You are on page 1of 2

UBATIZO WA MAJI

Waebrania 6:1-2
Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili
tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na
imani kwa Mungu,
na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya
milele.
Kulingana na mistari hii miwili, kuna mafundisho ya kwanza katika ukristo,
ambayo inatarajiwa mwanafunzi yeyote wa Kristo ayafahamu na kuyafanyia kazi
mara tu anapomwamini Kristo.
Mojawapo katika hayo ni Mafundisho ya mabatizo (Neno mabatizo ni wingi wa
ubatizo, nah ii ni kwa sababu kuna aina kuu mbili za ubatizo katika Kristo)
Ubatizo wa kwanza ni ubatizo wa Maji, na ubatizo wa pili ni ubatizo wa Roho
Mtakatifu. Aina hizi zote mbili ni mojawapo ya mafundisho ya awali kabisa katika
ukristo, na inatarajiwa mtu anapomwamini Kristo, basi apitie aina hizi zote mbili
za ubatizo.
Katika somo hili, tutaangalia kwa ukaribu sana kuhusu ubatizo wa maji, na
tutatazama kwa makini dondoo zifuatazo.
o Maana ya neno Ubatizo
o Ubatizo wa maji ni nini?
o Ni wakati gani ninatakiwa nibatizwe kwa maji?
o Ni aina gani ya ubatizo ni sahihi?
o Kuna faida gani za kubatizwa kwa maji?
Maana ya Neno Ubatizo
- Asili ya neno ubatizo ni neno la kiyunani, baptizo lenye maana zamisha au
tumbukiza
- Ukichunguza katika matukio ya biblia yaliohusisha ubatizo, utaona kilichotukia ni
kuzamishwa kwa aliyebatizwa, kwa sababu ndiyo maana halisi ya Neno ubatizo.
- Mfano mzuri ni katika kubatizwa kwa Yesu, dhahiri kabisa inaonyesha Yesu
alizamishwa majini.
o Mathayo 3:16
Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara akapanda kutoka majini; na
tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama
hua, akija juu yake;
Yohana alikuwa akibatiza katika mto Yorodani, na inaonyesha wazi kuwa Yesu
alibatizwa katika mto huo, na baada ya kubatizwa akapanda kutoka majini
- Pia hata katika ubatizo wa Roho mtakatifu, kinachofanyika ni mtu kuzamishwa
katika Roho mtakatifu, na baadaye kinachofuata ni kujazwa na Roho mtakatifu.
o Mttendo 2:2
Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu
ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

Kilichotokea hadi mitume wakabatizwa kwa Roho mtakatifu ni kwamba Roho
mtakatifu alishuka kama upepo uvumao, na kuijaza nyumba yote. Kwa hiyo
kwa kifupi nyumba nzima ilikuwa imejawa na Roho mtakatifu. Na tunaweza
kusema kwa wakati huo wanafunzi wote walikuwa wamezamishwa ndani ya
Roho mtakatifu.
- Kwa hiyo katika aina zote mbili za ubatizo zinahusisha mtu husika kuzamishwa,
na hiyo ni kulingana na maana halisi ya neno ubatizo.
- Kwa hiyo kama haihusishi kuzamishwa, basi hiyo siyo ubatizo wa kibiblia, bali ni
ubatizo wa kisasa kulingana na tafsiri za kisasa.

Ubatizo wa Maji ni nini?

- Baada ya kuelewa maana ya ubatizo, sasa tuangalie maana ya kubatizwa kwa
maji.
- Kwa kifupi kabisa, ubatizo wa maji hasa katika agano jipya ni kuzamishwa katika
maji kwa Jina la Yesu Kristo (Jina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu).
Ni wakati gani ninatakiwa nibatizwe kwa Maji?

You might also like