You are on page 1of 5

URAIA WA MBINGUNI NA DUNIANI

WAFILIPI 3:20-21

“Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni, kutoka huko tena tunamtazamia

mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakaye ubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na

mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote

viwe chini yake.”

Kuna aina mbili za uraia ambazo Binadamu anaweza kuwa nazo. Uraia wa duniani

hapa na uraia wa mbinguni.

Mtu anapozaliwa kupitia wazazi wa dunia hii (baba ba mama), anaandikishwa katika

kitabu cha serikali cha vizazi na vifo, ambacho kinapatikana wilayani, mahali pale

alipozaliwa mtu huyo. Kinaandaliwa cheti cha kuzaliwa mahali pale alipozaliwa. Hivyo moja

kwa moja anatambulika kuwa na uraia wa mahali pale, au nchi ile alipozaliwa.

Na hata baada ya kufa, mtu huyo atawekwa katika kumbukumbu la watu waliokufa,

katika kitabu cha vizazi na vifo pale wilayani, hivyo kumbukumbu lake linatoweka katika

dunia hii lakini bado anaandikishwa katika kitabu hicho pale alipokuwa raia wa nchi hiyo.

Uraia huu wa kidunia sio wa kudumu, kwa sababu ni wa muda mfupi tu, si wa milele.

Na wakati mtu anapokuwa na utambulisho wa uraia katika taifa hilo kama vile Tanzania,

serikali inakuwa na jukumu la kuhakikisha usalama wa raia huyu awe mahali pale

alipozaliwa katika nchi yake au awe sehemu nyingine kama vile nje ya nchi, Kuhakikishiwa

usalama wake ni kwa mujibu wa katiba ya nchi; kwa Tanzania ni haki ya kikatiba

kuhakikisha usalama wa raia huyo.

Pia kulingana na haki ya kuishi kila mtu anakuwa na haki ya kuishi na kupata kutoka

katika jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria. [haki ya kuwa hai sheria ya

mwaka 1984 Na. 15 ibala ya 6]

1
Hiyo ndiyo maana kunapotokea tukio lolote lenye kuhatarisha usalama wa raia

(ambaye ana uhalali wote wa kuishi au kufanya kazi mahali pale pasipo kuvunja sheria au

kufanya uhaini katika namna au njia yoyote), hapo serikali inachukua hatua za haraka za

kutetea usalama wake pia kumlinda na kutengeneza mazingira salama ya mtu huyo ili

aendelee kupata haki zake zote kikatiba na kisheria.

Hii ndiyo maana imeshatokea baadhi ya mataifa mawili kuingia mgogoro na baadae

kutibua uhusiano wa kidiplomasia baina ya hizo nchi mbili pale inapokuja kutambulika kuwa

raia wake amehatarishiwa usalama wake au hata kupoteza uhai wake katika mazingira

tatanishi akiwa katika nchi hiyo nyingine. Hii ni moja ya mambo ya msingi na nyeti kabisa

katika kuupigania uhai wa raia wa nchi husika.

Hivyo basi uraia huu wa kidunia (ambao si wa milele) ni wa lazima na muhimu

kuulinda kwa jitihada zote.

Kwa hiyo uraia huu wa kidunia ni uraia wa kimwili ambao ni muhimu sana

kuzingatiwa na unakoma pale mtu atakapotoweka, atakapotangulia kuondoka hapa duniani.

Kwa wakristo, wanasema atakapo lala. (kwa sababu upo wakati ataamka-siku ya mwisho

katika ufufuo).

Na hivyo tukiwa katika mwili huu na uraia huu wa duniani maandiko matakatifu

yanatuhimiza kuandaa mazingira ya kuishi kwa haki na kweli ili kujiandaa kwa ajili ya uraia

mwingine ambao ni wa milele na usio na kikomo hasa tukijua kwamba ipo hesabu ya kuja

kuitoa kulingana na kile tulichokifanya hapa duniani katika uraia huu wa muda mfupi.

Uraia wa milele ni wa mbinguni, unapatikana kwa kuzaliwa mara ya pili, kuzaliwa

kiroho, baada ya kumwamini Bwana Yesu Kristo, kumpokea na kubatizwa katika maji. Mtu

huyo anakuwa kiumbe kipya katika ufalme wa mbinguni (ulimwengu wa roho/usioonekana),

anakuwa amezaliwa katika ufalme wa Bwana Yesu Kristo. Anapokea uraia wa mbinguni.

Angalia hapa Yesu anaongea na mwalimu mkubwa sana wa kiyahudi jina lake Nikodemo.

2
YOH 3:1-6.

“.....Yesu akamjibu akamwambia Amini, amini nakuambia mtu asipozaliwa mara

ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia awezaje mtu kuzaliwa

akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa?

Yesu akajibu akasema, amini Amini nakuambaia mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho

hawezi kuuingia ufalme wa Mungu...... ”

Bwana Yesu anasema mtu hawezi kuuona [kuuelewa] ufalme wa Mungu. Maana kuna

kuuona na pia kuna kuuingi. Wapo waliouona (kuuelewa) lakini wasiingie kama Yuda

Eskarioti. Kwa sababu naye aliuelewa na kuuona na aliahidiwa kuuingia (LUKA 10:20)

lakini hakuingia (YOHANA 17:12).

Lakini kuingia katika ufalme wa Mungu tunaingia kwanza katika Roho, tunakuwa

wafalme katika ulimwengu wa kiroho. Watawala katika ulimwengu wa kiroho, tunaketi

pamoja na Kristo katika ulimwengu wa kiroho, EFESO 2:6 lakini tutaingia katika mwili

baada ya kutoka katika mwili huu wa uharibifu, wa magonjwa na wa kuzeeka.

Hivyo mtu huyo aliyezaliwa mara ya pili, ni raia wa mbinguni, amezaliwa katika

ufalme wa mbinguni, ameikana dunia na mambo yake yote. Naye kwa mujibu wa maandiko

matakatifu, basi hapa duniani anakuwa ni Balozi wa Bwana Yesu Kristo (2KOR5:20), kwa

sababu ipo siku atarudi katika nchi yake ya milele, ambako kuna maisha ya milele ya raha na

faraja. Na akirudi huko atatakiwa kwenda kutoa hesabu ya kazi zote alizofanya hapa duniani

akiwa katika nchi ya hii ya ugeni-duniani akiwa katika uraia wa kidunia ambao ni wa muda

mfupi tu.

Pia tunapokuwa katika uraia huu wa muda mfupi, tunajitahidi kutafuta tiba ya haraka

tunapopatwa na matatizo ya kiafya, hata tunaweka bima ya afya ili kujihakikishia afya njema

wakati wote wa maisha. Hii ndio maana yapo mataifa mengi yaliyojiwekea sheria ya utoaji

wa huduma za afya kwa kutumia utaratibu wa bima. Kwa mfano serikali ya Tanzania ipo

3
katika hatua ya kutaka kupitisha sheria itakayowafanya watu wote kuwa katika mfumo wa

bima ya afya. Hii ni kwa sababu kila mtu ana haki ya kuishi kwa kuhakikishiwa huduma ya

afya na ya uhakika wakati wote na mahali popote alipo.

Pia tunahifadhi madawa ya hospital na huduma ya dharura (first aid) majumbani,

kazini, shuleni,n:k ili kupata tiba ya awali endapo itatokea dharura ya kiafya katika mazingira

ambayo ni vigumu kumuona daktari muda huo huo. Wakati mwingine tunapata masomo

kutoka kwa matabibu na wataalamu wa afya kuhusu afya zetu kupitia vyombo vya habari

kama TV.

Hii yote inaonyesha kwamba tunapenda kuishi tena bila kuzeeka. Maana upo ukweli

kwamba kila mtu hapendi kuzeeka haraka. Hasa kama maisha yamekuwa na mafanikio na

matatizo ni machache yenye misukosuko ya nadra. Na hata kama leo hii ingetokea mtu

anauza kwa gharama kubwa sana dawa ya kurefusha maisha, basi watu wengi wangejitahidi

kuuza kila alichonacho ili kununua dawa hiyo ili apate kuendelea kufanya maendeleo yake na

kupata mafanikio aliyokusudia na kutimiza maono aliyojiwekea katika maisha.

Unaona jinsi ambavyo watu wanataka kuishi milele katika raha? Na huo ni uraia wa

dunia hii tiu, ni uraia wa muda mfupi tu, lakini unang’ang’aniwa kweli kweli.

Sasa basi ikiwa maisha ya dunia hii ni muhimu sana, je si zaidi maisha ya milele?

Ikiwa uraia wa dunia hii ni muhimu sana, je si zaidi uraia wa mbinguni? Uraia wa mbinguni

ulipotezwa pale Bustani ya Edeni, maisha ya milele yalipotea pale Edeni baada ya anguko la

Adamu na Hawa. Mahusiano kati ya Mungu na binadamu yalitibuliwa pale na hivyo kuingia

laana ya kifo kwa binadamu. Laana ambayo haikutakiwa kuwepo hapo kabla ya dhambi

Lakini Mungu wa upendo alimleta Bwana Yesu ili tupate uzima wa milele, naye ndiye mti

wa uzima, ili tuingie katika ahadi ya kuishi milele baada ya msamaha wa dhambi. Kwa njia

ya kuamini kifo na kumwagika kwa damu yake pale msalabani kalvari. Tunajihakikishia

nafasi yetu ya kuja kuishi milele katika ufalme wa Mungu.

4
Maisha ya milele, uraia wa mbinguni haununuliwi kwa fedha ili kuupata, wokovu

haupatikani kwa kutoa hongo ili kuupata ila ni kwa imani tunaokolewa, kwa neema tumeitwa

ili kuurithi ufalme wa Mungu.

Na hakuna njia nyingine ya kuingia katika ufalme wa Mungu ili kupata uraia wa

mbinguni ila ni kwa kumwamini Bwana Yesu. Kuamini ile kazi iliyofanyika pale msalabani

kalvari. Wapo watu wanaopinga wokovu kwa kusema kuwa njia ya kuingia katika ufalme wa

Mungu ni kutenda mema tu. Sasa huo ni upotovu kwa sababu kifo cha Yesu msalabani

kitakuwa hakina maana. Lakini yesu alisema kuwa yeye ndio njia, kweli na uzima

(YOHANA 14 :6). Kwa kumwamini Yeye tumepona (ISAYA 53 :5, 1PETRO2 :24).

Sasa mtu akisema kwamba anaingia katika ufalme wa Mungu kwa kuzijua amri za

Mungu na kuzishika na kuzitii na kukataa sadaka iliyotolewa pale msalabani kalvari ni sawa

na mtu anayetaka kwenda mbinguni kwa mguu. Yesu alisema pasipo yeye sisi hatuwezi kitu.

(YOHANA 15 :5) Hivyo ni lazima kuifuata kanuni aliyoiweka Mungu kwamba tunamuhitaji

Yesu ili tuweze kuwa mfano na sura ya Mungu kama ilivyokuwa pale bustani ya edeni, kwa

sababu tokea pale ndipo tulipoteza utukufu wa Mungu na Adamu wa pili (Yesu) ndiye

aliyeahidiwa kuja kutupatanisha na Mungu (2WAKORINTO 5 :19). Hakuna mtu

atakayejipatanisha na Mungu kwa kujitahidi kutenda mema na kushika amri za Mungu na

kumkataa Bwana Yesu. (LUKA 18:19-25) Tunaokolewa kwa neema, sio kwamba Mungu

anawatafuta wale wanaojua kutenda mema ndio awape wokovu, hapana. (WAEFESO 2 :8).

Mungu anawatafuta waliopotea ili waokolewe, waijue neema na wakae katika neema hiyo

(LUKA 19 :10). Hii ndio maana ni vigumu sana kuokolewa mtu anayeamini na kujijua kuwa

anamjua Mungu (YOHANA 8 :24).

MUNGU ATUBARIKI

0763-53-25-56

You might also like