposema ‘’Kwa
mfano wetu’’ni sawa kabisa nakusema ‘’Kama sisi’’ kwamba!
3
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Utakapomuona huyo mtu, aliyefanywa kwa mfanowa Mungu, ni


sawana umemuonaMungu. Yaani huyo mtu ameumbwa badala
ya Mungu; kwa lugha rahisi tunaweza kumuita huyo mtu ‘’mungu
mbadala’’, yaani mtu aliyeumbwa kwa lengo la kumuwakilisha
Mungu katika mwili wake kwa matendo ya roho, ndio maana
katika Biblia imeandikwa, ‘’kwa kuwa wote waongozwao na Roho
wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu’’ Rumi 4:14 Maana yake
ni kwamba! Japo mtu anaishi katika mwili wa damu na nyama,
hapaswi kuenenda kwa kutenda mambo ya mwilini, bali apate
kutenda mambo ya rohoni kwa kuongozwa na Roho wa Mungu
Neno ‘’Mfano’’ ni msamiati uliyotumika kufananisha kati ya mtu
na Mungu, lakini si katika maumbile; kwa kuwa Mungu yeye
ni Roho bila mwili, lakini mtu ni roho katika mwili. Kwa hiyo,
Mungu ametumia neno ‘’Mfano’’ili kuwakilisha au kufananisha
mamlakaya Munguyaliyowekwa juu ya mtu ili mtu apate kutawala
kile ambacho Mungu alitaka kutawala; akiwa na maana kwamba!
Huyu mtu, atasimamia Yaleyote aliyotaka kuyasimamia Mungu
sawa na ambavyo Mungu mwenyewe angesimamia.
ii. ‘’Kwa Sura yetu’’
Neno ‘’Kwa sura yetu’’ linawakilisha neno ‘’Kwa chapa yetu’’ au
‘’Kwa utambulisho wetu’’ ni kama Mungu anasema hivi ‘’tufanye
kitu kitakachobeba uwakilishi wetu’’ili kipate kutuwakilisha; Kwa
hiyo, ile suraya Mungu au chapa ya Mungu kwa mtu inabeba
utambulisho wa uhalali kuwa huyo mtu ni mali na milkihalali ya
Mungu. Mtu kuwa milki ya Mungu, ni matokeo ya mtu huyo kuwa
mali ya Mungu, kwa hiyo Mungu anatumia mali yake (huyo mtu)
katika kutawala mali yake (Dunia), yaani huyo mtu anatawala
mali isiyo yake kwa ajili yamwenye mali yake, ambapo mwenye
mali hiyo, anamiliki mali (Dunia) pamoja na huyo anayeitawala
hiyo mali (Mtu).

4
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kwa hiyo, mtu ni mali ya Mungu, na ametumwa na Mungu


kuitawala Dunia ya Mungu kwa niaba ya Mungu; hivyo mtu
anawajibika kwa Mungu, na sio kwa mchungaji wala wazazi
wake, na kama ikiwa mtu amefanya uwakilishi chini ya kiwango
cha matarajio ya Mungu juu ya uwakilishi wa huyo mtu, Mungu
anaweza kumtoa mtu huyo kwenye hiyo nafasi.
Lakini pia lile Neno ‘’Chapa’’ hutambulika Kama Muhuri wa Mungu,
hivyo Mungu anavyosema ‘’Kwa sura yetu’’ ni sawa kabisa na kama
kusema! kwa muhuri wetu (uthibitisho wa kimamlaka).Ndio maana
Efeso 1:13 inasema kwamba! ‘’Nanyi pia katika huyo, mmekwisha
kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena
mmekwisha kumwamini yeye na kutiwa muhuri na Roho yule wa
ahadi aliye Mtakatifu.
Na hapo anaposema ‘’Nanyi pia katika huyo’’ tunapaswa kujiuliza,
huyo nani..? Maana yake ni kwamba! Hapo anamzungumzia Kristo;
ambaye katika yeye tumelisikia neno la kweli (kuhusu haki yote na
hukumu na mapenzi ya Mungu kwa watu wote) juu ya wokovu wetu
tulioupokea kutoka kwake. Na tumethibitishwa na Roho kuwa sisi ni
wana wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu. Rumi 8:16 inasema
‘’Roho mwenyewe ushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi ni
watoto wa Mungu
Kwa hiyo; lengo kuu la Mungu kumuumba mtu, ni ili mtu huyo apate
kumuwakilisha Mungu katika Dunia juu yaKutawala. Ndipo Mungu
anasema kwamba! Sasa ‘’Tufanye mtu kwa mfano wetu, akatawale’’
Mpango wa mtu kuumbwa haupo kwa mtu, wala Lengo la mtu kuishi
duniani halipo kwa mtu, maana hakuna mtu aliyetaka kuja duniani,
bali Mungu ndiye aliyemleta mtu duniani, hivyo hakuna mtu wala
mzazi wa mtu, wala mganga wa kienyeji, wala mchawi, wala shetani
ajuae mpango na kusudi la mtu juu ya kuumbwa na kuishi kwake.
Hivyo mtu akitaka kuliishi kusudi na mpango wa kuumbwa na kuishi
kwake, ni lazima arudi kutii na kunyenyekea kwa Mungu ili Mungu
apate kumkweza kwa wakati wake kama ilivyoandikwa ‘’Nyenyekeeni

5
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

chini ya Mkono wa Bwana ulio hodari, naye atawakweza kwa wakati


wake’’Kwa kuwa kusudi na mpango wa mtu kuumbwa, ni wazo la
Mungu mwenyewe. Na lengo kuu ni ili mtu apate kutumika chini ya
mamlaka ya Mungu kama kiti cha Mungu ili Mungu apate kutawala
kupitia mtu. Kwa sababu hiyo, Mungu akaamua kumpa mwanadamu
mkono wa shirika kwa kumpa:
• Umilele
Mungu akamwambia Adamu kuwa ‘’Siku utakapokula hilo tunda,
utakufa hakika’’ Kumbe mpango wa Mungu ni mtu aishi milele ili
Mungu aendelee kuitawala dunia kupitia mtu, kwa hiyo; Mungu
anaweka misingi ya sheria ya uzima ili Mtu apate kuishi milele
bila kufa, kwa sababu mtu huyu akifa, itamlazimu Mungu aanze
kufikiri mpango mwingine wa namna ya yeye kuitawala dunia.Na
ukumbuke kuwa! Ule Mpango wa Mungu juu ya kuitawala dunia,
ni yeye Mungu kutawala kupitia mtu.
Kwa hiyo Mungu hana mpango kabisa wa kubadilisha hilo,
mtu anaweza kubadilika au kubadilishwa; lakini Mungu
habadiliki na wala Mpango wake hautabadilika kamwe. Ndio
maana utaona,Mungu anamtofautisha huyo mtu na vitu vyote
viliyoumbwa, kwa kuwa vitu vyote viliumbwa kwa neno, Mwa 1:3-
6. Lakini mtu hakuumbwa kwa neno, yeye aliumbwa kwa mkono
wa Mungu. Mwa 1:26-27
Biblia inaposema juu ya umilele, inamaanisha ni maisha yasiyo
na ukomo wa muda (Uhai wa milele). Uhai wa milele ni sifa kuu
ya Mungu tu, Mungu yeye ndiye wa milele; sasa Mungu kwa
lile kusudi lake juu ya mtu la kutaka mtu atumike kama kiti cha
utawala wa Mungu duniani, alimshirikisha sifa hiyo.
Sifa hii ya kuishi milele sio haki ya mtu, bali ni mpango wa Mungu
kwa mtu kutokana na ule mpango wake ili mtu aishi milele na
Mungu apate kumtumia huyo mtu kuitawala dunia milele; Mungu
alifanya hivyo, kwa kuwa hakuwa na mpango wa kubadili mfumo

6
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

wa kuitawala dunia nje ya mpango wake wa kumtumia mtu

• Utakatifu
Biblia inasema ‘’Mtakuwa watakatifu kwa kuwa Baba yenu wa
mbinguni ni mtakatifu’’ Math 5:48. Utakatifu nao kama ilivyo
kwa uzima wa milele, ni sifa ya Mungu na sio ya mtu; kama ni
sifa ya Mungu, kwanini ilikuwa ni lazima mtu awe nayo hiyo? Jibu
ni kwamba! Lazima mtu awe mtakatifu kwa kuwa Mungu anaishi
ndani ya huyo mtu.
Hapo anaposema kwamba! ‘’Mtakuwa watakatifu’’ ni sawa kama
anatuambia kuwa! Sikilizeni enyi watu, acheni kutenda dhambi;
jifunzeni kutenda mema, kwa kuwa Mungu aliye mtakatifu yeye
anakaa ndani yenu, na yeye kamwe hachangamani na wenye
dhambi; hivyo jitengeni na uovu ili mpate kujitakasa dhambi zenu,
ndipo Mungu atakapowafurahia ninyi na kuwatukuza pamoja
naye, au hamjuiya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na ya
kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu 1Kor3:16
Lengo kuu la Mungu kumpa mtu ushirika huu, ni ili kushirikiana
naye katika wazo la kutawala; yaani mwanadamu amekuja duniani
kama Balozi wa Serikali ya ufalme wa Mbinguniapate kuiwakilisha
mbingu katika dunia.
Hivyo Ilikuwa ni lazima kwa Mungu amtambulishe huyo mtu kuwa
ni muwakilishi wake aliyethibitishwa kimamlaka, yani ana mhuri wa
Mungu (Roho wa Mungu), ili kuthibitisha kuwa huyo mtu ni mali
halali ya Mungu kwa kuwa ule mhuri na ile chapa ndio utambulisho
wa umiliki. Ndio maana Yesu alipoulizwa kuhusu kumpa kodi Kaisari,
aliwaambia wale watu kwamba! ‘’Nionyesheni fedha ya kodi’’ndipo
wakamletea dinari; Yesu Akawaambia, ‘’Ni ya nani sanamu hii (sura)
na anuani hii (utambulisho)’’ wakasema ‘’ni ya Kaisari’’. Akawaambia
‘’Mlipeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu’’.
Math 22:15-22.

7
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kazi ya ule Muhuri kwa mtu, ni kutofautisha kati ya mtu aliye milki ya
Ufalme wa Mungu, na mtu aliyemilki ya ufalme wa ulimwengu huu.
Hivyo neno ‘’Kwa sura yetu, kwa mfano wetu’linamaanisha kwamba;
mtu aliumbwa kama Mungu wa dunia hii, ili apate kutawala kama
Mungu katika mwili, mtu anapopoteza uhusiano wake na Mungu, ile
nafasi, anapoteza nafasi ya kutawala na kuishi milele. Ndipo unaona
Adamu na mkewe wanajificha Mungu asiwaone. Mwa 3:8
Tafsiri ya lile neno linalosema ‘’Asiwaone’ linamaanisha kuwa Mungu
asiwakute kwenye ile nafasi yao ya utawala na umilele; kwa kuwa
hawana uhalali tena wa kuwa hapo, kwa kuwa hawana tena ile
chapa; yaani wamepoteza sifa ya kumuwakilisha Mungu katika miili
yao kupitia roho zao kwa sababu ya lile kosa (Kula tunda/Kutenda
dhambi). Kwao tafsiri ya neno ‘’kujificha’’, haikuwa na maana ya
kutoonekana kwa miili yao mbele za macho ya Mungu; ndio maana
Daudi anasema ‘’niende wapi nijiepushe na Roho yako? Niende
wapi niukimbie uso wako? Kama ningepanda mbinguni, wewe uko;
ningefanya kuzimu kitanda changu, Wewe uko; Ningetwaa mbawa za
asubuhi na kukaa pande za mwisho za bahari, huko nako mkono wako
utaniongoza; na mkono wako wa kuume utanishika. Kama nikisema
“Hakika giza litanifunika’’ na nuru inizungukayo ingekuwa usiku; giza
nalo halikufichi kitu, bali usiku huangaza kama mchana, giza na nuru
kwako ni sawa. Zab 139:7-12
Kwa hiyo neno ‘’Asiwaone’’ halimaanishi kwamba! Adamu na mkewe
hawatakuwepo kwenye mboni ya jicho la Mungu, hapana!
Bali neno ‘’Asiwaone’’ kibiblia, linamaanisha mtu kutokuwepo katika
nafasi (Position) yake mbele za Mungu; Kwa kuwa Mungu katika
kuumba kwake, alimpa mtu nafasi, (Position) ya kutawala dunia na
vyote vilivyomo ndani; lakini Adamu anaipoteza hiyo nafasi, kutokana
na kuasi ile sheria ya Roho wa uzima, ndio maana biblia inasema
‘’Asiwaone’’ maana yake ni kwamba! Hawapo tena kwenye ile nafasi
yao ambayo Mungu aliwapa.

8
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Hivyo; Adamu na mkewe wakajiuza kuwa mali ya shetani, kwa hiyo


hata walipotaka kutoka, haikuwezekana; kwa kuwa hawakuwa tena
mali yao wenyewe; wameuzwa chini ya utumwa wa dhambi na kuwa
mali ya shetani. Ndio maana imeandikwa ‘’Atendaye dhambi ni wa
Ibilisi/shetani, kwa kuwa ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo; kwa
kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi za ibilisi.
1Yoh 3:8.
Anaposema juu ya kuzivunja kazi za Ibilisi, haimaanishi Kuzigawanya
vipande vipande, bali anamaanisha kuzitengua,yaani kana kwamba
hazikuwahi kuwepo au kuzifanya kuwa batili, yaani zisizofaa kabisa.
Na miongoni mwa kazi za shetani zilizovunjwa ni pamoja na:
• Kupofusha fikra za watu na kuzitia giza
Kitendo cha kupofusha fikra za watu, ni moja ya kazi mahususi
za kimkakati za shetani katika kutekeleza mpango wake wa uuaji.
Yesu anasema ‘’Mwivi haji ila aibe, na kuchinja na kuharibu. Yoh
10:10a.Kwa hiyo katika kutekeleza mpango wake huu, shetani
amekamata akili za watu (amezitia giza) ili wasipate kumtambua
Mungu, na hata wakimtambua huyo Mungu, wasipate kumkubali
kuwa ndiye Mungu wa kweli. Rumi 1:21 inasema kwamba! ‘’Kwa
sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu
wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao
yenye ujinga ikatiwa giza’’.
Ibilisi hupofusha fikra za watu wasimtafute Mungu; imeandikwa
‘Toka Mbinguni Mungu aliwachungulia wanadamu, aone kama
yupo mtu mwenye akili amtafutaye Mungu; Zab 12:2-3; Kwa hiyo
baada ya kumtafuta Mungu wao wakajificha Adamu alijifichaili
kujitenga na Mungu, na shetani aliwatia giza wasimtafute Mungu
kwa lengo la kuua roho zao. Katika maisha ya mtu, uhai wake
haupo katika mwili wake; bali katika roho yake. Mwa 3:8.

9
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Na shetani hashambulii mwili wa mtu kwa lengo la kuudhofisha


mwili huo, bali hushambulia mwili wa mtu kwa lengo la
kuangamiza roho yake, ndio maana Yesu amesema ‘’Mwivi haji
ila aibe, achinje na kuangamiza’’ Kinachoangamizwa hapo sio ule
mwili bali ni ile roho, kwa kuwa roho ndio iliyobeba uzima hata
imeandikwa ‘’Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; Maneno
hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima’’ Yoh 6:63
ROHO NI NANI..?
Tafsiri ya neno Roho katika biblia; linabeba maana pana ya nafsi isiyo
na umbo au mwili; kwa Lugha ya kiyunani au Kigiriki, inaitwa ‘’Ruach’’
yaani upepo. Lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya Roho Mungu,
viumbe wa kiroho, na roho ya mtu. Nitakuelezea kwa ufupi.

∗ Roho – Mungu Babana Mungu Roho Mtakatifu


Mungu ni Roho Yoh 4:23; ndiye aliyeasisi uumbaji, yeye ndiye
aliyeviumba viumbe vyote vya kiroho na kimwili, yeye ndiyeasili
ya vitu vyote mbinguni na duniani,Mwa 1:1. Hana mwanzo wala
mwisho; Yeye ni moto ulao. Na Roho Mtakatifu ni nafsi tendaji ya
Mungu Baba; Roho Mtakatifu ni nafsi ya tatu ya Mungu
Mungu ana Nafsi tatu ambazo ni:

1. Mungu Baba

2. Mungu Mwana

3. Mungu Roho Mtakatifu

∗ Roho – mtu
Mwa 2:7 inasema ‘’Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi
ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
Lile neno ‘’Pumzi ya uhai” linabeba tafsiri ya neno ‘’Ruach” yaani
10
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

upepo (roho) ya mtu.. Kwa hiyo, roho ya mtu ni ile pumzi ya uhai
iliyotoka kwa Roho Mungu
∗ Viumbe wa kiroho
Viumbe wa kiroho ni viumbe wasio na mwili/umbo; viumbe
hawa hawaonekani kwa macho ya kawaida, na wanaishi katika
ulimwengu wa roho; wao wametokana na kuumbwa kwa asili
ya Moto ila sio moto. Viumbe hawa wa kiroho wamegawanywa
katika makundi tofauti kutokana na wajibu na majukumu yao
waliyopewa. Na Miongoni mwa viumbe hawa wa kiroho ni
pamoja na Malaika, akiwepo Lusifa au Shetani na jeshi lake.
Lusifa alipewa nafasi Mbinguni kuwa malaika mkuu kabla ya uasi
wake, na ni miongoni mwa malaika aliyeumbwa kwa utukufu
mkuu kuliko malaika wote wa mbinguni wakati huo.
Isaya anasema ‘’Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, ewe nyota
ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Isaya 14:12.
Kwa hiyo, uzuri na uwezo wake ukamdanganya, hata akatamani
kuichukua nafasi ya Mungu kwa kudhani kuwa zile sifa alizonazo
anastahili na yeye kuwa Mungu, ndipo akasema moyoni mwake
kwa kiburi kuwa; ‘’Nitapanda mpaka Mbinguni, nitakiinua kiti
changu kuliko nyota za Mungu; nami nitaketi juu ya mlima wa
mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini; nitapaa kupita
vimo vya mawingu, nitafanana na yeye aliye juu. Isaya 14:13-14
Kutokana na mawazo yake, alianzisha kampeni ya kuwashawishi
malaika wengine wa Mungu Mbinguni kumuunga mkono; na
alifanikiwa kuwadanganya na kuwashawishi theluthi ya malaika
wa mbinguni. Ufu 12:4a inasema hivi ‘’Na mkia wake wakokota
theluthi ya nyota za mbinguni, na kuziangusha katika nchi’’.
Lakini wakati huo lusifa akiwa anaendelea na huo mpango wake,
Mungu alikuwa anatambua kila kitu, ila Mungu alimuacha Lusifa
aendelee na uasi wake, kwa kuwa tayari ilikuwa ameshampangia

11
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

mpango wa kumtupa kuzimu, ndio maana anasema hivi ‘’Lakini


utashushwa mpaka kuzimu, mpaka pande za mwisho za shimo’’
Isaya 14:15. Lusifa alipojaribu kutekeleza mpango wake, ndipo
akatupwa kuzimu kama ilivyoandika katika Isaya 14:11 inasema
‘’Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, na sauti ya vinanda vyako;
funza wametandazwa chini yako, na vidudu vinakufunika. Ndipo
lusifa akaitwa shetani baada ya uasi wake
Kwa hiyo, licha ya kuwa kuna malaika wa mbinguni; lakini pia
kuna malaika wa kuzimu, ambao wanafanyakazi chini ya Lusifa,
na hii inatokana na ile vita iliyopiganwa mbinguni wakati wa uasi
wa lusifa. Imeandikwa ‘’kulikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na
malaika zake walipigana na Yule joka (Ibilisi au shetani) ambaye
ndiye lusifa, yule joka naye akapigana na malaika zake, lakini
hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
Ufu 12:17-19
Uasi ni tabia rasmi ya shetani, yeye ndiye aliyeasisi uasi juu ya
Mungu; alipoona hakufanikiwa katika mpango wake huo wa
kumpindua Mungu, ndipo alipotumia hila zake na kumshawishi
Adamu naye afanye uasi juu ya Mungu
Kazi ya lusifa/shetani kwa watu
Baada ya kushindwa kutekeleza adhima yake ya kumuasi Mungu, ile
tamaa yake ya kupata nafasi ya kutawala iliendelea ndani yake; Hata
alipotupwa kuzimu, bado aliendelea na mpango wake wa kuitafuta
hiyo nafasi ya utawala. Awamu hii, shetani hakutafuta tenanafasi
ya kuwa Mungu wa mbingu na nchi, bali aliitafuta ile nafasi ya
kuwa mungu wa duniahii, ambayo nafasi hiyo alikuwa nayo Adamu.
Na ili lusifa aipate hiyo nafasi; ilikuwa ni lazima afanye kwanza
vita na mwenye hiyo nafasi wakati huo ambaye ni Adamu. Na kwa
kuwaAdamu alikuwa na nafasi hiyo kiroho lakini akiishi katika mwili,
ndipo lusifa, yaani shetani alipofanya naye vita kiroho katika mwili,
maana ilimlazimu shetani avae umbo au mwili wa nyoka.

12
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Lusifa akaanzakutengeneza misingi na mikakati ya uharibifu wa kiroho


dhidi ya Adamu, ili Adamu amkosee Mungu; shetani akaingiza roho
ya uasi kwa Eva juu ya mpango wake wa kimapinduzi wa kutaka
kumpindua Mungu;shetani akamwambia mwanamke ‘’Mtakapokula
matunda ya mti huo hamtakufa, mtakuwa kama Mungu kwa kujua
mema na mabaya’’ bila kujua kuwa hivi ni vita, mwanamke akakubali
mpango huo na kumshirikisha mume wake, hivyo wakashirikiana na
shetani kutaka kumpindua Mungu. Ndipo shetani alipowashinda na
kuichukua nafasi yao ya kuwa mkuu wa ulimwengu hata imeandikwa
‘’Kwa kuwa mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa’’ Yoh
16:11b. lakini kwanza nafasi hiyo ilikuwa ya Adamu kabla ya dhambi
Adamu baada ya kuipoteza hiyo nafasi, alipoteza pia uhalali wake wa
kuishi edeni, na kwa sababu hakutaka kuondoka, ndipo alipojificha ili
aendelee kuishi kwa siri; lakini Mungu alimfukuza na kumtoa kwenye
bustani. Hayo ni miongoni mwa madhara ya dhambi
ROHO INAYOKUFA NDANI YA MTU KWA SHERIA

Tunapozungumzia roho iliyokufa ndani ya mtu, tunahusisha na tendo


la roho ya mtu, isiyo na mahusiano ya kiroho kati yake na Roho wa
Mungu (Kuvunjika kwa mahusiano ya kiroho kati ya roho ya mtu, na
Roho wa Mungu). Roho wa Mungu ni Roho Mtakatifu, lakini roho ya
mtu ni ile sehemu ya pumzi ya Mungu iliyoingizwa na Mungu kama
pumzi ya uhai ndani ya mwili wa Mtu, ili mtu apate kuwa nafsi hai
katika Mungu kama yasemavyo maandiko‘’Mungu akampulizia puani
pumzi ya uhai, mtu akawa nafsi hai). Mwa 2:26
Kwa hiyo,matokeo ya uhai wa mtu; ni uwepo wa roho yake ndani ya
mwili wake, lakini matokeo ya uhai wa roho ya mtu, ni uwepo wa
ushirika wa roho yake na Roho wa Mungu, ndio maana maandiko
yanasema ‘’Uhai wetu umefichwa katika Kristo’’ hata tena yanasema
‘’Kwa maana ndani yake yeye tunaishi, tunakwenda na kuwa na uhai
wetu’’. Mdo 17:28; hata tena imeandikwa ‘’Lakini kwetu sisi Mungu
ni mmoja tu, aliye Baba, ambaye vitu vyote vimetoka kwake, nasi
tunaishi kwake, yuko na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake

13
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

vitu vyote vimekuwapo, na sisi kwa yeye huyo. 1Kor 8:


Anaposema “Na sisi kwa yeye huyo’’ Anamaanisha kwamba! Uwepo
wa uhai na uzima wa maisha yetu, ni matokeo ya Bwana kwetu. Hivyo
uhai wa mtu ndani yake, ni matokeo kamili ya uwepo wa Roho wa
Mungu ndani ya mtu, (Uhusiano wa kiroho kati ya mtu na Mungu
wake), kwa kuwa Roho ndiyo itiayo uzima, wala mwili haubebi uzima,
bali hubeba roho wa uzima. Yoh 6:63 inasema ‘’Roho ndiyo itiayo
uzima, mwili haufai kitu;maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena
ni uzima’’
Mungu aliye nafsi tatu, akiisha kuumba mtu kwa sura na mfano wake
kwa kupitia mavumbi ya ardhi, alimpulizia huyo mtu puani pumzi ya
uhai; kwa hiyo mtu akawa nafsi hai.
Sasa huo uhai wa mtu katika nafsi yake, ni matokeo ya mahusiano kati
ya mtu na Mungu kupitia ile roho (Pumzi) ya Mungu ndani ya Mtu.
Ndivyo maandiko yanavyosema; Mwa 2:26 ‘’Mtu akawa nafsi hai’’
maana yake ni kwamba; hata kabla ya ile pumzi ya Mungu haijaingia
ndani ya huyo mtu, tayari mtu alishakuwepo, lakini hakuwa nafsi hai
katika mwili. Yere 1:5a anasema ‘’Kabla sijakuumba katika tumbo,
nalikujua’’.
Swali; Kama Mungu alimjua Yeremia kabla hata Yeremia hajaumbwa;
je! Yeremia alikuwa wapi wakati huo..? Kwa sababu;Mungu asingemjua
huyo mtu kama asingekuwepo mahali, maana yake huyo mtu kuna
mahali alikuwepo, ndio maana Mungu akamjua, lakini huyo mtu
hakuwa nafsi hai katika mwili, bali katika roho, mpaka pale Mungu
aliposhiriki uhai wa huyo mtu kwa kuingiza pumzi yake (Yaani kumtoa
huyo mtu kwenye roho na kumuingiza kwenye mwili).
Mtu ni roho ndani ya mwili, au kwa lugha rahisi unaweza kusema
kwamba! Mtu ni roho yenye mwili, iliyotoka kwa Roho isiyo na mwili.
Kwa hiyo uzima wa ile roho yenye mwili sio ule mwili wake, bali ni ile
Roho (Mungu) iliyoasisi uwepo wake katika mwili huo. Ndio maana
imeandikwa, ‘’Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu’’ Yoh 6:63;

14
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kwa hiyo watu wengi, wanapoona wanaishi, wanadhani vyakula


vyao ndivyo vinavyowapa kuishi; lakini ukweli ni huu, si kwa chakula
mtu kuwa hai, bali ni kwa Roho wa Mungu. Kwa hiyo, mtu akipoteza
uhusiano wake na Mungu; japo ataendelea kuwepo, lakini hatakuwa
na uhai ndani yake. Kwa kifupi ni mfu anayeishi

15
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

SURA YA PILI: MPANGO WA MUNGU KUKUUMBA KWA


MFANO NA SURA YAKE
MUNGU AUMBA MTU

‘’Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi’’ Mwa 1:1.


Maandiko yanatuonyesha kwamba! Mungu alianza kuumba mbingu,
halafundipo Mungu akaumba na dunia, na maandiko hayatuonyeshi
popote kwamba! Mungu alishauriana na yeyote, mahali popote, wala
wakati wowote, katika mpango wake juu ya kuumba kwake mbingu
na nchi, na anasema wazi kwamba; mpango wake wa kuumba dunia;
hakuiumba dunia iweukiwa (Utupu) bali aliiumba ili ikaliwe na watu.
Isaya 45:18 inasema ‘’Maana Bwana aliyeziumba mbingu asema hivi;
yeye ni Mungu, ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya, ndiye aliyeifanya
imara; hakuiumba ukiwa aliiumba ili ikaliwe na watu’’
Katika andiko hili, kuna vitu vitatu vya kuvitazama zaidi
1. Aliyeziumba mbingu
Anaposema ‘’Aliyeziumba mbingu’’ anamaanishahizo Mbingu
zipo nyingi; Ndio maana mfalme sulemani anasema ‘’Mbingu
za mbingu hazikutoshi’’ 1Falm 8:27 imeandikwa ‘’Lakini
je! MunguAtakaa kweli kweli juu ya nchi? Tazama mbingu
hazikutoshi, wala mbingu za mbingu; sembuse nyumba hii
niliyoijenga? Na Kristo Yesu naye, anasema ‘’Nyumbani kwa
Baba yangu makao ni mengi, la sivyo! Ningaliwaambia. Yoh 14:2
Mbingu ni nini?
Kwa hiyo Mbingu sio anga, bali ni makao ya Mungu, ni eneo la kiroho
lisiloonekana kwa macho ya kawaida, huko ndiko kiti cha Mungu na
makao ya viumbe wake wa Kiroho. Ndio maana Mungu anasema
‘’Mbingu ni kiti changu cha enzi, na nchi ni mahali pa kuweka miguu
yangu.Kwa hiyo Mbingu ni ulimwengu wa roho; na ndio asili ya

16
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

mwanadamu. Efeso 6:12 imeandikwa hivi ‘’Kwa maana kushindana


kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka,
juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika
ulimwengu wa roho’’huko ndio makazi makuu ya viumbe wote wa
kiroho pamoja na Muumbaji mwenyewe ambaye naye pia ni Roho,
yaani Mungu. Yoh 4:24 maandiko yanasema ‘’Mungu ni Roho’’.
Ulimwengu wa roho, upo katika makundi mawili ambayo ni:

i. Ulimwengu wa Roho wa nuru

ii. Ulimwengu wa roho wa giza


Kwaupande wa ulimwengu wa Roho wa nuru, (Mbinguni) huko ndiko
yaliko makao makuu ya Mungu, na katika ulimwengu wa roho wa giza
(Kuzimu), huko ndiko yaliko makazi ya shetani na wakuu wake pamoja
na malaika zake (pepo wabaya).
Ingawa ulimwengu huu umegawanyika katika sehemu hizi kuu mbili,
lakini bado Mungu ndiye mmiliki wa sehemu zote, ikiwa ni pamoja na
ulimwengu huu wa mwili; yeye anapatikana kote kwa wakati mmoja
wakati wote. Lakini pia utaona, japokuwa Mungu yupo sehemu hizi
zote, bado mazingira ya sehemu hizo yanatuonyesha kutokidhi yaani
kutotosheleza ukuu na uwepo wa Mungu kwenye maeneo hayo.

2. Aliyeiumba dunia
Anaposema ‘’Mungu aliyeiumba dunia’’hapo hasemi kuwa ‘’Mungu
aliyeziumba dunia’’ hapana! Yaani hatumii sentensi ya wingi, bali
sentensi ya umoja ili kuonyesha kuwa dunia ipo moja kati ya mbingu
nyingi. Ndio maana Mungu anasema ‘’msiwe na miungu mingine ila
mimi’’. Kut 20:3. Kwa nini Mungu atuzuie tusiwe na miungu mingine?
Jibu ni kwamba! Mbingu ziponyingi, maana yake roho nazo ni nyingi,
kwa maana ya miungu, ila Roho ni mmoja yaani Mungu. Ndio maana
anasema kwa ujasiri mwingi ‘’Niangalieni mimi mkaokolewe enyi ncha
zote za dunia, maana mimi ni Mungu, hapana mwingine. Isaya 45:22

17
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

3. Ili ikaliwe na watu


Katika hatua hii, inatuonyesha lengo kuu la Mungu la kuiumba
dunia, ni ili dunia ikaliwe na watu, yaani Mungu apate kumtuma mtu
kutoka Mbinguni katika roho yake, ili mtualiye roho apate kuishi
kiroho katika mwili kwa lengo la kufanya kazi ya kumuwakilisha
Mungu katika jukumu la kuitawala dunia. Kwa hiyo, mwanadamu
hakuja duniani kwa mpango wake mwenyewe, bali alikuja kwa
mpango kamili wa Mungu
Hivyo mpango wa Mungu ni kumpa mtu nafasi ya kutawala, na sio
kumiliki; ndio maana hakuna mtu mwenye kitu chake hapa duniani,
kwa kuwa kila kitu kilichopo duniani ni mali ya Mungu, yeye ndiye
anayemiliki vyote. Lakini unafikiri ilikuwa ni kwanini Mungu aumbe
dunia ili ikaliwe na watu? Ushawahi kujiuliza?
Kwa maana maandiko yanatuambia kuwa!Katika uumbaji wa dunia,
Mungu alitumia siku tano za kwanza kuhakikisha dunia na kila kitu
kimekamilika na kila vilipokamilika, akaona vema.
Sasa Kama Mungu aliona kuwa ni vema juu ya kazi yake; inamaanisha
kuwa aliridhika na kuifurahia kazi hiyo; sasa kwanini Mungu aumbe
mtu? Na pia utaona, wakati wote Mungu alipokuwa akiumba dunia
na vilivyomo, Mungu hakushauriana na yeyote juu ya kuumba vyote,
ila alitamka tu na ikawa; lakini alipopata wazo la kumuumba mtu,
alifanya kwanza kikao na kuwasilisha mswada wake katika Bunge
lake la Utatu Mtakatifu huko mbinguni, ulishawahi kujiuliza ni kwa
nini? Na ulipata jibu gani..? Tuendelee kwa pamoja kuipata sababu ya
kuumbwa kwetu, na sababu ya Bunge kujadili juu ya kuumbwa kwetu

Kwa nini Mungu amekuumba wewe..?


Hili ni swali la msingi ambalo kila mtu anapaswa kujiuliza, na asiishie
tu katika kujiuliza, bali aendelee mpaka afikie hatua ya kupata majibu
sahihi juu ya swali hili. Maandiko matakatifu yanatuambia kwamba;
‘’Mungu ndiye aliyeziumba mbingu na nchi’’ kitabu cha Mwanzo

18
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

1:1na Mungu anatuthibitishia wazi kwa kusema kwamba! Hajaiumba


hii dunia iwe ukiwa, Balialiiumba ili ikaliwe na watu. Isaya 45:18.
Lakini swali letu la msingi linabaki pale pale, kwanini uumbwe ili ukae
katika hii dunia? Maana Kama hutojua sababu ya kuumbwa kwako,
au kwanini upo duniani; hutokuwa na sababu ya kuishi, kwa sababu;
ile sababuya kuumbwa kwako, ndiyo inayokupa wewe msukumo wa
kutamani na kuhitaji kuendelea kuishi; ndio maana Paulo kwa kulijua
kusudi la Mungu ndani yake; anasema ‘’Kuishi kwangu ni Kristo, na
kufa ni faida’’. Filipi 2:21
Maana yake ni nini?
Maana yake ni kwamba, kama kusingekuwa na lile kusudi la Mungu
ndani yaPaulo, Pauloasingehitaji kuishi; kwanini? Ni kwa sababu
thamani ya maisha yake ipo katika kufa kwake; lakini kwa sababu ya
lile kusudi, anapaswa kuishi katika hilo. Kwa hiyoKama asingekua na
hilo kusudi ndani yake, tafsiri yake ni kwamba! Asingehitaji kuishi,
hivyo ndivyo ilivyo kwa watu wasiojua kusudi la kuumbwa kwao.
Hawatamani kuishi, ila wanataka kuishi tu kwa sababu wanaogopa
kufa.
Watu hawa wasiolitambua kusudi la kuumbwa kwao, mara nyingi wao
huwaradhi kupokea au kutenda kitu chochote pasipo kuhitaji kujua
faida au hasara zake, kwanini?Ni kwa sababu kwao hakuna kitu cha
kupoteza; kwa sababu hawajui kusudi la kuishi kwao. Lakini Mungu
alimuumba mtu, ili mtu apate kumuwakilisha Mungu katika dunia ‘’Na
tumfanye mtu kwa mfano wetu kwa sura yetu’’Mwa 1:26. Lile neno
‘’Kwa mfano wetu kwa sura yetu;ni sawa na kusema kuwa ‘’tuumbe
mtu badala yetu’’. Kwa nini Mungu alitaka waumbe mtu badala yao?
Ni kwa sababu kulikuwa na jukumu la wao kutekeleza kimwili katika
dunia, na kwa kuwa Mungu ni Roho, hawezi kuwajibika kimwili, ndio
maana alitaka aumbwe mungu mbadala (Mtu) atakayekuwa wa
asili ya mwili ili apate kwenda kutekeleza majukumu ya kiroho kwa
niaba ya Mungu, na majukumu hayo ni kutawala. Yaani tumeumbwa

19
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

kama mbadala wa Mungu kwa lengo la kuitawala dunia kwa niaba ya


Mungu. Na kwa sababu hiyo, ndio maana tumeletwa huku duniani
kumuwakilisha Mungu katika hilo jukumu. Paulo anasema ‘’Kuishi
kwangu ni Kristo’’ hii ni sawa nakusema ninaishi kwa niaba ya Kristo.
Na kusudi hili la Mungu kumuumba mtu kwa mfano wake na kwa sura
yake, lilikamilika pasi na shaka, na huyo mtu akawa nafsi hai. Mwa
2:7 inasema ‘’Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi,
akampulizia pumzi ya uhai puani; mtu akawa nafsi hai.
Nini maana ya nafsi..?
Nafsi kwa lugha ya Kiebrania huitwa‘’Nefesh’’naKiyunani ni
“Psyke”Nefesh ni neno linalomaanisha “Mtu anayehuishwa na pumzi
ya uhai’ anaposema ‘’Kuhuishwa na pumzi ya uhai’’ anamaanisha
kurudishwa kwa uhai kupitia roho (Pumzi) ndani ya mtu, ukisoma
kitabu cha mwa 2:7 inasema ‘’Bwana Mungu akamfanya mtu kwa
mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa
nafsi hai’’ kwa hiyo utaona, huyo mtu alipoumbwa haukuwa nafsi
hai, mpaka pale pumzi ya Mungu ilipoingia kwa huyo mtu, ndipo mtu
akawa nafsi hai. Na katika Zaburi 6:4 Daudi anasema hivi ‘’Bwana,
urudi, uniopoe nafsi yangu, uniokoe kwa fadhili zako’’anaposema
‘’Uniokoe’’ anatusaidia kujua kuwa! Uhai wake upo kwenye hatari ya
kuondoka, yaani roho yake kuachana na mwili wake na hivyo nafsi
yake inahatari ya kukosa uhai (Nafsi yake kushindwa kutafsiri uhai wa
mwili).
Pumzi ya uhai huitwa roho katika mwili wa mtu; na kwa kiebrania roho
pia huitwa Ruah. Nafsi ni chanzo cha uhai wa mwili wa mtu baada ya
roho (pumzi) kuingia kwa mtu. Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba! ‘’Mtu
wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai. 1Kor 15:45
Nefesh imetafsiriwa kama ‘’Nafsi’’ ‘’Maisha’’‘’Uhai’’‘’Uzima’’‘’roho’’
Neno hili humaanisha mtu aliyemzima (anayeishi) kwa kuungamana
kwa mwili wake pamoja na pneuma (roho ya Mungu), kwa nini?

20
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ni kwa sababu, maisha, au uhai au uzima wa nafsi ya mtu, ni roho yake


ndani ya mwili wake, lakini uzima na uhai wa roho ya mtu ni Roho
wa Mungu ndani ya roho ya mtu. Ndio maana imeandikwa kusema
kwamba!‘’Roho ndio itiayo uzima, mwili haufai kitu maneno haya
ninayowaambia ni uzima tena ni roho’’ Yoh 6:63. Na ukisoma 1Kor
2:14 pia imeandikwa ‘’Basi mwanadamu wa tabia ya asili, hayapokei
mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuuzi, wala
hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Nafsi ya mtu baada ya kufa,itakamilika katika wakati wa ufufuko;
hapo itakapobeba mwili mpya usioharibika, hapo nafsi hiyo haitakufa
tena, bali itaishi milele, wala nafsi hiyo haitaonja tena uchungu wala
nguvu za mauti ya mwili, baada ya mwili huu wa sasa wa kuharibika
kuharibiwa na mauti; hapo ndipo nafsi sasa itavaa mwili mpya wa
kutoharibika na itaishi milele. 1Kor 15:53-55 imeandikwa kuwa
‘’Maana sharti mwili huu uharibikao uvae kutoharibika, nao huu wa
kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutoharibika, na
huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno
lililoandikwa: Mauti imemezwa kwa kushinda. Ku wapi ewe mauti
kushinda kwako? U wapi, ewe mauti, uchungu wako?
Lakini pia Nefesh-nafsi unaweza kusema pia ni roho iliyoungana na
mwili katika kuishi, maana mwili pasipo roho, nafsi isingekuwa hai
katika mwili; ndio maana mara nyingine hutafsiriwa nafsi kama roho
(Uhai). Ndio maana imeandikwa katikaMath10:28 ‘’Msiwaogope
wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho pia, afadhali mwogopeni yule
awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanam.
Nafsi iliyotengana na mwili (Iliyokufa) ikiwa ilitenda haki wakati wa
uhai wake, inaweza kukaa peponi na Kristo hata kabla haijaja ilesiku
ya ufufuko wa mwilina kupewa mwili mpya.Imeandikwa katika Luk
23:39-43 kusema kwamba! Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika
ufalme wako; Ndipo Yesu akamwambia; Amini, nakuambia, leo hivi
utakuwa pamoja nami peponi.

21
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Na katika kitabu kile cha Matendo ya Mitume 2:27 inasema kwamba


‘’Kwa maana hautaiacha roho yangu katika kuzimu, wala hutamtoa
mtakatifu wako aone uharibifu’’
Lakini neno ‘’Nafsi’’ pia ni muunganiko wa:

1. Akili

2. Hisia

3. Utashi
Kwa kawaida nafsi ndio inayotutambulisha utofauti wetu, nafsi sio lile
jina lako, bali nafsi ni yule wewe wa ndani ambaye hauonekani, lakini
unazungumza, ndio maana utasikia mtu akisema ‘’mimi’’ lile neno
mimi hamaanishi ule mwili wake, hapana! Bali ule utu wake wa ndani
ambao ndio nafsi. Lakini pia nafsi inatumika kutafsiri lugha ya roho na
mwili, kwa kuwa roho na mwili havielewani kabisa, kuna wakati roho
inataka kutekeleza jambo Fulani, lakini mwili hautaki kabisa. Ndivyo
Yesu anavyowaambia wanafunzi wake, kwamba! ‘’roho i radhi ila
mwili ni dhaifu’’ Math 26:41. Katika maandiko haya utaona kwamba,
roho inahitaji kuomba ili kujiepusha na majaribu, lakini mwili hautaki
(dhaifu), ndio maana biblia inasema ‘’Nia ya mwili ni mauti, bali nia ya
roho ni uzima na amani’’ Rumi 8:6
Kwa hiyo kila uhai una nafsi, kwa sababu nafsi ndio inayotambulisha
uhai; kwa tafsiri rahisi, tunaweza kusema Nafsi ndio inayotafsiri lugha
ya uhai (Lugha ya roho), kwa maana pasipo nafsi, tafsiri ya uhai kwa
Adamu isingekuwepo, hata kama roho ya uzima (Pumzi ya uhai) tayari
iko ndani yake.Tunaona, Adamu hata baada ya kupuliziwa pumzi ya
uhai ndani yake, lakini bado mwili wa Adamu ulibaki vile vile kama
mdori. Mwa 2:7b, inasema mtu akawa nafsi hai.
Biblia inatuambia kwenye Mwa 2:7kwamba! Mungu alimuumba mtu
kwa mavumbi ya ardhi, lakini hapo bado mtu hakuwa na uhai, na
kisha Mungu akampulizia mtu huyo pumzi ya uhai puani mwake; hata

22
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

hivyobado mtu huyo hakuwa na uhai, mpaka pale nafsi iliposhiriki


kwa kudhihirisha uhai ndani ya mtu huyo (Adamu) ndipo mtu akawa
nafsi hai.
Uhai ni uzima katika nafsi, Mwa 2:7 inasema ‘’Mtu akawa nafsi hai’’
na uhai ni pumzi ya Mungu ndani ya mwili wa mtu, hivyo uhai wa mtu
ndio uzima katika nafsi ndani ya maisha yake; Rumi 7:6 inasema ‘’Bali
sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi
tupate kutumika katika hali ya roho’’ maana yake katika uzima, katika
nafsi zetu. Maana tulikufa kwa sababu ya nafsi na roho kushindana
katika mwili (Dhambi), Rumi 7:5 inasema ‘’Kwa maana tulipokuwa
katika hali ya mwili, tamaa za dhambi zilizokuwako kwa sababu ya
torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata tukaizalia mauti mazao’’.
Uhai wa mtu ni matokeo ya uwepo wa Roho wa Mungu ndani ya mtu
kwa asilimia mia moja, Mungu anaachilia uzima ndani ya roho ya mtu
katika nafsi ya mtu kwa njia ya Roho wake Mtakatifu.
Yoh 6:63 imeandikwa kuwa ‘’Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai
kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima’’ Hebu
jaribu kuangalia hivi (Roho ndiyo itiayo uzima) na (Maneno hayo
niliyowaambia ni roho). Utagundua kuna tofauti kati ya:
a. Roho
b. roho
Itiayo uzima ni Roho, unapoona imeandikwa (Roho) inamaanisha
Mungu au Roho Mtakatifu, kwa hiyo huyu Roho ndiye atiaye uzima,
(Mungu/Roho Mtakatifu), anatia huo uzima katika nini? Anatia uzima
katika roho ya mtu; Ukiona imeandikwa (roho), inamaanisha pumzi ya
Mungu ndani ya mtu, au viumbe wa kiroho ambao sio Mungu. Sasa
hapa, anamaanisha kwamba! Huyo Roho, hutia uzima katika roho ya
Mtu, maana yake ni kwamba! Huyo Roho alipoachilia uzima katika
mtu, huo uzima ulienda katika nafsi na sio katika mwili, ndio maana
anasema ‘’Mwili haufai kitu’’.

23
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kwa hiyo, uhai wa roho ya mtu ni matokeo ya ushirika wa Kiroho


kati ya Mungu na roho ya mtu ndani ya mtu husika, na ushirika huo
udhihirika katika nafsi, hata imeandikwa ‘’Ee Mungu, Mungu wangu,
nitakutafuta mapema, nafsi yangu inakuonea kiu,’’ Zab 63:1. Roho wa
Mungu akiachilia pumzi yake katika roho ya mtu, ndipo roho ya mtu
udhihirisha uhai wake katika nafsi. Na Roho wa Mungu hushirikiana
na roho ya mtukatika utakatifu na ucha Mungu, kwa hiyo kwa kadiri ya
kuongezeka kwa utakatifu katika roho na nafsi ya mtu, ndipo Roho wa
Mungu huachilia uzima ndani ya mtu, hivyo; msingi wa uzima wa mtu
umewekwa katika kutenda haki ya Mungu katika roho na kudhihirika
haki hiyo katika mwili kupitia matendo ya mwili; kwanini?
Ni kwa sababu Roho wa Mungu ni haki ya Mungu inayodhihirishwa
kwa sheria ya uzima wa Roho katika Kristo Yesu, kwa hiyo, ile sheria
ya uzima, ni matendo ya haki na utakatifu ambayo matendo hayo
hayatokani na matendo ya sheria (Torati), bali kwa njia ya neema
katika imani kwa Kristo Yesu Bwana wetu. Rumi 8:1-2 inasema hivi
‘’Sasa basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo
Yesu, Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu
imeniacha huru, mbali na dhambi na mauti
Kwa hiyo, mwanadamu kamili ni mtu yule mwenye uhai pamoja na
uzima ndani yake, kwa sababu mtu anaweza kuwa na uhai bila hata
kuwa na uzima, lakini mtu hawezi kuwa na uzima na asiwe na uhai;
kwa hiyo matokeo ya kuwepo kwa uhai bila uzima, inasababishwa na
shambulio kati ya roho na nafsi; kwa sababu, kazi ya roho ni kubeba
uhai na kuleta uzima katika nafsi, hivyo inapotokea kutoshirikiana
kati ya nafsi na roho katika mwili, kunaondoa ule ushirika kati yao,
na hivyo; nafsi kukosa kupokea uzima kutoka katika roho ya mtu, na
kisha husababisha mwili kuwa dhaifu.
Biblia inaposema kwa habari ya uzima wa milele, ni kwa sababu kuna
tofauti kati ya uzima na uzima wa milele. Lakini pia kuna uhai na uhai
wa milele; uhai ni hali ya maisha tuliyonayo katika ulimwengu huu,
lakini uhai wa milele ni yale maisha tutakayoyaishi mara baada ya

24
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

maisha haya ya sasa kupita na kuingia kwenye maisha mapya katika


ulimwengu mpya katika ufufuko wa wafu, baada ya maisha haya
kupita na kuingia kwenye maisha mapya, hakuna uhai utakaokufa
tena baada ya kufufuliwa.
Lakini ukweli ni kwamba! Sio kila uhai utakaofufuliwa,utakuwa na
uzima wa milele ndani,hapana! Bali kitu kimoja ambacho watu wote
hawatatofautiana katika uhai huo mpya, ni ile hali ya kuwa hai milele,
lakini watu watatofautiana katika hali ile ya uzima wa milele. Yuda
1:23 anasema ‘’Na wengine waokoeni kwa kuwanyakua katika moto’’
wananyakuliwaje?
Ni kwa kuwasogeza kwenye pendo la Mungu wangali hai ili wapate
rehema ya Bwana wetu, Yesu Kristo;waokolewe na kuacha dhambi
wapate uzima wa milele. Yuda 1:21; Na Yuda1:23 anasema ‘’Waache
uovu’’. Uhai wa mtu ni matokeo ya roho na uzima katika nafsi ndani
ya mwili wa mtu, lakini uzima wa mtu, ni ushirika wa roho ya mtukati
ya Roho wa Mungu na roho ya mtu katika kuitii na kuiishi ile sheria ya
Roho wa Uzima wa Kristo katika kutenda haki na utakatifu katika nia
ya Roho.
Kwa hiyo, baada ya ufufuo wa wafu, watu pekee watakaokuwa na uhai
na uzima wa milele, ni wale tu watakaokuwa na ushirika na Mungu
mbinguni katika Kristo Yesu; yaani wale ambao hawataingia katika
ziwa linalowaka moto milele. Ufu 20:4
Lakini wale watakaoingia katika ziwa hilo, watakuwa na uhai tu wa
milele, lakini hawatakuwa na uzima wa milele ndani ya uhai wao; kwa
kuwa uhai wao hauna uzima (Hawana ushirika na Kristo katika ufalme
wake). Ni lazima kujua kuwa! Uhai sio uzima, Ndio maana utakuta
mtu yupo hai, lakini yupo I.C.U, kwanini? Ni kwa sababu ana uhai,
lakini hana uzima ndani yake. Kwanini asiwe na uzima ndani yake?
Ni kwa sababu uzima hukaa katika nafsi kutokea rohoni, uzima wala
haukai kwenye roho, kazi ya roho ni kumpa mtu uhai na kutia uzima
katika nafsi ya huyo mtu.

25
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Nafsi inahitaji uhai wa roho ili yenyewe ipate kuwa na uzima, ikitokea
roho ikakosa kuwa na uhai, nafsi inakosa kuwa na uzima. Kama hivyo
ndivyo; je! roho hupata wapi uhai wake na uzima kwa ajili ya nafsi
yake? Mahali pekee ambapo roho hupata uhai wake na uzima wa
nafsi, ni katika ushirika na Roho wa Mungu. Na inapotokea roho ya
mtu ikakosa ushirika na Roho wa Mungu, nafsi inakosa uzima na roho
inakufa ndani ya mtu, kwanini? Ni kwa sababu nafsi imekosa uzima
kutoka rohoni, sasa nafsi inapokosa uzima kutoka rohoni; ndipo nafsi
inapoandamana na mwili; na biblia inatuambia kuwa; nia ya mwili ni
mauti. Sasa nafsi inapoandamana na mwili, inasababisha roho ya mtu
kukosa mshirika katika maisha ya mwili wa mtu huyo, na hivyo roho
inaondoka (Kutoka), huko ndiko kufa kimwili kunakotokana na kufa
kiroho.
Mwa1:26. Mungu anatuonyesha kwamba! Hakutuumba kwa bahati
mbaya, maana alikaa na jopo lake la mbinguni (Utatu Mtakatifu), ili
kutafakari sababu ya kuumbwa kwetu;na namna tutakavyoumbwa.
Na kwa kuridhia, jopo hilo la mbinguni lilikubalianakwa kauli moja,
kwamba;tuumbwe kwa sura na mfano wao.Hii inaonyesha ni jinsi
gani tulivyo wa thamani mbele za Mungu, maana mbali na kuridhia
jinsi ya kuumbwa kwetu, pia jopo hilo, lilipitisha maazimio ya Mungu
ya kutakatupate kutawala. Mwa 1:26a imeandikwa kuwa ‘’Tumfanye
mtu, kwa mfano wetu’’ na lengo lao ni ili mtu apate kutawala Mwa
1:26b, inasema ‘’Wakatawale’’
Neno la Mungu linaposema ‘’Kwa sura yetu na kwa mfano wetu’’
Kumbuka kuwa; hapahalimaanishi kwamba Mungu yupo kama sisi
jinsi tulivyo, hapana! Kwa nini?
Ni kwa sababu; Mungu ni Roho; hana mwili, Makao yake ni katika
ulimwengu wa roho, Hana mwanzo wala mwisho, hakuumbwa, ni
Mtakatifu, ndiye aliye wa kuabudiwa na kusujudiwa. Ndivyo Yesu
anavyomwambia shetani ‘’Nenda zako shetani, imeandikwa msujudie
Bwana Mungu wako, na umwabudu yeye peke yake. Math 4:10
Mungu aliumba Mtu kama kiti chakecha utawala, ili Mungu apate

26
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

kuitawala dunia kutokea katika ulimwengu wa roho katika mwili wa


mtu, kwanini? Kwa sababu Mungu yeye ni Roho, na Roho ni nafsi
kamili lakini isiyo na umbo/mwili; hivyo ili Roho/roho iweze kutawala
na kutekeleza adhima yake katika ulimwengu wa mwili, inamuhitaji
mtu aliye na mwili. Kwa hiyo, hakuna mtu anayetawala, bali Mungu
ndiye hutawala dunia kupitia mtu. Mtu yeyote asipokuwa na Mungu,
hawezi kuutawala ulimwengu, ndio maana Mungu akamuwekea huyo
mtu sheria ya utawala na kutawala. Mtu akipoteza msingi wa sheria
hizo, hawezi kamwe kutawala; sio kutawala dunia tu, hapana! Bali
hata kuitawala nafsi yake binafsi hatoweza
Kwa sababu, kwa asili mtu sio ule mwili; bali ni kile kilicho ndani ya
mwili, ni kitu kile kinachosema mwili huu ni wa kwangu.
Biblia inatuambia wazi kuwa, Mungu alisema kwamba; ‘’Tufanye mtu
kwa mfano wetu’’ lakini Biblia haituonyeshi hapo ambapo Mungu
akimfanya huyo mtu kwa mfano wake, kwa sura yake, badala yake
inatuonyesha Mungu akiwa anaumba mwili wa mtu; ili mtu huyo
anayefanywa kwa sura na mfano wa Mungu, apate kuishi katika
mwili huo. Ndio maana utaona, hata mara baada ya kuumbwa kwa
huo mwili, bado maandiko yanatuambia kwamba! Huo mwili ulikuwa
hauna uhai ndani yake, mpaka pale pumzi ya Mungu ilipoingia ndani
ya huo mwili kama mtu binafsi.
Ukisoma Mwa 2:7 inasemahivi ‘’Bwana Mungu akamfanya mtu kwa
mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtuakawa
nafsi hai’’ anaposema hivi, anakusudia kusema kwamba! Yale
mavumbi(udongo), hayakutumika kumuumba mtu, hapana! Bali yale
mavumbi yalitumika kuumba mwili kwa ajili ya mtu (Nyumba ya Mtu)
1Petr 2:5 inasema ‘’Mmejengwa muwe nyumba ya Roho’’ kwa hiyo,
mwili wa mtu, ni nyumba ya mtu aliye roho iliyojengwa na Mungu kwa
ajili ya mtu. Mtu mwenyewe, aliingia kwenye nyumba yake (Mwili)
akitokea kwa Mungu (Rohoni), na hapo ndipo alipopata kuwa nafsi
hai katika mwili, lakini hapo kwanza, alikuwa ni nafsi hai katika roho,
akiwa anaishi kwa Mungu akiwa kama sehemu ya Mungu mwenyewe.
Ndio maana Mungu anamwambia Yeremia, kabla sijakuumba katika
27
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

tumbo; nalikujua. Yer 1:5a. Maana yake ni kwamba, kuumbwa katika


tumbo, ni kuumbwa kwa mtu katika mwili wake, na kujulikana kabla
ya kuumbwa, ni uwepo wa mtu katika roho kabla ya mwili wake.
Kwa hiyo, msingi wa Mungu juu ya uumbaji, kwa kumuumba mtu,
alikusudia mtu asiwe na kikomo cha uhai wake, yaani Mungu alitaka
mtu huyu aishi milele bila Kufa. Na lengo la Mungu kumpa mtu uhai
endelevu, yaani uzima wa milele, ni kwa ajili ya Mungu kutengeneza
mahusiano ya kiutawala kati ya mtu na Mungu juu ya dunia, ndio
maana utaona; mtu alipopoteza nafasi hiyo ya ushirika na Mungu,
alipoteza sifa yake ya kutawala na kuishi milele (Alikufa).
Kwa mwanadamu yeyote kamili mwenye mwili aliye na uhai ndani
ya mwili wake asiyeulinda uzima wake kwa kujivunia uhai wake, basi
ajue kuwa,hata huo uhai wake nao utampotea; kwa kuwa uhai wa mtu
huthibitika katika uzima wake ndani ya nafsi. Unaona, Mungu baada
ya kumuumba mtu na kumpulizia pumzi ya uhai (kumpa roho ndani
yake) ndipo mtu akawa ni nafsi yenye uhai. Mwa 2:7. Kwanini? Ni kwa
sababu;Uhai wa mtu ni afya ya roho katika nafsi yake, ndio maana
inapotokea roho ya mtu imebeba uhai, lakini nafsi haina uzima, ule
uhai wa roho hauna kazi katika maisha ya mtu.
Hujawahi kuona mtu amejiua? Au Hujawahi kusikia mtu anatamani
kufa? Umewahi kujiuliza ni Kwanini? Ukiona mtu amefikia hatua hiyo,
Maana yake ni kwamba! Ana uhai katika roho yake, lakini ndani ya
uhai wake hakuna uzima katika nafsi yake. Unaweza kumuona mtu
na ukadhani ya kuwa ni mzima wa afya kwa jinsi unavyomtazama
na anavyoonekana, lakini kumbe ndani ya roho yake mtu huyo,
hakuna uzima. Mfano mzuri ni Yesu mwenyewe; yeye alipokuwa
bustanini Gethsemane, wanafunzi wake walipomtazama waliona
tumaini lao ndani yake, lakini hawakujua kuwa huyo wanayemuona
amebebatumaini lao, mwenyewe anahangaikia tumaini lake; hata
anasema “Roho yangu inahuzuni kiasi cha kufa’’ Mark 14:34.

28
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Mtu alipotezaje nafasi yake mbele za Mungu..?


Katika maisha ya kila mtu duniani, kuna makusudi ya Mungu; na katika
kila kusudi la Mungu, kuna taratibu zake za kusimamia kusudi hilo ili
mtu aweze kulitekeleza kusudi la Mungu kwake; kwa hiyo,Mungu
alimtengenezea mtu sheria, ili mtu apate kuenenda katika hizo. Na
Mungu alifanya hivyo kwa makusudi kwa kuwa hakuwa na mpango
wa kubadilisha mfumo wa kuitawala dunia nje ya kumtumia mtu, ndio
maana utaona; ingawa mtu huyu amepoteza sifa yake kwa kuvunja
sheria ya Mungu,lakini bado Mungu anatengeneza mpango mpya wa
kumtumia mtu mpya,ili kurudishatena mamlaka yake.
Kama tulivyosoma hapo kwanza; uhai wa mtu ni matokeo ya uwepo
wa Roho wa Mungu ndani ya roho ya mtu, kwa hiyo; ili mtu apate
kuwa hai, yaani aendelee kuwa na nafasi mbele za Mungu, maana
imeandikwa ‘’Mungu ni Mungu wa walio hai, sio Mungu wa wafu’’
Math 22:32. Basi inamlazimu mtu kulinda uhai na uzima wake, kwa
kushikamana na Roho wa uzima kwa Njia ya kumwamini,kumpenda
na kumtii mwana pekee wa Mungu; (Yesu Kristo), kwa kuwa ndivyo
ilivyoandikwa ‘’Maana jinsi hii, Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee; bali
awe na uzima wa milele. Yoh 3:16
Kwa hiyo; Njia pekee ya mtu kuulinda uhai wa roho na uzima wake,
ni kumwamini Kristo, na kuongozwa na Roho wa Mungu, ili asaidiwe
kuyashinda matendo ya mwili ambayo ndio nguvu kamili za mauti.
Imeandika hivi ’Basi nasema enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza
kamwe tamaa za mwili, kwa sababu mwili hutamani ukishindana na
Roho, na Roho kushindana na mwili, kwa maana hizi zimepingana
hata hamwezi kufanya mnayoyataka.Gal 5:16- 17
Kwa hiyo, jibu la swali la msingi linalouliza “Mtu anapotezaje nafasi
mbele za Mungu’’ ni kwamba! Mtu anapoteza nafasi yake mbele za
Mungu kwa kuacha kufuata mapenzi ya Mungu (Kumwamini Mwana
pekee wa Mungu) na kuifuata ile nia ya Roho ambayo ni uzima, na
badala yake; anafuata matendo ya mwili (Kumkataa Kristo) na ile nia

29
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

yake ambayo ni mauti. Mungu amefanya jambo jipya zaidi, sio tena
Mwanamke atamlinda mume wake, bali ni lile tendo la Mungu yeye
kuhamia ndani ya mwili wa Mtu; kwa hiyo, ikiwa hautaki kuipoteza
nafasi yako mbele za Mungu, kubali Mungu aishi ndani yako katika
Kristo Yesu.

30
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

SURA YA TATU: ASILI YA TORATI NA KAZI YAKE


ASILI YA TORATI

Biblia inatuambia kuwa! Torati asili yake ni ya rohoni; lakini imeletwa


kwa ajili ya mtu aliye wa asili ya mwili, na ukumbuke kwamba! Mwili
umenunuliwa na mauti (Dhambi); ndipo anasema; Nimeuzwa chini
ya dhambi. Ikiwa mwili umeuzwa chini ya dhambi, mtu hakuwa tena
mali ya Mungu, maana Mungu ni Mtakatifu; ikiwa sasa sio mtu wa
Mungutena, kwanini aliletewa torati ya Mungu?Maana imeandikwa
‘’Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni
mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. Rum 7:14.
Unaona hapa ni kama Mungu anajaribu kuingilia mamlaka, kwa kuwa
huyu mtu hakuwa mali ya Mungu wakati huo, kwa maana alikuwa
tayari ameshanunuliwa na dhambi/shetani; maana imeandikwa kila
atendaye dhambi ni wa ibilisi/shetani. 1Yoh 3:6. Ikiwa huyu mtu ni wa
shetani, kwanini Mungu alimuwekea torati?
Kabla ya kujibu swali hili, tuanze kwanza kwa kutazama torati ni nini;
torati ni sheria za Mungu, sasa kwanini Mungu amuwekee sheria mtu
asiye wake? Jibu ni kwamba! Sheria iliwekwa na Mungu kama ngazi
ili kumsaidia mtu aliye kwenye shimo la uvuli wa mauti aweze kutoka
kwa bidii zake mwenyewe; Mungu alifanya hivyo kwa makusudi na
kwa upendeleo ili mtu yeyote aliyechukia adhabu ya mauti ajipiganie
na kujitetea nafsi yake mwenyewe, kwa kutumia sheria ya Mungu ili
apande kama ngazi na kujitoa kwenye mauti na kupata uzima. Kwa
hiyo Mungu hakuleta sheria ili kuleta uzima, bali sheria ilikuja ili mtu
autafute uzima mwenyewe. Maana mpango wa Mungu juu ya uzima
kwa watu ni katika neema na sio katika sheria.
Sheria ni mfumo, kanuni na utaratibu uliyowekwa kwenye jamii, kwa
lengo la kusimamia tabia na kuongoza matendo yao katika jamii hiyo
husika. Sheria pia ni utaratibu unaotumika kutengeneza mifumo ya
kiibada na kiutawala kupitia mtu au kundi maalumu lililopitishwa au
kuidhinishwa kutekeleza wajibu huo. Kazi za sheria ni kuainisha haki
31
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

(mambo yaliyokubalika katika jamii husika ili jamii ipate kuyafuata),


na kuainishamakosa (mambo yasiokubaliwa na jamii husika ili jamii
isiyafuate). Sheria inasimamia kutoa haki kwa mujibu wa sheria
husika, na kutoa pia adhabu kwa kutafsiri matendo yasiokubalika na
yanayokubalika kwa mujibu wa sheria husika katika jamii, na kudhibiti
tabia na hulka binafsi za watu wa jamii hiyo.
Lengo kuu la sheria kwa jamii ni kuijengea jamii ustaarabu wa maisha
na kuamsha hari ya usawa ili kudumisha amani, furaha, haki, utu na
ustawi, na kuijengea jamii mfumo wa kusimamia watu, kuongoza
watu na kutawala watu.
Lakini torati nisheria za Mungu zilizowekwa na Mungu mwenyewe
katika Taifa lake la Israeli. Katika agano la kale, Mungu alijidhihirisha
katika watu aliowachagua kuwa watu wake kweli, na alionekana kwao
baada ya zaidi ya muda wa miaka 430 baadae, kwa wakati wote huo,
Mungu alinyamaza juu ya watu hawa, kana kwamba; hawakua watu
wake; na kwa kipindi hiki chote, watu hao walikuwa watumwa wa
Taifa lingine lisilomtambua Mungu wa kweli.
Watu hawa au Taifa hili la Mungu, ni mbegu ya utakatifu ambayo
Mungu alijisazia mwenyewe kutoka kwenye safina wakati ule wa
gharika, na mbegu hii iliandaliwa na Mungu kupitia kwa mtumishi
wake Nuhu.
Unaweza ukawa unajiuliza swali la namna hii, moyoni mwako, ni kwa
namna gani Nuhu alihusika kuliandaa Taifa hili? Jibu ni kwamba! Baada
ya Nuhu na familia yake kutoka kwenye Safina baada ya gharika, Nuhu
alianza kufanyakazi ya kilimo; na wakati wa mavuno, Nuhu alilewa
kwa divai ya mazao ya kazi yake, Mwa 9:21, inasema hivi ‘’Akanywa
Divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake.
Nuhu alikuwa na watoto watatu. Mwa 9:18

1. Shemu

32
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

2. Yafeth

3. Hamu
Sasa Nuhu akiwa amelala hapo katika hali ile ya utupu (Uchi), Hamu
aliuona utupu wa Baba yake, akaenda kuwaambia ndugu zake wawili;
na huyu Hamu ndiye baba wa Kanaani. Mwa 9:22. Weka alama hapo
anaposema “Hamu ndiye baba wa Kanaani” nitakwambia ni kwanini
Basi hao ndugu wawili wa Hamu; ambao ni Shemu na Yafethi, wao
walitwaa vazi, wakalitanda mabegani mwao wote wawili, wakaenda
kinyumenyume, wakaufunika uchi wa baba yao; huku nyuso zao
zikielekea nyuma, wala hawakuuona uchi wa baba yao. Mwa 9:23.
Nuhu akalevuka katika ulevi wake, akajua ambavyo mwana wake
mdogo (Hamu) alivyomtendea; akasema ‘’Na alaaniwe Kanaani, awe
mtumwa kabisa kwa ndugu zake’’.
Kumbuka “Hamu ndiye baba wa Kanaani” sasa hebu Jaribu kujiuliza,
Kanaani anahusika vipi na kosa la kuchungulia utupu wa Nuhu;Hata
adhabu ya kosa ielekezwe kwake?
Lakini Nuhu, anawabariki Shemu na Yafethi, ila katika Baraka hizo;
tunaona Yafethi ananafsishwa kuishi kwa Shemu. Ukisoma kitabu cha
Mwa 9:24-27utapata habari hii kwa urefu zaidi.
Sasa usisahau kuwa, “Hamu ndiye baba wa Taifa la Wakanaani” na
Shemu ndiye baba wa Taifa la Waisraeli. Na usisahau kuwa! Baraka
za Nuhu zilielekezwa kwa Shemu kumtawala Hamu, na Yafethi kukaa
kwa Shemu, kwa hiyo sio jambo la bahati nzuri au mbaya kwa Israeli
kurithi Taifa la Kanaani, ni mpango wa Mungu tokea wakati wa Nuhu.
Soma Mwa 11:10-26.
Kwa hiyo utaona, mpango huu wa Mungu kumtumia Abram ama
Ibrahimu kama mbegu ya utakatifu wake, ni matokeo ya uchaguzi wa
Nuhu kwa wanawe kutokana na matokeo ya matendo yao. Mungu
hakumchagua Ibrahimu kwa sababu ya matendo mema ya Ibrahimu,

33
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

bali alikamilisha kwa pendo na kwa uaminifu, neno la Baraka la Nuhu


kwa Shemu, na kutoka kwa Shemu, alizaliwa Arfaksadi kutokea kwa
Arfaksadi hadi Tera ni vizazi nane. Na Tera akamzaa Ibrahimu, na
kutoka kwa Ibrahimu alizaliwa Isaka, na kutoka kwa Isaka, alizaliwa
Yakobo, na kutoka kwa Yakobo, lilizaliwa Taifa la Israeli ambalo Mungu
aliliteua kuwa Taifa lake Takatifu na kulirithisha Taifa hilo nchi ya
Kanaani (Watoto wa Hamu yule aliyeuona uchi wa baba yake).
Hivyo ndivyo Nuhu alivyohusika na kuliandaa Taifa la Israeli kama
Mbegu ya utakatifu kwa Bwana Mungu wake, ndio maana leo; dunia
yote inajibarikia kwa Mungu kwa jina la Mungu wa Ibrahimu; lakini
chanzo cha Baraka za Ibrahimu ni Shemu.
Soma vizuri Biblia yako
Sasa Torati ndio iliyotumika kubainisha makosa (Dhambi) kwa Taifa hili.
Rumi 7:7 inasema ‘’Tusemeje basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini
nisingalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani,
kama torati isingalisema ‘’Usitamani’’ Kwa hiyo, ingawa kazi ya sheria
ni kuongoza watu katika kutenda haki,lakini pia sheria inatoa adhabu
juu ya makosa yaliyotendeka kwa mujibu wa sheria hiyo; ambayo
adhabu hiyo ni mauti, ndivyo biblia inavyosema kwamba! Mshahara
wa dhambi ni mauti. Rumi 6:23
Mauti ndio adhabu kuu kwa makosa ya sheria kama sehemu muhimu
ya malipo stahiki kwa makosa hayo. Na sheria hii (Torati), imepata
nguvu kutokana na dhambi kuingia duniani, kwa sababu dhambi
ilipoingia, ilisababisha kufa kwa mahusiano kati ya Mungu na mtu, na
kuwageuza kuwa maadui. Ndio maana Mungu anapokuja kwa Adamu
ili kuzungumza naye, Adamu anajificha; kwanini? Ni kwa sababu ya
ile dhambi kumtenga na Mungu wake, ndivyo yanavyosema maandio
kwamba; Dhambi zenu zimewafarakanisha na Mungu wenu. Isa 59:2
Lakini kabla ya dhambi, Adamu na Mungu hawakuwa maadui kabisa,
Mungu alikuwa anamtembelea Adamu na kuzungumza naye.

34
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Toka anguko la Adamu Edeni (Kutenda dhambi), na kujificha mbele


za uso wa Bwana Mungu wake; tendo hilo lilizalisha uadui kati ya
mwili wa mtu na sheria ya Roho wa uzima, kwa sababu ya udhaifu
wa sheria hiyo; ndio maana Yesu anasema ‘’Nimekuja kuitimiza torati,
sio kuitangua’’ Math 5:17. Kwanini aitimize? Hii inatuonyesha kuwa;
ile sheria (torati) ilikuwa na mapungufu kiasi cha kushindwa kutimiza
kusudi la Mungu kwetu. Hivyo dhamira ya mwili ikawa ni kupingana
na Mungu; na ndio maana mwili hautaki kumtii Mungu na hauwezi
kutii, kwa sababu mwili umebeba nguvu ya mauti iliyomo ndani ya
dhambi kutokana na ile sheria (Torati), Rumi 8:7; inasema ‘’Kwa kuwa
ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana hautii sheria ya
Mungu, wala haiwezi kuitii’’.
Kwa hiyo; bila kuwepo kwa ile sheria inayosema ‘’usile’’ Adamu
asingelikuwa na dhambi kwa kula hilo tunda. Kwanini? Ni kwa kuwa
ile dhambi ilikuwa dhaifu, sio kwamba haikuwepo, hapana! Dhambi
Ilikuwepo tangu mwanzo kwa sababu tayari shetani alishamuasi
Mungu na kufukuzwa mbinguni. Rumi 5:13 inasema ‘’Maana kabla ya
ile sheria (Torati) kuwepo, dhambi ilikuwamo duniani, lakini dhambi
aihesabiwi kuwa dhambi isipokuwapo sheria’’ kwa hiyo japo dhambi
ilikuwepo; lakini haikuwa na nguvu kabisa wala nafasi katika uhai wa
mtu (Haina kibali cha kuchukua uhai wa mtu) kwa kuwa hakukuwa na
sheria bado.
Lakini ilipokuja ile sheria, dhambi ilipata nguvu na kupata nafasi hata
kumtenga mtu na uhai wake.
Kabla ya sheria ya kutokula hilo tunda kuwepo, hilo tunda lilikuwepo;
lakini Adamu hakula; ila ilipokuja ile amri (Sheria), ikafanya ndani ya
Adamu na mkewe kila namna ya kutamani kula hilo tunda; kwa nini?
Ni kwa sababu dhambi bila ile sheria imekufa. Rumi 7:8 lakini kwa
sababu ya ile sheria, mauti ikaingia na Adamu ameshapata malipo ya
dhambi zake (kufa) kwa sababu ya kula tunda alilokatazwa kutokula
kisheria. Imeandikwa ‘’Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria;
ila ilipokuja ile amri, dhambi ikahuika, naminikafa. Rumi 7:9. Hapa
haimaanishi kuwa ile sheria ni dhambi, hapana! Bali ile dhambi ilikuja
35
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

kwa sheria, kwa sababu kule kutamani kusingekuwa dhambi kama


isingekuwepo sheria inayosema ‘’usitamani’’ na kwa ile sheria, mwili
ukawasha tamaa yake, kwa sababu nia ya mwili siku zote ni mauti.
Ndio maana imeandikwa kusema ‘’Kwa maana tulipokuwa katika
hali ya mwili, tamaa za dhambi zilizokuwako kwa sababu ya torati,
zilitenda kazi katika viuongo vyetu hata tukaizalia mauti mazao. Rumi
7:5
Hivyo kutokana na ile nia, mwili unapingana na ile amri ambayo ni ile
sheria ya uzima, hata hauwezi kamwe kushikamana na sheria hiyo,
hivyo mwili unafanya bidii sana kutoitii ile sheria, lengo lake likiwa
ni kupata kutekeleza adhima yake (Kutimiza mauti kwa mtu).Ndio
maana Neno linasema, ‘’Bali mkiishi kwa sheria mjue wazi mwataka
kufa’’ Kwa sababu mwili haukubaliani na hiyo sheria, na hautakaa
ukubaliane nayo kamwe. Paulo mtume kwa kulitambua hili anasema
‘’Lile nitakalokulitenda, silitendi; bali nisilolitaka ndilo nilitendalo’’
Rumi 7:15-17
Kama tukiishi kwa sheria twataka kufa, je! Tuishi kwa muundo gani
ili tupate kuwa hai? Jibu ni kwamba! Tunapaswa kuishi kwa neema.
Kama tunapaswa kuishi kwa neema; Je! Tusiitii sheria? Hapana! Kwa
kuwa hata neema nayo ilikuja kwa ile sheria, ili tukiadhibiwa (tukifa)
kwa sheria, tusamehewe (tuokolewe) kwa neema, kwa kuwa wokovu
wa Mungu hautokani na haki ipatikanayo kwa matendo ya sheria,
ndio maana imeandikwa mtu asijisifu, maana tumeokolewa bure kwa
neema bila msaada wa matendo yetu. Efe 2:8-9 inasema kwamba!
‘’Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo
hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa
matendo mtu awaye yote asijisifu.
Ikiwa wokovu hautokani na matendo ya haki (Kwa sheria), basi sheria
inayoamuru mema imekufa, yaani ile sheria; imeuliwa kwa Neema
ya Mungu iliyomo ndani yangu katika Kristo, kwa vile sheria ambavyo
isivyoweza kuzaa matunda, na kwa kuwa kamwe ile sheria haiwezi
kuzaa; Mungu aliiadhibu sheria iletayo mauti kwa mauti ya msalaba,

36
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

hata imekuwa dhambi hainitawali tena, kwa maana siwi tena chini ya
sheria, bali ya neema (Rumi 6:14).
Hivyo basi, japo ile sheria asili yake ni rohoni, bali iliwekwa kwaajili ya
matendo ya mwilini, hata ikashindana na mwili; na sheria ikashindwa
kuuthibiti mwili kwa kuwa mwili asili yake ni mauti, bali karama ya
Roho (Asili ya ile sheria) ni uzima,kwa kuwa sheria yenyewe asili yake
ni rohoni;ndio maana kumekuwa na vita ndani ya mtu hata mwili
ukishindana na ile nia ya Roho (Uzima).
Kwa hiyo, vitakati ya mwili na Roho, vimesababisha mwili kuharibu
uhusiano na Mungu (kufa kwa roho ndani ya mtu) utokanao na ile
sheria. Basi ikiwa roho yangu imekufa ndani yangu kwa ile sheria,
kama neno linavyosema kwamba! ’Tulikuwa wafu kwa sababu ya
dhambi zetu’’Warumi 7:9. Ikiwa dhambi ya mauti ipatikanayo kwa
sheria imeniua roho yangu ndani yangu, ni dhahiri kuwa; ile sheria
ya Mungu isemayo ‘’usile’’ huua, bali Roho wa Mungu uhuisha kama
ilivyoandikwa, ‘’Ikiwa Roho aliyemfufua Kristo katika wafu anakaa
ndani yenu, ataifufua na miili yenu iliyo katika kufa’’. Ebra 10:28.
Maana yake ni kwamba! Matendo ya haki ipatikanayo kwa sheria,
hayawezi kamwe kuhuisha uhai wa mtu uliyokufa ndani yake. Kwa
nini? Ni kwa sababu ile sheria iliyomtawala na kumuua wakati yu
hai, haimtawali tena. Hivyo kama haimtawali! Haiwezi kumuhuisha,
maana sheria inamtawala mtu akiwa hai; Rumi 7:1. Hivyo mtu akiisha
kufa; hawi tena chini ya usimamizi na mamlaka ya ile sheria. Ndio
maana anasema, ‘’Bali dhambi haitawatawala ninyi, kwa kuwa hamwi
chini ya sheria, bali ya neema’’. Rumi 6:14.
Anaposema ‘’Hamwi chini ya sheria” anamaanisha kwamba! Sheria
haikutawali; kwanini? Ni kwa sababu umekufa. Rumi 6:11a anasema
‘’Vivyo hivyo ninyi nanyi, jihesabuni kuwa wafu (mmekufa) kwa
sababu ya ile dhambi’’ Yaani mmekufa kwa matendo ya ile sheria.
Hivyo ingawa iko ahadi ya Mungu ya urithi wa wana, lakini ahadi hiyo
haipatikani kwa ile sheria; Sasa tuweje! Torati haipatani na ahadi za

37
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Mungu? Hasha!kwa kuwa ingalitolewa sheria iwezayo kuhuisha, haki


ya Mungu ingalipatikana kwa ile sheria. Gal 3:21. Lakini sasa, sheria
imegeuka kuwa adui kwa wana wa Mungu, badala ya kuleta ule uzima
uliourithi wa wana kwa Baba yao, sheria imeleta mauti. Ikiwa hivyo
ndivyo; basi ni wazi kuwa, sheria hiyo imefarakana na uzima kwa
sababu haiwezi kumpa mtu haki itakayompa uzima.
Sasa tuishi vipi ili tusife kwa sheria? Jibu ni hili; uchungu wa mauti ni
dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. 1Kor 15:56; Kwa hiyo ilikuzima
mauti ipatikanayo kwa sheria, ni kuacha kufuata nia ya mwili, yaani
tusiishi kwa kufuata mwili, bali tuishi kwa kuifuata roho; kwa kuwa
nia ya mwili ni mauti, bali karama ya Roho ni uzima, tena sio uzima tu;
bali uzima wa milele.Gal 5:18. Hivyo ikiwa hautaki kufa ndugu yangu,
usijitese bure kwa kujisumbua kutafuta haki ya Mungu kwa matendo
ya sheria, hapana! Bali itafute haki ya Mungu kwa njia ya Neema ya
Mungu katika imani (Kumwamini Yesu Kristo) ili upate uzima. Yoh
3:16na imeandikwa pia kwamba! ‘’Mwamini mwana wa Mungu upate
uzima bure’’ Filipi 3:9.
Anaposema kwamba! “Upate uzima bure” anatusaidia kujua kuwa!
Uzima huo, haugharamikiwi na mtu kwa matendo ya mtu yatokanayo
na bidii yake katika kuitumikia au kuifuata sheria; bali hupatikana
bure, hutolewa na Mungu mwenyewe kama zawadi (Neema) kwa
njia ya imani, maana yake anashauri watu waifuate Imani ya Mungu
kwa Njia ya Kumuamini Kristo Yesu, na ndani ya imani hiyo, ndipo
kulipowekwa huo uzima; maana yake ni kwamba! Ukiisha kuamini tu
na kuingia katika Pendo lake, moja kwa moja umeupata uzima.
Torati ililetwa na Mungu kwa mkono wa Musa kwa watu wa Mungu,
ili watu hao wapate kutenda haki (Matendo mema), na tunaposema
‘’matendo mema’’ tunazungumzia matendo yale anayoyataka Mungu
watu wake wayatende. Ndio maana utaona, sheria inakataza kuua,
lakini Mfalme Sauli, anatumwa na Mungu kwenda kuua kila mtu bila
kujali jinsia wala umri, na Sauli aliposhindwa kutekeleza agizo hilo,
ndipo Mungu akampokonya nafasi hiyo ya Ufalme, na badala yake
akapewa Daudi. 1Samw 15:1-3; Kwa nini? Ni kwa sababu, torati sio
38
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

yale maandiko kwenye kitabu, bali torati ni neno lolote la Bwana


litokalo kinywani mwake.

Haki ya Mungu haidhihirishwi kwa sheria:


Ukweli ni huu, kwamba; haki ya Mungu haidhihirishwi kwa matendo
ya sheria, kwa sababu Mungu ni zaidi ya sheria, tunapozungumzia
haki ya Mungu, hatuzungumzii matendo yanayoongozwa na sheria,
ya Mungu juu ya Mungu, kwa kuwa Mungu ndiye sheria yenyewe.
Mungu hana haki, bali yeye mwenyewe ndiye haki yenyewe; ndio
maana imeandikwa ‘’Mungu amefanya kila kitu kwa makusudi yake,
hata wabaya kwa siku ya ubaya’’ hii ni sawa na kusema, ‘’Mungu
hatendi jambo jema, bali kila atendalo Mungu ndilo lililojema’’ kwa
kuwa matendo mema na mabaya, hupimwa na Mungu kwa ajili ya
wanadamu, na sio wanadamu wanaopima matendo mema kwa ajili
ya Mungu.

Haki ni nini?

Katika kamusi ya Kiswahili, neno haki hutafsiriwa kama:


a. Kitu au jambo ambalo mwingine anastahili kulipata
b. Utendaji, ufuatiliaji na utumiaji wa sheria na kanuni
katika kutekeleza au kutimiza jambo
c. Mali/umiliki
Kwa tafsiri ya kamusi ya kisheria, neno haki lina maana ya kile mtu
anastahili kuwa nacho au kile anachoruhusiwa kufanya, au kile
anachostahili kupokea kutoka kwa wengine kwa mujibu wa sheria. Au
kwa lugha nyingine, tunaweza kusema kwamba; ‘’haki ni maslahi ya
mtu ambayo yanatambuliwa na kulindwa kisheria.

Sasa Kuna tofauti kati ya kutenda haki na kutoa haki

a. Kutenda haki

39
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Ni matendo ya adili au ya uadilifu kwa mujibu wa sheria, mtu


anapaswa kutenda matendo yanayokubalika kisheria katika
jamii husika

b. Kutoa haki,

Kutoa haki ni kumpatia mwengine kile au lile analostahili kwa


mujibu wa sheria ya jamii husika.
Kwa mujibu wa maana hizi zote, tunapata kutambua kuwa; Mungu ni
mwenye haki, lakini si katika utendaji wa kisheria, bali ni mtoaji wa
haki kwa watu waliyoitii sheria yake.
Mara nyingi, watu hudhani kwamba; Mungu ana haki (Hutenda
mema), hapana! Ukweli ni kwamba; Mungu hana haki (hatendi
mema) hata kidogo na wala hawezi kutenda mema kabisa (kuwa
na haki), kwanini? Ni kwa sababu, haki ni matendo yanayotokana
na kuitii sheria, na kazi ya sheria ni kumuongoza mtu katika njia ya
Bwana Mungu wake na kumtawala, sheria haimtawali Mungu wala
kumuongoza; kwa kuwa Mungu hayupo chini ya sheria.
Hivyo Mungu ni mwenye haki katika kutoa haki, na sio katika kutenda
haki, maana haki inatokana na sheria; lakini Mungu haishi kwa sheria,
bali yeye mwenyewe ndio sheria. Sasa unatumia mizani gani kupima
matendo ya Mungu hata upate kipimo kinachoitwa haki kwenye
matendo yaliyotendwa na Mungu?
Hapana! Bali Mungu ndiye huyapima matendo ya watu kwa mizani
yake na kutoa haki kwa watu waliotenda au kustahili kupokea haki.

40
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

SURA YA NNE: MAUTI NA CHANZO CHA KUFA KWA


ROHO NDANI YAKO
MAUTI NI NINI

Mauti ni hali ya kusitishiwa uhai kwa kiumbe hai, ni hali ya kukosa


Kuwepo kwa muendelezo wa maisha ya kitu au Mtu. Ndio maana
watu wakifanyabiashara halafu ile biashara ikakosa mwendelezo
wanasema imekufa, au watu wakiwa kwenye mahusiano ya uchumba
au ndoa, halafu mahusiano hayo yakakosa muendelezo na kufika
mwisho, wanasema uchumba au ndoa imekufa
Kadharika hata kwenye maisha ya Mtu katika mwili, uhaiunapokosa
ule muendelezo wa maisha ndani ya mtu huyo, maisha ya mtu huyo
yanakoma (Anakufa), kwa lugha rahisi, tunaweza kusema kwamba!
Mauti ni hali ya kukoma kwa ushirika kati ya roho, nafsi na mwili.
Kwa kuwa maisha yalianza kwa ushirika kati ya roho, nafsi na mwili.
Mwa 2:7 inasema ‘’Bwana Mungu akampulizia puani pumzi ya uhai,
mtu akawa nafsi hai; kumbe ule uhai alionao mtu ni matokeo ya
kushirikiana kwa roho, nafsi na mwili.
Na huo uhai ndio uliompa mtu nafasi ya kuishi hapa duniani katika
mwili, kwa hiyo inapotokea ushirika ule kuvunjika, ndipo tunasema
maisha ya huyo mtu yamekoma (Anakufa)
Lakini pia tukumbuke kwamba! Maisha ya mtu duniani, ni matokeo
ya ushirika na Mungu kiroho, hivyo ikitokea ushirika huo kuvunjika;
mtu huyo anakufa Mauti ya kiroho). Kwa hiyo sio ajabu kuona watu
wanatembea lakini rohoni wameshakufa
Na mauti pia inahusisha adhabu ya makosa kwa siku ya hukumu.

Asili ya Mauti
Asili ya mauti, ni dhambi, na dhambi hapo kwanza ilikuwa ni hali ya
kwenda kinyume na neno la Mungu. 1Kor 14:56 Uchungu wa mauti

41
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati; ndio maanaimeandikwa


‘’Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya; usile, kwa
kuwa siku utakapo kula matunda ya mti huo, utakufa hakika’’ Mwa
2:17. Lakini kwa siku hiziza leo, dhambi sio nguvu ya torati tena bali ni
kumkataa Kristo (Kutomwamini) Yoh 8:24 na dhambi ni uasi’’
Biblia inatafsiri kuwa; mauti kuu kati ya zote, ni ile mauti ya kiroho
(Mtu kukosa uhusiano mwema wa kiroho na Mungu), mauti hii ndio
msingi wa mauti zote. Mauti ni hali ya kukoma kwa uhai wa kiumbe
au kitu au jambo, na katika kamusi ya kiswahili, neno ‘’Kifo’’ ni hali
ya kutokuwa na uhai, au kukoma au kuwa na mwisho mbaya wa kitu
Fulani, lakini pia mauti ni hali ya kukosekana kwa uwepo wa maisha
(kuishi) kwa viumbe wenye uhai.
Kusudi la Mungu ni mtu aishi maisha ya milele. Huu umilele wa mtu,
ndiyo uhusiano wa kudumu uliyopo kati ya mtu na Mungu, kwa kuwa
Mungu kwa asili yeye ni Roho, na mtu ni roho ya Mungu inayoishi
ndani ya mwili wa mtu kimaumbile, ndio maana imeandikwa ‘’Bwana
Mungu akampulizia puani pumzi ya uhai, Mtu akawa nafsi hai’’ kwa
hiyo ile Pumzi ya Mungu ya uhai, ni roho kamili ya Mungu iliyoingia
ndani ya mwili wa mtu, hata mtu akapata kuwa nafsi iliyo hai katika
mwili kutokea rohoni, kwa hiyo, mtu na Mungu; wanaushirika katika
roho na sio katika mwili.
Hivyo, ushirika kati ya mtu na Mungu, umejengwa katika roho ya mtu
na sio katika mwili wa mtu, kwa hiyo; uhusiano uliyopo kati ya mtu
na Mungu, unadumu baina yao katika ulimwengu wa roho kama mtu
huyo akiitii sauti na maagizo ya Bwana Mungu wake. Na uhusiano
huu unapodumu, ndipo mtu hupokea zawadi ya uzima wa milele,
yaani uhai usio na kikomo cha muda wa kuishi. Lakini uhusiano huu
ukivunjika, hiyo ndio asili au chanzo cha mauti
Kwa hiyo, mtu hawezi kufa kama atadumisha uhusiano wake na
Mungu, kwa kuwa kifo sio mpango wa Mungu kwa watu wake, bali
kifo ni adhabu ambayo watu wanapokea kama malipo kwa dhambi
zao. Kwa maana pasipo dhambi hakuna mauti kamwe

42
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Sasa unaweza kujiuliza, Je! Mungu aliweka sheria makusudi ili tufe?
Au je! Tunakufa kwa kuvunja sheria makusudi? Jibu ni hapana! Sheria
iliwekwa kwa ajili ya kudhibiti matendo maovu ya wanadamu dhidi ya
Mungu wao, ili wapate kukamilika katika njia zao. Hivyo mpango wa
Mungu katika sheria, ni kutawala tabia na matendo ya mtu ili asiwe
kwa tabia kama mtu asiye na Mungu.Na hatuvunji sheria makusudi
ili tufe, bali kwa matendo ya mwili, ni vigumu mtu kuitii sheria, kwa
sababu nia ya mwili ni mauti.
Hivyo mwili hauwezi kuchangamana na sheria ya uzima kutokana
na vile tulivyorithi kutoka kwa mtu wa kwanza wa udongo (Adamu),
na kwa kuwa mwili asili yake ni mavumbi, hauwezi kufuata asili ya
roho; kwa kuwa, kutokana na matendo ya roho, hupingana dhahiri
na matendo ya mwili, hivyo matendo ya mwili, kamwe hayawezi kutii
wala kumtii Mungu kabisa.
Kwa hiyo, mwanadamu wa tabia ya mwilini, hawezi kumtii Mungu
katika mwili, sio kama hapendi, hapana! Bali kwa kuwa ile nia ya mwili
ni mauti, hawezi kumtii Mungu, kwa kuwa Mungu ni Roho; hivyo mtu
hata akitaka kumtii Mungu katika mwili, mwili unakataa japokuwa
mtu huyo hutamani kutenda yaliyo mema, lakini kwa asili kutokana
na ile sheria ya dhambi inayofanya kazi ndani; inapingana na sheria
ya Roho ya uhuru na uzima katika Kristo Yesu. Rum 8:5-8 imeandikwa
kwamba! ‘’Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya
mwili; bali waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho, kwa kuwa nia ya
mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani; kwa kuwa ile nia ya
Mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala
haiwezi kutii; wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
Unaweza kuwa unajiuliza swali hili, Je! Nifanye nini ili kuupata uzima
wa milele?
Kama tulivyoona, pingamizi kubwa kati ya uhai na mauti, ni matendo
ya mwili, ambayo kwa asili hayawezi kuitii ile sheria ya uzima. Kama
hivyo ndivyo, kamwe mtu hawezi kuwa mzima kwa jitiahada zake za
mwili; ikiwa kama kweli nia yako ni kuupata uzima wa milele, fanya

43
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

haya mambo yafuatayo:

1. Yauwe matendo ya mwili, yapinganayo na sheria ya

uzima
• Ingawa jambo hili sio rahisi hata kidogo, ni jambo lenye
maumivu katika nafsi ya mtu, kwa sababu yale uyapendayo,
hayo ndiyo yanayokinzana na sheria ile ya uzima hata
usiweze kuitii, kwa kuwa nafsi huvutiwa kutenda yale mambo
yaliyokatazwa katika sheria ya Mungu.
Lakini acha nikwambie, kwa kadiriile sheria ilivyowekwa (Torati)
ili kudhibiti makosa ya matendo na tabia za watu, ili mtu kwa
tabia apate kumtii Mungu; ndivyosheria ilivyozidi kutengeneza
uadui zaidi kati ya mtu na Mungu wake katika mwili wa mtu, kwa
kuchochea tamaa ndani ya nafsi kufanya yale yaliyokatazwa, hata
kujiongezea ujuzina maarifa zaidijuu ya kutenda mambo hayo
yaliyokatazwa. Kwanini? Ni kwasababu, nia ya mwili siku zote ni
mauti, kwa hiyo, mwili unashindana na ile nia ya roho ambayo
ni uzima na amani, ndio maana maandiko yanasema, kwamba!
‘’Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa
dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu kwa kumtuma mwanaye wa
pekee, katika mfano wa mwili, ulio wa dhambi, na kwa sababu ya
dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili. Rumi 8:3
Kwa hiyo, Mungu alipoona kwamba; ile sheria iliyowekwa kama
lijamu kwa mtu, haiwezi kuudhibiti mwili wa mtu, ili mwili upate
kumtii yeye aliyeuumba, ndipo Mungu akaamua kwa pendo lake,
kuiadhibu ile sheria yenyewe katika mwili wa Kristo Yesu, ili sisi
tusimpendeze Mungu kwa haki ya matendo ya sheria (Torati), bali
kwa haki ipatikanayo kwa neema katika Kristo Yesu Bwana wetu
kwa njia ya imani, mbali na sheria.Kwa maana, Mungu aliposema
na mtu kwa ile sheria ‘’usizini’’, ndipo sheria hiyo ikachochea na
kuamsha tamaa ya zinaa hata kufanya mtu azini hadi na viumbe wa

44
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

aina nyingine (Wanyama, ndege. N:k). Kwa hiyo, ili mtu apate kuitii
sheria (kupata haki kwa matendo ya sheria), amelikataa pendo
la Mungu aliyeimimina neema yake kwetu, hata tuhesabiwe haki
bure pasipo matendo yetu kwa njia ya kumwamini Yesu Kristo.
Rumi 3:24
Nguvu ya mauti
Nguvu ya mauti, ni hali ya kiutendaji inayofanyakazi ya kutenganisha
kati ya:

• Mungu na mtu (Kuvunja uhusiano kati Mungu na mtu


kiroho)

• Mwili wa mtu na roho yake (kuondoa uhai ndani ya


mtu)

• Kuzimu na Mbingu (Adhabu ya hukumu na uzima wa


milele)
Na mauti inapata kibali na haki ya kutekeleza kazi zake kupitia agano
la kuzimu na mauti, ambalo mtu ameagana na shetani. Isaya 28:18
inasema ‘’Na agano lenu mliloagana na mauti, litabatilika; tena
mapatano yenu mliyopatana na kuzimu hayatasimama. Pigo lifurikalo
litakapopita, ndipo ninyi mtakapokanyagwa nalo’’
Biblia inapozungumzia agano na mauti, inamaanisha kufanyika kwa
mapatano kati ya shetani na mtu, juu ya kumuasi Mungu. Ukisoma
biblia, utaona Mungu akiweka agano la uzima na mtu mbali na mauti,
ili mtu aishi milele bila kufa. Mwa 2:17, neno la Mungu linasema
‘’Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa
maana siku utakapokula matunda ya mti huo, utakufa hakika’’
Lakini kwa sababu ya uasi, mtu alilivunja agano hili la Mungu la uzima,
na kufanya agano la mauti na shetani kwa sababu ya tamaa na uasi.

45
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Mwa 3:1-6, hii ni habari ndefu, lakini ukisoma utaona shetani akifanya
mazungumzo na Adamu kupitia kwa Eva. Mazungumzo hayo yalilenga
moja kwa moja kwenye mikakati ya kutengeneza agano la mauti kwa
njia ya kumuasi Mungu, kwa matarajio ya Adamu kupewa nafasi ya
Mungu.
Agano lilipokamilika na uasi kuchukua nafasi yake ndani ya Adamu
na mkewe, ndipo dhambi ya kwanza ilipoingia na kuleta mauti kwa
mtu, kwa sababu; hapana mauti bila dhambi; kwa kuwa mshahara wa
dhambi ndiyo mauti, hapana dhambi bila uasi, ndio maana maandiko
yanasema kuwa; dhambi ni uasi. Hivyo, utaona mtu alifanya agano
na mauti kwa njia ya kuasi na kutenda dhambi. Hivyo, mtu akiisha
kumuasi Mungu na kutenda dhambi, amefanya mapatano na kuzimu
kwa kujitiisha na kujiinamisha chini ya mamlaka na himaya ya kuzimu,
ndio maana Isaya anasema ‘’Mapatano yenu mliyopatana na kuzimu’’
(Nguvu za giza).
Mapatano ni makubaliano ya majadiliano yaliyopata ridhaa kutoka
katika pande zote zilizoshiriki mjadala husika, na kutoka na azimio
moja, kama ambavyo shetani alijadiliana na Eva kwa niaba ya Adamu,
juu ya kumuasi Mungu, na kutoka na maadhimio ya kuasi. Mapatano
yanaweza kumshusha mtu nafasi yake kwa kumtoa katika nafasi ya
juu aliyokuwa nayo hapo awali na kumpa nafasi mpya ya chini, au
kumpandisha mtu katika nafasi yake, kutoka katika nafasi ya chini na
kwenda kwenye nafasi ya juu, hii hutegemeana na aina ya mapatano
(Makubaliano).
Kwa mfano: Esau na Yakobo. Mwa 25:29-34
Esau alikuwa mzaliwa wa kwanza Kwa mzee Isaka, na mdogo wake
aliitwa Yakobo; wawili hawa walizaliwa mapacha, kwa mujibu wa
sheria za urithi wakati huo, ilimpasa Esau kuchukua sehemu kwanza
ya urithi kuliko Yakobo. Lakini kwa sababu ya njaa yake, Esau; alikubali
kufanya mapatano ya kubadilishana nafasi ya uzawa na haki ya urithi
kati yake na Yakobo, ili Yakobo ampe Esau chakula chake na Esau
ampe yakobo haki yake ya nafasi ya uzaliwa wa kwanza.

46
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kwa hiyo, Yakobo akawa mkubwa kwa nafasi (position) dhidi ya Esau;
japo Yakobo alikuwa mdogo kiumri kwa kuzaliwa, lakini ile nafasi ya
ukuu kwa kuzaliwa, ilihama kutoka kwa Esau na kwenda kwa Yakobo,
na hivyo Yakobo akawa na haki ya kurithi Baraka za Esau kutoka kwa
baba yake, na Esau aliipoteza hiyo nafasi kupitia yale Makubaliano
aliyoyafanya na Yakobo kwa sababu ya kile chakula, kilichofanya
Esau adhani kuwa; nafasi ya uzaliwa kwake, sio kitu cha msingi sana
kwenye maisha yake kama ilivyo muhimu kwa chakula. Mwa 27:1-45,
soma tu, utajifunza mambo muhimu sana kwa ajili ya mafanikio yako.
Ukisoma mstari ule wa 32 kwenye sura hiyo hiyo ya 27, utaona Isaka,
yaani baba yake Esau na Yakobo, anamuuliza Esau, u nani wewe?
Kwanini Isaka amuulize swali hili Esau? Je! Isaka alikuwa amemsahau
Esau? Jibu ni kwamba! Esau alipoteza nafasi (kiti) cha ukuu, kwa hiyo,
alibaki kuwa mkubwa kiumri tu, lakini nafasi yake (position) ya urithi
kwake haipo tena; ndio maana baba anataka kumbariki, lakini haoni
ile haki ya Esau kubarikiwa kama mzaliwa wa kwanza.
Kwanini Esau asiwe na hiyo haki mbele ya baba yake? Ni Kwa sababu
Esau alimpa Yakobo haki hiyo. Wewe je! Umempa nani haki yako
Kwenye Mwa 27:1; tunamuona Mzee Isaka akiwa amepoteza uwezo
wake wa kuona, na akijua ya kuwa; anaweza kufa wakati wowote,
alimuita Esau mwanae, na kumtaka Esau kujiungamanisha na Baraka
zake kwa njia ya kumpatia baba yake chakula, kwa kuwa Baraka za
Esau kutoka kwa baba, zilifungwa kwenye moyo wa Baba yake (katika
pendo) ndio maana unaona baba anamwambia mwanae akisema
‘’ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili
nile; na roho yangu ikubariki kabla sijafa’’
Kwanini ilikuwa ni lazima kwa Esau kumpa baba yake chakula ndipo
abarikiwe? Na kwanini Esau ilikuwa ni lazima apewe chakula ndipo
atoe haki yake ya uzaliwa wa kwanza kwa Yakobo? Math 6:25 Yesu
anawaambia wanafunzi wake kuwa ‘’Kwa sababu hiyo nawaambieni,
msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini, wala miili yenu,
mvae nini; Maisha je, si zaidi ya chakula, Na mwili zaidi ya mavazi”

47
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Yesu anaposema ’Msisumbukie maisha yenu’’ anamaanisha kwamba;


tusisumbukie hali ya kuishi kwetu (uhai wetu) katika mwili; kwa nini?
Ni kwa sababu, kimaumbile, afya ya mwili ni chakula, hivyo kwa kuwa
Mungu anataka tuishi, atatupa chakula yeye mwenyewe kwa maisha
yetu. Na badala yake, Sisi tunatakiwa kusumbukia msingi wa kuishi
kwetu (Uhusiano wetu na Mungu), ndio maana Isaka anamwambia
Esau, kwamba! ‘’Na roho yangu ikubariki kabla sijafa), kumbe Baraka
zetu hazitokani na mwili, bali na roho’’ ndio maana Mungu anasema
‘’si kwa nguvu, wala si kwa uweza, bali ni kwa Roho wangu” Zekaria
4:6
Sasa ni kwanini Isaka hakuweza kabisa kumbariki mwanae Esau bila
Esau kuleta chakula..? Jibu ni kwamba; Chakula (Neno) ndio uzima,
ndivyo maandiko yanavyosema ‘’Mtu hataishi kwa mkate tu” kwa
hiyo, ukweli ni kwamba; tunahitaji chakula (Neno la Mungu) ili tuishi
kwa mujibu wa maneno hayo. Kwa hiyo, ili roho ya Isaka iwe na nguvu
ya kumbariki Esau, ilibidi ipate nguvu ya uhai,yaani iwe na uzima; kwa
maana ya Neno la Mungu (Chakula); kwa kuwa neno ndilo linalotia
uzima. Yoh 6:63
Lakini, chakula hicho (Neno la Mungu) kisipoungamanishwa na nafasi
ya mtu kupokea Baraka, mtu huyo hawezi kubarikiwa; kumbuka,
Esau alishauza nafasi yake ya kupokea Baraka (uzaliwa wa kwanza)
kwa chakula, hivyo hawezi kamwe kuzipokea Baraka hizi hata kama
ameleta chakula kile ambacho mbariki wake anakipenda. Kwa sababu
kile chakula kilihitajika kwa ajili ya Baraka za mzaliwa wa kwanza,
kwa hiyo Esau kwa kuwa aliuza hiyo nafasi yake, hakuwa na haki ya
kupokea hizo Baraka kutoka kwa baba yake;
Kumbuka hili, ni muhimu sana; hatubarikiwi eti kwa sababu ni wana;
bali tunabarikiwa kwa sababu tunastahili.
Ndivyo ilivyo kwa watu wengi leo, kwamba; wameokoka kweli, ni
sawa, lakini hawabarikiwi katika maisha yao, japo ni waombaji wazuri
na wanatoa sadaka nzuri mbele za mbariki wao (Mungu), swali la
msingi hapa, ni, hili, je! Uwezo wa Mungu wa kubariki umeisha? Au

48
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

uwezo wa watu kupokea Baraka ndio haupo?


Jibu ni kwamba:
Watu wamepoteza uwezo wao wa kupokea Baraka, (Yaani, wameuza
haki yao ya uzaliwa wa kwanza/Nafasi ya urithi) maandiko yanasema,
sisi ni warithi wa Mungu, turithio pamoja na Kristo. Rum 8:17. Basi
Kama sisi ni warithi wa Mungu, maana yake sisi ni watoto wa Mungu.
Maandiko yanathibitisha wazi kwamba!Kwa hakika sisi ni watoto wa
Mungu, tunaoshuhudiwa na Roho wa Mungu pamoja na roho zetu.
Rum 8:16-17 imeandikwa ‘’Roho mwenyewe ushuhudia pamoja na
roho zetu, ya kuwa sisi ni watoto wa Mungu, na kama tu watoto, basi
tu warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo.
Lakini je! Kama kweli sisi ni watoto wa Mungu, tunayo ile haki ya urithi
wetu kwa Mungu? Maandiko yanasema kuwa; waongozwao na Roho
wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Rum 8:14.
Swali ni je! Wewe Kama ni mwana wa Mungu; unaongozwa kweli na
Roho wa Mungu? Na Kama kweli unaongozwa na Roho wa Mungu
unajuaje? Imeandikwa, waliozaliwa na Mungu hawatendi dhambi, na
tukiongozwa na Roho, hatutazitimiza tamaa za mwili, kwa hiyo una
nafasi ya kujiuliza na kutafakari mwenendo wako, usije ukawa kama
Esau, anayeenda kubarikiwa kwa baba yake kwa nafasi ya Baraka za
Yakobo, utagombana na Mungu bure mwana wa Mungu.
Hebu rudia maandiko haya, Mwa 27:32, yanayosema ‘’Isaka baba
yake, akamuuliza u nani wewe.? Hapo anapomuuliza u nani wewe,
haulizii kwa habari ya jina, anauliza kwa habari ya nafasi (uzaliwa),
ambayo hiyo nafasi ndiyo inayompa Esau haki ya kurithi Baraka. Kwa
hiyo, Isaka anauliza kwa kuwa, Esau hayupo kwenye nafasi yake, na
badala yake yupo Yakobo. Je! Upo kwenye nafasi yako? Na kama
haupo, je! Nani yupo kwenye nafasi yako?
Kufa kwa roho ndani ya mtu, ni tendo linalotafsiri kuvunjika kwa
mahusiano na uhusiano kati ya Mungu na mtu huyo; mahusiano haya

49
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

yanapovunjika, mtu hupoteza nafasi yake ya kuishi umilele wake, na


badala yake anakua na maisha mafupi; yaani yenye ukomo wa muda
wa kuishi hapa duniani. Na kwa kuwa hakuna tena ushirika kati ya
Mungu na mtu, mtu huyo hukosa msaada toka kwa Mungu juu ya
mahitaji yake na hivyo hupoteza tumaini la uzima ndani yake.Lakini
Mungu kwa kuwa ni pendo, hudumu daima akituvuta kwake kwa
pendo lake, ili turejee kwake atuponye, ndio maana anasema; ‘’
Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi asema Bwana’’ Zekaria 1:3.
Wito huu wa Mungu kwa watu wake, unatokana na pendo la
Mungu kwetu; pendo hili la pekee la Mungu, ndilo linalosababisha
hata Mungu asimuondoe Roho wake ndani yetu, akisubiri tamko la
utekelezaji wa wokovu kutoka kwa Mungu juu ya mtu aliye tayari.
Hata sasa Roho wa Mungu ametulia ndani yetu, akisubiri tugeuke tu
ili atuokoe. Japo sisi tunamfanya Roho ahuzunike ndani yetu, kama
ilivyoandikwa, msimuhuzunishe Roho wa Mungu ‘’Wala msimzimishe
Yule Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye kwa yeye, mlitiwa muhuri
hata siku ya ukombozi. Efeso 4:30.
Kwa hiyo; tamaa ya Roho wa Mungu ni kutuhuisha katika ufalme wa
Kristo Yesu kwa njia ya kutukomboa kutoka kwenye njia ya mauti
kama yasemavyo maandiko matakatifu, kwamba! ‘Naye alituokoa
katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika Ufalme wa
Mwana wa Pendo lake. Kolosai 1:13’’ Hapa anaposema kuwa ‘’Naye
alituokoa’’ anamaanisha anayeokoa ni Mungu, na lengo la kutuokoa;
ni ili tupate kibali cha kuingizwa katika ufalme wa mwana wa pendo
lake (Yesu Kristo Bwana wetu), na ikiwa Mungu alituokoa kwa njia
ya mauti ya Kristo Yesu, ni dhahiri kwamba sisi sote tuliookolewa
tulikuwa mateka wa mauti hapo kwanza; na anatuambia kuwa;
tulikuwa chini ya mamlaka ya giza (kuzimu). Tukiwa mateka wa ile
dhambi ambayo katika hiyo, tumekuwa watumwa wa matendo ya
mwilini yale yapinganayo na Roho wa uzima wa Kristo aachiliae uhuru
kwa wote wanaomtii Mungu.

50
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Ndio maana maandikoyanasema ‘’Msimzimishe Roho wa Bwana’’


Kwanini? Ni kwa sababu, Roho wa Bwana amekaa kwetu kama nuru
iangazayo, ili apate kutuangazia nuru yake katika njia zetu; yaani
kutukemea tunapotenda mabaya.
Ambayo hayo ndio matendo ya giza yanayouficha uso wa Bwana
Mungu wetu hata asitazame uhitaji wetu. Efeso 5:13 imeandikwa
kusema ‘’Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru; maana
kila kilichodhihirika ni nuru.
Kwa hiyo kumbe, kila kitu ambacho hakikemewi ni giza, na giza ni
matendo yote yapinganayo na kweli ya Mungu, ambayo katika hayo,
mtu hawezi Kamwe kusimama mbele za Bwana wakati wa uhitaji, na
kupokea majibu ya haja yake; ndivyo maandiko yasemavyo ‘’Dhambi
zenu, zimewafarakanisha na Mungu wenu, hata mwaomba lakini
hataki kusikia’’.
Kwa hiyo, kila mtu ambaye nuru ya Roho inaangaza nafsini mwake,
inamuangaza iliapate kutenda kila tendo lililo jema.Efeso 5:9; inasema
‘’Kwa kuwa, tunda la nuru ni katika wema wote, na haki, na kweli’’.
Kwa hiyo; Mungu amemuacha Roho wake kama mbegu kwa ajili ya
siku ya wokovu (Neema yake), Mungu yeye kwa pendo lake siku zote
ataendelea kumuacha Roho wakeakisubiri mpaka siku utakapogeuka
(Kuokoka) au kuuacha ulimwengu (Kufa). Roho hii, ni tofauti na roho
iliyo ndani ya mtu (Pumzi ya mungu) ndani ya mtu ambayo kama
ikiondoka, basi uhai wa mtu hufikia kikomo (Kufa) kwa maana ya
kupoteza uhai wake. Roho wa Mungu hutusaidia kuuona upendo wa
Mungu juu yetu kwa njia ya Neno lake katika Kristo Yesu.
Katika uumbaji, Mungu alimuumba mtu mwenye asili, muonekano,
na tabia ya kipekee, kisha akamshirikisha mtu huyo umilele wake (hali
ya kutokuwa na mwisho wa ukomo wa uhai au kutokufa).
Lakini kwa sababu ya tamaa na uasi, mtu huyu alipoteza tunu hiyo
mpaka Mungu alipomrudishia tena kwa njia ya mwana wake wa
51
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

pekee; Yesu Kristo. Ingawa roho wa huyo mtu alikufa ndani yake kwa
sababu ya dhambi na makosa yake angali hai, alihuishwa kwa pendo
la Mungu katika Kristo ili ikiwa amekufa kwa dhambi, awe hai kwa
haki kwa njia ya Neema, ili atakapodhihirishwa, apate kuvalishwa vazi
la utukufu na heshima nyingi, na kurudishiwa maisha yake ya umilele
yaliyofichwa katika mauti yake kwa kutoitii sheria ya Mungu.
Mungu alimpa mtu dunia kama makao ya urithi wake, lakini kwa
sababu ya dhambi, mtu ameyakimbia makao ya urithi wake na kuwa
mateka wa shetani kwa sababu ya kukosa kutii.
Hesabu 35:28-29, Mungu anasema nasi maneno haya, ‘’Kwa sababu
ilimpasa kukaa katika mji wake wa makimbilio hata kifo chake kuhani
mkuu; lakini kuhani mkuu atakapokufa, huyo mwuaji atarudi aende
kwenye nchi ya urithi wake. Mambo haya yatakuwa ni amri ya hukumu
kwenu, katika vizazi vyenu vyote, na katika makazi yenu.
Katika Taifa la Israeli, Mungu aliweka sheria; kwamba, ikitokea mtu,
amemwua mwenziwe kwa bahati mbaya, ilimpasa kuiponya nafsi
yake mwenyewe. Kulitengwa mji maalumu wa makimbilio, ambapo
mwuaji huyo, alipaswa kukimbilia katika mji huo na kuuacha mji wa
urithi wake; na akiisha kuingia katika mji huo, hairuhusiwi kwa mtu
yeyote kumuua; maana ameiponya nafsi yake.
Lakini ikitokea, mwuaji amekamatwa nje ya mji, atauawa kama vile
naye alivyoua. Na kwa vile ulimwengu ulikwisha kuhamishwa kutoka
mahali pake (Watu wa Mungu kuondolewa kwenye kusudi), ilipaswa
warejeshwe kwa mauti yao wenyewe.
Lakini kwa lile Pendo kuu la Mungu Baba yetu; alikuja katika mwili
kwa njia ya Kristo Yesu mwanawe wa pekee, ili ulimwengu usipotee,
bali uokolewe katika mwana kwa njia ya imani. Maana maandiko
yanasema, ‘’Kwa maana jinsi hii, Mungu aliupenda ulimwengu,
(watu wake), hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila amwaminiye,
asipotee, bali awe na uzima wa milele. Yoh 3:16

52
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kwa hiyo, mwana alikuja duniani kama kuhani mkuu, kwa mfano wa
Melkizedek mfalme wa salemu (Mfalme wa Haki na Amani) ili katika
yeye, tuwe na haki mbele za Mungu na Amani duniani kote. Kwa hiyo
kama maandiko yanavyosema juu ya Yule muuaji, kwamba!Anahitaji
mauti ya kuhani mkuu ili yeye aweze kupata uhuru wake tena. Hivyo;
hawezi kujiletea uhuru pasipo mauti, ni mpaka pale itakapotokea
Mauti ya Kuhani mkuu, hapo ndipo, mtu huyo huurudia urithi wake;
kwanini? Ni kwa sababu ile dhambi imemfanya mtu huyu kuwa
mtumwa. Katika Isaya 5:13a Mungu anasema ‘’Kwa sababu hiyo, watu
wangu wamechukuliwa mateka’’
Hapo anaposema ‘’Kwa sababu hiyo” anatusaidia kutambua kwamba,
kabla ya kutekwa, kuna sababu (Jambo lililofanyika) ambayo ndilo
iliyopelekea watu hao kutekwa, anasema ‘’Kwa sababu hiyo’’ kwa
sababu ipi.?Yaani, ni kwa sababu ya ile dhambi iliyotokana na watu
kukosa maarifa, ndiyo hiyo iliyopelekea watu hawa waliokuwa huru
kuchukuliwa mateka; na anaposema ‘’wamechukuliwa’’ maana yake
wamehamishwa, hawapo tena katika mahali pao wenyewe.
Na aliyewateka, alifanya nao vitavya kiroho kwanza katika nafsi zao
na kuwashinda kupitianjia ya kuishindanisha sheria ya Mungu na
matendo ya mwili.Rum 7:23 inasema ‘’Lakini katika viungo vyangu,
naona sheria iliyo mbali inapiga vita na ile sheria ya akili zangu na
kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.
Kwa hiyo, unaona mtekaji alitumia njia ya kuwagombanisha watu na
sheria ya Mungu, na sheria iliposhindwa, ndipo akawachukua mateka
na kuwahamisha. Ndio maana utaona, Mungu kabla hajatuingiza
katika urithi wetu, (Katika ufalme wa mwanawe wa pekee Kristo Yesu)
alituhamisha kwanza baada ya kutukomboa, ndipo akatuingiza katika
ufalme wa mwana wa pendo lake. Kolosai 1:13
Kwa hiyo; ili waliotekwa wapate ukombozi (Uhuru wa roho na miili
yao), iliwapasa watarajie mauti ya Kuhani wao mkuu (Yesu Kristo).
Kwa kuwa katika yeye, amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
Kwa sababu hapo kwanza, makuhani walikuwa wengi; kwa sababu
walizuiliwa na mauti wasikae; bali yeye kwa kuwa akaa milele, anao
53
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ukuhani wake usioondoka. Naye kwa sababu hii, aweza kuwaokoa


kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye, maana yu hai siku zoteili
awakomboe. Ebrania 7:22-5
Mpendwa, haijalishi shetani amekutoa kwenye nchi ya urithi wako
kwa mateso ya namna gani, na sitaki kujua mateso hayo yamekutesa
kwa muda wa miaka mingapi hadi sasa, ninachoweza kukwambia ni
kwamba! Tayari kifo cha kuhani wetu mkuu (Yesu Kristo) kimekwisha
kutokea pale msalabani, mahali palipoitwa Golgotha, yaani; fuvu la
kichwa, nje ya mji juu ya kilima ili kwamba kila jicho lipate kumwona,
na kila mtu aweze kumwendea. Kwa hiyo tangu sasa unao uhuru
wako wa kurudi mahali pa nchi ya urithi wako, unachotakiwa kufanya
kuanzia sasa, ni kujionyesha kwa mshitaki wako kuwa sasa kuhani
wako amekwisha kufa, huku ukiwa na ushahidi wa neno na damu ya
kuhani. Ndivyo iliyoandikwa, ‘’Nao wakamshinda shetani Kwa damu
ya mwanakondoo na kwa neno lao la ushuhuda. Ufu 12:11
Damu hiyo ndio dhabihu ya agano jipya, ambalo Mungu amelifanya
na watu wake nyakati hizi; na agano hilo ni agano la urithi kwa wana
wa Mungu. Maana imeandikwa ‘’ Na Kama tu watoto, basi tu warithi,
warithi wa Mungu warithio pamoja na Kristo’’ Rum 8:17. Ndio maana
ilibidi Kristo kama kuhani mkuu wa agano jipya afe, kwa kuwa yeye
ndiye mjumbe wa agano jipya na urithi wetu ni katika yeye, ndivyo
maandiko yasemavyo ‘’Maana agano la urithi lilipo, ni lazima iwepo
mauti yake yeye aliyelifanya, Kwa maana agano la urithi lina nguvu
palipotokea kufa kwa mtu; kwa kuwa halina nguvu kabisa akiwa yu
hai yeye aliyelifanya. Ebra 9:16-17
Maandiko yanapoongelea juu ya agano lililo bora zaidi, maana yake
ni kwamba; kuna agano ambalo halikufikia katika kiwango cha ubora
kwa kadiri ya matarajio ya agano hilo. Ndio maana anasema ‘’Angalia
siku zinakuja, asema Bwana, nami nitawatimizia nyumba ya Israeli na
nyumba ya Yuda agano jipya, halitakuwa agano kama lile nililoagana
na baba zao, katika siku ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika
nchi ya Misri, kwa sababu hawakudumu katika agano langu, mimi
nami sikuwajali asema Bwana. Ebrania 8:7-9
54
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Agano la kwanza ni agano la Edeni, juu ya nyoka kupondwa kichwa


na uzao wa mwanamke; agano hili ni msingi wa uvunjifu wa agano la
kwanza lililo kati ya Mungu na Adamu; agano hili likaendelea mpaka
wakati wa Taifa la Israeli, Taifa ambalo Mungu amelichagua kama
kituo cha ukuzaji mbegu ya utakatifu kwa dunia, na kama kituo cha
vita vya kiroho dhidi ya ulimwengu wa giza. Imeandikwa ‘’Kwa maana
kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme
na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya
katika ulimwengu wa roho. Efe 6:12
Israeli wao walipotolewa katika nchi ya utumwa, walikabidhiwa lile
agano na Mungu, kwamba‘‘Yeye atakuwaBwana Mungu wao’’ hivyo
anawatakawaheshimu uwepo wake na wasiwe na mungu mwingine
ila yeye. Kutoka 20:1-5, ndivyo Mungu anavyozungumza na wana
wa Israeli, na kuwaambia ‘’Mimi ni Bwana Mungu wako, niliyekutoa
katika nchi ya misri, nyumba ya utumwa, usiwe na miungu mingine
ila mimi’’. Hapa Mungu anasisitiza akisema ‘’Usijifanyie sanamu ya
kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala
kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia. Usivisujudie
wala kuvitumikia; Kwa kuwa mimi, Bwana Mungu wako, ni Mungu
mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao hata kizazi cha
tatu na channe cha wanichukiao.
Kwa hiyo, unaposikia Mungu anasema juu ya kufanya agano jipya,
ujue wazi kuwa; ni dhahiri kwamba; agano hilo la kwanza lilishindwa
kutekelezeka, watu walijifanyia miungu yao, wakaabudu miti, mawe,
na vitu mbalimbali; ndio maana Mungu sasa anasema kwamba watu
hao‘’hawakudumu katika agano langu, nami sikuwajali” inamaanisha
kuwa; agano hilo halipo tena. Ndio maana leo Mungu anazungumzia
kwa habari ya kuwepo kwa agano jipya.
Anasema hivi, “Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya
Israeli baada ya siku zile, asema Bwana. Nitawapa sheria zangu katika
nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami nitakuwa Mungu
kwao, nao watakuwa watu wangu. Ebrania 8:10. Ukisoma kwa utulivu
hiyo Ebr 8:10, utaona kuna maneno yanapaswa kuzingatiwa maneno
55
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

hayo ni “Agano jipya” na “Siku zile” na “Sheria” na “Moyo” na “Watu


wangu”
Kwa nini nimekazia kwenye maneno hayo.? Nimekazia hapo ili tupate
kuyatazama hayo maneno kiundani kidogo, hapo anapozungumzia juu
ya agano jipya, anamaanisha kwamba! Kulikuwa na agano la zamani
hapo kwanza, lakini agano hilo halikudumu, kwa maana watu wale
waliyokuwa na agano naye, walishindwa kudumu na kuenenda sawa
sawa na matakwa ya agano hilo, kama anavyosema “Siku zile” siku
hizo ni zile ambazo watu walikubaliana na Mungu juu ya hilo agano,
lakini katika kuishi kwao;hawakuweza kudumu katika agano hilo.
Kwanini? Ni kwa sababu agano hilo lilikuwa na sheria ya kwenye
makaratasi (Torati), ndio maana Mungu anasisitiza kwenye agano
jipya ataweka sheria hizo kwenye mioyo (Roho Mtakatifu); maana
yake ni kwamba! Hatazibadilisha zile sheria, atatumia sheria zile zile
lakini zitaandikwa kwenye moyo baada ya kwenye kitabu; Kwa hiyo
sheria hizo zikiisha kuandikwa kwenye moyo, zitampa mtu kuzipenda
na kuzitenda, na hapo ndipo huyo mtu atakuwa mtu wa Mungu kwa
vile anavyodumu katika kutenda sheria za Bwana katika agano lake
Torati 32:28-29, Mungu anasema ‘’Maana hawa ni taifa wasio shauri,
wala fahamu hamna ndani yao. Laiti wangekuwa na akili, hata
wakafahamu haya, ili watafakari mwisho wao!
Ni nani hao taifa wasio shauri wala fahamu ndani yao? Ni watu wale
ambao, hawafahamu namna ya kutoka kwenye hali ya mauti ambayo
inawakabili, lakini hawataki shauri la Mungu la kumkubali Kristo
kuwa Bwana na Mwokozi wao; kwanini hawakubali? Ni kwa sababu
hawatafakari mwisho wao baada ya mauti yao. Maana laiti kama
wangelifahamu juu ya hatima yao baada ya mauti; wangeokoka
Bwana huwaita watu hawa kama watoto waasi. Anasema ‘’Ole wao
watoto waasi, asema Bwana; watakao mashauri lakini hawayataki
kwangu mimi, wajifunikao kifuniko lakini sio cha roho yangu, wapate
kuongeza dhambi juu ya dhambi. Isa 30:1

56
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Tunaona mtu wa kwanza kuasi ni Adamu, yeye aliasi kwa kuyakataa


mashauri ya Bwana, pale alipoambiwa na Mungu ‘Usile tunda” sheria
hii kwa Adamu aliichukuliakama mateso, ndipo akatafuta mashauri
mengine yasio ya Bwana Mungu wake, na kujikuta akiwa anaongeza
dhambi juu ya dhambi; kwanini? Adamu lijua kule kuitii ile sheria
ya Bwana ni kukiri udhaifu, hivyo nafsini mwake alitafuta namna ya
kujinasua kutoka katika sheria hiyo. Unaweza kujiuliza nimejuaje!
Lakini na wewe jiulize swali hili; je! Shetani angeweza kuwashauri
Adamu na mkewe kufanana na Mungu kama hawajawa na mawazo
hayo ndani ya mioyo yao?

Ukweli ni kwamba! Ile sheria ya Mungu, ndiyo iliyoweka tamaa ndani


ya moyo wa Adamu juu ya kumuasi Mungu. Kwa sababu, kabla ya
ile sheria; Adamu na mkewe hawakula lile tunda. Kwanini? Ndani ya
mioyo yao, hawakuwa na mpango wa wao kuwa Mungu, walitosheka
na ile hali yao ya kuwa watu; lakini ilipokuja ile sheria, ikaonekana
kama inawanyima uhuru wao, ndipo na wao wakatamani sasa kuwa
kama Mungu ili wasiwe tena chini ya sheria.

Hapo ndipo walipoanza kutafakari na kutafuta njia ya wao kufanana


na Mungu; na mwisho wakajikuta kwa kupitia ile tamaa yao,
wanaangukia mkononi mwa shetani na kudanganywa.

Hivyo ndivyo ilivyo kwa kizazi hiki cha ukaidi, kisichokubali sheria za
Bwana, wala hawataki ushari wake. Japo Bwana anawaita akisema
‘’Njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo’’

KWANINI TUNAKUFA?

Katika maisha ya kawaida, mtu alipaswa kuishi maisha ya milele, lakini


ili aishi maisha hayo; ni lazima kufuata utaratibu na masharti ya uzima
wenyewe. Kwa hiyo mtu anapokosa kutimiza au kutekeleza masharti
na kanuni za uzima huo, anapoteza sifa za kuwa na huo uzima; na
huko ndiko kufa.

57
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kwa hiyo, ile hali ya mtu kushindwa kutekeleza matakwa ya uzima


huo, inatafsirika kama kosa kisheria (Kutenda dhambi) Mwa 2:16-17
inasema, ‘’Bwana Mungu akamwagiza huyo mtu akisema, matunda
ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi
wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya
mti huo, utakufa hakika’’. Kwa hiyo tendo la Adamu la kula hilo tunda
alilokatazwa kula, jambo hilo linachukuliwa kama kuvunja sheria ya
uzima, na hivyo Adamu aliadhibiwa kama mkosaji wa sheria ya uzima
kwa kuhukumiwa kupokonywa uzima wenyewe (Kufa) kwa sheria.
Kitendo cha kuvunja sheria (kutenda dhambi), ni matokeo ya uasi,
ndio maana Bibilia inasema dhambi ni uasi.
Uasi ni nini?
Uasi ni kitendo kinachotafsiri hali ya kujiinua, kunakopelekea hali ya
kukiuka makubaliano, maagizo na sheria zilizowekwa ili kuzifuata. Na
mtu anaweza kuasi kutokana na kutoridhishwa na makubalino hayo,
au kuwa na tamaa ya kitu cha ziada ambacho hakipatikani kwenye
makubaliano hayo, au hali ya kujiona yeye ni bora zaidi ya mwengine.
Na mwasisi/mmiliki wa uasi ni lusifa/shetani; lusifa ni kiumbe wa
kiroho aliyeumbwa na Mungu katika kundi la viumbe aina ya malaika,
aliumbwa na utukufu mwingi kiuzuri, kisifa na heshima; alipambwa
kwa kila aina njema ya mapambo, ndivyo ilivyoandikwa. Isaya.
14:11-12 ‘’Fahari yako imeshushwa hata kuzimu, na sauti ya vinanda
vyako. Funza wametandazwa chini yako, na vidudu vinakufunika.
Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, ewe nyota ya alfajiri, mwana wa
asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa ewe uliyewaangusha mataifa
Lusifa yeye aliwahi kuwa malaika mkuu Mbinguni, asimamaye mbele
za Mungu; na hapa nasisitiza tena, ingawa aliumbwa na sifa zote hizo
na nyingine nyingi ambazo hata hazikuandikwa kwenye kitabu hiki,
lakini bado anabaki kuwa ni kiumbe wa kiroho kutoka kwenye kundi
la viumbe aina ya malaika.

58
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kwanini ni muhimu kufahamu kuwa lusifa au shetani, yeye ni kundi la


viumbe wa kiroho aina ya malaika?
Umuhimu wake ni kwamba! Itakusaidia kujua mipaka yake kiutendaji
na kiwango cha uweza wake wa kutenda mambo yake unaishia wapi,
kwanini? Ni kwasababu; Mungu na shetani au lusifa, wote ni Roho,
lakini kunatofauti kati ya Roho Mungu, na roho shetani, ingawa wote
ni nafsi. Lakini Nafsi Mungu hakuumbwa, yeye sio kiumbe wa kiroho,
bali yeye ni Roho.
Nafsi ni nini kwani? Nafsi ni jumla ya akili, hisia na utashi; Mungu
anamwambia Ibrahimu kwa kusema hivi ‘’Nimeapa kwa nafsi yangu,
hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuzidisha nitakuzidisha’’ Mwa
22:16-17
na ndio maana biblia inasema akili za Mungu hazichunguziki; na yeye
ndiye aliyeumba dunia na vyote viijazavyo, viumbe vyote ni mali yake
na kwake vyote vitarudi ikiwa ni pamoja na huyo lusifa/shetani.
Tofauti kati ya Mungu na shetani kinafsi ni kwamba:

- Nafsi Mungu
• Mungu yeye yupo kila mahali kwa wakati mmoja
wakati wote

- Nafsi shetani
Shetani yeye hawezi kuwa kila sehemu kwa wakati

mmoja
Kwa hiyo shetani au lusifa, baada ya kuona sifa za uzuri na utukufu
pamoja na heshima aliyopewa; alitamani kuwa zaidi ya Mungu,
ndipo akawaza ndani yake kama maandiko yasemavyo, ‘’Nawe
ulisema moyoni mwako, nitapanda mpaka mbinguni, nitakiinua kiti
changu juu kuliko nyota za Mungu; nami nitaketi juu ya mlima wa
mkutano, katika pande za mwisho za kaskazini. Nitapaa kupita vimo
59
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

vya mawingu,nitafanana na yeye aliye juu’’ Isaya 14:113-14


Kwa hiyo unaona asili ya uasi jinsi unavyoanza na kufanya kazi? Hapa
shetani anaona nafasi aliyonayo na maslahi ya nafasi hiyo ni kama
havifanani; yaani anaona anachokipata ni kidogo kuliko ambacho
anastahili kupata, hapo ndipo unaona shetani anatamani kunyanyua
nafasi yake (Kiti) zaidi ya Mungu.
Baada ya maadhimio hayo ndani yake, ndipo alipoanzisha kampeni
ya ushawishi kwa kuwashawishi theruthi ya malaika waliokuwa huko
mbinguni, na miongoni mwa malaika hao, wengine kati yao walikuwa
na vyeo mbinguni.
Lakini habari njema ni kwamba! Lusifa na malaika zake, walipigwa na
kutupwa; sio kutupwa duniani tu, bali kutupwaduniani na mwisho
kufungwa kuzimu moja kwa moja; yaani chini ya dunia. Maandiko
yanatuthibitishia hilo katika kitabu cha ufunuo, Ufu 12:7-9 inasema
‘’kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake, wakapigana
na yule joka, Yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake;
nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni.
Yule joka akatupwa, Yule mkubwa, nyoka wa zamani aitwae Ibilisi
na shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na
malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Maana yake ni kwamba, sasa lusifa/shetani na malaika zake; hawapo
tena mbinguni wala duniani, bali kuzimu alikofungwa yeye na wakuu
wake, lakini pamoja na hayo, bado tunahitaji kuishi kwa tahadhari
juu ya kiumbe huyu; kwa maana japo ameshindwa ile vita mbinguni,
lakini hakupokonywa ule uweza wake wa Kiroho na ile sifa yake ya
udanganyifu. Kwa hiyo anaweza kufanya mambo tukadhani kuwa ni
Mungu ndiye aliyefanya, na mwisho mambo hayo yakatutoa kwenye
nafasi zetu ambazo Mungu alituumba kwa ajili ya hizo; yatupasa kuwa
makini na matokeo ya kazi za kiroho zinazotendeka, na tunao mfano
mkubwa juu ya hilo.

60
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Maandiko matakatifu yanatuambia, kusudi la Mungu la kumuumba


mtu duniani, ni ili mtu huyo apate kutawala; ndio maana Mungu
anasema, na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu. Mwa 1:26
Baada ya Mungu kuazimia maazimio hayo, alimuumba Adamu na Eva;
na kwa uaminifu wa Mungu, aliwaweka katika bustani ya edeni kama
kituo au ofisi ya utawala; na Mungu hakuwaacha peke yao, bali kwa
nyakati zote za utawala wao alikuwa akiwatembelea bustanini.
Na kwa kipindi ambacho ushirika na mahusiano ya Mungu na Adamu
yalipoimarika, ndipo Adamu akajisahau na shetani akaingiza roho
ya uasi ndani ya Adamu na mkewe dhidi ya Mungu, kwa njia ile ile
ya kuwashawishi Adamu na mkewe kutamani kuwa kama Mungu,
jambo hili lilimuangusha Adamu, kwa sababu, lengo la shetani/lusifa,
halikuwa Adamu awe kama Mungu, bali ilikuwa ni kumkosanisha
Adamu na Mungu ili Adamu afukuzwe kwenye nafasi yake, na nafasi
hiyo lusifa aichukue yeye. Ndio maana utaona baada ya Adamu na
mkewe kufuata njia za shetani/lusifa, wanaingiwa na hofu dhidi ya
Mungu na kujificha.
Shida ni nini hata ikafikia kwa Adamu na mkewe wajifiche? Jibu ni
kwamba! Adamu na mkewe, Walifanya kitu ambacho katika akili zao
walitegemea katika hicho, Mungu akija kuwatembelea atawakuta na
wao wanaheshima sawa kama Mungu, lakini matokeo yake, badala
ya kukutwa wakiwa na heshima waliyotegemea, walishangaa kujikuta
wanakuwa watupu mbele za uso wa Mungu ndio maana wakajificha.
Kwa sababu mpango wa shetani ni kuwakosanisha na Mungu, hata
baada ya kugundua kuwa walichokifanya hakikuwa sawa mbele za
Mungu,wao hawakutafuta namna ya kutengeneza na Mungu wao,
badala yake; wanajificha mbele za Mungu.Mungu anauliza “Adamu
uko wapi?” unafikiri Mungu alikuwa anauliza kwa sababu Mungu
alikuwa hajui Adamu alipo? Hapana! Mungu alikuwa anajua kila kitu,
ila alikuwa anataka kuona Adamu na mkewe wanajutia makosa yao
na kutubu; lakini badala ya kutubu, wao wakaanza kutupiana makosa
kwa hiyo, japo Mungu alifungua huo mlango wa rehema kwa Adamu

61
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

na mkewe, wao waliufunga mlango huo kwa mikono yao wenyewe


kwa kukataa toba. Mungu akamfukuza Adamu katika Bustani hiyo.

62
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

SURA YA TANO: FALSAFA ZA UHAI WA MUNGU NDANI


YA MTU

NINI MAANA YA FALSAFA?

Neno falsafa (philosophy), ni neno linalotokana na lugha ya kigiriki,


likifahamika kama “Filosofia’’ filosofi ni neno lenye muunganiko wa
maneno mawili tofauti ambayo ndio yaliyounganishwa na kuwa neno
moja, na maneno hayo ni:

• Filo: likiwa na maana ya upendo

• Sofia: likiwa na maana ya Hekima


Kwa hiyo maana kamili ya neno hili, ni kupenda hekima
Falsafa ni jaribio (tabia ya kujaribu) kutafuta uelewa na ufahamu juu
ya jambo katika uumbaji na muumbaji, na kuelezea ulimwengu kwa
akili kwa kuunda hoja zenye mantiki.
KAZI KUU YA FALSAFA

Kazi kuu ya falsafa, ni kuchunguza kuwepo kwa, au kutokuwepo kwa


ukweli, ujuzi, mema, mabaya, lugha, haki N.k. Kwa kifupi, falsafa ni
njia ya mfumo wa kuuliza maswali magumu na kutafuta majibu yake,
na kwa sehemu kubwa, falsafa hutumika kwa ujumla wa mafundisho
au imani ya mtu, au kikundi cha watu
Kwa mfano:
Kuna falsafa za vyama vya siasa, falsafa za dini N:k
Katika muktadha huo, falsafa ya dini imepotosha ukweli halisi kuhusu
Mungu, kwa kushindwa kuchunguza swali la ‘’Mungu ni nani?’’ kisha
kutoa jibu sahihi kuhusu uhalisia wa Mungu. Kwa sababu hiyo, dhana
mbalimbali zimezalishwa katika dinimbalimbali, zikihusishwa na
uhalisia wa Mungu, kumekuwa na vitu mbalimbali (mapokeo ya dini),
63
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

vinavyodhaniwa kuwa vina uhusiano wa moja kwa moja na Mungu.


Lakini Mungu anasema kwenye Yer 3:16 inasema, kwamba! ‘’Kisha
itakuwa, mtakapoongezeka na kuwa wengi katika nchi hiyo, asema
Bwana, siku zile hawatasema tena, ‘’Sanduku la agano la Bwana’’
wala halitaingia moyoni, wala hawatalikumbuka, wala hawatalizuru,
wala hayatofanyika hayo tena
Mungu anadhihirisha wazi kuwa; nguvu zake hazipo tena kwenye
sanduku la agano (kwenye vitu vya upako), kwa hiyo hakutakuwa na
zile ibada zinazohusiana na vitu hivyo vya upako, yaani kulinyenyekea
sanduku hilo tena (Ibada za vitu). Kiuhalisia biblia haikatai mafunuo
na matumizi ya vitu hivyo; ikiwa ni Roho wa Mungu aliyeyafunua,
na hata mimi sipingi kwamba kuna watumishi waliopewa mafunuo
hayo na Roho. Na mafunuo hayo, yanaweza kuwa endelevu au ya
muda mfupi kwa ajili ya jambo maalumu, mimi sina shida kabisa na
watumishi waliofunuliwa. Lakini shida ni kwa wale watumishi wasio
na mafunuo, hawakai na kumsikiliza Roho Mtakatifu, na badala yake
wanaiga mifumo ya kiibada kutoka kwa watumishi wengine.
Lakini ni kwanini ibada hizo zinaendelea? Biblia inasema, wachungaji
wetu, hawatulishi kwa maarifa wala kwa ufahamu, hali iliyopelekea
watu kutafuta na kuamini vitu zaidi kuliko kumtafuta na kumuamini
Mungu.
Swali ni je! Falsafa ya dini, ni jambo lisilofaa katika imani?
Jibu ni hapana! Kwanini?
Falsafa za dini, ndio muongozo wa kuuliza na kupata majibu sahihi
kuhusu Mungu, kwa hiyo; bila falsafa za dini, tutapokea mapokeo ya
imani kutoka kwenye mawazo ya watu binafsi na kuona kama ndio
muongozo sahihi wa kimani kuhusu Mungu, kitu ambacho huwenda
kikatukwamisha kuupata ukweli kuhusu Mungu.
Ndio maana Biblia inasema, ‘’msiziamini kila roho, zijaribuni kwanza
mwone kama hizo roho zinatokana na Mungu au la! 1Yoh 4:4.
64
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Anaposema zijaribuni, anamaanisha kuzichunguza, na uchunguzi


huu, hautokani na vipimo vya maabara ya kimwili, bali na maabara ya
kiroho katika ulimwengu wa roho, ili kupata msaada utakaotuongoza
na kutusaidia kujiuliza maswali haya na kupata majibu sahihi juu ya
maswali hayo kuhusu roho hizo, na hapa ndipo panapohitajika filo
(upendo), na sofia (hekima) Filosofi.
Lakini kwa sababu ya kuamini kila roho, watu wamepofushwa fikira
zao; Bwana Mungu anapowatazama watoto wake, anawahurumiasana
kwa sababu wametawanyika na kukusanywa katika himaya ya shetani
kwa sababu ya kukosa maarifa, wamemezwa na uovu; ndipo Bwana
kwa huruma anawaita akisema kwamba! ‘’Rudini, enyi watoto wenye
kuasi, asema Bwana, maana Mimi ni mume wenu. Nami nitatwaa mtu
mmoja wa mji mmoja, na wawili wa jamaa moja, nami nitawaleta
hata Sayuni. Nami nitawapa ninyi wachungaji
Wanipendezao moyo wangu, watakaowalisha ninyi kwa maarifa na
fahamu. Yeremia 3:14-15
Yesu wakati anawaaga wanafunzi wake alisema kwamba! ’Hata nikali
bado ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi
sasa; Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza
awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake
mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo
atawapasha habari yake. Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa
katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Yoh 16:12-14
Yesu anaposema “Bado ninayo mengi ya kuwaambia’’ anamaanisha
kwamba! Kazi aliyoikamilisha hapa duniani, ilikuwa ni ile kazi yake ya
kutoa dhabihu ya ukombozi, na kuchukua funguo ya kuzimu na mauti;
lakini juu ya mafundisho na elimu ya ufalme, ni mchakato endelevu,
ambao hautafika mwisho mpaka pale Yesu atakaporudi kulichukua
kanisa lake; kwa hiyo hakuna mtu yeyote aliyefikia mwisho kujifunza
juu ya habari ya siri za ufalme wa Mungu kupitia mafundisho ya neno
la Kristo.

65
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kwanini? Ni kwa sababu Yesu hakumaliza kufundisha, ila aliacha kwa


kuwa aliona wanafunzi hawawezi kustahimili mafunzo mengi kwa
wakati mmoja. Swali la kujiuliza ni hili! Kama Darasa la elimu ya siri
za Ufalme wa Mungu linaendelea, na Yesu Kristo hayupo duniani;
tunajifunza Darasa hili kupitia njia gani?
Yesu anasema hivi “Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza
awatie kwenye kweli yote’’ kwa hiyo, darasa hili la siri za ufalme wa
Mungu tunajifunza kupitia njia ya Roho wa kweli.
Je! Kweli ni nini? Yoh 17:17 inasema ‘’Uwatakase kwa ile kweli, neno
lako ndio kweli’’ kumbe ‘’Kweli’’ ni neno la Mungu, inapotokea roho
yeyote akatufundisha elimu isiyotuingiza kwenye kweli yote (Neno la
Mungu); roho hiyo haitokani na Mungu na wala sio Roho wa Mungu,
kwa kuwa Roho wa Mungu anafanyakazi ya kuwaingiza watu kwenye
ufalme kamili wa Mungu; ndio maana Yesu anasema hivi huyo ‘’Roho
atawaongoza awatie kwenye kweli yote’’ kama tulivyojifunza kuwa
kweli ni neno la Mungu, na Neno ndiyo Mungu. Yoh 1:1 inasema
‘’Hapo mwanzo palikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu,
naye neno alikuwa Mungu
Kwa hiyo, kazi ya Roho Mtakatifu katika darasa hili la siri za ufalme wa
Mungu, ni kuwaongoza watu, na kuwatia kwenye mamlaka ya Mungu.
Ukiona mtumishi hafundishi habari za watu kutiwa kwenye kweli yote;
anaposema ‘’Awatie kwenye kweli yote” anamaanisha kuwaingiza
kwa Mungu, neno “Kuwatia” inaashiria tendo lisilo la hiyari ya mtu,
ni nguvu za yule ambaye akutia kwenye mamlaka yake. Kwa hiyo,
darasa la siri za ufalme wa Mungu, halilengi kufanya mambo ambayo
watu wanayataka, bali linawaongoza watu kwa ile nguvu na kuwatia
kwenye mamlaka ya Mungu kwa kufanya yale Mungu anayoyataka sio
watu wanayoyataka.
Lakini kazi ya Roho Mtakatifu, ni pamoja na kuzungumza na kanisa
kwa niaba ya Kristo; Ndio maana Yesu anasema ‘’Hatanena kwa shauri
lake, lakini kila atakalosikia kwangu atalinena’’ kwa hiyo kazi ya Roho
Mtakatifu, ni kuwasilisha maneno ya Kristo katika Kanisa la Kristo,

66
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

na hayo ndio mafunuo ya Roho. Kwa hiyo, mafunuo yasio akisi neno
la Mungu, na maono yasiyompa Kristo utukufu; hayatoki kwa Roho
wa Mungu, hayo ni mafunuo na maono kamili kutoka kuzimu kabisa,
wala haijalishi amefunuliwa au ameyaona nani, mafunuo ya Roho wa
Mungu ni juu ya yale yajayo, na wala hayalengi kumtukuza mtumishi
au Roho mwenyewe, bali ni kumtukuza Kristo
Falsafa za Mungu ni fumbo, ni siri iliyositirika katika ulimwengu wa
roho, watu wa mwilini, hawawezi kabisa kutambua siri hii. 1Kor 2:1-4
maandiko yanasema hivi, ‘’Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu,
sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa
hekima. Maana naliazimu nisijue neno lolote kwenu ila Yesu Kristo,
naye amesulibiwa. Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu
na hofu na matetemeko mengi. Na neno langu na kuhubiri kwangu
hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu,
bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe ya wanadamu,
bali katika nguvu za Mungu’’
Kazi kubwa ya mtumishi wa Mungu, ni kuzifunua siri za Mungu
katika Roho Mtakatifu, na sio kwa matendo na matamanio ya mwili,
bali Roho; na wala hafanyi hayo kwa ajili ya kupata utukufu yeye
mwenyewe, bali Kristo; ndio maana maandiko yanasema hivi ‘’Mtu
na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri
za Mungu. 1Kor 4:1.
Na anaposema hivi ‘’Mawakili’’ anamaanisha watetezi, kwa hiyo;
kwa mujibu wa maandiko haya, kazi kubwa ya watumishi wa Mungu,
kwa kizazi hiki cha nyoka, ni kuzifahamu siri za Mungu, kumtetea
Mungu kwa kumuwakilisha na kwa kufunua matendo ya uweza wa
siri za utukufu wake. Kumekuwa na mafundisho ya ajabu sana siku
hizi, watumishi wanawaaminisha watu kuwa! Miujiza ndio njia pekee
ya watu kumjua na kumuami Mungu; hakuna mafundisho ya watu
kumjua Mungu, watu wametegemezwa katika kuombewa, hawajui
kuomba wala kujisimamia kwenye shida zao katika msingi wa imani.
Kwa sababu hiyo, Mungu ametuteua, ili tuwajaze maarifa watu wake

67
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

pamoja na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri


hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba
vitu vyote. Efeso 3:9. Siri hii, hawafunuliwi watu kwa kuomba na
kufunga sana, bali kwa kumtafuta Mungu na kumruhusu Roho wa
Mungu afanye kazi zake ndani yako.
Falsafa ya Mungu inatuonyesha wazi kwamba! Mtu akiwa na Roho
Mtakatifu, hata kama alikuwa dhaifu kiasi gani wa imani, atakuwa
shujaa ghafla; ni kwanini? Ni kwa sababu, yule Roho wa Mungu
anatengeneza ushuhuda ndani ya huyo mtu kupitia maisha yake;
ndivyo tunavyoona kwa Daudi, haikujalisha ana umri gani, lakini kwa
sababu ya ule ushuhuda wake wa kuua simba na dubu na ushuhuda
wa yale matendo ya Mungu kwa Taifa lake, yalimpa nguvu na ujasiri
katika roho yake, hata Daudi akampiga Goriath na kumshinda, lakini
kumbuka! Huyo Goliath aliogopewa na Jeshi na Taifa zima la Israeli.
Maana yake ni nini?
Maana yake ni kwamba; hata paka akiitambua asili ya jamii yake,
anaweza kuwa chui kati ya jamii ya paka wasiojitambua, lakini chui
asiyejitambua asili yake, anaweza kuwa paka kwenye kundi la jamii
ya chui wanaojitambua.Mfano mzuri tumeuona kwa Daudi, yeye
anatuthibitishia kuwa; mwanajeshi dhaifu, ni sawa kabisa na raia
katika uwanja wa vita, lakini raia aliye jasiri, ni mwanajeshi kamili
asiye vitani; na hii ndio roho inayolitesa kanisa.
Kwa hiyo, tunapozungumzia Falsafa za uhai wa Mungu ndani ya Mtu;
tunazungumzia ile hali ya Roho wa Mungu kuishi ndani ya roho ya
mtu na kufanya roho ya mtu huyo kuwa na uhai katika mwili wake.
Imeandikwa ‘’Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya
dhambi; mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu;
mwili wake akauawa, bali roho yake akauhishwa, ambayo kwa hiyo
aliwaendea roho waliokaa kifungoni akawahubiri. 1Petr 3:19
Katika maandiko haya, tunaona jinsi ambavyo Kristo akiwa ameteswa
na kuuawa mwili wake, na sababu ya kuuawa kwa mwili wake, ni ili

68
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

roho yake iachane na mwili ipate kwenda kifungoni (Kuzimu) ambako


huko zimefungwa roho za watu wenye dhambi (Wafu) ili kuzitangazia
uhuru wao (Kuzipatia uhai mpya ndani yake), ili ikiwa zilikufa kwa
sababu ya kujitenga na Mungu (Kutenda Dhambi); yeye Kristo apate
kuzileta kwa Mungu (Katika haki).
Anasema ‘’Mwili wake akauawa, bali roho yake akahuishwa’’kwa
roho hiyo, alipata kuwaendea roho zao waliofungwa kifungoni, yaani
waliyo katika hali ya kufa (Kutokuwa na uzima ndani yao). Sasa Kristo
akiisha kuzihubiria hizo roho; akazitangazia uhuru wa uzima mbali na
mauti. Rum 8:2inasema ‘’Kwa sababu Roho wa sheria ya uzima ule
ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru mbali na sheria ya dhambi na
mauti’’kwa hiyo, japo hizo roho zilikuwa zimekufa, bali sasa zinaishi.
Jaribu kujiuliza! Kwanini zilikuwa haziishi? Jibu ni kwa sababu;
zilipoteza uhalali (Uhai wake) kutokana na kujitenga na Mungu
(Kutenda dhambi), lakini Mungu alipowarudisha kwa Roho wake
katika Kristo Yesu (Kuwahesabia haki) ndipo walipopata uhai mpya.
Math 27:52-53 inasema ‘’Makaburi yakafunuka, ikainuka miili mingi
ya watakatifu waliolala; Nao wakiisha kutoka makaburini mwao,baada
ya kufufuka kwake, wakauingia mji mtakatifu, wakawatokea wengi.

69
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

SURA YA SITA: KUSULIBIWA KWA SHERIA YA MAUTI


MSALABA

Rum 8:3-7imeandikwa
‘’Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu
kwa sababu ya mwili, Mungu kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe
katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi,
aliihukumu dhambi katika mwili; ili maagizo ya torati yatimizwe ndani
yetu sisi, tusionenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya
roho. Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili;
bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya
Mwili ni mauti, bali nia ya roho ni uzima na amani’’.
Tangu mwanzo wa uumbaji, mpango na wazo kuu la Mungu; ni
juu ya watu wake aliowaumba kwa mfano wake, kwa sura yake,
wapate kuishi maisha ya milele na kuitawala dunia milele. Mwa 1:26
‘’Mungu akasema ‘’Na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu;
wakatawale’’ Kwa hiyo mtu huyu aliyeumbwa ili atawale alitakiwa
kuishi milele. Mwa 2:17 ‘’Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema
na mabaya, usile; kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo
utakufa hakika’’ Kwa hiyo, unaona mpango wa Mungu kwa mtu huyo
ni uzima wa milele, ndio maana Bwana aliweka sheria ya uzima ili mtu
atakayeifuata hiyo, aishi kwa hiyo, lakini sheria hiyo ilifanya uadui kati
ya mtu na Mungu kwa kupitia vile viungo vya mwili wa mtu,hata vile
viungo vikafanya vita na ile sheria ya Roho wa uzima, hata imekuwa;
kila anayeishi kwa sheria hiyo, anakufa kwa hiyo sheria. Ndio maana
imeandikwa ‘’Kwa maana Mkiishi kwa sheria mwataka kufa’’
Kwanini sheria iue; wakati iliwekwa kwa ajili ya kuleta uzima? Jibu ni
kwamba! Ile nia ya sheria ya uzima, inapingana na ile sheria ya akili
zetu, na kufanya vita iliyopelekea mtu kuwa mateka wa matendo ya
mwili (Dhambi) hata kuleta mauti, kwa sababu nia ya mwili sio uzima;
bali ni mauti. Ndio maana mwili unapingana na ile sheria ya uzima
ili mwili upate kutekeleza matakwa yake ya kuua, ndio maana mwili

70
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

unaishambulia ile sheria na kumfanya mtu kuwa mbali na ile haki ya


uhai iliyopo katika nia ya roho, inayotokana na ile sheria ambayo ndio
inayomstahirisha mtu kupata ule uzima uliyo katika sheria ya Roho.
Kwa sababu ya ile sheria jinsi ambavyo imeshindwa kabisa kutekeleza
Mpango wa Mungu juu ya kuleta uzimakatika uhai wa mtu, ndipo
Mungu akaiadhibu ile sheria katika agano jipya kwa njia ya mauti
katika mwili msalabani, ili Sasa kutokana na ile nia ya Roho, ambayo
ni uzima; iliyopelekea Mungu kubadilisha mfumo wa namna ya mtu
kuupata uhai ndani ya roho yake kutoka kwa Roho wa Mungu; hivyo
akafanya kwanza upatanisho kwa Neema ili kumuhesabia mtu haki
pasipo matendo ya mtu huyo yatokanayo na ile sheria; bali ni kipawa
na zawadi ya Mungu kwa watu wake kwa njia ya Kristo Yesu, kisha
akaisulubu ile sheria yenyewe katika mwili wake mwenyewe juu ya
mti, ili kwa kufa kwake mwenyewe, aiadhibu sheria iliyoleta mauti
kwa mauti yake katika mti.
Unaweza kujiuliza swali hili
Je! Ile sheria, ilikuwa na hatia gani mbele za Mungu, na kwa kosa gani
hata ikaadhibiwa?
Nisikilize mpendwa! Wala ile Sheria (Torati), haikuwa na kosa lolote
kwa mtu mbele za Mungu. Rum 7:12 inasema ‘’Basi torati ni takatifu,
na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema. Lakini hiyo sheria iliyo
njema, haikuwa njema kwa matokeo ya kazi zake, maana ilileta mauti
kwa walio hai kwa sababu ya kazi zenyewe, ndio maana imeandikwa
kuwa ‘’Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria, lakini ilipokuja ile
amri; dhambi ikahuika, nami nikafa. Rum 7:9. Maana yake ni nini?
Maana yake ni kwamba! Nia ya sheria ni njema; ila mapokeo ya mwili
juu ya ile sheria ni kupingana na sheria na kutenda dhambi, ndipo
dhambi ikaleta mauti.
Kivipi? Ni kwa sababu, torati asili yake ni rohoni; na usisahau kuwa!
Nia ya roho ni uzima na amani, lakini nia ya mwili ni mauti, Ndio
maana utaona kuwa, japo torati ilikuja kuleta uzima, lakini yakatokea

71
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

mauti; Kwa nini? Paulo anasema ‘’Nikaona ile amri iletayo uzima, ya
kuwa kwangu mimi ilileta mauti. Rum 7:10; Sasa swali ni hili! Kwanini
ilileta mauti? Jibu ni kwamba! Ile dhambi iletayo mauti, ilipata nguvu
kwa ile amri (Sheri), ndipo hapo ikaanza kudanganya akili za watu na
kuwaua. Rum 7:11
Kwa hiyo, sheria haina kosa mbele za Mungu; bali upendo wa Mungu
kwa mtu, ndio uliyozidi kuwa mkuu kuliko ile sheria yenyewe. Kwa
maana ikiwa mtu alikufa kwa kosa litokanalo na sheria (Kutenda
dhambi), basi sheria yenyewe ilikuwa adui wa Mungu kwa lile pendo
la Mungu; kwanini? Ni kwa sababu, nia ya Mungu ni uzima kwa watu
wake kwa ile sheria; kwa hiyo ikitokea sheria kuleta mauti, inajenga
uadui kati yake na Mungu; kwa kuwa Mungu hakuweka sheria ili tufe
katika dhambi, bali sheria iliwekwa ili ilete uzima wa mtu mbele za
Mungu kwa haki pasipo dhambi.
Tuseme nini basi, je! Tuendelee kudumu zaidi katika dhambi ili kule
kuadhibiwa kwa ile sheria iletayo mauti kuongezwe katika msalaba?
La hasha! Maana Imeandikwa‘’Kama vile mtu alivyowekewa kufa
mara moja, na baada ya kufa hukumu; kadhalika Kristo naye akiisha
kutolewa sadaka ili azichukue dhambi za wengi, atatokea mara ya pili
pasipo dhambi kwa wale wamtazamiao kwa wokovu’’ Ebr 7:28-29
Kwa hiyo Kristo akiisha kuja katika mwili wa mtu ili kuiadhibu sheria
nakuihukumu mauti ile sheria iliyoleta mauti kwa mauti yake juu ya
msalaba, na kufanya amani; akapaa mbinguni, na amekaa katika kiti
chake cha enzi pamoja na Mungu Baba mbinguni. Akiisha kuliacha
Kanisa takatifu Duniani, Kama ilivyoandikwa ‘’Mtakuwa watakatifu,
kwa kuwa Baba yenu wa Mbinguni ni Mtakatifu’’, yeye aliihukumu ile
sheria, si kwa sababu ile sheria ni mbaya, hapana! Bali tabia za mwili
ndizo zilizoleta matokeo mabaya juu ya uhai wa mtu kwa ile sheria.
Kwa hiyo, Kristo akiisha kubatilisha ile sheria, ili mtu asihesabiwe haki
kwa matendo ya sheria, aliihukumu pamoja na dhambi kwenye mwili
wake ili watu wasitende dhambi tena, bali waokolewe katika dhambi
kwa njia ya mauti yake msalabani.1Petr 2:24 imeandikwa ‘’Yeye

72
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, ili
tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na
kwa kupigwa kwake mliponywa’’
Maana Bwana Mungu hakuiadhibu sheria ili tudumu katika dhambi,
bali aliiadhibu ili tusife katika dhambi zetu. Kwa maana kwa ile sheria
tuliifia dhambi mara moja, kwa ubatizo tulio batizwa katika Kristo
Yesu kwa njia ya mauti yake; basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya
ubatizo huo, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya
utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Kwa maana Kama tulivyounganika naye katika mfano wa mauti yake,
kadhalika tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; tukijua neno
hili, ya kuwa; utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa
dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; kwa kuwa yeye aliyekufa
ametuhesabia haki mbali na dhambi. Rum 6:2-7
Na kisha Bwana akaubadili mfumo wa watu jinsi ya kumuendea yeye
kwenye kiti chake cha enzi nje ya ile sheria; kwanini? Ni kwa sababu ile
sheria ilikuja kutoka rohoni kwa ajili ya mwili wa mtu aliyeumbwa na
Mungu, ili kwa sheria hiyo; huyo mtu apate kusimama na kuenenda
mbele za Bwana kwa ukamilifu. Lakini kwa sababu ya ule udhaifu wa
sheria; Mungu akamuondoa kwenye nafasi yule mtu aliyeumbwa na
Mungu, pamoja na kuiondoa ile sheria yenyewe kisha Bwana akampa
nafasi hiyo mtu mpya, ambaye hatokani na kazi ya Mungu (Kuumbwa),
bali ni mtu yule wa uzao wa Mungu mwenyewe.
Kwa kuwa; kwa lile tukio la Mungu kuiadhibu sheria kwa mwili wake,
wale walioadhibiwa mauti kwa ile sheria, waliachiliwa huru na ile
mauti iliyowapata kwa sheria baada ya sheria yenyewe kuadhibiwa
mauti na Kristo Yesu, maana kwa kufa kwake; amekivunja kiambaza
kilichowekwa kwa sheria na kulipasua pazia zito la hekalu lililokuwa
likipatenga patakatifu pa patakatifu. Akatuzaa mara ya pili kwa Roho
wake katika Kristo Yesu, kwa hiyo sisi sio tena mavumbi, bali ni roho.

73
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Na kwa sababu hiyo, hatuhitaji dalali, au mtu wa kati atakayesimama


ili kutuwakilisha au kutuhudhurisha mbele za Mungu, bali wenyewe
tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu pa patakatifu pasipofanywa kwa
mikono ya mtu kwa damu ya Mauti yake Kristo Yesu. Mpendwa!
haupaswi tena kupelekewa haja zako mbele za Mungu wako na mtu
mwingine, kwa kuwa wewe sasa ni mwana wa Mungu.
Ni mtoto gani anayesoma, unayemfahamu, ambaye akifukuzwa ada
shuleni, anamtuma mwalimu wake akamuombee ada Kwa mzazi wa
mtoto huyo? Haiwezekani hata kidogo! Bali mtoto yeye mwenyewe
ataenda Kwa baba yake na kumweleza hitaji lake. Sasa kwanini wewe
ukatubu kwa mtu na si kwa Mungu aliye Baba yako? Kwanini mtu
akuombee msamaha au msaada kwa Mungu Baba yako wakati unayo
nafasi ya kwenda mwenyewe kutubu au kuhitaji msaada?
Wewe ni mwana wa Mungu, wewe ni roho kwa kuwa Baba yako
aliyekuzaa ni Roho; imeandikwa ‘’Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na
kilichozaliwa kwa Roho ni roho’’ Yoh 3:6. Kwa hiyo hataki uenende
kwa sheria, bali kwa roho. Ndio maana imeandikwa kwamba! Mungu
anawatafuta watu wamwabudu katika roho na kweli” Yoh 4:23!
Yesu alikuwa akizungumza na mwanamke msamaria kisimani, na yule
mwanamke akamwambia Yesu kuwa “Baba zetu waliabudu katika
mlima huu, nanyi mwasema ya kwamba huko Jerusalemu ni mahali
patupasapo kuabudia; Yesu akamwambia yulemwanamke kuwa
‘’Mama unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika
mlima huu, wala kule Jerusalemu, Ninyi mnaabudu msichokijua, sisi
tunaabudu tukijuacho; kwanini? Ni kwa kuwa wokovu watoka kwa
Wayahudi; lakini saa inakuja, nayo sasa ipo ambayo waabuduo halisi
watamwabudu Baba katika Roho na kweli; zingatia (Waabuduo halisi)
kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Mungu ni
roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho
na kweli. Yoh 4:20-24
Katika mazungumzo haya, utaona yule mama ni kama anamwambia
Yesu, niambie ‘’Kunatofauti gani kati ya kuabudu kule kwenye mlima

74
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

walikoabudu baba zetu, na kuabudu huko Jerusalemu kwenu?


Yesu anamwambia ‘’Kule kwenye mlima mnaabudu msichokijua,
lakini kule Jerusalemu tunaabudu tukijuacho’’
Katika majibu ya Yesu, unaona Yesu anapomwambia hivi huyu mama,
“Saa inakuja, na sasa ipo ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima
ule, wala huko Jerusalemu’’hapa ni kama Yesu anamwambia yule
mama kuwa!Ibada sio mapokeo ya baba zenu, wala sio urithi wao kwa
roho zenu. Haijalishi umezaliwa na wazazi wanaoamini nini; swala la
imani ni haki na uhuru wa mtu binafsi kuabudu kile akijuacho, maana
linabeba hatma ya roho zenu. Lakini pia lazima ujue kuwa! Ibada
sio hali ya kuabudu katika eneo fulani, bali ibada ni kumjua yeye
unayemwabudu na namna ya kumwabudu. Na ya kuwa! Ibada za
sheria ni mapokeo tu ya dini zenu, ndio maana mnaabudu lakini hali
yenu kiroho haibadiliki.
Kwa hiyo, kama kweli mnataka kumwabudu Mungu, ni lazima mjue
kuwa! Yeye Mungu haonekani kwa macho ya kawaida maana ni
Roho; lazima kumuabudu katika roho, lakini ninyi mnaenenda kimwili
kuabudu Roho, ndio maana hampati matokeo halisi ya ibada zenu,
mnatimiza sheria za kuabudu tu. Ibada inayofanyika katika roho,
ni ibada inayomuabudu Mungu ambaye ni Roho, ibada hii, aihitaji
mfumo wa namna ya kuabudu; bali Roho mwenyewe ndiye mfumo
wa ibada. Ibada inayosimamiwa na Roho na kufanyika katika roho,
haiendeshwi kwa litrujia.
Na anaposema! ‘’Baba awatafuta watu kama hao watakaomwabudu
katika roho na kweli’’ anamaanisha kuwa; wapo watu wanaoabudu,
lakini hakuna anayeabudu katika roho na kweli, na sio kama hawapo
kabisa, hapana! Wapo, bali hawapo katika dini.

75
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

SURA YA SABA: ROHO UHUISHWA KWA NEEMA

Roho akiisha kufa ndani ya mwili wa mtu kwa sababu ya mtu kuvunja
ile sheria ya Mungu,ndipo hutokea kwa utengano wa nafsi ya Mtu
na Nafsi ya Mungu wakekiroho, kwa kuwa Mungu ni Roho yenye
Nafsi;lakini mtu ni roho na nafsi. Kwa hiyo, uhusiano uliyopo kati ya Mtu
na Mungu katika ulimwengu wa roho, ni matokeo ya kazi ya Roho wa
Mungu kumuunganisha Mungu na mtu katika ulimwengu wa roho;na
kikubwa Roho wa Mungu anachokifanya katika kuwaunganisha, ni
kukutanisha nafsi ya Mungu na roho na nafsi ya Mtu katika roho ya
mtu. Sasa inapotokea nafsi ya mtu ikikosa uhai ndani yake (kutokuwa
na ushirika na Mungu au kufa kiroho), mambo makuu mawili hutokea

1. Hofu ya mauti

2. Kupoteza uwezo wa kutawala


Kivipi..?
Mungualipomuwekea mtu sheriainayosema ‘’Walakini matunda ya
mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa kuwa siku utakapokula
matunda ya mti huo; utakufa hakika’’ hiyo ndio sheria ya uzima.
Siku Adamu alipokulatunda alilokatazwa, mambo matatu yalijitokeza
1. Alijificha kwa sababu ya hofu ya ile dhambi
2. Aliuonea haya uchi wake; yaani alifedheheshwa na ile
dhambi
3. Hakufa siku ile kama Bwana alivyosema, ‘’siku
utakapokula matunda ya mti huo, utakufa hakika’’
Unaweza kujiuliza maswali mengi sana ya msingi, kwanini Adamu
hakufa kama ambavyo aliambiwa akila atakufa? je! Mungu alikuwa
akimdanganya Adamu ili asile tu lile tunda? Au Mungu alitaka kujua
tu kama Adamu ataitii sheria yake? Kama ilikuwa ni kweli, kwamba;
76
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Adamu akila tunda atakufa siku ile hakika, mbona Adamu hakufa siku
ile kama alivyosema Mungu, na aliishi na kuzaa watoto?
Kama unamaswali kama hayo; acha nikusaidie kitu hiki, ni cha msingi
sana kukijua; kitakusaidia.
Mungu alikuwa anamaanisha kabisa kwamba; Adamu atakapokula
tunda hilo atakufa siku hiyo hakika, lakini Adamu alipokula tunda hilo
hakufa siku hiyo, kwanini? Ni kwa sababu Mungu wetu ni mwingi wa
rehema. Ndio maana utaona, Adamu alipojifanyia mavazi ya majani;
Mungu alimfanyia mavazi ya ngozi ya mnyama, swali ni hili; Je! Huyo
mnyama alichunwa ngozi akiwa hai? Hapana! Alichinjwa, je! Mungu
alimchinja mnyama huyo ili tu kumfanyia Adamu mavazi? Hapana!
Mungu alimchinja huyo mnyama ili kutoa sadaka ya upatanisho Kwa
dhambi za Adamu,ili Adamu asife kwa dhambi zake, ndio maana kwa
sadaka ile, Adamu alipata nafasi ya kuendelea kuishi.
Hiyo ndio Pasaka ya kwanza
Mnyama huyu, alikuwa na kazi kuu mbili kwa Adamu
1. Kuhuisha uhai – Uhusiano na Mungu, Adamu alipokula
tunda, kimwili alikuwa hai, ila kiroho alikufa.
2. Kusitiri
Kupewa nafasi ya upendeleo ili kufichiwa udhifu wake
Ndio maana mnyama alikufa ili Adamu aendelee kuishi, na mnyama
alivuliwa nguo zake (Ngozi) ili Adamu apate kuvalishwa na kufichwa
uchi wake; Mungu alifanya hivi makusudi kwa sababu yeye ni pendo,
ingawa Adamu alitenda dhambi, lakini Mungu anampa nafasi ya pili;
ndipo anachinja mnyama kama dhabihu kwa dhambi ya Adamu na
mkewe, ili kwa kufa kwa Yule mnyama, Adamu na mkewe wapate
msamaha wa dhambi zao (Kurudishiwa uhai wa roho ndani yao).
Biblia haituambii moja kwa moja katika agano hilo la kale juu ya jina la
77
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

mnyama huyo, wala kusema ni mnyama wa aina gani.


Lakini kwenye agano jipya, Mungu anaamua kukiweka wazi kizazi hiki
juu ya jina na aina ya mnyama huyo aliyechinjwa pale bustanini edeni
ili kurudisha uhai wa roho ya Adamu, na kumpa Adamu na mkewe
utukufu mpya. Mnyama huyo si mwingine, bali ni Mwanakondoo wa
Mungu, aliyefunuliwa kwa wakati ili aziondoe dhambi za ulimwengu
(Dhambi za asili toka kwa Adamu), ili apate kuleta haki na amani yake
ulimwenguni (Kwa uzao wa Adamu).
Ufun 5:11-13anasema kwamba! ‘’Wakisema kwa sauti kuu, Astahili
Mwanakondoo aliyechinjwa, kuupokea uweza na utajiri na heshima
na nguvu na utukufu na baraka.Na kila kiumbe kilichoko mbinguni na
juu ya nchi na chini ya nchi na juu ya bahari na vitu vyote vilivyomo
ndani yake, nalivisikia vikisema, ‘’Baraka na heshima na utukufu na
uweza, una yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na yeye Mwanakondoo,
hata milele na milele’’Je! Mnyama huyu aliyechinjwa, kwa dhambi za
watu hata akastahili yeye kupokea uweza, na utajiri, heshima, nguvu,
utukufu na Baraka hizi ni mnyama gani? Yoh 1:29 imeandikwa kuwa
‘’Siku ya pili yake amwona Yesu anakuja kwake, akasema; Tazama
Mwanakondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu
Biblia inatuthibitishia kuwa; mnyama huyo aliyechinjwa pale Eden ili
Adamu na mkewe wapate msamaha alikuwa ni Mwanakondoo.
Na Yohana Mbatizaji anasema ‘’Tazama Mwanakondoo wa Mungu”
Hii inamaanisha nini? Maana yake ni kwamba! Mnyama aliyechinjwa
kwa ajili ya anguko la agano la kwanza pale Edeni; ni Mwanakondoo,
namnyama aliyechinjwa kama mjumbe wa agano jipya ni Yesu Krito
ambaye ni Mwanakondoo yule yule aliyechinjwa ili kubatilisha agano
la kwanza, na sasa amechinjwa ili kulisimika agano jipya kwa damu
na Sadaka ya uhai wake. Kwa hiyo yeye ni mjumbe wa agano jipya.
Ambaye zamani zetu, amechinjwa msalabani; akiwa ameangikwa juu
ya mti mahali palipo na mwinuko (Mlima) ili kila mtu apate kumwona
na kumtambua mnyama aliyechinjwa kwa dhambi za watu; ambaye

78
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

katika yeye, sisi tumekombolewa.


Na sababu kuu ya kuchinjwa kwa mwanakondoo huyu, ilikuwa ni
kwa ajili ya kumrudishia (kumnunulia) Mungu watu ambao walijiuza
nafsi zao wenyewe chini ya dhambi, na kushikwa na nguvu za mauti;
ili kwa thamani ya damu ya Mwanakondoo, watu hao wawe mali ya
Mungu. Ufu 5:9 inasema hivi, nao waimba wimbo mpya wakisema,
hivi ‘’Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri
zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu
wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa.
Sikiliza mpendwa wangu; Yesu ndiye huyo Mwanakondoo wa Mungu,
ambaye alichinjwa katika msalaba, ili kwa mauti yake pale msalabani;
awakomboe watu dhidi ya mauti, na kwa lile vazi lake kama ngozi ya
mwanakondoo, ili apate kuwafunika watu utupu wao.
Ndio maana imeandikwa kuwa ‘’Sisi je! Tutapataje kupona, tusipoujali
wokovu mkuu namna hii‘’ Ebr 2:3; Na 1Petr 3:18 anasema ‘’Kwa maana
Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa
ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu;Mwili wake akauawa, bali
roho yake akahuishwa”
Maandiko yanaposema hivi ‘’Yesu alikufa’ haimaanishi kwamba! Yesu
alikufa Kama mwanadamu!Maana yeye hakushikwa na mauti kama
watu, hapana! Bali Yesu aliuacha mwili kwa njia ya mauti ili kwa njia
hiyo, apate kuiendea mauti. Biblia inasema ‘’Lengo kuu la Kristo kuja
ulimwenguni ilikuwa ni kuwakomboa wanadamu dhidi ya mauti, kwa
hiyo, kama angeshikwa na mauti asingeweza kuishinda mauti, maana
angekuwa mtumwa na mateka ya mauti.
Lakini kwa kuwa Kristo hakufa kama mwanadamu, yaanihakushikwa
na nguvu ya mauti, aliiadhibu mauti katika mwili, na kushuka kuzimu
zilipokaa roho zao waliyokuwa wamefungwa, kisha zikatoka roho hizo
katika mwili, na kuonekana zikitalii Jerusalemu kabla ya kwenda zao
Paradiso na Bwana. Imeandikwa ‘’Nitawashindia na nguvu za kaburi;
nitawaokoa na mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi,

79
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ku wapi kuharibu kwako? Kujuta kutafichwa na macho yangu. Hosea


13:14. HataBaada ya hayo ndipo mwanaume Yesu, anaonekana
akitoka kuzimu akiwa na funguo ya mauti na kuzimu, akiwa ameiacha
kuzimu imenyamaza na mauti imedhoofika hata imeandikwa ‘’Ku
wapi ewe mauti kushinda kwako? U wapi ewe mauti uchungu wako?
Kumbuka nilisema kwamba; Uhai wa roho ndani ya mtu, ni ile
hali ya mtu kurudishiwa mahusiano yake ya kiroho kati yake na
Munguwake,mahusiano hayo ndiyo yanayotafsiri uwepo wa uhai
halisi wa roho ya mtu, ndani yake.
Na mahusiano hayo yasipokuwepo, ndipo ule uhai wa mtu unafichwa
ndani ya mauti; kwa sababu hiyo,mtu asipokuwa na uhusiano wa
kiroho na Mungu, mauti inapata nguvu ya kuingia kwa mtu kwa sababu
ya ile dhambi iliyo kwenye nia ya mwilikupelekea mtu huyokuvunja ile
sheria ya uzima, kutokana na mwili kufarakana na Roho wa uzima, na
mtu kuvutwa na dhambi; na mwisho wa dhambi zake ni mauti; ndivyo
ilivyoandikwa, kuwa! ‘’Mshahara wa dhambi ni mauti’’ Rumi 6:23
Kwa hiyo mtu akikosa uhusiano na Mungu, tafsiri yake ni kwamba;
mtu huyo amekufa nafsini mwake, ndio maana Kristo Yesu anasema
‘’Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda ukautangaze
ufalme wa Mungu” Luka 9:60. Maana yake ni kwamba; aliyekufa,
ni mfu kwa sababu ya mwili wake na roho kuachana, lakini pia hao
wanaobeba sanduku la aliyekufa, wao nao pia ni wafukwa sababu ya
dhambi ndani yao ingawa wanaishi,.
Dhambi ni mapatano au makubaliano, yanayofanyika katika dhamiri
ndani ya nafsi ya mtu, kati ya mtu na shetanijuu ya kumuasi Mungu.
Ndio maana Yesu anasemana mtu anayetaka kuwa na uzima ndani
yake kwamba!“Yeye Atakaye kuiponya nafsi yake, aiangamize’’ kwanini
Yesu anatufundisha kuwa, njia kuu ya kuiponya nafsi ni kuiangamiza?
Jibu! Ni Kwamba!Nafsindio kituo cha uhai na uzima wa mtu.Mwa
2:7.‘’Mtu akawa nafsi hai’’ Nafsi ni Akili, hisia na utashi. Kwenye akili,
ndiko kunakofanyika mchakato wa kupembua mawazo, kisha; fikra

80
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

hutumika kutafsiri wazo zuri na baya; lakini hisia zenyewe ni mlango


wa fahamu, zinabeba utambuzi mzuri au mbaya, ambao unaweza
ukazalisha hisia za pendo, na uuaji, chuki, amani, wivu, hasira, upole,
utu wema, N:k. Hii hutegemea na nafsi ya mtu binafsi
Hii hutegemeana na aina ya mguso wa hisia ndani ya nafsi ya mtu. Na
mwisho ni Utashi ambao ni ule msukumo na uwezo wa mtu kufanya
maamuzi, ambao mfumo huu hutegemea kufanya maamuzi kutokana
na matokeo ya akili na hisia katika mawazo. Gal 5:24-25 inasema ‘’Na
hao walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo
yake mabaya na tamaa zake; tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa
Roho.
Kwa hiyo unaona; Yale mawazo ya nafsi, husulibiwa pamoja na mwili
ili nafsi na mwili viangamie pamoja, na vikiisha kuangamizwa, ndipo
mtu hubaki akiwa roho ndani ya mwili. Hawi tena na ile nia ya mwili
(Mauti) kwa kuwa mwili umekufa kwa kule kusulibiwa. Kwa hiyo,
mtu akiisha kuwa roho, hachangamani na mwili, bali huchangamana
na Roho wa Mungu, ndio maana imeandikwa “Tukiishi kwa Roho,
tuenende kwa Roho’’ mtu hawezi kuenenda kwa Roho kama bado
anatawaliwa na mwili, ni sharti mwili usulibiwe pamoja na mawazo
yake mabaya (Nafsi) na hapo ndipo mtu huweza kuenenda kwa Roho
hata kupata ule uzima ambao ndio nia ya Roho
Sasa kwanini ni muhimu kwa mtu kuiangamiza nafsi yake? Jibu! Ni Kwa
sababu, nafsi hushikamana na mwili, na mwili hupingana na Mungu
kwa ile sheria; mwili umenuia kutomtii Mungu, na kwa sababu ya ile
dhamiri ya mwili, hautakaa umtii Mungu kamwe. Rum 8:23, na nia ya
mwili ni mauti. Maana yake ni kwamba! Ukiacha nafsi yako iwe hai
ndani ya mwili wako, itakuangamiza Kwa sababu ya ile dhamira au
nia ya mwili wako; lakini Kama utaiangamiza nafsi ndani yako, roho
itachukua nafasi ndani, na kukupatia nia yake ambayo ni uzima; kwa
maana nia ya Roho ni uzima na amani. Rum 8:6. Ndio maana Yesu
anasema “Atakaye kuiponya nafsi yake, na aiangamize’’
Sasa kutokana nanafsi kushikamana na mwili wa mtu, imepelekea nia

81
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ya nafsi ya mtu kuwa ni mauti, kwanini? Ni kwa sababu nia ya mwili


ni mauti, na nafsi imeshikamana na mwili; unafikiri itakuwa na nia
gani kama sio mauti? Ndio maana shetani huitumianafsi hiyo kama
silaha yake kwaajili ya kumshambulia mtu na Mungu ndani ya mtu,
kwakufanya makubaliano na mtu juu ya kumuasi Mungu;
Na makubaliano haya, yanahusu haswa vitu vikuu viwili

1. Chakula (Neno la Mungu)

2. Ibada (Nani wa kuabudiwa?)


Katika kitabu cha Mwa 2:17 Mungu anamwambia Adamu kwamba!
‘’Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile; kwa
maana siku utakapokula matunda ya mti huo, utakufa hakika.Na
Yesu Kristo akiwa amefunga kule jangwani kwa kuongozwa na Roho
Mtakatifu, shetani alimfuata na kumwambia ‘’ikiwa ndiwe mwana wa
Mungu, amuru jiwe hili liwe mkate; Yesu akajibu, Mtu hataishi kwa
mkate tu, bali kwa kila Neno litokalo kinywani mwa Mungu’ Math 4:4
Kwanini nakuonyesha mambo haya! Ni ili upate kujua kuwa; mara
zote shetani anapotafuta nafasi ndani ya mtu ili akae yeye badala ya
Mungu, huanza kwa Neno la Mungu (Chakula). Kwa sababu anajua;
mtu bila Neno la Mungu (Chakula) hana uzima ndani yake, lakini
kwenye chakula (Kwenye Neno), kuna sheria; soma tena Mwa 2:17
Kwa hiyo anachokifanya shetani siku zote, ni kutuonyesha kuwa, ile
sheria ya Mungu yenye uzima katika kula (Katika neno lake), imebeba
dhamira mbaya ya Mungu juu yetu.Mwa 3:1b
Shetani anasema ‘’Ati’ Hivi ndivyo alivyosema Mungu, msile matunda
ya miti yote ya bustani?’’Mara zote, ukisikia neno ‘’Ati’’ ujue kuwa
linawakilisha lugha ya mashaka, na mara nyingi lugha hii, inatumika
na mtu anayetaka kukupa taarifa za uongo au anayetaka kubatilisha
taarifa ulizowahi kusikia kabla ya taarifa yake. Ukisoma Mwa 3:4-5
utagundua ile ‘’Ati’’ ya shetani ina maana gani. Anasema hivi ‘’Hakika

82
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakapokula


matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama
Mungu mkijua mema na mabaya’’
Je! Unafikri ilikuwa ni nia ya kweli ya shetani kwamba mtu awe kama
Mungu? Hapana! Shetani hakuwa na nia hiyo hata kidogo. Ila lengo
lake lilikuwa ni kumgombanisha mtu na Mungu wake, kwa kumfanya
Mungu aonekane mbaya, ili yeye shetani apate kuchukua nafasi ya
Mungu ndani ya moyo wa mtu.
Ni kama ambavyo leo shetani anavyowadanganya watu kwa maneno
ya uongo, utasikia mtu anasema kuwa ‘’Imeandikwa jisaidie nami
nitakusaidia’’ unafikiri hilo ni neno la Mungu kweli? Hapana! Mungu
ahitaji msaada wako ili yeye afanye kile unachoomba kwake, zaidi
tu ya wewe kumwamini yeye. Lakini shetani ameleta msemo huu
kwa makusudi ili kuhalalisha uchawi, uganga na ushirikina ndani
ya mioyo ya watu; ndio maana kuna watu hawafanyi biashara bila
kuloga, na watu wengine wanabatiza watoto wakiwa wamewavalisha
hirizi mikononi au viunoni. Watuwanatapeli,wanazini ili wapate
kusaidiwa gharama za maisha. Na ukiwauliza sababu za wao kufanya
hivyowatakwambia ‘’Imeandikwa, jisaidie nami nitakusaidia’’ sasa
jaribu kuwaambia wakupe hilo andiko linapatikana wapi; hapo ndipo
utakapogundua kuwa; akili za watu zimetiwa giza ili watu wasipate
kumtii na kumpendeza Mungu.
Imeandikwa ‘’Ambao akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na
uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu
ya ugumu wa mioyo yao. Ef 4:18
Mungu anasema ‘’Usile’’ shetani anasema ‘’Kula’’ unaweza kudhani
kuwa shetani ni mwema kuliko Mungu, lakini dhamira yake ni mbaya
kuliko tunavyoweza kufikiri, na shetani anafanya hivi kwa makusudi,
lengo lake likiwa ni kutaka watu wamuasi Mungu wao kwa kula
chakula (Kutumia neno la Mungu) kinyume na maagizo ya Mungu
mwenyewe ili wafarakanishwe na Mungu wao, apate kuwafanya watu
hao kuwa mateka wake na kuichukua ile nafasi ya Mungu ndani ya

83
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

mioyo ya watu.Kwanini anafanya hivyo? Ni ili yeye apate kuabudiwa


kama mungu; ndicho anachotafuta.
Ukisoma Math 4:5 anasema ‘’Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima
mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
akamwambia; Haya yote nitakupa, ukianguka na kunisujudia’’. Kwa
hiyo mpango mkuu wa shetani, ni kupata nafasi ya kuabudiwa na
mwanadamu kwa nafasi ya Mungu. Usisahau hili nililokwambia kuwa
shetani aliwahi kuwa malaika mkuu mbinguni, lakini alilaaniwa na
kuwa shetani kutokana na kiu yake ya uasi akitaka kuwa mungu, hiyo
kampeni bado anayo; usisahau.
Kwa hiyo, lengo kuu la shetani sasa kwa watu, ni kutaka kumfanya
Mungu aonekane na watu kuwa ni muongo; ndivyo hata alivyofanya
kwa Adamu, alimwambia ‘’Mungu muongo, anajua siku mtakapokula
tunda la mti huo wa ujuzi wa mema na mabaya, hapo mtafumbuliwa
macho yenu, nanyi sasa mtakuwa kama Mungu kwa kujua mema na
mabaya”. Na leo anajaribu kumshawishi Yesu Kristo ili Yesu amuone
Mungu kuwa ni mwongo, na anamshawishi kwa neno la Mungu lile
lile (Chakula).
Ndio maana anasema kwamba! ‘’Ikiwa ndiwe Mwana wa Mungu”
maana yake ni kwamba; shetani anajua kuwa imeandikwa ‘’Ndiwe
mwanangu mimi leo nimekuzaa’’ Shetani alipoona hakufanikiwa kwa
chakula, alimshawishi Yesu kwa mali, na kumtaka Kristo amwabudu
shetani ili shetani ampe mali hizo Kristo.
Huu ni mfumo ule ule anaoutumia shetani hata leo, amewadanganya
watu wengi kwa mali zake na kuwakosesha mbele za Mungu wao. Na
dhumuni lake ni kutaka kuteka ibada za watu ndani ya mioyo yao juu
ya Mungu
Na watu bila kujali au bila kujua, wameendelea kumwabudu shetani
kwa dhamira zao ili wapate mali, na wengine wanamuabudu shetani
wakidhani wanamuabudu Mungu kwa kukosa maarifa. Ndio maana
Mungu anasema hivi ‘’Ole wa watoto waasi, asema Bwana, watakao

84
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

mashauri lakini hawayataki kwangu mimi, wajifunikao kifuniko lakini


si cha roho yangu, wapate kuongeza dhambi juu ya dhambi’’ Hapa
Mungu anazungumza na watu wale ambao wanamwabudu shetani,
wakidhani wanamwabudu Mungu
Kumbuka; hiki anachozungumza Mungu hapa, ndio kile kilichotokea
kwa Adamu alipokataa mashauri ya Mungu yasemayo “Usile” yeye
akala; na hata baada ya kula na uchi wake kufunuliwa mbele za macho
yake, bado Adamu alitafuta namna nyingine ya kujifunika uchi wake
kwa kujifanyia mavazi ya majani ya mti, wala hakutafuta uhusiano wa
kiroho na Roho wa Mungu, na sababu kuu ya kutenda hayo ni uasi;
ndivyo Mungu asemavyo ‘’Ole wa watoto waasi’’ Kumbe kutokuwa na
ushirika na Mungu, na kukosa uwepo wa Roho wake, ni uasi.
Mungu apozungumzia habari ya mashauri, anamaanisha kuwepo kwa
mahusiano kati yake na mtu; sababu hauwezi kushauriana na yeye
usiye na mahusiano naye. Sasa ni kwanini watoto hawa wanatafuta
kifuniko? (Heshima). Jibu ni kwamba! Wapo uchi (Wamebeba aibu);
kwanini? Ni kwa sababu wametenda dhambi, ndio maana Mungu
anawaita watoto waasi. Kwa kuwa imeandikwa, ‘’Dhambi ni uasi’’.
Shida ya Mungu sio wao kuwa uchi, bali ni jinsi wao wanavyotafuta
kifuniko mbali na kifuniko cha Mungu (Roho wa Mungu). Jambo hili
ndilo lililomtoa Adamu kwenye nafasi yake pale alipokataa mashauri
ya Mungu, na kuamua kula tunda (Kutenda dhambi), baada ya Adamu
kutenda dhambi (kula tunda) kile kifuniko cha Roho wa Mungu
kiliondolewa na Utukufu ukaondoka; ndipo Adamu akajificha (kukataa
kutubu) kwa kuwa alikuwa uchi (bila utukufu), kwa sababu dhambi
inamtenga mtu na Mungu, ndio maana alipogundua kuwa yupo uchi
(Ametenda dhambi) alijifanyia mavazi ya majani, kifuniko kisicho cha
Mungu, na hatimaye alikufa.
Kadhalika kizazi hiki, baada ya kumtenda Mungu dhambi; tulikufa kwa
sababu ya ile nguvu ya dhambi (mauti), iliyomo ndani yetu. Tulipoteza
tumaini la uzima, na tukawa mateka wa mauti na kuzimu, kwa sababu
ya kushindwa kuitii ile sheria ya Mungu ya uzima iliyoandikwa ndani

85
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

yetu ili tuishi katika hiyo. Lakini baada ya sisi nasi kushindwa kuitii
ile sheria, ambayo ilikuwa ikitutawala ili tuishi katika hiyo, ndipo
tulipokufa; na mtu akiisha kufa, ahitaji tena sheria ili kuwa hai, kwa
sababu biblia inasema sheria kazi yake ni kumtawala mtu akiwa hai,
sheria haina nguvu ya kumtoa mtu katika mauti na kumpa uzima; kwa
hiyo ili mtu awe mzima, anahitaji nguvu nyingine itakayomuhuishia
uhai wake. Rumi 7:1
Na nguvu hiyo, ni mpango wa Mungu aliyokwisha kuuandaa tangu
anguko la mtu wa kwanza (Adamu) pale edeni, Mpangowenyewe ni
juu yayale mawazo ambayo Mungu anatuwazia kama anavyosema,
‘’Nayajua mawazo ninayo wawazia ninyi’’ mawazo hayo yamebeba
amani, na matumaini ya kukufuliwa kwetu (kuhuishwa kwa uhai
wa roho ndani yetu na kupata tena uzima udumuo). Yer 29:11; Bila
mpango huo wa Mungu, hakuna mtu anaweza kuwa na amani ya
kuishi (kuwa na uhusiano na Mungu) wala kuwa na matumaini ya uhai
ndani yake (Uhuru wa kiroho).
Mpango huo wa Mungu, umebeba nguvu yenye uweza wa kuiadhibu
mauti, ili kuwaachalia huru wale walio ndani ya tumbo la mauti
(kuwafufua waliyo katika mauti). Ndipo Mungu aliposema ‘’Nitaweka
uadui kati yako na huyo mwanamke na kati ya uzao wako na uzao
wake, huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.
Naomba rejea neno hili ‘’uadui kati ya uzao wako na uzao wake’’
hapa Mungu anazungumzia juu ya kuweka uadui huo kati ya uzao
wa shetani, na uzao wa mwanamke. Jambo la msingi la kutazama, ni
kwanini uadui huo usiwe kati ya uzao wa Adamu na uzao wa nyoka,
na badala yake Mungu anaweka uadui kati ya uzao wa nyoka na uzao
wa mwanamke?
Ngoja nikwambie,anguko la Adamu pale edeni, lilianzisha vita vya
kiroho dhidi ya utawala wa mwili (Adamu), kwa hiyo;kwa kuwa Adamu
ni mtu mwenye asili ya duniani, yaani asili yake ya mwili ni udongo,
hivyo katika vita hivi asingeweza kumshinda shetani kabisa, na hivyo;
ingesababisha mpango wa Mungu wa kumuumba mtu, kushindwa

86
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

kifikia kiwango chake cha mafanikio.


Ndio maana unaona, Mungu mwenyewe anaamua kuingilia kati vita
hivi, na kuja kufanya vita dhidi ya shetani katika mwili wa mtu. Na ili
Mungu aje kufanya vita hivi vya kiroho katika mwili, ilibidi na yeye
aje katika mwili, hivyo; ndio maana Mungu hakuhitaji mbegu ya mtu
inayobeba uharibifu ili itumike katika ujio wake, ndipo akaamua kuja
kwa mbegu yake mwenyewe isiyo na uharibifu.Ndio utaona, Mungu
akishuka katika tumbo la Mariamu
Maandiko yanasema, ‘’Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa
na dhambi zenu, ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya
ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho
Yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi. Efeso 2:1-2.
Anaposema mlikuwa wafu, anamaanisha kuwa; hao anaozungumza
nao ni watu walio hai kwa sasa, lakini hapo kabla; walikuwa wafu, na
kilichowaua ni makosa na dhambi zao. Nini chanzo cha wao kutenda
dhambi? Maandiko yanatuambia, sababu za dhambi zao, ni matokeo
ya kufuata kawaida ya ulimwengu huu, na kawaida za ulimwengu huu
ni matendo ya tamaa ya mwili, na chanzo cha tamaa hizo ni kumfuata
mfalme wa uwezo wa anga (lusifa/shetani).
USHINDI WA VITA VYA KIROHO DHIDI YA UHAI WA MTU

Maandiko matakatifu yanatuambia kuwa; mpango wa Mungu juu ya


watu wake, ni watu hao kuishi maisha ya milele (kutokuwa na ukomo
wa muda wa uhai, lakini shetani kwa vile anafahamu thamani ya kazi
ya uhai ndani ya mtu, na anajua thamani ya maisha haya ya milele,
amekusudia kuhakikisha anawatoa watu hao katika nafasi hiyo yenye
kusudi la Mungu kwa kuanzisha vita vya kiroho katika mwili kwa njia
ya kuwashawishi kutenda dhambi na kuwashinda. Hivyo watu hao
wakapoteza nafasi yao mbele za Mungu ya kuwa na uhai usio na
kikomo (maisha ya milele) ndani yao.

87
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Lakini siku zote mpango wa Mungu haupingwi, wala mawazo yake


hayabatilishwi kamwe, ndio maana; japo watu wametenda dhambi
na kujiondoa kwenye lile kusudi la Mungu alilotaka watu wake waishi
milele; bado Mungu amelirudisha wazo hilo kwa watu, ingawa hapo
kwanza ilikuwa ni mpango wa lazima kwa kila mtu kuwa na uzima huo
wa milele, bali sasa ni kwa njia ya ridhaa ya mtu mwenyewe kuchagua
kuwa na huo uzima. Kwa kuwa shetani alianzisha vita ulimwenguni,
dhidi ya watu wa Mungu na kuwashinda, ndipo Mungu akaamua
kuingilia kati vita hivyo vilivyokuwa kati ya shetani na watu; hata
anasema ‘’Vita ni juu yangu mimi asema Bwana’’
Unaweza kujiuliza, kwanini Mungu anataka watu wasijihusishe na
vita hivyo, na badala yake yeye kupigana vita kinyume cha adui yetu
shetani? Ni kwa sababu hakuna mtu anayeweza kupigana vita hivi na
kushinda kwa uwezo wake (Kujiokoa), kwa kuwa kila mtu tayari yupo
kwenye himaya na mamlaka ya adui shetani.
Maana walishachukuliwa mateka kutokana na wao kukosa maarifa ya
kivita. Isaya 5:13, anasema kwamba! ‘’Watu wangu wamechukuliwa
mateka kwa kukosa kuwa na maarifa’’ hivyo kitu pekee ambacho
mwanadamu amekosa katika vita hivi, ni maarifa, kwa hiyo mtu yeyote
asijisumbue kwa jambo lolote juu ya vita hivi vya ukombozi wa uhai na
uzima wa milele akidhani atashinda, bali kwa kila jambo tunapaswa
kumkabidhi Bwana wa Majeshi, Mkuu wa Vita vyetu, maana bila yeye
sisi hatuwezi neno lolote.
Wanafunzi wa Bwana Yesu walipoona kuna ugumu wa kuokoka,
wakamuuliza Yesu wakisema ‘’Ni nani basi awezaye kuokoka’’ NaYesu
akawajibu wazi na kusema‘’Kwa wanadamu hilo haliwezekani, bali
kwa Mungu yote yanawezekana’’ Math 19:25-26.
Majibu haya ya Bwana Yesu, yanatupa tafsiri panazaidi; ni kama Yesu
anasema kuwa ‘’kila mtu anayetaka kuokoka (Kurudisha uhusiano
wake na Mungu) ni lazima ajue wazi kuwa, hakuna jambo lolote
awezalo kulifanya ili kuokoka; zaidi ya kujikabidhi maisha yake kwa
Mungu mwenyewe anayeokoa’’. Kwa kuwa kila mtu ni mateka wa

88
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

matendo ya dhambi, hivyo; hakuna mtu aliye huru. Nyote mmetekwa


na kuhamishwa; kwa hiyo, vita hivi vya kiroho hamwezi kushinda.’’
Kwa maana hakuna mtu anayepigana vita kutokea kwenye kambi ya
adui yakekwenda Kwa mtu kupitia njia ya imani yake, bali huanzia
vita kwa mtu mwenyewe, na kwenda kwa adui kwa njia ya imani,
hapo ndipo ushindi utapatikana. Lakini sasa kwa kuwa watu wote
wameshachukuliwa mateka, ni dhahiri kuwa; maisha yao kwa sasa
yapo kwenye himaya ya adui yao, hivyo ni wazi kuwa, wakitaka
kupigana vita, ni lazima wataanzia kwa adui; kitu ambacho ni rahisi
wao kudhibitiwa na kuongezewa adhabu.
Hii ndio maana ya Yesu kusema,‘’hakuna mwanadamu anayeweza
kujikomboa’’ kwanini? Ni kwa kuwa hakuna mtu yeyote aliye huru, kila
mtu anamuhitaji yeye aliye huru ambaye anaweza kuwaweka watu
wake huru kweli (Yesu Kristo), na tumuachie vita vyetu ili atukomboe,
sisi kazi yetu ni kumwamini tu. Kwa kuwa Kristo ni Mungu aliyekuja
katika mwili ili kutusaidia udhaifu wetu dhidi ya vita hivi, ni hakika
katika yeye ushindi wetu upo.
Maana vita hivi si vya kimwili, bali ni vya kiroho katika mwili. Efeso
6:12, inasema ‘’Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na
nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili,
juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa hiyo
utaona katika vita hivi, shetani amejigawa katika sehemu kuu nne
muhimu kuhakikisha anashinda vita, sehemu hizo ni kama zifuatavyo:

1. Falme

2. Mamlaka

3. Wakuu wa giza

4. Majeshi ya pepo wabaya

89
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Anapozungumzia juu ya falme, anamaanisha kuwa; katika vita hivi


vya ukombozi wa kiroho, (Kurejesha husiano wa mtu na Mungu),
tunapambana dhidi ya serikali ya kifalme kamili, ambayo imejitwalia
nafasi hiyo kutokea kwenye anguko la Adamu, na serikali hii, makao
yake ni kuzimu. Hivyo silaha zao za vita zinatoka kuzimu, ambazo ni
nguvu ya mauti (Dhambi). Na Silaha hizi za kuzimu, ni zile nguvu,
zinaoshinikiza viungo vya miili yetu, kutumika kwa matumizi mabayaili
vipate kushambulia nafsi na roho zetu katika dhambi.
Imeandikwa; ‘’Nasema kwa jinsi ya kibinadamu, kwa udhaifu wa miili
yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu
na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe
na haki mpate kutakaswa’’. Mungu Anaposema hivi, anamaanisha
nini? Anamaanisha kwamba; serikali ya kuzimu, imetumia viungo
vyetu sisi wenyewe kutushambulia kwa njia ya kumuasi Mungu hata
tukapata mauti. Sasa Mungu anataka kutuponya, ila; njia pekee ya
kuponywa na Mungu (Kuhuishwa kwa uhai wa roho ndani yetu), ni
sisi kubadili mfumo wa matumizi ya viungo vyetu, ambavyo kwanza
vilitumika na kuzimu kwa njia ya uasi, sasa vitumike na mbingu kwa
njia ya haki, ili katika hiyo, tutakaswe na ule uchafu (Dhambi) hata
tuponyoke kwenye mauti na kufufuliwa kwa roho zetu
Kwa hiyo, silaha za kuzimu, ni nguvu inayoshikiniza viungo vya miili
yetu sisi wenyewe kutushambulia; kwa kutumika kutenda mambo ya
mwilini (Dhambi) ili kutekeleza kwetu adhimaya serikali hiyo ovu ya
kuzimu (Mauti), na matendo ya mwili ni dhahiri ndio haya: uasherati,
ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina,
faraka, huzushi, husuda,ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na
hayo, katika hayo nawaambia mapema ndugu, kama nilivyokwisha
kuwaambia, ya kwamba; watu watendao mambo ya jinsi hiyo
hawataurithi ufalme wa Mungu (Kuupata uzima wa milele)Galatia
5:19-21.
Kwa hiyo, tukitaka kutakaswa (kusamehewa dhambi zetu au kuwa
watakatifu), ili tupate nafasi ya kujiudhurisha mbele za Mungu na
kumkabidhi Bwana njia zetu, ni lazima tuvitoe viungo vyetu vitumiwe
90
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

na haki. Yaani, tufanye yale yanayostahili kufanywa kwa mujibu wa


Mungu wetu.
Lakini hatupaswi kuishia hapo (yaani kutoa tu viungo vyetu
vitumiwe na haki), kwa sababu anatuambia kuwa; ‘’tunashindana
na mamlaka’’‘’Mamlaka’’ ni wasimamizi ambao wamepewa nafasi
na serikali yao ya kuzimu ili kusimamia utekelezaji wa matumizi ya
viungo vyetu kwa ajili ya uasi.
Ndio maana, kuna wakati unaweza kujikuta uhitaji kwenda sehemu
yeyote, unajisikia kukaa nyumbani tu; lakini ghafla, mtu anakupigia
simu na kukualika sehemu ambapo ukifika huko, kuna namna yeyote
itakupelekea kufanya jambo ambalo katika hilo, utamkosea Mungu.
Ukiona hayo yametokea, ujue wazi kuwa; Yule mtu aliyekuita hakuwa
Yule unayemtambua; bali kuna roho ya kipepo iliyomtumia huyo mtu
ili kuhakikisha unatumia viungo vyako kama silaha ya kujiangamiza
wewe mwenyewe.
Lakini, katika vita hivi; tunapambana pia na wakuu wa giza.
Anapotaja juu ya wakuu wa giza, anatusaidia kujua kuwa, kuna aina
nyingine ya jeshi la serikali ya ufalme wa kuzimu, na kazi kuu ya jeshi
hilo ni kutia giza (kupofusha akili za watu). Efeso 4:18 imeandikwa
‘’Ambao akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa
Mungu kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu
wa mioyo yao’’.
Ndio maana Yesu anasema kuwa ‘’Mimi ni nuru ya ulimwengu’’ swali
la kujiuliza, ni kwamba; kwanini ilikuwa ni lazima Yesu aje kama nuru
ya ulimwengu? Ni Kwa sababu ulimwengu ulikuwa katika Giza. Ndio
maana imeandikwa ‘’Ondoka uangaze, Kwa kuwa nuru yako imekuja,
na utukufu wa Bwana umekuzukia’’ Isaya 60:1
Anaposema ondoka uangaze, anamaanisha huyo anayeambiwa, ni
mtu aliyejificha katika vita kwa hofu ya adui, akishindwa kuendelea
na vita kutokana na lile giza (Kukosa maarifa), lakini akiisha kuja huyo

91
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

nuru (Yesu Kristo), na kumwangazia huyo mtu (kupata maarifa), ndipo


huyo mtu anatakiwa kusimama ili aende akaangaze (kuondoa giza
kwenye fikra za wengine).
Shetani ametupotosha fikra zetu, ili tukose kuwa na maarifa ya kivita
ili apate kutushinda; ndio maana utaona, yeye anapigana nasi kiroho
kwa kuwa vita hivi ni vya kiroho, ila sisi tunapigana naye kimwili kwa
kuwa hatujui kuwa vita hivi si vya kimwili. Ndio maana Mungu kwa
kuliona hilo, na kwa wingi wa pendo lake kuu, akaja kwetu kama
Roho katika mwili, ili kupitia Roho wake, afanye vita vya kiroho na
shetani katika mwiliili apate kutuletea uhuru katika yeye. 2Gal 3:17
imeandikwa ‘’Basi Bwana ndiye Roho; walakini palipo na Roho wa
Bwana, hapo ndipo palipo na uhuru’’ kwa maana imeandikwa ‘’japo
tunaenenda kimwili, lakini hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili. 2Kor 10:3
Na hata japo Mungu mwenyewe, naye amekuja kwetu katika mwili,
lakini hafanyi vita kimwili
Na kazi kuu ya wakuu wa giza (Jeshi la kuzimu), ni kutufanya sisi kuwa
vipofu ili tushindwe kumuona Mungu aliyekuja kwetu katika mwili.
2Kor 11:3 ‘’Lakini nachelea; Kama Yule nyoka alivyomdanganya Hawa
Kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na
usafi kwa Kristo’’.
Kwa hiyo, kazi kuu ya shetani na jeshi lake, ni kutudanganya (kutia
giza fikira zetu) ili tusitambue kuwa Mungu ameshakuja kwetu katika
mwili ili kutusaidia katika vita vyetu. Ndiomaana imeandikwa, kila
roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili, yatokana na
Mungu. 1Yoh 4:3
Maandiko yaanaposema; ‘’kila roho ikiriyo kwamba Kristo amekuja
katika mwili’’, anamaanisha kuwa, huo mwili wenyewe sio Kristo, bali
Kristo mwenyewe amekuja kwetu katika mwili, mwili ulitumika kama
sehemu ya njia ya Kristo kuja duniani.
Kwanini mwili sio Kristo? Ni kwa sababu, Biblia inasema kuwa, ‘’Bikira
Atatwaa mimba, naye atazaa mwana mwanamume, nao watamwita

92
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

jina lake Emanuel; Mungu pamoja na wanadamu’’. Sasa ukumbuke


kuwa; Mtu ni roho, nafsi na mwili; lakini Mungu ni Roho yenye nafsi.
Kwa hiyo; Mpango wa Mungu ni kuja kuwa pamoja na wanadamu
(Watu), maana yake, tunazungumzia ujio wa Roho na Nafsi ya
Mungu kukaa na watu, lakini ukumbuke kuwa; watu ni roho, nafsi na
mwili; sasa ilibidi Mungu naye, japo ni Roho na Nafsi, achukue mwili
ili aweze kukaa na watu. Kwa hiyo, tafsiri ya Emanuel ni “Roho na
Nafsi ya Mungu iliyokuja kwa njia ya mwanamke bila mbegu ya mtu
(Mwanaume), akatwaa mwili kama mtu ili apate kukaa na watu’’
Kama hivyo ndivyo, Kristo ni nani basi? Jibu ni hili; Kristo ni Mungu,Yaani;
Roho na Nafsi iliyotwaa mwili; anayeishi pamoja nasi yaani pamoja
na wanadamu, Math 1:23. Kwa hiyo bikira ameshachukua mimba
tayari (Mariamu), na tayari amekwisha kumzaa mwana, (Yesu
Kristo). Filipi 2:6-11 anasema ‘’Ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna
namna ya Mungu, naye hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa
ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana utukufu,
akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena
alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa
mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Tena Mungu akamwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila
jina; ili kwa jina la Yesu Kristo kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na
vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa Yesu Kristo
ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba’’.
Maneno hayo, ni dhahirisasa kuwa; Munguameishakujifunua kwetu
katika mwili wa Kristo; na tayari yupo pamoja nasi.
Kuzaliwa kwa Kristo ni Mpango kamili wa Mungu ulioandaliwa tangu
mwanzo wa anguko pale edeni, Mungu aliposema ‘’Nitaweka uadui
kati yako na huyo mwanamke na kati ya uzao wako na uzao wake’’
Mwa 3:15. Na Kama tunavyoona wazi kuwa, mpango huu wa Mungu
wenye msingi wa ukombozi wa watu; haukuwekwa na Mungu dhidi
ya mwanaume na nyoka (shetani), kwanini? Ni kwa sababu, huo
uzao wenye agano la kuangamiza utawala wa nyoka (shetani) kwa

93
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kumponda nyoka kichwa, sio uzao wa kibinadamu; bali ni Mungu


mwenyewe anayekuja kwetu katika mwili wenye mfano wa mtu, ndio
maana Mungu anasema ‘’vita ni juu yangu mimi asema Bwana’’ kwa
kuwa vita ni vya Mungu, na kwa kuwa vita hivi ni vya kiroho katika
mwili, ilibidi Mungu aliye Roho, aje katika mwili (Kristo).
Kwa hiyo, uzao huu ni mpango mkakati wa Mungu kufanya vita na
shetani kinyume chetu ili kutuokoa; na kama Mungu anavyosema vita
ni vya kwake, hivyo; imempasa yeye mwenyewe kuwa katika mwili
usiyoharibika, ndio maana hakuhitaji mbegu ya mwanaume, bali
alikuja kwa mbegu yake mwenyewe (Roho mtakatifu) na kuhitaji yai
la Mwanamke ili katika yai hilo, yeye achukue mwili na kukaa kwetu.
Hii ni sayansi ya kawaida kabisa, jaribu kufikiri kwa hivi; Je! Unaweza
kuchukua yai la mwanamke na kulipandikiza kwenye mfumo wa uzazi
wa mwanaume na mwanaume akazaa mtoto? Haiwezekani kabisa, ili
huyo mwanaume azae, ni lazima abadilishiwe mfumo wake wa uzazi
na kuwekewa mfumo wa mwanamke.Lakini mwanamke, anaweza
kuwekewa mbegu za kiume kwenye mfumo wake wa uzazi; na bila
kujalisha ni mbegu za mwanaume wa aina ya kiumbe gani, lakini uwe
na uhakika kabisa kuwa; hiyo mbegu itazaliwa kiumbe kamili.
Sasa unisikilize nikuelekeze Sayansi hii ya Mungu; itakusaidia
Katika mfumo wa uumbaji, asili ya mwanamke ni mwanaume kamili,
Biblia inatuambia kuwa; Mwanamke ametokanana Mifupa na nyama
za mwanaume; kwa hiyo; mwanamke ni mwili wa Mwanaume; lakini
kiuhalisia kabisa, kwenye mwili wa Mwanaume, hakuna miili ndani,
bali kwa Mwanamke ndiko kuliko na miili. Kwanini? Mfumo wa uzazi
kimaumbile, haujamruhusu huyu mwanaume kubeba miili ya watu
tumboni mwake, ndio maana hata Mwanamke mwenyewe hakutoka
kwenye Mfumo wa uzazi wa Mwanaume, bali ametokana na Nyama
na Mifupa ya Mwanaume. Kiumbe pekee kilichobeba miili ndani ya
mwili wake, ni mwanamke tu; ndio maana, Maria aliweza kuwekewa
mbegu na kuzaa bila mwanaume, lakini Yusuph angewekewa yeye ile
mbegu, ingeharibika bila mtoto kuzaliwa. Amini ninachokwambia

94
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Huu ni mfumo wa kimaumbile kabisa, na wote tunakubaliana nao.


Kwa sababu Mungu alimuumba mwanamke kutokana na upweke
wa mwanaume; ndio maana Mungu ili kutolifanya zoezi hili kuwa
endelevu; akamuumba mwanamke akiwa na miili ya wanaume na
wanawake ndani yake, ili mwanaume apate kuitoa hiyo miili kwa
mwanamke kupitia asili yake (Mbegu) ili kwa mbegu hizo na miili
hiyo; wapate kuongeza idadi ya watu duniani. Ndio maana baada
ya kuumbwa mwanamke, ndipo Mungu anawabariki na kuwaambia
wakazae.
Sasa alichokifanya Mungu ili yeye apate kuja duniani katika mwili,
alihitaji kuweka mbegu yake (Roho Mtakatifu), kwenye mfumo wa
Mwanamke, lakini kwa sababu mwanadamu ni baridi, (Udongo) ilibidi
Mungu mwenyewe aiatamie mbegu yake.
Ndivyo alivyosema Gabriel ‘’Roho Mtakatifu atakujilia, na nguvu zake
aliye juu zitakufunika kama kivuli’’. Hapo anaposema ‘’Zitakufunika’’
hamaanishi kufunika Kama kwa shuka, bali kuatamia, yaani kama vile
kuku aatamiavyo mayai yake, au anavyovifunika vifaranga vyake chini
ya Mbawa zake.Kwanini ilibidi Mungu aatamie ile mbegu aliyoiweka
kwa mwanamke? Ni kwa sababu, mwanamke hakuwa na uwezo wa
kupandishahali ya joto la mwili wake hadi kufikia kile kiasi cha nyuzi
joto zinazohitajika kwa ukuaji wa mtoto tumboni kutokana na asili
ya mbegu yenyewe; maana Mungu ni moto. Kwa hiyo ndugu; usiwe
na mashaka na huu Uungu wa Yesu, Mungu ametumia sayansi ya
kawaida kabisa ili yeye apate kuja duniani. Uwe na hakika kuwa; Yesu
ni Mungu
Sasa Mungu amekuja katika mwili (Yesu Kristo) ili mtu apate kupokea
msaada wa Mungu katika vita hivi vya wokovu, sasa ili mtu apate
msaada huu, ni lazima mtu huyo amkaribishe Mungu moyoni mwake,
kwa kuwa tayari Mungu angaliko ulimwenguni, lakini si ulimwengu
mzima unaohitaji uwepo wake. Yoh 3:16. Ni lazima binafsi uamue
kuhitaji msaada wa huyo Mungu, yeye yuko tayari kutusaidia, lakini
aingilii uhuru wako kuamua njia za kujisaidia. Kama unazo za kwako,
yeye hana shida; ila acha nikwambie; njia pekee ni Mungu tu.
95
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Ebrania 9:27-28 inasema kwamba ‘’Kama vile mtu alivyowekewa kufa


mara moja, na baada ya kufa hukumu; kadhalika Kristo naye akiisha
kutolewa sadaka mara moja, iliazichukue dhambi za wengi, atatokea
pasipo dhambi, kwa hao wamtazamiao kwa wokovu (Neema ya
Mungu ya kusamehe makosa na kumuhesabia mtu haki bure); Ishara
ya kuwa umeamini katika neema, sio kuishi au kuwa mwaminifu
katika sheria, bali katika matendo yatokanayo na imani. Galatia 3:2;
inasema ‘’Nataka kujifunza neno hili moja kwenu, je! Mlipokea Roho
kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?
Hatukuokolewa kwa haki itokanayo na matendo ya sheria, bali kwa
kuamini kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. 1Yoh 3:16,
inasema hivi ‘’Katika hili tumelifahamu pendo; kwa kuwa yeye aliutoa
uhai wake kwa ajili yetu, imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili
ya hao ndugu’’
Kwa hiyo, hatuokoki kwa sababu tumejifunza kwa habari ya haki ya
sheria, bali ni kwa imani na kusadiki kuwa, wewe ni mwenye dhambi
na kuwa hauwezi kujiokoa mwenyewe, wala sheria haiwezi kukuokoa
wewe, hivyo unamuhitaji Yesu Kristo akusamehe makosa yako.
Na lazima kuamini kuwa Kristo ni Mungu aliyekuja kwetu katika mwili
1Yoh 4:1-2, aliyejitoa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi zako na za
ulimwengu. Maandiko yanasema hivi, ‘’Kwa moyo mtu huamini hata
kuhesabiwa haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Gal 2:16,
Rumi 10:4
Wokovu sio dini, wokovu maana yake ni kuzaliwa upya kwa roho
yako ndani yako, kwa maana kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na
kilichozaliwa kwa roho ni roho. Yoh 3:3-6.
ROHO KUHUISHWA KWA NEEMA

Tunapozungumzia habari za kuhuishwa kwa roho ya mtu ndani yake


tunamaanisha tendo la kuokoka (kuzaliwa mara ya pili), tendo la
kuokoka; kwa kawaida ni tendo la kiroho lisilohusiana na mwili, lakini

96
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

matokeo ya tendo hilo, hutafsirika katika mwili, kwa sababu sio mwili
unaookoka, bali ni roho ya mtu ndiyo inayozaliwa upya ndani ya mtu
na kuhuisha uhusiano wa mtu huyo na Mungu wake. Yoh 3:6. Ndio
maana imeandikwa, ‘’kilichozaliwa na mwili ni mwili, na kilichozaliwa
kwa roho ni roho. Kwa hiyo, tendo la kuzaliwa mara ya pili; ni hali
ya kurudishiwa uhusiano wa Mungu na mtu, na kupokea kile kipawa
cha neema ya kupokea nguvu ya kuishi milele mara baada ya maisha
ya awali yaliyo na ukomo wa muda wa uhai. Yoh 3:16 Efeso 2:14..
Mtu anapozaliwa mara ya pili, anapata uhusiano mpya na Roho wa
Mungu, na kufanywa mwana wa Mungu. Efeso 2:8
ROHO INAZALIWA KWA NAMNA GANI:

Mwa 2:7 Inasema ‘’Bwana Mungu akampulizia puani pumzi ya uhai,


mtu akawa nafsi hai” na ukumbuke kuwa, Mungu ni Roho; kwa hiyo,
kama Mungu ni Roho, na mtu ni Pumzi ya Mungu; basi, roho ya mtu;
huzaliwa na Roho ya Mungu. Sasa kama roho ya mtu huzaliwa na
Roho wa Mungu, kuna haja gani ya roho ya mtu huyo kuzaliwa mara
ya pili? Sikiliza, Biblia inasema ‘’Mshahara wa Dhambi ni mauti. Rum
6:23. Na Efe 2:1 inasema ‘’Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa
na dhambi zenu’’ Sasa kama tulikuwa wafu, maana yake hatuna tena
ule uhai wa Mungu katika roho zetu. Hivyo, kuzaliwa mara ya pili, ni
kurudishiwa uhai kwa njia ya neema katika Kristo. Na tunarudishiwa
uhai ule uliyopote katika mauti yetu, kwa kuamini, ila hapo kwanza
tulipewa uhai huo kwa kupuliziwa
NEEMA NI NINI..?

Neema ni neno la kithelojia, ni msamiati wenye tafsiri ya nenola


Mungu linalofanya kazi kwa wanadamu, ili kuwasaidia madhaifu yao
na kuwahesabia haki bure (bila kustahili).
Neema ni neno linalohusishwa pia na tendo la kuzaliwa mara ya pili
(Kuokoka). Neno la Mungu linasema hivi ‘’Hata wakati ule tulipokuwa
wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani
tumeokolewa kwa neema’’

97
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Katika biblia, neno ‘’Neema’’ limetokana na maneno mawili ya kigiriki


ambayo ndiyo yaliyotafsiriwa kama neema, na maneno hayo ni:
i. Charis (Khar-ece) – Ni neno lenye maana ya upendeleo,
wema na uwezesho. Neno hili limejitokezakatika biblia (Agano
jipya) mara 157
ii. Charisma (Khar-is-mah) – lenye maana ya karama
au kipawa kinachotolewa na Mungu bure au upendeleo
anaopewa mtu bila kustahili; Neno hili katika biblia (Agano
jipya) limejitokeza mara 17
Katika tafsiri ya biblia, karama na vipawa vyote vya Roho Mtakatifu
vinahesabiwa kuwa ni neema ya Mungu kwa watu wake. Kwa hiyo
tunaweza kusema kuwa ‘’Neema ni kipawa cha Mungu kwa watu,
kinachotolewa bure na kuachilia upendeleo na wema wa Mungu kwa
watu bila kustahili, Mungu anaachilia neema hii ili kuonyesha wema
wake katika pendo lisilo na sababu wala masharti.Neema ya Mungu
haiishi kutustahilisha tu, bali pia hutusaidia udhaifu wetu. 1Kor 15:8-
10
KAZI YA NEEMA KWENYE UHUISHO (KUOKOA)

Kazi kuu ya neema ni kutustahilisha pale tusipostahili (Tunahesabiwa


haki bure), na kutusaidia udhaifu wetu; kwa kuwa nia ya mwili ni
mauti, bali karama ya Mungu ni amani na uzima wa milele, na kwa
kuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi zetu, (tumekosa uhusiano na
Mungu), mfumo wa maisha yetu yanaendeshwa kwa kufuata mwili;
na maandiko yanasema wazi kuwa nia ya mwili ni mauti (roho kuacha
mwili/kufariki dunia).
Kwa hiyo; ilitupasa sote tuwe tumekufa kimwili pia, kama tulivyokufa
kiroho, lakini nia ya Mungu kwetu ni kutupatia uzima wa milele kwa ile
sheria ya uzima (Kutotenda dhambi), lakini kutokana na nia ya mwili;
inatuvuta kwenye mauti.Mtu anapokosa uhusiano na Mungu, anaishi
kwa kufuata mwili. Kwa sababu hiyo, hawezi kumpendeza Mungu kwa
sababu ya ile nguvu ya mauti (Dhambi) inayoishi ndani yake ikivutwa
98
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

na ile sheria dhaifu; Rumi 8:8 inasema kuwa ‘’Wale waufuatao mwili,
hawawezi kumpendeza Mungu.
Mtu kwa asili yake, ni mwenye dhambi; ndio maana Yohana anasema
‘’Enyi uzao wa nyoka, ni nani aliyewaonya ninyi?’’ Na dhambi ya mtu
sio yale matendo yake, bali ni ile hali ya roho yake kukataa sheria ya
Mungu, na kuushinikiza mwili kubeba mauti; Mwa 4:6-7 imeandikwa
kusema ‘’Bwana akamwambia Kaini, kwanini una ghadhabu? Na
kwanini uso wako umekunjamana? Kama ukitenda vyema, hutapata
kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo
inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde’’ sasa kwa sababu ya
hiyo dhambi,Ndipo Mungu akaamua kutustahilisha kupata uzima
wa milele bure (Kwa neema), bila kutegemea matendo yetu, kwa
kumwamini Yesu Kristo; yeye ndiye aliye asili ya wokovu wetu.
WOKOVU NI NINI

Wokovu ni msaada wa kuponya au kunusuru juu ya hatari Fulani, yaani


ni kutoa mtu au kitu katika hali ya kupata matatizo ya aina mbalimbali
kama vile: Mauti, Upotevu wa mali, N:K
Lakini kibiblia; wokovu ni nguvu ya asili ya Mungu inayokuja kwa mtu
ili kuleta msaada wa kuokoa (Kumtoa mtu katika hali ya ghadhabu ya
Mungu ya kutupwa katika ziwa la moto), yaani kumtoa katika hali ya
hatari ya mauti ya pili. Kolo 1:13. Nguvu ya wokovu ndio inayookoa,
Mwa 45:7, 1nyak 16:35; Ndio maana utasikia katika dunia, kuna kikosi
maalumu kinaitwa jeshi la wokovu, maana yake; wao hufanya kazi ya
kuokoa, lakini ni katika mambo ya kimwili. Isaya 49:8
Wokovu kwa msingi wa maandiko, ni zawadi itolewayo na Mungu
bure kwa mtu au watu bila kustahili na bila kulipia gharama yeyote;
zawadi hii tunaipokea kwa njia ya imani kwa kumwamini na kuiamini
Injili ya Kristo Yesu. Rumi 1:16. Wokovu ni kifurushi ndani ya Injili ya
Kristo, kama dhana ya ukombozi kwa watu uletwao na Mungu; na
injili hii iletayo wokovu, imetujia kwa njia ya neema katika msalaba
wake Yesu Kristo ili kudhihirisha pendo la Mungu juu yetu, kwa maana

99
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kristo ndio kikomo cha kiwango cha juu cha pendo la Mungu kwa
wanadamu.
Yoh 3:16 imeandikwa kuwa ‘’Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda
ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila amwaminiye
asipotee, bali awe na uzima wa Milele’’Kumbe mtu kutokuwa na
uzima wa milele ni kupotea?Je! Uzima wa milele ni nini sasa? Yoh
17:3 ‘’Na uzima wa milele ndio huu, wakujue wewe, Mungu wa pekee
wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma’’
Anaposema kuwa ’Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu’’
maana yake anatusaidia kutafsiri juu ya tendo lililobeba kiwango cha
upendo wake; Ambalo kwa tendo hilo, tunapata kufahamu kipimo
kamili cha pendo kamili la Mungu kwa watu wote.
Lakini, anataka tuone ambavyo haikuwa rahisi kwa Mungu kufanya
hicho alichokifanya kwa ajili yetu; ndio maana anasema hivi ‘’Hata’’
unaposikia neno hili ‘’Hata’’ ujue ni dhahiri kabisa kuwa; neno hilo
linawakilisha ugumu wa hatua iliyochukuliwa, au ujasiri wa kiwango
cha mwisho kabisa katika kufanya maamuzi. Na tendo lenyewe ni lile
la Mungu kumtoa mwanae wa pekee (Kristo Yesu), asiye na dhambi ili
afe kwa ajili ya dhambi za ulimwengu.
Kwa hiyo, pendo hili ndilo linalookoa, lakini ili mtu alipokee pendo
hili, ni lazima afikiwe na kuikubali Injili ya Kristo (Habari za neema ya
Mungu kwa watu), ambazo hazitokani na haki ya mtu ipatikanayo kwa
matendo ya sheria (Torati); kwa sababu kwa sheria (Torati) hakuna
mwenye mwili atakayeokoka, lakini mtu akifikiwa na injili hii ya neema,
na kuamini kwa moyo wake kuwa Kristo ni Mwana wa Mungu na
kukiri kwa kinywa chake kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu,
na Roho Mtakatifu akamuhuisha kutoka katika wafu, atapata wokovu.
Ndio maana imeandikwa ‘’Kwa moyo mtu huamini hata kuhesabiwa
haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu’’
Wokovu ni mpango kamili wa Mungu uliyoimarishwa katika falsafa
za Mungu mwenyewe juu ya kuhuishwa kwa roho za watu ndani yao,

100
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

(Kuzaliwa mara ya pili). Mpango huu ni madhubuti, na ni mali Kamili


inayotawaliwa na kumilikiwa na Mungu mwenyewe.
NANI ANAOKOA..?

Kazi ya kuokoa roho za watu (Watu kuzaliwa mara ya pili), ni wajibu na


jukumu la Mungu. Math 19:25-26
Maana yake ni kwamba!Hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa
kujiokoa wala kuokoa isipokuwa Mungu tu. Ndio maana maandiko
yanasema kwenye Kolo 1:12 ‘’Mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha
kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru’’. Kwa hiyo,
Mungu kwa kule kupenda kwake mwenyewe; Naye alituokoa kutoka
katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza kwenye ufalme wa
mwana wa pendo lake; ambaye katika yeye, tuna ukombozi, yaani
msamaha wa dhambi; Kolo 1:13.
Hapa anamaanisha aliyetukomboa na kutuhamisha hata kutuingiza
kwenye ufalme ni Mungu, lakini ufalme huo haukuwa ufalme wa
Mungu mwenyewe; bali ufalme wa Mwana wa Mungu (Yesu Kristo),
ambaye katika yeye huyo (Yesu Kristo), ndiye aliyefanyika sadaka
ya ukombozi wetu, yaani tumesamehewa dhambi zetu kwa njia ya
adhabu na mauti yake msalabani. Ndio maana anasema ‘’Ambaye
katika yeye, tuna ukombozi, yaani msamaha wa dhambi. Kwa hiyo
utaona maandiko jinsi yanavyoeleza juu ya sisi kuingia katika ufalme
wa Kristo kwa kupelekwa na Baba yake (Mungu).Yoh 6:44
Katika tendo la mtu kuzaliwa kwa mara ya pili; kinachotangulia kwa
mtu ili azaliwe, ni uwepo wa Roho wa Mungu (Neno la Kristo). Yoh
6:63 imeandikwa kuwa ‘’Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu;
maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima’’. Ndio maana
imeandikwa hivi ‘’Imani huja kwa njia ya kusikia, na kusikia huja kwa
Kristo). Rumi 10:17. Mtu akisikia habari za Kristo, ile Roho ya uhuisho
inaingia ndani yake na kukaa hapo, na hiyo Roho haitaondoka kamwe
hata ikiisha kumzaa mara ya pili, itaendelea kuishi ndani yake na
kumsaidia udhaifu wake.

101
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kazi kuu ya Roho ndani ya mtu, ni kumzaamtu mara ya pili, kwa hiyo
ikiisha kuingia ndani yako kwa lile neno la Kristo, itakaa hapo kusubiri
nguvu za Mungu mpaka zitakapokuja juu yako (Imani katika Kristo),
hiyo ndiyo itakayompa Roho Mtakatifu mamlaka kamili ya kuingia
chumba cha ndani cha roho yako, na nguvu zile za Mungu (Imani
katika Kristo Yesu) yaani Neno la ukiri, zitamsaidia Roho Mtakatifu
kusukuma mtoto ndani yako atokee,na kuzaliwa upya kwa roho yako
(kukamilisha tendo la Kuzaliwa mara ya pili au kuokoka). Maana
imeandikwa ‘’Kwa moyo mtu huamini hata kuhesabiwa haki, na kwa
kinywa hukiri hata kupata wokovu. Rumi 8:16
Kwa hiyo, mtu kuzaliwa mara ya pili, ni matokeo ya uwepo wa Roho
Mtakatifu juu ya huyo mtu, pamoja na uwepo wa nguvu ya Mungu
(Imani) ya mtu mwenyewe juu ya Mungu katika Kristo Yesu. Ndio
maana imeandikwa katika kitabu kile cha injili ya Luka 1:35, kusema
‘’Malaika akajibu akamwambia, Roho mtakatifu atakujilia juu yako, na
nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo, hicho
kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu mwana wa Mungu’’
Hata imeandikwa tena, ‘’Bali wote waliompokea, aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake’’.
Kumbuka kwamba; Imani (Kumwamini Yesu Kristo), ndio nguvu
pekee ya Mungu inayompa Roho Mtakatifu kibali cha kuizaa roho
yako, na hiyo imani ndiyo inayompa mtu nafasi ya kuishi. Ndio maana
imeandikwa ‘’Wenye haki wangu wataishi kwa imani’’ Habakuki 2:4,
Rumi 1:17.Kwa hiyo anayeokoa ni Mungu mwenyewe kwa njia ya
kuzaa upya roho zetu kwa Roho wake Mtakatifu Katika Kristo Yesu,
lakini njia ya wokovu wetu ni kumwamini Kristo Yesu kwa mioyo yetu,
na kumkiri kwa vinywa vyetu kuwa yeye ni Bwana na mwokozi wa
maisha yetu.
Je! Tunaokolewa kutoka wapi?
Biblia inatuambia kuwa; tunaokolewa kutoka katika nguvu za giza,
Mungu anatutoa katika hali ya mazingira ya dhambi kwa njia ya

102
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

dhabihu ya mwanae mpendwa Yesu Kristo, ili tupate kutolewa katika


hatari ya mauti ya pili (Adhabu ya kutupwa katika ziwa la moto).
Mpango wa wokovu ni ahadi, ni mkakati kamili wa Mungu wa
kurejeza mtu mpya katika ulimwengu mpya. Pia wokovu ni njia
kamili iliyoandaliwa na kutumiwa na Mungu mwenyewe kama njia
ya kumpokonya shetani utawala katika ulimwengu huu, aliyojitwalia
pale edeni baada ya kumlaghai Adamu na mkewe, kwa kuwashawishi
kula tunda (Yaani kutenda dhambi) kwa kukiuka agizo la Mungu.
Hali hii ya Adamu; ni sawa kabisa na hali ya kanisa la sasa, Kanisa
limedanganywa, na kuacha au kukiuka maagizo ambayo Mungu
alilipa Kanisa, na kanisa lilipaswa kutekeleza ili Mungu atukuzwe,
lakini limekiuka maagizo hayo na kufuatisha namna ya ulimwengu
huu, huko ni sawa na kuuza haki yake kwa sababu ya chakula (yaani
kula tunda au kutenda dhambi); kama alivyofanya Adamu.Ikiwa
kanisa halitaki kumtii Mungu, kamwe haliwezi kumpendeza Mungu,
na hivyo, kanisa lisitegemee kumwona Mungu akijidhihirisha.
Ndio maana utaona kanisa la leo, limejaa watu wanaotafuta miujiza,
lakini wao wenyewe hawana uhusiano na mwenye kutenda hiyo
miujiza. Tunamtumia Mungu kama mganga wa kienyeji tu, tunaenda
kupiga ramli na kutabana tu kanisani, hakuna ibada ya kweli; watu
wanataka unabii wa uongo, wanataka kutamkiwa Baraka tu, lakini
hawataki kujifunza njia za kubarikiwa. Ni lazima tuokoke, yaani
tumtafute Kristo kwa Bidii ili atuokoe.
Ndugu; Maisha ya dunia hii ni mafupi sana, na ni maisha yaliyojaa kila
aina ya vita na misukosuko yenye maumivu makali, na ubaya wa vita
hivi; havipiganwi kimwili; ni vita vya kiroho. Njia pekee ya kuvishinda
vita hivi, ni wewe kuacha kuishi kimwili, na kuanza kuishi kiroho kwa
njia ya kuzaliwa upya kwa roho yako kwa kumwamini Yesu Kristo.Lakini
pia; baada ya maisha haya kukoma, tutaanza maisha mapya yasio ya
kikomo; huko tutaishi milele; ilajinsi utakavyoishi huko,hutegemea
maisha ya dunia hii; Kama ukitenda vema sasa, utaishi maisha ya
furaha milele ukiwa na Kristo Yesu, lakini ukitenda vibaya, utaishi kwa

103
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

mateso na maumivu makali katika ziwa la moto ukiwa pamoja na


shetani milele. Uamuzi ni wako
Kwa kawaida, mtu aliye katika hali ya hatari ya Kifo (mauti ya pili),
hana uwezo wa kupambana na mazingira hayo ili kuyatetea maisha
yake yeye mwenyewe dhidi ya kifohicho, mwili wake huwa dhaifu
kwa sababu kazi ya kwanza ya mauti ni kudhoofisha nguvu za mtu na
kumtia hofu, hii inatokana na ile hali ya mwili kushindana na Roho; kwa
kuwa nia ya mwili ni kutaka mtu afe (Mauti), lakini neema (Karama) ya
Mungu, ni kumpa mtu huyo nafasi ya kuishi milele (uzima wa milele).
Kwa hiyo, kwa sababu ya ule udhaifu; uwezo wa mtu kujitoa kwenye
mauti ni sifuri kabisa, hivyo anahitaji msaada wa nguvu nyingine
isiyo mali yake (isiyo haki yake/Neema). Zekaria 4:6 anasema ‘’Si kwa
uwezo wala si kwa nguvu, bali ni kwa Roho yangu, asema Bwana wa
majeshi.
Mtu aliye katika hali ya kufa (Kiroho), hafanyi shauri lolote kati yake
na mwenye kuokoa, kwamba; nitakulipa kiasi hiki kwa kazi yako; la!
Wala muokoaji haombi malipo yeyote toka kwa mwenye kuhitaji
kuokolewa, tunaokolewa bure (kwa neema) kama sehemu ya zawadi
ya uhai wa pili na upendo waMungu. Ndio maana imeandikwa,
‘’Tumeokolewa bure, wala mtu awaye yote asijisifu’’Efeso 2:8-9
imeandikwa ‘’Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya
imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu,
wala si kwa matendo, mtu awaye yote asijisifu.
Hili neno ‘’Bure’’ linatafsirika kama ‘’Neema’’yaani, kupewa kitu au
haki pasipokustahili, ila Mungu anastahilisha kwa kupenda kwake tu,
ndio maana maandiko yanasema ‘’Hata wakati ule tulipokuwa wafu
kwa sababu ya makosa na dhambi zetu, alituhuisha pamoja na Kristo;
yaani tumeokolewa kwa neema. Efeso 2:5
Neno ‘’neema’’ ni huruma za Mungu zinazomsukuma kutusamehe na
kutustahilisha kustahili haki bure, bila sisi kutenda tendo jema lolote,
ni kipawa/zawadi ya Mungu kwa watu ili kuwatoa katika dhambi na
mauti (Kuwaokoa). Lakini ingawa zawadi hii hutolewa bure, lakini

104
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

bado imewekwa kuwa hiyari binafsi ya mtu kuikubali hiyo zawadi


NAMNA KUUPOKEA WOKOVU

Kama nilivyotangulia kusema, wokovu ni zawadi inayotolewa bure na


Mungu kwa watu wote, lakini sio wote wanaohitaji zawadi hii; hivyo
Mungu ameweka utaratibu wa kuipokea zawadi hii kwa wale waliyo
tayari, na namna ya kupokea zawadi hii ni kwa kufuata mambo haya
yafuatayo:

i. Kusikia habari njema (Injili ya Kristo)


Ni muhimu sana kwa mtu anayetaka kupokea zawadi hii, ajitahidi
kusikia habari za injili ya Kristo; kwa kuwa ndani ya injili hiyo, kuna
nguvu ya uhuisho (Imani). Imeandikwa ‘’Imani chanzo chake ni
kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. Rumi 10:17
Imani ni matokeo haswa ya kusikia, kila mtu anayeamini kitu
chochote, chanzo cha imani yake ni matokeo ya neno alilolisikia.
Hivyo ni hatari sana kwa mwana wa Mungu kuruhusu masikio
yako kusikia kila kitu, hii itakupandikizia imani mseto kutokana na
kusikia vitu vingi tofauti ambavyo vitakuingizia ndani yako imani
nyingi tofauti na kukosa msingi wa imani yako kwa Mungu, na
mtu mwenye nia mbili mbele za Mungu (Imani tofauti), mtu huyo
Mungu hawi radhi naye.
Ndio maana Mungu anasema ‘’Nayajua matendo yako, ya kuwa
hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au
moto! Basi kwa sababu unavuguvugu, wala hu baridi wala moto,
nitakutapika utoke katika kinywa changu. Ufu 3:15-16
Imani sahihi inatokana na kusikia neno la Kristo tu.
Hakuna mtu aliyezaliwa na imani, imani ni mgeni anayekuja kwa
mtu kupitia njia ya kusikia, hivyo chunga sana juu ya unachosikia.
Ndio maana Rumi 10:17b anasema hivi ‘’imani huja kwa neno la

105
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

Kristo’’ anaposema imani huja, anamaanisha hakuna mtu alikuwa


nayo hapo kabla. Kwa hiyo; kama unataka kupokea zawadi hii ya
wokovu, ni lazima kusikia Neno la Kristo. Usipoteze muda wako
kusikiliza habari za dunia hii, ni vema kulipa nafasi neno la Kristo ili
likuumbie imani ndani yako na kuyaponya maisha yako, kwa kuwa
hizo habari nyingine zitakuingizia imani nyingine ambazo zitakuua
tu.
Biblia inatuambia kwamba! ‘’imani ni kuwa na hakika ya mambo
yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasioonekana. Ebra 11:1
Katika andiko hilinimeona jambo la ajabu na kutishanimegundua
wazi kuwa; kanisa halijui maana halisi ya Neno Imani. Kwa kuwa;
kanisa linatambua imani ya kuombea wagonjwa, na kutenda
miujiza N:k lakini kwa mujibu wa andiko hili; imani ni zaidi ya hayo.
Kuna mambo ya msingi sana yamejificha katika andiko hili, na
kama tusipoyatafuta na kuyapata, kanisa litakuwa kwenye hatari
kubwa sana ya kusombwa na mafuriko ya miujiza ya kishetani kwa
kudhani kuwa ndio matokeo halisi ya imani katika Kristo
Neno ‘’Imani’’ linabeba mambo makuu matatu Kama ifuatavyo:
∗ Kuwa na hakika’’
Maandiko yanapotutaka tuwe na uhakika, ni lazima kwanza
tujue ni uhakika juu ya nini? Kwa maana hatuwezi kuwa na
uhakika bila kujua uhakika wenyewe ni juu ya kitu gani. Kwa hiyo
Munguanatusaidia kujibu swali hili kwa kusema ‘’Mimi ni Bwana
Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya
utumwa. Usiwe na Mungu mwingine ila mimi’’ maana yake ni
nini?
Maana yake ni kwamba;
Mungu anataka tuwe na uhakika juu yake, tubaki tukiamini katika
Mungu mmoja, kama anavyosema yeye mwenyewe kuwa ‘’Usiwe

106
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

na mungu mwingine, ila mimi” kwa tafsiri hiyo, neno ‘’Hakika’’


linatuthibitishia kuwa; hakuna Mungu mwingine ila yeye Mungu
wetu, na anatutaka tuamini juu ya uwepo wake, nguvu zake
(Roho wake Mtakatifu), na kuamini ujio wake katika mwili (yaani
kumuamini Yesu Kristo). Kwa hiyo Mungu anatutaka tusiwe na
miungu wengi kama watu wasio na hakika na Mungu wao. Yoh
14:1 anasema kuwa ‘’Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini
Mungu niaminini na mimi.’’
Kwanini ni muhimu kumuamini Yesu? Ni muhimu kwa sababu,
yeye ndiye aliyepewa dhamana na Mungu ya kutupatia sisi uzima
wa milele. Yoh 17:3
∗ ‘’Mambo yatarajiwayo’’
Anaposema kwa habari ya mambo yatarajiwayo, analikumbusha
kanisa juu ya ujio wa mara ya pili wa Kristo Yesu kuja kulichua
kanisa lake; jambo hili ni la msingi sana katika imani, ni lazima
kanisa katika kuamini kwake, litajarie juu ya ujio wa Kristo mara ya
pili. Kwa kuwa kanisa linapokosa taraja hili, imani na subira yake
vitapotea, na watu wakishapoteza taraja hili ndani yao, wataanza
kuishi kama sio wana wa Mungu; wakijichanganya katika mambo
ya dunia hii. Kuna mambo ambayo wapendwa wanayafanya,
ukijaribu kutafakari hata haupati jibu, je! Ni wana wa Mungu
wanaofanya haya;au wameshakengeuka? Na haya yote yanatokea
kwa kuwa watu wamechoka kusubiri, kwa kuwa hawanaimani juu
ya kuja kwa Kristo mara ya pili, hawana tena tarajio la kumpokea
Kristo pindi atakapokuja kulichukua Kanisa Lake. Ndio maana
watu wanahangaikia mambo ya mwilini tu.
Lakini neno la Mungu linatukumbusha juu ya kukesha; kwa kuwa
hatujui siku wala saa.
∗ ‘’Yasioonekana’’
Anaposema juu ya ‘’Yasioonekana’’analikumbusha kanisa juu

107
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ya kuamini mambo yatakayokuja, ambayo hayajapata kuwapo


tokea kuumbwa kwa ulimwengu huu. Ni muhimu sana kwa kanisa
la Kristo kujua kuwa, kuna mambo yatakayokuja, lakini mambo
hayo hayajapata kuwapo tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu;
mambo hayo ni yale ambayo jicho halijapata kuyaona, na wala
masikio hayajapata kusikia.
Yesu anasema moja kati ya kazi za Roho Mtakatifu ni kutupasha
habari sisi kama Kanisa la Kristo kwa mambo yatakayokuja. Yoh
16:13 inasema ‘’Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli,
atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena
kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena,
na mambo yajayo atawapasha habari yake.
Mambo hayo yatakayokuja, bayana ya mambo yasiyoonekana,ni
mambo yanayohusiana na Adhabu ya jehanamu ya moto ambayo
aliwekewa shetani na malaika zake, kwa hakika mambo haya ndio
ambayo hayajapata kuonekana bado, lakini Roho wa kweli wa
Kristo; anatupasha habari juu ya hukumu. Yoh 16:11 inasema hivi
‘’Kwa habari ya hukumu, kwa sababu hawaniamini mimi’’ Kama
kanisa halitaamini juu ya uwepo wa jambo hili, ni dhahiri kuwa
kanisa litakuwa pango la walanguzi, watu hawatakuwa na hofu ya
Mungu, na dhambi itatawala kanisa.
Kwa hiyo, msingi wa neno imani, ni mkusanyiko wa mambo haya
makuu matatu. Kwa hiyo neno, ‘’Imani’’ sio ile nguvu ya kuombea
wagonjwa, wala kutenda miujiza;ni zaidi ya hayo, kwa kuwa imani
hiyo ndio inayodhihirisha matokeo ya uwepo wake. Ndio maana
imeandikwa kuwa ‘’Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio’’.
Mark 16:17. Hivyo, hatuanzi kuwa na ishara kabla ya imani, bali
ishara zinafuata imani.
Maana yake ni kwamba! Ishara zinafanywa na wanaoamini, sio
wanaoamini ishara zitafanyika. Ndio maana Yesu anasema kuwa,
‘’Amini nawaambieni; Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo
mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya,

108
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

kwa kuwa mimi naenda kwa Baba. Yoh 14:12


Kwa hiyo Kristo anatusaidia kujua kuwa, hatuanzi kufanya hizo kazi
kabla ya kuamini, ni lazima sharti kuamini kwanza kisha ndipo hizo
kazi zitafanyika. Swali la kujiuliza ni hili; kama kazi hizo zinatanguliwa
na imani, je! Tunaamini nini? Jibu ni hili! Tunaamini juu ya mambo
matatu niliyokwisha kukueleza, ambayo ni:
1. Kuwa na uhakika juu ya Mungu mmoja, na kumwamini
Kristo
2. Kuwa na hakika juu ya kurudi kwa Kristo
3. Kuwa na hakika juu ya hukumu
Huo ndio msingi wa imani, na kazi na ishara zote zitokanazo na imani,
ndio maana ni muhimu kumuamini Mungu kwanza kabla hujaanza
kutafuta miujiza. Kumwamini Mungu ni kumkubali Kristo wake, kuwa
ni Bwana na mwokozi wa maisha yako (Kubali kuzaliwa mara ya pili au
Kuokoka). Ndipo Nikodemo Akamuuliza Bwana Yesu, je! Mtu aweza
kurudi kwenye tumbo la mama yake na kuzaliwa tena? Yesu akajibu,
‘’Amini amini nakuambia: mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho,
hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili,
na kilichozaliwa kwa Roho ni roho
ii. Dhihirisha matendo ya matamanio ya imani
Kama ndani yako una kiu ya kuzaliwa mara ya pili, dhihirisha kiu hiyo
kwa matendo yako, kama maandiko yanenavyo, kuwa; ‘’Imani huja’’
maana yake ni sawa na kusema ‘’imani ni kiumbe hai ndani ya mtu’’
na kiumbe hiki kinajitafsiri uhai wake kwa matendo. Yakobo 2:26
inasema ‘’Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo
na imani pasipo matendo imekufa.
Ukiisha kudhihirisha matamanio ya imani yako kwa kuonyesha kiu
ya kuchukia na kuacha dhambi, na shauku yako ya kuzaliwa mara

109
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ya pili itakusukuma kuongozwa sala ya toba ili kumpokea Kristo


awe Bwana na mwokozi wa maisha yako, baada ya hatua hiyo, sasa
Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo; wao wataubadili mwili wako na
matumizi yake; tangu hapo, mwili wako utakuwa ni hekalu takatifu
la Mungu. Imeandikwa ‘’Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la
Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi
si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi,
mtukuzeni Mungu katika miili yenu’’ 1Kor 6:19
1Kor 3:16 anasema hivi ‘’Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la
Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
Sasa uwe na uhakika kuwa; kama Mungu anakaa ndani yako kwa njia
ya imani, ujue ishara na miujiza vitakuwa sehemu halisi ya maisha
yako; kwa kuwa kazi kuu ya ishara na miujiza;ni kuutambulisha na
kuuthibitisha uwepo wa Mungu kwenye maisha ya Mtu. Ndio maana
imeandikwa ‘’Mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba
yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi
zenyewe. Yoh 14:11.
Kimsingi, kazi kuu za miujiza ya Mungu ndani ya mtu ni kumdhihirisha
mtu kuwa yeye ni hekalu takatifu la Mungu. Mungu hafanyi miujiza ili
kufurahisha watu, bali Mungu hufanya miujiza ili kutiisha fikra za watu
na imani zao; kuwa Mungu ni wa kuogofya, ili watu kwa tabia zao,
wasipate kumzoelea Mungu na kumfananisha na shida zao.
Tatizo lililopo ni kwamba! Kanisa limejazwa na watu walioongozwa
sala ya toba, lakini waliookoka ni wachache sana; hii imempa shetani
nafasi ya kufanya mazingaombwe yake na kumtukanisha Mungu
Kanisa limeshindwa kutofautisha kati ya kuongozwa sala ya toba na
kuokoka,

• Kuongozwa sala ya toba


Wokovu ni mabadiliko. Kut 3:3 inasema kwamba ‘’Nitageuka sasa

110
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

niyaone maono haya makubwa’’ Kwa hiyo, kuokoka ni kugeuka


na kuacha maono (Asili yako) na kufuata maono (Asili ya Mungu).
Lakini Kuongozwa sala ya toba, ni hatua ya kuingizwa tu kwenye
mchakato wa kugeuka (kutubu na kuacha dhambi), lakini wakati
ule unapoongozwa sala hiyo bado ndani yakohakunamabadiliko.
• Kuokoka, ni mchakato endelevu wa maisha, ni ile hali
ya kudumu katikakuyaishi maisha matakatifu, sio lile swala
la kuongozwa mara moja; ni jambo endelevu, kila wakati
tunapaswa kutenda mema na kutubia makosa yetu.
Lakini kwa kukosa ufahamu huo, wengi hudhani wameokoka, kumbe
ni Mateka wa mauti na kuzimu. Hawajaokoka japo wameongozwa
sala ya toba, lakini hawana ushirika na Roho wa Mungu, hawawezi
kujisimamia, badala yake hupenda kuombewa kwa kuwa hawana
nguvu ya maombi ndani yao. Kwa hiyo; hawana msaada wa maombi
kutoka kwa Roho Mtakatifu, ndio maana wanahangaika kutafuta
maombi. Hawajazaliwa upya, hawaongozwi na Roho. Rumi 8:14,
Waongozwao na Roho wa Mungu ndio wana wa Mungu;huyo roho
wako mwana wa Mungu, ni roho gani asiyejua hata kukuombea?

111
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

HITIMISHO
Napenda kusisitiza kuwa; kitabu hiki, ni Maongozo ya Roho Mtakatifu
mwenyewe kwa ajili ya Kanisa la Kristo,kama sehemu ya msaada wa
Mungu juu ya roho za watu wake, ili katika Kristo Yesu, apate kwa
huruma zake mwenyewe, kuwaponya watu hao na mauti ile ya pili,
kama ilivyoandikwa kwamba ‘’Nikaona wafu, wakubwa kwa wadogo,
wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi; na vitabu vikafunguliwa;
na kitabu kingine kikafunguliwa, ambacho ni cha uzima, na hao wafu
wakahukumiwa katika mambo hayo yaliyoandikwa katika vile vitabu,
sawasawa na matendo yao. Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo
ndani yake, Mauti na kuzimu zikatupwa katika ziwa la moto; Hii ndio
mauti ya pili, yaani, hilo ziwa liwakalo moto. Na iwapo mtu yeyote
hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima alitupwa katika
lile ziwa la moto’’ Uf 20:12-15
Ibilisi, mwenye kuwadanganya watu, akatupwa katika ziwa la
moto na kiberiti, alimo yule mnyama na yule nabii wa uongo; Nao
watateswa mchana na usiku hata milele na milele. Ufu 20:9-10.
Ibilisi atakapotupwa katika ziwa la moto, atatupwa pamoja na wale
waliodanganywa wakadanganyika. Imeandikwa ‘’Enyi watu wangu,
wawaongozao ndio wanaowakosesha’’ kwa hiyo kule kukoseshwa
hakumfanyi aliyekosa kutohesabiwa kosa, kwa sababu hiyo; Kristo
alikuja kutukomboa na udanganyifu wa shetani ili kutuepusha na ziwa
la moto. Uamuzi ni wa kwako
Bado unayo nafasi ndugu, ikiwa Mungu amekuhurumia kwa kiasi hiki,
hata akashuka mwenyewe duniani katika mwili, asiye na dhambi kwa
ajili ya wenye dhambi, na mwenye haki kwa ajili ya wasio haki. Ni nini
kinachokuzuia leo usiuone upendo huu mkuu wa Mungu juu yako?
Je! Ni njaa? Au wazazi? Au dini yako? Au Itikadi? Au kazi? Au utajiri?
Au elimu yako? Au heshima yako?
Acha nikwambie ukweli, ikiwa ni mojawapo kati ya hayo, au likiwepo
jambo lingine liwalo lote zaidi ya hayo; ujue wazi kuwa halitaweza
kukusaidia au kukutetea mbele za hukumu siku hiyo ya hasira kuu

112
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

ya Bwana itakapofunuliwa. Wakati ni sasa. Tafakari pendo hili, kisha


usifanye moyo wako kuwa mgumu kama farao wa Misri; je! Jeuri yake
ilimponya mbele za hasira ya Bwana? AuWewe je! Ni nini kitakuokoa
siku hiyo?
Wokovu sio dini;
Dini ni mpango wa watu wa kutafuta njia za kumwendea Mungu au
miungu, na njia hizo; ni matokeo ya mapokeo ya kufikirika na dhana
juu ya hali ya Mungu. Hakuna dini duniani kote inayoweza kumfikisha
mtu mbinguni zaidi ya Wokovu; maana wokovu ndio mpango na njia
ya watu kumwendea Mungu, ndio maana imeandikwa ‘’Mimi ni njia,
kweli na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi’’ unahitaji
usikie neno gani tena mpendwa, hata ufungue moyo wako? Ndugu;
sala na dua za marehemu, pamoja na sadaka watakazotoa ndugu
zako, zitaishia masikioni na mikononi mwao na kwa viongozi wa dini
yako; wala hazitafika kwako, wala kwa Mungu ili kukusidia. Amua
kujisaidia mwenyewe leo, kumkubali Kristo kuwa Bwana na Mwokozi
wa Maisha yako. Amen

113
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

SALA YA TOBA
Ikiwa uko tayari kumpokea Kristo awe Bwana na Mwokozi wako; sema
kwa imani na uaminifu maneno haya yafuatayo:
Sema
Eeeh Bwana Yesu, ninakuja mbele zako, mimi ni mwenye dhambi,
nimesikia habari zako, na ninakuamini sasa, ninataka kugeuka na
kuziacha dhambi, naomba unisamehe makosa yangu, dhambi zangu,
na kunisaidia kuziacha, unioshe kabisa kwa Damu yako, ulifute jina
langu kwenye kitabu cha hukumu, andika jina langu kwenye kitabu
cha uzima, tangu leo nakupokea uwe Bwana na Mwokozi wa maisha
yangu, ninamkataa shetani na kazi zake, ninakukiri wewe, ahsante
kwa kunisamehe, ahsante kwa kuniokoa. Amen
Sasa umeokoka
Kitu pekee cha kufanya sasa, tafuta kanisa wanapoabudu katika Roho
Mtakatifu, Yaani kanisa linaloamini katika Wokovu, upate kuendelea
kujifunza jinsi ya Kuishi maisha Matakatifu na usirudi tena kwenye
dhambi. Mungu akubariki na kukulinda siku zote

114
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

SALAMU ZA MWANDISHI

Basi Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji


Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu
Yesu, awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate
kuyafanya mapenzi yake; naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele
zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amen
Ebr 13:20

115
ROHO AKIFA NDANI YANGU KWA SHERIA TORATI HUADHIBIWA KWA NEEMA

116

You might also like