Professional Documents
Culture Documents
2022
Waebrania 9:16-22, “Maana agano la urithi lilipo, lazima iwepo mauti yake
aliyelifanya. 17 Kwa maana agano la urithi lina nguvu palipotukia kufa kwa mtu;
kwa kuwa halina nguvu kabisa, akiwa yu hai yeye aliyelifanya. 18 Kwa hiyo hata
lile la kwanza halikuanzwa pasipo damu. 19 Maana kila amri ilipokwisha kunenwa
na Musa kwa hao watu wote, kama ilivyoamuru sheria, aliitwaa damu ya ndama na
ya mbuzi, pamoja na maji na sufu nyekundu na hisopo, akakinyunyizia kitabu
chenyewe, na watu wote, 20 akisema, Hii ni damu ya agano mliloamriwa na
Mungu.
21 Na ile hema nayo na vyombo vyote vya ibada alivinyunyizia damu vivyo hivyo.
22 Na katika Torati karibu vitu vyote husafishwa kwa damu, na pasipo kumwaga
damu hakuna ondoleo.
1. Maana ya Agano
Kila agano lina mambo makuu matatu; kwanza AHADI; yaani manufaa ya hilo
agano au kusudi la hilo agano, pili kila agano lina MASHARTI, yaani mambo
yanayofanya agano liweze kudumu, tatu kila agano lina SADAKA, yaani kitu
ambacho kinatolewa ili mtu apate AHADI.
2. Maana ya Damu
Biblia inasema damu ni UHAI. Walawi 17:11 “Kwa kuwa uhai wa mwili u
katika hiyo damu, nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili
kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo
upatanisho kwa sababu ya nafsi”.
"Msipo ula mwili wake mwana wa Adamu, na kuinywa damu yake, hamna
uzima ndani yenu" (Yohana 6:53).
Dhambi huleta mauti (Warumi 6:23), “ili dhambi iwe dhambi hasa, huleta
mauti” yaani, dhambi humwaga damu (Warumi 7:13). Kwa sababu hii wana
wa Israel walitazamiwa kumwaga damu ya mnyama kila wakati walipotenda
dhambi, ili kuwakumbusha kuwa dhambi inaleta mauti, maana pasipo
kumwaga damu hakuna ondoleo la dhambi (Waebrania 9:22).
Kwa sababu hii, Adamu na Hawa walipojifunika wenyewe na majani ya mtini
hayakukubalika; badala yake, Mungu alimchinja mwanakondoo na kuwagawia
ngozi za kujifunika dhambi zao (Mwanzo 3:7, 21 Mstari wa 21 unasema,
“BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi,
akawavika”). Vivyo hivyo, dhabihu za wanyama wa Habili ilikubalika zaidi
kuliko matoleo ya nafaka na mboga ya Kaini, kwa kuwa alielewa jambo hili ya
kwamba pasipo kumwaga damu ingekuwa vigumu kusamehewa na kukubalika
kumkaribia Mungu (Mwanzo 4:3-5).
Ibrahimu. Mwanzo 17:10, “hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi
na wewe, na uzao wako baada yako, kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa”
Yeye hapo mwanzo aliitwa Abramu maana yake “Baba” maandiko yanasema
Mwanzo 17:5 Mungu akamwambia hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako
litakuwa Ibrahimu kwani nimekuweka kuwa Baba wa mataifa mengi”.
Biblia inasema katika Kutoka 2:23-24, “hata baada ya siku zile mfalme wa
Misri akafa, wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia,
kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa, Mungu
akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na
Ibrahimu na Isaka na Yakobo”.
Yesu amenituma ili uweke agano jipya na Yesu Kristo leo naye hatakuacha
milele. Israeli waligua, najua nawe unaugua, nafsi yako inaugua, natangaza
Mungu atakukumbuka leo.
Musa. Baada ya Mungu kutoa amri kumi, maandiko yanasema wana wa Israeli
walifanya agano na Mungu. Kutoka 24:8, “Ndipo Musa akachukua ile damu,
akainyunyiza juu ya watu akasema, hii ni damu ya agano ambalo Bwana
amefanya nanyi kufuatana na maneno haya yote”
Isaya 28:15 inasema “kwa sababu mmesema, tumefanya agano na mauti,
tumepatana na kuzimu, pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi, kwa
maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya
maneno yasiyo kweli”. Imeandikwa Isaya 28:18, “Na agano lenu mliloagana
na mauti litabatilika” Kwa damu ya mwana-kondoo kila agano lililowekwa na
mababu, agano na kuzimu, na waganga, na wasoma nyota, na wapiga ramli,
ili kuharibu maisha yangu, ninalifuta, sitalitumikia agano hilo kwa jina la
Yesu”.
Katika Yeremia 7:18, “Watoto huokota kuni, na baba zao huwasha moto, na
wanawake hukanda unga, ili kumfanyizia mikate malkia wa mbinguni na
kuwamiminia miungu mingine sadaka za kinywaji, wapate kunikasirisha
mimi”. Sadaka za kinywaji; kinywaji hiki ni damu inayotolewa kwa malkia wa
mbinguni na miungu mingine, na majini na mapepo.
4. Tabia ya Damu
Damu ina sauti, inaweza kulia na inaweza kuleta laana. Mungu amekataza kula
au kunywa damu kwa sababu hizi tatu. Mwanzo 4:10, “akasema umefanya
nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi”.
Kumbukumbu 12:23, “ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu
ndiyo uhai, na uhai usile pamoja na nyama”.
Damu inanena; Damu iliyomwagika chini inaweza kunena mema au yaweza
kunena mabaya, damu inenayo mema ni ya Yesu peke yake, Waebrania 12:24
inasema, “na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo
mema kuliko ile ya Habili.” Kumbe kuna damu inayonena mema (damu ya
Yesu Kristo) na pia kuna damu inayonena mabaya (damu ya ndege, wanyama,
hata watu). Damu yaweza kuongea mabaya juu ya mtu; damu ikimwagwa
hunena na ndio maana hata nchi yaweza kuingia kwenye matatizo kwa sababu
ya damu inenayo iliyomwagika.
Sasa kwa kujua kuwa kila damu iliyomwagwa inauwezo wa kusema, wachawi
hutumia tabia hiyo ya damu kufunga maisha ya watu. Kwa hiyo wanachofanya
wachawi au waganga ni kuchukua mnyama na kumchinja yule mnyama na
kuinuizia inene tatizo lako. Kimsingi; hii damu iliyomwagwa ndiyo inayoitwa
madhabahu ya tatizo lako. Na ndio maana waganga wa kienyeji huagiza kuku,
mbuzi au ng’ombe kwa ajili ya kumwaga damu ili inene mabaya juu ya mtu.
Yesu Kristo alipomwaga damu yake Kalvari alitupatia sisi uhai wake kabisa.
1 Wakorinto 5:7, “Basi jisafisheni mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa
donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu, kwa maana pasaka wetu
amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani Kristo”.
Damu ya Yesu inatupa wokovu na ushindi dhidi ya nguvu za giza na
mashetani. Katika Ufunuo 12:10-11, “Nikasikia sauti kuu mbinguni ikisema,
sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya
Kristo wake, kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye
awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. Nao wakamshinda kwa
damu ya mwanakondoo, na kwa neno la ushuhuda wao, ambao hawakupenda
maisha yao hata kufa”.
Kuna utakaso katika damu ya Yesu. Waebrania 13:12, “Kwa ajili hii Yesu naye,
ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe aliteswa nje ya lango”. Ni damu yake
ndiyo inatufanya watakatifu na kutuosha maovu yote. Tunaikimbilia kupata utakatifu
na kutufanya safi bila mawaa yoyote wala dosari.
Damu ya Yesu huondoa laana. Weka agano na Yesu leo. Mathayo 27:29,
“Wakasokota taji ya miiba, wakaiweka juu ya kichwa chake, na mwanzi katika
mkono wake wa kuume, wakapiga magoti mbele yake, wakamdhihaki,
wakisema, salaam, mfalme wa Wayahudi”. Hebu sema maneno haya;
“imeendikwa ardhi ililaaniwa itazaa michongoma na miiba, kwa damu ya Yesu
ilitoka katika taji la miiba, ninaifuta laana ya ardhi, sasa ardhi itazaa uzima,
furaha, na upendo.