You are on page 1of 2

KILA SAMAKI ANAYEVULIWA AMEBEBA SHEKELI

Lakini tusije tukawakwaza, enenda baharini ukatupe ndoana, ukatwae samaki


yule azukaye kwanza; na ukifumbua mdomo wake utaona shekeli ichukue hiyo
ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako - Mathayo 17:27.


Kutoka kwenye maandiko, kila mtoto wa Mungu ni tawi lizaalo matunda, na matarajio ya Mungu ni
kwamba kila tawi lizae matunda. Na siyo tu kuzaa matunda, bali kuzaa sana (Yohana 15:8). Hii ni kwa
sababu Baba yetu kule mbinguni anatukuzwa tunapozaa matunda sana.
Yesu alisema nitawafanya kuwa wavuvi wa watu. (Mathayo 4:19). Kutoka kwenye andiko la ufunguzi
hapo juu, kila samaki anayevuliwa amebeba shekel; ni shekeli yenye thamani kubwa. Thamani yake ina
uwezo wa kukomesha kila manyanyaso na masumbufu katika maisha ya kila mmoja. Lakini ni lazima
umvue samaki kabla ya kuipata shekeli. Haijalishi ni aina gani ya samaki. Kila samaki unayemkamata ana
shekeli mdomoni mwake.
SHEKELI INA THAMANI GANI?
Ugavi wa Kiungu
Kuvuna nafsi kunatuunganisha na ugavi wa kiungu. Kama ilivyoandikwa, Naye avunaye hupokea
mshahara. Mshahara unahusisha kazi za kimuujiza, watoto wa kimuujiza na Baraka za kila namna.
(Yohana 4:36/Luka 22:35)
Afya ya Kiungu
Kwa sababu Mungu ametutuma kama kondoo kati ya mbwa mwitu. Hivyo ametupa uweza wa
kukanyaga nyoka na nge ili kwamba kitu chochote kisitudhuru kwa namna yoyote. Pia, kila anayevuna
nafsi ni balozi/mjumbe na anastahili kinga kila eneo. Hii ndiyo sababu kuvuna nafsi kunakuhakikishia
ulinzi dhidi ya mashambulizi ya shetani (Luka 10:19/Mathayo 10:16)
Kibali cha Mungu
Tunapojihusisha na kazi ya Mungu hapa duniani, tunachochea kuachiliwa kwa kibali chake maishani
mwetu. Wokovu wa nafsi za watu ndiyo kusudi la msingi la Mungu hapa duniani. Kwa hiyo ni nafasi bora
sana ya kukutana na kibali cha Mungu. Hii ndiyo inafanya kibali kuwa urithi wa kila anayevuna nafsi.
Miongoni mwa mambo mengine, Kibali huleta ndoa za kimuujiza, urejesho wa ndoa, kuinuliwa, n.k.
(Zaburi 102:13-15)
Mipenyo ya Kiungu
Petro aliwekeza katika kuvuna nafsi za watu kwa kutoa mashua yake kwa Kristo naye akapokea mpenyo
wa kiungu kama faida. Kwa namna hiyo hiyo, kila atakayemruhusu Kristo amtumie kama chombo cha
kuwafikia watu wengine anastahili mpenyo wa kiungu. (Luka 5:1-7)
Ishara na Maajabu
Kuvuna nafsi kunaamuru kutendeka kwa ishara na maajabu yanayogusa kila eneo la uhitaji wa watu.
Nao wale wakatoka, wakahubiri kotekote, Bwana akitenda kazi pamoja nao, na kulithibitisha lile neno
kwa ishara zilizofuatana nalo. (Marko 16:20/Yohana 14:21)
Hatimaye, Yesu alisema, Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami
nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote
mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. (Yohana 15:16) Hii inafanya kuvuna nafsi kuwa ni fursa ya
kiagano kwa mahitaji yetu yote kutimizwa. Kwa hiyo, inuka na ujiandae kupata kazi za ajabu na matendo
ya ajabu katika mwaka huu mkuu kwa kujihusisha kikamilifu katika kuvuna nafsi na kuziimarisha, nawe
utapata mgeuko kamili katika kila eneo. Yesu ni Bwana!

You might also like