Professional Documents
Culture Documents
IN DAILY LIVING).
WAFASRI.......2024.
Utangulizi mfupi....
SURA YA 1
NIDHAMU YA MAJARIBU.
Kuishi maisha kama haya, kutoa ushawishi Kama huo,
gharama kwa kila hatua ya jitihada, kujitolea na nidhamu ni
kwasababu wengi hawaelewi wanavyokata tamaa kwa
urahisi katika maisha ya Kikristo. Wengi huweka wakfu
maisha yao kwa utumishi wa Mungu na hushangaa na
kukatishwa tamaa na hujikuta kukabiliwa na vikwazo,
kuzingirwa na majaribu na kuchanganyikiwa, wanaomba ili
wafanane na tabia ya Kristo, ili wafae kwa kazi ya Bwana,
na wamewekwa kwenye hali ambazo zinaonekana kuibua
uovu wao wote wa asili, makosa yanadhihirishwa ambayo
hawakutazamia kama yatakuwepo. Kama ilivyokuwa kwa
Israeli ya kale wanauliza "ikiwa Mungu anatuongoza
kwanini mambo haya yote yanatupata?". Ni kwa sababu
Mungu anawaongoza ndiyo maana mambo hayo
yanawajia. Majaribu na vikwazo ni njia zilizochaguliwa na
Bwana za nidhamu na alizoziweka kuelekea kwenye
mafanikio. Yeye asomaye mioyo ya watu anawajua
wahusika kuliko wao wenyewe wanavyojijua. Anaona
kwamba wengi wana nguvu na hisia ambazo, zikielekezwa
ipasavyo, zinaweza kutumika katika maendeleo ya kazi
yake. Katika majaliwa yake anawaleta watu hawa katika
nafasi na hali mbalimbali ambazo wanaweza kugundua
katika tabia zao kasoro ambazo zimefichwa kutokana na
ujuzi wao wenyewe, yeye amewapa fursa ya kurekebisha
kasoro hizo na kufaa kwa ajili ya utumishi wake. Mara
nyingi yeye huruhusu moto wa mateso ya kuwashambulia
ili wapate kutakasika. Ukweli ni kwamba Bwana Yesu
anaona ndani yetu Kitu cha thamani ambacho anatamani
kukiendeleza, ikiwa haoni chochote ndani yetu ili aweze
kulitukuza jina lake, asingetumia muda kutusafisha ndani.
Bwana Hatupii mawe yasiyofaa ndani ya tanuru lake, ni
madini ya thamani ambayo yeye husafisha. Mhunzi
huweka chuma kwenye moto ili ajue ni kwa namna gani
chuma kitakuwa. Bwana huruhusu wateule wake kuwekwa
kwenye tanuru la mateso, ili kuthibitisha jinsi walivyo na
kama wanaweza kufaa kwa ajili ya kazi yake. Mfinyanzi
huchukua udongo na kuufinyanga kulingana na mapenzi
yake, huunda udongo na kuufanyia kazi, huugawanya-
gawanya na kuupasua-pasua na kisha kuunganisha tena
pamoja, huuloanisha kisha anaukausha, huruhusu ulale
kwa muda bila kuugusa, wakati unapokuwa kamilifu na
kufaa, huendelea na kazi ya kuufanya kuwa chombo. Yeye
huunda umbo katika uimara na kuking'alisha chombo.
Hukausha kwenye jua na kuoka katika tanuru, hapo
chombo kinakuwa kimefaa kwa matumizi. Ndivyo
mfinyanzi mkuu amelenga kutufinyanga na kutuunda, na
kama vile udongo ulivyo mikononi mwa mfinyanzi,
hatupaswi kufanya kazi ya mfinyanzi, kile tunachoweza
kukifanya ni kujitoa ili kufinyangwa na mfinyanzi mkuu.
"Wapenzi, msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu,
unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni
kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoyashiriki
mateso ya Kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu
wake mfurahi kwa shangwe." 1 Petro 4:12-13.
Katika mwanga kamili wa Mchana na katika kusikia mziki
wa sauti nyingine, ndege aliyefungiwa hataimba wimbo
ambao bwana wake anatafuta kumfudisha, hujifunza vifijo
na lugha hiyo lakini sio wimbo tofauti na toni husika,
bwana wake humweka na kumfungia ndege huyo sehemu
ambayo ataweza kusikia wimbo atakaouimba bwana wake,
katika giza, ndege hujaribu na kujaribu kuimba wimbo huo
mpaka ueleweke, naye huvuma kwa sauti kamilifu, kisha
ndege huletwa kwenye mwanga na baada ya hapo
anaweza kuimba vizuri wimbo huo katika mwanga.
Ndivyo Mungu hushughulika na watoto wake, ana wimbo
wa kutufundisha na wakati tumejifunza katikati ya vivuli
vya mateso, tunaweza kuimba wimbo huo baadaye na
hata milele.
UJIRA
Kristo alipowaita wanafunzi wake wamfuate yeye
hakuwapatia matazamio ya kujifurahisha katika maisha
haya, hakuwapatia ahadi ya faida au heshima ya kidunia,
wala kuweka sharti lolote juu ya nini wanapaswa kupokea,
Kwa Mathayo alipokuwa ameketi kwenye ofisi ya ushuru,
mwokozi alisema "nifuate. Akaacha vyote, akaondoka,
akamfuata." Luka 5:27,28. Mathayo hakufanya hivyo kabla
ya kutoa huduma, hakusubiri na kudai mshahara fulani
sawa na kiasi alichopokea katika kazi yake ya awali. Bila
kuhoji wala kusita alimfuata Yesu. Ilikuwa inatosha kwake
kuwa pamoja na mwokozi, apate kuungana naye katika
kazi yake ndivyo ilivyokuwa kwa wale wanafunzi walioitwa
hapo awali. Wakati Yesu alipomwambia Petro na wenzake
wamfuate mara wakaacha mashua na nyavu zao, baadhi
ya wanafunzi hawa walikuwa na marafiki waliokuwa
wanawategemea kwa msaada, lakini walipopokea
mwaliko wa mwokozi, hawakupokea kwa kusita na kuuliza
"Nitaishi vipi na kuitunza familia yangu?" Walikuwa watiifu
kwa wito na wakati baadaye Yesu alipowauliza "Je! Hapo
nilipowatuma hamna mfuko, wala mkoba, wala viatu,
mlipungikiwa na kitu? Wakasema la!." Luka22:35. Leo
mwokozi anatuita Kama alivyomwita Mathayo, Yohana na
Petro kwa kazi yake. Ikiwa mioyo yetu itaguswa na upendo
wake, suala la fidia halitakuwa katika akili zetu, tutafurahi
kuwa watendakazi pamoja na Kristo, Na hatutaogopa
kumwamini yeye anayejali. Tukimfanya Mungu kuwa
nguvu yetu tutakuwa na mtazamo mzuri wa wajibu wetu
na matarajio yasiyo na ubinafsi, maisha yetu yatakuwa ya
kuchochewa na kusudi tukufu.
MUNGU ATATOA.
Wengi wanaodai kuwa Ni wafuasi wa Kristo wana moyo
wenye wasiwasi na kufadhaika kwasababu wanaogopa
kumtumainia Mungu. Hawataki kujisalimisha kikamilifu,
kwani wao wanajiepusha na matokeo kwamba
kujisalimisha huko kunaweza kuhusisha kutokupata amani.
Kuna wengi ambao mioyo yao inauma sana chini ya mzigo
wa utunzaji kwasababu wanatafuta kufikia kiwango cha
ulimwengu. Wamechagua kuutumikia ulimwengu na
wamekubali mashaka yake, wameiga desturi zake, hivyo
tabia zao zimeharibika na maisha yao kuwa uchovu. Hofu
yao ni kuzima nguvu za maisha. Mungu wetu anawataka
waweke kando nira hii ya utumwa, anawaalika kukubali
nira yake anasema, "Nira yangu ni laini na mzigo wangu Ni
mwepesi" Mtahayo 11:30. Wasiwasi Ni upofu na huwezi
kutambua siku zijazo, bali Yesu yeye anaona mwanzo na
mwisho. Katika kila shida yeye njia yake imetayarishwa
kuleta ahueni, "kwa kuwa BWANA, Mungu, ni jua na ngao,
BWANA atatoa neema na utukufu,. Hatawanyima kitu
chema hao waendao kwa ukamilifu". Zaburi 84:11. Baba
yetu ana njia elfu za kutupatia mahitaji yetu ambazo
hatuzijui, wale ambao wanakubali kanuni moja ya kufanya
huduma ya Mungu kuwa kuu zaidi, watakuta mashaka
yanatoweka na wataona njia iliyowazi mbele ya miguu yao,
utekelezaji kwa uaminifu wa majukumu ya leo ndio
maandalizi bora ya majaribio ya kesho, usikusanye pamoja
wajibu wa kesho na kuongeza kwenye mzigo wa leo. "Basi
msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia
yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake". Mathayo 6:34.
Hebu tuwe na matumaini na ujasiri, kukata tamaa katika
kazi ya Mungu ni dhambi na haina maana kufanya hivyo.
Mungu anajua kila hitaji letu kwa kuwa yupo kila wakati na
mahali popote mfalme wa wafalme. Mungu wetu
anayetunza maagano anaunganisha upole na utunzaji wa
mchungaji mwenye huruma. Nguvu zake ni kamili na ni
ahadi ya utimilifu wa uhakika wa ahadi zake kwa wote
wanaomtumaini. Ana njia ya kuondoa ugumu wa kila
namna, kwamba wale wanaomtumikia na kumheshimu
yeye aliyewaajiri atawaimarisha. Upendo wake uko mbali
na upendo mwingine wowote kama vile mbingu ziko juu ya
dunia. Yeye huangalia watoto wake kwa upendo usio na
kikomo na milele. Katika siu za giza wakati kuonekana
kunapoanza kufifia, uwe na imani kwa Mungu anafanya
mapenzi yake, anafanya mambo yote kuwa vema kwa ajili
ya watu wake. Nguvu ya wale wanao mpenda na
kumtumikia itafanya upya siku kwa siku. Ana uwezo na
yuko tayari kuwapa waja wake wote msaada wanaohitaji.
Atawapatia hekima ambayo mahitaji yao mbalimbali
yanadai. Mtume Paulo alijaribiwa alisema "Naye
akaniambia neema yangu yakutosha; maana uweza wangu
hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu
kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Kwa
hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na
adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu
ndipo nilipo na nguvu." 2wakorintho 12:9,10.
SURA YA 2
USITAMKE UOVU
Tukiwa na ufahamu wa uvumilivu mkubwa wa Mungu
kwetu, hatutapatikana tukihukumu au kulaumu wengine.
Wakati Kristo alipokuwa akiishi duniani, jinsi ambavyo
wenzake wangeshangaa, ikiwa, baada ya kumfahamu,
wangemsikia akisema neno moja la kulaumu, la
kushutumu, au la kukosa uvumilivu. Tusiwasahau kamwe
wale wanaompenda wanapaswa kumwakilisha katika
tabia.
"Kwa upendo wa kindugu mpendane, kwa heshima
mkiwatanguliza wenzenu." "Si kulipa ubaya kwa ubaya, au
matusi kwa matusi: lakini badala yake baraka; mkijua
kwamba mmeitwa, mpate kurithi baraka." Warumi 12:10; 1
Petro 3:9.
HESHIMA
Bwana Yesu anahitaji kutambuliwa kwa haki za kila mtu.
Haki za kijamii za watu, na haki zao kama Wakristo,
zinapaswa kuchukuliwa kwa uzingatiaji. Wote wanapaswa
kushughulikiwa kwa ustadi na upole, kama wana wa kiume
na wa kike wa Mungu.
Ukristo utamfanya mtu kuwa mtu mwema. Kristo alikuwa
mwenye heshima, hata kwa watesaji wake; na wafuasi
wake wa kweli watadhihirisha roho ile ile. Angalia Paulo
alipopelekwa mbele ya watawala. Hotuba yake mbele ya
Agripa ni mfano wa ukunjufu wa kweli pamoja na
ushawishi wa kuvutia. Injili haihamasishi upole wa
kawaida unaotawala ulimwengu, bali heshima inayotokana
na wema wa kweli wa moyo.
Kutenda kwa uangalifu zaidi wa mambo ya nje ya maisha
haitoshi kuzuia malalamiko yote, hukumu kali, na maneno
yasiyofaa. Utakatifu wa kweli hautafichuliwa kamwe
kama mtu binafsi anachukuliwa kama lengo kuu. Upendo
lazima ukae moyoni. Mkristo anayeendelea kwa ukamilifu
hupata motisha za matendo yake kutoka kwa upendo wa
kina wa moyo wake kwa Bwana wake. Kutoka kwa mizizi
ya mapenzi yake kwa Kristo huchipua nia isiyojipenda kwa
ndugu zake. Upendo humpa mmiliki wake neema, maadili,
na upendezi wa tabia. Huangaza uso na kudhibiti sauti;
inatengeneza na kuinua kiumbe kizima.
KUJIDHIBITI
Hatujawai kuwa peke yetu. Tumchague au la, tunae
mwandamizi. Kumbuka kuwa popote ulipo, ufanyapo
lolote, Mungu yupo. Hakuna kitu kinachosemwa au
kufanyika au kufikiriwa kinachoweza kuepuka kujua kwake.
Kila neno au tendo lako una shahidi - Mungu mtakatifu,
anaye chukia dhambi. Kabla ya kusema au kutenda, kila
wakati fikiria hili. Kama Mkristo, wewe ni mwanachama wa
familia ya kifalme, mtoto wa Mfalme wa mbinguni.
Usiseme neno, usifanye kitendo, ambacho kitaihujumu "ile
jina la thamani ambayo mmeitwa." Yakobo 2:7.
Jifunze kwa makini tabia ya uungu-ubinadamu, na daima
ujiulize, "Yesu angefanya nini kama angekuwa mahali
pangu?" Hii inapaswa kuwa kipimo cha wajibu wetu.
Usijitie mwenyewe bure katika jamii ya wale ambao kwa
sanaa zao wangepunguza azma yako ya kufanya mema,
au kuleta doa kwenye dhamiri yako. Usifanye kitu
chochote miongoni mwa wageni, barabarani, kwenye
magari, nyumbani, ambacho kingeonekana kidogo cha
uovu. Fanya kitu kila siku kuboresha, kizuri, na kuenzi
maisha ambayo Kristo ameununua kwa damu yake
mwenyewe.
SURA YA 3
NGUVU YA TABIA
Watu thabiti wanahitajika, watu ambao hawatasubiri kila
kizuizi kuondolewa katika njia yao na njia yao kuwa safi,
watu ambao watatoa hamasa na kuamsha ari za wengine
waliokata tamaa, watu ambao mioyo yao ina upendo wa
Kristo na ambao mikono yao ipo tayari kufanya kazi ya
Bwana wao.Baadhi ya watu ambao wanajiingiza katika
huduma ya kimisionari ni dhaifu, sio jasiri, hawana roho wa
Mungu na ni wepesi wa kukata tamaa. Hawana msukumo
na kazi hiyo. Hawana sifa chanya za tabia zinazotoa
uwezo wa kufanya jambo fulani—roho na nguvu isiyokata
tamaa. Wale ambao wangepata mafanikio lazima wawe
na ujasiri na matumaini. Wanapaswa kusitawisha sio tu
sifa tulivu, bali pia sifa tendaji. Wakati wakiwa na jukumu
la kutoa jawabu la upole linalogeuza hasira, wanapaswa
kuvaa roho ya kishujaa kuweza kukataa maovu. Kwa
upendo unaostahimili kila kitu, wanahitaji nguvu ya tabia
ambayo itafanya ushawishi wao kuwa na nguvu
chanya.Wengine hawana uimara wa tabia. Malengo yao na
mipango yao haina uendelezo wala ufafanuzi
unaoeleweka. Matumizi yake ni madogo sana katika
ulimwengu huu. Wanapaswa kuacha udhaifu huu, kukosa
maamuzi na uzembe. Ni lazima tuwe na uadilifu thabiti,
uadilifu ambao hauwezi kubembelezwa, kuhongwa, au
kutishwa.
UTAMADUNI WA KIAKILI
Mungu anatamani kila nafasi tunayoipata tuitumie katika
kujiandaa na kazi yake. Anategemea tuweke nguvu zetu
zote katika utendaji wake na kuweka mioyo yetu tayari
kwa kufanya kazi ya Mungu.Wengi wetu tuna sifa za
kufanya mambo makubwa katika kazi ya Mungu lakini
tunatimiza vichache kwasababu tunafanya kwa uchache.
Maelfu ya watu huishi katika haya maisha kama vile
hawajui lengo la kuishi, hawana viwango vya juu
walivyojiwekea kuvifikia. Kristo alilipa deni kubwa kwa ajili
yetu, na kutokana na deni hilo alilotulipia basi anatamani
sisi tuwe watu tunaojithamini. Usiwe mtu wa kuridhishwa
na viwango dhaifu. Sisi hatupaswi kuwa watu wa hivyo na
hata Mungu hajataka tuwe watu wa hivyo. Mungu
ametupa uwezo wa kufikiri, sio kubaki bila shughuli au
kupotoshwa kwa mambo ya kidunia na ya uchafu, bali
tuendelezwe kwa upeo wa juu, tuliosafishwa, tuliotakaswa,
tuliokuzwa, na kutumika katika kuendeleza maslahi ya
ufalme Wake.Hakuna anayepaswa kukubali kuwa mashine
tu inayoongozwa na akili ya mtu mwingine. Mungu
ametupa uwezo wa kufikiri na kufanya, na ni kwa kufanya
kwa umakini, ukimtazama yeye kwa hekima kwamba
utaweza kuvumilia matatizo. Simama katika tabia na hisia
za kipekee alizokupatia Mungu. Usiwe kivuli cha mtu
mwingine. Tarajia kwamba Bwana atafanya kazi yake
kupitia wewe hivyo hivyo ulivyo.Kamwe usifikiri kwamba
tayari umeshajifunza vya kutosha , na hivyo ukae na
kutuliza juhudi zako. Akili inayofanya kazi ndio kipimo cha
kuwa mtu. Unapaswa kuendelea kujifunza kila siku kwa
maisha yako yote, kila siku unapaswa kusoma na
kutendea kazi yale uliyojifunza. Kumbuka kwamba katika
nafasi yoyote utakayokuwepo unazaa matunda ya
muendelezo wa tabia yako. Chochote kile utakachokifanya,
kifanye kwa usahihi, kwa uangalifu; uishinde ile hali ya
kutaka kurahisisha kazi.
UNAFANYEJE KAZI?
Ile roho na misingi unayoitumia katika kufanya kazi zako
za kila siku, inapaswa iwe hivyo hivyo kwa maisha yako
yote. Wale wanaotamani kiasi maalum kisichobadilika
cha mshahara uliowekwa na ambao wanatamani kuwa na
matokeo mazuri katika kazi zao bila kukutana na
changamoto zozote sio ambao Mungu anawaita katika
shamba lake. Wale ambao wanajifunza namna ya kutumia
kwa uchache nguvu zao, akili na maadili sio watu ambao
kwao Mungu atawashushia baraka zale tele. Mfano wao ni
wa kuambukiza. Wapo tu kwa ajili ya maslahi binafsi. Wale
wanaohitaji kuwekewa uangalizi na kufanya majukumu tu
ambayo anakuwa amewekewa kwa ratiba ya siku hiyo si
miongoni wa wale Mungu atakaowatangaza kuwa ni
wema na waaminifu. Wanahitajika watumishi
watakaodhihirisha uwezo, uadilifu,na bidii, wale waliopo
tayari kufanya chochote kinachohitajika kufanywa.Wengi
wanakuwa hawana tija kwa kukwepa majukumu kwa
kuogopa kushindwa. Hivyo wanashindwa kupata elimu
hiyo ambayo ni matokeo ya uzoefu, na kusoma ambayo
kwayo faida zilizopatikana haziwezi kuwapata wao. Mtu
anaweza kubadili mazingira, lakini mazingira hayapaswi
kumbadilisha mtu. Tunapaswa kuchukulia mazingira kama
kifaa katika kufanya kazi zetu. Tunapaswa kuzoea
mazingira lakini hatupaswi kuruhusu mazingira yatuzoee.
Watu mashuhuri ni wale ambao walipingwa, kudhalilishwa
na kukataliwa. Kwa kuziweka nguvu zao katika vitendo,
vikwazo wanavyokutana navyo vinawathibitishia kuwa
kuna baraka chanya katika hilo wanalolifanya.
Wanajijengea kujitegemea. Migogoro na kuchanganyikiwa
inawapa jitihada za kumwamini Mungu, na nikwa uthabiti
huo unaokuza nguvu.
KUSUDI MOJA
Katika maisha ya Kristo, kila kitu alichofanya kilikuwa
chini ya mpango kazi wake aliokuja kuukamilisha. Na
ibada sawa, kujinyima sawa na kujitolea , utiifu uleule
katika neno la Mungu, udhihirike kwa wanafunzi wake pia.
Kila mmoja anayempokea Kristo kama mwokozi wake
binafsi atatamani kupendelea kufanya kazi ya Mungu.
Akitafakari kile mbingu kilichofanya kwa ajili yake, moyo
wake utaondoka ukiwa umejawa na upendo na shukrani
kubwa. Ana shauku ya kuonyesha shukrani zake kwa
kujitolea uwezo wake katika kazi ya Mungu. Anatamani
kuonyesha upendo wake kwa Kristo na kwa kile
alichofanya kwa ajili yake. Mtumishi mwema wa Mungu
atafanya vizuri katika kazi yake kwani kwa kufanya hivyo
atakuwa anamtukuza Bwana wake. Atafanya kwa usahihi
kwa ajili ya kufikia matakwa ya Mungu. Atajitahidi
kuboresha uwezo wake wote. Atafanya kila awezalo kwa
ajili ya Mungu. Tamanio lake kuu itakuwa ni Kristo aweze
kupokea heshima na huduma kamilifu. kuna picha
inayowakilisha fahali aliyesimama kati ya jembe na
madhabahu yenye maandishi; "Tayari kwa lolote", tayari
kufanya kazi kwenye mtaro au kutolewa kwenye
madhabahu ya dhabihu. Huu ndio msimamo wa mtoto wa
kweli wa Mungu, nia ya kwenda mahali ambapo kazi inaita,
kujikana nafsi, kutoa dhabihu kwa ajili ya Mkombozi.
SURA YA 4
MSHAURI WA KI_MUNGU
MWISHO.