You are on page 1of 106

MATUNDA 9

YA
ROHO MTAKATIFU

Daudi Pius

i
MATUNDA 9 YA ROHO MTAKATIFU

Hakimiliki ©Daudi Pius, june, 2023


Toleo la kwanza, June 2023
Mawasiliano:
Namba ya simu: +255 65 633 9872
+255 759487509
What'sApp: +255 (0) 65 633 9872
Instagram: @daudimballa
Barua pepe: mbaladaudi15@gmail.com
Msanifu wa Jalada:
Hakimiliki ©Onesmo Elisha Matula, 2023
Barua Pepe: oemaniceg@gmail.com
Facebook: Onesmo Matula
Maandiko Matakatifu ya Biblia katika kitabu hiki yamenukuliwa kutoka
katika tafsiri ya Swahili Union Version(SUV)
©Bible Society of Tanzania, 1997; ©Bible Society of Kenya, 1997

Hakimiliki Ya Mwandishi
Haki zote zimehifadhiwa. Hairuhusiwi sehemu yoyote ya kitabu hiki
kunakiriwa, kuchapishwa, na kuhifadhiwa katika mfumo wa kielektroniki au
kubadilisha maana yeyote ile bila idhini ya mwandishi.

ii
TABARUKU
Kitabu hiki ni kwa heshima ya Wazazi wangu Mzee Pius Mathias na Bi
Veronika Mathias ambao wamekuwa msaada mkubwa wa karibu kwangu
tangu nikiwa mtoto mdogo mpaka nimekua. Hata sasa wamesimama na mimi
kuniombea na kuniunga mkono kwa kazi hii ya utumishi. Bwana amewatumia
sana kubariki maisha yangu.

iii
YALIYOMO
UTANGULIZI ................................................................................................ v
SHUKRANI.................................................................................................. vi
SEHEMU YA KWANZA ..................................................................................... 1
ASILI YA MATUNDA ....................................................................................... 1
SEHEMU YA PILI ........................................................................................... 6
MATUNDA .................................................................................................. 6
SEHEMU YA TATU ........................................................................................ 10
MATUNDA YA MWILI .................................................................................... 10
SEHEMU YA NNE .........................................................................................24
ROHO MTAKATIFU .......................................................................................24
SEHEMU YA TANO ....................................................................................... 35
MATUNDA YA ROHO MTAKATIFU .................................................................... 35
SEHEMU YA SITA ......................................................................................... 39
MATUNDA TISA YA ROHO MTAKATIFU .............................................................. 39
1.Upendo. .................................................................................................. 39
2.Furaha.................................................................................................... 53

3.Amani. ................................................................................................... 57

4.Uvumilivu ................................................................................................60

5.Utu wema. .................................................................................................64

6. Fadhili. .................................................................................................. 68

7. Uaminifu. ................................................................................................71

8.Upole. .................................................................................................... 75

9.Kiasi. .....................................................................................................80

SEHEMU YA SABA ....................................................................................... 84

KAZI NA UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU ........................................................ 84

Umuhimu wa Roho Mtakatifu kwa mwamini. ............................................................. 92

KUHUSU MWANDISHI: DAUDI PIUS .................................................................. 97

MAREJEO .................................................................................................. 98

iv
UTANGULIZI
Kitabu hiki ni msaada mkubwa kwa MKristo kuishi maisha ya uhalisia ya
Kikristo katika kizazi hiki, ili kuleta uamsho na matengenezo ndani yake,
kukaa na Roho Mtakatifu ili kufanya mapenzi makamilifu ya Mungu. kitabu
hiki kinahusu Matunda tisa ya Roho Mtakatifu (Wagalatia 5:22-23) na nilikiita
"Matunda tisa ya Roho Mtakatifu" kwa sababu kinachunguza mada ya
Matunda tisa ya Roho Mtakatifu kwa kina na ufasaha. Hii ni kuhakikisha hata
kama ulipokuwa unasoma pengine hukuelewa Matunda tisa ya Roho
Mtakatifu ukiwa peke yako, basi kupitia kitabu hiki ukikisoma kwa umakini,
polepole ikibidi na familia yako yote itakuwa ni jambo jema sana litakaloleta
mapinduzi chanya katika maisha yenu ya kiroho.
Pia kitabu hiki kinaeleza kwa kina matendo ambayo MKristo anatakiwa
ayaishi, yaani maisha ya utauwa na ushindi dhidi ya vishawishi vya mwili
vinavyochochewa na tamaa za mwili pamoja na adui, na MKristo ili akamilike
anatakiwa haki yake kwa Mungu izidi haki ya waandishi,Mafarisayo na
washika dini ili kuurithi Ufalme wa Mungu,maana mwanadamu aliumbiwa
maisha mazuri, na ikitokea anapitia magumu huumia mno kiasi kwamba
hukumbuka maisha ya Edeni,lakini mateso yalianza pale mwanadamu
alipomtenda dhambi Mungu ndipo ushirika na uhusiano kati ya Mungu na
mwanadamu ukavunjika.Lakini ashukuriwe Mungu wa Mbinguni kwa kumtoa
mwanawe pekee Yesu Kristo ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima
wa milele.

v
SHUKRANI
Natanguliza shukrani zangu za dhati kwa Mungu Baba yangu wa Mbinguni,
Mungu muumba mbingu na nchi kwa neema zake nyingi kwangu, kwa kunipa
njozi ya kuandika kitabu hiki kinachohusu Matunda tisa ya Roho Mtakatifu,
nilikiita "Matunda tisa ya Roho Mtakatifu" kwasababu kinachunguza mada ya
Matunda tisa ya Roho Mtakatifu kwa kina na ufasaha.
Bila kuchoka kuwashukuru pia baba zangu wa kiroho:Mchungaji Yusuph Pius
wa kanisa la EAGT Nyida, Shinyanga Vijijini wakati ninapokuwa nyumbani;
na Mchungaji Joseph Chisina wa kanisa la EAGT Ng’ong’ona, Dodoma Mjini
muda wote nikiwa chuoni;Shukrani zangu pia ziende kwa mlezi na mshauri
wangu: Mwalimu Robert Richard(Bachelor of Education in Special needs)
kwa ushauri wa maudhui ndani ya kitabu hiki.
Uongozi wa CASFETA-TAYOMI Ndaki ya Elimu katika Chuo Kikuu cha
Dodoma nimeguswa sana na ushirikiano wenu mzuri katika utumishi na
malezi bora katika utumishi kila mara tukusanyikapo kumwabudu Mungu.
Pia shukrani zangu maalumu ziwaendee wazazi wangu wa kimwili, Mzee Pius
& Bi Veronika Mathias kwa malezi yao mazuri kwangu, Mungu wa Mbinguni
awabariki sana.
Siwezi kumaliza kuwashukuru ndugu Demetrio Felistian na Dorkas Pius
katika usanifu wa lugha. Ndugu Onesmo Elisha, Manase Shiku na William
Shija katika Usanifu wa Kitabu na maandiko; pamoja na watu wote kwa
mchango wao mkubwa katika kuhakikisha kazi hii inakamilika. Mchango
wenu ni mkubwa sana kwangu, zaidi sana Mungu wa Mbinguni awabariki!

vi
SEHEMU YA KWANZA
ASILI YA MATUNDA
Kabla Mungu kumuumba mwanadamu alimwandalia mazingira mazuri
yatakayomwezesha kupata mahitaji yake ya msingi ikiwemo matunda
(chakula). Biblia Takatifu inasema kuwa, Adamu alipewa kula matunda ya kila
mti, lakini akakatazwa kula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Na
akaonyeshwa sehemu mti huo unapatikana ndani ya Bustani ya Edeni,
kwasababu "Mungu hamjaribu mtu, bali mtu hujaribiwa kwa tamaa zake
mwenyewe". Lengo la Mungu kumuwekea mwanadamu matunda lilikuwa ni
kwamba mtu huyu ahisipo njaa, basi na ale. Mungu wakati anamuumba mtu
huyu alimwekea tumbo, kwahiyo Mungu alikumbuka yakwamba mtu huyu
atahitaji kula chakula. Maandiko yanasema 'tumbo ni kwaajili ya chakula, na
chakula ni kwaajili ya tumbo". Hivyo Mungu hakupenda kuona kiumbe chake
cha thamani alichokiumba yeye mwenyewe kihangaike na kutaabika, ndipo
aliumba kwanza mbingu na nchi na ndani ya nchi aliumba vitu vingi ikiwemo
na matunda. Lakini haimaanishi kuwa Mungu hakuwa na uweza wa kuumba
vitu vyote kwa siku moja, hapana, Mungu alikuwa na uweza wa kuumba vitu
vyote kwa siku moja tu, lakini Mungu aliumba vitu vyote taratibu taratibu, na
hii ni kwasababu Mungu ana "uweza" wala sio "uwezo", Uwezo na Uweza
ni maneno mawili tofauti.
 Tofauti iliyopo kati ya neno "Uweza" na neno "Uwezo" hii hapa
chini;

1
Moja, Uweza ni hali ya kuwa na nguvu za kufanya mambo yote. Mungu
anaweza mambo yote wala hakuna chochote cha kumshinda yeye. Sifa kuu ya
Mungu ni hii, ni yule anaye tangaza mwisho kabla ya mwanzo. Mungu alijua
yote hata kabla shetani (Shetani aliitwa Lusifa hapo mwanzo alipokuwa
malaika mzuri) hajawaza moyoni mwake kuwa kama Mungu, ndipo Lusifa
akawa shetani. Japo Mungu hakumkataza Shetani kumwasi. Lakini pia
Mungu alijua yote hata kabla ya anguko la Adamu. Yesu anasema yeye
alikuwepo tangu mwanzo na alichinjwa kabla ya misingi ya dunia kuwekwa,
maana katika Sheria za ulimwengu wa roho damu ya Yesu ndiyo iliyotumika
kumfukuza Shetani huko mbinguni; kwasababu hiyo malaika Mikaeli pamoja
na malaika wenzake walimshinda Shetani kwa ushuhuda wa mwanakondoo
huko mbinguni ndipo Shetani akatupwa chini, lakini kipindi hicho Yesu
alikuwa bado hajazaliwa duniani katika mwili wa damu na nyama lakini
alikuwepo katika Roho. Ndiyo maana nimekueleza kuwa sifa kuu ya Mungu
ni kuwa na uweza wa mambo yote.
Yeremia 51:15 “Ameiumba dunia kwa uweza wake, Ameuthibitisha ulimwengu
kwa hekima yake, Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.”
Yeremia 1:5 “Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka
tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.”
Nahumu 1:3 "Bwana si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi......"
Pili, Uwezo ni hali ya kuwa na nguvu za kufanya mambo kadhaa au baadhi.
"Ubongo wa mwanadamu hutambua rangi, lakini kwenye ubongo hakuna
rangi". Mwanadamu amepewa Uwezo na Mungu wa kufanya mambo baadhi,
lakini kuna vitu vingine mwanadamu hawezi. Mfano wapo wanadamu ambao

2
wana uwezo mkubwa wa kufikiri yaani kimasomo kama (wahandisi,
madaktari, marubani, wahadhili n.k) hawa wanauwezo mkubwa
darasa(kufikiri) lakini kuna mambo mengi hawaviwezi kama vile utakatifu,
hawana nguvu za kiroho.
Matendo ya Mitume 6:8 “Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa
akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.” Haleluya!
Sio hivyo tu, Mungu akamtengenezea Adamu na Bustani nzuri yenye kuvutia
mno na kisha akaweka kila aina ya matunda ili aitawale na kumiliki.
Mwanzo 1:29 " Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu,
ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana
mbegu, vitakuwa ndivyo chakula chenu;"
Kama ilivyo katika maisha ya kila siku ya mwanadamu kwamba
mwanaume(Baba) anawajibu mkubwa wa kuandaa mazingira mazuri pindi
mkewe apatapo ujauzito, kama vile kuweka fedha ya ziada kiasi kwamba
mkewe akijifungua tu basi iwe rahisi kumuhudumia mkewe pamoja na mtoto.
Lakini pia kisaikojia ubongo wa Baba huwa hauoni mimba pekee tu, bali
huwaza gharama zitakazo mkabili baada ya mkewe kujifungua, ndiyo maana
waswahili wanasema kuwa "Kulea mimba sio kazi, kazi ni Kulea mtoto."
Lakini pia mzazi anawajibu mkubwa wa kumpatia mtoto au watoto wake
mahitaji ya msingi kama vile Chakula, Elimu, mavazi n.k. Hivyo
mwanzilishi(Chanzo) wa kila aina ya matunda ni Mungu pekee. Ukisoma
Mwanzo 1:11 “Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na
mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani
yake, juu ya nchi; ikawa hivyo."

3
Kwahiyo hapa tunaona Mungu mwenyewe anaumba au anaamuru nchi itoe
vitu vitatu, ambavyo ni; majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda
uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya
nchi na ikawa hivyo;Lakini ikumbukwe kuwa muda huo hapakuwa na mche
wowote ule wa kondeni,Wala hapatakuwa na mtu wa kula matunda
hayo.mwenyewe. Mwanzo 2:4-5 “⁴ Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi
zilipoumbwa. Siku ile Bwana Mungu alipoziumba mbingu na nchi ⁵ hapakuwa
na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa
maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima
ardhi; Haleluya!
Lakini kwa Dunia ya sasa kutokana na kuongezeka kwa maarifa Duniani,
pamoja na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia , wanadamu wamevumbua
njia za kisayansi za kupandikiza mbegu za mimea zijulikanazo kama "Genetic
Engineering" na kuzalisha mazao ya kisasa (bandia) yaitwayo "Genetic
Modified Organisms"(G.M.O) ili miti ya matunda izae matunda mengi yakiwa
na umri mdogo.Na matunda yanayozalishwa yanakuwa na vinasaba(Koo)
tofauti na za kwanza , vinasaba hivyo vinavyozalishwa kwa njia ya kisasa sio
salama kwa maisha ya mwanadamu kwani vinasababisha changamoto
mbalimbali katika mwili wa mwanadamu ikiwemo, kubadilika Kwa
vinasaba(yaani DNA na RNA), kiasi kwamba humfanya mwanadamu huyu
apatwe na matatizo yakiwamo,mabadiliko yasiyosahihi katika mwili wa
mwanadamu mfano kwa wanawake mabadiliko ya hedhi kwenda tofauti na
kawaida au hapo awali, Kansa , kuzaliwa kwa watoto wenye shida mbalimbali,

4
na hii ni kwasababu ya Kemikali zinazochanganywa na wanaSayansi wakiwa
maabara pindi wanapopandikiza mbegu hizo.
Lakini serikali yetu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania bado haijaruhusu
Teknolojia ya Genetic engineering inayozalisha mazao ya kisasa yaani
"Genetic Modified Organisms" kuanza kutumika, japo tunatumia Teknolojia
zingine ndogo ndogo, ambazo hazina madhara makubwa kama vile, ufugaji
wa kuku wa kisasa, ufugaji wa ng'ombe wa kisasa, na upandikizaji wa mbegu
za kisasa. Nchi ya Kenya yenyewe imeruhusu mfumo huu wa mazao na
viumbe bandia yaani Genetic Modified Organisms kutumika nchini humo.

5
SEHEMU YA PILI
MATUNDA
Isaya 11:1-2 "¹ Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi
litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda. ² Na roho ya Bwana atakaa
juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya
maarifa na ya kumcha Bwana;"
Zipo aina mbalimbali za matunda zinazo pandwa na wanadamu. Hii ni
kutokana na; ustawi wa zao husika, aina ya udongo, upatikanaji wa maji au
mvua katika eneo husika. Hii ni kwasababu ya jiografia au tabia nchi
kubadilikabadilika kutokana na shughuli mbalimbali za wanadamu
zinazopelekea kuharibu Anga la Ozone (Ozone layer) linalozuia mionzi mikali
inayotoka kwenye Jua, zikiwemo; Viwanda, uchimbaji wa madini,
vinavyopelekea kuharibu Anga la Ozone, anga hili likiharibiwa husababisha
ongezeko la joto katika uso wa Duniani, kisha kupelekea mabadiliko ya tabia
nchi.
Matunda ni nini?
Matunda ni mazao ya mmea au mimea yanayohifadhi mbegu ambazo
hutokana na maua. kabla ya matunda kutengenezwa, hutengenezwa kwanza
maua ambayo hutoa harufu nzuri sana. Maua hayo huwavutia wadudu kama
vile Nyuki, Vipepeo na wengineo. Nyuki hao, hufanya uchafushaji pamoja na
kufyonza majimaji yanayopatikana kwenye maua ya mmea kabla ya tunda
kutokea, hivyo Nyuki hutengeneza asali inayotokana na mchanganyiko wa
maji maji wanayoyatoa kwenye mimea. Asali humsaidia mwanadamu kama
chakula lakini pia kama matibabu ya magonjwa kama vile, Vidonda vya

6
tumbo na ikitokea mtu amepata ajali ya moto asali hutumika kutibu, hiyo ni
moja ya faida ya maua ya matunda kabla ya tunda kutokea.
Baadhi ya matunda ni; Mapera, maembe, machungwa, mapeasi, Nanasi, ndizi,
parachichi, chenza, stafeli, topetope, zambarau, zabibu, mizeituni, papai,
nyanya, ntarari, furu,fenesi, tango, bibo, ukwaju."Tunda linaloongoza kuliwa
na mwanadamu kila siku ni nyanya."

Matunda hutoa lishe na virutubisho katika mwili wa mwanadamu pamoja na


viumbe wengine kama vile ndege, wanyama na wadudu, hivyo matunda haya
husababisha viumbe waimarike afya zao, ili waendelee na shughuli
mbalimbali za kila siku. Matunda hutoa vitamin kama vile Vitamin C na
Vitamin B complex.
Taifa la Israeli linaongoza kwa kilimo na uzalishaji wa matunda ya Zabibu
Duniani. Japo hata hapa kwetu Tanzania Mkoani Dodoma zabibu inalimwa.
Zabibu inastawi vizuri Mkoani Dodoma kuliko mikoa mingine hapa nchini.
Uzalishaji wa zao hili hapa nchini kwetu halizalishwi kwa kiwango kikubwa
ukilinganisha na linavyozalishwa kule Nchini Israeli.

 Utunze na kuuthamini mwili wako, kwani mwili wako ni hekalu la Roho


Mtakatifu wala sio mali yako mwenyewe.

1 Wakorintho 6 :19-20 "¹⁹ Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho


Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu
wenyewe; ²⁰ maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu
katika miili yenu."
Vaa nguo nadhifu, nzuri ambazo hazitaleta kero au maswali kwa watu wengine;

7
kumbuka kuwa wewe unaishi kwaajili ya watu wengine, na unavaa nguo sio
kwaajili yako tu, wewe huwezi kuona maajabu yoyote katika mwili wako,
kwasababu unaujua vizuri mwili wako kuwa wapi pakoje, hivyo unatakiwa
uvae nguo za kujistiri vizuri ili usiwape watu wengine shida.
Ukipata muda wa kula chakula kula vyakula bora, wala sio kujaza tumbo tu
yaani "upe pole mwili wako" kwa kula vyakula bora. Ni kweli umemwomba
Mungu na umepokea au umepata upako mwingi wa kihuduma, lakini
kumbuka kuutunza vizuri mwili wako ili afya yako isidhoofike hata
ikapelekea utumishi wako kuyumba.
Upako ni nguvu ya Mungu ambayo mtu hupewa kwa ajili ya utumishi wa kazi
ya Mungu. Lakini nguvu hii ya Mungu unayopewa na Mungu siyo kwa ajili
yako wewe tu bali na watu wengine.
Kuna aina mbalimbali za upako miongoni mwake ni;
1. Upako wa awali: ni upako ambao kila Mkirsto amepewa na Mungu
haijalishi anacheo au hana cheo, ana muda kidogo ama mrefu katika wokovu.
Katika upako huu MKristo hupewa Uwezo na Mungu wa;
(a)Kutoa pepo kwa Jina la Yesu Kristo.
(b)Kunena au kusema kwa lugha mpya.
(c)Kumkemea au kumpinga Shetani (kushika nyoka).
(d)Hata akinywa kitu cha kufisha hakitamdhuru.
(e)Ataweka mikono yake juu ya wagonjwa, nao watapata afya au uponyaji.
Marko 16 :17-18 "¹⁷ Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina
langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; ¹⁸ watashika nyoka; hata

8
wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu
ya wagonjwa, nao watapata afya."
2.Upako baada ya kuzitambua huduma na karama zako: upako huu mtu
huupata mara baada tu ya kuzijua huduma na karama zake alizopewa na
Mungu. Baada ya kutambua huduma, karama na vipawa ulivyopewa na
Mungu inakupasa kumtumikia Mungu, ndani ya kanisa kwa lengo la
kufaidiana na watu wengine, lakini epuka sana kujivuna na kuwaona wengine
hawawezi kutumika kama unavyotumika wewe, jishushe chini ndipo
utafanikiwa zaidi. Na umepewa bure na Bwana toa bure na wewe.
Matendo ya Mitume 5:12-15 “¹² Na kwa mikono ya mitume zikafanyika ishara
na maajabu mengi katika watu; nao wote walikuwako kwa nia moja katika
ukumbi wa Sulemani; ¹³ na katika wote wengine hapana hata mmoja
aliyethubutu kuambatana nao; ila watu waliwaadhimisha; ¹⁴ walioamini
wakazidi kuongezeka kwa Bwana, wengi, wanaume na wanawake; ¹⁵ hata
ikawa katika njia kuu hutoa nje wagonjwa, na kuwaweka juu ya majamvi na
magodoro, ili Petro akija, ngawa kivuli chake kimwangukie mmojawapo wao."
Haleluya!
3.Upako pindi majira ya utumishi yakifika: Aina hii ya upako mtu hupewa
na Mungu pindi wakati wake wa utumishi ukifika hata kama ni nani atajaribu
kishindana nae, lakina mtu huyu ataendelea mbele tu haijarishi vizuizi
vinavyowekwa mbele yake. Muda wa Mungu ni tofauti na muda wa
kibinadamu, muda wa Mungu ukifika kwa mtu haijalishi nani atakataa lakini
mapenzi ya Mungu lazima tu yatafanyika. 1 Samweli 3:4 “basi, wakati huo
Bwana akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.”

9
SEHEMU YA TATU
MATUNDA YA MWILI
Mara nyingi huwezi kujua uwongo kama ukweli haujaufahamu bado; maana
sheria au torati iliwekwa ili kuifunua dhambi, japo torati haikuonyesha ni
namna gani ya kuishinda dhambi. Neema na kweli imeletwa kwa mkono
waYesu Kristo ili kufunua dhambi na namna ya kuishida dhambi. Neema
ambayo Yesu Kristo ameileta siyo nyepesi kama unavyofikiria, kwasababu
Yesu Kristo hakuja kutangua torati na manabii, La! hasha , bali alikuja
kuitimiza (Mathayo 5:17). Kumbe torati ya Musa ilikuwa haijakamilika.
Mfano" ...Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini
naye moyoni mwake"(Mathayo 5:28). Vilevile huwezi kuyatambua matunda ya
mwili kama matunda ya Roho Mtakatifu hujayafahamu bado.
Matunda ya mwili ni nini?
Ni matendo ya mwilini ambayo mwanadamu anayafanya kwa kuendeshwa na
mihemuko ya mwili yaani tamaa za mwili wake. Na hii ilitokana na Wazazi
wetu wa kwanza (Adamu na Hawa) kuanguka dhambini kutokana na
ushawishi wa adui wa Mungu yaani Shetani kufanikiwa kumdanganya Hawa
ili ale tunda la Ujuzi wa mema na mabaya, kisha akampa na Mumewe naye
akala. Lakini inaonekana kuwa Hawa alijitetea kwa kusema kuwa
wamekatazwa na Mungu kula tunda la Ujuzi wa mema na mabaya, lakini
kadiri maongezi yalivyoendelea ndipo Hawa alianza kupitapita karibu na mti
huo wa ujuzi wa mema na mabaya,kisha kuutazama mti ule kuhusu yale
yaliyokuwa yanasema na Shetani Je ni kweli?. Hawa alipozidi kuyaona kila

10
siku matunda ya mti wa Ujuzi wa mema na mabaya, pale Bustanini Maandiko
yanasema kuwa Hawa aliyaona matunda ya ujuzi wa mema na mabaya kuwa;
1. Wafaa kwa chakula. Hawa alikuwa ni mwanadamu na alikuwa anakula,
lakini pia alikuwa anahisi njaa, na njaa ilipompata akakumbuka maneno
ya Shetani kuhusu tunda la ujuzi wa mema na mabaya kuwa lafaa kwa
chakula, ndipo akajisemea ngoja nikalitwae kisha nile. Watu wengi leo
wanashawishika na inawapelekea wanamtenda Mungu dhambi
kwasababu wanaona chakula kinafaa sana kwao kuliko kushika maagizo
ya Mungu.
2. Wapendeza macho. Dhambi inashawishi sana maadamu upo duniani,
lakini pia una macho, na una ona, maana dhambi ina onekana, ina macho
ndiyo maana inakukonyeza ili uifanye, dhambi ina sikia kwasababu
ukikubali itakwambia uifanye.
3. Nao ni mti wa kutamanika Kwa maarifa. Wanadamu wengi leo
wanamtenda Mungu dhambi kwasababu ya kutumia vibaya uwezo
waliopewa na Mungu wa kuvumbua vitu mbalimbali yaani maarifa, na
kufuata maarifa yao bila kumtegemea Mungu wanajikuta wameangukia
pabaya. Jifunze kuujaza ufahamu wako maarifa mema kuliko mabaya,
pia jitahidi kufahamu mema mengi kuliko mabaya.
Ayubu 22:21 "Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; ndivyo mema
yatakavyokujia."
Wapo watu wengi leo wanalalamika na kumnung'unikia Hawa kuwa ni
kwanini alikubali kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya, lakini
hawakumbuki kuwa na wao wanashindwa kuepuka, kuacha dhambi. Lakini

11
ashukuriwe Mungu Baba wa Mbinguni anayetupenda na hata akamtuoa
mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa
milele, hivyo Mwamini Yesu Kristo leo upate ondoleo la dhambi kisha
utabatizwa na ujazwe Roho Mtakatifu, hautakaa kumnung'unikia Hawa, hilo
ni kosa lililojitokeza, hivyo wewe una muda mzuri wa kutengeneza maisha
yako kwa Mungu.
Mwanzo 3:1-7"¹ Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa
mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo
alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? ² Mwanamke
akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; ³ lakini
matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala
msiyaguse, msije mkafa. ⁴ Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,
⁵ kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo,
mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
⁶ Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho,
nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake
akala, akampa na mumewe, naye akala. ⁷ Wakafumbuliwa macho wote wawili
wakajijua kuwa wa uchi, wakashona majani ya mtini, wakajifanyia nguo."

Nyoka (Shetani) anatumia neno "Ati!" kumjaribu mwanamke ya kuwa


anafahamu chochote kuhusu maaagizo ya Bwana Mungu. Hapa adui shetani
alikuwa na lengo la kumpima huyu mwanamke ni kwa viwango gani
anakumbukumbu kuhusu maagizo waliyopewa na Mungu, mwanamke
anamjibu Shetani kwa kumwambia kuwa, matunda yote wanaweza kula.

12
Lakini mwanamke huyu akaendelea kusema " lakini matunda ya mti
uliokatikati ya Bustani Bwana Mungu ametukataza tusile".
 Neno "lakini" kisheria ukilitumia mahakamani hufuta hoja zote za
mwanzoni ambazo mtu alizisema, hivyo mpendwa kuwa makini na kauli
zako ili zisikuponze badaye.

Lakini tunaona katika mstari wa nne kwenye hii Mwanzo 3:4. Nyoka (Shetani)
anamdanganya mwanamke kwa kumhakikishia maneno ya uongo kuwa;
 Hawatokufa. Shetani alimhakikishia kuwa hawatokufa, kumbe ulikuwa
ni uongo unao karibia na ukweli kwa kutumia neno " hakika" asijue
kuwa ni udanganyifu tu.
 Watafumbuliwa macho. Hawa bila kujua kuwa ni hila za shetani
alitamani sana afumbuliwe macho ili aweze kuona ya kuwa Je! yaliyomo
yamo kweli? hata leo hii wanadamu wengi wanajiingiza katika kuangalia
mambo yanayo pelekea kutenda dhambi na lengo lao ni kuona ni nini
hicho kilichofichika? Ni maombi yangu kwa Mungu akupe kushinda
vishawishi vya adui.
 Watakuwa kama Mungu. Hawa bila kufikiria vizuri alipoambiwa na
Shetani ale tunda ili awe na cheo kama cha Mungu alikitamani sana
cheo hicho. Hawa hakujua majukumu makubwa ya Mungu
anayoyafanya kuhakikisha kuwa viumbe wote wanapata mahitaji yao ya
msingi na ya kila siku kama chakula, ulinzi n.k wakiwemo
sisimizi,punda,nyani,binadamu, Simba,swala,panzi n.k Hata leo watu
wengi wanatamani kuwa katika nafasi ya Mungu wasijue kuwa Mungu
anafanyakazi muda wote bila kupumnzika, lakini pia wako watu

13
wanaomwomba ili watu wengine wasifanikiwe, wapo wengine
wanaomba wafe, wapo wanaoomba watu wengine wasife, wapo
wanaoomba wamiliki magari lakini hawana hata chanzo chochote
cha kipato, sijui gari hizo watakuwa wanaziwekea maji badala ya
mafuta!, wangepewa cheo cha Mungu hata tu dakika tano
wangechanganyikiwa nakwambia.
 Watajua mema na mabaya. Adamu na Hawa bila kujua kuwa mema
tayari walishayajua wakatamani pia na mabaya wayajue. Hawa bila
kujua kuwa anakaribisha kifo, akatamani ajue mema na mabaya asijue
kuwa anakalibisha balaa kubwa, lakini alifahamu kuwa Mungu hakuwa
na utani pindi anawaambia kuwa "hakika utakufa" na ilipotokea
mwanawe Habili kumwona amefariki, ndipo akajua kufa kupoje. Nguvu
ya kufa mtu imebebwa kwenye ubaya.
 Nia ya mwili ni mauti bali nia ya roho ni uzima na amani. Warumi 8:6-7
"⁶ Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. ⁷
Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii
sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii."

Kwahiyo tunaona kuwa nia ya mwili ni kufa tu, mwadamu anapopitia


magumu, maumivu makali na majonzi mazito hutamani kufa tu, haoni
umhimu wa yeye kuwa hai lakini sio roho yake inayotamani kufa, ngoja
nikuambie neno hili " Jaribu kuhudhuria misiba ili uone thamani ya uhai
wako ilivyo" . Mungu akusaidie upitiapo nyakati ngumu ili usimtende dhambi.
Mungu wetu anatupenda sana ndiyo maana katuletea Neema Kwa mkono wa
Yesu Kristo ili tujinasue au tuepukane na hukumu yake inayokuja, lakini kuna

14
aina kuu tatu za Neema.Yohana 1:16-17 "¹⁶ Kwa kuwa katika utimilifu wake
sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema. ¹⁷ Kwa kuwa torati ilitolewa kwa
mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo."
Neema ni upendeleo anaopewa mwanadamu kutoka kwa Mungu au kwa
mwanadamu mwingine.
Aina kuu tatu za Neema
i. Neema ya kupata kibali kwa watu: Ni upendeleo ambao
mtu hupata mbele ya kiongozi, mtawala, mwenye mamlaka
au mtu yeyote kuhusu jambo fulani ambalo watu wengine
hawajatendewa au hawajafanyiwa.
Esta 2:17-18 "¹⁷ Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake
wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko
mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake,
akamfanya awe malkia badala ya Vashti. ¹⁸ Ndipo mfalme
alipowafanyia karamu kubwa maakida wake wote na
watumishi wake, yaani, karamu yake Esta; akafanya
msamaha katika majimbo yote, akatoa zawadi sawasawa na
ukarimu wa mfalme.

ii. Neema ya kuokolewa: Ni upendeleo ambao mwanadamu


amepewa na Mungu ambao kimsingi hautokani na nafsi ya
mtu bali ni kipawa cha Mungu kwa njia ya imani. Shetani
humfanya mtu asiione Neema hii kuwa ya thamani. Yesu
Kristo alitupenda kwanza kisha akatuchagua. Kisitokee

15
chochote kile cha kukutoa kwenye Neema hii. Haijalishi hali
yako Kiroho ipoje.

Waefeso 2:8-9 "⁸ Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia
ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa
cha Mungu; ⁹ wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije
akajisifu."

iii. Neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji: Ni neema


ambayo mtu hupewa na Mungu akiwa ndani ya wokovu ili
kukikaribia kiti cha neema kwa ujasiri ili kupewa rehema, na
kupata neema ya kumsaidia wakati wa mahitaji. Hata mtu
aliyeokoka anahitaji hii neema ili imsaidie katika maisha
yake ya kila siku ndani ya wokovu.
Ebrania 4:16 “Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri,
ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati
wa mahitaji.”

 Matunda ya mwili, Biblia Takatifu inayaeleza vizuri katika kitabu cha


Wagalatia5:19-21 " ¹⁹ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya,
uasherati, uchafu, ufisadi, ²⁰ ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi,
wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, ²¹ husuda, ulevi, ulafi, na mambo
yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama
nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi
hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.

16
i. Uasherati
Uasherati ni ngono haramu ambayo kijana wa kike na wa kiume
hushiriki kabla ya ndoa. kitendo hiki vijana hushiriki kabla ya kufuata
ridhaa, kibali na utaratibu maalumu wa Mungu, pamoja na wazazi wa
pande zote mbili yaani upande wa wazazi wa kijana wa kiume, na
upande wa wazazi wa kijana wa kike.
1 Wathesalonike 4:3 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa
kwenu, mwepukane na uasherati;"
Sio mpango wa Mungu kijana au vijana kushiriki tendo la ndoa kabla ya
ndoa, Neno la Mungu linashauri, vijana wasiyachochee mapenzi, wala
wasiyaamshe mapenzi kabla ya wakati wake mpaka pale yatakavyoona
vema yenyewe, kwasababu Kila jambo lina wakati wake sahihi.
Wimbo ulio Bora 2:7 “Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na
kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata
yatakapoona vema yenyewe."
 Kijana usiifuatishe namna ya Dunia hii, kwani "Dunia ina sera
zake na mitazamo yake", Mfano sera ya Dunia kwasasa inahamasisha
ndoa za jinsia moja (Ushoga na Usagaji) na wanadai kuwa ni haki za
binadamu, lakini pia wanadamu wanajiingiza katika ndoa hizo bila hata
ya kujua madhara yatakayowapata baada ya kufanya tendo la ndoa
kinyume na maumbile. Halooo huko nje ni kubaya! hebu tulia kwa Yesu
Kristo. Dunia hii imezeeka, inalewalewa, inawayawaya kama machela.
Isaya 24:20 “Dunia inalewa-lewa kama mlevi, nayo inawaya-waya

17
kama machela; na mzigo wa dhambi zake utailemea; nayo itaanguka,
wala haitainuka tena."
Kijana zingatia mambo yafuatayo kabla ya kufanya tendo la ndoa kabla
ya ndoa, itakusaidia sana. Mwanzo 2:15 “Bwana Mungu akamtwaa
huyo mtu, akamweka katika bustani ya Edeni, ailime na kuitunza.”
maneno haya yanamaanisha kuwa;
(a)Kijana kaa Edeni (Edeni maana yake ni uweponi mwa Mungu). kabla
ya kumwomba Mungu mme au mke mwema ni lazima na wewe uwe
sahihi(mwema).
(b)Kijana fanyakazi Kwa bidii. Mungu alimwagiza Adamu afanye kazi
pale bustanini haijalishi kulikuwa na matunda ya kila namna. Mungu
anaposema"ailime" alikuwa anamaanisha kwamba ni lazima afanye kazi
sio kukaa tu.
(c)Kijana jitunze vizuri. Tunza utakatifu ili watu au Mungu asiwe na
maswali juu yak, ili watu wakikusingizia wakose ushahidi wowote wa
uwongo, bali wamtukuze Mungu kupitia wewe.
ii. Uchafu.
Ni hali ya kitu au binadamu kuwa najisi au haramu. Yuda 2:8
“Kadhalika na hawa, katika kuota kwao, huutia mwili uchafu, hukataa
kutawaliwa, na kuyatukana matukufu."
iii. Ufisadi.
Ufisadi(rushwa) ni kitendo cha utakatishaji mali za Umma. Au Ufisadi ni
matumizi mabaya ya mali za umma kwa manufaa binafsi ya mtu. Hii
inatokana na kutokuridhika na kile ambacho mtu huyu anakipata, hana

18
kabisa roho ya kuridhika haijalishi wengine hawana hata kidogo, lakini
yeye anajilimbikizia mali bila hata kuwa na huruma kwa wengine.
Hosea 5:2 “Nao walioasi wameongeza sana ufisadi wao; lakini mimi
ndiye awakaripiaye wote pia."

iv. Ibada ya sanamu.


Sanamu ni mfano wa kitu chochote, kitu halisi au cha kuwaziwa,
ambacho huenda kikatumiwa na watu katika ibada. kuabudu sanamu ni
chukizo kwa Mungu. Mungu alimpa Musa mtumishi wake amri ili wana
wa Israeli waenende kulingana na amri hizo.
Kutoka 20:4 "⁴ Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho
chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho
majini chini ya dunia."
Ibada ya sanamu kwa namna nyingine ni kile kitendo cha mwanadamu
kukipa kitu kingine nafasi ya kwanza kuliko Mungu. Mfano watu wengi
yamkini mpaka waKristo wamejitengenezea au wamejifanyia miungu
wanayoiabudu kwa siri bila ya wao kujua, kama vile kumpenda zaidi
mke/ mme, watoto, kazi, na vitu kuliko kumpa Mungu nafasi ya kwanza
ndani ya mioyo yao. Soma Mathayo15:8.
 Lakini ikumbukwe kuwa wakati Mungu anamuumba mwanadamu
alimwekea vitu kadha wa kadha ndani ya roho yake vikiwemo vitu hivi
viwili;
(a)Roho ya ibada. Roho ya ibada hapa inamaanisha kuwa kila
mwanadamu ndani ya roho yake amewekewa roho ya ibada yaani lazima

19
tu atamwabudu Mungu, na asipo mwabudu Mungu wa Mbinguni basi
ataabudu miungu mingine. Hata wewe mwenyewe ni mashahidi kabisa
huko kwenu wanadamu ambao hawaendi kanisani, kwa waganga wa
kienyeji au mizimu ya ukoo wanaenda, na hii ni kwasababu ndani ya
roho zao Mungu ameweka sehemu ya ibada. Ni heri kumwabudu Mungu
wa mbinguni.
(b)Roho ya uhuru wa kuchagua. Hapa inamaanisha kuwa kila
mwanadamu anauhuru wa kuchagua kufanya anachotaka lakini tu
asivunje sheria za nchi. Ni heri uchaguzi wako ukawa mwema wa
kumtumikia Yesu Kristo.
Yoshua 24:15 “Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana,
chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba
zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale
Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu
tutamtumikia Bwana.”

v. Uchawi.
Ni kitendo chochote cha kutafuta msaada wa rohoni au mwilini kwa
kupitia nguvu nyingine mbali na nguvu za Mungu, Biblia inakiita
Uchawi. Na ni wazi kuwa hakuna nguvu nyingine iliyo kinyume na
Mungu zaidi ya nguvu za shetani, Na uchawi kwa ujumla umebeba
mambo mengi yakiwemo, kuloga, kuagua, kutazama utabiri wa nyota,
kubashiri, kusihiri, kuabudu sanamu, hata kuamini baadhi ya movie au

20
magemu ambayo yanatoa maagizo fulani kukuaminisha kuwa unaweza
kupata maelekezo ya maisha yako mbali na nguvu za Mungu ni uchawi.
Japo baadhi ya serikali hapa Duniani haziamini juu ya uwepo wa uchawi
lakini uchawi upo na unatesa sana watu ambao hawajamwamini Bwana
Yesu Kristo na kuamini yakuwa alidhihirishwa ili azivunje kazi za
shetani.
Dhambi ya uchawi inafananishwa na dhambi ya uasi ukisoma kitabu cha
samweli.
1 Samweli 15:23 "²³ Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, Na ukaidi
ni kama ukafiri na vinyago; Kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye
naye amekukataa wewe usiwe mfalme."
vi. Uadui.
Ni uhasama kati ya mtu na mtu au kikundi kimoja na kingine, kabila
moja na lingine, au taifa moja na jingine. Mwanzo 3:15“nami nitaweka
uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake;
huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.”

vii. Ugomvi.
Ni hali ya kutokuelewana kati ya pande mbili au zaidi. Unajaribu
kupanda miiba kwenye njia yangu ipo siku utakuja kwangu kupitia hiyo
hiyo njia na ukiwa huna viatu, na hiyo hiyo miiba uliyoipanda
mwenyewe ndiyo itakayo kuchoma mwenyewe. Mithali 17:14,19 "¹⁴
Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi

21
kabla haujafurika. … ¹⁹ Apendaye ugomvi hupenda dhambi; Auinuaye
sana mlango wake hutafuta uharibifu."
viii. Wivu.
Ni kile kitendo cha kutokufurahia maendeleo ya mtu au watu wengine.
Asiyekufaa, anamfaa mtu mwingine, unaemwona hana maana kwako
atakuwa na maana Kwa wengine, ikiwa mmekosana ni wewe sio
kwamba akosane na kila mtu.
Mithali 27:4“Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani
awezaye kusimama mbele ya wivu.”
ix. Hasira.
Ni hisia iletayo matokeo hasi au mabaya kwa kitu au mtu mwingine,
watu wengine. Mithali 15:18 “Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali
asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.”
x. Fitina.
Fitina ni kile kitendo cha mtu kumchonganisha au kumsemea ubaya mtu
kwa mtu mwingine. Mithali 18:6“Midomo ya mpumbavu huingia katika
fitina, Na kinywa chake huita mapigo.”
xi. Faraka.
Faraka ni matengano, kubaguana kati ya ndugu, mtu mmoja na
mwingine, jamii moja na nyingine au taifa moja na lingine.1 Wakorintho
11:18“Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka
kwenu; nami nusu nasadiki;”
xii. Uzushi.

22
Ni uvumi wa maneno yasiyo halali yanayoenezwa na mtu au watu kwa
lengo la kumsema au kumchafua mtu, watu, taasisi, au serikali. Warumi
1:21“kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye
Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo
yao yenye ujinga ikatiwa giza.”
xiii. Husuda.
Husuda ni chuki, jicho baya, uadui au wivu. Mithali 28:22 “Mwenye
husuda afanya haraka kuwa tajiri; Wala haufikiri uhitaji utakaomjilia.”
xiv. Ulevi.
Ni hali ya mwanadamu kutumia kinywaji au vinywaji vikali,
vinavyompelekea kutokujielewa na kumfanya kuwa katika hali isiyo ya
kawaida. Mhubiri 10:17 “Heri kwako, nchi, mfalme wako akiwa mtoto
wa watu, Na wakuu wako hula wakati ufaao, Ili makusudi wapate nguvu,
wala si kwa ajili ya ulevi.”
xv. Uzinzi.
Ni ngono inayofanywa kwa hiari kati ya mwanaume aliyeoa na
mwanamke ambae sio mke wake, au kati ya mwanamke ambaye si mme
wake. Mathayo 5:27.

23
SEHEMU YA NNE
ROHO MTAKATIFU
Unabii wa ujio wa Roho Mtakatifu.
Kabla Roho Mtakatifu hajamiminwa kwa wote wenye mwili duniani, Mungu
aliwajulisha watumishi wake manabii juu ya ujio wa Roho Mtakatifu,
kwasababu Mungu huwa hatendi jambo lolote Duniani bila kuwajulisha
watumishi wake, lakini ikumbukwe kuwa hata hapo zamani Roho Mtakatifu
alikuwa anafanya kazi yake kwa nafasi yake lakini muda wake mwafaka
ulikuwa bado haujadhihirika waziwazi kwa wanadamu unaweza ukasema
ninamaanisha nini , ninamaanisha kuwa kipindi cha Agano la kale, Nafsi ya
Mungu Baba ndiyo iliyokuwa inatenda kazi.Lakini Mungu ni mwema
aliwamiminia wanadamu wachache tu Roho Mtakatifu, kwanjia ya kupakwa
mafuta wakiwemo manabii,waamuzi na wafalme mfano mfalme Sauli,
Mfalme Daudi.
Yoeli 2:28-29. "²⁸ Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho
yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri,
wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;²⁹ tena juu ya
watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho
yangu."

Hebu soma vizuri mchanganuo wa Nafsi za Mungu katika utendaji wa kazi


zake na kwa muda wake huu hapa chini.
 Mungu Baba alijulikana wakati wa Uumbaji wa mwanadamu. Mwanzo
1:1 " Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi"

24
 Mungu Mwana alijulikana wakati wa Ukombozi wa mwanadamu.
Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa mwanawe wa pekee ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na
uzima wa milele". Soma pia 1 Yohana 4 :14-15.
 Mungu Roho Mtakatifu alijulikana mara baada ya Yesu Kristo kupaa
kwenda mbinguni kwa Baba. Matendo ya mitume 2:1

Hatutajadili sana nafsi zile mbili (Mungu Baba, na Mungu mwana) lakini
tutajikita sana katika nafsi ya "Mungu Roho Mtakatifu."
Roho Mtakatifu ni nani?
Roho Mtakatifu ni Nafsi ya tatu ya Mungu wetu. Mungu ana nafsi tatu
ambazo ni, Mungu Baba, Mungu Mwana, na Mungu Roho Mtakatifu; nao
katika utatu wao ni Mungu mmoja tu.1 Yohana 5:8 “Kwa maana wako watatu
washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa
ni umoja." Hapa neno “Baba" Biblia inamaanisha Mungu Baba, "Neno" ni
Yesu Kristo (Mungu mwana), na Roho Mtakatifu.

Kipindi Mungu anamuumba mwanadamu, alimuumba kwanza


Adamu"roho"(Mungu ni Roho na Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu.
Kitabu Cha mwanzo 1:26 ‘...Na tumfanye mtu kwa mfano wetu na sura
yetu....’ ndipo Adamu roho akaumbwa),Kisha Adamu "mwili" (kwa
mavumbi ya ardhi) lakini mwili na roho zimepingana tangu mwanzo, ndipo
Mungu alimuumba "Adamu nafsi" ili kuunganisha mwili na roho kwa
pamoja, ndipo Adamu akawa nafsi hai; sawasawa na Nafsi tatu za Mungu. Na
ukiondoa au ukitenganisha kitu kimoja na vile vingine jina litabadilika na

25
kuwa jina jingine, ndiyo maana Mwili na roho vinapotengana (akifariki Dunia)
watu husema"tunaenda kuuzika mwili wa marehemu" Swali la kujiuliza
huyo marehemu Kaenda wapi? Mathayo1:18, 1:20, 3:11, 28:19, Rumi9:1,
14:17, 15:16, 1Korintho 6:19, 12:3, Efeso 4:30.

Ahadi ya Bwana Yesu Kristo kuhusu ujio wa Roho Mtakatifu.


Wakati Bwana Yesu akiwa bado hajaondoka majini (Mto Yordani) kubatizwa
na Yohana Mbatizaji, Roho Mtakatifu alimshukia kwa umbo la Hua au njiwa.
Na ni kwanini Roho Mtakatifu alimshukia Yesu kwa umbo la njiwa? Ni
kwasababu Yesu Kristo hakuzaliwa katika hali ya uchafu wala dhambi yeyote
(Luka 1: 35).
 Sifa tano za Hua/njiwa.

i.Njiwa ni msafi na pia hapendi kutua kwenye vitu vichafu.


ii.Njiwa ni mpole kuliko ndege wote (sio mgomvi).
iii.Njiwa huangalia kwa jicho moja Kwa umakini mkubwa.
iv.Njiwa ana mke au mme mmoja tu yaani sio kahaba.
v.Njiwa ana kasi kubwa ya kupaa angani.
Yohana 14 :16-18 "¹⁶ Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi
mwingine, ili akae nanyi hata milele; ¹⁷ ndiye Roho wa kweli; ambaye
ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali
ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.; ¹⁸
Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu."
Tunaona hapo kuwa wakati Bwana Yesu akiwa anamalizia huduma au kazi
yake Duniani aliwaambia wanafunzi wake wazi wazi kuwa hana budi kupatwa

26
na mateso mengi, kuuawa, kufufuka na kurudi kwa Baba, lakini wao
hawakuelewa, na akawaambia kuwa hato waacha yatima bali atamwomba
Baba ili awape msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu.

Hata sasa Roho Mtakatifu yupo Duniani ili kila mwenye uhitaji wa kumpata,
ajazwe nae. Roho Mtakatifu ndiye nguvu yetu, atusaidiaye kuweza kuuteka
ufalme wa Mungu.Matendo ya mitume 2:39 "Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili
yenu na watoto wenu, na kwa wote walio mbali, na kila mtu ambaye Bwana
Mungu wetu atamwita amjie."

Sababu ambazo Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake wakae kwanza


mjini Yerusalemu.
(a) Wasingeweza kuwa mashahidi wa kweli na waaminifu, kuhusu habari za
Bwana Yesu mpaka wajazwe Roho Mtakatifu na nguvu zake. Yohana 16:12-
15
(b) Kuwekwa wakfu katika maisha yao.1Samweli 16:13. maana Roho
Mtakatifu ni mafuta na utambulisho hata siku ya ukombizi.

Ahadi ya Bwana Yesu Kwa wanafunzi wake ilitimizwa mara baada ya siku ya
Hamsini baada ya Yesu Kristo kufufuka katika wafu, lakini ilikuwa ni siku ya
kumi baada ya Yesu Kristo kupaa kwenda mbinguni Kwa Baba, kwahiyo ni
siku kumi tu ambazo mitume walikaa bila Bwana Yesu Kristo, Ndiposa Roho
Mtakatifu akashuka kwa wanafunzi wa Bwana Yesu siku ile ya sikukuu ya
mavuno (yaani siku ya Pentekoste).

27
Taifa la Israeli huazimisha sikukuu zaidi ya kumi na moja Kila mwaka, ndiyo
maana unaweza ukashangaa kwamba ujio wa Roho Mtakatifu alikuja siku ya
sikukuu ya mavuno yaani Pentekoste, hebu tuzione hapo chini sikukuu hizo.
1.Sikukuu ya Majuma. Sikukuu hii husherehekewa na wana wa Israeli na
hairuhusiwi kuteka mateka na kwenda mwendo mrefu, siku ya sikukuu
hiyo.2Nyakati 8:13.
2.Sikukuu ya Pasaka. Ni sherehe ya kuazimisha ukombozi wa Waisraeli
kutoka misri. sherehe hii hufanywa Kila mwaka mwezi wa Abibu, na
iliazimishwa kwa kuchinja mwanakondoo (au mbuzi), na kumla kwa mboga
chungu na mikate isiyo na chachu. Kumb 16:1
Swali: Kwanini Wana wa Israeli walimuhifadhi mwana-kondoo siku nne
kabla ya kuchinjwa katika sikukuu ya pasaka. Je, Kuna ufunuo gani tunaweza
kupata katika tendo hilo? (Kutoka 12:6)
Jibu: Mungu aliwapa agizo la kuwatenga wana-kondoo Kutoka katika kundi
siku ya 10, Kisha siku ya 14 kuchinja. Maana yake ni kuwa sadaka/dhabihu
yao, ilipaswa itambulike mapema Kisha ikatengwa. Kama wangekaidi agizo
hilo na kuchagua mwanakondoo siku ile ile ya kuchinja au hata siku moja
kabla ilikuwa ni kosa mbele za Mungu.
Je! nakwetu sisi leo jambo hili linafunua nini?
Na sisi pia Bwana anapendezwa na dhahibu zenye maandalizi, ambazo
zimetengwa mapema. Mfano unapokwenda ibadani jijengee desturi ya
kumwandalia Mungu sadaka zako mapema na ikiwezekena siku kadhaa kabla.
Kwa jinsi unavyoandaa mapema ndivyo inavyokuwa na utukufu mwingi zaidi.

28
Lakini pia Unahakikisha unaitenga kabisa na hesabu zako nyingine (yaani
haiguswi), mpaka siku ya kumtolea. Hiyo itaifanya sadaka yako ipokelewe
Kwa furaha na Mungu, kuliko kufikiria kumtolea Mungu muda huo huo
wakati ulikuwa na nafasi ya kufanya maandalizi. Ndio ufunuo ulio nyuma ya
agizo hilo la Pasaka.
3. Sikukuu ya Pentekoste. ni sikukuu ya mavuno. ndiyo siku ambayo Roho
Mtakatifu alishuka Kwa mitume kumi na mmoja pamoja na wanafunzi
wengine wa Yesu Kristo waliokuwa nao siku ile. Matendo ya Mitume 2:1.
4. Sikukuu ya vibanda. iliitwa pia sherehe ya mahema, au sherehe ya
kukusanya. sherehe hii husherekewa mwezi wa Ethanimu (yaani mwezi wa
Saba). Mambo ya walawi 23:34.
5. Sikukuu ya Upatanisho au maungamo. Nehemia 10:33.
6. Sikukuu ya mwandamo wa mwezi (Mwandamo ni tendo la kufuatana
mwezi. Mwandamo ni mwezi mpya, ndio kwanza uonekane). Zaburi 81:3
“Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Wakati wa mbalamwezi, sikukuu yetu."
7. Sikukuu ya Tarumbeta. Hii ni sikukuu ya furaha ya wana wa Israeli kwa
Mungu.Hesabu 10:10.
8.Sikukuu ya kutabaruku. Yohana 10:22 “Basi huko Yerusalemu ilikuwa
Sikukuu ya Kutabaruku; ni wakati wa baridi."
9.Sikukuu ya kupelekeana zawadi.ni sherehe ambayo ilikuwa ikisherehekewa
na wayahudi dhidi ya ushindi walioupata kuhusu kuangamizwa na Hamani.
Esta 9:19.

29
10. Sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu. (Chachu ni hamira, kitu kitumiwacho
kuchachusha, au kuumua unga. Au Chachu ni kitu kinachoumusha unga).
Kutoka 34:18.
11.Sikukuu ya Purimu. Sherehe hii huazimishwa ili kukumbuka jinsi
wayahudi walivyokombolewa ili wasiangamizwe siku za malkia Esta.sherehe
hii iliazimishwa mwezi wa Adari (mwezi wa kumi na mbili). Neno "purimu"
humaanisha "kura". Esta 3:7

Viwango vikuu vitatu vya kujaa Roho Mtakatifu


Luka11:13 “Basi, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu
vipawa vyema, je! Baba aliye mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu
hao wamwombao?" Hii inamaanisha kuwa juhudi au bidii binafsi za mtu za
kumtafuta Mungu ndizo zinazomfanya mtu aongezewa viwango vya Roho
Mtakatifu kujaa ndani yake, hapa chini ni viwango vikuu vitatu vya kujaa
Roho Mtakatifu kwa mwamini.
1.Kujaa Roho Mtakatifu
Hiki ni kiwango cha kwanza cha kujaa Roho Mtakatifu kwa mwamini,
kiwango hiki huleta mabadiliko kwa mtu aliyeokoka kwa mara ya kwanza
alipokuwa mtupu yaani hajajazwa Roho Mtakatifu. Lakini pia hiki ni kiwango
cha kupokea au kupata Lugha mpya. Matendo ya Mitume 1:8“Lakini
mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa
mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na
hata mwisho wa nchi.”

30
Picha hapo juu ni glasi iliyo na maji, mfano unaoonesha jinsi mwamini
anapojazwa Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza, na inaoonesha kuwa bado
haijajaa zaidi kwasababu mwamini bado haja zama zaidi kuutafuta uso wa
Mungu.

2.Kufurika Roho Mtakatifu


Hiki ni kiwango cha pili cha ujazo wa Roho Mtakatifu kwa mwamini,
kiwango hiki kina kusudi la mtu kujijenga ndani yake ili kutengeneza ndani
yake. Na kazi zake ni kuvunja vunja tamaa mbalimbali za mwili za
mwanadamu ili aishi maisha matakatifu. Haleluya! Rumi 8:26“Kadhalika
Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi
itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza
kutamkwa."

31
Picha hapo juu ni glasi ya maji, mfano wa mwamini ambaye amejazwa kabisa
Roho Mtakatifu lakini bado haja batizwa.

3.Kubatizwa na Roho Mtakatifu


Hiki ni kiwango cha juu sana cha kujaa Roho Mtakatifu, ambacho Kila
mwamini anatakiwa abatizwe Roho Mtakatifu, kwasababu kiwango hiki
kinafanya kazi Kwa watu waliozama rohoni sana. Matendo ya Mitume 1:5 “ya
kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho
Mtakatifu baada ya siku hizi chache.”
Kiwango hiki kinapotokea kwa mtu, mtu huyu hupokea karama za rohoni,
kikiambatana na kazi zifuatazo.
i. kufurika nguvu ya Mungu ndani ya mtu.
ii. kukuonesha siri mbalimbali kutoka Kwa Mungu.

32
iii. kubomoa kazi za shetani.
iv. Kinaleta faraja Kwa mtu. Matendo ya mitume 7:60 "Akapiga magoti,
akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema
haya akalala. Na Sauli alikuwa akiona vema kwa kuuawa kwake."

Picha hii ya glasi ya maji inatuonyesha mfano wa mwamini ambaye


amebatizwa na Roho Mtakatifu yaani yuko katika bubujiko lisilo la kawaida,
mtu huyu yuko karibu sana na Mungu.

Kiashiria cha mtu aliye jazwa na Roho Mtakatifu ni kunena kwa lugha mpya,
lakini kunena kwa lugha mpya kumegawanyika katika sehemu kuu mbili
ambazo; - kunena kwa lugha za wanadamu, na kunena kwa lugha za
malaika yaani za mbinguni.
(a) Kunena kwa lugha za wanadamu: Ni lugha ya ki-Ungu katika lugha
usiyoijua, katika sauti ambayo haijulikani kwa yule anenaye. Roho Mtakatifu
humjalia mtu kutamka maneno ambayo nabii au mtumishi wa Mungu
mwingine anaweza kutafisri lugha hiyo. mfano mzuri ni ili siku ya Pentekoste

33
mitume walinena kwa lugha tofautitofauti kutokana na Roho Mtakatifu alivyo
wajalia kutamka.
Matendo ya mitume 2:3-4 "³ Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama
ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. ⁴ Wote wakajazwa Roho Mtakatifu,
wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka."
(b)Kunena Kwa lugha za malaika au mbinguni: Hii ni lugha ya ki-Ungu
katika lugha usiyoijua katika sauti ambayo ni ngumu kuilelewa. Roko
Mtakatifu humsaidia mtu kunena lugha ya mbinguni ambayo mwanadamu au
kiumbe yeyote hawezi kuielewa, kwasababu lugha hiyo haiwezi kutambuliwa
na mwanadamu yeyote, awe nabii, awe shetani au hata mtu yule anaye nena
lugha hiyo hawezi kujua anaomba nini lakini ndani moyo wake hujisikia
bubujiko tamu mno, isipokiwa wakutambua lugha hiyo ni Mungu pamoja na
Malaika . Warumi 8:26 "Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa
maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea
kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.” Haleluya!

34
SEHEMU YA TANO
MATUNDA YA ROHO MTAKATIFU

Hatuwezi jambo lolote kwa nguvu zetu kwa kuwa hatuna cha kujivunia bila
Yesu Kristo. Tunapiganiwa na Mungu ili tuishi ndani ya Yesu Kristo na Yesu
Kristo ndiye nguvu yetu. Na Bwana Yesu alisema kwamba hatatuacha yatima,
bali atamwomba Baba yake amtume msaidizi(Roho Mtakatifu) atakaye ishi
nasi milele. Hili alisema Yesu Kristo ili tusiwe na woga. Maana uwoga ni adui
wa roho yako.

Mpango wa Mungu kukufikisha mahali pa utulivu na kustarehe haizuiliwi na


jinsi ulivyoanza safari au hali uliyonayo kwa sasa. Mungu anaweza kufanya
jambo jipya muda wowote kwako. Haijalishi ulianza kwa ugumu kiasi gani au
vizuri namna gani na sasa hali ikoje. Mungu hamuachi mtumishi wake
atembee peke yake. Unapohisi upweke ndani yako kumbuka kuwa una Yesu
Kristo asiyemuacha mtu yeyote. Fukuza roho ya hofu maana haitoki kwa
Mungu.

Matunda ya Roho Mtakatifu; ni mazao au matendo tisa ya Roho Mtakatifu


ambayo yanatokana na Mungu mwenyewe kwa mwamini ili aishi katika
mapenzi ya Mungu wala sio katika mapenzi ya mwanadamu.matunda ya Roho
Mtakatifu ni matendo yanayodhihirisha uweza na uwepo wa nguvu za Mungu
ndani ya mtu au mwamini kwasababu Roho Mtakatifu humshudia mtu mambo
yampasayo kufanya na mambo gani yampasayo kuepuka ili aweze kufanya
mapenzi ya Mungu , haijalishi mapenzi ya mtu huyu hayafanyiki au

35
hayatendeki. Neno la Mungu linatuambia kuwa wanaoongozwa na Roho hao
ndio wana wa Mungu, hii inamaanisha kuwa mtu akiwa na Roho Mtakatifu
yaani Roho wa Mungu anamhuri wa Mungu hata siku ya ukombozi. Efeso
4:30 “Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye
mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi."
Kumbe siku ya ukombozi wetu Roho Mtakatifu atakuwa ni shahidi wa mtu
kunyakuliwa (kwa yule atakayekutwa hai), lakini kwa yule ambaye atakuwa
amelala mautini kwasababu alikuwa na Roho Mtakatifu, Roho Mtakatifu
atafanyika kama Sumaku yaani kiunganishi kati ya mtu na Bwana Yesu Kristo
mawinguni.
Mwanadamu alapo matunda ya kawaida, afya yake huwa nzuri kiasi kwamba
Kinga ya mwili wake huwa nzuri. Matabibu, wauguzi na wataalamu wa
masuala ya afya wanashauri kwamba katika kila mlo wowote ni lazima ule
matunda (chakula na matunda), sio chakula pekee, maana katika matunda
kuna virutubisho mbalimbali vinavyojenga na kulinda mwili dhidi ya
magonjwa mbalimbali; kwa mantiki hiyo sasa mwamini anatakiwa awe na
Roho Mtakatifu sawasawa ili afya yake ya kiroho iimarike.

Nimekuonesha Viwango vitatu vya ujazo wa Roho Mtakatifu kwa mwamini,


hivyo mtu anatakiwa ajazwe ujazo wa Roho Mtakatifu katika Viwango vya juu
sana yaani "Kufurika Roho Mtakatifu" ili aimalike katika maisha yake, hii
itamsaidia atambue Huduma, karama na vipawa ambavyo amepewa na Mungu
na ni namna gani ya kuliishi kusudi la Mungu ndani yake maana

36
asipolitambua kusudi la Mungu ndani yake itakuwa ni ngumu sana mtu huyu
kumpendeza Mungu.
Kila kazi ya mwanadamu itapimwa katika moto siku ya mwisho, hivyo kama
uliishi katika mapenzi ya Mungu yaani Roho Mtakatifu kazi yako itang'ara
sana, lakini kama hukuijua na kulifanya kusudi la Mungu ndani yako kupitia
uongozi wa Roho Mtakatifu kazi yako itateketea katika moto, japo mimi
sikuhukumu bali nakukumbusha tu.Ni maomba yangu kwa Mungu akupe
kujua kusudi lake ndani yako ili uweze kuyafanya mapenzi ya Mungu ndani
yako. Haleluya!
Bwana Yesu Kristo alikuja Duniani si kumkomboa tu mwanadamu na
kumwacha, bali alikuja kurejesha Ushirika (ulikuwa umevunjuka) na
uhusiano (ulikuwa umepungua) uliokuwepo hapo mwanzo kati ya Mungu
na mwanadamu kabla ya anguko la mwanadamu, lakini Yesu Kristo
alimwomba Mungu Baba amtume Roho Mtakatifu baada ya yeye (Yesu
Kristo) kurudi mbinguni ili ushirika na uhusiano aliourejesha kati ya Mungu
na mwanadamu usivunjike na kupungua tena.

Uhusiano ni nini?
Uhusiano ni hali ya kuwa na kiunganishi kati ya mtu na mtu, mtu na kitu
/Jambo/ shirika fulani. Uhusiano huo unaweza kuwa wa damu(ndugu), urafiki,
kikazi au kimapenzi.
Baada ya anguko la mwanadamu uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu
ulipungua, japo Adamu alibaki kuwa kiumbe aliyeumbwa na Mungu (Mungu
ni wa wote wenye mwili). Mfano mtoto akifukuzwa na Baba yake haimaanishi

37
kuwa mtoto huyo ndio amepoteza na jina la ukoo, yaani jina la ubini
wake(Babaye), hapana, bali majina yake hayatabadilika kamwe na kuitwa jina
la Baba mwingine.
Nini maana ya Ushirika?
Ushirika ni hali ya kuwa na umoja na ushirikiano kati ya watu au makundi
mbalimbali yenye malengo na maslahi yanayofanana. Ni hali ya watu
kuungana pamoja kwa ajili ya kufanikisha jambo fulani.
Mungu alikuwa na desturi kila siku ya kumtembelea Adamu pale Bustani ya
Edeni baada ya jua kupunga, lakini ushirika huu ulivunjika tu pale ambapo
Adamu alipotenda dhambi ndipo ushirika ukavunjika, na Mungu akamwacha
mwanadamu kwasababu ya dhambi zake maana Mungu ni mtakatifu na
hachangamani na dhambi, hivyo Bwana Yesu Kristo akaja kuurudisha tena.
Ushirika unahusisha kujenga mahusiano ya karibu kati ya watu au makundi
mbalimbali, kushirikishana mawazo na rasilimali, kuchangia kwa pamoja
kufikia malengo ya pamoja, na kusaidiana katika kufanikisha shughuli
mbalimbali. Ushirika unaweza kuwa chanzo cha mafanikio makubwa katika
kufikia malengo au kutekeleza shughuli mbalimbali.

38
SEHEMU YA SITA
MATUNDA TISA YA ROHO MTAKATIFU

Tumeumbwa kuishi na kuyatimiza yale ambayo Mungu amekusudia sisi


tuyafanye kwa uangalizi maalumu wa Roho Mtakatifu. Usiipuuze sauti
inayokuita kutenda jambo lolote lililo jema la kumpendeza Mungu maana
Roho Mtakatifu husema nasi kwa sauti ya upole. Umewekwa mahali
kuwahudumia wengine kwa vitu ambavyo Mungu ameweka ndani yako,
maana vitu ulivyopewa na Mungu siyo kwa ajili yako tu bali pia na watu
wengine. Usipuuze wala usidharau kufanya jambo linalompa utukufu Mungu.
Tumia karama uliyopewa na Mungu.

Wagalatia 5:22-23 "²² Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani,


uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, ²³ upole, kiasi; juu ya mambo kama
hayo hakuna sheria."

1.Upendo.
Upendo ni neno linalotumika kwa maana mbalimbali kuanzia hali ya nafsi ya
binadamu hadi kwa Mungu. Linatokana na kitenzi "kupenda" na kufanana na
pendo, mapendo, mapenzi.
Upendo ni amri mpya, pia kuu ambayo Bwana Yesu ametupatia kanisa lake.
amri hii hujumuisha amri zote kwasababu Upendo humfanya mtu kuthamini
vitu vya watu wengine zaidi ya vitu vyake, huu ndiyo Upendo ambao Bwana

39
Yesu aliuzungumzia, maana Mungu ni"Upendo". ukisoma kitabu cha 1Yohana
4:8 kinasema kuwa "Mungu ni upendo.”
Yohana 13:34-35 "³⁴ Amri mpya nawapa, Mpe ndane. Kama vile
nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. ³⁵ Hivyo watu wote
watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo
ninyi kwa ninyi."
1 Wakorintho 13:1-3 “¹ Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika,
kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. ² Tena
nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na
imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu
mimi. ³ Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili
wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

Upendo ni mojawapo ya hisia zenye nguvu tunazoweza kuziona. Wanadamu


wanatamani upendo kutoka kwa watu wengine ili wajisikie kuthaminiwa,
kuheshimiwa na kukubaliwa.
Hivyo Upendo ni mtihani wa kweli wa imani ya kweli, ndiyo maana Bwana
Yesu alisema "mtu amchukiaye ndugu yake mtu huyo ni muuaji kama wauaji
wengine.
1 Yohana 3:15 “Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya
kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake.”

40
Aina Saba za Upendo katika Biblia Takatifu.
Hapa tutaziona aina Saba za Upendo katika Biblia, pamoja na asili zake kwa
njia ya maneno saba ya Kigiriki haya yafuatayo; Eros, Storge, Philia, Agape,
Philautia, Pragma, na Mania. Maneno haya yakiwa na maana ya; upendo wa
kimapenzi, upendo wa familia, upendo wa ndugu, upendo wa Mungu, Upendo
wa kujipenda binafsi, Upendo wa kudumu, na Upendo wakuzingatia. Kama
tunavyofanya, tutaona nini upendo unamaanisha, na jinsi ya kufuata amri ya
Yesu Kristo ya "kupendana."
(i) Upendo wa Kimapenzi (Eros) ni nini?
Upendo wa kimapenzi huu ni upendo unaokuwa kati ya watu fulani
kusababisha watu hao kuwa na uhusiano wa kimapenzi kati yao. Kwa
utaratibu wa Mungu na jamii zilizo sawa sawa, Eros ni aina ya upendo
unaotakiwa kuwa kati ya watu wenye uhusiano wa ki-ndoa, yaani mtu mke na
mume au kati ya watu wanaoelekea katika uhusiano wa ki-ndoa wa mume na
mke. Aina zote za upendo zinahusisha moyo (nafsi) wa mtu, lakini Eros huwa
na sifa ya kuwa na hisia zenye nguvu zaidi toka moyoni kuliko aina zingine
zote za upendo. Eros ni aina ya upendo wenye nguvu kali sana ya hisia za
binadamu.
Upendo wa kimapenzi Biblia pia inausema kuwa, Upendo huu una nguvu
kama mauti. Jaribu kufikiria Upendo wa kimapenzi unafananishwa na mauti
au kifo, wakati mauti au kifo hakizoeleki, kinaogopesha na kinatisha watu
wengi, lakini Upendo ndiyo unafananishwa na mauti aseee! ni hatari sana.
Wimbo ulio Bora 8:6 “Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu
ya mkono wako; Kwa maana upendo una nguvu kama mauti, Na wivu ni

41
mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya
Yahu.
Mfano; Upendo wa Yakobo kwa Raheli. Mwanzo 29:10-30
Yakobo alipomkimbia kaka yake Esau, baada ya kuchukua haki ya uzaliwa wa
kwanza, alikimbilia nchi ya mbali, kwa mjomba wake Labani (Labani alikuwa
ni kaka yake na Rebeka) Labani alikuwa na binti wawili, mkubwa aliitwa Lea
na mdogo aliitwa Raheli. Biblia inasema Lea alikuwa na macho mazito au
makengeza, yaani ukimwangalia, utadhani amelala hivi, kumbe ndio anakuona
vizuri. Na Raheli alikuwa na umbo zuri la mwili na sura nzuri ya usoni. Hivyo
Yakobo alimpenda Raheli. Labani akamwabia Yakobo atumike kuchunga
wanyama wake kwa muda wa miaka saba (kama mahari), ndipo atampa Raheli
kuwa mke wake. Yakobo akapendezwa na hilo, na akakubali kutumika na
kufanya kazi za Labani kwa muda wa miaka yote saba ili ampate Raheli. Na
Neno la Mungu linasema, kwa jinsi Yakobo alivyompenda Raheli (kwa Eros -
kimapenzi kuwa mke wake), alifanya kazi kwa bidii kiasi kwamba, ile miaka
saba ilionekana michache sana.
Dalili na sifa za Upendo wa Kimapenzi.
✓Kukaa mawazoni kwa mtu anayependa.

✓Shauku kubwa ya kuwa pamoja kila wakati.

✓Heshima kubwa kwa mtu apendwae


✓Kumjali na kumtanguliza mtu apendwae.

✓Zawadi na gharama kwa mtu apemdwae.

42
✓Furaha na Amani kutawala moyoni.

(ii) Upendo wa Kifamilia (Storge) ni nini?


Upendo wa familia ni dhamana ya upendo ambayo inaendelea kwa kawaida
kati ya wazazi na watoto, ndugu, kaka na dada, Mjomba, shangazi. Mifano
mingi ya Upendo wa kifamilia zinapatikana katika Biblia Takatifu, mfano
upendo wa Yakobo kwa ajili ya wanawe, Martha na Mariamu walikuwa na
Upendo kwa ndugu yao Lazaro.
2 Wathesalonike 1:3 “Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa
ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upendo
wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi.”
Mfano; Upendo wa Baba kwa Mwana mpotevu. Luka 15:11-32
Tunasoma jinsi mwana huyu mdogo wa baba tajiri alivyoomba sehemu ya
urithi wa mali zake, kisha kwenda nchi ya mbali ili kuishi huko. Lakini Neno
la Mungu linaeleza jinsi kijana huyo alivyovutwa na dunia na kuharibu mtaji
wake wote wa mali alizopewa na babaye. kijana huyu alijiingiza katika anasa
za dunia na mwishowe alifilisika kabisa mali zote. Baada ya muda wa
mahangaiko alipata kibarua cha kulisha nguruwe wa mtu mmoja. Hali yake ya
kimaisha ilikuwa mbaya sana hata akatamani kula chakula cha nguruwe.
Lakini akakumbuka kuwa kwanini anateseka wakati kule kwao, baba yake ana
watumishi wanaokula vizuri kuliko anavyokula yeye, ndipo alipoamua kurudi
nyumbani kwao kwenda kuomba msamaha. Kwa hali ya mzazi wa kawaida,
kijana huyu alistahili kupewa adhabu kali sana; lakini kinyume chake, baba
yake mzazi alipomwona anakuja kwa mbali kwanza alifurahi, na alimpokea

43
kwa shangwe na furaha. Akamvika na mavazi mazuri, akamchinjia ndama
aliyenona na kumfanyia karamu kubwa ya kufana. Hiyo ni nguvu ya upendo
wa kindugu. Japo alichofanya mwana mpotevu si cha kupendeza, lakini nguvu
ya upendo wa kindugu inaweza kufunika uovu wote uliotendwa na ndugu
yenu. Watu wanaweza kuamua kusamehe au kufumbia macho makosa
yaliyotendwa na ndugu yao kwasababu ya nguvu ya upendo wa kindugu,
unaitwa kwa kiebrania storge.
Upendo wa kindugu, storge unafanana kwa sehemu na ule upendo wa ki-
Mungu wa agape.
✓Hauangalii hali ya nje ya mtu.
✓Hauna masharti ya kupendwa.

✓Hauna kikomo au mwisho wa kupendwa.


 Tofauti yake moja kubwa na upendo wa agape ni kwamba, upendo wa
kifamilia una kiwango au kipimo cha kupenda. Wanafamilia
wanapendana lakini kwa viwango tofauti; upendo wao haulingani.
Tofauti nyingine kubwa ni kwamba, kwasababu huu upendo wa
kifamilia unatokana na binadamu, basi ni lazima hautakosa madhaifu.
Ingawa ndugu wanaweza kuwekeana masharti fulani fulani ya kitabia ili
kuweka uelewano kati yao, hata masharti hayo yakivunjwa, na baadhi ya
ndugu wakasema wamefika mwisho, hawataki tena kumsaidia, lakini
mwishoni, baada ya hasira kutulia na muda kupita, utaona ndugu
wanainuka, wanajikongoja, kwenda kumsaidia ndugu yao. Hiyo ndiyo
nguvu ya upendo wa kifamilia.

44
(iii) Upendo wa Kirafiki (Philia) ni nini?
Upendo wa kirafiki ni aina ya upendo wa karibu sana ambao Wakristo wengi
hufanyiana. Upendo huu unaelezea dhamana ya nguvu ya kihisia
inayoonekana katika urafiki wa kina. Philia ni aina ya upendo zaidi katika
Maandiko, ikiwa ni pamoja na upendo kwa wanadamu wenzake, huduma,
heshima, na huruma kwa watu wanaohitaji. Dhana ya upendo wa ndugu
ambayo huunganisha waumini ni ya kipekee.
Upendo huu wa kirafiki ni Upendo wa kiwango kisicho cha kawaida, kwani
Upendo huu hupita hata ule Upendo wa wanawake.
Mfano. Urafiki wa Yonathani na Daudi. 1Samweli 18:1-4
Tunaona Yonathani anampenda sana Daudi baada ya kugundua vipawa vilivyo
ndani ya Daudi. Tunasoma kwamba Daudi alikuwa anajua sana kupiga muziki
na kuimba zaburi kwa Mungu, kitu kilichofanya Daudi awe karibu sana na
Mungu na kufunikwa na utukufu wa Mungu yaani upako. Hivyo Yonathani
alimpenda sana Daudi kwasababu Daudi ana upako, uliomsaidia babake (Sauli)
kufunguka kutoka katika nguvu za giza mara kwa mara. Hivyo Daudi akawa
mtu wa msaada sana katika familia ya Mfalme na katika serikali yake. Pasipo
Daudi kuwepo karibu, mambo yote ya ofisi ya Mfalme na nyumba yake
yanaharibika. Hicho kilimfanya Yonathani kumpenda sana Daudi. Na Daudi
naye akampenda sana Yonathani kwasababu Yonathani alimpenda yeye
kwanza, na pia kwasababu Yonathani alikuwa ni mtoto wa Mfalme.
Kukajengeka upendo mkubwa sana wa kirafiki kati ya Daudi na Yonathani,
Hivyo, Philia ni upendo wenye sababu au masharti.

45
Huu ni Upendo ambao marafiki hushibana sana kiasi kwamba hupeana
mpaka siri ambazo hata ndugu wa damu, Baba, na Mama ni ngumu sana
kushirikishwa, lakini rafiki yake lazima tu atamshirikisha, siri hizo zinaweza
kuwa ni siri katika, mahusiano, uchumi, pengine mpaka magonjwa.
Baadhi ya sifa za Upendo wa kirafiki.
✓Unaangalia hali ya mtu ya nje.

✓Una masharti yoyote ya kupenda.

✓Una kiwango au kipimo cha kupenda.


✓Una mwisho au kikomo cha kupenda.

(iv) Upendo usio na kipimo (Agape) ni nini?


Upendo usio na kipimo.ni aina ya upendo usio na kipimo, usio na maana kwa
wanadamu. Ni upendo wa Mungu unatoka kwa Mungu. Upendo wa Agape ni
kamilifu, usio na masharti, dhabihu, na safi. Yesu Kristo alionyesha upendo
huu wa kimungu kwa Baba yake na kwa binadamu wote katika njia aliyoishi
na kufa.
Yohana 3:16-18 " ¹⁶ Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata
akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na
uzima wa milele. ¹⁷ Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili
auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. ¹⁸ Amwaminiye
yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu
hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu."
 Ni ukweli usiopingika kwamba Haki ya Mungu Kwa wanadamu wote
imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni; -

46
✓Mungu ni wa wote: Inamaanisha kwamba, Mungu akisimama katika nafasi
yake ya Uungu wanadamu wote amewaumba kwa mfano wake. Ni Mungu ni
wa wote wenye mwili, ametuumba. Ndiyo maana Mungu huwaangazia jua
lake wema na waovu, huwanyeshea mvua yake wenye haki na wasio haki
Kwa kiwango sawa. Mathayo 5:45 “ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye
mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea
mvua wenye haki na wasio haki."
✓Mungu ni wa Wana: Mungu akisimama katika nafasi yake ya Baba wote
waliompokea anawapa nafasi ya kufanyika wana. Yohana 1:12-13 " ¹² Bali
wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale
waliaminio jina lake; ¹³ waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya
mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu."

Mfano; Upendo wa Msamaria mwema. Luka 10:29-37


Msamaria mmoja alimkuta mtu mmoja asiyemfahamu, ameanguka barabarani
kwasababu amepigwa na wanyang'anyi. Huyu Msamaria aliamua kumsaidia
huyu mhanga kwa kumsafisha vidonda vyake na kumchukua katika punda
wake na kumpeleka katika nyumba ya wagonjwa na si hivyo tu, bali alijitolea
hata kumlipia gharama za matibabu, kwa huyu mtu asiyemjua kabisa. Huu
ndio upendo wa ki-Mumgu ndani ya mtu. Hauangalii hali ya nje wala hauna
masharti; bali mtu huamua kuuachilia tu kwa mtu, kawasababu Mungu
ameumimina ndani yake kwa ajili ya mtu/watu wengine.
Sifa kuu nne za Upendo wa ki-Mungu.
✓Hauangalii hali ya mtu ya nje.

47
✓Hauna masharti yoyote ya kupenda.

✓Hauna kipimo au kiwango cha kupenda.

✓Hauna mwisho au kikomo cha kupenda.


(V) Upendo wa kujipenda binafsi(Philautia) ni nini?
Ni aina ya upendo wa kujithamini binafsi. Katika jamii zetu siku hizi watu
wengi wanashiriki aina hii ya upendo katika kujipenda na kuwa wabinafsi
yaani "umimi".
Kujipenda si vibaya lakini ni muhimu tujifunze kutoa na kupokea upendo
Kutoka kwa watu wengine. Kile ambacho hatupendi kufanyiwa tujifunze
kutowafanyia watu wengine pia.
Mwanzo 25:27-34 Katika Biblia aina hii ya upendo ilionyeshwa na
Yakobo alipotaka haki ya uzaliwa wa kwanza Kutoka kwa kaka yake ili
ampatie chakula, lakini pia alipochukua Baraka za kaka yake.
Mwanzo 25:27-34 “²⁷ Watoto wakakua, Esau alikuwa mtu ajuaye kuwinda
wanyama, mtu wa nyikani, na Yakobo alikuwa mtu mtulivu, mwenye kukaa
hemani. ²⁸ Basi Isaka akampenda Esau, kwa sababu alikula mawindo yake, na
Rebeka akampenda Yakobo. ²⁹ Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja
kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana. ³⁰ Esau akamwambia Yakobo,
Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa
hiyo walimwita jina lake Edomu. ³¹ Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo
haki yako ya mzaliwa wa kwanza. ³² Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu
kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi? ³³ Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza.
Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza. ³⁴
Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa,

48
kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa
wa kwanza."

(Vi) Upendo wa kudumu(Pragma) ni nini?


Ni aina ya upendo ambao msingi wake umejengwa katika kuaminiana tofauti
kabisa na Eros ambao upendo wake huwa ni washauku ya mapenzi ya kimwili
au kingono.
Pragma ni aina ya upendo ambao umekomaa na kukuzwa kwa muda mrefu
sana yaani ni Upendo wenye uvumilivu.
Mwanzo 29: 15-30 Katika Biblia aina hii ya upendo ilionyeshwa na
Yakobo alipomtumikia Laban miaka Saba mingine ili ampate Raheli.
Kwa bahati mbaya aina hii ya upendo ni nadra sana kupatikana katika jamii
kwa maisha ya sasa, siku hizi wanadamu hawana mpango wa uvumilivu wa
kuutazama upendo katika hali ya kukua bila kuwa na mpenzi. Ndiyo Maana
Neno la MUNGU likatukumbusha kwa kutuambia "Nawasihi, enyi binti za
Yerusalemu; Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona
vema yenyewe" Wimbo ulio bora 2:7

(Vii) Upendo wa kuzingatia(Mania) ni nini?


Ni aina ya upendo wa kimapenzi ambao unaweza sababisha mtu kuwa na
wazimu, msongo wa mawazo, wivu, au hata hasira. Upendo huu hutokea
baada ya kukosekana kwa usawa kati ya Upendo wa Kifamilia na Upendo
wakudumu.

49
Watu wengi wanaopata aina hii ya upendo wa kimapenzi huwa wanakabiliwa
na hali ya wazimu, wivu na hata hasira ya kuhisi kusalitiwa na wapendwa wao.
Wanaogopa kupoteza kile ambacho wamekipenda. Hofu hii ya kupoteza
huwafanya wafanye maamuzi magumu na yenye hatari zaidi kwa kile
kinachoitwa wivu wa mapenzi.
Tafiti zinaonyesha kuwa filamu nyingi za maigizo zinahusu maigizo ya
mapenzi, na inaonyesha kuwa baada ya ndoa ya mke na mme kuvunjika
maisha kati ya wanandoa hao yanazidi kuwa mazuri, lakini ni uwongo unao
karibia na ukweli. Lakini waswahili wanasema kuwa "Ukitaka kujua utamu
wa ngoma ingia ucheze" hivyo kwa wewe ambaye upo kwenye ndoa
usidhubutu kumwacha huyo mme au mke wako, kwani hakuna mwanadamu
aliyekamilika, na hukitaka kumpata mke au mme aliye kamilika kwamwe
hautampata, mwanadamu hajakamilika maana ikitokea akawa mkamilifu basi
huyo hatakiwi kuitwa mwanadamu bali anatakiwa kuitwa Mungu, maana
Mungu pekee ndiye mkamilifu.

2 Samweli 13. Aina hii ya upendo katika Biblia ilionyeshwa na Amnoni


kwa dada yake Tamari alivyompenda kiasi cha kuugua.
2 Samweli 13:1-15 "¹ Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi,
alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa
Daudi, akampenda. ² Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya umbu
lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni
vigumu kumtendea neno lo lote. ³ Lakini Amnoni alikuwa na rafiki, jina lake
Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi; naye Yonadabu alikuwa mtu

50
mwerevu sana. ⁴ Naye akamwambia, Kwa nini, Ee mwana wa mfalme,
unakonda hivi siku kwa siku? Hutaki kuniambia? Amnoni akamwambia,
Nampenda Tamari, umbu la ndugu yangu, Absalomu. ⁵ Yonadabu
akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako
atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje,
nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile
mkononi mwake. ⁶ Basi Amnoni akalala, akajifanya mgonjwa; na mfalme
alipokuja kumtazama, Amnoni akamwambia mfalme Mwache ndugu yangu,
Tamari, aje, nakusihi, aniandalie mikate miwili machoni pangu, nipate kula
mkononi mwake. ⁷ Basi Daudi akatuma mjumbe aende nyumbani kwa Tamari,
akasema, Nenda sasa nyumbani kwa Amnoni, ndugu yako, ukamwandalie
chakula. ⁸ Akaenda Tamari nyumbani kwa nduguye Amnoni; naye alikuwa
amelala. Akachukua unga, akaukanda, akaiandaa mikate machoni pake,
akaioka mikate. ⁹ Akalitwaa kaango, akaisongeza mbele yake; lakini alikataa
kula. Naye Amnoni akasema, Toeni watu wote kwangu. Wakatoka kila mtu
kwake. ¹⁰ Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula
mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea
Amnoni nduguye mle chumbani. ¹¹ Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili
ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu. ¹²
Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai
kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. ¹³ Nami nichukue wapi
aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli.
Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa. ¹⁴
Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko

51
yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. ¹⁵ Kisha Amnoni akamchukia machukio
makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale
mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka,
nenda zako."
 Jinsi ya Kupenda Kama Yesu Kristo.
Sisi sote tunataka kuwa na Upendo kama wa Yesu Kristo. Tunataka kuwa
na ukarimu, kusamehe, huruma na kupenda watu bila masharti. Hivyo
kuna haja kubwa sana ya kukaa karibu na Yesu ili atufundishe Upendo
wa kweli. Haleluya!
 Upendo mkubwa ni upendo juu ya umuhimu wa kuendeleza imani,
matumaini, na upendo katika tabia yetu ya Kikristo. 1 Wakorintho 13:13.
" Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika
hayo lililo kuu ni upendo"

Vipimo kumi na tano vya Upendo. (1 Wakorintho 13:4-8).


i.Upendo huvumilia, ii. hufadhili;
iii. upendo hauhusudu; iv.upendo hautakabari;
v. haujivuni; vi. haukosi kuwa na adabu;
vii. hautafuti mambo yake; viii. hauoni uchungu;
ix. hauhesabu mabaya; x. haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
xi.huvumilia yote; xii huamini yote;
xiii.hutumaini yote; xiv. hustahimili yote.
xv.Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika;
zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

52
2.Furaha.
Furaha ni ukunjufu wa moyo, uchangamfu wa moyo, tabasamu la dhati ndani
ya mtu linalobebwa na uso uliochangamka kisha kudhihirishwa na kicheko
cha amani. Uso wako ni picha tosha inayokuelezea wewe pamoja na mambo
yaliyomo kwenye moyo wako. Hatuwezi kuamini kuwa unafuraha wakati uso
wako ukiwa umekunjamana yaani umechora matuta- matuta kwenye paji lako
la uso.
Mithali 15:13 “Moyo wa furaha huchangamsha uso; Bali kwa huzuni ya
moyo roho hupondeka.”
Furaha kwa tafsiri ya kawaida, ni mihemko chanya ya kihisia inaotokana na
aidha kuridhishwa na jambo fulani au kupata kitu fulani. Lakini kumbuka
Fedha haiwezi kuleta maana halisi ya furaha ya kweli katika maisha ya mtu.
Kitendo cha Mbwa cha meno yake kuonekana nje haimaanishi kuwa
anacheka. Hii inamaanisha kuwa furaha sio kicheko tu bali furaha ni
uchangamfu wa uso kutoka moyoni mwa mtu, maana ndani ya moyo wa
mwanadamu kuna siri nyingi mno kiasi kwamba ikitokea Mungu akakufunulia
siri zilizopo ndani ya moyo wa mtu fulani pengine ulikuwa unamwamini sana
basi unaweza usimwamini tena kisha kumweka katika kundi la wanadamu
ambao sio wazuri. Biblia inasema kuwa moyo wa mwanadamu huwa ni
mdanganyifu tena unaugonjwa wa kufisha lakini Bwana ndiye awezaye
kuujua?
Yeremia 17:9-10 “⁹ Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa
wa kufisha; nani awezaye kuujua? ¹⁰ Mimi, Bwana, nauchunguza moyo,

53
navijaribu viuno, hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda
ya matendo yake."
Kuna mwanafalsafa mmoja alishawahi kusema "Shahada mahususi ya
mwanadamu ni furaha anayoitafuta kila siku”. Watu wengi huwa na
furaha zinazotokana na sababu mbalimbali zikiwamo; furaha ya kuoa au
kuolewa, watoto wao, mke au mme wake, familia zao, magari yao, farasi wao.
Lakini furaha ya kweli ipo ndani ya Yesu Kristo yeye atupaye furaha hata
katika wakati ambao watu wengine huwa hawana matumaini lakini Yesu
Kristo kupitia Roho Mtakatifu hutupa furaha kubwa na matumaini tele.
Mfano.Siku moja nikiwa naelekea kanisani, nilipishana na wapendwa wawili
yaani kijana wa kike na kijana wa kiume, na walikuwa wanazungumza stori
huku wakitembea, binti akawa anasema maneno haya;"siku moja alivaa gauni
moja refu hadi mama yake akamwuliza kuwa inakuwaje leo umevaa gauni
refu hivi! ama kweli Yesu yu karibu kurudi."Mzazi unapataje ujasiri wa
kusema maneno in haya ambayo kimsingi sio mazuri, yaani unashindwa
kumkanya mwanao! Mzazi nakusihi mlee mtoto wako katika njia impasayo
naye hataiacha hata atakapokuwa Mzee. Mpendwa acha kujifariji kama Binti
yule kwasababu yeye aliona kuvaa gauni au sketi fupi ndiyo furaha yake, ni
bora uvae nguo ndefu na nadhifu hata kama watu watakuona mshamba ni heri
uwe mshamba katika Dunia hii kwa muda kitambo halafu badae uje kuwa
mjanja uzima wa milele.
Nguvu iliyopo ndani ya furaha itokanayo na Roho Mtakatifu
(i) Furaha ina nguvu ya kupasua nchi au ardhi. kipindi Sadoki, kuhani, na
Nathani nabii na Benaya, mwana wa Yehoyada, na wakerethi, na Wapelethi,

54
walipompandisha Sulemani mwana wa Daudi juu ya nyumbu wa mfalme
Daudi babaye kumpeleka Gihoni, mda huo Sadoki ameitwaa ile pembe ya
mafuta katika Hema, akamtia Sulemani mafuta, watu walipiga panda na watu
wote wakasema Mfalme Sulemani na Aishi! Watu walifurahi furaha kubwa
mno hata nchi ikapasuka kwa sauti zao.
1 Falme 1:40 “Kisha watu wote wakapanda juu nyuma yake, watu wakapiga
mazomari, wakafurahi furaha kubwa mno, hata nchi ikapasuka kwa sauti zao.”
(ii)Furaha itokanayo na Roho Mtakatifu humsaidia mtu kustahimili majaribu.
Yakobo 1:2-4 "² Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia
katika majaribu mbalimbali; ³ mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu
huleta saburi. ⁴ Saburi na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na
watimilifu bila kupungukiwa na neno."
iii.Furaha itokanayo na Roho Mtakatifu humpa mtu nguvu ya kufurahi na
waliao. Inamaanisha kuwa, lia na wanaolia ili ukifika wakati wa kucheka
mcheke pamoja, maana ukicheka na mtu aliye lia peke yake wakati wa
kulia, utakuwa umechelewa kucheka nae wakati wa kucheka kwake.
Rumi 15:10 "Na tena anena, Furahini, Mataifa, pamoja na watu wake."
(iii)Furaha humkumbusha Mungu mambo mbalimbali aliyoyatenda kwako.
Hesabu 10: 9-10 "⁹ Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu,
kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha
kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za Bwana, Mungu wenu, nanyi
mtaokolewa na adui zenu. ¹⁰ Tena katika siku ya furaha yenu, na katika
sikukuu zenu zilizoamriwa, na katika kuandama miezi kwenu, mtapiga hizo
tarumbeta juu ya sadaka zenu za kuteketezwa, na juu ya dhabihu za sadaka

55
zenu za amani; nazo zitakuwa kwenu ni ukumbusho mbele za Mungu wenu;
mimi ndimi Bwana, Mungu wenu."
Uwapo nyumbani mwa Bwana yakupasa ufurahie kumwabudu Mungu maana
Mungu anatafuta watu wanaomwabudu katika roho na kweli,hivyo na wewe
kuwa miongoni mwa watu wanaomfurahisha Mungu maana ukimfurahisha
Mungu, yeye atajishughulisha na mambo yako mengi ambayo pengine
usingeyapata kwa kuomba peke yake,na hii ni kwasababu huwezi kumwabudu
Mungu katika roho na kweli kama hauna furaha, kumbuka wapo watu wengi
wanatamani japo kwa dakika chache tu waingie kanisani wamwabudu na
kumfurahia Mungu, lakini kwasababu ya afya zao sio nzuri yaani wapo katika
vyumba vya uangalizi maalumu yaani kwa Lugha ya kiingereza "Intensive
care unit"(ICU).
Mtu mmoja alisema "Waliookoka au walokole ni kikundi cha watu
walioumizwa au waliopigika kimaisha na shida, maumivu, manyanyaso,
mateso, matatizo mbalimbali ndiyo maana wameamua kumwamini Yesu
Kristo ili kupata pumnziko……...". Lakini mimi nasema kuwa hao walikuwa
ni walokole wa zamani, kwa sasa tunaokolewa kwa neema sio kutokana na
shida, matatizo, changamoto yeyote. Hivyo na wewe uwapo nyumbani mwa
Bwana mfurahie Mungu wako. Mfalme Daudi anasema kuwa alifurahia
walipomwambia twende nyumbani kwa Bwana kwani kuna mambo mazuri
nyumbani kwa Bwana hata kama umeumizwa, unawindwa, umenyanyasika
vya kutosha, nenda kakutane na Mungu wako kanisani. Zaburi 122:1
“Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana."

56
3.Amani.
Amani ni hali ya raha na salama bila ugomvi; ni kinyume cha fujo au vita.
Amani ni miongoni mwa Matunda tisa ya Roho Mtakatifu, tunda hili
hupandwa katika haki kwa watu pekee wafanyao haki. Ukisoma Yakobo 3:18
“Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.”
kitabu cha Isaya 32:18 “Na watu wangu watakaa katika kao la amani; na
katika maskani zilizo salama, na katika mahali pa kupumzikia penye utulivu.”
hivyo Mungu anajitambulisha waziwazi kuwa wanawe watakaa katika amani
na kuwa pumziko lenye utulivu.
Wafalme, Marais na wakuu wa Dunia, ndoto zao ni amani, mawazo yao ni
amani; na wanaitafuta amani kwa njia mbalimbali zikiwamo, kwa njia ya
mazungumzo ya amani, lakini ikishindikana kwa njia ya mazungumzo ya
amani ndipo wanatumia njia ya kumwaga damu yaani vita. Lengo lao ni
kuhakikisha salama, raha kwa wananchi wao. Mithali 11:14 “Pasipo mashauri
taifa huanguka; Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.”
Serikali za Dunia wanaandaa vijana wao na kuwafundisha mbinu na mafunzo
mbalimbali ya kijeshi au kizalendo ili kutengeneza jeshi la akiba, pia vijana
wao wawe wazalendo kwa nchi yao ili ikitokea vita wawe tayari kutetea na
kupigania nchi yao. Lakini amani ya kweli ipo Kwa Yesu Kristo. Zaburi
29:12b ".... Bwana atawabariki watu wake kwa amani."
Silaha nyingi hatari za kivita zinavumbuliwa na kuzalishwa kila iitwapo leo,
kama vile Nyukilia, mabomu, vifaru, bunduki za masafa marefu. Lakini
ikumbukwe kuwa silaha hizi hazitengenezwi ili kuangamiza wanyama, ndege
wa angani, samaki wa baharini, na wadudu wengine bali ni kwaajili ya
kumwangamiza mwanadamu ili tu usalama na raha viwepo. Silaha

57
huandaliwa wakati wa Amani. Kama lisemavyo Neno la Mungu kuwa
wasemapo Kuna amani na salama ndipo uhalibifu uwajiapo.
1 Wathesalonike 5:8 “Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo
uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba,
wala hakika hawataokolewa.”
Mataifa mengi ya Dunia yameungana pamoja ili kuunda Umoja wa mataifa,
lakini lengo kubwa la kuundwa kwa Umoja huo ni kuhakikisha amani kwa
wananchi wao. Mashirika mbalimbali yameanzishwa ili kuhakikisha haki za
binadamu, haki za kuishi, haki ya kulindwa n.k ili wanadamu wapewe, lakini
pia Mashirika haya yanatoa misaada Kwa nchi ambazo zimeathiriwa na vita.
 Aina kuu mbili za Amani
(i) Amani ya kweli. Hii ni amani inayotolewa na Mungu mwenyewe kwa njia
ya Bwana Yesu. Amani anayoizungumzia Yesu Kristo siyo tuionayo kwa damu
na nyama, bali ni amani ya moyo, maana kitovu cha amani ya mtu kinatoka
kwenye moyo wake (Mathayo 10:34-35). Yesu Kristo alisema kwamba
amani anatuachia, kiasi kwamba ulimwengu hauwezi kuitoa kwa sababu
wenyewe hauna. Yohana 14:27 “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa;
niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu,
wala msiwe na woga.”
Amani ya kweli inajengwa na vitu vitatu muhimu ambavyo ni; -kukubali,
kusamehe, na kuvumilia.
o Kukubali: ili uwe na amani ya kweli ni lazima ukubali au ukubaliane ya
kuwa wewe haujitoshelezi yaani haujakamilika asilimia zote mia moja
hivyo unahitaji kukamilishwa na watu wengine, zaidi sana kuongozwa

58
na Roho Mtakatifu, bila kufanya hivyo wewe utakuwa ni mtu wa
kulaumu tu watu wengine kwa kusema hupendwi, huthaminiwi na
kuheshimiwa.
o Kusamehe: Msamaha hufungua mambo mengi sana kwa mtu,
kwasababu tunaishi na wanadamu ambao hawajakamilika. Hata kama
mtu kakukosea na hataki kukuomba msamaha, msamehe tu ili uwe na
amani, ili pia na wewe upate kusamehewa na Mungu hatimaye
tukamwone Mungu wetu. Waebrania 12:14 “Tafuteni kwa bidii kuwa na
amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu
atakayemwona Bwana asipokuwa nao;”
Amani ya kweli imebeba msamaha wa kweli, unaishi na wanadamu
ambao hawajakamilika, ukiishi maisha ya kuwaona wengine kwamba ni
watu wazima tena wana akili timamu utakosa amani mpendwa, hivyo
msamaha huondoa vinyongo vyote na kuleta amani ndani ya moyo wako.
o Kuvumilia: Amani ni madini ya thamani kuliko madini yote hapa
Duniani, kwani unaweza ukawa na pesa, nyumba na mali, kama hauna
amani na ukawa na vitu vyote ni sawa na bure kabisa, kuwa mtu wa
subira huku ukivumilia upitiapo kipindi kigumu cha maisha kwani
maisha siyo mteremko tu, hata kama maisha ni mteremko, unaweza pita
kwenye mteremko mkali kiasi kwamba hautaweza kustahimili, tafuta
kwa bidii kuwa na amani na watu wote. Haleluya!

(ii) Amani ya uongo. Hii ni Amani inayotolewa au inapatikana kwa muda


mchache tu, lakini baada ya muda kidogo inatoweka ghafula kinafuata kilio
kisicho na majibu pamoja na maombolezo makuu. amani hii watu huitafuta

59
kwa njia isiyo sahihi kabisa kwanjia ya kutoa kafara, ili wawe na mali,
majumba, magari. Amani hii mara nyingi wanadamu huitolea kuzimu ili
wawe maarufu na ya kuwa wao ndio wao. Yesu Kristo alisema kwamba
"amani niwapayo mimi siyo kama ulimwengu utoavyo". Amani ya kweli ni
Yesu Kristo tu. Haleluya!

4.Uvumilivu
Uvumilivu ni hali ya kungojea kitu au jambo hadi litokee au litendeke, pasipo
kujali urefu wa muda au mabadiliko ya Ki-mazingira. Usiache kumwabudu
Mungu, maana tupo kwenye vita na watu ambao hatujui tuliwakosea nini,
na hatujui wanataka nini kutoka kwetu.
"Ufundishe moyo wako kuvumilia maana taarifa za kuvunja moyo ni
nyingi sana maadamu tu upo Duniani"Bila msaada wa Roho Mtakatifu
mwanadamu hawezi kuvumilia sawasawa kwa sababu hana nguvu au msaada
wa kumsaidia kustahimili majaribu, machungu, maumivu makali, na kila
namna ya shida , Bwana Yesu Kristo anaufananisha ufalme wa Mbinguni na
wanawali kumi, watano wao wenye busara, na watano wao wapumbavu
waliokuwa wamealikwa kwenye arusi pamoja na taa zao, lakini baada ya
bwana arusi kukawia,taa zao ziliishiwa na mafuta ndipo bwana arusi akaja na
kuwaacha wasio kuwa na mafuta ya akiba(ziada).
Mathayo 25:1-9 "¹ Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali
kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. ² Watano
wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. ³ Wale waliokuwa
wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; ⁴ bali wale

60
wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. ⁵ Hata
bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. ⁶ Lakini usiku wa
manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. ⁷
Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. ⁸ Wale
wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana
taa zetu zinazimika. ⁹ Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo;
hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao,
mkajinunulie."
Uvumilivu ni hali ya kustahimili machungu, magumu na shida mbalimbali ili
kufikia malengo au mahitaji ya mtu. Shujaa kama wewe, Mungu anakufahamu
sana. Je, wapata shaka juu ya uwepo wake Mungu? Shaka juu ya Nafsi yake?
Matendo yake? Uongezeke leo kwa kuomba mbele zake bila kumficha hata
jambo moja! Huyu ni rafiki wa karibu yako kuliko rafiki yako unae mwamini,
mchungaji wako, mzazi wako, mavazi yako. Ni jukumu lako kumwendea
Mungu kwa ujasiri! Yesu Kristo alisema kabisa ya kwamba "Ulimwenguni
mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu."
Yohana 16:33b "... Ulimwenguni mnayodhiki; lakini jipeni moyo; mimi
nimeushinda ulimwengu." Maisha yamegawanyika katika vipindi vikuu viwili
tu ambavyo ni Shida na Raha, katika kipindi cha shida mwanadamu anakutana
na changamoto suala la Uvumilivu linahitajika sana. kukosa Uvumilivu
kumewafanya wengi kushindwa kufanya maamuzi mazuri na sahihi
yatakayoleta matokeo chanya, badala yake wanajikuta wanaangukia kwenye
shida kubwa zaidi ya zile za kwanza.

61
 Usikikatie tamaa kile unachokitaka, ni ngumu kusubiri lakini ni
mbaya zaidi kujutia. Neema ya Yesu Kristo ni kuu mno, yeye ni
mwaminifu sana, anatimiza agano lake wala hamuachi mtu. Wakati
tunapoona ukuta na kuhisi hakuna kuendelea tena, yeye hutuonyesha
uzuri wa tuendako na hutokeza njia. Haijalishi safari imekuwa ngumu
kiasi gani, mwisho wa yote ni mzuri. Ukihisi kuchoka na kukata tamaa,
Kumbuka safari haukuianza mwenyewe bali Mungu alikupa nguvu ya
kuanza. Mwisho wa safari yetu ni mzuri na umebeba utukufu mwingi.
Yesu Kristo Akujaze uvumilivu na nguvu ya kusonga mbele na kushinda
kila roho za kukata tamaa. Hatuishi kwa ajili yetu wenyewe bali kwa
sababu ya Yesu Kristo.

 Faida Saba za kuwa mvumilivu


✓Humuwezesha mtu kufanya maamuzi sahihi. Ili mtu atoe maamuzi sahihi ya
jambo fulani ni lazima awe na ushahidi sahihi kuhusu jambo hilo, pia asiwe ni
mtu asiye kata tamaa mapema. Wote wanaoongozwa na Roho wa Bwana siyo
wepesi wa kukata tamaa ni kwasababu ya Imani yao kubwa kwa Mungu
inayosimamiwa na Roho Mtakatifu.
✓Humuwezesha mtu kufikia malengo. Neno la Mungu linasema katika kitabu
cha Mithali 29:18 “Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu
yule aishikaye sheria." Maono au malengo humfanya mtu kusubiri kwa
uvumilivu sana ili afikiye tarajio lake alilolisubiri iwe ni kwa muda mrefu au
mfupi.

62
✓Humuwezesha mtu kuokoka na hukumu ya Mungu. Neno la Mungu
linatuambia kuwa “Lakini mwenye kuvumilia hata mwisho, ndiye
atakayeokoka.” Mathayo 24:13. kuokoka maana yake ni kuepuka hukumu ya
Mungu. Hivyo mtu asipokuwa na Roho Mtakatifu ni mtu aliyepoa sana hana
nguvu ya kumsaidia au kustahimili magumu yote. Ni maombi yangu kuwa
Mungu akujaze Roho Mtakatifu ili uokoke na hukumu yake.
✓Humuwezesha mtu kupata vitu au watu sahihi. Mhubiri 3:1 “Kwa kila
jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.” hii
inamaanisha kwamba kila jambo hapa Duniani lina majira yake, kwahiyo
kama majira yake hayajafika haliwezi kutokea, hebu fikiria kuwa usiku
uingiapo kamwe huwezi ona Jua linatokea; hivyo hata kusudi la Mungu
kwa mtu Mungu hawezi kuliruhusu litendeke kama wakati wake haujafika.
kuwa mvumilivu tu mpendwa siku yako ya kucheka ipo, kama haipo hapa
Duniani basi Mbinguni utaikuta. Haleluya!
✓Humjengea mtu ushuhuda. Tunawasoma watumishi wa Mungu wengi sana
ambao walikuwa wavumilivu katika raha, majaribu, mateso, mafanikio; ndiyo
maana wakapata upendeleo wa kuwekwa kumbukumba ndani ya Biblia
Takatifu ili watu wengine tujifunze kwa hao walifanikiwa pia tuiige Imani yao.
✓Hukufanya uwe jirani mwema na unayefikika. Kuna watu wengi sana
ambao hawafikiki kirahisi kwasababu wana mawazo hasi, wanapenda siku
zote watendewe mema tu, hivyo wakitendewa mabaya huwa wakali mno, kiasi
kwamba wanakuwa na maneno makali kiasi kwamba watu wengine hukosa
namna ya kuwa nao karibu kwa kuhofia maisha yao yatakuwa hatarini. Mungu

63
akusaidie uwe ni mtu wa kufikika wahesabu wenzako wanapokukosea kuwa ni
sehemu tu ya uanadamu wao.
 "Chukua fundisho katika nyakati ngumu kwani zinakutambulisha upo
na nani, na watu wa aina gani." Huwezi kuwatambua watu gani
wanaoweza kusimama na wewe katika nyakati zote, kama vile ukiwa na
mali au hauna mali, una afya au mgonjwa, maskini au ukiwa tajiri; lakini
upitiapo wakati mgumu ndipo utaona au utajua uko na nani.
 Nakuombea upewe neema na Bwana Yesu Kristo ya;
i. Kudumu katika mafundisho. Usome neno la Mungu kwa juhudi na
ulielewe vizuri.
ii. Kuwa na ushirika imara na Roho Mtakatifu. Uombe kwa bidii na
maombi yako yajibiwe na Mungu.
iii. Kuhudhuria ibada na upewe haja za moyo wako. Maana kila ibada
ina umuhimu kwako.

5.Utu wema.
Maana ya Utu ni ile hali ya binadamu kutenda kadiri ya hadhi yake kati ya
wanyama na viumbe wengine inayomfanya astahili kupata haki zote za kijamii
kama vile elimu, chakula na maradhi. Maana ya Utu wema ni hali ya
kutokuwa na ubaguzi wa rangi, lugha, kabila, Taifa, dini, wakati wa kumsaidia
au kumpa mtu haki yake haijalishi ni mkubwa au mdogo, mnene au
mwembamba, mpole au mkali.
 Ukigundua kuwa maisha ni yako, ila mazishi yako ni yetu sisi, basi
utaishi na watu vizuri, acha dharau ndugu.

64
Hili ni tunda ambalo linaonyesha wema wa Mungu kwa waovu na wenye haki,
kwa sababu Mungu huwatendea mema wanadamu wote. Wakristo yawapasa
kufanana na yeye kwa kuwatendea watu wote mema.
Mathayo 5:45 “ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana
yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki
na wasio haki." Vile vile ameonyesha wema wake kwa kutuokoa.
Watu wengi leo wanapenda watendewe wema, lakina wao hawataki
kuwatendea wengine wema hapo ndipo changamoto inapoanzia. kumbuka
kuwavile unavyotaka utendewe wewe watendee vivyo hivyo na watu wengine.
 Mambo yatupasayo kuwatendea adui zetu.
1.Kuwasamehe na kuwaombea Baraka. Mwana wa Mungu usipende sana
kuwa na uadui na mtu yeyeto hii itakutofautisha wewe na mwanadamu
ambaye hajaokoka. Mungu wetu ni wa amani wala siyo wa machafuko.
Watakie baraka watu wengine hata kama wanakulaani. “Wabariki
wanaokuudhi; bariki, wala msilaani.” Ukisoma Warumi 12:14. “Lakini mimi
nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi.” Pia Mathayo
5:44. “Watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye
kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi Baraka.”
2.Kuwatendea mema. Mtendee wema kila mtu kama vile Mungu anavyo
kutendea wema wewe ukianguka dhambini. “Msimlipe mtu ovu kwa ovu.
Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Lakini, adui yako akiwa na nja,
mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya
moto kichwani pake. Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa
wema.” Warumi 12:17,20-21.

65
Kutokana na kuwatendea wengine wema Bwana wetu Yesu Kristo anakuwa
upande wetu kila wakati akitusaidia na kuwalipa kisasi adui zetu, wala hata
hatutatumia nguvu kubwa kujaribu kishindana nao, maana kisasi ni cha Bwana
Mungu wetu peke yake maana yeye ni halisi, mkamilifu, anajitegemea na
hajawahi kusema uongo, wewe msubiri Bwana ili ukauone wokovu wake.
Sharti linalohusu kutenda wema
Mtu anapotenda wema si vema kujionyesha au kutangaza ili watu wafahamu.
Mathayo 6:1 “Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi
mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa
Baba yenu aliye wa mbinguni." Kutokana na Neno hili tunajifunza ya kwamba
mema tuyatendayo ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Yeye pekee ndiye
anayestahi kutukuzwa kwa yale mema tuyatendayo.
Malipo kwa watu watendao wema.
Kama nilivyosema hapo juu kuwa malipo yanaanzia hapa hapa Duniani, hivyo
watendao mema wataurithi uzima wa milele.
Mathayo 25:31-40 "³¹ Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu
wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti
cha utukufu wake; ³² na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye
atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; ³³ atawaweka
kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. ³⁴ Kisha
Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, Njoni,
mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu
kuumbwa ulimwengu;³⁵ kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula;
nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha;³⁶ nalikuwa

66
uchi, mkanivika nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni,
mkanijia.³⁷ Ndipo wenye haki watakapomjibu, wakisema, Bwana, ni lini
tulipokuona una njaa, tukakulisha, au una kiu tukakunywesha?³⁸ Tena ni lini
tulipokuona u mgeni, tukakukaribisha, au u uchi, tukakuvika?³⁹ Ni lini tena
tulipokuona u mgonjwa, au kifungoni, tukakujia?⁴⁰ Na Mfalme atajibu,
akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao
ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi."

Malipo kwa watu wasiotenda wema.


Watahukumiwa na kuadhibiwa katika mateso ya moto wa milele.
Mathayo 25:41-46 "⁴¹ Kisha atawaambia na wale walioko mkono wake wa
kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele,
aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;⁴² kwa maana nalikuwa na njaa,
msinipe chakula; nalikuwa na kiu, msininyweshe;⁴³ nalikuwa mgeni,
msinikaribishe; nalikuwa uchi, msinivike; nalikuwa mgonjwa, na kifungoni,
msije kunitazama.⁴⁴ Ndipo hao pia watajibu, wakisema, Bwana, ni lini
tulipokuona wewe una njaa, au una kiu, au u mgeni, au u uchi, au u mgonjwa,
au u kifungoni, tusikuhudumie?⁴⁵ Naye atawajibu, akisema, Amin, nawaambia,
Kadiri msivyomtendea mmojawapo wa hao walio wadogo, hamkunitendea
mimi.⁴⁶ Na hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye
haki watakwenda katika uzima wa milele.

67
6. Fadhili.
Fadhili ni kusaidia au kutoa msaada kwa watu wengine bila kutaka wewe
kurudishiwa wema. Mungu ni msaada kwa kila mtu anayemkimbilia ikiwa
anampendeza.
Zaburi 144:2-3 “² Mhisani(mfadhili) wangu na boma langu, Ngome yangu na
mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini
yangu. ³ Ee Bwana, mtu ni kitu gani hata umjue? Na binadamu hata
umwangalie?"
Kumsaidia, mnyonge, mhitaji na maskini ni jambo jema na muhimu ambalo
Yesu Kristo ameagiza. "Kumbuka pesa humaliza matatizo, na matatizo
humaliza pesa"
Matendo ya mitume 20:35 "Katika mambo yote nimewaonyesha ya kuwa kwa
kushika kazi hivi imewapasa kuwasaidia wanyonge, na kuyakumbuka maneno
ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni heri kutoa kuliko kupokea."
Mfano wapo wapendwa makanisani imekuwa ikitokea ameshirikishwa jambo
zito au gumu na mpendwa mwenzake hawezi kumtunzia siri mpendwa
mwenzake yaani kichwa chake hakigandishi siri za watu wengine. Huu sio
upentekoste wapendwa, hebu tuigeni mfano wa Bwana Yesu Kristo.
Nini maana ya neno “fadhili za Mungu ni za milele”?
Fadhili za Mungu sio tu wema na ukarimu Mungu anaotufanyia sisi, bali
linamaanisha pia Upendo wa Mungu usioelezeka, upendo wa kusaidia, upendo
wa kuvumilia, Upendo wa kuokoa na upendo wa kutoa.
Ni wema usio na masharti, kwamba hatutendei fadhili zake kisa sisi
tumemfanyia kitu kwanza, au tumekuwa marafiki zake, Hapana. Anatenda
kama vile ni wajibu wake kufanya, Wema huo hauwezi kuelezeka, kwasababu

68
unagusa kila nyanja, ambazo haziwezi kufikiwa na mwanadamu yoyote yule,
au kiumbe chochote kile mbinguni au duniani.
 Mungu alikuwa tayari kumtoa mwanawe wa pekee sadaka ili sisi
tupate wokovu, Jiulize wewe unaweza kumtoa mwanao, awe sadaka
ili jirani yako ambaye hakusaidii chochote apone au afaidike?
Unaweza kufanya hilo?

Neno la Mungu linatuambia kuwa tuwatunze watu wa nyumbani kwetu wala


tusiwasahau, wapo wapendwa wengi leo wafanikiwapo huwasahau hadi ndugu
zako wa damu yaani kaka, dada, baba, mama; kisa mafanikio yao wanawaona
ndugu zao kuwa sio hadhi yao, Neno la Mungu linatuambia kuwa
usipowatunza au kuwajali wa nyumbani kwenu tayari umeikana Imani, tena ni
mbaya kuliko mtu asiyeamini. Mpendwa wajali watu wa nyumbani kwako au
kwenu waheshimu washike mkono kwa hali na mali.
1Timotheo 5:8 “Lakini mtu ye yote asiyewatunza walio wake, yaani, wale wa
nyumbani mwake hasa, ameikana Imani, tena ni mbaya kuliko mtu asiyeamini.”
Hata kama unawazidi Elimu wasidie tu maana ndugu zako wanajivunia
ya kuwa wewe ndiyo ndugu yao wa pekee ambaye una Elimu kubwa,
usiwabague kwa namna yeyote hata kama hawakukusaidia kipindi unasoma
pengine ulisoma kwa taabu sana lakini wasaidie tu haijalishi, dini zao,maisha
yao yapo chini sana maana kwa kufanya hivyo utawafanya wamwamini
Bwana Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao bila hata ya
kutumia gharama kubwa za kuandaa mkutano au mikutano mikubwa ya
Injili, kwa kufanya hivyo utajikuta siku ya Mwisho yaani siku ya hukumu
unapewa taji kubwa, nzuri ing'arayo sana.

69
 Mambo yampasayo anayesaidia masikini.
Asaidie kwa moyo safi bila kusikitika na wala si kwa ajili ya kujionyesha.
Umsaidiapo mtu, si vema sana kumtangaza, kumpiga picha na kuwaonesha
watu wengine kama kwenye magazeti baki nalo tu wewe, nakuomba uwe na
"kichwa cha kugandisha maneno"maana Kwa kufanya hivyo tutakuona
kuwa unaukomavu wa kiakili. Sio vizuri kumtangazia kama vile kwenye
magazeti kila mtu kitu unamwambia, tunza siri mpendwa mbona wewe siri
zako umezitunza tu vizuri, watunzie na wengine basi siri zao.

70
Kinachotokea kwa mtu anayesaidia masikini.
1.Haki yake inadumu na wala haitapotea ikiwa anadumu katika sheria za
Mungu.
2.Anabarikiwa. Hakuna mwanadamu yeyote hapa Duniani asiyependa
kuongezeka(kubarikiwa),ikitokea akawepo basi huyo ana matatizo yake
makubwa sana. Mithali 29:9 “Mwenye jicho la ukarimu atabarikiwa; Maana
huwapa maskini chakula chake."
3.Anajiwekea hazina mbinguni. Hazina neno jingine tunaita ni akiba, hivyo
ukiweka akiba yako mbinguni utakuwa unawekeza mambo makubwa sana
kuliko unavyodhani, kwani mbinguni hakuna wezi, lakini hazina yako
itakapokuwapo ndipo na moyo wako utakuwa pale.

7. Uaminifu.
Uaminifu ni hali ya mtu kutenda jambo fulani kwa namna ambayo mtu
mwingine atamwamini. Kwa lugha nyingine, uaminifu ni hali ya moyo
ambayo itampelekea mtu kuthamini na kutii utaratibu au jambo la mtu
mwingine, “hata kama hapati faida binafsi” ila anafanya kwa ajili ya
mwingine.
Mfano Kipindi mimi nasoma Sekondari Upili (A-level), Singida siku moja
nilitumiwa pesa kwaajili ya kulipa ada na mzazi wangu kiasi fulani, lakini
kiasi cha pesa nilichotumiwa ndio kilikuwa kiasi ambacho nadaiwa, sasa
nilienda kwa wakala kutoa pesa hiyo ili nilipe ada, cha ajabu nilipoitoa hela
hiyo wakala alijisahau akanipa hela yote bila ya kuondoa pesa ya makato. Je!
Ungekuwa wewe ungefanyaje? Lakini mimi kwa msaada wa Roho

71
Mtakatifu alinikumbusha nimrudishie wakala pesa ya makato, na nikampatia
yule wakala pesa ya makato yake, sijiinui, lakini nakuonesha ni namna gani
tunapaswa tuwe waaminifu. Neno la Mungu linatuambia kuwa tuwe
waaminifu hata kufa.
Uaminifu ni mojawapo ya tunda la Roho Mtakatifu katika maandiko
matakatifu. Tunajifunza uaminifu wa Mungu unaopatikana katika Neno lake.
Yeye amesema atatimiza yale aliyoahidi katika neno lake, si tu kwa wana
wa Israeli bali kwa watu wote wanaoishi sawasawa na Neno lake. Kwa
hiyo, kwa upande wetu inatupasa sisi nasi kuwa waaminifu kwa kuliishi na
kulitenda neno la Mungu.
Isaya 55:11 “ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu;
halitanirudia Bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika
mambo yale niliyolituma.”
Mtu aliye mwaminifu ni yule ambaye anatenda sawasawa na maagizo, sheria
na taratibu.
Uaminifu huwa unaanza katika vitu kama vile; -
1. vitu vidogo vidogo: Huu ni uaminifu wa mambo madogo madogo ambayo
yanaonekana ni ya kawaida sana, lakini vitu hivi vidogo vidogo ndivyo
vinamuweka mtu katika mazingira mazuri ya kuaminika kupita kawaida.
Kwamfano wewe mwenyewe kama ulishawahi kumkopesha mtu kiasi kidogo
cha pesa lakini mtu huyo uliyemkopesha akawa anakuzungusha zungusha tu
kukurudishia pesa yako au kukudhurumu kabisa, hivi ikitokea tena siku
nyingine akaja anataka umkopeshe pesa kiasi kikubwa je! utampa haraka au ?
Hilo naomba usinijibu nadhani majibu unayo wewe mwenyewe.

72
2.vitu vikubwa: Huu ni uaminifu wa mambo makubwa sana ambao watu
hufikia hatua ya kuaminiana kwasababu ya Uaminifu uliotengenezwa kwa
muda mrefu kutokana na vitu vidogo vidogo.Kwamfano mtu mwingine
anaweza kuaminiwa na mwajili wake mpaka kupewa hata Nywila (Password)
kama ya kadi ya benki, simu janja.Na hii ipo sana kwa mtu aliye mwaminifu
kwa Mungu, Mungu humuonyesha siri kubwa sana zilizofichika katika
Ulimwengu wa roho, na hii ni kwasababu ya kuwa mtu huyu amekuwa
mwaminifu kwa mambo mengi ambayo ameagizwa na Mungu.
Mfano. Kipindi nasoma sekondari (O-level) Shule fulani Shinyanga lakini
sitaitaja shule hiyo,Kuna rafiki yangu sitamtaja Jina lake alinishuhudia mara
baada ya kumaliza masomo yetu ya sekondari (O-level) kuwa ilimtokea
kupendwa na wadada wawili tuliokuwa tunasoma nao, siku moja miongoni
mwa wale wadada wawili alienda kuoga wakati anarudi kutoka bafuni alikuwa
amejifunga kitenge huku mwili wake ukiwa na maji maji yaani mbichi ili tu
kumvutia kijana wa kiume hisia zake, lakini rafiki yangu hakumjali binti yule,
sasa binti alichokifanya alitumia mbinu ya kumwita rafiki yangu aingie getoni
(chumbani) kwa binti, rafiki yangu ikambidi aende kusikiliza kile alichoitiwa ,
ile anafika tu chumbani kwa binti yule, binti akaufunga mlango kisha akatupa
kitenge chake pembeni akabaki na nguo za ndani tu kisha akamwambia kuwa
wafanye nae tendo la ndoa. Lakini rafiki yangu alikataa na akamwambia
kuwa hayuko tayari kufanya uasherati kwani atamtenda dhambi Mungu.
Binti akakosa cha kumjibu rafiki yangu, basi yule rafiki yangu akamwambia
binti kuwa amfungulie mlango ili atoke nje,na rafiki yangu akafanikiwa
kutoka nje bila hata ya kufanya tendo la ndoa.

73
Zilipita siku chache tu tena binti yule wa pili alimuita rafiki yangu chumbani
kwake, lakini rafiki yangu alishituka. Na alikataa kwenda chumbani kwa yule
binti.Kisha akimwambia kuwa amwambie tu kile anachotaka kumwambia
huku rafiki yangu akiwa nje, lakini binti yule alikaza kumwambia aingie
chumbani kwa binti, hatimaye rafiki yangu akasema ngoja niingie tu sijajua
anashida gani yawezakuwa anaumwa, alipofika chumbani kwa binti,kumbe
binti alikuwa amejifunga kitenge na akakivua mbele ya rafiki yangu wa kiume,
kisha binti akamwambia wafanye tendo la ndoa.Lakini rafiki yangu alikataa
akamwambia kuwa hawezi kufanya nae tendo la ndoa kwani atatenda
dhambi kwa Mungu.
Hata sasa katika Dunia hii iliyoharibika wako vijana waliojitunza vizuri kama
Yusufu mwana wa Yakobo ambaye alikataa kufanya tendo la ndoa na mke wa
mwajili(Boss) wake potifa. Unaposema haiwezekana kuvuka ujana bila
kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa ni wewe tu unaeshindwa wapo
wanaoshinda.
Vijana wengi wamejifariji kwamba wakioa/olewa wataweza kuwa
“waaminifu”. Jua neno hili, ukiweza kuwa mwaminifu sasa, ni ishara kwamba
hata huko mbele utakuwa mwaminifu; ukishindwa kuwa mwaminifu sasa, hata
ukioa/olewa unaweza pia ukashindwa kuwa mwaminifu. Zingatia neno hili,
ukiwa peke yako (ukiwa hujaoa ama kuolewa) na ukawa mwaminifu, huo
uaminifu wako ni wa thamani sana mbele za Mungu. Siku hizi utasikia vijana
wanapiga mahesabu ya kuoa/olewa ili kushinda tamaa za mwili; baada ya
kuoa wanagundua tamaa za mwili na majaribu ya uzinzi yameongezeka
maradufu! Kumbe ulipaswa kushinda ukiwa peke yako ndiposa ushindi huwa

74
dhahiri, kwamba hata sasa baada ya kuoa/olewa unashinda kwa sababu ya
Bwana, na sio aibu au hofu ya mwanadamu mwenzio. Kushinda dhambi kwa
sababu ya “hofu ya Mungu” ni tofauti na kushinda dhambi hiyo hiyo kwa
sababu ya “hofu ya watu”. Thamani za ushindi hizi mbili ni tofauti pia.
Hili jambo la kukosa uaminifu ukiwa peke yako limedidimiza uchumi wa
watu wengi. Mungu ameweka vitu “vichache” mkononi mwako, kisha akakaa
mbali kuangalia utafanyaje. Ukamsahau Mungu na watu wengine,
ukijipendelea kwa sababu uko peke yako na maamuzi yako.

8.Upole.
Upole ni kitendo cha kutokuonyesha madhara, kwa mtu au kiumbe kingine,
huwa unaambatana na utulivu. Upole unakuwa na maana zaidi pale ambapo
unauwezo wa kuleta madhara kwa kiumbe kingine lakini hutumii uwezo
huo kumdhuru.
Yeremia 11:19 “Lakini mimi nalikuwa kama mwana-kondoo mpole,
achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujua ya kuwa wamefanya mashauri
kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake, na
tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe
tena.”
Watu wengi sana wanashindwa kutofautisha kati ya Upole na Ukimya, na
wanadhania kuwa mtu mkimya anaweza kuwa mpole jibu ni hapana
kwasababu unaweza kumkuta mtu ni mkimya lakini sio mpole, na hii
inatokana na moja ya mambo yafuatayo, Ukimya ni tendo la nje bali Upole
huwa ni wa ndani, unakuta mtu hapendi tu kuongeaongea au hana stori

75
nyingi za kuzungumza, hivyo unaweza kudhania kuwa ni mpole kumbe sio,
kitu kingine ni nyuso za watu wengine huonekana kana kwamba ni za
unyonge lakini kumbe ni hatari.
Na wanadamu wapo ambao ni wapole lakini wapo ambao si wapole, hii
haipingiki kwa sababu Mwandishi Dag Heward -Mill ameandika kitabu
kinasema "mmoja wenu ni shetani", na anasimamia kwenye kitabu cha
Yohana 6:70 “Yesu akawajibu, Je! Mimi sikuwachagua ninyi Thenashara,
na mmoja wenu ni shetani?”. Na hii ni kwasababu yakuwa mnaweza
mkapatana kufanya jambo fulani kama, familia, kikundi, Taifa na kimataifa
lakini msaliti huwa hakosekani. Mfano Bwana Yesu Kristo alikuwa na
wanafunzi wake yaani mitume kumi na mbili lakini kuna mtume mmoja
aitwaye Yuda iskariote alimsaliti kwa kumuuza Kwa vipande thelasini vya
fedha kitu ambacho kilipelekea Yesu kusulubiwa msalabani.
Katika Biblia Takatifu ipo mifano ya watu wawili ambao wanashuhudiwa
kuwa ni wapole. ambao ni Musa (katika Agano la kale) na wa pili ni Bwana
wetu Yesu Kristo (katika Agano jipya).
1.MUSA
Musa ni mtoto wa tatu katika familia ya mzee Amlani, na Yakobed mamaye,
na ndugu zake ni Miriamu na Haruni.Musa historia inaonyesha kuwa alizaliwa
katika Bara la Afrika, katika nchi ya Misri.
Musa tunamsoma katika Biblia Takatifu kuwa ni mwanadamu wa kipekee
mpole sana. Utajiuliza ni kitu gani cha kipekee alichokuwa nacho Musa,
mpaka kikamfanya awe karibu sana na Mungu kwa namna ile? Ni kwasababu

76
ya Upole wake, Tunasoma; Hesabu 12:3 “Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa
mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.”
Musa aliwazidi watu wote waliokuwa Duniani kwa upole. Na hiyo ikamfanya
awe karibu sana na Mungu, kuliko wanadamu wote walioishi Duniani wakati
huo. Hata sasa, kanuni ya Mungu ni hiyo hiyo, tukitaka tumkaribie Bwana
sana, hatuna budi kuwa Wapole.

2.YESU KRISTO
Bwana Yesu Kristo anajitambulisha waziwazi kuwa yeye ni mpole.
Mathayo 11:28-2 "²⁸ Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye
kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.²⁹ Jitieni nira yangu, mjifunze
kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata
raha nafsini mwenu;"
Alikuwa ni mpole hadi sasa ni mpole naamu hata mauti ya msalaba mfano wa
mwanakondoo.mwanakondoo ni moja ya viumbe ambao ni wapole mno,lakini
haimaanishi kuwa hana nguvu, hapana, bali ni kiumbe asiyetaka kuonyesha
madhara kwa wengine. Na kwasababu ya upole huo, Bwana Yesu, ilimpelekea
mpaka Roho Mtakatifu kushuka juu yake kipekee sana kama Huwa (Njiwa).
Kumbuka sikuzote njiwa hatui sehemu isiyo na utulivu, wala hawezi kutua juu
ya mnyama mkali kama vile mbwa mwitu, bali anatua juu ya mnyama mpole
kama vile kondoo, na ndio maana Bwana Yesu alitambulika kama
mwanakondoo wa Mungu.kitu kingine njiwa ni msafi mno na ana mke au
mme mmoja tu.

77
Mungu alimtukuza Yesu Kristo kwasababu ya huruma yake kubwa kwa
mwanadamu hata akamkirimia jina lipitalo majina yote, na kwa jina lake kila
goti litapigwa na kila ulimi utamkiri., kwanini leo hii watu wote
wanamkimbilia Kristo, ni kwasababu alikuwa mpole sana rohoni. Sio
kwamba alikuwa mnyonge, hawezi kuangamiza, au kuharibu watu,
kumbuka anaitwa pia “Simba wa Yuda”, Tunajua tabia za simba sio upole.
Lakini yeye alikuja katika upole. Hiyo ndio sifa kuu ya mtu mpole.

Mambo yanayopatikana ndani ya moyo wa upole ni pamoja na;


i. Huruma. Upole unaotokana na Roho Mtakatifu ndani ya mtu, huleta
huruma kwa watu wengine, haijalishi wamekosea namna gani, ni
wakaidi kiasi gani, wapo kwenye hali ipi. Mungu hatuangamizi sio
kwamba ni wakamikifu sana, hapana, ni huruma tu za Mungu wetu
hatuangamizi.
ii. Usafi(utakatifu). Roho Mtakatifu huutaka utu wa ndani wa mtu kuwa
katika hali ya usafi. Roho wa Mungu huwa hakai sehemu iliyo chafu.
Utakatifu ndiyo vazi la mtu wa Mungu, maana Mungu wetu ni Mtakatifu
na amesema tutakuwa watakatifu kwa kuwa yeye ni Mtakatifu.
iii. Hauonyeshi madhara kwa wengine. Inamaanisha kwamba upole
hausababishi maumivu na madhara kwa viumbe wengine. Upole
hausababishi pia matokeo hasi kwa kiumbe chochote lakini haimaanishi
kuwa hana nguvu, la! hasha.
iv. Utulivu. Upole huleta amani ndani ya moyo wa mtu ili kusababisha
utulivu dhabiti uletao matokeo chanya.

78
v. Kujishusha. Upole humuonyesha mtu kuwa kama dhaifu. Hujumuisha
pia unyenyekevu ndani ya moyo wa mtu. Unyenyekevu humfanya mtu
kufikia hatua nzuri itakayopelekea kupewa haki yake na Mungu.
vi. Msamaha. Upole hupolekea kutoa msamaha kwa mtu hata kama
hajaobwa msamaha kwa yale mabaya aliyofanyiwa. Na lengo la mtu
kutoa msamaha ni kumfanya abaki na Amani, lakini pia na yeye apate
msamaha kwa Mungu.

Tunawezaje kuwa wapole?


a. Ni kwa kujishusha: Unapokubali kuonekana kuwa ni dhaifu, ni hatua
nzuri sana ya kuelekea upole, Lakini unapotaka kujiona wewe ni Hodari
wa mambo yote, ni ngumu kuwa mpole. Usipokubali kuchungwa, ujue
kuwa utabiki kuwa mbuzi sikuzote na si mwanakondoo
b. Ni kwa kuzizuia hasira zetu: Roho Mtakatifu ndiye awezae kuutuliza
ulimi usinene sawa na hasira zako, hivyo hatuna budi, kuwa watu wa
kuvizuia sana vinywa vyetu. Hasira huwa ndio chimbuko la ugomvi na
vita. Hivyo ukiweza kudhibiti hasira zako hata kama utaudhiwa kiasi
gani, hutojibu kwa hasira au kipumbavu, basi upole taratibu utaanza
kujengeka ndani yako.
c. Ni kwa kusoma Neno la Mungu na kuomba: Hii ni tiba kubwa sana,
ukitaka ujue hesabu soma kitabu cha hisabati, halikadhalika ukitaka uwe
na upole, usikwepe Biblia Takatifu. Kwasababu hiyo ndio
itakukumbusha, misingi ya kuwa mpole kama Kristo alivyokuwa.

79
Vilevile kuabudu, kunaukaribisha uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yako,
na hatimaye utafikia kiwango hicho.

Zaburi 119:11 “Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda


dhambi.”

9.Kiasi.
Kiasi ni ule uwezo wa kudhibiti jambo au tendo lisipitilize mipaka yake, yaani
litendeke kwa sehemu tu.
Kiasi ni kile kitendo cha kuishinda nafsi yako. Kuwa na uwezo wa kuitawala
nafsi na mahitaji yake, kuitanguliza roho kwanza maana ndiyo yenye uzima.
Uwezo huu unapatikana chini ya msaada wa Roho mtakatifu, vinginevyo
haiwezekani. Roho mtakatifu anatuwezesha kuikagua nafsi, kuitawala na
kuizuia pale inapotaka kwenda kinyume, kuifundisha jinsi ya kuenenda na
kutuwezesha kusema Hapana kwa nafsi.
Lakini ukipungukiwa na kiasi, ni uthibitisho mojawapo kuwa Roho wa Mungu
hayupo ndani yako. Kwasababu, huu ulimwengu una mambo mengi,
ambayo, pengine sio mabaya, lakini yakipitiliza matumizi yake, yanabadilika
na kuwa mabaya na sumu kubwa sana, kuliko hata matendo yenyewe
mabaya.
Baadhi ya nyanja au sehemu za kiasi ambazo Roho Mtakatifu anataka sisi
tuwe nazo.
(a) Katika ndoa.
Kutokuwa na kiasi katika tendo la ndoa, hupelekea watu wengi sana
kumtenda Mungu dhambi. Muda mwingi wanachowaza ni tendo lile tu,

80
akili zao zote zinafikiria humo, mpaka inawapelekea kukosa muda wa
kumwabudu Mungu.Hivyo kiroho chao kinapungua sana kwasababu ya
kuendekeza tamaa za mwili.
1 Wakorintho 7:2-5 “² Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na
awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake
mwenyewe. ³ Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na
ampe mumewe haki yake. ⁴ Mke hana amri juu ya mwili wake, bali
mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. ⁵
Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa
kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi
kwenu."
(b) Kiasi katika shughuli za ulimwengu.
Bwana ametuweka duniani tufanye kazi, pia tujitafutie riziki, lakini
anatutahadharisha, tusipitilize, mpaka kufikia hatua ya mioyo yetu
kuzama huko moja kwa moja hata tukamsahau yeye, hata muda wa ibada,
kuomba na kuwaeleza wengine Habari njema. Hiyo ni hatari kubwa sana.
(c)Kiasi katika huduma
Mungu anataka watumishi wake tuwe na kiasi, hamaanishi kiasi katika
kumtumikia, hapana, Mungu anataka sana tuzidi kumtumika kwa bidii.
Lakini Mungu anamaanisha kiasi katika kuifanya kazi yake, sio kila
muda unakuwa kanisani tu unashinda unamkanyaga shetani, nenda
kazini ukamkanyage Shetani na huko pia, mpendwa fanya na kazi
zingine ili usiwalemee watu wengine lakini pia jina la Mungu
lisitukanwe kwasababu ya uzembe wako unaotaka kuuendekeza.

81
(d) Kiasi katika haki.
Haki ni uhalali wa kupewa kitu fulani: Yesu Kristo alisema kuwa "haki
yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na mafarisayo, hamtaingia kamwe
katika ufalme wa Mbinguni" hapa Bwana Yesu alikuwa anamaanisha
kuwa,matendo, tabia, njia,mienendo,ya mwamini isipo wazidi
wanadamu wasioamini na washika dini (waandishi na mafarisayo)
kamwe hawataingia Mbinguni. Maana wapo waKristo wengi hawafanyi
haki wanasema na kusingizia kuwa wapo rohoni sana hata wanaacha
kushiriki masuala ya kijamii lakini wanadamu ambao hawamwamini
Kristo na washika dini wanafanya, matendo,tabia,mienendo na njia nzuri,
kama vile
 Kuwatembelea wagonjwa.
 Kuwapa chakula walio na uhitaji wa chakula.
 kushiriki katika misiba.
 Kuhudhuria ibada (Mfano waislam huabudu mara tano kwa siku,
lakini mKristo anaona kazi kweli kuabudu Ibada ya siku ya Jumapili).
 kutaka suluhu.
Ijapokuwa tunapaswa kuyatimiza hayo yote lakini hatupaswi kamwe
kujihusisha nayo zaidi na kuyapa nafasi ya kazi na sehemu ya Mungu
kama Baba yetu. Na hii ndiyo maana halisi ya kiasi katika kufanya haki.
Hatupaswi kujisikia huruma kuzidi sana hata tukajikuta tunatenda uovu
eti tukidhania tunafanya haki ya Mungu. Haleluya!

82
Mathayo 5:20 “Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi
hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika
ufalme wa mbinguni."
(e)Kiasi katika kunena.
Mithali 10:19 “Katika wingi wa maneno hapakosi kuwa na maovu; Bali yeye
azuiaye midomo yake hufanya akili”.
Kwanini haisemi, katika Uchache wa maneno, hapakosi kuwa na maovu? Ni
kuonyesha kuwa, unapokuwa mzungumzaji kupitiliza, ni rahisi sana kujikwaa
ulimi na kisha kumkosea Mungu, lakini ukiwa si mwepesi wa kuzungumza
zungumza, yaani kila taarifa au habari unachangia, basi utajiepusha na maovu
mengi

83
SEHEMU YA SABA
KAZI NA UMUHIMU WA ROHO MTAKATIFU
Binadamu bila Roho Mtakatifu ni kiumbe aliyepoa na dhaifu sana, pia hana
makali katika utu wake wa ndani yaani namaanisha kuwa MKristo ambaye
hana Roho Mtakatifu ninaweza kumfananisha na Mbwa mkali abwekaye
lakini hana meno na ni kilema. kwasababu mtu huyu hawezi kufikia utumishi
wenye nguvu wenye kusababisha mapinduzi makubwa katika ulimwengu wa
roho.
Ili mtu aweze kuwa mtumishi hodari, shujaa, mwenye nguvu na mwenye
makali ya kiutumishi yampasa kubatizwa na Roho Mtakatifu.
Baadhi ya kazi za Roho Mtakatifu kwa mwamini katika maeneo
mbalimbali:
1. Katika maombi.
i. Roho Mtakatifu anayaongoza maombi ya mtu katika mapenzi ya
Mungu.
Roho Mtakatifu humsaidia mKristo kuomba mbele za Mungu kwa
kuzingatia vipaumbe vinavyohitajika katika maombi ambavyo Mungu
anavitaka mtu aombe mbele zake.Mfano: Tambua nafasi ya Mungu yaani
Baba(Baba yetu uliye mbinguni), Jina la Mungu litukuzwe kwanza,
Ufalme wake uje, Mapenzi ya Mungu yatimizwe lakini mapenzi ya
kwako yavunjike, hapa duniani na mbinguni, Upewe riziki yako yaani
kile unachostahili wala siyo unayoyatamani wewe, omba toba au
msamaha wa dhambi zako lakini ili na wewe usamehewe dhambi zako
na Mungu ni lazima na wewe uwasamehe waliokukosea, Omba usitiwe

84
majaribuni lakini uokolewe na yule mwovu, msifu Mungu kwa kuwa
Ufalme, nguvu na utukufu ni za Mungu milele na milele na mwisho
malizia kwa kukiri kuwa na iwe hivyo(Amina).
Mathayo 6:9-13 “⁹ Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina
lako litukuzwe, Ufalme wako uje, ¹⁰ Mapenzi yako yatimizwe, hapa
duniani kama huko mbinguni. ¹¹ Utupe leo riziki yetu. ¹² Utusamehe deni
zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. ¹³ Na usitutie
majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako,
na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]."Kwa ufafanuzi zaidi
kuhusu vipaumbe vya maombi jipatie nakala ya kitabu changu
kiitwacho vipaumbele tisa katika maombi yaletayo majibu"
watu wengi leo wanalalamika kuwa maombi yao hayajajibiwa na
Mungu hii inasababishwa na mambo ambayo mtu huyu anayafanya
ikiwemo yafuatayo
(a) Wanaomba vibaya: watu wengi Wanaomba vibaya ili wakavitumie
kwa manufaa yao, ndiyo maana hawapati. Yakobo 4:3 “Hata mwaomba,
wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa
zenu.”
(b) Wanaomba ili waonekane na watu (wasifiwe) na wawe maarufu.
(c) Hawajui kuomba jinsi ipasavyo. Warumi 8:26-27 " ²⁶ Kadhalika Roho
naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi
itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza
kutamkwa. ²⁷ Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa

85
kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu."

ii. Roho Mtakatifu humsaidia mtu ni namna gani ya kujiungamanisha na


msaada wa Mungu.
Roho Mtakatifu humsaidia mwamini kujiungamanisha na msaada wa
Mungu. Inamaanisha kwamba wakati unaenda kumwomba Mungu,
wewe kwanza unanini? Mfano: Musa aliulizwa na Mungu kuwa ana nini?
Musa akajibu kuwa ana fimbo, hatimaye tunaona Musa anajibiwa
maombi yake kwasababu anakitu mkononi mwake. Mwana maombi
kumbuka kuwa, wakati unamwomba Mungu je! kuna jitihada au
mipango ipi ambayo wewe umeipanga kwanza kuhusu jambo
unaloliomba? Mfano mtu anaomba apewe gari je! unahela hata ya
kulipeleka gari lako gereji likipata hitilafu?
 Kuna wimbi kubwa la watu leo wanaenda kuombewa makanisani
ili wapate magari, pesa na majumba, naomba msiwafananishe
wachungaji wa kweli wa Mungu kuwa kama waganga wa kienyeji.
Lakini pia wanamaombi wengi wamejikuta wanafanya maombi ya vita
katika Ulimwengu wa roho lakini wanasahau kumwomba Mungu
awalinde na vilipizi vya adui, hivyo hupelekea kushambuliwa na adui
kirahisi.

2. Katika huduma na karama.


 Huduma, karama na vipawa ambavyo MKristo amepewa na Mungu
vinapaswa kulelewa au kuwa chini ya uangalizi wa Mchungaji.

86
Pamoja na kwamba Mungu kaiinua vipi huduma, Karama au kipawa
chako lakini Mungu huyo huyo kaweka vitu vya ziada kwa Mchungaji
ili akusaidie kufika kwenye hatima yako nzuri.

Roho Mtakatifu hugawa Karama, huduma na vipawa kwa aliyeokoka


kama apendavyo yeye kusudi tu kazi ya Mungu itendeke kwa ufanisi na
kwa kufaidiana ndani ya kanisa la Mungu.
1Wakorintho 12:4-7 “⁴ Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye
yule. ⁵ Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. ⁶ Kisha
pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi
zote katika wote. ⁷ Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa
kufaidiana."

i. Ualimu.
Ualimu ni karama iliyotolewa na Mungu kwa mtu ili awasilishe, aweke
wazi mafumbo, aeleze maana, mazingira, na matumizi ya Neno la
Mungu kwa ajili ya maisha ya msikilizaji.Kwa waalimu wa Neno la
Mungu Roho Mtakatifu huwasaidia kuwasilisha,kuweka wazi
mafumbo,kueleza maana, mazingira,na matumizi ya Neno la Mungu kwa
upana na undani kwa ajili ya maisha ya msikilizaji wa Neno la Mungu
kuliko kuwafundisha watu kwa mihemuko au kwa lengo la kuwarushia
washirika wengine risasi zitakazo umiza mioyo yao.
ii. Uinjilisti.
Uinjilisti ni karama ya utendaji kazi wa Roho mtakatifu ndani ya mtu
ashuhudiae (mwenye kuinjilisha) matendo makuu ya Mungu kwa lengo

87
la kuokoa roho za watu wasiingie jehanamu ya moto. Watu wa namna hii
wanakuwa na mzigo mkubwa kuwaeleza watu wengine habari njema za
ufalme wa mbinguni na uzima wa milele na kwa sababu hiyo
wanachukia sana kitu kinachoitwa dhambi ndani ya mwanadamu.
Kwa kuwa Yesu alizifia dhambi zetu msalabani, hivyo mwinjilisti
huchukizwa kumuona mtu anayeifurahia dhambi.
Roho Mtakatifu humsaidia mwinjilisti kutoa Injili ya Mungu ambayo
haijagushiwa kwa namna yoyote ile. Injili huambatana na msamaha wa
dhambi, kufunguliwa katika vifungo pamoja na kurudi kwa Bwana Yesu
Kristo mara ya pili ulimwenguni kuja kulichukua kanisa lake.
iii. Utume.
Maana ya mtume ni "aliyetumwa"
Roho Mtakatifu humsaidia mtume kupeleka habari njema za Yesu Kristo
sehemu ambazo hazijafikika, pasipo kuangalia mazingira yapoje,
masilahi binafsi ya mtu, wala pasipo kuogopa uchawi, au nguvu za giza
zilizopo katika eneo lile.
iv. Unabii.
Nabii ni mtu anayetumiwa na Mungu kutangaza makusudi ya Mungu, au
ni msemaji wa Mungu. Nabii huwa hatabiri tu bali pia kuwasilisha
mafundisho ya Mungu, amri zake, na hukumu zake.
Unabii umegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni huduma ya
unabii na karama ya unabii. nitakufafanulia kama ifuatavyo; -
Huduma ya unabii. Huduma hii ilihusika na uonaji au utabiri wa
mambo yaliyopita, yaliyopo, na yajayo. Hiki ni kipawa ambacho

88
kilitumika katika Agano la kale kwa watu maalumu ambao Mungu
aliwachagua kipindi hicho(Manabii).
Karama ya unabii: Hii ni karama ambayo inahusu masuala ya utabiri
wa mambo yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Karama hii inatumika katika
Agano jipya yaani kuanzia kwa Yohana mbatizaji, Yesu Kristo
mwenyewe na kanisa lote kwa ujumla. Kwahiyo hakuna haja yeyote ya
kwenda kutabiriwa na manabii wa uongo chakufanya wewe zama ndani
ya Roho Mtakatifu ndiye atakaye kuonyesha Siri za mambo
yaliyofichika, yaliyopita, yaliyopo na yajayo.
2 Petro 1:21 “Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya
mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu,
wakiongozwa na Roho Mtakatifu.”
v. Uchungaji.
Roho Mtakatifu humsaidia Mchungaji katika mambo matatu yafuatayo; -
(a) Kulisha wana-kondoo wa Yesu Kristo.
Hapa inamaanisha kuwa, jukumu la Mchungaji ni kuwafundisha
waongofu wapya (wachanga katika wokovu) Neno la Mungu kwa upole,
maana ni wachanga bado, wameokoka tu hivi Karibuni na kuna mambo
mengi hawayajui, lakini pia ni namna gani ya kuwafundisha kuomba,
kuvaa, kunyoa kusuka, kuzungumza, kuishi maisha ya utakatifu.
(b) Kuchunga kondoo wa Yesu Kristo.
Hii inamaanisha kuwa katika kitengo hiki Mchungaji anatakiwa
awaelewe waKristo au washirika wake kuwa wamegawanyika katika
makundi matatu, ambayo ni waKristo wakomavu wa Kiroho, washirika

89
waliodumaa na washirika wa kawaida. Hivyo Mchungaji anatakiwa
ayasaidie makundi haya yote matatu vizuri ili yasitawanyike lakini yote
yakamuone Mungu mbinguni. Mathayo 26:31.
(c) Kulisha kondoo wa Yesu Kristo.
Katika sehemu hii Mchungaji anatakiwa awafundishe kanisa lote
kwanjia kama vile, Semina za Neno la Mungu za ndani, na mikutano ya
Injili ya nje. Ikiwezekana azigawanye Semina hizo kutokana na makundi
kama vile, Semina ya vijana, Semina ya wababa, Semina ya wamama,
Semina ya watoto, Semina ya wainjilisti, waalimu, manabii, mitume.
Yohana 21:15-17 " ¹⁵ Basi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simoni
Petro, Je! Simoni wa Yohana, wewe wanipenda kuliko hawa?
Akamwambia, Naam, Bwana, wewe wajua kuwa nakupenda.
Akamwambia, Lisha wana-kondoo wangu. ¹⁶ Akamwambia tena mara ya
pili, Simoni wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Ndiyo, Bwana, wewe
wajua kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. ¹⁷
Akamwambia mara ya tatu, Simoni wa Yohana, wanipenda? Petro
alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, Wanipenda?
Akamwambia, Bwana, wewe wajua yote; wewe umetambua ya kuwa
nakupenda. Yesu akamwambia, Lisha kondoo zangu."

3. Katika ndoa na familia.


i. Kabla ya ndoa/uchumba.
Roho Mtakatifu humsaidia mwamini katika kumpata mke au mme sahihi
aliyeumbwa na Mungu kwa ajili yake wa kufanana naye. Japo unaweza

90
kumpata mke au mme kwa kufuata matamanio au matakwa yako binafsi
lakini siku moja utalia, utaomboleza na utajutia kuwa na huyo mke au
mme ambaye umemuoa/ kuolewa naye kwasababu huyo sio mkeo au
mmeo kutoka kwa Mungu. Roho Mtakatifu husema na mwana wa
Mungu ambaye ana uhusiano mzuri na Mungu yaani yule aliyejazwa
Roho wa Mungu, maana Mungu atasema naye mke au mme wake sahihi,
aliyeumbwa kwaajili yake na wakufanana naye.
Mithali 31:10-12 "¹⁰ Mke mwema, ni nani awezaye kumwona? Maana
kima chake chapita kima cha marijani. ¹¹ Moyo wa mumewe humwamini,
Wala hatakosa kupata mapato. ¹² Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote za maisha yake."
ii. Kwenye ndoa. Roho Mtakatifu huwasaidia wanandoa kuishi maisha
matakatifu, yakuaminiana, yakuvumiliana, yakufurahiana,
yakuvumiliana, yakutendeana wema, yakufadhiliana, yakupendana na
yakuheshimiana.
iii. wazazi na watoto. Roho Mtakatifu husaidia ndani ya familia kuona
thamani ya kila mwanafamilia katika familia ili familia iwe na Amani,
furaha, Upendo, kuvumilia, kuthaminiana, kuheshimiana kati ya Baba na
Mama, Baba na watoto, Mama na watoto, Watoto kwa watoto.
Waefeso 6:1-5 "¹ Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana
hii ndiyo haki. ² Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo
amri ya kwanza yenye ahadi, ³ Upate heri, ukae siku nyingi katika
dunia.⁴ Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni
katika adabu na maonyo ya Bwana.⁵ Enyi watumwa, watiini wao walio

91
bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa
moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;

4. Katika kunena na mazungumzo.


Roho Mtakatifu humwezesha mwamini kuwa shahidi wa kweli wa
Bwana Yesu Kristo, shahidi ni shuhuda wa jambo ambalo kimsingi
anaufahamu na taarifa sahihi nalo. Shida kubwa ambayo inayolikumba
kanisa la leo ni kwamba waKristo wengi sio mashuhuda wazuri wa
habari njema za Yesu ni hii ni kwasababu ya kumwekea Roho Mtakatifu
mipaka kwao.
1 Yohana 5:7 “Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye
kweli.”

Umuhimu wa Roho Mtakatifu kwa mwamini.


Mpango wa Mungu kukufikisha mahali pa utulivu na kustarehe haizuiliwi na
jinsi ulivyoanza safari au hali uliyonayo kwa sasa. Mungu anaweza kufanya
jambo jipya muda wowote kwako. Haijalishi ulianza kwa ugumu kiasi gani au
vizuri namna gani na sasa hali ikoje. Mungu hamuachi mtumishi wake
atembee peke yake. Unapohisi upweke ndani yako kumbuka kuwa una Yesu
Kristo asiyemuacha mtu yeyote. Fukuza roho ya hofu maana haitoki kwa
Mungu.

1) Ni ahadi iletayo nguvu kwa kila aaminiye.


Baada ya mwanadamu kupata ondoleo la dhambi lililotokana na toba,
kubatizwa ubatizo wa maji mengi mtu ana haki ya kupokea kipawa cha

92
Roho Mtakatifu, kwa kuwa hii ni ahadi iletayo nguvu kwa kila aaminiye,
watoto wake na kwa watu wote walio mbali na Kwa wate watakaoitwa
na Bwana Mungu wetu wamjie.
Matendo ya Mitume 2:38-39 "³⁸ Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe
kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu,
nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu. ³⁹ Kwa kuwa ahadi hii ni
kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na
kwa wote watakaoitwa na Bwana Mungu wetu wamjie".

2) Ni msaidizi atakaye ishi na nasi milele.


Msaidizi ni mtu anayetoa msaada wa kitu fulani kwa mwingine.
Mwanadamu amepewa uwezo na Mungu wa kufanya mambo kadhaa
lakini kuna mambo ambayo mwanadamu hayawezi, hivyo anahitaji
kusaidiwa na Roho Mtakatifu katika kweli yote kwasababu mwanadamu
hajitoshelezi.
Yohana 14:16-17 “¹⁶ Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi
mwingine, ili akae nanyi hata milele; ¹⁷ ndiye Roho wa kweli; ambaye
ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui;
bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani
yenu."

3) Ni mkamilishaji wa maisha ya utakatifu wa mtu.


Roho Mtakatifu amjiapo au amjazapo mtu humkamilisha kwenye kweli
yote, maisha ya utakatifu, kwasababu Roho Mtakatifu haneni kwa shauri

93
lake mwenyewe, bali mambo yote atakayoyasikia kutoka kwa Mungu
huyanena pamoja na kumpasha mtu habari za mambo yajayo.
Yohana 16:13 “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli,
atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa
shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo
yajayo atawapasha habari yake.”

4) Ni msaidizi wa mtu katika kuishi maisha matakatifu.


Roho Mtakatifu hufunua habari ya mambo matatu kwa mwamini
ambayo ni dhambi, haki, na hukumu ili mtu aweze kuishi maisha
matakatifu. Maana dhambi hufunua sheria, Haki hutoa faraja ya jambo
fulani na Hukumu hutoa faraja au adhabu.
Yohana 16:7-8 “⁷ Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi
mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja
kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. ⁸ Naye akiisha
kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na
hukumu."

5) Hutuletea taarifa za Mungu ndani yetu kwa njia ya ndoto, maono, sauti,
Neno, sauti ya upole nakadhilika.
Roho Mtakatifu hutuletea taarifa za Mungu kwa njia zaidi ya kumi na
hutusihi sana tusifanye mioyo yetu kuwa migumu hata tukapingana na
matakwa au mapenzi ya MUNGU.

94
Waebrania 3:7 “Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu, Leo, kama
mtaisikia sauti yake,”
6) Hutumia hukumu na adhabu kuturudi kama watoto wapendwao na
Mungu.
Roho Mtakatifu hutumia hukumu kutoa adhabu lakini si kwa lengo baya,
bali ni kwa lengo la kumrudi mtu kama mtoto apendwaye na Mungu ili
mtu huyu atubu kwa machozi ili awe msafi katika utu wake wa ndani.
Ufunuo wa Yohana 3: 19,22 (¹⁹ Wote niwapendao mimi nawakemea, na
kuwarudi; basi uwe na bidii, ukatubu.
²² Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia
makanisa. )
7) Hutusaidia kumtumikia Mungu kwa nguvu (nguvu ya kuwa mashahidi
wa kweli).
Roho Mtakatifu hututia nguvu ya kumtumikia Mungu kwasababu
mwanadamu ni kiumbe dhaifu sana, hivyo anahitaji kusaidiwa na Roho
Mtakatifu ili awe shahidi au shuhuda mzuri wa habari za Mungu kwa
watu wote.
Matendo ya Mitume 1:8 “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu
yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika
Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa
nchi.”

95
“Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na
amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini,
katika nguvu za Roho Mtakatifu.” Warumi 15:13.

96
KUHUSU MWANDISHI: DAUDI PIUS
Daudi Pius ni Mwalimu na Mwinjilisti wa Neno la Mungu katika Huduma. Ni
mzaliwa wa mkoa wa Shinyanga, Wilaya ya Shinyanga vijijini, kata ya Nyida.
Pia ni Mwalimu kwa taaluma na mfuasi wa Shahada ya Awali ya Elimu katika
Sayansi, Teknolojia, Habari na Mawasiliano (Bachelor of Education in
Science with Ict) katika Chuo kikuu cha Dodoma(UDOM) mwaka 2020-2023;
mahsusi kwenye masomo ya Kemia na TEHAMA. Katika muda wote wa
masomo shuleni na chuoni amekuwa ni mwanaumoja wa wanafunzi wa
madhehebu ya kipentekoste Tanzania waliookoka mashuleni, vyuoni, na vyuo
vikuu katika umoja wao unaojulikana kama CASFETA-TAYOMI. TAYOMI
(Tanzania Youth Ministries) ni huduma inayolea vijana mashuleni, vyuoni na
vyuo vikuu hapa nchini Tanzania. Na hivyo, CASFETA (Christ’s Ambassadors
Students Fellowship Tanzania) ni mkakati ulioanzishwa na TAYOMI ili kulea
vijana kutokea madhehebu mbalimbali ya kipentekoste yasiyokuwa na utata
wa kiimani. Hivyo amekuwa katika kumtumikia Mungu kwa ngazi mbalimbali
za uongozi tangu kanisani, shuleni na
chuoni pia.

Mawasiliano:
Namba ya simu: +255 (0) 65 633 9872
What'sApp: +255 (0) 65 633 9872
Instagram: @daudimballa
Email: mbaladaudi15@gmail.com

97
MAREJEO

Dag Heward-Mills (2016), Mmoja wenu ni shetani. Parchment House

Gasto Alex Didas. (-). Historia ya Biblia na waandishi wake. Mabatini-


Mwanza, Tanzania

Rev.Ndei Reuben. (2020), Sanaa ya uchumba hadi ndoa yenye majibu ya


maswali 100 tata yanayowahusu vijana. ISBN:978-9987-580-53-8

Mikaeli Memiri. (2016), Siri za utumishi madhabahuni. Gracious Printing


Press

98
MATUNDA9YAROHOMTAKATI
FU
t
KiabuhikiM atunda9yaRohoM t akat ifu nims aadamkubwa
kwaMKr it
sokuishimaishay auhals
iiay aKi i
krt
sokat kaki
i zazihikii
,i
l
e
kulta uamsho na mat engenezo ndaniy ake ,na kukaa na Roho
Mtakatf
iuilikufanya mape nzimakami lf
iuy a Mungu.ki tabu hiki
nahus
ki u Matunda tiay
s a Roho Mt akat f
iu(Wagal i
ata5 :22-23,na
)
l
niki
i t
ia"Matundat s
iayaRohoMt akat f
iu"kwas ababuki nac hunguza
maday aMat undat s
iay aRohoMt akatifukwaki nanauf asaha.Hiini
ki
kuhaki ha hat
s a kama ul pokuwa unas
i oma pe ngine hukue lewa
Matundatiay
s aRohoMt akatiuuki
f wape key ako,bas ikupi i
takitabu
kiuki
hi kioma kwa umaki
s ,pol
ni epolei kibidina f ami ay
i
l ako y ote
t
iakuwani ambol
j t
i ol
akal e amapi
t nduz ichany akat kamai
i shay nuy
e a
k i r o h o .

Piaki abuhi
t kikinaee
l zakwakinamat endoambay oMKr s
itoanatakiwa
ay s
ai ,
hi yaanimai hay
s autauwanaus hindidhidiy avishawihi
s vyamwi i
l
vinavyochoc hewanat amaaz amwii
l pamoj anaadui shetaniMKr
. s
ioi
t i
l
akami lkei
i natakiwahakiy akekwaMungui zdihakiy
i awaandi s ,
hi
Maf ars
iay o na washika diniiikuwe
l za kuurihiUf
t almewa Mungu.
Wanadamut ulumbi
i wamai shamazuriy akupe ndeza,nai napotoke a
tunapitiamagumut unaumi amnokiasikwambat unakumbukamai sha
yaEde niy alvy
i okuwamaz urinakami lf
iukablay akumkos eaMungu;
baaday akumt endaMungudhambi ndi poushii
rkanauhus ianokati ya
Mungu na mwanadamu ukavunjika.

KUHUS
UMWANDI
SHI
Daudi PiusniMwal i
munaMwi nji
lis
tiwaNe nola
Mungukat i
kaHuduma. Nimz al
iwawamkoawa
S
hinyanga, Wil
ay ay aS
hinyangavi j
ij
i
ni,
katay a
Ny i
da. PianiMwal i
mukwat aaluma namf uas
i
waS hahaday aAwal i
yaEl i
mukat i
kaS ay
ansi
,
Teknoloji
a,Habar inaMawas i
li
ano( Bachel
orof
EducationinSciencewit
hI c
t)katikaChuoki kuu
c
haDodoma( UDOM)mwaka2 020- 2023;
mahs us
i
kwe nyemas omoy aKemi anaTEHAMA.

You might also like